Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[106a]

 

 

 

Chachu ya Kale na Chachu Mpya

 

(Toleo 2.0 1995041-19980411

 

Neno chachu katika Agano Jipya limetumika kama mfano kwa vikilinganishwa kama chachu ya kale na chachu mpya. Tunatakiwa kuondoa kila aina yoyote ya mazalia ya chachu na pahala pake kiwekwe kitu kingine. Mfano huu una maana kuu sana ya kiroho kwa Mkristo. Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu inaeleweka kwamba inatufundisha kuhusu umuhimu wa kuweka mbali chachu ya kale ambayo ni uovu na udhaifu wote na kubakia na chachu ya uchaji wa moyo uliojaa roho na kweli. Pia kuna chachu nyingine katika sadaka ya Pentekoste ambaye nayo inafanya mfano kwa Kanisa katika mahusiano yake na chachu kuu ya Roho Mtakatifu.

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Copyright  ã  1995, 1997, 1998 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Chachu ya Kale na Chachu Mpya [106a]

 


Wazo dhana la dhambi ni kama inavyojulikana maana yake kuwa ni tendo la kuvunja au kuasi sheria au amri za Mungu.

1Yohana 3:4 inasema: Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi (au anom) au uvunjaji wa sheria [kwa mujibu wa Biblia ya Kiingereza ya KJV] au ni kutoka nje ya sheria.

 

Warumi 5:12-14 inasema: Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hiyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.

 

Kristo alichinjwa tokea mwanzo wa kuwekwa kwa misingi ya dunia.

 

Ufunuo 13:8 inasema: Na watu wote wakaao juu ya nchi watamwabudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.

 

Kwa hiyo basi, dhambi zilijulikana kuanzia mwanzo wa kuwekwa misingi ya dunia kama ilivyo kwa ajili ya wito wetu. Hali ya kufahamika au kujulikana tanmgia mwanzo hata kabla ya kuzaliwa kwa wateule kunaonekana katika Warumi 8: 28-30.

 

Warumi 8:28-30 inasema: Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.

 

Sheria ni zile amri kumi za Mungu na kila kinachotoka katika maelekezo ya hizo sheria kama zilivyotolewa na Mungu kupitia Kristo akiwa kama Malaika wa Mungu katika mlima Sinai iliyotolewa kwa nabii Musa. Sheria na amri hizi zinapatikana katika Agano la Kale na hivyo inaendana kwa kuingiliana na Agano Jipya. Kazi za hizi sheria au kwa mujibu wa mwanazuoni aitwaye ergon Nomou anamchukulia Paulo katika waraka wake kwa Wagalatia sura za 2 na 3 kuwa inagusa na kutoa uhalisi hasa wa kiini cha mafundisho ya dini zilizokuwapo katika karne ya kwanza baada ya Kristo yaliyojulikana kama Miqsat Ma’ase Ha-Torah au kwa kifupi MMT. Kwa ufupi ni kusema kuwa Kazi za Sheria ziko tofauti kutoka na kile sisi tunachokijua kama Amri kumi za Mungu. Fafanuzi za mtume Paulo haziwezi kuchukuliwa katika hali ya kutenganisha nazo (tazama majarida ya Kutofautisha katika Sheria [096], Pendo na Utaratibu wa Sheria [200], Maandiko ya Kazi za Sheria-au MMT [104] na Uhusiano Uliopo Kati ya Kuokolewa Kwa Neema na Sheria [082].

 

Mshahara wa dhambi ni mauti kwa ajili ya kuvunja sheria za Mungu.

Warumi 6:23 inasema: Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

 

Kwa njia ya sheria, tunafanyika kuwa ni watu wenye kujihadhari sana na dhambi. Sheria huufanya kila mdomo mbaya unyamaze kimya na kuwafanya wote wajione wana wajibika kwa Mungu.

 

Warumi 3:19-20 inasema: Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; kwa sababu hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.

