Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[143A]

 

 

 

Mbingu, Jehanamu au Ufufuo wa Kwanza wa Wafu

 

(Toleo La 1.0 20120428-20120428)

 

Ufufuo wa Kwanza wa Wafu ni ufufuo wa waumini waliokufa na imani sahihi kutoka kwenye Makanisa ya Mungu na utastokea wakati atakaporudi Masihi. Na hakuna fundisho lingine zaidi kusema tu kuwa utawahusu wale walio kwenye imani ya Ukristo wa kwelie ndio hasa wanaoongelewa hapa na kuelezewa.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Haki Miliki ã  2012 Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Mbingu, Jehanamu au Ufufuo wa Kwanza wa Wafu



Utangulizi

Kile kinachoendelea katika ulimwengu wa Kikristo wa zama zetu hizi ni kutojua jinsi inavyosema Biblia kuhusu kule wanakokwenda au kinachotokea au kuwapata wanadamu baada ya kufa na jambo muhimu sana. Wengi miongoni mwa hawa wanaoitwa Wakristo wataendelea kusisitiza kuwaeleza wafuasi wao kwamba wanapokufa wanakwenda mbinguni. Na wanaamini kwamba wale wote wasiopenda au kukubaliana nao bilashaka watakwenda Jehanamu, ambako wanadhani kuna mateso ya milele watakakokuwa na Shetani na mapepo. Na hivi ndivyo hata wanavyoamini na kufundisha Waislamu kwa mafundisho yaliyotokana baada ya zilizopotoshwa aya za zamani asilia. Na mahali ambako dhana nii potofu imejikita na kupata nguvu zaidi ni kwa watu wa imani ya Wakristo wanaoamini Utatu wan chi za Magharibi na wengi wao ni wale wanaotoka kwenye imani ya Wanosisti wa Kiantinomia na hasa wan chi ya Marekani. Na kile ambacho wale wanaojiita Wakristo wanachoshikilia ma kuamini kuwa ni kweli kuhusu mafundisho haya, kingewafanya wafukuzwe kutoka kwenye Makanisa ya Mungu yaliyokuwa kwenye Karne ya Kwanza au ya Pili, hata kwenye Kanisa la Roma ambako mafundisho ya uwongo yalianza kuingizwa kwenye Kanisa la Kikristo.

 

Kanisa zima liliamini kwamba Kristo atarudi kwa awamu mbili, na imani hii ya kurudi kwa Awamu ya Pili kulikuwa ni msingi wa tumaini la Ufufuo. Justin Martyr anaandika kutoka Roma mwka 154 akilielezea jambo hili kwa maneno machache tu kwenye Mdahalo wake aliofanya na Trypho. Kwenye Sura ya LII anaongelea kuhusu ujio wa awamu mbili za Masihi.

 

SURA YA LII -- YAKOBO ALITABIRI AWAMU MBILI ZA UJIO WA KRISTO.

"Na ilitabiriwa na Baba yetu Yakobo kwamba kutakuwa na awamu mbili za kuja kwa Kristo, na kwamba ile awamu ya kwanza atapata mateso, na kwamba baada ya kuja kwake atakuwa ni nabii au mfalme kwenye nchi yenu (Niliendelea), na kwamba mataifa watakaomwamini huyu Kristo mteseka ndio watakayemuona atakapokuja mara nyingine tena siku za mwisho. Na kwa ajili hii ndipo Roho Mtakatifu ameutoa ukweli huu kwa njia ya mifano, na kuagiza kwamba” Niliongeza “imesemwa kwamba ‘wewe Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu. Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa. Zaidi ya yote ni kwamba. Kile kilichokwenye nchi yako hakitashindwa kamwe, iwe ni nabii au mtawala, tangu kipindi walipoanza hadi wakati huyu Yesu Kristo alipokuja kwa mara ya kwanza na kupata mateso, hutaweza kuhatirika na kuaibika na kudai wala kuthibitisha hilo. Kwa kuwa ingawa unakubali kwamba Herode, ambaye ndiye katika kipindi chake aliteswa, alikuwa ni Muashkeloti, na haijalishi kuwa unakubaiana kuwa kulikuwa na kuhani mkuu kwenye nchi yako; ili kwamba hatimaye uwe na mtu atakayeshughulikia kazi ya kutoa dhabihu swaswa na ilivyoagizwa kwenye torati ya Musa, na kufanya shughuli nyingine zote za ibada zilizoamriwa, na pia [ulikuwa] na manabii waliondelea kutoa unabii hadi kuja kwa Yohana, (hata kwenye kipindi kile ambacho taifa lako lilipelekwa mbali utumwani Babeli, wakati nchi yako ilipopatilizwa na baa la vita na vyombo vitakatifu vilipochukuliwa mbali), hakukukosa kuwa na nabii miongoni mwenu, ambaye alikuwa ndiye bwana, na kiongozi, na mtawala wa taifa lenu. Kwa kuwa Roho aliyekaa ndani ya manabii wenu aliwatia mafuta wafalme wenu, na kuwaweka madarakani. Lakini baada ya kuja na kufa kwa Yesu Kristo kwenye nchi yenu, hakukuwa na wala hakuna mahali palipokuwa na nabii tena, na zaidi ya hapo mliacha kuwa na mfalme wenu, na nchi yenu iliaharibiwa vibaya, na kuachwa kama maganjo kwenye mizabibu, na maagizo kutoka kwenye Maandiko Matakatifu, kinywani mwa Yakobo yasemayo ‘nanyi mtapendwa na kuwa lulu kati ya mataifa’ ilionekana kuwa na maana ya kimfano tu ikiwakilisha kuja kwake mara mbili, na kwamba mataifa ndio walimwamini, aambo ambayo ni kwa kipindi kirefu sana mmekuwa mkilifikiri. Kwa wale mataifa walio na moyo safi na wasafi wa mioyo na wanaomwamini Kristo, ndio wanaotarajia kumwona atakapokuja tena duniani.

