Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[142]
Kwanguka Kwa Yeriko
(Toleo la 3.0 19951109-20000710-20091018)
Masomo haya yanahusu athari za unabii za kwanguka
kwa Yeriko na kuelezea jinsi mlolongo wa
mihuri saba na tarumbeta pamoja na bakuli za gadhabu ya Mungu inavyojitokeza
katika hadithi ya Yeriko. Umuhimu wa hadithi ya Rahabu imeonekana ikidhihirisha
kuongoka kwa watu wa mataifa na kulenga Masihi kama mtawala wa mataifa.
Christian
Churches of God
Barua pepe: secretary@ccg.org
(Hati miliki © 1995, 2000, 2009 Wade
Cox)
(Toleo. 2012)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Kunazo jumbe nyingi ambazo uibua na kuelekeza nyumbani hadithi ya kurejeshwa kwa kipindi cha miaka alfu moja (millenia). Kunazo sehemu nyingi za bibilia zinazo lenga hadithi hii. Ni mwafaka tukianzia na Uasisi wa Israeli. Kitabu cha Yoshua- sura ya 1, mstari wa 1 kinahusiana na kazi ya Israeli. Yoshua mwana wa Nuni ina maana kusaliwa kwa ukombozi kupitia kwa njia ya uvumilivu-yoshua (ama Yehoshua) lilikuwa ni jina la Kristo. Kunayo pia uwiano Katika kitabu cha Ufunuo na kile cha Yoshua pia, kwanguka kwa Yeriko. Kuna mafundisho ya kiroho Katika somo hili na, pia ni ishara kwa yale yatakayotokea Katika siku za mwisho, yalivyonukuliwa moja kwa moja kutoka kitabu cha Yoshua na kwanguka kwa Yeriko. Mengi kwayo hayajaeleweka vyema, sababu mafundisho hayajafunuliwa kikamilifu na, ni natumaini yangu kuwa, katika maelezo haya ambayo yame tajua kikamilifu, tunaweza kufichua na, tupate ufahamu fulani vile Mungu anaenda kuasisi matengenezo ya siku za mwisho, au baadhi ya Nyanja mbalimbali. Tunaanzia Yoshua1:1.
Yoshua 1:1 Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, (Biblia takatifu BT)
Tuna dhana mbili pale, Musa alikufa kama mtumishi wa Bwana. Kristo alikufa kama Mwana wa Mungu. Hivyo tulikuwa na jibuko mbili, hadhi ya mwana ikiwa kubwa kuliko ile ya mtumishi.Yoshua alikuwa mtumishi wa Musa.
Yoshua 1:2-3 Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli. 3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.
Hii ni baada ya maombolezo kwa siku thelathini, kwa ajili ya Musa, vile tunavyoelewa toka hapo awali, kutoka vitabu vya sheria. Musa hakuruhusiwa kuingia nchi ya ahadi. Mfumo wake ulikatisha ahadi hile naye mrithi wake alichukua Israeli Katika awamu nyingine. Huu ni mfano wa Masihi na mfumo wa Roho Mtakatifu kuwaelekeza Israeli katika awamu nyingine
Yoshua
1:4 Tangu jangwa hili na mlima huu,
Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka
bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.
(Biblia Takatifu BT.)
Si Israeli ya sasa tunayotazamia. Ardhi waliopewa Israeli limepitisha juu hadi Yufirati, katikati sambamba kwenda ziwa la magharibi na, jini hadi Misri.
Yoshua 1:5 Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako
siku zote za maisha yako;
Hii ni ahadi Mungu alifanya kwa Yoshua. Mpangilio ni kuwa Makamanda wa Israeli wamekabidhiwa hile ahadi, na wakitembea na Bwana, Bwana hatawapungukia wala kuwaacha, na Israeli itasimama. Hakuna taifa litainuka kinyume chake, Wakiwa wanatii sheria za Mungu. Hiyo ni ahadi ya mungu na jinsi ilivyo. Tukisiaja sheria za mungu, Mataifa yanaruhusiwa kututangulia na kutulazimishia sheria.
Yoshua 1:6-7 Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. 7 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. (Biblia Takatifu BT.)
Kuna ile dhana. Tunza sheria na tutafanikiwa. Tusipotunza sheria, tutashindwa. Yote haya yanapatikana Katika kumbumbu la Torati 28, baraka na laana. Ni muhimu kuelewa baraka na laana.
Mafundisho ya Biblia katika Kumbukumbu la
Torati.28 ni muhimu (Taz. Baraka na Laana (Nam.
75)). [The Blessings and the Curses
(No. 75)] Ahadi zote hizi zimefanywa ili taifa
lifanyike kichwa wala mkia. Taifa litakuwa mtaji na
wala si mkopaji. Tusipotunza sheria, tutawekwa chini ya mataifa mengine, na
tutakuwa wakopaji,na hicho ndicho kitakachofanyika kwa
watu wetu. Marekani ni inchi yenye madeni makubwa vile
haijawahi shuudiwa ulimwenguni.
Joshua 1:8-9 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. 9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako. (Biblia Takatifu BT.)
Kuwa hodari na moyo wa ushujaa limerejerelewa mara ya pili kwenye mistari michache Katika biblia. Ahadi ni kwamba tukitunza sheria, kutawekwa vikozi vya maelfu vitani. Kama hatutatunza sheria, moja wao maelfu kati yetu kupigana. Ndio aina ya ahadi awapao watu wake kama taifa. Wateule wamo Katika mataifa mengi na jukumu letu ni kuwaombea na kuwaimarisha, lakini watafanikiwa watakapo mcha Mungu na kutunza sheria wao wenyewe.
Tumefikia hatua ambapo lolote kwa hayo hayatatokea kwetu tena hadi pale ufufuo utakapofutiana kutakazua kwetu kupitia kwa njia ya moto.
Yoshua 1:10-15 Ndipo Yoshua akawaamuru maakida wa watu, akisema, 11 Piteni katikati ya matuo, mkawaamuru hao watu, mkisema, Fanyeni tayari vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wenu, mpate kuimiliki. 12 Tena Yoshua akawaambia Wareubeni, na Wagadi, na hao wa nusu ya kabila ya Manase, akasema, 13 Likumbukeni neno lile alilowaamuru Musa mtumishi wa Bwana, akisema, Bwana, Mungu wenu, anawapa ninyi raha, naye atawapa nchi hii. 14 Wake zenu, na watoto wenu, na makundi yenu, watakaa katika nchi aliyowapa Musa ng'ambo ya Yordani; bali ninyi mtavuka mbele ya ndugu zenu, hali mmevikwa silaha zenu, watu wote wenye nguvu, na ushujaa, ili mpate kuwasaidia; 15 hata Bwana atakapowapa ndugu zenu raha, kama alivyowapa ninyi, na wao pia wamepata kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa Bwana aliwapeni ng'ambo ya Yordani upande wa maawio ya jua.(Biblia Takatifu)
Dhana hii ni moja
kuwa Israeli si pekee watarithi taifa nzima la Israeli. Ardhi iliyo mashariki
mwa Yorodani pia ni sehemu ya urithi. Swala hili halijawai kueleweka vizuri. Tukirejerelea mfumo
wa kipindi cha miaka elfu moja, tutakuwa na mashamba yaliyo inje ya Israeli
kupeanwa kama urithi, na makabila ya Manasse na Rubeni na Gadi,(na pia Dani
Efuraimu)watatuaa ardhi maalum mashariki mwa Israeli.
