Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[131]
Siri za Mungu
(Toleo La 1.1 19950819-19981214)
Ufunuo wa Mungu
unajulikana na kueleweka kama ni Siri za Mungu na watumishi wake wateule. Mfano
wa talanta na wa wanawali wenye busara na wapumbavu vimeainishwa pia. Viwango
vya ufunuo wa Siri za Mungu vimeainishwa na kuekwa kwa mpangilio maalumu.
Christian Churches of God
Email: secretary@ccg.org
(Hatimiliki ã 1995, 1998 Wade Cox)
(tr. 2017)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu
bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina
la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe
Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote
atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja
ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Siri za
Mungu
Siri za Mungu
zimehawanyika kwenye kile kinachoweza kuitwa kuwa ni viwango au hatua za
ufunuo. Hatua ya kwanza imejuluishwa kwenye mafundisho ya msingi ya Uungu,
uhusiano wa maisha ya Kikristo, na mambo ya kiunabii yanayoathiri uelewa wetu
kuhusu Mpango wa Wokovu.
Roho Mtakatifu
anatoa uwezo wa kuzilewa ziri za Mungu kwa wateule wake na kuwafabtwa wawe
watumishi wanaozitumikia hizo Siri za Mungu.
1Wakorintho 4:1-5 Mtu
na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. 2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu
aonekane kuwa mwaminifu. 3 Lakini, kwangu mimi, si
kitu kabisa nihukumiwe na ninyi, wala kwa hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu
hata nafsi yangu. 4 Maana sijui sababu ya kujishitaki
nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni
Bwana. 5 Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati
wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na
kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa
Mungu.
Tito 1:7 inawaonyesha
wazee (the presbuterous au episkopon) kuwa ni watumishi wa Mungu.
Tito 1:7 Maana
imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno ,kwa kuwa ni wakili wa MUNGU;asiwe
mtu wa kujipendeza nafsi yake,asiwe mwepesi wa hasira,asiwe mlevi wala mgomvi,asiwe
mpenda mapato ya aibu.
Makatazo dhidi ya
kujipendelea (kujipenda mwenyewe au authade)
na ya kutojikweza (orgilon) au kunywa
sana mvinyo au kulewa, mandindano au uchoyo wenye lengo au msingi wa
kujinufaisha (aischrokerde) yanaonyesha
kupendwa na mtu ambaye na kwa yeye ambaye siri hizi zimefunuliwa kwake. Tafsiri
ya neno huperatas ambalo maana yake
ni msimamo, au mtumishi, kama mtumishi wa Kristo kwenye tafsiri ya KJV yamepotoshwa,
au yamekatazwa bila sababu za msingi, utendaji kazi wa mtumishi wa Siri za
Mungu na kwenye ukasisi au ukuhani, ambayo siyo maana yake. Wateule wote
wamepewa uwezo wa kuzielewa au kuzijua siri hizi kutegemea na uhusiano wao na
Mungu katika Roho Mtakatifu. Na hata hivyo, haifai kabisa kuwa mtu asiyebagua
kwenye kuelezea au kuzifafanua siri hizi.
Siri hizi wamepewa
kwa wale waliojitoa na kujikabidhi kikamilifu kwa Mungu katika Yesu Kristo.
Hakuna asiyelaumika kabla hajabatizwa. Hiyo haimaanishi kuwa ndicho kinachokusudiwa
kwenye andiko la Tito 1:7. Nia na kusudi la kufunuliwa kwa Siri za Mungu ni
moja ya kujitoa kusiko na ubinafsi kwenye kazi na wajibu huu.
Roho Mtakatifu
anafanya kazi pamoja nasi kabla ya
ubatizo na ndani yetu tangu tunapobatizwa
(soma jarida la Toba na Ubatizo (Na. 52)).
Hairuhusiwi kabisa kubatizwa na kisha usijitoe kuifanya kazi ya Mungu katika
Yesu Kristo. Mkururu wenyewe umefanywa ni kama kuma ilivyoelezewa kwenye siri
hizo, kufundishwa kwenye neno, na kisha kuandaliwa kulifundisha neno. Hicho
ndicho alichokimaanisha Mtume Paulo wakati alipoelezea kuhusu maziwa na nyama.
