Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[188]

 

 

 

Mvinyo Katika Biblia

(Toleo La 1.1 19970104-19990109)

 

Dhumuni la jarida hili ni kuendeleza yaliyoandikwa kwenye jarida la Uvijiteriani na Biblia (Na. 183) na kuandika au kutoa mtazamo na uwiano sahihi wa matumizi ya vinywaji vyenye kileo kutokana na jinsi Sheria au Amri za Mungu zinavyosema.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki ©  1997, 1999  Wade Cox)

(tr. 2014) 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Mvinyo Katika Biblia 


Kile kinachoitwa Siku hizi kuwa ni miungano ya Wakristo walio na kiasi na jumuia za makanisa pamoja na nyinginezo, zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza maana au kugeuza maana ya maandiko ya biblia. Ni maka ilivyokuwa kwenye mafundisho ya wavijiteriani ambayo pia imechangia kazi hii potofu ya kugeuza ukweli way ale yanayokusudiwa na maandiko ya biblia kuhusu mazingira yaliyoruhusiwa au kukatazwa kunywa kileo, lakini mafundisho yao yalituama kwenye makosa ya kujua mazingira yanayoelezewa na Maandiko Matakatifu na ni uasetiki dhaifu na usiofuata maandiko matakatifu ambao una tabia ya kutenda dhambi kwa sehemu zote mbili, yaani kwa Mungu katika sheria zake na Masihi kwa kuondolea mbali sheria zake.

 

Ni sawa na makanisa haya, kwa kweli yangeweza kumzuia Yesu Kristo asikubaliwa kubatizwa kwa ajili ya mtazamo wake na kwa ajili ya tabia yake ya kunywa mvinyo. Ni mtazamo huo huo wa kiasetiki ulishikiliwa kufundishwa na kuaminiwa kwenye jamii za Kiyudea kipindi cha karne ya kwanza iliyopingana na vyanzo vya imani za Wapythagorian na Wanostiki waliokuwa huko Kabbalah. Ni imani hii hii ya kiasetiki ndiyo iliyojipenyeza kwenye imani za Kiyahudi, Kiheathenism na hatimaye kwenye Ukristo. Hawa walikuwa ni waasetiki wale wale ambao walimuita Kristo kuwa ni mlafi na mpenda kunywa divai au mlevi kwa kuwa alikuwa anakunywa hadharani na kilamtu wakiwemo watuza ushuru na wenyedhambi (Mathayo 9:10-11; 11:19; Marko 2:15-16).

Mathayo 9:10-17 Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake. 11 Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? 12 Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. 13 Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi. 14 Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi? 15 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga. 16 Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi. 17 Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.

 

Maandiko haya mawili yote yanathibitisha kuwa Kristo aliketi chakulani na kwamba alikuwa pamoja na watu wengi alinywa mvinyo pamona nao.

Mathayo 11:19  Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.

 

Kuamini na kufundisha kwamba Kristo alikuwa anakunywa juisi ya zabibu wakati watu wengine waliomzunguka na wenyedhambi walikuwa wanakunywa mvinyo wenyewe na huku ikionyesha wazi kwamba alishutumiwa kwa kunywa nao ni jambo la kijinga na la kilaghai na kipuuzi. Hawa waliokutanika kunywa ni walewale ambao wengine wao walikuwa ni makahaba ambao hatimaye walikuja amini  na kuongoka.

Mathayo 21:31-32  Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. 32 Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.

 

Imani hii hii inayojifanya kujihesabia haki ndiyo iliyowaingiza hawa waasetiki leo na ndiyo sbabu uliyopelekea wenyedhambi na makahaba waurithi Ufalme wa Mungu wakiwaacha waliokuwa wakijihesabia haki wakiwa nje kipindi cha huduma ya Kristo. Marko anaandika habari hii hii akisema:

Marko 2:15-16 Hata alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata. 16 Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

 

Luka pia anaelezea habari ya kuongoka kwa watendadhambi hawa na uhusiano wao na kanisa (Luka 3:12). Wengi wa wafuasi waliokuwa kwenye kanisa la kwanza walikuwa ni waongofu waliotokana na watu hawa aliokuwanao wakijulikana kama wenyedhambi na makahaba ambao kwamba hawa asetiki wenye kujihesabia haki hawakuweza hata kuwashuhudia ama kuwakaribia.

Luka 5:29-35 Na Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake; palikuwa na mkutano mkuu wa watoza ushuru na watu wengineo waliokuwa wameketi chakulani pamoja nao. 30 Ikawa Mafarisayo na waandishi wao kuwanung'unikia wanafunzi wake, wakisema, Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? 31 Yesu akajibu akawaambia, Wenye afya hawana haja na tabibu, isipokuwa walio hawawezi. 32 Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu. 33 Nao wakamwambia, Wanafunzi wa Yohana hufunga mara nyingi, na kuomba dua; na kadhalika wanafunzi wa Mafarisayo; lakini wanafunzi wako hula na kunywa! 34 Lakini Yesu akawaambia, Je! Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa arusini, akiwapo bwana arusi pamoja nao? 35 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile.

 

Sababu iliyomfanya Kristo asijiangalie na kujijali mwenyewe ili kuwapendeza hawa waasetiki ni kwamba wao walijihesabia hakim no machoni pao wenyewe na kujihesabia haki kutokana na matendo yao yaliyotokana na mwenendo wao, kama inavyofanyika hata siku za leo. Hawauingii Ufalme wa Mungu wao wenyewe na kwa kukosea kwao kuwafundisha watu ukweli, wanawazuia wengine ambao wangeweza kutimiliza haki yote na kuuingia. Kristo alikunywa kileo pamoja na waamini wengine wa zamani.

Luka 7:29-34 Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. 30 Lakini, Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye. 31 Bwana akasema, Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini? 32 Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia. 33 Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. 34 Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.

 

Wanafiki kama hawa hawataweza kuuingia Ufalme wa Mungu kwa kupitia itikadi zao za kuwapendelea watu na huku wakishindwa kuzishika amri na sheria za Mungu.

Luka 15:1-7 Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. 2 Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao. 3 Akawaambia mfano huu, akisema, 4 Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone? 5 Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi.
6
Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea. 7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.

 

Watu hawa hawakuwa wadhambi tu kwa kuwa walikuwa wanakunywa kileo, bali ni kutokana na matendo yao ya dhambi. Lakini mkuu wao aliyekuwa anashirikiana nao bila kuwabagua kutokana na matendo yao ya dhambi, aliwaruzukia wokovu na msamaha wa dhambi watu hawa wote.

Luka 19:1-10 Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. 2 Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. 3 Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. 4 Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. 5 Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. 6 Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. 7 Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. 8 Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne. 9 Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. 10 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

 

Moyo wa mtu huyu ulikuwa ni wa unyenyekevu na wa kweli miongoni mwa hawa waliokuwa wanamshitaki na kumshutumu na washitaki wa ndugu zetu. Torati inaturuhusu kutumia kila aina ya kileo na sio mvinyo peke yake.

Kumbukumbu la Torati 14:22-26 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima. 24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako; 25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; 26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako

 

Hawa watetea imani ya ulaji wa mbogamboga tupu na kutokunywa kileo wanamsokoa Mungu na kuzipinga sheria zake na kuziona kuwa haziko sawa kutokana na madai yao ya kujihesabia haki. Madai waliyonayo watu hawa sio mapya. Yanatokana na imani ma mafundisho ya Wanostiki kama tulivyojionea kwenye jarida la Imani ya Kula Mbogamboga Tupu Kwenye Biblia (Na. 183) [Vegetarianism and the Bible (No. 183)]. Mabishano yanafanya madai kuhusu maandiko ya Biblia ili kukana ukweli wakidai kuwa eti mvinyo unaotajwa kwenye Biblia ukatolewa kwa maana chanya ulikuwa ni mvinyo wenye kileo na eti kwamba Kristo hakuunywa mvinyo huu wenye kileo. Samuele Bacchiocchi kwenye kitabu chake cha kuomba msamaha kwa waamini wenye mafundisho haya ya kutokunywa kileo, kitabu alichokipa kichwa cha somo Mvinyo Kwenye Biblia (Wine in the Bible), (abridged ed., Signal Press, Chicago, 1989) anajaribu kuendeleza kuelezea kwamba pale mvinyo ulipotajwa kwa matumizi chanya, haijalishi maneno yaliyotumika na tafsiri iliyotumika kuutaja mvinyo, kwa hiyo, mvinyo huu utakuwani ule usiochachuka, na ambao ni juisi tu ya zabibu, na kwa pale ilipoandikwa kutumika kwa matumizi asi, ndipo mvinyo huo utakuwa ni ule uliochachuka, pasipo kujali kuwa ni maneno hayohayo yametumika. Mtazamo na fundisho hili sio tu kuwa hauingii akilini au kuwa hayana ushawishi akilini, bali unaonyesha pia ukosefu mkubwa wa uelewa wa jinsi mchakato wa utengenezaji mvinyo ulivyo.

