Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[114]
Mithali 31
(Toleo La 2.0 19950520-20000211)
Andiko hili lisiloeleweka sana na linalohubiriwa au kufundishwa kimakosa
limefafanuliwa kwa kina kwa malengo ya kiroho. Mara nyingi sana wanawake
wamekuwa wakitiishwa kwa andiko hili kwa teolojia duni na isiyoeleweka. Maana
halisi iliyoko nyuma ya maandiko haya yanayoa nguvu halisi na za kweli kwa
wanawake na wajibu mkubwa zaidi kwa Kanisa.
Christian Churches of God
Email: secretary@ccg.org
(Hatimiliki © 1994, 1995, 2000
Wade Cox)
(tr. 2016)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani
yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe Hakuna malipo
atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu
fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila
kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya
pia yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org
na http://www.ccg.org
Mithali 31
Kuelewa Historia Yake Na Maana ya Kiroho ya Mithali 31
Jarida hili ni
mlinganisho wa Kanisa la Mungu la karne ya ishirini na mwanamke anayetajwa
kwenye Mithali 31. Tutaona jinsi lilivyokuwa limeandaliwa vizuri Kanisa katika
karne ya ishirini ili kuwa ni sawa na mwanamke wa Mithali 31 na jinsi hata kila
mmoja binafsi yake alivyokuwa ameandaliwa kwenye karne ya ishirini na moja ili
kuwa ni mwanamke mchapa kazi aliyenenwa kwenye Mithali 31. Kwa kweli sio
hadithi halisi ya mke wa mtu fulani, bali ni habari za Kanisa likilinganishwa
na Yesu Kristo. Ni habari ya wateule.
Kristo alituambia
wazi sana kwamba mabwana wa Umataifa huwa juu ya watu wao lakini haitakuwa
hivyo kwetu sisi. Agizo kuu kuliko yote kwa Kanisa lilikua kwamba yatupasa sisi
tuwe viongozi watumishi. Tulipaswa kuinua juu na kuwezesha, kuwatuliza na
kuwafariji waliovunjika mioyo, kuwaponya wagonjwa na kuwasimamisha miguuni
mwao, na tulipaswa kuwaandaa Israeli kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Tuliagizwa
kuutangaza wokovu kwa Wamataifa kwa jina lake.
Kanisa kwa
kipindi cha miaka efu mbili limekuwa likipinga utaratibu wa kicheo na madaraja
ya madaraka Kanisani. Wakati wowote inapotokea hivyo, tulishambuliwa na tulishurutishwa
kufarakana kutoka kwenye imani za ukengeufu na tulijikusanya na kujipanga tena
na kuanzisha Kanisa Jipya.
Kwenye miaka ya
1930, kikundi kimoja cha Kanisa la Mungu kilijiunga tena na kikafanyika kuwa ni
kikundi cha muhimu na maarufu sana miongoni mwa Waamerika. Kilianzisha mfumo wa
madaraja wa kiuongozi uliotoholewa kutoka kwenye mfumo wa Kanisa la Kikatoliki.
Kinaweza kuonekana kiuhalisia kabisa kuwa ni kama sehemu ya mafundisho ya
Wanikolai. Mafundisho ya Wanikolai yanaaminika kabisa yalitokana na mtu aitwaye
Nicolaus, lakini ilikuwa ni wazi sana yalitokana na maneno maili. Nikos: ambayo
maana yake ni shinda au kutawala juu ya, na laitoons: ambalo maana yake ni watu
na linalopelekea kuwepo neno laity
kama ni tofauti na huduma. Kristo alisema kuwa anayachukia mafundisho ya
Wanikolai. Jambo hili limefafanuliwa kama jambo mtambuka (sawa na ilivyo kwenye
jarida la Wanikolai (Na. 202)). Sababu inayompelekea Kristo kuyachukia mafundisho haya kwa upande mmoja
ni kwa kuwa yanawafarakanisha ndugu wapendwa. Hayalifanyi Kanisa kuwa mwanamke
wa Mithali 31. Hayamfanyi wanawake walioolewa wachapa kazi wa Kanisani kuwa
mabibi arusi wa Mithali 31. Inatupasa sisi sote kuwa ni wanawake wa Mithali 31.
Mithali 31 haihusiani na wanawake wote kwa ujumla. Sisi sote tumeandaliwa kuwa
mabibi arusi wa Kristo tukiwa tumetiwa nguvu au kuwezeshwa kiroho tukiwa bado ni
wanadamu, na tuwe tumeandaliwa ili kuwa ni sehemu ya Ufalme wa Mungu.
Mambo haya
hayakuwa ya kweli kwa ujumla wake kwa washiriki wote. Kilichotokea kilikuwa ni
kwamba mfumo wote mzima usio wa kimadaraja ya kivyeo uliojaribu na kunuia kuwashaishi
au kuwavutia watu ili kwamba vifanyike kuwa mambo haya. Watu ambao hakuwepo,
walijulishwa, alitengwa, na waliondolewa Kanisani. Walilazimishwa.
Kilichojitokeza ni kwamba kati ya asilimia sitini na sabini ya watu wote
waliobatizwa wa Kanisa hilo katika nchi za Marekani, Australia na Uingereza
waliitwa, wakabatizwa, na walitengwa na Kanisa, wakipokomywa ushirika au walifukuziliwa
mbali Kanisani, kwa kuwa walienda kinyume au haakuendana na na maadili ya
kijamii na kupenda au kutopendezwa na huduma.
Tuna kipindi
kifupi cha wakati ili kuupata ujumbe kwa watu wetu ili kuwafanya watubu, na
kuwalinda. Hii ni kwa kuwa maisha yetu na mfumo wetu umefungamanishwa na kwa
kadiri ile tunavyowatendea watu wetu wenyewe kama taifa.
Dhana
ya kuhusu mahali salama pa kukimbilia hanawatenda wateule na watu wengine
wanaoishinao kwenye jamii zao. Inasababisha mgawanyiko wa kiakili na kifikra
kati ya watu na Kanisa. Na ndiyo maana fundisho hilo ni la uwongo unaoendelea kuaminiwa
kwa kizai kimoja hadi kingine na linakanganya na kenda kinyume kabisa na
mafundisho ya Yesu Kristo aliyokuwa akiyafundisha kwa kupitia manabii na mitume
(sawa na ilivyo kwenye jarida la Mahali pa Usalama (Na. 194)).
Kitakuja kipindi
au wakati ambapo tutaacha kuwaombea watu wetu kwa kuwa watakwenda utumwani,
kama walivyoambiwa manabii “Msiaombee watu hawa”. Lakini hilo silo tunaloambiwa
kulifanya sasa. Itakuwa ni wazi sana wakati tutakapolazimika kuacha kuwaombea
watu hawa.
Ndipo dhana yote ya
kiutabaka ambayo imeendelezwa na mifumo ya kihuduma ya madaraja ya kivyeo
imefanyika vyema sana kwa utiifu wa kijinsia kwenye taasisi kama shughuli au
biashara. Inasimama kwenye kutoshikilia mambo ya kimsingi ambayo ilikuwa ndiyo
msingi wa ubatizo. Mtu habatizwi tu Kanisani. Bali mtu anabatizwa kwenye mwili
wa Kristo. Sisi sote tumebatizwa kwenye mwili wa Kristo, na kama kanisa
linapotoka na kupoteza mwelekeo tunawajibu wa kujiunga tena na kuanza tena,
kama tulivyofanya kwa kipindi chote cha miaka elfu mbili. Haijalishi ni kwa
mara ngapi tunajipanga na kuanza tena, bali kinachotakiwa ni jambo moja tu,
tumtii Yesu Kristo na kuiendeleza injili, na tunakusanyika pamoja tukia ni watu
wenye nia na msimamo mmoja ili tuweze kuifanya kazi na Mungu atatuongezea.
Mchakato wa toba
na wa uongofu na wa kuiosha miguu ya Yesu Kristo, na kuziwemba mbali dhambi
kiasi cha kama umbali wa Mashariki ilivyo mbali na Magharibi, ni ukeli mtupu. Toba
inayoendelea yapasa ieleweke na wote. Mchakato wenyewe ni kwamba mambo yote ya
watu walioitwa na kujiunga kwenye Kanisa. Inawapasa waachane na dhambi zao na inawachukua
muda mrefu. Kazi yetu ni kuwaunganisha pamoja kila mmoja wao, kumfanya kima
mmoja ajisimamie mwenyewe, na kumfanya kila mmoja aimarike. Mchakato huo
umepunguzwa na kuwa si kitu kwenye mfumo wa kingazi za vyeo au madaraka. Na hii
ndiyo sababu iliyompelekea Kristo kuwasimanga kutokana na jinsi walivyokuwa
wanatawala.
Mfumo na
utaratibu wa Mungu siyo wa kingazi za vyeo kwa maana ya uongozi wa kiutumishi.
Una mamlaka, lakini mamlaka hayasababishi kuwepo kwa aina ya matokeo ambayo
yanafanya na watu wa dunia kupitia mamlaka zake hizi za kivyeo. Tuna tofauti za
kingazi za madaraka kwa maana ya mtiririko wa kuanzia Mungu, Kristo na Kanisa,
lakini hiyo haisababishi kuwepo kwa mahusiano ya dunia. Kwenye ngazi za vyeo
vya kidunia, watu hudandia kwenye migongo ya ndugu zao ili wapate vyeo, na
wanaviona vyeo kwa namna nyingi sana za kiujanja. Wanaweza kupewa kazi ndogo
ndogo za kufanya sawasaa na uhusiano wao na huduma. Na iwapo kama hawana
manufaa sana kwenye huduma, wanapewa upendeleo mdogo. Na kama watakuwa na sifa
mbaya kwenye huduma, wanaweza kudhalilishwa kwa azi sana. Watu wanadhalilishwa
kwenye mfumo kama huo kwa kuwa haaendani na mchakato uliowekezwa ndani yao.
