Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[103]

 

 

 

Ushirika wa Meza ya Bwana

(Toleo 1.1 19950413-19981226)

 

Jarida hili huelezea maana mbalimbali zihusuzo sakramenti za Ushirika wa Meza ya Bwana. Siku ya maandalizi na Pasaka pia vimefafanuliwa. Utaratibu wa kuoshana miguu na makate na divai pia vime fafanuliwa kuhusu jinsi ya kutumia. Uhusiano uliopo kuhusu Kutoka katika utumwa na Pasaka vilevile vimeelezewa. Damu ya Agano Jipya na uingiaji wa kuhani mkuu Patakatifu pa Patakatifu ambaye alikuwa ni Masihi ni kutuwezesha sisi sote kuwa watoto wa Mungu. Maana ya Pasaka ashirio lake katika mausiano yake na aya nyingine (mf. Zab.34:20; Isa.52:13-15) imefafanuliwa. Maandiko yaliyoko katika Yohana 14 na Yohana 17 pia yametafsiriwa.

 

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

(Copyright ã  1995, 1996, 1998 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

 


Ushirika wa Meza ya Bwana [103]

 


Jioni hii pengine ni ya tukio takatifu sana kuliko siku zote zilizomo katika kalenda ya Mungu kwakuwa ni huu ni ukumbusho wa kifo cha Bwana na Mwokozi Yesu Kristo. Kuaadhimisha ibada hii kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha Yesu. Aya zifuatazo hutujfundisha asili ya ibada ibada hii, na maadhimisho yake.

 

Luka 22:7-16 inasema 7 Hata siku ya mikate isiyotiwa chachu ambayo ilipasa kuchinja Pasaka.8Akawaita Petro na Yohana akisema, mkaniandalie pasaka nipate kuila. 9Wakamwambia, Wataka tuandae wapi? 10 Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji, mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye. 11Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu anansema, Ki wapi chumba cha mgeni, nipate kula pasaka humo na wanafunzi wangu? 12 Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo. 13 Wakaenda, wakaona kama alivyo waambia, wakaiandaa pasaka.14 Hata saa ilipofika akaketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye.

 

Imedhaniwa na baadhi ya watu kuwa hii ilikuwa ni ile saa ya kuila Pasaka, lakini wazo hili sio sahihi.

15 Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; 16kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapo timilizwa katika ufalme wa Mungu.

 

Kristo alikuwa anasema kwa mifano Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; 16kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapo timilizwa katika ufalme wa Mungu.Luka 22:7-16 imetafsiriwa katika njia kadhaa chache ili kufikilia aya hii. Kristo hakula mlo unaohusu Pasaka. Yeye alikula Pasaka yenyewe. Imafafanuliwa kiuwazi sana na imeelezewa kirahisi. Alitamani sana kula nao lakini alijua kuwa angeuawa kisha yake. Kristo alisema hapa kwamba tena hiki hata itakapotimilika katika ufalme wa Mungu. Kwa kusema kwake hivyo basi Kristo alitabiri kifo chake kabla ya mlo wa Pasaka wenyewe. Kwa kweli yeye alikuwa ni Mwana Kondoo wa Pasaka.

 

Tunajua kuwa hizi zilikuwa ni Siku za Mikate isiyotiwa Chachu. Ulikuwa ni mwanzo wa Mikate isiyotiwa Chachu, wakati Pasaka ilikuwa inatolewa dhabihu yake.

 

Yohana 6, Kristo alifanya miujiza ya kulisha chakula wayu elfu tano kwa kutumia mikate mitano na samaki wawili. Ilikuwa ni ishara ya kuwa wateule wamekombolewa kwa kutokea katika makapu kumi na mawili Muujiza wa kutembea katika maji ulifanywa na Kristo kama ni sehemu ya wokovu wateule. Baada ya ile miujiza, kundi alilokuwanalo Kristo liligawanyika wengine wakamwacha kwa ajili ya yale mafundisho yake ambayo alisema 53Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho. (Yoh. 6:53-54)

 

Matokeo yake yalikuwa ni ya kusikitisha sana. Kazi ilibakia kwa Kristo mwenyewe na wale wanafunzi wake thenashara, na mmoja kati yao alikuwa ni shetani.Sasa hatua ya jambo lile ilikuwa na hatua ya chini sana ya kikazi. Kila mmoja alijikwaa na Bwana wao. Kisha hapo kazi ikawa imejengwa tena. Tunakumbuka pia kwamba hatimaye aliwawekawakfu sabini wengine na kuwatuma waende kuifanya kazi yake. Tunajua pia jinsi mapepo walivyowatii na ya jinsi hawa mapepo walivyo watambua na kuujua ukweli huu. Imeaandikwa mbinguni. Tunajua kwamba wale sabini waliendelea kufanya huduma. Tunajua kwamba Kristo aliwatuma waende kufanya kazi. Hata hivyo, linaloshangaza ni kwamba katika mlo huu wanaoonekana ni wale thenashara tu. Je, wako wapi wale sabini wengine? Na Je, wale wengine wengi waliobakia wako wapi? Yaani wale wafuasi wengine wa Kristo walikuwa wanafanya nini? Je, ni kwa nini Kristo aliadhimisha ile na wanafunzi wale thenashara tu?

 

Kuna majibu mengi sana vya kutosha kujibu maswali haya yote. Wale sabini walikuwepo pale kwa ajili ya Pentecoaste. Walikuwa hawajaliacha Kanisa. Haikosi kulikuwa na milo mingine mingi ya Pasaka ilivyo andaliwa na watu wengine kwa makundi yao. Kristo aliamua kula mlo wake (wa mwisho) na thenashara peke yao.Wale sabini haikosi walikuwepo sehemu nyingine zaidi wakishiriki Pasaka. Matendo ya wale sabini hufungulia aina mbalimbali ya kazi ambazo hapo zamani zilikuwa hazitiliwi maanani. Wanafunzi wengine sabini wakawepo pale. Kisha wakapunguzwa hadi kufikia idadi ya theneshara. Lakini wale sabini walikuwa bado wamewekwa wakfu na bado waliendelea kufanya kazi na kukua kiimani hadi kufikia siku ya Pentekoste kuanzia siku hii ya Karamu ya mwisho.

 

Hii sasa inatuelezea sisi kuwa kuna kazi mbalimbali katika kufanya kazi tangia mahuano ambayo aliyajenga, yakipotea na kuunganishwa tena. Yakijengwa na kisha kuimarishwa tena lakini. Kwa hiyo, katika Kartamu hii ya mwisho ilikuwa na inatoa ishara tofauti kidogo kuliko ingalivyoweza kufikirika hapo mwanzo. Wakati tunapofikiria kuhusu Karamu ya Mwisho, tunahusika na kuwafiria wale thenashara. Ingawaje hatuwezi kuwaweka watu katika dhana kuwa huenda walikuwepo watu wengine. Lakini Biblia inatueleza kuwapo inawezekana kuwa walikuwepo wengine wengi. Wale sabini waliwekwa wakfu na walikuwa ni wazee wa Yesu Kristo. Wao ni nguzo katika maeneo au mambo mengine yahusuyo kazi katika kutimiliza mahala pa wazee na kutimiliza mahali pa Pasaka na utimilivu wake na mgawanyo wake. Kuna idadi ya kubwa ya vitu inayoelekeana na hii.

 

Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu inahusisha yote mawili yaani siku ya maandalizi na Pasaka katika Sikukuu.

 

Mathayo 26:17-30 inasema 17 Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake waka mwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka? 18Akasema, Enendeni mjini kwa mtu Fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu; kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu. 19Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa Pasaka. 20Basi kulivyokuwa jioni aliketi chakulani pamoja na wale Thenashara. 21Nao walipokuwa wakila, alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti. 22Wakahuzunika sana, wakaanza kumwuuliza mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana? 23Akajibu akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika kombe, ndiye atakayenisaliti. 24Mwana wa Adamu aenda zake, kama ilivyoandikwa; lakini olewake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa. 25Yuda, yule mwenye kumsaliti, akamjibu, akasema, Ni mimi, Rabi? Akamwambia, Wewe umesema. 26Nao walipokuwa wakila, Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle, huundio mwili wangu. 27Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; 28kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 29Lakini nawaambieni, sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakayokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu. 30Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.   

 

Shughuli hii ilifanyika kama inavyosemahapa, kuwa ni katika siku ya kwanza yaMikate isiyotiwa Chachu. Kwa wakati ule,ilikuwa ni siku ya maandalizi, siku ya 14 ya mwezi, ilihesabiwa kuwa ni siku ya kwanzaya siku nane ya Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu, kwa hiyo ni hakika kuwa ilikuwa ni siku ya maandalizi ambayo tukio hili hilitokea. Siku hii ya maandalizi ilianzisha ashirio jipya. Ashirio hili linapatikana katika .maandalizi ya Pasaka inayokuja. Kwakuwa kutakuweko na kutoka utumwani kwa mara ya pili na makuhani wapya (Isa.66;20-21) Meza ya Bwana ni ishara ya maandalizi ya Kanisa kwa ajili ya utawala unaokuja wa milenia.

