Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[143B]

 

 

 

Ufufuo wa Pili na Kiti Kikubwa Cheupe cha Enzi cha Hukumu

 

(Toleo La 1.0 20120505-20120505)

 

Ufufuo wa Pili wa Wafu na Kiti Kikubwa Cheupe Cha Enzi Cha Hukumu ndiyo mwisho wa mambo yote tunayoyanona na kuyajua leo. Hii inachendana na tangia kipindi cha mwisho wa mfumo wa Milenia hadi kipindi cha kufuliwa kwa Shetani na Ufufuo Mkuu na wa watu wote waliowahi Kufa huko nyuma na kuhukumiwa na kuwaelekeza wale wote ambao hawajawahi kuishi huko nyuma bado.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Haki Miliki ã 2012 Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Ufufuo wa Pili na Kiti Kikubwa Cheupe cha Enzi cha Hukumu



Mfumo wa Milenia               

Siku ya kumi ya mwezi wa Tishri ambao pia ni Mwezi wa Saba wa Mwaka wa 49 wa Yubile ya 120, ambao kwa mfumo wa leo ni sawa na mwaka 2026 ambao Yubile itatangazwa. Vita zitakazopiganwa siku za  mwisho zimekuwa zikipiganwa na Masihi ametumwa ili kuja kuiokoa dunia kutokana na jinsi inavyojiharibu yenyewe. Shetani na malaika wengine walioasi watakuwa wamekwishatupwa katika Ziwa la Moto kwa kipindi cha miaka saba za mwanzo ambayo ni mzunguko wa miaka wa Sabato Saba unaoanzia mwaka 2013-2019 na dunia itajisalimisha kwa kristo na wateule wake baada ya kipindi cha Ufufuo wa Kwaza wa Wafu (tazama jarida la Mbinguni, Jehanamu au Ufufuo wa Wafu Na. 143A) [Heaven, Hell or the First Resurrection of the Dead (No. 143A)].

 

Ufunuo 20: 1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.

 

Kisha, Ufufuo wa Kwanza utakluwa umeshatokea tayari kama ilivyoonyeshwa kwenye jarida lililotangulia la Na. 143A:

4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. 6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.

 

Mfumo wa Imani potofu za miungu Juan a imani za Utatu na ibada za Jumapili na sikukuu za Krismas na Easter vitakuwa vimeondelewa na havipo tena hapa duniani pamoja na ukengeufu wake potofu wa kubadilisha mambo, ikiwepo ni pamoja mfumo na imani iliyowaharibu wengi ya Uislamu wenye imani kali, pamoja na mafundisho mapotofu yote ya masheikhe maarufu yajulikanayo kama Hadithi za Kiislamu. Na Uislamu pamoja na chuki zake utakuwa umetokomezwa kabisa. Hali ya iliyoko ya kuipotosha na kuigeuza dunia isifuate ukweli itakuwa imekoma pamoja na vifaa vyake kupigania, vyote vitakuwa vimekoma kabiusa.

 

Vita vya mataifa vitakuwa vimeletwa kwenye uwanda wa Megido na vitakomeshwa kwenye mpango mkuu ambao kwa sasa unaonekana kuwa ni eneo la uwanda wenye upana wa kilomita 66, n ani mahali ambapo kitovu cha Mlima wa Mizeituni ndipo kilipo.

 

Kipindi kihi, mataifa yote ya dunia yatakuwa yamefanywa yawe kwenye hali ya unyenyekevu na kuondokana na uasi uliosababisha kumwagwa kwa vile Vitasa vya Ghadhabu ya Mungu na kutakuwa kumefanyika marejesho mapya ya ukuhani wa Melkizedeki     (soma majarida ya Baragumu Saba (Na. 141), Vita ya Hamoni-Gogu (Na. 294); Kurudi kwa Masihi: Sehemu ya I (Na. 210A) na Kurudi kwa Masihi: Sehemu ya II: Vitasa vya Ghadhabu ya Mungu (Na. 210B0 [The Seven Trumpets (No. 141); War of Hamon-Gog (No. 294); Advent of the Messiah: Part I (No. 210A) and Advent of the Messiah Part II: Vials of the Wrath of God (No. 210B)].

 

Hekalu lililotabiriwa na nabii Ezekieli litakuwa mimeishajengwa na Masihi na mfumo mpya utakuwa umeshawekwa na kukamilika kabisa kwenye kipindi cha Yubile la Dhahabu ya mwaka 2077, ambayo ni Yubile ya hamsini ya Materejesho mapya kama uliofanuwa na Ezra na Nehemia (soma jarida la Yubile ya Dhahabu na Milenia (Na. 300) [The Golden Jubilee and the Millennium (No. 300)].                                                                                                

Kalenda kamilifu ya Mungu itakuwa imeisharejeshwa upya na kutumika, kama ilivyokuwa kwenye utaratibu wa Hekalu na Sabato, Mwandamo wa Miezi na Sikukuu zilizoamriwa na Mungu zitakuwa zimerejeshwa upya kwenye kila taifa na kwa kila mtu mmoja mmoja, na mtu au taifa litakalokataa kuitii wanapatilizwa kwa baa la njaa na tauni ya Misri (soma jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156) [God’s Calendar (No. 156)].

 

Marejesho yanayoelezwa kwenye kitabu cha nabii Isaya 65 na 66 na Zekaria 14 yatakuwa yameshafanyika pia kipindi hiki.

