Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[135]
Mashahidi (Wakiwemo Hawa Mashahidi Wawili)
(Toleo La 5.0 19950923-20000708-20070906-20081228-20130121)
Jarida hili
linahusu na utambulisho wa Mashahidi na wanabakia kuwa ni chanzo cha pekee cha
utambulisho wa kibiblia. Uwezekano mkubwa wa aina mbili umejadiliwa pia pamoja
na dhana yake kukijumuishwa na wakati unaoendea. Huenda hii ilipuuzia ufumbuzi
usiiofikirika kwa namna yoyote ile kama ni muhimu nan i uezekano wenye hamasa.
Majina mbalimbali yametumika kwa Mashahidi hawa Wawili watakaosimama kwenye
Hekalu la Mlimani huko Yerusalemu katika Nyakati za Mwisho. Majina yao wanaitwa
Mashahidi Wawili, Vinara Viwili vya Taa na Mishumaa Miwili Iwakayo. Pia
wanaitwa kama Mizeituni Miwili au Vinara Viwili vya Dhahabu visimamavyo mbele
za Mungu wa Dunia hii.
Christian Churches of God
Email: secretary@ccg.org
(Hatimiliki © 1995,
1997, 2000, 2007, 2008, 2013 Wade Cox)
(re. 2017)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani
yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe Hakuna malipo
atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu
fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila
kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya
pia yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org
na http://www.ccg.org
Mashahidi
Sehemu ya 1: Mashahidi
Wawili
Mashahidi hawa ni vinara viwili vya taa wanaosimama mbele ya mungu wa Dunia hii. Wanaunda jeshi kubwa na lenye nguvu nyingi sana la kiroho. Kila mmoja wao anashikilia vinara vya taa ni sawa kama yale kamanisa saba yalivyoshikilia kila moja kinara kimoja cha taa. Kwa hiyo wao ni silaha zenye uweza na nguvu sana za Mungu. Kwenye Sehemu hii ya 1 tutadadavua na kuonyesha uwezekano wa hawa ni akina nani na tutashughulika na dhana ya kipindi cha kuanzia mwaka wa 1996, ambao unahitimisha mwisho wa Nyakati za Wamataifa. Katika Sehemu ya 2 tutashughulika na jambo lingine kuhusu Mashahidi hawa linalochukua sehemu kubwa ya unabii wote.
Tutaanza na kuhesabia kipindi cha miaka thelathini ambayo hatimaye itaishitimisha Yubile hii na kuihitimisha kipindi cha miaka 2,000 cha Yubile ya arobaini ya Nyakati za Mwisho (soma jarida la Miaka Thelathini ya Mwiho: Pambano la Mwisho (Na. 219)). Mwaka wa 1996 ulikuwa ni wa maadhimisho ya 3,000 ya kuingia kwa Daudi mjini Yerusalemu. Haya yote yanauhusiano na hatua za maana na muhimu ambazo zinauka tangu mwaka wa 1996. Itakuwa ni miaka thelathini kamili hadi kufikia mwaka 2026 ili kufikiliza Milennia na zama za mapepo, na kuyaandaa mataifa yote kuyarejesha nyuma tena kwa ajili ya mwaka wa kuvuna mavuno maradufu, mwaka utakaoitangulia Yubilee ya mwaka 2027-28.
Mashahidi hawa Wawili wataanza huduma yao ndani ya kipindi hiki. Inaonekana kuwa inawezekana sana kuwa Mashahidi hawa Wawili wataanza kutoa unabii wao kwa kipindi chote kijacho cha miaka thelathini. Baadaye tutaainisha ni lini uwezekano wa kuanza huduma yao itaanza na ni mwandamano upi wa matukio utakaofuatana na kuzuka kwa vita mwisho na utakavyokuwa. Jarida hili linawahusu Mashahidi hawa Wawili.
Upimaji wa Hekalu umerejelewa ama kuelezewa kwenye Ufunuo 11:1-2.
Ufunuo 11:1-2 Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo. 2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili.
Mchakato huu wa kulipima Hekalu ni harakati rasmi zitakazofanyika katika Nyakati za Mwisho kukitanguliwa na harakati za Mashahidi Wawili, waliotajwa habari zao kwenye Ufunuo 11:3ff. hakuna mwanya wa wazi, na siyo kwa bahati mbaya kuona kwamba inaendelea mbele kwa haraka sana hadi kwenye suala hawa Mashahidi. Upimaji wa Hekalu ni harakati inayolitangulia tukio la ujio wa hawa Mashahidi. Sisi tu Hekalu la Mungu. Kwa hiyo upimaji wa Hekalu ni kuwaamusha wale walio ndani ya Hekalu la Mungu, na kuwachagua wale walioimara wanaobakia kuwa ni mawe yaliyohai ya Hekalu la Mungu. Wale wasiofaa – na kuna idadi kubwa sana ya watakaoonekana kuwa hawafai – watakaoondoleambali.
Upimaji wa Hekalu na mchakato wote mzima wa kuondolewa kwa wachungaji watatu kwa kipindi cha mwezi mmoja umeelezewa kwa kina – ni kama ulivyo mkururu wote wa mfano ashiria wa mchakato ulio kwenye Ezekieli 34, na maandiko kadhaa mbalimbali yanayohusika na dhana kama hizo kwenye jarida la Upimaji wa Hekalu (Na. 137). Hata hivyo, jarida hili hasahasa linawahusu Mashahidi hawa Wawili na uwezekano wa kuwa ni kina nani hawa, na kuna idadi kadhaa ya fikra za uwezekano wao, kwa wanaweza kuwa ni kina nani watu hawa.
Ufunuo 11:3-4 Nami
nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili
na sitini, hali wamevikwa magunia. 4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za
Bwana wa nchi
Kitu kimoja ambacho ni hakika ni kwamba; Mashahidi hawa Wawili hawafi wala
hawawezi kuuawa hadi pale kazi yao itakapohitimika. Huduma au kazi yao hiyo
itaanza na itafuatia mara moja ujio wa Masihi, na watafufuliwa.
Madai yaliyokwisha fanywa kuhusu Mashahidi hawa Wawili ni ya uwongo kabisa.
Kuna watu ambao wamekwishawahi kuonekana kuwa ni kama wangekuwa Mashahidi hawa
Wawili kwa nyakati mbalimbali. La msingi na linalotakiwa kujua tu ni kwamba
Mashahidi hawa hawafi sasa na dunia itashangaa watakapokuwa hapa juu ya sayari
hii. Mashahidi hawa hawatatoa nabii za uwongo. Hawatakuwa ni watu waliowahi
kuhudumu na kujulikana kwenye kanisa lolote hapa duniani na wakahudumu kwenye
karne ya ishirini na ambao kwa sasa wamekwishakufa.
Upimaji wa Hekalu utafanyika sambamba na
mkururu wa matukio ya harakati mbalimbali, ambayo yatakitangulia kipindi cha
siku 1,260, au cha miezi arobaini na miwili, au kipindi cha miaka mitatu na
nusu. Wote watahudumu kwenye wakati mmoja, wakielezea matukio mbalimbali.
Kwahiyo twaweza kudhania kwamba kumetajwa vipindi viwili, au ni kama
tunashughulika na mizani mbili tofauti ya nyakati kwenye maandiko ya kitabu cha
Ufunuo. Mzani wetu ni wakati, kwa msingi wa siku kuilinganisha na mwaka, na
tunaipata miaka 1,260 kamili ya dhiki na mateso kwa hesabu ya mwaka mmoja sawa
na siku moja, na kipimo kingine kinawakilisha kipindi halisi cha chini cha
miaka mitatu na nusu. Sote tunajua na tunakumbuka kwamba kulikuwa na kipindi
cha mateso ya watakatifu huko nyuma kilichodumu kwa kipindi cha miaka 1,260 tangu
mwaka 590 BK hadi 1850 BK, kilichoshuhudia Kanisa likiteswa na kanisa lenye
madaraja ya kivyeo lililopewa jina la Kanisa
la Mwanamke Kahaba. Hii ndiyo imani inayotajwa kwenye Ufunuo 7:1-18.
Kipindi cha
kuhudumu Mwashahidi hawa kimetengwa cha siku 1,260 watakapohudumu wakiwa
wamevaa magunia. Kipindi hiki kinalingana na kipindi ambacho nyua zilizo nje ya
Hekalu zitakapokuwa zimekanyagwa kwa miguu pamoja na Mji Mtakatifu, ambao ndio
Yerusalemu.
