Makanisa Ya Kikristo ya Mungu

[180]

 

 

 

Mji Wa Mungu [180]

 

(Edition 1.2 19961004-19991018)

 

Kitabu cha ufunuo kinaelezea wakati ambao Mungu ataanzisha Mji wake. Jaratasi hili linaelezea kuhusu hii Yerusalemu Mpya, mfano wake na maana yake.

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

(Copyright ã 1996, 1997, 1999 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Mji Wa Mungu [180]

 


Hatua ya mwisho ya shughuli za dunia zinalenga kenye Kiti Kikubwa cha Hukumu cha Ufunuo 20. Hii itachukua nafasi yake mwishoni mwa kipindi cha Milenia baada ya vita ya mwisho ya Uasi.

 

Ufunuo 20:7-10 Na hiyo miaka elfu ilipokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pande nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya ka vita; ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. 10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

 

Vita ya mwisho inahusisha shambulio kwenye kambi ya watakatifu itakayokuweko mjini Yerusalemu. Shetani atakuwa bado ana nguvu hata baada ya miaka elfu ya utawala wa haki kushawishi mataifa kufanya vita dhidi ya Kristo tena. Shida ya ndani ni kwa watu kujihesabia haki yao mwenyewe. Shetani atafunguliwa ili ashughulike na mgogoro mkubwa kwa mwanadamu kupewa uwezo wa kushiriki katika Ufalme wa Mungu. Baada ya hii, Shetani ataondolewa na nguvu zake za kiroho zitakoma na kutumika kama kumbukumbu ya Uasi. Ufufuo wa pili wa wafu hatimaye utachukuwa nafasi yake. Ufufuo wa pili wa wafu hatimaye utachukua nafasi pia.

 

Ufunuo 20:11-15 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawa sawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na Mauti na Kuzimu zikwatowa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

 

Tumejionea njia ya kuelekea kwenye ufufuo wa wafu na hukumu ya mapepo na ya mwanadamu. Hatua nyingine ya pili ni makabidhiano kutoka kwa Yesu kwenda kwa Mungu.

 

IWakorintho 15:20-28 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. 21 Maana kwa kuwa mauti illetwa na mtu, kadhalika kiyama ya wafu ililetwa na mtu. 22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristowote watahuishwa. 23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. 24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye; hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. 27 Kwa kuwa, Aliyevitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo. 28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliye mtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

 

Hatua hii ya kutiisha chini inajumuisha pia ile ya kuwa chini Yesu Kristo. Kristo yule ambaye hayuko sawa au usawa wa umilele ila zaidi sana ni sehemu ya hatua ya Mungu kuwa yote katika yote. Ili kwamba kuwe na Mungu mmoja na Baba wa wote juu ya ya wote, na katika wote (ona pia Waefeso 4:6).

 

Hatua hii inajumuisha uumbaji wa mbingu mpya na nchi mpya ambamo vitu vya zamani havitakumbukwa tena. (Isaya 65:17). Uzao au mbegu ya Israel itabaki mbele ya Mungu.katika utaratibu huu mpya. (Isaya 66:22) mpaka miili yote imekamilishwa kabisa baada ya ufufuo wa wafu kwenye mwisho wa kipindi hiki cha Milenia. Sayuni ni mji mwaminifu (Zak. 8:3). Yerusalemu mpya utatokea mbinguni (Ufunuo 3:12)

 

Tunangojea mbingu mpya na nchi mpya ambayo haki inakaa ndani yake (2Pet. 3:13). Mji wa Mungu ulisubiriwa na waaminifu kutoka angalau zama za Abrahamu (Waebrania 11:10). Haya yalikuwa ni maono ya mababa waanzilishi wa ttaifa la Israeli. Tumewekwa ndani ya Mji (Efe. 2:6,18-22). Zab 48 inaonyesha kuwa Mji wa Mungu uko juu ya Milima ya Utakatifu wake.

 

Waebrania 8:5 inaonyesha kwamba maskani au hema ya kukutania ya kidunia ilikuwa tu ni mfano au kivuli cha hema ya kiroho ya kimbinguni ya Mlima au Bustani ya Mungu.

