Makanisa ya Kikristo ya Mungu

 

 

[117]

 

 

Roho Mtakatifu

 

(Toleo 3.2 19940515-20010527) Ipo kwenye Kanda

 

Roho Mtakatifu amefafanuliwa kiundani sana kwenye jarida hili. Chanzo cha utata kuhusiana na utendaji kazi wa huyu Roho Mtakatifu na utendaji kazi wake kwenye Maagano yote la Kale na Jipya yote imefafanuliwa. Roho Mtakatifu anaonyeshwa kuwa ni nguvu za Mungu na sio nafsi kama mwanadamu. Namna ya jinsi ya utendaji kazi wake huyo Roho wa Mungu inaonekana kuwa ni msaidizi mwenye kuwapa msukumo wateule ili wafikie hatua ya kuwa elohim au theoi kama Kanisa la kwanza lilivyo ishindania imani kama Zekaria 12:8 inavyosema. Jarida hili limetayarishwa ili kufundisha na kufikia kiwango cha uelewa wa jambo lihusulo Uungu.

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Copyright © 1994, 1995, 1997, 1998, 1999, 2000 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

 


Roho Mtakatifu [117]

 


Jinsi ya Kuadhimisha Pentekoste

Wakati wa Pentekoste ni muafaka kwetu katika kuangalia na kuwekea uzito masuala mbali mbali. Kunaweza kuchukua nakili za muhimu sana kutoka kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 2, panapoweza kutuonyesha na kutufundisha njia sahihi ya jinsi ya kuadhimisha Pentekoste.

 

Matendo ya Mitume 2:1-21 inasema: Hatailipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi waliokaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. 6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenywe. 7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? 8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahidi na Wakapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia na Pamfilia, Misri na sehemu za Libya karibu na Kirene na wageni wakaao Rumi, Wayahudi na waongofu, 11 Wakirene na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu. 12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? 13 Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya. 14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, 17 Itakuwa siku za mwisho,asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataota ndoto. 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatbiri. 19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto na mvuke, na moshi. 20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri. 21 Na itakuwa kila atakaye liitia jina la Bwana ataokolewa.

 

Fungu hili la maandiko matakatifu linabeba idadi kubwa ya maelekezo. Kwanza kabisa, tuangalie aya ya 1.

 

Matendo 2:1 inasema: Hatailipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

 

Inaonyesha kuwa kuna ulazima wa kuwa na kusanyiko muhimu la Kanisa kwa siku hii ya Pentekoste. Ni Sikukuu ambayo tunatakiwa au kulazimika kutoka na kwenda kukusanyika kwa moyo mmoja katika mahali pamoja. Hivyo basi, suala si kujiuliza kama inatakiwa kuadhimishwa ukiwa nyumbani kwako, hapana ila tu ni kwa ule mwaka wa kutoa zaka ya tatu tu ndio unaoruhusiwa kwa watu waweza kuadhimisha Sikukuu hii wakiwa hata majumbani kwao lakini sivyo ilivyo kwa miaka mingine. Tunatakiwa na Mungu kuwepo kwenye kambi la maadhimisho ya Sukukuu ya Pentekoste katika mahali atakapopachagua alikalishe Jina lake palipochaguliwa kwa dhumini hili hili kama ifanyikavyo kwa Sikukuu hizi mbili nyingine, ambazo ni za Pasaka na Sikukuu ya Vibabda, kwa jinsi zinavyoadhimishwa na watu wasiende mbele za Bwana wakiwa mikono mitupu (Kum. 10:16).

 

Na inasema kuwa ‘Hata ilipotimia siku ya Pentekoste.’ Kwa maneno mengine, kuna mambo mawili muhimu kufanyika kwenye Sikukuu ya Pentekoste, yanayoshabihiana kati ya Sabato na siku ya Pentekoste. Hata ilipotimia walikuwako wote mahali pamoja. Kwa maneno mengine, kutokea siku ya Sabato wangeweza kukutanika pamoja kwenye Sikukuu ya Pentekoste. Pengine hili ni mtazamo wa Sabato ya pili baada ya ile ya kwanza (inaitwa Sabbatton deuteropro) ya Luka 6:1.

 

Kutokana na maadhimisho sahihi ya Kanisa kwa Pentekoste (hii ilikuwa ni adhimisho la Kanisa la kwanza la Pentekoste), Roho Mtakatifu akawashukia kwa nguvu nyingi. Wakaweza kusema kwa lugha mpya na wakaweza kutabiri matendo makuu ya Mungu na kumtumia Roho Mtakatifu. Ingeweza kusemwa kuwa ilikuwa ni maadhimisho yasiyo sahihi ya Pentekoste ikithibiti uwezo wa Kanisa kutumiwa na Roho Mtakatifu, na kuzuia kuadhimisha na nia safi.

 

Wakati walipoanza kusema kwa lugha ya ndimi na kutumiwa na Roho Mtakatifu, baadhi ya wale waliofika kuwatembelea Wayahudi waliokuwa wakiwasikiliza walisema kuwa walidhani walikuwa wamelewa. Petro akawajibu akasema kuwa ilikuwa ni saa tatu ya mchana. (aya ya 15). Hii inatupa muda kamili ambao ibada ya Pentekoste ilikuwa inafanyika. Saa tatu ya mchana ni sawa na 3:00 Asubuhi. Kwa hiyo, ibada ya Pentekoste lazima ianze saa 3:00 Asubuhi, na lazima tuchukue hatua za kuwa kila mmoja wetu yupo tayari katika siku ya Sabato ili kwamba sote tuwemo kwenye eneo la ibada ya Pentekoste kufikia saa 3:00 Asubuhi, muda kamili bila kukosa wala kuchelewesha.

 

Ni nani au kwa namna gani basi Roho Mtakatifu aliingia kwenye Kanisa siku ya Pentekoste? Je, ni kwa namna gani tendo hili linahusiana na Mungu?

 

Jarida la Mwanzo

Tumeshughulikia na mambo mawili ya kwanza yahusuyo muunganiko katika Uungu, kama unavyojulikana kwa wengi kama Mungu Baba, na Yesu Kristo kama Mwana wa Mungu. Hitimisho linalopatikana kutoka kwenye sura ya kwanza ya jarida letu la Matamko ya Msingi wa Imani ni kwamba Mungu Baba ndiye hakika Mungu wa pekee na wa kweli na kwamba Yesu Kristo niMwana wa Mungu na kwa kujua na kuamini hivyo ni muhimu katika kuurithi uzima wa milele (Yoh. 17:3)

 

Mungu Baba

Mwenye kustahili kuwa kwenye Ubora wa mambo ya Uungu katika ulimwengu wote ni Mungu. Yeye ndiye Mwenyezi, Muumbaji na Mwenye kuwezesha kuwepo kwa Mbingu, dunia na vitu vyote vilivyoko ndani yake (Mwa.1:1; Neh. 9:6; Zab. 124:8; Isa. 40:26,28; 44:24; Mdo. 14:15; 17:24,25; Ufu. 14:7). Ni yeye peke yake asiyeweza kufa na mwenye kuishi milele bila kufa (1Tim.6:16). Yeye ndiye Mungu na Baba yetu na Mungu na ndiye Mungu na Baba wa Yesu Kristo (Yoh. 20:17) Yeye ndiye Mungu Mkuu Juu ya miungu yote (Mwa.14:18; Hes. 24:16; Kum. 32:8; Mk. 5:7) Nandiye Mungu wa Pekee wa Kweli (Yoh. 17:3; 1Yoh. 5:20).

