Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[106b]

 

 

 

Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa [106b]

 

(Toleo 2. 1 19950416-20000423)

 

Mfano wenye kuashiria Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa ni utangilizi wa kipindi cha kungojea na kurudi kwa Masihi inayofanyika siku ya Jumapili baada ya ufufko wake jioni ya siku iliyopita, imefafanuliwa katika jarida hili. Muandamano wa matukio kuhusu sadaka na wazo la malimbuko pia yameelezewa humu ndani. Maana ya sadaka au dhabihu zilizokuwa zinatolewa katika Agano la Kale zinazoonyesha kuwa Kristo alizikamilisha kwa kufuka na kwake jioni ile pia vimefafanuliwa.

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Copyright  ã 1995, 1996, 1997, 1999, 2000 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org and http://www.ccg.org

 


Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa [106b]


 

Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa unahitajika utunzwe ili kuwezesha kuelewa maana halisi na timilifu ya sadaka ya Kristo, na uweza ambao alipewa kwa kufufuka kwake kutoka kwa wafu. Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa ni jambo la lazima sana katika utaratibu wa kale wa Israeli kwa mujibu wa sheria za Tora ambayo ni Torati. Kanuni za jinsi ya kuadhimisha inapatikana katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23:9-14 na pia katika kitabu cha kutoka 29:24-25 na kwenye maandiko mengine mengi. Imeeleweka vibaya tu na wanazuoni na kudharauliwa au kukataliwa na wengi (kwa mfano, imeondolewa kuorodheshwa katika jarida la mwana zuoni aitwae Schurer liitwalo Historia ya Wayahudi Wakati na Zama za Yesu Kristo, kwa Kiingereza linaitwa The History of Jewish People in the Age ofJesus Christ). Ni sheria ya lazima kuadhimishwa inayoenda sambamba na Sikukuu ya Pasaka na inaongoza mambo yote mawili yaani majira ya Pentekoste na kuliwa kwa mavuno ya mapya (Walawi 23:9-14). Ili kuiweka katika mtazamo wa kisasa, inatubidi kuangalia ishara ya majira ya kifo cha Kristo.

 

Ishara ya nabii Yona ilipaswa itimilike katika awamu na maeneo yote. Ishara pekee iliyokuwa imetolewa kwa huduma ya Kristo ilikuwa ni kutimia kwa ishara ya Yona. Kristo alisema kuwepo na utimilifu wa kuwemo tumboni mwa nyangumi au samaki mkubwa kwa muda wa siku tatu kamili yaani siku za mchna tatu na za usiku tatu kamili kama alivyo kaa Yona na kuwa ndivyo itakavyofanyika kwake, na alipaswa akae vivyo hivyo kwenye tumbo la ardhi immeze kwa muda wa siku tatu kamili yaani siku za mchana tatu na za usiku tatu (kama kwenye samaki yule mkubwa). Hii ilikuwa ni ishara pekee iliyotolewa kuashiria utumishi au huduma yake. Ishara ya Yona aina lingine zaidi ya kuwa aliishi ndani ya tumbo la yule samaki mkubwa kwa muda wa siku tatu yaani siku tatu mchana na siku tatu usiku. Ishara ya Yona ilikuwa na mahusiano na huduma kwa ajili ya watu wa Ninawi ambako kulikuwa na mahubiri ya siku tatu (au pungufu kidogo ya siku hizo tatu za mahubiri) kwa watu wa Ninawi, na siku 40 za kuitishwa wito wa toba. Wenyeji wa Ninawi walitubu lakini

 

wenyeji wa Yuda hawakutubu. Matokeo yake ni kwamba, Hekalu lote na kila kilichohusiana nacho vilichukuliwa mbali. Huduma ya Yesu Kristo ilibidi itokee katika muda na kwa mwandamano wa matukio sawa na vile ilivyotokea. Hii ilifuatia kuanzia wakati wa Yohana Mbatizaji aliyeimtangulia huduma yake, katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake mfalme Tiberio, ambaye inaaminika kuwa alianza kutawala katika kuanzia Oktoba ya mwaka wa 27BK. Ule Mwaka unaotangulia kwa mujibu wa kalenda hii ya kidunia kwa mwezi wa Oktoba kwa upande wa mashariki (tazama fafanuzi zilizoko kwenye jarida la Majira ya Kusulibiwa na Ufufuko [159]. Huu ndio wakati wa mwanzo kabisa unaoweza kuwekwa kwa kipindi cha mwanzo wa huduma ya Yohana Mbatizaji (tazama jarida lisemalo Kusomwa kwa Sheria Chini ya Ezra na Nehemia [250]. Alianza kwa kuwabatiza Isareli, kwa kulitaka taifa litubu na kumrudia Mungu. Kristo alibatizwa, mwanzoni kabisa mwa mwito wake, inaaminika kuwa ilikuwa ni mwezi wa Februari katika mwaka wa 28BK, kipindi cha wastani wa kama siku 50 hivi kuanzia siku ya Pasaka kwa mujibu wa hesabu za maandiko ya Injili. Baada ya Pasaka ya mwaka 28BK, Yohana mwandishi wa Injili anaonyesha kuwa Kristo na wanafunzi wake walikuwa pia wanawabatiza watu wengine maeneo ya mbali na Yerusalemu, na Yohana Mbatizaji na wanafunzi wake walikuwa pia wanabatiza watu huko Ainoni karibu na Salimu (Yoh. 4:17). Tunaona kuwa Kristo hakuanza kutoa huduma yake hadi pale Yohana Mbatizaji alipotiwa gerezani (Mat. 4:17). Kwa hiyo, Kristo alianza kutoa huduma wakati mwingine baada ya Pasaka ya mwaka 28BK mapema kabisa. Katika Injili hizi Zinazofanana hazielezei kiuwazi sana ni kwa kipindi gani huduma ya Kristo ilidumu, lakini Yohana katika Injili yake anaandika kwa uwazi sana anaelezea na pia anaelezea kuhusu Pasaka tatu. Katika mwaka wa kusulibiwa kwa Kristo wa 31BK, tunajua kuwa kulitakiwa kuwe na Pasaka nne, kwa miaka ya 28, 29, 30 na 31BK Maelezo ya Sabato za pamoja katika Luka 6:1 yamechukuliwa kutoka kwenye Pasaka nyingine ambazo zinaonekana kuto kuwa hivyo (tazama jarida la Majira ya Kusulibiwa na Ufufuko [159]. Kutokana na uandishi wa Yohana, ambaye amezitaja Pasaka tatu tu, mwaka wa kusulibiwa ungekuwa ni wa 30BK ambao unatoa idadi ya Pasaka na kipindi ambacho huduma yake ilidumu. Huduma yake isingeweza kuanza mapema sana kuliko wakati wa Pasaka ya mwaka 28BK, unaotoa sura ya wakati ambao Yohana Mbatizaji alitoa huduma, akianzia katika mwaka wa kumi na nne wa kutawala kwake Kaisari Tiberio. Isingewezekana kabisa kuwa kabla ya Oktoba 27BK. Ishara ya mwanzo wa huduma ya Yohana Mbatizaji katika Oktoba 27BK katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwa Kaisari Tiberio ambao pia ulikuwa ni mwaka wa Yubile, na ni mwaka wa kupigwa kwa baragumu za kutangaza Yubile iliyofanyika Oktoba ya mwaka wa 27BK. Yubile ile ilikuwa ya kutangaza ukombozi wa Israeli kupitia Masihi.

 

Masihi, kama ulivyo mfano wa Agano la Kale wa wito wa marejezo wa Yona, kwa mwanzo wa mahubiri ya wito wa marejezo ya Israeli na baadae mbiu ya Yubile. Matengenezo ya Yona yalifanyika katika mwaka wa kwanza, mwaka wa kurudi kwao, baada ya Yubile.

