Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[179]
Wimbo
wa Musa
Kwenye
Kutoka 15
(Toleo La 1.0
19981110-19981110)
Jarida hili la ufafanuzi linakwenda kushughulikia wimbo wa kwanza kati
ya nyimbo mbili za nabii Musa zilizo kwenye gombo za Torati. Unahusu ukombozi wa
Israeli. Wapili wake umo kwenye Kumbukumbu la Torati 32.
Christian Churches of God
PO Box 369,
WODEN ACT 2606, AUSTRALIA
Email: secretary@ccg.org
(Hati Miliki ©
1998 CCG, Thomas McElwain, ed. Wade Cox)
(tr. 2014)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na
kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la
haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa
au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi
zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya
lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.
Jarida hili linapatikana
Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Wimbo wa Musa Kwenye Kutoka 15
Somo lifuatalo lina mambo mawili yote, yaani sio kawaida na ni ya kipekee
sana. Mwandishi analiendea andiko akiwa na sehemu tu ya elimu ya kiuanazuoni, lakini
akiwa hajaelewa kwa kina chanzo cha kiroho cha mlinganisho wake, lakini akiwa
hajajikita kwenye vyanzo vya kimaandiko vya mlinganisho wake, na wala
hakutathmini ukweli mwingi wa kihistoria na kitamaduni unaopelekea tafsiri
yake. Anachagua kuyahifadhi baadhi ya maandiko yanayoashiria jambo hili. Mkazo
mkubwa umewekwa kwenye majaribio ya kifilolojia yanayojumuisha mlinganisho wa
maneno.
Kutoka 15:1 Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu
wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na
mpanda farasi amewatupa baharini.
Wimbo wenyewe unaanza baada ya kupuliza. Unatumika tena ukiwa kama jibu la
kiitikio kwenye sauti ya ridhimu ya kipulizio kwenye aya ya 21. Hii inaonyesha kuwa
aya ya kwanza inabeba maana na kiini hasa cha wimbo wote unaosifia ushindi mtukufu
wa Bwana. Wimbo wenyewe unahusu ukumbusho wa ukombozi wa watu wanaotoka
utumwani Misri na mashambulizi ya Farao kwenye Bahari ya Shamu. Ingawa matukio
mengi ya kukombelwa yanaelezewa kwenye Maandiko Matakatifu, bali hili moja
linabakia kuwa ni kuu la kukumbukwa ambalo kwa kipindi cha karne nyingi kadhaa
waumini wamekuwa wakilisemea. Wimbo huu wa ukombozi unaimbwa na wale ambao
wamepata ushindi dhidi ya mnyama na sanamu yake kwenye Ufunuo 15:3, ambako unachukuliwa
na kurudiwa Wimbo huu wa Musa ulioandikwa kwenye Kumbukumbu la Torati sura ya
32.
Kumbuka: Wimbo huu wa Musa umeandikwa kwenye maandiko ya vitabu vyote
viwili, yaani kwenye Kutoka 15:1-19 na Kumbukumbu la Torati 32:1-43, na kote
huko unasimama kama ushuhuda kwa Israeli ili kuwakumbusha kuzitii Sheria na
Amri za Mungu na matendo yake.
Wimbo huu unaonyesha wazi kumsifu YHVH, jina amblo limetajwa mara mbili
kwenye aya hii. Ushindi wenye utukufu mkuu namna hii unaweza uonekane kuwa si
kitu sana siku hizi, lakini ni vema kukumbuka kwamba silaha za kivita za
Wamisri ndizo zilikuwa zenye nguvu na za kisasa kuliko kwinginekokote duniani
kwa wakati ule. Ujumbe ulioko hapa ni kwamba ushindi wa kijeshi wa Mungu uko
juu sana, zaidi ya kiwango cha uwezo wa silaha zilitumiwa na watu na kwamba
kwake hizo hazina lolote kabisa. Tendo la kuigawanya bahari linaweza kudhaniwa
kuwa ni tukio linalotokana na natokea ya kimazingira yanayoweza kutokea wakati
wa kupwa na kujaa kwa bahari mahali pale, na wapinjgaji wanaweza kuweka dhana
wakisema kuwa bila shaka jambo kama hilo lingeweza tu kutokea mahala pale.
