Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[113]
Mithali
30
(Toleo La 1.0 20020810-20020810)
Dhumuni la jarida hili ni kuiainisha Mithali 30 kwa namna ya jinsi inavyomsisimua na kumpa hamasa msomaji ya kuzama na kufikiri kwa kina zaidi kutafakari kuhusu maisha yake. Imeandikwa kwa namna ambayo inatumainisha kumfanya msomaji aulize maswali ya kiudadisi na maana.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hatimiliki © 2002 Storm Cox, ed. Wade Cox)
(tr. 2016)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na
tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote
atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja
ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Mithali 30
Kwa mwanamke (au
Kanisa) ambalo Mungu ametupatia Mithali hii ya 31, kwa mwanamume (au kuhani au
kasisi) aliyetupa sisi Mithali 30. Mithali 30 ni mtazamo muhimu na wenye nguvu
sana mawazoni mwa mwanadamu na mwelekeo au maelekezo anayopasa kuyachukua.
Inaanza kwa kuionyesha toba na ubatizo.
Maneno ya Aguri
30 Maneno ya Aguri bin
Yake; mausia mtu huyu aliyomwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali.
2 Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu; Wala sina
ufahamu wa mwanadamu;
3 Wala sikujifunza hekima; Wala sina maarifa ya kumjua
Mtakatifu.
4 Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini?
Ni nani aliyekamata upepo kwa
makonzi yake?
Ni nani aliyeyafunga maji ndani
ya nguo yake?
Ni nani aliyefanya imara ncha
zote za nchi?
Jina lake ni nani?
Na ni nani jina la mwanawe, kama
wajua?
Safari ya maisha
inaanza kwa kugundua kwamba maisha ya zamani au ya kale ni muhimu na hayana
matokeo hasi. Tunajifanyia fujo na matatizo kwa dhambi. Kwa kumkataa Mungu na
busara iliyo kwenye Maandiko Matakatifu, uamuzi tuyafanyayo na yasiyo na maana.
Msukumo wa kijakamoyo wa maisha ya Misri yanatupelekea kutafuta mtindo wa
maisha wa kimaisha. Kuishi bila Mungu hayatoi makusudio na kusiwe na hatima
njema, kusiwe na sababu ya kuishi zaidi ya kuendeleza tu mtazamo wa shinikizo,
kwa namna yoyote inayoonekana kuonekana. Kwa wengine, ni udhalilisho mkubwa; kwa
wengine ni kwa njia ya ngono, na kisha kuna wale ambao kutokana na vita
isiyoisha kujipatia faida.
Dunia inayoamkia
kufanya kazi, husahau familia na marafiki; na inaelewa kidogo hitaji la upendo.
Mashindano hushuhudia juhudi za kila mtu mmoja mmoja ya kutambuliwa.
Upandishaji cheo unamaanisha utajiri zaidi, ongezeko bora la kiwango cha
kuongezeka kima, na kufikia zaidi kwa bidhaa na huduma. Yampasa mke afanye kazi
ili alipie bili. Watoto wanalelewa na wageni ili wazazi wamudu kuendesha gari
zuri. Tunasema, anaishi kwenye nyumba ndogo, kwa hiyo hafanyi vizuri sana. Ana
watoto wane, kwa hiyo inawezekana kuwa anafanya hivyo kwa shida na ugumu mwingi.
Anafanya kazi
masaa 80 kwa juma na haioni kabisa familia yake, ni mfanya kazi mahiri kiasi
hicho. Anavaa suti za gharama kubwa, ni lazima awe wa muhimu. Anakunywa sana
pombe; ni lazima awe na jakamoyo. Anakopa hela ili awachukue watoto wake
kuwapeleka mapumzikoni; kwa hiyo anatimiliza majukumu yake. Mke wake huvaa vito
vya gharama kubwa, anampenda kwa kiasi gani basi. Anamajukumu ya kuwajibika
kwayo, jaka moyo za kikazi zilimsababisha aende mbali kandoni. Anafanya kazi siku
saba za juma, akiungua. Hata hivyo, familia yake ina mahitaji.
Anautumia muda wa
bosi wake kwa kutandaza wavu; kazi hii ni ya muhimu sana. Anajihisi mzaa
matunda kwa kiasi gani unadhani. Yampasa arudi nyumbani kwa familia yake kama
usiku wa michezo.