(Mwanzo 49:5, 8-12, 18, 24)

 

Sehemu ya fafanuzi ya somo hili ilitajwa kwa kifupi sana na Justin Martyr kwenye Mdahalo wake na Trypho kwenye Sura ya LXXX.:

SURA YA LXXX – MTAZAMO NA MAONI YA JUSTIN KUHUSU UTAWALA WA MIAKA ELFU MOJA. NA AMBAO WAKATOLIKI WENGI WANAUKATAA. [Kumbuka kwamba jaribio la kutetea kile kilichojulikana baadae kama mafundisho potofu ya Waamini Utatu au Watrinitaria yatafutiwa uwezekano wa kujaribu kuyahalalisha hapa na inaonekana kwamba “Wakatoliki kadhaa waliyakataa” yalipoletewa wasome. Hatahivyo, ni maelezo ya haraka ya maandiko ya Biblia kwenye kitabu cha Ufunuo sura ya 20 (kwa mujibu wa Cox).

 

“Na kuhusu hili, Trypho alijibu, "Nadiriki kukuambia bwana, kwamba unapenda sana kubakia salama na sahihi kwa mambo yote, kwa kuwa unaweka hoja zako kwenye Maandiko Matakatifu. Lakini hebu niambie, je, unakubaliana kwa dhati na mahala hapa panaposema kuwa mji wa Yerusalemu utajengwa tena, na je, unakubali kwamba watu wako watakujarudi na kukutana pamoja, na kuwa watafurahi kwa furaha kuu pamoja na Kristo pamoja na mababa zetu wa zamani, na manabii, ambao makundi yote mawili ni watu wa taifa letu, na waongofu wengine walioungana nao kipindi cha kabla ya kuja kwa kristo wenu? Au je, mmekata tamaa na kukubaliana nayo ili kufanya tuchukiza na kututia kwenye utata?"

 

Kisha nilijibu, "Mimi sijakata tamaa sana, mwezangu Trypho, anataka kusema jambo moja na kufikiria lingine. Nilikubaliana na wewe hapo kwanza, kwamba mimi na wengine wengi tunawazo hili na [tunaamini] kwamba jambo hili litatokea, kama jinsi hiyohiyo ambayo wewe unaifahamu vizuri sana, lakini kwa upande mwingine nilikueleza maana yake kwamba wengi wa wale walio na imani thabiti na waaminifu na Wakristo wa kweli wanadhana na fikra tofauti. Zaidi sana, nilikuambia kwamba kuna watu wanaojiita Wakristo lakini wakiwa sio wachamungu kabisa, sio waadilifu, na waeneza mafundisho ya uwongo, wanafundisha mafundisho ya kufuru kila wakati, ni wakana imani ya kweli yaani waatheistiki, na wajinga. Lakini nataka ujue kwamba sisemi hilo kwako wewe pekeyako, lakini nitapeleka maneno haya, kwenye maeneo ya mbali kama nitakavyoweza, na kwa mambo yote yenye kutatiza yaliyofanyika na kutokea katikati yetu: ambayo nitayachukulia tendo la kukubaliana na mambo hayahaya ninayoyakiri mbele yako. Kwakuwa nimechagua kuyafuata mafundisho ya Mungu na sio ya wanadamu au kuwafuata wao, bali nitayashika yale [anayoyasema] yeye, Mwenyezi. Kwa kuwa, kama wewe umeshindwa na kuwa sawa na wale wanaojiita Wakriso, lakini wakiwa hawapendi kuiamini [kweli] yake, na wakiendelea kumkufuru Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo; kwa kuendelea kusema na kuwafundisha wengine kuwa hakuna ufufuo wa wafu, na kwamba roho zao wanapokufa zinakwenda mbinguni; huwezi kuwahesabia hawa kuwa ni Wakristo, hata kidogo, na kama kuna mtu anayeawapa uzito na kuwachukulia hivyo, basi na tukubali kuwa wao ni Masadukayo, au ni mtu aliye sawa tu kama imani ya Kigenisti, Kigeristae, Kigalilaya, Kihelenisti, Kifarisayo, Kibaptisti, ambao Wayahudi (hawasikiki wakikosa kuwavumilia ninapokuambia kuhusu hilo), ila wao [peke yao] wanajiita kuwa ni Wayahudi na wana wa Ibrahimu, wanaomwabudu Mungu kwa midomo tu, kama Mungu mwenyewe alivyosema, lakini mioyo yao ikiwa mbali naye. Lakini mimi na wenzangu wengine walio na ni Wakristo wenye nia safi kwa mambo yote, tumehakikishiwa kwamba kutakuwa na ufufuko wa wafu ye nia safi ut I and others, who are right-minded Christians, na kuwa tutatawala kwa kipindi cha miaka elfu mjini Yerusalemu, mji ambao utakuwa umejengwa upya, na kupambwa, na kupanuliwa, kama walivyotabiri manabii Ezekieli na Isaya na mabanii wengine.” (tumeongezwa ili kuonyesha msisitizo); (Ufunuo 20: 1-15)

