Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[141]

 

 

 

Baragumu Saba

 

(Toleo  2. 0 199509-20000902)

 

Baragumu saba za kitabu cha Ufunuo wa Yohana zinapelekea kwa Masihi. Vita vya mwisho ni sehemu ya mwandamano huu wa matukio. Mwandamano wenyewe wa matukio umeonyeshwa kiundani zaidi kwenye jedwali linaloonyesha jinsi matukio haya yatakavyotokea moja baada ya nyingine kuhusiana na hii mihuri na baragumu.

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

 

(Copyright ã  1994, 1995, 1999, 2000 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


 Baragumu Saba [141]

 


Utaratibu wa Mihuri Saba

Hapo mwanzoni, tumepitia kwenye masomo yahusuyo dhiki kuu na ishara zitokazo mbinguni na kpigwa muhuri kwa wale 144,000. Halafu tukajifunza kuhusu ule ukimya wa mbinguni unaodumu kwa kipindi cha nusu saa. Ukimya huu ni wakutisha. Sisi tumetiwa muhuri. Kwa hiyo kuna ukimya, ambao unaelezea matendo ya mchakato unaotupelekea kwenye katika ujio wa Masihi. Kila mmoja hapa duniani, kupitia ishara za mbinguni, anajua kuwa Masihi. Mara tu hizi ishara kutoka mbinguni zinapotokea, watu wanatahadharishwa kuhusu hizi ishara kutoka mbinguni jinsi zinavyotenda kazi. Wafalme na majemadari kwa hiyo wote wanasema “tufunike kutoka hasira za Yeye ajaye.” Inampasa Masihi aje, lakini bado hajafika bado. Ni dhahiri kabisa kutokana na hizi ishara za mbinguni, watu wengi sana wakiwemo watawala wa hii sayari, wanajua kuwa Masihi anakuja. Wote wanajua kuwa kuna kitu kinachokwenda kutokea.

 

Tutaipitia injili ya Mathayo na ile sura ya 10 na tutaona jinsi Kristo alivyosema:

Mathayo 10:16 inasema: Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu; …

 

Sisi sote ni kama kondoo walio katikati ya mbwamwitu. Sisi hatupo pale kwa nguvu zetu. Kwa kawaida, wakati kondoo anapopelekwa kwenye pori lenye mbwamwitu, basi anafanyika kuwa ni mlo wa nchana. Kwa hiyo ni kwamba hatuendi pale kwa nguve zetu ili kukabiliana na watu. Bali tunaenda kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

 

Maandiko yanaendelea kusema kuwa: basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua

 

Namna tunayoweza kulifanyia suala hili na nguvu za Roho Mtaklatifu, ili tusisababishe makwazo. Hata hivyo, tunasimama kwa ajili ya Bwana na hata hivyo tunakuwa mashahidi ingawa hatujawa na nguvu za kimwili kwa namna ya kama walivyo. nguvu za Roho Mtakatifu zinaweza kuvunja ngome. Sio udhaifu kwa maana ya Roho Mtakatifu kwamba tujitokeze kwao. Si kwa nguvu wala kwa bali ni kwa Roho Wangu asema Bwana wa Majeshi (Zek. 4:6).

 

Mathayo 10:17-24 inasema: jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga, 18 nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. 19 Lakini hapo watakapowapeleka msifikiri-fikiri jinsi mkatakavyosema, maana mtapewa saa ile mtakayosema.

 

Kila wakati tunatakiwa kuomba kwa ajili ya uvuvio ili kwamba, Bwana pamoja na Roho Mtakatifu watupe mambo ya kusema. Bwana yale tuyatakayo. Kwa kawaida, maandalizi ni ya muhimu kwa kazi yoyote njema. Hata hivyo, Bwana hutupatia mambo ya kusema tuwapo kwenye fadhaa na majaribu. Hutupatia yale tunayo yahitajii naye hufanya mambo ili kutufundisha somo vile vile. Hudhihirika kwa wazi kabisa kuwa kuna somo kwa njia ile tunayo fanyiwa. Kuna ajali chache sana katika maisha yetu. Tunajua kuwa Mungu anatushughulikika kwa kuwa mambo mengi yanayo tukia. Mambo kwanza kuangukia mahali na tunajua ndio maana yanatokea. Suala hili zima la Roho kunena na watu kupitia sisi hutokea kwa kupitia kwenye hii dhiki kuu hadi mwisho.

 

Roho hutushuhudia na kutuongoza yale tunayopaswa kuyasema na kuyatenda akituelekeza.

 

Maandiko yanasema: Kwa kuwa si ninyi mnenao, bali ni Roho .wa Baba yenu asemaye ndani yenu. 21 Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, wana watawainikia wazazi wao, na kuwafisha.

 

Hii imekuwa ikitokea kwa wateule hapa duniani kwa karne hii, na ni hakika ilitokea chini ya mfumo wa kikomunisti, na itaendelea duniani kote chini ya nguvu za mnyama (ambayo ni upanuaji wa mfumo wa tawala za mataifa).

 

Maandiko yanaendelea kusema: 22 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 23 Lakini watakavyo wafukuza mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.

 

Sasa hili ndilo andiko la msingi. Tutakuwa kwenye mwelekeo. Israeli itakuwa kwenye hali ya kushambuliwa na Israeli itashambuliwa. Israeli wote watakuwepo, na hatuongelei kuhusu Israeli walioko Yerusalemu na Israeli. Bali tunaongelea kuhusu mataifa ya Israeli. Watashambuliwa nasi tutakimbia kutoka mji huu hadi mji mwingine. Jambo hili halipo kitambo kirefu sana kutokea. Mchakato huu wote wa vita utakuwa hauna mpangangilio. Watu wengi hujaribu kupamba jambo hili kwa kulifanyia naigizo hasa waigizaji wa Hollywood, lakini uwe na hakika jambo hili halitakuwa zoezi zuri ama la kupendeza, na jinsi ya kuwanusuru watu ili wawe hai ni tatizo kubwa kukabiliana nalo. Baada ya ukimya huu, tumepewa baragumu saba.

 

Ufunuo wa Yohana 10:4-11 inasema: Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike. 5 Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni, 6 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele yeye aliyeziumba mbingu mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na nchi na vilivyomo, na bahari na vitu vilivymo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya, 7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika na saba watakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.

 

Siri za Mungu zimetimilika tu, zimekamilisha na kueleweka kwenye ile baragumu ya saba. Wakati tendo la kuwatia muhuri hawa 144,000 kukimalizika siri hii ifafunuliwa. Wakati ile ikianza na wakati mungu atakapo mimina Roho wake Mtakatifu kwa wateule, tutazifunua siri za Mungu, na kisha zitatimilizwa. Hapa ndipo waamini Utatu yaani Watrinitari na utaratibu wote uliopo utadhihirika kuwa ni wa uongo. Huduma ziilizotuama kwenye mtindo wa kimapokeo hazielewi fumbo au siri za Mungu kwa kuwqa wote wamepofushwa wasizijue. Ili kuzifikisha siri za Mungu kwa watu wote tunapaswa tusiache ai kuondoa vitu vinavyowapofusha. Tunaona haya yakitokea sasa (tazama jarida la Upimaji wa Hekalu [137]).