 

Mfano wa tatizo upo kwenye mlingaisho kati ya nchi ya Marekani na Ufaransa. Wafaransa wanakula kiwango kama hichohicho cha mafuta kwa kila mtu, sawa na wanavyofanya Wamarekani ila ina kiasi cha asilimia arobaini cha wanaopatwa mashambulizi ya maradhi ya shinikizo la damu zaidi kwa kuwa wao wanakunywa mvinyo wakati Wamarekani wengi wakiwa hawanywi ama kupendelea kunywa mvinyo. Haya ni mateso ya kibinafsi na ya kujitakia ambayo yanatokana na makosa ya kifikra inayotokana na mafundisho potofu ya Waprotestanti wa Kimarekani yanayotokana na makosa ya kutafsiri Maandiko Matakatifu na imani ya kiasetiki (yanayohusisha na mafundisho mapotofu ya ulaji wa nyama ya nguruwe na madawa kwenye maini, mama tulivyofafanua kwa kina kwenye jarida la TSheria ya Ulaji wa Vyakula(Na. 15) [The Food Laws (No. 15)].

 

Ukweli kuhusu imani hii ya wasetiki wanaojihesabia haki waliomuita Masihi kuwa ni mlevi na mpenda kunywa mvinyo au mlafi, kwa mujibu wa ushuhuda uliofanywa na Mitume watatu unathibitisha kuwa alikuwa anakunywa kileo. Iwapo kama ingewezekana kwa Kristo kuingia ma kunywa kileo kile kikiwa ni kitu kisicho chachuka ni kweli kwamba mitume wangeeleza ukweli huo kwa msisitizo na pasipo uficho. Ukimya wao kwenye jambo hili kunashawishi kuamini kuwa dhana hii sio sahihi. Mabishano yanatuama kutoka kwenye imani ya Wanostiki na yalidumu na kuendelea hadi kufikia zama ya Wanamatenmgenezo miongoni mwa Wamanicheani na Wamontana Wakathari au Wapuritani ambao ndio chanzo kikuu cha imani hii ya kiasetiki iliyoingia kwenye Uprotestanti wa leo. Bullinger ameyaelezea malumbano haya kwenye kitabu chake ukurasa wa Nyongeza (Appendix) 27 kwenye Biblia iitwayo Companion Bible.

 

Kamusi maarufu ya Biblia iitwayo The Interpreters Dictionary of the Bible, kwenye makala yake inapotaja Mvinyo, inasema kwamba unaotokana kwenye zama za kale za muungano wan chi za Syria-Palestina na ulikuwa maarufu kutokana na ubora wake uwingi na kiladha ya mvinyo (Vol. 4, uk. 849). Sinuhe Mmisri aliandika akisema kwamba eneo (nchi ya Yaa) ilikuwa na mvinyo mwingi zaidi kuliko maji (kwa mujibu wa Jarida la ANET 18-22; Pritchard, la The Ancient Near East, (Mashariki ya Karibu ya Kale), Vol. 1, uk. 7; sawa na ilivyoandikwa kwenye Hesabu 13:23,27). Ben Sirach anaielezea hii kuwa ni moja ya mambo mazuri...yaliyofanyizwa kwa watu wema (Ecclus. 39:25-26). Ingawa mvinyo ulitengenezwa zamani sana kutokana na mkomamanga na tarehe ama zama zake, mvinyo wa Wapalestina ulikuwa karibu na kuondolewa kutokana na juisi za zabibu zilizochacha (Interp. Dict., uk. 849; sawa na Wimbo Uliobora 8:2 umekuwa mkomamanga tena sambamba na mvinyo uliotiwa manukato). Tutajionea maneno manane ya Kiebrania yaliyotafsiriwa kama mvinyo kwenye Biblia. Kuyaelewa maneno haya kunaonyesha mwanga wa wazi kwenye somo hili la mvinyo kwenye Biblia.

 

Yayin

Neno yayin (kwenye SHD 3196) (huenda limetokana na lugha ya Caucasus kama ilivyo kwenye kamusi ya Interp. Dict., ibid.) linatokana na kiini au chanzo au shina la neno la yayanhadi kwenye neno chachuka au au kwenye uchachuko. Kwa hiyo inaufanya mvinyo kuwa kama ni kitu kilichochacha na kwa hiyo, mvinyo kuwa ni kinywaji chenye kuchacha, na kwa hiyo, inaweza pia kumaanisha kuwa ni kileo. Kwa hiyo inamaana pan asana, kama mvinyo wa sherehe na pia kuwa ni mvinyo uliowwekwa kwenye kiriba. Neno lililotumika kuuita kuwa ni mvinyo-mkali kwenye Mithali 23:20 kwa kweli ni neno lenye maana mbili ambayo ni wa walevi wanywao sana wa mvinyo au hii yayin (SHD 5433 na 3196). Kwa hiyo umamboleo umeendelea na mithali hii – na sio hali ya kujinyima. Neno Yayin limeandikwa mara 142 kwenye Maandiko Matakatifu na linahusisha mvinyo uliochachuka wa aina zote. Uandishi huu unaonekana kwamba wazee watakatifu sana wa zama za kale pia walikunywa aina hii ya yayin.

Mwanzo 9:20-21 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; 21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.  

 

Melkizedeki alimpa Ibrahimu hii yayin.

Mwanzo 14:18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.

 

Yayin inaelezewa kuwa ni kinywaji kinacholevya.

1Samweli 25:36-37 Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hata kulipopambazuka. 37 Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, mkewe alimwambia mambo hayo, na moyo wake ukafa ndani yake, akawa kama jiwe.

 

Yayin inaelezwa hapa kwamba ilipelekwa kwa Nabali. Neno linalosema kuwa alilewa sana kwa kweli linamaanisha kunywa kwa kuzidisha kiwango cha kawaida (SHD 7910, 5704, 3966; sawa na inavyosema kamusi ya Green’s Interlinear Bible). Yayin ni kiwango cha mwisho kwenye mchakato wa uchachishaji.

 

Ulevi wa Efraim ulishindwa (kushndwa) na hii yayin (Isaya 28:1). Yeremia anaeleza hiki akisema.

Yeremia 23:9 Katika habari za manabii. Moyo wangu ndani yangu umevunjika, Mifupa yangu yote inatikisika. Nimekuwa kama mtu aliye mlevi, Na kama mtu aliyeshindwa na divai;kwa ajili ya Bwana,na kwa ajili ya maneno yake matakatifu.

 

Kitabu cha fafanyzi cha Bullinger’s Companion Bible kinasema kwamba kutokana na maandiko haya yanaonyesha ilikuwa ni yayin bora sana na uliochachushwa kuwa kileo na wenye kulevya. Pia ni huu huu mvinyo aina ya yayin ndio uliotumika kwa matumizi ya mambo matakatifu na kwa ajili ya ibada za baraka.

Mwanzo 49:12  Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.

 

Baraka za Yuda zitachukua mkondo wake kwenye kipindi cha millennia kama Baraka kwa Israeli kwa ujumla.

Amosi 9:13-15 Angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka. 14 Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watafanyiza bustani, na kula matunda yake. 15 Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang'olewa tena watoke katika nchi yao niliyowapa, asema Bwana, Mungu wako.

 

Kwa hiyo watakunywa yayin kabisa. Neno asis pia linatumika na ambalo limetokana na neno asas – likimaanisha kikwazo – na linamaanisha ni mvonyo mpya wa mwaka wa kuvuna zabibu nnyingi. Tutaelezea zaidi hili hapo chini.

 

Biblia inaunganisha unywaji wa hii yayin kwa mwanadamu kama ni sehemu ya Baraka za Mungu.

Mhubiri 9:5-10 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. 6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua. 7 Wewe enenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako. 8 Mavazi yako na yawe meupe sikuzote; wala kichwa chako kisikose marhamu. 9 Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua. 10 Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

 

Hakuna madai yanayosema kwamba unywaji wa yayin utayatia unajisi au madoa mavazi ya kila mtu, lakini Mungu anayakubali matendo yao. Kudhania kwamba yayin ina sifa zote mbili za kuwa ni mvinyo unaolevya na usiolevya ni ya uwongo na kutia chumvi tu na zaidi sana yanainyisha kukosa uelewa kuhusu maneno haya na mchakato unaopitia utayarishaji wa mvinyo.

 

Kamusi inayojulikana kama Kamusi Kamilifu ya Kuuelezea Maneno Kuhusu Mvinyo wa Agano la Kale na Jipya (Vine’s Complete Expository Dictionary of Old and New Testament Words (uk. 288 ff)] inasema kwamba chimbuko la neno yayin yanaonekana kwenye lugha za Kiakadi, Kiugariti, Kiaramu, Kiarabu na Kiethiopia. Inasema kuwa ni neno la kawaida Kiebrania linaloelezea zabibu zilizochachuka. Kwa kawaida ulinywewa kwa burudani na ulikuwa ni kielelezo cha biashara (Ezekieli 27:18). Kamusi ya Strongholds iligawanywa wa watu pamoja nayo kwa lengo la kuzingira (2Nyakati 11:11).