 

Kila aliyesema na kuanza kufundisha kwamba watu wanapokufa wanakwenda mbinguni alikuwa sio macha-Mungu na alifundisha mafundisho mapotofu na yakufuru na hakukubalika na kanisa au alikuwa ni muasi wa imani ya kweli. Na kwa maneno mengine ni kusema kwamba mafundisho kama haya yangeweza kuwagawa kabisa.

 

SURA YA LXXXI – ANAJARIBU KUTHIBITISHA HOJA ZAKE NA MANENO YA NABII ISAIYA NA MAANDIKO YA KINABII. [Kumbuka kwamba Watafsiri hawa wa Kitrinitaria wa siku hizi wanadai kwamba hoja zao zinapata mashiko kutokana na muono wa Justin zaidi kuliko kulinganisha na mafundisho ya Kanisa la Mungu (aonavyo Cox)]

"Kwa kuwa nabii Isaya alilisema hilo kuhusu jambo hili la kipindi hiki cha miaka elfu moja akisema hivi: Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni. Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha. Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza. Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa. Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi. Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na Bwana, na watoto wao pamoja nao.Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema Bwana' Tunajua sasa kwamba maelezo yaliyotumiwa kwenye maneno haya 'maana kama siku za mti [mti wa uzima] ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi. ni dhahiri kabisa kwamba yanakitabiri kipindi hiki cha miaka elfu. Kwa kuwa Adamu aliambiwa kwamba siku atakapokula matunda yam ti ule atakufa, na tunajua kwamba yeye hakumudu kuishi miaka elfu. Pia tumezidi kujionea zaidi kwamba, maelezo ya kwamba 'Siku moja kwa Bwana ni sawa na miaka elfu’ yamefungamana na somo hili. Na zaidi sana ni kwamba kulikuwa na mtu fulani miongoni mwetu ambaye jina lake alikuwa anaitwa Yohana, na qambaye alikuwa ni mmoja wa Mitume wake Kristo, ambaye alitabiri kwa njia ya ufunuo aliopewa na kuonyshwa, kwamba wale wanaomwamini Kristo wetu, wataishi kwa kipindi cha miaka elfu mjini Yerusalemu, na kwamba ni kwa vipindi vya matukio ya siku nyingi na vipindi vifupi vitakavyofuatia yaani tangu ufufuo wa mwisho au wa pili wa wafu na utakaofuatiwa na hukumu au kiyama ya watu wote itakapofanyika na watu kuhukumiwa. Maneno hay ani sawa na kama Bwana mwenyewe alivyotuambia kwamba ' lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; wana wa Mungu wa ufufuo'

(Isaya 65:17; Zaburi 90:4; 2Petro 3:8; Ufunuo 20:4-5; Luka 20:35).

 

Kumbuka: Ni kwenye sura hii ndipo dhana ya “siku za Mti wa Uzima” imejengewa hoja yake na kuanzia kufananisha na kudhani kwamba kipindi cha kuishi watati wa Milenia utakuwa ni miaka elfu. Inaonekana kwamba dhana hii imetokana na mapokeo ya Warumi kwa jinsi wanavyoyatafsiri maandiko, na ndipo walipoliingiza jambo hili, na hawana chanzo kingine chochote. Tutaliona jambo hili tunapoendelea kulichambua hapo mbeleni.            

                                                           

Ufufuo wa Wafu kilikuwa ni imani isiyoelezeka kirahisi na ni imani tatanishi kwenye makanisa yaliyojiita ya wana Matengenezo kama tunavyoona kwenye ukiri wa imani yao (soma jarida la Uhusiano Kati ya Wokovu Kwa Njia ya Neema na Torati (Na. 82) [The Relationship between Salvation by Grace and the Law (No. 82)].

                                                           

Mlolongo wa Mambo ya Siku za Mwisho na Ufufuo wa Kwanza

Kwa mujibu wa jarida la Ufufuo wa Wafu (Na. 143) [Resurrection of the Dead (No. 143)] tunaelezea ukweli kwamba sio watu wote watakaofufuliwa kama Warefaimu. Lakini ni kweli kwamba kifo ni kitu kilichowekwa kumpata kila mmoja wetu na kwamba kila mtoto aliyetoka kwa Adamu atafufuliwa kwa ajili ya kuhukumiwa. Ni jambo bayana pia kwamba wamewekewa watoto wote wa Mungu wakiwemo malaika wateule wote ili waweze kuupata wokovu na ili mpango wa Mungu ukamilike na kutimilika kabisa. Mafundisho yaliyoanzishwa na kuendelezwa na makanisa ya Mungu kwenye miaka ya karne ya ishirini yakitokea Marekani hayakuwa sahihi na yaliposha mafundisho ya kweli ya Biblia na shutuma dhidi ya Haki na Wema wa Mungu na hali yake ya uweza wa kipekee wa Kujua mambo yote (Omniscience) na Uweza wake kwa mambo yote (Omnipotence). Moja kati ya mafundisho haya mapotofu ni lile la Ufufuo wa Tatu, ambalo tumelielezea na kulifafanua kwa kina kwenye jarida letu la Dhana ya Uwongo Kuhusu ufufuo wa Tatu (Na. 166) [The Fallacy of the Third Resurrection (No. 166)].