 

1Wakorintho 11:23-26 inasema 23 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa ninyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa  mkate, 24 naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 25 Na vivi hivi baada yakula akakitwaa kikombe, akisema, kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo,  kwa ukumbusho wangu. 26 Maana kila mwuulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

 

Usiku Usiku huu unatangaza kifo cha Bwana hadi ajapo, kama kanuni waliyowekewa Wakristo.

 

Sura yote ya Yohana 6 yahusu utaratibu wa  ishara hii inayotuongoza katika  maandalizi na kwa Pasaka. Kuna maana  maalumu katika kila sentensi moja ya  Yohana 6 na jinsi inavyomuandaa kila mtu  kwa ajili ya wito wake, sehemu yao kati ya  wateule na sehemu yao katika  makabila kama washiriki wa wale 144,000 na ule umati wa watu ulio chini ya wale mitume thenashara wakiyahukumu makabila..

 

Yohana 6:53-54. inasema 53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

 

Kuna kanuni kuu tatu kuzifuata ili kuurithi uzima wa milele. haya huwa hayahusishwi kwa

kawaida katika kushiriki Ushirika wa Meza ya Bwana. Mawili kati ya hayo yamo katika Yohana 17:3.

 

Kanuni ya kwanza Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Kanuni ya pili ili kuuridhi uzima wa milele ni kuwa na imani kwa Yesu Kristo kwakupitia kumjua Mungu wa pekee wa kweli.

Kanuni ya tatu ili kuuingia uzima wa milele ni kushiriki Pasaka na kuula mwili na damu ya Yesu Kristo (Yohana 6:53-54).

 

Haya ni masharti matatu unayotakiwa kutimiza ili kuuingia uzima wa milele. Masharti haya ambayo pia ni kanuni, hutegemea na utii alionao mtu. Yaani utii. Utii huu ni kwa Mungu wa pekee wa kweli kwa njia ya kuzishika sheria zake. Hii ni kanuni muhimu katika kumpendeza Roho Mtakatifu. Bila ya Roho Mtakatifu huwezi kuuingia Ufalme wa Mungu na kisha kuurithi uzima wa milele. Kwa hiyo kwa kupitia hizo kanuni tatu ndipo unalazimika kupitia ili uonekane kuwa umeshiriki kikamilifu kufikiliza unyenyekevu. Utii katika mambo yanayofuatia maadhimisho ya sheria za sikukuu na taratibu ambazo Kristo aliziweka kwa ajili ya kushiriki katika Pasaka. Kama hushiriki maadhimisho haya basi wewe huna sehemu wala ushirikika na Yesu Kristo.

 

Jambo la kwanza linalofanyika katika maadhimisho haya ya Meza ya Bwana ni tendo la kuosha miguu. Tendo la kumuosha mtu miguu yake lilikuwa ni la kawaida sana katika nyakati au siku za Yesu. Watu walikuwa wakiva viatu aina ya talawanda ambazo zilikuwa zinawakinga na hali ya mazingira iliyokuwepo wakati ule. Talawanda ni viatu vya wazi vyenye kuonyesha hata vidole. Zilikuwa kwa kweli ni aina ya viatu vinavyofaa sana kwa safari, kama tunavyofahamu. Watu walivaa talawanda kwa sababu zilikuwa zinapitisha hewa kirahisi na kuleta baridi na zilikuwa zinauzwa kwa bei rahisi na nirahisi pia kuzitengeneza, lakini vilikuwa vinasababisha sana miguu yako kupata vumbi kirahisi sana. Kwa kawaida, tendo la kuosha mtu miguu lilikuwa linafanyika kama ishara ya wenyeji kumwonyesha mgeni ukarimu wao wakati anapo anapo watembelea nyumbani kwao. Kwa kawaida watu wanakuwa wanaoga majumbani mwao lakini kwa ajili ya kutembea kwao mitaani au njiani walikuwa wanachafuka au kujisikia uchovu. Hivyo basi kwa tendo hili walikuwa wanauhishwa tena na kujisikia kuburudika. Kazi ya hii ka kuosha miguu ilikuwa ni kazi iliyokuwa ikifanywa na mtumwa duni na mwenye cheo cha chini sana. Mgeni alikuwa anapewa taulo na balasi la maji. Kwa kawaida ilikuwa inafanyika kipindi kile mgeni anapowasili tu au muda mfupi kabla ya kuanza kula chakula, kabla au wakati mgeni anapokuwa anajongelea meza. Tendo la kukataa kufanya kazi hii huashiria ukweli kwamba hakuna mtu mahali hapo aliyetayari kufanya kazi duni kwa ajili ya kumtumikia mtu mwingine.

 

Hili ni tendo linaloashiria kuwa tayari kutumikia wengine na dunia hii kwa hakika imekuwa na watu wenye msimamo usiopenda kujitoa kutumikia watu wengine (kama mtu hawamfahamu). Watu kwa kawaida hawapo tayari kukubali kujishusha chini kwa minajiri ya kuwainua wengine. Inagharimu mtu kuwa na moyo wa kipekee na ni Roho Mtakatifu tu ndiye anayeweza kufanyiza jambo hili kuwezekana. Ni mojawapo ya muhuri wa wateule (ambao ni watumishi wa Yesu Kristo) ambao kwa kweli wanaweza kufurahia kuwatumikia wengine; ambao wanaweza kuuchukulia ushindi wa ndugu zao wapendwa kama ni ushindi wao wao wenyewe na wanaweza kuinuana wao kwa wao. Hatua za kuhudumiana hazipo dhahiri kwa kulingana na mfumo uliowekwa chini ya mungu wa dunia hii. Mungu wa dunia hii ameweka mfumo (au kwa lugha nyingine ni kwamba elohim wa dunia hii ameweka mfumo) unaotegemeana na juhudi binafsi katika kujiweka katika kiwango au matabaka ya ubora na madaraja ya vyeo na kujitanguliza au kutumia mabavu kama wanyama. Wanyama wote wana utaratibu wa kuishi kwa kutumia mtindo wa mwenyenguvu mpishe. Mfumo huu wa maisha ya kutumia mabavu huwaamulia matokeo ya aina gani ya chakul watakacho kula, na msimamo wao wa kijamii utakuwaje, na hali zao za baadae zitakuwaje. Namna hii ya maidha haitakiwi sisi tuwe kama hivyo. Hatupaswi kuwa na fikara za namna kama hizo. Utaratibu huu wote mzima wa kuoshana miguu haupo tu kwa minajiri ya kutimiza lengo la ibada tu. Bali ni ishara ya kwamba tuko tayari kujinyenyekesha na kujiachilia kwa minajiri ya kuwajali na kuwatanguliza wengine. Tunaliona hili kutoka katika mtazamo wa ki-“tithenai” (yaani tendo la kuweka mbali vazi) na kujifunga kwa Kristo na taulo. Utaratibu huu wote ulikuwa unaashiria wakati Kristo kwa njia ya kimatendo kabisa aliweka chini mshipi wake na kanzu yake. Kwanza kabisa aliweka chini ile heshima yake ya kimbinguni yaani ya ki-elohim. Aliweka chini jambo hilo na kufanyika mwanadamu wa kawaida ili atuokoe sisi. Alijua kwamba alipaswa aje hapa chini ulimwenguni, sio kwa lengo la kuja kujionyesha tu kwetu, kwa sababu tuliishi chini ya mfumo ambao mashetani waliuunda. Bali alikuja duniani kama mwanadamu ili kuwaonyesha mashetani kuwa aliweza kunyenyekea kiasi cha kuyatoa maisha yake kwa ajili yetu.

