Makanisa Ya Kikristo ya Mungu

[138]

 

 

 

Upatanisho [138]

 

(Toleo 2.0 19951004-19990901)

 

 

Kuifahamu Siku ya Upatanisho pia ni muhimu katika kuifahamu kazi ya Masihi katika njia mchakato huu. Kusudi la upatanisho katika dhabihu ndani ya hekalu zime jadiliwa pamoja na kazi za upatanisho katika utaratibu wa siku  ya Yubile.

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

(Copyright © 1994, 1995, 1999 Wade Cox)

 

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:


http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Upatanisho [138]

 


Kitabu cha Mambo ya Walawi 23:26-32 kinasema: Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia 27 Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa Saba ni siku ya Upatanisho itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu, nanyi mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto. 28 Nanyi msifanye kazi yo yote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za BWANA, Mungu wenu. 29 Kwa kuwa mtu awayeyote asiyejitolea mwenyewe siku hiyo hiyo, atakatiliwa mbali na watu wake. 30 Na mtu yeyote afanyaye kazi ya namna yeyote siku hiyo, mtu huyo nitamwangamiza atoke katika watu wake. 31 Msifanye kazi ya namna yeyote ni amri ya milele katika vizazi vyenu, katika makao yenu yote. 32 Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtaziteza nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo sabato yenu.

 

Hivyo siku ya upatanisho ni Sabato ya kufanya mapumziko makuu. Kama haikutunzwa, wote wale watakatiliwa mbali kutoka katika watu wao. Kuondolewa huko ni kutoka katika taifa la Israeli ambalo wanajumlisha wateule kama Israeli wa Kiroho. Kwa hiyo basi, kushindwa kutunza Siku ya Upatanisho kuna maana ni kuondolewa toka kati ya wateule.

 

Kusudi la Upatanisho Kwenye Dhabibu za Hekalu

Dhabibu za Upatanisho zilikuwa ni kwa ajili ya kuweka wakfu Hekalu kwa msingi wa kila mwaka kwa sadaka za kuendelea za kusanyiko. Hii ilifanyika kupita makuhani, ambao wameamrisha kutoa ubani mtakatifu juu ya madhabahu ya Mungu. Ili kusiweko na mafundisho ya ki ukengeufu au ya mbele za Bwana. Dhabihu za upatanisho zilikuwa ni kwa ajili ya upatanisho wa Isareli ya Kiroho na ya asili kwa Mungu kupitia Yesu Kristo. Dhabihu za upatanisho zilikuwa ni shitaka dhidi ya Kuhani Mkuu.

 

Kutoka 30:1-10 nasema: Nawe fanya Madhabahu ya kufukizia uvumba; utaifanyiza kwa mti wa mshita. 2Urefu-wake utakuwa dhiraa moja, na upana wake dhiraa moja; itakuwa mraba; na kwenda juu kwake dhira mbili; pembe zake zitakuwa za kitu kimoja nayo. 3Nawe utaifukiza dhahabu safi juu yake, na mbavu zake kando kando, na pembe zake, nawe utaifanyia ukingo wa dhahabu kuizunguka.  4Kisha utaifanyia pete mbili za dhahabu, chini ya ukingo wake katika mbavu zake mbili, katika pande zake mbili utazifanya; nazo zitakuwa mahal pa kuitia miti ya kuichukulia. 5Na ile miti utaifanya kwa mti wa mshita, na kuifunikiza dhahabu safi. 6Nawe utaitia mbele ya lile pazia lililo karibu na sanduku la ushuhuda mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, hapo nitakapokutana nawe. 7Na Haruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza. 8Na Haruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uwe uvumba wa daima mbele za BWANA katika vizazi vyenu vyote. 9Hamtafukiza juu yake uvumba mgeni, wala sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, wala hamtamimina juu yake sadaka ya kinyweo. 10Naye Haruni atafanya upatanisho, juu ya pembe zake mara moja kila mwaka ataifanyia upatanisho, katika vizazi vyenu vyote; ni takatifu sana kwa BWANA.

 

Pazia lililosimama daima kama kizuizi kwa kusanyiko la Israeli. Uvumba wa daima ulikuwa unawakilisha maombi ya watakatifu kama maombezi kwa Israeli. Upatanisho katika hatua hii yalifanyika mara moja kwa mwaka.

 

Pazia hili lilipasuka kupitia sadaka ya Yesu Kristo ili tuweze kukutana na Mungu pale patakatifu pa patakatifu.