 

Tunapaswa kuangalia mchakato huu wote wa kila tarumbeta moja. Tunakwenda kwenye mlolongo wa matukio wa matendo yanayoharibu sehemu ya dunia. Wakati tunapoangalia kwenye tarumbeta tutaona kuwa zinahusu zaidi na za tatu. Kuna jambo lingine la tatu lililochukiliwa kwa sababu ya uasi unaotokea kwa Malaika wa tatu. Kila kitu hufanyika kwa sababu na kila kitu kinafanyika kwa maana ya kiroho.

 

Ufunuo wa Yohana 8:7-13 inasema: Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea

 

Tunatazamia kona uharibifu wa vitu vya mbinguni; hii nahusisha mazingira nk, na vyanzo vya mambo mengine, maangamizi ya mazingira ambayo yataunguza theluthi moja ya sayari ya dunia, miti na majani yote. Kwa hiyo, tunatazamia njaa kuu itatokea kwa ajili ya ukame. Mlolongo huu halafu utaendelea.

 

Maandiko yanaendelea kwa kusema: 8Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu. 9Wakala theluthi ya viumbe vilivyoko baharini, vyenye uhai, theluthi ya merikebu zikaharibiwa.

 

Milima inayo angukia baharini inamaana ya idadi ya fursa kutolewa kwa maana ya baragumu hii ya pili. Pengine sisis tunashughulika na kila kimoja wapo kwa kufanya kitu kile kile ambacho Musa alifanya kule Misri. Musa aliivunjilia mbali miungu ya Misri na kuvunja moyo Wamisri. Ni kwa nana hiyohiyo basi kusema kuwa mambo haya yote hubomoa miungu iliyoko kwenye sayari hii na kukaba shingo za watu tunashughulika nao; mfumo wa kidini na mafundsho na thamani ya hii sayari. Mfumo huu wote wa miti, nyasi, na baragumu ya kwanza utahusu na sehemu ya vuguvugu la imani potofu ya zama mpya na makaazi ya waroho au (wa animism); imani ya kuabudu miti na kuomba roho. Dini ya zama mpya inaelekea kuwa ni mfumo wa imani inayoamini kuwa vitu vyote vinatokana na sili moja yaani monism, ambayo chanzo chake ni imani ya waroho yaani animist. Wao huamini kuwa kuna roho katika kila kitu.

 

Ni machukizo kusema kuwa Mungu yupo kwenye kitu. Mungu hayupo kwenye mfumo wa kimonisti. Mungu sio wa namna ya imani tegemezi kwenye kitu kimoja yaani immanent. (Yeye yu bora sana na anaweza kuingia kwenye kitu chochote). Mungu aliumba kila kitu lakini hayumo kwenye kila kitu, kwa maana ya kama wanavyoamini hawa wa animism. Mchakato huu huendelea. Tutajionea jinsi vuguvugu hili la zama mpya litakavyo pamba moto na mafundisho yao yanayoitwa mchakato wa teolojia endelevu. Hapa ndipo wanapo angukia kumfanya Mungu kuwa ni wa aina hii ya muonekano wa hawa wa immanent. Huu ni mfumo wa Kibabeli. Utapamba moto tena kwa nguvu zaidi kwa walio na imani ya Mabudha. Utasimamiwa na Wabudha na kinachoitwa teolojia za uhuru wa kimashariki.

 

Kule kuonekana bahari ikipigwa kisha ikifuatiwa na milima ikiangukia baharini. Wa roho yaani animism wanaendeleza hadi kwenye imani ya dini ya Washinto, ambayo ni kutoka Ujapani. Mlima wao mtakatifu sana ni Fujiama, mlima wa vilkano. Nguvu za tetemeko la ardhi ambayo imeutupa mlima bajarini, hapa kwa mfano Fuiiama, inaonyesha kuwa Mungu hushughulika na imani ya Washinto na madhehebu mengine ya dini za mashariki. Kwa kawaida tendo la kuichukua volcano na kuitupa baharini, na kuharibu visiwa kutatufanya tuwe kwenye myumbo mkuu sana wa mavunjiko ya mfumo wa dunia. Sehemu ya vuguvugu hili la myumbo mkuu unafanyika sasa na Warusi, Wachina na Wamarekani wanaotengeneza milipuko ya nguvu za nyukilia kwa kufuata msingi ulopangiliwa vizuri na kuanzisha mavunjiko makuu ya dunia. Haya matetemeko ya ardhi tunayoyapata au kuyaona leo ni sehemu ya majaribio ya makusudi kabisa ya kiufundi wa mitambo inayolipuliwa kwa makusudi chini kwa chini ya ardhi. Wachina walipiga kura ya mwisho katika ya turufu kwa sababu hawakupata zabuni ya Michezo ya Olimpiki. Mlipuko wa nyukilia wa hivi karibuni uliotokea mwaka 1995 umesababisha msisimko kwa Ufaransa, lakini Uchina haitajwi kabisa. Ni kwa nini? Kwa kuwa hakuna mtu atakayeweza kuishawishi Uchina. Uchina ni nchi hatari zaidi kuliko Ufaransa. Hata hivyo, mataifa yote mawili yatashiriki kwenye machafuko ya vita vya mwisho. Watu wamegeuzwa na mawazo yao yaliyounganishwa na kuwa wazi kwa Shetani. Tunalotakiwa kufanya ni kujihadhari na yale yanayotokea. Watu hawa wanatumiwa ili kuiharibu hii sayari. Majaribio ya kiufundi ya mitambo au silaha yanayoendelezwa yanaimarisha mavunjiko na kutakuwa na mfululizo wa matetemeko ya ardhi ambayo yatakuwa na maana kuu. Tetemeko kuu la ardhi litakalotokea kwa ajili ya kutimiliza unabii wa ishara za mbinguni litakuwa ni tetemeko kuu sana la ardhi ambalo halijawahi kutokea au kuonekana hapa ulimwenguni. Haya mashindano ya utengenezaji wa silaha kali yanafuatana na mwandamano ulioko kwenye unabii. Yatakuwa na kitu cha kufanya na vuguvugu uimarisho wa hii milima, lakini pia ujenzi wa gamba la hii hauwezi kustahimili aina ile ya uimarisho, na kosa la San Andeas liko tayari kwenda.

 

Kuna matetemeko ya nchi kila mahali ya sayari ya dunia hii, lakini kubwa kuliko yote tiliyowahi kuyaona na ambalo halijawahi kutokea litakuja kutokea kama ishara ya mbinguni na litaharibu sehemu kubwa ya viumbe vilivyo hai, yaani watu na wanyama na vilivyomo baharini. Tetemeko la ardhi la mwisho litakuwa ni kuu kuliko yote yaliyowahi kutokea.

