Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[115]

 

 

 

Pentekoste Ya Sinai

(Toleo 3.1 19940514-20000510)

 

Kazi hii inafuatia kutoka majarida yanayohusiana na msafara wa Kutoka utumwani ikiwahusisha wote wawili yaani Musa na miungu ya Misri (tazama jarida la Musa na Miungu ya Misri) na pia Musa na msafara wa Kutoka utumwani (tazama jarida la Pasaka). Inashughulika kabisa na yule aliyetoa sheria pale Sinai na kwa namna gani. Mlolongo wa kutoka Sinai inafafanuliwa kwa matazamo wenye maana ya mtungo na mwonekano wa uelewa mzuri. Uweza wa jeshi la malaika kama ulivyotolewa kutika kwa Mungu pia ukitathiminiwa kwa mahusiano na utolewaji wa sheria na matukio ya Sinai.

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

 

(Copyright © 1994 (na kuhaririwa 1995, 1997, 2000) Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Pentekoste ya Sinai [115]

 


Tumejionea mlolongo wa nsafara wa Kutoka utumwani Misri chini ya Musa katika lile jarida la Pasaka [098]. Uataratibu wa kuondoka Misri ulianzia siku ya 15 mwezi wa Nisani kutoka eneo ambalo kutaniko lilikuwa yaani Ramesesi ambako Israeli waliondoka kulihama eneo lote la Gosheni. Mahali hapa msafara wa wanaume wapatao mia sita elfu, au laki sita wakifuatana na wanawake na watoto wao na watu wazima, pamoja na kundi la mchanganiko wa watu wasio Israeli na akiba ya makundi yote mawili yaliyoondoka kutoka Sukothi (kufanya vibanda au vijumba vya nyasi) (Hes. 12:37-38).

 

Msafara ulikuwa ni tendo lililopangiliwa kuwachukua Waisraeli kwenda Sinai ili kwamba waweze kupokea ufunuo kutoka kwa Mungu. Waisraeli walitolewa kutoka Misri na Malaika wa Uwepo au Malaika wa YHVH. Ilikuwa kwa kupitia malaika huyu ndipo Mungu alimchagua ili adhihishe sheria zake. Katika Waamuzi 2:1-3, Malaika wa YHVH anazungumzia kuhusu agano aliloliombea kati ya Mungu na Wana wa Israeli.

 

Waamuzi 2:1-3 inasema: Kisha malaika wa BWANA alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi; nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zibomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani? Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu. Ikawa, hapo huyo malaika wa BWANA alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia.

 

Malaika huyu alikuwa ni Malaika aliyekuwamo kwenye wingu lililoongoza msafara wa Kutoka utumwani katika Bahari ya Shamu na jangwani (Mdo. 7:36). Alikuwa ni Malaika aliyekuwemo kwenye kichaka aliyeongea na Musa (Mdo. 7:30,35). Alikuwa ni Malaika aliyempa Musa zile amri na sheria (Mdo. 7:38,53; Mwa. 3:19). Alikuwa ni yule Malaika aliyeongea kwa niaba ya Mungu pale Sinai (Mdo. 7:38). Malaika huyu alikuwa ni nyama na kinywaji cha kiroho ambaye kwayo, Israeli walibatizwa na Musa kwa njia ya Malaika katika mawingu (1Kor. 10:2), walizokula na kunywa jangwani. Zile nyama na kinywaji cha kiroho vilikuwa ni Mwamba wa kiroho uliokuwa ukiwafuata. Mwamba ule, ambao ni Malaika wa YHVH, alikuwa ni Yesu Kristo (1Kor. 10:4). Mungu ni Mwamba au mlima ambao Kristo alitokea.

 

Dhana za uwongo zimekuwa zinaenezwa kuwa logos kama neno la Mungu haliwezi kumaanisha msemaji bali lina maana ya matamko ya Mungu kama wazo la kicheo ili kwamba Malaika wa YHVH hakutangaza sheria lakini zaidi sana yule aliye tangaza sheria pale Sinai alikuwa ni Mungu kama Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Na kwamba wote walifanya kazi kwa pamoja pale Sinai. Dhana hii si ya kweli na ni upotofu.

 

Yohana analiweka jambo hili kwa wazi sana katika Yohana 1:18 na 1Yohana 4:12 kwa jinsi anavyosema.

 

1Yohana 4:12 inasema: Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.

 

1Yohana 4:13-15 inasema: Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. Na sisi tumeona na kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Kila akiriye kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.

 

Yohana alikuwa anaandika kiusahihi sana baada ya kifo cha Kristo na hata baada ya kuhusuriwa kwa mji wa Yerusalemu. Alikuwa anaweka kwa uwazi sana tofauti kati ya Mungu na Kristo. Alikuwa anatofautisha kati ya Kristo ambaye wanadamu walimuona na Mungu ambaye hawakuweza kumuona kwa wakati wowote iwe pale Sinai au mahali pengine popote pale. Katika Injili, kwenye Yohana 1:18, Yohana anasema:

 

Theon oudeis eooraken poopote maana yake:

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote;

 

monogenes theos ho

Mungu Mwana pekee

 

oon eis ton kolpon tou patrot,

aliye katika kifua cha Baba,

 

ekeinos   ezegesato.

Huyo ndiye aliyemfunua.

 

Tofauti hapa ni kati ya jina Theon na Theos. Theon ambaye hakuna mtu aliyewahi kumwona na Mungu Mwana pekee, yaani Theons, ambaye ni mtu mwingine aliyesema au kutangaza kwa niaba ya huyu theon (sarufi isemayo yeye ikionyesha maka mwanaume iliongezwa hapa ki makosa). Huyu Theos ndiye aliyekuwepo Sinai. Alikuwa logos aliyekuwepo tangia mwanzo wa uumbaji na Mungu (Theon, kama ilivyo katika Yohana 1:1). Mwanzo (arche) inayo ongelewa katika Yohana 1:1 ilikuwa ni uumbaji wa vitu au raslimali zote. Tafsiri iliyoko katika Yohana 1:1, imekosewa kama ilivyokosewa pia kwenye Tito 2:13 ambako imedaiwa kuwa inasema:

Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu Mungu mkuu na Mwokozi wetu.

 

Aya hii ilitakiwa iseme kama ifuatavyo:

Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo, (tazama kamusi ya Marshall’s Interlinear RSV).

 

Kristo ndiye mafunuo ya utukufu wa Mungu na Mwokozi wetu. Lakini yeye mwenyewe sio yule Mungu. Lakini waamini mafundisho ya Utatu wanashikia aya hii na kudai kuwa ni yeye. Makosa haya huweka msingi wa mafundisho ya kimakosa ya watu wanaoamini mafundisho ya uungu wa mingu wawili (Binitarian) yaliyoanza kufundishwa kwenye baadhi ya Makanisa kuanzia kwenye miaka ya 1960 (tazama kijarida kisemacho Je, Yesu ni Mungu? Lililoandikwa na Herbet W. Amstrong, kikachapishwa tena chenye kichwa cha somo la Habari Njema, mwezi wa Desemba 1982). Makosa haya yamefanyika kwa mkupuo kwa kuelewa vibaya maana hasa halisi ya Wafilipi 2:6 inayoelezea kuhusu umbo la Mungu inayofanyizwa kwa kuelezea au kuonyesha asili yake na hivyo kuendeleza makosa katika kuzidisha mbinu za kimafundisho ili kushawishi madai ya kuwa yeye ndiye yule Mungu.