 

Mapepo kwa ajili ya kule kuasi kwao hawana aina yoyote ya dhabihu kutolewa ili kuweza kuwapatanisha na kuwarudisha kwa Mungu. Hakuna aina yoyote ya dhabihu itakayo weza kutolewa itakayo mwezesha Shetani na Jeshi lake lote kuwapatanisha na Mungu kwa ajili ya dhambi zao. Na hata kama ingewezekana basi ingempasa mmoja afe. Kwa hiyo mmojawapo angelipaswa achukue mwili wa kibinadamu na akukubali kufa ili aweze kujipatanisha na Mungu na kuwaonyesha njia. Hii haina maana kuwa ni kwa sababu Mungu anapenda sana dhabihu ya damu la hasha. Hii ni kwa sababu alisema kuwa bila kupitia utaratibu huu mtu hawezi kuwa mali yangu. Alisema kuwa sitaweza kuishi ndani ya yeyote kati yenu ambaye hajaandaliwa kujinyenyekesha kiasi cha kuutoa uhai wake kwa ajili ya ndugu zake. Hivyo basi, kama hutajitoa maisha yako na kuosha miguu ya wapendwa ndugu zako ili kujishusha wewe mwenyewe, Mungu kamwe hataweza kufanya makao ndani yako. Na hili ni jambo lenye kuhuzunisha sana. Tumelishuhudia kanisa katika katika karne ya ishirini kwa jinsi lilivyofikia kiwango cha juu cha kutoa heshima kwa watu ya kibinadamu kiasi cha kufikia hatua ya kushindwa tena kutumikiana. Hali hii imepelekea Roho Mtakatifu aondoke kwao na kuwaacha. Kristo alianzisha mpango huu wa kitafrija kwa wafuasi wake ili iwe mfano wa kujitoa dhabihu. Sasa tutalipima wazo zima la kimatendo la kuosha miguu , zaidi kuliko vile lilivyokuwa hapo mwanzoni, kwa mtazamo wa kuwa hawa Jeshi la mbinguni kama viumbe wakiroho. Kila mojawapo ya mambo haya yana maana ya kiroho na matendo halisi ya kimwili. Dini ya Kiyahudi inaangalia kwa kurudi nyuma

kwenye Pasaka na kuiona katika mtazamo wa kimwili. Wakati ambapo sisi tuna-angalia mbele kwenye Pasaka na kuiangalia katika mitazamo yote miwili yaani ya kiroho na kimwili. Kristo alijua kuwa angeweza kusalitiwa hatimaye na kwamba alipaswa kuyatoa maisha yake kwa ajili yetu.

 

Yohana 13:1-5 inasema: Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo. 2 Hata wakati wa Chakula cha jioni; naye Ibilisiamekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti; 3 Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye ametoka kwa Mungu, 4 aliondoka chakulani, akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni, 5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.

 

Tendo lake la kuweka kando vazi lake muhimu (yaani tithenai) ilikuwa ni ishara ya utayari wa kuyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Kwa njia hii ya kuyatoa maisha yake ni ashirio la kuwa ametuosha sisi sote. Somo kuu na la msingi kuhusiana na kuoshana miguu kuonyesha kujitoa nafsi zetu na unyenyekevu. Mojawapo ya malengo ya Yesu yalikuwa ni kuwa tayari kuyatoa maisha yake kwa unyenyekevu, na kuwa tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili ya kil;a mmoja wetu binafsi yake, kama rafiki. Na kwa ajili hiyo basi, sisi pia tunapaswa kuwa tayari kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya wengine.

 

Yohana 13:6-8 inasema 6 Hivyo yu aja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? 7 Yesu akajibu, akammwambia, Nifanyalo wewe hujui hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. 8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.

 

Yawezekana sisi sote tunayajua maneno haya na tunaweza hata kuyakariri kutoka moyoni. Petro hakutaka aoshwe na yeye miguu yake kwa sababu nzuri tu alizokuwa nazo. Petro alimtaka kuwa na Masihi Mfalme. Hakujua chochote kuhusu Siku ya Upatanisho. Hakujua kuwa Kuhani Mkuu alikuwa anatembea mle ndani kwanza na vali la hariri kwa ajili ya kufanya ibada ya upatanisho na kufanya upatanisho. Kisha yake alikuwa anabadilisha na kuvaa jozi ya vazi jipya. Hakuwa na habari kuwa walikuweko Masihi wawili; wa kwanza ni yule aliyekuwa mnyenyekevu na kuvaa vazi wazi la hariri na wapili ni yule aliyetakiwa avalishwe vazi lenye hadhi ya Mfalme. Alimhitaji mtu mwenye kutawala, kwa mfano wa mfalme Dario au kama mojawapo ya wafalme wa Kiajemi, au Makaisari. Alitaka kumtetisha Yesu Kristo kwenye kiti cha enzi cha Makaisari ili aitawale dunia hii ki dhalimu kama Makaisari walivyokuwa wanafanya, lakini kwa kutokea Yerusalemu. Alitaka kupewa fursa ya namna ileile kama wakiyokuwanayo Warumi. Hizi ndizo zilikuwa fikara za Petro zilizomsukuma kutoa mchangio kama huu wa mawazo. Hiki ndicho kitu ambacho Petro kinampelekea kusema Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Alisema hivyo akimaanisha kuwa ilikuwa inaashiria kuwa tulikuwa tunaenda kuwa watumwa. Alifikiri kuwa nitamfanya Mrumi anioshe miguu. Hii ndiyo Petro aliyokuwa akiwazia. Lakini Kristo alielewa hilo. Hii ndiyo maana Kristo alijiondoa kutoka katika kwa makutano mara baada ya kufanya ule muujiza wa Yohana 6. Pia walinuia kumfanya Msihi awe Mfalme. Kristo wakati wa Ushirika wa Meza ya Bwana kwamba alikuwa miongoni mwao kwa kadiri ile tu alipokuwa ana watumikia.

 

Inapaswa kuangalia katika mtazamo wa kisaikolojia uliokuweko nyuma yao uliopelekea watu hawa kusema hivyo. Wao walikuwa ni Wazayuni waliokuwa wamejiamini sana katika viwango vya ubora wa kiitikadi. Petro alikuwa bado hajaongoka wakati huo. Kadhalika hakukuwa na hata mmojawapo wa wanafunzi hawa aliyekuwa ameongoka hadi kufikia wakati huu wakishiriki mlo huu. Walikuwa wamebatizwa tu lakini hakuna hata mmojawapo miongoni mwao aliyekuwa ameongoka. Tunaona jinsi Kristo alivyolielezea jambo hilo baadae. Alimwambia Petro nawee utakapoongoka waimarishe ndugu zako (Lk. 22:32). Petro hakuweza kuongoka hadi pale alipompokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Shetani alikuwa ameamriwa kumpepeta kama ngano (Lk.22:31) kwa mara ya kwanza ni kwa utaratibu kama vile Kristo alivyo mweleza wakati wa kushiri Meza ya Bwana. Hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa na Roho Mtakatifu hadi kufikia siku ya Pentekoste. Walikuwa wamebatizwa lakini kulikuwa na kitambo kati ya siku waliyobatizwa hadi kufikia siku ya waliyompokea Roho Mtakatifu. Sisi tunawekewa mikono ili kumpokea Roho Mtakatifu lakini hatumpokei kwa nguvu zinazolingana kama ilivyotokea kwao siku ya Pentekoste. Ya kwetu hii ni kama punje ya haradari. Labini hata hivyo watu hawa walikuwa bado hawajaongoka. Haya tunaweza kuyajua kwa kulinganisha yale ambayo Petro anayoyafanya. Somo kuu na lililo dhahiri hapa tunachojifunza ni kwamba Petro hakuwa tayari kujinyenyekesha ili kuyatoa maisha yake na kuwatumikia wengine. Hakuwa tayari kutoa huduma kwa Watu wa Mataifa au makabila ya Kipagani. Yeye alikuwa na Myahudi. Tunatakiwa tumtumikie mtu yeyote.

 

Tunahitaji kuruhusu miguu yetu ioshwe kama ishara ya kuwa maisha yetu yametakaswa na Kristo katika mtazamo wa kila siku, ili tuweze kuwa na sehemu na yeye katika Ufalme na kwa kweli katika kila kitu anachokifanya. Kama tutafanya hivyo, tutaurithi Ufalme kama alivyofanya. Petro aliujua umuhimu wa tendo hili lakini hakujua ilikuwa inaashiria nini.

Yohana 13:9-11 inasema Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu hata na kichwa changu pia. 10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. 11 Kwa maana alimjua yeye atakaye msaliti, ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.

 

Jambo linalotakiwa kulijua ni kwamba, kama utakuwa hujajiandaa kufanya kazi, na kujitoa na kuwa mshiriki wa mwili (ili kufanya hayo yafanyike), basi hutapata chochote kihusucho Ufalme. Lakini Petro anamwambia akisema. Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu hata na kichwa changu pia. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba hakutaka amkose asiwe naye. Akakemewa na mtazamo wake ukashughulikiwa. Alitaka kufanyike mambo mengine mengi kwa sababu hakuwa ameelewa maana ya kuoshwa miguu. Hakujua kuwa yeye aliye batizwa mara moja inatosha kwa siku zote. Wala hakika hakuelewa hayo, kwa sababu ya maashirio mazima ya kifo cha Kristo na dhabihu ilikuwa bado haijatolewa. Lakini alipaswa kujua kwa kupitia Agano la Kale, alipaswa ajue kupitia Maandiko Matakatifu yasemavyo kuwa Kristo itambidi afe n kwamba ni kwa kupitia kifo hiki cha Kristo pekee ndipo upatanisho kati ya wanadamu na Mungu unapatikana. Alipaswa aufahamu ukweli huu kwanza.

