Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[125]

 

 

 

Miandamo ya Mwezi Mpya

 [125]

 

(Toleo 2.019950708-19990810)

 

Umuhimu wa Kibilia wa kufanya marejesho ya maadhimisho ya Miandamo ya Mwezi Mpya na maadhimisho ya sikukuu chini ya Sheria vime tathiminiwa katika jarida hili. Utendaji wa siku za kwanza wa waalimu wa Torati maarufu kama walivyojulikana kwama marabi pia yamefanyiwa tathimini, sawa kulingana na vifungu aya maandiko vinavyoelezea jinsi walivyofanya kazi. Mahusiano ya Agano Jipya na maadhimisho ya Miandamo ya Mwezi mpya ni suala lililokuwa muhimu na kweli.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Copyright © 1995, 1999, Wade Cox)

 

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

Miandamo ya Mwezi Mpya [125]

 


Mwaka uliwekwa ili kuweka utaratibu wa kuanzishwa kwa mwezi wa kutolea dhabihu, ambayo inawakilisha dhabihu ya Pasaka ya Masihi. Mwezi ulianzia kipindi cha mavuno, ambao pia ulikuwa ni mwanzo wa mfululizo wa kipindi cha mavuno, ambacho ni cha mavuno ya shayiri. Kwa hivyo kisha yake ni kwamba, Mungu alichukulia fululizo huu wa utaratibu wa mavuno kupitia katika kila kipengele, ambacho kilikuwa ni cha vipindi vitatu vya mavuno. Navyo vilikuwa ni vya Pasaka na Mikate isivyotiwa Chachu, Sikuu za Majuma, na Sikukuu ya Vibanda au Makutaniko. Sikukuu ya Majuma ina wakilisha kama mfano wa mavuno ya Kanisa katika kipindi hiki cha kabla ya kurudi kwake Masihi. Hii ni hatua inayo endelea.

 

Kwa hiyo basi, Pentekoste ni mwanzo wa muandamano wa mambo unaotangulia miezi mwandamo mitano kuanzia mwezi wa Sivani hadi Tishri, ijapokuwa ipo saba katika mafuatano yake ukianzia mwezi wa Nisani hadi Tishri. Miezi hii mitano pia iliwakilishwa na mawe ambayo Daudi aliyachukua kutoka kwenya kijito cha maji (tazama jarida lisemalo Daudi na Goiliati [126]. Pia inawakilisha makanisa yale matano yaliyoonyesha ufanisi katika sura ya pili na ya tatu ya kitabu cha Ufunuo wa Yohana, yakiondolewa makanisa ya Sardi na Laodikia. Hatahivyo, haya matano ni endelevu kama yanayochukulia mahali pa hii miezi. Mwezi wa Sivani huanzisha uwekaji wa jiwe la msingi la Hekalu la Mungu. Hivyo basi, mwandamano wa mabo haya huhusisha na kuzaliwa upya (Du-uzu: au Tammuzi), au kizinga cha moto (Abu: au Ab) au vinara vya Kanisa na utakaso (Elulu: au Elul) wa wateule. Kwa hiyo, miezi hii kuanzia Simanu (Sivan) hadi Teshritu (Tishri) inahesabiwa katika mambo mifano ya Kikristo yaliyoachana na Ukristo mamboleo wa Kibabeli. Mmuliko wa 9-10 wa Abu ilionekana kana kwamba uliruhusiwa kwa ajili ya ibada za sanamu katika Israeli na matendo ya Kibabeli.

 

Mahusiano yalitegemea katika utendaji wa mwezi mdogo unaojiingiza katikati kama inavyoonekena katika miezi ile ya kawaida kumi na miwili. Israeli iliweka mfumo huu kupitia makabila yake. Israeli ina makabila thenashara. Haya yafuatayo ni kutokea upande wa Kaskazini: Dani, Asheri, Naftali, Yuda, Isakari, Zabuloni, Reubeni, Simeoni, Gadi, Efraimu, Manase Benjamini (tazama kitabu cha esabu 10:11 na mistari inayoendlea ikishabihiana na Ezekieli 1:4). Kabila la Lawi liliwekwa katikati ndani au likiizunguka maskani ya hema la kukutania. Kwa hiyo, kulikuwa na makabila kumi na mawili lakini kabila la Yusufu lina haki ya uzaliwa na limegawiwa kikamilifu kabisa urithi wake maeneo mawili na kufikiliza idadi ya makabila kumi na mawili pamoja na kabila la Lawi ambalo lilinyimwa kuwa na urithi ili liweze kufanya shughuli za kikuhani tu. Kwa hiyo ramani hasa ya kazi za hawa Israeli wa kimwili ilichorwa katika nyota wakati wa uumbaji. Mwezi wa Adari II unawakilisha ukuhani kama mwezi wa kumi na tatu sawa na kabila. Mwezi huu hutokea katika kila mwaka wa saba wa mzunguko wa miaka.

 

Mzunguko huu unawakilisha roho saba za Mungu kadiri zinavyofanya shughuli zake chini ya malaika walio katika yale Makanisa saba yaliyoko kwenye kitabu cha Ufunuo. Tatizo hili haliwezi kupata ufumbuzi au kueleweka bila ya kwanza kueleweka maana ya Miandamo ya Miezi Mipya.

 

Nafasi Ya Jumla ya Kihistoria

Sikukuu ya Mwandamo wa Mwezi, inajulikana kwa Wayahudi kama Rosh Hodesh, ilikuwa inaadhimishwa katika siku ya kwanza ya mwezi, wakati wa kutokeza kwa sehemu ya kwanza ya mwezi (kwa mujibu wa Hayyaim Schauss, katika jarida lake lisemalo Sikukuu za Kiyahudi Historia na maadhimisho yake, tr. Samuel Jaffe, Schocken Books, New York, 1938, p.275). kwa hiyo inafungamana na muonekano wa Mwezi Mpya.

 

Inasema: kulifikia wakati ambapo Rosh Chodesh ilikuwa ni sikukuu kubwa sana, zaidi sana na muhimu kuliko hata Sabato za kila Juma…Sababu mojawapo kuu ya kuifanya iwe muhimu kiasi hiki ilikuwa ni kutokana na ukweli kuwa tarehe za Sikukuu za Wayahudi zilitegemea sana na Mwandamo wa Mwezi (sawa tu na hii ya p. 274).

 

Hali hii ilitatiza. Biblia huonyesha kuwa ilikuwa ni muhihmu lakini haikufaa iwe ni kwa kiasi hiki kikubwa cha kuizidi Sabato. Ilikuwa ni muhimu sana kuzidi hata Sikukuu kama vile tunavyoiona.