 

Hema ya kukutania katika Israeli ilitandazwa ndani ya hekalu la Sulemani kulingana na maelekezo yalivyo katika (1Nya. 8:10-12) Mtandao huu ulikuwa unaonyesha kwamba Mungu alikuwa anaendeleza hema yake kimbinguni na kulitandaza muendelezo huo kukijumlishwa uumbaji huo wa mwandamu hapa duniani. Hii ilifanywa kwa amni na sio kwa vita ila ni kwa sharti la utii na unyenyekevu (1Nya 28:10). Hatimaye Mungu ataishi pale siku zote (Eze. 43:1-9). Hii ilifanywa kulingana na utaratibu wa ahadi (Eze. 43:10 mpaka 44:31). Ezek. 43:11 inaonyesha umbo la mtindo lenye kufanana na Surahs ambazo zimeandikwa kwa mintaarafu wenye kushbihiana na unabii na sheria (hii inaeleweka vizuri zaidi wakati tunaona kwamba Koran iliandikwa katika Surahs; kisha ikatolewa maelezo).

 

Ezekiel 43:11 Na ikiwa wameyataharikia yote walioyoyatenda, waonyeshe umbo la nyumba, na namna yake, na matokeo yake, na maingilio yake, na mambo yake yote, na maagizo yake yote, na kawaida zake zote, na sheria zake zote, ukayaandike machoni pao, ili walishike umbo lake lote, na maagizo yake, na kuyatenda.

 

Katika Ezekiel 43:10 tumeona kwamba maelekezo kuhusu hekalu yamefafanuliwa kwa Israel ili kuwafanya waone aibu kwa mauovu yao. Wao wenyewe wameambiwa kupima kielelezo chake. Kielelezo (kwa Kiebania. toknit, kwa mujibu wa Septuagint, LXX huitwa diagraphes) ni kipimo cha kutumia ili kuweza kutathimini na kupata kiwango chake.

 

Kristo hakuingia patakatifu palipotengenezwa kwa mikono ambayo ni nakala (kwa Kiyunani: antitypos au uwakilishi) wa kweli, ila kwa mbinguni kwenyewe, sasa aonekana katika uwepo wa Mungu kwa ajili yetu (Waebrania 9:24).

 

Mji wa Mungu Pia ni Bustani ya Mungu na Paradiso ya Mungu

 

Kitabu cha Mwanzo 2:8 inataja hali hii. Ezekiel 28 na Isaya 14 zinashughulika na ukweli kwamba Shetani alikua amewekwa kama na pamoja na kerubi mpakwa mafuta aliyefunikwa (maandiko haya ni mafumbo). Kwa maneno mengine, zinaonekana kuwa ni mbili kati yao. Ambazo zilitiwa nguvu na kupambwa kwa sanduku la agano. Kerubi huyu aliyetiwa mafuta mlinzi alimfukuza Shetani toka kwenye Mlima wa Mungu kama tunavyoona kutoka Ezekieli 28:16 (tazama Zab. 45:6-7 kwa mtiwa mafuta).

 

Mlinganisho wa aya za zamani katika mstari wa 16 kutoka katika Septuagint (LXX) na Origeni kulinganishwa na Biblia za Kiingereza za RSV, NRSV, NEB, TEV, Moffatt na Biblia iliyokuzwa (Amplified) huonyesha haya hii kama ilivyotolewa na Origen (De Principles, Bk.1.4)

 

Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umeteada dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.

 

Shetani alikuwa pia mtoto wa Mungu katika Mlima huu au Paradiso ya Mungu (Ayubu 1:6; 2:1; 38:4-7; ona pia jarida la Utawala wa Mungu [174] 1:2, Sehemu Wana wa Mungu.

 

Mji wa Mbinguni na Mlima wa Mungu vinalinganishwa na Mlima Kusanyiko. Bustani hii ya Eden au Paradiso ambayo iko mbinguni (2Kor.12:2-4) itashuka hapa duniani mahali ambapo pametayarishwa kwa ajili yake. Eneo hili litakuwa pia ni Edeni ya duniani. Tunajua kwamba Sayuni itakuwa kama Edeni (Isaya 51:3)

 

Edeni kama Bustani ya Mungu

 

Tunajua kwamba Mungu aliipanda bustani (Mwa.2:8). Ulingamnifu katika kitabu cha Mwanzo unahusiana na Kanisa na Kristo wakiwa kwenye ushindani na Shetani (Mwa.3:8-19). Mwanamke ni Kanisa ambalo linatamani kumuona mume wake (Mwa.3:15; Ufu.12, Eze.16). Uzao wake utaponda kichwa cha Shetani na yeye ataponda kisigino (Mwanzo 3:15) Uasi chini ya Shetani umesetwa (tazama Rum.16:20)

 

Mama yetu ni kanisa ambalo ni Yerualemu Mpya Mama yetu sisi sote (Gal.4: 26). Mbali na mji wa Mungu hakuna mama mwingine mbali na Hawa, mama wa wote ambaye ni mfano wa Kanisa.

