Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[140]
Mihuri Saba
(Jarida
2.0 19951109-20000825) Kanda
Jarida hili linashughulika na kufundisha kuhusu ile mihuri saba iliyoandikwa kwenye kitabu cha Ufunuo wa Yohana na linafafanua maana yake. Maendeleo ya mihuri hii katika kipindi cha zaidi ya miaka elfu mbili yametathminiwa na muandamano wa matukio ya hadi kurudi kwake kwake Masihi vyote vimeelezewa pia. Utaratibu huu unafikia upeo wake kwenye muhuri wa saba ambao kwa kweli ni baragumu ya saba.
Christian Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Copyright ©1994, 1995 1999, 2000 Wade Cox)
(Tr. 2005)
Masomo haya yanaruhusiwa
kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila
kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati
miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au
kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa
toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila
kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti
yetu ya:
http://www.logon.org
au http://www.ccg.org
Mihuri Saba [140]
Kitu cha muhimu kukumbuka ni kwamba, jarida hili linafaa lisomwe huku ukisikiliza mkanda wake wa kaseti ya radio.
Ramani-jedwali hii inayoonyesha jinsi muandamano wa matukio ulivyo, umeongezewa kwenye jarida la Baragumu Saba [141]. Kazi ya ratiba ya wakati huchukua kipindi cha Mihuri Saba na Baragumu Saba. Jedwali hili lilichapishwa mnamo mwaka wa 1985, kwa kweli likilenga kuonyesha kwamba isingewezekana kuwa Yesu Kristo angerudi kabla ya mwaka 1997 na kwamba mafundisho ya utaratibu wa miaka mitatu na nusu ya watu kwenda mahali pa usalama ulikuwa ni uwongo. Kuna idadi kadhaa ya fursa zinazoonyesha kuwa ujio wake ungefanyika mnamo mwaka 1997 au 1999 kwa kiwango cha mapema sana, au mara ngi zaidi baada ya hapo. Ramani hii ya jedwali hutuonyesha kuwa kuna Mihuri Saba, ambayo imegawanya kwenye Baragumu ya Saba Vikombe Saba vya ghadhabu ya Mungu. kukifuatiwa nakipindi cha wale mashahidi na kuna fursa tatu za kunyakuliwa kwa mashahidi hawa. Kukifuatiwa na kipindi kinachoitwa ni kipindi cha Taabu yake Yakobo. Watu wengi hudhani kuwa wanaweza kuachananacho, kuepukana au kukiweka kapuni. Hatutaweza kukifikia kipindi cha Milenia bila ya kupitia kwenye mlolongo huu. Huu ni unabii na hautaweza kutanguka. Hatutaweza kukwepa na wala hatutaweza kujificha ili kisitukute.
Kila kitu kitakachotokea kwenye ile ghadhabu iliyo kuu ya Mungu, na Baragumu ya Saba, zote zaweza kuepukwa. Hakuna kitu katika kitabu hiki cha Ufunuo katika maeneo haya inayohitaji kuchukua pahala pake. Tunaweza kukwepa hili, na sayari haiwezi kulikwepa hili kwa sababu ya muhuri wa kwanza ambao maana yake ni dini ya uwongo. Dini ya uwongo imemtangulia Kristo. Kristo sio muhuri wa kwanza, bali alifanyika kuwa chanzo cha mgongano ikianzia kwanza kabisa kuanzia pale Sinai, na pili ni kutoka ujio wake na kuhusuriwa kwake. Shetani alifanyika kuwa ni chanzo cha dini ya uwongo kuanzia siku ile aliyosababisha anguko la Adamu kwa kuijua kwake nafasi aliyokuwa nayo Hawa.
Hebu na tuangalie Wapanda Farasi Wanne aliyeko katika kitabu cha Ufunuo, wanaopatikana katika Ufunuo wa Yohana katika Sura ya 6.
Ufunuo 6 inasema: “kisha nikaona hapo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile mihuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda”
Hapa anaonekana Mwana Kondoo, Yesu Kristo akifungua mihuri. Muhuri wa kwanza ulivunjwa muda mrefu uliopita. Mihuri hii haitafunguliwa katika siku za mwisho. Muhuri wa kwanza unaendele kuendeleza njia yote hadi kufikia miaka ya 2000, na kila muhuri ni kielwlwzo. Zimefungua na kubakia zimefunguliwa na kuendelea. Kila moja ikionhezea kwa nyingine. Muhuri wa kwanza unaitwa Mshindi, hasa ni kwamba inaanzisha kutoka kwenye dini ya uwongo. Imeanza kwa mtazamo wa namna kama ya kanisa, na shirika, na taasisi iliyo katika fungamano la dini au madhehebu ya uwongo. Kwa sababu ya kupitia tofauti ya kimaoni ndipo tunapata mgawanyiko, jambo kuu zaidi linaloleta migawanyiko ni mfumo au utaratibu wa kimashirika yaliyoko kwenye hii sayari au dunia yetu unaotuama katika migawanyiko ya kati ya Kristo na Jeshi la Wateule watiifu, na Shetani na Jeshi lake la malaika waasi. Mgawanyiko huu umejitokeza wenyewe katika sayari hii kwa kupia namna au njia ya kidini. Utaratibu wote mzima wa dini zilizoko kwenye sayari hii kuashiria mfano uliokuwako kwenye vita vya kule mbinguni. Hakuna kinachojitokeza au kufanyika kwa bahati mbaya au kama ajali. Shetani amewekeza mawazo kati ya watu na mataifa.
Wazo dhana la kumweka Shetani mahali mbadala na Kristo ni uwekaji wa utaratibu au mfumo wa kidini ya dunia hii, maongozi au utawala wake na mfumo wake, kwa mfumo mwingine wa kimaongozi. Tazama jarida la Maongozi ya Mungu [174].
Mwana Kondoo ndiye awekaye utaratibu endelevu katika mguso kwa kuanzisha imani ya kweli kwenye hii sayari yetu; yaani neon la Mungu. Hiki sio kitu ambacho kwamba kinaanzishwa na halafu kinavunjwa tena. Shetani alikuwa na bado ni Nyota ya Asubuhi wa hii sayari. Kristo ndiye aliyejitoa kuwa dhabihu, aliyestahili ushindi na kuchuukua mahali pa Shetani kama Nyota ya Asubuhi, ya wakati wa kurudi kwake mara ya pili. Alilituma neno lake kweli hapa kwenye hii sayari kwa kupitia manabii na mababa wa imani na hatimaye kwa kila mmoja wetu.