 

Madhabahu haikutakiwa kuwa na uvumba usio mtakatifu. La muhimu zaidi ni kwamba haikutakiwa kunajisiwa na aina yoyote ya matoleo mengine. Mfano ulielekeza kwa Yesu Kristo na Kipawa cha Roho Mtakatifu katika ukweli ulio safi. Kwa hivyo hakuna kuhani anayeweza kwenda kwenye Siku ya Upatanisho huku akijua kabisa kuwa yuko katika au chini ya utaratibu wa uongo. Wateule wote ni makuhani, wakitoa matoleo ya ubani kupitia Maombi na kufunga. (Ufu. 5:8)

 

Ufunuo wa Yohana 5:8  inasema: Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya Watakatifu.

 

Hakuna hata mmoja atakaye linajisi Hekalu la Mungu huku akiwa na mahusiano na utaratibu wa uongo au kwa kuabudu kitu kingine badala ya Mungu. Kwa hiyo tendo la kumwabudu Kuhani ilionekana kama ibada ya sanamu. Ilikuwa ni Kuhani Mkuu ambaye alipaswa afanye upatanisho kwa ajili ya kusanyiko na yeye mwenyewe na kwa damu yake. Kristo aliingia mara moja kwa ajili ya wote Mahali Patakatifu juu ya ufufuo wake. (Ebr. 9:11-28).

 

Waebrania 9:11-28 inasema: Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. 13Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyo nyunyiziwa kwenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; 14basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? 15Na Kwa sababu hii mjumbe wa agano la jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. 16Maana agano la urithi lililopo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. 17Kwa maana Agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya. 18Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. 19Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji ya sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, 20akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. 21Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyuzia damu vivyo hivyo. 22Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. 23Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabibu zilizo bora kuliko hizo. 24Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi, bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; 25wala si kwamba ajitoe mara nyingi kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake 26kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake, 27Na kama vile watu walivyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu. 28Kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi;atatokea mara ya pili pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.

 

Matoleo wakati wa Upatanisho ilikuwa ni kwa hesabu ya wateule wa Israel. Hii ililipwa kwa thamani ya nusu shekeli ambayo ilikuwa shekeli ya Kiebrania na shekeli ya Wafoeniki, siyo ya Kibabeli. Hivyo malipo ni kwa uzito uliokuwa sawa na bei; na sio katika taratibu za kigeni. Ni uzito ulio wekwa kwa matoleo kwa mtu na haitofautiani kwa hali ya mtu. Hesabu hii ya Israel ilikuwa imefanywa na Mungu wakati wa kuwekwa msingi wa ulimwengu Ufunuo 17:18 na uzito na kuwekwa malipo yalilipwa mara moja kwa ajili ya wote na Yesu Kristo. Tendo hili la kuwekwa huru linaashiria kuwa wokovu uliolipwa si kwa ajili ya mazingira ya asili ya kila mtu, bali kwa dhabihu ya Kristo iliyotolewa mara moja na kwa wote. Hivyo kwa kuchukua makusanyo wakati Upatanisho humshambulia wakati wenyewe wa kufaa wa dhabihu ya Yesu Kristo. Ni kwa sababu hii kwamba kuna makusanyo matatu yaliyoelezewa kwenye kitabu cha Kutoka 23:14-18,

           

Kutoka 23:14-18 kinasema: Mara tatu kila mwaka utaniwekea sikukuu. 15Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba kama nilivyo kuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abibu (kwa maana ndio mwezi uliotoa Misri); wala hapana mtu atakaye onekana mbele yangu na mikono mitupu; 16 tena, sikukuu ya mavuno, hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani. 17Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU. 18Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi.

 

Kwa hiyo, Upatanisho ni ule umetengwa maalumu kutoka katika aina ya matoleo ya nayo husiana na ukarimu na baraka za kibinafsi. Hivyo pia ni Baragumu. Hiyo ni kwa sababu wala havihusiani na vitendo vya mtu au jitihada. Upatanisho ni hesabu maalum

 

Kutoka 30:11-16 BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 12Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapompa BWANA kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu, ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo atakapowahesabu. 13Nacho watakachotoa ni hiki, kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini) nusu shekeli kwa sadaka ya BWANA. 14Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishrini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka ya BWANA. 15Matajiri hawataleta zaidi, wala masikini hawataleta lilichopungua, katika hiyo nusu shekeli, watakapotoa hiyo sadaka ya BWANA, ili ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu 16Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hama ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu 

 

Hivyo hesabu ya wana wa Israeli kama ilivyoripotiwa katika kitabu cha Hesabu 1 ilikuwa kwa makusudi ya kijeshi. Kosa la Daudi katika kitabu cha 2Samuel 24 ilikuwa ni kwa sababu ilikuwa imefanywa, sio kulingana na sheria, kwa kusudi ambalo lilihalifu na kupotosha mawazo ya malipo kwa Israel na Masihi