 

Mara tu kifo hiki kitakapo wapatanisha wanadamu na Mungu wanatakaswa kwa kupitia ubatizo. Kila mtu aliyeshiriki sehemu yake katika ibada ya ubatizo, ametakaswa kupitia ubatizo kwa sababu ya kifo cha Kristo ambacho kwa wakati ule kilikuwa kikitarajiwa. Tendo la uoshaji miguu lilikuwa ni kumbukumbu ya kuafanyka upya ya kila mwaka. Ni kwa njia hiyohiyo,. Wageni walioakuwa wamealikwa katika karamu ya arusi ya Mwana Kondoo wamekwisha oshwa (walikuwa na bafu zao kupitia ubatizo). Walikuwa na mavazi yao tayari walitopewa. Mavazi yao hayana doa kwa sababu yameoshwa (katika damu ya Kriso). Miguu yao tu, kutokana na mapito ya duniani humu, yame sababisha kupatwa vumbi na inahitaji kusafisha kwa njia ya kurejesha hali upya kila mwaka.

 

Kwa hiyo, kwa kupitia utaratibu wa kuosha miguu kila mwaka unasafisha miguu yako, kimwili, kiroho, tunasafisha misingi ya miili yetu ya kiroho. Tunarudi na kutazama nyuma kuona mahali petu na Kristo ili kwamba tuweze kuendelea mbele kuelekea mwaka wa pili ulioandaliwa (na betri zetu zikiwa zimetiwa nguvu kama ukipenda) tayari kubeba majukumu tuliyopewa. Kwa hiyo basi, vazi letu na litunzwe liwe safi. Tunapaswa kuwa safi kwa sababu tuna sehemu pekee ya kufanya (kwa isha ya miguu) uchafuko. Kwa hiyo tunasafishwa tena. Hili ni wazo tunaloendanalo katika aya ya 10.

 

Katika ibadaya ubatizo, dhambi zilichukuliwa mbali nasi na zitaendelea kuchukuliwa kabisa. Hii ilikuwa ni hatua ngumu sana kuifahamu kwasababu Kristo alikuwa bado hajafa kwa wakati ule na watu walikuwa bado hawajaongoka. Kitu kile walichokuwa wanafanya ni kufanyiza mfumo ambao ungeweza kueleweka na sisi, ili kwamba tuweze kuvuta hisia zetu nyuma na kutathimini kila kitu walichofanya. Kisha hapo tuelewe kuwa taratibu na ishra gani zilikuwa. Kwa hiyo aliwaambia Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote;Tunahitaji kuosha tu na tunafanyika wapya. Hatuhitajiki kubatizwa kila mwaka. Tunachotakiwa kukifanya ni kuwa tunahitaji kuosha miguu yetu kila mwaka. Kama ishara hizi zenye kuburudisha zisingekuwa nzuri vya kutosha basi tungelazimika tuwe tunabatizwa katika kila baada ya miezi kumi na miwili ili kurudia mzunguko au kusingekuwa na maana na kile kinachofanyika wakati wa Ushirika wa meza ya Bwana. Mambo haya yote hufanyika kwa lengo la kutuhuisha upya sisi na kutuleta kwenye hali ya kudharauliwa na kupatanishwa na Mungu.

 

Kanisa la Korintho lilishindwa kwa sababu walishindwa kujileta wenyewe kwenye kiwango cha kuvutiwa na kujitoa kimahusiano yao na Mungu. Hawakujiandaa na kuwa tayari kushiriki mlo huu, chakula hiki cha jioni na Pasaka (au Usiku ule Maalumu wa Kuukumbuka Sana). Hawakujiandaa ili kutumia kipindi kile ipasavyo. Kama wangetii maandiko matakatifu yaliyoko katika Kumbukumbu la Torati 16, au hata kwa kule kula tu wakati wa ibada, wasingeweza kuwa katika hali ya kufikia kuifanya meza hii kuwa ni mahali pa kulewea, kama walivyokuwa wanafanya.

 

Jambo lingine tunaloliona hapa ni kuwa, Yuda wa Iskarioti alikuwa pia amebatizwa. Naye Yuda Iskarioti alioshwa miguu yake vilevile. Utaratibu huu wa kuosha miguu na kula mkate kunywa divai ulikuwa ni kwamba uoshaji miguu ulikuwa unafanyika mapema sana kabla ya kushiriki mlo. Yuda Iskarioti hakushiriki hadi pale divai ilipokuwa imesha nywewa tayari. Alishikiri kikamilifu taratibu zote za ibada na liki ni kitu ambacho tunatakiwa kukitia akilini sana. Yuda Iskarioti alikuwa amebatizwa, alishiriki kikamilifu katika kuoshana miguu, alishiriki pia kula mwili na kunywa damu ya Yesu Kristo, lakini tena Yuda Iskarioti aliruhusu nafsi yake ipagawe na kutumiwa na Shetani kwa sababu nia ya moyo wake ilikuwa ni mbaya.

 

Nia ya moyo wa Petro ulitamanishwa na wazo la ubora aliyonayo Shetani kwa hapa duniani. Aliyatazama maisha katika hali ya mfumo wa ngazi za kimadaraja. Lakini aliona makosa yake kwa haraka sana; ambao Yuda Iskarioti hakuuona. Kwa namna ileile, wanafunzi wengine waliomba waketi katika mkono wa kuume na mwingine mkono wa kushoto wa Kristo. Lakini hakuwa Yesu mwenye uwezo huo wa kufanya hivyo. Kristo sio Mungu. Mungu ameandaa viti katika mkono wa kuume na wa kushoto wa Kristo kwa sababu kuna kazi Fulani maalumu ambayo anataka ifanyike kwa ajili ya kufanya marejesho na upatanisho wa Jeshi.

 

Yuda hakusafishwa na kuwa safi moyoni nasi tutaendelea kuwaona kina Yuda Iskatioti wakiwemo kila mara. Kwa kweli, kama utasoma Biblia kutoka katika tafsiri ya “Knox” ya Vulgate, utaona kwamba Kanisa la Wafiladelfia liliruhusiwa kuwa na watu wanaotoka katika sinagogi la Shetani (yaani walio mali halisi ya shetani mwenyewe) waingie ndani yake. Sasa hii ni dhana halisi kabisa. Kuna watu maalumu walio kuwa wamechaguliwa na Shetani kufanya shughuli zake za kiuwakala ndani ya mfumo wa Kifiladelfia. Tunapaswa kutilia maanani ujanja ulioko nyuma ya dhana hii. Hizi zote ni dhana zinazotenda kazi katika hali ya kiroho. Sisi sio Wayahudi. Wala sisi hatuyafikiri mambo katika mtazamo wa kimwili. Bali sisi ni Wayahudi wa kiroho ingawa hatumo katika makabila yale ya Yuda. Sisi tu wanachama wa taifa la Israeli. Kuna tofauti kubwa. Lakini sisi tu Israeli wa kiroho kinadharia.

 

Tunachohitajika kufanya ni kuoshwa miguu tu kwa kadiri tulivyokuwa tumetakaswa kwa njia ya maji ya ubatizo na hivyo basi tumesafika mara moja na kwa siku zote. Tunachokifanya wakati wa Ushirika wa Meza ya Bwana ni kusafishwa miguu yetu. Kwakusema kweli na katika roho, tunakuwa tukikusanya madhambi kwa kadiri ile tunapokuwa tunaendelea kushi na kupitia katika mapito mbalimbali ya maisha, ndio maana tunahitaji kufanya ishara hii ya marudio ya imani ya nia yetu safi katika kufanya agano letu la ubatizo. Kwa hiyo basi ndio maana tunahitajika kuoshwa tena. Kwa mujibu wa dhana hii ya kiishara, tunakubaliana na tendo la kuoshwa tena kwa kadiri tunapoenda katika uoshaji wa miguu.

 

Katika Yohana 13:12-17 tunaiona tena dhana hii.

Yohana 13:12-17 inasema 12 Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? 1 3Ninyi mwaniita, Mwalimu, na Bwana, nanyi mwanena vyema, maana ndivyo nilivyo. 14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. 15 Kwakuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. 16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. 17 Mkiyajua hayo hari ninyi mkiyatenda.

 

Hapa anajaribu kuwaelezea kuhusu maana ya ishara hii kwa sababu wao hawakujua taratibu zake kama sisi tunavyozijua leo. Lakini maneno haya yameandikwa hapa ili sisi tujue kuwa kulikuwepo na ishara ambayo walitakiwa waijue. Kutokana na tendo la Bwana na Mwalimu kuwaosha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi ilikuwa hatimaye ni jambo la ajabu na la kushangaza alilolifanya Kristo. Wazo endelevu liliwekwa kuwa iendelezwe katika misingi ya umilele katika kujaribu kuiwekeza ikae na kuonekana umuhimu wake katika mawazoni mwetu yaani ni kwa jinsi na namna gani tunapaswa kutumikiana kila mmoja na mwingine.