 

Kwahiyo basi tunaona kuwa dhambi hufanya mtu ajisikie hukumu akilinganisha na sheria isemavyo, lakini sheria ni takatifu, ina haki na nzuri kwa sababu inatokana na asili ya Mungu (tazama jarida la Maagano ya Mungu [174].

 

Warumi 7:9-12inasema: Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa. Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti. Kwa maana, dhambi kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, kwa hiyo ikaniua. Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.

 

Hukumu inayotolewa kwa ajili ya kuvunja sheria ilishindwa kwa haki aliyokuwa nayo Kristo.

 

Warumi 5:18 inasema:Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.

 

Sheria haipingwi wala kupingana na ahadi za Mungu. Ahadi zilitolewa, hata hivyo, kwa njia ya kumwamini Kristo, mwombezi wetu, kwa waaminio.

 

Wagalatia 3:20-22 inasema: Basi aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja. Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria. Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.

 

1Timotheo 2:5 inasema: Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja Mwanadamu Kristo Yesu.

 

Sio kwamba wale wanaosikia sheria ndio wenye haki, bali ni wale wanao ziti. Sio kwamba wale waisikiao amri ya kwanza ya Mungu na huku wakimlinganisha elohim kuwa yu sawa na Mungu, au kwamba wale wasiozishika Sabato, na kujiwekea siku yao nyingine, au wale wanaojichongea sanamu, au wasiowatii wazazi wao au wenyekutamani mali za wenzao, au waongo au wezi. La hasha! Bali ni wale wampendao Mungu, sheria zake (Zab. 119:1-16, 97-106) na wanao wapenda wenzao.

 

Zaburi 119:1-16 inasema: Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria za BWANA. Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote. Naam hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake. Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii sana. Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako. Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo. Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako. Nitazitii amri zako, Usiniache Kabisa. Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako. Kwa midomo yangu nimezisimulia, Hukumu zote za kinywa chako. Nimeifurahia njia ya shuhuda zako, Kana kwamba ni mali mengi. Nitayatafakari mausia yako, nami nitataziangalia njia zako. Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.

 

Zaburi 119:97-106 inasema: Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa. Maagizo yako hunitia heshima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo siku zote. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako. Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya, Ili nilitii neno lako. Sikujiepusha na hukumu zako, Maana wewe mwenyewe umenifundisha. Mausia yako ni matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu. Kwa mausia yako nalipatia ufahamu, Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo. Neon lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. Nimeapa nami nitaifikiliza, Kuzishika hukumu za haki yako.

 

Warumi 2:12-16 inasema:Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo shaeria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria. Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki, kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, wenyewe kwa wenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea. Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na Injili yangu, kwa Kristo yesu.

 

Roho Mtakatifu na neema ya Mungu hazitufanyi kuwa huru na kuacha au kuwa mbali na umuhimu wa kuzitii amri za Mungu.

 

Warumi 6:15-18 inasema: Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha! Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii; mmekuwa wayumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki. Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.

 

Tumepitia katika tohara ya kiroho kwa njia ya Roho Mtakatifu. Kama tukizivunja sheria, basi tunafanyika kuwa bado hatuja tahiriwa na hivyo basi hatuwi wana wa maagano tena. Tunaangukia katika hukumu ya wale wanaotii na kuzishika sheria. Mtu anafanyika kuwa ni Myahudi iwapo kama yu mmoja kiundani, ametahiriwa katika Roho na sio kwa maandiko yaliyo tu yaliyomo vitabuni tu. Hata hivyo, tunayatii maandiko yakiyomo vitabuni kutoka ndani ya mioyo yetu, kwa njia ya mapenzi yetu ya hiyari.

 

Warumi 2:25-29 inasema: Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria, kutahiriwa kwako kumekuwa kumekuwa kutokutahiriwa. Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! Kutokutahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa? Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati? Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na torati ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.