Kwa kiasi cha ardhi, hakuna anayejua. Kunayo, hata hivyo ahadi iliyotolewa.
Yoshua 1:16-18 Wakamjibu Yoshua, wakasema, Hayo
yote uliyotuamuru tutayafanya, na kila mahali utakakotutuma
tutakwenda. 17 Kama vile tulivyomsikiliza Musa katika mambo
yote, ndivyo tutakavyokusikiliza wewe; Bwana, Mungu wako, na awe pamoja nawe tu, kama alivyokuwa pamoja na Musa. 18 Kila mtu atakayeiasi amri yako, asiyasikilize maneno
yako katika mambo yote utakayomwamuru, atauawa. Uwe hodari na moyo wa
ushujaa,
Utiifu kwa
kiongozi wa kitaifa ulikuwa wa maana
Joshua 2:1 Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko. (Biblia Takatifu BT)
Mbona haswa Yeriko? Sababu hapo ndipo mfumo ungeshugulikiwa. Yeriko
kama tunavyofahamu sasa, ilikuwa na kazi kabla ya
uwajibikaji wa kibiblia wa kuumbwa kwa Adamu .Imekuwa na shughuli karibu kutoka
7000 KY kuendelea. Hii haishughulikii nasaba na koo katika Biblia. Ina maana kuwa,
kulikuwa na uumbaji mwingine uliokuwa unaendelea
katika Yeriko (pengine kuendelea hadi gharika). Jina la Yeriko lamaanisha jiji
la mwezi, na kwamba inaokena kuwa ni la muhimu pia. Mwezi
ulikuwa mfano wa kiume katika Mashariki ya Kati kwenye
mfumo wa Kiarabu. Jua lilikuwa ni mfumo wa kike, na sifa
za mfumo wa kishetani zilielekezwa kwa mwezi, na sio kwa jua. Ibada ya Baali ni sehemu moja baadaye, lakini katika mfumo huu, mwezi pia, ulikuwa
ni kituo cha ibada (katika masomo, Ufufuo wa wafu (Nam. 143)). [The Resurrection of the Dead (No. 143)]
Wayaudi watajaribu kwa vyovyote kutuelezea
kuwa kwa kweli Rahabu hakuwa msherati.Ukweli wa mambo ni kuwa Rahabu alikuwa
kahaba Sababu kubwa ya wao kujaribu kwa maumivu kuangazia
ukweli wao kuwa Rahabu hakuwa msherati, ni kwamba ufalme nzima wa Israeli ni
tegemezi juu ya uzao wa Rahabu, na Kristo moja kwa hivyo ni mzaliwa wa ukoo wa
Raabu. Kwa hivyo Masihi ni mzaliwa wa moja kwa moja wa
ukoo wa kahaba, ambaye si Mwisraeli. Sasa hii ni
muhimu (Taz pia nakala hii Ukoo wa masihi (Nam.
119). Genealogy of the Messiah (No. 119)]
Shida yenyewe ulikuwa ni ule usherati wa Hekalu uliokuwa wa kawaida katika jamii nyakati zile. Kila mwanamke, katika kipindi chake cha utumishi wa Hekalu alikifanya cha ibada ya sanamu-mfumo wa miungu ya kike ya Asterothi au Astarite au pasaka ulikuwa na muundo mzima wa makahaba wa hekalu na hilo liliendelea mpaka wakati wa Kristo kusema. Katika Korinto, wakati wa kanisa katika Hekalu moja tu kulikuwa na makahaba 1000 waliosajilishwa kwa ukahaba. Kila mmoja aliusika katika hilo na watu walikuwa wanaitwa kukimbia mfumo huu na waingie Kanisani.
Rahabu alikuwa anashria mbele kwa ukombozi wa watu wa mataifa na ukombozi wa watu waliousika kwa kuwaleta ndani kutoka dhambini na kuwafikisha Israeli wakipatiswa na kutakazwa. Rahabu alikuwa babu wa Yesu Kristo na Mfalme Daudi. Kwa ukoo wake tulionyeshwa kuwa kutoka mwanzo ukombozi ulielekezwa kwa watu wa mataifa. Vilevile, msamaha kupaanuliwa kupitia kwa Roho mtakatifu.
Yoshua 2:2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi. (Biblia Takatifu BT)
Dhana hii ya kuwatuma watu wawili inahusu mashaihidi, na inahusisha dhana nzima ya mfumo wa Kanisa la Masihi. Tumetumwa wawili kwa wawili kukumbana na tabaka mbalimabli na miji, ili kuipeleleza. Tupo pale kuwatumia wanyonge, au watu wale ambao wamekabidhiwa ukombozi. Rahabu alipewa nafasi kuwa mshirika wa Israeli na kuokolewa chini ya ule mfumo, na tutaona ni vipi na ni kwa nini. Mara tutakapofahamu kilichotokea kwa Rahabu tutafahamu passaka na ukombozi ni kwa watu wa mataifa.
Yudah wangefahamu ukombozi kutoka kwa mataifa tu baada ya kumbukumbu la torati na ni kitabu
cha yoshua.
Yoshua 2:3-5 Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi. 4 Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka; 5 ikawa kama wakati wa kufungwa lango la mji, kulipokuwa giza, watu wale wakatoka, wala sijui walikokwenda; wafuateni upesi, maana mtawapata. (Biblia Takatifu BT)
Huyu mwanamke alijitayarisha kuficha watumishi wa Mungu aliyehai na alikuwa tiyare kukutana na adhabu ya Mungu wake mwenyewe, mfumo wake wa kisiasa na jeshi pia sifa, ili kuwalinda watumishi wa Mungu. Hilo ni takwa kwetu. Tunapaswa kuelekeza msahada wetu kwa watu wale wanatusaidia. Tunaitajika kuelekeza ukombozi, na kupanua maisha kwa njia ya ufahamu.
