Makanisa Ya Kikristo ya Mungu

[136]

 

 

 

Baragumu

(Jarida 1. 2 19950925-19970830)

 

Jarida hili linashughulika na mambo mawili yahusuyo Sikukuu ya Baragumu. La kwanza ni kuhusu kurudi kwa Masihi. Sehemu hii huelekea mbele kupitia maendeleo ya Kanisa kwa ujio na utawala wa milenia wa Kristo na kusanyiko lao Israeli. Jambo la pili ni Karamu ya Arusi ya Mwana Kondoo. Hapa hesabu za injili zimefanyiwa tathmini za kina na mlolongo wa matukio yanayozingira arisi hii ya Kristo na Kanisa pia yamejadiliwa. Jambo kuu kuhusu ukweli aina ya vazi la arusi la wateule ni la muhimu kwa Wakristo wote.

 

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Copyright © 1994, 1995, 1997 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org and http://www.ccg.org

 

 


Baragumu [136]

Sehemu ya 1-Ujio wa Kurudi kwa Masihi

 


Kusulibiwa na ufufuo

Kristio alitumwa hapa ulimwenguni ili kuwaokoa wanadamu kwa kuzichukua dhambi za ulimwengu (Mat. 1:21; Mat. 9:6; Mk. 3:28) kama Mwana-Kondoo (Ufu. 5:6-8). Kristo hapa ulimwenguni ili kuishuhudia kweli (Yoh. 18:37). Alichinjwa zamani kutika kuwekwa kwa misingi dunia kama zoezi la mplango wa kimbinguni uliowekwa kabla ya mambo yote na Mungu (Ufu. 13:8). Ufalme wake umekaribia kuja hapa duniani. Alikusudiwa na kujulikana hata kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu lakini alidhihirishwa mwishoni mwa nyakati kwa ajili yetu (1Pet. 1:20).

 

Kama wanadamu hawatamwamini Kristo kuwa ni Masihi, watakufa na dhambi zao (Yoh. 8:24). Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu ambazo tulizifanya sisi kwa mujibu ya vile yasemavyo Maandiko Matakatifu (1Kor. 15:3-4), akawatokea zaidi ya watu mia tano (1Kor. 15:5-6). Kristo alisulibiwa na kafufuka toka kwa wafu (Mk. 16:6). Baada ya kufufuka kwake, alipaa juu kwenda mbinguni kwa Baba yake ambaye ni Baba yetu na kwa Mungu wake ambaye ni Mungu wetu sisi pia (Yoh. 20:18). Ameketi katika mkono wa kuume wa Mungu pamoja na jeshi la malaika, mamlaka na uweza uko mikononi mwake (1Pet. 3:22).

 

Maendeleo ya Kanisa

Yesu alikuwa hayupo kwa muda mrefu ili kwamba idadi kamili iliyokusudiwa ya wateule iweze kuletwa kwake (Ufu. 7:3). Kanisa limeendelea kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu mbili ili kutimiliza mpango wa mpango wa wokovu. Mpango huu ulionekana kwa mfano wa mlolongo wa vinara vya taa vya Hekalu la Mfalme Sulemani (2Nya. 4:7). Kulikuwa na vinara kumi vya taa kila kimoja kikiwa na taa saba. Vinara hivi kumi vya taa viliwakilisha vipingi kumi vya zamu ya kuanzishwa kwa Hekalu la Mungu. Kinara cha kwanza kilimwakilisha Masihi. Vingine saba vinavyo fuatia huwakilisha makanisa saba yaliyo chini ya wale malaika wa yale makanisa saba. Vinara viwili vya mwisho viliwakilisha mashahidi wawili waliopewa uweza moja kwa moja na Mungu.

 

Kipindi kinachotangulia kurudi kwa Masihi kitakuwa na ishara ya dhiki kuu na ukengeufu wa kidini. Kristo alifundisha kuhusu mlolongo wa mambo utakavyokuwa katika mafundisho yake ya kinabii aliyoyatoa kwenye Mlima wa Mizeituni. Mafuatano ya mambo ya matengenezo yameashiriwa na jinsi mlolongo wa mambo ulivyo kwenye Siku Takatifu za mwezi wa Tishri. Siku ya kwanza ya mwezi wa Tishri ni Sikukuu ya kupigwa Baragumu. Sikukuu hii hutangaza ujio wa Masihi. Kisha kipindi hiki huendelea mbali hadi wakati mwingine ambacho kinatoa kielelezo kwa urefu wa kitambo cha siku za ndani ya mwezi wa Tishri. Mlolongo huu wa mambo ulitolewa kielezo na kipindi cha maombolezo kwa kifo cha nabii Musa siku kadhaa kabla hawajaingia nchi ya ahadi (Kum. 34:8). Maisha ya Musa yaliwakilisha vipindi vitatu vya miaka elfu mbili au ya idadi ya Yubile 120. Kipindi cha siku thelathini za mwisho kinaonyesha muda unaotakiwa kwa uanzishaji kipindi cha utawala wa Milenia. Kwa hiyo kipindi cha kuanzia Ujio wake hadi Upatanisho kimeashiriwa na kipindi cha Kupigwa kwa Baragumu na Siku ya Upatanisho.

 

Kipindi cha kuanzia Upatanisho hadi uanzishwaji wa mfumo wa Milenia kimefananishwa na kipindi cha Upatanisho wa msamaha wa dhambi hadi katika Siku Takatifu ya kwanza ya Vibanda. Sayari yetu ya dunia inaandaliwa kwa ajili ya tukio hili na ukweli ule unamaanishwa mkusanyiko unakaofanyika jioni ya Siku Takatifu ya kwanza na ambyo haiwezi kuachwa mpaka asubuhi (Kut. 23:19). Kristo alifundisha kuhusu mambo haya, katika Mathayo 24:3-51, akitoa humo mafunuo ya jumla ambayo hatimaye Mungu aliyatoa kwenye kitabu cha Ufunuo wa Yohana.

 

Mathayo 24:3-8 inasema: Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? 4 Yesu akajibu akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema , Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. 6 Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. 7 Kwa maana taifa litaongoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa , na matetemeko ya nchi mahali mahali. 8 Hayo yote ni ndiyo mwanzo wa utungu.

 

Mwandamano huu wa mambo kuanzisha utaratibu wa dini ya uwongo wa muhuri wa kwanza ambao unafuatiwa na mihuri mingine ya vita, njaa, magonjwa mazito mazito ya kuambukiza, na maafa. Jambo hili katika Ufunuo 6:1-17 limeendelezwa kufafanuliwa kwenye mafuatano ya majarida yahusuyo sikukuu ya Vibanda. Ufunuo wa Yohana 6:9-11 inahusika na fafanuzi za pili kutoka katika Mathayo 24:9.