 

Yesu Mwana wa Mungu

Yesu ndiye mzaliwa wa kwanza (prototokos) wa uumbji (Kol. 1:15) ambaye ni mwanzo (arche) wa uumbaji wa Mungu (Ufu. 3:14). Yeye ndiye mzaliwa wa pekee (monogene) Mwana wa Mungu (Mt. 3:17; Yoh. 1:18; 1Yoh. 4:9), aliyetungwa mimba yake kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na mwanamke bikira, Mariamu ambaye kwa makosa sana watu humwita Mary kwa Kiingereza na Maria kwa Kiswahili (Lk. 1:26-35). Yeye ni Kristo au Masihi (Mt. 16:16; Yoh. 1:4), aliyetumwa na Mungu ili awe Mwokozi na Mkombozi wetu (Mt. 14:33; Yoh. 8:42; Efe. 1:7; Tito 2:14).

 

Kutokana na mtazamo huu wa kiimani hivyo basi tunakabiliwa na ukweli na utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Wanaoamini mafundisho ya Utatu wanaelezea hii kama ni nafsi tatu kama fumbo la Imani kuhusu Mungu inayotokana na mawazo au mitazamo ya falsafa za Kiyunani. Chanzo cha mawazo haya kuingizwa kwenye Ukristo imefafanuliwa kwenye jarida la Chimbuko la Uumbaji wa Mungu akiwa kama Mwanzo na Mwisho [229] na Matumizi ya neno Fumbo la Imani [230]; na Chanzo cha Christmas na Easter [235].

 

Mtazamo wa muundo wa Wababeli, ambao uliingia kwenye mfumo wa wenye msimamo mkali wa kidini, ni udanganyifu wa wazi kabisa. Mafundisho haya yameliingiza Kanisa la Mungu kwenye maonyo ya nyakati za mwisho kwa kadiri vile dalili za kuja kwa Krjsto zinavyoonekana. Kristo alitoa ufafanuzi kwa alivyotenda ili kuonyesha kuwa yeye ni mwanzo au chimbuko la uumbaji wa Mungu.

 

Ushawishi wa mwanzo uliovuta watu wengi kwenye imani inayofundisha kuwa wanaweza kupata wokovu kwa kutegemea elimu, ujuzi au akili wanaoitwa Wa-Gnostiki kwenye Ukristo ulioanzishwa na Clement umefafanuliwa katika jarida la Chimbuko la Uumbaji wa Mungu akiwa kama Mwanzo na Mwisho [229]. Tutaona kuwa Clement alikuwa yuko sawa, kusema kuwa Mungu alikuwa ni chanzo chake na kwamba Aliumba kwa mapenzi yake mwenyewe na kwa kutokana na mapenzi yake vitu vyote vilifanyika (Ufu. 4:11). Kwa hiyo, Mungu ndiye muumbaji, lakini Kristo alikuwa ni chombo tu kutumika katika uumbaji na alikuwa ndiye mwanzo wake (tazama hapo juu)

 

Wazo la kwamba hekima wa kimbinguni ni mshauri wa Mungu na mwanzo wa wote alioumbwa na Mungu ni kwa mujibu wa mwandishi maarufu aitwaye Salvatore Lilla kwenye jarida lake la (Clementi wa Alexandria, Sura ya III, kutoka Oxford University Press, 1971, vifungu vya 192-230) likiongelea tabia za falsafa za Wayahudi wa Alexandria zilizotangulia za Philo. Kwa hiyo, Wayahudi wa Alexandria walijua kwamba hekima ilikuwa kitu cha kwanza kabisa miongoni mwa mambo mengine aliyoumba Mungu. Kwa hiyo ilitangulizwa na Mungu, kupitia neno la Mungu kisha kulileta kwenye matendo na kufungwa pamoja na Mungu, kwa hekima kama Roho Mtakatifu. Ni Sofia kwenye Mhubiri 1:4 na aliyefanyiza utunzi wa Mithali 8:22. Kitabu cha Hekima ya Sulemani kinaonyesha kuhusika kusaidia pamoja na Mungu katika uumbaji. Kitabu cha Mwanzo husema Roho ya Mungu katika Mwanzo 1:2. Waandishi waliokuwepo kabla ya Kristo walielezea kwa makosa sana jambo hili la nguvu za Mungu kama mwanadamu na makosa haya yameendelea kushikiliwa na kuaminiwa na watu hata siku za leo kama Roho Mtakatifu angetazamwa kama nafsi iliyo kama ya mwanadamu. Huu ulikuwa mwanzo wa mafundisho haya yenye makosa.

 

Ni jambo linalofikirika kuwa Roho ni mwanzo wa Mungu, kwa sababu kizazi cha uzao wa Kristo na elohim wengine walifanya hili lionekane muhimu kufikirika kwa pale kuwa ni mahali pa kufanyia kazi kwa uaminifu wao kwa Mungu.

 

Ili kuwepo kikamilifu imani ya kuabudu Mungu mmoja tu kama inavyounganishwa kwa wote. Mungu ndiye kiini cha viumbe vyote. Viumbe vyote katika Jeshi la watu wa Mungu wanafungamanishwa na yeye na Roho Mtakatifu. Ni kwa kupitia Roho Mtakatifu tabia za Mungu zinaingizwa ndani ya wote wenye mwili, kote kuwili yaani Kristo na kwa wateule wengine, na kwa wanadamu wote kokote kule. Hiyo ndiyo miundo na hadi pale tutakapoelewa mchakto huo hatuwezi kwa kweli kuelewa kile kinachotokea na Roho Mtakatifu. Hutokea hivi kwa sababu sheria za Mungu huanza kutoka kuwepo kwa wema wa tabia za Mungu. Kwa hiyo, haiwezi kuwa ni imani ya Kibinitaria, kwa sababu kuna hali kamilifu ya kuweka wema wote pamoja, na wema ule ni Mungu. Kristo alisema kuwa aliye mwema ni mmoja tu ndiye Mungu; kwani waniita mwema aliye mwema ni mmoja tu naye ni Mungu kwa sababu ya ukweli kuhusu uwekaji pamoja wema wote. Hatuwezi kuwa na mfumo wa dithist. Kuchunguza na kujiuliza maswali, kutilia mlinganisho na ufahamu wa akili za kibinadamu hupelekea kutupajibu la kuwa hatuwezi.

 

Sheria ya Mungu kuanzia tokea kuwa na uwepo wa wema wa tabia yake

Sheria ya Mungu kuendelea kutoka kwenye tabia ya Mungu hivyo husimama milele, kama Mungu mwenyewe alivyokuwa ni Mungu asiyebadilika hakika ni mwema akiwa kama ni makao ya wema wote. Hii inaonekana kwenye majarida ya Serikali ya Mungu [174] Upendo na Utaratibuwa Sheria [200] na pia Tofauti mbalimbali za Sheria [096].

