Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[128]
Melkizedeki
(Toleo La 2.0
19950729-19980907-20110618)
Utambulisho wa kiumbe anayejulikana kuwa ni Melikzedeki kila mara limekuwa ni tatizo kwa wanafunzi wengi wa Biblia. Jarida hili linaangalia mapokeo au desturi za kikuhani pamoja na kuonyesha tambulisho tarajiwa na sababu iliyo nyuma ya harakati za mtu huyu. Maana ya ukuhani wa Melkizedeki unaweza kueleweka vyema kutokana na jarida hili.
Christian Churches of God
Email: secretary@ccg.org
(Hatimiliki © 1995, 1998, 2011
Wade Cox)
(tr. 2016)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani
yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe Hakuna malipo
atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu
fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila
kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya
pia yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Melkizedeki
Utambulisho wa kiumbe anayejulikana kama Melkizedeki limekuwa ni somo linalochukuliwa kama la kukanganya kwa zaidi ya miaka kadhaa sasa. Wengine wameulinganisha utambulisho wa Masihi kwa Melkizedeki; wengine wamemjumuisha yeye na mababa wa zamani wa imani. Kutenganisha uwezekano wa utambulisho huu yatupasa kutathimini maandiko yanayofanana na kushabihiana na mtiririko wa kihistoria uliopo ambao aliishi kwao. Matokeo muhimu ya uwiano ya kuja na kuzaliwa kwa Masihi pia ni jambo linalohitaji kutiliwa maanani, iwapo kama, kwa mfano, mtu atafananisha na utambulisho wa Masihi. Kwa maneno mengine, kama mtu atang’ng’ania kusema kwamba Melkizedeki ni Yesu Kristo, inapasa ipimwe dhidi ya maandiko yanayofanana na madhara kwa wokovu wa mwanadamu kwa tukio kama hilo la ukuwili. Kipindi hiki kilikuwa pia ndani ya kipindi zama cha mababa wa imani walioishi baada ya gharika kuu ya ulimwengu wote. Hakuna shaka maana nyingine yapasa itoholewe kutoka kwenye vipaumbele.
Kipindi zama cha baada ya gharika kilishuhudia ulimwengu ukiwa na lugha na usemi mmoja na ukiwa chini ya kuhani mmoja. Mtazamo wa Kiyahudi ulikuwa kwamba kuhani huyu alihudumu huko Salemu chini ya Melkizedeki. Alama au utambulisho wa Melkizedeki umekuwa ni utata. Melkizedeki, kwa mujibu wa Midrash, alionyeshwa na Shemu (Rashi: soma kitabu cha Soncino).
Kwa hiyo aliitwa hivyo kwa kuwa alikuwa mfalme (melech) wa mahali palipokuwa mashuhuri kwa utakatifu wake (tsedek) [kwa mujibu wa Abraham ibn Ezra] N[achmanides] sawasawa kabisa: Alitawala mahali ambapo siku moja lilijengwa Hekalu ndani mwake ambamo kulikuwa na Maskani ya Takatifu ambayo iliitwa tsedek. Midrash inadondoa neno hili kuwa linamaanisha Yerusalemu kwa ujumla, kama ilivyoandikwa, Haki na Utakatifu ulikuwa ndani yake (Isaya 1:21) (kwa mujibu wa kitabu cha Ufafanuzi cha Soncino hadi Mwanzo 14:18).
Melkizedeki alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. Nachmanides anadumu kuamini kwamba ilikuwa ni:
Abrahamu tu ndiye aliyejua kwamba hiki ndicho
kilichompelekea yeye ampe zaka yake. Aliye juu Sana maana yake ni aliye juu ya miungu yote (N) (Soncino).
Rashi anasema na
kuamini kwamba mkate na divai alizotoa Melkizedeki na kumpa Ibrahimu vilikuwa ni
viburudisho kutokana na uchovu wa mapiganoni akawaacha huru wafungwa. Kw hiyo
alionyesha kwamba alimzaa Ibrahimu na asione uchungu kwa kumtoa mwanae achinjwe
(viz. Cherdorlaomer, etc.) (soma kitabu cha Soncino).
Mtu huyu ni wa muhimu pasi kujali mstari wa uzao wa waliohusika. Ni muhimu sana
kupewa heshima ya moja kwa moja ya uzao ya walipatwa na madhira. Maana ya mkate
na divai aliyopewa Ibrahimu kulihusiana moja kwa moja kwa maana ya Mkate na
Divai ambayo ilikuwa adilifu kwenye Mkate na Divai iliyoanzishwa na Masihi
kwenye Meza ya Bwana. Tukio hili liliangalia mbele kwenye mfano wa kuwepo kwa
Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa inahudumu kwenye ukuhani mpya wa mfano wa
Melkizedeki kama ulivyoanziashwa na Masihi.
Ukweli wa kwamba
Melkizedeki aliweka taswira ya tukio hili hailazimu kumaanishi kuwa yeye ni
Masihi. Kwa kweli, kama angekuwa hivyo, kuna sababu zote za matatizo kwenye
dhana ya sadaka isiyo na doa au dhambi ya Masihi. Je, yeye alizaliwa? Alikuwa
ni wa jinsia ipi, ni mwanaume? Na kama ni hivyo, je, alikuwa ndiye yule aliyezaliwa
na mwanamke bikira? Kwa hakika hakuwa ni wa mstari wa uzao wa Daudi. Na kama
alikua ni malaika, hiyo itakuwa ina maanisha nini na utaala wa Salemu kwa
wakati ule? Je, ulikuwa ni ukuhani wa namna gani ule? Kwa nini ukuhani wa
malaika haukuandikwa mahali popote? Ni nini matumizi aliyokuwanayo malaika kwa
zaka za vita? Na kama hakufa, basi tutasemaje kuhusu maandiko ya Yohana kuhusu
fundisho la Mpingakristo? Matatizo ya msingi yalielezewa kuhusu uhusiani wa
Masihi na Melkizedeki ni ulivyo mkubwa.
Somo au fundisho
kuhusu Melkizedeki mara nyingi halieleweki sana, hasa ni kwakuwa mtiririko na
maana za hadithi yenyewe haieleweki sana. Kanisa la Mungu, kwa kipindi cha
zaidi ya miaka elfu mbili, haikuwashikilia mtazamo usioeleweka kwenye somo au
fundisho, na ushauri kuhusu suala la hayakuonekana kuwa kama ni suala la
kimafundisho, au ni kitu muhimu kwa wokovu. Kwa hakika, hadi kwenye hatua
zisizovumilika ya Kanisa kwenye Krne hii, suala halijawahi kuonekana kama
kuhalalisha uthibitisho na uimara wa kimafundisho. Itasaidia kutathimini
historia ya kuijenga historia.