 

Mathayo 24:9-14 inasema:. Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. 10Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. 11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. 12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. 13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 14 Tena habari njema ya ufalme wa itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

 

Kwa hiyo, dhiki ya muhuri wa tano imeendelezwa kwa kipindi kirefu cha muda. Kinatangulia unabii wa Danieli ulioko kwenye aya ya 15 na unaendelea hadi kufikia kuhubiriwa kwa injili kwa kwa mataifa yote.

 

Mathayo 24:15-28 inasema: Basi.hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), 16 ndipo walio katika Uyahudi na walimbilie milimani; 17 naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; 18 wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. 19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! 20 Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya Sabato. 21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo. 23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yupo kule msisadiki. 24 Kwa maana watatokea makriso wa uongo, na manabii wa uuongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. 26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yupo nyumbani, msisadiki. 27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 28 Kwa kuwa popote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.

 

Kwa hiyo, kuna kipindi kirefu cha mateso na hatimaye dhuki inayosababishwa na vita. Wateule watateswa na hatimaye kutainuka kutoka kwenye mfumo huu wa mwisho mfumo wa dini ya uwongo ambao utaudanganya ulimwengu, na yamkini hata walio wateule. Awamu ya pili ni ile ya ishara za mbinguni ya muhuri wa sita wa Ufunuo 6:12-17.

 

Mathayo 24:29-51 inasema: Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu alija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. 31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu. 32 Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu, 33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. 34 Amini, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia. 35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. 36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. 37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilivyokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile alivyoingia Nuhu katika safina, 39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 40 Wataki ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. 41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. 42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. 43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiachia nyumba yake kuvunjwa. 44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yu aja. 45 Ni nani basi yule mtumwa mwaaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? 46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. 47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. 48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; 50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, 51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake oamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

 

Neno la msisitizo hapa ni kwamba kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yatimie lina tafsiri za aina mbili. Kitu jambo moja kilicho hakika ambalo ni kwamba Kristo alikuwa hamaanishi kuwa ni kizazi kilichokuwepo kwa watati ule. Kama angekuwa na maana hiyo, basi angekuwa ni nabii wa uwongo na kwamba, hakuwa Masihi. Mafafanuzi yake yana maana pana na halisi. Kizazi kimoja huchukua miaka arobaini. Nabii Musa na mtumishi wa Mungu aliishi kipindi cha vizazi vine au miaka 120. Hii inaweza kufananishwa na Yubile 120 kwa kulinganisha Yubile moja kwa kila mwaka ikichukuliwa sawa na (Yubile 120 huchukua kipindi cha miaka eflu sita). Kipindi cha mwisho cha maisha ya Musa kiliwakilisha Yubile arobaini au kipindi cha mwisho cha mpango wa miaka elfu sita wa wokovu. Kwa hiyo, Kristo alikuwa anasema kuwa kipindi cha mwisho wangemwona Masihi akikaribia na kwamba watu walioko hai akiwamo wasingepita wote. Sehemu ya tatu yenyewe isingepita zake.

 

Kipindi cha mwisho kinafunika kipindi cha miaka elfu mbili kutoka yubile ambayo Kristo alizaliwa na Yubile ambayo alianza kufanya huduma yake na kuwahukumu Yuda kwa Ishara ya Yona (tazama jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi mpya wa Hekalu [013]. Kristo alizaliwa kati ya miezi ya Septemba 6 KK na Januari 4 KK. Asingeweza kuzaliwa tarehe nyingine zaidi ya Januari 4 KK ikizingatiwa kuwa kifo cha mfalme Herode kilikuwa mwezi Marchi tarehe 4 KK. Kwa hiyo, alizaliwa kwa mzunguko wa wakati kamili au miaka kumi na nane kuanzia mwanzo wa Yubile ile, ambayo ni karibu mwezi Septemba 5 KK. Mwaka 1995, wakati wa maadhimisho ya kupigwa kwa Baragumu, yanayoanzia kipindi ambaco ni cha miaka elfu mbili kuanzia kutungwa mimba za Yohana Mbatizaji na Masihi. Maadhimisho ya siku ya Upatanisho mwaka 1996 hufanya pia mzunguko wa Yubile ya mwaka 1977/8, inayoadhimisha Yubile ya arobaini kuanzia kuzaliwa kwa Kristo. Vile vile mwaka 1996 huadhimisha kumbukumbu ya miaka 3,000 tangu Daudi alipoingia mjini Yerusalemu. Kipindi hiki kwa hiyo huhesabiwa kama mfano na maana ya kinabii. Masihi alianza huduma yake mwaka 28BK ambao ulikuwa ni mwaka wa kurudi baada ya Yubile ya mwaka 27BK ambao ilikuwa ni mwaka wa kumi na tano wa utawala wa mfalme Tiberio, tunao muona Yohana Mbatizaji akianza huduma yake. Kristo hakuanzisha huduma yake hadi Yohana Mbatizaji alipotiwa gerezani baada ya Pasaka ya mwaka 28BK. Kwa hivyo, huduma ya Masihi ilikuwa ni mwanzo wa zama mpya kuanzia mwanzo wa Yubile. Kipindi cha Yubile ya arobaini au kipindi cha miaka elfu mbili inaishia mwaka 2027. Mwaka 2028/9 ni mwanzo wa milenia ya saba, ambayo kwa mtazamo wa kale kipindi hiki kiliitwa ni cha Utawala wa Haki. Kipindi cha kuanzia miaka ya 1996 hadi 2025/6 ni kipindi cha miaka thelathini ambayo tunajihusha na maisha ya Masihi. Kipindi hiki tutajionea ujio wa Masihi na kutiishwa kwa hii sayari. Mfumo wa yubile unahitajika kuwa ni mwaka wa kuzidi kwa mavuno ikiitangulia Sabato ya saba ya mwaka 2026/7 na mwaka wa Yubile wa 2027/8. kipindi cha kupiganwa vita vya siku za mwisho na ujio wa Masihi unaoanzia mwaka 1996 na kuendelea hadi mwaka 2025/6. Masihi ataanza kutawala akitokea mjini Yerusalemu kuanzia siku ile ya utawala wa Mulenia. Vita ihusuyo nabii wa uwongo na ya mnyama itakayo jikita huko Yerusalemu itaanzia sawa sawa kuanzia mwaka 1996 na kuendelea.

 

jambo la mwisho la kutokea katika kipindi cha mwisho, kabla dunia haijaamuriwa kufanyiwa madhara kwenye utaratibu huu, ni hukumu ya wateule. Utaratibu wake ulitabiriwa katika kitabu cha mabii Ezekieli 34. Katika siku za mwisho, wachungaji watajilisha wenyewe na kuwaacha kondoo (Eze. 34:4-5). Kwa hiyo, wachungaji wataondolewa au kuachishwa kuchunga. Kristo atawahukumu kondoo kulingana na vile wao wanavyofanyiana kila mmoja na mwenzake (Eze. 34:17). Hii inaweza tu kufanyika viruri kwa kuwaachisha au kuwaondoa wachungaji. Kuondolewa huku pamoja na hukumu vimeelezewa katika kitabu cha Zekaria 11. Zekaria 11:3 inaongelea kuhusu ole kwa wachungaji.