 

Kwenye Injili ya Marko 10:18 Kristo alisema Kwa nini kuniita wema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. Wema wa Mungu hutumwongoza kila mmoja wetu kwenye toba (Rum. 2:4). Tabia za asili za Mungu zimetuama kwenye wema usiobadilika. Jeshi la malaika wa mbinguni hushiriki tabia zake za asili. Kwa hiyo wanashikilia kwa siku zote kwenye tabia hizi za asili za mbinguni na wema  wake. Kwa jinsi hiyo basi Kristo anabakia kuwa ni yeye yule, jana, leo na hata milele (aioonas) (Ebr. 13:8). Wateule kwa kushiriki kwao tabia hii ya asili ya kimbinguni (2Pet. 1:4), hufanyika kuwa ni sehemu ya ukuhani wa kimbinguni, kama wa Melkizedeki, ambao unahamishika (aparabaton) au asiyebadilika kwa kizazi hata kizazi (aioona) (Ebr. 7:24). Kristo aweza kuwaokoa wale wote wamjiao Mungu kupitia kwake (tazama Ebr. 7:25 hasa kamusi ya Marshalla’s Greek-English Interlinear inaeleza vizuri zaidi). Lakini yeye sio kiini cha kufanyiwa ibada na wala sio yule Mungu aamurishaye kwa mapenzi (tazama jarida la Mungu Tunaye Mwabudu [002]).

 

Sisi hatukaribiani na mfumo na utaratibu wa Wadheisti. Tunamkaribia Mungu kupitia Kristo na hivi ndivyo tunavyookolewa. Maandiko haya yote matakatifu yaweza kuwa ama yameacha na kudharau au yamekarabatiwa kwa makosa na wanaoamini juu ya ushirikishi wa miungu miwili yaani wa Binitaria na wenye kuomba Mungu kwa kupitia watu wengine yaani Wadheisti.

 

Sheria ya Mungu inapaswa kuishika na kuifuata kwa imani na sio kwa kwa kufanya kazi fulani kwanza (Rum. 9:32). Tuna Agano Jipya ambalo kwalo Bwana ameweka sheria zake kwenye nia ztu na kuziandika mioyoni mwetu. Yeye ndiye Mungu wetu na sisi ni watumishi wak, tumwabuduo yeye, na kuzishika sheria zake katika tabia zetu zilizogeuzwa (Ebr. 8:10-13). Hatuzishiki sheria za Mungu kwa kuwa tu zimeandikwa vitabuni. Wala hatuzishiki kwa kuwa kuna hukumu mwisho wake. Wateule hufikia kwenye kiwango pale tunapotaka kuzishika kwa kuwa tumehifadhiwa kwa kiasi kikubwa na ile tabia ya asili ya Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu, na kwamba Roho Mtakatifu huiongoza miguu yetu mmoja hadi mwingine kwenye sheria. Ni kwa kupitia Roho Mtakatifu tu ndipo tunaweza kuzishika bila ya kushurutishwa kwa kuwa mawazo ya mwanadamu (mawazo ya kimwili) ni uadui na Mungu. Wala huwezi kufanya unalolitaka. Mawazo ya mwanadamu hupenda tu kufuata zile njia ambazo ziko kinyume kabisa na asili ya wema wa Mungu. Roho Mtakatifu ndiye ambaye kwa kupitia kwake mawazo yetu huweza kuongoka. Sisi mara nyingi tunamfuata Mungu nje ya tamaa zetu, kwa kuwa yabia zake za asili hukaa ndani yetu na ni kinyume kabisa na tabia zetu zenye asili ya dhambi. Kwa hiyo, Roho Mtakatifu ni nini basi?

 

Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu kwa mujibu wa kitabu cha Matendo ya Mitume 2:4 ni chanzo asilia cha nguvu za Mungu ambayo Kristo aliahidi kuwaletea wateule (Yoh. 16:7). Yeye sio nafsi kama mwanadamu bali ni mgawanyo wa nguvu zilizo hai za Mungu. Yeye ndiye mwenye kutuwezesha kutufanya kuwa ni warithi wa tabia asilia za kimbinguni (2Pet. 1:4), kujazwa na nguvu za Roho Mtakatifu (Mdo. 9:17; Flp. 5:18) na hatimaye kwa Watoto wote wa Mungu (Ayu. 1:6; 2:1; 38:7; Rum. 8:14; 1Yoh. 3:1-2) na kufanywa warithi pamoja na Kristo (Rum. 8:17; Gal. 3:29; Tit. 3:7; Ebr. 1:14; 6:17; 11:9; Yak. 2:5; 1Pet. 3:7).

 

Roho Mtakatifu ametilewa na Mungu kwa wale wanaomuomba (Lk. 11:9-13) na anayemtii, hukaa kwa wale wanaozishika amri zake Mungu (1Yoh. 3:24; Mdo. 5:32). Watakatifu ni wale wazishikao amri za Mungu na wenye ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufu. 12:17, 14:12).

 

Katika kitabu cha Ayubu 38:7 tunaona kuwa kulikuwa na wana wa Mungu kabla ya kuwekwa kwa misingi ya dunia. Yesu Kristo hakuwa pekeyake mwana wa Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya dunia. Walikuweko wengine wengi. Hakuwa pwkeyake Nyota ya Asubuhi siku kabla ya kuwekwa Misingi ya dunia bali walikuwako wengine wengi.

 

Walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache, kwa kuwa Mungu ametoa ahadi kuwa kama tukimuomba yeye atatupa Roho wake Mtakatifu. Amemtoa huyo Roho Mtakatifu kwa mamilioni ya watu wake. Wengi wameshindwa, na kuwa wameitwa tu lakini sio kuchaguliwa. Usemi wa kitaaluma unasema wamenda kama mbwa anayeyarudia tena matapishi yake na kumtenda jeuri Roho.Mtakatifu. Watu kama hao hurudi nyuma hadi kwenye ufufuo wa pili. Lakini hawakupewa majukumu au kuhesabiwa kwa ajili yake, kwa sababu ilikuwa inajulikana kama wangeweza kuyafanyia kazi [pia tazama jarida la Mafundisho Potofu Kuhusu Ufufuo wa Tatu [166]]. Hawakujaliwa kuwekwa wakfu kabla; hawakujulikana hapo zamani kabla. malimbuko la tunda la Roho Mtakatifu hayakutolewa kwao kulingana na Warumi 8:23. Wamepewa Roho Mtakatifu lakini hawawezi kudumisha imani.

 

Roho Mtakatifu ni mfariji anayewaongoza watumishi wa Mungu kwenye kweli yote (Yoh. 14:16,17,26) (tazama jarida la Kweli ya Mungu, [168]. Uwezo wetu wa kuelewa kweli yote unategemea juu ya uhusiano wetu na Mungu kupitia kwa Roho Mtakatifu. Ni kwa njia ya kuendeleza uhusiano wetu na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu tu ndipo tunaweza kuielewa Biblia. Vinginevyo, tutayaona kama maneno ya kawaida tu. Watu wengi hawalielewi hili kwa sababu mahusiano yao na Roho Mtakatifu hayaendelezwi. Hili si suala la nguvu au uweza (na Roho Mtakatifu ndio nguvu). Roho Mtakatifu ni Roho wa uweza na itashuhudiwa kwetu katika siku za mwisho, kama nguvu, na wa akili timamu, na mwenye kuelewa ukweli. Kwa watu wengi, Biblia wanaiona kama ni maneno ya kawaida tu, kwa kuwa  hawakuwa watiifu na kukua katika Roho Mtakatifu.

 

Ni kwakupitia tu kwa Roho Mtakatifu ambaye mtume Petro alisema kuwa angefanya. Hii ndiyo maana Kristo amwambia una heri wewe Simoni Bari-Yona. Alielewa kwa kuwa Roho Mtakatifu aliwapa uwezo wa kuelewa. Hatupaswi kumlaumu mtu yeyote ambaye bado hajampokea Roho Mtakatifu. Ni kwa watu wale wale ambao hawajaitwa na ambao hawajapewa uwezo wa kuelewa. Tunapaswa kuwaombea. Tusisimame kinyume nao.