 

Kulikuwa na malipo kwa damu (yaliyoonyeshwa kwa nusu shekeli) kwa kuhesabiwa wana wa Israel kama kulivyokuwa na maana ya kiroho kwa kuhesabu. Pia ulinzi na uwezo wa Israel hakupimwa katika idadi. Haukupimwa katika nguvu, wala katika uwezo, ila kwa roho yangu anasema Bwana wa Majeshi (Zek. 4:6)

Tangazo la Yubile

Upatanisho pia ulitumika kutangaza Yubile, kwa kuwa Yubile ni msingi wa wataratibu wa Mungu wa kurekebisha mambo ya mwanadamu duniani. Maana ya kiroho ya Yubile itafafanuliwa siku zijazo.

 

Mambo ya Walawi 25:8-12 Nawe utajihesabia sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitaakuwa ni siku za sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda.9 Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu .10Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote waketio, itakuwa ni yubile* kwenu; nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake 11Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu  za mizabibu isiyopelewa. 12 Kwa kuwa ni yubile utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani.

 

Dhabihu ya Upatanisho

Dhabihu za Upatanisho zilifanywa kwa kutolewa mlomlongo wa wanyama. Hizi zimeorodheshwa katika kitabu cha Hesabu 29:7-11.

 

Hesabu 29:7-11 Tena siku ya kumi ya huo mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; nanyi mtazitesa nafsi zenu, msifanye kazi `yoyote ya utumishi; 8lakini mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza, ng'ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu, 9pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa huyo ng'ombe na sehemu ya kumi na mbili kwa huyo kondoo, 10na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba, 11na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.

 

Wanyama walichaguliwa kati ya wengine ambao walikuwa na mlingano kamili kama kwa kipimo cha efa ya unga. Dhabihu nzima iligawanywa kwa sehemu kumi lakini ilipimwa kwa uzani wa kumi na mbili kwa kumi ya yote. Kuna wanyama kumi pia.

 

Upatanisho kwa njia ya dhabihu kwa ujumla umeonyeshwa katika vitabu vya Kutoka 29:36, Mambo ya Walawi 1:4, 4:13-18, 20, 22-35, 5:6-10, 6:7, 10:17, 12:6-8, 14: 12 -32, 16:6, 10-34, 17:11, 19:22, Hesabu 15:22-28, 28:30, na Waebrania 9:22. Ni mawazo ya malipizo ya dhambi kwa njia ya matokeo ya hakika na yanayohusiana pia na mahitaji ya mtu katika kufanyiwa malipizo ya dhambi kama hatua zinazohusiana na kiwango na matokeo. Hakuna mashaka kuamini kuwa afya ya akili ya mtu pia inahusiana na hatua hii.

 

Dhabihu ya kuhani Mkuu pia ilikuwa na uhisiano na dhambi za mwanadamu na ahadi. Waebrania 5:1-14 inaonyesha matatizo ambayo yalijitokeza katika uhusiano mkamilifu wa Kristo na kujitolea kwake sadaka baada ya kuchaguliwa na Mungu. Kuhani Mkuu mwenyewe alikuwa amesongwa na udhaifu na hivyo anashugulika kwa upole na ujinga na ukaidi. Kwa sababu hii Mungu anawapa wanyonge msingi kwa Kristo ili kwa waweze kukamilisha na kutangaza hukumu kwa huruma. Kristo mwenyewe alisikika kwa hofu yake ya Kimungu.

 

Waebrania 5:1-14 Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matokeo na dhabihu kwa ajili ya dhambi, 2awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu, 3na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi. 4Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. 5Vivyo hivyo Kristo naye hakujifuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. 6Kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani milele kwa mfano wa Melkizedeki. 7Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; 8na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yalimpata. 9Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababa ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii, 10kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki. 11Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake, na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. 12Kwa maana iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 13Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 14Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.

 

Uwezo wa kutofautisha mema na mabaya na kula nyama ngumu ni alama ya wateule ambao waalimu wao wamefundishwa kwa vitendo katika kuvumilia mafundisho yenye uzima na kushughulika na kusahihisha makosa bila kujali kiini chake. Huu ni uweza wa Roho Mtakatifu katika kweli. Kuhani Mkuu alifanya Upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na makoza ya watu wengine. (Ebr. 9:7). Kristo alijifunza utii kupitia mateso na alisifika kwa hofu yake ya Kimungu.