 

Kutoka kwenye jarida la Ufufuo wa Wafu (Na. 143) tunajionea mambo yafuatyo:

 

Ufufuko

“Mungu hafanyi miujiza kwa ajili ya wafu hadi wafu waweze kumhimidi kutoka kuzimuni waliko (Zaburi 88:10a), na Wafu hawawezi kuinuka pia. Na fadhili zake kuzisimulia wakiwa makaburini (Zaburi 88:11) wakati wafu watakapofufuka. Ayubu alijua sana kwamba Mkombozi wake alikuwa yu hai (Ayubu 19:25) na kwamba hatimayake atasimama kwenye zamu yake hapa Duniani. Baada ya kuharibika kwa mwili wake, Ayubu alijua kwamba atamuona Mungu akiwa na mwili wake, yeye aliye upande wake, na kwamba atamwona kwa macho yake na wala sio kwa macho ya mtu [mwingine] (Ayubu 19:25-27).

 

Kristo aliwafufua wafu ili sisi tujue kuwa yeye nndiye Masihi (Mathayo 11:4-5). Lazaro alikuwa ni kielelezo cha uweza wake (Yohana 11:11). Maelezomeingine ni kwamba alipokuwa anasulibiwa pale, walikuwako wengine waliofufuka kutoka makaburini alipokuwa anakata roho. Mapokeo na imani ya Wayahudi kipindi kile ilikuwa ni kwamba watu hawa waliofufuka walikuja kuuawa tena baadae. Fundisho la ufufuo kama lilivyoelezewa na Msihi lilijulikana sana na lilitarajiwa  (Mathayo 14:2).

 

Ilieleweka kwamba hatutalala wote, bali ni kwamba tutakuja badilishwa wote katika siku ile ya mwisho wakati wa itakapopigwa baragumu ya mwisho (1Wakorintho 15:51). Kwa hiyo, wapendwa waumini waliolala kwa vipindi kadhaa vya vizazi na vizazi vya zama ya dunia, katika Siku ile ya Mwisho Masihi atakaporudi watafufuliwa wakati ambapo watakatifu wengine wakiwa wanaishi na wangali hai bado. Na kwa hiyo, wote watabadilishwa kutoka kwenye mwili wa kufa na kuwa na mwili usiokufa (1Wakorintho 15:44). Wale wote waliolala wataamka. Na wale wote watakaokutwa wakiwa hai na waliosalia hadi kuja kwake Bwana hawatawatangulia wale waliokwisha kulala (1Wathesalonike 4:13-15). Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.  (1Wathesalonike 4:16-17).

 

Tangu kipindi hiki cha ufufuo ndipo utawala wa milenia wa watakatifu utaanza. Watakatifu watayachunga na kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma (Ufunuo 2:26-27). Kuna idadi kadhaa ya alama ashirio kuhusu fimbo. Fimbo inauweza wa kuwaswaga mataifa ikiwa kama kitendea kazi cha udongo na isipinde wala kuvunjika kama yanavyofanya magugu au matete. Misri ilifananishwa na magugu ambayo ilinasa na kuzingirwa na kuiachiliwa na mikono ya Israeli wakati Israeli walipojufunza kutoka kwake. Watakapojifunza kwetu sisi, fimbo yao hawanasa.

 

Kwenye ufufuo hakutakuwa na kuoa wala kuolewa (Mathayo 22:30). Watakatifu watafufuka wakiwa ni viumbe wakio kwenye ulimwengu wa roho. Na hii ndiyo siku ambayo sisi sote tutakuja achika. Wale wote walioolewa watakuja achika tu. Hii ni talaka iliyo yalazima kabisa na isiyopingika. Tunaenda kuachika wote na kuolewa na Kristo, kila mmoja wetu. Hakutakuwa na tofauti ya kijinsia, hakutakuwa na wa jinsia ya kiume wala ya kike, na watakuwa na miili ya kiroho ambao watakuwa ni wana wa Mungu waliozaliwa kiroho, na ambao watafanya kazi na Kristo atakapokuwa kwenye utawala wake. Kristo alikufa kwa ajili yetu ili tutakapoamka kutoka kwa waliolala tuishi na yeye (1Wathesalonike 5:10).

 

Ni muhimu sana tujue kwamba ni watakatifu tu ndio watakakuwa na sehemu kwenye Ufufo huu wa Kwanza. Kwa mujibu wa lugha ya kiebania, maneno haya; Utakatifu na Haki yana maana moja na pengine hutumuka pamoja ambayo huitwa (tsedek) – na yanajulikana kuwa ni kitu kimoja tu. Kwa hiyo, mtu ambaye hajatubu na mwenye maisha ya dhuluma na asiyejali wala kutenda haki, hatakuwa na wateule kwenye Ufufuo huu wa Kwanza.”