Tunayafania kazi
yale yaliyo ya muhimu maishani mwetu. Tunawezaje kupenda kila kitu bila kujua
ni kwa nini? Yatupasa kufikiria; kwamba mimi ni mjinga sana kuwa mwanadamu.
Yatupasa tatupasa tujiulize wenyewe; je, nimesahau kitu chochote kilicho muhimu
maishani? Wazazi wangu walinilea wakinipenda – je, nimesahau hilo? Ni nani
anaweza kunifundisha jinsi ilivyo? Kwa hakika najua.
Naona masumbufu
ya dunia hii yananipotosha na kunirudisha nyuma. Naona kwamba utajiri
unawadanganya watu. Naona kwamba hisia ya moyo ni tajiri kuliko miamba. Naona
kuna ujinga kwenye dhambi. Naona Kristo ni mwalimu wangu. Najionea kuwa mhitaji
yuko safi. Napenda kujifunza jinsi ya kuishi. Napenda niwafundishe wengine.
Napenda wengine wajihisi kama ninavyojihisi mimi – kuwa niko huru. Napenda
kufanya kazi na watu wanaohisi kama ninavyotenda na kujihusisha na mambo ya
watu maskini na wajinga. Wakati wangu ni mzuri. Nazipenda sikukuu zangu na
saumu zangu. Ni zangu na
nazipenda. Nazihitaji pamoja na familia yangu yote.
Kwenye andiko hili
tunajionea rejea inayolitaja jina la Mungu na ukweli wa uwepo wa Mwana wa Mungu.
5 Kila neno la Mungu
limehakikishwa;
Yeye ni ngao yao wamwaminio.
Yeye ni Mungu wa
Pekee na wa Kweli anayeniongoza na amemtuma mwana wake kuja kuniokoa mimi.
Mimi najiamini sana
kwa kila nilifanyalo. Nimebatizwa
na Kristo ni mwalimu wangu. Kuna jibu kwa maswali yangu yote kama nitautoa muda
wangu kutembelea majarida haya na Maandiko Matakatifu na kujisomea. Najuma
kwamba kufanya hivyo kila siku, kwa kuwa sheria au Torati inanionyesha kile
inachotaka ninachohitajika kukifanya. Siwezi kupata madhara. Roho yangu
inalindwa na kundi kubwa la malaika. Mungu ananiambia kuwa aliiumba dunia kwa
muda wa siku sita. Ni kwa nini nisimwamini yeye? Mungu ananiambia kuwa
alipumzika siku ya Sabato. Kwa nini nifikiri vyovyote vingine? Mungu ananiambia
niwasaidie masikini kama afanyavyo yeye. Kwa nini basi nifanye vinginevyo tofauti?
Mungu ananiambia kuwa Kristo atarudi tena. Kwa nini naamini vinginevyo tofauti?
Mungu ananiambia kuwatembelea watu wangu na kutumia muda pamoja nao. Ni kwa
nini nifanye kinyume chake. Mungu ameniambia nifunge saumu ili niwe karibu na yeye.
Kwa nini basi nisimsikilize? Mungu ananiambia niende mahali pazuri
nikaadhimishe sikukuu na kununua kila ninachokipenda, na kwenda kujifunza neno
la Mungu pamoja na watu wangu na kwenda kula chakula kizuri. Ni kwa nini basi nisifanye
hivyo? Ziwezi kushindwa kwa kuwa naamini. Roho ananifanya niamini.
6 Usiongeze neno katika maneno
yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.