 

Madai ya kuwa ni Mungu aliyekuwa anasema pale mlimani Sinai na kuwa ilikuwa ni matendo ya watu watatu wanaofikirika kuwa miungu sio sahihi kabisa. Kifungu cha maandiko katika jarida la Malaika wa YHVH [024] inaonyesha kuwa ni uwongo ulio dhahiri kabisa na makosa makubwa kudai kuwa Musa alimuona Mungu Mkuu au Mungu Baba pale Sinai, au kwa wakati wowote ule katika msafara wa Kutoka utumwani, au popote na vyovyote vile. Aliongea na mjumbe wake yaani Malaika wa HHVH aliyekuwa ni Uwepo wake na aliyelichukua jina lake. Katika kitabu cha Kutoka 23:20-21 Mungu alisema kupitia Malaika wake kwamba angemtuma malaika wake ili awalinde wakati wa msafara wa Kutoka utumwani.

 

Kutoka 23:20-21 inasema: Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengenezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani, maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake (maandishi mazito yamewekwa ili kufanya msisitizo)

 

Wazo lililoko hapa ni kwamba Malaika huyu alilichukua jina la Mungu kama mamlaka. Nitakuwa kwa kadiri ile nitakavyokuwa akampa jina Yahwe au Yahova ikimaanisha kuwa Anasababisha kuwa ni mwenza katika hali yake ya elohim. Mungu alimpaka mafuta huyu elohim wa Israeli kama tunavyojua katika Zaburi 45:6-7.

 

Zaburi 45:6-7 inasema: Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele. Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzake.

 

Mungu huyu alipakwa mafuta na Mungu wake kwa mafuta ya furaha juu ya wenzake au washiriki wake (metoxous, LXX) au wandugu kama inavyosema Waebrania 1:8-9 ambako mtu huyu ameonekana kwa dhahiri kuwa ni Masihi. Kwa hiyo, Masihi ni mwenza shirikishi wa mungu, lakini bado kunabakia na hali ileile kuwa Mungu ni Mmoja tu. Maendelezo ya mabishano ya wale wanaoamini mafundisho ta utatu yanapatikana kwenye jarida lisemalo Maendelezo ya Muundo wa Ki-Plato Mamboleo [017].

 

Masihi aliwaleta Israeli kutoka Misri. Atenda chini ya maelekezo ya kutoka kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu. Alijulikana kama Mjumbe wa Mungu. hili limefafaniliwa kwenye jarida la Malaika wa YHVH [024].

 

Hesabu kwa ajili ya Pentekoste inapatikana katika Mambo ya Walawi 23:9-21.

 

Mambo ya Walawi 23:9-14 inasema: Kisha BWANA akanena na Musa na kumwambia. 10Nena wa wana wa Israeli, na ukawaambie, Hapo mtakapo kuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. Na siku hiyo mtakapoutikisa mganda, mtasongeza mwana kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba zilizochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini. Nanyi msile mikate wala bisi wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote.

 

Ulaji wa mkate na bisi masuke machanga kwa kati ya siku takatifu ya kwanza na na ya Mganda wa Sadaka ya Kutikiswa, ulikatazwa milele. Kama Kutoka 12 inavyo hitaji mkate usiotiwa chachu uliwe pamoja na mlo wa Pasaka siku ya 15 ya mwezi wa Nisani, tafsiri hapa kwa hiyo lazima iwe ni kwamba nafaka mpya zisitumike kabisa hadi pale Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa imesha tikiswa. Kwa hiyo, hesima ya klumfananisha Kristo kama limbuko inakubalika. Mtihani jaribio wa Yoshua 3:15; 4:18-19; 5:1-8, 11-12 uanonyesha mfano wa ulaji wa mazao mapya katika nchi ya ahadi, baada ya kufanyika kwa tohara. Mkate wa mana ulikoma mara baada ya nafaka mpya kuanza kuliwa. Imani ya Kiyahudi huifasiri siku hii, ya 16 Nisani kwa hiyo ilikuwa ni siku ya sadaka ya kutikiswa na kwamba sadaka ya kutikiswa kwa hiyo ifanyike kila mara siku ya 16 ya mwezi wa Nisani. Kuna maelezo mawili kuhusiana na hali hii ambayo yanatofautiana na mtazamo wa marabi. Uwezekano wa kwanza ni kwamba huu ungekuwa ni mwaka ambao kwamba Pasaka inekuwa ni lazima ifanyike siku ya 15 ya mwezi wa Nisani kama Jumamosi. Kwa hiyo, sadaka ya mganda wa kutikiswa ingeweza kufanyika siku inayofuatia. Hii ni adimu lakini huwa inatokea, kama ilivyotokea kama ilivyotokea mwaka wa 1994. Jambo la pili hata hivyo kufanya liwe wazi kuwa ni nafaka za zamani iliyokuwa ianliwa (tazama jarida la Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa, [106b].

 

Yoshua 5:11-12 inasema  Nao wakala katika mazao ya nchi aiku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya pasaka; mikate isiyotiwa chachu, na bisi, siku iyo hiyo. 12Ndipo na mana ikakoma siku ya pili yake, baada ya wao kuyala hayo mazao ya nchi; na hao wana wa Israeli hawakuwa na mana tena; lakini wakala viliwa vya nchi ya Kanaani mwaka huo.

 

Biblia ya Kiingereza ya Interlinear huendana sambamba na aya za Biblia ya Kiingereza ya tafsiri ya mfalme Yakobo yaani KJV. Neno hili lililotafiriwa kama nafaka za zamani limetokana neno la Kiebrania ‘abuwrwr. Neno hili linamaana ya kupitwa au kutunzwa na linatumika kwa nafaka zilizohifadhiwa tu (tazama kamusi iitwayo SHD 5669). BIBLIA ya Sonsino haitafsiri neno hili huelezea hili kama mazalia ya nchi kama ilivyo katika aya ya 11. Mafafanuzi ya baraza la marabi ya aya ya 11 yanasema kuwa inamaana ya mazalia ya nchi kuanzia mana ilipoacha kushuka chini, kama ilivyoelezewa katika aya ya kifungu cha maandiko kuwa:

Marabi walishikilia kuwa mazao mapya yalimaanisha, kwa Waisraeli walikuwa wanaleta sadaka ya kutikiswa ya ’mganda’ (omeri), kwa kufuatana na mujibu wa Mambo ya Walawi xxiii:10-14, asubuhi ya siku inayofuatia Pasaka jambo ambalo lilikuwa ni utambulisho wa wazi kwa siku ya pili ya baada ya Sabato pale (Rashi).

 

Maelewesho haya (na ya Rashi tu) ni ya uwongo kabisa. Neno muafaka kwa maana ya nafaka za zamani linaloweza kupelekea kwenye maana ya nafaka zilizohifadhiwa ghalani limeachwa kabisa katika biblia ya Soncico na kwenye fafanuzi za marabi.

 

Siku inayofuatia baada ya Sabato katika kitabu cha Walawi ilitafsiriwa kuwa kama Sabato ya Juma kwenye imani ya Kiyahudi ya karne ya kwanza na vile vile na Kanisa la Kikristo na bado ndivyo inavyotafsiriwa na imani ya Kikristo hadi kufikia siku za leo. Hadi kufikia wakati wa kuhusuriwa kwa Hekalu na kipindi cha utawanyiko mwaka 70BK, mfumo wa kalenda ilitayarishwa kwa mujibu wa mfumo wa Masadukayo.