Mwanzo 11:1-32 1 Nchi yote ilikuwa na
lugha moja na usemi mmoja. 2 Ikawa watu waliposafiri
pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome
moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. 4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele
chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi
yote. 5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara
waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 Bwana akasema,
Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza
kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili
wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana
akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo
ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya
waende usoni pa nchi yote.
Hapa tunaona kutawanyika kwa watu kutokana na mfumo uliokua umewekwa huko
Babeli, chini ya serikali iloyoanzishwa na Nimrodi huko na Akkadi, Ereki na Kalne.
Kutoka huko aliujenga Ninawi, Rehobothi na Kala (Wanzo 10:10-11). Kuhani wa
Mungu hatahivyo, alikuwa Shemu, akiwa ni mwana wa Nuhu. Nuhu aliishi miaka 350 baada
ya gharika kuu (Mwanzo 9:28) na alifariki akiwa na umri wa miaka 950 (Mwanzo
9:29). Shemu alikuwa ni kiini au mtumainiwa aliyewekwa kuhudumu kipindi cha
baada ya gharika kuu.
10 Hivi ndivyo vizazi vya Shemu;
Shemu alikuwa mtu wa miaka mia akamzaa Arfaksadi miaka miwili baada ya gharika.11 Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano,
akazaa wana, waume na wake. 12 Arfaksadi akaishi miaka
thelathini na mitano, akamzaa Sela. 13 Arfaksadi
akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na
wake. 14 Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi.
15 Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na
mitatu, akazaa wana, waume na wake. 16 Eberi akaishi
miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. 17 Eberi
akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, waume
na wake. 18 Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa
Reu. 19 Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia
mbili na kenda, akazaa wana, waume na wake. 20 Reu
akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. 21 Reu
akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, waume na
wake. 22 Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa
Nahori. 23 Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka
mia mbili, akazaa wana, waume na wake. 24 Nahori
akaishi miaka ishirini na kenda, akamzaa Tera. 25 Nahori
akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia na kumi na kenda, akazaa wana, waume na
wake. 26 Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na
Harani. 27 Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera
akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. 28
Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani,
katika Uru wa Wakaldayo. 29 Abramu na Nahori
wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori
aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska. 30 Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. 31 Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani,
mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika
Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko. 32 Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera
akafa katika Harani
Kuna idadi kadhaa
ya vipengele vya muhimu vinavyoibuka kwenye andiko lililoko kwenye Mwanzo 11. Cha
kwanza kinahusiana na umri wa Shemu na wengine. Kutoka kwenye maandiko
tunaanzisha tarehe au vipindi vya baada ya gharika kuu, tarehe za kuzaliwa na
kufa kwao. Miaka yenyewe ni ya kipindi chenye urefu mkubwa sana. Zama hizi
maalumu hazikubaliki kuwa ni vipindi vya wazi sana kwa nyakati za sasa. Kwa
kweli, kudhania kwamba nyakati maalumu hizi ni za kweli ni za kukaribisha kebehi.
Hata hivyo, waamini kuona kwa macho yao hawawezi kuwanayo wakati wote kwa namna
zote mbili. Kama Biblia ni ya kweli kihalisia na Melkizedeki alikuwepo ndipo
vipindi hivi maalumu na vya aina yake navyo ni vya kweli pia na Shemu ndiye
mlengwa au masimamizi. Hadithi za mataifa yanayoizunguka Kanaani huko Mashariki
ya Kati ambayo yalionyesha taswira pia hadithi zihusuzo kuanzishwa kwa miji.
Tabia hizi zilipaswa pia zionyeshwe mwelekeo kwenye hadithi za mataifa, huenda
kwa majina mengine. Yapasa ikumbukwe kwamba majina yalikuwa na maana na majina
waliyopewa mababa wa imani wa zamani ambayo sio lazima sana yafanane na yale
waliyojulikana kwayo kwenye nchi zingine. Kwa mfano, Nuhu alijulikana kwenye
Zama Maalumu ya Gilgamesh kama Uta-Napishtim
(aliitwa kuwa wa mbali sana) (soma
kitabu cha Budge, cha: Babylonian Life
and History [Maisha ya Wababeloni na Historia];, 2nd edn., London, 1925,
pp. 92ff.).
Kuna miingiliano
mikubwa sana zilizoko kwenye hadithi au ngano za Kimisri kuhusiana na hadithi
au habari ya Shemu kwenye nafasi yake kama muangamizaji wa dini potofu na
kikengeufu ya Wamisri. Mambo haya yote yanakanganya sana kwa kazi hii na
inapasa yashughulikiwe na mahali penginepo. Hadithi au ngani wa Kimisri ambazo
zinamwonyesha Shemu ni hadithi ya Typhon, kaka yake Osiris, ambaye aliiamuru
serikali ya Misri na kujaribu kuanzisha mtindo wa Kimisri kuwa ni kitu cha
kuigwa na kutawala ulimwenguni kote. Typhon anaonyeshwa kwa mwonekano wa kama
mtenda maovu aliyepangilia mbinu chafu na hila kwa washirika sabini na wawili.
Pamoja nao, alimkinga au kumlinda Osiris kwenye kifua kwa udanganyifu na
kumtupia kwenye mto Nile. Maana
yake hapa ni kwamba tarakimu hii ya sabini na mbili inahusiana na Baraza la
Utawala la Mungu.