Tungeweza kusema,
na imekua ikisemwa, kwamba kipindi hiki cha miaka 1,260 kilichoishia mwaka 1850
kiliushuhudia mji wa Yerusalemu ukiwa umekanyagwa kwa miguu, na imani au mfumo
mzima wote kwa kipindi kile chote kiliushuhudia Mji Mtakatifu nan chi yote ya
Israeli ikikanyagwa kwa miguu. Tangu mwaka 590 hadi 1850 hakukuwa nan chi au
jimbo la lililoshikamana lililotengwa kwa Waisraeli nan chi ilikuwa na mapigano
mengi kati ya Wazungu wa Ulaya na Waislamu. Unabii ule haukushuhudia watu
wowote wawili wakisimama kuhudumu huko Yerusalemu. Waadventista Wasabato
wanatafsiri na kuweka hoja zao kwamba Mashahidi hawa Wawili si wengine bali ni
Agano la Kale na Agano Jipya. Wanasema kwamba Maagano haya mawili yalichimbiwa/chini
ya ardhi kwenye Mapinduzi ya Wafaransa na wakatangaza kuwa Biblia imekufa, na
kwamba basi imani hivyo imekwisha mwishoni mwa Mapinduzi ya Ufaransa. Hata hivyo,
huo haukua mwisho wa kipindi na hayakuchukuliwa na kwenda juu Mbinguni bado.
Hakuna kilichotokea tangu mwaka 1850. Mapinduzi ya Ufaransa yalifanyika mwaka 1793
na siyo mwaka 1850 kabisa. Makanisa ya siku hizi, likiwemo vuguvugu la Waadventista,
yanajaribu kudai kwamba mambo haya yamekwishapita tayari ili kukwepa mambo yanayofundishwa
kwenye kitabu cha Ufunuo kwa kuwa kitabu cha Ufunuo ni nakala inayoogopesha
sana. Makanisa mengine yametunga na kubuni fundisho walilolipa jina la ‘hahala
salama pa makimbilio’.
Kipindi hili cha
Mashahidi kinahusisha manabii wawili watakaosababisha mvua kutonyesha wakati
wote wa kipindi cha kutoa unabii wao. (Sasa, ni budi ikumbukwe kwamba mvua
imekuwa ikinyesha kwa kipindi chote cha miaka 1,260.) mashahidi hawa wanatabiri
wakiwa wamevaa magunia kwa kipindi chote cha miaka mitatu na nusu.
Ufunuo 11:5-14 Na
mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na
mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. 6 Hao
wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao.
Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo,
kila watakapo. 7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao,
yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na
kuwaua. 8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule
mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao
aliposulibiwa.
Mji huo ni dhahirishahiri
Yerusalemu. Waadventista wana tatizo hapa kwa kuwa mji wa Paris haukuwa ndiyo
aliosulibiwa Kristo ndani yake.
9 Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na
taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa
kaburini.
Watu wa lugha
mbalimbali na mataifa wanafanya kuwe na idadi kubwa sana ya watu. Ni dhahiri,
inaweza kutendeka tu katika siku za wigo mkubwa wa mawasiliano na ya wengi,
kama ulimwengu wote utakuwa uwanaona watu hawa wakiwa wamelala kwenye mitaa na
wataacha hivyo hivyo bila kuzikwa. Hii huenda ni rejea kutoka kwenye mapokeo ya
zamani kwamba mtu ambaye hajafa kihalali au kikawaida kwa sheria ya Kiyahudi
asitangazwe au asichukuliwe kuwa amekufa hadi atakapoonekana kuwa bado amekufa
kwa muda wa siku tatu mchana na usiku. Inawezekana pia kwamba tunaona kiunabii
kipimo cha nyakati zikiwa nzito na zinazopungua, kila siku.
10
Nao wakaao juu ya nchi
wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa
manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.
Hii haijawahi
kutokea bado huko nyuma. Kwa hiyo ni wazi sana kwamba ni tukio linalokuja huko
mbele yetu.
11
Na baada ya siku hizo
tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu
yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.
Mashahidi hawa
walifufuka baada ya kuthibitika kuwa amekufa kwa siku tatu na nusu.
12
Wakasikia sauti kuu
kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu,
adui zao wakiwatazama. 13 Na katika saa ile palikuwa
na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba
wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza
Mungu wa mbingu. 14 Ole wa pili umekwisha pita, tazama
ole wa tatu unakuja upesi
Kuna idadi kadhaa
ya mawazo na mapendekezo kuhusu andiko hili. La kwanza ni kwamba Mashahidi hawa
hawawezi kuuawa hadi pale watakapohitimisha huduma na majukumu yao. Wanasimama
mbele ya mungu wa Dunia hii, ambaye ni Shetani (2Wakorintho 4:4), na wapo pale
ili kutoa ushuhuda au kuwahubiria watu mambo asiyoyataka yeye na yasiyotakiwa
na imani na mfumo wa ulimwengu huu. Hakuna kinachoonekana kukemewa hadi pale
kilipokemewa kwa kinywa cha hawa mashahidi wawili. Huo ndio mtazamo wa
kibiblia. Ulimwengu hauwezi kukemewa hadi unapokuwakuwa inakemewa kwa vinywa
vya mashahidi hawa wawili, na ndiyo maana wako wawili na ndiyo sababu
wanasimama pamoja dhidi ya mungu wa Dunia hii. Ni hadi hapo mwishoni wa miaka 6,000
ya kudumu kwa mfumo wa ulimwengu huu ndipo Shetani na mapepo watahukumiwa kwa
kupitia mfumo wake.
Wale wanaotafuta
kuwaua Mashahidi hawa watauawa kwa namna hiyohiyo. Hiyo ndiyo kanuni ya
kibiblia ya jinsi tunavyohukumu, na ndivyo tutakavyohukumiwa pia nasi; na hivyo
ndivyo itakavyowatokea watu hawa. Mungu atawafanyia kwa jinsi hiyohiyo
walivyowafanyia Mashahidi wake. Utaratibu wa kuwahukumu umeanzishwa Mashahidi
hawa. Haya ni marejesho mapya yatakayoanzisha utaratibu wa kuhukumu, ambao
utawezeshwa na kuakinizwa na Masihi atakaporudi. Hii ndiyo nguvu ya Eliya,
aliyekuwa na uweza wa kuuagiza moto kutoka Mbinguni ushuke chini uwauwe makuhani
waliokuwa wanaitumikia miungu ya uwongo (1Wafalme 18:1-46) na wale waliojipanga
kumdhuru yeye (2Wafalme 1:10-15) au kwa kweli walioonyesha dharau au utovu wa nidhamu
kwa watumishi waliochaguliwa na kutiwa mafuta au wajumbe wa Mungu wa kweli kama
tunavyomuona na Elisha pia (2Wafalme 2:23-24). Elisha alikuwa na uweza kwenye
maji pia (2Wafalme 2:19-22) na dhidi ya mvua. Mbingu ilifungwa kwa ajili ya dhambi
za watu walishuhudiwa kwenye vinywa vya mashahidi wawili (1Wafalme 8:35; sawa
na Mambo ya Walawi 26:19; Kumbukumbu la Torati 11:17). Nguvu hizi za Uliya
zilikuwa na maana sana. Zilitumika kwa njia nyingi na zilikuwa na utendaji kazi
wa namna mbalimbali.
1Wafalme 8:34-36 basi,
usikie huko mbinguni, ukawaachilie watu wako Israeli dhambi yao, ukawarejeze
tena katika nchi uliyowapa baba zao. 35 Ikiwa mbingu
zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili
mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, wakati ule
utakapowatesa; 36 basi, usikie huko mbinguni,
ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; unapowafundisha
njia iliyo njema, iwapasayo kuiendea; ukanyeshe mvua juu ya nchi yako,
uliyowapa watu wako iwe urithi wao.
Tunajionea
makundi mawili ya wateule,
watumishi wa Mungu (gurudumu la ndani), na Isaeli, ambao ni gurudumu la nje la
gari.
Mambo ya Walawi
26:19 Nami nitakivunja kiburi
cha uwezo wenu; nami nitazifanya mbingu zenu kuwa kama chuma, na nchi yenu kuwa
kama shaba
Hii ni hukumu
inayotokana na dhambi. Mashahidi hawa wanazichukua dhambi za dunia nyuma kwenye
kichwa chake.
Kumbukumbu la Torati
11:17 hasira za Bwana
zikawaka juu yenu, naye akafunga mbingu kusiwe na mvua, wala nchi isitoe
matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo Bwana.
Eliya alizifunga
mbingu kwa neno lake.
1Wafalme 17:1 Basi
Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa
Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua
miaka hii, ila kwa neno langu.
Ni wazi sana
kwamba Eliya alijua kwamba alikuwa na uweza juu ya mvua hata kwa kiasi kwamba
hata kama kulikuwa na umande au haukuwepo juu ya nchi, yeye alifunga tu. Ni
muhimu kwamba tujue Eliya alikuwa ni mtu wa namna gani kwa kuwa kuna dalili na
dondoo muhimu sana za kinabii kuhusu chimbiko la Eliya pia.