 

Matunda ya Roho Mtakatifu yameorodheshwa katika 1Wakorintho 12:7-11 na tunda la Roho limeelezewa kwenye Wagalatia 5:22-23 (tazama jarida la Tunda la Roho Mtakatifu, Na. 146. hatolewi kwa kipimo kwa mujibu wa Yohana 3:34 na Warumi 12:6. kwa kupitia yeye ndipo hatimaye Mungu hufanyika kuwa ni yote katika yote, kwa mujibu wa 1Wakorintho 15:28 na Waefeso 4:6. Karama na tunda la Roho Mtakatifu haviji kwa kupitia huduma na havikutabarukiwa kwa kulingana na utaratibu wa mgawanyo wa madaraja ya vyeo vilivyopangiliwa kibinadamu. Watu wengine karama ya kupambanua roho, neno la maarifa tarsiri za lugha, kufundisha. Wengine wamepewa karama za kuponya; wengine imani kiasi cha kuhamisha milima, zaidi ya wengine waliopewa karama za kusimamia shughuli za maongozi. Hili ni jambo ambalo Kanisa halijaelewa kuhusu mgawanyo wa ngazi za maongozi. mgawanyo huu wa maongozi huharibu uwezo wa kuelewa utendaji wa Mungu.

 

Waamini Utatu huweka madai yao kuwa Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya umoja uliofungamana wa Uungu. Huu ni uongo na ni fundisho lisilo la kweli. Fundisho hili linaweka kikomo cha uweza wa Roho Mtakatifu kutufikia sisi, ili kutuwezesha sisi kuwa na uweza wa kimungu yani elohim au theoi.

 

Roho Mtakatifu huanza kufanya kazi kuanzia wakati unapobatizwa. Roho Mtakatifu huwaleta wateule kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu (Ebr. 7:25). Malimbuko ya Roho Mtakatifu hutolewa kwa kila mmoja binafsi yake wakati wa ubatizo kwa mujibu wa Warumi 8:23, ambayo inasema wazi kuwa kufanywa wana hakukamiliki mpaka uje kwanza ukombozi wa mwili. Kwa hiyo tumezaliwa mara ya pili lakini tunaendelea kukua katika Roho kila siku ndani ya Kristo Yesu hadi kuufikia ukamilifu wa utukufu wa Mungu. Roho Mtakatifu ni Roho wa kweli (1Yoh. 4:6, 5:6) na kwa kusema kweli, tunaenelea kukua katika Kristo aliye kichwa cha kila lenye sifa njema (Efe. 4:15). Sio lazima sana kwetu kusema ukweli wote katika kila jambo. Wakati mwingine si busara kusema ukweli wote kwa kila jambo, kwa mfano tunapokuwa kwenye mazingira ya kutopendezwa na kitu fulani kwa ajili ya mtu fulani, hatulazimiki sana kuwa ni lazima tuwaeleze wenyewe hivyo. Tunatakiwa tujue wewenyewe tu. Yanaeweza hata hivyo yakawa ya kweli lakini pengine ni busara kunyamaza kimya tu. Huko si kuongopa kwa kuacha kusema ila ni busara iliyo njema. Kuna tofauti kati ya kusema uongo kwa kurukaruka kusema mengine na kunyamaza kimya. Ikiwa tukijizuia yaani kutosema kitu kwa wakati, kwa kweli, ambao tulitakiwa kusema kitu fulani hivyo basi hapo tunaongopa, kwakuwa tumekwepa kutoa ushahidi. Hivyo basi tunabeba ushahidi wa uongo kwa kunyamaza kwetu kimya. Hii ni muhimu. Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu (Rum. 8:14) na ni Roho wa imani (2Kor. 4:13) anaye chunguza kila kitu na hujua kila kitu (Kor. 2:10-11; 12:3).

 

Kwa hiyo, Roho Mtakatifu sio kitu kilicho peke yake kikijitegemea cha Mungu wa Utatu shirikishi, lakini yeye ni mwenye kutuwezesha sisi kufikia kua elohim. Hatuwezi kufika kwenye kima cha Eloah. Mungu alikuwa na jina la umoja akiwa kama Eloah. Sisi tunafikia kiasi cha kuwa elohim au theoi kwa kupitia Roho Mtakatifu. Hii ni tofauti ya muhimu kwa kuwa kwa ujumla wao watu kama matokeo ya juhudi za kuinguza kwao mafundisho ya wana Utatu, hawawezi kuelewa kuwa kuna Mungu mmoja tu, Eloah, na kwamba kuna familia moja ya elohim (pia tazama jarida la Zaburi Na.14). wanadhani kuwa ni kukufuru kusema kuwa tuta kuwa miungu midogo elohim kwa kuwa hawaelewi elohim ni nini na wako wapi. Lakini bado tutakuwa elohim (Zekaria 12:8). Roho huwakilisha kwa Mungu mawazo ya mioyo yetu na utu wetu na halafu hutukirimia tabia njema na wema asilia wa Mungu mwenyewe.

 

Yohana 10:34-35 inasema: Yesu akawajibu, je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? 35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka)………..

 

Katika kupelekwa kupitia Yesu Kristo akiwa kama mwombezi na elohim mpatanishi asimamaye kati yetu na Mungu, Roho Mtakatifu kumuwezesha Kristo kutusaidia, kutufundisha na kutufariji na kutuwezesha kuzifanyia kazi nguvu za Mungu. Roho humkirimia kila mmoja wetu vipawa ambavyo Mungu hupendezwa navyo kusudi aufaidie mwili ambao ni Kanisa kama ilivyoelezewa kwenye 1Korintho 12:7-11. Mungu ametukirimia sisi sote vipaji mbalimbali na kutuweka sote pamoja ili tuweze kufaidiana. Mungu ameweka ndani ya kila mteule kiwango fulani cha uweza ambao wengine haikuwa lazima kwao wawenao. Sote tunaifanya ile kazi ambayo tulipewa na Mungu tuifanye. Tumepewa watu wenye kamara mbali mbali na vipaji na Mungu amefanya kwa utukufu mkuu zaidi kwa wote. Mwili ulio kanisa hufaidika kwa utendaji kazi wa kila mmoja wetu, lakini tunaweza kuuzimisha utendeaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kama hatutavuta uzito wetu kila mtu binafsi yake, tunaweza kumzimisha Roho Mtakatifu. Tunaathiriana kila mtu na mwenzake kwa sababu hii ya kuwa sisi ni mwili mmoja. Kwa hiyo kama sisi hatuombi, kufunga saumu na kufanya kazi, tunapunguz nguvu au uwezo wetu na hizi sio nguvu zake mtu bibafsi, ni nguvu za Yesu Kristo. Hakuwa Musa yule aliyekaa pale na kuinua mikono yake juu; alikuwa na Haruni na Huri kwa pamoja walimshikilia mikono yake na kuiinua juu. Sio Kristo afanyaye kazi hii kwa ajili yake mwenyewe tu. Ni sisi kila mmoja wetu ndio tunaomshikilia Kristo mikono yake juu, yeye ambaye ni Musa ajaye. Inatupasa kufanya kazi. Kama hatutafanya kazi, hatutafikia mafanikio kwa kiasi kikubwa cha kadiri tunayoweza na ni watu wachache mno waliofikiwa na kuhubiriwa kweli ya neno hili. Kwa hiyo, watu wengi wamejikwaa na kuwa kiuadui wameathirika na hii imepelekea kazi yetu kuwa ngumu zaidi ya pale awali kwenye ufufuo wa pili. Wengi wa hawa watu wameharibiwa na kuifanya kazi yote ifanyike ngumu zaidi. Mapepo pia wamepewa kwa lazima usemi wa kicheko kwa kuwa sisi hatufanyi kazi na sio kwa sababu ya neema yetu tuliyonayo. Iwapo kama tukishindwa kabisa, itakuwa sasa kwamba mapepo wamehesabiwa haki kabisa. Hii ni hali kamili halisi ya ni kwa jijnsi gani vita hii ilivyo….kwa uhalali wa mapepo kwa sababu wamemkufuru Roho Mtakatifu.