 

Utendaji wa tetemeko la ardhi pia utaachilia mawimbi mazito katika vilindi vya bahari kutoka kwenye kingo zake. Mawimbi haya ya myumbo mkuu wa bahari yatachukuliwa hadi kwenye vitu vitumiwavyo kwa chakula, hadi kwenye mchapo mkubwa, na kutakuwa na mawimbi makubwa mekundu kuwahi kutokea baharini. Tatizo la wimbi au mkondo mkuu mwekundu litaongeza machafuko pia kwa ajili ya ukweli kwamba kuna kiasi kukubwa cha masalia ya nyukilia yaliyotupwa kwenye bahari ya Kati yaani Artic na bahari zinazo izunguka nchi ya Ujapani na kwenye bahari za kaskazini mashariki na manowari ya Warusi. Mabaki ya takataka za nyukilia yamewekwa kule kwa lengo la kutishia watu. Watu wengi kutoka kwenye kizio cha pemba ya kaskazini watakufa.

 

Tunaweza kujikuta tukijiuliza kusema, “je, watu wahawa wanawazimu, au je, hawawezi kuona kitu wanachofanya?” Ndiyo wanaona wanachokifanya. Wamefungwa kwenye moondo fulani na mchakato wa kimawazo, na hawawezi kubadili namna yao ya mtindo wa maisha.

 

Nchi ya Marekani (na za Magharibi kwa ujumla) zinamiliki sehemu kubwa ya nguvu za kinishati za dunia. Kwetu sisi ili kuifanya nchi ya India kufikia kwenye kiwango cha maisha ya Marekani, italazimika kutoa kwa asilimia 110 ya uzalishaji wote wa nishati za dunia. Kwa hiyo, ni wazi kabisa kuwa namna ya maisha yalivyo kwa Marekani haiaminiki. Wanatakiwa kubadili mwenendo wao, lakini hawawezi kutubu na wala hawawezi kubadili mwenendo wao na viongozi wa dini zao kwa kweli wanachangia kwa kuwatia moyo kuendelea kuishi aina hii ya maisha.

 

Mnamo mwaka 1994, kabla ya sikukuu, gazeti lichapishwalo katika mji mkuu wa Sydney liitwalo Mjumbe wa Asubuhi kwa Kiingereza the Sydney Morning Herald lilisema kuwa Warusi walisababisha kuzama kwa manowari ile ya Kirusi kwa ile gundi kali. Gundi kali hii ilikuwa ifikie kikomo chake baada ya kudumu kwa kipindi cha miaka 500. Wana weza kuivuta na kuikuta ikiwa salama kwa kipindi hiki cha muda wa miaka 500, hata hivyo, chombo cha kunasia sauti kilichookolewa kilichotengenezwa kwa madini ya platoni, kinaweza udumu kwa zaidi ya miaka 25,000. Sasa platoni hii inavuja ikiwa kwenye bahari ya kaskazini kwa mwaka wa pili, au kwa mwaka wa karibu sana baadae. Sasa tunayo mabaki mengine ya patoni ya manowari hii iliyozama yaliyoenda baharini mwaka ujao. Silaha hizi zote ndizo zitakazo sababisha maangamizi makubwa humo baharini. Utaratibu wa njinsi hatua zitakavyokuwa umeshawekwa. Hakuna aliyeweka manowari ya nyukilia pamoja na kuikwamisha cini ya bahari kama si kwa ajili ya uchoyo, tamaa na uzembe wa watu wanaounda hivi vitu. Wanayaharibu mazingira yao wenyewe. Kilichotokea huko Chernobyl kina maana kuu na kuifanya nchi ya Urusi ionekane kama mmea unaoitwa wormwood au mti wenye mabuu. Wanajenga mitambo ya nyukilia kwenye vitu na mahali ambapo pako nje ya kiwango kinacho takiwa, na hawakuweka sera yoyote ya kilinda kwa sababu hawakuwa na umiliki na hakuna watu wa kuwa ambia la kufanya kwa kuwa walikuwa watawala maimla. Walikuwa na utaratibu wao wenyewe wa ki wormwood. Nyota haihitaji kuwaangukia, kwa kuwa tayari ipo pale. Hii ilisababishwa na zege, na zege linavunjika na kuanguka chini. Kwa hiyo hawajui la kufanya. Zege sasa linakuwa ni kile chombo cha kurekodia matukio kwa hiyo wanakwenda kupata tofali kubwa la zege kwenda kushughulika na jambo hili.

 

Je, tunakwenda kuishia wapi? Mfumo huu hauaminiki. Wanatakiwa kubadilishwa. Theluthi moja ya bahari wanakwenda kufa. Sio kwa mauti ndogo. Theluthi moja ya merikebu zinaangamia kwa sababu ya kitu fulani kinatokea. Kuna mawimbi kama ya tsunami yanayo ambatana na vifo hivi, na kwa milima hii inayoangukia baharini, Krakatoa ni kisiwa kilichoko nchini Indonesia. Kwenye kisiwa kulikuwa na mlipuko wa volcano na ililipuka katika karne iliyopita. Ililipuka na nguvu za idadi kadhaa ya silaha za nyukilia. Jua lote na mwezi vilitiwa giza. Mlipuko ukaifunika dunia (vikiwemo vumbi, nk.) kwa kipindi cha miezi kadhaa. Ilienda chini pale pale kwa mlingano wa dunia. Milipuko hii ilisikika hadi kufika mbali zaidi hadi kwenye mji mkuu wa Australia. Ni urefu mkubwa sana mbali kutoka Indonesia kwenda Australia kiasi cha kusikia sauti ya mlipuko. Hii itakuwa sawa sawa tu na vile itakavyotokea.

 

Unabii wa hotuba au mahubiri ya kwenye Mlima wa Mizeituni unaongelea kuhusu jinsi uvumi wa bahari utakavyo watia hofu watu. Mawimbi ya baharini ya tsunami yanasafiri kwa kasi cha mwendo wa sauti ya karibu maili 700 kwa saa. Mawimbi yake hufikia kiasi cha urefu wa maelfu ya kipimo cha rula. Kwa matendo ya mlipuko wa tetemeko kubwa la ardhi, yatakwenda kufikia hadi kwenye futi 1,000 urefu wa kwenda juu. Tunakwenda kujionea mawimbi marefu kiasi cha futi 1,000 kwenda juu yakisafiri kwa mwendo wa kasi kiasi cha maili 700 kwa saa. Hebu fikiria jinsi sauti yenyewe na msukumo unaokwenda kutokea mkabala na mataifa haya. Hivi ndivyo thekuthi moja ya merikebu zinavyokwenda kuangamia. Watu watakuwa wakihofia kabisa. Mpaka pale tu kama tukijua kuwa inakwenda kutokea hivyo, na hii ni nyuma ya hili lote, tungeogopa sana. Tatizo letu halipo nyuma ya hii hofu. Woga dio tatizo letu kwa sababu tunajua ni kitu gani kinachokwenda kutokea.