Watu wameandaliwa kifikra kwa kuwafanya wafikie kujisikia wapo kwenye
mkandamizo hadi wakati kama ule ambao wanageuza na kurekebisha njia za mwenendo
wao, ili kuenenda sawasawa na mwenendo ambao umeanzishwa Kanisani na kisha
kusimamisha utendaji kazi wa hukumu yao. Utaratibu wa ngazi za kivyeo umebuniwa
ili kuahirisha hukumu ya kila mmoja na kulazimisha ukiri au utiifu kwenye mfumo
wa kimamlaka, ili kufanya kusiwe na hasira au uchungu wa kiroho au kisasi. Hii
ndiyo sababu ambayo chama cha Manazi kiliweza kisitisha hukumu ya kile
kilichoonekana kuwa ina mashiko kwa mwanadamu na kulazimisha kutokea kwa mauaji
mabaya ya holocaust. Mauaji haya ya holocaust yalikuwa ni matokeo ya moja kwa
moja ya usitishaji huu wa mfumo wa kiimla. Mfumo ule kwa jinsi ulivyo tu
ulibuniwa na kuratibiwa vizuri na Makanisa Makongwe ya Kanisa la Roma na Kanisa
la Kilutheri huko Ulaya hata kabla ya kuzuka kwa Vita Kuu ya II ya Dunia. Kama
Kanisa la Mungu, chini ya mfumo ule, lingepewa utawala au mamlaka huko
kusingekuwa na tofauti yoyote kati yake na chama cha Manazi, kwa vyovyote vile.
Angeangamiza makabila na vikundi na watu.
Dhana hii yote na
ile unabii ulioshindwa na ya jaribio muhimu la fundisho la Kanisa linafanya kuwe
na mfungamano wa madaraja ya vyeo vya Kanisa ili kwamba wale watu wanaotathimini
kwa kina mambo washambuliwe. Hii siyo sauti ya mchungaji. Ni nini walichukuwa
wanakifanya watu wa Beroya? Walikuwa wakiyachunguza Maandiko Matakatifu kila
siku na kuyapitia kwa kina kwa kulinganisha mambo yote, waone kama ndivyo
yalivyo. Hebu thibitisha mambo kama yana
ukweli au uwongo na utendee kazi uthibitisho ule. Mfano mmojawapo wa jambo
hili ulionekana kwenye matokeo ya jarida la Mteule Kama Elohim (Na. 1). Liliwekwa kwenye mtandao wa kielektroniki
na lilijadiliwa nchini kote Marekani. Mhubiri mmoja wa Kimarekani alitoa
mahubiri yaliyosema (akimshambulia mwandishi) kwamba Waberoya walithibisha mambo
yote, lakini hiyo ilimaanisha kuwa waliyachunguza Maandiko yote Matakatifu kila
siku na wakathibitisha kuwa kila kitu ni kweli. Hawakuyacgunguza mambo yote na
kuyaona kuwa ni uwongo, na kama walikuwa hawaelewi, basi hawakuwa anaandika vitisho
au mambo kama hayo. Walingojea hadi Kanisa lilipowaelewesha, na kama iliwachukua
miaka kumi na minne au zaidi halikuwa tatizo kwao. Walikaa tu na kuyachunguza
mambo yote kuwa sahihi, na siyo uwongo. Aina ile ya tabia na mwenendo usio na
ubaguzi unasababisha kuwa na upotofu wa kuridhia au kukubali na kuhiyari, na unapelekea
kutokamilika maendeleo ya kiroho ya mtu. Mkabiliano unakomesha uezo wa kila
mmoja wa kujiongeza kiuwezo kwa jina la Yesu Kristo. Inaifanya kazi ya adui
badala yake.
Matokeo yake ya
mwisho ya miaka ya chochote kilicho kwenye huduma kimepasa kumfanya mteule
atoke nje ya dunia na wadumazwe kifiziolojia na kisaikolojia kwa kiwango cha
vile walivyofanywa viwete. Ni kazi na wajibu wetu kulia na kuwajenga watu.
Sasa, tutajionea kwenye Mithali 31 ikisema hivyo.
Andiko
Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwenye Mithali 31 wakati inapotazamwa
kwa ukamilifu wake na kwenye uhusiano wake na lengo la kiroho. Kwa ujumla wake
imechukuliwa kuwa ni kama mgawanyiko wa kwato mbili lakini haikupasa ipasuke
kwenye kwato mbili. Mithali 31 ni somo la kiroho kwa uwezeshaji wa Kanisa pia. Hebu na tuiangalie hiyo Mithali 31:1-2
Mithali 31:1 Maneno
ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.
Mithali 31:2 Ni
nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa
nadhiri zangu?
Sasa aya hizi
mbili za kusisimua zina matokeo ya wazi sana. Mfalme Lemueli hakuwepo. Hakuna
kumbukumbu yoyote ya kuwepo kwa mtu yeyote yule aliyeitwa Mfalme Lemueli kwenye
historia ya wafalme wote wa Israeli. Basi huyu Lemueli alikuwa ni nani? Je,
neno Lemueli linamaana gani? Je, halimaanishi tu kuwa ni mfalme wa kimfano tu? Maneno
yanalosababisha kuwepo kwa neno Lemueli mi mawili: Lemo (kuelekea) na El au
Mungu, na linamaanisha kumwelekea Mungu au
aliyewekwa wakfu kwa Mungu (kwa mujibu wa Isaiah da Trani, Mesudath David; tazama
lwenye Soncino). Hii inahusiana na madhumuni na maana iliyo kwenye andiko la
Yohana 1:1: Hapo mwanzo kulikuwako
Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,
naye [elohim: Zaburi 45:6-7] alikuwa Neno (sawa na ilivyo kwenye kitabu cha A.E. Knoch, Concordant Interlinear NT)
Huu pia ni ujumbe
kwa Wateule. Dhana hii imeendelezwa na marabi (kama kuhusu Aguri; Soncino) kwamba
mama yake anasema kimsingi kabisa kabisa: Ni
nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? na Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu Kama lawama. Mama huyu anadhaniwa kuwa ni Bathsheba,
na kwamba huyu Lemueli alikuwa ni Sulemani. Kwa kulijaribu andiko la mama wa
Sulemani, habari yake iliyopo kwenye Midrash inahusiana na kwamba Sulemani
alimuoa binti wa Farao katika siku ya kuliweka wakfu Hekalu. Alimfanya awe
macho bila kulala usiku wote mzima kwa sauti ya muziki na kumfanya achelewe
kulala hadi asubuhi, na kakuwa alipokabidhiwa funguo za malango ya Hekalu wote
na kuzitunza chini ya mto wake wa kulalia basi utoaji wa dhabihu za asubuhi
ulichelewa, na ndipo mama yake alipokuja na kumpa nasaha zifuatazo. Maana yake
yalieleweka kwa marabi. Walilihusianisha andiko lile la ufunguaji wa Hekalu na
binti wa Farao ambaye alikuwa ni Mmisri. Dhana ya kuoa wanawake wa kigeni, au
Wamisri (wakidunia) kipindi cha kabla ya kuikalia nchi ya ahadi, kinawafanya
Wateule wasombe na kuwekwa mbali na majukumu yao ya kulifungua Hekalu kwa kuwa
ni sehemu ya msingi na mawe ambayo kwayo Hekalu linajengwa juu yake. Ilikuwa ni
siku ya kuliweka wakfu Hekalu ndipo inadhaniwa mambo haya yenye kukanganya
yalitokea. Maana yake ni kwamba andiko hili linahusiana na suala la kutabarukiwa
kwa Hekalu. Yatupasa tuwe makini na wala tusikepe au kuchepushwa na mambo
mengine yasiyo na ulazima. Maneno yaliyotangulia yasemayo: “Tena ni nini,
mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?” huenda yamefupishwa kutoka kwenye maneno
yasemayo ni kitu gani ninachotaka kusema
kukuambia wewe? nk. ambalo ni karipio la kwanza kwa utelekezaji wa kazi au
majukumu ya Hekaluni (soma pia kitabu cha Isaiah da Trani).
Kwenye aya ya
tatu inasema:
Mithali 31:3 Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo
wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.
Andiko hili
linamaanisha kuuhudumia au kuutunza ulimengu. Maneno yasemayo: kwa yeye
awaangamizaye wafalme, yanamaanisha moja kwa moja kwa anayesababisha wafalme wafutiliwe mbali – kwa maneno mengine, kupoteza
kiroho chetu. Kwa hiyo lengo la wazi la kuwafanya wafalme waondolewe mbali ni
kuwarekebisha tabia na mwenendo wao ambao unaweza kuwapelekea watu waasi kwa
idadi yao kubwa na kuangamiza kizazi cha kifalme. Kuangamiza na kukomesha
kabisa kwa wafalme ni mfumo wa lugha ya Kiaramu, (Ibn Ezra) kwa hiyo hakuna shaka
kabisa kuwa ni neno la uwingi kuhusu waflme. Jambo lililokuwa likijadiliwa hapa
ni kuhusu Mteule na kitendo cha kuwafanya au kuwaezesha Wateule wawe wafalme na
makuhani kwenye Ufalme wa Mungu. Aya ya nne inasema:
Mithali 31:4 Ee
Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu
waseme, Ki wapi kileo? (Soncino))
Sasa dhana hii ni:
Haionyeshi kabisa wafalme wakiwa wamelewa. Inawafanya wasiheshimike, na
kuondokewa na heshima kwa wanaowaongoza pamoja na kupotosha hukumu na kutengea
kazi mambo yao ya kimwili. Kwa hiyo hatuongelei kuhusu kitendo chenyewe cha
kunywa mvinyo, bali tunaongelea kuhusu ulevi. Anachomwambia Lemueli hapa
anasema kwenye tafsiri ya Soncino inasema:
Neno la Kiebrania la
jina hili ni Lemoel, huenda ni
mtabahinisho wa kutoka kwenye muundo na uandishi wake, ni kama kusema hii kwa
hakika haitokani na mtu mwenye jina na maana yake “(ametengwa na kuwekwa wakfu)
kwa Mungu” (Rabbi Rashi)
Rashi alijua
kwamba ni kama iliwekwa wakfu kwa Mungu na kwamba haikuwa sahihi kwa hakika kwa
wale waliowekwa wakfu kwa Mungu. Kwa maneno mengine ni kwamba inaalenga
Wateule. Maneno ya kusema wanapugua
kwenye maandiko lakini dhana inahitajika kwenye neno kere au iko wapi?
(Ralbag, Isaiah da Trani; Soncino.) Je,
haiwafai Waflame (kusema) Kikowapi kileo?