 

Dhabihu ya Yesu ilikuwa kama Upatanisho ambao uliamriwa kimbinguni (Lk. 2:30-31, Gal. 4: 4-5, Efe. 1:3-12, 17-22, 2:4-10, Kol. 1:19-20, 1Pet. 1:20, Ufu. 13:8) Upatanisho huu ulifanyika ili kukamilisha mpango wa Mungu ambao ulikuwa ni siri na hekima iliyofichika kabla ya zamani za kale kwa ajili ya kutukuzwa kwetu. (1Kor. 2:7)

 

Dhabihu ya Upatanisho ya Kristo imechukulia kama ya wokovu ambao utafunuliwa tayari katika siku za mwisho.

 

1Petro 1:3-21 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; 4tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. 5Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. 6Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali, 7ili kwamba kujaribu kwa imani yenu ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. 8Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; kwa kufurahi isiyoonekana, yenye utukufu, 9katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. 10Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. 11Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwapo baada ya hayo 12Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu waliohudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka Mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia. 13Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. 14Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; 15bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16Kwa maana imeandikwa Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 17Na ikiwa manmwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. 18Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 19bali kwa damu thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani ya Kristo. 20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 21ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.

 

Hayakuwa matarajio ya Bwana kwamba dhabihu ziendelee.

 

Zaburi 40:6-8 Dhabihu na matokeo hakupendezwa nazo, masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka. 7Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (katika gombo la chuo nimeandikiwa), 8Kufanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu

 

Mawazo hapa ni kwamba dhabihu ni kwa ajili ya malipizi ya dhambi ila hayo matoleo ya dhambi hayakutakiwa kwa pale ambapo sheria inatunzwa au kuadhimishwa kwa hiari. Mzunguko wa kitabu umelindwa ili kwamba utunzaji wa sheria ni uwe ni wa kutoka moyoni na wote wale wanaofanya hivyo wameandikwa miongoni mwa wateule.

 

Dhabihu ya Upatanisho ilieleweka kutoka kitabu cha Isaya 53:4-12 na kwa kuondolewa kwa dhambi kutoka kitabu cha Zekaria 5:5 Upatanisho ulifungua chemchemi kwenye nyumba ya Daudi kama ilivyokuwa imetabiriwa katika kitabu cha Zakaria 13:1 kwa ajili ya dhambi na uchafu na ilitimizwa katika Kristo Mat. 26:28; Lk. 22:20, 24:46; Yoh. 1:29, 6:51). Yohana 11:49-51 inaonyesha kiwango cha uelewa wa kuhani wa siku kupitia unabii.

 

Yohana 11:49-51 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawambia, Ninyi hamjui neno lolote; 50wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. 51Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo.

 

Yuda alifahamu dhambi yake, iliyodhihirika nafsini mwake na mwanamke katika efa, ilikapotumwa kwenda Babeli na pale ikaabudiwa (Zekaria 5:5-11, pia tazama fafanuzi za maelezo ya chini ya ukurasa yaani footnote kwenye Biblia ya Kiingereza ijulikanayo kama Annotated Oxford RSV). Kwa hiyo machafuko ya Kanisa kwa ajili ya mfumo Kibabeli yalitabiriwa na nabii Zekaria.

 

Matendo ya Mitume 17:2 inaonyesha kwamba Maandiko Matakatifu yanatangaza umuhimu wa dhabihu. Hivyo adhabu kwa kutokuangalia kundi lililonunuliwa kwa damu ya Kristo ni kubwa kwa kweli (Matendo 20:28). Kristo alitolewa dhabihu na kupaishwa kwa ajili ya haki yetu (Warumi 3:24-26; 4:25; 5:1-21). Hivyo tumepatanishwa na Mungu (2Kor. 5:18-19). Tumekombolewa toka ulimwengu huu wa dhambi (Gal 1:3-4 ili kwamba tuweze kupata uwezo wa kufanyika kuwa wana (Gal 4:4-5). Kwa upatanisho huu, Kristo alipasua lile pazia la hekalu sehemu mbili kilichotutenganisha na Mungu.

Waefeso 2:13-18 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. 14Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi wote tuliokuwa wawili kuwa mmoja, akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. 15Naye akiisha kuuondoa ule uadui wa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. 16Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba. 17Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu. 18Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho Mmoja.

 

Sheria ya amri za Mungu na maagizo zilikomeshwa na mwili wa Kristo zilikuwa ni sheria za kidhabihu zilizohusiana na mwili.

