Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[126]
Daudi
na Goliathi
(Toleo La 2.0 19950715-20000226)
Jarida hili
linahusiana na hadithi ya Daudi na Goliathi na mwendelezo wa maana kusudiwa ya
kiroho na kinabii ya harakati zinazohusiana na mazingirwa ya mgogoro huu.
Kuelewa kiini na fundisho kuu la hadithi kwa ukaribu kunahusiana unaokusudia
kwa ukaribu na ushindi wa Masihi dhidi ya utawala na imani za kidunia. Historia ya huko nyuma ya Wafilisti
kuikalia Nchi Takatifu imetolewa pia. Kuanza kuikalia kwa Waisraeli kwenye nchi
ya Kanaani kumeelezewa pia amoja na maelezo ya kina ya hadithi ya kuondolewa
kwa Sanduku la Agano pia kumeelezewa ili kujenga vita na kuanzishwa kwa ufalme.
Kuanzishwa kwa mstari wa uzao wa Daudi ni matokeo ya mwisho ya harakati hizi.
Christian Churches of God
Email: secretary@ccg.org
(Hatimiliki © 1995, 2000 Wade Cox)
(tr. 2016)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na
tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote
atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja
ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki..
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Daudi na Goliathi
Watu wengi wanaijua
hadithi ya Daudi na Goliath. Ni mojawapo kati ya hadithi kuu ya mara kwa mara
na zinazoheshimika sana kwenye Biblia na mara nyingi inasimuliwa ili kufundisha
jinsi mtu dhaifu, lakini aliye jasiri anavyoweza kumshinda mwenye nguvu, kwa
masaada wa Mungu. Hata hivyo kuna mengi kwenye hadithi hii kuliko yale
yaliyojitokeza tu kwanza. Kilichotendeka kwenye hadithi hii kinarudisha taswira
nzima hadi nyuma mbali na hata kabla ya kipindi hiki ambacho Daudi aliingia uwanjani
kupigana na Goliathi. Mkururu wote wa matukio uliwekwa kwa hisia yenye
kumwamini Mungu kuwa ndiye aliyeko nyuma ya tukio lote zima, ambalo lilikuwa ni
mfano na uwakilishi wa matendo au harakati za Masihi. Maana ya mambo yote
yaliyo kwenye hadithi hii yote ya Daudi na Goliathi, na historia ya huko nyuma
na hadithi yenyewe imeelezewa na kufafanuliwa kwa kina. Kuna maana yake nyuma
ya kila kitu kimoja kilichosimuliwa na kufanyika kwenye historian a nyuma ya
wahusika au wahusika wakuu au waprotogoni hawa wote, kwa kote kuwili, yaani kwa
Waiasraeli na kwa Wafilisti.
Kuna fundisho
maalumu lililowianishwa kwenye hadithi yote nzima ambayo ule mti unahusiana na
ushindi wa Masihi kwa imani za ulimwengu. Giliathi wa Gahi alikuwa shujaa wa
Wafilisti. Wafilisti walikuwa sio wenyeji wazawa wan chi ya Kanaani na
hawakuendelea kuwa taifa lililo ndani ya nchi ya Kanaani. Mwishoni mwa karne ya
kumi na tatu KK walikataliwa kuweka makazi yao kwenye kile kinachojulikana kuwa
ni maeneo ya Aegean. Walikuwa wameondolewa kwa njia ya mikururu ya maafa na
maangamizi makubwa yaliyouangamiza na kuupoteza ustaarabu wa Wahiti huko
Uturuki, na pia nguvu au mamlaka ya Wamycenaens. Miji mikubwa ya Wakanaani
iliangamizwa ia na Misri ilikupunguzwa au kupokonywa na kupunguzwa nguvu zake.
Kipindi hiki kiliwekewa alama yake na utawala au mamlaka kwenye nchi hii na
uaramia wa baharini.
Biblia inaelezea kwamba Wafilisti au Wafilistini, walikuja kwa barabara
wakitokea Kafitori au Krete (Yeremia 47:4; Amosi 9:7; sawa na Kumbukumbu la
Torati 2:23). Sehemu au pande za pwani kwa hiyo iliitwa Cretan Negeb au Negebu ya
Wakerethi (1Samweli 30:14 soma kwenye Biblia ya RSV). Wakrete pia wana
nasaba ya Wafilisti (Ezekieli 25:16; Sefania 2:5). Sura hizo zina uhusiano unaoendelea
wa kinabii pia. Kwahiyo, hata hivyo, hakuna ushahidi wa kiakelojia wa Wafilisti
kuikalia Krete. Kile tunachokijua ni kwenye Biblia inasema tu kwamba huko ndio
walikotokea. Kwa hakika kabisa hawakukaa Krete kwa namna au maana yoyote. Hawakuacha
ushahidi wa mambo mengi ya kiakiolojia. Ni wazi tu ulikuwa ni mpito endelevu.
Kwakweli lilikuwa ni wimbi au kundi la pili la Wakaz wa Pwani mwa Bahari. Kuna kitabu kilichoandikwa na Velikovsky
kinachoitwa Wakazi wa Maeneo ya Baharini,
ambacho ni cha muhimu sana, na Velikovsky ameandika hoja nzuri sana kuhusu
msalaba kwa wanazuoni kuhusu kipindi gani maalumu ulivyoanza na kuhusika.
Kinachofanyika hapa ni kuvichukua vipindi maalumu vya wanazuoni kinachoendana
sawa na wanahistoria wa kiakiolojia wa Kimisri hadi nyakati za Manetho, kwa nia
ya kuepuka mngongano au mkanganyiko. Jina Wafilisti limetoholewa kutoka mtindo
wa uandishi wa Kimisri la prst ambalo
ndilo jina mmoja wa wakazi wa maeneo ya baharini. Neno la Kiebrania la pelishti ni kiambishi cha kisifa kulichotoholewa
kutoka kwenye midhihirisho ya kieneo ya pelesheth.
Chimbuko au mashina ya uandishi wa Kifilisti mbili zote zimeandikwa Pilisti au Palastu. Hakuna etymolojia ya Kisemitiki kwa jina hili na
inaonekana kwamba ni ya mchanganyiko wa Kihindi na Kizungu, yaani Indo-European.
Kwa hiyo, neno Wafilisti (Pisisti), au Palastu (Palestina), limetoholewa
kutoka kwenye majina ya Wafilisti. Lakini watu walioko huko leo, Wafilisti, sio
watu walewale kama Wafilisti au Wapalastu, ambao walikuwepo huko katika nyakati
za Daudi. Waliuwa ni watu wa jamii ya mchanganyiko wa Wahidi na Wazungu ambao
hapo mwanzon waliishi Misri na baadae kwenye maeneo ya pwani mwa bahari.
Wafilisti waliishi
maeneo ya pwani ya bahari kwenye jimbo ambalo kwa sasa tunalijua kama Ukanda wa
Gaza na kwenye maeneo ya bara ya Kanaani. Hapa walishirikiana na kundi lingine
la watu wa makundi yaliyowasili hivi karibuni, ya Waisraeli. Chanzo cha
migogoro na matatizo, ambayo ilifikilisha kufikia ukomo wa Zama za Shaba na
mwanzo wa Zama ya Chuma, kumebakiwa kuwa ni mkanganyiko bado.
Dhana ya vita vya
kikanda imebishwa na wale walio kwenye maafa ya asili. Kwa hiyo, wanazuoni
wamekuwa wakijaribu kubisha kuwa au pengine ni vita vyao vya kikanda ndivyo
vimesababisha vuguvugu au mwondoko huu, au huenda ni maafa ya kiasili. Velikovsky
ni mtaalamu wa majanga na maafa ya asili. Anapinga kwamba mlipuko wa volcano ya
Thera ulisababishwa na kuondoka au mwenendo wa watu hawa na kwa ajili ya
kuwekwa tena kwa kipindi hii maalumu pia. Siri hii imeelezewa kwa kina zaidi
kwa kukosekana kwa maandiko tangu kipindi hii, na hivyo kukapelekea kukiweka
kipindi hii mwanzoni mwa Zama ya Chuma, kijulikanacho kama karne kuanzia ya
kumi na mbili hadi ya kumi na moja KK, kijulikanacho pia kama Zama za Giza
(usikichanganye na ile Zama ya Giza ya kipindi cha zama za kati kilichotokea
yapata miaka ba kukipa muda kipindi hiki cano caused the moveme, iliyofuatia).
Tulikuwanacho kabla ya kipindi cha zama kati, kile kilichokuwa kinajulikana
kama Zama ya Giza kwenye karne ya kabla ya kuanguka kwa Dola ya Warumi huko
Ulaya. Hivyo sivyo vipindi vya Zama ya Giza ambavyo watu hawa wanatajwa kwavyo.
Wanaviita kuwa ni Zama za Giza za Mashariki ya Kati, karne ya kumi na moja
kabla ya Kristo. Mwaka 1995 kazi ya uchimbuzi ilifanywa na Profesa Trude Dothan
pamoja na Profesa Seymour Gitin wa Chuo Kikuu kilichojulikana kama the Albright
Institute, kwenye maeneo hayo ya miji ya Wafilisti. Mji wa Ekron ulikuwa ni mji
mdogo wa Wakanaani wa Dunams 50 na uliangamizwa mnamo mwaka 1200 KK na mahali
pake palichukuliwa na mji uliozungushiwa vyema wa rudishwa tena kwa
kuzungushiwa Dunams 200.
Kazi ya uchimbuzi imefanyika huko Ashidodi, Ekroni na Ashikeloni. Ashidodi na Ekroni inaonyesha jamii iliyopangilika vizuri ya wahamiaji wapya waliotokea kwenye historia ya kimijini iliyoanzisha miji mikubwa na iliyopangiliwa vizuri juu ya maganjo ya miji midogomidogo ya Wakanaani (kwa mujibu wa malaka ya Abraham Rabinovich, Jerusalem Post, art. Nothing But a Name, June 17 1995, p. 8).
Miji mingine
miwili ya Wafilisti huko Pentapolis ni Gaza, ambao maganjo yake yako kwenye mji
wa sasa, na Gati au Gathi, unaoaminiwa kuwa ni eneo la Tel es-Safi siyo mbali
kutoka Ekroni. Adolphe Lods, aliyekuwa Profesa wa Kifaransa, anasema kwamba
Wafilisti walikuwa ni wenyeji na wakazi wa maeneo ya bahari, na kwamba Rameses
III alimrithisha kazi ya kuwasukumia kwenye mipaka ya Misri mwaka 1192 KK (Kwa
mujibu wa kitabu cha Israel, Hooke kilichotafsiriwa
na kina Routledge & Keegan Paul, London, 1962, p. 348), au huenda ni sahihi
zaidi kama miaka minane ya Rameses III (takriban mwaka 1188 KK; kwenye kamusi
ya Interpreter’s Dictionary of the Bible,
Vol. 3, p. 791). Walizuia baadhi ya desturi zao. Silaha zao na zana zao kama
zilivyoelezewa kwenye 1Samweli 17:5-7 zinafanana na za watu wa Asia Ndogo (ibid.).
