Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[118]

 

 

 

 

Tatizo la Uovu

 

(Toleo La 1.0 20131109-20131109)

 

Jarida hili linashughulika kuelezea kuhusu tatizo la uovu, na uweza wa Mungu wa kuelewa kila kitu na nadharia au dhana ya makatazo.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hatimiliki ©  2013 Wade Cox)

(tr. 2016)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Tatizo la Uovu



Tatizo la Uovu

Jarida hili linashughulika kuelezea kuhusu tatizo la uovu, na uweza wa Mungu wa kuelewa kila kitu na nadharia au dhana ya makatazo. Tutaona kwanza kabisa kwenye Mathayo 25:34. [34] Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

 

Inaendelea:

[35]  kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

 

Pointi ya muhimu ni kwamba Ufalme uliandaliwa kwa ajili ya wateule tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia. Msingi wa dunia ulikuwa [katabole SGD 2602]; uwekaji wa msingi wa dunia. Kwa hiyo, ufalme wa Mungu uliandaliwa kabla hata ya dunia haijaumbwa.

 

Hiyo iliibua mkururu wote wa matatizo lakini tutakwenda na kuendelea mbele kwenye nukuu nyingine nyingi zaidi kwanza.

 

Luka 11:50 inatupa wazo tena la kuhusu msingi wa dunia:

[50] ili kwa kizazi hiki itakwe damu ya manabii wote, iliyomwagika tangu kupigwa msingi wa ulimwengu;

 

Na aya ya 51 inaendelea mbele kwa kusema:

[51] tangu damu ya Habili hata damu ya Zakaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na hekalu. Naam, nawaambieni ya kwamba itatakwa kwa kizazi hiki.

 

Inaelezea kuhusu “kizazi hiki”. Kuna mambo mengi sana yamehusishwa. Kwanza kabisa ni kizazi cha mwisho cha zama za Hekalu tangia kifo cha Kristo na kuendelea hadi mwaka wa 70 BK.  Kisha ni cha mwisho ambacho kinahusiana na utimilifu wa dahari baada ya Nyakati za Mwisho. Lakini dhana ni kwamba damu ya manabii ilimwagwa tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia. Itakuwaje basi kwamba damu ya manabii imwagike tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia wakati tukiwa kwa kweli hatutafuti kujitenga na dunia bali ni kwa vifo vya manabii tu? Nabii wa kwanza alikuwa ni Adamu na alikufa kwa sababu ya dhambi. Kwa hiyo, mkururu wa wateule ulianzia kwa Adamu na mauti iliingia ulimwenguni kote kwa njia ya dhambi kupitia kwa Adamu.

 

Yohana 17:24 natuchukua hadi kwenye awamu nyingine ifuatayo:

[24] Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.

 

Dhana hapa ni kwamba Kristo alipendwa na Baba hata kabla ya kuwekwa kwa misingi ya dunia. Aya za 25-26 zinaendelea mbele kwa kusema:

[25] Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26 Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

 

Kwa dhana hii, ni kwamba Kristo anaashiria kuwa alikuwepo huko nyuma kipindi cha kabla ya kuzaliwa kake hapa duniani kutokana na maneno anayoyasema ya kwamba kwenye huu uhusiano wake na Mungu ulikuwa ni wa ulimwengu war oho tu kabla ya kuwekwa kwa misingi ya dunia hii. Kuna mikururu ya kimaelezo kwenye maandiko haya.

 

Sura ya kwanza ya waraka kwa Waebrania inamuongelea Kristo. Waebrania 1:10-11 inasomeka hivi:

[10] Na tena, Wewe,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikono yako; 11 Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu; Nazo zote zitachakaa kama nguo, (sawa na Zaburi 45).

 

Hii inamwongelea Kristo, lakini ilikuwa ni Mungu aliyeweka misingi ya dunia. Waandishi wa Kibinitariani na Kitrinitariani wanajaribu sasa kumtofautisha Kristo na Malaika wengine, na wanasema kwamba hili ni andiko la Melkizedeki wakati anaposema kwenye aya za 13-14:

[13] Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? 14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

 

Andiko hili limetumiwa vibaya kwa kusema kwamba kwa namna fulani Kristo anatofautiana na wana wengine wa Mungu na kwamba roho wahudumuo ni viumbe wa daraja la chini kuliko wale wawahudumiao wateule. Tena walikuwa ni viumbe hawa ambao walikuwa pamoja na Mungu tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia. Tunajua kutokana na maandiko ya Ayubu 38:4-7:

[4] Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. [5] Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? [6] Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, [7] Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

 

Kwa hiyo, kwenye uwekaji wa msingi wa hii dunia, nyota wote wa asubuhi, siyo ni mmoja tu au wawili, bali nyota wote wa asubuhi walikuwepo na wana wote wa Mungu walifurahia na kusherehekea tukio hili la kuwekwa kwa msingi wa dunia. Hii haiezekani kuwa iongelee kuhusu wanadamu kwa wanadamu. Kabla hii dunia haijaumbwa, hapo kabla yake kulikuwa na wanadamu wengi sana ndani yake, wana wa Mungu walialikwa na Mungu Baba, ili waweze kuona uumbaji wa hii dunia. Hii ni pointi ya muhimu sana, na andiko la muhimu sana. Waamini Utatu hawalisomi wala kulijadili andiko hili kwa kuwa hawawezi kulifafanua hili.

 

Andiko linalofuatia la kuliangalia ni la Waebrania 9:26 linalosomeka hivi:

[26] kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.

 

Ili kuzishughulikia dhambi ilimpasa Kristo ajitoe mwenyewe sadaka mara nyingi akiwa kama Kuhani Mkuu kwa kuwa andiko hili linasema:

[26] kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. 27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; 28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.

 

Au kama inavyoelezwa kwenye tafsiri ya KJV:

[26] kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. [27] Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; [28] kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.

 

Kristo alikuja mara moja ili kuzishughulikia dhambi na kisha atakuja kuwaokoa wale wanaomgojea kwa hamu kubwa. Kwa hiyo, dhambi ilikuepo tangu kuwekwa kwa msingi wa dunia, hususan tangu Adamu wakati alivyoingizwa mtegoni na kutenda dhambi na manabii wamekuwa wakiuliwa tangu kipindi cha Adamu, lakini alikuwa ni Kristo ndiye aliyekuja kuishughulikia dhambi. Yeye ndiye hatimaye aliyelitatua tatizo la dhambi kama tunavyoona kwenye 1Petro 1:20:

[20] Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu;

 

Ukisoma tangia aya ya 18:

[18] Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. 20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.

 

Hii inaibua vipengele kadhaa na vya muhimu katika kuushughulikia mfumo huu. Inajulikana kwa kupitia vifungu vinane vya maandiko kwamba mpango huu wa Mungu ulikuwepo kabla ya kuumbwa kwa dunia na ulihusika na dhambi na jinsi ya kuziondoa dhambi tangu Adamu na kuendelea hadi kwa Kristo na kuendelea hadi kwenye kipindi cha kukombolewa kwao wateule. Ufunuo 13:8 inaonyesha kwamba mchakato huu ni endelevu.

Ufunuo 13:8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia

au

Ufunuo 13:8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia

 

Andiko hili linaelezea kuhusu kipindi cha Joka na kipindi cha Mnyama na kipindi cha maasi makuu na kufuru za wadanamu kinyume chake Mungu. Aya ya 7:

 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.

 

Ni mwanakondoo ndiye aliyechinjwa tangu kuwekwa kwa msingi wa dunia nah ii inatuchukua sisi hadi kwenye mwisho wa wateule wote ili kwamba tujue wote kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka elfu mbili tangu kifo cha Kristo kutoka hapo hadi mwishoni mwa kipindi na cha zaidi ya miaka 1000 kwenye Milenia na miaka 100 ya Hukumu. Mchakato huu ulipangiliwa na kukusudia uwepo na Mungu, yote ikiwa chini ya uthibiti wa Mungu na wote ukiwa umejulikana na Mungu. Kwa hiyo Mungu ni mwenye uweza wa kujua kila kitu na kwa mambo yote. Uweza huu wa Kiomnishenti unaonyesha kuwa Mungu anajua yote na kila kitu kwa kiasi kwamba zama zote zijazo anazijua na kuzielewa. Kiumbe ambaye hajui mambo yajayo siku zijazo kwa kweli hawezi kuwa Mungu aliyetangaza mwisho tangu mwanzo kama tunavyoambiwa sasa.