1Wakorintho 3:1-23 Lakini,
ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni,
bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika
Kristo. 2 Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula;
kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, 3 kwa
maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna
husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa
jinsi ya kibinadamu? 4 Maana hapo mtu mmoja asemapo,
Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? 5 Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao
kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. 6 Mimi
nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. 7 Hivyo,
apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. 8 Basi
yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu
yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. 9 Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi
ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu. 10 Kwa kadiri
ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima,
naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie
jinsi anavyojenga juu yake. 11 Maana msingi mwingine
hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu
Kristo. 12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo,
dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila
mtu itakuwa dhahiri. 13 Maana siku ile itaidhihirisha,
kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila
mtu, ni ya namna gani. 14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu
yake ikikaa, atapata thawabu. 15 Kazi ya mtu
ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa
moto. 16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu,
na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama
mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la
Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. 18 Mtu
asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu
katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. 19 Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa
maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao. 20 Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya
kwamba ni ya ubatili. 21 Basi, mtu ye yote na
asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu; 22 kwamba
ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo
sasa,au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; 23 nanyi
ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.
Andiko hili la
kwenye 1Wakorintho 3 lilikuwa ni utangulizi kwenye mawazo yaliioelezewa kwenye
sura ya 4. Kazi yaliyofanya Makanisa ya Mungu katika karne ya ishirini ni
kinyume kabisa na kile alichokisema Mtume Paulo; kila moja linadai kuwa
yanawafuata wanadamu. Na ndiyo maana kazi hizi zilielezewa kwenye moto wa
ushuhuda wa uwongo na kuangamia kwa udhaifu wao wenyewe au dhambi zao. Mateso
na majaribu tunayoyavumilia ni kujaribu imani yetu na msingi wetu kwa kuwa sisi
tu hekalu la Mungu.
1Petro 2:1-5 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote,
na unafiki na husuda na masingizio yote. 2 Kama
watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili
kwa hayo mpate kuukulia wokovu; 3 ikiwa mmeonja ya
kwamba Bwana ni mwenye fadhili. 4 Mmwendee yeye, jiwe
lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba
ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa
njia ya Yesu Kristo.
Msimamo ambao unahitajika
unatuweka mbali ma maovu, uladhai, wivu na kusingizia au kuteta. Yatupasa
tufanye kazi kwa pamoja. Yatupasa tuwe kama watoto wachanga tukiyanywa maziwa
safi ya kiroho ili kwamba tuukulie wokovu. Kristo alikuwa ni jiwe lililohai la
kwanza lililochaguliwa na Mungu ambalo kwalo sisi tumeongezewa mmoja baada ya mwingine
kwenye ujenzi wa nyumba ya Mungu.
Kwenye kila jiwe
moja lililohai ambayo ni sisi, wengine wameongezwa. Ili ni budi tuwe wa kweli na
imara kwa kuelimika na tusimame pasi kuyumbishwa. Mawe yaliyohai yamepewa pia
manabii waliohai (Matendo 7:38) ambayo ni Maandiko Matakatifu, na tumaini
lililohai (1Petro 1:3) ambayo ni imani (soma jarida la Manabii wa Mungu (Na. 184)).
Hatupaswi tubakie
watoto wachanga tu kila wakati katika Kristo. Yatupasa tuendelee kukua kutoka
kunywa maziwa na kula nyama.
Waebrania 5:5-14 Vivyo
hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye
aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. 6 kama
asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki. 7 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye
kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi,
akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; 8 na,
ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; 9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa
milele kwa watu wote wanaomtii; 10 kisha ametajwa na
Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki. 11 Ambaye
tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa
mmekuwa wavivu wa kusikia. 12 Kwa maana, iwapasapo
kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu
mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si
chakula kigumu. 13 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa
hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 14 Lakini
chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa
kupambanua mema na mabaya.
Tunaona kwamba
Kristo hakujiinua mwenyewe kwa kuwa kuhani mkuu. Alichaguliwa na kupewa maagizo
na Mungu ambaye ndiye Mungu wake pia (Waebrania 1:8-9). Na kwa kuwa Kristo alichaguliwa
kuwa kuhani na ndivyo hata sisi tumechaguliwa kumfuata yeye kwenye ukuhani huo.