Yoshua 2:6-7 Lakini yeye alikuwa amewapandisha darini, akawaficha kwa mabua ya kitani, aliyokuwa ameyatandika juu ya dari. 7 Basi hao watu wakawafuata kwa njia iendayo Yordani mpaka vivukoni; na mara wale watu waliowafuatia walipokwisha kutoka, wakalifunga lango. (Biblia Takatifu BT)
Mfumo wa kifiduli ni wa kawaida wa mji, pale ambapo walifunga milango na kushindilia nyakati za usiku kwa kwogopa ufamizi. Hiyo ndio iliokuwa ulinzi nyakati zile.
Yoshua 2:8-10 Tena kabla hawajalala akawaendea juu darini, 9 akawaambia wale wanaume, Mimi najua ya kuwa Bwana amewapa ninyi nchi hii, na ya kuwa hofu imetuangukia mbele yenu, na ya kuwa wenyeji wote wa nchi wanayeyuka mbele yenu. 10 Maana tumesikia jinsi Bwana alivyoyakausha maji ya bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa huko ng'ambo ya Yordani, yaani, Sihoni na Ogu, mliowaangamiza kabisa. (Biblia Takatifu BT)
Waliamriwa kabisa kwangamiza sihoni na ogi, na watu walio katika sehemu tambalale (watu
waliousika na Nephilimu (Taz nakala
hii Nepthilim (Nam.
154)). [The Nephilim (No. 154)]
Yoshua 2:11-14 Na mara tuliposikia hayo mioyo
yetu iliyeyuka, wala haukusalia ujasiri wo wote katika mtu awaye yote, kwa
sababu yenu; kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, katika mbingu juu na
katika nchi chini.
12 Basi sasa, nawasihi, niapieni
kwa Bwana, kwa kuwa nimewatendea ihisani, ya kwamba ninyi nanyi mtaitendea
ihisani nyumba ya baba yangu; tena nipeni alama ya uaminifu; 13 ya kwamba mtawaponya hai baba yangu na mama yangu, na ndugu zangu
wanaume na wanawake, na vitu vyote walivyo navyo, na kutuokoa roho zetu na
kufa. 14 Wale wanaume wakamwambia, Uhai
wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha
itakuwa, wakati Bwana atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa
ihisani na uaminifu. (Biblia Takatifu BT.)
Rahabu alitambua kuwa Mungu wa Israeli ni Mungu. Ndiposa akawambia watu wake kwanza
tufahamu Mungu pekee wa kweli ili waende Israeli na
kufanyika kuwa baadhi ya wateule. Rahabu alichukuwa hatua ya kwanza kwa kumfahamu Mungu pekee wa kweli. Ndipo sasa alipata uwezo
wa kushugulikia mashaidi, kuwalinda na pale akifahamu
kuwa alitelekeleza kusudi la Mbinguni pamoja na kuwa angepata hifadhi sababu
aliwashughulikia watumishi wa Mungu aliye hai. Rahabu alipewa ufahamu kupitia kwa Roho Mtakatifu, kuwa Israeli watachukuwa nchi, na alitaka
waweze kuingia kwa agano nao.
Mtawanyiko unapatikana katika mafumbo ya kondoo na mbuzi, katika kitabu cha Matayo. Fumbo la kondoo na mbuzi ni kuhusu wale wanao watendea wateule ukalimu. Watatunukiwa na kuwekwa katika mkono wa kulia wa Mungu, na wale wasio watendea wateule ukalimu watawekwa katika mkono wa kushoto na kuangamizwa kama mbuzi. Hili fumbo halilengi kanisa, ni fumbo linalolenga mataifa ili mataifa wa fahamu kuwa wanahukumiwa vilevile wanavyotutendea.
Joshua 2:15-19 Ndipo akawashusha kwa kamba dirishani, maana nyumba yake ilikuwa katika ukuta wa mji; naye alikaa ukutani. 16 Akawaambia, Enendeni zenu mlimani, wale wanaowafuatia wasije wakawapata; mkajifiche huko siku tatu hata wao wanaowafuatia watakaporudi; kisha enendeni zenu. 17 Wale wanaume wakamwambia, Sisi tunataka tusiwe na hatia kwa ajili ya kiapo hiki ulichotuapisha. 18 Angalia, tutakapoingia katika nchi hii, funga kamba hii nyekundu katika dirisha hili ulilotutelemshia; nawe uwakusanye kwako nyumbani mwako, baba yako, na mama yako, na ndugu zako, na watu wote wa nyumba ya baba yako. 19 Itakuwa mtu awaye yote atakayetoka katika mlango wa nyumba yako kwenda njiani, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe, na sisi tutakuwa hatuna hatia; na mtu atakayekuwa ndani ya nyumba yako damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu, mkono wa mtu ukimpata. (Biblia Takatifu BT.)
Kuweka alama kwa Rahabu ni sawa na ule mfumo wa passaka. Kamba nyekundu ziliwekwa dirishani, vile damu ya passaka ilipakwa kwenye milango.
Alama hizi zilikuwa mfano kuwa agano limeafikiwa kati ya Isiraeli na mtu wa mataifa, au kuwa nyumba hii imejumuishwa ndani ya taifa la Israeli na maelekezo yalikuwa kwamba wangepaki ndani ya nyumba zao ilivyokuwa pia katika passaka. Hawakutoka nche ya nyumba zao. Na kama wangetoka nche ya nyumba zao, ni lazima damu ingekuwa vichwani vile ilivyokuwa katika njia za mji wa Misiri wakati Malaika wa mauti alipopita juu ya Israeli. Ndio ulikuwa umuhimu wa vitambaa vyekundu kwenye madirisha ya nyumba ya Rahabu. Inaonyesha pale kuwa, mkombozi uliruhusiwa kwa watu wa mataifa. Hiyo ni dalili ya kwanza, kwamba mataifa watatuzua familia ambazo zitaletwa ndani ya Israeli na kulindwa chini ya damu ya Agano la Kale na rehema ya Kristo inayoitajika katika Agano Jipya.
Yoshua 2:20-21 Lakini wewe ukitangaza habari yetu hii, ndipo tutakuwa hatuna hatia, katika kiapo hiki ulichotuapisha. 21 Naye akasema, Na iwe hivyo kama yalivyo maneno yenu. Akawatoa, nao wakaenda zao; naye akaifunga ile kamba nyekundu dirishani. (Biblia Takatifu BT)
Waliitajika kutunza imani. Haikuwa huduma ya kunena, na tena kubandilisha muungano wao. Mwanamke huyu alipaswa kutunza imani ili kudumisha agano. Kauli hii ina maana tunapaswa kutunza imani ili kudumu katika Israeli ya kiroho na tunapaswa kutunza agano pia, Tuzipotunza agano, agano kati yetu ufunjika.