Eliya alikuwa ni
Mgileadi. Gileadi ulikuwa ni ukoo au familia ya jimbo la Gadi (1Nyakati 3:14) ambao
walikuwa ni wakazi wa Gileadi. Waliishi pande za mashariki mwa Yodani. Kumbuka
kuwa kulikuwa na makabila matatu ambayo hayakwenda kwenye Nchi ya Ahadi na
milki yao iko nje ya Israeli – na hiyo ni dalili na ishara kwa Nyakati za
Mwisho. Milki ya milele imo katika Manase, Gadi na Reubeni. Tukichukulia
umiliki nchi wa Israeli kwa kuelekea unabii (ambayo kwa kweli ni kuanzia
kuanguka kwa Yeriko; soma jarida la Kuanguka Kwa Yeriko (Na. 142)),
Gadi ni kabila kubwa nje ya Israeli katika Nyakati za Mwisho. Anapeleka majeshi
katika Israeli sambamba na Reubeni na Manase ili kwenda kuchukua urithi. Gadi
na Reubeni watayachukua maeneo mbalimbali. Reubeni, Simeoni na Gadi wapo upande
wa kusini na moja lipo upande wa magharibi na urithi wao uko ulikuwa nje ya
Israeli. Manase walikuwa upande wa magharibi. Kwa hiyo kuna makabila mawili
upande wa kusini na moja upande wa magharibi katika Nyakati za Mwisho
yanayokwenda Israeli. Makabila hayo yanaonekana kuchukua urithi wao kama sehemu
ya makundi yaliyojiunga pamoja chini ya agano la haki ya uzaliwa wa kwanza waliyopewa
Efraimu. Walikuwa ni wakazi tofauti katikati ya Waefraimu na Manase ambao ndio
walipigana nayo chini ya Yefta (Waamuzi 11:4).
Jina Gileadi
yawezekana kuwa lilichukuliwa kutokana na jina la nchi iliyo na makorongo,
ikiwa inapakana na uwanda wenye rutuba wa Bashani. Eneo lake linasemekana kuwa
linapakana na Amoni kwa upande wa kusini mwa Bonde la Yordani upande wa
magharibi, sehemu za kusini na kaskazini mwa Yaboki na kwenye jangwa hadi
upande wa mashariki, na pembezoni mwa Bashani, maili chache sana kusini mwa
Yarmuki upande wa kaskazini, urithi au milki ya Gadi ilikuwa ni nchi iliyo na
mawe na makorongo zaidi kuliko nchi ya Manase. Utithi wa makabila haya yote mawili
ulikuwa ni nje ya Israeli ilichukuliwa kuwa ni ng’ambo ya Yordani. Kamusi ya The Interpreter’s Dictionary of the Bible
inashikilia kusema kwamba Gileadi ni kabila lionekanako wazi kuwa sambamba na
makabila ya Reubeni na Dani, na ni sawasawa na kabila la Gadi. Dhana iliyokuwepo
huko nyuma ya pamoja na makabila ya Efraimu na Manase haina sehemu wala
uhusiano na urithi wa Wareubeni na Wagadi na sehemu yao kwa Waefraimu, au umuhimu
na maana ya urithi wao nje ya Israeli katika Nyakati za Mwisho kama ilivyoonyeshwa
kwa kuvuka kwao mto ili kwenda uichukua nchi ya ahadi ya Israeli kwenye mfano
wa kwanza wa nyakati za Yoshua. Huo ulikuwa ni unabii na pia ni ukweli wa kihistoria. Kwa maana ya kiupana
zaidi walienea kwa undani zaidi pande za kaskazini huko Bashani na hata ng’ambo
za mbali za Yamuki.
Kama ni matokeo
ya mtafaruku huu, jimbo la Manase ni kitu kilichotajwa kama lineloendelea
kuijieneza na kujishamirisha katika Gileadi. Hata hivyo, ni kawaida tu makabila
haya ya Reubeni na Gadi peke yao ndiyo yaliyokuwa huko. Kwa hiyo Wareubeni na
Wagadi walimiliki eneo moja. Inaonekana kwamba kulikuwa na ufalme wa kipeke
yake uliokuwepo huko Gileadi ukiongozwa na mfalme Peka, mwana wa Remalia, tangu
miaka miaka ishirini iliyowekwa au kuandikwa kwenye utawala wake kwenye 2Wafalme
15:27. Hii inaonekana kuwa ilitokea yapata kama mwaka 750 KK katika sehemu
iliyobakia ya utawala wa Yeroboamu II. Alitawala huko hadi mwaka 735 KK. Alimuua
mtangulizo wake akisaidiwa na Wagileadi (2Wafalme 15:25). Hatimaye alijaribu
kuwaunganisha wote waliokuwa kwenye majimbo yote yaliyowazunguka ili wakapigane
na Waashuru. Waashuru walimshinda na wakawachukua Israeli wengi wao wakiwa ni
Wadileadi (2Wafalme 15:29), na tangu wakati huo wahakuwa tena sehemu ya ufalme
huu. Hivyo walichukuliwa kwenda mbali utumwani kwa sababu ya upinzani
waliouonyesha kwa Waashuru kabla Israeli wenyewe hawajachukuliwa kupelekwa
kijumla utumwani. Gadi na Eeubeni na maeneo ya mashariki yenye uasili na
ushawishi na Wamanase walichukuliwa na kupelekwa utumwani kabla Israeli
hawajaenda kijumla utumwani.
Kwa hiyi, Eliya
anaweza kuchukuliwa kuwa alikuwa alitokana na kabila hili la Gadi pia, akitpkea
kwenye maeneo ya urithi wa Israeli ng’ambo ya Yordani. Tukio hili lina maana
yake kwa Nyakati za Mwisho kama tukichukulia kwamba mfano au alama kurithi nje
ya Israeli kuna maana yake kwa Mashahidi na mgawanyo wa makabila. Kama
tunatarajia matukio ya Nyakati za Mwisho kwenye unabii, hayatatokea kwa Efraimu
wala kwa Manase. Eliya alikuwa wa kabila la Gadi. Kutokana na uweza tunaouona
aliopewa Eliya wa kuamuru kuwe na baa kubwa la ukame, kushusha moto uwaunguze
watu na mambo mengine, tunaona kwamba Mashahidi nao watakuwa na nguvu na uweza wa
Eliya kama ilivyonenwa na kuahidiwa kwenye Malaki 4:5-6.
Malaki 4:5-6 Angalieni, nitawapelekea Eliya
nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. 6 Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na
mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.
Nguvu na ueza wa
nabii huyu haupo tu kwenye masuala ya kutenda miujiza peke yake, bali pia ni
kuhusiana na uezo wa kurejesha tena mahusiano ya kifamilia hapa Duniani ili
ziweze kuokolewa. Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtangulizi wa nabii huyu, lakini
hakuwa ndiye nabii huyo.
Mathayo 11:12-14 Tangu
siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao
wenye nguvu wauteka. 13 Kwa maana manabii wote na
torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. 14 Na ikiwa
mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.
Hivyo Yohana alikuwa
ndiye Eliya. Lakini kulikuwa na nabii mwingine ambaye alikuwa na roho ya nabii
huyo pia (soma pia kwenye Marko 9:11-13).
Mathayo 17:10-12 Wanafunzi
wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa
Eliya kuja kwanza? 11 Naye akajibu, akawaambia, Kweli
Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, 12 ila
nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote
waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
Hata hivyo,
Yohana Mbatizaji alikuwa ni Eliya kwa mujibu wa ushuhuda wake mwenyewe (Yohana
1:21). Kristo alisema kwamba alitimiliza kazi hiyo, lakini itatokea kwa uweza
na nguvu nyingi katika nyakati za mwisho na Eliya mwingine.
Marejesho mapya
ya mambo yote yatafanyika chini ya mfumo huo wa Nyakati za Mwisho (Mathayo
17:11). Mashahidi wana ngvu na uweza huo. Marejesho mapya ya mambo yote ikiwepo
maadhimisho ya Yubile na Miandamo ya Mwezi Mpya pamoja na mfumo mwingine wote
ya Ufalme wa Mungu, na uwezo wote wa kuelewa. Hakuna mwalimu wa ulimwengu huu aliyefanya
mambo haya yote hadi sasa. Mambo haya yatatokea.
Kristo hakuanza huduma
yake ya kufundisha hadi pale Yohana Mbatizaji alipofungwa gerezani. Wakati
Yohana alipomalizia huduma yake, ndipo Kristo alioanza kufundisha. Mungu
hakumpa Kristo fursa hadi Yohana alipomaliza. Na ndivyo ilivyo kwamba Masihi
hatakuja hadi pale Mashahidi hawa watakapokamilisho huduma yao.
Kuna uwezekano wa
aina mbili katika kushughulika na Mashahidi.
Uwezekano wa Kwanza
Uwezekano wa
kwanza ni kamba maneno haya yanatafsiri ya moja kwa moja, na Eliya amehamishwa mbele
kwenye nyakati za kuhitimisha kazi ya maandalizi ya Masihi, na ni mmoja wapo,
au anayeyangulia, Mashahidi. Hivyo kuna uwezekano wa kwamba Eliya na mtu
mwingine (ambaye hajajulikana bado) wanaweza kuletwa kwenye nyakati ambazo
hazitaweza kuondolewa. Kuna watu wawili tu kwenye Biblia ambao hawakufa, na
Biblia imeeka na kuainisha wazi kuhusu kutwaliwa
kwao. Filipo alitwaliwa pia na Mungu kutokana na maono ya Mwithiopia lakini
alitokea tena na akafa baadae (Matendo 8:39-40).