Baraza la Sanhedrin lilikuwa la jumla ya watu sabini na mbili; hata hivyo, mara zote lilikuwa na wastani wa watu sabini na mbili kwa ujumla na baadae walijumuisha na Nasi. Masihi aliwatuma wale sabini baada ya kuwachagua na kuwateua (Luka 10:1). Walirudi na furaha, wakisema kwamba hata mapepo wanatutii (Luka 10:17). Mamlaka yalihamishiwa hapa kwenye Kanisa. Kwa matukio yote mawili, kwenye andiko hili limeorosheshwa kwenye makusi ya Marshall’s Interlinear kutoka kwenye maandiko ya Nestles kama hebdomekonta [duo] au sabini [na mbili]. Kwa hiyo, idadi hii ya sabini ilijulikana kuwa iliendana na nyongeza ya wawili, na kufanya jumla ya watu sabini na mbili. Hili kwa kweli ni Baraz la Elohim. Kwa hiyo, ngano au hadithi ya Osiris na Isis inamuweka Typhon kuwa ni kichwa cha Baraza hili lakini akiwa muovu kama adui wa Misri. (soma kitabu cha Bullfinch’s Mythology, Avenel Books, New York, 1979, pp. 293ff.). kwahiyo Typhon aliweza kusemekana kuwa anashikilia mahala la Kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana akiwa ni kichwa cha Baraza. Alionekana pia kufanana na Melkizedeki. Shemu anaonekana pia kwenye kundi hili. Hata hivyo, ng’ombe dume Apis anahusianishwa pia na Osiris, aliyeaminiwa na kuchukuliwa pia kuwa ni udhihirisho wa roho ya Osiris, na kujihamisha yenyewe hadi kwa kila mrithi Apis. Kwahiyo umaarufu umefungamanishwa kwenye hadithi au ngano za dume la ng’ombe linalichinjwa na ambayo ni dini potofu za kisirisiri. Wote wawili, yani Shemu ambaye ni kama mrithi wa Nuhu na wa dunia mpya, na Masihi, wana uhusiano unaofanana kwenye hadithi hizi. Kwa hiyo, Melkizedeki angeweza kuonekana akiwa ni kama anahusiana na wote wawili, Shemu na Masihi. Imani ya kiyahudi ilimuona yeye kama Shemu kwa sababu ya muonekano wa moja kwa moja. Waessene yawezekana, na kwa kweli, walifanya, kumchukulia kimfano yeye kama Masihi na Mikaeli.
Shemu aliishi baada ya gharika kuu kwa miaka 502 na maisha yake yana maashirio ya utawala kwa mataifa. Tumeandika jedwali kama ifuatavyo:
Mababa |
Umri
wa kumzaa motto |
Kuzaliwa |
Kufa kwake kwenye miaka ya kabla ya gharika kuu |
Shemu |
100 |
|
Gharika + 502 |
Arfaksadi |
35 |
Gharika + 2 |
Gharika + 440 |
Shalaki |
30 |
Gharika + 37 |
Gharika + 470 |
Eberi |
34 |
Gharika + 67 |
Gharika + 531 |
Pelegi |
30 |
Gharika+101 |
Gharika + 340 |
Reu |
32 |
Gharika+131 |
Gharika + 370 |
Serugi |
30 |
Gharika+163 |
Gharika + 393 |
Nahori |
29 |
Gharika+193 |
Gharika + 341 |
Tera |
70 |
Gharika+222 |
Gharika + 427 |
Harani Nahori Abramu |
|
Gharika + ? Gharika + ? Gharika+352 |
Kabla ya Gharika + 296. |
Mgawanyo wa mataifa ulitokea wakati Ibrahimu alipokuwa na umri wa miaka 48, alipokufa Pelegi miaka 340 baada ya gharika kuu (kwa mujibu wa kitabu cha Seder Olam Rabbah, Ch. 1).
Abramu (Ibrahimu) aliondoka Harani baada ya kifo cha Tera kipindi cha baada ya Gharika + 427 (mwaka 1921 KK kwa MT). alikuwa na umri wa miaka sabini na tano (Mwanzo 12:4). Hatuna uhakika kama mababu walikuwa wangali hai bado wakati alipokufa Tera na uingiaji wa Abramu huko Kanaani walikuwa Shemu, Arfaksadi, Shalaki na Eberi. Shemu alikuwa ni mkubwa wa kuzaliwa. Kwenye Mwanzo 9:26, Yahova (au Yehova) anatajwa kuwa ni Mungu wa Shemu, na Yafeti aliyeishi hemani mwake. Shemu ndiye anayebarikiwa hapa ingawa Yafeti ndiye mkubwa (Mwanzo 10:22). Kwa hiyo, Shem ndiye kuhani wa Mungu Akiye Juu Sana kipindi cha Ibrahimu. Mgawanyo wa wengine haujulikani, lakini Shemu aliwazaa Arfaksadi na Elamu na (ambao walijiengua baadae na kujitokeza kuwa Waashuru). Ufalme wa zamani wa Elamu, wakati ulipoungana na falme zingine, vikaunda chimbuko la dola ya Waashuru.
Kuhamahama kwa makabila kunaashiria kwamba mgawanyo wa mataifa kwenye miji na maeneo kunapunguza uwezekano wa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana huko Salemu kuwa ni huyu Shemu, au Arfaksadi, aliyepewa yanayojulikana kuwa ni makazi ya wana wengine. Arfaksadi alifariki kwenye mwaaka baada ya Gharika wa + 440 (1908 KK kwa hesabu ya miaka ya MT) kwa hiyo ni kama tu kwamba mababu walikuwa wangalipo bado na mkubwa ni yule aliye wa tofauti nao au aitwaye Mfalme Wangu Mtakatifu, ingawaje Salaki au
Eberi wana uezekano huo bado. Shemu ameitwa ni baba wa wana wote wa Eberi (Mwanzo 10:21). Hivyo inawezekana kwamba neno Waebrania lilienea mbali na Waisraeli hadi kwa watu wengine waliohusiana nao. Hili ni fundisho kwa haki yake yenyewe.
Baraka za Ibrahimu alizopewa na Melkizedeki kwenye Mwanzo 14:20 zinaelezwa (na Rashi) kuwa zilikuwa ni Baraka za kwanza kupewa Ibrahimu kwa kitendo hiki cha kupigana vita, na kisha Mungu kwa mumsaidia kwake yeye. Ukweli wa kwamba Ibrahimu alitoa zaka yake vyote alivyokuwanavyo unaonyesha kwamba uzao wake wangetoa zaka kwa makuhani (kwa mujibu wa Nachmanides). Zaka ilikusudiwa kuwa ni kama sadaka ya shukurani kwa Mungu, na kuhani pekee aliyestahili kuzipokea ni Melkizedeki. Tafsiri ya kimapokeo ya Kiyahudi, kwa hiyo, ilikuwa ni kwamba Melkizedeki alikuwa ni Shemu na kwamba huduma ya kikuhani ya baada ya gharika iliwekewa makao yake makuu huko Yerusalemu.