 

Kisha dhana hii inaendelea kwenye Ufunuo 17:8, ambayo inaendelea hadi mwishoni wa wakati wa kuanzishwa kwa utawala wa Shetani na nguvu za upotevu kwa ajili ya kuuthibiti na kuutawala ulimwengu.

[8] Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako

 

Mpango huu wa Mungu unawatilia maanani wanadamu wote walioumbwa na kisha unahusika na imani na mfumo wa milenia tunapokwenda kwenye Ufunuo 20 panapoelezea uanzishwaji wa kipindi cha milenia baada ya Shetani pamoja na malaika zake waasi kutupwa kuzimuni au huko tartaros. Ndipo watahukumiwa baada ya kipindi hiki cha milenia, baada ya kujitoa na kufanya kazi na miwajibiko wetu kutoka kipindi cha Ufufuo wa Kwanza wa Wafu hadi kwenye Ufufuo wa Pili wa Wafu. Na ndipo hatimaye watafunguliwa ili wafanye kazi zao za mwisho ambayo ni uasi mkubwa wa mwisho na kushawishi vita ya mwisho ya mwishoni mwa Milenia mapema kabla ya tukio la Ufufuo wa Pili wa Wafu. Haya ni maandiko yanayotuonyesha sisi kwamba mpango wa Mungu umeandikwa kwa wazi sana, na umepangiliwa, na kuainishwa kwa kina na Mungu anaongoza tangu kabla hayaweka kitu chochote cha kwanza kwenye ujenzi wa hii sayari. Kwa hiyo hii inashughulikia kuonyesha uweza wa Mungu wa kuelewa kila kitu na Tatizo la Uovu. Iwapo kama Mungu alikuwa na mpango tangu kuwekwa kwa msingi wa dunia, ni kwa nini basi aliiumba dunia na ili ikabiliwe na tatizo hili lingejitokeza na kwa hiyo yeye hawajibiki? Kwa kuwa alijua kwamba mambo haya yangetokea, je, anawajibika kwa kutokea kwake? Hili ndilo lile tatizo lijulikanalo kama Uhuru na Kujiamulia mambo. Kama Mungu alijua kuwa kuna kitu kinachoweza kutokea, basi kuna ukweli wa kwamba alijua kinachokwenda kutokea kunaweza kuhusishwa na uhuru wetu na kunaweza kufanya iamuliwe kwamba ingeweza kutokea? Kama inajulikana kuwa inatokea hapo mbeleni basi uweza huu wa Mungu wa kujua kila jambo utakuwa na maana gani?

 

Omnishensi maana yake maarifa ya kujua mambo yote yanayokusudiwa. Mtumishi aliwahi kusema mara moja: “je, Mungu anajua kila kitu? Je, Mungu anajua kuwa mimi naenda kuivuta hali hii ya ushwari kutoka mfukoni mwangu?” Jibu lake ni kwamba, ndiyo, ni kweli alijua. Anajua jinsi tunavyowaza. Anasema: “Nayajua mawazo yenu na wala siyo mawazo yangu.” Pointi ya kweli ilikuwa ni kwamba ni lazima Mungu ayajue mawazo yote ya kweli, vinginevyo hawezi kuwa ni mwenye uweza huu wa kujua kila jambo na kama hatakua na uweza huu wa kujua kila kitu, basi hawezi kuwa Mungu. Ni rahisi sana kiasi hicho. Ni budi pia awe ni mtawala wa viumbe wake ni kwa kuwa yeye ana uweza wa naomna zote au mwenye nguvu zote na anayeweza kuwaongoza viumbe wake na kuleta kile anachokipenda kifanyike. Alimpa mamlaka Shetani ya kushughulika na wanadamu. Hawajibiki na uchaguzi alioufanya Shetani na Malaika zake lakini uweza wake wa kujua kila jambo unahitaji kile anachokijua na kwamba anafungua milango ya kuleta mema kutoka kwenye uovu ule. Jinsi afanyavyo ndivyo ilivyoelekezwa kwenye Mpango wa Wokovu ulioainishwa hapo chini na imefafanuliwa kwa kina kwenye kitabu au jarida la Sheria ya Mungu Toleo La 3: Kalenda ya Mungu na Mpango wa Wokovu.

 

Uhuru umewezeshwa kwa kiumbe kwa kuturuhusu kuutenda kazi utashi, kwa sisi tuweze kufanya uamuzi wa kama ama tutafuata na kuzitii sheria za Mungu au kama hatutazifuata sheria za Mungu. Kwa hiyo, kama hakuna sheria hakuwezi kuwa na dhambi kwa kuwa bila ya sharia hakuwezi kua na dhambi. Akini sheria yaonekana kuwa ilikuwepo tangu mwanzo kwa kua inakuja kutoka kwenye asili na tabia halisi za Mungu. Kwa hiyo, sheria ni budi kwamba zilikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa hii dunia, kwa kuwa Mungu ni mambo yote ambayo torati ndiye asili na maana yake: mkamilifu na wa kweli, mwema, mpenda haki na mtakatifu.


vitu ambavyo tunafanyiwa sisi ili kuturuhusu tuwe na uhuru na kuhukumu vinawezeshwa na vinaulazima ni budi vitupe sisi uwezo wa kuweza kuingamiza hii sayari na tunaweza karibu sana tufanye hivyo. Kristo atapelekwa ka wale walio na hamu kubwa ya kumngojea. Atatumwa arudi kutuzuia na hali mbaya ya uharibifu mkubwa wa mwisho wa kuiharibu na kuiangamiza hii sayari kipindi cha hukumu na uongozi wa mapepo.

 

Mungu anajua haya mambo yote haya. Anajua kuwa anakwenda kufanya na aliamua kuturuhusu sisi tuwe na uhuru wa kufanya hivyo. Ni pekeyake huyu Mungu mwenye uweza wa kujua kila jambo na mwenye nguvu zote, omnipotenti maana yake ni uweza wote, omnishenti naana yake ni kujua vyote, omni maana yake ni yote, kukiwemo kilakitu, ni uweza na jumla ya hii. Hakuna sababu ya kuyajua mambo ambayo siyo nadharia ya kweli kana kwamba yapo kwenye mfumo mbovu wa kifikra ambao Mungu angeweza kuchoshwa nao bali ni vyema kuyajua mambo yote yaliyo ya kweli. Mungu alijua kila kitu tulichokifanya maishani mwetu na kila kitu tulichokuwa tunakwenda kukifanya. Sisi sote tuliochaguliwa kanisani, matendo yetu yaliwekezwa tumboni na kuamuliwa kabla hata hatujazaliwa. Tunajuaje hilo? Mungu anasema kwa kupitia Roho moyoni mwa Yeremia.

 

Yeremia 1:4-5 inasema:

[4] Neno la Bwana lilinijia, kusema, [5] Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

 

Kabla Yeremia hajatoka tumboni alitiwa mafuta au kuchaguliwa kuwa nabii. Ndivyo ilivyo kila mmoja wetu kanisani aliyechaguliwa kuifanya kazi ya Mungu katika nyakati hizi za mwisho tumechaguliwa hata kabla ya kutoka matumboni ili tuifanye kazi hii. Kwa hiyo basi Mungu alijua mambo yote mabaya tuliyokuwa tunayafanya katika maisha yetu yote. Alijua yale tutakayoyashindwa lakini bado alitutenga rasmi ili tuweze kuifanya kazi hii. Ni kwa nini alifanya hivyo? Iwapo kama ilikuwa inakwend kuwa hivyo kwa mteule, ni kwa nini asingebeba majukumu ya kimaadili ili kuhakikisha kwamba ni alio wema na wazuri tu ndio achaguliwe? Hicho sicho anachosema, au sivyo? Ni kwa nini tuliitwa? Ni ili kumshangaza Mwenyezi na kuimarisha udhaifu wetu na kushinda kwa kupitia uweza wake wa kujua kila kitu kilicho kidhaifu kwetu.

 

Warumi 8:26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

Kwa hiyo hata maombi yetu yanatafsiriwa tena.

 

[27] Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Kwa hiyo, mapenzi ya Mungu huongoza na kutuelekeza kwa wateule na yamefanywa kutoka wakati tulipotungwa mimba tukiwa kama kitoto kichanga kilichotungwa mimba tumboni mwa mama zetu. Je, hii inamaanisha kwamba Mungu, ajuaye kila kitu tunachokifanya angetoa kwa ajili ya dhambi hizo na kwamba sisi tunasamehewa kutokana na kuzitenda dhambi hizo? Hapana!