Yoshua 2:22-23 Watu hao wakaenda, wakafika mlimani, wakakaa huko siku tatu, hata wale waliowafuatia walipokuwa wamerudi; na wale waliowafuatia wakawafuatia katika njia ile yote, lakini hawakuwaona. 23 Kisha wale watu wakarudi, wakatelemka mlimani, wakavuka, wakamwendea Yoshua, mwana wa Nuni, nao wakamwambia habari za mambo yote yaliyowapata. (Biblia Takatifu BT)
Siku tatu kujificha milimani pia ni muhimu. Inatumika kwa dhana za dhadhari za kwanza. Siku tatu inatuonyesha dhana ya mavuno ya Israeli na Yuda ambapo katika siku ya tatu ukombozi wetu unafufuliwa (Hosea.6:1-20) inatumika pia katika wakati wa mashahidi wakiwekwa katika mitaa, kisha vitendo vitakavyofuata.
Yoshua 2:24 Wakamwambia Yoshua, Hakika Bwana ameitia nchi yote katika mikono yetu; tena zaidi ya hayo wenyeji wa nchi wanayeyuka mbele yetu. (Biblia Takatifu BT.)
Yoshua 3:1-4 Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao wakatoka Shitimu, wakafika mto wa Yordani, yeye na wana wa Israeli wote, wakakaa hapo kabla ya kuvuka. 2 Ikawa baada ya siku tatu, maakida wakapita katikati ya marago, 3 wakawaamuru watu wote wakisema, Mtakapoliona sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, na makuhani Walawi wakilichukua, ndipo mtakapoondoka hapa mlipo na kulifuata. 4 Lakini, na iwe nafasi kati ya ninyi na lile sanduku, kama dhiraa elfu mbili kiasi chake; msilikaribie mpate kuijua njia ambayo hamna budi kuiendea; kwa maana hamjapita njia hii bado. (Biblia Takatifu BT.)
Tunakumbana na dhana kuwa Sanduku. Ambalo kweli lilikuwa nguvu za Mungu lingeenda mbaee na kuitiisha nchi, na hiyo ndiyo ilikuwa nguvu ya Israeli. Siku tatu ziliwakilisha miaka tatu, ambayo ilionyesha utakaso wa Israeli katika siku za mwisho. Baada ya miaka mitatu Mungu alifufua ukombozi wa Israeli kupitia kwa mfumo wake, uliofananishwa na zanduku la angano.
Umbali unaonekana kama safari ya siku ya sabato. Unuo wa uwepo wa kimbingu (Shekina) utaodhiirisha njia katika siku za mwisho.
Yoshua 3:5-13 Yoshua akawaambia watu, Jitakaseni; maana kesho Bwana atatenda mambo ya ajabu kati yenu. 6 Kisha Yoshua akawaambia makuhani, akasema, Liinueni sanduku la agano, mkavuke mbele ya hao watu. Wakaliinua sanduku la agano, wakatangulia mbele ya watu. 7 Bwana akamwambia Yoshua, Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote, wapate kujua ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wewe, kama nilivyokuwa pamoja na Musa. 8 Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la agano, ukawaambie, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani. 9 Basi Yoshua akawaambia wana wa Israeli, Njoni huku, mkayasikie maneno ya Bwana, Mungu wenu. 10 Yoshua akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa hatakosa kuwatoa mbele yenu Mkanaani, na Mhiti, na Mhivi, na Mperizi, na Mgirgashi, na Mwamori, na Myebusi. 11 Tazama, sanduku la agano la Bwana wa dunia yote linavuka mbele yenu na kuingia Yordani. 12 Basi sasa twaeni watu kumi na wawili katika kabila za Israeli, kila kabila mtu mmoja. 13 Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la Bwana, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yatatindika, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama chuguu. (Biblia Takatifu BT.)
Hii ni muujisa wa bili wa kufuka maji, ili kutuaa nchi ya ahadi. Tulitoka misiri, kupitia bahaari nyekundu chini ya Masihi, iliyo dhana ya kupitia majini chini ya ulizi wa Mbinguni kufika nchi kafu, mabayo ni mfano wa kuja kwa Masihi na kuanzishua kwa Kanisa nyikani kwa miaka arobaini, ambayo ni mfano wa sherehe arobaini za yubilee, kujumuisha miaka elfu mbili ya siku za mwisho. Awamu ya pili ilikuwa wafuke Yorodani, kupitia majini, ambayo yalitawanyishwa kama ishara ya pili kutokana na uzaidisi wa Musa, aliyechukua uwezo wa uongozi wa Muza. kwa hivyo kuna kurudi kwa Masihi mara ya pili. Hii tena inaashiriwa na vitendo vya Elija na Elisha wakitawanyisha maji ya Yorodani
(2Wafalme 2:14-15)
Yoshua 3:14-15 Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu, 15 basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno), (Biblia Takatifu BT)
Haikuwa tu mchekejo wakati wa mavuno, Yorodani iko kwenye mafuriko. Ndio maana ilikuwa lazima Yoshua kuweza kukusanya maji ya Yorodani katika kusanyiko moja, ili waisraeli wapite. Kuvuna kwa kanisa kunatekelezwa wakati Yorodani imo katika mafuriko; kwa njia nyingine chini ya shida na dhiki (Yeremia 12:5; Ufunuo 12:15-16) Huu ni ufahamu kutokana na msemo huu, kama hautatembea na waume kwa amani utawezaje kukimbia na farasi wakati wa mafuriko ya Yorodani, ni kusema, wakati wa vita vya mavuno ya siku ya Bwana. (Yeremia 12:5 KJV)
Yoshua 3:16-17 ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko. 17 Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.(Biblia Takatifu
BT)
Ni wajibu wa ukuhani kulinda taifa katika kazi kwenye nchi ya ahadi. Walikuwa na kazi maalumu kuleta watu ndani ya Israeli. Ndio kusema, utunzi wao uliitajika kuandaa taifa kuchukuwa uriithi wake. Wateule hawatapokea urithi wao ila kuwe na mtu fulani atakaowafundisha vile watachukuwa uriithi. Lazima tuelewe jinsi ambayo agano limetolewa na lazima tujiandae kwayo, na lazima tuwe tumekua kiasi cha umri fulani ili kutekeleza uamusi. Hizo ni amri za watu wetu. Mtu hatawapa watu urithi wakiwa wajanga pado. Watawekwa chini ya ulinzi mpaka pale watakapokuwa nauwezo wa kutekeleza urithi wao inavyostahili. Ni wajibu wa ukuhani kuwandaa watu kupokea urithi wao. Huo ni mfano kuonyesha ni kwa nini ukuhani ulikuwa na msimamo wa kujitegemea pale Yorodani ndipo wakafuka salama.