 

Kuanzia kipindi hiki cha utawanyiko, Mafarisayo walianza kudai kuweka utaratibu wao wa kufuata katika kufanya maamuzi ya masuala ya kalenda. Taarifa za kalenda chini ya rabi kwa jina la Hillel II ikaanza mwaka 358BK ilionekana Pentekoste ikawekwa siku ya 6 ya mwezi wa Sivani. Pengine hili lilikuwa ni zoezi la kisiasa au pengine sivyo. Hakuna mashaka kuwa utaratibu wa kutumiwa ili kuamua siku ya Pentekoste ni kwa kuhesabu hadi idadi ya siku hamsini kuanzia siku ya Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa na kuishia siku inayofuatia ya Sabato ya saba. Siku hii inayofuatia mwisho wa Sabato ya saba inaangukia tu kwenye siku ya siku ya kwanza ya juma, yaani Jumapili. Jaribio la kuifanya siku ya 6 ya mwezi wa Sivani kuwa ni Sabato na hatimaye kuitangaza siku ya pili kuwa Pentekoste Pili ni fitina au hila ya iliyo dhahiri kabisa. Maelekezo ya andiko hili yako wazi kabisa. Ukristo umeelewa utaratibu kwa kipindi cha miaka kama elfu mbili. Imani ya kale ya Kiyahudi pia walielewa hii. Ni kwa nini basi marabi wa Kiyahudi waliacha kwa makusudi kabisa andiko ili kuwawezesha kuitunza Pentekoste kwa siku kamilifu wakati wazo zima la Pentekoste kiutendaji ni kwa kuhesabu siku hamsini? Kulikuwa na nini pale kuhesabu na tarehe kamilifu? Inakuwaje siku ile inayofuatia Sabato ya saba isiyo Jumapili?

 

Maelezo pengine yanapatikana katika jarida la Ishara ya Yona na madodoso yake kwa ukristo. Maelekezo kuhusu kuichukua siku ya 6 Sivani inahusisha na utata wa utaratibu wa mgawanyo wa Kumi na Nne (Quarto-deciman) iliyosababisha ukaidi uliopelekea Rumi kuzimisha au kukomesha [tazama jarida la utata juu ya utaratibu wa Mgawanyo wa Kumi na Nne, (Quatodeciman [277]). Mamlaka ya marabi ingeshindikana kabisa kuzuilika kuigizwa kwenye mgongano ya siasa za ndani ya kikristo, ambayo ilionekana kutafutiwa uwezekano wa kuepushia mbali. Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa isingewezekana kufanyika siku ya 16 Nisani ya mwaka 30BK (au mwaka 31-32 BK kwa ajili hiyo) na bado wangetunga jaribio ambalo Kristo aliweka Kanisa. Ishara ya Yona ilikuwa ni kwa Kristo kuwemo kwenye moyo wa nchi kwa muda wa siku tatu kamili, yaani siku za mchana tatu kamili na siku za isiku tatu kamili sawa kama vile Yona alivyokaa kwenye tumbo la samaki mkubwa (tazama jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi upya wa Hekalu [013].

 

Mathayo 12:39-41 inasema: Akawajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. 40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. 41 Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.

 

Hii ilitakiwa kuwa ni ishara pekee ya huduma ya utumishi wa Kristo. Kwa hiyo, kitu chochote kile kinachoweka mchanganyo au kwendana kinyume na ishara hii ni cha uwongo. Katika mwaka 30BK, siku ya 14 Nisani kwa hiyo ilikuwa ni siku ya Ijumaa (tazama jarida la Majira ya Kusulibiwa na Ufufuo [159]. Kristo alifufuka siku ya Jumamosi jioni na alikuwa anangojea kupaa mbinguni Juamapili asubuhi wakati Maria Magdalena alipomkuta pale kabla ya mapambazuko kuanza (Yoh. 20:1). Kwa hiyo basi, ishara ya Yona ilihitajika kutimizwa kwa siku tatu kamili za machana na siku tatu kamili za usiku. Hii ndiyo inayofanya kuwa haiwezekani kwa Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa kufanyika siku ya 16 Nisani. Tukio la mwaka 30BK linaonyesha kuweko hali ya kuto kuwezekana kama ilivyotokea kwa mwaka 31-32 BK. Imani ya Kiyahudi walijua kuwa ingewezekana kuwa hivyo. Pia walijua kuwa Kristo alipaswa kuuawa katika mwaka 30BK wakati wa Pasaka ambao ulikuwa ni mwaka wa tatu kuanzia kuanzilishwa kwa huduma ya utumishi wa Yohana Mbatizaji ambao pia ulikuwa ni mwaka wa kumi na tano wa Kaisari Tiberio ulioanzia mwezi Oktoba mwaka 27BK. Mahesabu ya Yohana yanafanya iwe haiwezekani kusulibiwa kuwe wakati mwingine mbali na majira ya Pasaka ya tatu tangia hapo. Kwa maneno mengine, inawezekana tu kuwa katika Pasaka ya mwaka 30BK kwa mujibu wa Yohana. Lakini maelekezo zaidi yanafanyika kwenye Injili zinazofanana zinapoingiza Pasaka nyingine ya nne kwenye mlolongo huu. Hatahivyo, siku ya maandalizi ya Pasaka ya siku ya 14 Nisani ya mwaka 31BK ilikuwa siku ya Jumapili ya tarehe 25 Marchi na hiki kilikuwa ni kipindi kirefu kufanyika kwa tarehe ya kusulibishwa na Ukristo hadi ilipogunduliwa ilikuwa inaacha kabisa dhana ya kudhani kuwa kusulibiwa kulifanyika Ijumaa na kuwa kwa kuamini hivyo kunafanya zipunguzwe siku fulani ilikuwa lakini baada ya karne ya saba (tazama jarida la Kalenda na Mwezi Mwandamo: Maahirisho au Maadhimisho? [195].

 

Hii ilileta mchanganyo kwa kweli iliifaidia dini ya Kiyahudi kwenye karne mara tu baada ya kifo cha Kristo. Dini ya Kiyahudi ilikuwa inapoteza washirika wakiwa wanajiunga na Ukristo. Ikapelekea kupigana vita vikubwa vilivyoleta madhara makubwa sana kati yao na utawala wa Warumi. Kuanzia katika karne ya pili, dola ya Rumi ilifikilia kuvutiwa sana na imani potofu ya kidini iliyokuwa inafanya ibada zake kwa kuabudu jua na kuamini kuwa tendo la kusulibiwa lilifanyika siku ya Ijumaa na ufufuo ulikuwa siku ya Jumapili. Dini hii ilitunga na kuwa chanzo cha mafundisho haya yenye makosa ambayo yalianza na kuendelezwa kufundishwa. Imani hii ilichanganywa na mapokeo yake na imani za kidini za kishirikina na kipagani zilizokuwa zinafanya shughuli zake kwa siri na kuvutia watu wengi waliokuwa wanaishi nchi za upande wa Mashariki na dini iliyokuwa maarufu zaidi kati ya hizi potofu iliitwa Dumuzi ambayo iliutangulia Ukristo kwa miaka mingi sana. Jina la dini hii ya Dumuzi ambayo pia ilijulikana kama Tamuzi lilitokana na imani yao ya kuwepo kwa mungu wa majira ya baridi (Spring) mwenye jina hilo ambaye kulingana na imani yao waliamini kuwa alikuwa anakufa na kufufuliwa. Hali hii ikaupekelea Ukristo kuingia kwenye utata au mgongano iliojulikana kama mnganyo wa kumi na Nne (Quartodeciman). Sikukuu hii ya kipagani katika kusherehekea sherehe hizi iliitwa Easter wakati ambapo Sikukuu ya Wakristo wa Kiyahudi iliitwa Pasaka. Sikukuu hii ilikuwa inaenda kwa utaratibu wa kimzunguko, ikitegemea chanzo chake na kalenda ya mzunguko wa mwezi-mwandamo. Sikukuu ya Easter ya kipagani ilikuwa inategemea kalenda ya mzunguko wa zote yaani jua/mwezi-mwandamo. kwa pamoja na ambayo iliweka msingi wake kwenye siku za mzunguko wa jua lakini ikihesabiwa kuanzia mwezi mwandamo. Utaratibu wa kuhesabu kufikia adhimisho la Easter kwa sababu ya ukweli huu, maranyingi hubadilika badilika kulinganisha na maadhimisho ya Pasaka, vilevile kwenye mwezi.