 

Upatanisho una maana mwingine ambapo inahusiana na Mpango wa Wokovu katika siku za mwisho. Utaratibu wa sikukuu ya mwezi wa Tishri inaonyesha mlolongo wa matukio utakavyokuwa katika siku za mwisho. Baragumu huashiria ujio wa Yesu Kristo kama Masihi wa Israel katika siku za mwisho. Atautiisha ulimwengu. Kuna pengo kati ya Baragumu na Upatanisho na kati ya Upatanisho na Vibanda. Mapengo haya yana maana yake. Hakuna pengo kati ya Vibanda na Sikukuu Iliyo Kuu ya Mwisho. Hizo pia zina maana yake. Mapengo kati ya Baragumu na Upatanisho na kati ya Upatanisho na Vibanda huwakilisha ukweli kwamba mlolongo huu hufunika kipindi cha muda ambacho kinahitaji utaratibu wa vitendo. Jambo kubwa ni kwamba utaratibu wa kipindi cha Milenia unaowakilishwa kwa maadhimisho ya Vibanda hauwezi kutambulishwa hadi kuweko na matengenezo kupitia kutiishwa kwa sayari hii na Mungu. Kutiishwa kunatoa taswira na sikukuu ya Baragumu na upatanisho unatoa taswira na Upatanisho. Upatanisho na Mungu ni adhimisho la mfano wa jinsi Shetani atakavyofungwa kwa kipindi cha miaka elfu moja kama ilivyoelezwa katika Ufunuo 20:4.

 

Dhabihu ya upatanisho inatoa taswira kufungwa kwa shetani katika kibindi kabla ya Milenia kikitolewa taswira yake na sikukuu ya Vibanda. Dhabihu hii ina patikana katika kitabu cha mambo ya Walawi 16:1-34.

 

Mambo ya Walawi 16:1-34 BWANA akanena na Musa, baada ya kufa kwa hao wana wawili wa Haruni. walipokaribia mbele za BWANA, wakafa, 2BWANA akamwambia Musa, Sema na Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wowote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa, maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema. 3Haruni akaingia katika patakatifu na vitu hivi; ng'ombe mume mchanga kwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume kwa sadaka ya kutekelezwa. 4Ataivaa ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake, atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani, hayo ndiyo mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini, na kuyavaa. 5Kisha atatwaa mikononi mwa mkutano wa Waisraeli mbuzi waume wawili, kwa sadaka ya dhambi; na kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa. 6Na Haruni atamtoa yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake. 7Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweke mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania. 8Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili, kura moja kwa ajiri ya BWANA, na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. 9Na Haruni akaleta mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya BWANA, na kumtoa awe sadaka ya dhambi. 10Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za BWANA ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli. 11Na Haruni atamsongeza ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili yanafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake; naye atamchinja yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake 12Kisha atatwaa chetezo kilicho na makaa ya moto yatokayo katika madhabahu iliyo mbele za BWANA, na kozi mbili za uvumba mzuri uliopondwa sana mikononi mwake, naye atauleta ndani ya pazia. 13Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za BWANA, ili moshi wa ule uvumba ukistiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa. 14Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na kuinyunyizia kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba. 15Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya vile vile kama alivyo fanya kwa damu ya ng'ombe, na kuinyunyiza ndani ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema. 16Naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja na katikati ya machafu yao. 17Wala hapakuwa na mtu katika hema ya kukutania, wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapo toka nje, baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa alili ya nyumba yake, na kwa ajili ya mkutano wote wa Israel. 18Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za BWANA na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madbabahu kwa kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke. .

 

Dhabihu hii inawakilisha tendo la kuwafanya watu wamtukuze Mungu kupitia sadaka ya Yesu Kristo. Hatua hii huashiria upatanisho wa Israel. Hakuna mtu aliyeweza kuingia kwenye Hema ya kukutania mpaka Upatanisho wa Kuani Mkuu uwe umefanyika.

 

Hatua nyingine inafanyika baada ya upatanisho ukiwa umefanyika. Kwa hiyo mbuzi wa pili hawakilishi kwa njia yoyote dhabihu ya upatanisho ya Yesu Kristo. Matumizi ya mbuzi wawili yanatoa taswira ya hukumu ya kupenda kuwa na mafanikio kushidwa kwa viumbe. Upatanisho umeshafanyika tayari na umekamilika kama unavyoonekana kwenye aya nyingine (Law.16-20) inatoa taswira yake.

 

20Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania na madhabahu, atamleta, yule mbuzi aliye hai; 21Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. 22Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu, naye atamwacha mbuzi jagwani.