Lakini tofauti iliyopo kati ya tukio la kiasili na la kimiujiza ni pan asana
kulitathmini kiasi cha kuuzidi uellewa wa kibinadamu. Ni ukweli ulio wazi
kabisa kuwa matengenezo ya umbile na vitu vilivyoko duniani ni mojawapo ya
muujiza mkubwa unaotosha kushuhudia, na ni kitu kikubwa sana zaidi ya ule wa
kuigawanya bahari. Bado watu wanashangaza kwa kutolichukulia jambo hili kuwa ni
muujiza mkubwa kwenye mawazo yao. Yupende, tusipene, ukweli unabakia kuwa tukio
hili ndilo oja ya matukio yaliyowahi kujitokeza mara moja tu pasi kujirudia, na
kipindi chake kilikuwa cha muhimu sana ili kuwapa hitaji lao wana wa Israeli.
Na kwa hakika kilikuwa ni cha muhimu sana ambacho kwacho uingiliaji wa Mungu
ulifanywa na kuonekana kwa hawa Israeli wa kale kwenye Maandiko Matakatifu.
Kutoka
15:2 Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu
wangu. Yeye ni Mungu wangu,
nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
Aya hii inaumuhimu na utajiri mkubwa katika kumuelezea Mungu, tena haielezei
kitu kingine chochote zaidi ya tabia na uweza mkubwa wa Mungu mwenyewe na jinsi
alivyo. Zote zinahusianishwa na jinsi uhusiano wake ulivyo na mwanadamu. Kitendo
cha kugundua kuwa Mungu ni nguvu ni cha kutambua kuwa kwa peke yangu siwezi
kuifanya kitu chochote, lakini kwamba kila kilichofanyika ni mali ya Mungu.
Hakuna uweza unaoweza kufantika zaidi ya ule wa Mungu. Kima cha utegemevu wa
mwanadamu kwa Mungu na ukaribu wake kwa Mungu ni zaidi ya uwezo wa uelewa wa
mwanadamu.
Mungu ndiye wimbo wangu, au kwa tafsiri nyingine Zaburi. Zaburi imeliiyata
kuwa ni makao ya Mungu kwenye Zaburi (tazama Zaburi 22:3). Hapa inaonyesha kuwa
Mungu ni Zaburi. Kama mtu kisema maneno kama hay oleo, basi watu wengi
wangemuona kama anakufuru. Ukweli ni kwamba Mungu ni hatafuti wala
kiupapasapapasa na chochote kile ambacho mwanadamu anakutananacho sio Mungu
aishiye, bali ni makazi yake na namna ya ufunuo inatokana na kikomo cha upeo wa
mwanadamu. Hakuna mtu aliyewahi kumuonja Mungu (Yohana
1:18; 1Timotheo 6:16). Anajidhihirisha mwenyewe kupitia Roho Mtakatifu. Kwa
hiyo, kwa ueuewa na uzoefu wa kibinadamu, Zaburi ambayo kwayo Mungu anadhihirishwa
kwenye moyo wa mwanadamu ndiyo inayomwezesha mwanadamu kumjua Mungu. Zaburi ni
Mungu. Makosa ya kihistoria yanayofanywa ili kulijua hilo yamesababisha dini ya
Kiyahudi imeendelea sana zaidi ya dini ntingine za kale kama zile za Siddur au
kitabu cha ibada kama kilivyo kitabu cha Zaburi, kikiendelea kwa toleo moja
hadi linguine la vitabu vya nyimbo za kidini. Imani ya kikristo inaonekana
kwenye mbali zaidi. Maandiko Matgakatifu ndiyo pekee yanayotuongoza kwenye
ibada ya kweli pamoja na maombi bidii, ushuhuda na kusifu. Siyo Zaburi peke
yake, bali pia baadhi ya Maandiko Matakatifu, kama vile kitabu cha Ufunuo,
kimeandikwa wazi kwa nia ya kusifu na na kusikika kwenye ibada. Kama Maandiko
Matakatifu yanajumuisha mguso wa Mungu, ndipo inaweza kushauriwa
kuchukua mahala pa Zaburi kwenye vitabu vya nyimbo ili kuchukua mahala pa Mungu
aliye kwenye Maandiko Matakatifu na hivyo kuwa ni ibada ya sanamu.