 

Kanisa linakabiliwa na wale wasemao kuwa ni Wayahudi lakini wanasema uongo. Wakati mwingine madai ya uwongofu wa Israeli yanaendana sambamba na mwenendo wa wale waliokuwa wanapingana na imani ya Kisemiti. Kutodai kwao haki ya kuwa warithi na kukumbatiwa kusiko epukika na kujihudhurisha kwao na Israeli kwa njia ya kuongoka na kuwa kama washiriki wa pamoja katika Israeli ya kiroho, waongofu hawa wa uongo wanadai kuwa ni Israeli wa kiroho, lakini wakiukataa ukweli halisi utokanao na mwelekeo na mfano wake.

 

Ufunuo wa Yohana 3:9 inasema: Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.

 

Hapa, neno lilitumika kuelezea aina ya kuabudu ni ile ijulikanayo kama proskuneo ambalo lina maana ya kufanyiana mshikamano wa kunyoosheana urefu wa mikono kuelekea usoni mbele ya mtu unayemheshimu. Kwa hiyo, neno lililotumika kuelezea kuabudu halina maana kuwa limetumika mara zote likihusisha na tendo la kumfanyia Mungu ibada au kumpa heshima. Hatima ya hawa Makristo au Israeli wa uongo itakuwa katika mwisho wao ni kusujudu mbele za wateule ambao walikuwa wakiwatesa.

 

Sheria hizi zimeandikwa mioyoni mwetu au katika fahamu zetu kuanzia siku ya kuongoka kwetu.

 

Waebrania 8:10 inasema: …nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaiandika; Nami nitakuwa Mungu wao, Nao watakuwa watu wangu.

 

Hivyo basi, haija komeshwa au kuondolewa. Kwa kuzitenda na kuzifundisha amri hizi tunaitwa wakuu kabisa katika Ufalme wa Mungu.

 

Mathayo 5:17-20 inasema: Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la sikuja kutangua bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali atakaye zitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

 

(tazama pia jarida linalosema Maskini Lazaro na Tajiri [228]. Msisitizo wa sheria ni juu ya kumpenda mwenzako kama nafsi yako.

 

Mathayo 7:12 inasema: Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo, maana hiyo ndiyo torati na manabii.

 

Lakini kwanza kinachotangulia ni upendo wa Mungu.

 

Mathayo 22:36-40 inasema: Mwalimu, katika torati ni amri gani iliyo kuu? Akawaambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo iliyokuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati zote na manabii.

 

Kwa jinsi hii tumefanyika kuwa wana (wa kiume na wa kike) wa Mungu.

1Yohana 3:2-3 inasema: Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijajulikana bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama zlivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.

 

Kwa hiyo sisi tunaenenda kwa mujibu wa 1Yohana 3:4.

1Yohana 3:4 inasema: Kila atendaue dhambi, afanya uesi; kwa kuwa dhambi ni uasi.go vyenu vitumiwe kwa uchafu na uasi mpate kuasi au uvunjaji wa sheria.

 

Utakaso wa wateule unapitia katika utaratibu wa kuziacha dhambi zetu mbali. Hii inachukua sura halisi ya mfano wa chachu ya uovu na madhaifu.

 

1Wakorintho 5:6-8 inasema: Kijisifu kwenu si kuzuri, Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo, basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale wala kwa chachu ya uovu na ya ubaya, bali kwa yasiyo chachuchika, ndio weupe wa moyo na kweli

 

Mtume Paulo alikuwa anataja mlolongo wa mambo hapa. La kwanza lilikuwa ni kwamba Kristo alikuwa ni Mwana Kondoo wa Pasaka, dhabihu ya Pasaka wekwa na kutolewa na kuhani mkuu ambazo kwa kulingana na sheria za Mishna ilitakiwa awepo kondoo mmoja tu. Mwana zuoni Schurer anaunga mkono hoja hii kwa kusema katika jarida lake la Historia ya Wayahudi Zama za Yesu Krito, kwa Kiingereza likijulikana kama The History of the Jewish People in the Age of Jesus Christ (vol. 1, p.522). Jambo la pili muhimu kufahamika ni kwamba chachu sio dhambi lakini la msingi ieleweke kuwa kuna aina mbali mbali tofauti za chachu. Chachu iliyokuwa inatumiwa zamani ilikuwa na vyanzo vya mambo machafu.