 

Bustani inakuwa ni Kanisa kwa mujibu wa kitabu cha Wimbo ulio Bora 4:12-16; 5:1 (tazama jarida la Wimbo ulio Bora (Na.145). Katika Busatani hii kuna Mti wa Uzima ulioko katikati ya Paradiso au Busatani ya Mungu (Ufu. 2:7). Wateule wana haki ya kuuendea mti huu kupitia Kristo na sheria za Mungu (Ufu. 22:14).

 

Adamu, kabla ya kuanguka kwake,alikuwa na ruhusa kwa Mungu kama lilivyo Kanisa baada ya Ukombozi wa Ubatizo. Miti ni vitu halisi vya kiroho (tazama majarida la Kuanguka kwa Misri [036], Unabii ju ya Mikono iliyovunjika ya Farao; tazama Ezek 28). Wote walikuwa chakala cha kuliwa lakini wawili walikuwa maarufu. Shetani anaonekana kufananishwa na mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Ezek.28:12-13; 31:8-9). Miti mingine iliuhusudu mti huu. Shetani alikuwa katika. Bustani hii. Mawazo ya kujificha katika miti mwingine yanaashiria hamu ya kuwela lawama kwa wakufunzi au waamuzi. Uhusiano wetu na Mungu uko mwishoni

 

Mlima Sayuni, Mji Mtakatifu, Mlima wa Mungu na Kanisa la Mungu Vimeelezewa Sawa na Makao ya Mungu

 

Mungu ndiye mjenzi wa Mji (Ebr.11:9). Yeye pia ni jiwe la gumegume la kutahiria (Yos.5:2) mwamba wa Israel ambao juu yake misingi ya mawe imewekwa au kulazwa (Kum.32:15,18,30-31; 1Sam.2:2; Isa.26:4; Isa.51:1-2) na kutoka kwayo Masihi alitokana (Dan 2:34,45). Mji huu umejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, Yesu mwenyewe akiwa ndiye Jiwe Kuu la pembeni kama makao ya Mungu (Efe.2:19-22).

 

Zaburi 68:15-16 inaonyesha kwamba Mungu anachagua kuishi katika Mlima wa Bashani. Hii, kwa hiyo ni uhamisho wa makao na kuyapeleka kwenye hekalu la Mungu kwenye dunia hii. Hii inahusiana na Zaburi ya 48 kama ulivyokusudiwa kuwa Mji huu wa Mungu katika Mlima wa Utakatifu wake.

 

Kisha, Mungu atakuja hapa duniani na kuhamisha mamlaka ya uongozi wa hapa duniani. Kisha dunia itajawa na utukufu wake (Isa.6:3). Mungu na Mwana kondoo watakuwa nuru ya utaratibu huu.

 

Ufunuo 21:1-2 “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbinguza kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapana habari tena. 2 Nami nikaona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya ukishuka toka mbinguni kwa Mungu umewekwa tayari kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

 

Hapa, Mji Mtakatifu pia unakuwa kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa tayari kwa mumewe. Bado wateule wayo tayari karamu yao arusi na Kristo. Muungano huu wa mwisho kuelekea kwenye muunganisho wa Jeshi zima la mbinguni chini ya himaya ya Yesu Kristo.

 

Ufunuo 21:3-4 Nikasika-sauti kubwa ikitoka katika kile kiti cha enzi ikisema, tazama maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti aitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maunivu hayatakuwapo tena.kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

 

Tofauti iliyoko hapa ni kwamba Mungu mwenyewe atakuwa pamoja na wanadamu kuliko Kristo kama mjumbe wa Mungu na Roho Mtakatifi kama alivyotolewa kama kiini cha tabia ya Mungu. Utaratibu mpya utakuwa ni wa kutokufa utakao tolewa na Mungu katika uumbaji wake. Roho Mtakatifu ni chokaa ya kujenga na kuuunganisha Mji wa Mungu pamoja kama ilivyofundishwa.