Alifanywa mkamilifu kama tunavyotakiwa na sisi tuwe wakamilifu. Tunatakiwa
tufanye kazi kwa imani. Tumeagizwa tufanye kazi kwa ajili ya okovu wa wanadamu
kwa njia ya mahubiri na kulifundisha neno la Mungu. Lakini kuna bado miongoni
mwetu sisi wanaoweza kufanya kazi, lakini wakiwa bado hawana uwezo na wakidumu
kunywa maziwa. Udhaifu huu kwenye imani inatokana na makwazo au huzuni zisizotambulika
au kwenye uovu na hasira. 1Wakorintho 13 inaonyesha kwamba upendo wapasa uwepo
kwa wateule. Ni jambo lisiloruhusiwa kabisa kubatizwa na kisha kujitenga au
kuioa kwenye huduma kwenye jeshi la Bwana. Hakuna mtu anayetia mkono wake
kulima na kisha kurudi nyuma atakayefaa kuingia kwenye Ufalme wa Mungu (Luka
9:62).
Sio kwa bahati mbaya kwamba Mfano wa Wanawali
Werevu na Wapumbavu unakafuatia mara tu baada ya Mfano wa Talanta kwenye Mathayo
25.
Mathayo 25:1-30 Ndipo
ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka
kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa
wapumbavu, na watano wenye busara. 3 Wale waliokuwa
wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao
pamoja na taa zao. 5 Hata bwana arusi
alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. 6 Lakini
usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. 7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa
zao. 8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara,
Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini
wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi;
afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. 10 Na
hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari
wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. 11 Halafu
wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. 12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. 13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
Mfano wa Wanawali
Werevu na Wapumbavu unaelezea kwa namna moja kile kilichoelezewa kwenye Mfano
wa Talanta lakini ni kwa mwelekeo mwingine. Jambo la kwanza kuhusu wanawali
hawa linahusika na mwajibiko binafsi wa kila mtu kwa Mungu akiwa kama bibi
arusi wa Kristo ili kuandaliana kila mmoja na mwingine katika Roho Mtakatifu.
Ni mtu tu binafsi anaweza kufanya maandalizi hayo. Jambo la pili, na ambalo
linahusiana kwenye Mfano wa Talanta linahusu kazi ya kuzaa matunda katika Roho
Mtakatifu kwenye Ufalme wa Mungu. Jambo moja haliwezi kuendelea kuwepo pasipo
kuwa na lile lingine. Maendeleo ya kiroho ya mtu pasipokuwa na mwingiliano wa
pamoja na kazi kwenye imani ni kazi bure au haina maana.
14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri,
aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. 15 Akampa
mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa
kadiri ya uwezo wake; akasafiri. 16 Mara yule aliyepokea
talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine
tano. 17 Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye
akachuma nyingine mbili faida. 18 Lakini yule
aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. 19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale,
akafanya hesabu nao. 20 Akaja yule
aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka
kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. 21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu;
ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya
bwana wako. 22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili,
akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili
nilizopata faida. 23 Bwana wake
akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache,
nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 24 Akaja
na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu
mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; 25 basi
nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo
yako. 26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe
mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya
nisipotawanya; 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa
watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. 28 Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo
talanta kumi. 29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na
kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. 30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la
nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Talanta
zinazoongelewa kwenye mfano huu hazimaanishi talanta au vipawa au uwezo wa
mwanadamu tu, pekeyake. Bali zinamaanisha karama za Roho Mtakatifu na nafasi au
fursa ya kiutendaji waliopewa wateule na Mungu ambao wanamtumikia kwao na
kutimiliza kazi yake. Kila mmoja alipewa kipimo cha utajiri wa Ufalme wa Mungu.