Mungtu anakuwa ndiye wokovu. Huu ni mchakato wenye hatua nne. Unaanza kwa
kumtambua Mungu kuwa ndiye muweza na kwamba ndiye pekee anayepaswa kutegemewa
na mwanadamu na kuwa na uhusiano naye wa karibu iwezekanavyo. Hatua ya pili ni
kujua kwamba Maandiko Matakatifu ni Mungu mwenyewe, sawa na kama mwanadamu
anavyomjua Mungu anapofunuliwa kwake kupitia Roho Mtakatifu. Hatua ya tatu ni
wokovu kwa njia ya uwepo wa Roho Mtakatifu kama Mungu alivyo ndani yetu. Hatua ya nne ni kuutafsiri wokovu: Yeye ni Mungu.
Hapo ndipo hali ya kukombolewa inapokamilika. Ni kufanya makao ya Mungu, kwa
hiyo tunapaswa kuimba Zaburi za ukombozi, sifa za Israeli ambao ndio watu wake.
Mungu amechagua kuishi ndani ya wateule kama alivyoishi katikati ya Ishraeli.
Na kwa hiyo wanakuwa ni Hekalu la Mungu. Uimbaji wa muziki uliovuviwa wa Biblia
kwa Roho Mtakatifu kwenye ibada kunafanya sujenzi imara wa Hekalu la Mungu.
Mahekalu ya wananadamu yanajengwa kwenye eneo fulani na kwa hiyo yanastahimili
hali ya kumilikiwa na hatimaye uharibifu na udanganyifu. Hekalu la Mungu
hujengwa kwa Wana wa Mungu waliozaliwa kwa Roho na wanaoabudu siku za Sabato,
ambalo ni hekalu lililochaguliwa, jengo, lisiloweza kushikika na ambalo umbo
lake linakuwa sawasawa kwenda juu kwake na upana wake kwa uwepo wa Roho
Mtakatifu na linajumuisha uwepo wa Yeye Asiyeonekana. Hatimaye, hekalu la Mungu
linajengwa kwa kuyasoma Maandiko Matakatifu, na sifa za Israeli, ambazo zinapatikana
tena kwa umuhimu wake yanavyopatikana kwa kila mwenye sauti, macho, sikio, au
akili. Nitamtukuza yeye kila mara, ni marudio yaliyo kile kwenye mawazo ya
kwamba nitamjengea makao.
Mtume Paulo huenda alifikia kwenye ukweli usiotatiza wala kufungiwa kwenye
kweli isiyofikirika uliokuwa kwenye maelekezo haya pale aliposema kwamba miili
ya wateule walio katika Kristo ni hekalu la Mungu. Mtume Petro alienda moja kwa
moja kwenye ukweli huu kwa kusema kwamba “Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za
thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu,...” (2Petro 1:4).
Kutoka 15:3 Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake.
Kiebrania kwa kweli kinatumia neno iish
au man kumtaja BWANA. Ingekuwa ni
kupingana na Maandiko Matakatifu kwa kuyatatiza yenyewe kwa yenyewe katika
kuelezea ubinadamu kwa Mungu kwa namna yeyote. Hesabu 23:19 inasema wazi kwamba:
Maana iish Eel, Mungu si mwanadamu. Maelezo
yake yangeweza kuwa yanahusiana kiufananisho na malaika wa BWANA, ila dhana
iliyoo hapa inaonekana wazi kwamba ayah ii inamzungumzia Mungu mwenyewe. Kwa
Kiebrania hairuhusiwi kutenganisha maneno mawili ya maelezo yaliyofanwa, nah ii
iko miongoni mwa hizo. Kile kinachotakiwa kuelezea na kufafanua ni neno lote
zima linalosema iish milhaamaa, au mtu
wa vita. Namna hiyo, neno hili halielezei hali ya ubinadamu au ukosefu wake.
Bali linaashiria shughuli za kijeshi. Kwenye jambo hili, shughuli za kujeshi ni
mojawapo ya wokovu. Maelezo yake yana maana kwamba Mungu anaokoa.