 

Tunapoendelea kwenye aya ya 28:

[28] Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Kilakitu kinafanya pamoja kwa nia njema hata dhambi tunazozitenda lakini hiyo haimaanishi kwamba tuendelee kutenda dhambi, vinginevyo tutakua tunamsulibisha Kristo kwa mara nyingine tena. Na ndiyo maana walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache ili kwamba wale walioitwa na akaendelea kutenda dhambi na kushindwa kwenda kwenye Ufufuo wa Pili wa wafu hawajachaguliwa na Mungu hapo mwanzoni. Tunajua kwamba kwa sababu ya andiko hili. Kwa hiyo tunajua kwamba kila jambo linafanya kazi kwa pamoja kwa nia njema na kwa uzuri kwa wao wanaompenda Mungu na kwa wao walioitwa sawasawa na makusudio yake. Kumbuka kwamba ni kwa mujibu wa makusudio yake. Hili ndilo andiko la muhimu na la msingi. Aya ya 29 inafafanua ka kina mkururu huu:

[29] Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

 

Ni kwa njia ya uweza huu wa Mungu wa kueIewa kila jambo ambao ndipo anajua sisi ni kina nani, kile tunachotakiwa kukifanya na kile tunachoweza kukifikilia. Kwa mfano, alijua kwamba Daudi atakuja kutenda dhambi ya uzinzi na Bathsheba na kwamba atamuua Uria Mhiti kwa kumpeleka kwenye mstari wa mbele na kwenye mapigano makali ili akafie huko na aliwaamuru majenerali wake wafany hivyo. Mungu alijua kuwa atafanya hivyo tangu kuwekwa kwa msingi wa dunia. Alizijua dhambo zote za Daudi na ndipo Nathani alitumwa kwa Daudi akamhukumu Daudi kwa kuchagua mwenyewe aina ya hukumu kwa midomo yake mwenyewe. Nathani akampa hadithi ya mwanakondoo mdogo ambaye alikuwa amechukuliwa na mchungaji tajiri aliyekuwa na kondoo wengi sana aliowamiliki wakati menzake maskini alikuwa na mmoja tu. Daudi alishangazwa sana kama kitu kama hicho kinaweza kufanyika na akakasirika sana na akasema kuwa huyo tajiri anapaswa alipe mara nne ya kile alichodhulumiwa yule mtu maskini. Kwa hiyo hukumu yake ilimgharimu afiwe na watoto wake wanne. Hiyo ndiyo ilikuwa hukumu. Tendo la wizi linahukumia kwa kulipa fidia mara nne ya kile kilichoibiwa kwa mujibu wa torati. Daudi alimuiba mke wa Uria na kisha akamuua Uria kwa hiyo watoto wake anne walikufa kama matokeo ya dhmbi ile. Hiyo inamfanya wana wote wa Daudi na matendo yao kwenye mashaka, kitendo cha kumpoteza mtoto, na kumpoteza Absalomu na hivyo inaendelea. Yote yay ale yaliyotoka kenye kinywa chake Daudi mwenyewe yalitokana kwa kuamuliwa na mtu mwenyewe, na siyo na Mungu. Mungu alimtuma nabii ili akampe utata wa jambo ili kwamba Daudi ajihukumu mwenyewe. Kwa jinsi hiyohiyo wakati Musa alipokwenda kwa Farao, alijihukumu mwenyewe kwa kinywa chake mwenyewe. Wakati aliposema kuhusu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa Israeli ndipo alitangaza kifo cha wazaliwa wa kwanza wan chi yote ya Misri. Mungu hakupanga hapo kwanza hambo hili. Na ndiyo maana Musa alisema: “Bwana, amejihukumu mwenyewe kwa kinywa chake menyewe.”

 

Ingawaje Mungu anajua kile tunachokifanya, anaujua moyo na anajua tunachokwenda kukifanya. Hatuwezeshi sisi kukitenda hicho na hili ndilo Tatizo la Uovu. Mambo hayapangwi. Maamuzi ni kiti kisichokuwepo, mchakato wenye maana kwenye harakati za mwanadamu.

 

Kwa kuirudiaaya ya 29 na hadi aya ya 31 tunasoma hivi:

[29] Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi..

 

Roho Mtakatifu yampasa atupondeponde na kutupa umbo zuri ili kutufanya tuwe na tabia za Kristo.

 [30] Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.

 

Kwa kupitia uweza wake Mungu wa kujua kila jambo, anajua kile tunachokwenda kukifanya; anajua nani wa kumtumia. Anawaita watu wale wakati unapokuwa ni muda kwa wao kuongoka, kubatizwa, ili awezeshwe kuwa na tabia za Kristo. Kisha wakati anapowaita, anawahesabia haki. Uhesabiwaji haki kama tulivyozoea kwa lugha ya uchapishaji ni kuzipangilia kurasa na kuruhusu kuchapishwa ili ukurasa huo uwe umelingana, kukiwa kumepangiliwa vizuri na bila kasoro. Hiyo ndiyo haki au utakatifu unaoenenda na Roho Mtakatifu katika kumuandaa mteule ili aweze kuwa na tabia za Kristo kwa kupitia mapenzi ya Mungu.

 

Aya za 31-32:

[31] Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? 32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

 

Dhana hii ya kuitwa lakini sio kuchaguliwa inaendana kinyume na hali ya kukusudiwa tangu mwanzo na uweza wa Mungu wa kujua kila kitu ambao kwamba watu wengi wameitwa kwenye mwili wa Kristo wakiwa hawajakusudiwa tangu mwanzo na Mungu kuwa waitwe. Hiki ndicho kilichotokea kwenye nyakati za mwisho kwenye kipindi chote cha zama za Wasardi na Walaodikia. Tumeona wote hii na watu wengi walio kwenye kanisa la zama ya Wasardi ya Makanisa ya Mungu nay a Walaodikia walikuwa wameitwa lakini hawakuchaguliwa na walikuwa ama wamekufa au walikuwa wametapikwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu kwa kuwa walikuwa vuguvugu. Mungu hakuwaacha washinde; bali hawakuwa wamechaguliwa tu kwenye kwenye mahali pa kwanza. Hawakuitwa kwa uweza huu wa kujua kila kitu wa Mungu; waliitwa kwa kuwa waliusikia ujumbe bali hawakumudu kuufuata ujumbe huo wote.

 

Dubia imefanywa kuwa adui wa sheria za Mungu na kalenda za wapagani zinajaribu kufanya isiezekane kuishika Kalenda ya Mungu kama tutakapo kwenda kujadili kwa kina kwenye Toleo la 3.

 

Wengi wanajua kile kinachohitajika kwenye imani lakini bado hawaishiki kwa kuwa ni vigumu sana kwao; kwa kawaida sasa kwa sababu ya Miandamo ya Mwezi Mpya. Katika nchi ya Marekani ni vigumu sana kuzishika Siku Takatifu kwa kuwa likizo yao siyo ndefu sana kwa hiyo ni vigumu sana. Sabato siyo kwamba ni jaribio la wateule peke yao na haijadumu kwa kipindi cha miongo mingi sana nchini humo. Kipimo au jaribio la wateule ni maadhimisho ya siku za Miandamo ya Mwezi Mpya na Sikukuu kamili za maadhimisho ya Pasaka na Idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa siku nane, kuiadhimisha sikukuu hii sawasawa na ilivyoagizwa kwenye Kumbukumbu la Torati 16 inayoelekeza jinsi inavyotakiwa kuzishika sikukuu hizi, hasahasa sikukuu ya Pasaka. Tusipoiadhimisha sikukuu hii basi tunakuwa tumeshindwa na ni jaribu la siku za mwisho.

 

Na zaidi sana, Mungu amewaacha wanadamu na mapepo watende dhambi kwenye kipindi cha mpango wake kwa kuwa ameruhusu utaratibu wote urejeshwe upya na hakuna uhai wowote itakaoweza kupotea licha ya maumivu na iwewe vilivyojitokeza kwa makosa na dhambi za wanadamu na kushindwa kwao kuzishika Sheria au Torati ya Mungu. Mpango huo wa Wokovu utaelezewa pia kwenye Toleo la 3.

 

Kwa hiyo uweza wa kuelewa kila kitu wa Mungu hauamui kile tunachokifanya, zaidi ya kile ambacho Mungu anakijua tu kile tutakachokifanya na anajua kwamba ni nini malengo yetu na maamuzi yetu. Biblia inasema; “na Daudi hakutenda dhambi tena” na Mungu Mungu alijua kuwa Daudi hatatenda dhambi tena na Nathani alisema hivyo. Mungu alimshughulikia Daudi na alimtumia. Kwa sababu ya ukweli kwamba Sulemani alitenda dhambi, ufalme ulikunguwaa au kutatizwa kuendelezwa salama na mtoto wa Sulemani lakini siyo katika siyo kwenye mstari wa uzao wake hadi Sulemani alipokufa (soma 1Wafalme sura ya 11).