Dini ya kweli kujiimarisha na watu walioko na kuwaimarisha katka uthabiti wa kupingana na Jeshi la malaika waasi yaani mashetani au mapepo. Hii itajieleza yenyewe kiuwazi sana kwa mataifa yote yatakayo ikabili Yerusalemu kwa ubaya wakati wa kurudi kwake Kristo katika siku za mwisho. Utaratibu huu endelevu wa dini ya uwongo kiundani kabisa unafuatia katika muhuri unaofuata au wa pili wa vita.
Ufunuo 6:3-4 inasema: 3Na alipofungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo! 4 Akatoka farasi mwngine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
Muhuri wa kwanza ulianzishwa na Shetani ukikusudia kulishambulia kanisa kwa kuanzisha mafundisho ya imani ya Kinostiki ambayo yana sititiza kuhusu kumwamini Mungu kwa kutumia ujuzi na kwamba ujuzi ni mlango muhimu kwa wokovu, imani ambayo msingi wake ulikuwa huko Alexandria. Aliweka imani hii ya Kinostiki kwenye Fumbo za siri za Dini potofu, na mfumo wa Kitafiti au udadisi wa Kirumi ambao ilikuwa ni mfumo wa kipagani. Walikuwepo Makardinari huko Roma miaka mingi hata kabla ya kuzaliwa kwa Kristo na walikuwa wanavaa mavazi mekundu, na walikuwa wanavaa kofia aina ya vibandiko kama balaghashia. Walikuwepo wanawali mabikira huko Roma siku nyingi sana kabla ya Kristo hajazaliwa, na wanawali hawa walikuwa ni sehemu ya mfumo au utaratibu wa Hekalu lililokuweko huko Versa la dini au imani ya kipagani. Walikuwa na utaratibu wa muhimu wa Makaldinari hawa ambao walikuwa ni wasaidizi wenza wa Kiongozi mkuu au Papa. Maofisa hawa wa kidini ndio waliongoza serikali. Sio utaratibu au mfumo wa Kikristo. Utaratibu ule ulifanyika kuwa ni sehemu ya utoaji adhabu wa mfumo mbovu na wa uongo wa Shetani.
Mfumo wa kimseto wa Kiyunani na Kirumi ambao chimbuko na msingi wake ulituama kwenye imani ya Kiplatoni na mafundisho yake ya kuhusu maongozi ulichukua kwa kuiga ule aliouweka Kristo, walifanya hivyo kwa makusudi ili kuwayumbisha. Hivyo ndivyo hatimaye dini ya uwongo ikaanza rasmi. Ili kuwezekane kuanzisha mfumo huu shirikishi wa mseto wa Kiyunani na Kirumi, walianzisha mafundisho ya kuweka mabaraza. Mababa au mapadri wa kanisa katoliki wa Kapadokia walianzisha mafundisho kuhusu Mungu yaliyotegemea msingi wake kutokana na Mtaguso wa Baraza la Nikea, ambalo kwanza kabisa lilikuwa ni chanzo cha imani kuhusu miungu miwili yaani Wabinitaria, na ambayo sio fundisho la Kamisa kabisa. Imani hii ya Kibinitaria ni matunda ya mafundisho ya Kanisa Katoliki yaliyotokana na mtaguso wa Nikea, mnamo mwaka 325BK. Ilikuwa ni hatua muhimu kwa kutambulisha imani ya wanachokiita wenyewe kuwa ni Utatu Mtakatifu katika mtaguso wa Kostantinopo mwaka 381BK.
Muhuri wa kwanza ulisababishwa na migawanyiko tuliyoiona ikitokea kwenye Mabaraza kwenye karne za nne na tano. Mtaguso wa Elivira ndio ulianzisha wazo la kuifutilia mbali siku ya Sabato na kukomesha maadhimisho yake, mnamo mwaka 300BK. mtaguso wa Nikea wa mwaka 325BK ulibadilisha utaratibu wa kibiblia wa Uungu na kuanzisha utaratibu na fundisho jipya la kwamba Yesu Kristo yuna cheo sawa cha uungu na umilele na Mungu Baba. Kwa hapo, hawakuingia ndani sana kushughulika na nafasi ya Roho Mtakatifu. Walifanikiwa kwa muda wa miaka miwili. Lakini Mfalme Costantino akagundua kwamba kulikuwepo na wafuasi wa Athanasi wakijulikana kama Waathanasia, ambao sasa walikuwa wanajiita Wakatoliki, ambao pekeyao walikuwa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa pale mjini Roma na kwa maeneo mengine. Aliyekuwa nguzo hasa ya nguvu na ushawishi katika Dola hii ya Rumi kwa siku zile na ambaye alikuwa ni muumini lakini visivyo sahihi sana wa imani inayoamini Uungu wa Mungu mmoja tu wa pekee na wa kweli yaani Waunitaria aliyeitwa Arians, ambaye alikuwa msaidizi mshiriki. Askofu mwingine wa Waunitaria walifukuzwa na kwenza ukimbizini pamoja na Arius (neno au jina la Waariani walipewa kwa kudihakiwa, tazama jarida la Kuimarishwa Na Baba [081] walikuwa ni Waunitari tegemezi. Kulikuwa na idadi kubwa ya mataifa ambao hatimaye walikuwa wasaidizi tegemezi. Maaskofu hawa waliitwa tena wakaapishwa na kupewa mamlaka ya kikanisa au ya kimaongozi ya kidini. Tazama jarida la Imani ya Kiariani na Uariani Nusu [167] na la Vita vya Waunitaria na Watrinitaria [268].
Tofauti kati ya utaratibu wao wa Kimaongozi ilikuwa ni kwamba mmoja ulilemea kwenye utaifa zaidi na ule mwingine ulilemea zaidi kwenye ufalme. Athanasi alipendlea sana maongozi ya kidunia na bado wanaendelea kufanya kwa namna ya mtindo ule kuelekea hadi mwisho.