 

Utaratibu wa kuhesabu unaonekana kuwa umeangukia kwenye makosa kimakusudi kabisa (tazama jarida la Kalenda na Mwezi-mwandamo: Maadhimisho au Maahirisho? [195]. Kwa kuanzisha hili kosa la Easter, Ukristo ukalazimika kupata mwaka ambao Pasaka uliwahi kuwa siku ya Ijumaa. Tukio hilo lilitokea mnamo mwaka 33BK, ambayo ilikuwa imechelewa sana ikilinganishwa na hasabu za Injili. Mwaka 30BK ilikuwa ni mapema zaidi mno kwa kadiri ilivyokuwa kwa zile Pasaka nyingine tatu zilizotajwa na Yohana. Mwandamano hauruhusu kuzidi wala kupungua. Kosa la Pasaka ya nne, kusukumia hesabu kwenye mwaka wa 31BK, ina siku ya 14 Nisani katika siku ya Jumapili tarehe 25 Marchi kama ilivyoonyesha hapo juu.

 

Pasaka ya mwaka 33BK ilikubalika na dini ya Kiyahudi. La kwanza, ingeweza kutoa uwezekano shirikishi kwa mahitaji muhimu ya Wakristo kwa siku ya Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa kwa siku ya Jumapili kutoka kwenye Ijumaa ya kusulibiwa. Hii ilikuwa na matokeo mawili. Inaonekana kukubaliana na Rumi-ili kuzuia mateso na kukubali kuharibu ukweli uliokuwa kwa Wakristo waaminifu na imani yao kuhusiana na ukweli kuhusu Kristo kuwa ni Masihi. Ilifanya kuwa rahisi kwa mamlaka ya baraza la marabi kuelezea kuwa Kristo sio Masihi hivyo kuzuia, muda wa miaka elfu mbili, kuongoka kwa watu kutoka dini ya Kiyahudi. Dini ya Kiyahudi ilikuwa inaweza kuonyesha, kwa watu wake wenyewe, kinamna ya kwamba Kristo hakuwa kaburini kwa siku tatu mchana na siku tatu usiku kama ukihesabu kwa siku hizo yaani kama kusulibiwa kulifanyika siku ya Ijumaa na kufufuka siku ya Jumapili. Ni ukweli rahisi na pia unaoleweka vizuri kwamba ni ikiwa kama tu alikuwa kaburini kwa siku tatu kamili mchana na siku tatu kamili usiku, lakini vinginevyo atakuwa basi hakufa kulingana na sheria za Kiyahudi. Zaidi sana, kwa kukosa kuyajua maandiko, kwa kupewa elimu dhaifu ya ustawi wa jumla katika jamii katika ligha ya kale ya Kiebrania, waliweza kuendelea kufanya hila kwa makosa makubwa au machache kwa wakati wote. Kuanzia kushindikana kwa utaratibu wa Mgawanyo wa Kumi na Nne (Quarto-decimans) walikuwa na usalama kwa kiasi cha juu au cha chini kwa sehemu zote za mateso na uongofu. Kwa hiyo, Pentekoste ya siku ya 6 Sivani inakubalika kwa sehemu zote mbili yaani kwa Wayahu na kwenye Ukristo mamboleo kwa sababu zilizo tofauti. Ni makosa kabisa na ni kutoenenda na ukweli wa Ishara ya Yona. Hakuna Mkristo wa kweli atakayekubaliana na Pentekoste ya siku ya 6 Nisani na kumkana Mahisi. Ila ni ile hila ya kijanja. Kwa hiyo, dini ya Kiyahudi imekuwa ikienda kinyume na Mungu kwa kipindi cha miaka elfu mbili. Masihi alibidi awe Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa. Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa ilibidi itolewe siku ya Jumapili mwaka 30BK au Israeli hakukubalika wala kukombolewa.

 

Ilikuwa kwa sababu hii ilimfanya Maria Magdalena asiweze kumgusa Kristo pale kaburini (Yohana 20:15-17). Alikuwa kwenye utaratibu, kama alivyosema, wa kupaa kwenda kwa Mungu akiwa kama malimbuko. Wakati hili lilipokamilika, aliweza kurudi na kuwaruhusu wanadamu, kama vile Thomaso, kumgusa. Kupaa kulikofanyika kabla ya Pentekoste kulikuwa kwa pili na kwa mwisho. Haikuwa mavuno. Kristo alitimiza hili kama Mganda wa Kutikiswa kama pia alivyotimiliza sadaka zote kama Mwana Kondoo wa Pasaka.

 

Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa ulikuwa kwa ajili ya kukubalika kwa Israeli.

Mambo ya Walawi 23:15-21 inasema: Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mlioyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba, hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea BWANA sadaka ya unga mpya. Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA. Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza wana kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng’ombe mume mmoja, na kondoo waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa aka zao kwa BWANA, pamoja na sadaka yao ya unga, na sadza kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza iliyosogezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. Nanyi mtamsongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wana kondoo wawili waume wa mwaka wa kwanza kuwa dhabihu ya sadaka za amani. Kisha kuhani atawatikisa pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA, pamojana wale kondoo wawili; watakuwa watakatifu kwa BWANA, wawe wa huyo kuhani. Nanyi mtapiga mbiu siku iyo hiyo; kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi yoyote ya utumishi; ni amri ya milele katika makao yenu yote, katika vizazi vyenu.

 

Mganda wa Kutikiswa ulikuwa ni wa kwanza miongoni mwa mazao yote. Limbuko la mavuno ya Mungu alikuwa Kristo (tazama jarida la Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa [106b].