 

Katika kipindi hiki, taifa la Israeli litakuwa limehafanyika upya na utaratibu au mfumo wa Kitaifa wa Mikunjo Mitatu au wa Tarakimu ya Sitini ambao umeenea kutoka Ashuru na pande za Kaskazini kutoka kwenye Milima ya Medes na Kurds inayoelekea hadi huko Frati na Israeli, utashikisha nchi ya Syria na Lebanon, hadi kwenye nchi za Jordan, Israeli, Gaza, Edom una Moab una kuelekea hadi Ghuba ya Aqaba na kwenye Mito ya Misri ambayo yalisukumiwa pande za kusini na kufunga kingo za Bahari ya Shamu kama ilivyotabiriwa. Nchi ya Misri ilikuwa imeshirikishwa na mfumo wa kiutagu wa kitaifa ambao uliwekwa kwenye mipangilio ya barabara zao za ndani na utaratibu wao wa kusafirishaji, kama ulivyotabiriwa.

 

Nchi ya Israeli ilitawaliwa na utawala wa pamoja wa makundi ya kikabila uliotoka kwenye makabila yaliyoikalia ardhi kutoka mto Frati hadi Mito ya Misri, na kutoka Bahari ya Mediterranean hadi kwenye Jangwa la Arabia. Mifumo yote ya imani za kidini katika Mashariki ya Kati utakuwa umeondolewa na Makanisa ya Mungu yatakuwa yamepewa mamlaka na kutawala kutokea Yerusalemu. Watakuwa wanatawaliwa na baraza kuu la kimataifa ambalo litakutana kila mwaka katika siku ya 1 ya mwezi Tishri (au wa Saba) na siku ya 22 ya mwezi huo huo wa Tishri, ambao pia ni Mwezi wa Saba. Kila taifa ambalo halitazitunza au kuazimisha Sikukuu hizi za Mwezi wa Saba, hayatapata mvua kwa majira yake muafaka na pia yatapatwa na madhara ya magonjwa ya Wamisri kwa nchi zao zote (Zekaria 14:16-19). Wale ambao hawataitunza Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya wakiwa kama binafsi au kitaifa, watakufa kama ilivyotabiriwa na nabii Isaya 66:23.

 

Kristo na wateule, kama anavyosema Mungu kupitia kwa Roho wake Mtakatifu, watawatawala mataifa kwa fimbo ya chuma. Kutakuwa na mfumo mmoja wa kiutawala utakaowekwa kwa mujibu wa isemavyo Biblia, mfumo utakaoenea kwenye mataifa yote, ambao kwamba watateulliwa wakuu wa makumi, wa hamsini, wa mamia, wa maelfu, na migawanyo yake mingine (soma jarida la A3) na kutakuwa na dini MOJA tu. Na mifumo na imani zote za dini nyingine zote za uwongo itakuwa imekwishafutiliwa mbali duniani kote kwa kipindi cha miaka ishirini na tano ya vita vya mwisho vitakavyofanyika kwenye miaka ya 2001-2026. Idadi ya watu theluthi mbili ya wakazi wote wa dunia wataangamizwa na kuteketezwa kwenye vita hivi na kisha idadi nyingine ya theluthi iliyobakia watapunguzwa pia kwa kamio la kumiminwa kwa Vitasa vya ghadhabu hii ya Mungu kwa kuwa dunia HAITATUBU.

 

Kitakapoanza kipindi hiki cha Milenia ambacho kitajumuisha makabila yote na mataifa nchini mwao watakuwa na idadi ya takriban watu milioni 500 watakaokuwa wanaishi hai.

 

Ni pale inapokuwa jambo la dhahiri ndipo mataifa watakubwa na baa la njaa jadi kufa, na watakufa hakika wasipoyatubia matendo yao maovu na kuamua kuzitii na kuzishika Amri na Torati ya Mungu watakayopewa na kuziadhimisha na kuzishika Sabato zake, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zilizoamriwa na Mungu. Kwa ajili hiyo inaonekana kwa dhahiri kabisa kwamba watakapotaka kunywa maji na kumwagilia mimea yao na watakapohitaji matunda ambayo yatawaponya mataifa, ndipo watapaswa kuchagua jambo moha, yaani kuchagua kuzishika amri za Mungu au kufa.

 

Baada ya Yubile ya 121 (ambayo wakati mwingine itakuwa kwenye mwaka unaojulikana kama wa 2077, kwa mfumo wa kipagani wa kizamani ambao utakuwa umekomeshwa kabisa) itakuwa ni rahisi na rahisi zaidi. 

 

Yubile moja hadi nyingine dunia itakuwa na uzao zaidi na wanadamu wote watakuwa kwenye zama ya amani. Hakuna atakayeweza kuiona vita tena, na watakaoijua ni wale watakaokuwa wazee tu na ndio ambao wataikumbuka jinsi ilivyokuwa.

 

Watu watakaokuwa kwenye ulimwengu wa Kiroho na ambao watakuwa na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza wataitawala dunia kama mapepo walivyokuwa wanatawala siku zilizokuwa kabla yao walipokuwa na Shetani ambaye pia alijulikana kama ni Nyota ya Alfajiri hapa duniani kipindi cha kabla ya Kurudi kwa Masihi ambaye kwa kipindi hiki atakuwa ni Nyota Mpoya ya Alfajiri.