 

Malipizo ya dhambi za watu kwa kutumia mbuzi ni taswira ya hukumu ya Jeshi la malaika waasi walio chini ya himaya ya Shetani au Azazeli ambalo lilikuwa ndilo jina ambalo kwalo alijulina katika kipindi cha Waebrania. Nchi ya pekee inatafsriwa kama nchi ambayo imekitiliwa mballi (tazama Biblia ya Kiingereza ya Soncino). Hatua ya kukatiliwa mbali kuondolewa kutoka uwepo wa Mungu. Hii haikuweza kuhesabiwa na Kristo, zaidi kuliko tafsri kutoka kwenye fafanuzi juu ya msalaba kwamba Mungu alimuacha ambayo ni kutoka Zaburi 22 kama tujuavyo kuwa hatukufanya hivyo. Isaya 14-12 inaonyesha kwamba alikuwa ni Nyota ya Mchana au Lusfa na hivyo Azazeli alikatiliwa mbali na kutupwa hapa chini hadi kwenye ardhi na kupelekwa chini ya shimo. Mfumo wa. Shetani, ambao ni wa Kibabeli, ni ule ambao ume katiliwa mbali kutoka kwenye mafanikio yote. Rashibam anashikilia kuamini kwamba kuwa na maana ya nchi kukatiliwa mbali katika fungu la maandiko katika kitabu cha Walawi 16-22

 

23Na Haruni ataingia katika hema ya kukutania, naye atavua mavazi yake ya kitani, aliyo vaa alipo ingia katika patakatifu, atayaacha humo; 24naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na kuvaa nguo zake, na kutoka na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe, na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu. 25Na mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu. 26 Na mtu yule amwachae mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji na baadaye ataingia katika marango. 27Na yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya marango, nao watachoma moto ngozi zao, na nyama yao na mavi yao. 28Na yeye awachomaye moto atafua nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia marangoni.

 

Tumeona hapa kwamba mbuzi wa Azazeli amepelekwa jagwani au kwenye shimo mapema kabla ya Upatanisho. Mbuzi huyu aliye ondoshwa lazima aoshwe kwene maji na hatimaye anaweza kurudi kwenye kambi. Hii inatoa taswira halisi ya upatanisho wa ubatizo kwa njia ya maji baada ya kufungwa kwa Shetani. Mlolongo huu umefanywa ili wateule washiriki katika kufunga baada ya Majilio na kama muhimu kwa upatanisho.

 

29Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajitaabisha roho zenu, msifanye kazi ya namna yo yote, mzalia na mgeni akaaye kati yenu. 30 Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi, mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za BWANA. 31Ni sabato ya raha ya makini kwenu, nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele. 32Na kuhani atakayetiwa mafuta na kuwekwa wakfu badala ya baba yake, ataufanya huo upatanisho, naye atayavaa mavazi ya kitani, yaani, yale mavazi matakatifu. 33Naye atafanya upatanisho kwa ajili ya patakatifu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya hema ya kukutania, na kwa ajili madhabahu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya makuhani, na kwa ajili ya watu wote wa kusanyiko. 34Na amri hii itakuwa amri ya milele kwenu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kila mwaka. Naye atafanya vile vile kama BWANA alivomwamuru Musa.

 

Usemi wa kwamba nanyi mtazitesa nafsi zenu unapotumika kwenye Maandiko Matakatifu, yanaelezea kuhusu kufunga (kwa mujibu wa Abraham ibn Ezra, Nachmanides, Soncino). Hatua ya kufunga ni kufungua vifungo vya uovu ambazo Shetani au Azazeli alileta duniani. Azazeli, kama ilivyoelezwa, lilikuwa ni jina lililotumiwa kwa mmojawapo kati ya waliokuwapo kwenye Jeshi lililoasi akishirikiana na Shetani. Azazeli amefanyika kuwa ni taswira ya mmojawapo wa malaika waasi. Mhimili mkuu alikuwa Semyaza kwa mujibu wa Kitabu cha Kiethiopia cha uandishi wa Enock 6:7,8:1,13 ambacho kinaonyesha kuwa Azazeli ilikuwa ni neno lililotumika kumuelezea mkuu wa malaika wawaasi walioanguka, sawa na Shetani (tazama pia kamusi iitwayo Interpreters Dictionary of the Bible, Vol. 1, p 3-15). Uhusiano kati ya mapepo na huyu mbuzi kunaonyeshwa kwenye zimwi au jini lililokuwa linaabudiwa kama miongoni mwa miungu ya Warumi na Wayunani aliyekuwa na umbo la mbuzi ambaye pia ameelezewa katika Isaya 13:21; 34:14 na kitabu cha Mambo ya Walawi 17:7.