Walitohoa desturi
za Wakanaani pamoja na miungu yao walikuwa ni miungu halisi wa Kisemitiki:
Dagoni, mungu wa mazao; Atargatis-Derketo, mungu-mke wa Ashikeloni, ni aina ya kushaniri kila mahali kwa
Astarte Msemitiki (ibid., p. 349). Mengi yameandikwa kuhusu Dagon, kwamba
ni kama alionyeshwa kwa umbo la samaki, lakini Dagon alikuwa ni mungu wa nafaka
kwa mujibu wa Lods. Ndivyo ilivyokuwa pia, kwamba ibada za Astarte zilikuwepo
huko chini ya Atargatis-Derketo. Astarte wa Wapalestina au wa Wafilisti anatajwa
kwenye maelezo yaliyovumbuliwa huko Delos; Baal-Zebubu “mungu wa mainzi”, mungu
wa Ekroni. Huyu ndiye alikuwa wa mungu wao mwenye umbo la mjumuiko wa miungu
yote au muundo. Kimsingi, ilikuwa ni imani na muundo wa kisemitiki iliyotuama
kwenye imani za Kibabeloni. Kwa hiyo, Wafilisti waliichukua dini na imani ya
Kibabeloni. Miungu hii ilikuwa ya mrengo wa imani za Kibabeloni, na Wababeloni
walikuwa ni Wasemitiki.
Maelezo ya kina
kuhusu imani hii yameandikwa kwa kina kwenye jarida la Utakaso na Tohara (Na. 251).
Makuhani wa Attis
ambao waliandamana katika karne ya nne kuwa wakristo wahiba anane zao. Mipangilio ya ukristo wa kisasa wa
jua ambayo watuma jina pasaka kwa rubundji wa mpangilio na kuutumiza Ahere na
mfano ya miniyu na mungu mengine. Tertulian anasema Atargatis alikuwa miungu ya
Syria. Kitabu cha Wamakabayo kinasema waliitu jua kuwa Hadard wamaanisha mwana
wa kiume wa jua. Talmud analiita Taratha. Kule Armenia yeye ni Tharatha yeye ni
kama miungu ya wasemetu Ishalar.Athtar au kwa upesi Anglo saxon Easter. Strabo na Hesychus pia wanamjua na Athara
na malezo ya delos waaiita. Aphrodite (ERE ibid.) Askelon, Karnaim na Delos
walimtumikia Astarte. Inavyojulikana kama Derketo kwa Askelon na miungu yake ya
Chini Ilikuwa Samaki. Hiihuonekana kuwa mwanzo wa Mermaid. Lucian hawezii
akamtambua roho ya wanasiria kule Hierapolis na muundo wa Askelon, kwa sababu
roho huo kwa Heirapolis alikuwa na muundo kamili ya binadamu na akamwita. Hera,
lakini akakubali unaweza kutambulishwa na Rheokuna kutiamini ambayo na chache
kuwa moja na roho moja. Wanafunzi wa Atargatis na Astarte hawakula samaki, na
maumbile yao ilitambulisha miungu hayo kama moja na roho sambamba. Roho
ulitambulishwa miungu hayo kama moja na roho sambamba. Roho ulitambulishwa na
eneo ambayo ulikuwa tofauti kwa mafikirio ya watu wa kawaida vile alivyokuwa.
Ishtar kule Asssyria kule Nineveh na Arbela. Jina la kutumia ya Hierapolis ni
Mabog na inamaanisha nyakati kule Aramaiz (cf. ERE, ibid.). Umoja wa maji na
nyakati pia.
Kutokana na kitabu
cha 2Wamakabayo 12:26 Yuda Mmakabayo aliliendea kinyume Hekalu la Atergatis la huko Karnion mwaka 164 KK
na akawaua watu 25,000. Paton anahitimisha kwa maandiko yake yaliyo kwenye 1
Makabayo 5:43 kwamba imani na dini potofu ya Atargatis haikustawi tu huko
Hieropolis na Askalon, bali huko Bashani pia. Tofauti zilizopo kati ya Damascus
na Banias huko Kefr Hauwar zinaashiria dalili ya kwamba hekalu lilikuwepo huko
na pia idadi ya utofauti za huko Delos, zinaweka tarehe za muda mfupi sana
kabla ya kuanza kwa zama za Ukristo, ikimuonyesha yeye na Hadadi na pia
kumuonyesha yeye kama Aphrodite (sawa na isemavyo ERE, vol. 2., p. 166). Kwa
hiyo, yeye ni mwenzi wake Hadad, mungu jua au Baali. Ni kama alivyokuwa Rhea,
alimfanyia Attis ambaye anaelezewa pia na yeye.
Paton pia anasema
kuwa maandiko ya Ovid ya mwaka 17 BK inatuambuia vile vile Dereto miungu ya
siria na Atargatus na uonyese maneno mapya kuwa alibadilishwa kuwa samaki kule
Bamboyce, jina la ugiuku inayomaanisha Hierapolis maandiko ya Strabo yamwaka 24 BK Inasema.
Artargate (au
Artagate kwenye baadhi ya MMS) Wasyria wanamwita Artara, lakini Ctesia wanaiita
Derketo. Hapa Artagatus anatambuliwa na “Artar (Athtar, Astarte). Kwa njia hiyo
ambapo anatambulika na Aphrodite kuluyana na marelezo ya Delo (ERE ibid).
Cornitus (mwaka 68 BK)
anasema kwamba samaki na bata zilikuwa vitu safi kwake Atargatis miungu mke wa
Wasyria. Hii imeaminiwa penye mfano ya samaki kule Ronia ilijitokeza katika
karne ya kwanza. Wakristo hawangetengeneza mfano wa imani yao kujaa kilichokuwa cha shetani kuabudiwe kule
palestina kwa karne nyingi na katika
nyakati za Kristo. Pliny kwa mwaka 79 BK anasema kwamba Ceto anaabudiwa kule
Yafa. Pliny na Strabo wanasema mabaki ya kiumbee cha ziwa ziwa kuhuekwa Joppa. Wote
wawili, yaani Piny na Ceto wanaongelea kuhusu sanamu kubwa skeleton ya jitu au
kiumbe wa baharini iliwekwa huko Yafa. Ceto huenda anachukuliwa kama mabadiliko
ya Derceto na kusema lakini paton anasema hii haionekani (ERE ibid.). Pliny
anaiona Atargatis kama Dereto na kusema kwamba ahabudiwe kule Hierapolis au
Bambyce au Mabog. Plutarch anasema kulikuwa mahali pa maji ya kuweka samaki
ilyoheshimiwa na kusema miungu huyo aliabudu hapo, Inatambuliwa na Aphrodite na
Hera au miunguanayetengeneza kutokana na moshi ya hewa mbegu ya kila kitu (ERE
ibid.). Dhibitisho sahihi ilitolewa na maandiko ya Lucian ca 200ce na mshahidi
kiume yeye wa SiriaVile tumeandika katika angependeka kufahamu kama Hera LAKINI
paton akasema hakuna ubabaishi tunakumana na Atargatis (ERE ibid.). Kwa hiyo
miundo wa Atargatis, Ishtar au Astarte, Ashitaroth au Easter ni moja ya tabia
ambazo zimekaliwa kwa biblia inavyohusu hivi mafikirio.Fikira ya ushafishaji
inahusu mpango ya kutolewa kwa tabia ya huo nabudilaji. Inatuonya nyua kuhusu
muundo wa Shahabu ya ndama chini ya majina kadha (sawa na ilivyo pia kwenye
majarida ya Ndama wa Dhahabu (Na. 222)) na lile la
(Utakaso na Tohara (Na. 251)).
Kwahivyo utakaso wa Attis na Easter bado uliendelea kule kule Siria hadi mwaka 200 CE.
(Imukuliwa tena kutoka kwenye jarida la W.E. Cox la Pinata (Na. 276) Christian Churches of God, 1999.)
Viongozi waliitwa seren ambalo lilitumiwa tu kwenye lugha ya Kiebrania ikijumuishwa na
lugha ya Wafilisti. Ni wazi na dhahiri sana kwamba neno la lugha yao wenyewe
linashabihiana na neno la Kiyunani la turranos.
Biblia ya Kisyria inalitaja neno hili truno
na kwa lugha ya Targum ni turono
(ibid.). miji mitano ilianzisha shirikisho. Kwa mfano, mwana mfalme wa Gathi
wakati mwingine anafanywa kuwa mfalme lakini ni Mfalme wa Gathi peke yake, na sio
wa Wafilisti wote. Hawakuwa na mfalme wan chi nzima. Kulikuwa na mabwana watano
wa Wafilisti. Sehemu ya upande wa Dori ulimilikiwa na washirika wa Wafilisti,
Wazekali, ambao ni kundi jingine la “wakazi wa maeneo ya bahari”. Hawakuwa ni
wa kundi hilohilo moja. Wafilisti walifikia kupata umaarufu kimaajabu sana kwa
uwashindi wa Waashuru chini ya Senikarebu mwaka 701 KK. Kwa kweli hawakufika
kilele cha nguvu zao hadi hatimaye wapolishwa na Waashuru. Ilifanyika kuwa miji
ya watu waliostawi ambayo ni mataifa pia ndani ya mfumo wa kiuchumi wa kifalme,
kwa kuwa walikuwa ni watohoaji wakuu. Waliziainisha mila na desturi zao na waliziiga na kuzihusianisha kimila.
Kwa namna hiyohiyo ndivyo dini za usiri za Kibabeloni ziliga na kutohoa. Hiyo
ilikuwa ni kusababisha kabisa mauti au kifo chao, kwa kuwa hawakuwa na mfumo
wala utaratibu maalumu wa kimila, ambao uliwafanya wawe ni watofauti. Watu hawa
waliiga imani ya kidini ya Wababeloni na ndipo hatimaye walikithi vigezo kwenye
mfumo wa kiuchumi wa Waashuru.
Hatimaye, waliangamizwa
na Wababeli kwa kuwa walifanyika kuwa ni mji wenye mataifa yenye watu
waliostawi ndani ya mfumo wa utawala wa Waashuru. Kwa hiyo hatimaye Wababeloni
waliwaangamiza Waashuru, kwa kuwa walikuwa wameiga vitu vingi sana kutoka kwenye
imani ya Waashuru. Walikuwa wamefanana sana na kujulikana na Waashuru. Walikuwa
ni wa mwisho kusikilizwa kwenye orodha ya watumwa ambao ulishurutishwa au
ksababishwa na dini. Ekroni iliangamizwa na Nebukadneza mwaka 603 KK. Orodha
iliyokutikana kwenye matukio ya mafanikio ya Wababeloni yanaonyesha kutokea tangu
karne ya tano KK huko Nippuri ukitaja matukio ya utumwa wa Is-qal-lu-nu
(Ashkelon) na Hazatu (Gaza). Gitin anaonyesha kwamba rekodi hii inaonyesha kupotea
na kutokomea kwa Wafilisti kutoka kwenye kurasa za historia (soma kitabu cha
Rabinovich, ibid.). yuda, Lawi na sehemu ya makabila walirudi kutoka utumwani
Babeli, Wafilisti hawakurudi. Ufafanaji wa kiutamaduni wao na Waashuru ulikuwa
ni wa hali ya juu sana na kwamba hawangeweza kumudu kuishi kama utambulisho wa
kimila, kwa mujibu wa Gitin. Hali yao ya kimaadili ilihusiana au kufanana na
washiriki au marafiki wa Aegean wa huko Cyprus baada ya kuonyesha mpangilio
kwene miji ya zamani kidogo iliyopelekwa kwenye maeneo mapya na kuanzisha mila
au desturi tofauti iliyowasababisha wao wamudu kuishi. Kwa hiyo, ustaarabu wa Aegean,
ndugu wa Wafilisti, walioishi huko Cyprus, waliweza kuondoka na kujongea kwenye
maeneo mapya na walimudu kuishi kwa kuwa hatimaye walianzisha desturi na mila
zao zilizotofauti. Na hii ndiyo sababu ya pekee iliyowafanya wamudu kudumisha.