 

Watu watakuwa wameanza kuishi kwa miaka mingi na watakufa wakiwa umri Yubile nah ii itakuwa hivyo kama watakuwa wakelaaniwa kwa dhambi zao (Isaya 65:17-25). Watu wataanza kuishi kwa miaka mingi kama walivyoishi mabab zetu wa zamani. Wao waliishi kiama mingi kama ilivyo siku za maisha ya miti na ni watenda dhambi tu ndio watakaokufa mapema. Watenda dhambi hawa ni wale ambao kwa kawaida hujihesabia haki wao wenyewe. 

 

Mungu ambaye ni Elohim akawatokea, bali waliendelea kuwatweza na kuwadharau wateule na wakatenda dhambi na dhambi zao hizo ndizo ziliwapelekea kuingia hukumuni na kupatwa na maafa na vifo vya watu wanaokataa kutubu.

 

Wateule hawa na watakaotukuzwa na kuitwa elohim watakuwa ni wale waliotubu dhambi zao kipindi kile walichojitokeza na kuwaongoza wakazi wa dunia hii kwenye kipindi cha Milenia.

 

Mwishoni mwa kipindi hiki cha miaka elfu ya Milenia, dunia itakuwa na mwonekano wa kupendeza sana kama ilivyokuwa siku za Bustani ya Edeni ilivyokuwa hapo kabla na kama ilivyokuwa siku za Uumbaji za Adamu. Waliaminika kuwa walikuwa wanajua vizuri zaidi kuliko walivyokuwa washauri wao na Masihi ambaye alikuja kuwaokoa baadae. Walikuwa na lugha moja tu na hakukuwa na jambo lililowashinda kulifikia. Walikuwa wamepoteza maarifa ya kujua sababu iliyopelekea dunia ile ya kwanza iangamizwe. 

 

Sasa kilikuwa ni kipindi cha Mungu kuwajaribu. Katika mzunguko wa Sabato ya Sita utakaokuwa kwenye kipindi cha mwisho wa Milenia kwenye Yubile ya 140 (yaani mwaka 3013-3019) ndipo Mungu wetu ambaye ni wa Pekee na wa Kweli ambaye pia ni Eloa, atamwambia Kristo na wateule waliofufuliwa kwenye Ufufuo wa Kwanza na Wateule wengine wasimame nyuma na ataijaribu hii dunia kwa mara nyingine tena.

 

Hatimaye, ndipo kitafika kile kipindi cha kuachiliwa kwa Shetani na Makaika wake wengine Waovu watoke kifungoni kwao kwenye Ziwa la Moto ili wawadanganye tena mataifa walioko ulimwenguni kote.

 

Vita ya Mwisho

Kipindi cha Shetani kitakuwa kimeisha kwa kipind hiki cha miaka saba tui li kwamba dunia iweze kuokolewa. Atakuwa amepewa kipindi hiki tena na Mungu ambaye amekiweka kipindi chake cha miaka elfu sita, na zawadi na wito wa Mungu ni mambo yasiyotenguka.

 

Ndipo Shetani atakuwa kipindi cha miaka saba tu cha kuwajaribu watu wote wakaao juu ya uso wa dunia.

 

Kuanzia mwaka wa 3018-3027 Shetani na malaika zake waovu watakuwa wameishaondolewa mbali na kupelekwa duniani na watakuwa wanaenda huku na huko ili wakayadanganye mataifa. Ataruhusiwa kuifanya kazi ya kuvuruga na kuwafanya watu wadharau Umuhimu wa kuitunza Torati tena. Kipindi hiki kifupi kitakuwa ni cha kazi za Shetani na kuukosesha ulimwengu wote na kuuasisha. Watakaoonekana kuwa ni tofauti kwenye kipindi hiki ni wale watakaokuwa ni wateule na waaminifu waliochaguliwa kutumika kwenye kazi ya kutoa dhabihu za Asubuhi wa Hekalu lililotajwa na nabii Ezekieli. Kundi hili linawawakilisha wateule walio kwenye Makanisa ya Mungu yatakayokuwa kwenye utaratibu huu wa kipindi hiki cha Milenia, na kwa kwa jinsi hiyohiyo ndipo Dhabihu ya Asubuhi iliyokuwa inatolewa siku za Agano la Kale ilikuwa inawakilisha Umati Mkubwa wa wale watakaokuwa kwenye Ufufuo wa Kwanza kilichopita kwenye vipindi vya yubile 40 za kuwa kwao jangwani. Maadhimisho ya Sabato, Miandamo ya Miezi, na Sikuzote Takatifu au Sikukuu Zilizoamriwa pamoja na Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa za mara 72 kwa mwaka, zinawakilisha wale Mababa zetu na Manabii na Wateule ambayo jumla yao ni watu 140,000 wanaowakilisha Makanisa ya Mungu (soma jarida la Mavuno ya Mungu, Sadaka za Mwandamo ya Mwezi, na Wale 140,000 (Na. 120), [The Harvests of God, the New Moon Sacrifices, and the 144,000 (No. 120)].

 

Idadi wa wale waliojiunga kuasi iliongezeka na kisha walienda mbele wakimwelekea Masihi na hiyo Kambi ya Watakatifu itakayokuwa mjini Yerusalemu. Mlolongo huu wa mfuatano wa mambo umeandikwa kwenye kitabu cha Ufunuo 20:7-9.

 

Ufunuo 20: 7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.

 

Kisha vifungu vigumu vya maandiko haya vinatokea kwa kuwa jina linalohusishwa lilisababisha mchanganyo kwa watu wengi ambao hawakuweza kuelewa Uzuri na Upendo wa Mungu na mpango wake alionao kwa Wateule na Wokovu mkuu wa viumbe wake wote, kwa nyanja zote mbili, yaani Kimwili na Kimbinguni.