Melkizedeki kama
Masihi
Madai ya kwamba Masihi alikuwa ni Melkizedeki yanapotosha usahihi wa kilichokusudiwa na maandiko ynayotanabaisha mstari wa vizazi. Kulikuwa na mtazamo halisi wakati wa Kristo kwenye baadhi ya madhehebu ya Kiyahudi, kama tunavyoambiwa kutoka kwenye Gomgo zilizogunduliwa kwenye Bahari ya Chumvi maarufu kama the Dead Sea Scrolls, kwamba huyu Melkizedeki alikuwa ndiye Masihi. Mtazamo huu pia ulijumuishwa na dhana ya kwamba Masihi alikuwa pia ni Malaika Mkuu Mikaeli. Mtazamo wa kwamba Melkizedeki alikuwa Masihi yaonekana kuwa umetuama kwenye ukweli wa kwamba Masihi alipasa aje kutenda mambo mawili. Hii inaweza kuwa imeelezewa na idadi kubwa ya unabii, lakini la msingi zaidi ni huduma ya kuhani mkuu katiku ya Upatanisho, ambapo kulikuwa na ukuwili wa kimavazi, ukiwakilisha huduma za kikuhani nay a kusamehe dhambi na maovu yote kutoka kwenye mavazi ya hariri, na kubadilishwa kwa kuhani mkuu na kuwa wa huduma ya kifalme hapo mwishoni, kukimaanisha pia mfalme Masihi. Kwa hiyo ujio wa kwanza ulikuwa ni wa kikuhani na wa pili ulikuwa wa mfalme Masihi. Yuda ilikuwa chini ya kongwa la Warumi na walimhitaji mkombozi. Hivyo huenda wengine waliona kuwa ndani ya Melkizedeki kuna huduma ya kuhani. Masihi alitabiriwa kuhani baada ya aina ya Melkizedeki kutoka kwenye Zaburi 110:4.
Zaburi 110:1-7 Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako. 2 Bwana atainyosha toka Sayuni Fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako; 3 Watu wako wanajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako. 4 Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki. 5 Bwana yu mkono wako wa kuume; Ataseta wafalme, Siku ya ghadhabu yake. 6 Atahukumu kati ya mataifa, Ataijaza nchi mizoga; Ataseta kichwa katika nchi nyingi. 7 Atakunywa maji ya mto njiani; Kwa hiyo atakiinua kichwa chake.
Kutoka kwenye aya
ya 1 ya Zaburi tunajua kwamba ni Masihi anayetajwa. Kuchaguliwa kwake hapa ni
kwa kuwa kuhani milele baada ya kuwa wa mfano wa Melkizedeki. Haikusema kwamba
Masihi ni Melkizedeki.
Kutokana na gombo
za Dead Sea Scrolls (DSS) (Damascus Rule [Sheria
za Damascus] VII hususan pia kwenye maganjo yaliyopatikana pangoni [esp.
also the fragment from cave IV]) tunajua kwamba Masihi alikuwa na marejeo mawili;
Masihi wa Haruni (au Masihi kuhani) na Masihi wa Israeli (au Masihi mfalme). Gombo
hizi za DSS jamii iliamini kwamba walikuwa ni Masihi mmoja (tazama kenye kitabu
cha Vermes, The Dead Sea Scrolls in
English, p. 49 kwa kuyajadili maandiko haya).
Gombo hili la DSS
limetoa mkururu wa madondoo kumi na tano kutoka kwenye pango la XI juu ya
Melkizedeki. Yalichapishwa mwaka 1965 na A.S. van der Woude. Maandiko yenyewe
yapo kwenye aina ya kazi ya wachimbuzi ya madrashi ambayo kwamba utangazaki wa
uhuru kuwatangazia mateka katika siku za mwisho (Isaya 61:1):
… inaeleweka kama
kuwa sehemu marejesho ya jumla ya raslimali kwenye mwaka wa Jubile [Mambo ya
Walai 25:13], iliyoonekana kwenye Biblia [Kumbukumbu la Torati 15:2] kama msamaha
wa madeni. Mkombozi wa kutoka mbinguni ni Melkizedeki. Anayetambulika kama
malaika mkuu Mikaeli, yeye ni kichwa au kiongozi wa ‘wana wa Mbinguni’ au ‘miungu
wa Haki’ ns inatajwa kama elohim na el. Maneno haya ya Kiebrania kwa kawaida
humaanisha ‘Mungu’, lakini kwa maana halisi maalumu mapokeo ya Kiyahudi pia yanamwelezea
elohim kama kimsingi sana anachukuliwa kama ‘mwamuzi’. Hapa Melikizedeki
anaonekana kama anasimamia Hukumu ya mwisho na kuhukumiwa kwa mshirika wa
mapepo, Beliali/Shetani, Mkuu wa Giza, mahali pengine pia anaitwa Melkiresha’
[soma pia kitabu cha Vermes, ibid., pp. 253,260]. Tukio kuu la ukombozi
linatarajiwa kutokea katika siku ya Upatanisho mwishoni mwa mzunguko wa Yubile ya
kumi. Maandiko haya asilia yanaonyesha mwanga wa muhimu siyo kwenye umbo la
Melikizedeki tu alivyoandikwa habari zake kwenye Waraka kwa Waebrania sura ya vii,
bali pia kwenye mwendelezo wa dhana ya Masihi kwenye Agano Jipya kwenye Ukristo
wa kwanza. (Kuhusu umasihi na huduma zake soma kwenye kitabu cha G. Vermes, cha
Jesus the Jew [Yesu Myahudi], London,
1973, pp. 129-59, 250-56)... Mwaka huo wa Yubile [kila mmoja wenu]mtairudia
kila mtu milki yake. [Walawi 25:13]; na hivyohivyo, Na jinsi ya maachilio ni hii, kila
mkopeshaji na akiache alichomkopesha mwenziwe, wala asimlipize mwenziwe wala
nduguye; kwa kuwa imepigwa mbiu ya maachilio ya Bwana [umetangazwa]. [Kumbukumbu
la Torati 15:2]. [Na utatangazwa kwenye] mwishoni mwa siku kuhusu watumwa kama
[Alivyosema, Kuwatangazia uhuru
waliofungwa [Isaya 61:1]. Tafsiri yake ni
kwamba Yeye mwenywe] atawaunganisha kwa Wana wa Mbinguni na kwenye urithi wa
Melkizedeki; [kwa kuwa atapiga] [kura] zao akijumuisha mahala pa Melkizedeki,
atakayewarudisha wao huko na atawatangazia wao uhuru, na kuwasamehe [makosa
yao] waliyoyatenda kwa maovu yao yote (Vermes, ibid., p. 266).