 

Dhana yenye kufikirika ya kuwa huenda Kristo alibatizwa yapata mwezi wa Februari, inatokana na ujenzi mpya ulioko katika siku 50 zilizochukuliwa kuwa ni maalumu yaani zisizo za kawaiada kuanzia Pasaka, kwa mujibu wa maandiko matakatifu. Inawezekana kabisa kuwa Kristo huenda alibatizwa siku za nyuma mapema kidogo kabla ya wakati huu, na inawezekana kuwa hivyo zaidi hasa kama itachukuliwa kuwa hasabu hizi zimechukuliwa kwa mujibu wa utaratibu wa Mishna (unaopatikana kupitia kwa majumlisho ya kale ya Wayahudi waliochukulia kuwa Mishna ilikuwa wakati wa Kristo) mwaka wa Wafalme uliohesabiwa kuanzia siku ya 1 Nisani. Kwa hiyo, mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Tiberio, kwa mujibu wa Wayahudi, ulichukua mahala pake kuanza tangia siku ya 1 Nisani. Kwa hiyo ilitoa nafasi kwa Yohana Mbatizaji kuanza huduma yake kuanzia mapema kidogo kuliko wakati ule na pengine kwa Kristo angeweza kutaingaza Yubile katika Oktoba kwa kupiga baragumu la mbiu ya Upatanisho.

 

Ni mwandamano wa matukio hivyo hivyo kama ilivyotokea kwa Kristo, na hatimaye kwa Yubile ya pili ya mlolongo wa mwisho. Huduma ya Kristo ilikuwa nyuma kwa miaka mitatu, ikitimilizia katika Pasaka ya mwaka 30BK (au 31BK kutegemeana na makosa ya baadhi ya wahesabuji), iliyo anzia siku ya Jumatano. Pasaka ya Kibiblia ya siku ya 14 Nisani iliangukia siku ya Jumatano ya mwaka wa 30BK, ili kufanya kwamba siku hizi tatu yaani siku za mchana tatu na za usiku tatu ziweze kutimilika, na kumfanya Kristo atimize unabii wa kuwa ndani ya tumbo la kaburi kwa siku za mchana tatu na za usiku. Alifufuka kutoka kaburini siku ya Jumamosi jioni wakati wa jua kuchwa, na aliutumia muda wote wa usiku akiwa ndani kaburini au karibu yake akingojea tukio hili la pili lililo muhimu mno la mfano.

 

Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa unaonekana kuwa ulikuwa unatikiswa majira ya saa 3 kamili ya asubuhi siku ya Jumapili asubuhi wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Sadaka ya jumla ya kutikiswa ilikuwa inaletwa na wale wanaokuja kufanya ibada na ilifanyika kwa kushirikiana na makuhani (Kut. 29:24-25). Tunajua kwamba Wasamaria na Masadukayo waliitunza Jumapili ya Mganda wa Kutikiswa na Jumapili ya Pentekoste. Hili ni jambo muhimu katika historia. Wayahudi hawaadhimishi ibada ya Mganda wa Kutikiswa kwa sababu wanautunza mwezi wa Sivani siku ya 6 kuwa ni Pentekoste, ambayo ilikuja kwa kufuata mapokeo ya Mafarisayo kwa mujibu wa kanuni za baraza la marabi wa dini ya Kiyahudi, baada ya kuhusuriwa kwa Hekalu. Tunajua kwamba Wasamaria huitunza siku ya 14 na 15 na wazo la Mganda wa Kutikiswa na kuhesabiwa kwa homeri kutoka Jumapili wakati wa Sikukuu. Kwa hiyo muundo wa kipindi cha Hekalu na haki yake moja kwa moja, ikijumlisha Wasamaria, kila mara waliitunza Pentekoste siku ya Jumapili.

 

Ni Wayahudi tu ndio waliitunza katika mwezi wa siku ya 6 ya mwezi wa Sivani na ni baada tu ya kuhusuriwa kwa Hekalu.

 

Wazayuni walioko sasa wa mfumo wa kimamboleo hawafanyi hivyo. Kwa hiyo, Pentekoste ilikuwa inahesabiwa kuanzia siku hii. Nafasi ya hawa (wenye imani ya Masadukayo) walishikilia hivyo hadi kuhusuriwa kwa Hekalu yapata mwaka 70BK (tazama jarida la F.F. Bruce, art. Calendar, katika Kmusi iitwayo Illustrated Bible Dictionary, ed. by J.D. Douglas and N. Hillyer, VIP. 1980, vol. 1, p. 225). Baada ya utawanyiko, nafasi ya hashima ya Kifarisayo ilikulika kimatendo na tofauti inakisiwa katika Mishna (Hag. 2:4). Baada ya utawanyiko, Mganda wa kutikiswa ulijulikana kuwa unatikiswa katika Siku Takatifu ya kwanza ya mikate Isiyotiwa Chachu, na kisha Pentekoste iliamuliwa kwa kuangukia katika siku kamilifu, ijulikanayo kama siku ya 6 ya mwezi wa Sivani. Tendo hili lilikuwa halifuatwi katika siku za ukuhani wa Hekaluni na hata siku za baadae hadi mwaka wa 70BK na, hata, wakati wa Kristo.

 

Pengine ni muhimu tujue kuwa neno Shibboleth lililoko katika lugha ya Kiebrania lina maana zote mbili yaani kijito kinacho tiririka (kama ilivyo katika Isa. 27:12; Zab. 69:2,15) na pia suke la nafaka (Mwa. 41:5-7, 22-24, 26; Rut. 2:2; Ayu. 24:24; Isa. 17:5) au kichala cha ukuti (Zek. 4:12). Huenda Mataifa Wasio Waisraeli walikuwa wanatamka neon hili Thibboleth (au pengine kwa kwa sauti ya kugugumia yenye tamko ‘sh’, tazama Biblia ya ISBE, art. Shibboleth, Vol. 4, p. 478). Kristo alichukua kote kuwili, yaani kijito kinachotiririka na wa kwanza au limbuko la mavuno ya nafaka. Neno lililotumika katika Walawi 23 ni hata hivyo limetuama katika omeri lenye maana ya lundo dogo (la nafaka iliyopunguzwa).

 

Tunaweza kupata majira ya Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa kutoka katika Mambo ya Walawi 23.

 

Walawi 23:9-14 inasema: 9 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia. 10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuma mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; 11 naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. 12 Na siku hiyo mtakaoutikisa mganda, mtamsongeza mwana kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. 13 Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini. 14 Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machnga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote.

 

Hii ni hatua ya mfano. Ni kutokana na sadaka hii ilikuwa inaashiria kuwa mavuno mapya yanaliwa kama mkate na kama nafaka katika sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kuanzia wakati wa sadaka za asubuhi (inakadiriwa kuwa kama saa 3 asubuhi) ya Jumapili ya Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa, mkate unaruhusiwa kuliwa, au kuokwa (kama kuokwa), mahindi au masuke ya kijani ya mahindi iliyotengenezwa kwa mazao mapya. Kwa maneno mengine, kuanzia Pasaka mkate usiotiwa chachu unaliwa pamoja na Pasaka. Ilikuwa ni budi ifikirike kuwa hakuna aina yoyote ya mkate, wala mkate usiotiwa chachu wowote kuliwa kuanzia siku ya 15 mwezi wa Nisani na kuendelea kwa mujibu wa maandiko haya matakatifu. Mafafanuzi ya marabi walielewa kuwa ni mkate unao tokana na mavuno mapya (kwa mujibu wa Abrahamu Ibin Ezra Soncino). Mafafanizi haya yabatosheleza dhana ya kusema kwamba mkate wa Jangwani uitwao mana ulikoma baada ya Pasaka ya Kanaani wakati mazao ya nchi mpya yalipokuwa yanaliwa (Yos. 5:12). Ni dhahiri kuwa ilikuwa ni nafaka za zamani zilizokuwa zinaliwa siku ya pili yake baada ya Pasaka katika nchi mpya ya Kanaani (Yos. 5:11). Kwa hiyo, utofautisho kati ya nafaka mpya na za zamani zilizofanywa na ibin Ezra ziko sahihi kabisa. Nafaka mpya na za mazao haviwezi kuliwa hadi Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa imefanyika kufuatana na Sabato. Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa hufanyika baada ya Sabato ya wiki (au huitwa Shabbat) na sio ile Shabbatown ya Siku Takatifu. Utaratibu wa kuhesabu majuma kwa Sabato saba kamili za majuma, inawezesha kufanyika kwa sadaka, na kufikia kwenye Sikukuu ya Pentekoste, kuwa katika siku nyingine yoyote mbali na siky ya kwanza ya juma, au Jumapili, kwa siku zote mbili yaani siku ya Pasaka na Pentekoste.