 

Tendo la kutoa dhabibu kwa mapepo, majini au zimwi limeelezewa pia kama ni ukengeufu kitabu cha Kumbukumbu la Torati 32:17 na 2Nyakati 11:13-15. Ukengeufu huu unaoleta matokeo ya kuondolewa kwa ukuhani katika Israeli kwenda Yuda (2Nya. 11:13-15).

 

Wazo ambalo Kristo alipewa na Shetani akiwa pale jangwani, na kwa hiyo tunaona hapa kuwa pia mbuzi akiharibiwa na yeye, inewezekana pia iongezwe. Kwa namna yoyote ile, upatanisho ulikuwa umeshafanyika tayari wakati huo mbuzi alipokuwa anapelekwa jangwani. Zaidi sana, wazo la kunajisika kwa mbuzi halitokani na Kristo. Hivyo basi, dhambi za ulimwengu ziliwekwa kwenye mabega yake hazikumkatilia mbali Kristo kutoka kwa Mungu kama yunavyoweza kujionea wenyewe katika Zaburi 22:24.

 

Zaburi 22:24  Maana hakuridharau teso la mteswa, Wala hakuchukizwa nalo; Wala hakumficha uso wake, Bali alipomlilia akamsikia.

 

Tendo la kujitesa kwa kufunga linaonekana katika Isaya 58. Israeli hawamrudia Masihi wakati wa malilio yake. Mataifa yatajipanga kupiigana na yeye na ulimwengu utatiishwa kwa mshangao mkubwa, kwa ajili ya uovu wake n uasi wake. Kipindi hiki lazima kifuatiliwe na maonyo ya siku za mwisho

 

Isaya 58:1-60:22

 Isaya 58: Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao. 2Walakini watanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasio acha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki; hufurahi kumkaribia Mungu. 3Husema Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. 4Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. 5Je! kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! ni siku ya mtu kujitaabisha mtu nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! utasema ni siku ya kufunga, na kukubaliwa na BWANA? 6Je! saumu niliyoichagua siyo ya namna hii? kufungua vifungo vya uovu, kuziregeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? 7Je! siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja na wewe? 8Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde. 9Ndipo utaita, na BWANA ataitika, utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; 10na kama ukimkunjullia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa, ndipo nuru yako itakapopanuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. 11Naye BWANA atakuongoza daima, atashibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui. 12Na watu wako watajenga mahali palipo na ukiwa, utainua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipoinuka; na mwenye kurejeza njia za kukalia.13Kama ukigeza mguu wako asiiharifu Sabato, usifanye anasa anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiitra Sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala hayatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; 14ndipo utakapo jifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipo inuka, nitakulisha urithi wa Yakobo  baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.

 

Mashauri ya Bwana hapa yalielekezwa baina ya uhusiano wa ndani kati ya watu wa Mungu na taifa ambalo ni la Israel. Kwa hivyo haiwezekani kuachanisha mwenendo wa mmoja ndani ya wateule na kwa taifa hilo. Kwa kiwango hicho hicho kinahitajika katika tendo binafsi. Tendo hili ni sababu ya kutengwa na Mungu.

 

Isaya 59 Tazama mkono BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa; wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusika; 2lakini maovu yenu yamewafarikisha na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusika. 3Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu, midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya. 4Hapana adaiye kwa haki, wala hapana hatetaye kwa kweli, hutumainia ubatili, unena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu. 5Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka. 6Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao, kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo  mikononi mwao. 7Miguu yao hukimbia mabaya, nao hufanya haraka humwaga damu isiyo na hatia, mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao. 8Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao, wamejifanyizia njia zilizopotoka, kila apitae katika njia hizo hajui amani. 9Kwa sababu hiyo hukumu ya haki i mbali nasi, wala haki haitufikilii, twatazamia nuru na kumbe! latoka giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu. 10Twapapasa-papasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho, twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao walioanda tumekuwa kama wafu. 11Sisi sote twaunguruma kama dubu; twaomboleza kama hua, twatazamia hukumu ya haki lakini hapana, na wokovu, lakini u mbali nasi. 12Maana makosa yetu yamezidi kuwa mengi mbele zako, na dhambi zetu zashuhudia juu yetu; maana makosa yetu tunayo pamoja nasi, na maovu yetu tumeyajua; 13katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena jeuri na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni. 14Na hukumu imegeuka ikaenda nyuma, na haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia. 15Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachae uovu alifanya kuwa mateka, naye BWANA akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki. 16Akiona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndiyo ulioleta wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia. 17Akajivika haki kama dereya kifuani, na chapeo cha wokovu kichwani pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa uwivu kama joho. 18Kadiri ya matendo yao, kwa kadiri iyo hiyo atawalipa, ukali kwao wampingao, malipo kwa adui zake, naye atarudishia visiwa malipo. 19Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumuzi ya BWANA. 20Na Mkombozi atakuja Sayuni, kwao waachao maasi yao katika Yakobo, asema BWANA. 21Tena katika habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema BWANA, roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu nimeyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA , tangu leo hata milele.