 

Biblia inatoa mlinganisho wa dhahiri kabisa kati ya Mwandamo wa Mwezi na sikukuu hizi (Hes. 10:10). Sikukuu ya Mwezi Mpya ilikuwa ni siku ya Sikukuu na ilisherehekewa katika siku iliyotangulia siku ya Mwandamo wenyewe wa Mwezi (kwa mujibu wa New Catholic Encyclopedia, vol. 10, McGraw Hill, Ny, 1967, p. 382).

 

Hapa inasema: Katika siku za mwanzo za zama za marabi siku za Mwandamo wa Mwezi zilianzishwa na baraza lao lililojulikana kama Sanhedrin katika Yerusalemu, baada ya kukubaliana na ushuhuda wa kujionea kwa macho kutoka kwa wale waliodai kuwa wameuona mwezi umeandama. Wakati mwingine marabi kwa makusudi kabisa waliweza kuahirisha hii Rosh Hodesh ili kuilinda Siku ya Upatanisho inapokuwa imeangukia siku za Ijumaa au Jumapili. Kalenda ya kudumu iliwekwa kutegemeana na kalenda iliyoitwa ya Hillel II katika mwaka 358 BK, na hii ilitoa siku maalumu ya kuadhimishwa kwa kila ujio wa siku ya Rosh Hodesh ambayo ilitegemeana na mtazamo wa sayari za angani na mjumlisho wa mahesabu (kwa mujibu wa Ensaikolopedia ijulikanayo kama Encyclopedia of Judaism, na Geoffery Widoger, Macmillan, Ny, 1989, p. 502).

 

Kumbuka kuwa huu ulikuwa ni wakati wa siku za mwanzoni kabisa zama za marabi. Hii ilikuwa baada ya kuharibiwa kwa Hekalu mnamo mwaka 70 BK. Kwa hiyo basi, mapokeo ya hawa marabi kuhusu Mwezi Mpya yalikuwa yameegemea katika Kalenda ya Hillel kuanzia 358 BK. Haikuwa na mamlaka yoyote ya kibiblia

 

Hakuna kabisa mashaka kwamba Mwandamo wa Mwezi kwa zama za kale ilikuwa ni angalau muhimu kama ilivyo Sabato.

 

Maadhimisho ya Mwezi Mpya kwa siku zile za kale yalisimamia katika kiwango kama kile cha Sabato. (J. Wellihausen, Prolegomena to the History of Israel, 1885, p. 113)

 

Mwandamo wa Mwezi Mpya ilikuwa kwa hakika ni wakati mtakatifu, na ilikuwa kama tunaweza kuwaamini baadhi ya wanazuoni, walioadhimisha muda baada ya muandamo wa Mwezi Mpya. Hisia hii ilitegemea na propaganda za marabi. Ilikuwa haifanyiki kwa namna ile. Mwanzo huu ulio halisi ulizingatiwa pamoja na dhabihu maalumu (Hes. 28:11-15) ambazo zilikuwa zinapigiwa baragumu (Hes. 10:10; Zab. 81:3). Hata kazi za kawaida zilikuwa hazifanywi.

 

Katika Mwaka Mpya wakati wa Mwandamo wa Mwezi ambao ni mwezi wake wa Kwanza, ambao ni wa Abibu kulikuwa na ishara maalumu (Zab. 81: 3-5; kama inavyoonyesha katika jarida la Mwandamo wa Mwezi na Mwaka Mpya [213]. Mwezi Mpya wa Mwezi wa Saba ulikuwa pia unatolewa dhabihu maalumu (Law. 23:24-25; Hes. 29:1-6).

 

2Wafalme 4:23 inasema kuwa mambo yote mawili yaani Mwezi Mpya na Sabato zilichukuliwa kama ni vitu vinavyotoa fursa katika kuwaomba ushauri manabii, na nabii Ezekieli anauelezea kwa kina Mwezi Mpya kama ni siku maalumu ya kufanya ibada (Eze. 46:1,3).

 

Zaburi 121:6, inasema kuwa mwezi ulikuwa unaweza kumuathiri mtu binasfi, pengine kutokana na kushirikishana na mawazo kama tujuavyo maana halisi ya neno jua na anga yaani lunacy.

 

[Yudea na Uzayuni wa kisasa unaingiza mambo haya]. Mwanzoni kabisa, Mwandamo wa Mwezi Mpya ulikuwa kwa hakika bado haujawekwa mahala pake kufuatana na hesabu za kufuata mambo ya nyota na anga, lakini ilikuwa haklika imetangazwa baada ya ushahidi wa kuhakikishwa kuwa mwezi umeisha andama. Mamlaka ya kirabi yalishikilia kuwa katika kila ssiku ya 30 ya kila mwezi, wanachama wa halmashauri ya Mahakama Kuu lilikusatana katika viwanja vya mahakama vya Yerusalemu, vilivyokuwa vinajulikana kwa jina la Beit Ya’azek, mahali walipokuwa wanakutanika ili kusikilizia ushuhuda wa mashahidi wawili waaminifu; na hatimaye waliitakasa Mwezi Mpya. iwapo kama mwezi huu mpevu wa mwandamo haujaonekana hadi kufikia siku hii ya 30, basi maadhimisho haya ya Mwezi Mpya yataadhimishwa pasipo shaka yoyote siku ya 31. ili kutoa taarifa kwa umati kuhusu mwandamo wa mwezi, kwa sababu walikuwa wanawasha katika Mlima wa Mizeituni na hatimaye kwa nchi nzima na kwa maeneo yote wanayoishi katika hali ya Utawanyiko

 

[Kisha ilisemekanakuwa] katika siku za mbele yake, hata hivyo, Wasamaria walianza kutumia nguzo kama hizi kwa kuwasha moto uliowashwa kwa makosa halmashauri ya Baraza Kuu ikatuma wajumbe kwa lengo la kutaka kuondolewa jamii hizo. Wayahudi wale waliokuwa wakiishi mbali na Yerusalemu walikuwa wanaiadhimisha katika kila siku ya 30 ya mwezi kuwa ni siku ya Mwezi Mpya. Katika mazingira ya namna hii walipokuwa wamearifiwa kuhusu uahirishwaji wa siku hii hadi kufikia siku ya 31, basi waliiadhimisha siku hii ya pili kama ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Mwezi Mpya (RH 1:3-2:7). Siku za katikati ya karne ya nne, ndipo wataalamu walianzisha kalenda ya kudumu na ndipo ukawa mwisho wa ile njia ya zamani ya kutumia matarishi wa kuzunguka ili kutoa matangazo ya Mwezi Mpya ikawa imekoma kabisa. Masalio ya matendo yale ya asili ya zamani ni, hata hivyo yaliendelea kufanywa kwenye taratibu za kwenye masinagogi za utangazaji wa mwonekano wa Mwezi Mpya katika siku ya Sabato iliyotangulia kabla ya siku ya kuonekana na siku ya kufanyia maadhimisho yake (kama inavyosema: Encyclopedia Judaica, vol. 12, p. 1039).