 

Sikukuu ya mikate Isiyotiwa Chachu inaadhimisha ukweli kwamba tumekombolewa na Kristo kutokana kwenye chachu na kuwa kwenye hali isiyo na Chachu tena, katika hali ya kweli ya moyo na ukweli wa neno. Tunapaswa kuadhimisha sikukuu hizi kwa ajili hii.

 

Sababu ya tatu ni kwamba, tulikuwa bado hatujampokea Roho Mtakatifu aliyetolewa siku ya Pentekoste.

 

Roho huyu alikuwa ni chachu mpya kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.

Mathayo 12:33 inasema: Akawaambia mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia

 

Kipimo hapa ni mwandamano wa matukio kuanzia kwa Mungu hadi kwa Kristo hadi kufikia wateule. Kwa hiyo, mwana mke hapa ni Kanisa, chachu ni Roho Mtakatifu na vipimo vitatu ni ngazi za kimahusiano ndani ya familia ya Mungu. Vyote hivi vingekuwa chachu. Mungu angakuwa ni yote katika yote na ndani ya yote (Efe. 4:6).

 

Mfano wa mikate miwili siku ya Pentekoste, ambayo imetiwa chachu, ina mahusiano ya moja kwa moja na kwenye dhana hii (tazama jarida lisemalo Pentekoste katika Sinai [115].

 

Wazo tunalohitajika kuwa nalo ni kwamba tunatakiwa kuondoa chachu za kale zisiwepo katika sikukuu. Na tuweke kando mbali nasi aina madhaifu ya kila namna na kuelekea kwenye maendeleo ya tabia za utakatifu na haki katika Roho. Hii inatakiwa itazamwe kama ni ujenzi wa Pentekoste, inayo fanyika kama mfano wa malimbuko yetu katika mavuno baada ya Kristo. Mavuno haya hutangulia yale mavuno makuu ya Sikukuu ya Vibanda au ya vijumba vya nyasi kwa sababu NI KITU KINACHO ENDELEA KWA KIPINDI CHA MIAKA ELFU MBILI. Hivyo basi ni kusema kuwa hukumu Yetu ni SASA.

 

Mfano wa mwandamano wa mambo kuelekea ujenzi wa Pentekoste ni kwamba kipindi cha majuma saba inayotoa mfano wa kipindi cha Yubile kama kinavyohusiana na wanadamu. Maisha ya mwanadamu yalipunguzwa kutoka umri wa miaka 120 hadi miaka 70 tu. Wana kipindi cha miaka 50 tu cha kuendeleza hadi kfikia ukomo wa hatua ya mwisho ya maisha yao na kufanya ushirika na Mungu katika ufufuo wa wafu. Hii ilionekana kama mfano katika kila eneo lihusulo mambo ya imani. Basi inaashiria pia kwa kipindi hiki cha siku 50 ya Pentekoste. Ilitolewa mfano kwa kila ufundi wa kikandarasi wa Hekalu la Mungu lililojengwa na mfalme Suleimani, kutokana na maelekezo na malighafi za kujengae alizokuwa amepewa.