 

Siku hii imetajwa hapa kama siku ya pili baada ya Sabato, ukijulikana kama, siku ya kwanza ya juma au Jumapili. Kwa hiyo, Pentekoste lazima iangukie kila mwaka siku ya Jumapili inayofuatia Sabato ya saba, ambayo ni siku ya hamsini kuanzia siku ya Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa. Sadaka ya Kutikiswa unaashiria kwa uwazi sana kuwa ni siku iliyofuatia Sabato ya wiki ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kwa hiyo, Pentekoste haiwezi kuhesabiwa kutoka katika siku takatifu ya kwanza ya Mikate Isiyotiwa Chachu kama ilivyokwisha kudaiwa kutoka kwenye kalenda ya Hilleli-ila tu kama siku hiyo itaangukia siku ya Jumapili. Kifungu cha maandiko kilichopatikana katika baraza la wazee sabini yaani LXX kinahusiana na kitabu cha Mambo ya Walawi 23 na Pentekoste ilifanywa kwa kufuata mujibu wa Pentekoste ya siku ya 6 Sivani kama ilivyofanyiwa tathmini kwenye jarida la Pentekoste: Kulinganisha na Walawi 23:11-22 katika Septuagint (Na. 173). Maana ya dhabihu ya Mkate Usiotiwa Chachu ni hivi:-

 

. Mikate miwili ya wonyesho ilikuwa inawakilisha utendaji kazi wa Roho Mtakatifu kutoka kwenye majilio mawili ya Masihi akiwa kama kuhani na Masihi na akiwa kama mfalme Masihi wa Israeli. Hapa chachu hutumika kama alama ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni mtendaji mkuu kiungo kwa haya malimbuko ya mavuno ya wateule ambayo hutokea kuanzia Pentekoste ya mwaka 30BK.

 

. Vile vinara saba huwakilisha roho saba za Mungu kama malaika wa Makanisa saba.

 

. Lile Dume la ng’ombe au ndama dume ni ngo’ombe Dume wa Efraim, pembe za nyati ni Masihi (Kum. 33:17, Hes. 23:22 pia tazama Yer. 31:18).

 

. Kondoo waume wawili wanawakilisha mashahidi wawili wa siku za mwisho.

 

. Sadaka za dhambi na sadaka za amani huwakilisha upatanisho wa wateule kama mhusika kwenye kufanyiwa Upatanisho wa jumla.

 

Hatua kumi ngazi za msafara wa Kutoka utumwani zilifanyiwa pia mfano wa vinara kumi vya taa za kwenye hakalu la Mungu zikikunjuka kupitia miaka elfu mbili. Maendelezo ya msafara wa Kutoka Ramesesi ulikuwa kwenye hatua zake. Hatua ya kwanza ilikuwa ni Sukothi.

 

Sehemu ya kusanyiko la Ramesesi halikuhesabiwa kama hatua. Vivyo hivyo, Yohana Mbatizaji hakuhesabiwa kuwa mmoja wapo miongoni mwa zile taa za marejezo.

 

Kutoka Sukothi Israeli walielekea Ethamu (aya-thawm jina la Wamisri asilia, au Buthani: LXX) (Kut. 13:20; Hes. 33:6-8). Kutoka Ethamu Waisraeli walielekea Migdoli (maana yake ni mnara) (Kut. 14:2; Hes. 33:7) ambapo ni kabla ya Pi-hahirothi kwenye Bahari ya Shamu. Kutoka Pi-hahirothi, Wana wa Israeli walivuka Bahari ya Shamu na kuendelea mbele mwendo wa siku tatu hadi kufika Mara (maana yake uchungu kwa sababu walishindwa kuyanywa maji yaliyokuwapo pale, au Pricriae LXX) (Kut. 15:23; Hes. 33:8-9). Maji ya Roho Mtakatifu yalifanyika yawezekane kunywewa kwa kutumia mti mmoja (Kut. 15:25) mti ule alikuwa Masihi.

 

Kutoka Mara walitua marago na kuweka kambi Elimu (maana yake ni mitende; Bene Eliym maana yake ni Wana wa kiume wa Mungu) (Kut. 15:27; 16:1, Hes. 33:9-10). Kulikuwa na chemichemi ya visima kumi na viwili na mitende sabini. Hii iliwakilisha makabila kumi na mawili ambayo kila moja wapo lililishwa kutoka kwenye kijito ambavyo walitakiwa waamuzi kumi na wawili wa Israeli. Mitende kumi na miwili ilikuwa inawakilisha miti sabini ya wazee (Kut. 24:1,9), ya baraza la Sanhedrini na hatimaye baraza la wazee (Lk. 10:1,17). Jina Elimu limechukuliwa kwenye neno Eyil lenye maana ya nguvu, kwa hiyo mtemi, au kondoo mume, au mnara; kwa hiyo mti wa mpingo au mti imara. Kwa hiyo mtazamo unauwezo wa kupanua hadi kwenye maana ya Elimu au Eliym  maana yake yenye nguvu au miungu midogo kama inavyosema katika Zaburi 89:8. Mtazamo hapa ni kwamba ni Elohim au Eliym ya kwa jinsi ya lugha za kimfano na zenye kujaa mafumbo. Kwa hiyo, idadi ya sabini imechukuliwa kuwakilisha baraza pana la Jeshi la mbinguni. (Kwa hiyo, hawa sabini (wawili) zaidi ya miaka 2,000 kuunda msingi wa wale 144,000). Israeli waliingia jangwa la Sini baada ya Elimu kuelekea Sinai siku ya 15 ya mwezi wa pili (inadhaniwa ilikuwa ni Sabato?). Lile baraza la LXX linasema kuwa walitua marago na kuweka kambi katika Jangwa la Sini kukabili karibu na Bahari ya Shamu kutoka katika hatua ile waliingis kwenye jangwa (Hes. 33:11-12 LXX).

 

Watu walipewa mana kula mahali hapa. Kwa hiyo, baada ya mti wa Masihi na chemichemi na miti ya wele thenashara na wale sabini ambao Kristo aliwachagua kabla ya kufa kwake, waliingia jangwani. Walinung’unika na wakalishwa nyama ya kware wakati wa jioni na asubuhi. Kutoka hapo walilishwa mkate wa Mbinguni ambayo ni Yesu Kristo.

 

Kutaniko la wana wa Israeli liliendelea mbele kutoka Jangwa la Sini hatua kwa hatua kwa kufuata utaratibu kwa kadiri ya amri za Bwana (Kut. 17:1). Wakatua marago na kuweka kambi mahali paitwapo Dofka (maana yake kubisha hodi, kuiita nyota ya alfajiri. altarikh ambayo kwa lugha ya Kishemu, mf. Katika lugha ya Kiarabu, Nyota ya Alfajiri au yeye abishaye hodi au yeye ajaye usiku – ambaye ni Sara kwa mujibu wa kitabu cha Korani).

 

Kisha wana wa Israeli wakaweka matuo ya kambi huko Alushi (jina hili maana yake hayaeleweki) na kutoka Alushi waliweka matuo Refidimu (maana yake kitalu au kichala mnara, yenye kuenea nje au kwenda mbele) (Kut. 17:1; Hes. 33:14-15). Hivyo walisafiri katika mwendo wa kutangatanga ingawa inaonekana kuwa kikomo cha mwisho cha safari yao ilikuwa iwe kama inavyoonekana katika kitabu cha Hesabu 10 ila sasa amri hii haikufanyika hadi walipoondoka Sinai katika mwaka uliofuatia (Hes. 10:11). Kulikuwa hakuna maji pale Refidimu (Refidini, Hes. 33:14 LXX). Hii huwakilisha mwanzo au chanzo cha njaa au ukosefu neno la Mungu. Kutoka Refidimu walifika Sinai.

 

Hatua hizi kumi zinawakilisha hatua kumi za marejeo au matengenezo ya Masihi kwa kupitia yale Makanisa saba hadi kwa mashahidi wawili watakaokuwepo katika kipindi cha utawala wa milenia na zama mpya ya dunia. Hizi hatua kumi huwakilishwa na vinara kumi vya taa vya Hekalu la Sulemani ambako kulikuwa na vinara saba na meza kumi za mikate ya wonyesho. Mlolongo wa mwisho wa hawa mashahidi wawili unaashiria muunganiko au mlolongo wa kutangatanga. Kwa hiyo, Jeshi hawapo kwenye mwili au kundi moja.