 

Ilifanyika kuwa kama mtindo katika matarajio ya elimu ya kijamii na masomo ya maendeleo ya mambo ya dini yaliyolenga kuhitimisha matakwa ya Kibiblia kuhusu Sabato hizi na miandamo ya Miezi Mipya kama ni mambo yaliyokuwa yanaenda sambamba kwa ajili ya utiifu wa watu kutoka katika jamii ya Kiebrania-Miandamo ya Mwezi Mpya ilichukuliwa kama ni masalio ya mawazo ya imani fulani zilizokuwa zinafanya ibada za kumuabadu mungu mwezi. Schauss pia alikuwa na mtazamo huu wakati alipoandika jarida liitwalo Sikukuu za Kiyahudi (p. 274). Pia alivichukulia vitabu vya Musa yaani Torati kama viliandikwa katika awamu mbili, awamu ya kwanza kabisa ni ile ya kale iliyoandikwa kabla ya utumwa wa Babeli, na ile ya pili ni ya baada ya utumwa wa Babeli wakiwa wamesharudi toka utumwani. Anadai kuwa awamu ya kwanza ya uandishi huu haigusii wala kuelezea habari za sikukuu. Anaweka madai yake kwa kuhitimisha na ukweli kuhusu kuwa Miandamo ya Miezi haikuelezewa katika maeneo kadhaa ya vitabu hivi kama vile Kutoka 23:14-19; 34:17-26; Kumbukumbu la Torati 16, wala katika Walawi 23. Kwa hiyo, anakiona kitabu cha Hesabu kuwa lazima kitakuwa kipo katika ile awamu ya mwisho ya uandishi. Aliendelea kusema kuwa hakukuwa na ushahidi wowote kuthibitisha mawazo au mtazamo huo. Huu ni mwanzo wa mabishano ya wanazuoni waliobobea katika kutetetea imani waliopo katika nyakati zetu hizi. Sababu ya kweli kwa sehemu kama hii ni kwamba kurudi kwao utumwani hakukuchangia kufanyika kwa marejesho yote.

 

Baada ya kurudi kwao kutoka katika Utumwa wa Babeli hali ya michanganyo ilifikiwa; Mwandamo wa Mwezi yaani Rosh Chodesh haikuhesabiwa kuwa ni siku ya kukuadhimishwa kikamilifu, wakati ambao kufanya kazi kulikuwa kumekatazwa, lakini dhabihu maalumu iliandaliwa kwa siku ile Hekaluni.

 

Katika siku hii Wayahudi walikuwa wanafanya utaratibu fulani maalumu ili kuukaribisha mwezi mpya: kulikuwa na maombi maalumu kufanyika kwenye sinagogi siku ya Sabato inayotangulia Mwandamo wa Mwezi, na kulikuwa na maadhimisho ya kuutakasa Mwezi Mpya yaliyo fanyika kwa namna ya kutoa baraka maalumu yaliyokuwa yanafanyika kwa njia ya uimbaji katika viwanja vya wazi wakati Mwezi Mpya ulipokuwa unaandama (kwa mujibu wa: Schauss, p.274).

 

Baadae ilikuja kuchukuliwa katika hali isiyo na umakini kwa kufuatiwa hali iliyojitokeza ya kupunguzwa kwa ile maana, ikatokea kwamba hata fafanuzi za mambo haya zilikuwa hazitolewi kikamilifu. Mfano ni huu unaoonekana katika rejea ifuatayo kutoka katika jarida lijulikanalo kama Dhana ya Kiebrania kuhusu Majira na Umuhimu wake katika Maendeleo ya Sabato, lililoandikwa na Diana R. Angel, katika Chuo Kikuu cha Huko Marekani kiitwacho The American University, Washington, 1976.

 

Inayosema: hakuna aina yoyote ya biashara iliyofanyika katika siku ya mwandamo wa mwezi mpya (katika siku iliyofuatia siku ya kwanza ya kuandama kwa mwezi mpevu unavyochomoza mawinguni). Sadaka iliyokuwa inatolewa katika ibada za mwandamo wa mwezi mpya kwa kweli zilizidi kiwango chake kwa zile zilizokuwa zinatolewa katika ibada za siku ya Sabato (Hes. 28:11-5; Eze. 46:4-7). Hata hivyo, umuhimu wa kidini kuhusu mwandamo wa mwezi ulianza kupungua wakati ambapo ule wa Sabato ulizidi kupata nguvu na kutiliwa maanani (pp. 69-70).

 

Mifano zaidi kuhusiana na upunguaji huu wa taratibu taratibu unaonekana katika jarida la mwanazuoni mmoja aitwaye Widoger. Linalosema:

Bado haieleweki vema kuhusu ni lini au ni kwa namna gani Mwandamo wa Mwezi ulipoteza taratibu zake za maadhimisho. Hali hii ilitokea wakati ule Wayahudi waliporudi kutoka katika utumwa wa Babeli mwishoni mwa karne ya sita KK. Ikaanza kuwa sio miongoni tena mwa siku za mapumziko kamili, lakini wakaifanya kuwa ni siku ya mapumziko ya nusu-siku, kama ilivyo ile Hol ha-Mo’ed (yaani zile siku zilizo katikati ya siku ya Pasaka waliyoadhimisha Israeli Misri hadi kufika kwao sehemu inayoitwa Sukoti ambazo ziliruhusiwa kufanya kazi) wakati marabi walipo kataza aina zote za kazi muhimu na wanawake walipaswa kupumzika kufanya kazi zao za ususi na ufumaji. Kukawepo na ushurutishaji ili kukithi haja masharti ya kiuchumi kunawezekana ikawa pengine ndio sababu iliyowafikisha kwenye hali hii ya kushushia hadhi maadhimisho haya ya Mwandamo wa Mwezi, na hasa kwa vile walivyokuwa hakuna sababu za kidini au za kihistoria kwa kusimamisha kufanyika kwa kazi katika siku hizo. Na kwa ajili ya muda, vilevile hata kwa wakati ule taratibu hizi za mapumziko magodo zilipo ondolewa na kufanywa kuwa ni siku za kawaida tu za kufanya kazi kama zilivyo kwa siku nyingine zozote, isipokuwa kwa ajili ya mabadiliko Fulani Fulani ya kiliturujia (kama asemavyo: Widoger, op. cit, p. 502).