 

Sadaka ya kondoo mume na utikisaji wa malimbuko humuashiria Kristo aliye limbuko la kwanza aliyepaa mbinguni kwa Baba yake. Linganisha na kifungu cha maandiko matakatifu kinacho muongelea Maria Magdalena. Katika Injili ya Yohana 20:1, 14-18, tunakuta kwamba Kristo alikuwa amengojelea katika usiku ule. Alikuwa ameisha kufufuka na alikuwa anangojea kupaa kwenda kwa Baba, jambo ambalo lilitimilika kufanyika siku ya jumapili asubuhi baada ya yote. Ufufuko wake ulifanyika siku ya Jumamosi usiku, na Kristo akasubiri hadi jumapili asubuhi kuwa tayari kupaa kwenda mbinguni.

 

Yohana 20:1 inasema: Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalena alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.

 

Kwa hiyo, katika saa ya mapema sana asubuhi, wakati kukiwa giza bado, kwa maana ya kuwa kabla ya nuru ya kwanza ya siku ya jumapili asubuhi Maria Magdalena alikuja kaburini na akamkuta Kristo ameisha kufufuka tayari. Maelezo hayohayo ya namna moja yanapatikana katika injili ya Luka.

 

Luka 24:1 inasema: Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, Walienda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoyaweka tayari.

 

Neno litumikalo hapa linamaana ya kwenda chini kwa kima cha chini sana (kwa Kiyunani husemwa orthros bathus). Neno hili lisemalo siku ya kwanza ni mojawapo ya juma ambayo ni kutoka machweo ya Jua ya Jumamosi hadi machweo ya Jua ya Jumapili. Injili ya Marko 16:2 inaonyesha kuwa ilikuwa ni mara tu wakati wa maawio ya jua. Yesu alikuwa ameisha fufuka tayari. Kwa hiyo, ufufuko huu ulichukua pahala pake siku ya jumamosi jioni, ikitolewa mwelekeo wa muda na maongozi ya siku za Pasaka katika mwaka wa 30BK.

 

Yohana 20:15-17 inasema: 15 Yesu akamwambia, mama, unalilia nini? Unamlilia nani? Naye huku akidhani ya kuwa ni mtunza bustani, aka mwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. 16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu). 17 Yesu akamwambia, Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Nimepaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yeau, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

 

Sababu hapa ni kwamba alikuwa anangojea kupaa. Asingependa kutiwa unajisi kwa kuguswa na mtu yeyote mwenye mwili. Alikuwa anangojea ili aweze kutimiliza dhabihu hii. Alikuwa anakwenda kutikiswa kama limbuko, ilikwamba hatimaye achukue pahala pake kule mbinguni akiwa kama kuhani wetu mkuu. Ilikufanya hilo, tunajua usemavyo Waraka kwa Waebrania, kuwa alipaswa achukue dhabihu ya damu na kuingia Patakatifu pa Patakatifu. Dhabihu ile ya damu ilikuwa ni yeye mwenyewe, na aliletwa hapa kwa kusudi hilo tu.

 

Ashirio hili linamaanisha kuwa Mungu alihitaji kiongozi wa watu wake ambaye alikuwa tayari kujitoa dhabihu kwa manufaa ya watu wake. Shetani hakuwa tayari kufanya hilo. Shetani alikuwa na mwelekeo tofauti na mawazo tofauti, ambayo ilikuwa sio njia ya Mungu. Mwelekeo wa Shetani ulikuwa ni wa kujitanguliza yeye mwenyewe kwanza; na mwingine awayeyote atakuwa wa pili. Mungu alinuia kutuonyesha sisi kwa njia ya mfano wa kujitoa sadaka, kwa namna ya kujitoa wewe mwenyewe kwa ajili ya maisha ya ndugu zako, ili iwe ni mfano wa kuufuata sisi sote. Aliye wa kwanza wetu, kiongozi wetu, alipaswa atuonyeshe sisi mambo yatupasayo. Halikuwa ni jambo la bahati nasibu au ajali kuona kuwa wanafunzi wote wa Yesu isipokuwa mtume Yohana walikufa vifo vya mateso yaani walifia imani. Haikuwa ni jambo la kama ajali au nasibu. Walionyesha, kwa namna ile ile moja kwamba Bwana wao alivyo onyesha, upendo wao kwa wote miongoni mwa wapendwa ndugu zao katika kujaribu kuwashinda washitaki wao na nguvu za ulimwengu huu, na kutuonyesha sisi sote ni kwa jinsi gani tunapaswa kuonyesha mfano katika ulimwengu huu. Ule ulikuwa mfano wenye nguvu sana. Nguvu kuu za kweli juu ya hili ni kujua kuwa Mungu anao mpango unao wajumuisha wote wenye mwili. Sio tu kwa ajili ya ilimwengu wa kiroho unaoshughulikiwa kwayo. Ni ulimwengu wa kimwili, na ulimwemgu wa kiroho ulioasi dhidi ya mpango wa uumbaji na kufanya idadi kubwa ya makosa na idadi ya matatizo katika uumbaji, ambayo inahitajika dhabihu ya Kristo na vita. Tendo lote zima la Mganda wa Kutikiswa limeunganishwa kwa pamoja na hizo dhabihu. Kristo alitimiliza katika dhabihu hii idadi ya dhabihu nyingine pia, zote zilizo fungamanishwa na Mganda wa Kutikiswa (tazama jarida la Naona Kiu [102]).

 

Tutaona katika baadhi ya dhabihu na kuona baadhi ya mifano yake. Ni mambo yaliyo katika kina sana kushughulika na mawazo ya sadaka za dhabihu katika jarida hili. Mlolongo wa Usomaji wa Sheria unaonyesha ufafanuzi wa dhabihu na jinsi walivyokuwa inafidiwa. Maelezo mafupi ya baadhi ya dhabihu tutayaona pale.

 

Kama tulivyokwishaona, Kristo alipaswa aweze kufufuka kabla ya asubuhi ya siku ya kwanza ya juma kufuatia Sabato ya wiki kwa sababu alikuwa ni Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa ambaye ni limbuko la mavuno yote kama inavyosema Kutoka 29:24-27.