 

Ufunuo 21:5-8 Naye yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama nafanya yote kuwa mapya. Akanimabia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. 6 Akanimbia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. 7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. 8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

 

Hapa Mungu anatoa pia uzima wa milele katika ufufuo wa wafu wa pili. Ikizingatiwa akilini kwamba ufufuo wa wafu wa kwanza utakuwa tayari umeshafanyika kwa kipindi cha miaka elfu mojailiyopita, hapa tunazungumzia kuhusu ufufuo wa pili au ufufuo wa jumla unaoleta uzima wa milele kwa kila anayetubu pia. Mungu Baba pia ni Mwanzo na Mwisho. Kristo amepewa nafasi kama protos na eschatos au wa kwanza na wa mwisho kutoka kwa Baba. (tazama Ufu.1:8-17 sio kama inavyosema Biblia ya Kiingereza ya KJV). Kuna tofauti katika maneno haya. Kutokuwa na sifa za kupata uzima wa milele katika ufufuo wa pili wa wafu zimeorodheshwa hapa. Wale wote ambao hawatubu wanaruhusiwa tu kufa na wanachomwa kama makapi au takataka.

 

Ufunuo 21:9-14 Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nikuonyesheyule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo. 10 Akanichukua katika roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akaniionnyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu, 11 wenye utukufuwa wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri; 12 ulkuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na mawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. 13 Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu, na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu. 14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.

 

Mji Mtakatifu ni nyumba ya kiroho. Inajumuisha watoto wa Mungu. Mji Mpya Mtakatifu wa Mungu umetuama katika muundo ule ule kama alivyopewa Musa pale kwenye mlima wa Sinai. Umegawanywa katika sehemu nne ya tatu, na kufanya kumi na mbili. Kabila kumi na mawili ya Israeli ni msingi wa mgawanyo huo. Mataifa wote wa kila nchi wametengwa kwa makundi yaha kumi na mawili. Mitume kumi na wawili ni waamuzi wanaoongoza kabila hizi kumi na mbili (Mat.19:28). Mitume kumi na wawili ni misingi kumi na miwili ya Mji huo. Wao ni mawe kumi na mawili ya Israel iliyotumika katika historia ya unabii (Yos. 4:5). Wale 144,000 wametengwa kwa watu 12,000 kwa kila kabila (Ufu. 7:5-8). Hapa nia ya serikali ni kugeuza ngazi za kiutawala wake. Ni moja ya msaada ambapo mitume ni msingi na Mji unatuama juu ya misingi huo.

 

Ufunuo 21:15-16 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake. 16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake ni sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.

 

Wateule wa utaratibu wa Wafiladelfia wanafanywa kuwa nguzo katika Hekalu la Mungu (Ufu. 3:12). Ushindi ndio ufunguo ufanyao kazi kwa kipindi cha Milenia na kuwekwa katiku kwenye Mji wa Mungu.

 

Kupimwa kwa Hehalu kumechukua nafasi kwenye Ufunuo11:1. Hiyo naos au Hehalu ilikuwa ukweli ni wateule. Mji huu hauna Hekalu kama tutakavyoona. Mji huu ni hema yote kama unavyoendeleza uwepo wa Mungu kwa kila mmoja binafsi ukijumuisha kuta zake na utaratibu wake. Hii ni nyumba ya kiroho wa viumbe wanaoishi milele bila kufa tena.

 

Mji huu una jumla ya ukubwa wa dhira au maili kumi na mbili elfu (sawa na yadi mia mbli na ishirini) urefu kwenda juu kwake na upana wake. Ukubwa pia unategema juu ya wazo la elfu kumi na mbili ya kila kabila ila hapa imefanywa ili kuufanya Mjini kuwa wa mraba. Urefu wa stadioni (uwingi wake ni stadia) kimapokeo ya Kiyunani ilikuwa futi 600 – mfano ni sawa na yadi 200 kwa wastani. (Kwa mujibu wa Kamunusi ya Kiingereza iitwayo: Smith’s Dictionary of Greek and Roman Antiquities). Kulikuwa na miraba 400 katika stadioni moja sawa na yadi 215.5 (kwa mujibu wa kamusi iitwayo Interp Dict of the Bible, vol.4 p.838)