 

Tena watu wa jamii ya Wayahudi waliadhimisha Miandamo ya Mwezi kama ilivyofanywa na Kanisa. Katika uwingi wao wote hata hivyo walipatwa na msituko na kuziona shughuli za biashara wakizifanya kama walivyofanya kwa siku za Sabato na kwa siku za sikukuu kama tunavyojua.

 

Ndiposa inaposema: “…, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na Sabato nayo, tupate kuandika ngano?…” (Amosi 8:5).

 

Kwa Wayahudi, Sabato ilikuwa ni siku muhimu sana katika mwaka. Kwa kweli, mwandishi wa majarida na mwanazuoni Diana Engel anaitaja siku ya Sabato kwa sababu:

Iliadhimishwa zaidi kuliko siku nyingine yeyote au amri nyingine yeyote ile. Ilwekewa mkazo kwao zaidi kabisa ya kiwango kile walivyoamini au kusimamia kwayo. …ilikuwa haiwezekani kusisitiza zaidi ni kwa kiasi gani Sabato ilivyokuwa na maana kwa Israeli, au ni kwa jinsi gani walivyokuwa wanaiona na jinsi walivyokuwa wanaitukuza. (p. 83).

 

Lakini kwa hakika hawakuielewa! Hawakuelewa maana yake ya kiroho kuhusu Sabato ni sawa na walivyoshindwa kuelewa Miandamo ya Mwezi Mpya. MIANDAMO YA MWEZI MPYA ILIBIDI IPUNGUZWE KATIKA UMUHIMU WAKE NA KANUNI ZA KIRABI ZA KIDINI YA KIYAHUDI KWA SABABU ILITISHIA AHIRISHO LA MFUMO WAKE YENYEWE. Isingeweza kuondolewa moja kwa moja kwavile Biblia imeweka wazi sana katika kufundisha jambo hili na kwa hiyo, ilibidi ipunguzwe tu ule umuhimu wake ili kwamba kalenda ya uwongo iweze kuanza kufundishwa na watu waanze kuitumia. Hii yote ilifanyika baada ya kuangushwa kwa Hekalu.

 

Kwa mujibu wa kijarida kiitwacho The Lion Handbook of the Bible (eds. D & P Alexander, Lion Publishing, 1984) inasema:

 

“Kalenda ya Wayahudi wenye imani au msimamo mkali ina miezi kumi na miwili inayoanzia katika kila mwandamo wa mwezi mpya (mwandamo ulodhahiri)” (p.112).

 

Hakuna ushahidi uliotajwa katika katika usemi huu (mwezi mpevu uliodhahiri). Wazayuni waliowengi, na inaonekana pia kwa wanazuoni walio wengi waliokuwa katika karne ya ishirini, tofauti kabisa na ushahidi tulionao na kwa matendo yao na hisia zitokanazo na akili yao timamu, huuchukulia Muandamo wa Mwezi Mpya kama ni mwezi mpevu. Hii siyo kabisa kitu muhimu. Kalenda ya Wasamaria, ambayo bado inaendelea kuwepo hadi leo, hushuhudia hili kuwa ni jambo la uwongo.

 

“Neno hili la pili kutoka katika Lugha ya Kiebrania yaani hodesh, kwa maana halisi na nyingine ni ‘upya’ wa mwezi mpevu” (utaona haya ukisoma Encyclopedia Britanica., 15th edition, Vol. 15, p. 465).

 

Neno chodesh haliwezi kuwa na jambo lolote la kufanya na mwezi mpevu. Mwezi mpevu ni aina nyingine ya mfumo wa ibada ambayo ilikuwa inafanywa na kuelekezwa kwa mungu aliyejulikana kama mungu Sin au dhambi na Baali ambaye pia alijulikana kama Ashtoreth ukiwa ni mfumo wa kiibada na uliokuwa unahitaji kuweko na dhabihu ya mwanadamu (waweza kujifunza hayo ukisoma majarida ya Ndama wa Dhahabu [222] na Chanzo cha Christmas na Easter [235]. Msingi wake wenye tafsiri mbalimbali una maana ya kufichika. Jarida la Britanica linaendelea kwa kusema tamko hili (ambalo ni nusu tu iliyo kweli), ambalo ni kinyume kabisa na dhana za Kiebrania linaendelezwa katika maneno ya ki-mfano.

 

Hapa inasema: “Katika kalenda ya kidini, mwanzo wa kila mwezi ulikuwa unaamuliwa kwa kuadhimishwa kwa mwandamo wa mwezi mpevu, na siku ya Pasaka ilikuwa inafungamanishwa na uvunaji wa shayiri” (sawa na isemavyo hapo juu).

 

“…mwandamo wa mwezi mpevu kwa hiyo ni kuzaliwa upya au uingizwaji wa ule wa kale kwa mwezi mpya (sawa na hapo juu., p. 573)”

 

yapata kama mwaka 344BK na wakati Fulani katika kalenda ya iliyojulikana kama ya Hillel yapata mwaka 358, maadhimisho yaliyokuwa dhahiri ya Mwezi Mpya yalichukua mahali na mahesabu ya kisiri ya kufuata sayari zilizo angani. Meza za kisasa zinatoa hakikisho la kuweka mbadala halisi na mkamilifu.

 

“Kalenda ya (Kiyahudi) ni ile yenye mfungamano na katika hali inayo jitegemea ya Mwandamo wa Mwezi Mpya wa kweli. (Encyclopedia Britanica, opp. Cit., p. 466).

 

Sababu ya kweli ni hii kwamba Wayahudi ilibidi waelekeze maadhimisho hadi watakapopata mfumo mpya wa upangaji wa mahesabu (soma jarida za Kalenda ya Mungu [156] na Mwezi na Mwaka Mpya [213]).

 

Nafasi ya Kibiblia

Sikukuu ya Mwandamo wa Mwezi Mpya ni miongoni mwa sikukuu muhimu za Bwana. Imeorodhehwa katika kitabu cha Hesabu 10:10

 

Hesabu 10:10 inavyosema: Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizo amriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

 

Dhabihu zote zilitimilizwa katika Kristo. Sikukuu au Sabato hizi zenyewe hazikuondolewa.

 

Dhabihu zilizohitajika zilibadilishwa kutoka katika umuhimu wake na hadi kwa dhabihu ya kiroho kwa kila siku kwa mwandamano wa Siku Takatifu, kutoka kwenye Sabato hizi hadi sikukuu za Miandamo ya Mwezi Mpya. Dhabihu kwa mujibu wa Sheria ilikuwa inatolewa kwa njia ya machangizo maalumu iliyoko chini ya mwajibiko kwa mamlaka ya taifa. Mchango wa Mwana wa Mfalme imefafanuliwa katika jarida lisemalo Namna ya Kutoa Zaka [161].