 

Tatizo walilonalo watu wetu wengi katika karne ya ishirini ni kwamba kumekuwa na ushindani wa hali ya juu sana kushindania mambo mbalimbali, matokeo yake ni kwamba wanajikuta ni vigumu sana kukubali kujitia chini ya kiwango cha watu wengine katika hali ya kudumu. Hali hii ya kimashindano yaliyoko katika jamii zetu imakuwa ni mtego uliowanasa na kuwala wengi. Watu wanafundishwa kufanya mashindano ya kila aina ya ngazi katika maisha. Watu wamefundishwa kuwa wajione hawajakamilika au kufikia utoshelevu kama watakuwa hawajafikia utimilifu wa malengo waliyojiwekea katika viwango vinavyostahili katika mfumo waliojiwekea. Hii ndio maana tuna viwango vikubwa sana vya kitakwimu vya watu wanaojitoa mhanga maisha yao kwa kujiua wenyewe hasa kwa watu kutoka rika ya vijana. Wajapani pia wana idadi kubwa sana ya kitakwimu ya watu wanaojiua miongoni mwa vijana wao inayotokana na hali hii ya kuishi katika mfumo wao wa kimashindano. Wanalazimika kufikiri kwa kulinganisha fikira zao na jinsi zinavyo endana na mfumo wao wa kimashindano. Wanatamani waweze kuishi maisha bora. Wanatamani kufikia malengo yao ya mafanikio. Wanatamani wasome hadi kufikia ngazi ya Chuo Kikuu na wanatamani wapate huko digirii hatimaye. Jamii zao zinazowazunguka hawataweza kuwathamini kama hawataweza kufikia malengo yao ya limafanikio. Sasa hii inatokana na dhana ya kupewa tunu mbalimbali kwa ajili ya bidii yao inayotokana na hali hizi zisizo weak mlingano halisi. Watu huchukulia dhana na mitazamo hii yote na kiasi cha kuwafikisha mahali pa kupoteza mwelekeo wa kulinganisha uthamani wa kila mtu binafsi yake na jinsi ya kumthamini mwingine. Kristo atakaporidi atafanya marejesho ya baadhi ya maeneo atakiwayo mwanadamu kufanya yaani hali ya kujikana na kujitoa dhabihu ambazo anazizungumzia na mbazo sisi tunahusika kwazo.

Kristo amesema katika aya 16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.

 

Sasa hili na wazo alilolitumia alipokuwa anakazia kuelezea sehemu yake mwenyewe kuwa yuko katika daraja lililo chini na Mungu ili tuweze kuelewa sisi sote si wakuu na hatuna matarajio kuona Malaika au Jeshi lililoanguka wakichukuliwa au kukubalika na Mungu. Tunafanya tendo hili la kuoshana miguu kwa nia ya kuonyeshana kuwa tunaendeleza katika uangalifu mkubwa sana sehemu yetu wenyewe na kiroho na Yesu Kristo.

 

Na sasa, kwa kufuata maelekezo ya Yesu na mfano wa maisha yake, basi tutaoshana miguu.

***

 

Ishara hii ya kuoshana miguu ina tafsiri kuu mbili muhimu. Kwanza, ilikuwa ni tendo la kimwili, na katika 1Wakorintho 10, ukisoma kuanzia aya ya 1 utaelewa kuwa wokovu wa kimwili wa watu wetu ulifanyika kama ni mfano kwetu sote ilikutuandaa kwa ajili ya awamu ya pili ya wokovu. Kwa kupitia ubatizo tunashiri katika Roho Mtakatifu ambaye alifungwa kwa wana wa Israeli kabla ya kuja Kristo.

 

1Wakorintho 10:1-13 inasema: Kwa maana, ndugu zangu, sipendi  mkose kufahamu kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita chini ya wingu; wote wakapita chini ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa kinywaji kilekile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. 6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyo tamani. 7 Wala msiwe waabudu sanmamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi, kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. 8 Wala tusiwe waasherati, kama wengine wao walivyo fanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. 9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. 10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyo nung’unika, wakaharibiwa na mharabu. 11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 12 Kwa  hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. 13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha njaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

 

Aya ya 6 inagonga kengele ya onyo kwenye vichwa vyetu. Waliona kazi kubwa sana. Iwapo kama yeyote yule kati yetu angekuwepo pale basi tungeshangaa sana kubwa ambayo Bwana aliwafanyia wana wa Israeli wakati alipowatoa nje chini ya uongozi wa nabii Musa wakati wa msafara wao ule, kutoka kwao na yale mapigo. Kama tungeliyaona matendo hayo basi tungeweza kushangazwa sana kuuona uweza wa Mungu. Sababu mojawapo lililowafanya walishindwa ilikuwa ni kwa sababu hawakuwa na Roho Mtakatifu. Hii haimaanishi kuwa sisi ni watu bora sana katika eneo lolote zaidi kuliko wale walivyokuwa lakini lililo muhimu tu hapa ni kwamba Mungu ametuchagua, ili amuweke Roho wake Mtakatifu ndani yetu, ili atusaidie kuzishinda kila aina ya mvuto wa mambo ya kimwili na matatizo yetu wenyewe.

 

Aya ya 7 inaendelea kutaja matatizo kadhaa ambayo aliyaona, ijulikanayo kama ibada ya sanamu.

 

Aya ya 11 inaonyesha kuwa ilitokea kwao kama maonyo. Hayakuwa ni maonyo kwa wale waliouawa. Wao wamesha kwisha kufa tayari. Yalikuwa ni maonyo kwa Israeli waliosalia na ilikuwa ni ishara dhahiri ya maonyo. Na pia yalikuwa ni maonyo kwa ajili yetu. Aya ya 12 hutufundisha kuwa Mungu huruhusu sisi sote tujaribiwe lakini Mungu hataruhusu majaribu hayo yafikie kiwango cha kutufanya sisi tushindwe kustahimili naye hutoa mlango wa kutokea tuwapo majaribuni. Kwa maneno mengine, ni kuwa kuna mlango wakati wote tulio wekewa. Kila mara kuna hali ambayo inaweza ukajikuta ukiwa kwenye njia panda na kisha unafanya maamuzi.

 

Imeandikwa Watu waliketi, kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze, Inanakumbushia ashirio la matendo ya ibada za sanamu na aina zake zote ambazo zilifanyika kwa nyakati hizo. Bwana na Mungu mwenye wivu na kamwe hata kubali achukuliane na aina yoyote ya ibada hizi za sanamu. Aina yoyote ya mawazo na tamaa za uzinifu ni dhambi kufanywa tayari rohoni. Ni dhambi kufanya hivyo kwa watu waliogeuka na kumrudia Mungu wao. Uzinzi kwa ufupi ni dhambi itendwayo kimwili, ni sawa na ibada ya sanamu ambayo ni dhambi ya kiroho. Na hiindio maana talaka imeuhusiwa kwa sababu ya uasherati, kwa sababu Mungu aliwaacha Israeli kama vile mume ampavyo talaka mwanamke muasherati kwa ajili ya kuabudu kwao sanamu. Mungu aliwapeleka Israeli mbali jangwani na Mungu aliwahukumu kwa ajili ya dhambi hizo.

 

Kwa mujibu wa amri hii inayokataza uzinifu, watu hawa wakatunga jinsi ya kumjaribu Kristo na wateule, kwa kujaribu kumtia Kristo majaribuni, mahala ambako wengi waliangamia. Walifungamanisha na kiwango cha kimwili matatizo makuu ya kiroho tunayo kabiliana nayo kusababishwa na Jeshi la waumini dhaifu ambao hata kati yao wameanguka na kushindwa kabisa katika mambo ya imani; ambao walikuwa ni washiriki wa Kristo katika madhabahu na wana wa Mungu. Kwa hiyo, mambo haya yote yako pale ili kututayarisha na kutuonyesha mahali tunapotakiwa kuweka malengo yetu na viwango ambavyo tunahitaji kuviweka. Hii inakuonyesha wastani wa chini wa kiwango cha chini cha ule mlingoti wa mchezo wa kuruka juu ulivyo, lakini tumepewa mti wa kutusaidia kurukia. Sisi haturuki juu ya mlingoti wa kipimo, bali sisi tunaruka zaidi na mti wa kurukia kwa kuwa tunaye Roho Mtakatifu na watu wale hawakuwanaye. Sisi tuna kiwango cha juu sana. Wakati mwingine wateule hushinwa kufikia hata viwango vya kawaida vya Watu wa Mataifa au Wapagani ambao hawana Roho Mtakatifu kabisa.

1Wakorintho 10:14-20 inasema 14 Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi nisemalo. 16 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 Kwakuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. 18 Waangalieni hao waisraeli waliokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? 20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani. Hamuwezi kunywea kikombe cha Bwana na katika meza ya mashetani.

 

Sasa hili na wazo linalo ashiria. Ni dhabihu ya madhabahuni inayoamua kuwa wewe u-mali ya nani, nani unayemwabudu na unafanya ibada zako kwa kutumia kitu gani. Madhabahu ile unayoiendea pia huamua ni Mungu gani unaye mwabudu na hii ni ishara muhimu kupita zite kukabiliana nayo. Huwezi kujongelea madhabahu ya miungu ya uwongo bila kuwa na woga, adhabu yake ni kifo.

 

Tendo la kutoka utumwani na Pasaka humaanisha kushindwa kwa Jeshi lililoanguka na mwanzo wa zama za elohim mbele ya Mungu Baba, na Yesu Kristo Mwanawake.