 

Kutoka 29:24-27 inasema: 24nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisa view sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA. 25Kisha uvitwae vile vitu mikononi mwao na kuviteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa, view harufu nzuri mbele ya BWANA; ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. 26Kisha twaa kidari cha huyo kondoo wa kuwekwa kwake Haruni kwa kazi takatifu, na kukitikisa-tikisa kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; nacho kitakuwa ni sehemu yako. 27Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa na lililoinuliwa juu vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Haruni, na huyo aliyekuwa kwa ajili ya wanawe

 

Sadaka hizi kwa hapa ni kwa ajili ya uwekaji wa wakfu wa Manukato ya kikuhani. Kristo alikuwa ni kuani mkuu mpya mfano wa Melikizedeki. Kutoka 29:29-30 inaonyesha kuwa Mganda wa Kutikiswa wa kwanza ulikuwa ni kwa ajili ya kumtakasa kwa kumweka wakfu kuhani na kazi yake kati Wana wa Israeli kwa Sadaka zao za Amani. Uwekaji huu wa wakfu ulikuwa wa mavazi yakuhani kwa mujibu wa Kutoka 29:29-30 ili kwamba waweze kutumika katika Mahali Patakatifu. Kwa hiyo, Kristo aliyaweka wakfu mavazi ya wateule kwa Sadaka ya Kutikiswa ili kwamba waweze kuwekwa wakfu kama makuhani na wavalishwe na kufaa kupaendea au kuingia kwenye madhabahu takatifu sana. Kuvalisha kwa kuhani wa mwisho na wateule kumeelezewa katika kitabu cha nabii Ezekieli 44:17-17 sawa na Zekaria 3:5; Mathayo 22:11-12; Ufunuo 3:4, 18; 6:11; 7:9, 13; 16:15.

 

Mambo ya Walawi 7 kuanzia aya ya 1 inaelezea juu ya dhabihu ya Sadaka kwa ajili ya Makosa yaliyovuka kiwango cha kawaida maarufu kama dhambi ya hatia. Dhabihu kwa ajili ya Dhambi zilizozidi viwango vywa kawaida ni sadaka kwa makuhani.

 

Mambo ya Walawi 7:5-7 inasema: 5 na kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kwa BWANA kwa njia ya moto; ni sadaka ya hatia. 6 Kila mtu mume miongoni mwa makuhani atakula katika sadaka hiyo; italiwa katika mahali patakatifu; ni takatifu sana. 7 Kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo, na sadaka ya hatia ni vivyo; sheria yake ni moja; huyo kuhani afanye upatanisho kwayo, ndiye atakaye kuwa nayo.

 

Sadaka hii ya Mwenye kufanya Uovu Mkuu au dhambi ya hatia, pia ilitimilizwa katika Kristo, ili kwamba kila mwanamume, kila kazi ya kikuhani, kabila lote la Lawi, kila kuhani, alitakiwa awekwe wakfu kwa Bwana. Kristo amewatakasa na kuwaweka wakfu kila aliye mteule; kila mmoja aliyechaguliwa na kuletwa kwenye imani, akiwa kama kuhani. Wanaume wote wa Israeli walikuwa wote wamewekwa wakfu kwa ajili ya dhabihu ya Pasaka ambayo ilikuwa ni ya jumla. Kulikuwa na mwana kondoo wa Pasaka mmoja tu aliyetolewa na kuwakilishwa mbele ya kuhani mkuu katika Yerusalemu. Utakaso wa jumla wa mwili wa taifa kama makuhani ulikuwa ni ishara kwa siku za mbele kupanuliwa kwa huduma ya kikuhani hadi kwa wateule Kanisani kuanzia dhabihu ya Pasaka na kuanzishwa kwa Kanisa siku ya Pentekoste kukitiliwa maanani kutoka Mganda wa kutikiswa. Dhabihu na sadaka zote zilikuwa ni ishara tu ya mambo halisi yajayo.

 

Sadaka za daima haikuwa ni sadaka ya makuhani katika ujumla wake. Migawanyo iliyokuwapo kwa makuhani na kazi zao zilikuwa pia za namna hiyo hiyo katika makabila, ili kwamba taifa iligawanywa na kila milki ilipeleka wawakilishi wake Yerusalamu ili kutoa dhabihu. Wakati inapokuwa kwamba mgawanyo wa milki Fulani ipokuwa kwenye zamu yalikuwepo maombi na utaratibu wa kutoa dhabihu kulingana na migawanyo yao na maeneo ili kwamba utaratibu mzima wa utoaji uwe ni sehemu ya maisha yao Israeli na uweze kuendelea bila kukoma watu wa pande zote wakiwajibika na kuwekewa utaratibu katika maombi na katika kutoa dhabihu. Kila mmoja kwa nafsi yake katika Israeli alijisikia kuwajibika kufanya kazi hata za dharura kwa kufuata migawanyo yao ya kazi za kikuhani. Hii ilikuwa ni kioo cha ubebaji wa majukumu ya makabila. Kwa hiyo basi makuhani hawakufanya shughuli zao kama ni kiungo kilichojitenga kwa taifa. Hii ndiyo maana Kanisa la Mungu haliwezi kuachanishwa na taifa.

 

Tumewekwa wakfu na Kristo kama Sadaka ya Ondoleo la Dhambi zilizozidi mpaka wa kawaida au pia ziliitwa dhambi za hatia kwa mujibu wa aya ya 11, hadi kufikia chini ya sura ya 20, 25, hadi kwenye Maziwa na Sadaka ya Kuiniliwa. Sadaka hizi, yaani Sadaka za Amani, vile vile Kristo alizitimiza ili kwamba sisi tuwe na amani, na ili kwamba yeye afikie malengo ya kutimiza unabii uliotolewa na nabii Isaya, kama alivyo muita kuwa ni Mfalme wa Amani. Alifanyika kuwa ni Sadaka ya Amani. Alijitoa mwenyewe kwa ajili ya amani, na alifanya zaidi ya dhabihu ya Sadaka ya Amani. Wakati unaposema kuwa Kristo alitimiliza aina zote za dhabihu, hakuzitimiza tu kwa ajili ya kuwepo kwake. Bali sadaka yake ilitimiliza matakwa ya dhabihu, ambazo zilikuwa zielekeze katika maisha yake.

 

Dhabihu zenyewe ni somo kamili linalotimiliza milolongo ya Sheria (soma jarida la Sheria za  Mungu [L1] na [252-263]). Ili kuonyesha yale mambo ambayo kwa kweli Kristo aliyatimiliza kwa kifo chake. Tunahitaji kupitia na kupima kila kipande au kipengele cha sheria. Kuzijua dhabihu ni sawa na kuelewa kitu cha msingi katika asili ya Kristo ilivyotimiliza kila asilia ya kitu kimoja kimoja, na kutupatanisha sisi na Mungu. Ndani na kwa kupitia dhabihu hizo sisi tumepatanishwa na Mungu.

 

Mambo ya Walawi 7:29-31 inasema: 29 Nena na wana wa Israeli uwaambie, Yeye asongezaye dhabihu yake ya sadaka za amani kwa BWANA, atamletea BWANA matoleo yake, kutoka katika ile dhabihu ya sadaka zake za amani, 30 mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kuteketezwa kwa moto, mafuta yake pamoja na kidari atayaleta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA. 31 Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu lakini hicho kidari kitakuwa cha Haruni na wanawe.

 

Tendo la kuwaweka wakfu kwa huduma ya kikuhani kwa njia ya sadaka za Wana wa Israeli kwa mara ya kwanza inaonekana katika kitabu cha Kutoka 29 inavyoendelezwa. Kuwekwa wakfu na hisia za makuhani zimeendelezwa kwa dhabihu zilizokuwa zikitolewa zikiitwa kama Sadaka za Amani na kwa hiyo zinamtolea mfano Masihi.

 

Mambo ya Walawi 7:32-34 inasema: 32 Mguu wa nyuma wa upande wa kuume mtampa kuhani kuwa sadaka ya kuinuliwa kutoka katika hizo sadaka zenu za amani. 33 Katika wana wa Haruni, huyo atakayesongeza damu ya sadaka za amani, na mafuta yake yeye, atapata mguu wa nyuma wa upande wa kuume kuwa sehemu yake. 34 Kwa maana, hicho kidari cha kutikiswa, na huo mguu wa kuinuliwa, nimevitwaa kwa wana wa Israeli, katika dhabihu zao za sadaka za amani, nami nimempa Haruni kuhani na wanawe, kuwa haki yao ya milele kutoka kwa wana wa Israeli.