 

Mungu anatujua jinsi tulivyo na kile tunachokifanya na anajua kuwa tunajaribu na kujitahidi. Anatupa njia kutoka kwenye majaribu haya yote nan i suala la kuwa tuhakikishe kwamba tunaweza kujiinua juu na kuendelea mbele na kufanya Mungu anachotutaka tukifanye kwa kadiri tunavyoweza. Huu kwa kweli ndiyo utaratibu wa muhimu wa wito wetu na wa uweza huu wa Mungu wa kujua kila kitu na wokovu wetu ndipo unahesabiwa haki na unalingana na kimo cha kuwa sawa na Kristo akiwa ni kama mzaliwa wa kwanza wa ndugu wengi. Sisi tu wale walio watakatifu, wateule wake Mungu wanaozishika amri za Mungu na imani na ushuhuda wa Yesu Kristo kama tunavyosoma kwenye Ufunuo 12:17 na 14:12.

 

Wana wa dunia hii hawajaitwa kwenye mwito wa wateule wanaohesabiwa kuwa na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza wa wafu, na wameachwa tu kwenye mambo yao hadi utakapofika wakati wa kuwashughulikia. Kwa wengi wao, na kwa kweli wengi wao, hawatashughulikiwa hadi watakaposhughulikiwa kwa kuhumu kwenye Ufufuo wa Pili wa wafu. Mungu hasababishi maovu. Bali huwa anaruhusu tu yatokee na anaitimiliza mipango yake licha ya kile kinachofanyika ulimwenguni.

 

Sehemu ya 2: Dhana ya Makatazo

 

Makatazo kwa Kiumbe

Tutaona sasa utaratibu na mfumo wa Sheria au Torati nan i dhana ipi ya usawa na haki tunayoweza kuiainisha kutoka kwenye tabia za Mungu na sharia zake. Zinakuwepo kutoka kwa muumba, mwajibiko wa kihisia na kimaudili kwa matumizi sahihi ya kile alichokiumba. Kama kuna uumbaji wa hisia au wazo, kiasi cha kwamba, kuna kitu cha uumbaji na uumbaji umefanywa kama uumbaji fikra au wazo na muumbaji, ndipo kuna makatazo yaleyale kwa muumbaji ya kuanzisha utaratibu wa usawa wa kijamii na wa haki, yaani, sababu na lengo la uumbaji inayohusiana nayo na matendo yaliyo sawasawa na tabia ya kiumbe aliyeipangilia na kuianzisha.

 

Mtu angeweza kusema kwmba kiumbe asiye na maadili angeweza kuanzisha kitu chochote kwa sababu yoyote, lakini ikiwa kama mtu fulani anajaribu kuzalisha kiumbe kitendacho kazi ndipo hicho kinapaswa kitende kazi kwa mujibu uliosawa na tabia au asili ya kiumbe kilichokiumba.

 

Mungu na Sheria hawatofautiani, ambayo ni kamilifu, ya kweli, ya haki na ni njema. Sharia inatokana na tabia asilia ya Mungu.

 

Tutamuona Mungu kuwa ni chimbuko la uumbaji usiofananoshwa na chimbuko la usawa wa kijamii na haki au utakatifu.

 

Falsafa zimejaribu kuanzisha na kuendeleza nadharia ya ulinganishaji wa wastani wa uezeshaji ya kijamii na wafikiriaji wamehusishwa kwa miaka mingi kwa kuendeleza kitendo hiki asilia cha mfumo wa kijamii na mpamgilio wake. Siasa zimeendelea zikiwa kama vitu muhimu vya kuweka mpangilio mifumo hiyo ya kijamii. Nyingi zake zilishindwa, kwa kuwa wanasiasa ni watu wasiozingatia maadili au wapotofu na muda mrefu uliopita waliziondolea mbali jamii hizo zisizoweza kuainisha uwezeshaji kwa muda mrefu na kwamba mifumo ya kijamii inaweza kuhongwa kwa maslahi binafsi na kujipigia kura wao wenyewe ili kujipatia fedha na raslimali kutoka kwenye mfumo wa kijamii. Kwa umuhimu unaomaanisha kwamba umeangukiliambali. Ilionekana kwa Wababeloni, Wayunani, Warumi na kisha kuendelea hivyo hadi huko Ulaya, China pamoja na mifumo yake mbalimbali ya kijamii na huko Misri. Imeanguka chini tu kwa njia ya kutofanana na maslahi yake binafsi.

 

Moja ya tatizo kubwa kwenye sharia na utaratibu wa jamii ni kwamba kuna mgongano usio sawa. Uwekaji ainisho wa uwezeshaji ndani ya mfumo kwa maneno machache na ukituama kenye usawa wa kijamii kwa haki ya kila mmoja imeshindwa kuainisha uwezeshaji kwa muda mrefu.

 

Kuna tatizo la kiuelewa la kifalsafa kwenye muainisho wa uwezeshaji kwa ugawaji wa bidhaa na huduma na kanuni za kijamii zinashindwa kwenye mkanganyo huu usio wa kawaida. Nadharia pekee inayosimama hadi kenye muainisho huu wa uezeshaji kwa kiwango kikubwa unatuama kwenye muainisho wa nadharia ya makatazo.

 

Nadharia ya makatazo ndiyo njia pekee ambayo jamii inaweza kudumu kwa muda mrefu. Tunapozitazama sheria za Mungu, zinaweka tasira kwenye sheria hizo za Mungu kwenye nadharia hii ya makatazo au miiko.

 

Amri Kuu mbili ni amri zinazomlenga kila mtu binafsi yake kwa pande mbili. Amri Kuu ya Kwanza ni kwamba mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote na kwa roho yako yote. Amri Kuu ya Pili ni kwamba mpende jirani yako kama nafsi yako.

 

Yapili inafanana na ile ya Kwanza lakini moja inamhusu Muumbaji akiwa kama chimbuko na kusudi au lengo na mlengwa anayeshikamanisha viumbe pamoja. Kwa hiyo, usiwe na miungu wengine ila mimi, niliyo Mungu wa Pekee na wa Kweli. Kiumbe huyo anakuwa ni kiini cha familia ya ulimwengu, kiroho na kibinadamu. Ulimwengu wote mzima unaendeshwa au kupewa msukumo na ile ya Kwanza, kisha ya Pili kwa maana ya kujifanyia sanamu za kuchonga au kujiwekea sanamu au vitu kwenye madai au mbadala wa Mungu na halafu kulitaja au kulitumia Jina la Mungu pasipo sababu. Amri hii ya Tatu inaenda kwenye mamlaka ya kuutumia uweza au nguvu za Mungu. Wakati unapochukua kitu fulani, jina, pasipo sababu, basi unalitumia vibaya kwa malengo mapotofu mamlaka yaliyowekwa kwenye uumbaji wa Mungu. Unapotosha na kukengeusha mfumo aliouweka Mungu.

 

Kwa kawaida inabidi kuwe na mfumo wa utaratibu ulioekwa kwenye mfumo ule na utaratibu huu unapasa uonyeshe maana mwelekeo na utaratibu wa kijamii. Muda umekisha tengwa kwa ajili ya utaratibu mzima ili kwamba iendane kwa mujibu sawa na mapenzi ya Mungu kwa kupitia sheria yake, ilitenda kazi kwa lengo hili kama alivyouelekeza ulimwengu kuwepo na kutenda kazi.

 

Amri hizi nne zote zinahusiana na Amri Kuu ya Kwanza na inatenda na kuruhusu harakati za wanadamu pamoja na harakati za kilimwengu kwa mujibu sawa na mapenzi ya Mungu. Kuna mielekeo mine rahisi iliyokusudiwa kwenye uwekaji mambo yote katikati ya kimahusiano na kuhakikisha kwamba hakuna harakati zozote zingine zinazoingilia kati na uhusiano ule na utaratibu ule.

 

Hakuna atendaye mambo vibaya au kwa upotofu kwenye mfumo unaochukua mamlaka yale bure na inatenda kazi kwa mujibu sawa na mfumo au utaratibu wa kalenda iliyowekwa kwenye sharia za Mungu. Huo ndio mfumo wa makatazo ambao Muumba ameuweka kwa mahali pa kushughulikia na mawazo ya wanadamu, ili kwamba viumbe wale wote awajibike sawasawa na mapenzi yake na maelekezo yake.