Mafunzo pekee tunayohitaji kujifunza kutoka kwa Wafilisti hata hivyo ni kuhusu
wajibu wao kama nguvu ya upingaji dhidi ya Israeli ambayo ilisababisha kuwepo
kwa kitisho cha nje kikubwa vya kutosha kuwalazimisha Israeli waungane kama
taifa chini ya Sauli. Kushindwa kwa huko Ebeneza kulikuwa ni hamasa au changamoto.
Hata hivyo, mchakato ulikuwa umekwisha kwa kipindi kilichoongezwa.
Kwa hiyo kile
kilichotokea ni kile alichoamua Mungu ili kulianzisha taifa la Israeli kwenye
Nchi ya Ahadi. Mlolongo wa maafa ulianza na Israeli wakaenda utumwani Misri.
Adui aliamua kuwaweka watu wake mwenyewe wapate nafasi na fursa nzuri ya
kuwazia Israeli wasiweze kuichukua na kuikalia nchi ya Kanaani au ya Israeli;
kwa maneno mengine ni kwamba ili wasiweze kuimiza ahadi. Kwa hiyo watu wa asili
ya maeneo ya pwani mwa bahari Wafilisti, ndipo wakawekwa katika Israeli
wakijaribu kujikusanya na kuzuia kuingia na kutamalaki kwao Israeli kama taifa.
Kama wangefanya hivyo, wangeweza kuihakikishia dini ya Kibabeloni kuwa ilikuwa
bora na maana sana kuliko ile ya Waisraeli, na ndipo dini tuliyonayo sisi
isingeweza kuwa na nafasi au kuingizwa na kuanzishwa humo. Dini ya Kibabeloni
ingeweza kuichukua dini hii mapema sana. Na kwamba vita iyiyoko ya imani ya
Kibabeloni dhidi ya imani ya kidini ya mchanganyiko wa Ukristo na dini ya
Kiyahudi, ingali inakuja bado na vita hiyo inapigwa vita kati siku hizi za
mwisho. Imani ya Kibabeloni
ni imani ya dini iliyo kubwa sana hapa duniani kwa sasa. Wafilisti waliileta au
kuiwakilisha dini ya Kibabeloni. Vita hivyo ni vile vinavyopiganwa
ikihitimishwa sasa, katika nyakati hizi za mwisho.
Mateso na dhuluma
walizofanyiwa Israeli na Wafilisti ilishuhudia makabila ya Dani na Yuda
yakijisalimisha na kuwatumikia maadui wao waliowashambulia (soma Waamuzi
16:1-3). Hatimaye walienenda kinyume na makabila ya Ufraimu na Benyamini ambao
waliyashinda. Katika Israeli, huenda kabila la Yusufu, ndiyo waliasi na Wafilisti
wakawashambulia. Mungu amekuwa akitenda kazi na Waisraeli kwa kipindi hiki
chote. Rehea nyuma kwenye majarida ya Samsoni na Waamuzi (Na. 73), na Jeshi la Gideoni na Nyakati za Mwisho (Na. 22), ambapo tutajionea jinsi Mungu alivyokuwa
anashughuika na Israeli zaidi ya kipindi kile cha Wakanaani na Wafilisti. Kila
mara walipoangukia kwenye dhambi Mungu aliwaacha ili wagawanike na kuvunjika,
na kisha wakati walipokuwa wanageuka na kumrudia waliimarishwa na kujijenga
tena. Kwa sababu hii, aliendelea kwa sababu za kimsingi sana dhidi ya Wafilisti
ili kuwarejesha na kuwaimarisha tena Israeli kwa kipindi kilichokusudiwa. Aliweka
mpango wa kumuinua kuhani mwaminifu (1Samweli 2:35) ambaye angefanya kila kitu
sawasawa na mapenzi na nia ya Mungu. Kuhani huyu ndipo angeomba kwenye uwepo
wake (NB).
1Samweli 2:35-36 Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu,
atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika
nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi
wangu milele.
36 Kisha itakuwa, ya
kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako atakwenda kumsujudia, apate
kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia, Tafadhali unitie katika
kazi mojawapo ya ukuhani, nipate kula kipande kidogo cha mkate.
1Samweli 3:1 Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.
Kuna uhusiano na
uhitajiko wa Kimasihi kwenye andiko hili. Linasema, kuna kuhani mwaminifu aliyeinuliwa, ambaye
atakayefanya sawasawa na mambo yote yaliyo kwenye moyo wa Mungu, na katika nia
yake. Atakwenda kumjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wake
milele. Sasa Samweli alikufa!
Kuna kuhani aliyeinuka
atembee mbele za Mungu milele, mbele za mtiwa
mafuta, na mtiwa mafuta huyo ni Masihi. Kwa hiyo kuna kuhani aliyeinuliwa atembee
mbele za Masihi milele. 1Samweli 2:36 ni unabii kwa kuhani wa Israeli kwa kuwa
ukuhani umetiwa unajisi na ulipaswa kuombea uwepo wake. Ni unabii mkuu na wenye
nguvu sana!
Samweli aliawekwa
kuwa ni nabii na Bwana basi maneno yake na yasiangukie chini.
1Samweli 3:19-21 Samweli akakua, naye Bwana alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lo lote lianguke chini. 20 Nao Waisraeli wote, toka Dani mpaka Beer-sheba, walitambua ya kwamba huyo Samweli amewekwa kuwa nabii wa Bwana.
Kisha Samweli aliwakusanya
pamoja Israeli huko Shilo kwa kutegemea kile kilchojulikana kama mapenzi ya
Mungu. Kumbuka kuwa, Yerusalemu ulikuwa sio makao makuu au mji mkuu na wala
haukuwa huko Hebron. Maskani ya Mungu ilikuwa huko Shilo.
21 Naye Bwana akaonekana tena huko Shilo; kwa kuwa Bwana akajifunua kwa Samweli huko Shilo, kwa neno la Bwana.
1Samweli 4:1-11 [Ikawa siku zile Wafilisti walikusanyika ili kupigana na Israeli,] nao Waisraeli wakatoka juu ya Wafilisti kwenda vitani;wakatua karibu na Ebenezeri ,nao Wafilisti wakatua huko Afeki. 2 Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao lililokuwa uwandani wapata watu elfu nne.
Hapa tunawaona
Israeli wakimtii nabii wa Mungu lakini wakishindwa kwa upanga. Matokeo ya uadui
huu yalitegemea kwenye uwepo wa kimwili wa Sanduku la Agano. Mungu alikuwa
anawaimarisha Israeli na kuwaambia kuwa ‘hampo sahihi machoni pangu;
hamjajiandaa’. Kwa hiyo anaweka masharti ambapo nakwenda kuwaunganisha na
kuwaweka pamoja Israeli, kwa kuwa kila mtu wakati huu alikuwa anafanya kile
alichokuwa anakiona kuwa ni chema machoni pake mwenyewe na walikuwa kwenye
makundi tofauti mbalimbali. Walikuwa chini ya makabila na kulikuwa hakuna uongozi
wa kati. Mungu alikuwa anakaribia kuwafanya wawe ni mhimili wa uongozi. Waliona
kuwa wameshindwa, kwa hiyo hatimaye waliamua ‘ni jinsi gani tunaweza kushinda?’
‘Najua kuwa Mungu ametuweka hapa, na tuende sasa tukalitwae Sabduku la Agano na
kisha tukalitangulize hilo Sanduku mbele yetu tuendapo mapiganoni’. Kwa kuwa
walikuwa na uwepo wa kimwili wa Sanduku hili la Agano walidhania kuwa hiyo
inatosha. Hawakujua wala kushukuru kuwa lilikuwa ni alama tu ya sheria au
torati ya Mungu, tabia na mapenzi yake. Ni kama walivyo Wayahudi wa leo hawayaoni malengo ya kiroho ya uhusiano na
Mungu. Kuna makusudi ya kiroho kwa haya yote.
3 Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona Bwana ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la agano la Bwana toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu. 4 Basi wakatuma watu kwenda Shilo, nao wakalileta toka huko sanduku la agano la Bwana wa majeshi, akaaye juu ya makerubi; na Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwako huko pamoja na sanduku la agano la Mungu.
Kile anachokifanya Mungu hapa ni kwamba
analichukua Sanduku la Agano kutoka kwenye Maskani na anasema: “Nakwenda kuweka
uwepo wangu ujulikane matika Israeli”. Kwa wakati ule wana wa Eli (Hofni na Finehasi) walikuwa waovu. Ukuhani
ulikuwa umepotoka na kukengeuka kabisa; wkatoto wake wakawa wanafanya ngono na
wanawake hekaluni. Walidai na kupokea rushwa. Walipotosha hukumu kwa kupokea rushwa
na Eli hakuwakemea. Samweli aliuona uovu kwenye huduma ya kikuhani chini ya
Eli. Aliuona uovu wa Hofni na Finehasi na tutaona kwamba Samweli alifanya kitu
hichohicho. Samweli alikuwa ni nabii wa Mungu lakini hakuzikemeadhambi au
makosa waliyoyafanya watoto wake mwenyewe ambayo aliyaona yakifanywa wakati wa
Eli yakitendwa na kina Finehasi na Hofni. Haya ni makosa yanayofanyika kila
mara. Viongozi wa Makanisa ya wateule, kwa kweli wanaweza kuziona familia zao
zilitenda maovu na mapotofu na warithi wao wanaweza kuyaona hayo nab ado
wakawaacha watoto wao wayafanye hayohayo. Hivi ndivyo ilivyotokea kwa Eli, na
hiki ndicho kilichotokea kwa Samweli. Kwa sababu ya hiyo, utawala ulichukuliwa
wote kabisa na ukuhani. Utawala au uongozi wa Israeli ulichukuliwa kutoka wa
waamuzi na kwenye ukuhani, na wakapewa wamonaki, mikononi mwa uongozi chini ya
mfalme. Kwa hiyo Mungu aliwachukua kina Hofni na Finehasi pamoja na Sanduku la
Agano kutoka Shilo, na kuwaweka kwenye nafasi ambayo waliuawa kwayo kwa kuwa
walikuwa wamemtia unajisi na kumfanya asifae mchungaji wa Sanduku la Agano. Hii
ilipuuwa na kutotiliwa maanani.