 

Masihi alieleweka kuwa alikuwa Masihi wa Haruni wakati alipokuja kwa mara ya kwanza. Alikuwa ni Masihi kuhani. Kwa mujibu wa gombo lililopatikana katika Bahari ya Chumvi linathibitishwa kuwa mtazamo wa Masihi ulikuwa ni kwamba alikuwa awe na vipindi viwili vya kujilia kwake (tazama jarida la mwana zuoni aitwaye G. Vermes lisemalo Gombo za kutoka Bahari ya Chumvi toleo la Kiingereza au Dead Sea Scrolls in English, re Damascus Rule VII and fragment from the Cave IV).

 

Mambo ya Walawi 8:27-29 inasema: 27 kisha akaweka vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe, na kuvitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA. 28 Kisha Musa akavitwaa tena mikononi mwao, nakuviteketeza juu ya madhabahu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa vilikuwa vya kuwaweka wakfu, na harufu nzuri; ilikuwa dhabihu iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto. 29 Kisha Musa akakitwaa kile kidari, akakitikisa huku na huku kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; ni sehemu ya Musa katika kondoo mume wa kuwekewa wakfu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.

 

Tunazungumzia kuhusu mwandamano wa matukio ya sadaka. Huu ni mtazmo wa Sadaka ya Kutikiswa, unaowaweka wakfu makuhani na manabii.

 

Mambo ya Walawi 9:21 inasema: 21 na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kuume, Haruni atavitikisa huku na huku view sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA, kama Musa alivyo agiza.

 

Hii inaonyesha mwendelezo wa utaratibu wa kupatanisha wa makuhani.

 

Mambo ya Walawi 10:14-15 inasema: 14 Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe, kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wana wa Israeli. 15 Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha kutikiswa, Watavileta pamoja na dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto za hayo mafuta ili kuvitikisa view sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kisha vitakuwa ni vyako wewe, na vya wanao pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama BWANA alivyo agiza.

 

Nje ya utaratibu wa Sadaka ya Kutikiswa, makuhani walipewa kazi, ambayo ilikuwa ni sehemu katika Sadaka ya Kutikiswa. Sehemu ile sasa inaenea kwa wateule, na inaonyesha upatanisho wetu na Kristo, kama ni sehemu ya Sadaka ya Kutikiswa.

Mambo ya Walawi 14:12-20 inasema: 12 kisha kuhani atamshika mmoja katika hao wana kondoo waume, na kumsongeza awe sadaka ya hatia, pamoja na hiyo logi ya mafuta, kisha atavitikisa kuwa ni sadaka ya kutikiswa nbele za BWANA; 13 kisha atamchinja huyo mwana kondoo mahali hapo wachinjapo sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, ndani ya mahali patakatifu; kwa kuwa hiyo sadaka ya dhambi ilivyo ya kuhani, na vivyo sadaka ya hatia, ni takatifu sana, 14 kisha huyo kuhani atatwaa katika hiyo damu ya sadaka ya hatia, naye kuhani ataitia katika ncha ya sikio la kuume la huyo atakayetakaswa, na katika chanda cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole kikuu cha mkono wake wa kuume; 15 kisha kuhani atatwaa katika hiyo logi ya mafuta, na kuyamimina katika kitanga cha mkono wake mwenyewe wa kushoto, 16 kisha kuhani atatia kidole cha mkono wa kuume katika hayo mafuta, yaliyo katika mkono wake wa kushoto, naye atayanyunyiza hayo mafuta kwa kidole chake mara saba mbele za BWANA; 17 na katika yale mafuta yaliyobaki mkononi mwake kuhani aliyetia ncha ya sikio la kuume la huyo atakayetakaswa, na katika chanda cha gumba la mkono wa kuume, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kuume, juu ya damu ya sadaka ya hatia; 18 na mafuta yaliyobaki, yaliyobaki, yaliyo katika mkono wa kuhani, atayatia juu ya kichwa cha yeye atakayetakaswa; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, mbele za BWANA. 19 Kisha kuhani atasongeza sadaka ya dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili yake atakayetakaswa kwa sababu ya unajisi wake; kisha baadaye ataichinja sadaka ya kuteketezwa; 20 kisha kuhani ataisongeza hiyo sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, juu ya madhabahu na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.

 

Kifungu hiki cha maandiko matakatifu kinasema kwaa kwenye kokwa ya kwamba dhabihu ya Yesu Kristo ilikuwa na maana gani. Sadaka zilitolewa ili kusafisha, kwa damu, kila mmoja mmoja katika Israeli na lilikuwa ni jukumu la kuhani kupitia dhabihu kumsafisha kila mmoja. Kristo alitimiliza dhabihu hii kwa njia ya damu yake mwenyewe (na damu ni uhai wa mwili) na imetusafisha sisi mara moja tu na kwa siku zote. Damu ya Kristo ilikuwa ni iliashiria mfano wa suke la ngano katikati ya kundi la miiba na kwa kidole gumba chake na vidole vingine kwenye misumari msalabani. Kutoka katika hatua hii wateule walipewa uweza wa kufanyika kama makuhani wa kuombea msamaa wa dhambi Israeli. Tunaposema kuwa Kristo anatutolea dhabihu ya kutuombea msamaha wa dhambi sisi, huu ni utaratibu na utimilifu wa dhabihu na mfumo ambao alitufanyia upatanisho kwao.

 

Mambo ya Walawi 14:21-24 inasema: 21 Tena kwamba ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana kondoo mmoja wa kiume, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, na kufanya upatanisho kwa ajili yake, na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba ulio changanywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta; 22 na hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kama awezavyo kuwapata; huyo mmoja atakuwa sadaka ya dhambi na wa pili atakuwa sadaka ya kuteketezwa. 23 Hata siku ya nane atawaleta kwa kuhani, mlangoni pa hema ya kukutania mbele za BWANA, kwa ajili ya kutakaswa kwake. 24 Na kuhani atamtwaa huyo mwana kondoo, wa sadaka ya hatia, na hiyo logi ya mafuta, naye kuhani atayatikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.

 

Sisi sote hatuwezi kulipa gharama. Hapa kuna matoleo kwa masikini ambao hawataweza kumudu kutoa zile dhabihu. Hakuna hata mmoja kati yetu angaliyeweza kulipa dhabihu hizi, kwa hiyo Kristo alitulipia. Hivyo basi Kristo alijitoa mwenyewe kuwa ile dhabihu iliyokuwa inahitajika hapa katika Walawi 14:21. alifanyika kuwa huyu Mwana Kondoo ka kutusafisha sisis bila kujali kama tu matajiri au masikini, kwa sababu hakuna hata mmoja angaliyeweza kumudu dhabihu ya msamaha wa dhambi. Hii ndiyo maana ya kuwa makusanyo ya matoleo yanayofanywa sio sadaka rasmi. Hii ni kodi. Ni kosa kuchngiza matoleo ya sadaka katika Siku ya Upatanisho. Hakuna mtu atakaye ingia kwenye Hekalu la Mungu au katika Hema ya Kukutania, atakayetoa zaidi au pungufu kuliko mtu mwingine yeyote katika Siku ya Upatanisho. Ni matukano au kufuru kwa Mungu, na ni dhahiri jambo lililo dhahiri kabisa kuwa kufanya hivyo ni kinyume kabisa na Sheria ya Torati. Tumekuwa tukizivunja sheria hii mara nyingi sana katika siku za nyuma kwa kuifanya hii kuwa kama ni sadaka ya kawaida na kumtolea Mungu. Imekatazwa kabisa. Kristo alilipa kodi ile kwa ajili yetu na Kristo akiwa kama Masihi ataanzisha tena mfumo ule. Sisi binafsi yetu hatuwezi kulipa kodi ya msamaha wa dhambi. Hivyo basi Kristo alitulipia, na alikamilisha kodi ile kwetu.

