Makanisa ya
Kikristo ya Mungu
[178]
Zaburi 110
(Chapisho La 2.0 19970904-20000712-20070509)
Zaburi hiI fupi lakini ni ya muhimu sana. Sura hii ni moja
kati ya sua 134 zinazipotoshwa na Wasoferim ambayo kwayo Yahova (au Yehova)aligeuzwa
jina lake na kuitwa Adonai. Ilianza kwa kutambulisha kwamba hii ni Zaburi ya
Daudi. Lakini aya haimtaji Daudi bali inamtaja Bwana wa Daudi. Na mtu huyo ni
Masihi, na ndiye anayetajwa kama Yehova kwenye
Zaburi ya 110:5 na neno hili lilibadilishwa na kuwa Adonai kama tutakavyoona.
Christian
Churches of God
PO Box 369, WODEN
ACT 2606, AUSTRALIA
Email: secretary@ccg.org
(Hati
Miliki © 1996, 2000, 2007 Wade Cox)
(tr. 2014)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili
yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama
yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la
haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa
au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi
zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya
lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.
Jarida
hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Zaburi 110
Zaburi
110:1-7 Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata
niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako. 2 Bwana
atainyosha toka Sayuni Fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako; 3 Watu wako wanajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa
uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako. 4 Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele,
Kwa mfano wa Melkizedeki. 5 Bwana yu mkono wako wa
kuume; Ataseta wafalme, Siku ya ghadhabu yake. 6 Atahukumu
kati ya mataifa, Ataijaza nchi mizoga; Ataseta kichwa katika nchi nyingi. 7 Atakunywa maji ya mto njiani; Kwa hiyo atakiinua kichwa
chake.
Zaburi hiI fupi lakini ni ya muhimu sana. Sura hii ni
moja kati ya sua 134 zinazipotoshwa na Wasoferim ambayo kwayo Yahova (kimakosa
kabisa alitajwa kwa jina la Yahwe au Yehova) andiko lililo kwenye sura ya 110:1
linatumia mtaji wa adoni, ukweli wa
kwamba umetumika na Waunitariani wenye itikadi kali ili kuonyesha inaashiria
kwamba neno Bwana kwa masuala ya
kibinadamu mwenye umbo la mmiliki, bwana au bwana. Hata kamusi ya Strong
inaorodhesha hii kwa hivi ndivyo ilivyo. Hatahivyo, mfananisho huu usio na
mashiko ulikataliwa na Bullinger akionyesha kuwa ilivyomtaja waziwazi Adonai akiwa
ndiye aliyeketi Mkono wa Kuume wa Mungu. Neno lililotumika kwenye Zaburi 110:5 asili
yake lilikuwa linamtaja Yahova lakini
lilibadishwa na kuwa Adonai kwa muundo uleule wa kiuandishi wa neno Adoni kama inavyoonekana kwenye
Zaburi 110:1 na inamaanisha Adonai na inamtaja Yahova.
Zaburi hii inashughulikia kwa wazi viumbe wawili wa
mbinguni ambao mmoja wao ni mdogo kwa mwingine na akiwa amekei kwenye mkono wa
kuume wake. Huyu mdogo pia anaitwa Yahova (rejea kwenye jarida la Malaika
wa YHVH (Na. 24) [The Angel of YHVH (No. 24)]. Wasoferimu
walibadilisha jina Adonai ili kuupa mashiko ukweli wa umbunguni wa Masihi kwa
kumshirikisha na Yahova kuwa ni Mungu wa Pekee na wa Kweli. Inaanzia na utambulisho
kwamba Zaburi hii ni ya Daudi. Wakati kwamba aya hiii haimtaji kabisa Daudi
bali Bwana wa Daudi. Hivyo basi, mtu aliyekusudiwa hapa ni Masihi. Baraza la
marabi wanalitumia andiko hili kwa ufafanuzi ujnaomtaja Ibrahimu wakihusianisha
na kitendo chake cha kuonana na Melkizedeki kwenye aya ya 4 (tazama ufafanuzi
wa Soncino kuhusu Zaburi hii (kurasa za
371-372) na kumbukaa pia kitabu cha Kienrania cha MT kwenye aya zotte mbili). Hata
hivyo, Ibrahimu alimpa zake Melikizedeki kwa hiyo tunalazimika kumtaja Masihi
hapa na huduma yake ya kikuhani ambaye ni Ibrahimu ni mdogo kwake. Anatajwa
kuwa ni Yahova (au wengine wanamuita Yehova) kwenye Zaburi 110:5 na hii
ilibadiloishwa kuwa Adonai kama tutakavyoona huko mbele.