 

1Wakorintho 10:21-22 inasema: Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?

 

Hakuna michanganyo. Wakati unapohusisha mafundisho ya Mpinga-Kristo na meza haramu, basi unamhusisha munguwa uwongo. Ushiriki katika kushiriki meza ya mashetani umekatazwa. Ushiriki huu unahusika na hali ya kutoa sadaka au kupokea. Huruhusiwi kutoa au kupokea zaka au sadaka kutoka kwa miungu ya uwongo. Zaka na sadaka za makanisa kma hayo ni dhahiri kuwa yanapingana na maelekezo yaliyoko katika Matendo 15:19-29; 21:25-26; 1Wakorintho 8:1-13; 10:13-33, hususan aya ya 21; 2Wakorintho 6:16; 1Wathesalonike 1:9-10; 1Yohana 5:20-21 (inayosema  kuna Mungu mmoja tu wa pekee na wa kweli na Yesu Kristo ndiye Mwanawe) na Ufunuo 2:14,20. Haturuhusiwi hata kuchukua fedha kutoka kwa watu wanaopata mapato yao kutokana na kujiriwa kwao kutumikia katika mashirika au taasisi hizi za miungu ya uwongo. Ikiwa kama hujui mahali ambapo nyama unayopewa au kuumia imetolewa sadaka kwa miungu wa uwongo au kwa miungu migeni, basi hilo halina matatizo kula kwasababu unakula bila kujua kwa utukufu wa Mungu. Lakini iwapo utakuwa unajua chanzo chake, kuwa ni sadaka iliyotolewa kwa Mashetani, hapo huna tena budi usitumie. Mafundisho kuhusu utatu mtakatifu ni mojawapo wa mafundisho haya mapotofu ya miungu ya uwongo.

 

Kuna mkate mmoja tu, ambao ni mwili wa Kristo, unaotufanya sisi sote kuwa mwili mmoja, tunaposhiriki mkate huu mmoja. Kuna kikombe kimoja tu, kikombe cha Bwana. Je, tunamchukiza Kristo kwa pale tunaposema kuwa kuna Mungu mmoja tu? La, hasha! Wala si makosa. Kristo ni Bwana na Kiongozi wetu, lakini yeye si yule Mungu wa pekee wa kweli. Kristo hukaa ndani yangu na hukaa ndani ya kila mmoja wetu, kama vile sisi sote tulivyo kombolewa kutoka katika nguvu za mauti.

 

Lakini ashirio hili hutufanya tuwe tumetengwa kandoni. Ule Msafara wa kwanza wa Ukombozi Lilihusu kututoa kutoka utumwani Misri na kuanzishwa kwa taifa la Israeli, ili kwamba mahali pale ambapo Mungu atapatumia katika kufunua mipango yake kupitia manabii wake.

 

Yeremia 31:31-34 inasema 31Angalia siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 32Si kwa mfano wa agano lile ninilolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA. 33Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, watakuwa watu wangu. 34Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, wakisema,Mmjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA.

 

Tutaendelezwa na Roho Mtakatifu kufikia mahali ambapo sisi sote tutamjua Mungu. Hii ndiyo neno linasema kichwa cha Yesu ni Mungu na kichwa cha kila mwanamume ni Kristo. Kwa kuwa tuna Roho Mtakatifu tunamfahamu Mungu na kumfahamu Yesu Kristo kila mmoja wetu. Hii ni kutimiliza Maandiko matakatifu kutoka katika unabii wa Yeremia. Hii ndio maana hakuhitajiki mtumishi wa Mungu yeyote kujiingiza kati ya yeyote kati yetu na Yesu Kristo. Hakuna mtumishi anayeweza kukuambia kuwa wewe hustahili kufanya jambo Fulani maalumu ambalo limeelekezwa katika Biblia na kukuondoa katika majukumu. Hakuna mtu anayeruhusiwa kupunguza maelekezo yanayo elekezwa na sheria, wala hakuna kabisa kati yetu aliyepewa uweza huo.

 

Hata lile Agano linaloelezewa kuwa litafanywa, linahitaji dhabihu ya damu (soma jarida lisemalo Agano la Mungu, Na. 152).

 

Mathayo 26:26-28 inasema: 26 Nao walipokuwa wakila, Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle, huundio mwili wangu. 27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; 28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.  

 

Hivyo basi, Kristo alifanya agano na sisi; lakini agano lilihitaji kama yalivyo maagano yote, dhabihu ya damu. Kristo alifanywa kuwa kuhani wetu mkuu kutokana na Waebrania 8:3.

 

Waebrania 8:3 inasema:3Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa

 

Kuhani Mkuu aliingia hadi Patakatifu pa Patakatifu na dhabuhu ya damu. Ishara hii ilikuwa na maana ya kutuongoza sisi au kutufikisha kwenye dhabihu ya Kristo kama dhabihu ya damu. Kristo kama kiongozi, alijitoa mwenyewe kwa ajili yake pia. Hakuna aina yoyote ya dhabihu ambayo ingeweza kuwa bora kiasi cha kutosha, wala ambayo ingezewa kukithi haja halisi kwa kiwango ambacho Munga anachorikiria, na kukithi haja ya vile mawazo yetu sisi yalivyo.

 

1Wakorintho 10:24 inasema 24Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya wenzake.

 

Hili ni wazo sawa linalotokana na tendo la kuoshana miguu. onyo hili lilitolewa na Kristo, kwa kuwa Kristo hakujitafutia faida zake mwenyewe, lakini ametutajirisha; vitu ambavyo vilikuwa ni vya kwetu, na kufanya hivyo, aliingia mahali pa dhabihu ambapo aliyatoa maisha yake kama kielelzo kwetu kwamba tunatakiwa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya wengine. Wazo hili la mwili wa wokovu kuwa kama mkate inaonekana katika Yohana 6:58.

 

Yohana 6:58 inasema: 58Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali alaye chakula hicho ataishi milele.

 

Mkate ule wa jangwani yaani Manna ilikuwa ni ashirio, la mfano kwetu, kuwa tutatakiwa kula mkate wa Yesu Kristo. Mkate ule ulikuwa kutoka mbinguni. Ilikuwa inaashiria kuwa hakuna kitu ambacho tungeweza kukifanya au kutosheleza. Ilikuwa ni kwa kupitia Kristo na dhabihu yake ambavyo tungeweza kufikia kiwango cha kuwa Wana wa Mungu.

 

Marko 14:22 inasema: 22 Nao walipokuwa wakila, alitwaa mkate, akabariki, akawapa, akisema, Twaeni; huu ndio mwili wangu

 

Inatakiwa ifanyike leo.

 

Bwana Mungu, Baba wa Milele, tunakuomba ubariki mkate na divai. Tunakuomba uvuvio wako kwetu ili tuelewe maana za ishara hizi. tunakuomba hayo kwa jina la Kristo Yesu. Amina.

 

Agano lililoelezewa katika Yeremia 31:31 haliangalii mbele kwenywe agano la milele. Agano lile lingeweza tu kuweko katika siku hizi, na kuanzishwa kwa mintaarafu ya kuendelea.

 

Luka 24:39 inasema 29 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikeni shikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa navyo.

 

Kwa hiyo, damu ya Kristo ingetakiwa mara moja tu. Na mara baada ya Kristo kupaa mbinguni kusinge kuweko tena dhabihu, kwa kuwa angekuwa na mwili wa kiroho. Na kufanya kusiwepo tena na hatua nyingine zaidi ambayo agano lingeweza kuhitajika au kuelezewa. Lilianzishwa pale na kisha limekuwa ni agano endelevu na la kudumu. Divai ni ishara ya dhabihu ya kuhani mkuu, ambayo hutolewa kwa kila mwaka, kupitia damu ya madume ya ng’ombe, ambayo kuhani mkuu alikuwa anaingia nayo Patakatifu pa Patakatifu. Kristo kupitia dhabihu yake alipasua kizuizi cha pazia lililokuwa lina watenganisha, na mara ile, akaingia Patakatifu pa Patakatifu mara moja na kwa ajili ya wote na kutuwezesha sisi sote vilevile kuingia pia katika uhusiano na Mungu, na kumpokea Roho Mtakatifu. Ili kuweza kuyafanya haya inatubidi sisi tupate msamaha wa dhambi ambayo ilikuwa ni ishara ya dhabihu ya Kristo.

 

Waebrania 1:3 inasema: 3Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu

 

Dhabihu hii ilikuwa na maana mbili, na divai ilikuwa pia ni ishara ya Kristo ambaye alitenda mambo kama divai.

 

Yohana 15:1-6 inasema:Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na baba yangu ni mkuliwa. 2Kila ta wi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililo waambia. 4Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. 6Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi  na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.

    

ya divai kuwa inatokea kwenye matunda ni mfano wa Roho Mtakatifu, ambaye kila mmoja wetu anatakiwa kuwa na tunda la Roho, kupitia Kristo kwa nguvu za Mungu. Ishara iliyo rahisi kuhusu dhabibu ya Kristo imeashiriwa katika mifano hii miwili ya mkate na divai. Sasa tunaweza kushiriki divai.