Na kwa hiyo
inaonekana kwamba Melkizedeki alikuwa anachukuliwa kuwa ni Malaika Mkuu Mikaeli
na kwamba alikuwa ni Masihi pia ambaye amepewa mamlaka ya kuhukumu. Hii imetuamanishwa
kwenye andiko la Zekaria 3:1-10, linaloonyesha pia upinzani wa Shetani kwenye mchakato
huu. Mtu huyu pia alijulikana, kutoka kwa hii, kuwa ni Elohimu anayewahukumu
watakatifu wake Mungu, kama ilivyoandikwa kwenye Zaburi pale iliposema kwamba:
ELOHIM [Mungu] asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu. [Zaburi
82:1]. Na ilikuwa kuhusu yeye ambaye alisema, (Kusanyiko la mataifa na
likuzunguke, Na juu yake uketi utawale. ELI
(Bwana) atawaamua mataifa, [Zaburi 7:7-8]. Pia kwa pale aliposema, [Hata lini
mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya?. Selah [Zaburi 82:2], tafsiri yake kuhusu Shetani na roho za kura
yake [yeye] alieasi kwa kuziachiliambali sheria za Mungu kuzifanya…Na
Melkizedeki atalipa kisasi kwa kisasi cha hukumu ya Mungu…na [atawatoa kutoka
kwenye mikono] ya Shetani na kutoka kenye mikono ya [roho za] [kura] yake. Na
‘miungu yote [ya Haki’] watakuja kumpa msaada [ili] kushuhudia [kuangamia] kwa
Shetani....(kutoka kwenye kitabu cha Vermes, p. 267).
Isaya 52:7 inatumia neno elohim kwa maana ya ujio wa Masihi huko Sayuni (soma
Waebrania 12:22-23).
Inaonekana kutoka kwenye maandiko ya Vermes kwamba
hakukuwa na shaka kwamba maandiko yanayotajwa yalikuwa ya Masihi. Hakukuwa na
shaka pia kwamba Shetani alipewa kazi ya nguvu kwenye hukumu. Neno uwingi wake linatumika kuonyesha
mgawanyo wa kazi za nguvu takatifu, kwa mujibu wa mchakato wa uliopatikana Hekaluni,
wa majukumu yote na vipindi vya kazi kwa kura au kwa uwingi. Baraza la miungu
kwa hiyo wanaonekana kuwa ni kama wateule na Malaika watiifu ambao wamekwishapewa
uweza. Kuonekana kwa Melkizedeki kuwa ni kama Masihi ndiko kulikoonekana ni
kama kuwa na nguvu na mashiko sana kulikopelekea kuishawishi Jumuia inayoamini
yaliyo kwenye Gombo la Bahari ya Chumvi wakati wa Kristo, na uhusiano
unaokutikana kwenye Kitabu cha Waebrania. Uwiano wa kwenye Kitabu cha Waebrania
hata hivyo, inachukuliwa kutoka kwenye andiko la Waebrania 7:6-8.
Waebrania 7:6-8 Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa
hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi. 7 Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na
mkubwa. 8 Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa
hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yu hai.
Andiko hili
linaonyesha kwamba mtu huyu alitajwa kama ni mtu asiyekuwa na mstari wake wa
uzao. Haijadaiwa kwamba hakuwa na uzao.
Tofauti imefanywa
kwenye andiko hili, hata hivyo, kwamba zaka zilipokelewa na mtu mwenye damu na
mwili. Hapa inadaiwa kwamba zilipokelewa na mtu ambaye ilishuhudiwa kwamba
anaishi, huu ni msingi wa uhusiano wa andiko hili na Masihi. Hata hivyo, Waebrania
7:11 inasema wazi kabisa kwamba Masihi alikuja kama kuhani mwingine.
Dhana ya kuishi
inaweza kutokana na Roho Mtakatifu aliyewapa uzima mababu hawa, kama
alivyofanya kwa watu wa nyumbani mwake Daudi. Kwa hiyo, andiko lililo kwenye
Waebrania 7:8 linaweza kuonyesha kuwa linataja nafasi ya Roho Mtakatifu kwa
Melkizedeki kama ni mmoja wa wateule. Sio lazima kwamba andiko hili liwe
linamhusu Masihi.
Waebrania 7:11 Basi, kama ukamilifu ulikuwapo
kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na
haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe
kwa mfano wa Haruni?
Kwa hiyo, kubadilishwa
kwa ukuhani kulihusiana pia na kubadilika kwa sheria. Hivyo, Melkizedeki
alikuwa ni wa aina yake ambaye alianzishwa tena kwa Masihi na kwa mteule.
Ukuhani wa Melkizedeki
ni sehemu ya ahadi ya Mungu.
Waebrania 6:17-20 Katika neno hilo
Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake
yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; 18 ili
kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi
kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini
yale yawekwayo mbele yetu; 19 tuliyo nayo kama nanga
ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, 20 alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa
kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki
Hapa Masihi
alifanyika kuwa kuhani wa milele baada ya aina ya Melkizedeki. Hakuonyeshwa
kama kuhani. Yeye ni Kuhani Mkuu milele baada ya hapo. Kwa hiyo, Melkizedeki
alianzisha utaratibu. Jesu alikwenda akiwa kama mtangulizi kwa niaba yetu. Kwa
maneno mengine, yatupasa sisi pia kuwa makuhani wa aina hiyo.
Waebrania 7 inaonyesha
uhusiano wa Melkizedeki na ukuhani.
Waebrania 7:1-28 Kwa maana Melkizedeki huyo,
mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa
akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya
kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena,
mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
.