 

Wana wa Israeli wakashambuliwa na Waamaleki huko Refidimu (Kut. 17:8). Kwa hiyo, walipokuwa kabla hawajafika tu Sinai katika matuo ya kambi la tisa, Wana wa Israeli wakashambuliwa na Waamaleki. Watu hawa walitakiwa waangamizwe kabisa wote maangamizo makuu sana kwa ajili ya kuwashambulia Israeli. Hii inatoa mfano kwa jinsi itakavyokuwa angamizo la siku za mwiisho kama lilivyonyeshwa katika kitabu cha Ufunuo 12:15-16. Hukumu hii inaongelewa kwa lugha ya mifano kama habari ya kondoo na mbuzi katika (Mt. 25:32-33), ambako mataifa yatahukumiwa kulingana na jinsi walivyowafanyia wateule kwa kipindi cha majaribu yao. Ilimlazimu Musa kuinua mikono yake juu kwa kipindi chote cha mapigano. Ili kufanikiwa kufanya hili, iliwabidi Haruni na Huri wamkalishe Musa juu mwambani, unaosimama kama nguvu za Mungu, nao wakasimama mmoja mkono wa kuume na mwingine wa kushoto wakimshikilia mikono yake. Jambo hili liliashiria ile hali ya kubadilika kwake sura (Mk. 9:4-5) na humwakilisha elohim wa Kristo, Musa na Eliya. Uweza wa Kristo kwa bidii yake ya kila mara mfululizo hadi kufikia ukamilifu wa dahari wa Siku ya Bwana. Yoshua wa kabila la Efraimu alipigana kwa siku nzima kutwa hadi kuzama kwa jua (Kut. 17:13). Baada ya Amaleki kushindwa, Musa akatembelewa na Yethro kuhani wa Midiani aliyekuwa anamtumikia na kutoa dhabihu kwa Mungu aliye hai yaani Bwana (Kut. 18:12). Ishara ya ukweli wa jambo hili linashabihiana na upatanisho na uongofu wa siku za mwisho.

 

Kuanzishwa kwa Utaratibu wa Waamuzi dhumini lake lilikuwa ni kuwekeza busara ya marejesho ya sheria zitakazo tumika kwenye mfumo wa utawala wa milenia. Yethro aliyasema haya katika kitabu cha Kutoka alijua kwamba Yehova ndiye Mungu mkuu kuliko miungu elohim yote.

 

Kutoka 18:11 inasema: Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa unyeti.

 

Hapa anaongelea juu ya YHVH wa Israeli aliye kuhani mkuu wa elohim chini ya Eloa au Elyoni, Mungu Mkuu Sana.

 

Wakati wa mwandamo wa tatu wa mwezi wakati walipokuwa wanaondoka Refidimu na kuweka matuo yao huko Sinai, Musa alipanda kwenda mlimani kwenda kupokea sheria na amri za Mungu na ili waweze kutengwa mbali kama watakatifu wa Mungu, ufalme wa kikuhani (Kut. 19:5-6), Hii ilitangulia ili kuashiria mafafanuzi ya kitabu cha Ufunuo 4 na 5. Israeli alichukuliwa kwenye mbawa za tai (Kut. 19:4) kama ilivyo kwa Kanisa (Ufu. 12:14). Mbawa hizo ni mbawa za Kristo.

 

Baada ya siku tatu, asubuhi ya siku ya tatu katika kipindi hiki cha giza, Musa alitakiwa pale mlimani. Musa akatumwa amlete Haruni kule juu pamoja naye, lakini watu walizuiwa kama ilivyokuwa kwa makuhani walivyotakiwa wajitenge na kutakaswa (Kut. 10:24). Kujitakasa na kutengwa huku kulikuwa ni mfano wa matayarisho ya ubatizo ili kwamba wawe tayari kupokea nguvu za Pentekoste katika kuja kwake Masihi. Kwanza kabisa, iliashiria kupewa kwa sheria ambazo ni utaratibu wa asili ya Mungu, na pili, ulikuwa unaashiria nguvu za Roho Mtakatifu toka kwa Masihi. Hesabu 11:25 inaonyesha kuwa Roho alimwagwa na kufurika kwa wazee sabini. Roho akasababisha waliokuwemo kambini, majina yao ni Eldadi na Medadi, watoe unabii ambacho katika kitabu cha Hesabu 11:29 ilichukuliwa kama changamoto kwa uongozi wa Musa. Musa aliwauliza kama walikuwa na wivu kwa ajili yake na akasema kuwa alitamani sana kama watu wa Mungu wangekuwa wote manabii. Na jumla ya idadi ya wote waliokuwepo kwenye tukio hili ilikuwa ni watu sabini na wawili.

 

Kipindi kilichokuweko kuelekea utoaji wa sheria katika Pentekoste chini ya Musa kilikuwa kinawakilisha kipindi kile chote cha kinachoelekea ujio wa Masihi. Aliwakilisha kuandikwa kwa sheria ndani ya mioyo ya Israeli kwa misingi ya kiroho.

 

Kisha Musa akapewa sheria kama zilivyoelekezwa katika kitabu cha Kutoka 20 kama ifuatavyo:

. Mungu akanena maneno haya yote akasema,

Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.

. Usiwe na miungu [Elohim] ila mimi.

. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa, BWANA, Mungu wako ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana uovu wa baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami huwarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.

. Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

.Ikumbuke siku ya Sabato na uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala mtumwa wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

. Usiue.

. Usizini.

. Usiue.

. Usimshuhudie jirani yako uwongo.

. Usitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.

 

Amri hizi za Mujngu zilikuwa kwenye makundi mawili. Nne za kwanza ziliwakilisha upendo wa Mungu. Zile sita nyingine ziliwakilisha upendo wa Wateule kwa kila moja na mwenzake. Kanisa Katoliki la Roma limejaribu kuiacha au kuiruka amri ya pili kwa kutumia ujanja wa kuiunganisha kijanja na ya kwanza na kuigawanya ile ya kumi iwe sehemu mbili; kwa kusema kuwa usitamani mke wa jirani yako na mali yake. Mgawanyo huu wa uwongo umechukuliwa kutoka kwenye utaratibu wa mambo katika Kumbukumbu la Torati 5:21 ambako umetanguliza kutaja wake mbele ya nyumba katika mlolongo wake. Ni kitu cha lazima kufanya mgawanyo wa uwongo kwao kwa sababu wao ni maarufu au wazoefu katika uvunjaji wa sheria na amri za Mungu kwa kubobea katika machukizo ya kuabudu sanamu za wale wanaowaita watakatifu na kuabudu misalaba na kuweka wanaoitwa watawa. Matendo ya kupiga magoti mbele yao au kuwasujudia kumekatazwa na ni machukizo makubwa. Ki uvunjaji wa sheria na amri za Mungu.