Kila moja imewekwa juu yake mwenyewe kazi au wajibu wa upimaki wa kipimo atakaporudi
sawasawa na utajiri aliopewa. Wakati mtu anapopewa kiasi kidogo tu ilitegemewa
kwamba kiasi hicho kingejumuishwa na nguvu na utajiri wa wale waliopewa dhamana
pamoja na usimamiz au ulimzi wa utajiri ili kuwianisha na marejesho ya hesabu
hizo. Kwa hiyo kila mtu ambaye yeye mwenyewe hawezi kutimiliza kazi ni lazima
waziweke talanta zao kwenye bwawa la pamoja ili kwamba mkakati wa kuwianisha ifikiwe
au utimilizwe kutokana kwa kila mshirika wa mwili wa Kristo. Kitendo cha kushindwa
kutenda kazi kwenye wajibu wa kila mmoja ili kwamba kazi ifanyika kwa pamoja
kunamfanya kila mtu kuhukumiwa na kukataliwa kwenye ufufuo wa pili wa wafu.
Wajibu wa wateule
ni wa namna zote mbili, yaani wa kiroho na kimwili. Mambo ya kimwili ni ya kifedha.
Kwa hiyo matendo ya wote au ya jumla ya Kanisa yamewekwa kwenye utumishi mzuri;
hakuna mtu kwa hiyo atakayesimama peke yake na asiisaidie kazi. Kazi imeonekana
imesimana imara kutokana na mafundisho yenye uzima kwenye Siri za Mungu na ibada
zake.
Kutokana na
utambulisho wa mafundisho na wajibu wetu bdipo tunaendelea kutoka utumiaji wa
maziwa hadi ulaji wa nyama. Nyama ni kwa ajili ya wateule, ambayo inafuatia
kutoka kwenye utumiaji wa maziwa waliyopewa kama watoto wachanga, ni nyama ile
ile ambayo Kristo aliikomesha kwenye Yohana 4:34-38.
Yohana 4:34-38 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende
mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake. 35 Hamsemi
ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni
macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa
mavuno. 36 Naye avunaye hupokea mshahara, na
kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate
kufurahi pamoja. 37 Kwa maana hapo neno hilo huwa kweli,
Mmoja hupanda akavuna mwingine. 38 Mimi naliwatuma
myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu
yao.
Chakula cha Kristo
au nyama vinavyoelezea hapa ilikuwa ni kazi ya Mungu. Kazi hii ilikuwa ni
mavuno ambayo tunashiriki kwayo. Mpanzi na mvunaji wanafurahi pamoja. Kwa hiyo
Kristo anavuna mahali asipopanda. Mungu kwa kupitia Roho Mtakatifu anafanya
kazi kwa kupitia wateule wanaopanda mbegu kwa kazi ya wengine nasi tunavuna.
Sisi tunapanga pia ili kwamba wengine wavune. Kwa hiyo tunashiriki sote kwa
furaha tuliyopewa na Kristo. Hakuna kati yetu aliye wa Paulo wala wa Apolo. Ni
kama alivyokuwa Paulo, sisi sote tu watumwa (doulos) wa Mungu (Tito 1:1).
Yatupasa
tujitahidi iwezekanavyo kuiharakisha kazi ya Mungu kwa namna yake. Yatupasa
tuzae matunda.
Tito 3:13-14 Zena, yule mwana-sheria, na Apolo, uwasafirishe kwa bidii,
wasipungukiwe na cho chote. 14 Watu wetu nao
wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe
hawana matunda
Hapa tunaona
kwamba Kanisa linaonekana kwamba wale waliosababisha mafarakano kwenye kazi kwa
kuwafuata watu wanakemewa kwa kuambiwa kuwa wamemsaidia mteule mmoja na Paulo
ambaye alichukuliwa kuwa ni wa kundi linguine. Kazi ya Mungu sio ya mtu yeyote
ili kwamba hakuna yeyote mwenye mwili atakayejivuna wala kujitukuza (1Wakorintho
1:29). Basi kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu ya msingi wa kazi ya
Mungu (1Wakorintho 3:10).
1Wakorintho 3:5-9 Basi
Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu
kama Bwana alivyompa. 6 Mimi nilipanda, Apolo akatia
maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. 7 Hivyo, apandaye
si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. 8 Basi
yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu
yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. 9 Maana
sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la
Mungu.
Kila mtu yapasa
aangalie jinsi anavyojenga, ila kujenga ni lazima. Haijalishi ni wapi tunapofanya
kazi, la msingi tu ni tunafanyaje hiyo kazi. Kwa kweli tusiwafuate watu.