 

Zekaria 11:3-13 inasema: Sauti ya wachungaji, ya uchungu mwingi! Kwa maana utukufu wao umeharibika; Sauti ya ngurumo ya wana-simba! Kwa maana kiburi cha Jordani kimeharibika. 4 BWANA, Mungu wangu, alisema hivi, Lilisheni kundi la machinjo, 5 ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe BWANA, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii. 6 Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema BWANA; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa wenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa mikononi mwao. 7 Basi nikalilinda kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge sana. Kasha nikajipatia fimbo mbili; nami nikaiita ya kwanza, Neema, na ya pili nikaiita, Vifungo; nikalilisha kundi lile. 8 Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walizichukia. 9 Ndipo nikasema, Sitawalisheni; afaye na afe; atakayekatiliwa mbali na akatiliwe mbali; nao waliosalia, kila mmoja na ale nyama ya mwili wa mwenzake. 10 Nikaitwaa hiyo fimbo yangu, iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili nipate kulivunja agano langu nililolifanya na watu wa kabila zote. 11 Nayo ikavunjwa siku ile; na hivyo wale kondoo wanyonge walionisikiliza wakajua ya kuwa neno hili ndilo neno la BWANA. 12 Nikawaambia, Mkiona vema, nipeni ujira wangu; kama sivyo, msinipe. Basi wakanipimia vipande thelathini vya fedha kuwa ndio ujira wangu. 13 Kisha BWANA akaniambia, Mtupie mfinyanzi kima kizuri, hicho kilichotiwa kima na watu hao. Basi nikavitwaa vile vipande thelathini vya fedha, nikamtupia huyo mfinyanzi ndani ya nyumba ya BWANA.

 

Andiko hili katika Zekaria 11:3-13 ni unabii unaohusu kuharibiwa kwa mfumo wa maongozi ya kimungu katika Israeli na kushindwa kwa mfumo wa kikuhani. uthabiti wa Neema ilikuwa ni anano na Israeli. Masihi alikuwa ni Masihi wa Haruni aliyechukua neema iliyotolewa kwa Israeli na kuipanulia wigo wake hadi kwa Mataifa. Hapa unabii unatimia wa kuwa makuhani walimsaliti na kuwalipa wasaliti wake vipande thelathini vya fedha. Zaidi sana, kiasi kile cha fedha kilitakiwa kitiwe kwenye hazina. Hata hivyo, fedha zilipaswa ziondolewe kwa kuwa zilikuwa ni fedha za damu. Vipande thelathini vya fedha vilionekana kudharauliwa sawa kama kima cha kumnunulia mtumwa (tazama tafsiri ya Biblia ya Soncino, kwenye kitabu cha Kutoka 21:32), lakini pia ilipimwa kama kipande kimoja kwa kikundi cha baraza la Mungu. Pia tatizo la kuharibiwa kwa wachungaji watatu kwa mwezi mmoja kumeelezewa na Biblia ya Soncino ili pengine kuelezea aina tatu ya watawala katika Israeli walioitwa wafalme, makuhani na manabii.

 

Kwa hiyo, uondozi wa Israeli unaondolewa kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kipindi hiki cha mwezi mmoja kimeelezewa kwenye kitabu cha nabii Hosea 5:7. Huu ni mwezi mwandamo mpya wa uangamivu.

 

Hosea 5:5-7 inasema: Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; kwa sababu hiyo, Israeli na Efraimu wakajikwaa katika uovu wao, Yuda naye akajikwaa pamoja nao. 6 Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng’ombe wamtafute BWANA; lakini hawatamwona; amejitenga nao. Wametenda kwa hila juu ya BWANA, maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawala pamoja na mashaba yao.

 

Biblia ya Soncino inaendeleza fafanuzi zinazoonyesha majaribio mbali mabli kuonyesha hawa wachungaji watatu walikuwa ni kina nani. Kwenye tafsiri ya Talmud, walidhaniwa kuwa ni Musa, Haruni na Miriamu.

 

Wanaotetea wazo la zama za kabla ya siku za uhamisho wa utumwa wa Babeli wanadhania kuwa hawa watakuwa ni wale wafalme wa mwisho wa Israeli, yaani Zekaria, Shalumu na Manahemu, au pamoja na wafalme wa mwisho wa Yuda, yaani, Yehoazi, Yehoyakimu na Sedekia (kwa mujibu wa rabi Kimchi). Watetezi wa mtazamo wa zama za Wamakabayo wanadhani kuwa watu hawa watakuwa ni makuhani wakuu fulani waliokuwepo kwa nyakati zile kama vile Yasoni, Lysimaki na Menala; au penyine ni Yuda wa Makabayo mwenyewe pamoja na ndugu zake kina Yohathani na Simoni (kwa mujibu wa rabi Arbarbaneli), aliyetawala watu kwa kipindi cha mwezi mmoja tu wa miaka, yaani miaka thelathini. Mtu mmoja aitwaye Driver huangalia kwa uangalifu mkubwa sana pale anaposema kuwa, ‘Usemi huu unaonekana kuwa utatokea kwa wakati fulani, ambao hatutaweza kuujua kwa sasa’. Neno mwezi mmoja huenda ukawa ni usemi usemi wa kawaida lenya maana ya muda mfupi (kama ilivyo katika Hosea 5:7). Muunganiko wa ratiba ya majira ya kipindi cha miaka thelathini kwa mwaka kulinganishwa na siku moja misingi yake imekaziwa kwenye mawazo ya watoa fafanuzi. Huu pengine ni msingi wa utambulisho wa Musa, Haruni na Miriamu kama watu watatu kwa sababu ya kipindi cha kwanza cha siku thelathini za maombolezo. Kanuni hii ya kuhesabia mwaka sawa na siku inaonekana ikielezewa na unabii huu. Kwa hiyo, tunaonekana kushughulika na kipindi hiki cha miaka thelathini wakati machungaji hawa watakapokuwa wameondolewa kutoka na kondoo watapewa uwezo wa kukisimamia wenyewe. Hii italingana na dhiki na kipindi cha kuja kwake.

 

Fimbo hii ya Neema ilifanya kazi kama ulinzi hadi pale utimilifu wa Mataifa uwasili. Kwa hiyo, vita vya mwisho vitachukua pahala pake katika kukamilisha unabii uhusuo siku za Mataifa Wapagani. Hii ilivunjwa, ili kuondoa ulinzi wa Israeli (pia tazama tafsiri ya Sonsino).