Yoshua 4:1-8 Ikawa, hapo hilo taifa zima lilipokuwa limekwisha vuka Yordani, ndipo Bwana akanena na Yoshua, akamwambia, 2 Haya, twaeni watu waume kumi na wawili katika hao watu, kila kabila mtu mmoja, 3 kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende nayo mawe hayo, mkayaweke nchi kambini, hapo mtakapolala usiku huu. 4 Basi Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa amewaweka tayari tangu hapo, katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja; 5 naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la Bwana, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli; 6 ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni nini maana yake mawe haya? 7 Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yalitindika mbele ya sanduku la agano la Bwana; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalitindika; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele. 8 Basi wana wa Israeli walifanya vile vile kama Yoshua alivyowaamuru, nao wakatwaa mawe kumi na mawili pale katikati ya Yordani, kama Bwana alivyomwambia Yoshua, sawasawa na hesabu ya kabila za wana wa Israeli; wakayachukua wakavuka nayo hata mahali pale walipolala, nao wakayaweka nchi kuko huko. (Biblia Takatifu BT)
Hii ni maana ya nguzo kutolewa kati ya makabila ya Israeli kuwahukumu Waisraeli. Nguzo kumi na mbili ambao ni watu walioteuliwa walifanywa mitume, na wakawa waamusi wa Israeli. Waliangaziwa awali katika kitabu cha Waamusi, na Waamusi waliotawala Israeli. kulikuwa na Waamusi kumi na wawili, na mitume kumi na wawili, na wote ao jumla ni takribani ishirini na nne, ambayo wanajumuisha kiasi cha wazee pamoja na Kristo wanaosunguka kiti cha Enzi cha Mungu. (Taz ufunuo sura 4 na 5)
Yoshua 4:9 Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo. (Biblia Takatifu BT)
Kulikuwa na mawe kumi na mbili yaliyowekwa Yorodani na kulikuwa na mawe kumi na mbili yaliyojengwa kama mathabau. Kuna umuhimu katika tukio hilo. Mawe kumi na mbili yaliyowekwa Yorodani yalitumika kama ishara ya mpaka kuenda upande upande na yana uhusiano na nyota kumi na mbili na Jeshi lililoanguka (kutoka DSS na maandiko mengine ya Kiyuda) kuna ishara kwa dhana ya baraza la wazee, na kiasi cha wazee waliojitoa. Yako pale kwonyesha kuwa wale wazee kumi na wawili waliojitoa hawangeingia katika Ufalme wa matengezo
Yoshua 4:10 Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hata mambo yote Bwana aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka. (Biblia Takatifu BT)
Taifa lilivuka makuhani wangali
wanatekeleza kazi yao, na walisuhia maji. Hii ndio muhimu. Kuhani hatashindwa, ama
taifa litakatishwa katik harakati zake za kuingia nchi ya ahadi. Ikiwa
makuhani watashindwa, wadhaifu watashindwa pia kupata urithi wao. Hii ndio sababu ukuhani unaoondolewa
katika nyakati za mwisho na mahala pao kuchukuliwa na
watu wengine (Taz nakala hii: Kupima Hekalu (Nam.137)).
[Measuring the Temple (No. 137)]
Yoshua 4:11-24 Ikawa watu wote walipokuwa wamekwisha vuka kabisa, hilo sanduku la Bwana likavuka, na hao makuhani, mbele ya macho ya hao watu. 12 Na wana wa Reubeni, na wana wa Gadi na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wakavuka, hali ya kuvaa silaha mbele ya wana wa Israeli, kama Musa alivyowaambia; 13 walipata kama watu arobaini elfu hesabu yao, wenye kuvaa silaha tayari kwa vita, waliovuka mbele ya Bwana, waende vitani, hata nchi tambarare za Yeriko. 14 Siku ile Bwana alimtukuza Yoshua mbele ya macho ya Israeli wote; nao wakamcha, kama walivyokuwa wakimcha Musa, siku zote za maisha yake. 15 Kisha Bwana akanena na Yoshua, akamwambia, 16 Haya, uwaamuru makuhani, hao waliolichukua sanduku la ushuhuda, kwamba wakwee juu kutoka mle katika Yordani. 17 Basi Yoshua akawaamuru hao makuhani, akawaambia, Haya, kweeni mtoke Yordani. 18 Ilikuwa, hapo hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana walipokwea juu kutoka mle kati ya Yordani, na nyayo za miguu yao hao makuhani zilipoinuliwa na kutiwa katika nchi kavu, ndipo maji ya Yordani yaliporudi mahali pake, na kujaa na kuipita mipaka yake, kama yalivyokuwa hapo kwanza. 19 Na hao watu wakakwea kutoka Yordani siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi Gilgali, katika mpaka wa mashariki wa Yeriko. 20 Na yale mawe kumi na mawili waliyoyatwaa katikati ya Yordani Yoshua akayasimamisha Gilgali. 21 Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini? 22 Ndipo mtakapowaarifu watoto wenu mkisema, Israeli walivuka mto huu wa Yordani, kwa njia ya nchi kavu. 23 Kwa sababu Bwana, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hata mlipokwisha kuvuka kama Bwana, Mungu wenu, alivyoitenda Bahari ya Shamu, aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka; 24 watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa Bwana, ya kuwa ni mkono wenye uweza, ili wamche Bwana, Mungu wenu, milele. (Biblia Takatifu BT)
Hiyo ilizunguka muujiza wa kufuka. Watu walitoka Yorodani siku ya kumi ya mwezi wa kuanza na wakajenga uko Gilgali mashariki kando ya Yeriko. Siku ya kumi ya mwezi wa kwanza vile tujuavyojua, ni siku ya kutenga kondoo ya passaka. Siku ya kumi ya mwezi wa kwanza ina umuhimu wa kiroho. Ndiyo siku Masihi aliingia Yerusalem kujinchwa.
Mawe kumi na mawili waliootoa Yorodani, Yoshua alijengea pale Gilgali.
Yoshua 5:1 Ikawa, wafalme wa Waamori, waliokaa ng'ambo ya Yordani pande za magharibi, na wafalme wote wa Wakanaani, waliokuwa karibu na bahari, waliposikia jinsi Bwana alivyoyakausha maji ya Yordani mbele ya wana wa Israeli, hata tulipokwisha kuvuka, basi mioyo yao iliyeyuka, wala haikuwamo roho ya nguvu ndani yao tena; kwa ajili ya wana wa Israeli. (Biblia Takatifu BT)
Hii itatokea katika siku za mwisho. Kutakuwa na vijana walio kama simba kote kote katika Israeli.