 

Sheria au Torati ni kigezo ambacho kinaelekea kutoka kwenye tabia zake kwa kuwa huwezi kuweka sheria ambayo ni kinyume na tabia na asili na malengo ya Muumbaji wa ule mfumo na utaratibu wake. Kwa hiyo hakuwezi kuwa na mfumo unaoruhusu uumbaji ambao haundi sawa na tabia inayoendana na Kiumbe ambaye ameiweka iwepo. Vinginevyo, mfumo wa kifalsafa utaivunjilia mbali na Muumbaji akatabilwa na kitu fulani ambacho kitakuwa kinatenda kazi yake kinyume kabisa asili yake. Na hiyo ingeathiri uweza wake wa ajabu wa kujua kila kitu na uweza wake wa kuwa wa nguvu zote, Uweza na mamlaka yake juu ya uumbaji na uweza wake wa kupanga na kuona mbali utaratibu na mfumo ambao ameuumba. Kiumbe huyu hawezi kuwa Mungu kama kuna mfumo uliowekwa ambao ni kinyume kabisa na tabia na asili yake.

 

Kenye Amri Kuu ya Pili tunaanzisha familia kwenye Amri ya Tano. Familia hii inachukua ponti ya kati kuelekea kwenye Amri ya Pili kama ya Kwanza ambapo Amri Kuu ya Kwanza imeweka pointi ya kati na kusudi la uumbaji. Na hii ndiyo sababu ya kwamba familia hii inashambuliwa wakati wote na wapinga mifumo na taratibu za kijamii. Na ndiyo maana Shetani amejaribu kuuanzisha, na imani ya Kibabeloni imeanzisha mfumo na imani ambayo ni mkakati au jaribio la mwisho kwa ajili ya maslahi ya familia na mfumo wa kijamii, ambayo kwayo kila mara inavunjika na kuanguka na hauwezi kudumu au kuendelea.

 

Kwa hiyo, ndivyo tunakuwa na miongozo kwenye amri ya Sita, ya Saba, ya Nane, ya Tisa na ya Kumi zinazotoa mwongozo kwa harakati za mwanadamu zikihusiana na yeye mwenyewe.

 

Kuna maagizo ya kulinda uhai ili kwamba familia iwe na wajibu wa kwanza wa kuanzisha uhai na kuendeleza uwepo na mpangilio wa familia ili kwamba uhai uendelee kwenye utaratibu wa kisheria wa Mungu ulio sawasawa na sheria zilizowekwa na Muumbaji. Na ndiyo maana kwamba matendo ya ufiraji na usagaji yanapingana na tabi na asili halisi ya familia. Na ndiyo maana kijamii hayakubaliki na ndiyo sababu ya kwamba ytahukumiwa na hayatakuwepo wakati atakapokuja tena Masihi mara ya pili. Na hii ndiyo sababu ya kwamba jamii inaparaganyika wakati huu na itaendelea kuwa mbaya zaidi na zaidi hadi wakati huu wa dhamira ya jamii itakapofikia kiwango cha kuharibika kabisa.

 

Kanuni hii ya kuwezesha iishi inachukuliwa kwa maana kinyume kwa kuua akati agizo linasema “usiue”, lakini wajibu ulio kwenye dhana ya agizo ni kwamba “ulinde uhai.”

 

Hutaweza kuua watu walio kwenye jamii isipokuwa ipo kwenye amri na maamrisho ya Mungu. Kwa mfano, huwezi kufutilia mbali ongezeko la wanyama; huwezi kuondolea mbali kwa viungo vha mnyama. Yakupasa ujue kama unachukua vifaa vinavyolika au vilivyoruhusiwa kuliwa vilivyotengwa kwenye sharia ya vyakula ili viliwe kwamba uviache hai vitu vizalishwavyo vya viungo hivyo na kwamba usimchukue mama na uzao wake; usiwachukue na kuwaua na usiwaachie uwezekano wa kuendelea kuzaana. Uhakikishe kwamba kuna maeneo yaliyotengwa ya kulinda viungo hivyo. Hayo yote yamejumuishwa kwenye Amri ya Sita isemayo; Usiue, kwenye ile isemayo ukiache hai.

 

Kwa jinsi hiyohiyo isemayo “Usizini” inautendaji wake maalumu kwenye kuilinda familia ili kwamba harakati zote za jamii zinasukumwa kwa kuilinda kila familia na kwamba haijavunjiliwa mbali. Jambo hili kwa hiyo linarudisha nyuma kwenye dhana ya maagizo. Kuna maagizo kwa familia na kwa kila mmoja, kwa kuwa kila mmoja anatoka kwenye familia, na inaanzishwa kwa njia ya mwanaume na mwanamke. Haitokani na wanaume wawili au wanawake wawili na kunaagizo pia la kuhakikisha kuwa watu hawa wawili wakae pamoja.

 

Inayofuatia ni ile isemayo “usiibe” inaelekea kuishirikisha familia na mifumo ya kijamii kutenda kazi kwa weledi mkubwa. Kwa utaratibu wa utoaji wa zaka, ambayo ni sheria na agizo la Mungu, kanuni ya kijamii imewekwa na kuandaliwa kwa misingi endelevu. Zaka ya Kwanza inahakikishia kwamba mtaratibu au mfumo wa kimaagizo na kisheria uwe umelindwa. Kwa hiyo utaratibu wote mzima wa mfumo wa haki unapangiliwa na kulindwa na viongozi wa mifumo iliyopangiliwa. Ndiyo maana zaka imetakiwa kanisani na kanisa limeagizwa kuweka utaratibu na mfumo wa usawa wa kijamii na wa haki. Na hii ndiyo sababu kitendo cha kumpendelea mtu kanisani kwa kiasi fulani ama ya kutisha kama kitendo cha ufisadi wa kupokea rushwa mahakamani. Hii ndiyo sababu Makanisa ya Mungu yaliangamizwa kwa kuwa mengi yake yalikuwa yanawapendelea watu. Mifumo ya kijamii na mifumo ya kidini hadi siku hii ni ya kuwapendelea watu na haitendi haki, ikitenda kazi kinyume kabisa na sheria zilizowekwa na Mungu kwenye Amri Kuu ya Kwanza na ya Pili.

 

Kwa hiyo zaka moja inawezesha mfumo wa kiserikali na kufanya msukumo kwingine zaidi kwa fedha, zaidi kuliko utoaji sadaka wa hiyari mara tatu kila mwaka kama ilivyoagizwa kwenye torati, kutofanya hivyo ni wizi na ni kuyatumia vibaya mamlaka ya kimahama. Kwa hiyo ingeikanganya Amri ya Nane isemayo “usiibe.” 

 

Haki ya kijamii ya familia kwayo yenyewe na kwa watu wengine imejumuishwa kwenye zaka ya pili. Zaka ya pili imetengwa kando kwa hiyo familia inaweza kutenda kazi za Amri ya Nne iliyoweka na Mungu. Majukumu yote ya Amri Kuu ya Pili kwa maana ya haki ya kijamii na usawa kwa fedha ya ziada ambayo imetolewa kwa lengo la kuzisaidia familia zingine ndani ya utaratibu wa kijamii ulioanzishwa. Ndiyo maana ndipo sheria inatenda kazi kwenye makundi enezi tangu kumi hadi la hamsini, mamia na maelfu. Wakuu wa makumi wako pale ili kuhakikisha usawa wa kijamii kwenye utaratibu wa kijamii kwenye utaratibu wa kijamii ili kwamba kila fedha za ziada zinazohitajika, zisizoweza kupatikana kwa kupitia Zaka ya Pili kwa maana ya usawa wa kijamii. Hii inafikiwa kwa Mwaka wa Tatu. Mwaka wa Tatu unaendeleza mvuto au msukumo wa kufunikiza katika mwaka wa hamsini wa Yubile.

 

Muundo huu umetuama kwenye kipimo cha mrithi wa hukumu isemapo “usiibe” ambapo pana mambo fulani ya muhimu; marejesho ya mara nne kwa kila kitu kilichoibiwa. Mara tu unapomrudishia mtu mara nne kutokana na utajiri wako wote, na kama itawezekana basi tumika kwenye miaka iliyobakia kweny mzunguko wa Sabato kama mtumwa kwa mtu mwingine kwa kuwa ulikitumia vibaya kitu ambayo mtu alikwishaanza kudhania kabla hawapata fedha kwenye jamii. Hii ni lazima ishurutishwe na viongozi wa mfumo huu wanatenda mambo kama waamuzi au mahakama kwenye ukuhani hawawezi kushikilia ofisi iwapo kama wanayatumia vibaya mamlaka waliyopewa kwenye Amri ya Tatu na kama wamekengeuka.