 

Zekaria 11:14 inasema: Ndipo nikaikata vipande viwili fimbo yangu ya pili, iitwayo Vifungo, ili nipate kuuvunja udugu uliokuwa kati ya Yuda na Israeli.

 

Hapa muungano kati ya Israeli na Yuda umevunjika. Mambo mawili ya utawala yanaonekana kutenganishwa. Tunajua kwamba Ufalme wa Mungu uliondolewa kutoka Yuda na kupewa taifa linaloonyesha matunda ya Ufalme. Kwa hiyo, uvunjaji wa fimbo ya Umoja ulihitaji kusimikwa kwa wale sabini (na wawili) (Lk. 10:1, 17) kama baraza jipya la Sanhedrin na ukuhani mpya. Ukuhani huu ulitakiwa uendelee kwa miaka mingi sana mpaka siku za mwisho. Kisha kungeonekana kuinuka kwa mchungaji mwenye kuabudiwa kama sanamu.

 

Zekaria 11:15-17 inasema hivi: 15BWANA akaniambia, jitwalie tena vyombo vya mchungaji mpumbavu. 16 Kwa maana, lazima, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuzirarua-rarua kwato zao. 17 Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kuume; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kuume litakuwa limepofuka.

 

Kuharibiwa kwa kondoo kunaonekana kama ni tatizo kubwa. Sehemu ya pili ya unabii huu inapatikana katika Zekaria 13:7-9.

 

Zekaria 13:7-9 inasema hivi: Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, akisema BWANA wa majeshi; mpige mchungaji, na kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo. 8 Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema BWANA; lakini fungu la tatu litabaki humo. 9 Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio watu wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.

 

Hii inaongelea kwa siku za mwisho. Kondoo wametawanyika. Theluthi mbili watakatiliwa mbali na theluthi moja watabaki wakiwa hai. Theluthi moja nayobakia watajaribiwa kwa moto wa ile dhiki. Watanunua kwa Bwana dhahabu iliyosafishwa kwa moto. Hiki ni kipindi kitakachotangulia mapema kabla ya kurudi kwa Masihi. Mtazamo huu wa mwisho wa muhuri ya tano, wa sita na wa saba unachukua kadiri ya miaka thelathini kukamilika. Wakati wa kipindi hiki chote, taifa zima la Israeli, kwa mtazamo wa kote kuwili, yaani kimwili na kiroho, litashughulika na utaratibu wa jinsi ya kuwa na utawala wake wa kifalme, kikuhani na kinabii ulioondolewa, na watu wake kuuawa. Waliosalia katika taifa lile watakuwa kama wana simba wadogo kati ya mataifa. Mchakato huu utaelezewa kwenye jarida la Kupimwa kwa Hekalu [137]. Kwa kipindi chote cha miaka thelathini ya Masihi kitaondoa kabisa utawala wa kidunia na mifumo yote ya kidini, kifalme, kikuhani na za manabii wa uwongo.

 

Ujio wa Kristo wa Mara ya Pili

Kristo alikuja kwanza akiwa kama dhabihu kwa ukombozi na msamaha wa dhambi. Hakuja kwanza akiwa kama Mfalme Masihi na hii ilikosa kueleweka na Wayahudi wa siku zake zile. Wao walitegemea kuwa na mfalme mshindaji (Mat. 27:11,29,37; Lk. 23:2-3,37-38; Yoh. 19:14-16). Walakini alitambuliwa na baadhi yao kwa kupitia Roho Mtakatifu, kama Mfalme wa Israeli (Yoh. 1:49; 12:13-15) ili kutimiliza unabii (zek. 9:9).

 

Marejesho ya mfumo wa Biblia kupitia ujio wa Masihi yanapatikana katika Zekaria 14:4. Kristo alisema kwa mifano, kwamba ilimpasa yeye atoke kwanza kisha arudi tena (Lk. 19:12). Yesu atakuja tena kwa uweza, akiwa na Jeshi la malaika wa mbinguni (Mat. 25:31) akiwa kama Mfalme Masihi (Ufu. 17:14). Kuja kwake kutakuwa wazi bila uficho wowote kama nuru imulikavyo kutoka mawinguni (Mat. 24:27). Atatawala kwa uweza akizungukwa na watakatifu (Ufu. 20:4).

 

Masihi atakuja au kufikia juu ya Mlima wa Mizeituni. Akiwa na wateule, ataanzisha utawala wale. Atalijenga tena Hekalu (Mdo. 15:16). Atauanzisha tena mfumo wa kibiblia kukiwemo maadhimisho ya vipindi vya Siku Takatifu. Wakati huo, mataifa yote watalazimika kutuma wajumbe au wawakilishi wao huko Yerusalemu kwa ajili ya kuishika Sikukuu ya Vibanda, vinginevyo, mvua haitanyesha kwao katika vipindi vyao vya majira ya vyua (Zek. 14:16-19). Atamuangamiza asi au mwana wa kuasi wakati atakapokuja (2The. 2:8) na, hatimaye atatamalaki nguvu za mamlaka yote ya dunia. Mtu wa kuasi atakuja kwa mfano wa kutenda kwake Shetani kwa uwezo wote na ishara na ajabu za uwongo (2The. 2:9). Ukengeufu huu umeletwa kwenye Hekalu la Mungu kwa sababu hawakakabali kuipenda kweli wapate kuokolewa. Kwa hiyo, Mungu awaletea nguvu za upotevu ili wauamini uwongo kwa kuwa hawakuipenda kweli katika sehemu ya kwanza (2The. 2:10-12). Bwana atauangamiza mfumo huu wa ukengeufu kwa pumzi ya kinywa chake kwa ufunuo wa kuwepo kwake wakati atakapokuja (2The. 2:8). Ukengeufu huu hutokea miongoni mwa wateule ili kwamba kama ikiwezekana iwezekane kuwadanganya yamkini hata walio wateule (Mat. 24:11,24).

 

Utawala wa Milenia wa Kristo

Utawala wa Milenia wa Masihi umeelezewa kisahihi katika kitabu cha Ufunuo 20:2-7. Kipindi cha miaka elfu moja kimeelezewa kama cha Milenia au Chliadi. Kristo ataanzisha utawala wake hapa kwenye sayari hii utakaochukua kipindi cha miaka elfu moja akitawala pamoja na watakatifu waliofufuliwa (Ufu. 20:3-4). Shatani atafungwa kwa miaka hii elfu moja na kufungwa kuzimu au kwenye shimo lisilo na mwisho wa kina chake au kwa lugha nyinge huitwa tartaros, mahala pa malaika walioasi (2Pet. 2:4).