Zaburi 110:1 Neno
la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui
zako Kuwa chini ya miguu yako.
Hapa Yehova anamwambia kiumbe anayeitwa Bwana Wangu (Adoni)
ambaye ndiye Bwana wa Daudi. Kiumbe huyu ni Adonai. Namna ya kiuandishi
iliyotumika kumuelezea kiumbe huyu mtakatifu kwa Kiebrania kama kiumbe mwingine
lakini mmoja akielezewa kwa kufananishwa na mwanadamu na mwingine akielezewa
waziwazi kuwa ni Yahova kana kwamba hili
lilikuwa ni neno la asili. Kwa hiyo Waserafimu waliibadlisha andiko hili.
Andiko hili limenukuliwa kutoka kwenye Mathayo 22:41-46, Matendo 2:34-35 na Waebrania
1:13.
Huyu Yehova
anayetajwa hapa ni Yehova ne’um. Hizi
kwa kweli ni semi au lugha za Kinabii zinazotumika kumtaja Yahova. Mara zoe
zinatumika kwa usemi wa haraka na wa moja kwa moja kumjata Yehova na mara chache
kwa nabii (kama kwenye Hesabu 24:3,15), au Daudi (katika 2Samweli 23:1) (tazama
kwenye Companion Bible, fn. to v.1). Huyu
Bwana Wangu anayetajwa hapa ni Bwana
wa Daudi, yaani Masihi. Kwa hiyo, Nasihi alikuwa ni Bwana wa Daudi, wakati ambapo bado alikuwa
kwenye mlolongo wa kizazi cha mababu zake. Mwishoni mwa Zaburi kwenye aya za 5-7
inaonyesha ulikuwa ni unabii na ulikuwa haujatimilika bado.
Mathayo 22:41-46 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo? 42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. 43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, 44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako? 45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? 46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.
Kwa hiyo alikuwa amewekwa wakfu tayari tangu mwanzo, ili
aweze kumuombea Daudi na huku akiwa wa uzao wake pia (tazama pia jarida la Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa
Kwake Kimwili (Na. 243) [The Pre-Existence of Jesus Christ (No. 243)].
Andiko linalosema, Uketi
mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako. limenukuliwa
mara saba kwenye Agano Jipya (Mathayo 22:44; Marko 12:36; Luka 20:42; Matendo
2:34; Waebrania 1:13; 10:13; 1Wakorintho 15:25). Kifungu hiki kinatokana na
neno lenye maana sawa na kusema kuseta miguu shingoni mwa adui (kama kwenye Yoshua
10:24).
Inamaanisha kuwaseta maadui zake Masihi chini ya miguu
yake. Kwenye Agano Jipya la Kiyunani limetumika neno tithemi linalomaanisha ni
lazima atawaseta (tazama kwenye Companion
Bible, ibid.). 1Wakorintho 15:25 inachukuliwa kuwa ni aya ya pekee kuelezea
kipindi atakacho sio tu kwamba atawaseta miguuni pake bali chini ya miguu yake kitakapofika kipindi cha utawala wake
Kristo mwenyewe (Mathayo 25:31; Ufunuo 3:21) inatajwa kwenye andiko lile badala
ya kusema katika kipindi atakachokuwa Baba yake kwenye Kiti chake cha Enzi,kama
ilivyoonekana kuandikwa maeneo mengi (ibid.). Kitabu cha fafanuzi cha Soncino kinaepuka
kuonyesha nia ya Masihi kwenye zaburi hii.
Zaburi 110:2 Bwana atainyosha toka Sayuni Fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako;
Neno fimbo ya nguvu
ni usemi wa Kiebrania unaomaanisha kwa
fimbo yako yenye uweza au fimbo ya
kifalme yenye uweza mkubwa (tazama kitabu cha fafanuzi cha Soncino). Tunatakiwa kushughulikia
fimbo kuu yenye uweza wa kufanya kazi zote inayofanya kazi mbili zote, yaani ya
kikuhani nay a kifalme, na aliyopewa Masihi hapa akiwa ni mwana wa Daudi.