 

Stadioni kumi na mbili elfu ni =2,586,000 yadi, au 1,469 maili; au kilometa 2,364. Kwahiyo, kipimo cha ukuta ni 2,158,896 za maili za mraba au 5,586,624 za kilometa za mraba. Ukipimwa kwa kipimo cha stadia, Mji wa Mungu ni 1,728,000,000,000, za stadia za mraba. Stadioni ni sawa na kubiki 400. Dhira moja ni kipimo cha malaika na cha mwanadamu (angalia hapo chini). Yaani 1,728,000,000,000x400 inaweza kuwa jumla ya vipimo vilivyo husika.

 

Mji wa Mungu unatuama katika mgawanyo wa kiroho wa kikuhani wa wale watu 144,000.

 

Mji wa Mungu ni wa mraba uliokamilika kama Patakatifu pa Patakatifu katika Hekalu la Sulemani lilivyokuwa na mraba mkamilifu wa dhira ishirini. Madhabau ya Ezekieli 43:16-17 ni dhira kumi na mbili urefu na dhira kumi na mbili upana wake. Kwahiyo ukubwa unakuwa ni upanuzi wa mawazo ya Patakatifu pa Patakatifu na madhahabu. Kwa hiyo Mungu anapanua na kujinakilisha mwenyewe. Muundo wa Mji wa Mungu unategemea na uchaguzi wa wateule ambao wanaunda na muundo na ukubwa wake.

 

Ufunuo 21:17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibiandamu, maana yake, cha malaika.

 

Kuna Jeshi la malaika elfu moja katika halmjashauri kuu ya utawala. Mmoja kati ya elfu ya wandamu waliombolewa (Ayu. 33:23). Malaika huyu wa ukombozi alikuwa elohim wa Israel (Mwa. 48:15-16).

 

Ukuta ulikuwa dhira 144 za mraba na kipimo cha malaika hapa ni sawa na kile cha mwanadamu. Kwa hiyo, wanadamu hapa wanakuwa kama malaika au ndugu wa walio sawa na walio katika ulimwengu wa kimalaika kama watoto wa Mungu kulingana na ahadi za Kristo katika injili ya Luka 20:36. Kama tukidhani kutoka kwenye aya hii inayohusiana na hawa watu 144,000, kuna makundu 1,000 ya 144 yakifanya ukuta na muundo wa nje wa Mji wa Mungu. Tunaweza kuona kuwa mabaraza mawili ya watu 72 (yaitwayo hepdamakonta [duo] ya Luka 10:1,17) ndani ya 144. Hata hivyo, kulikuwa na makundi 1,000 ya Jeshi la malaika. Kulikuwa na 2,000 mara 72 katika 144,000. Hivyo watakuwa 2,000 kwa utaratibu wa wawili (au idadi ya 288,000 ya wanadamu na malaika) katika utawala wa ulimwengu mpya wa katika Kumbukumbu la torati 4:19 ukitawaliwa kutokea hapa duniani.

 

Ufunuo 21:18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yapsi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.

 

Utaratibu mzima utakuwa kama dhahabu iliyosafishwa kwa moto. Hakutakuwa na dhambi na itaonekana na wote kuwa nzuri na kamilifu.

 

Ufunuo 21:19-21 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi, wa tatu kalkedoni, wa nne zumaridi; 20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto. 21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.

 

Misingi ya Mji ilikuwa ni mitume kumi na wawili. Kila moja ya misingi hii umewekwa kama jiwe la thamani kama alama ya uwezo wake wa kurudisha nuru. Mawe yote ya thamani yamepimwa kwa kitu cha kurudisha nuru. Nuru ni Mungu na Mwana-kondoo. Kila moja katika kumi na mbili ana thamani ya kipekee.