Nimebatizwa na
naijua kweli. Ufunuo anaoutoa Bwana unatosha. Je, nahitaji watu waniambie
kwamba ni mimi ndiye niliyeviumba vitu hivi? Je, nahitaji watu waniambie kwamba
ni mimi ninayeweza kukulinda wewe? Je, naweza mimi kukupa uzima wa milele? Je,
naweza mimi kukupa mahali pako mbinguni? Je, naweza mimi kulijenga kanisa na
kuwaondolea watu dhambi zao? Je, mimi naweza kukutawala wewe? Je, sisi hatuma
Bwana wetu tayari na je, hatutajua tayari jinsi tunavyopasa kuishi? Je,
hatujajua sisi tayari mambo ya kufanya kila siku? Je, hatujawa tumeshawishika
tayari kwa mng’aro wa uumbaji na maajabu ya mwanadamu mwenzetu? Je,
hatujashawishika tayari na kweli? Je, hatuoni kwamba kila Andiko Takatifu linafungamanishwa
na kuwashikilia au kuwagusa watu wote pamoja? Je, hatuoni minyumbuliko na rangi
ya dunia? je, tunawezaje kuthibitisha ukamilifu wake? Je, tunayakata na
kuyaondoa masikio ya mtu na kuyarudishia tena kwa kuyashona au, kuikata miguu
yetu ili kuifitisha kwenye shimo. Biblia imevuviwa na ni kweli. Imani yangu
inatuama kwenye ukweli huo. Kama
si hivyo, basi mimi ni sokwe. Mimi ni mnyama asiye na uhai. Naweza kuua na kubaka bila kujijua na
pasipo kuwa hivyo. Biblia ndiyo inanifanya kuwa mwanadamu. Biblia inanifanya
niwe wa hakika. Biblia inanitambulisha mimi kwa Mungu.
7 Mambo haya mawili
nimekuomba;
Usininyime [matatu] kabla sijafa.
8 Uniondolee ubatili na uongo;
Usinipe umaskini wala utajiri;
Unilishe chakula kilicho kadiri
yangu.
9 Nisije nikashiba nikakukana,
Nikasema, Bwana ni nani?
Wala nisiwe maskini sana nikaiba,
Na kulitaja bure jina la Mungu wangu
Ni kwa nini
sifanyi kama anavyosema Mungu? Usimfiche kitu chochote mwanadamu. Kwa nini
nahisi kama najilinda na kujitetea mwenyewe kwa kujidanganya? Ni nini
anachoweza kukifanya mwanadamu ili anidhuru mimi? Je, kuna kitu chochote nilichokitenda
kibaya sana? Ni kwa nini nisiwe mtu ninayethibiti hatima yangu; kujiamini na
majivuno ya kujiona kuwa mimi ni kiumbe niliyeumbwa na Mungu? Mimi ni mtumishi
mtendakazi wa kanisa, mume na baba, kaka na dada, mama na mke, mjomba,
shangazi, binamu na rafiki. Je, nahitaji kuwa zaidi? Kwa nini napenda kuwa
chini? Kwa nini tunadanganya? Maisha ni rahisi. Tunalala; tunaamka; tunakula;
tunapenda na tunafanya kazi. Tunakunywa na tunacheka na kuwakumbuka watu wetu.
Tunakwenda kanisani wakati tunapoweza. Tunajumuika; tunasoma; tunangojea kwa
uvumilivu mwingi na tunaomba. Kwa nini kunakuwa na uhitaji wa ziada au kwanini
tunahitaji zaidi na ni kwa nini kunahitajika kuukanganya ukweli ulio dhahiri na
ulioko mbele yetu?
Kwa nini nataka
mambo mengi sana? Kwa nini nahitaji kutiliwa maanani kwa namna hiyo? Wakati
ninapokuwa nayo yote, sihitaji chochote. Je, ndipo hapo nakuwa simhitaji muumba
na Mungu wangu? Ninafikaje hapo? Kama fedha zinaweza kupotosha, kwa nani kwa
basi nijitaabishe na kujitoa mhanga? Kama hunipendi hadi niishi kwenye makazi
au nyumba nzuri na kuendesha gari zuri na la gharama, unaweza ukanienda mimi kwa
vyovyote vile? Utajiri na mali zangu zinategemea watu wengine. Iwapo kama
tungemwelewa Mungu kwa kuwa wakamilifu, kwa nini basi atutake tufunge saumu?
Kama tulimlipa mtu ili atupandie mazao, ni kwa kiasi gani basi tungeyaelewa masuala
ya uumbaji? Ni kwa jinsi gani mtoto anaweza kuelewa uumbaji asipochezea na
kutunza wanasesere? Watoto waishio mjini hawajawahi kumona ng’ombe kabisa.