 

Watakatifu wale waliochinjwa vichwa vyao kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu na neno la Mungu na wale ambao hawakumuabudu yule mnyama na sanamu yake au kuipokea chapa ya alama yake kwenye vipaji vya nyuso zao au mikononi mwao, watafufuliwa na kutawala pamoja na Kristo kwa kipindi cha miaka elfu moja (Ufu. 20:4). Huu ndio ufufuo wa kwanza (Ufu. 20:5). Hao wafu waliosalia hawatakuwa hai hata itimie hiyo miaka elfu moja (Ufu. 20:5). Huu ndio ufufuo wa pili au wa watu wote.

 

Wakati huu wa kipindi cha miaka elfu, Kristo ataanzisha Ufalme utakaofuata mujibu wa sheria za kibiblia alizozitoa pale Sinai. Hii itatokea na kufanyika kutoka siku ile atakayosimama juu ya Mlima wa Mizeituni (Zek. 14:4,6). Mataifa yatajipanga kwa vita kuikabili Yerusalemu na yataangamizwa (Zek. 14:12). Na kila aliyesalia katika mataifa yote watakwea kwenda kila mwaka ili kumuabudu Bwana wa Majeshi na kuishika Sikukuu ya Vibanda au ya vijumba vya nyasi (Zek. 14:16). Maadhimisho ya Sabato na ya Siku Takatifu itakuwa ni ya lazima na sheria na amri zitatoke Yerusalemu. Mataifa yale ambayo hawatatuma wajumbe au wawakilishi wao huko Yerusalemu kwa ajili ya kuishika Sikukuu ya Vibanda, mvua haitanyesha kwao katika vipindi vyao vya majira ya vyua (Zek. 14:16-19).

 

Mwishoni kabisa mwa Milenia, Shetani atafunguliwa tena ili apate kuwadanganya mataifa tena wa ulimwengu mzima (Ufu. 20:7-8). Watakutanika tena kwa vita, lakini wataangamizwa kwa moto (Ufu. 20:9); na Shetani ataangamizwa. Kisha ya hapo, ule ufufuo wa jumla ya watu wote utatokea, na hukumu itawekwa (Ufu. 20:13-15).

 

Ujio wake utaambatana na ishara na miujiza mikubwa kwa uweza na utukufu mkuu (Mat. 24:27,30; Ufu. 1:7). Ujio wake utakuwa ni wa dhahiri ukiambatana na ishara kutoka mbinguni (Ufu. 6:12). Nguvu zitakuwa za mbingu zitatikisika. Jua litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga wake (Mat. 26:64; Mk. 14:62; Lk. 21:27; Mdo. 1:11).

 

Kristo atakuja kwa sauti ya malaika mkuu Mikaeli na kwa mlio wa parapanda ya mwisho (1The. 4:16-17; Ufu. 11:15). Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake wote, ili aweze kutukuzwa na watakatifu wake (2The. 1:10), pamoja na malaika wake, atawatenga watu na kuwashughulikia (Mat. 25:31-46).

 

Wateule, wale 144,000 na wale wote walio wa Ufalme wa Mungu, waliopewa Roho Mtakatifu kwa njia ya toba na kwa ubatizo wa watu wazima, wazishikao amri za Mungu, watafufuliwa wakati wa kuja kwake Kristo. Huu ni ufufo wa kwanza. Hao wafu waliobakia hawatakuwa hai hadi ufike mwisho wa Milenia. Huu ndio ufufuo wa pili (Ufu. 20:4). Wateule wanatakiwa kuwa na tumaini na kufikiria ujio wa Masihi (1The. 2:19; Ufu. 22:20). Wateule wanatakiwa kukaa katika hali isiyo na lawama kabisa, katika utakatifu wakiwa tayari kwa ujio wa Kristo na Jeshi lake la malaika watakatifu (1The. 3:13; 1The. 5:23). Kuipenda kweli ni muhimu ili kuweza kuokolewa (2The. 2:10). Bwana atamuua muovu wakati atakapokuja tena na ufunuo wa kuwepo kwake na pumzi za kinywa chake (2The. 2:8). Kanisa limeonywa kuwa macho na kuto lala kwa kuwa halijui saa ya kuja kwake Bwana (Mk. 13:35-37; Ufu. 3:3,11). Kristo anarudi kutoa hukumu ya haki na kufanya vita na wale wote wanaokataa kuzishika amri za Mungu (Zab. 96:13; Ufu. 19:11). Kristo atarudi na kushughulika na wanadamu kwa ajili ya matendo yao yote (Ufu. 22:12).

 

Kusanyiko la Israeli

Masihi atarudi ili kuiokoa hii sayari, na sio kuja kuiangamiza. Kuanzia mwanzo wa huzuni mateso yatachukua mkondo wake. Hii sayari itajiangamiza yenyewe. Masihi atawaokoa wateule.

Mathayo 24:9-22 inasema: 9Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao wataua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. 10 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana 11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. 12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. 13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 14 Tena habari njema ya ufalme wa itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. 15 Basi.hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), 16 ndipo walio katika Uyahudi na walimbilie milimani; 17 naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; 18 wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. 19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! 20 Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya Sabato. 21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.

 

Dunia itajiangamiza yenyewe. Masihi hatafanya hivyo. Atakuja kuuzuia mchakato huo.

 

Wakati wa kurudi kwake Masihi, wateule na wale waliopona kutoka Israeli ya kimwili, baadhi ya wale waliokuwa makuhani, watakusanyika mjini Yerusalemu wakitokea pamba nne za nchi (Isa. 11:12; 66:19-21).

 

Isaya 66:15-24 inasema: Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. 16Kwa maana BWANA atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi. 17 Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema BWANA. 18 Nami nayajua matendo yao na mawazo yao wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu. 19 Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa. 20 Nao watawaleta mdugu zenu wote kutoka mataifa yote kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA, kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi. 21 Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na Walawi, asema BWANA. 22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyo kaa. 23 Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA. 24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machini pa wote wenye mwili.

 

Kipindi hiki tutajionea uanzishwaji tena dini yenye mfumo wa kibiblia itokanayo na msingi wake kwenye kalenda ya enzi za kale ya mfumo wa mwandamo wa mwezi. Masihi ataanzisha tena maadhimisho ya Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zingine ikiwa kama ni mchakato wa marejesho ya sheria. Hii itafanyika kwa uweza na nguvu kupitia kwa majeshi ya Mungu. Kisha tutakwenda kwenye kipindi kikuu zaidi. Wale wasio batizwa waliobakia watakuwa kwenye ulinzi mkamilifu wa kimungu na watawakuza na kuwaendeleza Israeli na mfumo wa ulimwengu mpya wa Milenia. Watu hawa watajionea kama kitu rahisi kuingia hukumuni katika ufufuo wa wafu. Wateule watafanyika kuwa ni viumbe wa kiroho kwenye mchakato ambao sisi leo tunautathmini. Mchakato huu ni Arusi ya Karamu ya Mwana Kondoo.