Kwa hiyo mfalme Kostantino akaamini kwa siku zile kwamba yule aliyekuwa anahitaji mamlaka ya kidunia ndiye alikuwa mwenye nguvu kuliko, lakini haikuwa hivyo. Utaratibu endelevu alioanzisha vita vya Athanasi kumbukumbu zake hazikuratibiwa au kutunzwa kwa uzuri sana, au kutangazwa, kwa sababu Wakatoliki hualiandika vitabu vya Historia. Historia ya vita vya Wariani imewekwa kwenye orodha ya kazi wanazoziita kama Matoleo ya Siri. Kazi hii inahusiana na utaratibu endelevu wa jinsi mfumo wa Kibabeli ulivyoanza wenyewe tu na jinsi ulivyoenea na kukubalika katika sayari hii. Mfumo huu wa kibabeli umeipindua hii sayari yetu, kama Kristo alivyosema katika maneno yake kuwa ingekuwa.
Ndharia ya Vita vya Haki (tazama jarida la Nadharia ya Vita vya Wenye Haki [110] ni matokeo ya melendelezo ya mawazo ya Waathanasi. Vita hivi vinafanyika kuwa ni kitu cha kila mara kikituzunguka kwenye jamii yetu. Kwa mara ya kwanza tunaona kuwa tunapata hili wazo la vita vya kidini. Kuanzishwa kwa Uislamu chini ya Mtume Muhammedi yalikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya Watrinitaria. Muhammadi alianza kuhubiri maneno ambayo yakusudia kuondolea mbali mafundisho ya Waathanasia wenye kuamini uungu wa miungu mitatu yaani Watrinitaria ambayo aliyaona kama mafundisho mapotofu na ya uwongo, na kuwaunganisha Waarabu chini ya dini moja ya umma wa Muhammadi wenye kuamini na kumwabudu Mungu mmoja tu peke yake yaani Wamonothei. Kitabu cha kurani kinauweka Ukristo katika makundi mawili ya majina. Kundi la kwanza wanaitwa Watu wa Kitabu na kundi lingine wanaitwa wakristo tu kwa ujumla. Tofauti hizi kwa sasa zimepotea kwa kuwa Wakristo walioko leo katika mtindo wa umamboleo hawawezi kuelewa tofauti hiyo kwa mara moja tu. Tofauti hiyo inahusu Watrinitaria waliopigana na Uislam na ile ya Kanisa linalopitia mateso la Wapergamo ambalo linaloungana na Uislamu katika kuamini juu ya Mungu mmoja wa pekee na wa kweli.
Mifumo na taratibu hizi za dini za uwongo walitiwa nguvu wote kwa kujaribu kudharau na kufanya hila ili kuzuia ushawishi wa kujitanua wa Kanisa halisi linaloshika Sabato. Tumekuwa na waumini waongofu kwa idadi ya mamilioni. Baraza la kuhoji na kuhukumu au kutesa watu lilianzishwa na Kanisa la Rumi likikusudia kuweka pingamizi kulizuia Kanisa la Kweli halisi lisiokolewe, na kusudi jingine lilikuwa ni kuimarisha nguvu za imani ya Watribitaria. Sababu itakayowafanya wasiweze ni kwamba Mungu hataweza kuwaacha wafanye kilicho nje ya Biblia. Kwa kadiri vile iendeleavyo kuishi Biblia, basi kila atakayeisoma ataweza kufunguliwa macho yake kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Mihuri hii kuwa ni kielelezo. Waislamu/Wakristo waliendelezwa vema kupitia Ottomani na mfumo wa kituruki. Wakati wete kulikuwa na matengano kati ya Uislamu na Ukristo, na kati ya Uislamu na mfumo wa kimashariki. Kulikuwa na mfumo wa kupooza nguvu uliowekwa kule Urusi chini ya Khazar, Dola ya Kiyahudi, ambako makabila ya Ashkenazi na makundi mengine waliongoka na kuingia kwenye dini ya Kiyahudi yapata kama mwaka 740BK. Ulikuwa ni uamuzi wa kisiasa. Ikiwa kama watakubali kuwa Waislamu, basi ile hali ya kutengwa itaondolewa na kuingizwa mfumo wa kimagharibi, na wangeweza kufikia mwisho wa vita vilivyokuwako kati ya Wakristo na Waislamu.
Lakini kama watakubali kuwa Wakristo, wangeendelea kuwekewa pingamizi na mpaka kwa upande wa kingo za mashariki. Kwa hiyo bado wangeendelea kuwa kwenye vita bila kujalisha walifamnya nini. Hii inahisiwa kuwa huenda ilikuwa ni sababu ya wao kuwa Wayahudi kwa sababu ndio ilikuwa njia muafaka ya uamuzi wa katikati. Mwishoni walihusuriwa kuwa kama Dola na wakaenda Ulaya. Lakini walichanganywa kwenye makabila ya Yuda kwa ushawishi wa marabi. Walipewa urabi na kuongezwa kwenye jamaa ya wana Abrahimu. Lakini migawanyiko hii na vita hivi viliendelea kwa nyakati zote hadi kufikia siku hizi za zama tunazoishi leo, zikipelekea Mauaji ya Kuangamiza Halaiki ya watu. Mauaji haya hayatokani na mtazamo wa kuwa ni ziku za mwisho tu. Mambo haya yalianza tangia karne nyingi zilizopita na yanaendelea, na yanahusiana na mateso. Matokeo ya vita yalikuwa ni magonjwa ya kuambukiza kama ya tauni (pakanga) yatokanayo kwa ajili ya ukosefu wa mfumo bora wa kupangilia taratibu mipango miji kwenye jamii zetu, kisha mhuri wa tatu ukafunguliwa.
Mihuri hii inaendelea na inaendelea, vita hadi magonjwa ya kuambukiza ya , hadi njaa na kisha kifo. Muhuri wa nne ni kitu kinachoendelea, na vinashirikishana au kushabihiana.
Muhuri wa tano wa Dhiki Kuu una mambo mawili ndani yake. Ilifunguliwa wakati vita hivi vya kidini vikianza. Hata hivyo, wakati mfumo wa Waathanasi unakamilika kikamilifu, ilianza kama kikundi, au mlolongo wa mateso tunayoyajua kutokana na unabii wa biblia kama miaka 1,260 iliyopitia kuanzia mwaka 590KK hadi kufikia mwaka 1850 na mihuri na inakoma na Dola Takatifu au ya kidini ya Rumi, ambayo kwa sasa inafunuliwa. Hata hivyo, ina maana kwa siku za baadae.