 

Roho Mtakatifu anaweza kuzimishwa (1Thes. 5:19) kwa namna ya kukataliwa au kuhuzunishwa (Efe. 4:30) na huweza kufanikiwa na kupoteza wateule . kwa hiyo sisi tunaweza kupewa uweza huu wa Roho Mtakatifu, kumkulia, na halafu kuanza kumfanyia kazi  au kutenda dhambi, ambazo kuzuia uwezo wetu wa kushughulika mambo haya. Dhambi hizi huzuia kiwango chetu cha kukua, na kwa kadiri tufanyapo dhambi, tunapunguza uwezo wetu katika maeneo mengi na tunamuhuzunisha Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hutuacha tunapokuwa tunatenda matendo ya dhambi. Kila mmoja wetu ameruhusiwa aende kwa kufuata hatua hizo, mahali tukijua kwamba tumepoteza nguvu katika uweza wa Roho Mtakatifu kwa ajili ya yale yanayoendelea ndani ya fikara zetu.

 

Tunda la Roho Mtakatifu ni Upendo, kwa mujibu wa Wagalatia 5:22. hii ndiyo dalili kuu ya kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, iwapo kama tukijikuta hatupendani kila mtu na mwenzake, basi Roho Mtakatifu hayupo dhahiri mahali hapo. Hivi ndivyo ni kwa vipi Roho Mtakatifu anavyo jidhihisha. Upendo ndio wa kwanza kwa kuwa ndiyo tabia za asili za Mungu. Ni jambo linalofikirika kwa upande mweupe na halina madhara yoyote. Linatokana na tabia asilia za wema wa Mungu. Wateule wana upendo kiasi hiki kwa wengine na hii inafikiliza kwenye upendo wa agape.

 

Kutoka kwenye jarida la Wimbo ulio Bora [145], tumeona kuwa Wayunani hawakuwa na pengine kifalsafa hawakuuelewa upendo wa agape. Halikuwa wazo au neno la Kiyunani. Wao walikuwa na upendo wa kierosi na upendo wa fileo. Hawakuelewa utaratibu wa kingugu kwa kuwa agape sio neno la Kiyunani. Linatokana na utenzi wa kitabu cha Wimbo ulio Bora. Ni uhamishaji wa kiuandishi wa neno la Kiebrania ‘ahab (awhab’). Hapa ndipo tulipo pata neno agape. Ni suala la uhamishaji tu wa kiuandishi. Wayunani hawaelewi hili hata sasa kwa maana ya kifalsafa zao, kwa kuwa wanategemea kwenye utaratibu wa Kiplatoni na utaratibu wa Uplatoni-mamboleo, na mfumo wao wa kidini unamagumu ndani yake kwa sababu wanategemea falsafa zao katika kuitafsiri Biblia.

 

Roho ni wa muhimu ambaye kwa yeye tunamuabudu Mungu kama ilivyo elezewa katika Wafilipi 3:3. Kwa hiyo hawezi kuwa Mungu kama apswaye kuabudiwa na kuwa awe sawa na Mungu Baba. Iwapo kama Roho ni msaidizi wetu ambaye kwayo tunaweza kumwabudu Mungu Baba, atawezaje tena kuwa ndiye anayepokea utukufu wa ibada zetu. Hii ni hatua rahisi ya kuifikirika. Roho Mtakatifu hawezi kuwa ni mlengwa wa kupokea utukufu wa ibada zetu wala kuabudu kitu Fulani na kitu fulani kile ni kina haki yake. Hawezi kuwa antufungamanisha kwenye kitu fulani na kwa wakati huo huo akiwa ndiye kwa yeye huyo tunafikia kuabudu na kukiwa na muingiliano na kitufulani na kuwa kitu kile kwa kadiri kilivyo chenyewe kimetenganishwa, usawa na hisia ni ya kibinadamu kikamilifu. Kwa mwenye akili timamu ni upuuzi kufikiri jambo hili kuwa hivyo na kuwa ni mjadala. Tunapaswa kuabudu msaidizi ambaye kwayo tunamwabudu mlengwa. Basi atakuwa yeye ni msaidizi na yeye huyo ni mlengwa. Roho Mtakatifu kwa kweli ni nguvu anayemtia nguvu Kristo.

 

Mungu humfanya Kristo kuwa ni Baba wa milele (Isa. 9:6 sawa na ilivyo pia kwenye jarida la Isaya 9:6 [224] ambako utaona kuwa walikuwepo aina nyinsi sana ya mababa kule mbinguni na duniani (Efe. 3:15). Aina hii yote ya ubaba au jamii walipewa majina na Mungu Baba, na hii ndiyo sababu tunapiga magoti mbele yake Mungu Baba, tukimuabudu yeye (Efe. 3:14-15).

 

Tunaweza kulipima wazo hili kwenye Zaburi 89:25. Zaburi 89 inaongelea kuhusu Daudi mtumishi wake akiwa amesha pakwa mafuta. Kuanzia aya ya 20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu. Aya ya 24…Na kwa jina langu pembe yake itainika. Zaburi 89 tunasimulia kuhusu baraza la watakatifu na Mtakatifu Mwenyezi. Kuanzia aya ya 25 Nitaweka mkono wake juu ya bahari, Na mkono wake wa kuume juu ya mito. Aya ya 26 Yeye ataniita, Wewe baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu. Aya ya 27 Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia. Wazo la Mungu Baba lilijulikana kwenye Agano la Kale, lakini hili ni wazo lingine ambalo Baba alikuwa kuwili kote yaani Mungu Baba na imeendelea hadi kwa Kristo kupitia Isaya 9:6. Na kuna aina nyingi ya ubaba, mbinguni na hapa duniani. (Efe.3:15) aina hizi zote za ubaba au jamaa ziliitwa Mungu Baba ambaye kwayo tunapiga goti mbele ya Mungu Baba na kumuabudu kwa mujibu wa Waefeso 3:14-15. Tunafanya hivi kupitia Roho Mtakatifu.

 

Kristo alikuwa ni mzaliwa wa kwanza au mzaliwa wa kwanza wa pekee katika uumbaji. Kupitia yeye vitu vyote vitu vyote viliweza kufanyika mbinguni na duniani, vinavyoonekana na visivyoonekana, ama view ni viti vya enzi au falme au usultani au mamlaka, vitu vyote viliumbwa kwa yeye na yeye. Kristo alikuwepo kabla ya vitu vyote na na kwa yeye, vitu vyote vinaungananishwa pamoja (Kol. 1:16-17). Lakini ni Mungu aliyemfanya awepo yeye na ndiye aliye kubali kwa matakwa yake mwenyewe kuwa uumbaji udumu kuwepo na utemgemee Kristo. Kwa hiyo, Kristo Kristo sio Mungu kwa maana ile kama aliyonayo Mungu Baba alivyo Mungu mkuu na kuwa ni yeye tu ndiye asiyeweza kufa (1Tim. 6:16) aishiye na kwenye uwepo wake milele ypte. Yeye sio ni kiumbe kilichoumbwa na Kristo hapa [tazama majarida ya Dhumuni la Uumbaji na Dhabihu ya Kristo [160] na Utawalawa Mungu [174]]. Mungu ameumba kwa mapenzi yake na Kristo amepangilia utaratibu wake.