 

Andko la Mithali 31:4-7 ndilo pekee linaloashiria kwenye Biblia kukataza kutokunywa mvinyo kwa baadhi ya watu walio kwenye daraja fulani na sababu zake fulani maalumu na hasa wafalme 

Mithali 31:4-7  Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo? 5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni. 6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.

 

Makatazo haya yanapingana na wale walio madarakani kutoa maamuzi au hukumu kwa mujibu wa Torati ili wasisahau kutoa hukumu kwa ajili ya kulewa kinywaji kingi na kikali. Mvinyo unamfanya mtu achangamke hata akiwa hajanywa bado (2Samueli 13:28). 

 

Ujumbe huu wa kunywa kwa kiasi na furaha au kuwa na kiasi kwa kila jambo, ni ujumbe uliorudiwa mara kwa mara kwenye Biblia. Mvinyo na pombe kali vilikuwa ni vitu muhimu vilivyotumika kwenye sherehe na maadhimisho ya namna mbalimbali mbele za BWANA kwenye Sikukuu (soma pia makala ihusucho Mvinyo kwenye kitabu hichohicho). Jaribio lolote la kufundisha vinginevyo, linatupeleka kwenye upotoshaji wa dhahiri wa Maandiko Matakatifu. Mwandishi Vine anasema kwamba yayin inasababisha ulevi wa dhahiri wa vileo (uk. 289) na inatumika kama kisarufi cha tirosh ambazo kwamba zote zinaweza kulevya (ibid.). Yayin inaweza kutajwa kuwa ni mvinyo kwa hatua nyingi mbalimbali.

 

Mnazarayo

Kiapo cha Mnaziri kinaendana sio tu na kutokunywa mvinyo peke yake, bali pia huhusishwa ma kujitenga au kutokula hata mbegu au tunda za zabibu au aina yoyote ya kitu kinachohusiana na zabibu (Hesabu 6:3-4,13-21).

Hesabu 6:3-4. atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka. 4 Siku zote za kujitenga kwake asile kitu cho chote kilichoandaliwa kwa mzabibu, tangu kokwa hata maganda. atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka

 

Maneno haya yanahusisha na mivinyo aina ya yayin na mishrat anavim ambazo zimeelezewa kama zabibu. Rabi Mkuu wa Sinagogi la Katikati ya Sydney, Rabi Franklin, ndiye aliye na mtazamo wa kwamba huu ni mchanganyo ama uharibifu wa tafsiri kati ya mvinyo na juisi ya zabibu hakuna msingi wowote wa kudai kutumika kwa neno hili la yayin au maneno menguine yoyote ua mvinyo unapokuwa kwenye mchakato wa kutengenezwa kwake vinatajwa kwa jina linguine zaidi ya lile la mvinyo uliochachuka na kulevya. Anasema kwamba tofauti iliuoko hapa kuhusu Wanadhiri au Wanazarayo wanaohusishwa kwenye makundi yote mawili ni aina ya aina ya mivinyo na juisi ya zabibu. Anarudia kutaja kutokunywa kwake kileo mwishoni mwa kiapo chake. 

Hesabu 6:13-21 Na sheria ya Mnadhiri ni hii, zitakapotimia hizo siku za kujitenga kwake; ataletwa mlangoni pa hema ya kukutania; 14 naye atasongeza sadaka yake kwa Bwana, mwana-kondoo mmoja mume wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa, na mwana-kondoo mmoja mke wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume mmoja mkamilifu kwa sadaka ya amani, 15 na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, mikate ya unga mwembamba iliyokandwa kwa mafuta, na mikate ya kaki isiyochachwa, iliyotiwa mafuta, pamoja na sadaka zake za unga, na sadaka zake za kinywaji. 16 Na kuhani atavisongeza mbele za Bwana, naye atasongeza sadaka yake ya dhambi, na sadaka yake ya kuteketezwa; 17 naye atamsongeza huyo kondoo mume kuwa dhabihu ya sadaka za amani kwa Bwana, pamoja na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu; kisha kuhani atasongeza sadaka ya unga nayo, na sadaka yake ya kinywaji. 18 Naye Mnadhiri atakinyoa kichwa cha kujitenga kwake, mlangoni pa hema ya kukutania, kisha atatwaa hizo nywele za kichwa cha kujitenga kwake, na kuzitia katika moto ulio chini ya dhabihu ya sadaka za amani. 19 Kisha kuhani atautwaa mkono wa huyo kondoo mume uliotokoswa, na mkate mmoja usio chachu atautwaa kikapuni, na mkate mmoja wa kaki, naye ataitia mikononi mwa yule Mnadhiri, baada ya kunyoa kichwa cha kujitenga kwake; 20 naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana; kitu hicho ni kitakatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa, na paja la kuinuliwa; kisha baadaye Mnadhiri ana ruhusa kunywa divai. 21 Sheria ya Mnadhiri awekaye nadhiri ni hiyo, tena ni sheria ya sadaka yake atakayomtolea Bwana kwa ajili ya kujitenga kwake, pamoja na vitu vile ambavyo aweza kuvipata zaidi; kama nadhiri yake awekayo ilivyo, ndivyo impasavyo kufanya kwa kuiandama sheria ya kujitenga kwake

 

Baada ya kukamilisha kiapo, Mnazarayo alikunywa yayin. Zaidi sana ni kwamba kiapo cha kujinyima vinywaji hakikugawanyika. Amri ilikuwa ni kwa namna yoyote. Masihi hakuwa Mnadhiri na wateule wamepewa amri kuu ya ukuhani. Hatahivyo, Mnadhiri alikunywa yayin baada ya kuhitimisha kipindi cha nadhiri zake. Hivyo basi, tunaona kwamba hii yayin ilitumika kwenye mambo ya kidini na sherehe au maadhimisho matakatifu na kwenye Sikukuu zilizoamriwa na Yahova (Kumbukumbu la Torati 14:24-26). Yayin ilikuwa ilitolewa na kumwagwa kama sadaka ya kinywaji kwa Yahova (soma Kutoka 29:40; Walawi 23:13 na Hesabu 15:5).

 

Hakuna tofauti yoyote ile hapa kabisa, iwe ya Kibiblia wala ya kihistoria, kuhusiana na jina la hii yayin ambalo lingeweza kutumika kuelezea maana ya hii yayin yenye kulevya. Kitendo cha kudai kwamba Mnadhiri alijitenga na unywaji wa kileo hiki cha yayin na kwamba alikunywa aina hiyohiyo ya kinywaji kisicholewesha cha yayin, kama hiyo ingewezekana kipindi cha kuhitimisha nyapo zake ni kujaribu tu kuweka dhana fikirika ambayo haina mashiko yoyote kabisa ya kihistiria na kwenye ukweli. Neno lililo sahihi kuiita juisi ya zabibu kwa lugha ya Kiebrania ni mishrat anavim.

 

Tirosh

Yayin inatengenezwa kutokana na Tirosh ingawa yayin inaweza kuwa imezoeleka. Kamusi ya “The LXX” inaitumia neno oinos katika kutafsiri aina hizi zote mbili za yayin na tirosh. Neno tirosh (kamusi ya SHD 8492 imeandika tîyrôsh) linatokana na neno asilia la kwenye (kamusi ya SHD 3423 yarashkuendelea au kumiliki (kwa kuwafukuza wapangaji wetu wa zamani). Kwa hiyo inaweza kumaanisha kuteka, kunyang’anya, kurithi, au kufukuza. Ni mali iliyolowa na yautepetevu. (au divai mpya) na unaitwa tirosh (kwa mujibu wa kitabu cha fasiri cha the Companion Bible) kwa kuwa inakuwa na mashiko kwenye nia iliyo kwenye maana asilia. Kamusi ya Strong inaamini kuwa inaweze kufanyika kuwa ya kulevya upya na mvinyo mtamu. Inaonekana mara 34 kwenye Agano la Kale. Tirosh inakuwa ni utenzi wa kishairi unaoelezea mvinyo unaotumiwa kidini. Kwenye maandiko ya Qumran, imetumiwa kwenye uhitimisho ya yayin (Kitabu cha fasiri cha Interp. Dict., ibid.). matumizi haya ya neno hili huenda yanahusiana na dhana iliyo miongoni mwao ambayo ilikuwa ni kundi kamilifu, kwenye uwekaji mbadala wa ukengeufu wa kikuhani wa Hekaluni. Walikuwa pia wanatokana na imani ya waasetiki.

 

Maranyingi Tirosh inachukuliwa inatokana na zabibu ya mavuno kutoka kwenye Mwanzo 27:27-28.

Mwanzo 27:27-28 Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana. 28 Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo.

 

Malumbano haya yalitumiwa na Samuele Bacchiocchi (kwenye kitabu chake cha Mvinyo Kwenye Biblia [Wine in the Bible], Signal Press, 1989, uk.22). anaamini na kufundisha kuwa kutumika kwake kuwe ni kwa zabibu au kwa juisi ya zabibu njema kwa kuwa zilikuwa zimekwisha kuvunwa tayari pamoja na nafaka na mafuta. Bullinger amekwisha elezea hili tayari na kuendelea kuamini kwenye maelezo yake hainishi kwa kutumia neno synedoche kutaja kimiminika na vitu vigumu (mahindi – nafaka au ngano – SHD 1715 dagan na mvinyo tirosh). Dagan kwa hiyo ni maongeo ya mashambani. Bacchiocchi anafanya shutuma zisizo za kawaida dhidi ya Masihi kwenye nukuu zake zilizo kwenye ukurasa wa 43 kuhusu muujiza wake wa maji na mvinyo (Yohana 2:10).