 

Mambo ya Walawi 23:11-14 inasema: 11 naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. 12 Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. 13 Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara inayosongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa ni harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini. 14 Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote.

 

Sadaka ya Kutikiswa

Mganda wa Kutikiswa ulikuwa Masuke la kijani la shayiri iliyokuwa inatolewa na Israeli. Neno lililotumiwa kuuita mwezi wa Abibu lina maana ya masuke ya kijani. Ilikuwa inatolewa kwa Yerusalemu, lakini walikuwa hawakusanyiki moja kwa moja kutoka Yerusalemu. Mavuno ya shayiri ilikuwa inaletwa kwa kipindi chapata kama majuma matatu mapema kwa upande wa kusini, ukanda wa uwanda wa pwani na kwenye upande wa uwanda wa Yordani. Mavuno ya jumla pia huonekana meupe katika mavuno na yameiva kikamilifu. Hii ni tofauti na Mganda wa Kutikiswa. Zaidi ya yote, Mganda wa Kutikiswa pia uliwakilisha na dhabihu Mahali pengine. Pasaka ilitunzwa katika Misri wakati wa zama za Hekalu kwa mahali Pakuu au kwa Kiingereza Elephantine kuanzia kipindi cha Hekalu na hadi wakati wa kuhusuriwa kwake yapata kama mwaka 410KK kwa mujibu wa mwana zuoni aitwaye Vidaranag Mmisri aliyekuwa anaishi ngomeni huko Knub. Hekalu hili kutolea dhabihu kwa kipindi chote ambacho Hekalu la Yerusalemu lilihusuriwa na katika maanguko. Hekalu lilijengwa upya katika Misri na Kuhani Mkuu Onias IV katika mwaliko wa mfalme Ptolemi Philometa tangia yapata mwaka 160KK na iliendelea mbele hadi kufungwa kwake kwa amri ya Kaisari Verspasian katika mwaka 71BK. Hekalu hili lilikuwa huko Leontopoli kwa jina heliopoli au Jiji la jua kama ilivyokuwa imetabiriwa na Mungu kupitia nabii Isaya (Isa. 19:19, tazama Biblia ya RSV). Ilikuwa hapa nuru ilikuwa katika Goshen kipindi cha ule Msafara halisi wa kutoka utumwani na ilikuwa kwa hapa Yusufu alimchukua Masihi akiwa mtoto ili kwamba matabiri ya unabii katika Isaya na Hosea utimie. Miji mitano iliyotajwa katika gombo la nabii Isaya 19:18 inawezekana huenda ilikuwa ni Leontopoli na Heliopoli (waliihesabia kama ni miji miji iliyotengwa mbali), Dalfne, Migdoli na Memfili (tazama Biblia iitwayo Companion Bible, n. to v. 18). Isaya 19:18 inasema kuwa moja kati ya miji hii itaitwa ni miji ya haki au ha-zedek ambayo imewekwa kisomi katika LXX. Hii ni kwa sababu Kristo alilazimika kwenda kule na kutokea pale aliitwa kwa Israeli. Kwa hiyo kama ilikuwa sio kuchanganya hili katika Yerusalemu lililozaa jina hili pia (Isa.1:26), ilibadilishwa kusoma cheres ambayo kwa Kikaldayo lina maana ya jua na kwa Kiyunani inaitwa heliopoli. Kwa mujibu wa Biblia, tafsiri ya Mfalme Yakobo iitwayo KJV, imeita kama Mji wa Maangamizo ambavyo sio sahihi (Mji wa Maangamizo kama inavyosema KJV inasomeka kuwa Jiji la jua katika Biblia ya Kiingereza ya RSV). Mfumo huu wa dhabihu wa Misri ni waukivuli au wa kimfano. Mji ilikuwa ni wenye haki kwasababu na nyumba ya Masihi. Dhabihu ya Masihi ilikuwa imeenea hadi kwa Wamisri na halafu, wokovu ulikuwa wa watu wa Mataifa. Mtazamo mzima wa Mganda wa Kutikiswa haueleweki. Mganda wa Kutikiswa ulikuwa ni wa kwanza katika mavuno ya Israeli wote hata miongoni mwa watu wa Mataifa. Kwa hiyo ilikuwa haileti maana kuuhusisha Yerusalemu. Tamaa ya kuuhusisha mji wa Yerusalemu inatokana na hali ya kugeuzwa kwa sheria za zaka na mfumo ulioanzilishwa wakati wa kipindi cha baadae cha Hekalu la pili, ambalo lilijaribu kuweka pamoja zaka zote kwenda Yerusalemu.

 

Matendo ya mapotofu pia yaliakutikana katika karne ya ishirini baadae miongoni Makanisa ya Mungu katika Amerika. Hakuna msingi wa kibiblia kthibitisha madai haya (tazama jarida la Utoaji wa Zaka [161].

 

Sadaka hii ya Kutikiswa inaanzia hesabu kuelekea siku ya Pentekoste. Ni kutoka katika siku hii ndipo unaanza kujihesabia.

 

Mambo ya Walawi 23:15-17 inasema: 15 Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mlioweka mganda wa sadaka ya kutikiswa, zitatimia Sabato saba, 16 hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini, nanyi mtamsongezea BWANA sadaka ya unga mpya. 17 Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu ya kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu iwe malimbuko kwa BWANA.

 

Mikate hii miwili ni yenye chachu ndani. Chachu maranyingi sana kwa makosa kabisa imeonekana kama ni mfano wa dhambi. Siku hizi hamsini katika Jumapili hii inatangulia na Sabato ya kila wiki, inayoendeleza Sikukuu ya Pentekoste inayoashiria mfumo wa Yubile kwa wanadamu. Siku hizi hamsini zinaashiria miaka hamsini ya maendelezo ya kazi za Roho Mtakatifu kwa wanadamu. Sadaka hii pia inaonyesha kushuka kwa Roho Mtakatifu kwa wateule. Kwa hiyo tulimpokea Roho Mtakatifu kama watu wenye uweza kwenye Pentekoste ya kwanza. Chachu ilikuwa ni Roho Mtakatifu. Hivyo alitimiliza mfano wa sadaka iliyotiwa chachu.

 

Mambo ya Walawi 23:18 inasema: 18Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtaongeza wana kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng’ombe mume mmoja na kondoo waume wawili, watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA, pamoja na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

 

Vile vinara saba ni mfano wa Makanisa saba ya Mungu. Yule ng’ombe mume ni mfano wa ng’ombe mume aliyekuwa anatolewa dhabihu kama kiongozi mkuu wa watu wetu, na wale kondoo madume wawili ni mfano wa mashahidi wawili. Hii pia ilikuwa inashiriwa na vinara vya taa vilivyokuwemo Hekaluni, vinavyotuongoza kwenye kurudi kwa Masihi. Yopo kumi katika mlolongo wake.

 

Mambo ya Walawi 23:19-20 inasema: 19 Nanyi mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wana kondoo wawili waume wa mwaka wa kwanza kuwa dhabihu ya sadaka ya amani. 20 Kisha kuhani atawatikisa pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA, pamoja na wale wana kondoo wawili, watakuwa watakatifu kwa BWANA, wawe wa huyo kuhani.