Nusu ya mwisho ya aya inalifunua jina la Mungu. Ili kulijua jina la mtu au
sifa zake njema au umaarufu wake (kwa Kiebrania neno hili linachukua maana zote
mbili) linamaanisha kile anachoweza kukifanya mtu kwa matakwa yake mwenyewe.
Mwanadamu anahitaji wokovu kwa kila kipindi, na kulijua jina la Mungu ni kujua
pa kuelekea kumrudia, na kuwa na uwezekano wa kumrudia yeye.
Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa
baharini, Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama
jiwe.
Bwana, mkono wako wa kuume umepata fahari ya
uwezo, Bwana, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui.
Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini
wanaokuondokea, Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu.
Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji
yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, Vilindi
vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.
Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya
nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu
utawaangamiza.
Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza;
Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu.
Maelezo ya tukio lililotokea kwenye Bahari ya Shamu yanavutia na kupendeza
na hata sauti yake ina nguvu kubwa. Jambo kuu linaloweka ugumu kwenye andiko hili
maelezo va kielimu dini au kiampomofolojia ya Mungu. Jambo kama hilo linaweza
kufafanuliwa na tabia ya maandiko ya kale ya Kiebrania ya kutumia maneno
hayohayo kwa kukazia na kushangaa. Kwa mapokeo ya desturi za nje na ndani za
kale yanaonyesha uwepo mkubwa wa dalili za kitamaduni au athropolojia na ugumu
zaidi kuliko ilivyoshauriwa hapo mwanzoni kiasilia. Mfano elekezi upo mwanzoni
kabisa mwa neno lililoandikwa kwenye kifungua hiki linalosema “mkono wako wa
kuume.” Hata kama Mungu anamkono wa kuume au la, andiko hili haliashirii kwa
namna yoyote ile. Usemi wa Kiebrania wa mkono wa kuume” unamaana ya “nguvu” au
“uweza” kama unavyofanya mkono wa mwanadamu. Ili kuchagua kuwa huenda ni namna
ya tafsiri, au ni kiuhalisia zaidi kuliko nyingine.
Mawazo yamezoea kushughulika na mifano ya tabia za Mungu inayoonekana kuwa
ni vigumu kwenye maelezo ya elimu ya mila na desturi, lakini huu ni ubaguzi tu.
Neno “mheshimiwa” lililo kwenye aya ya saba ndilo linaloweka ugumu hata kama
msomaji aliliruka na kuliacha pasipo kujua ugumu wake. Neno g’oon linatokana na vebu inayomaanisha kukua kwa kurefuka. Kuelezea kwa kwa
njia ya mfano kimo au urefu wa Mungu ni kumfanya Mungu kuwa ni eneo, jambo
ambalo ni matatizo kwa kweli kama yalivyo masomo ya mila na desturi za watu au
anthropomojia.
Jawabu kwa matatizo yote mawili ni rahisi kujua kwamba lugha ya mwanadamu
haitoshi katika kuelezea ukuu na uweza wa Mungu. Kwa hiyo hatupaswi kuchukulia
maelezo yake kama yanatosha kumuelezea Mungu. Kwa hiyo, kunasababu ya
kumdhihirisha Mungu katika uhusiano wake na mwanadamu, na sio katika umuhimu wa
asili yake. Na kwa nia hiyo ziko sahihi sana, kihalisia na kwa kushangaza.
Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama
wewe? Ni nani aliye kama wewe,
mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi ikawameza.
Kifungu hiki kinaanza kwa kuuliza swali: Nani aliye kama Mungu? Maelezo
haya yanaonyesha cheo cha Malaika wa Bwana aliyeandikwa kwenye Danieli 12:1: akisema
Na kwa kipindi hicho, Mikaeli
atasimama... na kwenye Danieli 10:13,21. Kuna
viumbe kumi na mmoja kwenye Biblia ambao pia wanaitwa kwa jina hili. Kusudi
mkazo ulioko kwenye jina hili ni kukumbusha kuwa hakuna aliye kama Mungu kwa
kuanzia usemi wa swali hili la kihamasa. Baadhi ya mambo ya kianthropomofia yanaonekana
kuhusiana zaidi na Mungu kwenye Biblia kuliko ukweli wa kwamba inataja malaika
wa BWANA ambaye anaonekana wazi kuwa ni mpeleka taarifa za ufunuo kwenye
maandiko mengi yaliyopo (Mwanzo 16:7, 22:11 nk.) na huenda kwenye maandiko mengine
mengi zaidi.