 

Maandiko yanasema: 10 Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji. 11 Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu

 

Hata kama iwe ni nyota ya kweli ile iliyoichafua sayari au kama ni takataka za nyukilia ni vigumu kujua. Ila inasema kuwa ni nyota na sisi tutaitumia maana hii hii halisi iliyoko kama ilivyotajwa. Hakika inachafua theluthi ya maji. Kwa hiyo, mfumo wa sayari yetu unapungua maana au mwelekeo wake, na unafanyika kuwa ni mahali pasipo kalika.

 

Mchakato huu unatokea kwa sababu watu wanaiharibu hii sayari kwa mpangilio uliowekwa kimsingi. Hali hii itazidishwa ili kuwashughulikia.

 

Maandiko yanaendelea kusema: 12 Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya juu ikapigwa, na theluthi mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theuthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, wala usiku vivyo hivyo.

 

Sisi sasa tunangojea milipuko itakayosababisha giza kuu la kuifunika dunia yote. Pengine na inawezekana sana kuwa huenda kutakuwa na sababu ya pili ambayo yaikuelezwa hapa. Kwa hiyo, matendo haya yatazidisha mchakato wa mateso yatakayoikumba hii sayari. Kima cha usawa wa bahari kitainuka au kupanda juu na visiwa vitafunikwa. Wazo la visiwa vitakimbilia mbali linahusisha mambo mawili:

 

1. Tatizo la usawa wa ardhi kulinganisha na kina cha bahari.

2. Tatizo la mchakato wa mateso yatakayo ikumba dunia yetu hii.

 

Hebu na tuangalie kina cha usawa kinachohusu bahari. Kilindi cha Magharibi mwa bahari ya kati, yaani Antarctic kina maji yenge barafu chini ya kilindi cha usawa wa bahari. Kwa mujibu wa wanasayansi, kuna kina cha kutosha kufanya usawa wa bahari wa kama futi 15 hivi kama barafu ile ikiyeyuka. Hali hii yote inazidisha mwenyendo wa mchakato wenyewe. Mara tu kingo za bahari hii ya kati yaani Antarc na nchi ya Greenland zikienda na ongezeko la joto la bahari, hufikia kiasi cha kina cha futi 200 na pengine inawezekana kuwa hata na futi 100 zaidi. Watu walioko chini ya kina hiki hupata fursa ya kuwa chini ya bahari.

 

Kinachotokea baadae ni kwamba theluthi moja ya mito itaharibiwa kama mito itafunikwa. Kilindi cha Mississippi, Ulaya ya Kaskazini, Thailand, nchi yote ya uwanda wa chini wa Uchina, mabakuli yote ya vyakula vya Wachina yatatwaliwa au kusombwa. Kisha wakati msukumo huu utakapowekwa kwenye hii sayari ili kuwezesha uwezekano wa maisha yaendelee kuwepo. Wakati vita kuu inapokuwa ni ya lazima katika kuwapanga watu ili kuwapatia waliosalia bakuli za chakula, kwa sababu bakuli kuu za chakula zitakuwa zimeondolewa. Halafu tutaona ni kwa nini tunaenda hadi kwenye hatua ya pili, ambayo ni Ufunuo 8:13. Huu ni mwanzo wa hizi ole.

 

Maandiko yanasema: 13 Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga.

 

Kuna ole tatu. Sisi bado tutarudi nyuma kwenye mwandamano unaofuata. Tumeupata ule muda wa taabu yake Yakobo, na Israeli wanahusishwa. Tumesikia habari za dhiki kuu. Pia tumepewa mashahidi wa siku za mwisho. Hadi kufikia hapa tunarudi kwenye Ufunuo 11:1.

 

Kuna michakato miwili.

 

Ufunuo wa Yohana 11:1-19 inasema: Nikapewa mwanzi kama fimbo, na mmoja akaniambia, Inuka ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo. 2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili. 3 Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.

 

Hakalu linapimwa kutokea juu (tazama jarida la Upimaji wa Hekalu [137]. Hii inatokea na imetokea. Huduma inapimwa. Hii pia imetokea. Kwa kipindi cha muda wa miezi 42, wateule kama taifa watatakaswa. Tunaelekea kwa kupitia mchakato wa kupimwa kwa wateule. Mchakato huu utaanza mara hii. Wateule watapewa mamlaka ili kufanya majukumu kila mtu na mwingine na hii ndio sehemu ya njia tunayopimiwa.

 

Baada ya kuanza kwa upimaji ule, mashahidi wawili watasimama huko Yerusalemu wakiwa wamevaa nguo za magunia. Watu hawa watasimama kwa muda wa miaka mitatu na nusu (tazama jarida la Mashahidi [135].

 

Maandiko yanaendelea kusema: 4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. 5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. 6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo kila watakapo. 7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye naye atawashinda na kuwaua. 8 Na mizoga yao itakuwa katika njia za mji ule mkuu, ulitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa.

 

Kristo alisulibiwa pale Golgotha nje ya mji wa Yerusalemu. Mashahidi hawa wanaufananisha mji wa Yerusalemu kama Sodoma na Misri kwa ajili ya uasi na ukengeufu ulioko ndani yake. Maana yake hapa ni kwamba, watasimama ili kushughulika na nguvu za Mungu. Wataongea na watu watajaribu kuwaua, lakini watu hao watawafanyia kwa namna ile ile waliyowafanyia mashahidi. Kila atakayejaribu kuwaua kwa risasi atauawa kwa kupigwa risasi. Watalindwa. Hakuna mtu atakayewaua kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu mwaka. Watakuwa ni watu wasioharibika. Wataagiza moto ushuke kutoka mbinguni na ikawa hivyo. Waweza kuzifunga mbingu. Hakuna vyua itakayonyesha kwenye hii sayari yetu kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu na nusu mwaka, hadi pale watakavyoiamuru. Kwa kipindi hiki wataweza kuibadili bahari ili kuwa damu. Mambo haya yatakuwa na matokeo ya moja kwa moja kwa maafisa hawa wa Mungu, yakikwaruza chini makoo ya watu wa sayari hii, mchakato mzima wa waabudu sanamu wa sayari hii. Tumeishapigwa muhuri tayari hadi kufikia hatua hii. Tunatokea kwenye dhiki kuu. Kanzu zetu zimesha fanywa kuwa nyeupe kwa damu ya mwana kondoo tutaona hili likitokea. Wakati huu wa kipindi cha miaka mitatu na nusu mwaka tutaona yakitokea. Tutawatazama watu hawa na wataona mambo haya yakitokea kwenye hii sayari. Kuna kitu kimoja tu tulichopewa, nacho ni kwa mkate wetu na maji vitapatikana kwa uhakika. Mungu atatulisha kwa mana. Tunaweza kujiuliza kwamba “ni kwa namna gani tutaweza kupata huu mkate?” Wakati tukipungukiwa na mkate, kumbuka ahadi za Mungu. Mkate wetu na maji vtakuwa vya hakika. Tutalishwa kwa namna ile ile kama Waisraeli walivyolishwa jangwani. Ni suala la kuamini tu. Tunatakiwa tuwe na hakika iliyo yakini ya yale tunayoyafanya na yale tunayoyaongea kwa sababu tunatakiwa kujiweka sisi wenyewe pamoja na waatu wetu kwenye tatizo hili.