Je, umekwishawahi
kuuonja mkate uliouoka wewe mwenyewe? Inauma sana kuwa na njaa, lakini vyakula
vingine havitoshelezi wala kushibisha kabisa. Nipe nyanya kutoka chunguni
mwako; ladha yake haiwezi kufanana. Kwa nini nilazimike kuwa na gari wakati naweza
kutembea kwa miguu yangu? Kwa jinsi hiyo ndivyo ninapowaona ndge. Ndiyo shauku
na mpangilio wa jamii za kisasa zilizopo zinazotufanya sisi tudhoofike na tuwe na
shauku.
10 Usimchongee mtumwa kwa bwana wake;
Asije akakulaani, ukaonekana una hatia.
Maka Mungu
anasikia kila kitu tukisemacho, na anajua kila kitu tukifikiricho, ndipo
tunapokuwa tunafikiri vibaya juu ya mtu mwingine ndipo tunamsengenya au
kumsingizia mtumishi kwa bwana wake. Basi na tusichukulie fursa hiyo kwa wale
walio watiifu na waadilifu kwene nafasi zao. Dunia inajali watu wake wote na
watu wa mionekano na tabaka mbalimbali na wenye mawazo mbalimbali na viwango
vya hekima na busara. Ninachotufanya tuwe bora, lakini uwezo wetu wa kusamehe
kama Baba anavyotusamehe sisi. Ni ninii kinachokufanya wewe uwe mwenye hekima
zaidi kuliko nilivyo mimi? Je, kila kitu wakati wote kinafanya kazi zake
kikamilifu sana kwa jinsi tutarajiavyo? Naweza kupika chakula, lakini wewe
unaweza kukarabati chungu kilichovunjika. Mwanamke anaweza kucheza vyema, lakini
wewe mwanaume unaweza kuchora picha kubwa. Kwa hiyo, watu wengi wana muda na
mimi, kwa niinini basi name nisiutenge muda wangu kwa kwa ajili ya wengine? Kwa
nini namchukia ndugu yangu na kufanya uadui naye? Kwa nini namuumiza dada
yangu? Kwa nini namsababishia Baba ajisikie maumivu kwa kuwadhuru-kuwaumiza watoto
wake? Kwa nini nataka ulichonacho wewe wakati nikiwa tayari nimekwisha kuwa nayo
zawadi kama hiyohiyo uliyonayo? Uwanaume wangu unategemea na uwezo wangu wa
kufanya kazi na watu wengine. Nawahitaji watu wengine na wengine wananihitaji
mimi pia. Kwa nini nimzuie mtu anayenisaidia wakati nahitaji sana msaada wake.
11 Kuna kizazi cha watu
wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao.
12 Kuna
kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe; Ambao hawakuoshwa uchafu wao.
13 Kuna
kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka
sana.
14 Kuna
kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili
kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
Mimi ni nani
nisiyekuwa na mama yangu na baba yangu na ni wao ni nani wasipokuwa na wazazi
wao? Ni wao tu ndio walionileta mimi hapa duniani na ni Kristo tu ndiye anayeweza
kunisafisha kwa kuniosha dhambi zangu. Ninawezaje kujishawishi mwenyewe kwa
mazingira mengine yoyote? Unawezaje kunishawishi mimi kuwa unaweza kufanya
kulifanya hilo badala yao? Unaweza kunipatia uhai nje ya familia na umilele nje
ya uumbaji? Ni nani wewe hata unijaribu mimi kwa mawazo yaliyo kinyume na
hivyo? Mimi sikuomba nizaliwe; wala sikuomba niwepo, na wala sikutuma maombi.