Kuna mawazo yanayotofautiana katika kutafsiri maneno ya Yesu yaliyo kwenye
Yohana 8:58 (Yeye
Ibrahimu asijakuwako, mimi niko) yanayosababisha kudai kuwa malaika huyu wa Bwana
ndiye aliyetumwa duniani na kuzaliwa binadamu. Malaika wa Bwana ana mamlaka
makubwa anapokuwa anayanena maneno ya Mungu moja kwa moja, katika nafsi ya
kwanza, kana kwamba hakuwa na maisha hapo kabla ya kuzaliwa kwake duniani. Yesu
anaonyesha jambo hili kwa kusema maneno yaliyo kwenye Yohana 5:30: “Mimi siwezi
kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni
ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake
aliyenipeleka. Hii ni namna fulani ya ushiriki wake kwenye asili ya kimbinguni 2Petro 1:4.
Maelezo au usemi miungu au Eeliim kwenye aya ya 11 yamewekewa
maelezo yake kwenye jalada la chini ya ukurasa kwenye tafsiri ya KJV ikimaanisha
wenye mamlaka. Hii kwa kweli inaonyesha
kuwa ni kidokezo cha neno Eel kwenye Biblia,
ambayo inatumika kwa namna mbalimbali sawa na neno Elohim. Limetumika kama uweza katika maeneo mengi kadhaa (Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu, Kumbukumbu la Torati 28:32; Nehemia 5:5; Mithali
3:27 nakadhalika). Na hata imetafsiriwa wema
mkubwa Zaburi 80:10(11). Inamtaja kwa wazi mungu wa uwongo kwenye maandiko
kadhaa, kama vile kwenye Waamuzi 9:46, na kwa sanamu za kuchonga ama kusubu
kwenye maeneo mengine kama vile Isaya 44:10,15,17. Wakati mwingine ni neno la
jumla kwa wote wawili yaani Mungu wa kweli na miungu ya uongo kama kwenye Kutoka
34:14. Ila mara nyingi inamtaja Mungu wa pekee na wa kweli kama ilivyo kwenye Mwanzo
14:18; 17:1; 21:33; 31:13; na 33:20, ambapo vyeo vyake vinaunganika nayo.
Inatumika tu pale inapomtaja Mungu, ni ya kawaida sana kuonekana kwenye vitabu
ninginevyo kama vya Ayubu, Zaburi, na Isaya (Ayubu 5:8; Zaburi 5:4(5); Isaya
5:16 et al.).
Lakini tuko hapa kukabiliana na matumizi maalumu ya neno lililo kwenye
uwingi wenye mamlaka, ambao
inaonekana kwamba kujumuisha kikundi cha miungu ya uwongo au mingineyo, wanaweza
kuwa wanadamu wenye mamlaka au viumbe wengine wowote. Kutoka 15:11 ni andiko la
kwanza linaloonekana kutaja kitu kingine zaidi kwa kutumia neno Eeliim. Mlinganisho na maandiko machache
mengine yanaonyesha kuwa maelezo haya ni neno la kitaaluma kwenye kusanyiko
linaloitwa kwa dhahiri la wana wa Mungu (Ayubu
1:6; 2:1 nk.), nyota za alfajiri (Ayubu
38:4), malaika (Isaya 1:9 nk.), na nyota za Mungu (Isaya 14:16). Zaburi 29:1:
Mpeni Bwana, enyi wana wa
Mungu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu;. Inavyosema hapa ni wana wa mwenyezi, maelezo yaliyopo kwa wazi hapa ni kitabu cha
Ayubu. Zaburi 82:1: Mungu asimama katika
kusanyiko la Mungu;… Maelezo yanaweza kuwa yalitafsiriwa vizuri kuwa kusanyiko kubwa au mkusantiko wa Mungu. Inaelezwa kwa wazi sana kuwa mkusanyiko huu
sio wa namna nyingine ila ni wa wanadamu. Zaburi 89:6(7): Maana
ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na Bwana? Ni nani afananaye na
Bwana miongoni mwa malaika? 7 Mungu
huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka. Andiko hili
linafanana sana na Kutoka 15:11. Ila inafafanua kwa karibu sana yule ambaye kwa
hakika anahusika. Wenye nguvu hawa
sio wale wanadamu wenye nguvu walio maarufu kwenye utawala wa Misri, bali ni
viumbe walioko mbinguni. Aya hii inawahusisha
pia wana wa mwenyezi walio kwenye
Ayubu 29:1 katika dhana ya kusanyiko la mbinguni. Kwa hatua hii maelezo ya
Zaburi kuhusu kuangukia mahali pa ufafanuzi wao kuhusu jukumu la Kutoka 15:11.