 

Mwandamano huu wa Sadaka hii ya Kutikiswa, inaelendelea hadi kufikia Pentekoste, kisha ina utaratibu wake endelevu. Mlolongo huu wa utoaji sadaka uliwekwa ili kuashiria kile ambacho kingetokea kwetu. Hakuna kati ya idadi yote ya dhabihu isiyo na maana yake. Kila kitu kilichomo kwenye dhabihu kinaelekeza kile ambacho Mungu alikuwa anakwenda kutufanyia. Hii ndiyo sababu kulikuwa na vinara saba, kuashiria mfano wa Makanisa saba, ambayo yangefuatiwa na ng’ombe mume mmja na kuwa kwenye nyongeza kwa kondoo waume wawili. Haya yote yanaashiria shughuli kutoka Pendekoste hadi kurudi kwa Masihi, na kazi tunayotakiwa kufanya katika kuipatanisha sayari hii na Mungu. Tunakazi kubwa kuweko mbele yetu ya kuwarejeza watu wa Mataifa hadi kufikia utimilifu wao na kuwafundisha maana ya mambo yaliyotabiriwa na Mungu yaani siri za Mungu. Sisi ni watumishi wa siri za Mungu, na kwa namna yoyote ile wawili kati yetu kwa pamoja kufanya na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni

 

Mathayo 18:18-20 inasema: 18 Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani; yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. 19 Tena nawaambia ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.

 

Sio utendaji tu ya wazee wa Kanisa. Watu wanaweza kusoma hayo katika haki zao wenyewe. Mamlaka yamewekwa na uwakilishi umetokea mara mbili. Sio tu kwa wakati ule ambao Kristo alimwambia Petro na wanafunzi wengine, Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, n.k. Pia inatokea mahali pengine kama tunavyoona na lolote wawili wetu tutakalolifunga litakuwa limefungwa na mbinguni. Kwa maana hiyo ni kwamba watu wawili wanaweza kuanzisha Kanisa na tusiache kukutanika pamoja. Utaratibu unaturuhusu kuendelea mbele kutoa sadaka hizi, kwa njia ya hatua hizi za mfano hadi kurudi kwa Masihi na ukamilifu wa dahari. Kwa sababu ya matatizo tunayo kabiliana nayo, lazima tuweze kujipanga vizuri kwa msingi endelevu. Zana zile tulipewa ilikwamba tuweze kuutimiza nabii zote zinazohusu dhabihu hizi. Dhabihu hizi kama zilivyo zenyewe tu ni unabii tosha.

 

Kitabu cha Hesabu 5:25 inaelezea tena Sadaka ya kutikiswa inayohusika na sadaka kwa ajili ya wivu.

Hesabu 5:25 inasema: 25 Kisha ataitwaa hiyo sadaka ya unga wa wivu, kwa kuiondoa mikononi mwa huyo mwanamke, naye ataitikisa sadaka ya unga mbele ya BWANA, na kuisongeza pale madhabahuni

 

Sadaka ya wivu ilikuwa ni Sadaka ya Kutikiswa kwa ajili wa kumpatanisha mwanamke kwa mume wake (hes.5:12-31). Sadaka ya Kutikiswa kwa ajili ya upatanisho kwa sadaka ya wivu ni mfano wa kumpatanisha mteule wa mataifa kwa mume wake. Mwanamke aliye laaniwa kwa kufumaniwa akizini (Hes. 5:21). Hivyo ndivyo ilivyo kuwa Israeli amelaaniwa kwa ajili ya uzinzi. Masihi aliwapatanisha Isrselina Jeshi kwa Mungu kwa njia ya Sadaka ya Kutikiswa. Mfano wa upatanisho wa watu waasherati kwa Mungu mwenye wivu.

 

Hesabu 6:13-27 inasema: 13 Na sheria ya Mnadhiri ni hii, zitakapotimia hizo siku za kujitenga kwake, ataletwa mlangoni pa hema ya kukutania, 14 naye atasongeza sadaka yake kwa BWANA, mwana kondoo mmoja mume wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa, na mwana kondoo mmoja mke wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya amani, 15 na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, mikate ya unga mwembamba iliyokandwa kwa mafuta, na mikate ya keki isiyochachwa, iliyotiwa mafuta, pamoja na sadaka zote za unga, na sadaka zake za kinywaji. 16 Na kuhani atavisongeza mbele za BWANA, naye atasongeza sadaka zake za dhambi, na sadaka zake za kuteketezwa, 17 naye atamsongeza huyo kondoo mume kuwa dhabihu ya sadaka za amani kwa BWANA, pamoja na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu; kisha kuhani atasongeza sadaka ya unga nayo, na sadaka yake ya kinywaji. 18 Naye Mnadhiri atanyoa kichwa cha kujitenga kwake, mlangoni pa hema ya kukutania kisha atatwaa hizo nywele za kichwa cha kujitenga kwake, na kuzitia katika moto ulio chini ya madhabahu ya sadaka za amani. 19 Kisha kuhani atautwaa mkono wa huyo kondoo mume uliotokoswa, mkate mmoja usiotiwa chachu, atautwaa kikapuni na mkate mmoja wa keki, naye ataitia mikononi mwake yule Mnadhiri, baada ya kunyoa kichwa cha kujitenga kwake; 20 naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kitu hicho ni kitakatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa, na paja la kuinuliwa, kisha baadaye Mnadhiri ana ruhusa kunywa divai. 21 Sheria ya Mnadhiri awekaye nadhiri ni hiyo, tena ni sheria ya sadaka yake atakayomtolea BWANA kwa ajili ya kujitenga kwake, pamoja na vitu vile ambavyo aweza kuvipata zaidi; kama nadhiri yake awekaye ilivyo, ndivyo impasavyo kufanya kwa kuiandama sheria ya kujitenga kwake. 22 Kisha BWANA akanena na Musa na kumwambia, 23 Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyo wabarikia wana wa Israeli, mtawaambia; 24 BWANA awabarikie, na kuwalinda; 25 BWANA akuangazie nuru ya uso wake, na kukufadhili. 26 BWANA awainulie uso wake, na kuwapa amani. 27 Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli, nami nitawabarikia.

 

Sio jambo lililotokea kwa bahati mbaya kuona kuwa mng’aro wa Bwana juu ya watu umechukua nafasi yake hapa kufuatia na nadhiri ya Mnadhiri na ya Sadaka ya Kutikiswa kwa ajili ya upatanisho wa Mnadhiri. Kusudi la kiapo cha Mnadhiri ilikuwa ni kumpatanisha na kumsogeza karibu na Mungu kiroho, kwa sababu sheria kama ilivyo tu peke yake, haiwezi kukupatanisha na Mungu. Njia pekee ya kumuwezesha mtu kuwa karibu na Mungu wakati wa Agano la Kale ilikuwa ni kwa kuweka nadhiri ya Mnadhiri. Mahojiano au mitihani ilifanyika kisha walinyolewa vichwa vyao, kisha walikatazwa wasitumie mvinyo, na kwa kujitakasa kabisa kwa kufaa kwa kuwa karibu kama unavyo takiwa katika sheria za kimwili. Yohana alikuwa Mnadhiri kwa kuonyesha mwendelezo wa mpito kuelekea kwenye hali ya Umasihi. Kristo hakuwa Mnadhiri. Alikata nywele zake kama ilivyokuwa inatakiwa katika sheria na alikunywa mvinyo ulio chachwa au wenye kulevya (tazama jarida la Mvinyo katika Biblia, [188]. Alitengwa mbali na Roho Mtakatifu.