 

10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.  

 

Andiko hili linafanya ionekane kana kwamba Shetani atatupwa kwenye Ziwa la Moto. Ufafanuzi na ukweli ni kwamba huyu Diabolos au ibilisi atatupwa katika Ziwa la Moto. Hii inaashiria kwamba Mungu atafanya kisasi kikubwa na ataawadhibu Shetani kwa hukumu ya milele na milele, lakini hivyo sivyo isemavyo Biblia kwenye maandiko yake ya Agano la Kale kuwili kote, yaani katika Isaya 14 na Ezekieli 28. Katika Isaya 14: 6-20 tunasoma unabii uliotolewa dhidi ya Shetani, alitajwa kwa lugha fumbo ya Mfalme wa Babeli, ambaye alitaka kujifanya yeye mwenyewe kuwa ni Mungu Mwenyezi au Aliye Juu ya Yote.

 

Kwenye maandiko haya, Shetani anawekwa kwenye kundi la Mfalme wa Babeli, Mtawala wa Ashuru na pia nchi ya Ufilisti inatabiriwa itaangamizwa na kuteketezwa na moshi huu utakaotokea pande za Kaskazini. Sayuni inafanywa mataifa yote yanayozunguka na kuitegemea, nah ii inahusisha malaika anayetafuta uwezi wa kujifanya yeye mwenyewe kuwa ni Mungu Mwenyezi aliyeletupwa chini kuzimuni. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba aliuawa lakini hakuzikwa. Na ambaye hatimaye alifanywa mwanadamu na alifanika kuwa ni kama dhaifu kama walivyo wao.

 

Isaya 14: 1 Maana Bwana atamhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena, naye atawaweka katika nchi yao wenyewe; na mgeni atajiunga nao, nao wataambatana na nyumba ya Yakobo. 2 Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta mpaka mahali pao wenyewe, na nyumba ya Israeli watawamiliki, na kuwafanya watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana; nao watawachukua hali ya kufungwa watu wale waliowafunga wao, nao watawamiliki watu wale waliowaonea. 3 Tena itakuwa katika siku ile, ambayo Bwana atakupa raha baada ya huzuni yako, na baada ya taabu yako, na baada ya utumishi ule mgumu uliotumikishwa; 4 utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema, Jinsi alivyokoma mwenye kuonea; Jinsi ulivyokoma mji ule wenye jeuri! 5 Bwana amelivunja gongo la wabaya, Fimbo ya enzi yao wenye kutawala. 6 Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu, Kwa mapigo yasiyokoma; Aliyewatawala mataifa kwa hasira, Ameadhibiwa asizuie mtu.

 

Kumbuka kuwa mara tu baada ya Mfalme wa Babeli kutwezwa chini na mfumo wake kuharibiwa, ndipo ulimwengu wote utabakia kwenye amani.

 

7 Dunia yote inastarehe na kutulia; Hata huanzilisha kuimba. 8 Naam, misunobari inakufurahia, Na mierezi ya Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti aliyetujia.  

 

Kwa hiyo, hii inaonyehs jinsi atakavyotwezwa. Viongozi wa Lebanon watakuwa ni walio kwenye ulimwengu war roho tu na nchi ya Lebanon itafungamanishwa kikamilifu kwenye mwili wa Israeli chini ya masihi. Pia kumbuka kuwa kaburi ambao pia hiutwa Sheol au Hades, litakuwa na matarajio ya kukutana na malaika huyu ambaye pia ni Lusifeli Mleta Nuru au Shetani, atakapokuwa anapelekwa chini shimoni, kuzimuni.

 

9 Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi.

 

Ndipo viongozi wanadamu watamwambia Shetani maandiko yafuatayo hapo atakapokuwa ameshushwa kuzimuni kaburini na mautini. Watajua kwamba amekuwa ni dhaifu kama walivyo wao na mamlaka au utawala wake aa mifumo yake yote itakuwa imeshushwa chini kuzimuni pamoja naye. Ameelezewa kinaga ubaga kwenye aya ya 12 kuwa yeye ni Lusifeli.

 

10 Hao wote watajibu na kukuambia, Je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! 11 Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. 12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!

 

Huyu hawezi kuwa ni kiumbe mwingine bali ni Shetani ambaye pia alijulikana kuwa ni Nyota ya Mchana au Nyota ya Asubuhi wa hapa Duniani. Kiumbe huyu hakosi atakuwa ni miongoni mwa Malaika waasi na waovu kama tunavyomuona kwenye andiko hili.

 

13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.

 

Kumbuka pia kwamba kiumbe huyu atakufa na atalala na funza wakimfunika chini na juu yake. Kwa hiyo anaonekana kuwa na haiba ya mwili wa kibinadamu. Pia kumbuka lile swali liulizalo: “Je, huyu sio yule mtu, nk.” Yeye ni mwanadamu, ila hatazikwa kama wafalme wa dunia hii wanaotukuka. Yeye pamoja na malaika wenzake waasi hafazikwi bali wanalala kwenye mawe ya dunia.

 

 16 Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme; 17 Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? 18 Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe; 19 Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu. 20 Hutaungamanishwa pamoja nao katika mazishi, Kwa maana umeiharibu nchi yako, Umewaua watu wako; Kizazi chao watendao uovu hakitatajwa milele

 

Kisha Bwana atatangaza hukumu kwa mfumo ule na kwa malaika wengine wote.