 

Kufuatana na mashahidi hawa tunaenda kwenye baragumu ya tano.

 

Ole ya Kwanza

 

Ufunuo wa Yohana 9:1-21 inasema: Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota ikitoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. 2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. 3 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyonayo nge wa nchi. 4 Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu chochote kilicho kibichi, wala wala mti wowote, ila wale watu wasio na muhuriya Mungu katika vipaji vya nyuso zao. 5 Wakapewa amri kwamba wasiwauwe, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu. 6 Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.

 

Watu wengi wahitaji kufa katika kipindi hiki, lakini hawataweza kufa. Shimo lisilo na mwisho la nzige litaambatana pia na malaika wanne watokao kwenye shimo la uharibifu waliofungwa katika Frati. Malaika hawa wapo hapa ili kufanya mauaji makuu yatakayo angamiza theluthi moja ya wanadamu wote. Hapa tunazungumzia kwa habari ya vita, mafuatano ya mambo na silaha za sumu za kuangamiza halaiki. Zitafanyakazi kwa kufuata maelekezo ya mapepo.

 

Maandiko yanaendelea kusema: 7 Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi wakiowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kuna taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu. 8 Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. 9 Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii ya chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani. 10 Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao. 11 Na juu yao wanaye mfale naye ni malkia wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.

 

Apolioni maana yake ni mharibifu.

 

Wazo lililoko kwenye Biblia ya Kiingereza iitwayo Annotated RSV linasema kuwa tauni ya nzige wa kipepo linalojumlisha na roho chafu zinazo ogofisha na zinazo washambulia wale wapanda farasi kuwa ni (wanasema kuwa) pengine ni Waparthi. Waparthi ni kabila linalotokea katika nchi ya Irani. Inaweza kuwa ni baadhi yao, lakini yawezakuwa ni madai ya uongo. Tukirejea kwa habari ya ile nyota inayoanguka kutoka mbinguni, inaweza kuwa ni mmoja kati ya wale malaika waasi waliotupwa chini, au inawezekana ikawa ni Shetani mwenyewe, na kisha kwa tukirudi kwenye ile aya ya 3 wanaongelea kuhusu kuhusu nzige na kadhalika.

 

Watu hawa wanaona kuwa kuna mahusiano kati ya malaika muasi ba vita na Shetani. Jeshi la kipepo haliendi kukata tamaa. Dunia hii itachukuliwa kwa nguvu. Wakati Kristo atakapokuja hapa, inakwenda kuwa kwa lazima na kikosi cha jeshi la malaika. Hawaendi kutoa wito tu wa ‘kusema tokeni, ni wakati wa kurudi kwangu’. Bali tunaenda kumuona Shetani akitupwa duniani na kufungwa kuzimu. Habari hii inaonekana kwenye hadithi ya “Vita vya Nyota”. Kurudi kwa Jedi ana Ewoks, na Darth Vader ana tukuzwa na kuharibiwa na Luke Skywalker. Sisi ni ewoks. Habari hii inahusiana na mchakato wa kumzuia Yesu Kristo.

 

Kwenye mkanda wa sinema wamemuonyesha Darth Vader akitubu mwishoni. Msaada wake umepita mfano. Tunaposoma kitabu cha nabii Isaya sura ya 53 tutamjia Darth Vader ni nai. Wamerudia tu mpango wa habari yenyewe. Yesu atakuwa sasa ni kijana mbaya anayetumia vibaya ule ubora wake. Kila muunganiko wa waasi kwa kweli ni wa vijana wazuri. Hata wamepewa majina ya wapepo, kwa mafano, Obe-one-Kenobi. Hii moja ni ya lugha ya Kiebrania yenye maana ya roho za ukoo. Obe-l ni roho ya ukoo. Inatokana na kugugumia kwenye chupa. Inatumika pia kwa wapunga pepo wenye sauti za kuigiza. Ilikuwa ni Obe kwenye mapango ya Endori. Luke Skywalker ni jina la kujipachika la kishamani. Yeye awezaye kutembea mawinguni kutoka kwenye mfumo wa kishamni. Mambo haya yote na tuyawekeze kwenye mioyo ya watoto wetu, ili waujue na kuukumbuka ukweli. Hivi ndivyo walivyoifanya hii sayari itembee kinyume na Yesu Kristo wakati ajapo mjini Yerusalemu, kwa sababu wataona yote haya na watafanywa wamuone yeye kama adui. Ni propaganda za kimtindo wa porojo zinazofikiriwa zinaweza kuleta amani. Hakuna cha zaidi ila ni ujumbe wa uongo na unabii wa uongo umetolewa na hadi kufikia wakati huu sisi hatuja dhihirisha cho chote.

 

Baada ya kipindi hiki cha miezi hii mitano ole ya kwanza itaishia. Lakini zinabakia mbili nyingine zinakuja.

 

Maandiko yanazidi kuelezea: 12 Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye. 13 Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu, 14 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue hao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati. 15 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mezi na mwaka ili kwamba waue theluthi ya wanadamu. 16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao. 17 Hiyo ndivyo niilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao walitoka juu yao wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto wa moshi na kiberiti. 18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo wa moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao. 19 Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao, maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wadhuru kwa hivyo.

 

Vifaru vya kivita vitasafiri vikiambatana na bunduki nyuma yake. Mtutu wa bunduki utatoa mshindo pamoja na kikomeo ndani yake, kinachoonekana kama nyoka mwenye kichwa. Mtume Yohana alikiona kitu hicho kwenye maono, akajaribu kuezea akifananisha na ndege aina ya helikopta na vifaru vya kivita vilivyokuwemo katika karne ya kwanza. Mtume Yohana likuwa bado hajaona kabisa silaha ya aina kama ile. Kitu kikubwa sana zaidi ya vyote alichowahi kuona kilikuwa ni mtambo wa kivita uliokuwa unatumika siku zile za zamani uliokuwa unaitwa ballista, ambao ulikuwa kama manati makubwa uliokuwa unatumika na Warumi. Kwao wao, jambo hili au maneno haya yalikuwa si kitu cha kuaminika au kusadikika.

 

Baragumu ya Sita.

 

Maandiko yanasema: 20 Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda. 21 Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.

 

Mchakato huu unapelekea kuwaleta wao kwenye toba.