Mama yangu na baba yangu walipendana na kuishi pamoja kwa maelekezo ya Mungu na
ndivyo ilivyo hata kwa mimi pia. Familia ni mujumuisho wa baba na mwana na mama
na mimi ni mtoto—inaweza kuwa ni ya namna nyingine yoyote ile? Simjui mwingine
yeyote zaidi. Je, ni tofauti na mtu mwingine yeyote hapa duniani? Je, hatupo
sisi sote sawa kwenye jambo hili? Je, sio kwamba watu weusi na weupe, Waasia na
Wahindi wote wameumbwa kwa namna moja? Je, sio watoto wa wafalme na wa mamalkia
wameumbwa kutokana na mpango mmoja huo huo kama watokanavyo watoto wanaozaliwa
kwenye vichochoroni au makazi duni? Je, mahitaji yao hayafanani? Je, kazi na
majukumu yao hayafanani? Je,
thawabu zao hazifanani na na za sisi wengine wote? Wewe ni nani unayedhania
kuwa mahitaji yako ni makubwa sana kuwaliko wengine na kwamba unastahili kuwa
na umuhimu kwa kuwa una nembo fulani kwenye shati lako? Kama uhadhania hivyo,
basi wewe husomi vitabu vilevile nivisomavyo mimi. Ni Mungu tu ndiye anayeweza kutulisha
sisi. Ni Mungu tu ndiye anayeweza kutupatia sisi maji na ni Mungu tu ndiye
anayeweza kutufundisha sisi kweli. Kwa nini uchukue kilicho kidogo alichonacho
ili kuongeza kwenye lundo lako lisilo na kitu?
15 Mruba anao binti wawili,
Waliao, Nipe! Nipe!
Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe,
Naam, vinne visivyosema, Basi!
16 Kuzimu;
na tumbo lisilozaa;
Nchi isiyoshiba maji;
na moto usiosema, Basi!
Ni kwa nini
tunajidanganya sana sisi wenyewe? Maisha yetu ni haki endelevu. Kwa nini tunapenda kile ambacho tulichomudu
kujishawishi sisi wenyewe kuwa ni cha mhimu sana? Kristo alisema:
“Baba
yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, 10
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupe leo riziki yetu. 12 Utusamehe
deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. 13 Na
usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na
nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]”
Sikioni kitu
kingine chochote kuhusu waosha vyombo au waosha sahani, vito vya thamani,
magari, sikukuu, sofa za ngozi, watengeneza juisi, mashine za kutengeneza
kahawa, mkandamizo au shinikizo, mashine zinazooka mkate, wasafisha mazingira
kwa mashine za kiatomatiki ambazo hazihitaji kusukumwa huku na huko na vitu
vingine cha kuchokesha zinazojiri mapema sana asubuhi. Sio dhambi kuwa na vitu
hivi, lakini ni kujiuliza vina umuhimu gani kwenye maisha yetu? Tunahitaji
kuishi kwa kiwango kipi? Je, kuta nzuri na zinang’arazo zinazojengwa, zinatufanya
tuwe mbali na kutenganisha mbali na vile kunavyovihitaji kwa kweli? Je, ninafanya
vya kutosha ili kujielewa sisi ni kina nani, au ninajaribu na kujitahidi
kukupatia wewe vitu ninavyodhani kuwa unavyivihitaji? Sikihitaji hiki,
nakihitaji, sijali hukusu ulichonacho, bali najali tu vile ulivyo. Watu walio kanisani
ni matajiri sana ulimwenguni kwakuwa wapo kanisani. Sipendi kuwa tajiri sana na
kama unanichukia kwakuwa mimi ni maskini, basi mimi ni tajiri zaidi kuliko
wewe. Kama unanipenda, ndipo ninakuwa tajiri zaidi, na kadiri unavyonipenda
ndipo ninapozidi kuwa mkuu zaidi.
17 Jicho la mtu amdhihakiye babaye,
Na kudharau kumtii mamaye;
Kunguru wa bondeni wataling'oa,
Na vifaranga vya tai watalila.
18 Kuna mambo matatu yaliyo
ya ajabu kwangu,
Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.
19 Mwendo
wa tai katika hewa;
Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba;
Mwendo wa merikebu katikati ya bahari;
Na mwendo wa mtu pamoja na msichana.