Tazama jarida la Hukumu ya Kabla ya Kurudi Kwake [176].
Ufunuo 6:5-6 inasema: Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mzani mkononi mwake. 6 Nikasikia, kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.
Matokeo ya mwisho ya maradhi ni njaa na kupungukiwa, na kufikia kiasi cha kupewa chakula kwa mgao, kwa kipimo maalumu. Wazo la kuyadhuru mafuta na divai lina maana ya kiroho. Mafuta ni Roho Mtakatifu, sadaka ya kinywaji ya Bwana ni wateule wake. Tunamiminwa kama sadaka ya kinywaji kwa Bwana. Hapa pana maana ya kulindwa kwa wateule wakati wa kipindi hiki chote cha kugogwa Mihuri. Kwa hiyo ni dhahiri kuwa tutapitia kwenye vipindi vya dhiki na kuuawa tukiifia imani, lakini kama sadaka ya kinywaji kwa Bwana kwa ajili ya sababu maalumu za imani ya kidini.
Ufunuo 6:7-8 inasema: Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! 8 Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, wauwe kwa upanga, na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.
Maendelezo haya kama robo ya nchi hatimaye yatakubali uangamivu huu. Sio kwa kusema tu wanajipanga kwa vita. Bali inaendelea hadi kufikia siku za mwisho. Wonekano huu wa baragumu na Vikombe ni kuonyesha kuwa mambo haya yatakuja kutokea. Tunajua ya kwamba muandamano huu wa mlolongo wa matukio kuwa yapo. Sayari hii ya dunia inaendeshwa na mawazo waliyobadilishwa, ya Shetani. Tunashughulika na mapepo wanaojaribu kusimamisha au kurudisha nyuma kazi na mipango ya Mungu isiendelee mbele au kufanikiwa.
Tunatakiwa kuchukua taadhari kwa hayo na kujua kile kinachotokea. Mahali petu palipo salama ni imani katika Bwana, na kwa kujua yale anayoyafanya. Na kujua kuwa Mungu ndiye mpangaji na anasimamia; yanatokea kwa sababu nzuri, na kwamba inakwenda kutokea. Maandiko Matakatifu yanafungukiwa wazi mbele ya macho yetu.
Dhiki kuu wakati wa muhuri wa tano imejulikana kama Sikukuu ya Vibanda ya mwaka 1993. kwenye Sikukuu ile kulitangazwa kikamilifu tena na tena kuwa, kupitia kwa Papa mpya Mwenye Mamlaka juu ya wengi. Wateule wanakabiliana na mateso makuu. Mwaandishi, Morris West aliweka pahala palipo wazi kabisa mambo yote yahusuyo waraka wake wenye nguvu za kisheria kwa watu wengi. Alisema kuwa itaanzisha tena uwanja kwa ajili ya kuwahojia watu.
Ufunuo 6:9-10 inasema: “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?”
Hili ni la kwanza kati ya mawili. Kila mmoja wao alipewa kanzu nyeupe na kuambiwa wasubiri kwa kitambo hadi pale idadi ya hao ndugu zao watumishi wenzao ipate kutimilika, ambao walipaswa kuuawa kama na wao wenyewe walivyouawa. Jambo hapa ni kwamba watu hao walikuwa kwenye makundi mawili. Baadhi yao ni wale wapendwa waliouawa kwa kuchinjwa kwa ajili ya ushuhuda wa neno la Mungu na kundi la pili ni la wale mashahidi ambao walikuwa na ushuhudandio wakawa wanalia (rudia kusoma tena hapo juu). Kwa hiyo wanangojea. Walikuwa kwenye ulinzi wa Mungu, lakini waliruhusiwa wafe.
Suala hapa sio kuwa hako hai na
wanazungumza au kuongea na Mungu, bali damu yao ndiyo inayolia, wakiwa wenyewe
wamelala pale, chini ya madhabahu, wakingojea ufufuo wa kwanza. Ni agano na
Kristo kama swali la msingi kuuliza: “Kwa kweli wewe ndiwe ujueye na kuweza
yote, kwa nini imetupasa sisi kufa?”
Kwa nini wao walikufa? Hili ni jambo lililo wazi. Ni kwa ajili ya neno la Mungu na ushuhuda waliokuwa nao. Sisi tuko kwenye ulinzi wa Mungu, hata hivyo, baadhi ya wateule watapaswa kupitia kwenye kuuawa kwa ajili ya ushuda wa imani yao ili watumike kama mashahidi kwa ulimwengu. Tayari wateule wewngi sana wameisha uawa na wengine wengi wameisha uawa pamoja nao. Mara tu dini ya uwongo unapoanzishwa, ikiliacha neno la Mungu kando, na vitu vikawa vina tafsiriwa tena na tena kwa upya, machungu ya mioyoni na chuki hufuatia.
Hatimaye makatazo na mateso hufuatia. Baraza la mwisho la kuhoji lilifanyika kwenye Kasio ya Papa kati ya miaka ya 1823 na 1846. Mwana historia wa zamani kutoka kwenye kitengo cha kidini kinachoitwa cha Majesuiti aitwaye Malaki Martin, ameandika kwa urefu sana kuhusu jambo hili, kwenye jarida lake linaloitwa Kufifia na Kuanguka kwa Kanisa la Rumi (Decline and Fall of the Roman Church) vifungu vya 254-255). Mwandamano wa mambo ni kwamba, kuanzia mwaka 1823, walifikia mahali ambapo walikuwa wakieneza chuki katika kila mji, na watu 200,000, kwenye Kasio za Kipapa, wakihumiwa kupelekwa kwenye tundu la wanyama ili wauawe huko, au kufungwa gerezani maisha yao yote. Aina hii yote ya watu walichukuliwa kwenye jambo hili; wakaidi wa kisiasa, nk. Zaidi sana ilipewa msukumo ikikisudiwa kuwamaliza au kuwafutilia mbali watu walionzisha pale chini ya Zama za Wathiatira waliokuwa kinyume na mfumo wa Kikatoliki. Mwisho wake, ilipelekea uharibifu wa mfumo wenyewe wa Kikatoliki chini ya miaka ile 1,200 iliyoishia mwaka 1850. Ilianguka chini kwa sababu watu wasingeweza kuchukuliana nalo. Waliitisha kura ya maoni kujadili jambo hili katika mwaka 1850 kwa wale waliohitaji kwenye Kasri ya utawala wa Papa au kuwa chini ya Serikali ya Jamhuri ya Rumi. Watu 1,505 walipenda kubakia kwenye utawala wa mfumo wa Papa. Na mwingineyo yeyote (132,681) walipiga kura kinyume chao, kwa sababu hawakuhitaji kitu chochote kufanya kutoka kwenye mfumo wa kisiasa wa Kanisa Katiliki la Rumi wa kimaongozi ya Kanisa.