Yoshua 5:2-8 Wakati huo Bwana akamwambia Yoshua, Haya, jifanyie visu vya mawe ya gumegume, watahiri tena wana wa Israeli mara ya pili. 3 Basi Yoshua akajifanyia visu vya mawe ya gumegume, akawatahiri wana wa Israeli huko Gibea-haaralothi. 4 Na sababu ya Yoshua kutahiri ni hii; watu wote waliotoka Misri, waliokuwa waume, hao watu waume wote waendao vitani walikufa katika bara njiani, baada ya wao kutoka Misri. 5 Kwa kuwa watu wote waliotoka walikuwa wamekwisha kutahiriwa; lakini watu wote waliozaliwa katika bara njiani walipokwisha kutoka Misri, hao hawakutahiriwa. 6 Kwa kuwa wana wa Israeli walitembea muda wa miaka arobaini barani, hata hilo taifa zima, yaani, watu waume waendao vitani, waliotoka Misri, walipokuwa wameangamia; kwa sababu hawakuisikiza sauti ya Bwana; nao ndio Bwana aliowaapia ya kwamba hatawaacha waione hiyo nchi, ambayo Bwana aliwaapia baba zao kwamba atatupa sisi; nchi ijaayo maziwa na asali. 7 Na watoto wao, aliowainua badala yao ndio hao aliowatahiri Yoshua; kwa kuwa wao walikuwa hawakutahiriwa, kwa maana walikuwa hawakuwatahiri njiani. 8 Ilikuwa walipokwisha kutahiriwa taifa zima, wakakaa kila mtu mahali pake maragoni, hata walipopoa. (Biblia Takatifu BT)
Kutahiri kurejeshwa katika siku za mwisho. Kile kisu cha mawe ambacho Yoshua alitahiri israeli kilikuwa mfano wa Mungu ambaye ni kisu anaye tahiri nyoyo za Israeli. Ni dhana kuwa wana wa Israeli jangwani watatahiriwa kiroho na kujiandaa kukabidhiwa uriithi wao. Waisraeli wote watapewa ufahamu. Sisi tu wachache lakini tumeitwa kuwa taifa kubwa. Taifa lisilofahamu chochote. Hawatalizaidia. Tusitamke hivi, “tu heri kuliko wao” na tulikuwa na upunguvu kama wao hapo awali. Wao ni watu wetu na mungu anawapenda kadiri anavyotupenda sisi, walakini ameonelea kutuweka hapa kufanya kazi, ili kutuandaa na kutuinua juu. Taifa lile lote watatairiwa kila mmoja watakapoingia Israeli. wale ambao bado hawajajiandaa ufupi watakufa.
Yoshua 5;9 Bwana akamwambia Yoshua, Siku hii ya leo nimeivingirisha hiyo aibu ya Misri iondoke juu yenu. Kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Gilgali, hata hivi leo. (Biblia Takatifu BT)
Gilgali ina maana kwondolea; kwondoa. Bwana alitumia dhana ya kwondoa kuikemea Misiri. kukabiliana kwa kizazi hiki cha sherehe ya arobaini na mbili ya miaka elfu mbili ya hofu, itaondolewa kutoka kwa watu wetu. Yoshua ambaye ni Masihi aliondoa dhambi za Ulimwengu.
Yoshua 5:10-12 Basi wana wa Israeli wakapanga hema zao huko Gilgali; nao wakala sikukuu ya pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi, jioni, katika nchi tambarare za Yeriko. 11 Nao wakala katika mazao ya nchi siku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya pasaka, mikate isiyotiwa chachu, na bisi, siku iyo hiyo. 12 Ndipo ile mana ikakoma siku ya pili yake, baada ya wao kuyala hayo mazao ya nchi; na hao wana wa Israeli hawakuwa na mana tena; lakini wakala katika viliwa vya nchi ya Kanaani mwaka huo. (Biblia Takatifu BT)
Huo ndio ulikuwa wakati walikula tunda, vile walikula manna. Walilishwa na Mungu ili kuishi na wakaendelea hadi walipokuwa tiyare kupokea urithi wao. Tutalishwa na Bwana kwa miaka elfu mbili. Kila mmoja wetu amelishwa na kutunzwa, na kujitolea nafsi zetu kwa Bwana. Hatutapungukiwa. Mkate wetu na maji ni ya kweli. Kila mmoja wetu ataudumiwa na tutashugulikiwa. Hatutapewa maisha ya kifahari maana sisi si watawala wa Dunia hii. Tutakuwa na muundo wote utakaoshughulikiwa kwa njia hiyo ili tuwe tumejiandaa. Wakati tutatuaa urithi wetu, na kuingia ndani, hapo ndipo tutakula tunda, na taifa lote watakula tunda la mfumo wa kipindi cha miaka elfu moja. Hawajakula bado. Dunia kwa ujumla haijala tunda la Masihi, na la nchi takatifu ya ahadi, (kurejeshwa kwa millennia)
Yoshua 5:13-15 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? 14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? 15 Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo. (Biblia Takatifu BT)
Yoshua akabithiwe anachositahili. Alikuwa jasiri. Mtu angefikiria kuwa mtaro huu ni hofu. Kamanda huyu, kapteni huyu wa kikosi cha Bwana, alikuwa Yesu Kristo Yoshua alijijua na akaanguka chini kifudifudi. Chombo hiki kilinena sawa na vile Malaika wa Agano alinena kwa Mussa. Alikuwa mshirika mmoja, ni yule yule. Aliinamia uwepo wa Mungu, na tukiwa katika uwepo wake, tu katika mbele za Mungu katika ujumbe.
Yoshua 6;1-5 Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. 2 Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. 3 Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita. 4 Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao. 5 Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili. (Biblia Takatifu BT)
Muzunguko wa Yeriko unawakilisha mihuri saba na tarumbeta saba na bakuli saba za ghahabu ya Mungu ya ufunuo wa siku za mwisho. Kila mmoja anasunguka kwa mpangilio, na katika siku za mwisho kuna ishara saba. Mwisho wa sauti kubwa ya mkuu wa Malaika ambayo tutasikia ikiangusa kuta za Jiji na mifumo ya dunia na kunyakuliwa kwa Ulimwengu. Itaporomosha chini uwezo wa Shetani. Huo ndio mfano wa Yeriko. Inaushisha moja kwa moja kwa ishara saba, tarumbeta saba, na bakuli saba za ghahabu ya Mungu.