 

21 Fanyeni tayari machinjo kwa watoto wake. Kwa sababu ya uovu wa baba zao; Wasije wakainuka na kuitamalaki nchi, Na kuujaza miji uso wa ulimwengu. 22 Nami nitainuka, nishindane nao; asema Bwana wa majeshi; na katika Babeli nitang'oa jina na mabaki, mwana na mjukuu; asema Bwana. 23 Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema Bwana wa majeshi

 

Kumbuka kwamba mabaki yote ya Babeli yatakatiliwa mbali. Mfumo wake wa imani ya kuabudu Jua na Dini zake za Siri na Fumbo na mfumo wake wote wa imani ya kidini vitakuwa vimekomeshwa pamoja nay eye mwenyewe Shetani au Lusifeli.

 

Pia mfumo na taratibu za Kiashuru zitakuwa zimeharibiwa zote, lakini tunajua kwamba nchi ya Ashuru imetokana na mkono wa kaskazini na Israeli kwenye kipindi cha mwanzoni mwa Milenia, na ndio uliounda mfumo wa imani ya dini ya Babeli ambao umetangazwa kuwa “umeanguka” kwenye ufunuo sura ya 18.

 

24 Bwana wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea; 25 kwamba nitamvunja huyo Mwashuri vipande vipande katika nchi yangu, na juu ya mlima wangu nitamkanyaga chini ya miguu yangu; ndipo nira yake iliyo juu yao itakapoondoka, na mzigo wake utatoka mabegani mwao. 26 Hilo ndilo kusudi lililokusudiwa duniani mwote, na huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote. 27 Maana Bwana wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma?

 

Kumbukakwamba utaratibu huo ni kwa mataifa yote na ni Mungu ndiye anayeukomesha. Hii ni dini ya waabudu Jua na na walio kwenye vuguvugu la Ibada za miungu mingine ya kipagani ambazo zomejiingiza kwenye mataifa kwa kupitia imani ya Utatu na Dini nyine zilizoko kwenye mataifa hayo, yakiwemo mafundisho ya Hadithi ya Waislamu.

 

Wakati unabii kuhusu nchi ya Ufilisti na Palestina ulipofuatia kutolewa. Walikuwa wamepunguzwa na kuwa kama hakuna kit una hatimaye wakafanyika kuwa ni sehemu ya Ufalme wa Sayuni chini ya Masihi kwenye kipindi cha mwanzoni mwa Milenia.

 

28 Ufunuo huu ulikuja mwaka ule alipokufa mfalme Ahazi. 29 Usifurahi, Ee Ufilisti, pia wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye 30 Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa. 31 Piga yowe, Ee lango; lia, Ee mji; Ee Ufilisti, pia wote, umeyeyuka kabisa; Maana moshi unakuja toka kaskazini, Wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake. 32 Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa Bwana ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake wataona kimbilio.

 

Hatimaye tunajionea kwenye kitabu cha nabii Ezekieli ile sura ya 28 ikisema kwamba Lusifeli anajifanya kuwa kama Kerubi lililotiwa mafuta na wakfu ambaye hatimaye anatupwa hadi hapa chini duniani

 

Ezekieli 28 1 Neno la Bwana likanijia tena, kusema, 2 Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu. 3 Tazama, una hekima kuliko Danieli; hapana neno la siri watu wawezalo kukuficha; 4 kwa hekima yako na kwa fahamu zako umejipatia utajiri, nawe umepata dhahabu na fedha katika hazina zako; 5 kwa hekima yako nyingi, na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, na moyo wako umeinuka kwa sababu ya utajiri wako; 6 basi, kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu; 7 basi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watautia uchafu mwangaza wako. 8 Watakushusha hata shimoni; nawe utakufa kifo chao waliouawa kati ya bahari.

 

Kumbuka pia kwamba inaposemwa kwamba yeye ni mungu na ambaye ameletwa hapa chini na kuuuawa kwa kuchinjwa kwa ajili ya wanadamu. “Mfalme wa Tiro” ni jina lingine la Shetani. Mungu amamtweza kwenye unabii na kumuuliza: “Je, utaweza bado kusema kuwa mimi ni mungu mbele ya hao waliokuua?”

 

9 Je! Utazidi kusema mbele yake huyo akuuaye, Mimi ni Mungu? Lakini u mwanadamu, wala si Mungu, mkononi mwake akutiaye jeraha.
10 Utakufa kifo cha hao wasiotahiriwa, kwa mikono ya wageni; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.

 

Tena kwa hali hii Mfalme wa Tiro anajulikana kama kuumbe aliyekuwa huko Edeni, kwenye Bustani ya Mungu. Aliwekwa huko na mlinzi aliyewekwa wakfu rasmi ambaye ni Kerubi wa Mungu. Walikuweko viumbe wawili wa wadhifa huu waliowekwa pale, na mmoja wao alikuwa ni Masihi kipindi alichokuwa kabla ya kuzaliwa kwake na mwingine alikuwa ni Shetani. Kwa hiyo kiumbe huyu Shetani hatimaye atakufa kama wafavyo wanadamu wote.

 

11 Tena neno la Bwana likanijia, kusema, 12 Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri. 13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. 14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. 15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. 16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. 17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.

 

Kumbuka kwamba Mungu yeye, Shetani, amepatia unajisi patakatifu pake kwa maovu na dhambi zake nyingi. Kisha tazama jinsi Mungu alivyomfichua.