 

Msimamo unaokazia imani hii unadai kwamba Kristo asingeweza kutengeneza kimiujiza kiasi kingi cha mabalasi yanayokadiriwa kuwa idadi ya magaloni 120 na 180 ya mvinyo wenye kulevya na kuwapa wanaume, watoto waliohudhuria na kukusanyika kwao huko kwenye arusi ya Kana, pasipo kulaumiwa kwa kulewa kwao. Mtazamo na msimamo wa Maandiko Matakatifu na kimaadili vinahitaji “mvinyo mwema” uliotengenezwa na Kristo ulikuwa ni mvinyo mwema, wa juisi ya zabibu zisizochachushwa na kulevya. Mtazamo huu unaungwa mokono na mtazamo ule ule uliotumika kuelezea hili, ambao unajulikana kama kalos, ambao unaonekana kwamba kimaadili ni mzuri na bora sana, badala ya ule unaojulikana kama agathos, ambao ni mzuri tu sana.

 

Mabishano haya yasiyo ya kawaida wala umuhimu ya Bacchiocchi yanadhania kwamba huenda Masihi aliutengeneza kwa kiwango kisichohitajika cha mvinyo iwapo kama ungekuwa na kileo kabisa basi wahudhuriaji wa arusi hiyo wangeweza kuwa wamelewa kwa kunywa kiasi hiki cha magaloni 120-180 kwenye mabalasi sita yaliyokuwa na metretes mawili au matatu (ilivyodaiwa kuwa ni firkin kwenye biblia ya KJV). Madai haya yamefanyika pasipo uelewa wowote wa kipindi cha muda ambao sherehe hii ilichukua. Kwanza kabisa, kijiji cha Kana ilijumissha wageni wa namna mbalimbali wakiwemo wanafunzi wakiwa kama ni wageni waliokuja ghafla. Vijiji vyote viwili kwa kawaida vilihusika na ndipo sherehe pia ilikwisha, baadae kidogo kwa kipindi cha juma moja zaidi. Hii ingewahusisha mamia wengi, kama sio maelfu au zaidi ya wahudhuriaji au wageni waalikwa.

 

Tungeweza kudhania kwamba metretes iliyohusishwa hapa ilikuwa ni kipimo cha Aeginetan ambacho ni sawa, kwa mujibu wa Cleopatra, Galen na Didymus, wakiwa kama Wababelonia, Waashuru au Antiochean metretes na kwamba hii sio tafsiri ya Kiyunani peke yake itokanayo na kijineno kidogo cha Kirumi amphora. Metretes ya wa Aeginetan ilikuwa na ukubwa wa mita tanotano mbili zaidi ya metretes ya Attic ambayo ilikuwa na ukubwa nusu ya amphora ya Warumi iliyoendeleza ujazo wa magaloni mengine manane (tazama Kamusi inayoitwa Smith’s Dictionary of Greek and Roman Antiquities, second ed., London, 1851, art. Metretes, p. 762). Kwa hiyo tunajikuta sasa tukiwa na magaloni kati ya sita na kumi yanayoongezwa kwa mawili au zaidi ya magudulia matatu katika kila magudulia sita. Kwa hiyo tunakuwa sasa na magaloni idadi ya kati ya 72 na 180 – na siyo kati ya magaloni 120 na 180 kama inavyosema tafsiri ya  RSV na jinsi inavyoonyesha. Lakini ikumbukwe pia kwamba hakuna dalili inayoonyesha kipindi kilichotumika kusherehekea arusi hii kuwa kiligharimu siku ngapi, wala idadi ya waliohudhuria hawajulikani (nukuu iliyochukuliwa kwenye Yohana 2:1 kwenye tafsiri ya the Companion Bible inasema kuwa iliendelea kwa kipindi cha takriban juma moja). Mvinyo unaoonyeshwa kutumiwa hapa ni ule wa aina ya oinos ambao umetumika kwenye tafsiri ya the LXX kutafsiri kutoka kwenye lugha asilia ya Kiebrania ambayo inauita yayin ambao ni mvinyo uliochachushwa na kulevya na ambao ndio huu unaoitwa tirosh kwa maana hii na ulivyotumika hapa.

 

Kitabu cha fasiri cha the International Standard Bible Encyclopedia (pp. 1050ff.) inaonyesha kwamba metretes ulikuwa na kiwango sawa bath, wakituamanisha kulinganifu na kitabu cha fafanuzi cha Josephus (cha A of J, viii, 2.9 [57]), na pia fafanuzi yake ya kwamba kor ilikuwa ni sawa na vipimo kumi vya metretes – wakati kwamba ni kama vipimo kumi vya baths (xv, 9.2 [314]). Kwa hiyo, magudulia huenda yalikuwa ni sawa na vipimo  vya baths mbili au tatu. Kila bath moja ulinganifu wake ulikuwa ni kama wastani wa lita 39 (ISBE, p. 1051). Kwa hiyo, magudulia haya yalikuwa na ujazo wa wastani ya kati ya lita 78 hadi 117 kila moja.

 

Kitendo cha kuishiwa mvinyo kwenye sherehe ya arusi ya Wayahudi kilikuwa ni maka msiba au maafa kwenye mawazo na desturi ya Wayahudi na kwa watu wengine wengi pia. Kingeweza pia kuchukuliwa kama kielelezo cha hatima ya maisha ya familia. Huenda hali ilijitokeza hivi kwa ajili ya idadi ya wahuduriaji ilikuwa kubwa kuliko ilivyotarajiwa na ilichukua siku nyingi kuhitimishwa kuliko ilivyotarajiwa. Muujiza ulihitajika kufanyika katika siku ya pili ama ya tatu ya siku saba hizi za sherehe. Siku tatu zingehusisha siku ya tatu baada ya tukio la mwisho, ambazo kwazo walishindwa kwenye sherehe nah ii huenda ilikuwa ndiyo nia iliyokuweko kwenye Yohana 2:1. Hii ndiyo ilikuwa ni Kana ya Galilaya iliyokuwa kwenye barabara ya kutoka Nazareti kuelekea Tiberio na ambako Mesihi na familia yake na marafiki zake walikuweko, na ambayo huenda ilihusisha wakazi wengi wa Kana na Nazareti. Mamia wengi huenda walikuwepo. Na mkuu wa meza alishuhudia ukweli kwamba kulikuwa na idadi ya kati ya magaloni 72 hadi 180 na ambayo ndiyo yalihitajika kutumiwa na watu wale kwa kipindi siku kadhaa walizojumuika pale na kwa msingi huu mgao ungeweza kuwa ni wa magaloni kati ya 18 hadi 45 ya mvinyo kwa siku.

 

Kwa idadi ya watu mia mbili, ambao huenda wangekuwa ni waafidhina sana, basi wasingekuwa na zaidi ya mgao wa viroto wviwili kwa siku kwa kila mtu na huenda ungekuwa ni mgao chini ya hapo. Kiroto komoja cha mvinyo kwa siku au pombe nyingine ni kiwango kizuri sana kumpa mtu kwa siku moja. Hii ilikuwa ni sherehe. Badala ya kujaribu kumtwika mzigo wa dhambi Masihi (kama wanavyoonekana kujaribu kumtia hatiani kutokana na mawazo yao kwa jinsi yanavyoshindwa kukubaliana na ukweli huu) kwa kuwa ni ukweli usiopingika kabisa kwamba Masihi alitengeneza mvinyo mzuri pale arusini, na tunatakiwa kuangalia ukweli wote ulioko nyuma yake kuliko kuuchukulia kwa namna nyingineyo. Masihi alitengeneza mvinyo (kwa mujibu wa SGD 3631) aina ya oinos au yayin kwenye arusi na kwa ubora wa namna hii kama ulivyokuwa unajusifika kwa ubora na kwa wingi uliohitajika sawa na mahitaji yalivyokuwa. Neno kalos (SGD 2570) linamaanisha nzuri au bora lakini hasa linamaanisha ubora kama kuwa cha thamani au uzuri wa kimuonekano au kwa matumizi na huwa inatofautishwa na agathos (SGD 18) ambayo ni uzuri wa ndani (tazama fafanuzi za kamusi ya Strong’s). Hakuna mtazamo wene kanuni ya kimaadili hapa kuhusiana na umuhimu wa juisi ya zabibu na mvinyo. Zaidi ya yote ni kwamba hakuna dalili kwamba hizi zote zilinywewa kwenye sherehe za arusi. Ukweli wa kwamba maana ya neno divai hii njema ilitunzwa au kuhifadhiwa mahali hadi kufikia siku ya mwisho ulifanywa ili ionekane kuwa tunaongelea kileo. Mabii Elisha alifanya muujiza kama huohuo wa mafuta na hakuna dhana kwamba kiwango au muujiuza ulikuwa ni sawa na halisia (2Wafalme 4:1-7). Inadhaniwa na kudaiwa tu na watu wanaoona kuwa ni mapepo kuwako kwenye magudulia ya mvinyo.