Hii inatimiliza unabii wa yule Mnyama akilirudisha kwenye uasherati. Itageukia kufanya uasherati tena katika siku za mwisho na kuliharibu kabisa. Lakini ile miaka 1,260 iliishia kwa yule Mnyama kurudia kwenye uasherati, na kuharibu nguvu zake. Ilitimilizwa kwa sehemu na Napoleoni alipokuchukua mamlaka mnamo mwaka 1815 Alivunyilia mbali Utawala wa Kipapa na Ksri zake zote za kile kilichoitwa Dola Takatifu ya Kirumi. Alipigwa na kushindwa katika Mapigano ya mahali paliyoitwa Waterloo, ambaye hatimaye alipelekwa uhamishoni na kisha akauawa. Wakati alipouawa ikaanzishwa tena. Mnamo mwaka wa 1823, miaka minane baadae, wakati Kanisa Katoliki la Roma likiwa limerudi tena kwenye upeo wake wa kushikilia hatamu za nguvu, kwenye maeneo ambayo kimwili na utendaji waliyatawala, walianzisha yena yale mabaraza ya kuhukumu watu kwa makosa ya kidini.
Kunachangamoto ihusuyo ubora wa kidunia. Kuna aina tatu za mbinu kutumika katika kuanzisha mfumo huu wa dini hii ya uongo. Wa kwanza ni mfumo wa unaozingatia Ulaya kuifanya ndio mhimili wake ambao kwayo, Rumi inajaribu kupata uwezo wa kiutawala na kuingoza hii dunia. Mbinu ya pili ni mfumo wa kidunia ambao kwayo Utawala wa Marekani unadhani kuwa unaweza kufanikiwa kuitawala hii dunia. Kutokana na mfumo huo, huu mfumo wa kimataifa wa kiuchumi utatafuta kufanya kazi. Mfumo wa tatu ni wa kupitia nchi za Asia ambao ndio kwanza unaendelea sasa. Kwa lugha ya kibiblia tutauita ‘muungano wa wafalme wa pande za Mashariki’. Maneno yaliyoko kwenye kitabu cha Ufunuo hutwa anatoli helios, ambalo maana yake ni Wafalme wa Jua lichomozalo, sio wafalme wa Mashariki. Lakini itakuja kutuama katika Upande wa Mashariki mkabala wa Uchina na Ujapani.
Hiyo itakuwa ndani ya miaka minane, kuwatia watu millioni 1.5 chini ya utiisho wa kisiasa. Utaratibu wa kiakili wa muhuri huu wa tano ni unaangamiza vyote. Katika siku za mwisho, kama inavyosemekana:
Ufunuo wa Yohana 6:11 inasema: “Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao”.
Vazi hili jeupe la mshono wa kanzu ni wafia
dini Ufunuo
wa Yohana 3:14-22 inasema:
“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenaye yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumbwa kwa Mungu, 15 Nayajua matendo yako, ya kwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. (22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa)”
Huu mfumo wa Walaodikia kwa kweli ni sehemu ya mfumo wa siku za mwisho. Wakati tunaposoma ahadi yaliyo ahidiwa Makanisa yaliyoko kwenye kitabu cha Ufunuo, tutaona kuwa kuna makanisa manne yaliyojiandaa na kuwa tayari kwa ujio wa Masihi. Matatu yameisha enda na yamebakia manne yakiendelea kuwepo, nayo ni: Thiatira, Sardi, Filadelfia na la Laodikia kwa utaratibu ambao umewekwa. Mavazi haya meupe ni yale yale mavazi meupe ambayo hawa watu wamepewa, waliochinjwa kwa ajili ya ushuhuda wa neno la Mungu na kwa ushuhuda waliokuwa nao. Kanisa la Walaodikia halithamini chochote na linajidhania kuwa liko tajiri. Litapita kwenye moto wa utakaso ili kwamba baadhi ya washirika wake waweze kuokolewa.
Kuna ahadi lililopewa kanisa la Wafiladelfia inayosema:
Ufunuo wa Yohana 3:11 inasema:Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Yeye shindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu. Biblia ya tafsiri ya RSV inasema: Wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaanndika juu yake jina la Mungu wangu”. Lakini KJV inasema Wala hatatoka humo kwenda nje kabisa.
Biblia tafsiri ya Interlinear inasema na wala hatatoka nje tena. Wafiladelfia wamewekwa kwenye mahali ambapo wanatolewa nje ya makutaniko yanayojifanya kuwa ni Hekalu la Mungu, kwa kuwa wanakishikilia sana kile walichonacho. Hawana ule udhaifu ambao Walaodikia walikuwa wanaendana nao. Wanalishikilia sana neno la Mungu, kuliendeleza na kukua katika nguvu za imani. Wamefanyika kuwa ni nguzo kwenye Hekalu la Mungu.
Wanafanyika kuwa ni nguzo za kati kati zinazoshikilia Hekalu katika mahala pake. Nondo za chuma za kujengea zikifungwa na kuwekwa sawa sawa kwenye nguzo, huunda au hufanya msingi mzuri wa mfumo wa kutegemeza uimara wa Hekalu. sababu ya wao kuwa nguzo ni kwa kuwa wamekuwa imara zaidi; wao ni wasaidizi tegemezi. Kuelewa ni kiini. Mtu hawi Mfiladelfia kwa kuwa ni jina tu la kanisa fulani, lakini ni kwa sababu ya yale anayoyatenda na kusema. Ni kwa ile kweli ya neno ndiyo inayotulinda sisi.
Ufunuo wa Yohana 3:10, inasema hivi:
“Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyotayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi”.