 

Amri ya Nane inasema “Usimshuhudie jirani yako uwongo.” Kwa hiyo rekodi sahihi katia jamii ni ya muhim sana. Yapasa kuwe na rekodi nzuri ili kuhakikisha kunakuwa na hukumu ya haki na mashahidi wa uwongo ni budi wahukumiwe pasipo huruma kwa mujibu wa mfumo huu. Shahidi wa uwongo anayeshuhudia uwongo ili kupotosha haki ili kuwezesha matendo yasiyo ya haki chini ya sheria ile iliyochukuliwa kama ni hukumu kwa mtenda maovu aliyepewa shahidi wa uwongo imetumika au kutolewa.

 

Mashiko ya mkururu huu yanafuatia moja baada ya jingine na inalazimisha kutazamwa kwa mfumo wote wa sheria na wa familia. Haiwezi kuruhusiwa kupotoshwa. Zinakuwepo kwa kila mmoja wajibu wa kuulinda mfumo huu wa sheria. Torati inajionyesha kama taswira ya Amri Kuu Mbili na yote hii inatokana na Tabia na asili ya Mungu kwa dhumuni la Uumbaji. Kimsingi inatakiwa iwepo na idumu kwa maana ya uumbaji, utaratibu wake na lrngo lake. Kwa hiyo wote ni lazima afuate mmojaa baada ya mwingine. Na ndiyo maana Amri ya Kumi inasimama katikati maka mhimili wa sheria yote kwa maana ya kwamba kusudi la nia na moyo. Na ndiyo maana imeandikwa yote mioyoni mwetu na mawazoni mwetu na ndiyo maana Roho Mtaakatifu ni wa muhimu kwetu ili kutuwezesha kuichukulia hii hadi kwenye Amri ya Kumi na kuielewa tabia na kanuni ya sheria.

 

Mfumo huu utauhakikishia kuwa na usawa wa kijamii na haki ulimwenguni kote. Utahakikishia ulinzi wa kimazingira wa kila kiungo kwa kiumbe, na itahakikishia kwa njia ya sheria za vyakula pamoja na zaka zilizotolewa vizuri.

 

Pia, kama mizunguko ya Sabato inaagizwa na kuanikizwa na sheria kwenye Amri ya Kumi, mazingira yamewekwa, ardhi ina Sabato zake na kila mmoja anaweza kukusanjika kwenye mwaka wa Sabato. Mwaka wa Tatu wa mzunguko wa Sabato unatoa raslimali, za aina mbili zote, za nafaka na za fedha kutokana na mwelekeo wa raslimali ha hakuwezekani kuwa na kitu kama hicho cha wizi kwa riba. Mataifa watakopa lakini watatakiwa tu kulipa. Hukumu yake ni iwapo kama taifa linapaswa kulipa ndipo litalipa kutokana na raslimali au mali zao na zaka ili kuondokana na matatizo linayokabiliana nayo kwakuwa limeshindwa kujichukulia ama Amri Kuu ya Kwanza au Amri Kuu ya Pili. Limeshindwa kutoka kwenye wajibu wake kwenye usawa wa kijamii na uwezeshaji wake kwa kupitia nadharia hii au Sheria ya Makatazo ambayo ni Sheria au Torati ya Mungu.

 

Ushindwaji wowote wa muundo wa kijamii utashushwa kwenye kushindwa kwa nadharia ya muongozo wa kuendesha kwa kila mmoja, kwa kuwa hawaoni kuwa kuna muongozo wa kuufanya mfumo huu ufanye kazi. Mungu ameweka juu yao amri hizi, ambayo ni miongozo ya kila mmoja na familia zilizo kwenye muundo huo, na koo na makabila, na wanatenda kazi kama amri kamili na mifumo ya miongozo na kama hutazitunza utaangushiliwa mbali kwa kushindwa, au kwa kujitenga na kushikilia kwenye dunia hii iliyolaaniwa. Wakati Shetani alipovunja kanuni ya umuhimu na ulazima wa kuzishika sheria, ndipo dunia ilipolaaniwa, kwa kuwa umuhimu wa kuzishika sheria ulishuka kwa kupitia nadharia za usawa wa kijamii kwa sheria inayotokana na tabia ya \mungu hadi kwenye nadharia ya mwongozo inayofanana na Amri Kuu ya Kwanza na ya Pili kama ilivyoainishwa kwa kina kwenye Amri ya Kumi na kanuni zake elekezi zinazofuatia kutoka hapo.

 

Dunia ililaaniwa kwa kuwa agizo la kuzishika sheria lilikuwa limevunjwa. Wakati Mashahidi wanapokuja na wanaporudisha tena agizo la sheria ya mfumo wa kijamii watarudi nyuma kwenye mfumo sahihi wa muongozo kwenye kila mzunguko kwenye Mzunguko wa Mwaka wa Sita mavuno makubwa ya ziada ili kuiwezesha miaka ya Sabato na Yubile iweze kuadhimishwa bila shida. Mwaka 2025 haijalishi ni kwa kiasi gani dunia imeharibika kutakuwa na mavuno makubwa mara dufu kwa ajili ya maadhimisho ya miaka ya Sabato na Yubile. Hii ni kwa lengo la kuuwezesha mfumo wa Sabato na Yubile ili kwamba ulimwengu wote uweze kuelimishwa vizuri kwenye mwaka ule wa Sabato na kisha uwe tayari kuchukua pahala pake kama ulivyowekwa tangu mwishoni mwa Sikukuu ya Vibanda ya mwaka 2027. Tangu siku ya Kwanza ya mwezi wa Nane ambao ni mwaka wa Tisa unajitokeza na kuchukua mahala pake wakati ardhi yote itakapofanywa upya. Kilimo na maandalizi vinafanywa ili kwamba mavuno ya kwenye mwaka wa Kwanza wa mzunguko unaofuatia, Yubile ya 121 inapoanza. Ndipo kwa hiyo dunia itaanza kufanywa upya.

 

Kile tutakachokwenda kukifanya ni kuisaidia dunia irejee upya kwa kufuata na kuzitumia sheria hizi na kwenye nadharia ya mwongozo wa kijamii kwa kutumia Amri kumi za Mungu na mifumo yote midogomidogo ya sheria. Hakuna atakayepotea.

 

Yerusalemu utafanywa upya na Hekalu litajengwa huko Yerusalemu kwenye nusu ya kwanza ya Yubile ya 121. Kila mwaka kila taifa hapa duniani watapeleka wawakilishi wao huko Yerusalemu ili kupewa maelekezo kwa ajili ya mwaka unaofuatia. Kutakuwa na utaratibu wa kisheria utakaoanzishwa na kisha kurekebishwa kwa mfumo au kanuni ya mafundisho ya kila mmoja yakitokea huko Yerusalemu kila mwaka.

 

Kwa kuwa taifa lolote lisilopeleka wawakilishi wake kwenda kuishika sikukuu ya Vibanda, Zekaria 14:16-19 imeweka wazi sana kitakachowapata. Hawatapata mvua kwa wakati muafaka na watateseka kwa mapigo ya tauni ya Misri, ambavyo kwamba, kama kutakuwa na mfumo wa kilimo cha umwagiliaji pahala pake kwenye taifa ambapo wanadhani kwamba watajiondoa kuwa ni sehemu ya mfumo huo kwa ajili ya umwagiliaji watapigwa kwa tauni na hawataepuka kukumbwa na ukame. Ulimwengu mzima wote utafanya kama ulivyoambiwa.

 

Mfumo huu kwenye Torati, unatuama kwenye nadharia hii ya maelekezo kumwelekea Mungu kwenye Amri ya Kumi hadi kwenye Amri zote. Kutakuwa na utaratibu au utawala utakaoiongoza au kutawala kipindi hiki cha Milenia, kwa Tabia au Asili ya Mungu hadi mwishoni mwa Ufufuo wa Pili wa Wafu na hukumu ya watu wote na kisha tutaendelea mbele kuiongoza dunia.

 

Mfumo huu utakuwa ungaliko bado kuwa kuwa unatokana na Tabia na Asili ya Mungu na tutafanana sote kuwa sawa na Kristo na kwamba Tabia hiyo itajiweka ndani yetu na itatawala jinsi tunavyofanya kazi kwenye utawala huo.