 

Hivi ndivyo hawa mashahidi wanavyosema: Tubuni! Na kama hamtaki tutawaangamiza. Lakini wao wanakataa kutubu; kwa hiyo wanapata pigo na baragumu halafu ikifuatiwa na ya pili, ya tatu, nk, na hatimaye sayari itagugumia kwa kite cha huzuni na wataenda vitani. Theluthi moja ya dunia itauawa katika vita hii kwa kuwa hawakutubu. Tunapaswa tuhakikishe kuwa watu wajue kuwa wanaweza kutubu. Tunatakiwa tuwaeleze sababu inayowalazimu wao kutubu. Hakutakuweko na aina yoyote ya majadiliano na mashahidi hawa. Haya hayatatokea nje ya uzio wa maongozi ya Mungu. Haya yatatokea kwa maelekezo kutoka kwa Yesu Kristo kupitia kwa mashahidi hawa wawili. Tutakuwa kwenye himaya ya mchakato huu. Hatuna kitu tunachotakiwa kukiogopa kutokana na mchakato huu.

 

Maandiko yanaendelea kusema: 20 Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda. 21 Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.

 

Sayari yetu hii itapiga kite cha huzuni chini ya mchakato huu. Vita hii itaua theluthi moja ya wanadamu wakaao chni ya mbingu. Tulikuwa na Vita Kuu ya Kwanza iliyokuwa inapiganwa kwa ajili ya kuondoa Ushenzi na kuwekeza Usataarabu katika miaka ya 1914-18, lakini haikuua theluthi moja ya wanadamu. Ile ilikuwa ni vita iliyokomesha aina yote ya mapigano madogomdogo. Halafu tukarudi kwenye jambo hili tena katika miaka 25. Lakini hivi vyote havifui dafu kabisa ikilinganishwa na vita hivi vya mwisho. Halafu kutafuatiwa na milio saba ya ngurumo kama ya radi ambayo itaambatana na mchakato mzima wa unabii huu.

 

Ufunuo wa Yohana 10:1-11, inasema: Kisha nikaona malaika mwingine menye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake ni kama nguzo za moto. 2 Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi. 3 Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao. 4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike. 5 Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni, 6 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya; 7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.

 

Ngurumo saba za radi zina shemu muhimu ya ujumbe, ambayo tatokea katika siku za mashahidi hawa, katika siku za mwisho. Mwishoni mwa wakati huu, siri za mwisho za Mungu zitafunuliwa. Siku 1,200 zitaisha na ukame na magonjwa yatakuja.

 

Maandiko yanaendelea kusema: 8 Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilisema nami tena, ikisema, Enenda ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mikono ya yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi. 9 Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia cuhungu tumboni mwako bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali. 10 Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila, nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu. 11 Wakaniambia, imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme.

 

Kisha itakuja Ole ya Tatu

 

Ufunuo wa Yohana 11:11-14 inasema: Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho yauhai itokayo kwa Mungu itawaingia, watasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu itawaangukia watu waliowatazama. 12 Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama. 13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukana Mungu wa mbingu. 14 Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu unakuja upesi.

 

Ujio wa Masihi

Kutokana na ujio wa hawa mashahidi tunajua kuwa ni mwisho wa ole ya pili. Vita vya baragumu ya sita itatokea na kisha vitaisha. Mashahidi hawa wawili wataishia mwishoni mwa vita ya baragumu ya sita kisha watakwenda mbinguni. Huu ndio utakuwa mwisho wa baragumu ya sita na ole ya pili. Ni mgawanyo ulio dhahiri wa mstari. Mapenzi ya Mungu na yafanyike. Mashahidi na wafanyike. Kila mmoja atawachukia. Tunalijua hili kwa sababu wote wanapeana zawadi kila mtu na mwenzake za kupongezana baada ya hawa mashahidi wakifa. Hakutakuwa na toba. Watarudia mtindo wao wa maisha waliyokuwa wanayatenda mbele ya hawa mashahidi.

 

Kitabu cha Ufunuo wa Yohana katika zile sura za 12 na 13 zinahusika na Kanisa. Wateule ni wadau muhimu katika kufanikisha mchakato huu. Wateule wanahusishwa kwenye kifungu hiki cha Biblia. Mchakato wote mzima wa kushughulikia ilimwengu huu ni wa muhimu katika kuchagua na kuwaelekeza wateule. Kwa hiyo wateule watashughulikiwa kwanza kabla ya yote. Watatiwa muhuri, na Dhiki Kuu wakitiwa muhuri na umati wa watu na maangamizi yanaandaliwa. Tunahukumiwa. Kisha dunia itashughulikiwa. Dunia haitaweza kutubu. Kisha mwandamano huu wa mambo yanaelekea kwenye Ufunuo wa Yohana 11:15, ujio wa Mashihi.

 

Kwa hiyo, tunamtazamia Yesu akirudi kwenye mlima wa Sayuni. Kwenye kitabu cha Ufunuo sura ya 13 tunamouna mnyama akiushughulikia wanadamu. Ufunuo wa Yohana sura ya 12 inashughulika na mfumo wa Kristo. Ufunuo 13 inahusika na mfumo wa mnyama. Zote mbili zinaendana kwa wakati mmoja yaani sambamba. Haitatokea baada ya ole ya pili na katikati ya wakati wa ujio wa Masihi. Mifumo hii ya miwili ya utendaji wa kazi sambamba kabisa mapema kuelekea au wakati kipindi hiki cha hizi ole.

 

Ufunuo wa Yohana 14:1-20 inasema: Kisha nikaona, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. 2 Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakipiga vinubi vyao; 3 na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi. 4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. 5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.

 

Hali hii ya kutotiwa uchafu au kunajisika na wanawake inamaanisha kuwa wao ni wanawali wa kiroho. Wanawake ni sarufi inayotumika kuelezea makanisa kwa hapa duniani. Pia kuna uwezekano wa kuwa watu hawa ni makabila. Wale 144,000 watachukuliwa kwa kipindi cha majira hayo. Uchaguzi wa wale 144,000 ni kwa mchakato wa makanisa kwa milenia mbili (pia tazama jarida la Mavuno ya Mungu, Dhabihu za Miandamo ya Mwezi, na wale 144,000 [120]; Miandamo ya Mwezi [125]; na Miandamo ya Mwezi Mpya katika Israeli [132]. Malumbano yanaweza kuendelea kuwa tunashughulika na umati wa watu 144,000. Jambo hili linaweza kuelekezwa mahali pengine popote.

 

Mlolongo wa hawa 144,000 ni kuwa wao bado ni washiriki kwenye, au kwa ushirikiano na, ule umati mkubwa. Kazi yetu kubwa tuliyonayo ni kusaidia taifa zima na sayari yote ya dunia. Hatufaswi kuogopa ikiwa tunaweza kuwa kwenye kwenye kundi moja la upande Fulani au kwenye lile lingine. Kusema kuwa ni mataifa gani haya ni ni mapema mno bado. Utambulisho wa mataifa unahitaji kuwa unaendelezwa zaidi. Hata hivyo, kila mmja anakwenda kuwa katika Israeli mwisho wake. Kila mmoja anakwenda kuwa ni Israeli wa kiroho kwa kipindi chote cha Milenia, au vinginevyo watakufa.