 

Milango ya Mji ulikuwa na lulu moja. Lulu hiyo moja ni lulu ya bei kubwa ya wito wa Mungu (Mat.13:46). Lulu imetengenezwa kutoka kwenye mbegu iliyopandwa katika ganda la samaki wa baharini au chaza. Mbegu yaweza kuwa mchanga au changarawe. Pwani imetengeza lulu kwa kuiwekea tandu wa lulumizi juu ya mbegu. Mbegu hii ni mbegu ya haradari ya wito kama wa Roho wa Mungu. Ndio maana kila mlango una lulu moja. Kila mmoja lazima itengeneze lulu yake yenyewe na kuingia katika Mji wa Mungu kupitia malango ulio mwembamba (Mat. 7:14) kwa hiyo lulu ni wito wa Mungu ambayo ni njia ya kuingia katika huu Mji. Kila lulu imetengenezwa kutoka mbegu ya mwanzo na kujengwa na Roho Mtakatifu kama mazao ya pwani yenyewe au ya mtu binafsi. Hakuna mtu anayeweza kutoa nafasi hii ya kuingia au mazao hayo kwa mwingine. Hii ndio maana wale wanawali werevu hawakuweza kutoa mafuta ya taa zao kwa wanawali wapumbavu ambao hawakuwa na mafuta ya kutosha.

 

Malango ya Mji kusema ukweli yamejengwa juu ya sheria na ushuhuda (Isa. 8:20). Imejengwa utandu juu ya utandu, agizo juu ya agizo, mstari juu ya mstari (Isa. 28:10). Hii inafanya maarifa ya siri ya Mungu (Mat. 13:11-17,18-23).

 

Ufunuo 21:22-27. Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake. 23 Na mji ule hauitaji jua wala mwezi kuuangazia, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. 24 Na Mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake. 25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. 26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake. 27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

 

Sisi sasa tumeendelea mpaka kufika kwenye sehemu ambayo tumeona kuwa hatuhitaji Hekalu kama Mungu na Kristo wanakaa na kutamalaki utaratibu wote. Milenia ilikuwa ni kipimo cha gari kwa muundo mpya. Jeshi lote wanaongoka na muundo wote wa Mataifa unafanyika kuwa na mahusiano na Mji huu na kwa kweli sehemu yake kupitia wateule na utawala. Wote wanaongozwa na Roho wa Mungu ndio watoto wa Mungu (Rum. 8:14). Mpango huu wa Mungu uliwekwa kabla ya kuwekwa msingi wa ulimwengu.

 

Ufunuo 22:1-5  Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo, 2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwemo ndani yake. Na watumwa wote watamtumikia, 4 nao wamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. 5 Wala hapatakuwa na usiku tena, wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.

 

Mti wa uzima unarudishwa na tunda linatolewa kwa kuwaponya mataifa chini ya migawanyo kumi na mawili ambayo imetuama kwenye makabila kumi na mawili ya Israeli. Hivyo kila taifa limepandikizwa kwenye kabila moja.

 

Maisha ya kuishi bila kufa yametolewa kwa mataifa na wameponywa. Muundo wa utawala wa mbinguni bado utakuwa katika mgawanyo ambao Mungu alifanya chini ya watoto sabini wa Mungu wakati wa mwanzo (Kum. 32:8 kwa mujibu wa Biblia za RSV, LXX DSS). Mgawanyo wadunia ulifanyika kwa kufuata utaratibu wa makabila kumi na mbili katika robo nne ya duara kama tulivyoona kulikuwa na aina ya mwanzo na ya asili, lakini wakati huu hakutawa na kasoro yoyote katika utaratibu huo. Migawanyo hiyo inategemea kwenye sehemu ya tatu na ya thelethini, ya sabini na ya 120 na kuendelea chini mpaka 12,000 ya kila kabila. Wateule walipewa utawala chini chini ya jua kwa Milenia (Lk. 19:17-19) wakiwa kama malaika (Mat. 22:30). Ni watoto wa Mungu (Mat. 5:3-11). Nafasi hii imeendelezwa kwa mataifa yote. (Mat. 8:11), ikiwa ni furaha ya Mungu Baba (Lk. 12:32). Migawanyiko hii hufanya kazi kama wafalme na makuhani kwa uumbaji wa awamu nyingine ya maendeleo ya ulimwengu. Migawanyo 1,000 yaliyotajwa hapo juu na yanayotemea muundo wa wale 144,000 ambao wao wenyewe wana miundo mbinu yao yenyewe. Migawanyo hii ya 1,000 ya Jeshi la malaika linajumuisha pia na Jeshi la wanadamu 1,000. Hii basi itafanya mabaraza mawili ya 2000 ya 144 walioongelewa hapo juu, ya wotw wawili yaani wanadamu na malaika.