Tukiachana mbali na msisitizo ulio kwenye Zaburi, tunakutana na Isaya 14:13:
Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda
mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi
juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Iwe kwa namna
nyingineyoyote au la, tunaitambua aya hii kama inamtaja Shetani, kwa kadiri
mapokeo ya Kikristo yanavyojua na kuichukulia, kuna maeneo mawili yanayoonyesha
wazi kuwa ni malaika wa mbinguni/ ya kwanza ni pale inaposema kuwa ni nyota za Mungu nay a pili ni pale
inaposema kuwa mkusanyiko. Nyota za
Mungu wanaweza pia kutafsiriwa kama nyota
kuu, ambazo zinawatenga na kuwatofautisha na zile nyota zinazotoa nuru
tunazoziona usiku wenye giza na usio na mawingu.
Danieli 11:36: “Naye mfalme atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na
kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa
miungu, naye atafanikiwa mpaka ghadhabu itakapotimia; maana yaliyokusudiwa.” Maelezo yasemayo Mungu wa miungu yaliyopo hapa
yanatamkwa pia kama Eel eeliim. Andiko
linaonysha wazi kuwa Mungu ndiye anayetawala kwenye mkusanyiko wa eeliim.
Kutoka 15:12 inasema kwamba hawa wenyen mamlaka kuwa ni Wamisri/ inaonekana
kuwa ni vyema sana kama tungelijua neno eeliim
lililo kwenye aya ya 11 kuwa halimaanishi malaika waaminifu walioko kwenye
baraza la mbinguni na wanadamu wanaoshirikiana nao, bali hata kwa wasio
waaminifu na wenye dhambi wakiwemo wenye mamlaka wa Misri. Andiko linalofuatia
kutoka kitabu cha Ezekieli linaonyesha kuwaelezea hawa mwenye mamlaka wa Misri wakiwa
kwenye uangamivu wao pamoja na waasi wote waliokuwa kwenye baraza la mbinguni
la malaika. Ezekieli 32:21: Walio hodari watasema naye, toka kati ya kuzimu pamoja
nao wamsaidiao; wameshuka wamelala kimya, hata wasiotahiriwa, hali wameuawa kwa
upanga. Neno eeliim limetafsiriwa hapa kama wenye nguvu (wengi).
Kutoka
15:13 Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa
uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.
Kifungu hiki kinabeba dhana ya wateule waliochaguliwa na Mungu. Wazo la
kukombolewa au ukombozi kwenye Biblia lina misingi mikuu miwili. Wa kwanza ni
ukombozi wa kila mzaliwa wa kwanza, ambalo ni kitendo cha kutambua ama kujua
kwamba vitu vyote ni mali ya Mungu. Tendo hili limeelezewa vema sana kwenye
maandiko kadhaa yaliyoko nyuma kabla ya andiko hili, ambayo ni Kutoka 13:2 na
kadhalika., na inaonyesha mfano wa wazi kwenye Kutoka yenyewe, ambayo inachukua
mahala pake kwenye andiko ambalo Mungu anamtaka mzaliwa wa kwanza wa Misri, na
kupita juu kwenye nyumba zote walizopaka damu kwenye miimo ya milango yao (tazama
Kutoka 12:12,13). Ukombozi mwingine mkuu kwenye Biblia ni ule anahusu kumuokoa
mker wa ndugu aliye kufa wa ukoo wa lawi, wa ukoo wa lawi, ambaye alikuwa
maarufu sana aliyeandikwa kwenye hadithi ya Ruthu. Wateule wanakuwa mali ya
Mungu kwa mujibu wa kitabu hiki cha Kutoka, kwa namna ya mfano kama mzaliwa wa
kwanza aliyekombolewa, au mke aliyekombolewa. Huu ni mwangukio mwingine wa
usemi wa kinabii kwa Mungu kuwa ni kama Baba na bwana, na ni ibada ya sanamu
kama ukahaba wa ndoa ya kiroho.