5 Na sanduku la agano la Bwana lilipoingia kambini, Israeli wote wakapiga kelele kwa sauti kuu, hata nchi ikavuma. 6 Nao Wafilisti waliposikia mshindo wa zile kelele, walisema, Maana yake nini mshindo wa kelele hizi kubwa katika kambi ya Waebrania? Wakatambua ya kuwa sanduku la Bwana limefika kambini. 7 Wafilisti wakaogopa, maana walisema, Mungu ameingia kambini. Wakasema, Ole wetu! Kwani halijawa jambo kama hili tangu hapo. 8 Ole wetu! Ni nani atakayetuokoa na mkono wa miungu hawa walio hodari? Hawa ndio miungu waliowapiga Wamisri kwa mapigo ya kila namna jangwani. 9 Iweni hodari, na kufanya kiume enyi Wafilisti, msije mkawa watumwa wa Waebrania, kama wao walivyokuwa watumwa wenu; fanyeni kiume, mkapigane nao. 10 Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu. 11 Hilo sanduku la Mungu Likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa Eli, wakauawa.\
Sanduku lilikua
na madhara yaliyo kinyume. Wafilisti walipigana kwa nguvu zote kwakuwa walikuwa
kwenye kitisho. Israeli elfu thelathini waliuawa wakiwemo watoto wa Eli. Mungu
aliwauwa makuhani hawa na akalitoa Sanduku la Agano mikononi mwa Wafilisti.
Jambo hili lilifanyika mahususi mikononi mwa mtiwa mafuta wake nabii. Kwa nini?
Jibu lake lilikuwa ni kwamba Israeli walipoteza vigezo vya kuwafanya wastahili
kusimama mbele za Mungu kwa utaratibu au vigezo zilivyokuwepo. Zaidi sana ni
kwamba Mungu alikuwa bado ana kazi ya aliyotaka waifanye Israeli na isingeweza
kufanywa kwa utaratibu ule ya upangiliaji au mpangilio. Kwa hiyo Mungu
ilimlazimu kuwaacha n aka kufanya kwake hivyo ilimbidi kuwaangamiza makuhani
pia. Alisababisha Hofni na Finehasi aende vitani, na aliwauliambali na kisha
watu takriban 30,000 pamoja nao.
Kuondolewa kwa
Sanduku la Mungu mikononi mwa Wafilisti kulibidi kuwaonyesha Wafilisti pia
kwamba alikuwa wanaabudu vinyago au sanamu zisio na uweza. Sanamu ya Dagoni ilitengenezwa
ikiwa inajionyesha jinsi ilivyokua imeliangukia Sanduku la Agano (1Samweli
5:3-5). Ilikuwa imeliangukia Sanduku la Agano na ilikatika kichwa chake na
kuangukia kwa mwonekano wa kulisujudia sanduku kwa paji la uso ake. Kuna maana
kutokana na kitendo hiki. Kitendo hiki cha kukatika na kuondolewa kichwa chake
na mikono yake kutoka kwenye kiiliili kinahusiana na dhana ya kuwatia mhuri
watu kwa mintaarafu ya imani ya mungu ao. Umetiwa mhuri kwenye paji la uso na
mikononi kwa mawazo yako yahusuyo kwenye imani hii ya kidini na kwa kuwa ni kifaa
au chomo cha kuchukua na kueneza imani ile kwa kazi yake na kwa matendo vya
kijamii. Kwa hiyo, mpangilio wa kijamii na kiuchumi wa imani umeonyeshwa
kitaswira na mikono, na dhamira ya kifikra au eshwa kitaswira kwa paji la uso.
Na ndiyo maana, utiaji mhuri wa imani kwenye paji la uso na mikononi. Watu hawa
walipigwa pia na maradhi ya majipu (1Samweli 5:6; 6:4). Maradhi haya ya mjipu yametajwa
pia kwenye Kumbukumbu la Torati 28:27 kuwa ni moja wapo ya dalili za laana na
tauni ya Misri. Tunajua kuwa haya ni haemoroids, au maganjo. Wafilisti walikua
na aina zake nyingi yaliyoaua watu wake wakati walipokuwa na Sanduku la Agano
na waliwapa majipu matano ya dhahabu na panya watano wa dhahabu, kila mmoja ni
kwa kila bwana mmoja a mabwana wa Wafilisti, ni kama sadaka za kupigiwa kura
kwa Sanduku lilipokuwa linarudi baada ya miezi saba (1Samweli 6:1-14). Walikuwanalo
kwa kipindi cha miezi saba na halikuwawanyia kitu chochote ila ni mateso tu.
Bwana aliapa ushuhuda ka njia ya kitendo hiki kwa pande mbili zote, yaani kwa
Waisraeli na kwa Wafilisti.
Kwa kupitia dharura
hii, Mungu aliianzisha serikali kuu na kiti cha enzi ambacho siku moja Masihi
angekirithi. Alikuwa anaweka mfumo wa kurithi ajapo Masihi. Kwa hiyo matukio
yanayozingira uanzishwaji wa mfumo a kifalme pia yanakwenda sambamba na
makusudio yake.
Kwanza kabisa,
ufalme ulinzishwa kwenye mstari wa uzao wa Sauli wa Benyamini. Benyamini
lilikuwa ni kabila dogo zaidi kati ya makabila yote na kwa kweli lilikuwa
karibu lifutiliwe mbali kwa kutokuwepo kwake kwenye matukio yaloyotangulia (Waamuzi
20 & 21). Mambo yaloiyosababisha Benyamini wafutiliwe mbali katika Israeli
hayakuwa na maana yoyote. Soma Waamuzi 20 na 21 na utaona kwamba Benyamini
walifutiliwa mbali, karibia kwa mtu (kulikuwa na idadi ya watu anaume 600 walioachwa
katika Benyamini). Walipewa wanawake wa makabila mengine wawaoe, ili kwamba
Benyamini wasiweze kufutiliwa mbali kabisa. Lakini dhambi iliyowapelekea
wafutiliwe mbali inatokea ka msingi a kila siku wa watu wetu. Ni ka kiasi gani
unaweza kudhani Mungu atahifadhi hasira yake dhidi ya makabila ya Israeli wakati
hakuwa amemwachia ama kuwasamehe Benyamini kwa uovu wao mmoja tu?
Ufalme ulianzishwa
na Mungu kwa kupitia nabii Samweli. Yapasa iulikane pia kwamba Samweli
hakuwaadibisha watoto wake, ni kama alivyofanya Eli tu kwa kushindwa kuwakemea
atoto wake kina Hofni na Finehasi aliokuwa pamoja naye. Wanasaikolojia wengine
wangepinga kwamba Samweli alikuwa amelelewa na kukulia kwenye nyumba ya Eli,
hekaluni, na hivyo alidhani kuwa namna ya kawaida ya kuwalea atoto wake. Hiyo
ni kweli. Kama tutawaona wakilelewa kwa namna hiyo pasipo mfano mwingine wowote,
basi tungezania kuwa hiyo ndiyo namna kufanya hilo. Samweli alijionea matokeo
ya kina Hofni na Finehasi, lakini aliwalea watoto wake mwenyewe kwa nana hiyohiyo.
1Samweli 8:1-22 Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli. 2 Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba. 3 Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu. 4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; 5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote. 6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana. 7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.
Wazo shirikishi: Hawakudhania
kuwa Mungu angeingilia kati na kumuinua nabii mwingine ahusiane na wana.
Walidhani kuwa waikuwa wanakwenda kupigwa na Yoeli na Abia wana wa Samweli. Hawakugundua
kuwa Mungu alikuwa amewatoa kina Hofni na Finehasi watoke na kwenda kwenye
uwanja wa vita au wa mapigano, wakati wakiwa hawana nia wala wazo la kwenda
vitani, na kisha akawachinja huko. Hawakuwa na ujasiri, au imani, ya kuamini
kuwa Mungu angewaondolea mbali kina Yoeli na Abia kama alivyowaondolea mbali
kina Hofni na Finehasi. Walitaka kujiwekea Mfalme wao wenyewe na utakuta kwamba
ndipo ufalme ulivyoanzishwa, lakini Mungu aliruhusu jambo hili kutokea kwa
sababu mbalimbali. Mungu aliruhusu jambo hili kutokea ili kwamba ufalme uweze
kuanzishwa, na kiti cha enzi kilianzishwa kwa ajili ya ujio wa Masihi.
8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. 9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki. 10 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana. 11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. 12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake. 13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji.
Wazo shirikishi: Wahatawatafuta
farasi wako; hawataitafuta nchi yako; hawatakuwa wanapura nafaka zako; bali
watakuwa wanaifanya kazi ya mfalme; watakuwa wanavuna mazao yake. Hawatakuwa
wanatengeneza vitu dhaifu jikoni kwako; bali watazitengeneza jikoni kwa mfalme.
14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake. 15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake.
Wazo shirikishi: Zaka
yako haiendi hekaluni mwako sasa, bali inakwenda kwenye shughuli za kimaongozi
za ofisi ya mfalme, na hatimaye ataitumia kwa malengo yake mwenyewe.
16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe. 17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake. 18 Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; Bwana asiwajibu siku ile. 19 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu; 20 ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu. \
Wazo shirikishi: Walimhitaji
atokee mtu fulani kwao aliye kama Wafilisti; mtu fulani mkubwa na shujaa; mrefu
kwa kimo na mabega yake zaidi ya wote, ambaye wangemkubali na kusema ‘wewe
jitokeze na upiganenaye kwa pigo moja tu na kummaliza’, kwa kuwa nyakati hizo
vita ilikuwa inaamuliwa na mtu mmoja tu mwenye nguvu. Ka hiyo, majeshi
yaliwaacha mashujaa wapigane na kwa jinsi hivyo iliepusha watu wengi wasife.
Walihitaji mfalme ambaye atawatangulia mbele mapiganoni kuwapigania na ndipo
wangejua kile walichokuwa wanakifanya.
21 Samweli akayasikia maneno yote ya watu,
akayanena masikioni mwa Bwana. 22 Bwana
akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli
akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake.
Kile anachokitenda
Bwana hapa ni kwanza kabisa kuwekeza mioyoni mwa Israeli jinsi anavyofanya
mfalme anayetokana na mfumo mbaya wa kiroho na jinsi alivyo. Anasema, ‘hivi
ndivyo mfalme asiye na chembe yoyote ya maongozi ya Roho Mtakatifu
atakavyofanya. Hiki ndicho mtakachokwenda kukabiliwa nacho’. Kwa namna hiyohiyo
kwamba aliwaweka waamuzi na utaratibu uliokuwa chini ya manabii walioishi kabla
ya wakati huo. Mchakato huu ulionyesha udhaifu wa mfumo wa wa kiserikali. Kwa
hiyo aliuendeleza mfumo na utaratibu huo kwa kupitia Daudi na Masihi.
Ililazimu Israeli
waende utumwani na wapate kutenganishwa na Yuda; kwa hiyo Masihi alitokea katika
Yuda kipindi cha utawala au kongwa za Warumi katika karne ya kwanza ili kwamba
Kanisa ndipo lianzishwe kama awamu ya mwisho. Kwa hiyo, kwanza kabisa
alianzisha ufalme huu katika Benyamini na ufalme ungeweza kubakia katika
Benyamini kwa kuwa sehemu ya Benyamini walibakia ndani ya Yuda. Waliuondoa
kutoka Benyamini hadi Yuda.