 

Sehemu ya 2–Karamu ya Arusi ya Mwana Kondoo

 

1Wathesalomike 4:16-17 inasema: 16Kwa kuwa Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

 

Amrisho la malaika mkuu (Mikaeli) ni mwanzo wa muingiliano wa Jeshi la malaika wa mbinguni kwa mambo ya wanadamu. Inaashiria mwisho wa miaka elfu sita uliokuwa ni wa utawala wa Jeshi la pepo wachafu au malaika waasi. Amrisho hili kutangulia kwa kitambo ufufuo wa kwanza wa wafu, wa wale wateule wanajulikana au kuitwa kama walio kufa au kulala katika Kristo. Watu hawa ni wateule ambao wanaitwa kama waliolala (1Kor. 15:6,18; 1The. 4:13-15; 2Pet. 3:4). Pamoja na wale wa Kanisa ambao wako hai bado hata kuja kwake Masihi, watakwenda kuwa pamoja na Masihi huko Yerusalemu wakati atakapokuja.

 

Tukio hili linasuburiwa kwa muda mrefu ili kuungana na Masihi. Kwa lugha ya kibiblia katika vitabu vya injili, tukio hili limeitwa kama karamu ya arusi. Mfano wa tukio la karamu ya arusi unamengi ya kusema kuhusiana na aina ya watu wanaihisishwa Kanisani na wanaoanzisha wateule.

 

Mfano wa kwanza ni ule wa wageni walioalikwa. Wazo la wageni walioalikwa katika siku ya Bwana sio wazo lililotokana na mtazamo wa Agano jipya. Inaendeleza unabii uliotolewa katika Sefania 1:7.

 

Sefania 1:7-18 inasema hivi: Nyamaza kimwa mbele za BwanaMUNGU. Kwa maana siku ya BWANA i karibu; Kwa kuwa BWANA ameweka tayari dhabihu, Amewatakasa watu wake. 8 Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya BWANA, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni. 9 Na katika siku ile nitawaadhibu hao wote warukao juu ya kizingiti, waijazao nyumba ya bwana wao udhalimu na udanganyifu. 10 Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka mlimani. 11 Haya! Lieni, ninyi mkaao katika Makteshi, maana wafanyabiashara wote wameangamia, hao wote waliokuwa na mizigo ya fedha wamekatiliwa mbali. 12 Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. 13 Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake. 14 Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu. I karibu nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko! 15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya  fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu, 16 Siku  ya tarumbeta na kamsa, juu ya miji yenye maboma, juu ya buruji zilizo ndefu sana. 17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama zao kama mavi. 18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia, itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.

 

Kwa hiyo, wageni wameandaliwa kwa ajili ya siku ya Bwana. Mwisho mkamilifu na wa ghafla wa dunia hii hata hivyo unatanguliwa na kukaliwa kwa Yerusalemu.

 

Luka 21:24-27 inasema: Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa na kuchukuliwa katika mataifa yote, na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia. 25 Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; 26 watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbingu zitatikisika. 27 Hapo ndipo mtakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

 

Ishara hizi za mbinguni zimeelezewa katika Agano la Kale katika:

Isaya 13:10 kuwa: 10Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.

 

Na

Yoeli 2:10 inaposema: Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza

 

Ishara kutoka mbinguni zinaangukia kwenye mlolongo kamili katika kitabu cha ufunuo inatajwa kwenye muhuri ya sita.

Ufunuo wa Yohana 6:12-17 inasema: 12Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, 13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa , na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba na milima, 16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja, naye ni nani awezaye kusimama?

 

Muhuri ya sita yenye ishara za mbinguni huashiria kwamba ulinzi wa ndugu wapendwa unakaribia. Na kuwa mateso yanaonyeshwa kutoka kwenye muhuri ya tano kama ipo kwenye hatua mbili.

 

Ufunuo wa Yohana 6:9-11, inasema: 9Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. 10Wakalia kwa sauti kuu wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? 11Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao

 

Kwa hiyo, ndugu wapendwa walioko kwenye mateso mamoja waliambiwa wangojea mlolongo wa mauaji yaliyopangiliwa ya ndugu zao wapendwa katika mateso yanayo kuja au masumbufu unaofuatia baadae.

 

Mwana wa Adamu amepewa Ufalme kwa mujibu wa Danieli 7:13-14.

Danieli 7:13-14 inasema hivi: 13Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. 14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.

 

Kwa hiyo, Mwana wa Adamu alitolewa kwa Mzee wa Siku na kwamba yeye alipewa Ufalme wa Mungu. Huu ndio mlolongo na nafasi ya Kristo ambayo haiwezi kueleweka na wanaoamini mafundisho ya Utatu yaani Watrinitaria.

 

Ufalme umetolewa na kupewa Kristo na umezingiwa na uweza na unaambatana na uangamivu wa mfumo wa dunia. Tuliona mchakato huu kwenye jarida la: Kuanguka kwa Misri; Unabii wa Mikono Iliyovunjika ya Farao [036] kutoka katika Ezekieli 32:1-8.

 

Ezekieli 32:1-8 inasema: Ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA likanijia, kusema, 2 Mwanadamu mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, ukamwambie, Ulifananishwa na mwana-simba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa mguu wako, na kuitia uchafu mito yao. 3 Bwana MUNGU asema hivi; Nitautanda wavu wangu juu yako, kwa kusanyiko la watu wa kabila nyingi; nao watakuwa katika jarife lanmgu. 4 Nami nitakuwa juu ya nchi kavu, nitakutupa juu ya uso wa uwanda, nami nitawaleta ndege wote wa angani watue juu yako, nami nitawashibisha wanyama wa dunia yote kwako wewe. 5 Nami nitaweka nyama yako juu ya milima, na kuyajaza mabonde kwa urefu wako. 6 Tena kwa damu yako nitainywesha nchi, ambayo waogelea juu yake, hata milimani, na mifereji ya maji itajawa nawe. 7 Nami nitakapokuzimisha, nitazifunikiza mbingu, na kuzifanya nyota zake kuwa giza; nami nitalifunika jua kwa wingu wala mwezi hautatoa nuru yake. 8 Mianga yote ya mbinguni iangzayo nitaifanya kuwa giza juu yako, nami nitatia giza katika nchi yako, asema Bwana MUNGU.

 

Hivyo basi, kuna dhiki kuu inayotangulia ishara kutoka mbinguni na ambazo zinahusisha mateso ya wateule.

Mathayo 24:29-31 inasema: Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu alija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. 31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.

 

Dhiki kii inayoelezewa katika Mathayo 24:29-31 sio ile dhiki ya kumiminwa kwa kikombe cha ghadhbu ya Mungu inayoonekana katika ile baragumu ya saba. Mlolongo wa mambo haya unaelezewa kwenye jarida za Mihuri Saba [140] na Baragumu Saba [141]. Lugha iliyotumiwa kwenye vitabu vya injili wakati mwingine hubadilisha mlolongo wa matukio ya dhiki kuu. Mfano wa fumbo la wageni sasa lita tathminiwa.