Andiko hili linaelezea
kwamba jina Melkizedeki linamaana zote mbili, yaani mfalme wa Salemu, au mfalme
wa amani. Uelewa wa Kiebrania kwa mujibu wa watu wote wawili, Milik na Vermes ni
kwamba neno Melkizedeki maana yake ni Mfalme
Wangu ni wa Haki (au Utakatifu) na ni mfalme wa Jeshi la nuru. Jina la
Shetani ni Melkiresha’ maana yake ni Mfalme
Wangu ni Udhaifu (soma utunzi wa
J.T. Milik, wa Jarida la Masomo ya Kiyahudi
[Journal of Jewish Studies], 1972, pp. 126-135 na pia utunzi wa Vermes, op.
cit., pp. 252-253). Hakuna shaka kwamba tunaelezea kuhusu vita vya Shetani
dhidi ya Masihi vitakavyotikea katika nyakati za mwisho kwa mtazamo wa Gombo la
Bahari ya Chumvi au DSS.
hana
baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai
wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Anaaminika kuwa
hakuna na baba wala mama na asiye na wazazi (apatoor, ametoor, agenealogetos). Hana wala mwanzo, wala mwisho wa
siku zake wala misho wa maisha yake, lakini anafanana na Mwana wa Mungu na anaendelea
kuwa kuhani milele. Mtazamo wa kimasihi wa andiko hili unaonekana kutuama
kwenye mawazo ya kubuni kwamba hakuwa na uzao na kwamba alikuwa ni wa milele.
Na kwamba basi alikuwa ni Masihi. Andiko linasema kwamba alifafana na Mwana wa
Mungu. Halisemi kwamba alikuwa ni Mwana wa Mungu. Neno lililotumika ni aphomoioo: kufanana kwa ukaribu zaidi,
au kufanya ifanane au kufananisha. Kwa hiyo, alifanywa kuwa kama Mwana wa
Mungu. Lengo ni sawa tu na kuwepo wa kiumbe huyu, akiwa ni mmoja wa mababu
muhimu na mashuhuri wa imani, alithibitika kuwa ni kama Mwana wa Mungu, kwa
kuwa wote alikuwa ni wateule, katika roho, na akafanyika kuwa kuhani wa aina
ambayo ilichukua nafasi ya Haruni hata ingawaje ukuhani ule wa Haruni ulikuwa
haujawepo bado. Andiko linasomeka kwamba alibakia
kuwa kuhani wa milele {tazama kamusi iitwayo Marshall’s Interlinear). Neno kuhani
aliyeendelea kuhudumu milele limetafsiriwa kimakosa ili kumaanisha uzima tele
au uzima endelevu. Hili sio tatizo zaidi ya kuwa tu kwa maana hiyohiyo ni kama
wateule wanavyitwa waliolala mauti.
Maana ya maandiko
haya yameainishwa hapo chini, kwa kuhusianisha na sharia zinazotumika kwenye
huduma ya kikuhani.
Basi,
angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu,
alimpa sehemu ya kumi ya nyara. 5 Na katika wana wa
Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao,
yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya
Ibrahimu. 6 Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa
kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye
aliye na ile ahadi.
Andiko hili linasema
pia kwamba mtu huyu pasi kuhesabia wazazi
kutoka kwao (soma kamusi ya
Marshall’s Interlinear) alipokea zaka kutoka kwa Ibrahimu. Hayasemi kwamba
hakuwa na wazazi.
Wala haikanushiki
kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa. 8 Na hapa wanadamu wapatikanao na
kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yu hai.
Andiko hili ni
andiko muhimu sana kutokana na madai kwamba Melkizedeki hakuwa mwanadamu. Ni
madai kama hayohayo yamefanywa na wateule. Hawafi bali wanalala mautini (1Wakorintho 15:6,18).
Tena
yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi
alitoa sehemu ya kumi; 10 kwa maana alikuwa
katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye. 11
Kitendo cha kumpa
zaka kuhani kilikuwa kinaonyesha kwamba sharia zilizo kwenye torati ya Mungu
zilikuwepo na zilikuwa zinaendelea, na kwamba hazikuanzishwa na Musa na
makuhani Walawi.
Basi,
kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria
kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa
Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?
Hapa Masihi
anaonyesha wazi sana kuwa ni kama kuhani mwingine wa mfano wa Melkizedeki.
Hakuna undani wala uhusiano wowote hapa unaoonyesha kwamba Melkizedeki alikuwa
ni kiumbe huyu huyu. Wakayi hili likiwa ni kama lenyewe ndipo kunakuwa na shaka
kisodo kwamba mwandishi wa waraka kwa Waebrania basi ungekanganya mwelekeo
hasilia. Alichukuwa anajaribu kukifanya ni kusisitiza uhisiano uliopo kati ya
Masihi na Melkizedeki, kwa kuwa inaonekana kuwa ni suala muhimu kwamba matarajio
ya madgehebu ya dini ya Kiyahudi yaliyokuwepo katika karne ya kwanza yaliwategemea
wote wawili, yaani kwamba Mikaeli ni ana haiba zote mbili, yaani kwamba ni
Masihi na Melkizedeki. Waraka kwa Waebrania ulifungamanisha uhusiano ndani ili
kuonyesha kwamba unabii ulikuwa umetimia kwa Masihi, kuwa ni kama kiumbe aliye
wa mfano wa Melkizedeki, na mtangulizi wa huduma ya kikuhani wa wateule wa aina
hiyo. Utaratibu au mfano wake ulikuwa ni kwamba hakuzaliwa na wala hakuna na
wazazi kwa kuwa wateule walipaswa kuchaguliwa kutoka kwenye makabila yote ya
Israeli na hatimaye kutoka kwa Wamataifa, ambao wenyewe amejiunga kwenye
makabila hayo wakihudumu kama makuhani. Kwa hiyo, mstari wote mzima wa wateule
ulikuwa usio na mama, wala baba, wala uzao kwenye ukuhani. Kigezo cha
kuchaguliwa hakikutegemea na mambo kama hayo.
Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo
ibadilike. 13 Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa
mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hiyo aliyeihudumia
madhabahu. 14 Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu
alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lo lote juu yake katika
mambo ya ukuhani.
Kupanuliwa wigo
kwa huduma hii ya kikuhani zaidi ya Walawi umeelezewa na kufafanuliwa wazi sana
kwenye andiko hili. Andiko linaelea mbele kwa kumfananisha Masihi na
Melkizedeki.
Tena
hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya
Melkizedeki; 16 asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo
ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo; 17 maana
ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki. 18 Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa
sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake; 19 (kwa
maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini
yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu.
Nia ya kuondoa au
kufutilia mbali wazazi kama lengo la andiko limefanywa liwe kitu rahisi tu hapa.