 

Muujiza wa kubadili maji kuwa divai huenda ni mfano wa moja kwa moja wa mjadala uliopo kwenye mfumo wa imani za duniani kwa mafundisho yanayolinganisha maji kuwa sawa na Yuda na mvinyo kuwa sawa na Kanisa linaloongozwa na Roho Mtakatifu. Mvinyo hauashirii tu damu ya Masihi peke yake, ambayo ilikuwa ni kitu pekee muhimu ili kumpokea Roho Mtakatifu, bali ni ukweli muhimu mwingine kuwa mvinyo ni tunda mzabibu wa Bwana. Hakuna shaka kuwa muujiza ulikuw wa muhimu au kiwango chake kilikuwa sahihi kulinganisha na mahitaji.

 

Shutuma zisizo za kawaida na zisizo sahihi kuhusu mvinyo imefikia kiwango cha juu kwenye kitabu cha fafanuzi za Bacchiocchi ukurasa wa 49 kwenye makala hii.

Kama kuna umuhimu kuhusu kikombe [kwenye Mlo wa Meza ya Bwana] ambacho ni cha mvinyo wenye kulevya, basi Kristo kwa hakika asingesema: “Kunyweni ninyi nyote” (Mathayo 26:27; cf. Marko 14:23; Luka 22:17), hususan kwa pale tunapoona kwamba hili lilikuwa ni adhimisho la kikombe cha Pasaka ambacho hakujumuisha tone la mvinyo peke yake, bali na vikombe vingine vitatu. Ndipo Kristo kwa kweli alisema na kuwaamru “wote” miongoni mwa wanafunzi wake akiwamuru wanywe kikombe, ambacho ni cha mvinyo wenye kileo. Kunabaadhi ya watu ambao kwao huona kwamba kila aina ya kileo kina madhara tu. Watoto wqadogo wanaoshiriki mlo wa meza ya Bwana wasiruhusiwe kwa namna yoyote ile kugusa mvinyo. Kuna wengine ambao kwao kitendo cha kunywa mvinyo kidogo tu au hata wakipata harufu tu ya aina yoyote ya kileo kunaamsha tama au hamasa ya kupenda ama kuendelea kulewa hadi kufikia kiwango kibaya. Je, Kristo aliyetufundisha kuwa tunapoomba tuombe “Usitutie majaribuni” angeweza tena kuifanya ibada hii ya ushirika wa meza yake iwe ni mahala pasipoepukika pa kuwatia watu wajaribuni kwa baadhi yao na kuifanya iwe hatari kwa wengine? Mvinyo unaonywewa kwenye Mlo wa Ushirika wa Meza ya Bwanaa hauwezi kupokelewa bure ama kwa kwa maana mbaya kwa kadiri ulivyokuwa ni wa kilevi na unalevya.

 

Aina hii ya kuhoji na kudadisi ni ya kipuuzi. Kulikuwa na wanaume watu wazima kumi na wawili jumlisha na mwingine mmoja aliyekuwa mhusika wa mlo huu. Kwa hiyo, kuhusu kikombe au kipimo kidogo cha mvinyo kwa kila mmoja ilitolewa. Watoto hawaruhusiwi kushiriki mlo huu kwa namna yoyote ile. Inaonekana kwamba tofauti iliyopo kati ya siku ya 14 na 15 Nisan haieleweki na Bacchiocchi. Hakukuwa na madai yoyote kwenye Kanisa ambalo vinywaji visivyo na kileo havitumiwi kwenye ushirika wao wa Meza ya Bwana. Kwa kweli, Katiba au Imani ya Mitume inaonyesha kwamba ilijulikana kama ya kuruhusu ama kunywa kileo na ni sehemu ya mchakato wa kidini (Bk. VIII, Ch. XLIV, and Canon 51, 53, ANF, Vol. VII, p. 503). Kwa hiyo, mvinyo unatafsiriwa kuwa ni kileo na Kanisa kwa mfano mmoja liliuchukua na kuutumia kwa kiwango cha kuhakikisha kuwa lingekuwa ni jambo au suala ya Wakorintho. Ufafanuzi au tafsiri ya kuwa mvinyo ule haukuwa na kileo kwa jinsi alivyoutoa Masihi, inajaribu kutafuta sababu zisizo na mashiko za kujitafutia kujitia hatiani. Wanadai wamba iwapo kama Masihi alikuwa na mvinyo halisi basi angekuwa ametenda dhambi. Kwa nini? Kwa kuwa watu hawa wana mafundisho na imani ya kiasetiki. Ni watu wa aina ileile waliokuwa kwenye mkumbo mmoja wa namna nyingine wa kumshutumu Masihi na kumuita kuwa ni mlevi na mlafi. Huenda wangeweza kumkatalia asibatizwe kwenye kanisa lake mwenyewe. Kanisa kwa mabadiliko yake mbalimbali ya kimifumo, yamekuwa yakikitoa kikombe hikihiki cha ushirika kwa kipindi cha miaka 2,000 bila ya matatizo yoyote na watu wengine wowote ila kwa hawa wasetiki peke yao.

 

Hakuna shaka yoyote ile kuamini kwamba yayin iko tofauti na tirosh na zote mbili zinatumika kwenye burudani za vileo kama tunavyoona kwenye kitabu cha nabii Hosea.

Hosea 4:11  Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.

 

Tirosh inatokana na tunda zilizokamuliwa za zabibu.

Mithali 3:10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.

 

Matukio ya ibada za ubarikio na ulinzi wa Mungu yalifanywa kwa kuhusisha aina hii ya mvinyo.

Isaya 62:8 Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.


Yoeli 2:24 Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta.

 

Pia tofauti inakuja kutokana na sehemu ya laana.

Mika 6:15 Utapanda, hutakunywa lakini hutavuna; utazikanyaga zeituni, lakini hutajipaka mafuta; na hizo zabibu, lakini hutakunywa divai.

 

Tofauti hii inaonyesha kwamba tirosh ni kinywaji kilicho kwenye mpito wa kuchachuka na kulevya wakati kwamba yayin inatengenezwa na yenyewe ni mvinyo mpya. Neno tirosh limetafsiriwa kutoka kwenye neno la Kiyunani kama lilivyoandikwa kenye kamusi ya SGD 1098 gleukos likimaanisha kuwa ni divai mpya au njema na ilitumika na mvinyo mtamu na uliochachuka na wenge nguvu kubwa kulevya (Strong’s).

Matendo 2:12-16 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? 13 Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya. 14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,

 

Hakuna shaka kwamba hii must au tirosh au gleukos zilikuwa ni aina ya mvinyo mchachu na wenye kulevya. Mtume Petro hakupinga kuwa hawakunywa mvinyo. Kile alichokanusha ni madai ya maadui zake kuwa walikuwa walevi, zaidi ya kiwango chao cha unywaji wenye kiasi, bali kwa msingi wa ukweli kwamba ilikuwa ni majira ya saa tatu ya mchana muda ambao hawakupaswa wawe wamelewa. Hii ilitokana na madai kwamba walikuwa wameamka mapema sana alfajiri na wakaenda kufuatilia kileo cha pombe kali.

Isaya 5:11 Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!

 

Mitume walikunywa mvinyo, kama invyoonekana kwenye ushuhuda wa Biblia. Ulikuwa ni mvinyo ulevyao. Na iwapo kama hawajakunywa mvinyo wa kweli, basi ingeonyeshwa kwenye Biblia pia na ukweli wa mambo ni kwamba haikusemwa hivyo kamwe. Mtume Paulo hakuwaambia Wakorintho kuwa wasinywe mvinyo, bali aliwaasa wafanye mambo kwa heshima na nidhamu, na kwa staha na utaratibu majumbani mwao (1Wakorintho 11:21-22).

1Wakorintho 11:21-22 kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. 22 Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo. 23 Kwa mkwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. 22 Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.

 

Alimwambia Timotheo anywe mvinyo kwa minajiri ya afya yake      (1Timotheo 5:23).

 

Makatazo yaliyotolwa ya unywaji wa mvinyo mkali kwa wateule yanahusu kwa makuhani wanapomkaribia Mungu kuhudumu hekaluni mwake.

 

Mambo ya Walawi 10:9 Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;

 

Hili ni jambo linaloonekana kwa wazi kabisa na la msingi kuhusu unywaji wa vileo mbele za Mungu. Mzee wa kiume ama wakike hatakiwi kubobea au kuzoelea ulevi (dedoulomenas) au kuwa mtumwa wa ulevi wa aina yoyote ya mvinyo au pombe. Mtu hatakiwi kuwa mtumwa wa ulevi (1Timotheo 3:3,8; Tito 2:3). Imeandikwa Sophron kwenye Tito 1:8 ikimaanisha hekima au mtazamo mwema au uangalifu (na ndivyo ilivyo pia kwenye Tito 2:2,5; 1Timotheo 3:2; sawa na Marko. 5:15; sawa na ilivyoandikwa kwenye kitabu cha fafanuzi cha Marshall’s Interlinear maeneo mengi).