Wssije wakanywa na kusahau kile kilichoamriwa na kuipotosha haki kutokana
na vile walivyo athirika. Dhana hii inamaanisha kwamba Mteule anaweza kuwa
amelewa kutokana na kunywa kileo kingi na kwa sikukuu zao na kwa maisha yao
wenyewe binafsi na kuisahau sharia na, pia, kwa kuisahau sharia au torati na
hatimaye wanaipotosha haki kutokana na chochote kinachoonekana kuwasumbua au
kuwatesa.
Mithali 31:5 Wasije
wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
Kwa Kiebrania ni
neno la umoja; na kila mmoja wao hunywa na kuisahau aya ya 5 (Daath Mikra), na
kwamba kile kilichoamriwa kinaeleweka au kujulikana (na Meiri) kuwa ni sharia
za kitaifa, na hivyo kuwa ni sharia isiyo ya kikatiba kabisa. Dhana ya
kuzisahau sharia za kitaifa na kuyafanya mambo kinyume na sharia kabisa kulionekana
au kulichukua taswira kwa Wateule kwa kipindi cha zaidi ya miaka arobaini.
Tumeziona katiba za makanisa zikichanwa na kukiukwa sana; tumeyaona makabrasha
yaliyovunja kiapo yakiwasilishwa au kupelekwa kwenye mamlaka za nchi.
Tumejionea namna nyingi za udhalimu na uvunjifu wa heshima na ufujaji mkubwa
kubwa za fedha, ambazo ni kama yalivyo mambo haya, kama kujinyima au kujitenga
na starehe, yakifanyika kinyume na malengo au makusudi ya kanuni na miongozo ya
kibiblia kama tutakavyoeza kujionea kutokana na malengo yaliyo kwenye aya ya 5 ya
Mithali 31. Maafisa au viongozi walikiuka mambo ya haki. Watu walienda na
wamefuatilia haki zao na hawakupata chochote. Kwa kweli, wengine wamefikia hata
kutengwa au kupokonywa haki yao ya ushirika kwa kuwa walikuwa wamesema ukweli
fulani. Watu wengine wamekuwa akilaghaiwa na kudanganywa na kuteswa na hawakujumuishwa,
na kwa hiyo, walivunjwa moyo. Dhana hiyo hasahasa wameambiwa Wateule hapa, kwa
hiyo haki na utakatifu ni neno hilihilo moja na lina maana hiyohiyo moja kwenye
Kiebrania. Kama tutaipotosha haki, basi tutakuwa tunaupotosha utakatifu. Ni
kitu hichohicho kimoja. Hatuwezi kuwa watakatifu pasipo kuwa watu wa haki.
Kanisa linao
wajibu wa kuhukumu mambo yake lenyewe. Kama mtu ataleta kesi Kanisani, Kanisa
linapaswa lihukumu kwa uangalifu mkubwa na kwa haki. Hatupaswi kuwampendelea
watu, na hatupaswi kuipuuzia au kuidharau haki. Na wala hatupaswi kuichelewesha.
Inapasa ichekechwe kwa kina na kumalizwa, na yapasa ifanywe kwa huruma na
izingatie rehema. Kwa hiyo sehemu kubwa zilizopelekea Kanisa la karne ya
ishirini kushindwa kwenye uingizaji au utiaji huu wote yaliyoko hapo hadi hapo
chini kwenye aya ya 5. Sehemu kuu moja ambayo Kanisa limekuwa likikabiliana
nayo ni kuabudu miungu ya uwongo. Mengi yameshindwa kwa kuwa hayakuwa
yamevuviwa na kutiwa nguvu ya kujiendesha au ya kuendelea mbele. Yamefanyika
viwete pamoja na waumini wake; yakijifungamanisha kwenye taratibu za masharti
na mazingira yao. Watumishi wake wamejikuta wakiwa kwenye vilio na kutokwa
machozi kwenye kipindi chote cha mchakato huu. Imetabiriwa kuwa itakuwa hivyo.
Wote wataomboleza kutokana na mfumo huu wote mzima lakini wamenaswa kwenye
imani ambayo imewakamata na kuizoea kiasi cha kana kwamba hakuwa ndugu wapendwa
wowote walio na uwezo wa kutenda matendo ya kutoa hukumu ya haki na, bali pia
na hata huduma zenyewe hazina uwezo wa kutoa hukumu ya haki mtu akatenda kwenye
utoaji hukumu yenye mashiko kwa mtu. Ni lazima sentensi zitolewe kutoka kwenye
hukumu yetu.
Sasa kama
tukisema kuwa suala lenyewe ni ibada ya sanamu, basi yatupasa tuitendee kazi
hukumu tunayoiweka. Mtu anaweza kusema, “hivyo si sahihi, bali mimi nitaendelea
kufanya makosa, Kristo ndiye ajuaye; Kristo ataingilia kati”. Tumekuwa tukitiwa
nguvu na Yesu Kristo kuhukumu na kutenda mambo kwa hukumu hiyo. Tunapouchukua
mfumo wa kimilenia, tutahukumiwa kwa jina la Yesu Kristo. Kristo haendi kufanya
kazi kwa niaba yetu. Bali Kristo anakwenda kuingilia kati kama tuko mahali
fulani huko Asia, tukiyatenda mambo lutoka Yerusalemu, tukiyatazama mataifa.
Tutapewa mamlaka ya kutenda hivyo. Tutaona hilo baadae kwenye kitabu hikihiki
cha Mithali. Ni kupewa kwetu mamlaka ambako kunatufanya tufanye mambo na
yatupasa tutiwe nguvu ya kutenda kazi chini ya uwakilishi huo. Kile
kinavhotokea ni kwamba Kanisa limekuwa likijivuta vuta kwa mwendo wa kiwete.
Uwezo wa watu kutenda kazi chini ya uwakala huu na kutenda mambo kwa hukumu ya
haki unasuasua. Kwa hiyo, kimsingi haiwezekani kujisukuma yenyewe kwa matendo
yaliyotuama kwenye maarifa ya kweli na ya uwongo. Hilo ni kosa kubwa sana
linalomfanya mtu asistahili kuuingia Ufalme wa Mungu, na ndiyo maana Kanisa
litatapikwa litoke kwenye kinywa cha Mungu.
Inasema kwenye
aya za 6-7
Mithali 31:6 Mpe
kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. 7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu
yake.
Wazo la kuutoa
kinywaji kikali au kilevi ingawa ni cha zaidi ya hali ya kujing’ima limekuwa
likilaumiwa na ulevi umepinga vikali sana; ni kutokana na Mithali 23:29ff. Ilikubalika
na kuungwa mkono kuwa ulevi ulikuwa ma matumizi yake sahihi. Mvinyo huleta furaha moyoni mwa mtu kwa mujibu
wa Zaburi 114:15 na uliumbwa na Mungu kwa malengo hayo.
Kama mfalme atajifunza
kujizuia kuto kunywa kileo, yeye pia alikuwa na jukumu la kugawa mvinyo kwa
wale waliopenda kunufaika kutona nao, (kwa mujibu wa Saadia Gaon; Soncino).
Utoleaji huu wa
mvinyo ni kutolewa kwa kiini, na utolewaji wa nguvu za kiroho. Viongozi wote
walikuwa na wajibu wa kuwatia nguvu wasaidizi wao na waliokuwa wanawaongoza kwa
maana ya kutenda na kuelewa kwa maarifa na haki. Hayo ni maandalizi ya
watakatifu. Kwake yeye ambaye yu tayari
kupotea inamaanisha ni kwa wale waliopondeka rohoni na waliopitia au kuitwa
kwenye kundi la Wateule. Wametolewa kwa Wateule ili watiwe nguvu. Wanahitajika
kufungamanishwa na kupewa msaada wa kimarejesho. Wazo la kunywa kileo ni wazo
la kuweka wigo au uzio tu. Mara nyingi, watu wanaolaghaiwa kufanya hila wamepewa
mbinyo wa kilevi cha aina ya brand kama kileo kikali kama ilivyorejeshwa upya,
na hivyo ndivyo ilivyojulikana na marabi. Uchungu
wa nafsini ulijulikana kuwa ulimaanisha kutaabika
kwa maumivu makali ya kiakili, na kwa wale wanaoteseka kwa maumivu ya
kiakili au kifikra (Rashi anaamini) ilitenda kazi kama kitia hamasa au kiamsha
hisia. Dhana hapa ni kwamba kuna jambo na maana ya kiroho kwenye mvinyo huu.
Inataja sadaka ya mvinyo na sadaka ya kinywaji, na kwamba tumemiminiwa sadaka
ya kinywaji na Bwana kwa namna nyingi.
Maendeleo yetu ni
kama hivyo kwamba tuna wajibu wa kushikamanisha pamoja madogo ya sisi sote,
kumuinua juu kila mmoja, na kuwapa faraja na kuwatia moyo. Siyo suala tu la kusema,
“Ooh, waone wale, ni wadhaifu kiroho”. Sisi sote tu wadhaifu kiroho kwa namna
moja au nyingine. Uimara wa kiroho una wajibu wake wa kuwainua na kuwaleta walio
dhaifu zaidi kiroho na kuwafikisha kwenye kiwango chao tarajiwa. Sisi sote tuna
wajibu wa kujiandaa ili kuifanya kazi kubwa zaidi. Tunapaswa kuiinua juu idadi
kubwa ya watu walio na uwete wa kiroho. Ndipo nadharia hii inaenda hadi kwenye
kanuni ya haki. Aya za 8 na 9 vinasomeka hivi:
Mithali 31:8-9 Fumbua
kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao;
9 Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie
maskini na wahitaji haki yao.
Dhana ya ububu imewekwa kwa lugha ya mfano. Ikiwa kwa sababu yoyote ile mtu
hataweza kusihi mambo yake mwenyewe (kwa mujibu wa Metsudath David; Soncino), uwezo
unahitajika wa kuwa wasemaji. Wanatakiwa kuhakikisha kwamba kila mmoja anaelewa
mambo muhimu ya sharia nay a wokovu. Ateule wanahitajika kunasibu mambo yao
kwenye maombi. Mtu hawezi kumtia nguvu mtu mwingine bila ya mtu mingine kuomba
na kufunga kwa ajili yao. Daudi aliomba na kufunga kwa ajili ya adui zake.