Wakumfuata ni Mungu kwenye mafundisho yenye uzima.
Siri za Mungu
zinafunuliwa kwa hatua moja hadi nyingine.
Hatua ya kwanza
inahusiana na kumjua Mungu, kuwa ni nani na yupoje. Kujue uwepo wa maovu na
asili au tabia zake na madhara ya dhambi kunawaongoza kwenye shauku ya kufanya
uamuzi wa kutubu na hatimaye kuelewa umuhimu wa kubatizwa na neema ya Mungu
iokoayo. Mchakato huu umeingizwa kwenye misingi endelevu ya maisha ya mtu.
Kuuelewa uhusiano uliopo kati ya Torati au sheria na dhambi, na wokovu na neema
ni mchakato endelevu na wa kina zaidi. Kushindwa kuyaelewa au kuyajua masuala
ya neema ni sababu ya msingi ya mtu au watu kujihesabia haki.
Hivyo Mpango wa Wokovu ni jambo muhimu na la msingi kuelewa kupitia kwenye
vipindi vya Siku Takatifu. Mwendelezo wa kutoka Sabato za kila juma hadi kwenye
Miandamo ya Mwezi Mpya unakamilisha mkururu uelewa. Hii ni kwenye awamu au
hatua ya pili ya uelewa. Kuyaelewa mataifa yaliyohusishwa kwenye unabii pia ni
sehemu ya awamu au hatua ya kwanza, ambayo inaendeleza kutokana na kuielewa
Israeli ya kiroho. Uelewa wa kwanza na wa msingi katika kuelewa kile
kinachojulikana kama Nyakati za Mataifa (soma jarida la Kuchanganua Ratiba ya Zama (Na. 272)). Hatua au awamu ya pili inaanzia na kuchanganua
kile kinachojulikana kama Ujio wa Masihi na kuanzishwa kwa kipindi na utawala
wa Milenia.
Mkururu wa
matukio ya nyakati za mwisho na uanzishwaji wa utawala na mfumo wa milenia vinaeleweka
sana kutokana na maadhimisho ya Siku Takatifu. Mkururu wa harakati ni jambo
linguine tofauti.
Tungeurejelea
mchakato huu kwa kutumia jedwali.
Hatua ya 1
Maziwa
1. Waioitwa
kwenye maarifa ya kwanza nay a msingi ya Biblia:
a) Dhana na nadharia ya kwanza nay a msingi ya Uungu. Baba ni Mungu.
b) Kristo kama Masihi kwenye mzunguko wa kuzaliwa alikufa ili awaokoe wenyedhambi.
c) Roho Mtakatifu ni uweza wa Mungu, ingawa sisi tunafanyika wamoja na Mungu.
2. Kuelewa historia
ya Biblia na ya Israeli:
a) Mababa wa imani.
b) Wokovu wa kimwili wa Israeli kutoka Misri.
c) Wokovu wa kiroho katika Masihi.
3. Asili na uhakika wa unabii kwa maagano yote mawili, yaani Agato la Kale na Agano Jipya:
a) Mababa wa imani na Musa hadi Waamuzi.
b) Wafalme hadi manabii wadogo.
c) Unabii wa Agano Jipya tangu Kristo hadi Ufunuo.
4. Maisha ya Kikristo:
a) Mtu mmoja mmoja binafsi.
b) Familia.
c) Kijamii.
5. Mambo ya
kuyaendeleza kwenye Imani:
a)
Wajibu kwa Mungu kwenye mahusiano binafsi.
b)
Kulisaidia Kanisa kwenye kazi zake.
Misingi hii ni
budi ilindwe kabla ya mwendezo halisi haujafanyika.
Hatua ya pili
inaendeleza ile ya kwanza kwa viwango vya juu na kunaanzisha uelea wa kina
zaidi wa maana ya manabii kwenye unabii na Mpango wa Wokovu.
Hatua ya kwanza
ilipelekea kuelewa mkururu wa kihistoria. Hatua ya pili inapelekea kuelewa uwiano
wa kiroho na kazi ya unabii Kanisani na utendaji au utimiligu wake. Kutokana na
uelewa sahihi wa manabii kwenye hatua hii, nyakati za mataifa zinaweza
kuelezewa na kuhamishwa kwa mamlaka kunaweza kuonekana kwenye unabii na kazi na
wajibu wa watu na wa taifa kunaweza kuelezewa.