 

Ezekieli 45:14-17 inasema 14 na sehemu ya mafuta iliyoamriwa, katika bathi ya mafuta, ilikuwa sehemu ya kumi ya bathi katika kozi moja, ambayo ni bathi kumi, yaani homeri; maana bathi kumi ni homeri moja; 15 na mwana kondoo mmoja wa kundi katika mia mbili, katika malisho ya Israeli yenye maji kwa sadaka ya unga, na kwa sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka ya amani, ili kuwafanyia upatanisho, asema BWANA MUNGU. 16 Watu wote wa nchi watatoa toleo hili kwa ajili ya mkuu katika Israeli. 17 Tena itakuwa kazi ya mkuu kutoa hizo sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na sadaka za vinywaji, katika sikukuu na katika mwezi mpya, na katika Sabato, katika sikukuu zote za nyumba ya Israeli zilizo amriwa, atatengeneza sadaka ya dhambi, na sadaka ya unga, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaska za amani, ili kufanya upatanisho kwa nyumba ya Israeli.

 

Dhabihu ilikuwa ni zaka za mafuta na nusu ya zaka ya zaka kwa ajili ya dhabihu ya nyama. Hii ilikusanywa na mwana wa mfalme kwa ajili ya utoaji wa dhabihu kwa siku za Sabato, Miandamo ya Mwezi Mpya, Siku Takatifu na dhabihu. Kwa hiyo, nikusema kuwa sio sahihi kusema kwamba zaka ilikomeshwa na dhabihu kwa sababu ni dhahiri kuwa zilikuwa zinatolewa ki pekee pekee. Maandiko haya vilevile linahusika na malimbuko kutoka katika Ezekieli 44:29-30 na kwa wengine wengi wanaofanyika kwa ajili ya marejesho ya Israeli katika nchi yao. Masihi kwa hiyo atakuja kuweka tena mfumo ambao kwamba unadhaniwa kuwa umeishafanyika tayari kutokana na kusulibiwa kwake kama wengi wanavyo dhani, na maandiko matakatifu hayawezi kutanguka. Hii itakuwa ni kwa ajili ya uponyaji wa kiakili wa mataifa, lakini jambo hili litaamuliwa kwa namna ya kipekee.

 

Sikukuu ya Mwandamo wa Mwezi ilikuwa inachukuliwa kama Sabatown au Sabato Takatifu. Dhabihu zilitolewa, kama tulivyoona hapo juu, kama kumbukumbu.

 

Hesabu 28:11-15 inasema: 11 Tena katika mwanzo wa miezi yenu mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba; 12 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng’ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kama sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja; 13 na sehemu ya kumi moja ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa sadaka ya unga kwa kila mwana kondoo kuwa sadaka ya kuteketezwa ya harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. 14 Tena sadaka zake za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng’ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo mume, na robo ya hini kwa mwana kondoo; na ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka. 15 Tena mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka yakuteketezwa ya siku zote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

 

Tumeona katika maandiko haya matakatifu kwamba Miandamo ya Mwezi Mpya ilikuwa ni budi iwe katika kila mwezi kuelekea katika miaka yote ya mwaka. Ni kwa umuhimu huohuo unafanyika katika Mwandamo wa Mwezi Mpya kama inavyofanyika kwa sikukuu nyingine na Sabato zake.

 

1Nyakati 23:31 insema: 31 na kumtolea BWANA sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za Sabato, za mwezi mpya, na za sikukuu zilizo agizwa, kwa hesabu kadiri ya agizo lake, daima mbele za BWANA.

 

Tunaona hapa kuwa Miandamo ya Mwezi Mpya kwa kweli inaingiliana katikati ya Sabato na Sikukuu hizi. kama ilivyo kwa Sikukuu na Sabatoe hizi, zinafungamana kati ya dhabihu na Miandamo ya Mwezi Mpya ilitimilika ndani yake Masihi, hatahivyo, adhimisho lenyewe la miezi halikukomeshwa.

 

Adhimisho hili halikuhitaji kutafsiriwa ua kufananishwa na ibada za muabudu mwezi, ambazo kabisa hakika zimekatazwa.

 

Kumbu kumbu la Torati 4:19 inasema: 19 tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishiwa na kuviabudu na kuvitumikia, ambvyo BWANA, Mungu wako, amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.

 

Kumbukumbu la Torati 17:3 inasema:3naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyovyote, nisivyoagiza mimi,

 

Tendo la kuadhimisha Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya pamoja na uwekaji wa sikukuu kumetolewa ili kuweka alama ya Mpango wa Mungu na katika mtiririko wa mzunguko wa uumbaji. Kalenda ya jua hauwezi kufanya utendaji kazi huu.

 

Kuanzia marejesho ya Pasaka katika siku za Mfalme Hezekia baada ya Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu, Hezekia alifanya marejesho ya siku za Miandamo ya Mwezi Mpya sambamba na sikukuu. Hakuna marejesho yatakayokamilika hadi pale Miandamo ya Mwezi Mpya yamerejeshwa kisahihi sana katika mahali pa haki yake katika mfumo (tazama jarida lisemalo Jaribuni Kila Jambo, Kanisa la Mungu, katika Kweli, Vol.2, Issue 1,p.6).

 

2Nyakati 31:3 inasema 3 Tena akaweka sehemu ya mfalme ya mali zake kwa sadaka za kuteketezwa, yaani, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa za Sabato, na za mwezi mpya, na sikukuu, kama ilivyoandikwa katika torati ya BWANA.

 

Tunaona pia katika Ezra 3:5 ikielezea kuwa maadhimisho ya Miandamo ya Mwezi Mpya yalirejeshwa na Ezra. Kwa hiyo basi marejesho yote mawili makuu yalihusishwa na marejesho ya Miandamo ya Mwezi Mpya.

 

Ezra 3:5 inasema: 5 na baadae sadaka ya kuteketezwa ya daima, na ya mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za BWANA, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliyemtolea BWANA sadaka kwa hiari yake. 

 

Miandamo ya Mwezi Mpya ndio mwanzo wa au ni siku ya kwanza ya mwezi (Hes. 10:10; 28:11). Hakuna mfumo unaojitegemea wenyewe katika kuwekwa tena katika mwanzo wa mwezi ulioko bado. Kalenda ya Hillel imeondoshwa na haipo kwa sababu ya ukweli huu.

 

Kalenda inayotegemea mzunguko wa jua ni alama ya Watu Watakatifu. Katika nukuu hii katika Kutoka 12:2, mwana zuoni aitwae Mekilta anasema kuwa “mataifa” hutambulikana kwa jua, lakini Israeli kwa mwezi.