Mungu alimpeleka
Sauli kwa Samweli.
1Samweli 9:15-21 Basi Bwana alikuwa amemfunulia Samweli, siku moja kabla Sauli hajamwendea, akisema, 16 Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia.
Walikuwa chini ya
kongwa na walikuwa wanamlilia Bwana na ndiyo maana alitenda hivyo, kwa kuwa
walikuwa wamemrudia Bwana.
17 Hata Samweli alipomwona Sauli, Bwana akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu. 18 Ndipo Sauli akamkaribia Samweli langoni, akasema, Tafadhali, uniambie, nyumba ya mwonaji iko wapi? 19 Samweli akamjibu Sauli, akasema, Mimi ndimi mwonaji; tangulia mbele yangu ukwee mpaka mahali pa juu, kwa maana mtakula pamoja nami leo; kisha, asubuhi nitakuacha uende zako, nami nitakuambia yote uliyo nayo moyoni mwako. 20 Na wale punda zako waliopotea siku hizi tatu, usijiudhi kwa ajili yao; maana wameonekana. Na yote yaliyotamanika katika Israeli amewekewa nani? Si wewe, na nyumba yote ya baba yako? 21 Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila ya Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo?
Mungu aliamua
kumuinua mfalme kutoka kwenye ukoo mdogo na duni kuliko yote, wa kabila dogo
kuliko yote katika Israeli. Sauli alitunukiwa na kutukuka ila hakujua ni kwa
nini na alishangaa kwa nini alikuwa ameheshimiwa na kutunukiwa kiasi hicho.
1Samweli 10:1-12 Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake. 2 Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu? 3 Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai; 4 nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. 5 Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri; 6 na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine. 7 Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe. 8 Nawe utatelemka mbele yangu mpaka Gilgali; nami, angalia, nitakutelemkia huko, ili kutoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja sadaka za amani; siku saba utangoja, hata nitakapokujia, na kukuonyesha yatakayokupasa kuyafanya.
Kwa hiyo ilimazimu
angojee kwa siku saba zaidi. Kuna maana ashiria ya mchakato huu wote wa
ukaribisho kwenye andiko hili. Unatafuta dhabihu na mkate na kitu cha kumpa
mfalme kwa mujibu saa na maagizo ya torati. Sasa Biblia inasema kwamba kila mtu
atakayekuwa mtawala wa Israeli ni kutunza rekodi za maandiko yote yaliyo kwenye
torati ili kwamba anapotawazwa kuwa mfalme asiipotoshe sharia. Kila mfalme
yampasa awe na nakala yake ya torati ili imwandae kuwaongoza Israeli. Huu ni
wajibu wa kila kiongozi wa watu – kujiandaa nafsi yake kwa kujisomea torati. Mkururu
uliopo hapa ni kwamba Sauli alipewa mikate miwili na manabii. Jambo hili linaashiria
kutolewa kwa torati na kutolewa kwa uweza wa kuielewa Biblia kwa Sauli akiwa
kama mfalme. Roho ya torati au sheria, ndipo ikamshukia mfalme ili kukamilisha
wajibu wake akiwa kama kiongozi. Hii ilikuwa ni kuonyesha kuwa chini ya utawala
wa kifalme, uongozi na Roho Mtakatifu atawekwa juu ya mfalme, kama ilivyokuwa
hatimaye kwa Daudi. Sasa ilimpasa angoje kwa siku saba, na siku hizi saba
zilishuhudia vitisho vikubwa.
9 Ikawa, alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu akambadilisha moyo; nazo ishara zile zote zikatukia siku ile ile. 10 Basi, walipofika Gibea, tazama, kikosi cha manabii wakakutana naye; kisha roho ya Mungu ikamjilia kwa nguvu, naye akatabiri kati yao. 11 Ikawa, wote waliomjua zamani walipoliona jambo hilo, kwamba, tazama, huyo anatabiri pamoja na manabii, ndipo watu wakasemezana, Ni nini hilo lililompata mwana wa Kishi? Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii? 12 Naye akajibu mtu mmoja wa mahali hapo, akasema, Na baba yao n'nani? Kwa hiyo ikawa mithali, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?
Kile wanachokisema
ni kwamba ‘Ni roho gani waliyenaye?’
Samweli aliwaita
watu wakusanyike pamoja huko Mispa na akawaelezea maana ya kuwa na mfalme na
majukumu yake kwa watu.
1Samweli 10:17-27 wana huko Mispa 18 akawaambia wana wa Israeli, Bwana, Mungu wa Israeli,
asema hivi, Naliwatoa Israeli kutoka Misri, nami naliwaokoa ninyi na mikono ya
Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea; 19 lakini leo
mmemkataa Mungu wenu, naye ndiye awaponyaye katika misiba yenu yote na shida
zenu; nanyi mmemwambia, Sivyo, lakini weka mfalme juu yetu. Basi, sasa,
hudhurieni mbele za Bwana, kwa kabila zenu na kwa elfu zenu. 20
Basi Samweli akawaleta kabila zote za Israeli karibu; na kabila ya
Benyamini ikatwaliwa. 21 Kisha akaileta kabila ya
Benyamini karibu, kwa jamaa zao; jamaa ya Wamatri ikatwaliwa. Akaileta jamaa ya
Wamatri karibu, mtu baada ya mtu; kisha Sauli, mwana wa Kishi, akatwaliwa;
lakini walipomtafuta hakuonekana. 22 Basi wakazidi
kumwuliza Bwana, Amebaki mtu asiyekuja huku bado? Naye Bwana akajibu, Tazama,
amejificha penye mizigo. 23 Basi wakaenda mbio
wakamleta kutoka huko; naye aliposimama kati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu
wote, tangu mabega yake kwenda juu. 24 Samweli
akawaambia watu wote, Mnamwona mtu huyu aliyechaguliwa na Bwana, ya kuwa hakuna
mtu mfano wake katika watu wote. Ndipo watu wote wakapiga kelele, wakasema,
Mfalme na aishi! 25 Kisha Samweli aliwaambia watu
madaraka ya ufalme, akayaandika katika kitabu, akakiweka mbele za Bwana.
Samweli akawaruhusu watu wote, waende kila mtu nyumbani kwake. 26 Sauli naye akaenda nyumbani kwake huko Gibea; na pamoja
naye wakaenda kikosi cha watu, ambao Mungu alikuwa ameigusa mioyo yao. 27 Walakini wengine wasiofaa kitu wakasema, Huyu je!
Atatuokoaje? Nao wakamdharau, wasimletee zawadi.
Ni wazi sana kabisa, kwenye andiko hili, walikuwa wanabahatisha kifikra za kama wanaopiga kura ili kuamua ni kwenye familia ipi ambayo mfalme huyu atatokea. Hawakumkuta Sauli, kwa hiyo Bwana aliwaambia mahali watakapomtafuta. Ni wazi sana kuwa aliogopa. Haukuwa ni mwanzo mzuri au wenye kutia moyo na bahati sana wakati mfalme anapokutwa amejificha, ingawaje alikwishaambiwa kuwa unakwenda kuwa mfalme.
Mungu alikuwa
amewaandaa watu pamoja na Sauli. Hii imeonyeshwa kama ishara ya kuwagusa mioyo yao. Sauli alijaribu
kujiepusha na majukumu yake hapo kwanza. Mungu alikua amewapa Israeli mfalme
ambaye alionekana kuwa ni stahili au sahihi kwao na mwenye umbo lisilo la
kawaida kwa mwonekano wan je, hata hivyo, Mungu alijua atakachokwenda kukifanya
kutoka moyoni. Mrithi wake aliyechukua nafasi yake alikuwa ni wa tofauti naye
sana. Hata hivyo, Mungu aliamfanya Sauli kuwa mfalme. Wakati Samweli alipikuwa
mzee aliwaelezea Israeli majukumu yao wanayowajibika kumfanyia mfalme.
1Samweli 12:13-25 Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, Bwana ameweka mfalme juu yenu. 14 Kama mkimcha Bwana, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya Bwana, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata Bwana, Mungu wenu, vema! 15 Bali msipoisikia sauti ya Bwana, mkiiasi amri ya Bwana, ndipo mkono wa Bwana utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu. 16 Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, Bwana atakalolitenda mbele ya macho yenu. 17 Leo je! Si mavuno ya ngano? Nitamwomba Bwana, kwamba apeleke ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu ni mwingi sana, mlioufanya machoni pa Bwana, kwa kujitakia mfalme. 18 Basi Samweli akamwomba Bwana, naye Bwana akapeleka ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa Bwana sana, na Samweli pia. 19 Watu wote wakamwambia Samweli, Utuombee sisi watumwa wako kwa Bwana, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme. 20 Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata Bwana, bali mtumikieni Bwana kwa mioyo yenu yote. 21 Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili, 22 visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe. 23 Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka 24 Mcheni Bwana tu, mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote; maana, kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu. 25 Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya, mtaangamia, ninyi na mfalme wenu pia.
Dhumuni la andiko
hili ni kuwaonyesha watu kwamba wanawajibika kwa Mungu na kwamba kama mfalme
ataviandama vinyago au sanamu na dini ya uwongo, ndipo hakutakuwa na namna
nyingine ya kumfanya mtu yeyote ajitoe na kumfuata Mungu kikamilifu.
Wawakuruhusiwa kumfuata kiongozi wa haiba au aina yoyote ambaye hamtafuti au
kumfuata Mungu wao. Hilo ni wazi. Imeonyeshwa wazi hapa kwamba kama wanafanya
maovu makubwa kihivyo, ndipo pande zote mbili, yaani, wao pamoja na mfalme
wataangamizwa kama atakavyofanyiwa mfalme. Lakini kila mmoja ana wajibu wa moja
kwa moja kwa Mungu na hilo ndilo lengo la andiko hili. Inaonyesha kwa wazi sana
kwamba hakuna mtu aliyeondolewa kwenye wajibu huu kwa Mungu. Kwa mtu yeyote
anayemsimamia au kumtunza yeye.
Sauli alikuwa
amepewa majukumu maalumu na pia maelekezo kwa kupitia nabii. Uasi wake ulipelekea
kuugharimu hata ufalme wake. Suala hili la kunpokonywa lilijumuishwa kwenye
dhabihu aliyoitoa huko Mikimashi halieleweki vyema sana.
1Samweli 13:1-15 Sauli alikuwa na umri wa miaka kadha wa kadha hapo alipoanza kutawala;naye akatawala miaka kadha wa kadha juu ya Israeli. 2 Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini; nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake. 3 Yonathani akaipiga hiyo ngome ya Wafilisti, iliyokuwako huko Gibea, nao Wafilisti wakapata habari. Naye Sauli akapiga tarumbeta katika nchi yote, huku akisema, Na wasikie Waebrania. 4 Waisraeli wote wakasikia habari ya kwamba Sauli ameipiga hiyo ngome ya Wafilisti, na ya kwamba Waisraeli wamepata kuwa makuruhi kwa Wafilisti. Basi hao watu wakakusanyika pamoja kumfuata Sauli huko Gilgali. 5 Nao Wafilisti wakakusanyana ili wapigane na Waisraeli, magari thelathini elfu, na wapanda farasi sita elfu, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni. 6 Hata Waisraeli walipoona ya kuwa wa katika dhiki, (maana watu walifadhaishwa), ndipo hao watu wakajificha katika mapango, na katika vichaka, na katika miamba, na katika mashimo, na katika mabirika. 7 Hata baadhi ya Waebrania walivuka Yordani, wakaingia nchi ya Gadi na Gileadi; lakini Sauli alikuwa akaliko huko Gilgali, nao watu wote wakamfuata wakitetemeka.