 

Wateule wameitwa watoke kwenye dunia hii ili waishi maisha utumishi wamtumikie yeye na wajitoe wakfu kwake. Walioitwa ni wengi, lakini wateule ni wachache (Mt. 20:16; 22:14). Wateule wamechaguliwa, kama Kristo alivyochaguliwa na Mungu (Lk. 23:35). Wateule wamechaguliwa na Kristo (Yoh. 6:70; 15:16,19) kwa maelekezo ya Mungu (1Pet. 2:4). Mungu hututoa sisi kwa Yesu Kristo. Kristo hatampoteza hata mmoja, bali wote aliopewa na Mungu Baba; lakini ni ni kwa Mungu Baba huyu alyetupa sisi Kristo, sio Kristo aliyetuteua sisi. Ametutoa sisi nje kwa maelekezo yatokayo kwa Baba.

 

Ili kuwasaidia, wateule walipewa maarifa ya kujaliwa kuzijua siri za mungu. Roho Mtakatifu alikuwa ni mtendaji mkuu ambaye kwayo walipewa majaliwa haya ya kuzijua siri za Mungu na za Ufalme wa Mungu (Mk.4:11}. Kwa kuwa hekima ya Mungu huongelewa kwa mifano na fumbo (1Kor. 2:7) ambazo hunenwa na watumishi wa Mungu (1Kor. 2:7; 15:51). Kwa kuwa mapenzi ya Mungu hufundishwa kwa mifano na fumbo (Efe. 1:9) ambayo Mungu amewapa watumishi wake kwa njia ya ufunuo. Zaidi sana, mafumbo haya yamo kwenye utumishi wa Kristo kupitia wateule wake. Mtume Paulo aliandika hivi:

 

Waefeso 3:2-6 inasema: Ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; 3 ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nivyotangulia kuandika kwa maneno machache. 4 Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. 5 Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; 6 ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;

 

Kwa hiyo ni Roho Mtakatifu anayewezeshwa kuzifahamu siri za Mungu na za Kristo na kuwaleta Mataifa Wapagani ndani. Lakini sio sheria. Sheria zinadhihirika kwa Roho Mtakatifu.

 

Roho iliyondani ya Waamini Utatu wa

Imani na mafundisho ya Waamini Utatu wa Mungu wametenganisha Teolojia kutokana na kile kinachoitwa uchumi wa wokovu kwa ile hali ya Yesu Kristo kuja duniani na kufanyika mwanadamu. Neno economia maana yake, kimsingi, kufanyika kwake mwili Yesu Kristo na jinsi Mungu alivyo jidhihirisha kupitia kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Teolojia hii kwa umakini ilihusisha vipimo vya kibinadamu kwa kulinganisha na tendo hili la kufanyika mwanadamu na hali ya kawaida ya uzaliwa wa mwanadamu kwa jinsi utendaji wa Mungu, ikizingatiwa utaratibu wa hatua za kukamilika kwa kiumbe (au ya utendaji wa Mungu). Kama ilivyoandikwa kwenye jarida la Maendelezo ya Muundo wa Uplatoni-mamboleo [017], jarida la mwanazuoni maarufu LaCugna lisemalo [MUNGU PAMOJA NASI: Utatu na Maisha ya Mkristo, (GOD FOR US: The Trinity and Christian Life), Harper, San Francisco, 1991], katika kushughulika na maendelezo ya mafundisho ya Utatu na utenganishaji wa teolojia kutoka kwenye Mpango wa Wokovu (au fundisho lihusulo mpango wa wokovu wa mwanadamu) kama lilivyo funuliwa kwa kufanyika kwake Kristo kuwa mwanadamu, ikumbukwe kwamba Wakapadokia wliiwekea msingi wa mwanzo wa teolojia kwenye muelekeo ambao zaidi sana ulichngia kutenganisha dhana ya uchumi na teolojia. Kimelea hiki au chanzo, kimepelekea kwenye:

 

Kupitia kwa mpingamizi Mzushi-Dionysius na, kuwa teolojia ya Gregory wa Palana (Sura ya 6) kinasema.

 

Katika Magharibi ya Ulatino, katika kipingi cha mara tu baada ya mtaguso wa Nikea, wanateolojia kama vile kina Hilary wa Pointias na, pengine kwa kiwango cha juu zaidi, Marcellus wa Ancyra, alishikilia kuamini kati ya muunganiko kati ya ukweli wa kimbinguni na ubanifu wa wokovu. Augustine alizindua mkabiliano wote mpya. Hatua yake ya kuanzia ilikuwa siotena mpangilio wa kimadaraka wa Baba bali muhimili wa kimbinguni unaojumuisha kisawa sawa kwa nafsi tatu [tumekazia kwa kuweka maandishi mazito]. Badala ya kuuliza tabia asilia ya teolojia kama ilivyofunuliwa katika kufanyika kwake mwanadamu Kristo na kufanyika kwa uungu na Roho Mtakatufu [msisitizo umewekwa kwenye maandishi mazito]. Augustine aliulizia kutaka kuandika kuhusu Utatu kuweza kupatikana kwenye mioyo ya mwanadamu. Udadisi wa Augustine wa mlingano wa ‘kisaikolojia’ kwa mahusiano ya kiintratinitarian ingamaanisha kuwa mafundisho ya waamini utatu hatimaye yangehusikana na mahusiano ‘endelevu’ kwenye uungu, ikiunganishwa kutoka na vile tunavyomjua Mungu kupitia Kristo katika Roho (LaCugna, p.44).

 

Inaongoza kupeleka watu kwenye kile kiitwacho kama Hadithi za imani za Kipagani (ukitazama jarida la Hadithi za imani za Kipagani Sura ya 1 Uenezaji wa Hadithi za Upagani wa Wababeli [B7_1].

 

Roho Mtakatifu ndiye anayetusaidia ili sisi tufikie mahali pa kuwa miungu wadogo (yaani elohim). Roho Mtakatifu ndiye awezeshaye hata Kristo afikie kwenye kima cha Mungu (awe elohim). Waamini mafundisho ya Utatu wamejikita kwenye mafundisho mengine yanayoitwa ya Roho, kwa kuwa wanaona mambo ya mbinguni kwenye roho na kutafuta kuwa sawa na Mungu Baba, jambo ambalo hawako hivyo na wala hawawezi kuwa, na wala haiwezekani hata kwa mmoja wetu kuwa hivyo. Kwa mujibu wa Wafilipi 2:6, sisi hatutafuti kufikilia kuwa sawa na Mungu Baba, kama alivyofanya Kristo kuwa hakushikilia usawa wowote na yeye Mungu.