 

Jina la Mungu limewekwa kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu. Hivyo mamlaka ya Mungu kwa ulimwengu yatakuwa kwenye utawala chini ya Kristo Viumbe hawa watauhukumu ulimwengu. Wote ni elohim (Zek. 12:8) Watatawala dunia yote (Zab. 8:1-9; Dan. 2:44-45), na kutatolewa sheria mpya kabisa za kutumika ulimwenguni (Dan. 7:27,12:3; Kumb 4:19).

 

Ufunuo 22:6-9  Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za unabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi. 7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki. 8 Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo. 9 Naye akaniambia, Angalia, usimfanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki.Msujudie Mungu.

 

Aina yoyote ya ibada inastahili afanyiwe Mungu tu, au Eloah, pekeyake (Kum. 32:17). Wajibu wa wateule ni kuitii Biblia kama ni amri ya Mungu. Wateule wapewa kuelewa unabii kama vile inavyokuwa ni amri ya Mungu katika haki yake yenyewe. Hivyo, unabi wa Agano la Kale na Agano Jipya zinakuwa ni agizo au sheria ambazo wateule lazima wazitumikie kama zikiangukia kwenye uwezo wake. Hivyo, matengenezo ni agizo kwa wateule (soma Isa. 66:19-24). Tumeweka mikono yetu kwenye jembe na hatupaswsi kuangalia nyuma.

 

Ufunuo 22:10-14 Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. 11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; mwenye uchafu azidi kuwa mchafu; na mwenye haki, na azidi kufanya haki; na matakatifu azidi kutakaswa. 12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.. 14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake

 

Amri kwa hiyo inatoa haki kwa ule mti wa uzima lakini kupitia neema katika Kristo, mfano ushuhuda wa Yesu Kristo. Kwa hiyo ubatizo kutoka katika ushuhuda wa Masihi una hitajika sana kwanza kwa wokovu na ili kuweza kutimiliza sheria. Maonyo kwa ajili ya uvunjaji wa sheria yamerudiwa mara nyingi sana na kuwafanya watu kushindwa. Mawazo ya watu hawa huwa nje ya Mji wa Mungu hayamaanishi kwamba watu hawa bado watakuwa wanaishi wakati Mji huu utakapokuja. Ina maana kwamba walishindwa kuingia kwenye Mji huo wa Mungu wakati wa kipindi cha kujengwa kwake ambacho kilikuwa kutoka wakati wa mababa watangulizi wa imani na cha manabii mpaka mwaka 30BK, na kwa Kanisa kutoka mwaka 30BK mpaka Majilio, na kutoka Majilio hadi ufufuo wa mwisho wa wafu na hukumu. Wale wote ambao hawakutubu watachiliwa mbali nje.

 

Ufunuo 22:15-21 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabudu sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. 16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina la Mzao wa Daudi; ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi. 17 Na roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. 18 Namshuuda kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamuongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na mtu yeyote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. 20 Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu. 21 Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina

 

Kuelewa kitabu cha Ufunuo kumefunuliwa katika siku za mwisho. Uwezo wa kutenda juu ya ukweli ni kigezo cha kukazia. Kuelewa maana ya mpango wa wokovu kumetolewa katika mazungumzo ya wazi. Katika siku za mwisho, ujumbe umetolewa lakini hawakutubu. Kipindi hiki cha mwisho ni wakati wa kutisha. Mungu alimpa Shetani mamlaka ya kuona matokeo ya mwisho ya utaratibu wake. Ulimwengu unajiangamiza wenyewe na utaendelea kufanya hivyo, lakini bado tu hawatatubu. Hivi karibuni tu muda utafupishwa katika hiyo dunia inaweza kuokolewa.

 

Kristo amepewa mamlaka ya kutumwa na Mungu. Yeye ni mwanzo na mwisho. Mungu ametimilika, na kumkabidhi vitu vyote. Vitu hivi vyote vimepewa bure kwa mwanadamu katika anayemtii Mungu katika kuzitunza amri zake. Kristo anahimiza sheria za Mungu ili tuweze kupata uzima wa milele. Sisi ni Mji wa Mungu, uliojengwa katika msingi wa mitume katika Yesu Kristo.

 

q