Jeshi hili kubwa
liliwatokea kinyume chao. Wafilisti waligundua kwamba walipaswa kushughulikia
tishio hili, kwa kuwa Israeli walijiunga na kujikusanya chini ya mfalme na hilo
lilikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa maangamizo ya Wafilisti, kuliko hata walivyoamini
Waisraeli hapo kwanza. Walikuwa ni kundi lililotawanyika la makabila hadi
wakati huu. Wakiwa pamoja na mfalme walijipanga wenyewe kupigana na Wafilisti
na mabwana wao.
8 Akangoja siku saba, kwa kadiri ya muhula uliowekwa na Samweli lakini Samweli hakuja Gilgali; na hao watu wakatawanyika mbali naye. 9 Sauli akasema, Nileteeni hapa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani. Akaitoa sadaka ya kuteketezwa. 10 Hata mara alipokwisha kuitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, kumbe! Samweli akatokea. Naye Sauli akatoka kwenda kumlaki na kumsalimu. 11 Samweli akasema, Umefanya nini? Naye Sauli akasema, Ni kwa sababu naliona ya kuwa watu wanatawanyika mbali nami, na wewe hukuja siku zile zilizonenwa; nao Wafilisti wamekusanyika pamoja huko Mikmashi; 12 basi nikasema, Wafilisti watanishukia sasa mpaka Gilgali, kabla sijaomba fadhili za Bwana; kwa hiyo nalijishurutisha, nikatoa sadaka ya kuteketezwa. 13 Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya Bwana, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele. 14 Lakini sasa ufalme wako hautadumu; Bwana amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye Bwana amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile Bwana alilokuamuru. 15 Basi Samweli akaondoka, akapanda kutoka Gilgali mpaka Gibea ya Benyamini. Naye Sauli akawahesabu watu waliokuwapo pamoja naye, wapata kama mia sita.
Vita ilikuwa
imepangwa na kukabiria. Samweli alikuwa amesema kwamba atakuja kwa wakati
muafaka. Sauli alidhani kwamba alikuwa amechelewa kufika. Kwa hiyo, kwa kujua
kinachotakiwa kufanywa, ndipo akaamua achukue jukumu lisilomhusu yasiyo yake ya
nabii. Samweli alikuwa hajaacha bado jukumu la kuwaamua Israeli, kwa hiyo,
majukumu yalikuwa hayajatolewa yote na kupewa mfalme. Samweli bado alikuwa
anaifanya kazi na majukumu ya nabii. Kile kilichotokea kwa kweli ni kwamba
Samweli alikuwa amechelewa. Sauli alikosea amekosea kuhesabu kipimo cha wakati.
Huu ndiyo uhusiano wa nyakati za mwisho na ujio wa Masihi, wakati wanaposema ‘Bwana
wangu amechelewa kuja kwake’. Inaonyesha pia umuhimu kuwa na dalili ya utii kwenye
mamlaka ya kisheria ya Mungu kupitia nabii wake. Jinsi ya kuwajua manabii wa
Mungu ni kuwapima kama wananena sawasawa na sharia au torati na ushuhuda (Isaya
8:20). Kama hawaneni sawasawa na sharia au torati na ushuhuda, hakuna nuru
ndani yao, au kwao hakuna mapambazuko; hakuna nyota ya mchana; na wala hakuna
nyota ya asubuhi. Ufalme wa Sauli uliondolewa kwa sababu hakumtii mtangulizi
wake aliyemtia mafuta. Aliondolewa na Mungu alimuweka mwingine. Kwa suala hili
ilifanywa kwa kupitia nabii yuleyule ambaye alikuwa hajafa bado.
Hadithi hii inaonyesha jinsi Sauli alivyotenda
dhambi pia kwa kuyahesabu majeshi ya Mungu aliyehai. Daudi pia alitenda dhambi
hii hii. Kwa sababu ya dhambi ya Daudi, watu 70,000 walikufa. Jambo hili linashabihiana
pia na nyakati za mwisho. Kitendo cha kuhesabu siku hizi saba kinashabihiana na
kipindi maalumu fulani. Sauli
alianza kuhesabu siku ya mapema zaidi. Alihesabu sehemu ya siku. Kwa hiyo, alikuja
kwenye siku ambayo Samweli alipasa awepo hapo na Samweli hakuwepo, kwakuwa
alikuwa siku moja zaidi ya mapema yake. Alifika siku ya sita badala ya siku ya
saba. Hiki ni kitu fulani ambacho watu yatupasa kukijua na kukitia akilini.
Mungu alipeleka
maelekezo mengine kwa Sauli kwa kupitia Samweli kushabihiana na Waamaleki,
maelekezo ambayo yalikuwa ni ya muhimu sana baadae na pia kama tutakavyoona pia
kutoka kwenye Kitabu cha Esta.
1Samweli 15:1-23 Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya Bwana. 2 Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. 3 Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. 4 Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari waliopanda farasi mia mbili elfu, na watu wa Yuda kumi elfu. 5 Sauli akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. 6 Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Enendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. 7 Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri, unaokabili Misri. 8 Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. 9 Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa. 10 Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, kusema, 11 Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha. 12 Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia ukumbusho, akageuka, akapita, akatelemkia Gilgali. 13 Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na Bwana, nimeitimiza amri ya Bwana. 14 Samweli akasema, Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? 15 Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa. 16 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia Bwana usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. 17 Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha kabila za Israeli? Naye Bwana akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli.18 Kisha Bwana akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia. 19 Mbona, basi, hukuitii sauti ya Bwana, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana? 20 Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. 21 Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali. 22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. 23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
Sababu yao
fikirika ilikuwa ni kwamba kama walichukua kondoo hizi zote kutoka kwa Wamaleki
wasingepaswa kuchukua asilimia kumi ya mifugo yao. Torati ilisema wazi sana
kwamba mlichukua mateka au nyara zisizofaa na mlitoa zaka juu yake pia, na
mliwapa watu. Lakini hakikuwa ndicho Mungu alichowaambia wakifanye. Wakuhitaji
ng’ombe wala mifugo ya Waameleki. Hatujui ni nini hasa ilikuwa sababu yake ilikuwa
nini. Huenda walikuwa ameathirika kwa magonjwa na huenda wangesababisha
maambukizo ya magonjwa kwenye mifugo ya wana wa Israeli. Huenda wangekubalika tu
kwa shughuli za utoaji dhabihu tu peke yake. Hatujui na hatujaambiwa lolote.
Bali alipenda kila kitu kiangamizwe na alipenda Agagi wa Waamaleki auawe pia,
ka kuwa Waagagi, wana wa Agagi, walikuwa hatimaye ndio kitisho cha kuwepo kwa
jamii ya Wayahudi.
Fundisho lililoko
hapa ni kwamba ufalme a wateule umetabiriwa kuwa ni waaminifu na watiifu. Kama
unapenda uwe ni mmoja wa wafalme wa nyakati za mwisho, iwapo kama unapenda uwe
mfalme na kuhani, basi yakupasa uwe mtii. Mfumo wote mzima unahitaji watu
watiifu. Mungu hapendi kuonyesha kiburi; bali anawahitaji watiifu na anaataka
watu watakaofanya kazi. Kiti cha enzi cha ufalme wa Israeli kilichukuliwa na
Masihi kwa ajili ya utiifu wake (Wafilipi 2:6). Kristo hakujaribu wala kudai
kuwa anausawa wowote na Mungu, bali alikuwa mtii hadi kufa. Wateule wamepewa
sheria naushuhuda ili kuupima utiifu wao kwenye amri za Mungu, hadi kufa kwao,
na wanauawa kwa ajili ya kuzishika kwao amri hizi za torati, hasa amri ya kwanza,
ya pili na ya tatu, kabla ya amri ya nne.
Kitu cha muhimu
hapa ni kwamba utii ambao Mungu aliuhitaji ni ule wenye matokeo ya muda mrefu.
Watu waliambiwa kuwaangamiza hata watoto, hata watoto wachanga wa Waamaleki.
Hawa wote walibidi kuuawa. Hili ni andiko la ajabu na lisilo la kawaida. Watu
wangesema ‘ni kwa sababu gani Mungu alifanya hivyo?’ Amri yenyewe ilikuwa ni ya
namna gani. Waamaleki angeweza kuwa tishio na kuwaangamiza Yuda katika siku za
baadae. Mtu wa uzao wa Hagagi, Hamani, ndiye alikuwa adui mkubwa kwenye Kitabu
cha Esta (soma jarida la Ufafanuzi wa Kitabu cha Esta (Na. 63)). Tisho hili kwa usalama wa Israeli linahusiana
pia na nyakati za Mwisho. Sehemu hii inataja kuhusu ufalme wa Masihi kama
tunavyoona kutoka kwenye mwendelezo wa andiko hili.
1Samweli 15:24-29 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya Bwana, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. 25 Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu Bwana. 26 Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la Bwana, Bwana naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. 27 Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. 28 Basi Samweli akamwambia, Leo Bwana amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe. 29 Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute.
Ndivyo ilivyo,
kwamba usimikaji na utiaji mafuta wa kiongozi wa watu wa Mungu utegemee na utii
wake kwa Mungu. Kiongozi yeyote wa watu wa Mungu asiye mwaminifu na mtiifu
kwenye torati ama sheria za Mungu, anapungua vigezo vya kufanya astahili kuwa
na uhalali wa kutawala. Hili ndilo somo hasa linalotokana na andiko hili.
Samweli alimuua Agagi kwa mikono yake mwenyewe na kisha alikata maasiliano yake
na Sauli siku ya kufa kwake (1Samweli 15:35) lakini hakuacha kumuombolezea wala
kuomba. Ndivyo itupasavyo hata sisi pia. Hatupaswi kuacha kuwaombolezea au
kuaombea viongozi wa watu wetu hata kama watakuwa watenda dhambi.
Kisha Mungu
akamwambia Samweli amtie mafuta Daudi. Ndipo na sisi tunakwenda kumsimika kwa
kumweka mbadala mfalme.
1Samweli 16:1-7 Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. 2 Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu. 3 Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako. 4 Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani? 5 Naye akasema, Naam, kwa amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye dhabihu. Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu. 6 Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake. 7 Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.
Sauli alikuwa
mrefu sana kiasi kwamba kichwa chake na mabega yake viliwazidi Israeli wote,
lakini Sauli alikuwa muovu. Hivyo Mungu aliuona moyo na alijua kile
kilichotakiwa kifanyike.