Hii imechukuliwa ili kumaanisha kuwa kuna mahali pa usalama. Mafafanuzi haya yote ya kuweko mahali pa usalama hayamaanishi kuwa watu wanakwenda kuwekwa mahali popote pamoja ambapo hakuna mtu atakayepajua mahali gani walipo. Ni kwa ajili ya ukweli kuwa sisi tuna mkono wa Mungu uliowekwa juu yetu. Kanisa la Walaodikia katika siku hizi za mwisho linakabiliana na mlolongo wa matatizo kwa kuwa halipo tayari kusimama kwenye kweli. Hatimaye litatapikwa litoke nje ya ufufuo wa pili.
Saa ya kujaribiwa itakuja mara baada ya kurudi kwake Masihi. Hii ina maana ya kuwa tutakuwa pamoja na Masihi arudipo.
Kuna kundi moja waliotolewa nje ya Sinagogi na wanashughulikiwa. Wanapiga kura kwa miguu yao ni kundi dogo. Watatolewa watoke saa ya kujaribiwa. Hakuna hakika ya kudumu kuwa kama kuna mmoja kati ya watu hawa hawata lazimika kugharamika kuyatoa maisha yao kwa ajili ya imani yao kwa Mungu. Hakuna mtu mwenye kutuhakikishia kuwa hatutapitia kwenye mateso. Hakuna mwanadamu mwenye mwili, lakini Mungu na Yesu Kristo ndio wanaojua pale tulipo, kuna nini ndani yetu na kile tunachoweza kukivumilia au kukibeba. Tunajaribiwa kwa moto.
Tunachotakiwa kukifanya ni kujiandaa nafsi na mioyo yetu ili kushughulika na uwezekano wowote. Kuna idadi kubwa ya ahadi kwenye makanisa mbali mbali. Kwa mfano, tunapotazama katika kitabu cha Ufunuo 2:24 tunaona pale ahadi kwa Watiathira. Wana matendo makubwa katika mwanzo na mwishoni, na matendo ya mwisho ni makubwa kuliko yale ya kwanza. Walivumilia kwa kipindi cha miaka 1,260 ya mateso. Idadi kubwa ya wafia dini waliuawa wakati wa kipindi hiki. Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wowote wasio na mafundisho hayo, (ya kutoa sadaka ya vyakula kwa sanamu) wasiozijua fumbo za Shetani…Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapo kuja. Kipindi hiki cha zama za Wathiatira kitakuwepo tena katika siku za mwisho, na kwa ndugu zetu wapendwa wa kule Ulaya. Kristo haweki mzigo mwingine wowote tena juu yao. Wameisha pitia tayari kupitia mateso ya wafuasi wa Stalini. Wamepitia kipindi cha miaka 1,260. Wamepitia vipindi vya mateso kwa kipindi kirefu. Dhiki kuu imewekwa kwao kwa kipindi cha mamia ya miaka.
Kama hatuko tayari kujitoa dhabihu kwa ajili ya Yesu Kristo basi hatuna shirika naye. Kuna mtume mmoja tu ambaye hakufa kwa kwa kupitia mateso ya kidini, anaitwa Yohana. Alikuwa ni yeye peke yake na ndiye aliye andika kitabu hiki cha Ufunuo. Ilifanyika hivyo ili tuweze kujua nini kitatokea kwetu katika siku za mwisho. Hakuna kitu laini na rahisi tunachokisikia hapa ndani yake.
Tunapaswa kuelewa kinachotokea katika mlolongo huu. Israeli watapitia kwenye kipindi cha Taabu yake Yakobo. Sisi tutakimbilia, mji mmoja hadi mwingine, na watu wetu hawataimaliza miji yote ya Israeli mpaka Mwana wa Adamu ajapo (Mt. 10:23). Huu ni mstari au aya ya kuikumbuka. Wazo la kukimbilia miji mmoja baada ya mwingine ya Israeli hutuambia sisi kuwa kuna taifa lililoko mbioni. Kuna wakimbizi, nk. Kukata tamaa ni silaha ya Shetani. Anaitumia hali hii kwetu, hasahasa wakati tunapokuwa tumepewa unafuu kama mahali pa usalama. Ikiwa hatimaye tukivumilia mateso, na kuvumilia mambo haya yote yalitoandikwa kwa ajili yetu, tunaweza kukata tamaa.
Hakuna ufumbuzi ulio wa lelemama. Tuna kazi itupasayo kufanya chini ya mfumo huu. Kutoka hapo kinachofuatia ni dhiki kuu, tunapofikia kwenye hatima yale. Lengo kuu na halisi la Shetani kuwaondolea mbali wateule.
Sababu inalolifanya Kanisa kugawanyika
vipande vipande ni kwa kuwa Mungu amewaweka watu kwenye maeneo mbalimabli, ili
kulisimamisha Kanisa lisirudi nyuma katika nyakati hizi za mwisho. Shetani
anapenda kuwasimamisha au kuwazuia wateule, kwa kuwa wateule ni kiini, uti wa mgongo
wakati wa utawala wa Milenia. Kitu tunachotakiwa kwa kweli kukijua ni kwamba
Kristo atatulinda, kwa ajili ya haki mkate wao na maji vitakuwepo hakika.
Wateule ndio sababu peke yake kwa Kristo kuingilia.kati mambo yaliyoko kwenye hii sayari yetu. Wateule watapelekea zaidi ya idadi ya hawa 144,000, zaidi ya makutano makuu kwa mataifa na kwa Israeli, vikundi vya kimwili ambavyo vilikusudiwa na Mungu ili kuunda sehemu ya mfumo wake. Kumbuka ule unabii wa mti wa mzabibu. Lakini ni kwa ajili ya wateule tu vinginevyo ulimwengu huu wote ungeweza kuangamizwa. Kristo anaingilia kati ili kwamba asiwepo hata mmojawapo wa watu wale walio kwenye mpango wa Mungu, asianguke chini na kushindwa kuelekea hadi mwishoni mwa njia ya Milenia, wabaguliwe. Mungu ameshaamua tayari kuwa nani anayekwenda kuitwa na kwa kiwango gani. Sio mapenzi ya Mungu kuwa yeyeto mwenye mwili apotee na hii hutuambia sisi ya kwamba hakuna mwenye mwili atakaye potea. Kristo ataingilia kati kwa ajili ya wateule. Hatamuacha mteule yeyote apatwe na mateso ya maumivu yoyote hadi pale atakapo watumikia watu wa Mungu. Iwapo kama tutateseka kwa maumivu yoyote, tunajua kuwa ni kwa sababu Kristo hawezi kututumia sisi na nguvu zetu ili tuwe mashahidi wa mfumo au utaratibu wa Mungu. Kila mtu amekosea. Wote hufanya kitu fulani kama shahidi wa njia fulani na kufanya kupitia mfumo ule. Ulimwengu wote umedanganyika. Kuna idadi kubwa sana ya makanisa kwa wakati mmoja, mengi kati ya hayo yanafundisha watu kuhusu fundisho la kunyakuliwa na kwenda mbinguni, na kwamba watanyakuliwa na kwenda mbinguni na kuishi huko wakati Kristo atakapokuja, na kuwa kila mahali hapa duniani pataharibiwa isipokuwa waamini tu, kwa kuwa wao ni sehemu ya “mfumo wa wateule”.