 

Mlolongo wa Mambo

Kuna mambo ambayo yanapaswa yatangulie kabla hajarudi Masihi. Mambo hayo yote yatakuwa kwenye mtiririko uliopangiliwa tangia zama za uumbaji. Kanisa limekuwa kilamara linajua kwamba kipindi hiki ni cha miaka efu sita ambacho kinawakilishwa na amri ya kufanya kazi kwa siku sita za juma la Uumbaji. Kwa hiyo, kipindi hiki kilikuwa ni cha siku sita za kwanza za juma na Sabato iliwakilisha Mapumziko ya Sabato na Kristo ambayo yanapaswa yawe kwa kipindi cha miaka elfu ya milenia kwenye Utawala wa Kristo. Kwa hiyo, ni lazima Kristo arudi kwanza ili kuanzisha utawala wake wa Milenia. Ataweka Kiti chake cha Enzi huko Yerusalemu na mamlaka itakayoenea ulimwenguni kote.

 

Kwenye mlolongo huu wa mambo tutajionea dunia ikionywa kwa kuwa Mungu hafanyi jambo lolote ila ni lazima awaonye watu kwanza kupitia watumishi wake manabii..

 

Mwishoni mwa Zama hizi tutashuhudia Vipindi vya Mwisha wa Wamataifa ambacho kimeelezewa sana kwenye majarida ya Kunguka Kwa Misri (Na. 36) [The Fall of Egypt (No. 36)] na Kuamguka kwa Misri Sehemu ya II: Vita Vya Mwisho (Na. 362) [Fall of Egypt Part II: The Wars of the End (No. 362)].

 

Kwa mujibu wa jarida la Kalenda ya Mungu (Na.156) [God’s Calendar (No. 156)], mfuatano wa matukio ya kinabii umekamilika kwa mujibu wa jinsi Kalenda inavyoonyesha ukilinganisha na mfumo wa mzunguko wa yubile. Mfumo huu unachukuliwa kutoka kipindi cha kufungwa kwa Bustani ya Edeni hadi kuifikia Yubile ya 120 ambayo inaishia kwenye mwaka wa Yubile wa mwaka 2027 ambayo ni jumla ya miaka 6000 tangu kipindi Mungu alipoilaani hii dunia.

 

Kizazi cha Mwisho cha miaka 40 kilianza kwenye kipindi cha Upimaji wa Hekalu kilichanza mwaka 1987, na inaenda sawa na kinavyosema kitabu cha Ufunuo 11:1. Awamu ya mwisho ya kabla ya kurudi kwa Masihi ni ile ya Kuonywa kwa Mataifa, kazi itakayofanywa na Mashahidi Wawili walioandikwa kwenye Ufunuo 11:2, na kama ilivyoelezewa kwenye jarida la Mashahidi, Wakiwemo hawa Mashahidi Wawili (Na. 135) [The Witnesses including the Two Witnesses (No. 135)].

 

Ili kukifikia kiwango hiki ambacho kwacho Malaika wale waasi watahukumiwa, Shetani atafungwa kuzimuni kwa kipindi chote cha Milenia. Ili kuupata mlingano mzuri na usiolemea upande mmoja italazimu kumwondoa na kumfungia kuzimuni Shetani pamoja na mapepo wake kwenye kipindi hiki atakachokuwa anarudi Masihi. Tendo hili litafanyika kwanza likitangulia tukio la kurudi kwa Kristo.

 

Ufunuo 20:1-4 inasema: Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache. Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu

 

Watu hawa wote wanawezakuwa ni wale waliouawa au walioteswa na kuwekwa kwenye mazingira yaliyoapelekea kushundana nayo na kuyapinga. Hakuna uweaekano wa kuyaepuka mateso. Tunapokuwa kwenye Ufufuo wa Kwanza, tutahukumiwa. Tumekuwa tukipitia kipindi cha mateso.

 

Ufunuo 20:5-10 inasema: Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu. Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

 

Watu hawa hawatakufa kwa maana ya kuwa wanateseka sasa. Wengi miongoni mwa walioko duniani leo wawapiti kwenye hukumu sasa. Kwa hiyo, wale watakaoamshwa kwenye Ufufu wa Kwanza ndio wale wanaohukumiwa sasa. Nasi tunapitia vipindi vya aina hiyohiyo vya kupitia kwenye mchakato wa kupimwa na kurekebishwa. Kisha tunapitia kwenye mlolongo wa kufikia kwenye mchakato wa Hekalu, mfumo wa Yubile unaoadhimishwa kila baada ya miaka saba, na kwa kupitia kwenye mzunguko ule ule hadi utufikishe mahali ambapo Mungu atatufanya tuwe na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza. Sehemu nyingine iliyobakia ya dunia wataamshwa na kurudiwa kwenye uangalizi wa Ufufuo wa Pili (Ufunuo 20:11-13).

 

Ufufo huu wa Pili unaotajwa hapa imeongelewa kwenye jarida la UUfufuo wa Pili na Kiti Kikubwa Cheupe cha Hukumu (Na. 143B) [The Second Resurrection and The Great White Throne Judgment (No. 143B)].