Kama Eliya ni
mmoja wa Mashahidi, basi itamlazimu kuungana na mwingine atakapohudumu na
kusimama huko Yerusalemu. Ndivyo inavyoonekana kuwezekana kabisa ndivyo
yanavyosema Maandiko Matakatifu. Watu wawili peke yao waliowahi kutwaliwa kabla
ya kufa kwao kwa mujibu wa biblia ni Eliya na Henoko. Kaka hivyo ni sahihi, ndipo
unabii wa Yeremia 4:15 unawatangulia, kwa kuwa hakuna aliye wa mchanganyiko wa
makabila mawili ya Dani na Efraimu kama alivyo nabii huyo. Henoko alikuwa wa
kwanza kutwaliwa. Huduma yake ilikuwa ni kukishuhudia kizazi kilichokuwepo
kabla ya Gharika Kuu. Mwingine alitwaliwa kwenye upande mwingine wa Gharika Kuu
na mwingine kwenye upande mwingine wa Gharika Kuu, kwa kuwa hawa Mashahidi wanahitaji
kueneza na kudhihirisha mwendelezo wa hila za utawala wa Kishetani na
maangamizo yake. Dunia ilihukumiwa na kuangamizwa kwa haki na utakatifu wa
Henoko. Sababu inayopelekea umuhimu wa Henoko ni kwamba uwepo wa watu wa
kipindi cha kabla ya Gharika Kuu hususan Wanefili na kuangamizwa kwa Dunia hadi
hapo na kwa njia ya Gharika Kuu. Kuangamizwa kwa ujumla kwa Dunia kutatokea au
kutafanyika mwishoni mwa kipindi cha miaka 6,000. Kwa hiyo, tuna awamu moja ya
maangamizo yalitofanywa na Gharika Kuu iliyohukumiwa dhidi ya Henoko.
Mwanzo 5:18-32 Yaredi
akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. 19 Yaredi
akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. 20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na
miwili, akafa. 21 Henoko akaishi miaka sitini na
mitano, akamzaa Methusela. 22 Henoko akaenda pamoja na
Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. 23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na
mitano. 24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye
akatoweka, maana Mungu alimtwaa. 25 Methusela akaishi
miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki. 26 Methusela
akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa
wana, waume na wake. 27 Siku zote za Methusela ni
miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa. 28 Lameki
akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana. 29 Akamwita
jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu
ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana. 30 Lameki
akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume
na wake. 31 Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na
sabini na saba, akafa. 32 Nuhu alikuwa mwenye miaka
mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.
Dunia haikuwa imeangamizwa
mpaka alipokufa Methusela. Mungu alituma Gharika Kuu katika mwaka wa kufa kwake.
Akiwa ni mwana wa Henoko, Methusela alilelewa kwenye maisha ya haki na
utakatifu na akajaaliwa aishi zaidi ya nyakati zake, na Dunia haikuangamizwa
wakati mtoto wa Henoko na mjuu wake wakiwa wangali hai hapa duniani. Ilikuwa ni
kwa kitukuu wa Henoko ambapo Bwana alipoweka mpango wa pili wa kuwaokoa walio
kwenye mstari wa uzao wa Adamu. Henoko alikuwa ni baba yake Methusela. Hakuwepo, kwa kuwa Mungu alimtwaa; lakini
hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu (Yohana 1:18). Halikadhalika Henocko hakuwa kiumbe
mwenye mwili atakayefufuliwa kwenye ufufuo wa wafu. Kristo alikuwa ndiye mzaliwa
wa kwanza wa waliokufa (Wakolosai 1:18). Kwa hiyo Henoko hakuwa ametwaliwa
baada ya Yesu Kristo. Yesu Kristo ndiye kichwa au kiongozi na wa kwanza wa wana
wa ufufuo. Alikuwa ni kiumbe wa kwanza kufufuka na mwanadamu wa kwanza
kufanyika kuwa roho. Kwa hiyo, Henoko hakutwaliwa akiwa kama kiumbe wa kiroho.
Kwa hiyo Henoko huenda ama alikufa au alihamishwa kwa nyakati mbalimbali. Jambo
hili laweza kutokea tu kama muda utakuwepo kama nadharia na dhana isiyo na
mashiko yake maalumu. Eliya alitwaliwa pia. Kwa kawaida anachukuliwa kuwa ni
kama alikufa, kama walivyo watu weote mbali na Kristo. Ulimwengu wa kiroho
hauwezi kubadilika kuwa wa kibinadamu hadi kwenye ufufuo wa wafu (soma majarida
ya Ufufuo wa Wafu (Na. 143) na Ufalme wa Milele wa Mungu (Na. 144)).
2Wafalme 2:1-17 Ikawa,
hapo Bwana alipopenda kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya
alitoka Gilgali pamoja na Elisha. 2 Eliya akamwambia
Elisha, Tafadhali, kaa hapa; maana Bwana amenituma niende mpaka Betheli. 3 Elisha akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako
iishivyo, sitakuacha, Basi wakashuka mpaka Betheli. Basi wana wa manabii,
waliokuwako Betheli, wakatoka kuonana na Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya
kuwa Bwana atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akasema, Naam, najua;
nyamazeni. 4 Eliya akamwambia, Tafadhali, kaa hapa,
Elisha; maana Bwana amenituma niende mpaka Yeriko. Akasema, Kama Bwana
aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Nao wakafika Yeriko. 5 Basi wana wa manabii, waliokuwako Yeriko, wakamkaribia
Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa Bwana atamwondoa bwana wako leo, asiwe
mkubwa wako? Akajibu, Naam, najua, nyamazeni. 6 Eliya
akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana Bwana amenituma niende mpaka Yordani.
Akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Wakaendelea
mbele wote wawili. 7 Basi watu hamsini wa wale wana wa
manabii wakaenda wakasimama, kuwakabili kwa mbali; na hao wawili wakasimama
karibu na Yordani. 8 Eliya akalitwaa vazi lake la juu,
akalikunja, akayapiga maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka
pakavu. 9 Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya
akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa
kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.
10 Akasema, Umeomba neno gumu; lakini, ukiniona
nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona, hulipati.
Huku
sio kumpotosha na kumvunja moyo Elisha, kwa kuwa alipaswa kuamini kwa moyo wake
wote kwamba alikuwa na mamlaka kamili ya Roho Mtakatifu, ili kuanzisha mambo
ambayo alipaswa kukamilisha mambo aliyotakiwa kuyakamilisha. Hakuna nafasi ya
kuonea mashaka kiimani ya kuyatendea kazi mamlaka ya Roho Mtakatifu. Kama
Mashahidi walionea shaka kitu chochote kabisa, basi wasingeweza kutendea kazi
mamlaka hayo ambayo walitakiwa kuyatendea kazi. Wanayatendea kazi mamlaka kwa
imani kwa njia ya Roho Mtakatifu.
11
Ikawa, walipokuwa
wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa
moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa
kisulisuli. 12 Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu,
baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa;
akashika mavazi yake mwenyewe, akayararua vipande viwili. 13 Kisha
akaliokota lile vazi la Eliya lililomwangukia, akarudi, akasimama katika ukingo
wa Yordani. 14 Akalitwaa lile vazi la Eliya
lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye
alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka.
Elisha alifanya
kilekile kabisa alichofanya Eliya. Alikuwa anayatendea kazi mamlaka yake katika
Roho kwa mwelekeo mwingine, akionyesha kwamba alikuwa na uweza na mamlaka.
Alikuwa anafanya hivyo mbele ya makuhani wa Israeli. Walikuwa wakitazama kutoka
mbali na kutazamia kimsingi kushuhudia kuhamishiwa kwa nguvu za Mungu. Walitaka
kuona kile kilichokuwa kinaendelea na Eliya na kungetokea nini kama Eliya
akiondoka. Kilichotokea ni kwamba mamlaka na nguvu hizi zilihamishwa kutoka
kwake na akapewa Elisha.
15
Na hao wana wa
manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa
juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake. 16 Wakamwambia, Angalia, wako hapa pamoja nasi watumishi
wako watu hamsini walio hodari; waende, twakuomba, wamtafute bwana wako; isiwe
labda roho ya Bwana imemtwaa na kumtupa juu ya mlima mmoja, au katika bonde
moja. Akasema, Msiwatume. 17 Wakamsisitiza hata akaona
haya, akasema, Haya! Watumeni. Basi wakatuma watu hamsini; nao wakatafuta siku
tatu, wasimwone.
Hii ni habari ya
kwanza ambayo kimsingi tuliyonayo tunapokuwa na mkururu wa siku tatu tu baada
ya kuondoka kwa Eliya.
Ina maana kwa
kiwango cha juu sana kwamba hapa Roho ya Eliya kumwingia Elisha. Hivyo, roho ya
Eliya iliaminika kuwa ilihama na inahamishika. Kwa hiyo kufumba kulikuwa dhana
ya muhimu sana. Nguvu na ueza huu wa kiroho ndipo ilijulikana kuwa ni kama
alitolewa na ili kwamba nguvu za Eliya iweze kujidhihirisha kwa watu wengine.
Hii ina maana ya kwamba awe wa pili kwa Elisha. Eliya anachukuliwa na waandishi
wengine kuwa iliamriwa ije baada ya kutwaliwa kwake. Hili ni jambo lingine kwa kuchora
mchoro.