Mathayo 22:1-14 inasema: Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mithali, akisema, 2Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. 2Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja. 4Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni nimeandaa karamu yangu; ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchunjwa, na vyote vimekuwa tayari, njooni arusini. 5Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake, 6nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, wakawauwa. 7Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao. 8 Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini walioalikwa hawakustahili. 9 Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni asurini. 10 Watumwa wake wakatoka wakaenda njia kuu wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni. 11 Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. 12 Aakamwambia, Rafki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa. 13 Mfalme akawaambiada watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

 

Wageni waalikwa walikuwa ni watu watakatifu ambao hawakumpokea Mashihi. Watumishi waliopoleka mwaaliko walikuwa ni wale manabii waliouawa kwaajili ya uenezaji wa habari njema za dini kwa siku zao. Mafarisayo walielewa kwamba Kristo alifundisha mambo yaliyohusiana nao na walitafuta kumuua (Mat. 22:15) ili wapate kumuua kama walivyowafanyia manabii kwa vipindi vya zama mbali mbali za huko nyuma.

 

Kwa hiyo, Wayahudi walishika kutoka kwenye fursa iliyoondolewa ya kikuhani, na ya Ufalme wa Mungu ulioenea hadi kwa Watu wa Mataifa. Kwa hiyo, wateule walitokea katika mataifa yote na pia walikuwa mchanganyiko na mazuri na mabaya. Mwili wa Kanisa halikuanzishwa kwa watu wenye mawaa na hawakuweza kusimama kwenye hukumu ya mashitaka waliyoshitakiana wao kwa wao kama walivyoitwa na kama kwa jinsi ile walivyoitwa.

 

Kipindi cha mpito wa hukumu kinapita kuanzia Lawi hadi Dani katika kurudi kwa Mashihi. Wakati Masihi atakapoanzisha wake katika Ufalme wa Mungu kutoka Yerusalemu halafu hukumu itaanza kutolewa kwa makuhani. Lawi watachukua nafasi zao kama mojawapo ya makabila ya Israeli ndani ya wale 144,000. Dani wataunganishwa hapa na Efraim kama sehemu ya Yusufu. Hata hivyo, mambo kumi na tatu yaleishapita kutoka kwa Lawi hadi Dani katika Milenia na hukumu kasha imetuama kwa Dani kwa kulingana na mujibu wa ahadi ya haki ya uzaliwa wa kwanza inayopatikana kwenye kitabu cha Mwanzo 49:16. Dani watamngojea Masihi kumiliki haki ya uzaliwa wa kwanza kama tunavyoona kwenye kitabu cha Mwanzo 49:18.

Mwanzo 49:16-18, inasema: Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya kabila ya Israeli; 17 Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia. Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali. 18 Wokovu wako nimeungoja ee BWANA.

 

Lawi wanakuwa ni kundi la kumi na tatu kama ilivyokuwa kwa Lawi wakati Yuda alipokuwa anatawala. Mabadiko haya na Masihi kama tunavyoona kutoka katika Mwanzo 49:8-12.

 

Mwanzo 49:8-12, inasema: 8Yuda ndugu zako watakusifu, Mkonmo wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. 9 Yuda ni mwana-simba, kutoka katika mawindo, mwanangu umepanda; Aliinama akajilaza kama simba mke, ni nani atakaye mwamsha? 10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake. Hata atakapokuja yeye mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. 11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu. 12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.

 

Kusanyiko la watu litakuwa huko Shilo au Masihi. Utawala utapita hadi kwa Masihi na hukumu hadi kwa Dani. Simeoni na Lawi wamekuwa wakitawanyika kati ya makabila ya Israeli kwa sababu ya ukatli wao. Walakini, hanao urithi wao kwenye karamu ya arisi ya mwana kondoo kwa idadi ya watu 12,000 miongini mwa watu 144,000. Sawa na kama ilivyo kwa Reubeni alipewa urithi wake kwa ajili ya asili yao kwa Yusufu kwa sehemu ya upendo wa baba yake kwa Yusufu. Wakati huo, Reubeni watakuwa wanapoteza haki yao ya uzaliwa wa kwanza kwa Yusufu hatahivyo watamlinda (Mwa. 37:21,29-30).

 

Vazi la Arusi

Moja kati ya aina ya mambo ya lazima ni kwamba, kila mgeni lazima awe na vazi la arusi. Vazi hili pia linajulikana kama kanzu nyeupe ya wafia dini kutoka Ufunuo 6:11 na pia kutoka katika Ufunuo 7:9-14.

Ufunuo 7:9-14 inasema: Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikonini mwao; 10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aliye katika kiti cha enzi na Mwana-Kondoo. 11 Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mnele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu, 12 wakisema, Amina, Baraka na utukufu na hekima na shukurani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele. Amina. 13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? 14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanaotoka katika dhiki ile kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.

 

Kwa hiyo, hawa wametoka kwenye dhiki ile kuu. Walikamilishwa kwa kupitia dhiki kuu na neema ya Mungu katika Yesu Kristo.

 

Masharti ya kuwemo kwenye arusi ni kuitwa na Mungu kama tunavyoona kwenye fafanuzi ikisema kuwa walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache. Hii imeelezewa katika jarida la Toba na Ubatizo (No. 52). Mfano wa wanawali wenye busara na wapumbavu linaonyesha pia uhalisi wa Ufalme wa Mbinguni.

Mathayo 25:1-13 inasema: Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. 3 Wle waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. 5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. 6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. 7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. 8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. 10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. 11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. 12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. 13 Basi kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.

 

Tendo la kuposa amaana yake ni kutanguliza kitu fulani ili kuonyesha udhati wa kuoa au ni kama nusu-ndoa na kwa hakika mila hii ilikuwepo kule Mashariki ya Kati katika siku ambazo Kristo alikuwa anatoa mfano huu. Kuposwa na Kristo kumeandaliwa na Mungu anayewatoa kwa Kristo katika ndoa.