Kulitakiwa kuwe na dhana ya marejesho mema nay a kistaarabu. Badala yake, kile
tunachokiona ni wazo la kwamba “Bwana,
mshugulikie mtu yule, mvunje, mnyenyekeshe, mwangushe hadi chini”. Sisi sote, kwa hatua ileile, tumekua na
hatia kwa viango vingi mbalimbali. Mchakato ule wa dhana ni urithi wa
kujihesabia haki. Kujihesabia haki ndiyo dhambi pekee ambayo haiwezi
kushughulikiwa na Mungu kwa kuwa inamfanya mtu ashuke chini na sisi tuinuke
juu. Na ndiyo maana iliyomfanya Kristo kutoa mfano wa Farisayo na mtoza ushuru
(mkusanyaji wa ushuru), ambapo mtoza ushuru alisema, nihumie mimi mwenye dhambi, na Farisayo alikuwa anasema, nakushukuru,
ee Bwana, kwa kuwa mimi sipo kama watu wengine.
Wazo lenyewe
yapasa liwe kwamba tunawaheshimu wengine vizuri zaidi kulio sisi wenyewe, na
kwa kufanya hivyo tunawainua watu wengine. Hili ni moja ya sababu kwa nini
mfumo wa uongozi wa kimadaraja kila mara unaanguka chini, kwa kuwa watu wanaopenda
kupanda juu ndiyo wale wasiostahili kabisa kupanda juu. Hili ni suala la
kuliangalia na kujihadhari nalo. Watu wakuu na walio kimbelembele na
wajipendekezao ndio watapewa kipaumbele. Wenye mwenendo au tabia ya kujikomba
na kujipendekeza watatunukiwa zawadi ili kwamba waweze kuwarudisha nyuma
Wateule, kwa kuwa Wateule wanawachukulia wengine vizuri kuliko wao wenyewe.
Watu walioongoka ambao wanafaa sana kuchukua nyadhifa wanasema, “oo hapana, yeye ni nzuri na anafaa kufanya
hivyo, nadhani yatupasa tumpe fursa”. Haya ndiyo mawazo aliyonayo mwongofu,
na ndiyo maana wakati wote Wateule wanaishia mwanzoni chini bila kupandishwa
daraja lolote lile, kwa kuwa wao huwainua watu juu kuliko wao wenyewe, na watu
hawa ambao wao wenyewe wanakuwa hawajaongoka wanakimbilia au kuvutiwalia na nafasi
hizo kwa lengo la kujipatia madaraka. Wanapenda kujikweza juu hadi kileleni na
wanaposhindwa kujipatia njia zao wenyewe ndipo wanajaribu kuyavuruga mashirika
kwa kuyagawa na hata kuyavunjiliambali au kwa kufanya kitu kingine zaidi.
Lakini mchakato wenyewe halisi ni kwamba tunapaswa kuwajenga n kuwainua watu
juu. Na kama kuna kitu kiko vibaya basi tunahiyari ya kusema hivyo.
Wakati Musa
aliposhuka chini kutoka kwenye mlima wa Sinai na kisha wao wakajitengenezea ndama
wa dhahabu, Musa alifanya kitu kimoja. Wala hakusema, “Oo sawa, wenzangu nisikilizeni, Nadhani tupige kura”, au “tutamngojea Kristo afanye kitu fulani”. Musa
alichukua hatua moja kwa moja. Alisimama upande na kuufuta upanga wake na akiwa
pamoja na Walawi akawaua watu takriban elfu tatu (Kutoka 32:24-28). Sasa hii
inatuambia jinsi Yesu Kristo alivyoshughulikia jambo hili. Na hivi ndivyo jinsi
Kristo anavyoingilia kati, kwa kuwa anatutia nguvu sisi jinsi ya kutenda, na huo
ndiyo mfano ambao unapasa utumike. Wakati Fineusi alipoona ibada ya sanamu alitembea
ndani na kulirusha panga lake kwa watu hao wawili waliokuwa hemani. Hakungojea
hadi kuambiwa.
Mchakato wa
kuwatia nguvu watu na kuwaambia watu walio mabubu kuwaongoza waelekee kwenye hukumu
ya haki ni kitu cha kama wale ambao hawawezi kupata hukumu ya haki ni lazima
wahakikishiwe hukumu ya haki na Wateule. Yatupasa kuichunguza dunia,
kuyashughulikia mahitaji ya watu wetu. Hivyo ndivyo tunavyoweza kufanya kwenye
kipindi cha Milenia. Tunakwenda kuichunguza dunia na kuwainua watu na kuongea
nao. Sauti itakuwa sikioni mwao ikisema, hii
ndiyo njia, ifuateni. Hivyo ndivyo tunavyokwenda kuwa sisi. Tukiwa kama
viumbe wa kiroho itatupasa tutiwe nguvu kuwachukua watu hawa wote. Kwanza
kabisa itatupasa kujifunza kufanya hivyo hapa. Yatupasa kujifunza kuweza kunena
masikioni mwa watu wanaohitaji mwongozo, na ndiyo maana yatupasa tujifunze
kuongea.
Wazo lililo kwenye aya ya tisa ni, Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie maskini na wahitaji
haki yao. Aliyepangiwa uharibifu maana yake ya moja kwa moja ni, wana wote
wa kupita, na Rashi anafafanua hii kuwa ni kama mayatima waliopoteza walinzi
wao, na Ibn Ezra, kama mtu aliyehukumiwa hukumu ya kifo; hicho ndicho
linachomaanisha andiko hili. Wateule wote wa taifa la Israeli na ambao hawajaitwa
bado wapo chini ya hukumu ya kifo. Sisi hatupo chini ya hukumu ya kifo. Bali tupo hukumuni
sasa. Kwa hiyo tupo kwenye wajibu wa kuwaambia Israeli walio kwenye hukumu ya kifo.
Yatupasa kuwainua juu watu hawa.
Meiri na Isaiah
da Trani wanalifafanua andiko hili kuwa linamaanisha, wenyemili wote ambao hatimaye watapita kwa kufa hapa duniani. Kwahiyo
tunaona, marabi walielewa mfano wa kina wa jambo hili. Ni Ufalme wa Israeli
ndiyo uliokuwa na wajibu huo. Hawa ni wafalme (Wateule) walio na wajibu kwa
wote wenye mwili, kwa kuwainua juu na kuongea na wao walio mabubu. Tuna wajibu
wa kuomba dua kwa Mungu, kwa kupitia kwa wazee ishirini na wanne, kwa kuongea
moja kwa moja na Mungu kwa jina la Yesu Kristo ili kwamba Malaika wa Mbinguni, chini
ya muundo wake, Baraza lake, wawaombee moja kwa moja, na watatenda kazi kwa
maombi yetu. Na ndiyo maana wazee ishirini na wanne mahala pao wana vikombe
vilivyojaa maombi ya watakatifu; vikombe vya dhahabu. Ni maombi yetu ndiyo
yanayowaombea mabubu; kwa wenye mwili waliokusudiwa kukumbwa na maangamizi.
Hili si kuwa ni agizo tu kwa Mfalme Sulemani. Bali hili ni agizo la kiroho
kwetu sisi. Sulemani hakuwatawala watu ote wenye mwili.
Kwa hiyo sisi
tunapita kenye sehemu ya kwanza inayohusiana na Ufalme, na wafalme hawa kwa
hakika ui mabibi arusi wake Kristo. Na ndiyo maana Mithali 31 ina sehemu mbili.
Aflame wenyewe, Wateule, wapo kwenye haiba mbili kwa kweli, wafalme na
wanawake. Kuna maana kuwili kwenye Mithali 31. Kila mmoja wetu ni bibi arusi wa
Kristo.
Mithali 31:10-11 Mke
mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. 11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
Sasa hii
inahusiana na mfano. Mume wake, Yesu Kristo analiamini Kanisa, na Wateule na hapungukiwi
faida, kwa kuwa Wateule wanamfanyia kazi Kristo kwa kuwaleta watu hukumuni. Kwa
mujibu wa vitabu vya ufafanuzi vya Soncino kuhusu dhana ya kuwa mke, utahwaji
umefaywa mara nyingi kuhusu mwanamke asiye mwaminifu kwenye Mithali na kwamba
yawezekana kuwa mtunzi alidhania ni busara kuhitimisha kitabu kwa kumsifia vya
kutosha mke mwema. Hivi sivyo ilivyokuwa kabisa. Kitabu hiki cha Mithali
kimeishia kwa kumsifia vya kutosha Mteule na wajibu wake uliopo kwenye kitabu
chote cha Mithali, na busara iliyotolewa kwa njia ya Roho Mtakatifu ya kuwatia
nguvu Wateule katika nyakati za mwisho ili waweze kuja hukumuni. Ndiyo maana
sura hii inahitimisha kitabu cha Mithali.
Kazi yenyewe iko
tofauti na ni utunzi unaojitosheleza kama inavyoonekana wazi kutokana na ukweli
kwama imefanyizwa ndani ya utaratibu wa kichemshabongo ya kialfabeti.
Mwanamke mwenye
busara na mwema ameelezewa kuwa ni msimamizi mahiri wa nyumba, nan i Baraka kwa
familia yake. Mumewe anawezeshwa kuyamudu masuala ya umma, na mi mtu
anayeheshimika kwenye jamii. Maisha yake hayana ubinafsi au mwenye kujijali na
kujivuna; anawapenda na kuwahudumia maskini, na nimmwema kwa watu wote. Imekuwa
ikisemwa kweli sana kwamba, ‘Hakuna kinacholinganisha maandiko ya zamakale na huu
ni uthibitisho au ushuhuda wa muhimu na heshima na utu binafsi wa mwanamke’ (kwa
mujibu wa Abrahams; Soncino). Inawezekana sana, shairi hili lilikuwa ni kazi ya
mwalimu aliekua anaunga mkono na kushadidia maisha ya nyuma za waishio ndoa za mke
mmoja kwa namna iwayoyote, konsonanti zenye mtazamo mzima wa kwenye kitabu chote
cha Mithali, nyumba yote ilikuwa imetawaliwa na mwanamke mmoja. Kwa mujibu wa
matumizi ya kimapokeo, shairi hili linatumiwa kuimbwa kwenye nyumba za Wayahudi
kwenye mkesha wa Sabato (PB. p. 123). Inaeka kiwango kikubwa na cha hali yha
juu sana cha umwanamke, ambayo ilitoholewa, na lilikuwa halisi kwenye nyumba
nyingi za Wayahudi (Soncino).