 

18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao

 

Kumbuka kwamba hatimaye Mungu alikichukua kiumbe hiki kwenye mwisho mbaya sana na kwamba hatakuweko tena milele.

 

 19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.

 

Kwa hiyo tunaona kwamba kiumbe hiki hatimaye kimefikwa na msiba mkuu sana mwisho wake na hakitakuweko tena kabisa milele. Kwa hiyo la kujiuliza ni kwamba, je, ni horo gani hii ya Diabolos itakayoangamizwa na kuzamishwa kabisa kwenye Ziwa la Moto?  Jibu ni kwamba: ni roho ya Shetani ambayo itaondolewa ili ashughulikiwe yule kiumbe ambaye hatimaye alifanyika kuwa Shetani na ambaye hapo nyuma alikuwa ni mkamilifu tangu siku alipoumbwa. Basi kiumbe huyu atauawa na hatimaye yeye pamoja na viumbe wengine miongoni mwa wale Makaila Waasi watafufuliwa wakiwa kama wanadamu wa kawaida na watakuwa kwenye upande wa watu wote watakaofufuliwa pamoja nao. Mabadiliko haya yameonekana kwenye mfano fumbo wa Tiro hadi Sidoni ambako Mungu aliuonysha Utukufu wake katika Sidoni lakini kwa utakatifu wake na kwa kule kuonekana kwake kwa watu, ndipo kila mtu atajua kuwa yeye ni Mungu aliyeko peke yake na kwamba hakuna Mungu mwingine zaidi yake.

 

20 Neno la Bwana likanijia, kusema, 21 Mwanadamu, uuelekezee Sidoni uso wako, ukatabiri juu yake, 22 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee Sidoni, nami natukuzwa kati yako; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu ndani yake, na kutakasika ndani yake. 23 Maana nitampelekea tauni, na damu, katika njia kuu zake, na hao waliotiwa jeraha wataanguka kati yake, kwa upanga juu yake pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.

 

Kisha kwenye maandiko haya ya unabii, Mungu anawarudia Israeli pale anaposema kwamba wajirani wote wa Israeli hawataweza kuwaumiza na kwamba ndipo watajua kwamba yeye ndiye BWANA Mungu.

 

24 Wala hautakuwapo mchongoma uchomao kwa nyumba ya Israeli; wala mwiba uumizao miongoni mwa wote wamzungukao, waliowatenda mambo ya jeuri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.

 

Kwa hiyo, mataifa watajua kwa jinsi Mungu atakavyoingilia kati na Ufufuo wa Israeli ambao mfumo wa kidini utawekwa  na Masihi na ambao utabidi kufuatwa, na ndpo mafundisho ua uwongo ya Hadithi za Kiislamu na Utatu wa Wakristo vitakavyodhihirika kuwa ni ya uwongo, sawa na mafundisho mengine ya Talmudi yaliyo kwenye imani ya Kiyahudi, haya yote yataondolewa mbali.

 

25 Bwana MUNGU asema hivi; Nitakapokuwa nimewakusanya nyumba ya Israeli, na kuwatoa katika watu ambao wametawanyika kati yao, na kutakasika kati yao machoni pa mataifa, ndipo watakapokaa katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu, Yakobo. 26 Nao watakaa humo salama; naam, watajenga nyumba, na kupanda mashamba ya mizabibu, na kukaa salama; nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu juu ya watu wote, wanaowatenda mambo ya jeuri pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao.

 

Kwa hiyo inaonekana wazi kutoka kwa mashahdi hawa wawili walio kwenye Biblia kuamini kwamba Shetani atapelekwa kaburini na kuuawa kama mwanadamu. Roho hii ingeweza kuondolewa na akangojea Ufufuo wa Pili wa Wafu akiwa kama kiumbe mpya aliye tayari kurekebishwa na kufundishwa hadi kuufikia wokovu pamoja na Malaika Waasi wengine wote waliomfuata na ambao hawakuweza kutubu kwa kipindi kile.

 

Mwisho wa Kipindi cha Milenia

Hapa ndipo vita ile ya mwisho iliyopelekea kipindi hiki cha Milenia itakomeshwa. Nasi tutabakia na wafu wote walioasi hapo kabla na ambao watakuwa  wa namna zote mbili, yaani walio wakimwili na wakiroho ambao ni Wateule Hai ambao hawakuasi, tutakaokuwa na Masihi na Wateule waliotokana na Ufufuo wa Kwanza. Wale Wateule walio sehemu ya Ufalme wa Mungu lakini walikufa kabla ya mwisho wa Milenia, katika mazingira ya au kwa hali iliyokuwa mwanzoni mwa Milenia, watakuwa kwenye kundi moja na wafu wengine wote waliobakia.

 

Kwenye kipindi cha mwishoni mwa Milenia, dini potofu ya upotevu nay a siri itakuwa imerejeshwa upya tena na Shetani na dini kuu inayoamini mzunguko wa kimaumbile wa viumbe vyote na uzawa w amara nyingi wenye mabadiliko tu ya kimaumbile na kiviumbe (reincarnation) itakuwa imeandaliwa kwa ajill ya Ufufuo wa Pili. 

 

Ni katika kipindi hiki ndipo utamaliziwa ule mlolongo wa mambo ya ufufuo.

 

Ufufuo wa Pili

Kila mtu aliyewahi kuishi hapa duniani atakuja kufufuliwa ili awe na mwili unaoishi, kama ilivyotokea kwenye tukio la Ufufuo wa Kwanza. Na ndipo watagawanywa kwenye makundi mawili.