 

Sikukuu za PASAKA na VIBANDA hazikuwekwa kwa ajili tu ya kufayia mahesabu ya jumla ya mzunguko wa jua, lakini ni kwa kutegemea mwandamo wa mwezi mpya wa mwezi ambao ilitokana kwayo. Sikukuu ya PENTEKOSTE ilitegemeana na adhimisho la Pasaka kwa heshima yake…. Ingawa haiwezekani kuweka ukumbusho kamili. Bali inaonekana kuwa huenda ikawa hapo mwanzo Sabato ilikuwa ni sehemu ya mzunguko huu wa asili wa majira, ikihusisha na majira ya mwezi, na kwamba, kufuatana na mtenganisho wa Sikukuu Miandamo ya Mwezi Mpya kuliendelezwa kama maadhimisho yaliyo tenganishwa, hii ni kwa mujibu wa kamusi ya (The Interpreter’s Dictionary of the Bible, vol. 3, article New Moon, p. 544)

 

Makisio kuhusu Sabato na Miandamo ya Mwezi ni pengine imetegemea katika mfumo wa maadhimisho tunayoyaona katika jarida la Kazi za Aya zihusuzo Sheria-au-MMT [104]. Ambayo wana zuoni maarufu Strugnell na Qimron wametafsiri kutoka katika jarida la DDS (tazama Bib. Arch. Review, Nov-Dec, 19994). Kanuni zote za kihistoria za Kiyahudi zinazohusu utangazaji wa Miandamo ya Mwezi kutoka siku ya Sabato inayotangulia ilijumlisha na mafundisho ya elimu ya unabii wa siku za mwisho. Asili ya maadhimisho ya uumbaji wa Mungu wa mwezi kama “ishara” ya agano lisilovunjika kwa Israeli, “wakati” ambao mcultus unakuwa umevalishwa (Zab. 104:19; Mhu. 43:6-8. (sawa na ilivyo tafsiriwa katika International Dictionary, angalia pia katika Ber. R. 13d). Kwa  hiyo kalenda ni sehemu isiyoweza kutenganishwa katika agano lake na Israeli.

 

Mwandamo wa Mwezi Mpya ulichukuliwa kama ni ishara ya utoaji wa maono na unabii, huenda ni kutokana na 2Wafalme 4:23 lakini kiuhakika sana ni katika Ezekieli 26:1; 29:17; 31:1; 32:1; sawa na Isaya 47:13, Hagai 1:1). Hii ni moja kwa moja inakanusha mawazo ya wataalamu wa mambo ya nyota na wanajimu wa mfumo wa Kibabeli kama tunavyoweza kuona katika Isaya 47:13.

 

Isaya 47:13 inasema: 13 Umechoka kwa wingi wa mashauri yako, basi, na wasimame hao wachukuao fataki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayo kupata.

 

Matabiri ya kila mwezi yalikuwa yanafanyika kwa kuzingatia awamu za kila mwandamo wa mwezi, hivyo ikawa imegeuza mfumo mzima

 

Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya yote mawili kwa pamoja yaliingizwa katika mapumziko ya kutofanya kazi kama vile tuonavyo katika kitabu cha Amosi 8:5. Ni siku ya kufurahia. Furaha na vicheko zilizokusudiwa kwa ajili ya Siku Takatifu ziliondolewa kama isemavyo Amosi 2:11.

 

Hosea 2:11 inasema: 11 Tena nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na Sabato zake, na makusaniko yake yote yaliyoamriwa.

 

Hii ilikuwa ni kwa sababu ya kutokuwa waaminifu na kushika ibada za sanamu. Mungu huwaadhibu watu wake kwa ajili ya hawazishiki Sheria zake. Matokeo yake ya mwisho ni kwamba, aliharibu utajiri wa taifa.

 

Hosea 2:12 inasema: 12 Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila.

 

Saumu ya kufunga na kuomboleza zisimamishwa katika siku za Miandamo ya Mwezi Mpya. Sote tunajua ya kwamba kupitia Israeli hadi kufikia kipindi kile cha Masihi kwa mujibu ya vitabu vya Apocrypha ukisoma kitabu cha (Yudithi 8:6). Sherehe na tafrija zilipigiwa mbiu na baragumu (Hes. 10:10; Zab. 81:3).

 

Zaburi 81:3 inasema: 3 Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.

 

Mwandamo wa Mwezi Mpya wenye kuashiria miezi ni hasa kwa mahususi iliadhimishwa kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

 

1Samweli 20:6 inasema: 6 Baba yako akiona ya kuwa sipo, basi sema, Daudi alitaka sana nimpe ruhusa, aende upesi Bethlehemu, mji wake, kwa maana iko huko dhabihu ya mwaka kwa ajili ya jamaa yake yote

 

Mwandamo wa Mwezi Mpya wa Nisani ulikuwa ni ishara dhahiri na Mwandamo wa Mwezi wa Tisrhi kwa kadiri ulivyo wanyewe tu ni Sikukuu ya Kupiga Baragumu (tazama pia jarida la Kupiga Baragumu [136].

 

Ezekieli 45:18-20 inasema: 18 Bwana MUNGU asema hivi, Mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utatwaa ng’ombe mchanga mume mkamilifu; nawe utapatakasa mahali patakatifu. 19 Na kuhani atatwaa baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi, na kuitia juu ya miimo ya milango ya nyumba, na juu ya pembe nne za daraja ya madhabahu, na juu ya miimo ya lango la ua wa ndani. 20 Nawe utafanya vivyo hivyo katika mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, kwa ajili ya kila mtu akosaye, na kwa ajili ya mtu aliye mjinga, ndivyo mtakavyoifanyia nyumba upatanisho.

 

Usafishaji au utakaso wa mahali patakatifu kulitanguliwa na Mwandamo wa Mwezi Mpya wa Mwezi wa Kwanza (Nisani) mwanzo wa mwaka mtakatifu (sawa na lisemavyo jarida la Utakaso wa Hekalu la Mungu [241]. Hii ilihusu pia utakaso wa Uwa wa ndani. Hii ilikuwa inawakilisha wateule kama lile gurudumu la Ndani lililonenwa katika maono ya nabii Ezekieli. Utakaso wa maovu na makosa ilifanywa kuwa ni kitu muhimu kufanyika katika siku ya saba ya Mwezi wa Kwanza yaani mwezi wa Nisani. Makuhani walikuwa wamejitayarisha wenyewe na taifa zima.

 

Mwandamo wa Mwezi Mpya wa Mwezi wa Saba ulikuwa pia ni wa muhimu sana.

 

Walawi 23:24 inasema: 24 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, kutakuwa na kutaniko takatifu.

 

Nehemia 8:2 inasema: 2 Naye Ezra, kuhani, akaileta torati mbele ya kusanyiko, la wanaume na wanawake, na wale walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza ya mwezi wa saba.