 

********

Pengine ni muhimu kuelewa kuwa mkate na divai, ambao sisi tumeshiriki muda mfupi uliopita, umeongeza kiwango fulani cha uelewa wetu juu ya dhabihu ya Kristo ambayo haikuweza kufahamika kwa kupitia Mwana Kondoo wa Pasaka. Mifupa ya yule Mwana kondoo haikuweza kamwe kuvunjwa ili kuashiria kuwa ilikuwa ni mifupa ya mtu mwenyehaki ambaye mifupa yake ilibakia bila kuvunjwa ili kutimiza unabii wa Zaburi 34:20, lakini mwili wa Kristo ulivunjwa pale msalabani. Mkate unawakilisha mwili wa Kristo ambao umefanya watu wengi wa aina mbalimbali na ndio maana mkate umemegwa vipandevipande. Damu ya mwana kondoo haikuwa kamwe inanywewa, lakini sisi tunakunywa divai, kama ishara ya damu ya Kristo iliyomwagika kwa ajili yetu. Imesemekana kwamba unaposhiriki ishara hizi, tunatakiwa kwenda hadi kwenye siku ya pili ili kuelewa kuwa Kristo anakwenda kupata mateso makali kwa ajili ya dhambi tulizozifanya sisi. Tutafakari mojawapo ya jumbe za kinabii zinazohusiana nazo, ambao uko katika Isaya.

Isaya 52:13-15 inayo sema:13 Tazama  mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana. 14 Kama vile wengi walivyo kustaajabia, (uso wako ulivyokuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), 15 ndivyo atakavyo wasitusha mataifa mengi; wafalme wanamfumbia vinywa vyao; maana mambo yasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.

 

Isaya 53:1-12 nayo inasema:Ni nani aliyesadiki habari tuliyoiona? Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani? 2 Maana alikua mbele zake kama mche mwororo. Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. 3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. 4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu na kuteswa, 5 Basi alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 6 Sisi sote kama kondoo tulio potea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. 7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake. Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. 8Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakaye simulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya waliohai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu. 9 Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake; 10 Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake; 11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki, Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao. 12 Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja na waliohodari, Kwa sababu alimwaga nafsi yake hadi kufa, Akahesabiwa pamoja na wakosao, Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.

 

Tunaona kuwa nabii Isaya alielewa asili hasa ya Kristo. Tunaona kwamba nabii Isaya alionyeshwa ailitakiwa afe na kuhesabiwa na wakosaji au waovu na ya kwamba ataona uzao wake. Lakini sasa ni kwamba Kristo hakuwa ameoa na wala hakuzaa watoto, lakini unabii unayemhusu yeye unasema kuwa ayaona uzao wake. Unabii huu ulipaswa kutimizwa. Sisi ndio wazaliwa wake wa kwanza tuliotolewa kwa Yesu Kristo. Pia sisi ni bibi arusi wa Kristo na uzao wetu wapaswa kuwa ni mwanzo wa zama za hukumu yenye haki, kwa jina kipindi hiki kinaitwa miaka elfu moja ya Milenia. Hawa uzao unaoelezewa hapa watajumlishwa na Kristo ili kutawala na yeye katika sayari hii na dunia iatkuwa itakuwa na utengamano halisi na mkamilifu na Mungu. Hivi ndivyo unabii unavyosema. Hii ndio maana tumefananishwa na bibi arusi. Kristo atakuwa ndiye baba yetu wa milele kwa mujibu wa Isaya 9:6. Yeye ayakuwa baba yetu nasi tutakuwa bibi arusi wake na uzao wetu utaunda mfumo wa milenia, wale wote waliofundishwa katika unyofu na haki. Ni kwa kupitia katika mlo huu tu ndipo tunaweza kuelewa haya au kuchukua pahala pake.

 

Mara baada ya wanafunzi walipokuwa wameshiriki tafrija hii, Yesu aliwapa maelekezo makuu na muhimu.

Yohana 14:1-31 inasema: Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi nanyi mwepo. 4 Nami niendako mwaijua njia. 5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 7 Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa  mnamjua, tena mmemwona. 8 Filipo akamwambia, Bwana tuonyeshe Baba, yatutosha. 9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwepo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; Basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? 10 Hamsadiki kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo nanone niyasemayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzitenda kazi zake. 11 Mnisadiki kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. 12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya, naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 13 Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya. 15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi Mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambao ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye anakaa ndani yenu. 18Sita waacha ninyi yatima; naja kwenu. 19 Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mtaniona. Na kwasababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 20 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. 21Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 22 Yuda (siye Iskariote) akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? 23 Yesu akajibu akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutashuka kwake, na kufanya makao kwake. 24Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu ila ni lake Baba aliyenipeleka. 25 Hayo ndiyo niliyowaambia nilipokuwa nikikaa kwenu. 26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa ajili yangu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa, niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. 28 Mlisikia kuwa mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba; kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. 29 Na sasa nawaambia kabla haijatokea, kusudi itakapotokea mpate kuamini. 30 Mimi sitasema nanyi maneno mengi sana, kwa maana yu aja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. 31 Lakini ulimwengu ujue nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru, ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.

 

Tunaposoma Yohana 14:3, tunaona Kristo akiwaambia wanafunzi wake kwamba alikuwa anaenda kuwaandalia makao (na yetu sisi pia). Vyumba vyote katika Hekalu la Mungu vilijaa makuhani. Vyumba hivi vya hekaluni vilijengwa kwa kufuata utaratibu maalumu katika kujazwa na kazi za kikuhani kutoka kwa kuhani mkuu hadi eneo la chini yake. Kila chumba kilichoandaliwa kwa ajili yetu kinatoa ishara ya kwamba sisi tumechaguliwa, kila mmoja wetu kama kuhani wa Mungu aliye hai. Hii ndiyo maana ya mfano wa vyumba ambavyo Kristo anatuandalia.

 

Katika Yohana 14:4-7 tunaona kwamba kwa ufahamu wetu tumjuavyo Yesu Kristo, katika kushiriki kwetu katika dhabihu tunaweza kumjua Mungu. Wakati mtu yeyote akikuambia kuwa Mungu ni fumbo na hawezi kufahamika, utajua sasa ya kuwa wasemao hivyo bado hawajaongoka na hawamo miongoni mwa wateule. Kwa sababu ni kazi yetu, kupiitia dhabihu ya Yesu Kristo, kushiriki kikamilifu kutaka kumjua Mungu. Kama ukisema kuwa Mungu ni fumbo, basi ni wazi kuwa humjui na haumo miongoni mwa wateule na wala wewe si wa Kristo. Ili kumjua Mungu wa pekee na wa kweli na mwanawe Jesu Kristo, ni jambo muhimu kwa ajili ya kuuingia uzima wa milele (Yoh. 17:3). Kukataa hilo ni kujitenga ama kwa Baba yetu au kwa Mwana wake Yesu Kristo.

 

Katika Yohana 14:10-12, tunaona kuwa kazi zenyewe zinashuhudia (kazi zetu zinatushuhudia) kuwa Baba yumo ndani yetu au yu pamoja nasi.

 

Katika Yohana 14:13-20, tunaona kuwa kwasababu Mungu alimpa Kristo uweza wa kuishi naye pia ametupa uweza wa kuishi. Kwa kuwa Kristo yu ndani ya Baba, na Baba yu ndani yetu. Sisi tu ndani ya Kristo na ndani ya Baba nao wote wawili wamo ndani yetu. Mfumo wowote unaojaribu kututenganisha sisi na Kristo na Baba ni wa uwongo na mafundisho kama hayo ni mapotofu. Ni kama jaribio la kutuibia haki yetu ya uzaliwa wa kwanza kwa kutumia uwongo.

 

Katika Yohana 14:21-23, inaonekana waziwazi kabisa kuwa wote wawili wanakuja na kufanya makao ndani ya kila mteule anayempenda. Katika aya ya 24; tunaona kuwa ushikaji wa amri za Mungu ni wa muhimu kwa ajili ya kumpendeza Roho Mtakatifu na nikazi ya kila mteule kwa Mungu na kwa Mwanawe.

 

Aya ya 27 iko dhahiri kabisa. Roho Mtakatifu hutufungamanisha sote pamija, Baba, Mwana na watoto wote wa Mungu. Kila mmoja wa wana wa Mungu ameshikamanisha pamoja na Baba kwa namnia ilwile moja. Sisi sote ni warithi pamoja na Kristo, tuliofungamanishwa na Baba kwa Roho Mtakatifu aliye mwezesha Kristo na wengine wetu wote kufanyika elohim.

 

Aya ya 28 inaelezea jinsi tulivyopatanishwa na Baba. Kama Baba asingekuwa ni mkuu basi angeenda kwa Yesu Kristo.