Sisi sote ni watu wa Mungu. Wateule ni kiini tu miongoni mwa watu wa Mungu ambaye ni zaidi ya wateule. Kila kinachotokea kwa watu wetu ni sehemu ya muandamano wa matukio kuelekea kwenye mwisho wa Muhuri wa saba. Muhuri wa saba huishia mwishoni mwa mwa vikombe saba vya ghadhabu ya Mungu. Ni mwandamano wa matukio mkamilifu.
Wateule hawasimami mbali kutoka kwenye taifa. Wateule bila kuwa na taifa ni dhana ya bure.
Mfano wa Musa pale Sinai ni sawasawa. Alijiweka mbele ya Malaika wa Bwana, kujitoa ili auawe ili kwamba watu wake wapate kuokolewa.
Huu ndio mfano wetu. Tunatakiwa kumuomba Mungu, kufunga saumu na kufanya kazi kwa pamoja katika msingi endelevu ili kuwaokoa watu hawa. Mungu ametuita tutoke ili kwamba tuweze kujiandaa sisi wenyewe. Inatubidi tusafishe mawazo yetu yatokanayo na mfumo wa kidunia. Kwa lugha rahisi ni kusema kuwa hebu na tuyararue mawazo yetu na vitu vinavyoyatia unajisi. Sisi tu watatakatifu wa Mungu na na inatulazimu tusikaribishwe na mfumo wa kidunia makaribisho yenye kuvutia akili. Inaweza kuzigeuza nia zetu, kurudisha nuyma au kuathiri uwezo wetu wa kujitoa sadaka kwa Bwana. Hatuwezi kujieleza nia zetu kwa njia inayoshiria ubaguzi wa dhahiri, au kwenye mikanda ya runinga, nk. Ambavyo ni vitu vinavyoshambulia utaratibu mzima wa kiroho tunaojaribu kuujenga. Angalia Runinga yako kwa uangalifu sana, na kama ikiwezekana fanya hivyo sasa hivi kama ipo karibu yako. Kama hatutaweza tutajidhoofisha wenyewe na kushindwa kufikia viwango vya kujitoa sadaka kwa Bwana.
Dhiki Kuu itapita wakati ambao wateule wakiwamo, ambao ni Israeli wote. Lengo zima hapa ni kuharibu hali yetu ya kiroho, au uhusiano wetu na Mungu, kwa kuwa sisi sote ni wateule wake. Ni suala tu la wakati gani kila mmoja wetu ameitwa na kuhukumiwa. Taifa lile ni watu watakatifu, nasi tumetengwa na kuwekwa kando ili kufanyika makuhani wa Mungu. Kazi yetu ni kuwa na taifa ambalo watu wake watajua kuwa wao ni watu watakatifu, na kuwa kuna uwezekano wa wao kwenda kwenye kipindi cha majaribu na kwamba hakuna muda wa kucheza lelemama. Tunatakiwa kujinyenyekeza sisi wenyewe kwa Mungu.
Askari hutegemea nguvu za kijeshi na anafikiria kwa frikira za kijeshi. Huyo ni mtu ambaye anaelekea kwenye mrngo wa kuongoka. Matendo ya asili ya kimwili ni kupigana au kuwapigavita watu. Nabii Musa hakufanya hivyo. Musa alikuwa ni Jemadari. Musa aliwachukua watu wake katika mazingira ambayo hakuna jemadari wa namna yeyote angaliyeweza kufanya hivyo. Musa aliwachukua mpaka mahali panapoitwa Pi-ha-hiroth. Walishindwa kuvuka bahari; hawakuwa na mitumbwi, hakuna kamba za kuvukia, hakuna kurudi nyuma, hakuna muda wa kutosha kulianda jeshi la kutosha lenye kuweza kukabiliana na jeshi la Wamisri. Hakuna Jenerali, au hata askari mwenye cheo cha koplo, je, duniani ingaliwezekana fanya hivyo? Lakini ilifanyika ili kuonyesha kuwa tumaini halipo kwa nguvu au uweza, lakini ni kwa Roho wa Mungu. Kwa ajili hii ndio maana mataifa yenye nguvu kuu zaidi ya Israeli yatashughulikiwa kwanza. Yuda kwa sasa liko miongoni mwa makabila dhaifu sana, ndilo litaokolewa kwanza (Zek. 12:1).
Inaonekana kwamba Roho Mtakatifu anakwenda kuvunja nguvu za mataifa. Watu wanatumiwa kupitia Roho Mtakatifu, ili kuonyesha uimara kupitia waliodhaifu kuwa Mungu yumo kwenye uangalizi.
Kwa nini tunadhani kuwa Musa aliwatia Israeli mahali pale, na farasi wa vita na kuja nao? Lakini Musa hakusema “jifanyieni madaraja matatu, chimbeni mashimo machache simamisheni michongoma kwenye ardhi na tutajipatia silaha kali zenye kuweza kufanya maangamizi na nitakuwa nimepata silaha kali na bora kama kombeo”. Hapana, hakusema hivyo. Bali alisema simameni tu mkauone wokovu wa Mungu. Hakuna hata mtu mmoja aliyeinua mkono wake juu. Hivi ndivyo inavyokwenda kutokea katika kipindi hiki. Tunaenda na kuzungumza na watu wetu na kuwainua juu na kuwatia moyo.
Mungu anakwenda kuwashughulikia watu hawa wote. Kifungu cha maandiko ya Baragumu huonyesha kwa hakika jinsi inavyokwenda kutokea.