 

Mtu aljitenga mwenyewe na utaratibu na nia ilikuwa ni kujitenga ili kuwa karibu na Mungu. Samsoni alitengwa mbali kama Mnadhiri toka kuzaliwa kwake ilikwamba Roho Mtakatifu katika uwepo wake aweze kudhihirika ndani ya Samsoni kwa siku za maisha yake (tazama jarida la Samsoni na Waamuzi [073]. Hiyo itadhihirisha uweza na mwandamano wa mambo ya Roho Mtakatifu. Kile alichokifanya akiwa kama Mnadhiri ni kile tunacho kikamilisha bila kuenenda kwa mujibu wa viapo vya Mnadhiri. Sisi hatuhitaji kuwa Wanadhiri kwa sababu, katika Sadaka ya Kutikiswa, Kristo alitupatanisha kama Wanadhiri kufikia hatua tunapoweza kula na kunywa mkate na divai ya Yesu Kristo. Sababu ya Mnadhiri kuishi maisha ya kujinyima au kujikana kwa mambo ya kimwili kutoshiriki kunywa mvinyo ilikuwa ni kwa sababu hawakuwa na Roho Mtakatifu, na alipatanishwa kama hatua ya kwanza ili kutuonyesha kuwa wasingeweza kujipatanisha bila ya Kristo na kwamba bila ya Kristo na kwamba Roho Mtakatifu hakuwepo ndani ya maisha ya Mnadhiri. Njia pekee ya kuwafanya wawe karibu zaidi ilikuwa ni kwa utakaso. Lakini bado wasingeweza kuwa na Roho Mtakatifu, ingawaje viapo vya Unadhiri vilifanyika, hadi pale Mungu atakapo mjaalia mmoja mmoja binafsi, kama vile Samsoni, alivyobahatika. Kristo alitupatanisha sisi ili kwamba tumpokee Roho Mtakatifu aliyetolewa mfano kwa njia ya divai na tufanyika kuwa ni sehemu ya mwili wa Kristo, aliyetolewa mfano kwa njia ya mkate, bila kulazimika kunyoa vichwa vyetu, kujitenga na kuchukua taratibu za Sadaka za Kutikiswa. Kwa kupitia dhabihu ya Kristo, alitupatanisha sisi kama Wanadhiri wa Mungu. Ile nadhiri ya Unadhiri haina umuhimu tena kwetu. Haina maana kwetu kwa sababu kwa hakika inapunguza viwango vyetu tu na wala haisaidii kuviongeza. Sisi ni Wanadhiri kwa kufanyika mara moja na kwa siku zote kwa Mungu. Yote yamefanywa na kukamilishwa na Kristo.

 

Kwa hiyo, nuru ya uso wa Mungu inatumulikia, na jina la Mungu limewekwa juu yetu, kama sehemu ya Wana wa Israeli. Hii ndiyo maana ya kifungu cha maandiko matakatifu ya Hesabu 6:27. Jina la Mungu wetu limewekwa juu yetu, juu ya vipaji vya nyuso zetu na kwenye mikono ywtu ya kuume.

 

Hesabu 18:8-10 inasema: 8 Kisha BWANA akamwambia Haruni, Tazama, nimekupa wewe ulinzi wa sadaka zangu za kuinuliwa, maana, vitu vyote vya hao wana wa Israeli vimewekwa wakfu, kwa ajili ya kule kutiwa mafuta kwenu, kuwa haki yenu milele. 9 Vitu hivi vitakuwa vyako katika vile vilivyo vitakatifu sana, visiteketezwe motoni, matoleo yao yote, maana, kila sadaka yao ya unga na kila sadaka yao ya dhambi, na kila sadaka yao ya hatia watakavyonitolea, vitakuwa wakfu sana kwa ajili yako wewe na kwa wanao. 10 Utakula vitu hivyo kuwa ni vitu vitakatifu sana, kila mume atakula vitu hivyo, vitakuwa vitakatifu kwako wewe.

 

Sadaka ya kuinuliwa, na vitu vyote vilivyopigiwa mbiu na wana wa Israeli viliwekwa kati ya makuhani. Ambavyo vilihamishwa wakati Patakatifu pa Patakatifu palivyoanzishwa kama mawe yaliyo hai ya wateule. Wakati Hekalu lilipoondolewa, mamlaka ya kikuhani pia yaliondolewa, na utaratibi wa Melikizedeki ulichukua pahala pa Haruni. Vitu hivi vyote hatimaye vilihamishiwa kwetu. Tukafanyika kuwa makuhani wa Mungu kupitia Yesu Kristo. Sisi ni Hekalu la Mungu kama mawe yaliyo hai.

 

Hesabu 18:11-18 inasema: 11 Tena kitu hiki ni chako; ile sadaka ya kuinuliwa ya kipawa chao, maana, maana sadaka za kuinuliwa zote za wana wa Israeli; hizi nimekupa wewe, na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu milele; kila mtu katika nyumba yako aliye safi atakula hizo. 12 Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zbibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa BWANA, amekupa wewe hayo. 13 Matunda ya kwanza yaivayo katika yote yaliyo katika nchi yao, watakayomtolea BWANA, yatakuwa yako, kila mtu aliye safi katika nyumba yako atakula katika vitu hivyo. 14 Kila kitu kilichowekwa wakfu katika Israeli kitakuwa chako. 15 Kila kifunguacho tumbo, cha wenye mwili wote watakachomsongezea BWANA cha wanadamu na cha wanyama, ni chako, lakini mzaliwa wa kwanza wa binadamu, hunabudi utamkomboa, na wazaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi utawakomboa. 16 Na hao watakaokombolewa katika wanyama hoa tangu aliyepata umri wa mwezi mmoja utamkomboa, kama utakavyohesabu kima chake, kwa fedha ya shekeli tano, kwa shekeli ya mahali patakatifu (nayo ni gera ishirini). 17 Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe, au mzaliwa wa kwanza wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, hutawakomboa hao; maana ni watakatifu hao, utanyunyiza damu yao katika madhabahu na kuyateketeza mafuta yao kuwa sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto, iwe harufu ya kupendeza. 18 Tena nyama yao itakuwa nyama yako wewe, kama kile kidari cha kutikiswa, na kama mguu wa nyuma wa upande wa kuume, itakuwa yako.

 

Mlolongo huu unaongelea kuhusu kila kilicho safi katika Israeli, na mzaliwa wa kwanza yuko safi. Sadaka hizi na dhabihu hizi ni mifano. Divai na sadaka ya kinywaji ni wateule. Ni kwa wale tu waliobatizwa katika mwili wa Yesu Kristo waliosafishwa kwa maana ya sadaka na dhabihu. Kile ambacho kilikuwa kuhesabia tena ni dhana ya kusafiwa katika Israeli, kuweza kukubalika na Mungu. Sadaka hizi zote hubeba sura ya kutikiswa mbele za Bwana ili kwamba watokee mbele za uso wa Mungu na wachukuliwe kwenye mfumo.

 

Kristo alianzisha mlolongo huu wa kutikiswa, malimbuko katika siku hii ya Jumapili, mlolongo wa utoaji sadaka, mmoja baada ya mwingine, kwa wakati wote hata utimilifu wa Mataifa uwasili na wale 144,000 katika Israeli wamehesabiwa au kutiwa muhuri na idadi ya wateule imeisha kamilika kutoka kwenye mataifa yote. Dunia haitaweza kudhuriwa hadi pale mtu wa mwisho kati yetu awe amekwisha kuhesabiwa, kubatizwa, kombolewa na kutikiswa mbele za Bwana. Wakati wamwisho kati yetu atakapokuwa amechukuliwa kutoka katika mataifa, ndipo ule mwisho utakapokuja.

 

Katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana, tunaona malaika akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu. (Ufu. 7:3). Kristo ndiye alikuwa limbuko la mavuno ya shayiri, ikiashiriwa na hujduma zake na Sadaka ya kutikiswa liyofanyika siku ya Jumapili. Kwa tendo kama hilo, aliweka katika hisia mlolongo wa matukio ambayo ingelileta nje jeshi la makuhani. Ingawatenga na kuwaweka wakfu kwa Mungu. Ingetutenga sisi kwa Milenia. Hii ndiyo ishara ya huduma hii na inaanzisha, kitu ambacho hakifanyiki kwa bahati mbaya, muelekeo kwenda kwenye Pentekoste, na Pantekoste ni ishara ya ukombozi wa wateule wa ufufuko wa kwanza.

 

q