 

Sheria na amri hizi zinatokana na asili ya Mungu. Kwa hiyo wateule, kwa maana ya uweza wa kimbinguni, uitwazo Roho Mtakatifu, ni warithi wa asili hii ya kimbinguni (2Petro 1:3-4). Kwa hiyo, utendaji wa kiroho wa sheria hufanyiwa kazi na wateule nao wanahukumiwa kiuwazi uzidio. Kutamaki kitu chochote alichonacho jirani yako, kuona wivu au, mbaya sana bado chuki na hasira. Kamusi ya Kiingereza iitwayo The Oxford Universal Dictionary inaielezea husuda kama hivi:

Inahisiana na mkuleta madhara kumwangalia mtu (katika mtazamo mbaya) kama, madhara, uovu, uadui – 1707.b. kama tr. L. Invidia,Kisicho kawaida au kisicho maarufu – 1679.2. Kudhuru, kudhuru 1460.3. Kufanyiza na III kufanyizwa kwa wakati kwa mtazamo wa nasibu nyingine iliyo mzuri zaidi…4.a. Kufananishwa –1635, b. Kutamani bahati ya mwingine 1723.5. Tamaa, msisimko – 1607.

 1) mpito Kujisikia husuda kwa waliobahatika zaidi kwa kutilia maanani hali ya kutoridhika na mali za mwingine za (mwingine aliyefanikiwa zaidi). Pia kwa mtazamo binafsi: kujipendelea kuwa kwenye ngazi sawa na ya (mwingine) katika heshima sawa au kuchukuliwa na (kitu kingine ambacho mwingine anacho2). 2) Kujisikia kuona kijicho kunyume na mwingine – 1630. 3) mpito wa kufanyika kijicho au kufanyia kazi hali ya kijicho na unyimi….

 

Ni kitu kimoja kutumia neno kwenye mtazamo wa kusifiana sawa kama na kusema Nakuonea husuda furaha zenu au mahusiano yenu au chochote kile. Ni mwingine tu kujihisi msukumo. Kwa kutoa au kuonyesha husuda au mlango wa hisia kunapelekea kupenda kushambulia na kumharibu mtu mwenye kupenda kuonyesha dalili. Uvunjaji wa amri ya kumi kupelekea udufu wa uvunjaji wa amri ya kwanza pia. Vitu vyote vichukiwavyo huwa ni vya Kimungu. Kwa hiyo, adui huangukia kwenye dhambi hii wakati anapotafuta kumpingua Mungu. Kumchukia Mungu na hutafuta kuwa Juu ya Yote.

 

Isaya 14:13-15 inasema: 9Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako. Naam, walio wakuu wote wa dunia; huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi. 10 Hao wote watajibu, na kukuambia, je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! 11 Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. 12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. 16 Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme; 17 Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake…

 

Kifungu hiki cha maandiko matakatifu kinapaswa kifananishwe na Zaburi 75:2; 82:1; Ezekieli 28:12-14. Ni Kristo ambaye sasa analipokea kusanyiko na kutoa hukumu ya haki. kupandishwa daraja hutokana na ama kutoka mashariki ama kutoka magharibi, ama kutoka kusini. Lakini Mungu ndiye hakimu; yeye humshusha mmoja, na kumwinua mwingine (Zab. 75:6-7). Elohim huyu husimama kwenye makusanyiko la mwenyezi [Kwa Kiebrania, El au Miungu]. Yeye hufanya hukumu katikati ya miungu yaani elohim (Zab. 82:1, tazama Biblia iitwayo Interlinear Bible). Kerubi lililofunika lilichukua mahali pa Mungu, Shetani aliumbwa akiwa mkamilifu lakini aliipoteza nafasi yake kwa ajili ya uasi wake.

 

Ezekieli 28:11-19 inasema:Tena neno la BWANA likanijia, kusema. Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana, MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri. Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shobamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi yako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta ufunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huku na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. Kwa wingi wa uchuuzi wako, watu walikujaza udhalimu ndani yako nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi, mimi nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao wamekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao. Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele. (tumetia maandishi mazito ili kuweka msisitizo).

 

Huyu ni kiumbe mwenye nguvu za asili ametambika kama mwanadamu. Kwa hiyo anaweza kutambulika kama kerubi aliyefunikwa la mfumo wa kibinadamu kama inavyosema Ufunuo 4:7. Akatupwa hadi kwenye shmo la kuzimu na anatakiwa ashughulikiwe na aondolewe nguvu zake hatua kwa hatua-kwanza kutoka katika anguko lake na pili, kutoka katika kupunguzwa na kuondolewa kutoka kwenye uzima wa milele. Ili kuunda nguvu kuu za asili kwa mahala na wakati muhimu na kupunguza uweza wake kwa sababu muda, mjumuisho, na nguvu, kimwili, vitakuwa lazima zihusike na maelekezo ya kitu kile kile.

 

Shetani atakuwa ameangamizwa kwa moto kutokea ndani yake. Yeye anatakiwa kuwa ni chanzo cha ziwa la moto na amewekewa, na kwa kweli ni chanzo cha nguvu za asili ambazo hatimaye zitaharibiwa na kutoweshwa kabisa na mfumo wake (tazama jarida la Hukumu ya Mapepo [080]).

 

Moto huu uko sawasawa na moto au mwali wa moto ulia kutoka kwenye midomo ya vinywa vya wale washahidi wawili walioko kwenye Ufunuo 11:5. moto wa mwali wa moto utakao watesa wale wote watakao mwabudu yule mnyama na sanamu lake na kupokea muhuri wake ukitangulia na ghadhabu ya Mungu. Moshi wa maumivu ukipaa juu kwenye Nyakati za Nyakati, ili kuwafanya wale wenye walio na alama ya mnyama wasipumzike usiku wala mchana (Ufunuo 14:10-11). Kwa hiyo huu moshi wa maumivu hautakuwa wa milele kakini ukweli ni kwamba utakuwa kwa kitambo tu wakati wote wenye chapa ya mnyama.

 

Na waliokuwa wanapotezwa na manabii wa uwongo watauawa na hatimaye ufufuo w pili. Yule mnyama na yule nabii wa uwongo watatupwa wakiwa hai katika Ziwa la Moto (limnen tou puros) maana yake ni unaowaka na kuunguzwa na madini ya mlipuko yaitwayo kibiriti.

 

Ulimwengu ni theioo na inadhaniwa madini ya brimstone au sulpher yaani kibiriti yana maana ya kutoka kwenye mtazamo wa uzuri wa neno la theois yenye maana ya vitu vya mbinguni. Sawa kabisa isemavyo Ufunuo 9:17 ina theoodeis au kito cha thamani kama (theion na eidos). Wazo hapa ni kwamba kuwa na umbo la kiutauwa au la kimbinguni. Kwa hiyo, Ziwa la Moto laweza kuwakilisha nguvu za mbingu ya kiroho kwa myazamo wa mambo ya mbiguni (kama vile, nguvu za kiroho za Shetani zilivyokuwa).

 

Mawazo haya huhusiana na nguvu za kiroho za siku ya Pentekoste. Hii tena ilielekeza mbele kwenye dhabihu ya Masihi na kupokelewa kwa Roho Mtakatifu.

 

Wale wote wenye chapa ya mnyama watakuwa basanizo (watataabika au kuteseka) na hii puri na theioo mbele za malaika watakatifu na mbele ya Mwana Kondoo. Hii kapnos au moshi wa maumivu yao utapanda hadi juu milele na milele (Ufu. 14:11), iki maanisha hadi wakati utawala wa Milenia. Wazo na mtazamo kama huo huo ni lile la maangamizo ya mwana wa kuasi au asi atakayeangamizwa kwa nuru (epiphaneia) ya uwepo wake Kristo (2The. 2:8).