Nyakati za mwisho
zinaweza kuwataswirishwa pamoja na mabadiliko na mchakato wa iliyofafanuliwa ya
mwisho. Baadhi ya mambo haya yanaweza kuelezewa au kufafanuliwa kwa wasio na
habari, na mengine yanaweza kuwa yasielezeke yakiwa bado. Kwa hiyo ni lazima
kazi kimsingi igawanyike kwenye hatua kadhaa na mteule peke yake lazima
aendelee hadi kwenye hatua ya pili. Kwa hiyo awamu ya kwanza imekutaswirishwa na
kuunda msingi wa ujumbe kwa wasio washirika. Kuna mambo ambayo ni lazima
yaongezwe kwenye bodi ya uandishi. Hata hivyo, kuna mambo fulani ambayo hayako
sahihi kabisa kuwapatia wengine.
Kristo alilielezea jambo hili kwa namna mbili. Ya kwanza ni pale alipokuwa
akiutoa mfano wa Siri za Mungu. Kutowapa na kuwaficha taarifa wengine na kuwapa
walio kwenye ushirika kulifanywa kwa makusudi kabisa.
Mathayo 13:10-17 Wakaja
wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano? 11 Akajibu,
akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao
hawakujaliwa. 12 Kwa maana ye yote mwenye kitu
atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho
nacho atanyang'anywa. 13 Kwa sababu hii nasema nao kwa
mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. 14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia
mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. 15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio
yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao,
Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. 16 Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio
yenu, kwa kuwa yanasikia. 17 Kwa maana, amin,
nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi,
wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.
Kwa hiyo kuelewa
kunategemea pia na matumizi. Wale wasioweza kuona na kusikia watapoteza kile
walichokuwanacho. Watasikia lakini hawataelewa kabisa. Siri za Ufalme wa
Mbinguni zinsemwazo hapa ni sawa tu na neno musterion
au ufunuo wa mambo ya siri za Mungu. Ujumbe wa mfano huu umerudiwa pia kwenye Marko
4:10-20.
Marko 4:10-20 Naye
alipokuwa peke yake, wale watu waliomzunguka, na wale Thenashara, walimwuliza
habari za ile mifano. 11 Akawaambia, Ninyi mmejaliwa
kuijua siri ya ufalme wa Mungu, bali kwa wale walio nje yote hufanywa kwa
mifano, 12 ili wakitazama watazame, wasione; Na
wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa. 13 Akawaambia, Hamjui mfano huu? Basi mifano yote
mtaitambuaje? 14 Mpanzi huyo hulipanda neno. 15 Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao,
wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni
mwao. 16 Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye
miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, mara hulipokea kwa furaha; 17 ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache;
kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara hujikwaa. 18 Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu
walisikiao lile neno, 19 na shughuli za dunia, na
udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno,
likawa halizai. 20 Na hawa ndio waliopandwa penye
udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda,
mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia.
Kristo alielezea
madhumuni yake kwao wakati alipokuwa peke yao. Kuuelewa mfano huu kunategemea
mmoja baada ta mwingine. Kila kitu kilicho kwenye Biblia kipo hapo kwa
makusudi. Kila kitu lona maana makusudi yake. Kila kitu kina maana: kila
tarakimu, kila jambo, kila mkururu.
Kristo alificha wasijue
ili kwamba watu wasije wakaitwa kabla ya wakati na kisha wakaingia hukumuni.
Neno la Mungu ni takatifu na ndilo limefichwa kwa wale wanaolitumia vibaya.
Mathayo 7:6 Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala
msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao,
wakageuka na kuwararua.