 

Ufufuo Wenyewe na Halisi

Kwenye ufufuo wa Mashahidi wale Wawili tunajionea kwamba watachukuliwa kwa sauti kuu ya malaika mkuu ili wakutane na Bwana. Ni katika kipindi ndipo Masihi atakuja wenye Mlima wa Mizeituni, ambao utagawanyika sehemu mbili.

 

Mlima wa Mizeitumi utagawanyika sehemu mbili, mlima mmoja utakuwa upande wa Kaskazini na mwingine Kusini jambo litakalofanya kuwepo bonde kuu sana litakalopita karibu na mji wa Yerusalemu lenge urefu wa takriban kilometa 66. Mji wa Yerusalemu utabakia kuwa kwenye nyanda za juu na tetemeko la ardhi litauharibu mji huu. Bonde hili lililotokea litasababisha kuwepo kwa kiini asili cha nchi mpya ya makabila na Rasi au Peninsula ya Sinai itasogea upande wa kusini na na kukutana na ndimi za Bahari ya Shamu (Zekaria 10:11; 14:4).

 

Mara tu baada ya mabadiliko haya ya kimazingira yatakapowathiri wateule wake waaminifu, ndipo mababa waliotutangulia katika imani, na manabii na wale walioshikilia mafundisho sahihi ya kanisa na waliobatizwa ubatizo wa watu wazima na kumpokea Roho Mtakatifu na kuishi maisha ya mateso, watafufuliwa kutoka kwa wafu kutoka kwenye maeneo watakakokuwa na wale waliohai watawangojea (1Wathesalonike 4:15). Mara tu baada ya tukio hili la kufufuliwa ndipo mwili wote wa wateule wa Mungu ambao ni Makanisa ya Mungu, watabadilishwa kwenye kipindi hiki cha Milenia, na kumlaki Bwana mawinguni na kupekekwa mjini Yerusalemu ambako watakuwa na Masihi na kutawala naye.

 

Hapo ndipo Karamu Kuu ya Arusi ya Mwana-kondoo itafanyika (soma jarida la Baragumu (Na. 136) [Trumpets (No. 136)].

 

Haitoshi tu kule kumwita Yesu au kuomba kwa jina lake na kumwita yeye Bwana.

 

Ili kuwa na sehemu na kukaribishwa kwenye Karamu ya arusi, inampasa kila mtu atimilize viwango vifuatavyo. Na ni lazima afanya mambo yafuatayo:

  1. Lazima abatizwe akiwa mtu mzima aliyetubu kwa huduma itakayofanywa na watumishi waliokubalika na.uongozi wa ushirika wa Kanisa la Mungu (Matendo 3:19).
  2. Halafu anatakiwa awekewe mikono ili ampokee Roho Mtakatifu baada ya kubatizwa (Matendo 8:17).
  3. Kisha anatakiwa kuwa ni mshirika mwaminifu kwenye mojawapo ya Makanisa ya Mungu yanayoutarajia utawala huu wa Milenia na anapaswa ajaribiwe imani yake.
  4. Inampasa ayatunze mavazi yake yasinajisike kwa kutiwa doa hata moja.
  5. Itampasa kuwa mwaminifu kuzitunza Amri za Mungu na Ushuhuda au Imani ya Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12).

 

Kusudi la kushiriki Ushirika wa Meza ya Bwana ni kujiosha na kujitakasa tena kwa tathmini nafsi ya kila mtu kwa kila mwaka na kuwafanya wajiandae kwa tukio kuu la Ufufuo wa Kwanza.

 

Na ikiwa mambo haya hayafanyiki kwa uaminifu na ukamilifu sana na kwa kumaanisha, basi mtu hataweza kupewa vazi lile la arusi kwa kuwa atakuwa hajazitii badi amri za Mungu na maelekezo ya Kristo na ndipo watakapoondolewa kwenye adhimisho kuu la karamu hii ya arusi kwa mojawapo ya njia zifuatazo. Kama hawatakuwa mjini Yerusalemu, basi watakuwa moja wapo ya sehemu zifuatazo:

 

  1. Wataachwa wamesimama na kushangaa tu wakati waliobaki wote wamechukuliwa kwenda Yerusalemu ambako watakuwa na Masihi.
  2. Iwapo kama watakapkuwa huko Yerusalemu watabakia kuwa ni viumbe wa kawaida wenye damu na nyama na kukataliwa kuwa na wateule na kuondolewa.

 

Kwa namna nyingine twaweza kusema kwamba kutakuwa na kilio kikubwa na maombolezo na kusaga meno kwa wale watakaokataliwa kuwa na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza kwa kuwa hakutakuwa na majadiliano. Sio suala la kumwita Kristo kuwa ni Bwana tu huku ukiendelea kuyatunza na kuyaamini mafundisho potofu ya mungu jua, bali kinachotakiwa ni kuzitii amri za Mungu. Wale wanaomui Kristo Bwana na huku wakiwa hawayatendi yale anayoyasema, watakuwa kwenye maumivu makubwa sana na hakutakuwa na majadiliano au udhuru. Hali ya kuondolewa itaendelea kwenye makanisa ya Mungu na kuwa kama ilivyokuwa kwa   Wasardi na Walaodikia, imani itakayoondolewa na kuachwa kuelekea kwenye kipindi cha Milenia ambazho wanadamu watakuwa wamekufa au wamebakia hali ya uvuguvugu (soma isemavyo Ufunuo sura ya 3).