 

Katika aya ya 30 tunaona kuwa kumbe mungu wa dunia hii hana uweza juu ya wana wa Mungu.

 

Ni jambo muhimu kufahamu kuhusu namna ambavyo mahusiano na Baba yalivyo rekebishwa. Ukweli wa jambo hili ni kwamba yamerekebishwa na Roho Mtakatifu, kwa kupitia jinsi tunavyozishika sheria katika upendo wetu kwa Kristo. Tumeshiriki mwili na damu ya Kristo na kuunganishwa na Kristo kwa lengo maalumu na kwa nia hiyo ni kutuifanya kuwa ni kitu kimoja na Baba. Ibada ya Ushirika wa Meza ya Bwana ni hakika hutupatanisha sisis na Mungu. Sio ya kutufikisha kwenye kikomo cha uhusiano wetu na Yesu Kristo. Ukomo wetu mzuri ni kutufanya tuwe wamoja na Kristo ili kwamba sote tuwe na umoja na Mungu. Hakuna kutengana kati yetu. Ni jambo lazima kuwa na umoja na Kristo ili tuwe na umoja na Mungu.

 

Katika kufunga Ushirika wa Meza ya Bwana hushughulikiwa na Uungu na uhusiano wetu na Mungu.

Yohana 17:1-26 inavyosema: Maneno hayo aliyasema Yesu, akainua macho yake kuelekea mbinguni, akisema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako pia akutukuze wewe; 2kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili uliompa awape uzima wa milele. 3Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

 

Kuna Mungu mmoja tu na wa pekee, na Yesu Kristo ni Mwana wake. Ukifahamu jambo hilo utaurithi uzima wa milele.

 

Yohana 17:4-5 nayo inasema: 4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile ulinipa niifanye. 5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

 

Kristo alihitimisha kazi yake katika hali ya kumtukuza Mungu. Kisha aliomba akinukuu kutoka kwenye mwanzo wake hadi kwenye utukufu ule ambao alikuwanao na Mungu kabla ya kuwekwa kwa misingi ya dunia.

 

Yohana 17:6-8 inasema: Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. 7 Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. 8 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika kwamba yametoka kwako, wakasadiki kuwa hakika wewe ndiwe uliye nituma.

 

Kristo ndiye aliyewezesha jina la Mungu kufahamika kwa watu ambao Mungu alimpa Kristo. Wateule wamelishikilia neno la Mungu. Yeye hakuwa yule Mungu wa pekee wa kweli. Lakini Hata hivyo, waliamini kuwa Mungu alimtuma.

 

Yohana 17:9-10 inasema: 9Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu, bali wao ulionipa, kwa kuwa wao ni wako; 10na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao.

 

Hahusiano ya kina kati ya wateule na Mungu na Kristo yako dhahiri katika kifungu hiki cha maandiko matakatifu.

 

Yohana 17:11 inasema:11Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini wamo ulimwenguni.

 

Kutoka katika aya ya 11 tunaona kwamba Kristo amepewa jina pia na mamlaka na Mungu. Inatokana na dhana ya Kiebrania. Mahali jina linapotolewa unabeba uweza wa mamlaka iliyototewa. Kwa ajili hii ndio maana Musa alikuwa anaitwa elohim yaani mungu mdogo. Kristo alikuwa anachukulia mfano wakati wateule wakiwa wamebakia hapa duniani. Wamepewa dhamana na Mungu. Wote wawili yaani Mungu na Kristo pamoja na wateule wote ni kitu kimoja.

 

Yohana 17:12 inasema:12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi niliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

 

Katika aya ya 12 inasema ili andiko litimie. Haikuwa kwamba Yuda Iskarioti hakuwa na uwezo wa kuchagua, kwa kuwa alikuwa amefanya. Alipewa fursa ya kuokoka lakini alishindwa. Sio kuwa ni kwa sababu asingeweza kufanya hivyo. La hasha! Alipewa fursa lakini kwa uovu uliokuwa umeujaza moyo wake ambao ulijulikana kutoka kuumbwa kwa misingi ya dunia. Kwa muda mrefu sana maandiko haya matakatifu yalikuwa yameandikwa, hivyo ilijulikana kuwa matukio haya yangetokea na kwamba Kristo ilimpasa awe na mwanafunzi ambaye hatimaye angemsaliti. Mungu hafungwi na matatizo yetu yanayohusu nyakati, na ya umbali kama tu alivyo kwamba ufahamu wake uliamua kabla kuwa Yuda Iskarioti angefanya dhambi. Mungu hakumfanya yeye afanye jambo hilo. Lakini Mungu ni kwamba alijua tu kuwa angefanya hivyo. Kuna tofauti kubwa sana.

 

Yohana 17:13 inasema: 13 Na sasa naja kwako, na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

 

Kutoka katika aya ya 13 tunaona kwamba Kristo alisema kwamba tulipaswa kuelewa kile ambacho kilikuwa kinampata kwa manufaa yetu na kuwa furaha yake iweze kutimizwa ndani yetu.

 

Yohana 17:14-16 inasema:14 Mimi nimewapa neno lako, na ulimwengu umewachukia kwa kuwa; wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu

 

Dunia huwachukia wateule kwa sababu wao huishi kwa kulitii neno la Mungu. Kristo alitoa neno, yaani Logos (hapa hujulikana kama logos) kwa wateule. Hivyo basi Logos ni maelekezo au sauti halisi ya Mungu ambayo haikutokana wala kuwa na mahusiano na ubinadamu wa Yesu Kristo. Hii ni tofauti na neno pseudo-logos linalolikuta katika 1Timotheo 4:2 lenye maana ya mtu anaye ongea uongo (ukisoma Marshall’s Interlinear).

 

Wateule wametakaswa na kweli ambayo ni neno la Mungu.

 

Yohana 17:17 inasema: 17 Uwatakase kwa ile kweli; neon lako ndiyo kweli.

 

Wateule wametumwa ulimwenguni kama Kristo alivyowatuma kondoo kati ya mbwa mwitu wakali.

 

Yohana 17:18-19 inasema: 18 Kama mvile ulivyonituma mimiulimwenguni, nami vivyohivyo nawatuma hawa ulimwenguni. 19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.

 

Aya ya 19 inapelekea kwenye kutakaswa na kweli. Kweli ni utakaso wa Roho Mtakatifu. Kristo alitakaswa na kweli ili kwamba na sisi tuweze kutakaswa. Basi na kusiwepo uwongo kabisa miongoni mwa wateule.

 

Yohana 17:20-21 inasema: 20 Wala si hao tu ninao waombea, lakini na wale watakao niamini kwa sababu ya neno lako. 21 Wote wawe na umoja, kama wewe, Baba ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, hao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe iliye nituma.

 

Aya za 20-21 inaelezea ukweli kuwa dunia itajua tu kuwa Kristo ametumwa na Mungu kupitia ushahidi hakika wetu sisi. Kama hatuta hatutaweza kuonyesha hilo basi ulimwengu utakosa kujua ukweli kama Mungu alimtuma Kristo. Ni kupitia sisi kuwa mfano dunia watamuona Yesu Kristo na kujua kuwa alitumwa na Mungu na kuwa kweli alitimiza lengo lake. Huu ndio wajibu tuliopewa wateule. Wakati mwingine watenda dhambi wameitwa watoke dhambini kwa nia tu ya kuonyesha uweza wa Mungu. Wanafanyizwa upya na kufundishwa jinsi ya kutenda katika utumishi kwa Mungu wa pekee wa kweli, ili kuwashangaza katika uweza (1Kor. 1:27).

 

Tunashiri katika utukufu wa Kristo ili kwamba tuwe wamoja na Mungu.

Yohana 17:22-23 inasema:22Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23Mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue kuwa ndiwe uliye nituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.

 

Katika aya ya 23 tunasoma kwamba hakuna tofauti kwa upendo wa Mungu kwa Yesu Kristo na upendo wa Mungu kwa kila mmoja wetu. Mungu hana upendeleo kwa yeyote. Hampendi Yesu Kristo zaidi kuliko ampendavyo yeyote yule miongoni mwetu, kwakuwa hakuna dhambi wala uovu wowote ndani ya Baba yetu-na tendo la kupendelea watu ni dhambi. Kama Mungu angempenda zaidi Kristo kuliko anavyotupenda sisi basi angekuwa ni mwenye upendeleo ambao ni dhambi. Lakini Mungu hutupenda sisi sote katika hali ya usawa na kikamilifu kabisa.

 

Yohana 17:24-26 inasema:24 Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. 25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26 Nami naliwajulisha jina lako, tena nita wajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

 

Iko siku moja pia ambayo sisi tutavaa utukufu wa Mungu kama ule aliokuwa nao Kristo.

 

Baada ya hii, Kristo na wanafunzi wake waliimba nyimbo, kisha wakatoka nje.

Marko 14:26: Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni

 

 Ibada itaishia vivyohivyo kwa kuimba tenzi za nyimbo. Mfano ni ule unaosema Bwana ndiye Mchungaji wangu.

 

q