 

Kwa hiyo, Mwandamo wa Mwezi wa Saba ilianzia kwa marejesho ya kupitia usomaji wa sheria ambao ulitokea na kufanyika kwa kila mwaka wa saba wa mzunguko wa Yubile katika kipindi chote cha kutaniko la Sikukuu ya Vibanda (sawa kama lisemavyo jarida la Usomaji wa Sheria za BWANA kwa Ezra na Nehemia [250].

 

Kumbukumbu la Torati 31:10-12 inasema: 10 Musa, akawaamuru, akisema, Mwisho wa kila mwaka wa saba, wakati wa maachilio, wakati ulioamriwa na sikukuu ya vibanda, 11 Israeli wote wafikapo ili kuonekana mbele za BWANA, Mungu wako, mahali pale atakapopachagua, aisome torati hii mbele ya Israeli wote masikioni mwao. 12 Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako, wapate kusikia na kujifunza kumcha BWANA, Mungu wenu, siku zote atakazo kaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki.

 

Nehemia 8:18 inasema: 18 Tena siku baada ya siku, tangu siku ya kwanza hata siku ya mwisho, akasoma katika torati ya MUNGU. Wakafanya sikukuu muda wa siku saba; na siku ya nane palikuwa na kusaniko la makini, kama ilivyoagizwa.

 

Ishara ya mfano hapa ni kwamba mwaka wa saba au mwaka wa Sabato hapa unawakilisha mzunguko wa milenia wa miaka elfu moja, ambao unaanzia na tendo la kurudi kwa Masihi, ambaye ataamuru Sheria kutoka Yerusalemu. Sheria hizi hatimaye zitaenea ulimwenguni kote zikiyatiisha mataifa. Tendo la kusoma hizi sheria wakati wa Sukukuu ya Baragumu, wakati wa matengenezo ya Nehemia, ilikuwa inaelekezea kinabii marejesho yatakayo ya Masihi na kutokana na sikukuu ya Baragumu (sawa na lisemavyo jarida la Mlolongo wa Ratiba ya Kila Nyakati [272].

 

Kutoka katika jangwa la utawanyiko Mungu kwa hiyo atashughulika na taifa la Israeli na kulirejeza. Wateule wa Kristo ni sehemu hii ya Israeli na watashughulikiwa na pamija na taifa hili.

 

Hosea 2:14-23 inasema: 14 Kwa hiyo angalia, mimi nitamshawishi, na kumleta nyikani, na kusema naye maneno ya kumtuliza moyo. 15 Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile aliyopanda kutoka nchi ya Misri. 16 Tena siku hiyo itakuwa, asema BWANA, utaniita Ishi, wala hutaniita tena Baali. 17 Kwa maana nitayaondoa majina ya Mabaali kinywani mwake, wala hawatatajwa tena kwa majina yao. 18 Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege wa angani, tena na wadudu wa nchi, nami nitavivunja upinde na upanga vitoke katika nchi, nami nitawalalisha salama salimini. 19 Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema. 20 Nami nitakuposa kwa uaminifu; nawe utamjua BWANA. 21 Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema BWANA; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi; 22 nayo nchi itaiitikia nafaka na divai na mafuta; nayo yataiitikia Yezreeli. 23 Nami nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeye asiyepewa rehema; nami nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, Ninyi ndinyi watu wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu wangu.

 

Upandikizwaji wa taifa hapa ni kama mzabibu wa Bwana, ambao ni taifa lote zima la Israeli (Isa. 5:7). Rehema ya Mungu ni marejesho chini ya Masihi kwa namna zote mbili yaani kupitia Roho Mtakatifu na kwa Milenia.

 

Ushahidi upo kuonyesha kuwa Miandamo ya Mwezi Mpya ilikuwa inaadhimishwa katika Makanisa ya Kikristo katika aina zote mbili za makanisa yaani kwa yale yaliyokuwa chini ya uangalizi wa mitume na kwa yale yaliyokuwa katika mataifa ya utawanyiko. Kuhusu utaratibu iliotumika katika kuadhimisha sio jambo la kuliwekea hukumu.

 

Wakolosai 2:16-17 inasema: 16 Basi mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au Sabato; 17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

 

Kanisa liliendelea kuadhimisha siku hizi likiwa katika hali ya utawanyiko na pia waliendelea bado kuadhimisha katika Ulaya katika miaka ya karne ya kumi na saba (tazama jarida lisemalo Mgawnyiko wa Jumla wa Makanisa Yanayoshika Sabato [122] na lile la Wasabato katika Transylvania lililo andikwa na Samueli Kohn (1894), (ambalo tafsiri yake ya Kiingereza imechapishwa na mtambo wa uchapishaji uitwao CCG Publishing, 1998). Miandamo ya Mwezi Mpya ilikuwa inaamuliwa kwa maadhimisho halisi hadi kufikia wakati wa kalenda ya Hillel yapata kama mwaka 358 BK. Baada ya kuangamia kwa Hekalu, ilikuwa ni kazi ya Baraza Kuu Tukufu la Marabi lililokuwa linapanga siku. Usomaji mahsusi wa sheria za Musa yaani Torati kwa siku kama ilivyo andikwa katika Hesabu 28:1-15 na Zaburi 104 pia ilisomwa. Kalenda ya Hillel pia ilikuwa inaimbwa ili kuashiria sikukuu hizi. Kuanzia katika karne ya kumi na sita, siku iliyokuwa inatangulia Mwandamo wa Mwezi Mpya ilikuwa ni siku ya kufunga kwa Wayahudi ambayo waliipa jina la yom kippur (sawa na ilivyo katika Interp. Dict.). Hakuna shaka yoyote kwamba tukiona Mwandamo wa Mwezi bado unaendelea kuadhimishwa, na wana wa Yuda wanajua kuwa bado inatakiwa kuadhimishwa hadi leo. Hata hivyo, hakuna vizuizi vya kibiblia vinavyoweka sharti za kufunga kwa namna yoyote ile.

 

Kuahirishwa kwa kalenda ya Hillel na utaratibu huu wa kufunga katika kila siku ya kwanza, kunatupa hakika kuwa ni hakika Yuda bado wanaendelea katika siku ya Mwandamo wa Mwezi Mpya jambo ambalo lilikatazwa wakati wa zama ya hududma za Hekaluni.

 

Marejesho ya mwisho kabisa yatafanywa na kukamilishwa na Masihi wakati wa kurudi kwake, kama tunavyoona katika kitabu cha Isaya 66:20-23. Israeli wote watarejeshwa na kurudishwa kutoka katika mataifa waliko wakati wa marejeo ya msafara wa mwisho utakao fanana na ule wa Kutoka kwao utumwani Misri wakati wa kurudi kwake Masihi.

 

Isaya 66:20-23 inasema: 20 Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi. 21 Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na walawi, asema BWANA. 22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyo kaa. 23 Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.