 

Utaratibu huu uliwakilisha Hekalu ambalo lilikuwa ni Hekalu lililo hai la Kanisa. Lilikuwa na ngazi saba kwa upande wa mbele. sita kati ya hizi ilikuwa imepandana juu yake kwenye ukingo wake na ya saba ilikuwa ndio ukumbi mkuu stahili, ambao ulikuwa unaelekea katika Patakatifu pa Patakatifu. Tusingeweza kuingia kwenye hatua hii ya mwisho hadi pale Kristo alipokufa na kupasuliwa kwa pazia la hekalu na kufanya uwezekano wa sisi kuingia ndani yake. Hii ni ishara yenye kuonyesha mfano wa majuma saba ya kuelekea siku ya Pentekoste. Katika eneo hili la mwisho Roho M<takatifu aliingia kwenye Kanisa na kumfanya Mungu awe ni yote katika yote na ndani ya yote. Haya yalikuwa ni mavuno ya jumla. Kristo ndiye alikuwa huu Mganda wa Kutikiswa au ni suke ororo la kwanza la shayiri kama mganda wa kitikiswa uliokatiliwa mbali ukiwa katika uchanga wake wa ujana. Mavuno ya pili yanaanzia na kipindi cha ngano kisha inaendelea hadi kipindi cha Makusanyo, ambacho ni awamu ya tatu ya mavuno ya Mungu. Awamu hii ya tatu kinawakilishwa na siku takatifu katika mwezi wa saba.

 

Pentekoste ni ni kilele cha hitimisho la mwisho katika kutolea mfano kama endelezo la kila mtu binafsi yake akiwa kama Hekalu la Mungu. Mwanzo wa utangulizi wa mafuatano ya mambo kuanzia Pentekoste unaashiria kuwa mavuno ni jambo linalo endelea hadi kufikia ujio wa pili na Kusanyiko la Milenia. Siku Iliyo kuu ya Mwisho ni kwa mji wa Mungu wakati Ufalme utakapo kabithiwa kwa Mungu rasmi na Kristo na hatimaye Mungu atakuwa ni yote katika yote kama mji wa Mungu.

 

Kwa hiyo basi, chachu katika Pentekoste haipo kwa mfano wa dhambi. Bali inaonyesha mfano wa uondoaji wa dhambi yote katika matokeo ya mwisho ya Yubile ya miaka wakati ambao Mungu kupitia Roho Mtakatifu ameendeleza tabia takatifushi ya haki kwa watoto wote wa Mungu. Kwahiyo wanafanyika kuwa ni waongofu kamili na halisi.

 

Wongofu huu unahusika na uondoaji wa aina yoyote ya mifumo mizima ya matendo ya dhambi kwa kila mmoja binafsi yake kwa kipindi cha kuitwa na kuitikia wito, kuhesabiwa haki na kutukuzwa kama tunavyoona katika Warumi 29:30.

 

Kama tunampenda Kristo, basi tutazishika amri zake (Yoh. 14:15). Sheria zinahusisha na kumpenda Mungu na kumpenda jirani yako. Ikiwa kama hatumpendani sisi kwa sisi ambao tunaonana kwa macho, je, tunawezaje kumpenda Mungu ambaye hatumuoni kwa njia ya tunda la Roho ambalo ni upendo? (Wagalatia 5:22).

 

1Yohana 4:11-13 inasema: Wapenzi, Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu aliyemuona mungu wakati wowote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake.

 

Kumbuka kuwa mtume Yohana kwa uzuri baada ya Krsto na alikuwa amemwona Kristo tena na kukaa kifuani pake, kama tusomavyo Yohana 1:18, inavyosema kuwa hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu wakati wote. Ni kwa kupitia pendo la Mungu tu lililo ndani yetu ndilo lituwezeshalo sisi kuwa wakamilifu. Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili ya kondoo. Hakuwaachilia mbwa mwitu wawashambulie na kuwararua. Lakini zaidi sana, aliyatoa maisha yake kwa ajili yao (Yoh. 10:15, 13:37).

 

Kama nilivyosema hapo kabla na kasha nasema tena: nahesabia kuwa ni jambo la heshima sana kwa mimi kuwa ni mmoja watu.

 

Hakuna mtu aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake (Yoh. 15:13).

 

q