 

Chemer

Andiko lililoandikwa tunalolikuta hapa kuhusu mvinyo ni chemer (SHD 2561) na pia chamar (SHD 2562) kutoka kwenye (SHD 2560) châmarkupasha moto. Kwa hiyo, linamaanisha tkuchachisha na hamira au chachu; kuchachusha kwa kuifanya ionekana nyekundu. Maneno haya yanatoka kwenye kitabu cha (SHD 2564) chemar au bitumen. Chemer nk, linaonekana mara nane na linatumika kuelezea mvinyo bora na mwekundu uliotokana na mchakato wa kuuchachusha, na kamusi ya SHD 2562 inautaja huu kama ni ule mvinyo mwekundu.

 

Kumbukumbu la Torati 32:14 inaongelea juu ya siagi safi ya zabibu.

Kumbukumbu la Torati 32:13-14 Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume; 14 Siagi ya ng'ombe, na maziwa ya kondoo, Pamoja na mafuta ya wana-kondoo, Kondoo waume wa Kibashani, na mbuzi, Na unono wa ngano iliyo nzuri; Ukanywa divai, damu ya mizabibu.

 

Biblia tafsiri ya Interlinear Bible inaonyesa kutoka kwenye maandiko yake muhimu na tafsiri yake kwamba andiko hili limemaandikwa hivi: na kutoka kwenye damu ya mzabibu utakunywa mvinyo (au chemer).

 

Bwana ameruhusu, nwa kwa kweli amewapa kitu hiki wakitumie Israeli.

Isaya 27:2-3 Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni. 3 Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.

 

Uzao huu wa mvinyo safi na mwekundu uligawanywa kwa maelekezo ya Koreshi na Artashasta kwa Israeli ili wakamtumikie Mungu wa Mbinguni. 

Ezra 6:9 Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng'ombe wachanga, na kondoo waume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa;

 

Ni vigumu kutengeneza chemer isiyo na kuilevi hata kama uangalifu wa namna yoyote ile ukiwekwa kuwalinda wasiotumia ukawekwa. Kuamini kwamba mchakato unaotajwa wa kuchemsha unamaanisha ni wa kukausha tu ili kuondoa unyevuunyevu kwenye mvinyo ili kuufanya uwe nimvinyo usio na madhara ambao ni juisi za zabibu peke yake ni jambo lisilosahihi kabisa. Bullinger anasema Marabi waliuita mvinyo bora, kwa kuwa ulikuwa hauchanganywi na maji, na kwa kuwa ule ulioshanganywa na maji unachosha kichwa na ubongo au fahamu (Companion Bible, App. 27, III).

 

Shekar

Neno hili lilivyoandikwa kwenye kamusi ya (SHD 7941) limetafsiriwa kumaanisa kileo kikali na linatokana na neno shakar (SHD 7937) likimaanisha kuwa kuweweseka au kulewa. Ni kileo kinacholevya kwa ukali sana au pombe kilichotengenezwa kwa shayiri, asali au mtama. Ni kileo kilichosawa na whisky au gongo au ni kama pombe kali.

 

Kinatumika kama sadaka ya kinywaji kwa Bwana kilichotumika Mahali Patakatifu na ilitolewa kama Baraka kwa sikukuu.

Hesabu 28:7 Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa robo ya hini kwa mwana-kondoo mmoja; hiyo sadaka ya kinywaji, ya kileo, utammiminia Bwana katika mahali hapo patakatifu.

 

Sheria ama kanuni ya sikukuu inajumuishwa na Baraka hii moja kwa moja na inahusiana na uuzaji na ulaji kwenye sikukuu vikitumika vyote viwili, yaani yayin na shekar.

Kumbukumbu la Torati 14:25-26 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; 26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako

 

Kusema au kuamini kuwa vinywaji hivi vilikuwa havina kileo ni ibishi wa kipuuzi.

 

Asis

Neno hili linatokana na neno asas linaloashiria au kumaanisha mvinyo mpya au mtamu wa mwaka vintage. Neno hili linaonekana kwenye Isaya 49:26.

Isaya 49:25-26 Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu. 26 Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na wote wenye mwili watajua ya kuwa mimi, Bwana, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo. 

 

Mtazamo huu unawezakuwa ulitokana na maana iliyo kinyume ingawaje ilikuwa inahusiana na baraka na ulinzi wa taifa. Hata hivyo, dhana iliyotumika kuelezea kwenye Yoeli 3:17-18 na Amos 9:13 inaonyesha kuwa ni baraka inayotolewa na Mungu na imeelezea kuwa hivyo na yeye. 

Yoeli 3:17-18 Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe. 18 Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya Bwana, na kulinywesha bonde la Shitimu

 

Amosi 9:13 Angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka

 

Hii asis ni Baraka ya millennia ya Mungu.

 

Sob’e

Neno hili linahusu kila aina ya kinywaji chenye kileo na linatokana na neno sab’a linalomaanisha kunywa, kupitiliza kiwango cha ulevi au kuwa mlevi. Kuchanganya mvinyo na maji kulichukuliwa kama ni kitendo cha kughoshi au kupunguza ukali na hakikutakiwa kufanyika. Nabii Isaya analiyumia neno hili akimaanisha kuwa kitendo cha kupunguza ukali kuwa ni adhabu.

Isaya 1:22 Fedha yako imekuwa takataka, divai yako imechanganywa na maji.

 

Nabii Hosea analitumia akimaanisha kuondoa uwezekano wa kujiburudisha.

Hosea 4:18 Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu.

 

Kusudi la kutumia hivyo huenda halionekani vizuri kama ilivyo kwenye tafsiri ya RSV ambako limetumika kuelezea utumwa au kuzoelea kilevi zaidi kuliko aina ya sob’e ikiwa imetiwa nguvu.

Hosea 4:18 Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu.

 

Mambo mawili haya yanahusu uwezo mdogo wa taifa.

 

Mamsak

Neno Mamsak (kwenye SHD 4469; kutoka kwenye SHD 4537 lenye maana ya kuchanganya hasa kwenye mvinyo) linahusu mvinyo uliochanganywa au uliowekwa manukato. Mithali 23:30 inalitumia kwa maana kwamba ni kitu cha kulevya tu kabisa. Ukaaji wake haukutakiwa uwe mrefu sana zaidi ya unavyokaa yayin na kinywaji hiki – zaidi ya kutokunywa. 

Isaya 65:8-12 Bwana asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote. 9 Nami nitaleta uzao toka Yakobo, na mrithi wa milima yangu toka Yuda, na mteule wangu atairithi, na watumishi wangu watakaa huko. 10 Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng'ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. 11 Bali ninyi mmwachao Bwana, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandika meza kwa ajili ya Bahati, na kuijazia Ajali vyombo vya divai iliyochanganyika; 12 mimi nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu nilipoita hamkuitika; niliponena, hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia.

 

Hapa, mamsak inatumika kama sadaka ya kinywaji lakini Mungu anawalaumu kuwa waliitumia kwa kwenda kuimwaga milimani wakiwapa miungu mingine wa uwongo. Hawa ni wale walioandaa meza kwa Bahati (RSV). Ni sadaka ka kinywaji kwa Eloah peke yake

Isaya 65:8-12  Bwana asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote. 9 Nami nitaleta uzao toka Yakobo, na mrithi wa milima yangu toka Yuda, na mteule wangu atairithi, na watumishi wangu watakaa huko. 10 Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng'ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. 11 Bali ninyi mmwachao Bwana, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandika meza kwa ajili ya Bahati, na kuijazia Ajali vyombo vya divai iliyochanganyika; 12 mimi nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu nilipoita hamkuitika; niliponena, hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia.

 

Mungu wa Wababelonia wa Bahati alikuwa ni anaitwa Gad (SHD 1408) jina hili hutamkwa gawd, anayeitwa Baal-Gad kwenye Biblia na anajumuishwa na kikosi kazi (tazama fasihi ya Strong’s). Yahova anaona wivu hapa kwa ajili ya wao kuwatolea sadaka hii ya kinywaji mungu mwingine. Hainana maana kwa kitendo hiki cha kupunguza nguvu za kileo au thamani ya vinywaji vyenye kileo za mamsak ikiwa ni sadaka ya kileo.

 

Shemarim

Neno hili (kwa mujibu wa SHD 8105) huitwa shemer (im; uwingi) limetokana na jinsi lilivyoandikwa kwenye (SHD 8104) shamar maana yake kuhifadhi au kulinda au kuhudumia. Imetafsiriwa kama dregs. Kwa mapokeo ya siku za zamani kale, mvinyo uliruhusiwa kubaki na mabaki ya machicha au makapi kwenye viriba au viroto. Ilikuwa na utamu sana. Ulitakaswa baada ya kipindi fulani na kisha kusafishwa uwe bora zaidi.