Sababu iliyofanya
liimbwe kwenye mkesha wa Sabato ni kwamba tulikuwa tunatumika ili kwamba dunia
iingie kwenye Sabato, Mapumziko ya Milenia ya Yesu Kristo, na tunafanyika kuwa
mabibi arusi wa Yesu Kristo ili kusaidia kuendelesha maongozi ya familia ya
mwanadamu. Kwa hiyo ndipo tunatenda mambo kama wazazi pamoja na Yesu Kristo ili
kuileta familia ya mwanadamu kwenye hukumu na kwenye wokovu. Tumepewa taswira ya kuwa kama mabibi arusi
wa Kristo wa familia ya mwanadamu.
Wazo la imani ya dothi salama ni kwamba mume ana
imani kubwa kwa mpangilio na uongozi wake wa uchumi wa nyumbani (kwa mujibu wa
Metsudath David). Wateule hapa ndio wanaoendesha shughuli za kiuchumi wa nyumbani.
Kinachojitokeza kwenye mifumo ya madaraja ya kiuongozi ya Kanisa kama walivyokuwa
wamefundisha ilikuwa ni hivyo kwa kuwa mtindo wa kuhaulisha madaraka au mamlaka
ulishinikizwa kwenye kwenye huduma hadi kwa mtu binafsi mmoja mmoja
waliokusudia kutompa nguvu. Wanaume walitendea kazi kile kilichoachwa na
mamlaka ndogo kwa kuwaambia wake zao jinsi ya kutumia majiko, jinsi ya kufanya
majumbani, ni kiasi gani cha fedha kitumike, au na mengineyo. Uhaulishaji wa
mamlaka kwa kweli uliiba mamlaka kutoka kwenye viwango ambavyo kwavyo vingeweza
kutendea kazi. Kanisa la sasa la Mungu, kwa tabia mkabiliano wake wa kimamlaka,
liliathiri uwezo wa watu kujaribu kupambanua hukumu kwa viwango vyake vyote.
Hili ni kosa amalo linapasa kulishinda. Watu wanapaswa wafundishwe jinsi ya
kutiwa nguvu kama Mithali inavyowahamasisha watu.
Siyo kushindania
madaraka. Ni suala la kuitendea kazi hukumu isiyo ya ubaguzi kwenye kupenda
uhusiano. Sasa hiyo inaendelea mbali zaidi ya familia ya kila mmoja kwenye
Kanisa kwa ujumla. Mamlaka hayapasi kuchukuliwa; bali kwa kweli hukabidhiwa.
Kadiri mamlaka yanavyotplres ndipo huepo na umahiri zaidi na uwajibikaji na
ukomavu kwa watu ambao kwao mamlaka hayo yalitolewa vitakapokuwa. Yatupasa kuwatumikia
watu ili kuwafanya wachukue nafasi zetu nia yetu ni kumfanya kila mmoja
Kanisani amudu kuifanya kazi ya huduma, kila mmoja. Wakati tunapomfanya kila
mmoja kufika kwenye kiwango kizuri cha uelewa pale walipowezeshwa wakiwa kama
mabibi arusi wa Kristo, ndipo tutakuwa tumelifikia lengo letu na tunawaleta
watu wengi zaidi na zaidi kanisani, kwa lengo la kuwainua juu kwenye kiwango cha
pale walipowezeshwa na kutiwa nguvu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Ni suala la
kuandaa majeshi ya watumwa. Ni suala la kuandaa majeshi ya wana wa pekee wa Kiroho
wa Mungu mwenye uweza. Sasa tunakwenda kwa kupitia andiko linalofuati.
Mithali 31:12 Humtendea
mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
Hii inamaana
kwamba uhalalishaji kamili wa kujiamini anapokuwa naye na anapomuweka mahali.
Mithali 31:13 Hutafuta
sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
Maana yake ni
kwamba anajiona au kujichukulia mwenyewe kuona kwamba kuna mgawanyo mkubwa wa
mali au malighafi ambayo kwayo yanaweza kutumika katika kutengenezea nguo muhimu
(hiyo ni kwa mujibu wa Rashi na Metsudath David). Dhana yenyewe ni kwamba
Kanisa linaandaa mavazi kwa ajili ya watu wengine, kwa ajili ya watoto au
familia. Tuna wajibu sio tu wa kuandaa mavazi yetu peke yake bali pia kuyaandaa
mavazi kwa ajili ya watu wengine ili kuwasaidia kuingia hukumuni, na
kuwahakikishia kuwa kuna mgawanyo mkubwa wa mavazi haya kwa ajili ya hukumu.
Kwa maneno mengine, ni kusema kwamba tuna wajibu wa kuandaa taarifa na chakula
cha kiroho kitakachowafanya watu kuvikwa kwenye mavazi ya haki na utakatifu, na
tunafanya hivyo siyo tu kwa njia ya kuyachapisha neno la Mungu bali pia ni kwa
kujichunga nafsi zetu wenyewe na kujaliana kila mmoja na mwenzake, na kwa
ulimwengu, kwa kupitia maombi yetu na maendeleo yetu.
Wazo au dhana ya
kwamba matendo ya hiyari pamoja na mikono yake vinaendana pamoja, anafanya kwa mujibu sawa na ipendavyo mikono
yake.
Anatengeneza malighafi
kuwa mavazi mazuri sana, kazi yake hufanyika kuwa ni moja ya mambo anayopendezwa nayo. Ni kana kwamba
mikono yenyewe, inapenda sana kufanya kazi, (kwa mujibu wa Rashi; Soncino).
Hii ni amani na
furaha inayotokana na Roho Mtakatifu. Mataifa yetu yote yanapaswa yawe na amani
na furaha na upendo, na amani yetu inapita uelewa wetu wote.
Mithali 31:14 Afanana
na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
Sasa usemi wa kama merikebu za biashara unachukuliwa
kuwa unamaanisha ambayo inaingiza bidhaa
kutoka nchi za mbali;
Ni sawasawa na
kusema, yeye hategemei vitu anavyovitoa na kuvigawa kutoka kwenye vyanzo
vilivyo karibu na mkono wake, bali anavitafuta kutoka nchi za mbali zaidi, ili
kupata chaguo lake kubwa kuliko yote ili lipatikane (Daath Mikra; Soncino).
Ni kweli, mfano huu
uko wazi sana. Wokovu wetu unatokea mbali zaidi kwa kupitia Roho Mtakatifu. Kwa
hiyo chakula chetu kinatokea mbali sana na chakula chetu ni kuyatenda mapenzi
yake yeye aliyetutuma (Yohana 4:34).
Mithali 31:15 Tena
huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na
wajakazi wake sehemu zao.
Kwa hiyo kabla ya
hakujakuchwa huenda kuoka mkate, na kuandaa chakula kinachohitajika wakati wa
mchana (kwa mujibu wa Malbim; Soncino). Kwa hiyo anatoa chakula na kuwapa watu wa nyumbani mwake, na sehemu kwa
watumishi wake, ni kinyume kabisa na dhana ya uongozi wa kimadaraja ambapo
kwamba Kanisa linatakiwa kutoa sehemu ya vitu lilivyonavyo kwa wahitaji walio
ndani yake tu. Siyo suala la kuwaambia watumishi ni nini wanachokitaka na
ambacho hawatakifikiria. Inawapa hamasa ili kwamba wawe wameandaliwa vyema
kufanya kazi zao. Usemi wa watumishi wake
unamaanisha watumishi wa kike walio kwenye nyumba yake. Wao nao ni walengwa
wa huduma za kazi nzitobzito (kwa mujibu wa Malbim). Iwapo kama watumishi wa
kike wa majumbani hawatunzwi na kuhudumiwa vizuri au kuelekezwa vyema bdipo
hawataweza kutia mafuta taa zao kwa Roho Mtakatifu na watakuwa sehemu ya
wanawali wapumbavu na sio wenye busara. Wamejita kutoka hapo ili kwamba waweze
kuwafanya wtumishi wanawake kwenye daraja la wenye busara – kwenye ufufuo wa
kwanza wa wafu – unaohitaji kuwaisha kwa bidii na kwa umakini mkubwa na Kanisa
chini ya Roho Mtakatifu.
Mithali 31:16 Huangalia
shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
Anatafakari thamani
na umuhimu wa amani na kuilinganisha kama ardhi inayouzwa, na kutoshelezwa
nayo, akiiongeza kwenye mashamba ya familia (kwa mujibu wa Metsudath David).
Dhana hii
imechukuliwa kutoka kwenye usemi usemao: kila
mmoja wetu anawajibu kwa wale walio walio majumbani mwetu, na wale walio kwenye
uangalizi wetu, ili kuwapeleka kwenye shamba. Ndipo sisi tunatazama kwenye mashamba
mengine na kuwaleta watu hao kwenye majukumu ya kulizalia matunda Kanisa.
Kwa matunda ya mikononi mwake, anapanda mizabibu: kristo mdiye mtunza mizabibu. Kwa hiyo
Kristo huchukua kile tulichokipanda na huikatia miti. Kwa hiyo ndipo anakwenda
kwa kupitia mchakato ulioelezewa kwenye mfano wakati wanapoingia hukumuni.
Kwenye mfano wa mkulima au mtunza miti ya mizabibu (Luka 13:7-9) Kristo anawaleta
kwenye mkururu wa miaka mitatu ya kuyaona matunda yake; mwaka wan ne, kuchimba
au kuukata na kuuondolea mbali; meaka wa tano ni wa rehema; mwaka wa sita ni wa
wateso na majaribu makubwa; mwaka wa saba ni wa mapumziko, na kadhalika ka
kupitia mzunguko wa miaka saba wa Yubile. Mizabibu inaletwa au kuingizwa kwenye
mifumo ya Kanisa ili kwamba Kristo awatunze na kuwafanya wazae matunda.
Mizunguko ya miaka sab asana inatumika ili kufanya hivyo kwa kulinganisha na
kiwango. Sharia zimewekwa zinazohusu utunzaji wa miti kwa kuwa kuna mambo ya
kimwili, na kuna sababu za kiroho pia. Sababu za kimwili huziwakilisha zile za
kiroho. Watu wanaokuja Kanisani wana miaka mitatu wakati mambo yanapoonekana
ahvitokei popote pale, na wanasaidiwa, na wanakua, na ni furaha na shamra
shamra. Katika mwaka wa tano wanapewa mwaka wa rehema na katika mwaka wa sita
Roho Mtakatifu anashuka hadi kiwango cha chini sana, na wanakuwa wamechosha katikati ya macho yao kwa hiyo wanaona jinsi
walivyodumu na kuvumilia na kile walichojifunza.