Nguvu hizi za
Eliya zilihamishiwa pia kwa kufunika kwake. Manabii walimtafuta Eliya kwa siku
tatu baada ya kutoweka kwake. Jambo hili lina maana yake. Kipindi cha baada ya
kufa kwa Mashahidi kitakuwa pia cha siku tatu na nusu. Siku tatu zinahusiana na
ishara ya Yona na zinapatikana kwa kanuni ya kulinganisha kwa kipimo cha mwaka
sawa na siku moja pamoja na huduma ya Masihi. Mfano wa mwisho ni kwenye vifo
vya hawa Mashahidi. Uwezekano wa kwanza kwa hiyo ni kwamba ni Eliya na Henoko
walitwaliwa kwa wakati wote. Hiyo ingeonekana kama kichekesho, lakini kama tunawatafuta
au tunapowaona Mashahidi kwenye Biblia tunaona kuwa wapo watu wawili na
hawakufa, ambapo inaashiria na kuonyesha kwamba yawezekana kabisa kwamba
walitwaliwa na kusafirishwa kwa wakati wote wakiwa kama Mashahdi Wawili. Usishangae
tunapoliona gari la Eliya likiwashusha kina Eliya na Henoko mjini Yerusalemu.
Huu ndiyo uwezekano uliopo. Kwa hakika ndiyo maelezo, au ufafanuzi ambayo
vinginevyo hayapo na inayoondoa utofauti.
Mtazamo huu ulikuwa ni mtazamo asilia wa wakati
wa Kristo na pia ni wa kanisa la kwanza. Mashahidi watarajiwa walikuwa ni Eliya
na Henoko na kwamba inabakia hivyo hadi katika karne ya ishirini na yasiyo na
maana wala mashiko ya Makanisa ya Kisabato na mengineyo.
Uwezekano wa Pili
Uwezekano wa pili
ni kwamba Mashahidi wa Nyakati za Mwisho watautendea kazi uweza na nguvu
zilezile za Eliya. Huo ndio mtazamo wa kimapokeo iliopo kwenye Makanisa ya
Mungu ya Marekani. Mtazamo wa kwanza sio wa kimapokeo huko Marekani lakini
ulikuwa ni mtazamo wa zamani wa mahali penginepo. Mtazamo wa siku hizi huko
Marekani kusema kwamba walikuwa manabii wawili na wangali wanaishi hata sasa
hapa duniani. Ni budi watakuwa wangali hai wakati huu, wakitabiri wakati wenyewe
muafaka na kusisitiza ushikaji wa Torati. Ili kuandaliwa, watapaswa kuwa na
umri wa miaka zaidi ya thelathini ili waanze kuhubiri – vinginevyo watakuwa
wameihalifu Sheria ya Torati. Kwa hiyo, wanapaswa kuwa na umri wa zaidi ya
miaka thelathini kabla hawajafundisha na miaka thelathini kuanzia mwaka 1996
hadi 2026, na ndipo wataanza kuhudumu kwa miaka mitatu kabla ya mwaka 2026.
Muda mfupi sana ujao watakuwa hapa duniani mnamo mwaka 2023. Hiyo inamaanisha
kwamba watapaswa wawepo hai sasa, na kwa muda mfupi sana, umri wa mwaka mmoja
mwaka 1995.
Manabii hawa wawili yaonekana wanazitendea kazi nguvu hizi, wakiwa
wanajulikana kama ni manabii wa Nyakati za Mwisho. Andiko linaonyesha kwamba
hawa ni mizeituni miwili na vinara viwili vya taa wasimamao mbele ya mungu wa
Dunia kwa hiyo wao wanakabiliana uso kwa uso na Shetani. Kumbuka kuwa Shetani
alimkabili uso kwa uso Kristo hapo kwanza. Shetani alihukumiwa kwa kuhukumiwa
kwa kumhukumu kwake Kristo. Hata hivyo, kwa aliji hiyo, Mashahidi hawa
wanasimama mbele mungu wa Dunia hii na wanamkabili Shetani. Mfano kama huohuo
unatumika kwenye Zekaria 4:3,11,14. Tunaona sehemu ya kwanza inahusiana na ujenzi
wa Hekalu kwa kutumia roho saba za Mungu.
Zekaria 4:1-10 Na yule malaika aliyesema nami
akanijia mara ya pili, akaniamsha, kama mtu aamshwavyo katika usingizi wake. 2 Akaniuliza, Unaona nini? Nikasema, Nimeona, na tazama,
kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake, na taa zake saba
juu yake; tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwa taa zote zilizo juu yake; 3 na mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume
walile bakuli, na mmoja upande wake wa kushoto. 4 Nami
nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu,
vitu hivi ni nini? 5 Ndipo malaika
aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La,
Bwana wangu. 6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo
neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni
kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.
Hii
ni aya moja wapo ya aya za muhimu sana kwenye Biblia: Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa
roho yangu, asema Bwana wa majeshi. Hakuna kitakachotokea humu duniani kwa kushurutishwa au nguvu
au uweza mkubwa au nia kuu ya vitu hivyo. Itakujatokea kwa kupitia Roho wa
Mungu na ndiyo maana Mungu atafanya kazi katika Siku za Mwisho kwa kupitia watu
hawa wawili watakaonena katika Roho wa Mungu.
7 Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya
Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu
kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.
Ni
nini maana ya kichwa cha jiwe kilichopo? It is Messiah.
8 Tena neno la Bwana likanijia, kusema, 9 Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na
mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi
amenituma kwenu. 10 Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo
madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli;
naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote.
Kinara cha taa kilikuwa
ni kinara kimoja tu cha Maskani inayoonekana kwenye Kutoka 25:31 na kwenye
Hekalu la Pili. 1Wamakabayo 1:21 na 4:49 inaonyesha kwamba kwenye Hekalu la
pili walikuwa na kinara kimoja cha taa saba. Tunauona uwongo wa taa kwenye Duara la juu ya
lango la Tito au Titus huko Roma. Wakati Hekalu lilipobomolewa na majeshi
yakavichukulia mbali vyombo na mapambo ya dhamani ya Hekaluni, walichukua pia
kinara cha taa kubwa cha Hekalu la pili. Kwa hiyo tukio hilo lilichorwa kwenye
duara la zege la langoni likiashiria kuhusuriwa kwa Hekalu. Kwa hiyo, kulikuwa
na kinara kimoja cha taa au kinara cha taa kwenye Maskani, na kwenye Hekalu la
pili kulikuwa na kinara kikubwa kimoja kilichokuwa na taa saba.
Kwenye Hekalu la
Sulemani kulikuwa na vinara kumi vya taa kama tunavyoona kwenye 1Wafalme 7:49 (sawa
na Yeremia 52:19). Kuna dhana mbili zinazotofautiana zilizopo. Kwa hiyo
kulikuwa na kinara kikubwa kimoja chenye taa saba pamoja na halafu taa kumi.
Hawa Mashahidi wenyewe ni vinara viwili vya taa wanaosimama kwenye ama upande
wa kinara kile kikubwa ambacho kilimwakilisha Masihi. Hiyo ndiyo maana yake. Masihi
alikuwa ni kinara cha katikati cha taa, ya nane. Kutoka Masihi kulifuatia
makanisa saba. Kwenye kamanisa haya saba ndipo tunakuta vinara viwili vya taa
vya Mashahidi Wawili, vikiweka jumla ya idadi yake kuwa kumi kwa ujumla. Mfumo
wa mara kumi ulikuwa ni kitu kilichoonekana kwenye Hekalu la Sulemani. Andiko
la pili linaataja Mashahidi hawa, ambao ndio vinara kumi vya taa kwa upande wao
wa kuume. Hekalu la Sulemani lilionyesha mkururu wa taa hivi kumi kama zikisimikwa
kwenye ile ya kwanza ya zile saba. Kwa hiyo taa hizi kumi kwenye Hekalu la
Sulemani zilimaanisha Masihi, makanisa saba na Mashahidi Wawili. Mashahidi hawa
Wawili walipaswa kufanya kazi ya Makanisa ya Sardi na ya Laodikia, ambayo yote
yameshindwa. Kwa hiyo Mungu anaonyesha kwamba Si
kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi. (Zekaria 4:6).
Hekalu ni Kanisa
la Mungu. Suala hili limerudiwa na Zekaria (sawa na Zekaria 4:11) kama kwamba
amekuwa hajajibiwa bado kwenye mfano wa kwanza. Hii inaashiria harakati au
mkururu wa mambo wa pili.
Zekaria 4:11-14 Ndipo
nikajibu, nikamwambia, Ni nini mizeituni hii miwili iliyo upande wa kuume wa
kinara cha taa kile na upande wake wa kushoto? 12 Nami nikajibu mara ya pili,
nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile
mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao? 13 Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni
nini? Nikasema, La, Bwana wangu. 14
Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao
karibu na Bwana wa dunia yote.