Sayuni inayotajwa hapa ni kitovu cha ufalme wa Masihi (sawa
na Warumi 11:25-27). Andiko linalosema, utawale
katikati ya maadui zako, likiwa limewekewa alama ya mkato au koma, linamaanisha
kuwa ni neno linaloashiria amri kutoka kwa Mungu (Soncino).
Warumi 11:25-27 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.
Andiko hili linapaswa kulinganishwa na lile la Isaya 59:20
na Luka 21:24. Kuja kwa Masihi huko Sayuni na kwa wale watakaoacha maovu katika
Yakobo. Kwa hiyo, kwa muda wake uliokusudiwa wa nyakati za mwisho za Mataifa,
Masihi atakuja kuwakomboa Israeli na kuuanzisha mfumo na utawala wake kutoka
Sayuni.
Zaburi 110:3 Watu
wako wanajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea
tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako.
Usemi unaosema watu
wako watakuwa tayari siku hizo za mamlaka yako linamaanisha kwamba watajitoa
kwa hiyari ya mioyo yao yote katika siku
utakazokuwa mtawala. Watakuwa ni sadaka ya hiyari ya aina kama iliyoko
kwenye Kutoka 35:29; 36:3; 1Nyakati 29:9,14,17; Ezra 3:5; 8:28. Hii ina chanzo kimoja na
ile ya Waamuzi 5 (Soncino). Neno uweza
wako linamaana alisia ya kusema jeshi
lako. Kipindi hiki kwa usemi wa wazi ni wa kipindi cha jeshi la Bwana la
Siku za Mwisho. Watu watatoa mifugo yao kwa kiwango chake halisi (cf. Soncino).
Maneno yasemayo uzuri wa utakatifu yanaonekana kuonekana kwenye
maeneo au sehemu za ndani (au juu) [fn.
v. 3). Soncino inadai kwamba ayah ii inamaanisha kwa heshima ya utakatifu, sawa
na Zaburi 29:2; 96:9. Heshima ya utukufu ni vazi la kikuhani (Soncino) – ambayo
kwamba ile kanzu au vazi jeupe ya wateule. Jopo la marabi liligawanyika
kimtazamo kwa kuihusianisha hii na Daudi. Lakini tafsiri za kina Kimchi na
Hirsch zimetafsiri mkuu wa patakatifu wakilihusisha
andiko hili na mji wa Yerusalemu.
Andiko hili linaielezea kama [kama umande] utokao tumboni kabla ya asubuhi nilokuzaa wewe [mwana]
(sawa na Zaburi 2:7). Ilipaswa kusiwe na alama ya nukta baada ya neno asubuhi. Tunashughulikia wazo la mwana
ambaye alikuwepo tangu mwanzo hata kabla ya kuzaliwa kwake duniani, na kuwekwa
wakfu kabla ya asubuhi au hata kabla ya nyakati za umilele. Ana umande wa mwana
(hapa anaonekana akiwa kijana) (tazama
tafsiri ya Companion Bible).
Zaburi 110:4 Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.