 

Wakati huo Masihi atakapokuja, atamuua Asi yaani Mwana wa Kuasi audanganyae ulimwengu, kama tunavyojua ilivyo andikwa katika Waraka wa pili kwa Wathesalonike. Kisha, sayari yote inakuwa chini ya milki ya Masihi kiutendaji, katika mipango, kuanzia kutoka kwa wale 144,000 hadi kwa lile kundi kubwa na katka kipindi chote cha Milenia.

 

Maandiko yanaendelea kusema: 3 na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi. 4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. 5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.

 

Hadi pale tutakapoujua wimbo waliopewa wale 144,000 hatuujui kama tupo miongoni mwa hawa 144,000.

 

Na wala uongo haukuonekana vinywani mwao. Hii ndio kiini cha siri ya utauwa wao au hali yao ya kuonekana wakiwa hawana doa. Huu ni uthibitisho wa utukufu wao kwa Mungu na katika kweli yake na tunatakiwa kuwa tumejitoa kikamilifu kwenye kweli ya Mungu. Wakati mwingine ukweli huwa haupendezi na huwa mchungu. Tumejitoa kwenye ile kweli ya Mungu na kweli hutuweka huru. Hii ni kweli iliyo halisi. Tutakuwa miongoni mwa wale 144,000 kama tukijitoa, na tukiwa tayari kufa kwa ajili ya kweli ya Mungu.

Maandiko yanaendelea kusema: 6 Kisha nikaona malaika mwingine, akaruka katikati ya wingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji. 8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo wa ghadhabu uasherati wake. 9 Na mwingine, malaika wa tatu, akafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu waye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, 10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila apokeaye chapa ya jina lake. 12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu. 13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa, Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao wafuatana nao. 14 Kisha nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali. 15 Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa. 16 Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautuma mundu wake juu ya nchi, nchi ikavunwa. 17 Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali. 18 Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana. 19 Malaika yule akautupa mundu wake katika nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu. 20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka kama shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili.

 

Hiki ni kiasi kikubwa sana cha damu. Ukubwa wa kipimo cha ujazo yaani stadia 1,600 ni sawa na wastani wa maili 5. Hiki ni kiasi kikubwa sana cha idadi ya watu waliokufa. Tunamuongelea Kristo atakayechukua hatamu za mamlaka ya hii sayari yetu na tunamuonglea yeye kisha kuwashurutisha watu hawa kutobu. Wakati atakapokuja Masihi akifikia juu ya mlima wa Mizeituni tutakuwa pamoja naye (tazama jarida la Baragumu [136], ili kupata maelezo zaidi kuhusu kurudi kwa Masihi). Siku ya Upatanisho inahusu katika kuipatanisha hii sayari yetu na Mungu; ili kuileta hii sayari kwenye toba na kuiandaa kwa ajili ya kipindi cha Milenia. Kuna mlolongo wa mambo katika nyakati kati ya ujio wa Kristo na mwanzo wa zama za Milenia na kile kinachotoka kwenye kikombe cha hasira ya Mungu.

 

Ufunuo wa Yohana 16:1-21 inasema: Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi. 2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, na wale wenye kusujudia sanamu yake. 

 

Watu hawa watawatesa wateule. Watahukumiwa kwa ajili hii, lakini ni kwa kipindi kifupi tu cha maisha kama Kristo atakavyo ushughulikia mfumo wa dunia wa ibada za sanamu. Atauvunjilia mbali. Hili si suala tu la kuwaadhibu watu hawa. Ni suala la kuwaleta watu kwenye mahali ambapo Mungu anaweza kugeuza nia zao ili wapende kuelekea kwenye kipindi cha Milenia. Baadhi ya watu kwa kufikia hadi kwenye hatua kipindi hiki cha muda hakiwezi kuhusishwa katika hali iliyopo. Mfano wa siku za mwisho imeonyeshwa katika habari zihusuzo Sodoma na Gomora, ambapo mtazamo wa nia zao yalionekana kana kwamba Mungu alikusudia kuwaua. Kuangamia kwa Sodoma kulifanywa na malaika akitekeleza maelekezo kutoka kwa Kristo kwa wakati ule, na Lutu akachukuliwa nje ya ule mji.

 

Sababu iliyo mfanya mke wa Lutu ageuke jiwe la chumvi ilikuwa ni alikiuka masharti ya mfumo ambao kwayo Mungu alimtoa nje ya ule mji. Hii ilifanyika ili iwe mfano wenye kutuonya sisi. Mke wa Lutu aliangamia ili kwamba tuweze kujua kwamba sisi hatuwezi kuchukua kitu chochote kutoka kwenye mfumo huu kwenye Milenia. Sababu ni kwamba kila nusu mfumo na kila sehemu ya nusu mifumo ya mifumo tulionao sasa ni maovu ya kiurithi, katika kila eneo lake.

 

Ndiyo maana mfumo wa milenia utafanywa kwa kufuata sheria za Musa kikamilifu. Sheria za Musa alipewa musa na sisi kwa pamoja na Kristo. Tunakwenda kuweka mfumo aliopewa Musa azifanyie kazi.

 

Maandiko yanaendelea kusema: 2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, na wale wenye kusujudia sanamu yake. 

 

Machukizo na uovu yazidiyo yote ni wazo la kimwili na kiroho. Tukiiga mfumo wa kimungu, tunaigiza mlolongo wa matatizo. Mtazamo wa kimwili ungehusiana na usomaji wa ya alama ya vimelea uenezaji wa matatizo yanayo husiana na ukweli huu. Alama ya vimelea huenda zikagongwa kwenye mikono na kwenye sehemu ya mbele kwa ajili ya kuwamiliki umati, nk. Ukweli ule ule wa kuwepo kwa mfumo wa kidunia utasababisha maumivu haya. Vitu hivi sio kwamba Mungu anatoa hukumu kwao, lakini ni kudhoofisha moja kwa moja matatizo yatokanayo na matendo yao. Kila tunachokifanya kina matokeo yake.

 

Wakati wa vita umuhimu wa ulinzi utaongezeka na matatizo yataenda sambamba na hali hii.

Maandiko yanaendelea kusema: 3 Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya katika bahari vikafa.

 

Kila chenye uhai kitakufa. Wameitwa ili kufanya toba chini ya mashahidi mahali ambapo theluthi moja watakufa, lakini kwa jambo hili wataangamiza bahari. Wataangamiza kila kitu.

 

Maandiko yanasema: 4 Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji, zikawa damu. 5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi; 6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, wewe umewapa damu wainywe; nao wamestahili.