 

Kwa hiyo muundo rahisi, Amri hizi Kumi, ambayo kwayo sheria au torati yote imetuama kwayo ni msingi wa sheria za kijamii. Kitendo cha kuziweka pamoja amri zote wakati wa Usomaji wa Torati, katika kila mwaka wa Sabato, kinaonyesha jinsi Amri hizi Kuu zinavyoiongoza jamii na kanuni zake.

 

Kwa hiyo mchakato huu unatoa uhakikisho wa kwamba Taatizo la Uovu limepungua. Utashi wa mwanadamu bado unabaki lakini kuna adhabu na imeekwa wazi lakini mfumo wa kijamii unaoongoza jamii. Hukumu iliyoorodheshwa hapa zimekatazwa kabisa kwa hukumu ya kifo, kwa kuwa kwenye kila moja yao, mwendelezo wa uvunjaji wa amri unaendana nayo ni hukumu ya kifo. Tumepewa fursa ya kutubu, kurudiwa na kurejeshwa upya, lakini hakuna mwingine yeyote hapa duniani anayeweza kujitokeza kwa ukmilifu na kwa utashi akazivunja sheria hizi. Mara nyingi sana jamii huzivunja na dunia huzivunjiliambali na Mungu huingilia kati.

 

Kwenye utawala wa Milenia kutakuwa na uingiliaji kati wa moja kwa moja mwaka wa hadi mwingine na mataifa yatakuwa yametiishwa kwa kuhukumiwa kwa kushindwa kwao kuzishika sheria. Kwa hiyo hawataweza kuipuuza na ulimwengu wote mzima watazishika maagizo ya sheria kama zilivyoamriwa na kuelekezwa kwenye kalenda ya Mungu na kwa kupitia sheria, ili kwamba kusiwe na kutofautiana na kuna haki ya kijamii na mpangilio katika ulimwengu wote mzima. Malaika wa mbinguni na Ufufuo wa Kwanza wa wafu vipo pale ili vitokee. Wakati Ufufu wa Kwanza wa waf utakapotokea, yeyote miongoni mwetu atakayeachwa akiwa hai na huku akingojea waliokufa wafufuke na sisi sote kwenda Yerusalemu tukiwa kama viumbe wa kiroho. Kwa hiyo tunawajibika kwa kufanya kazi pamoja na malaika wa mbinguni kwa kuiongoza na kuitawala dunia.

 

Muundo wa sayari umepangiliwa na unaendeshwa kwa maongozi au uthibiti wetu, na siyo na malaika toka mbinguni, kwa kuwa wajibu wa kuwahukumu mapepo na hukumu ya mapepo kwenye Ufufuo wa Pili wa wafu tumepewa sisi. Na kama tunavyofanya hivyo kwa niaka elfu ya Milenia ndipo mapepo wanachukizwa au wanakasirishwa sana kwa mwenendo wetu.

 

Sheria hizi zote na jinsi tunavyozilazimisha na jinsi muundo wa sayari unavyoendeshwa kwenye utawala wa millennia kunaamua kile kinachotokea na kuwapata mapepo na inatumika kama jambo la kuamsha hisia kwenye hukumu yetu.

 

Wa mfano, tunapowahukumu wao kwa shuruti na bila kuwahurumia, mapepo wangekuwa na sababu kubwa sana wa kuonyesha makosa ya utendaji kazi wetu wa majukumu yetu na hukumu yetu ya uwezeshaji wao wa majukumu yao. Ndiyo maana hukumu imewekwa kwetu iliwekwa pia kwa Kristo.

 

Matendo ya Kristo yaliyohukumiwa na Shetani kwenye vita pale jangwani. Shetani alishindwa na akahukumiwa na Kristo. Kristo hakushindwa, bali Shetani ndiye alishindwa.

 

Kila nnoja wa Malaika waasi atahukumiwa na wale waliopewa vyeo au nyadhifa kubwa za kufanya hivyo kwenye utawala wa millennia. Viongozi wa mataifa kwa maana ya uongozi wa kiroho watahukumiwa na viongozi wa mataifa walio na nyadhifa zinazolingana, kama wale Sabini. Hao viongozi muhimu wa kiroho wa watakatifu wateule watawahukumu viongozi muhimu na wakuu wa kiroho wa malaika walioasi na kwa hiyo watakwenda.

 

Utawala huo utadumu kwa kipindi cha miaka elfu na kisha kwa miaka mia kitakuwa cha upangiliaji wake na cha merejesho mapya. Hiyo itendelea hivyo kiasi cha kwamba hatimaye sisi sote tutaielewa dhana hii yote ya usawa wa kijamii na jinsi ulimwengu wote unavyohitaji sheria za Mungu ili kutenda kazi sawasawa.

 

Na ndiyo maana kalenda hii takatifu yapasa iendane sawasawa na majira. Na ndiyo mwaka mrefu wa Kibabeloni kwenye kalenda inayojulikama kama ya Kiyahudi au ya Hilleli inaweka kichekesho au kituko, mzaha, wa kuudhihaki mfumo uliwekwa hapa duniani na Mungu ambayo kwayo inaonyesha hilo kwa kuwa wanaweka mwaka mrefu kwenye miaka tofauti na kwa hiyo vipindi na majira yanakuwa nje na utaratibu au mfumo aliouweka Mungu kwa maelekezo sahihi kwenye Amri ya Nne ambayo imepotoshwa kabisa na watu hawa hawa wanaojifanya na kudai kuwa wanaenenda sawasawa na maagizo ya torati au sheria za Mungu. Kibaya zaidi ni kwamba Makanisa ya Mungu wamejilimbikizia dhambi kwa kumfuata Hilleli kwenye makanisa mengi katika karne ya ishirini.

 

Wayahudi wamejisimamishia mfumo ambao hautaweza kufanya kazi na wanajua kuwa haufani kazi. Walifanya hivyo kwa makusudi kabisa na Kanisa la Mungu likiwa chini ya uongozi wa Herbert Armstrong lilitohoa kalenda ile. Wanajua kuwa haiwezi kufanya kazi na walijua pia kwamba ilikuwa sio imani halisi ya mwanzoni iliyoaminiwa na kutumia Hekaluni wakati wowote tangu hapo na kuendelea hadi kuangamizwa kwa Hekalu mnamo mwaka wa 70 BK. Wanalijua hilo, lakini bado kwa makusudi kabisa wanasisitiza kuishika kalenda hiyo, hata kwenye Makanisa ya Mungu, na wanafanya hivyo kwakuwa huduma zao hazina ujasiri wa kuwaambia ukweli na kuyakubali matokeo ya kushindwa kwao.

 

Hiyo haitaendelea kwa kipindi kirefu sana. Itafikia mwisho kwenye kipindi kifupi sana. Mipindi cha miaka elfu sita alichopewa Shetani karibu kinafikia mwisho wake.

 

Sayari hii karibu inakwenda kuangamizwa kwa hiyo yampasa Kristo aje mapema kwa kuwa sayari ipo kwenye hali mbaya sana.

 

Mataifa yamejiwekea mfumo ambao hauwezi kushikika au kuonekana na wao kabisa. Japani imetengeneza mitambo kadhaa ya nyukilia kama inavyojulika kuwa ni ukanda wa matetemeko ya ardhi; matukio ya volcano yanalikumaa sana maeneo haya. Wataifutilia mbali pia ile hali ya hewa ya ubarafu iliyoko kwenye ncha ya kaskazini mwa dunia, hususan kwenye maeneo ya Pacific. Ni kama vile mapepo wamewaharibu akili zao kwa kiasi cha kuwafanya wafikie hatua ya kuto jail chochote kile kama na wao hawataweza kuishi. Hapo ndipo mahali hata sisi tunaonekana kuwa.

 

Viongozi wa mataifa wanazituia silaha kali na za maangamizi zinazotumia hata kemikali kuwaua watu wao wenyewe. Haya yanaweza tu kuwa ni mawazo ya kimapepo. Mapepo watakuwa wamechukua utawala na kuongoza uongozi wa mataifa yaliyo ukanda wa Mashariki ya Kati na viongozi wa Kimagharibi. Hakuna cha kuwianisha kuhusu kile kinachotokea. Hakuna kitu wanachokifanya ambacho kinaendana sawasawa na amri hizi, iwe ya Kwanza wala Amri Kuu ya Pili au Amri nyingine yoyote inayotokana kwenye Amri hizo Kuu Mbili, na kwenye Amri Kumi. Hawaishiki yoyote kati ya hizo zote na kwa hiyo ulimwengu hauwezi kumudu kuwepo. Mfumo huu unashindwa kidogo kidogo na watu watakuwa masikini zaidi kwa kuwa wanaziweka fedha mifukoni wao wenyewe kwa zaidi na kwa ziada ya ulazima wa wa jamii iendelee kushi au kuwepo.