 

Wafilipi 2:6 inasema: 6ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;

 

Teolojia ya Kilatini ya nyakati za miaka ya karne za kumi na mbili hadi ya kumi na sita (yaani miaka ya 1100-1500) ambayo wana historia huuita ‘Medieval’, walimfuata Augustine na kutenganisha teolojia kutoka na uchumi na elimu ya mpango wa wokovu (kwa lugha ya kiteolojia huitwa ‘soteriology’ maana yake ni kifupi ni mpango wa wokovu). Utaratibu wote ukawa umegonganishwa na Hadithi za imani za Kipagani za Waplotini mamboleo.

 

Kumbukumbu muhimu za LaCugna ni kwamba, kuanzia Augustine, Mtawala wa Baba hakuwa na maana ilu kuu tena. Imani ya Utatu huweka dhana ya usawa wa kimungu. Hii ni hatua ya pili ikifuatia kutoka madai ya uongo ya usawa wa kimungu. Waamini mafundisho wa miungu miwili (Wabinitaria) na wenye kuamini mafundisho ya miungu mitatu (Watinitaria) huweka madai ya yanayodai usawa wa kimungu.- kisha wanadai kuhusu usawa wa viumbe wawili. Roho Mtakatifu hudaiwa kuwemo pale, kwa aina yoyote ile ya mwonekano utakao pendekezewa na kisha ni kushindwa kwa dhahiri kwa mafundisho ya imani ya Utatu. Cheo kikuu kilicho sahihi ilikuwa ni cheo lilikuwa wazo la madhihirisho ya uungu kwa kila mmoja, ikijulikana kama utendaji kazi wa Baba kwa njia ya Roho Mtakatifu, ambaye hutokea kuroka kwake kupitia Yesu Kristo. Ni kitu kile tu ambacho hawakuonea hamu. Maelekezo haya kupitia Yesu Kristo alimuwezesha kusimamia na kuwaelekeza kila mmoja binafsi yake kwa mujibu wa wa mapenzi ya Mungu ambaye aliishi ndani ya kila mteule. Kristo hakuwa ni chanzo cha kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Yeye alikuwa ni mwangalizi kiunganishi. Alifanya kazi zake kwa ajili ya Mungu sawa sawa na alivyokuwa anafanya wakati wote na kwa kufuatana na mapenzi ya Mungu. Lakini hata hivyo hakuwa Mungu. Waamini mafundisho ya Utatu wamepoteza muelekeo wa ukweli huu, kwa kweli, hawakuelewa kamwe kuuelewa ukweli wenyewe. Kama anavyosema LaCugna kuwa:

 

Teolojia ya umoja-tegemezi wa Mungu wa miungu mitatu inaonekana kuwa imeongezewa katika kutilia maanani juu ya Mungu mmoja (kifungu cha 44).

 

Wanateolojia wa Kiyunani waliingiza dhana ya teolojia ya Mungu aishiye kwa tegemezi la utatu shirikishi. Huu ulikuwa ni mfumo wa imani za kale, na hakuna kilichofanana na mafundisho ya Biblia wala na mafundisho ya Ukristo wa kweli. Wao ndio walioongezea elimu ya kiteolojia ndani yake. Kimsingi chimbuko la elimu ya teolojia ilimkosea kiufundishaji Roho Mtakatifu na kuharibu au ilifunga uwezo wetu wa kuelewa utendaji kazi wa Roho Mtakatifu.

 

Hali hii iliathiri sana msingi wa jinsi Wakristo walivyokuwa wakiomba. Hatuwezi kumtumia Roho Mtakatifu kwa njia ileile kama ni msaidizi au kiungo muhimu katika kumwabudu Mungu, kwa sababu sisi tumepewa Roho Mtakatifu hapa akiwa ni kiungo muhimu kwa ajili ya kuabudu. Na huku akifnyika mwenyewe kuwa ni mlengwa wa kuabudiwa. Tunawezaje kuabudu kitu ambacho kimo ndani yetu? Kwa kweli ni dhana ya kipumbavu kufikirika. Hiyo inakuwa ni kama uoto (narcissism). Ni ibada ya kujiabudu mwenyewe, kwa kuwa Roho Mtakatifu yuko ndani ya kila mmoja wetu. Hivi ndiyo maana, hawamuombi tena kwa Baba peke yake kupitia jina la Mwanae kama Biblia inavyotuagiza (kutoka Mt. 6:6,9; Lk. 11:12) lakini wao huomba kwa Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Hii ndiyo tofauti ya kimsingi. Wana wa Utatu wamejitoa kwa kusema: ‘tunaomba kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu’. Hawaombi sawa sawa na jinsi ile kristo alivyotufundisha sisi kuomba- ’Lolote mumwombalo Baba kwa jina langu nanyi mtapewa’. Sisi huomba kwa Baba. Uhusiano wetu ni wa mmoja mmoja na Baba. Ni kupitia Roho Mtakatifu na tunaomba lolote kwa jina la Mwalimu wetu, Bwana wetu, Mtawala wa maisha yetu, Aliye wa pekee kwetu, lakini hatuombi kwake na hatumwabudu yeye na hii sio heshima ni kufuru.

 

Zaidi sana, maendelezo za kisomi teolojia ya viwango vya tabia za watu kwa namna ilivyo yenyewe tu. Lakini jumba lote lilijengwa kwa kutozingatia au kwa ghiliba ya Biblia. Na ndiyo maana Wanautatu hawathubutu kamwe kuipitia vifungu vyote vya Biblia wanapotoa fundisho hili na hutafsiri kimakosa na hunukuu ki makosa vifungu vingine muhimu na huacha na kupuuzia vingine wasivyoweza kuvigeuza. Lakini mfumo wao umeegemea kwenye mrengo wa Hadithi za imani za Kipagani na Uplatoni. LaCgna anaelezea kama ifuatavyo:

 

Wakapadokia (na pia Augustine) walienda kwa kutilia maanani sana zaidi ya elimu ya maandiko matakatifu ya uchumi kwa kuuweka uhusiano wa Mungu kwa Mwana (na Roho) kuwaweka kwenye usawa wa kimadaraja ya mbinguni (kifungu cha 54).

 

Mungu mmoja aishiye kama ousia katika tofauti tatu kitu kidhaniwacho kuwa shirika ya utatu wa uungu (hypostases) chenye maana moja ileile [tazama majarida ya Mhimili wa Uumbaji wa Mungu kama Alfa na Omega [229] na Mteule kama Elohim [001]].

 

Mamlaka ya Roho Mtakatifu kuweza kufanya kazi zake kwenye ngazi ya mwingiliano wa kimbinguni humaanisha kuwa mteule hawezi kushiriki kwenye tabia za asili za Mungu kama Kristo alivyoshiriki kwenye asili ileile. Madai haya ni tofauti kabisa na yasemvyo maandiko matakatifu. Wateule hushiriki kwenye tabia za asili za kimbinguni (2Pet. 1:4). Sababu ya madai haya ni kwamba ni madanganyo ya Shetani. Yanafanyika ili kuvunja uhusiano wetu na Mungu na kutuzuia kuendeleza mahusiano yetu na Mungu kwa njia ileile moja ambyo Kristo alikuwanayo na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu, ili kwamba ituzuie sisi kufanyika kuwa ni warithi pamoja na Kristo. Kama hatujapata uhusiano wa namna ileile na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu kama Kristo alivyofanya, hatuwezi kuwa warithi pamoja naye. Warithi maana yake ni kwamba tunarithi kila kitu kilekile na yeye. Itawezekanaje kwa sisi kuwa warithi pamoja na mtu ambaye yuko tofauti kabisa na utaratibu wa kibinadamu? Tunawezaje kuwa warithi pamoja na Mungu? Hii haileti maana. Aina hii ya mawazo imefikisha kwenye hatua ya kupelekea kwenye karne ya ishirini mawazo ya kimamboleo yaliyokuwepo kwenye zama za karne ya pili yamerudi hata miongoni mwa makanisa yaliyo kwenye mrengo wa kuikubali na kuishika Sabato, kiasi cha kufikia kwenye kiwango cha kwamba wameungana kudai kuwa Yesu ni Mungu kama mtu mmoja. Hii inatokana na Mungu aitwaye Attis.