Nukuu inasema simama kwa Bwana wa dunia yote. Hawasimami
kwa Bwana. Wanasimama kwa Mungu wa Mbinguni na wanasimama na Masihi anayechukua
sehemu ya kuwa Bwana wa Dunia yote. Wanaongelea juu ya vinara vya taa na wanasi,a,a
kwa Bwana wa Dunia yote, lakini wakiwa ni mashahidi wanasimama mbele ya mungu
wa Dunia hii. Kwa hiyo wanasimama mbele na kumkabili Shetani, lakini wanasimama
ama upande wa Yesu Kristo
anayeichukua nafasi ya Shetani. Hili ni andiko lingine linaloonyesha kwamba Shetani,
kama Nyota ya Asubuhi, amepewa nafasi na Yesu Kristo kama mungu wa Dunia hii.
Mwandamano huu wa
matukio imeanza baada ya kipindi kijulikanacho kama Nyakati za Mataifa. Tunajua
kwamba Hekalu liliangamizwa na mfumo au utaratibu wote ulichukuliwa utumwani
Babeli. Harakati hizi zapasa ziishie kwenye Wakati wote wa Wamataifa na iliathiri
imani zote mbili, yaani ya Kiyahudi na ya Kikristo. Na ndiyo maana kanisa la
uwongo au kanisa la yule Kahaba linaitwa pia Babeli Mkuu na Mama wa Makahaba (Ufunuo
17:5). Unabii huu unakutikana kwenye Zekaria 5:1-11.
Agano la Kale
laweza kujisimamia lenyewe. Agano Jipya ni ufafanuzi wa Agano la Kale, na siyo
mbadala au ukiukaji wa Agano la Kale. Agano la Kale linajisimamia kama lilivyo
kama tutalielewa. Hatuhitaji kuwa na Agano Jipya ili litusaidie kuuelewa Mpango
wa Wokovu na matendo ya Yesu Kristo kwa nyakati zake kama tutalielewa vizuri
Agano la Kale. Agano Jipya linahitajika kwa kuwa linalithibitisha Agano la Kale
na Agano Jipya linafafanua na linathibitisha kile kinachomaanishwa na Agano la
Kale. Tunaweza kukosea na Agano la Kale kama hatutalielewa vizuri. Kwa hiyo
Agano Jipya linalithamanisha na kulithibisha kiusahihi na kiukamilifu zaidi
maana ya nabii za Agano la Kale. Imani potofu na za uwongo zimelixhukua hilo na
kukiweka kiambishi cha ni msingi Wake lenyewe. Kwa Kiebrania inaandikwa
kwa umoja wa kike. Shinatri ni nchi ya Kibabeloni. Wanawake wawili wanaunda
mifumo na imani mbili, yaweza kuwa ama ya kitaifa (kwa mujibu wa Companion Bible) au imani za kidini.
Maana ya kina na ya ndani ni kwamba imani za Kiyahudi na Kikristo ziliharibiwa zote
na imani ya Kibabeloni. Na hayo ndiyo maana yake halisi.
Zekaria 5:1-11 Basi, nikainua macho
yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la chuo lirukalo. 2 Akaniuliza,
Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la chuo lirukalo; na urefu wake ni dhiraa
ishirini, na upana wake dhiraa kumi. 3 Ndipo akaniambia, Hii
ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye
atatolewa kama ilivyo upande mmoja, na kwa hiyo kila aapaye atatolewa kama
ilivyo upande wa pili. 4 Nitaituma itokee,
asema Bwana wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwivi, na katika nyumba
yake yeye aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katikati ya nyumba yake,
na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.
Hawa
siyo tu kwamba ni farasi tu ambao watu waliishi nao; bali walikuwa ni farasi wa
ibada. Utaratibu na imani ya kidini na Hekalu ziliharibiwa au kuangamizwa. Hata
mawe ya Hekalu yaliangamizwa kwa kuwa walikuwa wanaapa kwa uwongo kwa jina la
Mungu. Hii ndiyo imani ambayo iliyochukuliwa kwenye Hekalu na kwamba ndiyo
iliondolewambali kipindi cha ushahuhuda wa Yesu Kristo. Hii ndiyo imani pia
ambayo iliyochukuliwa na kuingiza kwenye imani ya Kikristo na kuuharibu au
kuupotosha kabisa Ukristo pia. Ndoto na mitazamo hii – yote mbili za Hekalu la
Kiyahuzi na Ukristo mkongwe – zitaangamizwa. Hiyo ndiyo maana yake. Mwishoni
mwake kila ndoto au mtazamo wa kila dini na majengo ya hapa duniani ya wanaodai
kuwa ni Wakristo yatabomolewa na kuangushwa chini. Wengi wataangamizwa, wawe ni
kama wana daraja za kiurithi ama sivyo.
5 Ndipo yule malaika aliyesema nami
akatokea, akaniambia, Inua macho yako sasa, uone ni kitu gani kitokeacho. 6 Nikasema, Ni kitu gani? Akasema, Kitu hiki ni efa
itokeayo. Tena akasema, Huu ndio uovu wao katika nchi hii yote; 7 na tazama, talanta ya risasi iliinuliwa; na tazama,
mwanamke akaaye katikati ya hiyo efa. 8 Akasema,
Huyu ni Uovu; akamtupa chini katikati ya ile efa; akalitupa lile jiwe la risasi
juu ya mdomo wa ile efa. 9 Ndipo nikainua macho
yangu, nikaona, na tazama, wanawake wawili walitokea, nao upepo ulikuwa katika
mabawa yao; na mabawa yao yalikuwa kama mabawa ya korongo; wakaiinua ile efa
kati ya dunia na mbingu.
Talanta au
kipaji cha kuongoza (kwa Kiebrania kikkar) ni karibu sana na kusema kuwa
ni santuri ya mviringo ambayo inafanyika kuwa ni kifuniko cha efa. Upepo kwenye mbawa zake ilikuwa ruach
ao roho. Hivyo yalipata nguvu kwa nguvu za kiroho. Mfumo na imani hii ya kidini
imepewa nguvu na Duniani kote na imetajwa au kuelezewa na Mashahidi katika siku
za mwisho. Mfumo na imanii hii imefikishwa mwishoni na ujumbe wa malaika kwa
Injili ya Ufalme wa Milele wa Mungu. Mfumo na imani hii itaangamizwa kwa ujumbe
huo.
10 Ndipo nikamwambia yule malaika
aliyesema nami, Hawa wanaipeleka wapi efa hii? 11 Akaniambia,
Wanakwenda kumjengea nyumba katika nchi ya Shinari; tena ikiisha kutengenezwa,
atawekwa huko mahali pake mwenyewe
Mfumo na imani hii
vililazimika vichukuliwe na kupelekwa utumwani Babeli, na imani ya Kibabeloni
ilianzishwa kwa sababu ya muundo mbaya na mpotofu wa kidini wa Israeli.
Kipindi hiki
kinaishia kwa nyakati saba au miaka
2,520. Ni kama tulivyoona kwenye jarida la Kuanguka kwa Misri (Na. 36): Unabii Kuhusu
Mikono Iliyovunjika ya Farao, kipindi hiki kinaanzia tangu mwaka 605 hadi 525 KK na kuishia kwenye miaka ya
1914 hadi 1995/6 BK. Huu ndiyo mwisho wa Utimilifu wa Mataifa. Awamu ya mwisho ya
miaka thelathini kwa hiyo ilianzia kwenye miaka ya 1996/7.
Kipindi hiki ndicho kinapelekea ujio wa Masihi. Mashahidi ni sehemu ya muhimu
sana ya harakati hiyo.
Dola ya Mnyama
itaruhusiwa kuwaua baada ya watakapohitimisha kutoa huduma yao ya unabii. Mii yao itaachwa ikiwa imelala mitaani kwa
muda wa siku tatu na nusu. Mashahidi hawa watafanya matendo kama yaleyale
aliyoyatenda Musa huko Misri. Magonjwa ambayo Musa aliyaamuru yawapate Wamisri
yaliwapata kwa kusababishwa na imani yao ya kiroho kama Mashahidi
watakaposhughulikia imani ya Byakati za Mwisho.
Mchakato huu uliathiriwa
na Eliya aliyeshuhudia dhidi ya dini na imani potofu za uwongo za dini
iliyokuwepo huko Israeli. Kwa hiyo Mashahidi hawa watashuhudia dhidi ya dini ya
uwongo, kwa pande mbili zote, yaani kwa Waisraeli na kwa mataifa. Mfululizo wa
unabii wao na upeo au kiwango chake vitatolewa baadae. Watu hawa wawili
watakaofanya kazi na matendo ya Musa na Eliya, wangali bado hawajachukua nafasi
zao. Muda muafaka wa kutangulia ujio wa Masihi. Kipimo cha Hekalu utaanza au
kutangulia kitendo hiki. Uwa wa Nje utakanyagwa kwa miguu wakati wa kipindi
hiki cha huduma ya hawa Mashahidi (Ufunuo 11:2-3).
Sehemu ya 2
Kuna jambo linguine kuhusu hawa Mashahidi linalojiri kwa upana zaidi kwenye
unabii na jaribio kuliko hawa manabii wakuu wawili watakaosimama mjini Yerusalemu
katika Nyakati za Mwisho kwa siku 1,260 wakiwa wamevaa nguo za magunia. Jambo
hli limeeleweka vibaya na mara nyingi limekanganywa na walivyo hawa wawili
wenyewe.