 

Mungu amebakiza mvinyo kwa Wamataifa, ambao ndiyo walikuwa makapi. Hii ina pande zote mbili za asi na chanya. Upande asi ulikuwa kwamba Mungu alihifadhi wokovu kwa Wamataifa. Jambo hili halikueleweka vizuri kwa Yuda. 

Zaburi 75:8 Maana mkononi mwa Bwana mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.

 

Hapa tunakutana na mvinyo mzuri zaidi wa aina ya yayin uliohifadhiwa na Mungu ukiwa ni kama Baraka za watu wake ukiwa umetolewa na kupewa wao kwenye kikombe kilichoshikwa mkononi mwake. Jina la mvinyo huu ni yayin foams (SHD 2564). Shemarim ulioko hapa unajulikana kama dregs lakini mwonekano uliopo ni kwamba umeachwa na baraka kamili zikiwa zimeachwa kwa Israeli ambao wameachiwa mataifa. Hakuna uwezekano za kuwa kwamba maneno yao yanaweza kuhusishwa na mvinyo usiochachuka. Mchakato ni kwamba  ni mapishi endelevu. Wokovu ni kwa Wamataifa na kwamba mtazamo wake chanya ulioonekana hapa ni usio wa kimungu ambao utafanywa kwa kushiriki kikombe kitakatifu cha Bwana. Hii imefundishwa mara nyingi ikitajwa kama ni kikombe cha hasira za Mungu. Hata hivyo, mapenzi ya Mungu ni kwamba hapendi yeyote mwenye mwili apotee apotee.

 

Shemarim ni matokeo ya mwisho kwenye mchakato wa mapishi ya mvinyo. Hii ni Baraka iliyohifadhiwa kwa ajili ya sikukuu na Mungu. Kwa hiyo, shemarim ndiyo matokeo ya mwisho ya mchakato na unafananishwa pia kwa Wamataifa ikiwa ni kama mvinyo wa mwisho wa Mungu.

Isaya 25:6 Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.

 

Wazo la kuihifadhi kwenye mabalasi linakubalika na mtazamo wa kibinadamu aliyeko kwenye viriba. Kwa hiyo neno hili linatokana na hali hii ya kusinyaa bila kutibulika kwa viriba. Na hii ndiyo pekee inamaanisha viriba vikukuu. Wanadamu wapo kwenye hali hii, na wanakemewa kwa kukaa kwao nyuma ya viriba.

Sefania 1:12 Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya

 

Hali hii itakuwa katika siku za mwisho wakati watu watakapokuwa kwenye maisha ya ukengeufu na maasi makuu pasipo kuwa na hofu ya Mungu. hawatajisumbua kujitakasa ili wapate kukubalika na Mungu. Na hii ndiyo hali halisi kwa siku hizi. Hii ndiyo ilikuwa hali ya Wamoabu na Mungu aliwapatiliza. 

Yeremia 48:11 Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.

 

Suala hapa ni kwa huu mvinyo kuwa kwenye viriba vikukuu ambao ulikuwa kwamba haujachachushwa wala kuchanganywa au kutakaswa na Moabu walikuwa hawajaenda bado utumwani na walitengwa na Mungu na Mungu alikuwa anakwenda kuwapatiliza hawa Moabu kwa kutumia njia yake mwenyewe.

 

Mlinganisho hapa hata hivyo unaonyesha kuwa mvinyo uliotulia pasipo kutikiswa wala kuchanganywa, ulipata nguvu au kuimarishwa kutokana na ladha ya mtio wa makapi ya zabibu, na pia kutokana na vitu vingine kutoka nje na wadudu (Mathayo 23:24). Hii ndiyo hadithi ya kutoa mnanaa kunakosemwa na Kristo. Mvinyo wa kale ulihitaji mvinyo mpya (Mhubiri 9:10; Luka 5:39). Haya ni matokeo ya kuhitajika kwa mvinyo uliochachika.

 

Mvinyo umetumika kwa dawa kama tulivyojionea kwenye 2Samweli 16:2 na 1Timotheo 5:23 na ulitumika pia kwa kusafishia majeraha kwa walioumia (Luka 10:34).

 

Waumini waliomfanyia Mungu ibada walileta kiriba cha ngozi chenye mvinyo walipokuja kutembelea kuhiji Hekaluni (1Samweli 1:24; 10:3). Ulimwagwa chini kwenye kingo za madhabahu (Mhubiri 50:15; sawa na alivyoandika Josephus A of J, III, ix, 4), na ulikuwa na maana sawa na mwonekano sawa na wa damu – kwa hiyo mafundisho ya Kristo akiwa kama Kuhani Mkuu wakati alipotoa dhabihu kwa damu yake mwenyewe ili kulitakasa Hekallu. Hii ilifanyika kwa kutolea mfano mvinyo. Hata hivyo, haikuweza kujitoa sadaka yenyewe – kwa hiyo, mwili na damu ya Kristo vinaiashiria dhabihu (Kutoka 29:40; Mambo ya Walawi 23:13; Hesabu 15:7,10; 28:14; nk. Sawa na kamusi ya Interp. Dict., ibid.). Mvinyo umetajwa pia kwenye maadhimisho ya Pasaka kwenye kitabu cha Yubile 49:6 na, kwa sababu hii imeandaliwa na Ross (Interp. Dict., ibid.) ambayo ilikuwa hakijatumika bado kwenye maadhimisho ya Pasaka hadi kipindi cha Wahellenisti. Hata hivyo, makatazo dhidi ya unywaji wa bia na sio mvinyo kwenye maandiko gombo za Elephantine (tazama Pritchard, op. cit.) yanasema kwamba Ross amekosea.

 

Maagano yote mawili, yaani Agano la Kale na Jipya yana namna inayousifia mvinyo na kutoa maonyo juu yake. Nabii Habakuki anaonya kwa kuuelezea mvinyo kuwa ni kitu kidanganyifu (Habakuki 2:5; sawa na Hosea 4:11). Mika analalamika akisema kwamba watu wake wanataka wahubiri watakao ongelea mvinyo na unywaji wa vileo vikali (Mika 2:11). Nabii Isaya anawakemea wachungaji wanaopendezwa na unywaji wa mvinyo na wenyewe kunywa pombe kalikali (Isaya 56:11-12; sawa na Hosea 7:5) na makuhani manabii walioaminika na wenye maarifa makubwa kwa ajili ya unywaji wa mvinyo (Isaya 28:7). Makatazo yaliyoko kwa makuhani kunywa mvinyo wakiwa kwenye zamu zao hudumani yamo kwenye Mambo ya Walawi 10:9 na Ezekieli 44:21.

 

Uaminifu na kiasi ni ufunguo muhimu kwenye mtazamo na lengo la Biblia. Mithali inayachukua maonyo yaliyopo dhidi ya unywaji unaopitiliza na sio na kiasi walla hadhari (Mithali 20:1; 21:17; sawa na 23:20-21; 23:31-35).

 

Mtazamo juu ya kuachana kabisa kutokunywa mvinyo unakutikana kwa Warekabi. Hata hivyo, waliapa sio kutokunywa tu huu mvinyo, bali pia walikataa kujenga majumba (Yeremia 35:6-7). Kiapo hiki kilichukuliwa kutokana na hisia ya uchungu wa mababu zao lakini kwanamna yoyote nyingine ile walianzisha tabia kama kawaida au Mungu aliwafunulia au kuwataka wafanye hivyo.

 

Zaburi inamsifu Yahova kwa kutoa mvinyo ili kuuburudisha moyo wa mwanadamu (Zaburi 104:15; sawa na Waamuzi 9:13; Mhubiri 10:19).

 

’Ashishah

Neno hili linatokana na neno ’ashah linalomaanisha kuweka kwa kukandamiza. Neno hili ndiyo chanzo cha mchanganyo kwenye maandiko ya biblia na limepata mashiko yake na baraza lenye kiasi ili kuonyesha kwamba mchakato unaoongelewa au kuhusishwa unafanya dozi nzito kuliko mvinyo. Imetafsiriwa kama flagons ya mvinyo kwenye biblia ya KJV. Ni kimiminika kilichogandishwa kilichotengenezwa kwa zabibu zaweza kuwa ni za kutoka kwenye makapi, au kutoka kwenye keki tamu ya zabibu zilizokaushwa au za makapi yaliliyokamuliwa (Companion Bible inasema hivyo). Daudi aliwapa watu keki ya masalia haya na sio ya mvinyo uliokorogwa. Neno hili ni tofauti kabisa na halina uhusiano na maneno mengine yoyote yaliyotumiwa kuutaja mvinyo na yanayouelezea kiusahihi mchakato wa utengenezaji wa  mvinyo kama kileo cha zama kale. Mchakato huu wa kuitengeneza keki hii ngumu ya makamuo unafahamika na una neno lake mahsusi kwa lugha ya Kiebrania.

2Samweli 6:19 Akawagawia watu wote, mkutano wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. Basi watu wote wakaenda zao, kila mtu nyumbani kwake.

 

Hii imerediwa kwenye 1Nyakati. Kwa hiyo, bilahaka tunaongelea juu ya chanzo tofauti na mchakato.