 

Kwenye kitabu cha Waefeso 1:22 tunaambiwa kuwa Mungu alikabidhi vitu vyote chini miguuni mwa Kristo na kuwa alimfanya kuwa kichwa juu ya mambo yote kwa Kanisa (ambaye ni sisi) ambalo Mungu alilimwinua Kristo:

alipomfunua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vyote chini ya miguu yake, akaweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.

 

Kwa hiyo, Kristo amepewa mamlaka juu ya kila jina, kama jina lake lenyewe lilivyobeba mamlaka. Amepewa mamlaka juu ya kila kitu ili kwamba Kanisa lifikie kwenye urithi kupitia Kristo ambaye kwa yeye ukamilifu wa Uungu ukae kimwili (kol.2:9). Neno hili lililotafsiriwa Uungu hapa ni theotetos lenye maana ya Umungu au ile hali ya kuwa Mungu. Sasa Thyer anasema kwamba umungu (theot) hutofautiana na umbinguni (Theiot) kama vile ute unavyotofautiana na ubora au kima (Thayer’s, p. 288). Maana yake hapa ni haya, ukamilifu wa chanzo cha Mungu hukaa kimwili katika Krosto. Ni ukamilifu huu wa chimbuko tuliopewa ili kwamba ili kwamba watu wote wapewe tabia mpya za asili ya Mungu (kol. 3:10). Hatuwezi kuwekewa tabia asilia za Mungu hadi pale mwenendo wetu uruhusu hali ya sisi kustahili kuwa miungu wadogo na mali ya Mungu. Watakuwa bila kujali kuwa ni Wayahudi au Wayunani lakini wote ni wake Kristo kwa kuwa yeye yuko zaidi ya yote (Kol. 3:11). Yeye huendeleza wanaume, ingawa nguvu za Roho Mtakatifu ili kuweza hatimaye kumfanya Mungu awe ni yote ndani ya yote (1Kor. 15:28).

 

Wakati vitu vyote vikiwa chini yake, kisha Mwana mwenyewe pia atajinyenyekesha kwake yeye aliyeweka vitu vyote chini ya mamlaka yake, ambapo Mungu atakuwa ni [(yote ndani ya tote) (panta en pasin) (tazama pia kamusi ya Marshall’s Intrneliar na pia Kol. 3:11, panta kai en pasin)]

 

Wana Utatu wameanza kutafsiri hii inayofuata kuwa kila kitu kwa kila mtu ili kuekuka ukweli wenye maana uhusuo upana wa uweza wa Mungu kama ni chanzo muhimu kuelekea kwa kila mtu kama ilivyofanyika kwa kristo kwa mujibu wa vifungu hivi vya maandiko. Ni Kristo yule anayetuvika ukamilifu wa Mungu (Efe. 3:19)-ukamilifu wa Kristo wa kuwa mfano wa sura ya Baba (Efe. 4:13).

 

Ni kwa ajili hii tunafanyika kuwa na mfano au eikon wa sura ya Baba kama ilivyokuwa kwa Kristo na kwa hiyo sisi kufanyika kuwa ni watoto wa Mungu na warithi pamoja na Kristo wa Ufalme wa Mungu (Rum. 8:17; Yak. 2:5); warithi kwa sawasawa na ahadi (Gal. 3:29) wa wokovu (Ebr. 1:14) na warithi pamoja na neema (1Pet. 3:7). Sisi tu warithi pamoja na Kristo wa neema. Kwa hiyo, neema haitangulii mbele ya Yesu Kristo. Inatangulia kutoka kwa Mungu. Huu ndio msingi mkuu!

 

Waefeso 3:14 inasema: Kwa hiyo nampigia Baba magoti, 15ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani utaitwa.

 

Neno familia hili hapa lina maana ya patria au ubaba. Yaani ni ‘baba’ mdogo aweza kuwa pengine wa familia ya nyumba husika au wa familia ya nyumba ya Mungu, aliyepewa jukumu la madogo katika muonekano majukumu makamilifu ya kila kiongozi kila nafasi ikiiangukia familia.

 

Kwa hiyo utaratibu huanzia kwa Mungu hadi kwa Kristo ukishukaka mpaka kwa mwanaume aliye kichwa cha familia ya nyumba husika (1Kor. 11:3), ambaye anapaswa agawanye majukumu kama Mungu afanyavyo kwa Kristo na kwa Wana wengine wa Mungu, ambao ni elohim na kwa jinsi hao elohim warudipo kuyagawa majukumu yao kwa wale walio chini yao. Haya yote hufanyika kwa Roho Mtakatifu. Uhusiano wetu kama kila mtu binafsi ni wa moja kwa moja kwa Yesu Kristo, na sio kwa mtu yeyote aliyeko humu kwenye sayari yetu. Roho Mtakatifu ni uwezo na nguvu ambaye kwayo tunawezeshwa kuwasiliana moja kwa moja na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.

 

Roho Mtakatifu ndiye kiunganisho, anayeunganisha mambo yote haya kimoja kwa kingine na kufikilia uwezo wa kuwa elohim kwa kila mmoja kwa Jeshi la mbinguni. Hakuna swali lolote kuwa Roho Mtakatifu kuwa ni Mungu kwa mtazamo wa kwamba yuko tofauti na kila mtu binafsi na huwezesha kwenye mahusiano ya mwingiliano wa kimbinguni wenye muunganiko shirikishi wa watu watatu. Sisi sote ni Wana wa Mungu na kwa hiyo ni warithi pamoja na Kristo kwa namna ile ile moja. Tendo la kumuabudu Roho Mtakatifu lingechokuliwa kwa mtazamo wa kujiabudu mwenyewe, kama ikikubalika kwa maana ya kuwa Mungu hufanyika kuwa ni yote katika yote. Kwa hiyo basi, kumuabudu kumekatazwe kwa sababu zenye maana sana na makatazo haya yanaingia akilini, maana ni kama ibada ya kujiabudu mwenyewe kwa maana ya kuwa ni sehemu ya mwanadamu mwenyewe. Ni kwa kweli ni uweza au uweza utujengao na kutuwezesha kitabia na sio kuwa ni Mungu mwenyewe. Roho Mtakatifu hutuwezesha sisi kupata uwezo wa kufanyika elohim au theoi.

 

Kwa njia hii vile vile tunafanyika kuwa wenye kufanyika wa maana na Baba kama alivyo wa muhimu Kristo. Hii imeelezewa kwenye jarida la Kuimarika na Baba [081].

 

Wazo la kuwa Roho Mtakatifu ni kitu kidhaniwacho kuwa shirika ya utatu wa uungu (hypostases) na Mungu ni wazo au fundisho la Wayunani, ambalo limefafanuliwa kwenye jarida la Matumizi ya Neno Hypostasis [230]. Bila ya Roho Mtakatifu hatuwezi kufanyika kuwa wana wa Mungu.

 

 

 

 

 

 

 

q