1Samweli 16:10-23 Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. 11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. 12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. 13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama. 14 Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. 15 Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua. 16 Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona. 17 Basi Sauli akawaambia, Vema, nitafutieni mtu aliye stadi wa kupiga kinubi, mkaniletee. 18 Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye Bwana yu pamoja naye. 19 Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe, akasema, Nipelekee Daudi mwanao, aliye pamoja na kondoo. 20 Yese akatwaa punda, wa kuchukua mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, akampelekea Sauli kwa mkono wa Daudi mwanawe. 21 Basi Daudi akamwendea Sauli, akasimama mbele yake, naye akampenda sana; naye akapata kuwa mtu wa kumchukulia silaha zake. 22 Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana ameona kibali machoni pangu. 23 Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.
Daudi alikuwa na uweza au nguvu juu ya mapepo katika Roho Mtakatifu, na kwa jinsi hiyohiyo sisi tunayo nguvu pia dhidi ya mapepo kwa Roho Mtakatifu. Huu ndiyo ulikuwa ujumbe uliokusudiwa kwenye andiko hili.
Daudi alitiwa mafuta awe mrithi stahiki na akawekwa kwenye nyua za nyumba ya mfalme kwenye nafasi au daraja la chini sana ili kwamba aweze kujifunza mbinu za vita na za amani. Alikuwa amepewa Roho wa Bwana ili kwamba aweze kuyafanya mambo makuu zaidi. Na ndipo Daudi alifanywa kuwa kiongozi wa watu katika Israeli kwa mazingira yasiyo ya kawaida.
1Samweli 17:1-11 Wakati huo Wafilisti walikusanya majeshi yao kwa vita, nao wakakusanyika huko Soko, ulio mji wa Yuda, wakatua kati ya Soko na Azeka, katika Efes-damimu. 2 Naye Sauli na watu wa Israeli wakakusanyika, wakatua katika bonde la Ela, nao wakapanga vita juu ya hao Wafilisti. 3 Wafilisti wakasimama juu ya mlima upande huu, na Waisraeli wakasimama juu ya mlima upande huu, napo palikuwa na hilo bonde katikati. 4 Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja. 5 Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa shekeli elfu tano za shaba. 6 Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega; yake. 7 Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia. 8 Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi. 9 Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia. 10 Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane. 11 Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana.
Mtu huyu alikuwa
na urefu wa takriban futi kumi kenda juu kwake, mwenye silaha za kutisha. Ni
vigumu sana kusimama mbele ya silaha zinazoendeleza aina ile ya mtindo wa nguvu
wakati zinaporushwa na kulengwa wewe. Walitiwa hofu. Mfano ashiria wa Goliathi
wa Gathi ni kama mfumo au aina ya sanamu ya nembo ya kidola ya dola ya Babeli paoja
na warithi wake waliofuatia baadae walioonyeshwa kwenye sanamu ya Danieli Sura
ya 2. Huu ni mfano mwingine wa mnyama menye nguvu mwenye kichwa kikubwa. Imani
ile inahusu na mkururu wa dola nyingi na kuangamizwa na Masihi kwenye hatua
zake za mwisho za dola ya wafalme kumi wa nyakati za mwisho, wakati wa lile
jiwe ambalo ni Masihi litakapozipiga kwenye miguu yake. Hiyo ni Danieli sura ya
2. Kwenye tukio hili, Goliathi hapigwi miguuni. Bali anapigwa sawia katikati ya
macho yake, ni sawia kwenye paji lake la uso, mahali ambapo mihuri ya imani
inapigwa. Goliath anahusika na imani za kidini na kwamba kichwa kinabakia kuwa
ni kitu cha msingi cha hadithi hii. Hadithi hii inaendelea hadi kwenye andiko
la 1Samweli 17:12 kana kwamba Daudi hakuwahi kuwa pamoja na Sauli na kwa kweli
hadithi yenyewe inaweza kushabihiana na mchakato usiohusiana. Una mkururu mmoja
wakati unapoanzisha jinsi roho alipochukuliwa kutoka kwa Sauli na kupewa Daudi.
Wakati Daudi alipompokea, alichukuliwa kutoka kwa Sauli na Sauli akateseka, na
Daudi ndipo akafanyika kuwa mwenye nguvu nab ado alipewa jukumu la kuwa ni
mchukua silaha wa Sauli. Alifanyika kuwa mtu wa mkono wa kuume wake. Mkururu
huu unaendelea.
Daudi alikuja
kwenye uwanja wa vita ili kutoa efa ya mahindi na mikate kumi kwa ndugu zake.
1Samweli 17:17-54 Ndipo Yese akamwambia Daudi mwanawe, Haya! Sasa uwachukulie ndugu zako efa ya bisi, na mikate hii kumi, ipeleke upesi kambini kwa ndugu zako; 18 ukampelekee akida wa elfu yao jibini hizi kumi, ukawaangalie, wa hali gani, kisha uniletee jawabu yao. 19 Basi Sauli, na watu wote wa Israeli, walikuwa katika bonde la Ela, wakipigana na Wafilisti. 20 Daudi akaondoka asubuhi na mapema, akawaacha kondoo pamoja na mchungaji, akavitwaa vitu vile, akaenda, kama Yese alivyomwamuru; akafika penye magari, wakati lile jeshi walipokuwa wakitoka kwenda kupigana, wakipiga kelele za vita. 21 Nao Waisraeli na Wafilisti wakajipanga, jeshi hili likikabili jeshi hili. 22 Basi Daudi akaviacha vile vyombo vyake katika mkono wa mlinda vyombo, akalikimbilia jeshi, akafika, akawasalimu ndugu zake. 23 Hata alipokuwa akisema nao, kumbe! Yule shujaa alitokea, yule Mfilisti wa Gathi, jina lake Goliathi, akitoka katika jeshi la Wafilisti, akasema maneno yale yale; naye Daudi akayasikia. 24 Na watu wote wa Israeli walipomwona yule mtu wakakimbia, wakaogopa sana. 25 Watu wa Israeli wakasema, Je! Mmemwona mtu huyu aliyepanda huko? Hakika ametokea ili awatukane Israeli; basi, itakuwa, mtu yule atakayemwua, mfalme atamtajirisha kwa utajiri mwingi, naye atamwoza binti yake, na kuifanya mbari ya baba yake kuwa huru katika Israeli. 26 Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai? 27 Nao watu wakamjibu vivyo hivyo, wakisema, Ndivyo atakavyofanyiwa mtu yule atakayemwua. 28 Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu; na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa? Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi chako, na ubaya wa moyo wako; maana umeshuka ili upate kuvitazama vita. 29 Naye Daudi akamjibu, Je! Mimi nimekosa nini sasa? Je! Si neno kubwa hilo? 30 Naye akamgeukia ili kumwelekea mtu mwingine, akasema naye jinsi ile ile; na watu wakamjibu tena jinsi ile ile kama ya kwanza. 31 Na maneno hayo aliyosema Daudi yaliposikiwa, watu wakamweleza Sauli; naye akatuma mtu kwenda kumwita. 32 Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.
Daudi alikuwa na
akili sana na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye na aliona madhara au kitisho
cha huyu jitu alichokuwanacho kwenye hili jeshi. Walikuwa wanayeyuka mioyo yao
kila siku kwa kuwa hakuna mtu aliyediriki kujitokeza kukabiliana naye. Hili ndilo
lilikuwa tatizo na Daudi aliligundua na alijua kuwa yapasa awepo mtu wa kujitoa
mhanga kukabiliana naye. Hili pia ndilo tatizo letu hata sisi, kwa kuwa
hatuipigi vita imani; kwa kuwa hatulineni neno la Bwana kwa ujasiri mkubwa. Kwa
kuwa sisi idadi yetu haichukui asilimia yoyote kwenye mamilioni, basi watu wetu
hukata tama kwa sababu wao ni wachache mno idadi yao. Yatupasa kushuhudia imani
yetu kwa ujasiri mwingi hata kama tupo wachache, kwa kuwa tunapigana na maadui wa
Mungu aliyehai na wao hawapo hivyo. Haijalishi tu wachache kiasi gani, hatupasi
kuyeyuka mioyo kwa kile tunachokifanya. Hili ndilo fundisho.
33 Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake. 34 Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi, 35 mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua. 36 Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.
Daudi alikuwa na
kusudi na alilijua kusudi la Mungu. Alielewa kwa njia ya Roho Mtakatifu kwamba
hakuna kitakachoyashinda majeshi ya Mungu aliyehai na hakuna kitakacho limudu
hilo.
37 Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe. 38 Ndipo Sauli akamvika Daudi mavazi yake ya vita, akamtia chapeo cha shaba kichwani, akamvika dirii. 39 Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu. Basi Daudi akavivua.
Masharti ya vita
ni kujaribu kwa kupasha moto wa silaha zako kabla hujatoka. Daudi hakuwahi hata
kuijaribu ngao yake. Alikuwa hajaivaa kabisa. Haiingii akilini kuona unakwenda
kupigana na kitu ambacho hujawahi hata kukijaribu bado na wala hujakizoea. Usitoke na kwenda kupigana vita ukiwa na
silaha usizozijua matumizi yake. Mungu ametupa sisi mavazi ya kujikinga na
unaweza kujisomea kuhusu silaha hizo kwenye Agano Jipya. Silaha ya Bwana
imejaribiwa na kuhakikishwa. Daudi aliziacha silaha alizokuwa amepewa na aliichukua
fimbo yake mkononi mwake na akayachagua mawe laini matano kutoka kwenye kijito
na kuyaweka kwenye mkoba wake wa kichungaji. Sasa jambo hili ni la muhimu sana.
fuko wake silaha alizokuwa amepewa nazo gao Daudi hakuchagua kuyapiga majeshi
ya Wafilisti, na mashujaa wa Kifilisti. Hakuchagua kupigana kwa silaha zilizokubalika
na kuruhusiwa za ulimwengu huu. Imani ya Kibabeloni haikuwa inakwenda kushindwa
kwa mfumo wa silaha zilizoruhusiwa na mfumo wa ulimwengu huu. Daudi alitumia
kitu kingine na cha tofauti. Alichukua fimbo mkononi mwake pamoja na mawe laini
matano, aliyoyachukua kutoka kijitoni. Maana yake ashirio iko wazi sana. Fimbo ya
Daudi ni utawala wa Masihi na uweza uliowekwa ndani yake kwa njia ya Roho
Mtakatifu. Mawe malaini tano ya kijitoni ni makanisa matano ya Mungu yanayoifanya
hivyo katika siku za mwisho, yakiwa yamechaguliwa kwa kupitia maji yaliyohai ya
Roho Mtakatifu. Mfuko wa kichungaji ni nguvu za ulinzi za Masihi. Mambo ya
kuyafikiri pale ni yale mawe matano tu kwa kuwa makanisa mawili ya Mungu hayafanyi
hivyo kwenye Ufalme. Makanisa ya Wasardi na Walaodikia yametupwa nje ya Ufalme.
40 Akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti. 41 Huyo Mfilisti naye akamsogelea Daudi na kumkaribia; na mtu yule aliyemchukulia ngao yake akamtangulia. 42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri. 43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake.
Mara tu alianza
kunuizia miungu yake kinyume na Roho Mtakatifu kutoka kwa Mungu aliyehai,
ambaye ka hakika sana kabisa ndiye mlengwa wa vita hivi.
44 Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni. 45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
Sasa hii iko wazi
sana; kwamba Mungu alimpeleka Daudi kwa makusudi na Daudi ananena kwa Roho Mtakatifu.