 

Ufunuo 20 inasema. 11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

 

Kundi la kwanza ni la wale waliostahili kuitwa wana wa Mungu. Hawa ni wale waliobadilishwa na kuwa ni viumbe katika ulimwengu wa roho na kushiriki kwenye hukumu ya wana wa Mungu.

 

Kundi lingine ni la wale waliowahi kuishi hapa duniani na walikuwa ni wa uzao wa Adam una ambao walifufuliwa wakiwa ni viumbe wenye uhai na wanaoishi, wakiwemo wale malaika wote Waasi ambao hawakutubu.

 

Kwenye kundi hili walikuwepo pia waumini kutoka kwenye Makanisa ya Mungu ambao walionekana kutokuwa na sehemu kwenye ufufuo wa Kwanza na hawakuwa na sehemu kwenye kipindi kile cha Milenia. Hawa ni wale wanaoitwa ni wa zama za kanisa la Sardi na la Laodikia au twaweza kuwaita kuwa ni wale waliosababishwa kufanya makosa na watu wengine (kama inavyosema Ufunuo 3). Ni makosa makubwa sana kuamini kuwa dhana ya Ufufuo wa Tatu ni ya Mungu kama wanavyodhania kwamba ndicho kipindi ambacho atawafufua waliosalia wote na kuwachoma kwenye Ziwa la Moto kama ndiyo adhabu yao. Mafundisho haya mapotofu yamekuwa yakifundishwa sana kwenye karne ya 20 kweny Makanisa haya haya ya Mungu. Mungu hana tabia ya kuhurumia hivyo na wala hana tabia ya kugeuza geuza mambo. Bali yeye ni Mungu mwenye Uweza wote (Omnipotent), na Anajua mambo Yote (Omniscient) na ni Mkamilifu na wa Uhakika. Makosa haya yameelezewa kwenye jarida la Uzushi wa Ufufuo wa Tatu (Na. 166) [The Fallacy of the Third Resurrection (No. 166)].

 

Kiti Kikubwa cha Enzi Cheupe cha Hukumu

Walioitwa ni wengi bali Wateule ni wachache na wale ambao hawajachaguliwa ndipo watakapo ufufuliwa na hatimaye watapewa fursa ya pili ya wokovu. Hiki ndicho kipindi chao mwafaka cha kuitwa kwao na kuhukumiwa kwao na kuokolewa pia.

 

Ulimwengu mzima wa wale wote ambao hawakuwa na fursa ya kuokolewa na ambao wameenea kwenye vikundi mbali mbali vya makabila na kwenye familia kubwa kubwa na ambao wamefundishwa tena sawasawa na inavyosema sheria na ushuhuda.

 

Watapaswa kufundishwa upotofu ulio kwenyey mafundisho mapotofu ya imani za kuamini Uzaliwa mwingine (Reincarnation) na mafundisho ya kizushi ya Waanimism, Washamanism, Wabuda, Wahindu na Hadithi za Kiislamu na Ukristo wa Kiantinomian unaoamini kuwa Maarifa yanaweza kumwokoa mtu na Dini nyingine za Siri za waabudu Jua.

 

Wadante walikuwa na mapapa wa daraza za chini sana za jehanamu lakini sisi tutawapa tu mavazi na kuwaambia warudi tena shuleni pamoja na watu wote waliowapokea. Ili kuwalinda na waalimu wengine wote wa uwongo inaweza kuwa kazi ngumu sana kwenye kipindi cha kwanza, wakati watu watakapokijua kile walichowafanyia, na hasa walichoyafanyia Makanisa ya Mungu yaliyopotoshwa kwa mafundisho ya uwongo.

 

Kusudi la Hukumu hii inalenga hasa kuwaelimisha na kuwarekebisha wanadamu na kizazi cha malaika, kwa ajili ya makosa yao na kuwatayarisha kwa ajili ya uzima wa milele wakiwa ni wana wa Mungu wakiwa kama elohim. Ni kwa sababu hii ndiyo Mungu alimtuleta Kristo, kwanza kabisaa ili ashughulike na kuziondoa zambi zetu na pili ni kuwaokoa wale wote watakaokuwa wanamngojea kwa hamu.

 

Kwa mwisho huu, malaika hawa waasi na wanadamu watawekwa kwenye kiwango kimoja tu cha hukumu. Lakini sio mpango wa Mungu kuona mwenye mwili yeyote akipotea na kwa hiyo tunakabiliwa na kazi ya kuuelimisha tena umma wote wa watakaokuwa kwenye Ufufuo wa Pili. Wote haw ani wale walio kwenye umbo la mwili la kibinadamu; kama wale wasofanya toba na ambao hawakurekebika na kukubali kuzishika amri za Mungu kupitia kwa Masihi ambaye ni kiongozi wao na hawataweza kuishi hai na kukutwa na Mauti ya Pili

 

Wote watakaokuwa kwenye Ufufuo wa Pili watakutana na mambo wanayostahili kuwanayo wale walio kwenye kundi la walio kwenye Mauti ya Pili kama hawatatubu na kuupokea wokovu.