Yoshua 6:6-7 Bali Yoshua, mwana wa Nuni, akawaita makuhani, akawaambia, Lichukueni sanduku la agano, tena makuhani saba na wachukue tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana. 7 Naye akawaambia watu, Piteni mbele, mkauzunguke mji, na hao watu wenye silaha na watangulie mbele ya sanduku la Bwana. (Biblia Takatifu BT)
Makuhani saba, walio na tarumbeta saba za pembe za kondoo wakiume wanawakilisha malaika saba ambao wamekabidhiwa tarumbeta saba kupuliza. Kunao pia malaika saba wa kanisa saba za mifumo ya Ulimwengu. Malaika saba wataibua kanisa saba kwa miaka elfu mbili, ili kutuandaa kutuaa mfumo wa mwisho. Watu wa Mungu wote wanaletwa nche chini ya Malaika wa kanisa saba. Vilevile kunao wachugaji na wsimamizi nane (au wafalme wa) wanaume walio inuliwa kufanya hiyo kazi (Mika 5:5). Mpangilio huu unatekelezwa pamoja na mchakato wa masihi vile Mika 5:1-4 inavyonena kuhusu Masishi na kwendelea hadi amani ya millennia kutoka 5:5ff. Amani hii ufuata vita vya waasiria ndio kusema inaangazia utawala wa kazi kazini na mifumo ya Kibabuloni ya siku za mwisho. Hapa tunaona simba jibukizi wa Yakobo kati ya mataifa. Mifumo ya uongo ya Yakobo itaharibiwa, pia ya mataifa (Mika 5:9-14)
Yoshua 6:8-9 Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale makuhani saba, wenye kuzichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele za Bwana, wakatangulia, wakazipiga hizo tarumbeta; nalo sanduku la agano la Bwana likawafuata. 9 Wale watu wenye silaha walikwenda mbele ya hao makuhani waliozipiga tarumbeta, na wale waliokuwa nyuma wakalifuata hilo sanduku; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda. (Biblia Takatifu BT)
Zanduku la Aguno ni nini? Kimsingi kulikuwa na vitu vingi ndani yake vikiwemo bao za sheria, fimbo ya Aron pamoja na manna.
Katika kutajua kwa mara ya mwisho kwa zanduku la Agano kulikuwa tu bao za sheria.
Katika hatua hii kulikuwa na ukumbusho wa vitu tulikuwa navyo. Kuliluwa na mamlaka ya Ukuhani pamoja na manna ambayo tulilishwa pale jangwani pamoja navyo kulikuwa na bao za sheria. Awali vitu hivi vilipitishwa mbele yetu kuonyesha kuwa Bwana yuko nasi na kwamba sisi ni watunzi wa sheria. Dhihirisho lote lilikuwa kwonyesha kwamba Israeli wanatunza sheria ya Mungu. Kila mtu katika Israeli alitembea hatua moja baada ya nyingine kufuata sheria. Ndio maana ilifanyika hivyo. Ilifanyika kutuonyesha sisi, na kila mshirika wa Israeli, kwamba matembezi yote jangwani ni kwa ajiri ya kufuata sheria za Mungu, na tukasahau hilo. Tunuajaribu kuandika sheria upya.
Yoshua 6:10 Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lo lote lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele. (Biblia Takatifu BT)
Ni kusema, siri za Mungu zilifichwa na kutolewa chini ya maagizo hadi hile siku itawekwa wazi na
kutangazwa. Ndio sababu Dunia haijawa na ufahamu. Kwa
kuwa vitu hivi vilisikiliwa chini ya maagizo na
utaratibu kuwa, katika siku za mwisho, siri zita wekwa wazi (kama ujumbe wa
malaika wa kwanza). Sisi tu walinzi wa siri za Mungu (Taz. Nakala
Siri za Mungu (Nam. 131)). [The Mysteries of God (No. 131)]
Yoshua 6:11-14 Basi akalipeleka sanduku la Bwana liuzunguke huo mji, likauzunguka mara moja, kisha wakaenda kambini wakakaa kambini. 12 Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao makuhani wakalichukua sanduku la Bwana. 13 Na wale makuhani saba wakazichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana, wakaendelea wakazipiga tarumbeta; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la Bwana; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda. 14 Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja, wakarejea kambini; ndivyo walivyofanya siku sita. (Biblia Takatifu BT)
Wakati watakapoingia kwenye nchi ya ahadi, watakuwa wanafuata Sanduku. Sasa kuna mabadiliko katika utaratibu wa hatua za vita. Wana ulinzi tangulizi na ulinzi nyuma na zanduku imelifadhiwa. Kuna mabadilko kimfano kutokana na kufuata Zanduku la Agano kwingia nchi ya ahadi nyuma ya sheria za Mungu, hadi kusimama mbele na nyuma Mwanzoni kwa ulinzi wa kibinadamu, kama walinzii wa sheria. Mfumo huu utakapoanza baada ya awamu ya kwanza, watakuwa walinzi wa sheria za Mungu. Chini ya muhuri wa kwanza, dini za uongo zilianzishwa. Ni kutoka wakati huo sheria ilipaswa kulindwa na wateule, kwa hivyo hatua za utaratibu wao uliingiliwa na sheria aingeondolewa kutoka kwa dhana ya kanisa na taifa.
Yoshua 6:15-17 Ikawa siku ya saba wakaondoka asubuhi na mapema wakati wa mapambazuko, wakauzunguka mji vivyo hivyo mara saba; ila siku hiyo waliuzunguka huo mji mara saba. 16 Hata mara ya saba makuhani walipozipiga tarumbeta, Yoshua akawaambia watu, Pigeni kelele; kwa maana Bwana amewapeni mji huu. 17 Na mji huu utakuwa wakfu kwa Bwana, mji wenyewe na vitu vyote vilivyomo; isipokuwa Rahabu, yule kahaba, ataishi, yeye na watu wote walio pamoja naye nyumbani, kwa sababu aliwaficha hao wapelelezi tuliowatuma. (Biblia Takatifu BT)
Hizi ni tarumbeta saba na sauti pia.. Tarumbeta ya saba ni uharibifu chini ya bakuli za ghadhabui ya mungu.
Yoshua 6:18-19 Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtayafanya matuo ya Israeli kuwa yamelaaniwa na kuyafadhaisha. 19 Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa Bwana; vitaletwa katika hazina ya Bwana.
Kuna maelekezo maalumu hapa. Kila kitu kuhusu mfumo ule kilikuwa kiangamizwe isipokuwa sanamu ambazo zilikuwa za dhamani, zilizopeanwa katika Hekalu la Bwana chini ya mfumo wa utawala wa kidini ili ziweze kutumika katika huduma ya Mungu na havingeruhusiwa kuchafua watu. Huu ni mfumo ule ule utatumika wakati wa kipindi cha mika elfu moja. Vyuma na vitu vinavyotumika kama siraha na vinavyotumike kwa manufaa. Wakati tutaenda katika vita vya Armageddoni tukagundwa kiasi kikubwa cha sanamu pamoja na siraha vitakusanywa na kutumika, kutoa rasilimali kwa Israeli katika kuwasisiwa kwa millennia.