 

Kwa hiyo, nguvu za Roho Mtakatifu hutoka kwa Mungu ikionyesha asili yake ambayo kwa jinsi ilivyo yenyewe ikikomesha na kuangamiza Jeshi la malaika walioasi na kuanguka. Roho Mtakatifu huwapa uwezo wateule wote naye huondoka na kuwaacha wale Jeshi la waasi wasiomtii Mungu. Uwezekano ule wa kuangamizwa, kwa lazima, lazima uendelee hadi kwa Kristo au hakuna jaribio imara au ulinganisho kinyume ambavyo Shetani amekwisha hukumiwa.

 

Kristo alistahili kwa utii wake kuwa Kuhani Mkuu, akiwapatanisha kikamilifu wanadamu na Mungu. Walikuwa wameondolewa bila huruma kutoka kwa Mungu kwa ajili ya uasi wake Shetani na Jeshi la malaika walio asi waliokuwa wamebeba majukumu kwa ajili yao. Jeshi hili la malaika walioanguka na waasi watahukumiwa kwa matendo ya wateule, kwa namna zote mbili yaani kwa utii wao wa sasa na umakini wao kushikilia majukumu yao kwa kipindi cha maongozi ya utawala wa Milenia. Kwa hiyo, Malaika hawa waasi hawawezi kuhukumiwa kikamilifu hadi pale tutakapokuwa tumekamilisha kazi yetu yote.

 

Jinsi ya kuitambua dhambi na uasi kunachukuliwa kutoka kwenye amri kumiza Mungu kama kitu cha kwanza. Kuasi ni kama dhambi ya uchawi (1Sam. 15:23) kwa sababu wazo hili humzuia mtu kuwa na hiyari katika upinzani au kuwa mbali na mapenzi ya Mungu. Shetani, kwa kutafuta kwake kuingiza na kushurutisha mapenzi yake dhidi ya yale ya Mungu, akaasi na hivyo, akaanzisha imani ya miungu wengi. Imani ya kuabudu Mungu mmoja tu humzuia mtu kwenye mawazo ya kufanya michanganyo chini ya mapenzi ya Mungu. Hivyo basi, hakuna Mungu yaani elohim mwingine yeyote kabla au mahali pa Mungu au aliye sambamba na yeye au aliye sawa au kufanana na yeye na wala hana wa kumfananisha katika u-milele wake au aokoaye aliye katika mkono wake wa kuume.

 

Kwa hiyo, kuanzia kupokelewa kwa amri kumi za Mungu katika Pentekoste tunaona kuwa nguvu za Mungu zinafanya ziwepo kwetu sote. Kutokana na asili ya Mungu huwepo sheria zote na Roho Mtakatifu. Pentekoste ya pale Sinai ilikuwa ni ya wakati muhimu mno na ilielekeza mbele kwenye hatua ya kumpokea Roho Mtakatifu na Kanisa.

 

Suala hili kuhusu amri za Mungu na sheria liko kwenye mfano wa Kristo na kijana mmoja kama ilivyoandikwa katika Mathayo 19:16-22.

Mathayo 19:16-22 inasema: Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia Kwa nini kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo. Waheshimu baba yako na mama yako, na mpende jirani yako kama nafsi yako. Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena? Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

 

Mtu huyo alikuwa na upendo kwa wanadamu. Hatahivyo, hakuweza kuyaweka mawazo yake katika upendo wa Mungu na hazina ya mbinguni.

 

Mawazo lililohusishwa yalikuwa tu ni zile amri sita za mwisho zilizotajwa, lakini ile ya nne haikutafundishwa zaidi sana kama inavyohitaji kuhusu kumpenda jirani yako kama unavyojipenda wewe-kwa kuwa kwa tamaa unamshambulia na kumwangamiza jirani yako. Kutokana na amri hii unaangukia kwenye uvunjaji wa amri ya nne za kwanza kama ya pili, ya tatu na ya nne zikifuatiwa kutoka na ile ya kwanza na kwanza inavunjwa na ile ya kwanza na ya kwanza inavunjwa na ile ya kumi. Ibada za sanamu ni uasi na husuda au fitina. Kutoka uasi na husuda kusababisha chuki. Kutoka kwenye chuki huelekea kwenye vita au machafuko. Sawa sawa tu na jinsi ilivyo ni kuwa kutokana na tamaa huzaliwa mataa mbaya ya ngono na uasherati, ambayo nhusababisha machafuko kati ya mtu na jirani yake kupitia mke wake kwakuwa wao ni mwili mmoja. Kutokana na tamaa mbaya huchipuka uporaji na kutokana na uporaji huchipuza chuki, kwakuwa wizi na uporaji ni machafuko. Kutokana na ushuhuda wa uwongo huchipuza kukosesha haki inayosababisha uchoyo au woga na hivyo, kusababisha uvunjaji wa utoaji haki.

 

Kwa hiyo basi, kama amri moja kati ya hizi ikivunjwa, basi huwa zote zimesha athirika na kuvunjwa nasi tunakuwa kwenye hali ya kujisikia hukumu na dhamira mioyoni mwetu kwa ajili ya sheria hii. Sheria hutusimamisha kwenye asili ya Mungu na hivyo, sheria sio shinikizo lakini ni matokeo tu ya toba.

 

Utaratibu huu wote mzima wa Sheria kwenye Pentekoste hutuelekeza kwenye ubatizo wa moto. Kanisa halipokei nguvu tu. Nguvu zilikuwa za uongofu kwa kuiwakilisha asili ya Mungu Kanisani. Huo mndio mfano wa moto. Katika siku ya Pentekoste ile ya kwanza ya Kanisa, tabia za Mungu zilidhihirika kwa kuonekana moto ukimkalia kila mmoja wao na kuwekeza sheria ndani ya mioyo yao.

 

Tunaishika Sabato kwa vile Roho Mtakatifu hutushuhudia sisi kutoka katika wongofu wetu, sio kwa kushurutishwa lakini kwa maana inayoingia akilini ihusuyo uongofu wetu. Sisi ni washiriki wenza, katika umbo la Mungu, kama alivyokuwa Kristo ambaye hakuona kuwa ni kitu cha kushikamana nacho kwa kule kuwa kwake sawa na Mungu (Flp. 2:6). Kwa hiyo, sisi tunatii tu mapenzi yake kama ilivyokuwa kwa Bwana wetu Masihi. Kutokana na kumfahamu kwetu Mungu wa pekee wa kweli na mwanae wa pekee Yesu Kristo tunaurithi uzima wa milele (Yoh. 17:3). Utii wetu kwenye sheria za Mungu ni jambo muhimu la pili la kufaa na hutokana na uelewa kumjua Mungu wa pekee na wa kweli, Eloah au Mungu Mkuu aliye Juu sana amabaye ni Baba yetu na Mungu na Baba wa Bwana wetu Kristo (Yoh. 20:17).

 

Msafara wote wa kutoka utumwani hadi kufikia Pentekoste pale Sinai kulionyesha maendeleo ya Israeli hadi kufikia huduma ya Masihi na kusulibiwa kwake na upatanisho wake kwa kupokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste kunako mwaka 30BK. awamu ya pili ya safari yao ya miaka 38 jangwani hufananishwa na kipindi cha Kanisa kuwepo jangwani kwa kipindi cha Yubile 38 na hii itafafanuliwa vizuri zaidi kwenye jarida lijalo.

 

q