 

Hawa wote wanaoamini imani ya Utatu ya Kiantinomia na Kinostiki wataondolewa kutoka Yerusalemu na kupelekwa kwenye maeneo yao ya kikabila. Kila mmoja wa waumini hawa wa imani hii ya Kiutatu ya Kianyinomia na mafundisho yao ya kikengeufu na makuhani wao wataondolewa kutoka Yerusalemu na kupelekwa kwenye maeneo yao ya kikabila zao na kuletwa chini ya Maagizo na Sheria za Mungu na kwa mujibu wa Kalenda yake, wakiwa ni wanadamu kamili, wakamilifu sana (Isaya 66:23; Zekaria 14:16-19).

 

Wale watakaoikubali na kupigwa Alama ya Mnyama wataangamizwa kwa vitasa vya ghadhabu ya Mungu. Hii ni Dhiki Kuu itakayoupata ulimwengu wote na ambayo kwa wateule watakwenda kutunzwa au kuepushwa kama watakavyokuwa wamefufuliwa na wazao wao wataweza kulindwa na wao kama walivyo sasa Wateule walio Watiifu hapa duniani wakiwa chini ya Masihi wakihudumu ukuhani kama wa Melkizedeki. (soma jarida la Melkizedeki (Na. 128) [Melchisedek (No. 128)].

 

Msisitizo na mkazo wa Torati utafanywa upya na Mashahidi kina Eliya na mvua haitanyesha kabisa kwa majira yake kwa watu wote, ila itanyesha kwa kufuata majira yake kwenye yale mataifa tu yatakayokuwa yanazitunza Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu Zilizoamriwa na Mungu. Bali mataifa yale yote ambayo hayataiadhimisha na kuifuata Kalenda takatifu na Torati yake, hayatapata mvua kwa majira yake yanayotakiwa na watateseka kwa magonjwa ya tauni ya Misri.

 

Mambo Yatakavyokuwa Kipindi cha Milenia

Kitu kitakachofuatia itakuwa ni kusimika kanuni za utawala wa Masihi huko Yerusalemu.

 

Wale watu 144,000 wataunda kundi la watakaotumika kwenye Ukuhani na kusimamia mambo ya uongozi katika Yerusalemu. Kundi Kubwa Sana la watu litagawanywa kufuatia Makabila na mataifa na watakuwa ndio viongozi na walinzi wao wa kiroho badala ya mapepo ambao watakuwa wameishaondolewa katika kipindi hiki na kutupwa shimoni, kuzimuni na kufungwa humo kwa kipindi cha miaka 1000 ya utawala wa Milenia (kama inavyosema Ufunuo sura ya 7 ambayo ni nukuu kutoka kitabu cha Zekaria)

 

Wale watakaoikataa Chapa ya Mnyama na huku wakiwa hawazishiki sawasawa amri za Mungu na Ushuhuda wa Imani ya Kristo na ambao pia hawajafikia viwango vya kuwafanya kuwa na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza, wataingia kwenye kipindi hiki cha Milenia wakiwa ni wanadamu wa kawaida. Watu hawa watakuwa kwenye kundi la watu wa kawaida.

 

Kundi la kwanza ni lile la watoto wa wateule ambao walikuwa ni wadogo sana kipindi hicho kiasi cha kushindikana kuwabatiza na hawakuwepo kwenye Ufufuo wa Kwanza. Hawa watachukuliwa na kupewa mamlaka ya kuwa wafalme na makuhani watakaokuwa wanatawala kutoka mjini Yerusalemu.

 

Kundi linalofuatia litakuwa ni la Waisraeli Asilia ambao watakuwa ni Wanadamu wa Kawaida ambao watakuwa ni sehemu ya wale walio kwenye Wokovu Mkuu na Waliotolewa kama inavyoonekana kwenye kitabu cha nabii Isaya 66: 18-24.

 

Wengine waliobakia wote watakuwa ni wale wa mataifa yote na ambao hawakuwa ni sehemu ya mfumo wa yule Mnyama na waliobakishwa wakiwa ni wanadamu wa kawaida na ambao wanakwenda kuwa ni sehemu ya mataifa ambao watafundishwa neno la Mungu na Taratibu au Kanuni ya Torati yake.