Daudi anaongea na mtu anayetegemea nguvu zake mwenyewe za kimwili na silaha za
kimwili. Silaha zetu zina nguvu ya kuziangusha ngome na hizi ndizo silaha za
siku za mwisho. Hayo ndiyo mapigano au pambano la siku za mwisho.
46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. 47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.
Huhu ni kijana asiye
na silaha, anayeongea na jitu lenye urefu wa futi kumi kwenda juu na mwanajeshi
aliyefunzwa vizuri, aliye na mbeba silaha wake, ambaye alijiandaa vizuri na
mwenye uwezo wa kumuua Daudi mwenyewe. Ndipo alijitokeza nje dhidi ya watu hawa
wawili. Mmoja wapo alikuwa ni jitu la urefu wa futi kumi na aliyepata mafunzo vizuri
ya kijeshi.
Hapa tunaangalia
idadi ya matatizo. La kwanza ni kwamba tunashughulika na aina ya silaha ya
Daudi. Hakuwa amezoezwa kuvaa au kutumia silaha ya Sauli kwa kuwa silaha za
vita vyetu hazipo sawa na zile za dunia hii. Masihi alikuwa hajafunuliwa bado kwao.
Daudi alikuja kwa jina la majeshi ya Mungu aliyehai. Kuangamizwa kwa nguvu za
mataifa ni sawa na kule kwa nyakati za mwisho. Neno Wafilistimu lililotoholewa
kutoka kwenye neno Pereset au wakazi wa maeneo ya bahari linakuwa pia ni
ndharia iliyohusiana au kufafa na Kitimu ya nyakati za mwisho. Wakitimu
walikuwa ni maadui walioorodheshwa kwenye Magombo ya Bahari ya Chumvi, maarufu kama
the Dead Sea Scrolls. Israeli kwenye karne ya kwanza waliwaona watu hawa kama
wanaokuja wakitokea kwenye merikebu za baharini, yaani wakazi wa maeneo ya
baharini. Majitu walikuwa wamehusiana na Wanefili ambao walikuwa ni matokeo au
uzao wa malaika waasi (soma jarida la Wanefili (Na. 154)). Goliathi wa Gathi alikuwa jitu
na Israeli kwenye karne ya kwanza walielewa kuwa hawa majitu kuwa ni uzao wa
Wanefili. Waliwakilisha imani ya malaika waasi na mikakati yao. Imani iliyobuniwa
na kutungwa ya mapepo. Hivyo, imani hiyo ingeweza kuwekwa kwa matendo ya mfalme
mpya, Masihi. Mawe matano yaliyo ndani ya mfuko a kichungaji ni makanisa matano
yaliyo na sehemu yake kwenye ufufuo wa kwanza wa wafu. Makanisa ya Wasardi na
Walaodikia hayatakuwa na sehemu kwenye ufufuo wa kwanza wa wafu kwa namna
yoyote ile. Makanisa hayo yana watu mmoja mmoja binafsi tu kwenye kundi hilo.
Kanisa la Sardi limekufa na la Walaodikia limetapikwa kutoka kwenye kinywa cha
Mungu. Ni watu mmoja mmoja tu binafsi yao kwenye makanisa hayo ndiye anaweza
kuuingia Ufalme wa Mungu.
Goliathi aliuawa
kwa jiwe moja tu. Tunaona kwamba kutokana na mkururu wa Makanisa, ni hazima
liwe ni la mwisho. Hata hivyo, ujumbe wa malaika wa kwanza ni mchakato
endelevu, ambao unahitimisha au kukamilisha kwenye mamlaka ya nyakati za misho.
Mayokeo yake ya mwisho ya mchakato huo ni kuangamizwa kwa dini ya uwongo ya
Kibabeloni kama tunavyojionea kutoka kwenye mfululizo wa matukio ya ujumbe wa
malaika (Ufunuo 14:6-12).
Ufunuo 14:6-12 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji. 8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake. 9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, 10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake. 12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Moja kwa moja
kutoka na ujumbe wa malaika wa kwanza kutapelekea kuanguka kwa Babeli kama jiwe
kutoka kwenye kombeo ya mfalme wa Israeli.
Nia ya vita hii
kati ya Daudi na Goliathi ilikuwa ni ili kwamba majeshi ya Mungu yaweze kujua
kwamba Bwana haokoi kwa nguvu wala kwa
uweza bali ni kwa roho wangu asema Bwana wa Majeshi (Zekaria 4:6).
Tena licha ya
usemi huu, Daudi hatimaye aliyenda dhambi ya kuwahesabu Israeli (2Samweli 24:1
ff.; 1Nyakati 21:1 ff.). Dhambi hii ilisababisha vifo vya watu 70,000 katika
Israeli. Dhambi ya kuwahesabu majeshi ya Bwana ni dhambi ya kwanza ya uongozi
wa nyakati za mwisho. Siyo tu kwamba ni taifa ambalo limekaliwa kupita wastani
wake na kikosi cha kijeshi. Makanisa ya Mungu katika nyakati za mwisho
yametahesabu majeshi ya Mungu hadi mchakato mchakato ni kutokuwepo kwenye lugha
ya watu wetu – kama tutarudi nyuma kwenye dhana au wazo la kuangamizwa kwa
malaika. Hapa Daudi anamtegemea Mungu. Alimkabili Goliathi na akasema kwamba
anakwenda kumwangamiza na kumuua Goliathi. Imani yake ni kubwa hapa na kwa
kweli anakwenda kumwangamiza. Lakini hatimaye alipokuwa mzee alianza kutegemea
kwenye idadi ya wanajeshi wake kama alivyosema Napoleon: Mungu yupo upande a bataliani kubwa; au alivyosema Stalin: Ni vikosi vingapi alivyonavyo Papa? Kitendo
hiki cha kuyahesabu Makanisa ya Mungu katika nyakati za mwisho ni dhana moja
ileile. Utamalakiji huu na uhesabuji,
kwa tarakimu, kwa kile kinachoitwa ‘matunda’, ni machukizo machoni pa Mungu.
Mchakato huu umepelekea kukaliwa au kujazwa tena na watu walioketi vitini na
sio wanaofundisha, na sio kuwaweka watu kwenye mwili wa kanisa na sio kuwatayarisha
kwa kazi zao. Matokeo yake watu hao wataondolewa sehemu yao kwenye Ufalme wa
Mungu. Watu elfu sabini watakufa na kukabili ufufuo wa pili wa wafu kwa sababu
ya kushindwa huko. Wakumbushao watakabili mchujo kama ngano. Mchakato huo na
habari zake vimefafanuliwa kwa kina kwenye jarida la Upimaji wa Hekalu (Na. 137). Ni habari ndefu na inayohusika.
48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti. 49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.
Ni namna hiyohiyo
kwamba mungu wa Wafilisti alianguka, na ndivyo alivyofanya hata shujaa wao.
Mhuri wa Mungu upo katikati ya macho, na hili jiwe, ujumbe huu wa Mungu aliyehai,
ulikuwa ni kuangamiza mfumo na imani pale walipotiwa mhuri, kwa jina la mungu
wao. Na iliua shujaa wao na
aliangukia paji lake la uso.
50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.
Hiki ndicho kinachotokea
katika nyakati za mwisho. Hatutahitaji upanga na tutayaangamiza majeshi ya
mungu wa dunia hii. Tutawaangamiza mamilioni kwa mamilioni katika nyakati za
mwisho na hakutakuwa na upanga mikononi mwetu.
51 Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia. 52 Nao watu wa Israeli na wa Yuda wakainuka, na kupiga kelele, nao wakawafuata Wafilisti mpaka ufikapo Gathi, na mpaka malango ya Ekroni. Nao majeruhi wa Wafilisti wakaanguka kando ya njia iendayo Shaarimu, mpaka Gathi, na mpaka Ekroni. 53 Kisha wana wa Israeli wakarudi kutoka katika kuwafukuza Wafilisti, wakateka nyara marago yao. 54 Naye Daudi akakitwaa kichwa chake yule Mfilisti na kukileta Yerusalemu; lakini silaha zake akaziweka hemani mwake
Kuna wazo la
maana na muhimu sana hapa. Kichwa cha imani hii kiliondolewa kwa kutumia upanga
wake mwenyewe. Kwa jinsi hiyohiyo Masihi atayashusha hadi chini kwenye bonde la
kukata maneno, majeshi yote ya ulimwengu katika siku za mwisho, na atawaua kwa
silaha zao wenyewe. Mataifa haya yote, moja baada ya jingine, yatashushwa
chini. Majeshi yao yote yatashushwa chini na kuangamizwa.
Tazama, kichwa
kimeletwa hadi Yerusalemu lakini silaha zake ziliwekwa kwenye hema la Daudi.
Yerusalemu haukuwa bado mji wa Sauli. Na kwa kweli hata Sanduku la Agano
lilikuwa huko Shilo na Daudi angeuweka huko Hebroni kabla ya vitu vyote viwili,
yaani maskani na utawala wake havijahamishiwa vyote huko Yerusalemu. Wakati Daudi
alipokileta kichwa cha Goliathi hadi Yerusalemu, alikuwa anatazama mbele
kuelekea kwenye siku zijazo, kwenye ujio wa Masihi, wakati kichwa cha imani na
dini ya Kibabeloni itakapoondolewa na mfumo wa kiutawala, mfumo na imani ya
kidini vitakapopewa Masihi na kila kicha kitakapochukuliwa na kuletwa hadi Yerusalemu.
Utawala wake ungetawala kutoka Yerusalemu. Silaha yake iliwekwa hemani kwake,
kwa jinsi hiyohiyo nao mikuki yake na silaha zake ambazo zilikusanywa kutoka
kwenye vita vya Armagedoni. Mambo haya yote yatachukuliwa na kukwamishwa. Ufafanuzi
wake ni kwamba mambo haya yote yaliyokusanywa yatadumu katika Israeli kwa miaka
saba. Kutakuwa na mali nyingi na za kutosha za kuzitumia nje ya majeshi, wakati
watakaposhushwa chini, ili kuwaacha Israeli aendelee kwa kipindi chote cha Milenia.
Kwahiyo muundo
unakuonyesha kwamba hii siyo historia tu, peke yake inayohusu kijana akiliua jitu
kubwa na lenye vidole kumi kwenye mguu mmoja kwa jiwe la kwenye kombeo. Bali
hii ni habari au hadithi ya Masihi. Ni hadithi ya ufalme uliowekwa na kusimamishwa
imara mikononi mwa Mungu aliyehai na kwamba imani na taratibu hizi, na silaha
ya dunia hii, na vifaa vya kivita ambazo Shetani amewafundisha watu wetu
kuzitumia zitaondolewa. Zitakuwa silaha zao ambazo Shetani amewafundisha watu
wetu wazitumie, ndizo kwa hakika zitauharibu kabisa mfumo huu, na kuwawka watu
wetu chini ya Masihi huko ka watu wetu chini ya Masihi huko Yerusalemu. Uwekaji
wa kiongozi huko Yerusalemu ulikusudia kuonyesha kwamba serikali na mfumo wote
mzima wa Serikali au utawala na wakidini utakuwa huko Yerusalemu.
q