Mashahidi wameorodheshwa kwenye Biblia. Ni kina nani haa na Biblia
inawazungumziaje?
Kwenye Isaya 43, Mungu anampajina Yakobo na Israeli kama mashahidi wake.
Isaya 43:1-13 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye
aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita
kwa jina lako, wewe u wangu. 2 Upitapo katika maji
mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika
moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. 3 Maana
mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri
kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. 4 Kwa
kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda;
kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya
maisha yako. 5 Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe;
nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi; 6 nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana
wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia. 7 Kila
mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi
nimemwumba, naam, mimi nimemfanya. 8 Walete vipofu
walio na macho, na viziwi walio na masikio. 9 Na
wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye
kuhubiri neno hili, na kutuonyesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao,
wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli. 10 Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi
niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla
yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. 11 Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana
mwokozi. 12 Nimetangaza habari, nimeokoa, nimeonyesha,
na hapakuwa mungu wa kigeni kati yenu; kwa sababu hiyo ninyi ni mashahidi
wangu, asema Bwana, nami ni Mungu. 13 Naam, tangu siku
ya leo, mimi ndiye; wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi
nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
Kumbuka kwamba kwenye andiko hili tuna Yakobo na Israeli waliotajwa kama
watu tofauti.
Kwenye kifungu hiki, tunaona kwamba Mungu ndiye aliyemuumba Israeli (sawa
na ilivyo kwenye Isaya 44:2,21,24) na ni mkombozi (Isaya 41:14; 48:17; 49:7). Mungu
anawaita kwa jina nao ni watu waliokaribu nan i mali halisi ya Mungu (sawa na
isemavyo Isaya 45:3-4; Kutoka 19:5; 33:17).
Mungu huwalinda watu wake kwenye hatari zote (Zaburi 66:12). Hapa tumeona
kwamba kusamehewa kwa Israeli kunajumuisha mataifa ya Afrika (Misri na Ethiopia)
na Uarabuni (Sheba). Cyprus ilitarajiwa kuyashinda mataifa haya yote (kama
usemavyo ufafanuzi wa Annotated Oxford
Bible, kwenye Isaya 43:3c-7). Msamaha huu hapa kwa kweli ilihusiana na
wokovu wa Wamataifa.
Kutokana na Isaya 43:8-13 tunaona mlingano ufuatao ukijitokeza:
·
Israeli anaweza kuongoka (aya ya 8);
·
Mataifa yanakwenda kukusanyika pamoja lakini hawataweza
kuishinda miungu yao.
Kutokana na kipengele hiki, Mungu anatangaza kwamba hakuna na hatakuwepo
mungu mwingine (sawa na Isaya 41:23-24; 48:5).
Kutokana na Isaya 43:14 hadi 44:5 tunaona unabii unaohusu Ukombozi na
Marejesho mapya ya Israeli. Hapa tunamuona Mkombozi na Mtakatifu wa Israeli
wakiwekwa mrejeo sawa. Mkombozi ametajwa mara nyingi kwenye Isaya kuliko mahali
pengine popote. Katika Mwanzo 48:15-16 tunaona kwamba Malaika wa Ukombozi
alikuwa ni elohim wa Israeli (sawa pia na Isaya 43:1; 54:5; 59:20; Yeremia
50:34; sawa pia na Isaya 41:14; 47:4; 48:17 kwa neno hili ma Mtakatifu).
Kwenye Isaya 43:22 tunaona Yakobo na Israeli wakitajwa tena kwa kutofautishwa.
Isaya 43:22 Lakini hukuniita, Ee Yakobo, bali umechoka nami, Ee Israeli.
Mungu anafanya hivyo tena kwenye Isaya 43:28.
Isaya 43:28 Kwa hiyo nitawatia unajisi wakuu wa patakatifu,
nami nitamfanya Yakobo kuwalaani, na Israeli kuwa tukano.
Kwenye Isaya 44:1 ananena tena kwa wote lakini wakati huu ni kama kwa mmoja.
Isaya 44:1-5 Lakini sikia
sasa, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na Israeli, niliyekuchagua; 2 Bwana, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye
atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe,
Yeshuruni, niliyekuchagua. 3 Kwa maana nitamimina
maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga
roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa; 4 nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na
mifereji ya maji. 5 Mmoja atasema, Mimi
ni wa Bwana; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu
ya mkono wake, Kwa Bwana, na kujiita kwa jina la Israeli.
Hivyo, wawili hawa wako tofauti lakini wako kwenye mfumo wa mtu mmoja. Pia
tunaliona jina Yeshurun (SHD 3484) likijitokezwa
kwenye uwili huu. Neno Yeshurun linatokana
na shina la neno yashar (SHD 3474) lenye
maana ya kuwa mkweli au kunena kinagaubaga. Ina maana ya kufanya jambo moja kwa moja au kunena
kinagaubaga. Inapelekea dhana ya usawa na haki.
Tunaona hapa kwamba Mungu alimkomboa Israeli si kwamba alistahili lakini ni
kwa ajili ya uhusiano wake wa Kiagano na taifa hili. Mungu ndiye mfalme wao na
ufalme ule utakuwa umerejeshwa wakati yeye ajaye ambaye haki inakaa ndani yake
nani mfalme wa haki.
Mungu anaonyesha hapa kwamba atawafanya Israeli kuwa ni kama mtu mnyofu.
Kwa hiyo, Yeshurun itaunganishwa pamoja na Yakobo. Yakobo ni jina la baba yao
alipoanza safari ya imani, na Israeli ni jina alilokuja kuitwa baadae. Jina hili
lilikujakuwa pia ni jina la taifa la wana wa Yakobo. Kwa hiyo ukuwili unaonekana
wazi kabisa.
Kiumbe anayenenwa hapa ni Yahova, Mfalme wa Israeli na Mkombozi wa Israeli.
Yeye ndiye Yahova wa Majeshi. Hapa kuna watu wawili waliotajwa kwenye Zaburi 45:6-7.
Kiumbe huyu hapa ni haElohim aliyetajwa mahali pengine kama Yahovi wakati neno Yahova wa Majeshi halikutumiwa na yeye.
Anawatangaza hapa tena kuwa wao ni mashahidi wake.
Isaya 44:6-8 Bwana,
Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa
kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. 7 Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na
kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na
yatakayotokea, wayatangaze. 8 Msiogope wala msifanye hofu; je!
Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko
Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.
Mungu huyu ndiye Mungu Mmoja, wa Pekee na wa Kweli
(Yohana 17:3) na zaidi yay eye hakuna elohim. Wengine wote ni wadogo kwake. Tafsiri
ya RSV ina neno linaloishia na kifungu kisemacho: “Hakuna Mwamba? Simjui mwingine”. Hii inaonekana
kuwa imefichwa kwa Watrinitaria wasijue kea sababu ya mfano wake.
Isaya 44:8 Msiogope wala msifanye hofu; je!
Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko
Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.
Kwa hiyo, Mwamba mmoja ulikanganya pia mawazo ya mrengo wa kibaba wa hoja
za Petro zilizokuzwa na kuakinishwa na Kanisa Katoliki la Kirumi.
Dhana iliyoko
hapa ni kwamba Mungu anasughulika na Yakobo na Israeli kama mashahidi wake kwa
mataifa. Uwili unaotajwa hapa sio uwili wa Israeli na Yuda. Ni uwili wa kimwili
na kiroho. Yakobo ni jina aliloitwa baba mchamungu ambaye alikujakuwa Israeli,
jina ambalo maana yake ni kwamba atatawala
akiwa Eli. Kwa hiyo maana yake ni kwamba taifa ni shuhuda mmoja na Kanisa
ni shahidi mwingine. Kwa hiyo, ni Kanisa ndilo linalofanyika kuwa mwili au bodi
ya Israeli na litatawala kama Mungu au elohim, kama Malaika au Mjumbe wa Yahova
akiwaongoza (Zekaria 12:8).
Dhana ya Israeli kulinganishwa na Kanisa imeainishwa kwa kina kwenye
majarida ya Mithali 31 (Na. 114); Agano la Mungu (Na. 152); Wimbo Uliobora (Na. 145); Ufafanuzi Kuhusu Esther (Na. 63) na Upimaji wa Hekalu (Na. 137).
Ni siri kubwa na nyeti sana ya Mungu na kweli ya Kanisa. Kwa hiyo, sio wote
waliomo katika Israeli ni Waisraeli, na siyo wote walio wana wa Ibrahimu ni
watoto wake au uzao wake.
Warumi 9:6-11 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio
wa uzao wa Israeli. 7 Wala hawawi wote wana
kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa; 8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali
watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao. 9 Kwa
maana neno la ahadi ni hili, Panapo wakati huu nitakuja, na Sara atakuwa na
mwana. 10 Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye,
akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, 11 (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala
hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si
kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),
Hivyo Yakobo alikuwa Mwisraeli wa kimwili ambaye ahadi ya haki ya uzaliwa
wa kwanza alipewa, na kupitia kake yeye makabila yalibarikiwa (Wanzo 49:1-33).