Huduma ya kikuhani imetokana siyo tu na heshima ya kimwili bali pia ni kwa nguvu
ya maisha au uhai usioweza kupatwa na madhara (soma Warumi 1:4). Hivyo basi Roho
Mtakatifu alimpa uweza na mamlaka kwa Melkizedeki kama alivyofanya Ibrahimu na
mababu wengine wote wa imani, pamoja na Daudi, Waamuzi na Manabii na kuendelea
hadi kwa mitume na wateule. Umuhimu wa andiko hili siyo kwenye ukweli kwamba
Melkizedeki angekuwa ndiye Masihi, lakini, zaidi ni kwamba ni muhimu sana kama
hakuwa hivyo.
Na kwa
kuwa haikuwa pasipo kiapo, 21 (maana wale
walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye
aliyemwambia, Bwana amea pa wala hataghairi, Wewe u kuhani wa milele;) 22 basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano
lililo bora zaidi
Ni ushuhuda wa
Mungu kwamba wateule waliitwaa ofisi. Masihi alipewa ofisi kwa kuahidiwa na
Mungu kwa kiapo.
Ukuhani wa Kilawi
uzifikia kikomo kwa kifo ndipo aliacha kuendelea kuhudumu. Watakuwa na sehemu
kwenye ufufuo wa pili wa wafu. Alio kwenye utaratibu wa Melkizedeki watakuwa na
sehemu kwenye ufufuo wa kwanza wa wafu. Wale wateule wanaufufuo mwema (Waebrania
11:35).
Tena
wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae; 24 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake
usioondoka.
Mwendelezo wa
milele unatokana kwa kupitia kifo hadi ufufuko wa wafu. Ukuhani haujaondolewa kutoka
kwa wateule, ni kama ulivyokuwa haujaondolewa kutoka kwa Masihi na kwa mababu
wa zamani wa imani.
Naye,
kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai
sikuzote ili awaombee. 26 Maana ilitupasa sisi
tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa
na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu; 27 ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu
wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa
ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa
nafsi yake. 28 Maana torati yawaweka wanadamu walio na
unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya
torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.
Hivyo Masihi alikuwa
ni utimilifu au upeo kwenye utaratibu huu mpya wa kikuhani unaoenea hadi kwa
wale waliokuwa wamechaguliwa na Mungu, waliomchagua Masihi na kumfanya awe
mkamilifu milele.
Tumeona kwamba baadhi ya madhehebu ya
Kiyahudi yanamchukulia Masihi kuwa ni kama Mikaeli (kutokana na Danieli 12:1).
Dhana au nadharia zilizotuama kwenye ukweli wa kwamba ni Mikaeli imedumu kuaminiwa
ma Waisraeli, na Taifa la Israeli alipewa Yahova na Mwenyezi Mungu wakati
alipoyagawanya mataifa sawasawa na wana wa Mungu (sawa na ilivyo kwenye Kumbukumbu
la Torati 32:8 tafsiri za RSV, the LXX na ya DSS). Jina Melkizedeki lina maana
yake, nayo ni: Mfalme Wangu ni Mtakatifu
au Mfalme Wangu ni Mwenye Haki (maneno
haya haki na utakatifu yanaendana sawasawa) (soma kitabu cha Vermes, cha Dead Sea Scrolls in English [Gombo za Bahari
ya Chumvi, toleo la Kiingereza], ukurasa wa 253). Iliadhaniwa pia kwamba
Melkizedeki lilikuwa ni jina la kiongozi wa Jeshi la Nuru, ambaye tumeona kuwa
ni kazi ya Masihi (kitabu cha Vermes, ukurasa wa 260).
Mawazo hayoyote yanafanyika kutokana na
maandiko yaliyoharibiwa ya Agano la
Amramu. Hivyo ingeweza kuendelea kuaminiwa kwa dhana hii ya umuhimu wa
ujumuisha wa Melkizedeki-Masihi kwa Waessene. Hata hivyo, Melkizedeki hadi
Masihi wakati kuna tatizo kubwa kuhusu dhana ya kuzaliwa kwake hapa duniani
kulikuwa kwa mabadiliko ya kimaumbile ya kutoka aina moja ya kiumbe na kuja
kwenye aina nyingine na la sadaka. Sasa tutautazama uhusiano uliopo kati ya sheria
na ukuhani.
Cheo hiki kinaonekana kuwa ni kama cheo
cha kiurithi cha mfalme wa Yerusalemu (au Urusalaim).
Mamia ya miaka baada ya Ibrahimu tunakudana na mfalme mwingine akiwa na cheo
kama hichohicho, Bwana wa Utakatifu au
Bwana Wangu ni Mtakatifu, kipindi cha
kuingia kwao Israeli na kuikalia Kanaani wakiongozwa na Yoshua. Ndipo kwenye
Yoshua 10:1 tunakutana na Adonisedeki,
ambaye ni mwingine tofauti na Melkizedeki, akitawala Yerusalemu. Jina lake la
kicheo kwa mwonekano wake wa tofauti, kwa hiyo ni la kurithi na linamuashiria Masihi
kwa ubora wa utawala wake kutoka Yerusalemu, na huenda alionekana kwa jinsi hii
na Daudi pia. Kwa namna hii pia wateule ni makuhani wa aina ya Melkizedeki, kwa
kuwa wanatawala pamojanaye kutoka Yerusalemu wakiwa ni elohimu (sawa na Zekaria 12:8; Ufunuo 7:1-17).
Dhana ya Wakristo ya kwamba Melkizedeki ni
Masihi inatokana na kutokuelewa kwao andiko la Waebrania 7:3. Neno la kwamba hana
baba, mama na wazazi (apator nk.) linakusudia
kuonyesha umuhimu wa kumjumuisha kwenye uzao wa Haruni (Nehemia 7:64) kwa
huduma ya ukuhani wa Kilawi.