 

Marejesho haya ya Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya yatafuatana na kurejeshwa tena kwa Sikukuu zote.

Zekaria 14:16-19 inasema: 16 Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Yerusalemu, watakwea mwaka baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme, BWANA wa majeshi, na kuishika sikukuu ya Vibanda. 17 Tena itakuwa, ya kwamba mtu awayeyote wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, BWANA wa majeshi,mvua haitanyesha kwao. 18 Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitakunya kwao; itakuwa tauni, ambayo BWANA atawapiga mataifa, wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda. 19 Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya mataifa yote, wasiokwea ili kushika sikukuu za Vibanda.

 

Kwa hiyo basi, hakutakuwepo na marejesho yaliyo makamilifu hadi pale Miandamo ya Mwezi itakaporejeshwa pamoja na sikukuu hizi. Katika jamii hii ya kisasa ambayo inaweza kuwa ni vigumu sana kabisa. Na hii ndio maana mfumo huu wa dunia utararuliwa mbali kwanza na Masihi atakapo rudi. Mataifa yatarejeshwa tena kwa Sheria itakayotolewa  kuanzia Yerusalemu.

 

Miandamo ya Mwezi hi ya muhimu kwa ustawi wa mwanadamu. Imechukuliwa pahala pale na ile inayoitwa kalenda ya mfumo wa dunia kwa kufuatana na siku ya kipagani ya kutolewa dhabihu. Katika nchi ya Marekani (USA), kalenda hii ya kidunia inabeba sikukuu zake kuu zilizochukuliwa kulingana na siku zinazo endana na matukio ya zamani ya kipagani. Jambo hili linabidi pia lisidharauliwe.

 

Siku za Sabato na Miandamo ya Mwezi ziliadhimishwa kwa namna moja ileile hasa kufuatana na masuala ya kazi na shughuli mbalimbali. Mwenendo wa jinsi ya kufanya katika ufanyaji wa biashara yaani kuuza na kununua ilikuwa imakatazwa kabisa na ndivyo ilivyo pia hata kwa siku zetu hizi kwa maadhimisho ya yote mawili yaani Miandamo ya Mwezi na kwa siku za Sabato.

Amosi 8:4-6 inasema: 4 Lisikieni hili, ninyi mnaopenda kuwameza wahitaji, na kuwakomesha maskini wa nchi, 5 mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na Sabato nayo, tupate kuandika ngano? Mkiipunguza efa na kuiongeza shekeli, mkidanganya watu kwa mizani ya udanganyifu; 6 tupate kuwanunua maskini kwa fedha, na wahitaji kwa jozi ya viatu, na kuziuza takataka za ngano.

 

Hali ya kuweka mkazio wa marufuku hizi ni jambo lililo nyeti sana kwa Israeli wa siku zetu. Hata hivyo, kwa kweli hakuruhusiwi na hakuwa uwezekano wowote wenye kujenga udhuru kiasi cha kutoa uwezekano wa kutenganisha Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya, zaidi kuliko kwa sikukuu kwa njia ya kutofautisha na Amri Kumi za Mungu kama Sabatown.

 

Hata hivyo, zote inabidi ziadhimishwe. Hakuna marejesho yaliyo weza kufanyika au yatakayo weza kufanyika kikamilifu hadi pale Miandamo ya Mwezi itakapoweza kurejeshwa.

 

Nabii Amosi anaenda ndani umbali wa kwamba anatangaza hukumu juu ya Israeli kwa kushindwa kwao kuzishika Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya kisahihi na katika ukamilifu wake.

 

Amosi 8:8-12 inasema: 8 Kwa ajili ya hayo, je! Haitatetemeka nchi, na kuomboleza kila mtu akaaye ndani yake? Naam, itainuka yote pia kama huo Mto; nayo itataabika na kupwa tena kama Mto wa Misri. 9 Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifnya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana. 10 Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upaa katika kila kichwa; nami nitafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu. 11 Angalia siku zinakuja asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu cha kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya BWANA. 12 Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la BWANA, wasilione.

 

Hukumu yenye kupatiliza moja kwa moja kwa ajili ya kudharau kutii neno la Mungu ni kwamba kile tulichonacho kitaondolewa. Janga la njaa litaikumba dunia kama hukumu kwa ajili ya kutotii huku. Kuzitia unajisi Sabato na Miandamo ya Mwezi kwa njia ya kufanya matembezi na kuendekeza kufanya biashara katika hali ya kujificha na kukosa uaminifu katika kuvunja Sheria ni sababu ya kwanza ambayo ni kosa kubwa. Nyumba ya yakobo iliadhibiwa kwa kutawanywa kwa mataifa kwa ajili ya machukizo haya ingawa walishika na kujitahidi wasipoteze hata punje ya ngano katika ungo.

 

Amosi 9:8-15 inasema: 8 Angalieni macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia; lakini sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo, asema BWANA. 9 Kwa maana, angalieni, nitatoa amri, nami nitaipepeta nyumba ya Israeli katika mataifa yote, kama vile ngano ipepetwavyo katika ungo, lakini hata chembe moja iliyo ndogo haita anguka chini. 10 Wenye dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, Mabaya hayatatupata nyuma wala mbele.

 

Inabidi iangaliwe kuwa wana wa Israeli, wanaosema kuwa maovu hayatawapiga kikumbo, wataangamia. Kipindi hiki ni cha mwisho kama ilivyo kwa siku za mwisho inavyojulikana kama ni Siku ya Bwana. Shughuli na matendo haya yatatangulia mara moja kabla ya marejesho ya Kimasihi. Marejesho haya yatafuatiwa na maangamizo makuu ya ulimwengu wa vita, ambayo tunaitarajia kutokea, kuukumba ulimwengu kwa maafa makuu yaani ya matumizi ya nguvu za kisasa za nyukilia kwa ajili ya kipindi cha Vita vikuu vya Tatu vya Dunia.

 

Mistari ya 11-15 inasema: 11 Siku hiyo nitaiinua tena nyumba ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale; 12 wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote yaitwayo kwa jina langu, asema BWANA, afanyaye hayo. 13 Angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondosha divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka. 14 Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; watafanyia bustani, na kula matunda yake. 15 Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang’olewa tena watoke katika nchi yao niliyowapa, asema BWANA, Mungu wako.

 

Lakini hali hii ya hatari inaweza kuepukika kwa kupitia kuzingatia Mpango wa Mungu kwa njia ya toba. Miandamo ya Mwezi Mpya ni nfano kwa mfumo huo, ambao kwa pamoja na Sabato na sikukuu zinatoa maelekezo ya mpango wa Mungu ulivyo.

 

 

 

 

 

 

 

q