Walioitwa
wanapewa majaribu. Wengine wanashindwa mitihani yao wanapojaribiwa na
wanajikusanya na kujikongoja na kusimama tena/ katika mwaka was aba wanapea
mapumziko, na mzunguko unakwenda na kuendelea kwenye viwango vya juu zaidi.
Tunaona jinsi ilivyofanyika hivyo kutokana na mfano wa Samsoni (soma jarida la Samsoni na Waamuzi (Na. 73)).
Inaonekana ni
kama limekuwa ni tatizo kubwa lakini hiyo ni dhana ya upandaji wa shamba la
mizabibu ilivyo. Mungu ameotesha mimea na anatuambia sisi mizabibu ni nini na
ni kina nani ni mizabibu lakini sisi ndiyo tunaopanda na kuyalima nahamba hayo ya
mizabibu. Yesu Kristo naye aliliima na kuitunza mizabibu. Mungu ametupa sisi
miti, na tunaipanda, Yesu Kristo anainyeshea, na Roho Mtakatifu anaihakikishia
ukuaji wake. Unabii unatuambia kwenye Isaya 5:7 hili shamba la mizabibu ni kitu
gani: Kwa maana shamba la
mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli.
Tutaitathimini
dhana iliyo kwenye aya ya 16 – ya ulimaji au utunzaji wa shamba la mizabibu –
kwa upana kidogo kutokana na ufafanuzi wa kitabu cha Soncino. Matunda ya mikono yake inaeleweka kuwa
ni fedha zilizokusanywa au zilizopatikana kutoka kwenye kazi zake za ufundi wa
kushona nguo (kwa mujibu wa Metsudath David). Ni matunda ya mikono ya Kanisa, ambayo kwa kweli
ni wanaoongeka kwa Bwana.
Na anapanda ni usemi unaofanana na nyumba ambayo Mimi (Sulemani) nimeijenga kutokana na 1Wafalme 8:44. Hii haionyeshi kumaanisha
kwamba kazi ya kupanda na kulima ilifanyika kwa mikono yake yeye mwenyewe (kwa
mujibu wa Ibn Ezra). Sulemani anatajwa kuwa amelijenga Hekalu, na Sulemani
aliyajenga matofali kwa ugumu sana. Ni Sulemani ndiye aliyelijenga hekalu hili,
kwa kuelekezwa. Hii ndiyo dhana yenyewe: kwamba kila mtu anafanye au ahusike
kwenye ujenzi na kila mmoja Kanisani aendeleze nadharia hii kama sehemu ya kazi
hii. Kwa hiyo shamba la mizabibu lilikuwa ni ya kinyumbani iliyotenenezwa na
kupangiliwa vizuri, chimbuko la dhana iliyo kwenye 1Wafalme 5:5, ya kila mtu
kuwa chini ya mti ake wa nzabibu. Tunaona uelewa wa kiroho wa dhana hiyo kwenye
Agano Jipya.
Mithali 31:17 Hujifunga
nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
Aya hii inaweka
taswira ya yeye akiipangilia kazi yake kwa nguvu na msukumo mkubwa. Mkanda wa viunoni mwake uliokaza: Ibn
Ezra na Metsudath David wanaelewa jambo hili kuwa ni uwezo wa kuongea, ulio na nguvu kama mkanda. Unatumiwa
sana na Mungu kwenye Zaburi 93:1: Amejifunga
mwenyewe kwa mkanda wenye nguvu (Soncino). Anafunga viuno vyake kwa nguvu
kama Mungu alivyojifunga mwenyewe kwa nguvu. Kwa hiyo ndivyo tunaliongelea
Kanisa kuwa linajifunga lenyewe kwa nguvu za Mungu. Inafanana na kama tukirudi
hadi nyuma kwenye Zaburi na pia kwenye Zakaria 12:8 Nayo
nyumba ya Daudi itakuwa kama Elphim, kama Malaika wa Bwana mbele yao.
Na anaiimarisha mikono yake: Kuifanya mikono yake iwe imara kunamaanisha
mkono wa kuume wa Mungu na mkono wa kuume ambao unamaanisha kabisa kuwa ni Yesu
Kristo (Zaburi 44:3), nasi tu mikono ya Mungu kama tunapenda kuweka kwa namna
hiyo.
Mithali 31:18 Huona
kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
Hivyo ni kwamba,
nchi anazofanyanazo biashara na anakuta kutokana na uzoefu (sawa na ilivyo
kwenye Zaburi 34:9 ambapo vebu yake imetafsiriwa tafakari). Kwa hiyo analinganisha na kile kinachotokana na tunda
lake, ambapo anafanya. Yatupasa kuhukumu kutokana na kile linachojitokeza
kutoka kwenye matunda ya matendo yetu, na ambavyo kwamba tunavyozitafakari sheria
za Mungu na kutafakari yale tunayoyatenda, au jinsi tunavyoshughulika au jinsi
tunavyohudumiana kila mmoja na mwingine, na jinsi tunavyolitia nguvu Kanisa.
Taa
yake haitoki nje kwa usiku. Hii ni dhana ya kimapokeo ya huko Mashariki ya
Kati. Metsudath David anayatafsiri maneno haya kama anafanya kazi wakati wa sehemu ya mwanzoni ya usiku, na anaamka mapema
(aya ya 15) ili kuongeza mapato yake ambapo ni kufanya biashara (Soncino).
Kuna utendaji
kazi makini wa somo husika na (kwa mujibu wa Soncino), inawezekana kabisa,
kinachotajwa ni kwa ukweli wa kwamba hapo mwanzoni walikuwa wanawasha taa
wakati wote na kuicha ikiwaka nyumbani (sawa na ilivyo kwenye Yeremia 25:10;
Ayubu 18:6). Kitendo chake cha kutoka nje kilichukuliwa kuwa ni uchuro na mkosi
au bahati mbaya kubwa sana. Usemi wa siku hizi wa watu jamii ya Bedouin ni
kwamba analala gizani ili kuonyesha
mazingira ya hali ya umaskini (Soncino). Ni kweli, kwa sisi, taa haizimiki usiku na inaeleweka.
Kristo anaandaa taa
au kinara cha Kanisa na Roho Mtakatifu anayafanya mafuta ya taa hiyo yawake.
Taa hii hatimaye itakwenda na kutumika kwenye alo wa arusi ya Mwanakondoo. Taa
hizo ni za watu wenye busara kuliko kuwa ni za wanawali wapumbavu, ambao taa
zao hazikuzimika usiku. Mwana arusi alikuja usiku wa manane na walikuwa tayari
kuingia hukumuni na kwenye karamu ya arusi ya Mwanakondoo kwa kuwa taa zao
hazikuzimika. Wanawali wapumbavu waliziacha taa zao zizimike, kwa hiyo kwenye
Mithali 31 tunaona kwamba ndipo mwanamke huyu alikuwa makini sana anayeifanya
taa yake iwe inawaka wakati wote nyumbani mwake. Tutaona huko mwishoni kwamba
Mungu na Kristo watakuwa ni taa za Hekalu la Mungu.
Mithali 31:19 Hutia
mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
Fafanuzi zinasema
kuwa aya hii inapasa kuunganishwa na kile kinachofuatia; hakuna muda
unaopotezwa kiuzembe. Kazi yake nyingine inayohitimishwa, anatumia muda wake wa
kupumzika kwa kuandaa na kutengeneza au kushona mavazi na kuwapa maskini na watu
wa nyumbani mwake (kwa mujibu wa Malbim). Kwa hiyo Kanisa halipaswi kuwa zembe
na vivu. Wakati wanaposhughulika na majukumu ya kila siku wanatengeneza macazi
kwa ajili ya maskini. Wanaandaa na kuwasaidia wapendwa waaminio walio hukumuni
wawe wameinuliwa. Wanawasaidia watoto wao wasome na waelimike na wanawafanya
watu wa nyumbani mwao wawe imara.
Mithali 31:20 Huwakunjulia
maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
Ingawa ametingwa
na shughuli nyingi za kazi zake, bado anakuwa hawasahau na kuwaacha maskini na
wenye uhitaji wanaomjia bali anaukunjua mkono wake na kuwapatia mahitaji yao.
Na kwa kufanya kwake hivyo, anajipatia faida kutokana na kazi zake anazozifanya
na kila apatapo faida, hauzuilii mkono wake wala kusita kuwapa maskini (kwa
mujibu Meiri) ili kwamba faida iliyopatikana kutoka kwenye kazi zake zote irudi
kwake na itumike kwa mambo muhimu yanayoeleweka. Tunafanya kazi ili kuendeleza
na kuwahudumia kwa moyo ndugu zetu Wateule. Tunaendeleza kwa kumuwezesha kila
mmoja na kuwafanya waongezeke kiidadi.
Mithali 31:21 Hawahofii
theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo
nyekundu.
Ni majira ya
baridi kali, lakini haogopi umande wala theluji. Vazi hili jekundu linawakilisha
mavazi ya kifahari. Tunaweza kulilinganisha na 2Samweli 1:24 na Yeremia 4:30.
Kwa kuwa familia kwa kawaida walivaa mavazi haya ya thamani nay a bei kubwa, ni
wazi sana sasa kwamba walipewa na mavazi yenye kutia joto mwilini wakati wa
majira ya baridi kali (yaani, kwa mujibu wa Isaiah da Trani). Dhana yenyewe ilikuwa
ni kwamba: haijalishi kama walikuwa wamekabiliwa na adui yao. Mavazi ya Wateule
yanatosha kuwafukuzilia mbali maadui, ili kuwalinda vijana na wadhaifu au wagonjwa
na wadhaifu wasioweza kujisimamia wenyewe, na kuwapatia mavazi na leso au
kilemba kinachoendana sawa na vyeo vyao, kwa kuwa wao ni wafalme na makuhani.
Mithali 31:22 Hujifanyia
mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
Mwenyewe alikuwa
amechoshwa na mavazi yasiyo ba bei kubwa na yakikapuku (Metsudath David).
Mavazi yake yalinunuliwa kwa sadaka ya Mwanakondoo na kufuliwa kwa damu.