 

Dhana mojawapo iliyokuwepo na iliyofundishwa kwenye makanisa ya Mungu lakini haipo kwenye maandiko ni ile ya kudhania kwamba wateule wataishi miaka 1000 ya kipindi hiki cha Milenia na hawatakufa. Fundisho hili halina msingi wake kutoka kwenye Biblia bali ni dhana fikirika tu na ambayo walioitunga wamejenga hoja zao kwa kulinganisha tu na kipindi cha kudumu kwa zama za Milenia na matukio yaliyoandikwa, hasa andiko lile linalosema dunia itadhurika na ndipo miti itachipuswwa kandoni mwa mto kutoka Yerusalemu ambayo itawaponya mataifa, kama tunavyoona kwenye kitabu cha Zekria 14:8 nk. Dunia yote itaelimishwa tena kwa maana ya kufanya vyema mifumo ya maisha na utaratibu wa vyakula na muundo wa Torati na Amri za Mungu. Hiyo haitatokea kwa maramoja na umri wa mwanadamu hautarejeshwa ama kurekebishwa upya hadi kuwa kama ilivyokuwa kipindi kile cha Bustani ya Edeni. Kutakuwa na uharibifu mwingi sana utakaokuwa umefanyika hapa duniani. Na hii haina maana kwamba maisha au umri utaongezwa na kuendelea, ndiyo maana tunasema na kuonya kwamba hii ni dhana potofu na yauongo kudhania kwamba umri wa kuishi mwanadamu utabadilika kwa harama na mara moja hadi kuwa ni miaka 1000.

 

Vita vitakavyopiganwa na kuonyeshwa kama Vitasa vya Ghadhabu ya Mungu vimeelezewa kwa kina kwenye jarida letu la Mangojeo ya Masihi Sehemu ya Pili: Vitasa vya Ghadhabu ya Mungu (Na. 210B) [Advent of the Messiah Part II: Vials of the Wrath of God (No. 210B)].

 

Kwahiyo, mji wa Yerusalemu utajengwa upya na Hekalu litajengwa na mfumo wake kurudishwa tena kwa kipindi hiki chote cha miaka 1000 hadi kwenye kipindi kile ambacho kwa sasa kinajulikana kama ni cha miaka kati ya 3015-3027 wakati mapepo yatakapofunguliwa tena kutoka kuzimuni yalikokuwa yemefungiwa pamoja na Shetani, ili waende tena huku na huko kuwadanganya mataifa na kuielekea kambi ya Watakatifu walioko Yerusalemu ili kupigavita na kuuharibu au kuupindua utawala wa Mungu hapa duniani. Jambo hili litatokea kwenye kipindi cha miaka ishirini ya mwisho ya yubile ya 140 ya mfumo wa kuwepo kwa zama yote ya dunia.

 

Mchakato wa kuiengeneza na kuufanya upya mji wa Yerusalemu kutachukua muda wake kwa kipindi chote cha kuanzia mwanzo wa Milenia hii mpya hadi mwishoni mwa Hukumu itakayofanyika kwenye Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe kama tunavyoona kwenye Isaya 65:17-25. Kwa mujibu wa aya hizi, tunafikia kudhani kwamba kipindi hiki cha Hukumu kitachukua miaka 100, ambayo ni kuanzia mwaka 3027 hadi 3127 ambao pia ni mwaka wa Yubile. Hapa ndipo tutakapojionea Nji wa Mungu ukishuka kutoka kwa Mungu na kuja hapa duniani (soma jarida la Mji wa Mungu (Na. 180) [The City of God (No. 180)].

 

Iwapo kama kipindi kinachotajwa kwenye Isaya 65 cha miaka 100 ni cha kwenye milenia na kitaendelea hadi kwenye kipindi kile cha Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe, na kwamba mtenda dhambi atakufa akiwa na umri wa miaka 100 na kwamba hiki ni kima cha chini cha umri wa mtu na kufanya kipindi kizima kiwe ni cha jumla ya miaka 1100, hivyo basi Hukumu itaishia kwenye miaka 100 na ndipo watenda dhambi watakufa na miili yao itateketezwa kwa moto. Ongezeko la kipindi cha kuishi wateule litaendelea kadiri kipindi hiki cha Milenia kitakavyokuwa kinaendelea.

 

Kazi ya wateule itakuwa ni kuwahukumu mapepo hawa kwa kipindi chote cha milenia.

 

Baada ya kukomesha kwa uasi, mapepo watauawa na kisha viumbe wote waliowahi kuishi watafufuliwa na kuwepo kwenye kile Kiti Cha Enzi Kikubwa Cheupe cha Hukumu au kwenye Ufufuo wa pili wa Wafu au Kiyama ya Wafu, ambako kwamba viumbe wote, wawe Wana wa wanadamu waliozaliwa na Adamu au waliotokana na Malaika Waasi walio wa Shetani, wote watafufuliwa na kupewa fursa ya wokovu kama ulivyotolewa na Kristo kwa mpango wake na dhabihu yake.

 

Mafundish ya uwongo ya Ufufuo wa Tatu wanayofundisha na kuamini wafuasi wa Herbert Armstrong hayana mashiko yoyote na wala hayana mahali pa kujengea hoja na hayana sehemu kabisa kwenye Makanisa ya Mungu. Na yameelezewa kwa kina sana kwenye jarida letu la Upotofu Kuhusu Fundisho la ufufuo wa Tatu (Na. 166) [The Fallacy of the Third Resurrection (No. 166)].

 

Jinsi mlolongo wa mambo utakavyokuwa kipindi hiki cha Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe cha Hukumu umeelezewa kwa kina zaidi kwenye jarida letu la Ufufuo wa Pili na Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe cha Hukumu (Na. 143B) [The Second Resurrection and The Great White Throne Judgment (No. 143B)].

 

 

q