Swali linalofuatia ni kwamba huyu aliyekombolewa au mteule ni nani basi?
Kuna mambo mawili ya kutimia maanani: moja inaheshima na nyingine ni shirikishi
tu kwenye tendo la ukombozi wa Pasaka na Kutoka. Hiin ni barua halisia inayoonyesha
maana muhimu ya historia. Ni watu halisia wasio na uzaliwa wa Israeli miongoni
mwa waliokombolewa (Na kundi kubwa la watu
waliochangamana mno wakakwea pamoja nao; Kutoka 12:38). Kwa
ajili ya kuheshimu wito wa kupaka damu kwenye miimo ya milango yao, baadhi ya
watu wasio hata wa nasaba ya Kiisraeli, kulikuwa na uwezekano mkubwa kuwa hata
bkulikuwa na watu wengine waliokuwa na nasaba wa Kiisraeli hawakujumuishwa miongoni
mwa wale waliokombolewa.
Hata hivyo, mambo yote mawili yana maana yake. Kwa ajili ya mtawanyiko wa
Waisraeli, inawezekana kabisa kuwa hakuna mtu miongoni mwa walio hai leo
anayetokana na uzao huu wa wale waliokombolewa wakati huu wa Kutoka kwao
utumwani. Kama ukweli ungejulikana, basi wengi wangeshangaa sana kuona asilimia
ya wazaliwa wanaoonekana leo kama ndio wenhyewe. Hata kwa Wayahudi walioko
uhamishoni, siku zijazo wameijaza dunia, ili kufikia kiwango cha kwamba yale
makabila kumi yaliyopotea yaweze kuikaribia kuijaza dunia. Hata hivyo, ushiriki
wa mlo wa Pasaka na Kutoka kama vinavyotendeka kwa kiwango cha kidunia zaidi ni
kitendo cha muhimu sana. Jinsi mtu anavyofanana na Wimbo huu wa Musa ni
mwonekano wa muhimu kwake.
Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao
Ufilisti utungu umewashika.
Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu
wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka.
Hofu na woga umewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako
wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee Bwana, Hata
watakapovuka watu wako uliowanunua.
Sehemu mbili za mwisho za utenzi huu mkuu zinaelezea makundi mawili
yanayokabiliana: waliokombolewa na waoga walioshindwa vita. Maelezo ya kwanza hapa
yanaelezea kwa kusisitiza jinsi waliopigwa walivyofikishwa kwenye hali ya
kumcha Mungu kwa ushuhuda wa ukombozi wake uliotolewa na wale waliokombolewa kwenye
Bahari ya Shamu. Hii inaenea zaidi ya Wamisri hadi kwa wale wanaompinga Mungu
kwenye mataifa yote.
Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa
urithi wako, Mahali pale ulipojifanyia, Ee Bwana, ili upakae, Pale patakatifu
ulipopaweka imara, Bwana, kwa mikono yako.
Bwana atatawala milele na milele.
Kwa maana farasi za Farao na magari yake na
wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, Bwana akayarudisha maji ya
bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya
bahari.
Fungu hili la mwisho linarudia na kujenga umuhimu wa fundisho muhimun za utenzi kwenye maelezo yake ya
waliokombolewa. Kama vifungu vilivyotangulia yakienda zaidi ya Wamisri, basi
hii inaenda zaidi vipindi katika kuangalia mbele kwenye ushindi wa dunia ya waliokombolewa.
Wanapokea urithi wao na wanafanywa waishi kwenye Hekalu hilihili la Mungu,
ambapo Bwana atatawala milele na milele.
q