 

Ukumbozi ni ule wa Masihi katika siku za mwisho na ukombozi huo utakuwa katika nguvu chini ya maelekezo ya Mungu. Mchakato huu utakuwa ni wa ulimwengu mzima na utakamilika. Kisha mataifa yote yatawageukia Israeli ili kutafuta hekima yenye kuwapa mwangaza na maongozi. Matengenezo yatakayofuata ukombozi huu ni ya kuendelea.

           

Isaya 60 'Ondoka uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia. 2Maana tazama, giza litafunika dunia, Na giza kuu litaifunika kabila za watu, Bali BWANA atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako. 3Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako. 4Inua macho yako, utazame pande zote, Wote wanakusanyana wanakujia wewe, Wana wako watakuja kutoka mbali, Na mabinti zako watabebwa nyongani. 5Ndipo utakapo na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka, Kwa kuwa wingi wa habari utageuka kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia. 6Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana na Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; na kuzitangaza sifa za BWANA. 7Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu. 8Ni nani hawa warukao kama wingu, na kama njiwa waendao madirishani kwao? 9Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merekebu za Tarashishi kwanza, ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako, kwa ajiri yake mtakatifu wa Israeli, kwa kuwa amekutukuza wewe 10Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika gadhabu yangu nalikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu. 11Malango yako nayo yakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.

 

Matengenezo yatafikiwa kupitia mataifa ambayo yanakubali kufanya kazi ya kuanzilisha Israel kuwa ni Taifa Takatifu. Sababu ziko wazi. Mataifa walio kinyume na imani ya Semitiki kuelekea Sayuni kama mji wa Yuda na Israel yaliyo kinyume na Mungu.

 

12Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu Wasiotaka kutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa. 13Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, Mberoshi na mtidhari mteashuri pamoja; Ili kupamba mahali pangu patakatifu; Nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu.14Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli. 15Na kwakuwa umeachwa na kuchukiwa, Hata ikawa hapana mtu aliyepita ndani yako, Nitakufanya kuwa fahari ya milele, Furaha ya vizazi vingi. 16Utanyonya maziwa ya mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe utajua ya kuwa mimi BWANA ni Mwokozi wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa Yakobo. 17Badala ya shaba nitakuleta dhahabu, Na badala ya chuma nitakuleta fedha, Na badala ya mti, shaba, Na badala ya mawe, chuma; Tena nitawafanya wasimamizi wako wawe amani, Na hao wakutozao fedha kuwa haki. 18Jeuri haitasikiwa tena katika nchi yako, Ukiwa na uharibifu hazitakuwa mipakani mwako, Bali utaziita kuta zako, Wokovu, Na malango yako, Sifa. 19Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana, wala mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake; Bali BWANA atakuwa nuru ya milele kwako. 20Jua lako halitashuka tena, wala mwezi wako hautajitenga; kwa kuwa BWANA mwenyewe atakuwa nuru yako ya milele; Na siku za kuomboleza kwako zitakoma. 21Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; Chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe, kazi ya mikono yangu mimi mwenyewe, Ili mimi nitukuzwe. 22Mdogo atakuwa elfu, Na mnyonge atakuwa taifa hodari; Mimi, BWANA nimeyahimiza hayo wakati wake

 

Tunajishughulisha na mchakato endelevu wa kwenye aya hizi. Kwanza kwbisa, ni wazo la kuteseka na matumizi ya imani katika kuendeleza mkandamizo wa matesa na, la pili ni ombi kwa Bwana kwa kujihesabia haki sisi yetu sisi wenyewe kwa kuutumia mfungo wa saumu kama silaha. Matokeo yasiyozuilika ya hali hii ya kujihesabia haki mwenye ni mkandamizo wa mateso na Bwana hushughulika na hii katika Maandiko Matakatifu kwa ajili ya kufunga. Kuharibika kwa watu na Majilio na matengenezo vinaonekana kwenye sura tatu zilizotajwa hapo juu. Mfungo wa saumu ya kujipatanisha sisi wenyewe na Mungu na kuleta mfumo au utaratibu chini ya Masihi kwetu kwa haraka sana. Hebu na tuwe na bidii na kufunga saumu katika upendo na matumaini.

q