Uumbaji ni kitu
kikubwa sana kuliko kingine chochote nilichowahi kukiona. Mawazo ya Mungu ni
ukurasa ulio wazi. Tembea nje na soma kitabu. Hatujiulizi kabisa kama kuna
Mungu, bali ni kwa nini hakuna mwingine? Ni wazi na dhahiri sana na ni kwa wazi
sana. Ulimwengu hauwezi kuwepo kwa ujuzi au uelewa wa kisayansi bila kuwa na
kuingiliwa kati. Ni mtu ytu yupi anayeweza kuuota mti? Ni mtu yupi anayeweza
kumbuni ndege kwa kumchora asipokuwa ameonyeshwa yupoje? Malaika walilia kwa
furaha baada ya kuumbwa ulimwengu huu. Ni nili ilikuwa mara yako ya mwisho ulipowahi
kuulilia ulimwengu huu na waliomo ndani yake? Kama hujawahi kuulilia ndipo
nakushauri uingie ndani na kuanza kufanya hivyo. Ni bustani yako. Umuumbwa kwa
ajili yako. Ni zawadi kutoka kwa Mungu. Unashukuru kwa kiasi gani basi kila
siku? Basi na uitunze bustani hii na uisafishe na pigania kuilinda. Kila siku
fanya kitu kizuri ili kuiokoa. Walinde na kuwatunza wanyama na mimea yake
iliyomo ndani yake. Usiiongezee ahadi ndani yake. Ikiwezekana tumia mtindo wa
kutembea kwa migugu na usiendeshe gari.. tumia basi unaposafiri hata hivyo.
Kama itatumika tena ndipo tumia tena. Kama ikivunjia, ndipo vunja na wewe. Kama
itageuka na kuwa kitu kinginechochote, basin a uibadilishe na kuwa kitu
kinginechochote. Usichague kwa kupiga kura – kasha ukamfanya mmoja wao kuwa ni
uumbaji. Ni muhimu sana kuliko kulinda, barabara au hukumu ya kifo.
Kama unampenda
Mungu unayapenda mawazo yake na utaziheshimu karama zake. Je, yanipasa kuelewa
hilo? Kwa nini nahitaji kumwelewa mwanamke na ni kwa nini mwanamke anahitaji
kumwelewa mwanaume? Je, huu si uwongo wa ajabu wa kisirisiri? Je, haifanyi iungo
cha kuongeza kwenye rangi? Je, hamu haisababishi nguvu? Je, upendo sio safari?
Kwa nini ni muhimu kuyapima na kuyachanganua mambo yote? Je, kuzijua siri zote,
mambo yote kunanifanya kuwa mtu mzuri sana? Sio kule kujua kila kitu ndiko
kunakotufanya tumpende Mungu. Bali kunatufanya tumheshimu Mungu zaidi.
Kunatufanya tuuheshim uumbaji wake zaidi.
20 Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke
mzinifu;
Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu.
21 Kwa ajili ya mambo matatu
nchi hutetemeka,
Naam, kwa ajili ya manne haiwezi
kuvumilia.
22 Mtumwa
apatapo kuwa mfalme;
Mpumbavu ashibapo chakula;
23 Mwanamke
mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.
Yatupasa tujue kwamba
ni kwa kupitia kanisa tu tunaokolewa na kwa kupitia kanisa tu ndipo tunaweza
kuvishinda vita dhidi ya uovu. Kanisa kongwe la kizamani, mwanamke kahaba wa
kidini, linafunua kinywa chake na kusema “sijafanya ubaya wowote”. Tutafanyika
kuwa wafalme. Kristo anatulisha chakula, kwa hiyo hatuwezi kudanganywa na
tunafanyika kuwa watawala wa nyumba. Dunia haitabakia kama ilivyo wakati
tunapolifikia lengo hili. Mume wetu atatupenda na wa mwisho atakuwa wa kwanza.
Ni nani
anayependa dunia hii iliyopo isimame? Yatupasa tufanye kazi ili kuifanya
ibadilike na kuitayarisha ili Kristo achukue hatamu. Kanisa ni kitu cha muhimu na muhimu kwa maisha
yetu. Basi na usiende kuzini na mwanamke huyu kahaba wa kidini. Je, huoni kuwa
ni vizuri sana ukalala kitandani kwako mwenyewe?
24 Kuna viumbe vinne duniani
vilivyo vidogo;
Lakini vina akili nyingi sana.
25 Chungu
ni watu wasio na nguvu;
Lakini hujiwekea chakula wakati
wa hari.
26 Wibari
ni watu dhaifu;
Lakini hujifanyia nyumba katika
miamba.
27 Nzige
hawana mfalme;
Lakini huenda wote pamoja vikosi
vikosi.
28 Mjusi
hushika kwa mikono yake;
Lakini yumo majumbani mwa
wafalme.