Hapa neno
upanga linahusiana na lile lililo
kwenye aya ya 1 kama Unabii au Fikra za Mungu. Hapa tunaona kwamba Masihi aliwekwa wakfu kuwa kuhani wa
milele baada ya kufanyika hivyo Melkizedeki (soma Mwanzo 14:18; Waebrania
5:6,10; 6:20; 7:1-28). Marabi wanajaribu kuifananisha hii na Daudi kwa kujaribu
kuiepusha na ukweli wa kwamba ni Masihi aliyekusudiwa na kitendo cha kuhamisha
huduma ya kikuhani. Kuweka mashiko jambo hili kunachukuliwa na inavyosema 2Samweli
8:18 ambapo limetumika neno cohen linalomaanisha
wana wa Daudi na ambalo linalenga viongozi
wakuu—lakini neno cohen. Madhaifu
ya Daudi ni mifano yenye kuonya (2Samweli 6:14) na alitoa sadaka za kuteketezwa
na sadaka nyingine za amani (2Samweli 6:17). Hata hivyo, hii ilikuwa ni kazi ya
Mfalme kama tunavyoona kwenye Ezekieli na pengine pengi na haihusiani na uanzishaji
wa utaratibu mwingine wa kikuhani. Tunaona kwenye Agano Jipya kwamba utaratibu
na kazi hii alipewa Masihi na kutoka kwa yeye likapewa Kanisa. Walawi
walitafsiri jambo hili kimakosa. Tafsiri ya Companion Bible inatafsiri vibaya maana
ya ukuhani hapa pia. Ulifunguliwa kwa Wamataifa wasio na uhusiano wa kinasaba
na usio na mwanzo wala mwisho. Ukuhani wa Haruni uliendelea kwa kupia kizazi
kimoja hadi kingine kwa kufuata nasaba ya kuzaliwa hadi kutoka Lawi. Masihi
alikuwa ni wa ukoo wa Daudi na Daudi hakuwa wa ukoo wa kikuhani. Masihi alikuwa
wa ukoo wa Lawi pia kupitia ukoo wa nyumba ya mama yake (tazama jarida la Kizazi
cha Masihi (Na. 119) [Genealogy of the Messiah (No. 119)]. Alitabiriwa kuwa
atatoka ukoo wa Lawi kupitia kwa Shimei, na kwa Daudi kupitia Nathan (soma Zekaria
12:12). Ukuhani wa Haruni ndio ulioenea kwenye mbadilishano huu ulijumuisha sio
Yuda peke yao bali ni kwa Israeli na kwa Wamataifa. Mungu hatajutia wala
kujilaumu kwa yule aliyemchagua (tazama pia jarida la Melkizedeki (Na. 128) [Melchisedek (No. 128)].
Zaburi 110:5 Bwana yu mkono wako wa kuume; Ataseta wafalme, Siku ya ghadhabu yake.
Andiko hili
lilibadilishwa na Wasoferimu kutoka kwenye jina Yahova (au Yehova (kutoka) mkono wako wa kuume na isomeke Adonai mkono wako wa kuume (soma
machapisho ya Nyongeza au Appendix 32 hadi kwenye tafsiri ya Companion Bible kwenye orodha hiyo). Ubadilishaji huu ulifanywa
kwa kuwa kulikuwa na jina lililoonekana wazi la Yahova (au Yehova) ambaye
alikuwa ni mdogo kwa Yahova wa Majeshi ambaye ndiye alikuwa Bwana wa Daudi, Masihi,
ambaye pia anatajwa kama Yahova lakini sio Yahovi (au Yehovi) ambaye ndiye Yahova
wa Majeshi. Tofauti hii imefunikwa na neno au jina la Yehova (SHD 3068) na Yehovi
(SHD 3069). SHD 3068 kila mara linakosewa kwa kuitwa Adonai na Yehovi (Yahovi)
(SHD 3069) kila mara inalikita elohim inapokuwa inataja. Kwa namna hii Wayahudi
walitafuta kulinda hadhi yenye ukweli kuhusu umoja wa Mungu kwa jina la Yahova wa
Majeshi (soma kamusi ya Strong’s ili
kupata ufafanuzi zaidi). Yahovi (Yehovi) kwa hiyo alikuwa ndiye Mungu wa
Majeshi Aliye Juu sana. Yahova (Yehova) alikuwa ndiye elohim wa Israeli akiwa
ni msaidizi wa mambo ya mbinguni. Kwa hiyo, Masihi atawashinda wafalme wote
itakapofika siku yake iliyowekwa tayari kwa ajili yake (maarufu kama siku ya
hasira ya Bwana Mungu) iwakayo.
Zaburi 110:6 Atahukumu kati ya mataifa, Ataijaza nchi mizoga; Ataseta kichwa katika nchi nyingi.