 

Mbinu mpya zinazokuja ni hazistahimiliki na zinasaidia utajiri zaidi kuliko kuwa kwenye familia, familia zenye kipato kidogo kwenye jamii. Vitu hivyo haviwezi kubakia vikitenda kazi kwa kuwa haviko imara. Mifumo hatari wa kimatibabu ya Wamarekani na ni kile kinachoitwa wa kidini ambao unapuuzia majukumu yake kwa dhana ya miongozo ya sheria ya biblia. Uwezo wetu wa kuthibiti madawa ya antibayotiki unapungua kutokana na kuzuiwa na ngome imara za mihadarati zimeweka makazi yake Marekani na Ulaya ambako faida zake zimeondolewa na wasifanye utafiti mpya. Hawataweza waachiliwe tu waendelee kuishi.

 

Na ndiyo maana Dola ya Kirumi, wakati walipoona kuwa wangeweza kuipatia fedha tu kutoka kwenye utajiri wa dola yao, walianguka kiuchumi kwa kuwa hawakuwa wakilipa Ankara zao. Marekani hailipi Ankara zake. Itafilisika kwa kuwa deni lake linakadiriwa kuwa ni la dola tirioni 19 katika mwaka 2013. Ni wazi kabisa kwamba haiwezi kulipa kiasi hicho pasipo kuipangilia tena jamii yake. Wanaanza kuligundua hilo na Ulaya inagundua pia kwamba Marekani haiwezi kulipa madeni yake. Mfumo wake unashurutishika; hautengamai. Inakwenda kuendelea zaidi sasa kwa kiwango kinachoongezeka hadi mfumo wetu kamili wa kiuchumi uangamie na tuende kwenye vita kamili vya dunia, kwa muda mfupi sana ujao.

 

Sababu iliyowaplekea Wajerumani wamchague tena kiongoi wao mkuu wan chi ni kwa sababu ya maamuzi magumu wanayotaka kuyachukua kwa Ulaya nzima, lakini Wahafidhina wanataka kuifana Ujerumani iwe kiongozi wa Shirikisho la Ulaya nzima. Wataufanya ulimwengu ulipe na hiyo haitawezekana kwa kuwa yote hii inaangamiza kinyume na nadharia hii ya muongozo, ambayo ndiyo njia ya pekee ambayo shria za Mungu ndiyo inayoweza kuifanya iwe ni jamii inayotenda kazi, kwa kuwa inatokana na tabia au asili halisi ya Mungu.

 

Kwa hiyo utaratibu huu ni nguvu kubwa iliyohusiana kwa mwingiliano, iliyoshikamana, kanuni ya utaratibu wa kisheria na intokana na tabia ya Mungu. Hadi tunapoilazimisha tena kanuni hii ya kisheria, jamii itaendelea kupungua na hatutaweza kuiingiza kimbadala na kitu kinginechochote ambacho kinafanya kazi kwa kuelekezwa au kwa kusukumwa kwa kuwa Mungu hukiongoza kwa njia ya asili na tabia yake aliyonayo. Na mfumo usipoendana na tabia ya Mungu hauwezi kufanya kazi.

 

Hapo ndipo tulip oleo, ambapo uovu unatiririka kutoka kwenye kushindwa hadi kwenye kuzitendea kazi sharia za Mungu kama zilivyowekwa na kuelekezwa kwenye taratibu na maamrisho ya torati ya Mungu na maovu yote yanatokana na kushindwa kuzifanya amri na sheria za Mungu zifanye kazi na kuifanya familia kuwa ni kama muundo wa kijumuia ya jamii zetu.

 

Kwenye kila moja ya taratibu hizi na mifumo yake, Mungu ndiye kiini na hakuna mfumo mwingine unaoweza kuwekwa kwenye kituko kwenye mfumo ule. Wengi walio kwenye mfumo ule hawafai wachukuliwe kimzaha au kudharauliwa. Yapasa ifanywe kwa mujibu uliosawa na utaratibu wa kijamii na kanuni ya utakatifu iliyowekwa kutoka kwenye kalenda ya Mungu. Hiyo hatimaye inatoa uhakika kwamba utaratibu wa mwanadamu unaweza kuendelea kwa uangalizi wa familia na kwa kupitia familia hadi koo, hadi makabila, hadi mataifa.

 

Taratibu na imani hizo zinategemeana na Amri ya Sita ya kufanya iishi; ya Saba katika kuifanya familia iwe kama taasisi itendayo kazi; ya Nane inakihakikishia kila kitu kimezalishwa kwa umiliki sahihi na wajibu. 

 

Utaratibu huu unaendana kwa utoaji wa zaka; Zaka ya Kwanza inathibitisha utaratibu wa kawaida wa zaka na utaratibu wa kimahakama, utaratibu wa haki na usaa; kisha kwa kupitia Zaka ya Pili ni kwa ajili ya kupata ustawi mwema kwenye jamii. Sheria au kanuni ya ulaji wa Vyakula iliyotolewa na kupewa wakazi wa dunia hii inaelekeza kile tu kinachostahili kuliwa na kwamba taratibu nyinginezozote zinaunda misingi ya kanuni za vyakula kwenye aina zingine zote za vyakula vilivyoagizwa kwenye kanuni hii.

 

Sababu inayokufanya usile krili na dagaa kamba na pweza ni kwa kuwa wanafanya misingi ya muundo mdogo wa samaki wote walioruhusiwa kuliwa. Mara tu unapowala unaharibu lishe yako kwa kuwa uzito wa madini chuma yao kwenye mfumo wa milolongo ya chakula kwenye bahari inapita kwenye maeneo mengi tofauti ya miili ya samaki hao.

 

Mazingira ya Kibenthiki

Usile viumbe wenye magome walioko baharini, chaza, kome na vitu kama hivyo kwa kuwa hawa ni mawakala wa kazi ya kuchuja na kuondoa uchafu na kuifanya bahari ibakie kuwa safi. Kwa kuwala viumbe hawa unajilisha pia virusi aina ya gastroentero na kuviingiza mwilini mwako na kuudhuru au kuuharibu mfumo wako wa kiafya.

 

Sheria ya Vyakula ya Biblia inakinga au kuzuia magonjwa mengi yanayopitia kwenye nyama za wanyama na vyakula najisi. Soma jarida la Sheria za Vyakula (Na. 15) CCG).

 

Usiwaue viumbe wote walio hai kwenye maeneo yako. Kwa mfano, kumekosekana ndege mruko wa wa kinadharia tu au wala mizoga huko Italia kwa knwa Wataliano huua na kula kila kitu kinyume kabisa na maagizo ya sharia au torati ya Mungu. Kumekuwa hakuna idadi kubwa ya ndege wakubwa katika Italia kwa kipindi cha mamia ya miaka sasa kwa kuwa wanaua na kula kila kitu. Wachina nao wako hivyohivyo. Samaki maarufu wakubwa wamemalizika. Watamkamata papa kwa nia ya kumkata mikiwa yake tu ili wamtengeneze supu. Haya ni maazo mapotofu. Hali hii haipaswi iruhusiwe kuendelea au vinginevyo watakuja kuhukumiwa. Jambo hili linafanya hivyohivyo na Wajapani na wengine wengi.

 

Elimu inatakiwa ili kwamba watu wajue sharia za Mungu ni zipi na sababu ya kwanini wanatakiwa kuzishika na kunapaswa kuwe na hukumu na hukumu yenyewe yapasa iwe kali na itokane na maagizo ya torati. Biblia inaeleea aina zote za hukumu na zinapasa ziweje..

                                                           

Jarida hili linashughulikia kuelezea Tatizo la Uovu, na uovu ni nini, na unatoka wapi nan i kwa nini dunia ipo kwenye mwonekano uliyonayo sasa. Kwa nini imekuwa mbaya sana? Imekuwa mbaya sana kwa kuwa hatuzishiki sheria za Mungu.

 

Hatutaweza kufanyika kuwa Mungu; hatutaweza kuwa elohim hadi tutakapofikia kwenye kiwango cha kwamba Roho Mtakatifu yuko ndani yetu ili kwamba tuweze kuenenda kama Mungu. Hili ndilo lengo letu kuu.

 

Mimi nimesema, Ndinyi miungu? (na maandiko hayawezi kutanguka); (Yohana 10:34-36)                                     

q