Majira yanakuja haraka
wakati kuusema ukweli kutakuwa ni utaratibu wa siku ili kwamba jizazi hiki
kibaya, kiovu na cha zinaa kitapokea wito wa toba. Kipimo cha wateule kinafuatia
pia kwa wito au kuitwa kwa mkururu wa mwisho wa wale 144,000. Mkutano mkubwa
umechukuliwa hapo pia kwenye mchakato wa mwisho. Wajibu umeorodheshwa hapa ni
kama kuwa mwaminifu. Masumbuko ya dunia yanaonekana kama yanaingilia kati au
yanatatiza uwezo a wale wanaolisikia neno na wasitende na wasifanye kazi na
washirika wengine walio kwenye mwili wa Kristo. Kama wewe ukiwa mtu binafsi
hushiriki kwenye mikusanyiko au ibada za
kila juma na wengine pale unapoweza na kufanya kazi ili kusaidia kazi basi
hutaweza kuurithi Ufalme wa Mungu. Usidanganyike kwa kujitafutia udhuru kutokana
na kushindwa kwako mwenyewe kuchukua hatua. Kama hutaweza kusaidia kazi basi
huna sehemu nayo na kwa hiyo hutakuwa na sehemu kwenye Ufalme huo. Kama
huisaidii kazi kwa fedha zako kama unavyotakiwa kuwa ndipo ujue kuwa unamuibia
Mungu (Malaki 3:7-12).
Malaki 3:7-12 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande,
mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia
ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani? 8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia
mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na
dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana
mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Leteni
zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa
njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya
mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala
hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake
kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. 12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya
kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
Hakuna kitu cha kutenganisha
kwenye jambo hili. Kazi ya
Mungu ni wajibu wa wote. Suala la kutoa zaka ni la jambo lingine na ambalo
limeainishwa kwa kina kwenye jarida la Tutoaji wa Zaka (Na. 161)). Hata hivyo, sio suala la kuwa na shahada tu.
Kuna malumbano makubwa kama ukweli wa mambo, kuhusiana na kusaidia kazi. Huu ni
wajibu wa wote. Kila mteule anao wajibu kuutafuta ushirika wa wapendwa
unaolihubiri neno la Mungu – kinagaubaga. Mara tu kazi hiyo inapoonekana ndipo
inapasa isaidiwe na kuungwa mkono.
Kristo hakuacha
kufanya kazi kwenye hatua yoyote kwa kipindi cha karne zote ishirini zilizopita.
Anafanya kazi sasa. Kama hufanyi kazi kwa hamasa kubwa na kuusaidia mwili ule
utakuwa kwenye fungu la watakaofufuliwa kwenye ufufuo wa pili wa wafu. Hii ndiyo sababu ya kwamba kutakuwa na
vilio na kusaga meno. Wengi watagundua na huku wakiwa wamechelewa sana kwamba
walikosea njia kwa kutokuzitumia talanta walizopewa na Mungu. Usiruhusu hali
hii ikukute hata wewe. Nenda! Ukauze ulichonacho na umfuate Kristo.
Mathayo 19:16-21 Na
tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili
nipate uzima wa milele? 17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini
ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. 18 Akamwambia,
Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, 19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako
kama nafsi yako. 20 Yule kijana akamwambia, Haya yote
nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena? 21 Yesu
akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini,
nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Mungu atammwaga
Roho na, katika hizi siku za mwisho, siri hizi zitafunuliwa ili kwamba Jeshi
lote la Malaika walioko mbinguni waelewe hekima kubwa na iliyojificha ya Mungu.
1Petro 1:12 Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao
wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa
yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu
aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.
Malaika hawa
wanatamani sana kuichunguza hekima ya Mungu na kama sisi tunaujua au tunauelewa
Mpango wa wokovu.
1Wakorintho 2:1-7 Basi,
ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha
wa maneno, wala kwa hekima. 2 Maana naliazimu nisijue
neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa. 3 Nami
nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi. 4 Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya
hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, 5 ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali
katika nguvu za Mungu. 6 Walakini iko hekima tusemayo
kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia
hii, wanaobatilika; 7 bali twanena hekima ya Mungu
katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa
utukufu wetu;
Kwa hiyo tunatukuzwa tunapokuwa tumechaguliwa, tumeitwa, tumehesabiwa haki na
kisha kutukuzwa (Warumi 8:29-30).
Kitendo cha siri
hizi kufunuliwa katika siku za mwisho kitaonyesha hekima ya Mungu kwa pande
mbili zote, yaani mbinguni na Wateule wanadamu.
q