Yeye asiyewatunza
watu wa nyumbani mwake mwenewe ni mbaya kuliko asiye amini. Hatuhitaji kuwa
imara sana, bali tunahitaji kuwa wene bidii na wenye akili na busara nyingi.
Jipange kwa kujiandaa kwa ajili ya nyakati fupi. Je, mkulima hujaza pumba kwenye
mazao mazuri kwa ajili ya ukame – au huwa anakwenda mapumzikoni? Je, tunazijenga
nyumba zetu kwenye mchanga ulio kwenye ukanda wa fukwe za pwani ili
zizoelewembali na mapigo ya mawimbi? Je, tunapenda mfalme wetu ajue kule
tunakokwenda kupiga kwata? Je, Kristo anahitaji kuketi mezani kwako hata kabla
hujapenda kwenda kanisani? Hata nzige, panzi wakubwa, wanajua kwamba ni nini
kazi yao inayowapasa kuitenda. Je, tunataka Kristo atubebe mikononi mwake na
kutufanya tuvinjari kwenye kasri yake? Enyi wanyama watambaao, hebu na
awafanyie hivyo. Je, tunausikiliza unabii na kutii maonyo yake? Je, siyo Farao
aliyejiandaa kwa baa la ukame? Tunajua kwa kuwa maneno ya Mungu yanathibitisha kweli
yote. Acha chakula chako a chakula chako, jenga nyumba mahala pazuri, timiliza
majukumu yako na mruhusu Kristo akubebe.
29 Kuna watatu wenye mwendo wa
kupendeza,
Naam, wanne walio na mwendo
mzuri.
30 Simba
aliye hodari kupita wanyama wote;
Wala hajiepushi na aliye yote;
31 Jimbi
aendaye tambo; na beberu;
Na mfalme ambaye haasiki.
Wakati Kristo, mkono
wake utakapokuwa nay eye kikamilifu sana. Wakati tunapoenenda kanisani na wote
wakiwa na umoja na kutimiliza majukumu yao, basi Kristo anajivunia nao na
hawazuii. Tunapigana na majeshi ya Shetani tukiwa pamoja na Kristo. Sisi tuko
makini vitani. Kristo anatutaka tupigane naye huyo adui. Anatembea mbele
kupitia kwa maadui na anashinda vita vyote wakati kanisa linaposonga mbele
pamoja naye. Nguvu za kanisa haziwezi kupingwa; uweza wa kanisa hauwezi kupuuzwa.
Sisi tu jeshi lake. Hatubebi mabunduki, wala hatutawaliwi au kuenenda kwa
kanuni za namna moja maka hizo. Sisi tu kwenye jeshi la wanaojitolea, wadhaifu,
tuliofanywa kuwa imara kwa malengo maalumu na mikakati maalumu.
32 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza;
Au ikiwa umewaza mabaya;
Basi weka mkono wako juu ya
kinywa chako.
33 Kwa
maana kupiga maziwa huleta siagi;
Na kupiga pua hutokeza damu;
kadhalika kuchochea hasira
hutokeza ugomvi.
Fikiri kile
ukisemacho na fanya kabla hujatelekeza uamacho. Usitafute sifa na heshima kwene
hii dunia unapokuwa hujaalikwa. Jiulize mwenyewe: ni kwa nini nilikukasirisha?
Kwa nini ulikusudia kuniumiza? Je, iki? Kinapendeza? Hakiendani na upendo? Je,
tunasema mambo yetu tukiwa na agenda za siri? Manabii wengi wa uwongo huja na
kusema maneno yasiyo ya kweli na hata yasiyo na maana. Je, wewe ni mmoja wao?
Je, unamtafuta roho akuongoze, au unaongozwa naye? Au unataka mamlaka ya
kuwatawala wengine kwa ubatili? Kwa nini nafanya mambo yasiyo takiwa kufanywa
hivyo wakati kila nilichonacho ni sahihi hapa?
Pendaneni kama Mungu na Kristo wanavyotupenda sisi.
[1] Kwa kujibu wa Tafsiri za Kiingereza za The Holy Bible: English Standard Version. 2001 (Pr 29:27-30:33). Good News Publishers: Wheaton
q