 

Kwa hiyo, wanatakiwa kujiandaa kwa ajili ya arusi yao. Mafuta ya taa ni taa za Roho Mtakatifu. Mafuta yanatakiwa yaongezwe. Wale ambao hawakuchukua mafuta ya akiba pamoja nao ni wale ambao hawajajiandaa kwa njia ya ubatizo wa Roho Mtakatifu kwa njia ya toba. Idadi kubwa ya Wakristo wa jina tu au wakawaida hapa duniani hawajabatizwa. Wamedanganywa na walimu wa dini za uongo wa siku za leo. Kitendo cha wanawali wenye busara haumaanishi ubinafsi hapa kama mfano unaotolewa kuelezewa kuwa wokovu ni kitu cha kukichukulia kibinafsi. Wale waliokuwa tayari waliingia kwenye karamu ya arusi na wale ambao hawakuwa tayari walifungiwa nje. Wale wanawali wapumbavu walimuendea wakasema Bwana Bwana utufungulie. Kristo alisema hawajui. Hili ni shitaka maalumu yaani kwa wateule kumjua Kristo na Mungu wa Pekee wa Kweli aliyemtuma (Yoh. 17:3). Hili ndilo sharti la kuingia uzima wa milele. Kama hujui kuwa Kristo sio huyu Mungu wa Pekee wa Kweli, basi ni kwamba wewe humjui Kristo na yeye hakujui wewe. Hivyo ni kusema kuwa hutaweza kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni, hata kama utakuwa ulipewa malimbuko ya Ufalme wa Mungu wakati ilipoposwa au kuchumbiwa. Hawa wanawali wapumbavu ni wale ambao waliitwa lakini hawakuteuliwa kwa ajili ya ufufuo wa kwanza. Wataingia kwenye uhusiano katika ufufuo wa pili pamoja na kundi kubwa la Wakristo.

 

Kristo alisema katika injili ya Luka 6:46.

Luka 6:46-49 inasema: Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? 47 Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. 48 Mfano wake ni mtu ajenngaye nyumba, na luchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba, na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuutikisa; kwa kuwa umejengwa vizuri. 49 Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara, na maanguko yake nyumba ile yakawa makubwa.

 

Hapa tunaelewa kwamba msingi wa wito unatuama katika neno la Mungu kama lilivyotolewa na Masihi. Kushika amri ni muhimu ili mtu aweze kuwa na sehemu katika huu Ufalme chini ya Masihi aliwa kama Mfalme. Haitoshi kuliitia bure tu jina la Bwana.

 

Mathayo 7:21-23 inasema: Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nita waambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

 

Kwa hiyo, kule kuwa na uwezo wa kutoa unabii na kutoa pepo hakutoshi. Mambo haya yanaweza kufanywa pia na Shetani. Kipimo ni kutimiliza kuzishika amri na sheria za Mungu. Kifungu cha maandiko kilichopo katika injili ya Mathayo 25:1-13 kinaelezea na baaadae kifungu cha maandiko katika Mathayo 25:14-30.

Mathayo 25:14-30 inasema: Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. 15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. 16 Mara yule aliyepokea talanta tanoenda, akafanya biashara nazo, akachukua faida talanta nyingine tano. 17 Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. 18 Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. 19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. 20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. 21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu, ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi, ingia katika furaha ya bwana wako. 22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili, tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. 23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usichopanda, wakusanya usipo tawanya; 25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi, tazama, unayo iliyo yako. 26 Bwana wake akajibu akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya, 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba, nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. 28 Basi, mnyang’ang’eni talanta hiyo, mpeni yule aliyenazo talanta kumi. 29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atang’ang’anywa. 30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

 

Sharti ni kutoa zile kazi zilizowekwa kwako kwa namna bora zaidi iwezekanavyo. Haitoshi kule kuwa pale tu. Unatakiwa ufanye kazi. Matumizi ya vipaji ni kama dhahabu iliyotilewa na Masihi. Kanisa la Walaodikia lilifikiri kuwa lilikuwa yajiri. Ufunuo 3:14-22 inaonyesha mazingira ya lile kanisa.

 

Ufunuo 3:14-22 inasema: Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumbwa kwa Mungu. 15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu; wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka na maskini, na kipofu, na uchi. 18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao mimi nawakemea na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye asikiaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti chake cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie nano hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

Kanisa hili linajihesabia haki. Linadhani kuwa lina utajiri wote wa Ufalme wa Mungu na kwa kweli limetapikwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Kanisa hili, isipokuwa kwa baadhi ya watu binafsi, walitatiwa wanunue mavazi kwa njia ya mateso.

 

Zaidi ya makanisa yote, kanisa hili la mwisho ambalo udhaifu wake ulikuwa dhahiri. Kanisa la Laodikia lilikuwa na nguvu ya kifikra lilichechemea kiroho. Wakati linapokuwa pata changamoto na unabii katika ezekieli 34 na Malaki 2:1, kanisa ni dhahiri lilimuacha Mungu. Kwa hiyo, karamu ya mwana kondoo ni chanzo cha huzuni kwenye kanisa hili. Nguo nyeupe hapa zinaonekana kununuliwa kwa moto wa dhiki kuu. Wanafaidika kwa kuwa na bidii na kutubu. Toba ni kitu kilichopungua kwenye kanisa hili. Hali ya kujihesabia haki katika uongozi wake ndio kitu kilicho lipofusha macho kanisa hili. Kama hii ni zama ya mwisho basi ni kwa ajili ya mlolongo mwingine wa majaribu. Uongozi wa zama za kanisa la mwisho una maasi au ukengeufu mkuu ikiwemo miongoni mwa huduma yenyewe.

 

Kuna zama nne za kanisa vilivyopo katika kurudi kwa Masihi. Kutoka katika Ufunuo sura za 3 na 3 tunaona kuwa kuna masalia ya zama za Wathiatira, masalia wa Wasardi, masalia wa Walaodikia na masalia wa kanisa la Wafiladelfia. Yote mawili yaani la Sardi na la Laodikia yako kama ama yamekufa au yametapikwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Kwa hiyo, watu binafsi kutoka kwenye makundi haya kufanya ufufuo wa kwanza lakini huduma zao na teolojia zao haziendi sawa na mapenzi ya Mungu.

 

Wakati wa ujio wa Masihi, ni muhimu au lazima amuangamize kwanza mtu wa kuasi yaani asi au mwana wa ukengeufu. Asi mwana wa ukengeufu, ameelezewa kuwa ishara zake ni kwamba ataketi katika Hekalu la Mungu. Kwa hiyo yeye atakuwa ni mdogo kabisa katika hesabu ya Wakristo. Wateule hawataukubali Ukristo huu wa ki mamboleo uliokubalika na wengi kuwa ni miongoni mwa Hekalu la Mungu. Mfumo wa dini ya uongo umeitwa ni uasherati. Kwa hiyo, inakuja kiwazi kabisa kuwa kanisa la siku za mwisho lazima lijuike na mfumo andamizi ambao sisi tunaujua kama asi mtu wa kuasi na mwana wa ukengeufu. Kondoo hata hivyo wanatawanyika na mjumbe amewekwa kwa katika siku za mwisho ili kurarua kondoo mbali na mikono ya wachungaji na kuwapa kutawalana ili kwamba waweze kuhukumiwa. Mchakato huu inaitwa ni Kipimo cha Hekalu. Kimeelezewa katika jarida la Kupimwa kwa Hekalu (Na. 137).

 

q