Lakini alikuwa ni baba wa kimwili wa taifa. Baba wa kiroho alikuwa Mbinguni
na kwa hiyo, taifa lilifanyika kuwa la aina mbili; na Wamataifa ndipo waliitwa
kwenye taifa la Israeli na siyo la Yakobo. Paulo anaonekana kuwa anafanya
tofauti hiyo pia kwenye waraka wake wa 2Wakorintho 11:22 na anawataja Wayahudi na
Waisraeli.
Yacobo alikuwa ni shahidi wa Mungu kwa muda mrefu hadi kuanza kwa Kanisa.
Kanisa lilifanyika kuwa shahidi tangu kipindi cha Masihi na kuendelea.
Mgawanyiko huu unashabihi kwenye kipindi cha ufalme miaka – 1,000 tangu kipindi
cha Daudi hadi cha Masihi na miaka 2,000 tangu kile cha Masihi wa Haruni hadi Masihi
wa Israeli (au Ujio wa kwanza na wa pili).
Kipindi hiki kilitajwa pia na jeshi Sauli, ambalo aliligawanya kwa 2,000 na
1,000 na akawaweka kwake mwenyewe chini ya usimamizi na uangalizi wa Yonathan. Hii
iliashiria falme za kimwili na za kiroho ambazo kwanza ndizo Daudi alikuwa ni
mfano wake daudi alionyesha kuelekea Masihi. Hakuna shaka kuhusu andiko hili na
maana ya Warumi.
Waisraeli wa sasa ni Kanisa. Hivyo, ni kwenda mbali zaidi kulitendea kazi
andiko hili kwenye Isaya hadi kwenye andiko lililo kwenye Ufunuo 11:1-14.
Ufunuo 11:1-14 Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka,
ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo. 2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime,
kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini
na miwili. 3 Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili,
nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia. 4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile
vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. 5 Na
mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na
mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. 6 Hao
wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao.
Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo,
kila watakapo. 7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao,
yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na
kuwaua. 8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule
mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao
aliposulibiwa. 9 Na watu wa hao jamaa na kabila na
lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao
kuwekwa kaburini. 10 Nao wakaao juu ya nchi wafurahi
juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii
hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi. 11 Na
baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia,
wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama. 12 Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni
hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama. 13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na
sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko
lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu. 14 Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu unakuja
upesi.
Hapa tunaona kwamba manabii wawili wamekuwa wakitajwa kwa namna kwamba
wametabiri kwa musa wa siku 1,260. Wamekuwa na uweza wa kuzifunga mbinguvu
wakati wa kipindi chao hiki cha kutoa unabii na kuifanya mvua isinyeshe kabisa,
na hawatauawa hadi watakapo hitimisha kutoa unabii wao. Baada ya kuuawa kwao,
watalazwa mitaani kwa siku tatu na nusu na hatimaye watapaa juu mbinguni.
Mtu anaweza kusema kwamba kulikuwa na mambo au mitazamo miwili kuhusu
unabii huu kwanye hilo kwamba siku 1,260 za mateso zilikuwa pia ni miaka 1,260
ya kudumu kwa ile iliyojulikana kama Dola Takatifu ya Kirumi, iliyodumu tangu
mwaka 590 hadi 1850 BK wakati kweli ilipopigwa maufuku watu kuihubiri au
kuifundisha. Baraza la mahakama ya kidini la mwisho lilifanya kazi tangu mwaka 1823
hadi 1846 na takriban watu 200,000 walihukumiwa kifo, au wafungwe maisha na picha
au michoro, iliyopo kwenye Nchi ya Papa peke yake. Wengine wapatao 1,500,000 walewekwa
kwenye kifungo cha uchunguzi wa kisiasa (kama kinavyosema kitabu cha Malachi
Martin cha: The Decline and Fall of the
Roman Church [Kudhoofika na Kuanguka kwa Kanisa la Kirumi], kurasa za
250-254).
Hapa tunafika kwenye kichekesho lakini chenye mashiko wa Mashahidi hawa
Wawili kuwa ni taifa na Kanisa. Taifa na Kanisa ni mashahidi wanayoyashuhudia mataifa,
lakini wote hawa hawatauawa katika Siku za Mwisho, na miili yao haitalala
kwenye mitaa ya Yerusalemu kwa siku tatu na nusu.
Tunajua kutokana na Isaya kwamba kutakuwa na tukio
kuu sana la Kutoka la mataifa kwenye Nchi ya Ahadi katika nyakati za mwisho
ambapo kutafanyika tulio la kutoka la Misri lisikumbukwe tena.
Isaya 66:18-24 Nami nayajua matendo yao na mawazo yao;
wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao
watauona utukufu wangu. 19 Nami nitaweka ishara
kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na
Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu
wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu
wangu katika mataifa. 20 Nao watawaleta ndugu
zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika
magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka
mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli
waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi. 21 Na
baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na Walawi, asema Bwana. 22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya,
zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu
litakavyokaa.23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya,
na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi;
maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo
machoni pa wote wenye mwili.
Hivyo, taifa halitauawa na Waisraeli wataendelea kuwepo. Ni wazi sana
kwamba watakuwa na kazi ya kufanya katika kipindi cha Milenia. Kwa hiyo, maneno
yaliyoko kwenye Ufunuo 11 hayawezi kuwa yanalitaja taifa na uzao wa Yakobo.
Kwa hiyo kazi
ya aina hizi mbili za makundi zinajulikana na ziko wazi. Kazi ya kwanza kama
mashahidi halisi wa kimwili na kama mashahidi wa kiroho kwa kipindi cha zaidi
ya miaka elfu mbili ya Kanisa kuwa jangwani. Taifa la Israeli lilikuwa pia ni
watu ambao walipewa majukumu ambayo Kristo aliyasema wakati aliposema kuhusu
wajibu kuwa umeondolewa kutoka Yuda na wamepewa wanaozaa matunda (Mathayo
21:43).
Mashahidi hawa kwa hiyo ni awamu ya mwisho kwenye mchakato huu na watauawa
baada watakapokuwa wameifanya kazi yao. Hii imefanywa kwa sehemu na Masihi kwa
kazi aliyoianzisha mzingi wake kwa siku tatu, mchana na siku tatu usiku kaburini
na kisha akasubiri hadi asubuhi aenda mbinguni akiwa kama Mganda wa Kutikiswa.
Hivyohivyo ndivyo itatokea mwishoni. Ni kama walivyouawa Kristo na Yohana
kwa kuwashuhuda kwao Yuda, ndivyo itakavyokuwa pia kwa Mashahidi hawa wa
Nyakati za Mwisho watakavyouawa. Watu wa dunia yote watabadilishana au kupeana
zawadi kwa kusherehekea kuuwawa kwao. Hii haiwezi na haitaweza kufanyika kuhusu
taifa la Israeli na Kanisa. Na kama iliwahi kuwa hivyo, basi Maandiko yangekuwa
yametanguka, lakini Maandiko hayawezi kutanguka. Mmoja ni mfano wa mwingine.
Kanisa linasimama kama shahidi anayeishuhudia dunia. Wengi wa wateule
waliopo Kanisani wamekuwa wakiuawa kwa sababu za Kiimani kwa kipindi chote cha
zaidi ya miaka 1,260. Hata hivyo, sio wote watakaouawa katika siku za mwisho. Na
kwa jinsi hiyohiyo, ndivyo taifa nalo litadumu. Sababu ya kurudi kwa Masihi ni kwa faida ya
wateule. Kama hatarudi wakati Mungu atakapokuwa anakifupisha kipindi hiki cha siku
za mwisho, hakuna mwenye mwili atakayeachwa akiwa hai.
Mathayo 24:21-22 Kwa
kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu
mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22 Na
kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya
wateule zitafupizwa siku hizo.
Siku hizo zitafupishwa kwa ajili ya wateule. Kama wateule wote wangekuwa
Kanisani, na kuwa na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza wa Wafu, hivyo basi
lisingekuwa ni suala la ama siku hizo zingefupishwa au siyo. Bali atarudi ili
kuwaokoa wale walio taifa litakaloingia kimwili kwenye Milenia na kutawala kama
wafalme wa kimwili na makuhani ili kuufanya Mpango wa Mungu uhitimike.
Kwa hiyo hawatakufa na kulala mitaani. Ushuhuda ni mchakato endelevu, na
mwishoni utawahusisha manabii wakuu na mashuhuri wawili pia na wakiwa wamepewa
majukumu hayo na Kanisa na taifa kwa karne nyingi.
Kwa hiyo Kanisa na taifa vitafanya kazi kwa mambo yafuatayo:
·
Kutokana na ufalme wa kimwili huko Yerusalemu hadi
kwenye ufalme wa Masihi na wa kiroho wa Kanisa pamoja na kuangamizwa kwa Hekalu
la kimwili; na
·
Kutokana na miaka 1,260 ya kuanzia mwaka 590 hadi
mwaka 1850 BK.
Kuna ushabihiano wa kimwonekano wa Mashahidi Wawili wa siku 1,260 za mwisho
au miaka mitatu na nusu ya mapema sana kabla ya kurudi kwa Masihi.