 

Kila mmoja miongoni mwa wtu hawa atapewa kipindi cha miaka 100 cha hukumu ya Mateso au Kurudiwa kwa wale watakaokuwa wamefufuliwa wakiwa na umri wa miaka 20. Na kila ambaye hakuwahi kuishi, pasipo kujali umri waliokuwa nao wakati wanakufa, hata watoto wadogo sana kama nusu mamba, watapewa maisha mapya kama watu wazima waliokomaa na kisha wataishi miaka 100. Mwishoni mwa miaka hii 100, kila mtu atakayekuwa hajakamilisha Hukumu na kuupokea wokovu wa Masihi atakufa. Na miili yao itatupwa na kuchomwa kwenye Ziwa la Moto.

 

Tendo hili litawajumuisha Malaika Waasi ambao hapo mwanzoni walikuwa na Shetani. Hata Shetani atapewa fursa ya kutubu. Ni kwa ajili hii ndipo Kristo alitoa mfano wa mwana mpotevu (soma majarida ya Kondoo Aliyepotea na Mwana Mpotevu (Na. 199) [Lost Sheep and the Prodigal Son (No. 199)] na Hukumu ya Mapepo (Na. 80) [The Judgment of the Demons (No. 80)].

 

Ndiyo maana mwishoni Kristo alikwenda Kuzimuni (Tartaros) baada ya kufufuka kwake na kuwahubiri mapepo waliokuwa wanashikiliwa kule Kifungoni.

 

Kila mtu ataweza kuishi. Mungu aliyajua maasi ya hawa malaika na alipanga kuwa Watu wote wapate kuokoka na Kristo alisulibiwa kama kondoo wa kuchinjwa tangu kuwekwa kwa misingi au kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu.

 

Sisi sote tulichaguliwa na kutengwa kwa makusudi mazima ya Mungu na tuliitwa kwa kipindi muafaka. Kila mmoja wetu aliwekwa wakfu na kutengwa na kazi zetu zilijulikana na kubarikiwa kipindi tukiwa hatujawahi hata kutungwa kwa mamba zetu tumboni mwa mama zetu (kama isemavyo. Yeremia 1:5 na pia Warumi 8:29-30).

 

Na ndiyo maana wengine wameachea na hawajaitwa na watakuwemo kwenye Ufufuo wa Pili. Watu wengi wamekuwa hawana Roho Mtakatifu na kujua kwamba wateule wanapaswa kujikana na kujitoa kwa ajili ya wokovu wa wale waliokuwa hawajaishi bado, akiwemo Shetani na Malaika wake Waovu. Usipojitoa ili kulifanikisha jambo hilo, hautakuwa tayari kwa ajili ya Ufufuo wa Kwanza na kuwa na sehemu yetu kama wateule na wana wa Mungu. Hata hivyo, Mungu hakusema kwenye kitabu cha Zaburi, na Kristo akatuambia imeandikwa kwenye Torati yetu kwamba Mimi nimesema, Ndinyi miungu (elohim), Wana wa Aliye Juu na maandiko hayawezi kutanguka (Yohana 10:34-35; sawa na Kutoka 22:9,28 na Zaburi 82:6). Andiko hili la kwenye Zaburi linahusisha na Malaika Waasi watakao “kufa kama wanadamu na kuanguka kama mmoja wa wafalme”

 

Ni Shetani ndiye aliyewafundisha wanadamu kwamba Malaika Waasi hawatakufa kwa kuwa wao ni roho. Hii ni propaganda tu ya kuwafanya mapepo wasitubu. Hakuna fundisho popote lililokazana kukataza au kuzuia kimaandiko kuwa mapepo wanaweza kutubu. Mapepo wanaishambulia kila inapoonekana. Kuwa hiyo kuna makundi mawili ya mwisho wa Kiti Kikuu cha Enzi Cheupe cha Hukumu. Wale waliokwisha kupita kwanza na wakiwa wameukubali na kuupokea wokovu na kubadilishwa miili yao, na kambi nyingine ni ya wale waliokataa kutubu na wakafa tu na kuchomwa moto. Lakini siyo mapenzi ya Mungu kuwa watu wapotee na kuonyesha kwamba sio mapenzi yake. Kwa kweli, wale walioshindwa kuamini na kuishi kwenye imani hadi mwisho hawatakuwa na sehemu kwenye huu Ufufuo wa Kwanza kwa kuwa walikuwa wanayapinga mapenzi ya Mungu. Hata hivyo, wale wote walio kwenye Ufufuo wa Pili watakabiliwa na Mauti ya Pili na kufa moja kwa moja, wakiwemo papepo.

 

Na ndiyo maana fudisho la kuzaliwa tena lilifundishwa na mapepo wakikususia kuwadanganya wale walio kwenye Ufufuo huu wa Pili. Wale wote walio kwenye kipindi hiki cha Milenia na Ufufuo wa Pili watazitunza Sabato, Miandamo ya Mwezi, na Sikukuu Zilizoamriwa kwa kuifuata Kalenda ya Mungu. Na wale wasiozitunza hawataishi.

 

Mji na Makao ya Mungu

Mara baada yah ii dunia kusafishwa na wacahmungu wote kubadilishwa miili yao na kuwa wana wa kiroho wa Mungu, ndipo sasa itakuwa tayari kwa kurudi na kuja kwa Mungu hapa duniani kwenye Mji na Makao ya Mungu (soma marida la Mji na Makao ya Mungu (Na. 180) [The City of God (No. 180)]

 

Mara tu baada ya kutokea hili ndipo atakwenda kuutawala ulimwengu huu na dunia ikiwa ni kituo chake kikuu cha uumbaji wake wote na akiutawala ulimwengu wote kutoka katika Mji au Makao yake Mungu..

 

q