Yoshua 6:20-21 Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili mbele; wakautwaa huo mji. 21 Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee, na ng'ombe, na kondoo, na punda, kwa makali ya upanga. (Biblia takatifu BT)
Si mtazamo mzuri, walakini ndio utokea. Mfumo wa ulimwengu utaangamizwa, na ni tu wale ambao wanaweza kutumika kuibwa mfumo mpya ndio watabaki hai.
Yoshua 6:22 Naye Yoshua akawaambia wale wanaume wawili walioipeleleza nchi, Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo mwanamke mwenyewe na vitu vyote alivyo navyo, kama mlivyomwapia. (Biblia Takatifu (BT))
Wakati tunasema ukuta ulianguka, nyumba ya Rahabu ilikuwa katika ukuta. Lazima kulikuwa na ulinzi wa kimbingu kwa Rahabu, kushikikiria nyumba yake imara, kwamba hata kama ukuta wa Yeriko ulianguka nyumba yake ilifadhiwa kimiujiza. Ilikuwa ashirio la kimiujiza la uifadhi wa mataifa walioteuliwa kuingia katika urithi wa Israeli chini ya ulinzi wa Mbinguni, na hiyo ilikuwa muujiza. Inaonyesha kuwa pahali pa kimbilio pake Rahabu palikuwa katika ukuta na ni ule ulioanguka mfirimgo kwake, kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa juu ya Rahabu. Dhana ya pahali pa usalama ni popote pale Mungu ameweka mkono wake juu yetu. Tutaona maelfu wakianguka sehemu ya mkono wetu wa kulia na pia wa kushoto. Tutawaona wakifa na kwanguka chini kwa tauni na maradhi. Tutawaona wakiaga kwa kemikali na vita, na tutaishi. Hizo ni nguvu za Mungu, na hatuelewi kwamba hatuna imani. Ikiwa tunafikiria kuwa tunafaa kunyakuliwa kwenda pahali pa kimbilio, imani yetu ni dhaifu na hiyo ndiyo shida na watu wale ambao wamefungwa kwa miuungano ya biashara. Mungu ametia mkono wake juu yetu na tutakula na kunywa (mkate na maji yetu ni hakika, isaya33;16), Hadi tutakapofikishwa kwa Masihi, wakati atakapotia miguu yake katika mlima wa miseituni, na kwa hilo tuna uhakika. (Taz Nakala Pahali pa kimbilio (Nam. 194)). [The Place of Safety (No. 194)]
Yoshua 6:23-27 Basi wale vijana wapelelezi wakaingia, wakamtoa
Rahabu, na baba yake, na mama yake, na ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa
navyo, wakawatoa na jamaa zake wote pia; wakawaweka nje ya matuo ya Israeli. 24
Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote
vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya
chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya Bwana. 25 Lakini Yoshua
akamhifadhi Rahabu, yule kahaba, na watu wa nyumba ya baba yake,
na vitu vyote alivyokuwa navyo; naye akakaa kati ya Israeli hata leo; kwa
sababu aliwaficha wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko.
26 Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na
alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga
tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza
wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume
aliye mdogo. 27 Basi Bwana alikuwa pamoja na Yoshua; sifa zake zikaenea katika nchi ile yote. (Biblia Takatifu BT)
Yeriko imejengwa upya. Watu walioweka miundo mbinu ya yeriko kutoka mwanzo, lazima walijkaza
na kwangamiza vijana wao wa kiume, na ndio maana
hakuna amani katika Yeriko. Hakutakuwa na amani katika
Yeriko hadi pale Masihi atarudi, na watu hawa wataaga. Mkataba wa amani uliosingatiwa katika mji ule ni mpotovu na
kushindwa.
Yoshua 7:1 Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana wa Israeli. (Biblia Takatifu BT)
Hii ni mfano wa shida zilizoingia katika sheria kupitia Yuda. Yuda waliheba sheria na, hadi leo hii, sheria haitimizwi katika Yuda sababu waliacha sheria. Urithi uliondolewa Yuda na ghadhabu ya Mungu ikatiwa Israeli sababu ya Yuda.
Yoshua 7:2 Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu na Bethaveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, Pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai. (Biblia Takatifu BT)
Tena walianzia uharibifu na upatanisho (vile wamerikani walizoea kusema katika vietnamu) juu ya mataifa mengine. Hiyo ndiyo inatokea, tunaingia ndani na kwanzisha msingi na tena kwendelea kukumbana na taifa baada ya lingine. Matengenezo ya kipindi cha miaka elfu moja ya sayare hii inafanyika kwa msingi wa utratibu. Kuna kipindi cha maombolezo, kuna kipindi cha kufanya kazi, na kazi itafanywa kwa utaratibu kushugulikia mataifa yote. Yanaletwa yote kiutaratibu katika hile ghadabu ya Mungu ili kukabiliwa na kuangamizwa kama kikundi chini ya bakuli saba za ghadhabu ya Mungu, na tarumbeta ya saba, iliyoukuwa mfano Israeli kote. Upatanisho kwa mpangilio wa sayare hii hapo utaimalika ili mfumo wa millennia uweze kujengwa na kwa amani tutamiliki ulimwengu kipindi cha miaka elfu moja.
Katika mafundisho haya mafupi ya Biblia tumepata ufahamu jinsi Israeli walivyoelewa kutoka kitabu cha Yoshua ambacho kitabu cha Ufunuo kinanena. Kila kitu katika biblia kimeunganishwa. Kwa kuwa Wayaudi hawana Agano Jipya hilo haliwahebusa, tunavyoona kutoka kwa mafundisho ya kitabu cha Eastha. Yuda anayo Yoshua na wote wanao Estha na wimbo ulio bora na wanaelewa matokeo ya mwisho yalivyo. Mtu hahitaji Agano Jipya ili kuelewa kitachotokea katika siku za mwisho. Mtu anaweza kubashiri kila kitu katika Agano Jipya kutoka kwa maandiko, ambayo ni Agano la Kale. Agano la Kale litatuelezea mwanzo kutoka mwisho vile kristo alinena chini ya maelekezo ya Mungu kwa Manabii.
Kupitia Yoshua, tunauwezo wa kupata mtazamo mpana wa ukweli ulio endelea wakati tulichukua Israeli katika mara ya kwanza.