Mithali 31:23 Mume
wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
Hii imechukuliwa
na wafafanuzi kuwa inamaanisha kuwa alijulikana
kuwa maarufu kwa uzuri na umaridadi wa mavazi yake (kwa mujibu wa Rashi), ambako
kulimpaisha juu kwa makadirio ya wakazi wa mji aliokuwa akiishi. Kile inachokimaanisha
hapa ni kwamba mume wa mwanamke huyu alifanywa ajulikane na kuwa maarufu kwa uenezaji
wa mafundisho ya Wateule; na kwamba neno la injili ya Ufalme wa Mungu
limetangazwa na kuhubiriwa na Kanisa ili kwamba mtu mume, Yesu Kristo, awe
anajulikana ulimwenguni kote.
Huketi pamoja na wazee wa
nchi ni
dhana ya utoaji wa hukumu. Dhana hii inahusisha pia na uanzishwaji wa Ufalme wa
Mungu ambao ni wa Kristo. Kwa hiyo umefanywa na Kanisa ambao ni Wateule kwenye
kipindi cha milenia. Wateule wanalazimika kuchukua nafasi yao kwenye jukumu la
kuhukumu, ambalo ni sehemu ya makemeo yanayoendelea pia pamoja na harakati za
utoaji hukumu kwenye ufufuo wa pili wa wafu.
Mithali 31:24 Hufanya
nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.
Andiko hili kwa
kweli halipo sahihi sana. Mavazi ya nguo
ya hariri: neno hili limetokea tena kwenye Waamuzi 14:12ff. na kwenye Isaya
3:23.
Kwenye kifungu kilichofuatia,
kimejumuisha kwenye orodha ya wanawake vilemba vya wanawake. Kilikuwa ni cha
mraba au cha pembe tatu cha hariri nzuri kilichovaliwa kama vazi la nje, au
kama mtandio uliovaliwa mwilini anapokuwa analala kitandani (kwa mujibu wa Daath
Mikra).
Mavazi ya hariri
pia yalivaliwa na kuhani mkuu katika hatua za kwanzakwanza za huduma ya
Upatanisho, alipokuwa ni kuhani wa kuwaombea na kuwafanyia watu upatanisho,
kabla hajaanza kuhudumu (au hajaanza kazi) kitambaa kitakatifu na cha kifalme hakijaanza
kutumika kama ni vazi la kuhani mkuu mwishoni mwa mkururu wa shughuli za
Upatanisho (soma pia jarida la Upatanisho (Na. 138)).
Dhana ya huafungulia mishipi kwa wafanya
biashara tafsiri yake halisi ni anafanya
biashara (kwa usemi rahisi na unaoeleweka ni aliwapa), kwa hiyo vebu yake siyo aliwapa. Tulifanya biashara sawasawa na ilivyoandikwa kwenye Ezekieli
27:12, na msukumo wake hapa umechukuliwa na wanaufafanuzi Daath Mikra kuwa
inamaanisha alifanya biashara zaidi kuliko kusema alitoa. Alitoa au aliwapa mishipi,
au mavazi ya hariri. Auni ya neno mishipi
ni umoja wa pamoja, na mikanda imekuwa ikivaliwa kwa kawaida kwa
kuzungushiwa viunoni, na kwa matajiri, ambazo zilikuja elezewa kuwa ni imedariziwa
au kunakshiwa. Wafanyabiashara hawa
kwa kawaida walikuwa ni Wakanaani au
wafanyabiashara wa Kifoenike. Kwa hiyo, anachokifanya ni kuwapa mishipi,
kusaidia kuwatia nguvu, wageni, Wamataifa. Mkururu wake ni kwamba kwa kweli
Kanisa linasaidia na ni nuru kwa Wamataifa kwa kadiri linavyoendelea kutoa
msaada wa aina hii na wa mavazi kwa mataifa yote ya Wamataifa.
Mithali 31:25 Nguvu
na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.
Fursa kuu na
uwezo wa kifedha na wa kiheshima unaotokana nayo ndivyo vilidhaniwa kuwa ndiyo
maana hasa ya andiko hili. Kwa kweli, nguvu na utukufu ni nguvu muhimu katika
Roho Mtakatifu. Ukuu wa Roho Mtakatifu ni kwamba tumevikwa vazi la haki na silaha
za Bwana kama anavyosema Mtume Paulo.
Anaucheka wakati ujao: Tabia zake na wokovu wake ndivyo
vinavyomfunika. Tabia hizi zimezalishwa kwa vazi moja baada ya linguine (kwa
mujibu wa Ibn Ezra). Hii inatokana na maandiko ya: Nawe uvikwe mavazi ya utukufu na ya kutukuka (kutokana na Zaburi 114:1) na pia, Makuhani wako na wavikwe haki (kutokana
na Zaburi 132:9). Makuhani wamevikwa na vazi la haki na utakatifu na nguvu na
utukufu vinatokana na nguvu za Roho Mtakatigu mwenye haki na utauwa. Andiko
linalosema kwa wakati unaokuja maana
yake ya moja kwa moja ni kwa siku ya
baadae (Ibn Ezra, Meiri). Hili ni Kanisa katika siku za mwisho.
Mithali 31:26 Hufumbua
kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
Tafsiri ya
Soncino inasema, wakati anapoongea, maneno yake yanagubikwa na maana nzuri na umakini
(kwa mujibu wa Meiri). Kwa hiyo mizania ya unenaji imepimwa. Kusudi la unenaji
ni kuwainua juu watu, kuonyesha makosa kwa wema na upole, na kutumia unenaji
kwa kipimo kama njia bora na ya kiupendo ya kuwarekebisha watu makosa yao na
kuuweka wazi uovu.
Mithali 31:27 Huangalia
sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
Kwa kuongezea
kwenye amri zilizotolewa, anaonekana kuwa wao wanaondolewa tu na kutolewa nje
na kusimamia kila kipengele cha nyumbani kwamba kiwe kwa kuzingatia heshima na
kicho au hofu ya Mungu (kwa mujibu wa Metsudath David). Kila kitu kimefanywa
kwa utaratibu, kwa usahihi, na kwa kumhofu Mungu.
Wala hali chakula cha
uvivu maana yake ni kwamba ana nguvu nyingi na kila wakati emetingwa kwa shughuli nyingi. Kusoma ni
muhimu sana kwetu sisi sote, ili tujiandae sisi wenyewe kuzikamilisha kazi hizi
na kuwasaidia wapendwa ndugu zetu.
Mithali 31:28 Wanawe
huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
Huamka mapema: Ibn Ezra anaelewa vebu hii kama ni kuamka asubuhi na, kukikuta kila kitu
kikiwa kimeandaliwa vyema, watoto huonyesha shukurani zao kwake. Yaweza kuwa
ilionyesha maana yake ni kusimama mbele yake kama mlengwa na anayestahili
kuheshimiwa, mapokeo yanayotokana na andiko la Mambo ya Walawi 19:32.
Sasa mwisho wake,
si kwamba watainuka tu mbele ya Kanisa la Wafiladelfia, bali pia watafanywa
walale chini wakisujudu kwa vipaji vya nyuso zao ili kusujuidu. Wale wasemao
kuwa wao ni Wayahudi na kumbe sio, watafanywa waje kuabudu, ambavyo ni kusujudu,
mbele ya Wafiladelfia.
Sio suala la
kuinuka tu na kusimama kwa heshima kwa maana ya Kanisa, na hayo ndiyo yawe
maana yake. Bali inachukua hatua ya mbali zaidi ya kwamba ni kuamka tu peke
yake mbele ya Kanisa, kwa ujumla hasa kwa Wafiladelfia. Wale walio kenye imani
potofu za uwongo kwa kweli wamefanywa wajinyenyekeshe kwa kuwa Wafiladelfia
walidhaniwa na kuonekana kwao kuwa wamepotoka, lakini watu waliosema kuwa wao
ni Wayahudi na kumbe sio.
Tafsiri ya Talmud, kutoka
Kiddushin 31(b) inamuonyesha Rabbi mmoja kwamba, wakati wowote alipoisia sauti
ya nyayo za mama yake, alisikika akisema kwa heshima kuwa --’Nasimama mbele ya
Shekina (Mahali Patakatifu)’ (Soncino).
Kwa hiyo mfafanuzi
huyu wa maneno ya marabi kwenye tafsiri ya Talmud alijua kwamba Maskani
Matakatifu tunayoiongelea hapa ni Shekina, ambayo kwamba Kanisa ni wakala au
mfano hazina yake (1Wakorintho 3:16-17). Rabi anaitaja hapa akifanyia rejea kwa
mama yake, lakini Shekina bado ipo Kanisani. Roho Mtakatifu, nguvu na uweza wa
Mungu, ndicho kitu ambacho kinaliwezesha kwa kulipa nguvu Kanisa ili kwamba
watoto wa watu wetu na kila mmoja peke yake, Wateule, wainuke na kuwaita
wamebarikiwa, na Kristo atukiri mbeye ya Baraza la Wateule. Usemi wa kumwita amebarikiwa ni wa moja kwa moja
zaidi, na kumsifu (inatokana na
Zaburi 72:17 na Wimbo Uliobora 6:9 (Canticle 6:9)).
Mithali 31:29 "Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini
wewe umewapita wote."
Aya hii inatoa maneno ya sifa ya mume wake (Daath Mikra). Hizi ndizo sifa
za Kristo. Neno Mabinti ni usemi wa
kishairi wa kimapokeo utumikaa kwa wanawake (kutokana na Mwanzo 30:13; 34:1;
Canticles ii.2 and vi.9) (Wimbo Uliobora 2:2 and 6:9)),
Ni kama ilivyo wazi
sana kutokana na nukuu za aya mbalimbali, hii haimaanishi wanawake wasioolewa
peke yao, ambao bado wanaishi kwenye majumba na familia za baba zao, bali pia
hata kwa wanawake walioolewa, ambao ni miongoni mwa watu wetu tuwajuao kwamba
ni ‘wanawake wenye silaha’. Na hata itakuwa ni mjumuisho na kwamba hata kama
baada ya ndoa, wakati wote mwanamke alibakia kuwa ni mwanachama wa familia ya
baba yake, na kwa hiyo aliendelea kuitwa binti yake, kama ilivyokubalika na
kuelekezwa kwenye Hesabu [36], kwamba miongoni mwa Waebrania, binti aliyeolewa,
ambaye hajaondoka bado kwenye nyumba ya baba yake, bali pia atakuwa anahesabiwa
yu bado kwenye kabila hilo (Soncino).