Tatizo lililoko duniani ni kwamba watu hawapendi kutubu. Wazimu huu unaweza kukomeshwa sasa hivi, kama tutawafanya watu katika nchi hii watubu. Tunaweza kufanya jeshi la malaika waizunguke nchi hii. Na tuombe ili kwamba Bwana atume malaika zake walizunguke taifa hili na tunaruhusiwa kulialika taifa hili kuja kwenye toba, na ili kwamba tufanyike kuwa nguzo, kwenye utawala wa Milenia, katika dunia hii.
Mungu anashughulika na sisi kupitia madhaifu yetu, na anatuonyesha madhaifu yetu. Anatuondolea yaliyo madhaifu na kutufanya tuwe imara. Hatupo hapa kwa ajili ya uwezo wowote wa nguvu zetu wenyewe. Bali tupo hapa kwa sababu ya kwa sababu ya udhaifu wetu, na baadhi ya madhaifu yako dhahiri. Tumeitwa ili kuvikwa uweza na sio kwa ajili ya uweza au nguvu zetu wenyewe. Hata hivyo, kwa tukiwa na Roho Mtakatifu tunayo nguvu. Tutaweza kuvumilia haya yote, na Mungu hatatia tena mzigo mwingine juu yetu tusioweza kuustahimili. Sio mmoja wetu ataweza kuulizwa kitu chochote ambacho Mungu hawezi kutupatia kikamilifu.
Wokovu wetu hautaweza kudharauliwa na Dhiki hii kuu. Tutaletwa na kuendelezwa au kuhuishwa. Tutajua watati ule Dhiki hii kuu itakapoisha kwa ajili ya ishara za mbingu, na kutakuwa na baraka nyingi kwetu.
Muhuri wa sita uko katika Ufunuo 6:12:
Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba na milima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja, naye ni nani awezaye kusimama?
Huu ni utaratibu mbovu sana. Tunajua kwamba hii itatanngaza mwisho wa kipindi cha dhiki kuu. Hii itakuwa kama manyunyu ya kuashiria kuwa ukombozi wetu umekaribia. Utaratibu ule huruhusu kuongezeka kwa mwandamano wa mambo. Ishara hizo za mbinguni hutia muhuri wa kuitwa watoke wale 144,000 kwa tukio la mwisho.
Ufunuo wa Yohana 7:1-8 inasema: Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote. 2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, 3 wakisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. 4 Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu. 5 Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu. 6 Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu. 7 Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu. 8 Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benjamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.
Maana yake ni kwamba hii haifuati makabila ya kawaida. kabila moja linakosekana, na kabila linajumlishwa. Kabila la Lawi kwa kawaida halihesabiwi miongoni mwa makabila, lakini katika kifungu hiki cha maneno wanajumlishwa. Kabila la Dani linawapa urithi wao. Dani haipo miongoni mwa wale 144,000 kama kabila lililotengwa. Kabila la Yusufu kwa kawaida huyazunguka makabila ya Efraimu na Manase. Pia kabila la Yusufu limetajwa pamoja na kabila la Manase. Kabila la Manase limetajwa mbali na kabila la Yusufu! Tena Yusufu limetumika tu mara nyingi kama kikundi kilichoundwa kutokana na mchanganyiko wa makabila kwenye nakala za Maandiko Matakatifu za huko nyuma. Kwa hiyo, kabila la Dani linaunganishwa pamoja kwenye kabila la Efraim na kuunda kabila la Yusufu kwa eneo lao lenye watu 12,000 katika siku za mwisho, katika wale 144,000. Hii nyio maana yake. Pia inatuonyesha kuwa Dani na Efraimu ni wamoja kama watu katika siku za Mwisho. Wamechanganywa kwa maana ya urithi wao wa kiroho. Jambo hili halifai lidharauliwe. Pia hukumu imewekwa katika Dani sawasawa na ahadi aliyoahidiwa ya haki yake ya uzaliza katika kitabu cha Mwanzo 49:16-18. Dani alihukumiwa kufanyika kwake mfano katika Yuda wakati wa Vita kuu ya Pili ya Dunia.
Ufunuo 7:9-17 inasema: Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikonini mwao; 10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aliye katika kiti cha enzi na Mwana-Kondoo. 11 Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mnele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu, 12 wakisema, Amina, Baraka na utukufu na hekima na shukurani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele. Amina. 13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? 14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanaotoka katika dhiki ile kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo. 15 Kwa hiyo mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. 16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. 17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.
Kwa wakati huu, wale 144,000 watakuwa wametiwa muhuri, ili kupata idadi kamili kwa kuweka maongozi. Chini ya viumbe hao kuna idadi kubwa ya watu ambao wamefikiwa. Hawa, hawakuchukua au kupigwa muhuri wa alama ya mnyama na wanaingizwa kwenye Dhiki Kuu. Kristo hawahitaji watu wenye nia mbili au waoga. Inatupasa tumuogope Mungu zaidi kuliko wanadamu. Tunaandaliwa ili tukabiliane na mfumo huu wa mwandamano wa matukio. Pia tunaandaliwa ili tuwasaidie hawa watu na kwa kupitia umati huu mkubwa ili kwamba mpango yakinifu ufanyike na Kristo mapema kabla ya kurudi kwake. Kisha wakati Masihi ajapo, atashughulika na ulimwengu uliobakia wa wale wote wenye chapa au alama ya mnyama na atayatiisha mataifa hayo. Kuna umati mkubwa na wengi sana. Sisi tutafanikiwa kwa maana ya kuwatoa watu nje. Sisi hatuyaongoi mataifa, bali sisi tunawavuta watu watoke. Kuna umati mkubwa wa watu wanaoelekea kuuelewa ukweli. Kwa hatua kama hii huashiria mwagiko wa maji. Kisha kunaonekana ukimya wa kiasi cha nusu saa.
Muunganiko wa hawa 144,000 umefanyika kwa mlolongo wa dhabihu kama zilivyoamriwa kwa kufuata misingi ya kila mwaka kwa kipindi cha zaidi ya Yubile arobaini. Hii imeelezewa kwa kutenganishwa sehemu nyingine.
Ufunuo wa Yohana 8:1 inasema: Hata alipofungua Muhuri ya Saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. Nami nikawaona wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba.
q