 

Hakutakuwa na maji safi mazuri hapa kwenye hii sayari. Kwenye ya mhuri ya nne robo watakufa kwa baa la njaa na magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza kama tauni na mengine. Kwenye vita baragumu ya sita theluthi moja ya watu watakaokuwepo duniani watakufa. Sasa tunaenda hadi kwenye hatua ya kuwa zaidi ya nusu ya sayari imekufa kabla hayajaanza mafuatano ya matukio haya. Kiasi cha watu bilioni mbili watakufa kwa ajili ya ghadhabu ya hasira ya Mungu. Tunaona maangamizi ya dunia.

 

Maandiko yanaendelea kusema: 7 Nikasikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni zakweli, na za haki, hukumu zako. 8 Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto. 9 Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.   

 

Mungu anauweza juu ya tauni. Anaweza kuikomesha hii kwa kitambo kimoja. Kwa nini tuiache nusu ya hii sayari ife? Tunachotakiwa kufanya ni kutubu. Hakuna anayesema Nimekosea na kufanya vibaya, tafadhali Bwana nionyeshe njia. Hatuhitaji kuona nusu ya sayari ikifa kabla ya kufikia toba. Tunaweza kumuona Mungu akishughulika nasi sasa. Kwa nini hawawezi kuona hili tena baadae? Watu hawa baada ya haya yote yaweza bado hudhani wanaweza kulazimisha maneno kwa Mungu.

 

Maandiko yanasema: 10 Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu, 11 wakamtukana mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao.

 

Sisi tuko Yerusalemu kawa viumbe wa kiroho chini ya ulinzi wa Kristo, tukishughulika na hili wakati inapokuwa inatokea. Tunashughulika na sayari hii ya dunia mkono kwa mkono na Kristo.

 

Maandiko yanasema: 12 Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili nia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.

 

Sayari yetu hii inavunjika. Wafalme wa Mashariki na Anatoli Heliou, au Wafalme wa jua lichomozalo ambao watakuja kupitia mto Frati. Jeshi kubwa sana kutoka mashariki wataingia Israeli na kuelekea mjini Yerusalemu.

 

Maandiko yanasema: 13 Nikaona roho tatu za uchafu, zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaona aibu yake). 16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa kiebrania Har-Magedoni.

 

Baragumu hii ya malaika wa sita inaonekana kuwa ujio wa Masihi kunahusiana na kukauka kwa mto Frati, na kwamba Masihi hatakuja hadi wakati huu. Inatokea kuwa Masihi atakuja Yerusalemu na hatimaye kuhusishwa na wakati wa muda wa malaika wa sita.

 

Baragumu ya Saba

 

Maandiko yanasema: 17 na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. 18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu mwanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokubwa tetemeko hilo. 19 Na mji ule ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo wa ghadhabu ya hasira yake. 20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.   

 

Tetemeko hili la ardhi pia ni kubwa sana kuliko lile tetemeko la ardhi lenye maana ya kutiliza unabii wa ishara za mbinguni kwenye ule mhuri ya sita. Tatizo linakuwepo kwa kadiri mihuri inavyoendelea. Muhuri ya sita ilitoa onyo kwa dunia kuhusu ujio wa Masihi na hasira ya Mungu, lakini tena hawakutubu. Tendo hili la mwisho linaharibu mfumo mzima wa dini za uongo na matendo ya Shetani hapa kwenye sayari yetu.

 

Kuna muhutasari wa elimu-dhana iliyotiwa ikaweko na watawa wa Kanisa Katoliki la Rumi wa kipindi cha miaka ya kati ya 1100-1600 kijulikanacho kama kipindi cha medieval (inayodhaniwa kuanzishwa na Ticonius, aliyedhaniwa kuwa ni muumini wa mafundisho ya Kidonati, aliyemshawishi Augustine). Mafundisho haya kusema kuwa baragumu na vitasa hivi vya ghadhabu ni marudio tu ya maelezo yaliyo kama dhana tu.

 

Ni dhana isiyo kubalika kabisa, ingawaje kuna baadhi ya mambo ya msingi yanayoridhia kwa yale liyoyasema Kristo kwa sehemu zote mbili yaani kwenye mhuri ya sita na kwenye baragumu ya sita isemayo “Tazama naja”. Neno hili limewekwa katika mabano katika mwishoni mwa Aya ya 15. Wazo halisi hapa ni kwamba pengine ni kwamba mambo haya yanaendelezwa na kufanyizwa kwa mwelekeo endelevu ili kwamba mito igeuke na kuwa damu, na kirahisi iweze kuwa vibaya zaidi kama inavyotangulia hadi hatimaye Kristo awe anashughulika na sayari yote. Hii ni sehemu na haitaweza kuelekezwa kikamilifu katika jarida hili. Kuna umuhimu katika hili. Kile kinachowezekana ni kwamba kuna ujio wake na halafu watu watajipanga ili kupigana naye pale mjini Yerusalemu, na kuwa itaongeza matokeo wake.

 

Mwandamano wa hizi baragumu n mihuri kwa maana ya kufanya mito kuwa damu kumewekwa tayari kwenye dhana. Mawimbi mekundu nk, tayari yamesha kuwepo baharini. Yamesha anza tayari kuwepo. Hayaja ua bado theluthi moja ya mito na theluthi ya samaki walio hai, ila yamesha anza. Kitu ambacho Biblia inakiweka ni kwamba, mchakato huu unaendelea na kwamba kila moja wapo ya baragumu ni matokeo ya matendo ya zamani.

 

Hatima yake ni kwamba Kristo atashughulika na kila mtu. Baada ya Kristo kuichukua hii sayari kwa zile baragumu na kumimina vile vitasa kisha atakuwa tayari kwa ajili ya ile vita vita kuu ya Mungu Mwenyezi. Vita hii ni ya Ezekieli katika muhuri ya sita. Hatuta shughulika na unabii wa Ezekieli hapa.

 

 

Ufunuo wa Yohana 16:12-16 inaelezea vita vya Har-magedoni au vita vya nabii Ezekieli. Pia kuna rejea zinazofanana kwenye kitabu cha Luka 19:27.

 

Luka 19:27 inasema: Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu. 

 

Hii sio maelezo ya mwisho. Msitari huu mmoja ni vita vizima vya Har-magedoni. Mataifa yatashushwa chini na kuchinjwa mbale ya Kristo kwenye hivi vita hivi.

 

Maandiko yanasema: 17 na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. 18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu mwanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokubwa tetemeko hilo. 19 Na mji ule ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo wa ghadhabu ya hasira yake. 20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.   21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe, kwa maana pigo lake ni kubwa mno.

 

Mfumo huu wa kidini ya dunia hatimaye utaharibiwa na kuangamizwa. Makanisa mengi ya ya Wakristo wa kweli yata angamizwa na huyu mnyama. Hivi ndivyo hizi Sura za hizi za 17 na 18 zinavyosema. Hii ni ngumu na itafafanuliwa katika siku zijazo

 

q