Neno lisemalo mwanzo wa siku na mwisho wa maisha linamaana
umuhimu wa kuanza kuhudumu au kufanya kazi akiwa na umri wa miaka thelathini na
kuacha kufanya kazi akiwa na umri wa miaka hamsini (Hesabu 4:47). Kuhani Mkuu
alirithi huduma ya kuhani wakati anapokufa mtangulizi wake. Melkizedeki hakuwa
na ulazima huo. Waraka kwa Waebrania unanukuliwa kwenye tafsiri ya kamusi ya Marshall’s Interlinear kwamba alikuwa
mwanadamu (Waebrania 7:4). Aliumbwa umbo sawa kama Mwana wa Mungu (Waebrania
7:3) lakini hakuwa kabisa Mwana wa Mungu, aliyekuwa ni kuhani mwingine (Waebrania 7:11). Kwa hiyo wateule wote wanaweza kushiriki
kwenye huduma ya kikuhani, wakiwa wamefanyika kama Mwana wa Mungu, pasi kujalisha
na uzao wanaotokea, wakiendelea hata milele. Ni kama alivyokuwa Melkizedeki,
nasi tunaweza pia kukisia. Waessene walilipotosha andiko kwa maslahi ya
kimalipo kama walivyo wahafidhina wa siku hizi. Suala la Wapaulicians ambao pia
waliamini kuwa mtazamo huu waliitwa Wamelkizedekiani, lakini walimfanya awe ni
tofauti na Masihi kama mwombezi kutoka mbinguni (soma pia jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa ya Washika Sabato (Na. 122)). Yaonekana kuwa kitabu cha Waebrania
kiliandikwa kwa lengo la kusahihisha makosa lakini kwa chenyewe kimejikuta
kikirekebishwa kimakosa pia. Midrash anaamini kuwa alikuwa Shemu (Rashi) akiwa
mfalme (melek) wa mahala pa haki (tsedek) (kwa mujibu wa Abraham ibn Ezra
& Nachmanides). Mahali hapo palikuwa ndipo ambapo hekalu lilijengwa kwa
Maskani Takatifu, ambapo Midrash panapachukulia kuwa ni Yerusalemu kwa vyovyote
kutokana na andiko lisemalo Haki imewekwa
kwake (Isaya 1:21) (ibn Ezra & Nachmanides, soma pia Soncino, linganisha na Mwanzo 14:18).
La muhimu zaidi, dhana ya kwamba Baraza la Elohimu lilikuwa sahihi na
halipingiki kama litakuwa limeeleweka vyema kwa maandiko ya Agano la Kale yanayomtaja
elohim. Mfumo saidizi wa Elohimu umeeleweka
kwa upande mmoja, lakini umekosa kueleweka vyema kawa kuahusianisha na Mikaeli
na Melkizedeki.
Ufunuo 4 & 5 inaonyesha kwamba kundi
hili limehesabu viumbe wapatao thelathini wakiwemo makerubi wa nne. Vipande thelathini
vya fedha vilihitajika ili kumsaliti Kristo (Mathayo 27:3,9 sawa na Zekaria
11:12-13) kwa kuwa ilikuwa ni uovu dhidi ya mhimili wote wa Uungu. Viongozi
wanalaumiwa kwa kusimamia maombi ya watakatifu (Ufunuo 5:8) na Kristo ndiye Kuhani
wao Mkuu. Alikuwa ni mshiriki wa baraza la Viongozi aliyeonekana kuwa
anastahili kukifungua kitabu cha mpango wa Mungu ili awaokoe au kuwapata watu
waliosamehewa makosa yao na kuwafanya wawe ufalme na ukuhani wa Mungu wetu –
yaani Mungu wa Baraza hilo na Kristo (Ufunuo 5:9-10).
Sadaka ya msamaha wa wanadamu ni sehemu ya
marejesho mapya ya nyakati za mwisho, ambayo yatafanyika wakati wa ujio wa pili
wa Masihi akiwa Mfalme wa Israeli; ujio wake wa kwanza ulijulikana kama Masihi
wa Haruni. Ujio huu wa kwanza wa Masihi ulikuwa ni wa ongoleo la dhambi na wa
uanzishaji wa ukuhani wa Melkizedeki. Marejesho ya nyakati za mwisho
yaliejulikana kuwa ni upanuzi wa wigo elohim
kama ilvyoonyeshwa kwenye Zekaria 12:8. Kwenye marejesho ya nyakati za Mwisho,
wakati atakapokuja Masihi huko Sayuni kama ilivyokuwa ikielezewa na kueleweka kwenye
Waebrania 12:22-23, mkururu wa matukio yanayohusiana na kuulinda Yerusalemu na
kuimarishwa kwa wakazi wake walio kwenye mji huo kwa ajili ya utawala wa
Milenia. Tena tazama kwamba Zekaria inaendelea mbele kwa kusema:
Na yeye aliye dhaifu
miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama
Mungu (elomih), kama Malaika
wa Bwana [Yehova] mbele yao. (msisitizo
umewekwa ili kusisitiza).
Maana yake hapa yalikuwa kwamba Zekaria alipewa
neema ya kuelewa kwamba Malaika wa YHVH alikuwa elohim, na kwamba watu wa nyumbani
mwa Daudi (ambaye alikuwa amekwisha kufa kitambo) waliungana na wale ambao
hatimaye watakuwa elohim, wakiwa kama ni sehemu ya watu wa nyumbani mwa Daudi.
Zekaria aliandika mwishoni mwa kipindi cha
Biblia, kikiwa ni moja ya vitabu vya mwisho kuandikwa (inadhaniwa ni kama mwaka
wa. 410-403 KK, Nyongeza ya 77 ya tafsiri ya Companion Bible inasema hivyo). Uelewa
ma mkururu huu kwa hiyo haukupotoshwa kwa kipindi chote kirefu cha ukusanyaji
wa maandiko haya.
Hitimisho la kwamba ni Melkizedeki haliwakilishi kwa ujumla mtazamo wa
Kanisa la Mungu kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu mbili. Imekuwa ikiaminika
hivyo na vikundi vingine na baadhi ya madhehebu au dini za Kiyahudi. Inaonekana
kuwa Masihi hakuwa Melkizedeki, bali kwamba kuendelea kwa uzima wa milele kwa
Melkizedeki kwa kupitia kwenye huduma yake kwa Roho Mtakatifu kumekuwa
hakueleweki. Ukeli wa jambo lenyewe sio wa mihimu kwenye imani, wala kiini cha
fundisho hili sio muhimu kwa mtu kukubalika kwenye ushirika. Mahala pa muhimu
kwenye majukumu ya Masihi huenda kunadhoofisha hoja ya kuingizwa kwa wateule
kwenye huduma hii ya kikuhani wakiwa kama elohim tu kuliko kulienekeza jambo
lenyewe. Uhusiano wake kwa hakika unatuama kwenye utunzi wa fundisho kwa kutumia
andiko lililo kwenye aya moja tu peke yake.
q