Tunapoolewa,
tunaindizwa kwenye familia ya watu wake Mungu.
Mithali 31:30 Upendeleo
hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye
atakayesifiwa.
Aya zinayohitimisha
ni za muono wa mtunga shairi kwenye taswira hapa iliyochorwa, na masomo au mafundisho
anayotaka kuyawekeza kwa msomaji. Hausifii uzuri wa mwanamke, lakini sio muhimu
na la maana sana, na sifa kuu zaidi ya zote kwa mwanamke; tabia na mwenendo ni
kigezo halisi na cha kweli (Isaiah da Trani; Soncino)
Rehema inadanganya sana. Monekano wa nje wenye rehema zaidi haounyeshi
hali halisi iliyoko ndani ya tabia na hulka za mwanamke. Uzuri ni mwonekano wa
ngozi. Maandiko ya Marabi yanajumuisha ripoti au habari kwamba kwenye matukio
mawili kwa mwaka, ‘mabinti wa Yerusalemu walikuwa wanatoka mitoko maalumu
wakiwa wamevalia nguo nyeupe, ambazo zilikuwa zimeazimwa, ili kwamba
wasimuaibishe mtu yeyote ambaye hakuwa nayo yake mwenyewe. Ndipo mabinti hao wa
Yerusalemu walitoka nje na kucheza kwenye mashamba ya mizabibu. (Ndipo wanawake
hawa wazuri au warembo walipiga kelele na kusema), ‘Ewe kijana wa kiumbe, hebu
inua macho yako na umwone ni yupi unayeweza kumchagua ili awe mke wako.’ Ndipo
wanaume kutoka familia mbalimbali tofauti walijibu, ‘msiutumainie uzuri na
urembo, bali ni kwenye familia,’ na (walioko nyumbani kwake waweza wasiwe wala
na uzuri wala uungwana), aliinukuu aya hii. Kigezo cha ‘familia’ kiliashiria
kwamba yule binti alikuwa na tabia njema aliyorithishwa na kulelewanayo, na kwa
hivyo yawezekana kabisa anaweza kuwa ni wa tabia nzuri (Soncino).
Mafundisho haya
yote, wakati yalipotokea Yerusalemu, ni mafunzo mazuri kwetu. Dhana yenyewe ni
kwamba tumepewa Neema sisi kwa njia ya wokovu wa Yesu Kristo. Hatuwezi
kuwaambia wenye nguvu Kanisani na watu wake kwa miomekano. Tunawaambia kwa matunda
yake ya kiroho. Kanisa la Walaodikia lilikuwa tajiri, lenye nguvu na imara kwa
hiyo lilidhania, lakini bado machoni pa Mungu lilikuwa maskini, mnyonge, kipofu
na uchi. Lilihitaji kununua dhahabu iliyosafishwa kwa moto na nguo nyeupe.
Walitakiwa wajioshe kwa damu ya Yesu Kristo, kimsingi, kwakuwa hawakuwa wanafaa
kuingia hukumuni na walitapikwa watoke kinywani mwa Mungu, lakini bado walionekana
kama wazuri. Kwa wao, uzuri ulikuwa ukiwadanganya.
Bali mwanamke amchaye
Bwana, ndiye atakayesifiwa. Hii ni tabia na mwenendo au tabia muhimu nay a msingi inayofaa
awenayo mwanamke anayestahili sifa zilizotajwa hapo juu (kwa mujibu wa Isaiah
da Trani) na kwamba ndizo tabia na mwenendo unaofaana na wa muhimu kwa Wateule.
Kumcha Mungu ni chanzo cha hekima na ni muhimu kwa Wateule kwenye uelewa wao. Yohana
17:3 ni wazi sana kwamba kuna Mungu mmoja tu, wa pekee na wa kweli, na kwamba
Yesu Kristo ni Mwana wake, na hicho ndicho kigezo muhimu sana kuaimini ili mtu
aurithi uzima wa milele. Na kama hatumchi Mungu huyu wa Pekee na wa Kweli na
tukadhani kuwa tunaweza kuiabudu miungu mingine na kuendelea kucheza na dhana
au nadharia za pale tulipo na bwana wetu ni yupi na ni nani tunayejiandaa
kwaye, ndipo ni hakika kwamba hatutakuwa hapo.
Mahali ambapo kanisa linaendeleza hisia za imani potofu mawazoni na uimla
wa kiteolojia au madaraja ya kivyeo au ya kiuongozi, hawataweza wenyewe kuingia
kwenye hukumu. Hatutaweza kuliwezesha Kanisa na kulipa nguvu chini ya mfumo huu
wa kimadaraja ya uongozi. Na ndiyo maana wamekuwa wakikemewa au kushutumiwa na
wamekuwa wakifanywa hivyo kwa kipindi cha takriban miaka elfu mbili sasa.
Kanisa la Mungu limeweka msingi wake kwenye uongozi au huduma ya kitumishi, na
limetuama kwenye uwezeshaji wa kila mmoja na mwingine kwa upendo na kujitoa
sadaka.
Mithali 31:31 Mpe
mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni
Hebu na liwe na
sifa njema kwa kila linachokifanya (kwa mujibu wa Metsudath David). Tutahukumiwa
sawasawa na tunayoyafanya. Tutapewa sifa nyema kamili, kwa mujibu wa mfano wa
talanta, kama tutapewa talanta kumi na tukazitumia na kurudisha faida mara kumi
yake. Tutapewa thawabu au miamala ya kile tunachokifanya. Kama tutakuwa
tumepewa talanta na kisha tukaifukia mchangani, ndipo tutakuwa tumeondolewa
mbali. Inasema kuwa hebu na
matendo yake na yamsifu malangoni mwake. Inamaana ya kwamba ingawa harakati zake
zinathibitika nyumbani mwake, kutokana na kutambulika kwake angelipwa kwa wazi
kabisa malangoni kwa mchango wake mkubwa na wa muhimu anaoutoa kwa manufaa na
maendeleo ya jamii. Sasa haisemi kitu chochote kabisa kuhusu hilo, kama
anavyoitafsiri Rashi. Haisemi kwamba harakati zake zimekubalika nyumbani
kabisa. Haya ni mawazo yanayotokana na mapokeo na uelewa wa Kiyahudi kabisa.
Yamelidandia pia Kanisa la Mungu katika karne ya ishirini. Harakati za wanawake
hazikuwa zinahusiana au kutegemewa na masuala au mahitaji ya nyumbani. Na
harakati za Kanisa hazihusiani na masuala ya nyumbani. Wanawake wanapaswa
kuwezeshwa na waume zao na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu na waliwezeshwa ili
waxhukue nafasi yao kwenye Ufalme wa Mungu. Kanisa nalo ni hivyohivyo, na sisi
sote tukiwa kama mabibi arusi wa Kristo, yatupasa kutiwa nguvu au kuwezeshwa na
yeye. Tunawezeshwa na kutiwa nguvu kwa harakati za Yesu Kristo kwa njia ya Roho
Mtakatifu na runachukua nafasi yetu kwenye Ufalme wa Mungu. Tunatoa mchngo
mkubwa na wa muhimu sana kwenye jamii na tunajaribiwa kupenda kusifiwa au kupongezwa
malangoni ingawaje Kristo amesema kwamba hakutakuwa na kitu kama hicho cha
kusifiwa kitakachofanyika kwetu. Itakuwa hivyo wakati ule tu tutakapouchukua
ufalme na ndipo tutasifiwa na kupongezwa malangoni kwa kuwa totakwenda kuwa
waangalizi na warekebisha makosa kwenye zama yote ya utawala wa Milenia.
Wataona, tukiwa na Yesu Kristo, kile tunachoweza kukifanya. Hitler alisema
akiwa amevuviwa na mapepo, maneno yaneno yaliyotafsiriwa kutoka lugha ya
Kijerumani akisema: Baada ya vita kwisha,
wataona kile tulichokifanya na kukisudia. Hivyo ndivyo hasahasa inafanana
na itakavyokuwa kwa Wateule zaidi kuliko na hata ilivyojitokeza kwa watu wa
Ujerumani. Kutakuwa na vita vingine, lakini ni baada ya vita vya mwisho ambayo
itakwenda kushuhudia vile tulivyokuwa na kwa kuwa tunakwenda kuirejesha upya
tena hii dunia. Israeli atakuja kutoka upande wa kaskazini wakiwa mkono kwa
mkono na Waashuru. Tutafanya hivyo tukiwa ni Wateule kwa kuwezeshana kila mmoja
kwa roho wa uweza na wa akili timamu katika Roho Mtakatifu. Tunaweza kudiriki kuhukumu
na kushughulikia watu ambao hawaelewi au wasioweza kuyatendea kazi mafundisho ya
Yesu Kristo. Kwa sasa sisi tuna timazi ya haki ya kupima na kurejea kile
kilichofanyika kwa kipinsi chote cha miaka arobaini na kule tunakotakiwa tuende.
Licha ya ni kwa kipindi gani kilichopo, nan i vigumu kuitendea kazi, bali
ni kwamba tuko kwenye nyakati za mwisho. Ni wachache tu ndiyo wangepinga au
kubisha hoja hiyo. Ni suala tu la ni lini. Tunahitaji kutiwa nguvu na kutiana
nguvu ili kupata kwa kupitia mchakato ule na kuwasaidia Wateule, na kulisaidia
tgaifa letu. Hawatakwenda kupata hilo iwapo kama tukiwa kwenye usalama. Sisi tu
sehemu yao. Sisi tu Wateule, na taifa hili ni kama mahali tulipopandwa mbegu
ambapo tunaing’oa na kuitupa nje mizabibu, kwa mujibu sawa na maelekezo ya
Mungu, na kuwapandikiza kwenye mashamba ya mizabibu.
Tutapewa watu
hawa wote kwa wakati huohuo kati ya sasa na kwenye ufufuo wa pili wa wafu ili tushughulike
nao. Tunachotakiwa kukifanya ni kwamba ni kuwasaidia kwa upendo na wema.
Yatupasa kuishinda mifumo hii ya uongozi wa madaraja na kivyeo na tuelewe
kwamba kile tunachokitenda kinawawezesha kuwatia nguvu kila mmoja yeyote yule na
kwamba tunatenda mambo yetu tukiwa ni kama watumishi na kuwaongoza kwa
kuwatumikia, ma siyo kwa kujifanya mabwana juu ya kila mmoja wao.
q