Masihi ndiye hakimu atakayeyahukumu mataifa (pamoja na
Wamataifa). Hebu na awahukumu watu wote [maeneo
yote] yatakuwa yemefurika mizoga mingi (tazama vitabu vya kina Kimchi, sawa
na Soncino). Kwa hiyo, vifo vya wengi vimetabiriwa vitatokea. Neno la Kiebrania
limetumika kuelezea miili ya waliokufa limemaanisha sawa na waliiohai
walioandikwa kwenye (Mwanzo 47:18) na mili iliyokufa au maiti. Ibn Ezra anaelewa
hivyo kwa mtazamo au uelewa wa kale, mataifa yatakuwa na nguvu za kiidadi. Wengine
wanafikiri kuwa inataja au imanaanisha mizoga ya waliochinjwa au kuuawa. Hirsch
anaelewa kuwa hii inawalenga wahanga walio kwenye mataifa waliokuwa wanawadhulumu.
Mpango wa Wokovu unaonyesha kwamba itakuwa ya namna zote mbili (tazama hasa
Ufunuo 20:1-15). Masihi atawaondoa viongozi wa mataifa. Kwa hiyo, maongozi ya
mfumo wa dunia yataondolewa. Kichwa kimoja peke yake ambacho ni mfano wa
Shetani na kuangamizwa kwa utawala na dini ya mnyama itakayokuwa chini ya imani
na mafundisho ya nabii wa uwongo wa Siku za Mwisho (Ufunuo 19:11-21). Hii inaelezea
pia uzao wa mwanamke ambaye ni Masihi (Mwanzo 3:15). “Mataifa mengi” yametajwa
kama nchi kubwa.
Aya hii inayofuatia kwa kweli inaanza na neno la
Kiebrania Mem au Kutoka. Hii inahusiana na aya ya 3
hapo juu.
Zaburi 110:7 Atakunywa maji ya mto njiani; Kwa hiyo atakiinua kichwa chake.
Usemi wa Naye
atakunywa vijito akiwa njiani unahusianishwa kitendo cha kumuinua kichwa
chake. Hii inamaanisha kuhamishwa kwa
mamlaka. Kimchi anasema kwamba andiko hili kwenye haki ya umoja hapa huenda
linaweza kuonesha katika uwingi pia(Soncino). Kichwa kilichoandikwa kwa umoja
kilichoondolewa ni kile cha Shetani katika mataifa (pia soma Zaburi 98:22 kwa
kifungu hiki kinamuonyesha kiongozi wa
wanaume wanaopigana (sawa na Rashi, Soncino). Hapa ilimaanisha kiongozi wa
waasi. Kwa jinsi hii, Shetani ni Mpingakristo, na mengine yoyote yanayoendelea
kwenye mfumo wake ni itikadi zenye lengo la Mpingakristo. Kichwa kilichoinuliwa
juu ni uongozi wa Mungu wa kweli kupitia Roho Mtakatifu. Masihi anakunywa roho
hii. Kwa jinsi hii, anatimilika kwa hali zote kuwa na hali kamili ya Uungu au
kuwa Theotetos. Huu ni uweza wa
kimbinguni (soma kitabu cha Thayer’s).
Kristo alijazwa na nguvu za mbinguni na alijazwa na Uungu. Aya ya 10
inatuonyesha kwamba hata sisi tumejazwa na Uungu wa Kristo au na hii Theotetos.
Hii inaonekana kwa ile dhana ya kuwepo kwake kabla ya
kuzaliwa kwake kwa mipango ya Mungu kunakosemwa kwenye Ufunuo 7:9-15. Mwanadamu
aliyekombolewa na Wazee au Baraza wako mbele za Mungu. Kwa ajili hii Mungu
anatukuzwa. Wazee wanazitupa taji zao mbele za Mungu wakimaanisha kuwa wanaweka
na kuuachilia mfumo wao wote kwa Mungu wa Pekee na wa Kweli na kwa hiyo
wanakuwa ni wenye kuamini juu ya Mungu mmoja. Na wanapokuwa kwenye kiti hiki
cha Enzi, kila mmoja anapangiwa ofisi yake na mamlaka yake na uweza wake.
Kwa jinsi hii ndiyo maana tunaviinua vichwa vyetu kwa
kunywa kutoka kwenye vijito, ambavyo ni Roho Mtakatifu.
Metsudath David anasema kwamba ushindi utapatikana
kikamilifu kama matokeo ya mwingilio kati wa Mungu (sawa na Soncino, fn. to v.
7). Huu ndyo mwisho wenyewe kamili hadi kufikia maasi na marejesho mapya yatakayofanywa
na Masihi aliyeketi Mkono wa Kuume wa Mungu.
q