1 Nyakati 16:3 Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.

 

Wimbo Ulio Bora unalitumia neno hilohilo ikimaanisha ni keki ziliyotengenezwa kwa ubora wake. Uhusiano uliopo hapa ni kama keki iliyochanganyika au ya zabibu na maepo.

 

Wimbo Ulio Bora 2:5 Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera, Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.

Hosea 3:1 Bwana akaniambia, Enenda tena, mpende mwanamke apendwaye na rafiki yake, naye ni mzinzi; kama vile Bwana awapendavyo wana wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikate ya zabibu kavu.

 

Kinachoonekana hapa ni upenzi wa keki tamu za zabibu. Hakuna mwonekano ama ushahidi unaoonyesha kwamba mvinyo umehusishwa hapa kwa kutumika kwa mtazamo tofauti. Kwa kweli ni kwamba mtazamo asi kuhusu keki za zabibu unaoonekana hapa una mtazamo wa namna mbili unatajwa kwa mambo mengine yaliyotengenezwa kwa mvinyo. Nukuu za Bacchiocchi kuhusu tofauti za mrengo wa chanya au asi haziwezi kubakia kwenye hali ya kudhania tu au kuchunguza.

 

Utengenezaji wa hii kwa kutumia kimiminika heenda ungejumuiaha mchakato kama huu. Ushauri wa mtaalamu mashuhuri aitwaye Mr Peter Leske kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Mvinyo katika Chuo huko Australia anasema kwamba juisi ya zabibu inaanza kuchachuka na kulevya kuanzia masaa kumi na mawili baada ya kukamuliwa kwake (kutegemea na kiasi cha joto kilichopo). Mchakato huu unaweza kuongezwa nguvu zake kwa kuchemshwa. Utengenezaji huu unalazimu kuondoa kiasi kikubwa cha maji ili kuondoa nguvu za mchachuko kwa kuua nguvu za hamira inayoifanya ichachuke. Hii inakuwa lazima irudiwe kwa mashatri yaliyokuwepo kwenye mapishi ya siku za kale. Matokeo yake ni kuwa na kimiminika kugumu na kilichounguzwa. Kwa hakika, hii inakuwa ni jam inayofanya mchakato na mapishi yake yanakuwa hayajawa kwenye kiwango kizuri cha mvinyo. Katika siku za lake, mchakato huu ulihusianisha kiwango kamili cha kilichokubalika na kulingana cha utengenezaji wa jam. Kwa teknolojia ya leo inayotumia mashine, chakato huu unakuwa na nguvu sana na unakuwa na mapungufu madogo ya upunguzaji ambao ni muhimu. Hata hivyo, mmiminiko mdogo na utamu wa sukari unatengeneza gramu 700 kwa lita moja – wakati kwamba gramu kati ya 150-200 kwa lita moja. Tekinolojia ya Biblia inaonyesha kwamba kile kilichotengenezwa hakikuchukuliwa tu kuwa ni mvinyo. Aina hii ya mvinyo unaoitwa ’ashishah ambao unaweza kukamuliwa ili kuitengeneza keki tamu iliyo kama jam ngumu inatengenezwa kwa namna au ya makapi au kwa majimaji ya jam. Hii ndiyo sababu iliyomfanya Daudi apewe mgao wa mkate. Kwa Kiebrania aina hii pia haina kwenye kundi la ubora la mvinyo.

 

Vintages ya Kale

Ilitumika kwenye mapokeo ya Wamisri ambao walihitaji uletwe mvinyo kutoka kwenye wilaya zote ambako walikuwa wameuivisha kwa wingi kuliko walivyofanya Wafaransa. Ingawa Biblia haujumuishi jina la mvinyo huu kwenye simulizi zake inaipotaja aina ya mivinyo ya Palestina, bali maeneo yanayoizunguka Hebron ilijulikana sana katika maeneo haya ya Yuda. Maeneo kadhaa wa kadha majina yaliyotumika kuuita yalikuwa viticulture (tazama kitabu cha Abel-Kera-Mim Anab; Beth-Haccherem; Eschol). Zabibu za Sibmah pia zimetajwa na nabii Isaya, yamefika hata Yazeri, yalitanga-tanga hata nyikani; (Isaya 16:8). Mvinyo wa Syria ulijulikana na kuwa maarufu sana ulimwenguni kote, kama ulivyokuwa mvinyo wa Helbon na mvinyo wa Uzali (Ezekieli. 27:18-19).

 

Zabibu zilikuwa zinavunwa mwezi nwa Augost na Septemba ni zilikuwa zinatawanywa kwa kuanikwa juani kwa kitambo kabla hazijafanywa kuwa mvinyo. Msimu wa zabibu ulikuwa unatokea mwezi wa Septemba, ikitajwa juhusianishwa na Sikukuu ya Vibanda (Kumbukumbu la Torati 16:3) (tazama kwenye Interp. Dict., art. ‘Wine’, p. 850).

 

Zaburi 8, 81 na 84 zinataja mambo ambayo kwa mujibu wa Gittith – kuwa ni sawa na mzizi au kiini kilichotumika kutengeneza vat ya mvinyo – na kwenye kamusi ya Interpreters Dictionary of the Bible inadhani kwamba yawezekana kuwa ni matokeo ya Zaburi. Zabibu zilichumwa (kwa mujibu wa Heb. walk sawa na Nehemia 13:15; Ayubu 24:11; Isaya 16:10) na kweye vikundi. Kwa hiyo, nabii Isaya 63:3 anaitaja kuwa ni uvunaji na ukamuaji mvinyo peke yake. Ukamuaji wa mvinyo ilifanywa kwa namna mbili – kwa upande wa juu na wa chini uliounganishwa na mtambo. Upande wa juu ulikuwa mpana mara mbili na mrefu kuliko ulwe wa chini. Zabibu zilishindiliwa kwa upande wa juu ukijumuishwa na ule wa chini. Katika kipindi zama cha Warumi, shinikizo tatu au nne ziliunganishwa kwenye mkandamizo huu wa kukamua. Mavuno ya zaituni yaliyofuatia baadae, huenda ziliwekwa na kukamuliwa kwenye shinikizo moja (Interp. Dict., ibid.). hatua ya kwanza na uchachushaji ulianza kwa kipindi cha masaa kati ya sita au kumi na mawili baada ya kuanza kwa ukamuaji kwenye shinikizo la chini. Kisha mvinyo ulimiminiwa kwenye magudulia (Yeremia 13:12; 48:11) au kwenye viriba ili uchachuke zaidi na kuhifadhiwa. Na ndiyo maana ya usemi wa |Kristo wa kusema kwamba msiweke mvinyo mpya kwenye viriba vikukuu (Mathayo 9:17; Marko 2:22; Luka 5:37-39). Tatizo ni kwamba mvinyo uliochachuka hujitanua na kushinikiza. Ngozi ya kiriba inapopata unyevunyevu unajitanua kwa majimaji yanayojishinikiza. Ngozi ya mvinyo wa kale unakuwa umekwisha kupitia mchakato huu wa kujitanua na unakuwa hauna tena upenyo wowote uliobakia wa wa kusababisha kufanya mkandamizo wa majimaji haya yanayojieneza. Kwa hiyo, mvinyo mpya utasababishia mshinikizo na kukitanua hadi kukipasua kiriba kile chenye ngozi mpya. Ni lazima kingeweza kuwa na ujazo wa kuishinikiza ngozi mpya. Isingewezekana kabisa kwa Kristo kmdhania kwamba alikuwa anamaanisha hapa juisi ya zabibu. Ila ni dhahiri kabisa kwamba alikuwa anasemea juu ya mvinyo wa kale uliochachuka na wenye nguvu ya kupasua kiriba. Na ndivyo ilivyo pia kwenye Ayubu 32:18-19.

Ayubu 32:18-19  Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza. 19 Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya li karibu na kupasuka.

 

Kwa hiyo, mlinganisho ulioko na Roho Mtakatifu umechukuliwa. Mchakato wa kuchachuka ndio unaotokea kwa wateule. Sisis tu tunda la mzabibu ambaye ndiye Mungu kwa kupitia Roho Mtakatifu. Kristo ndiye mwili na ndiye mzabibu wa kweli. Shamba la mzabibu la Bwana wa Majeshi ni Nyumba ya Israeli na watu wa Yuda ndio wakulima wa shamba hilo (Isaya 5:7).

 

Mvinyo ulikuwa unatolewa kwa moyo wa ukarimu sana kwenye sherehe za arusi na neno la Kiebrania kuhusu sherehe kama hii au tamasha ni manywaji au unywaji (SHD 4960 mishteh, tazama pia kwenye Interp. Dict., p. 851). Kwa hiyo, mvinyo kwa ujumla ulijumuishwa kwenye utoaji wa zawadi kwa wenye mamlaka, kama walivyofanya kina Abigaili na Ziba kwa Daudi (1Samweli 25:18; 2Samweli 16:1).

 

Kwa makubaliano ya kibiashara, Sulemani alimpa Hiramu mabalasi 20,000 ya mvinyo miongoni mwa vitu vingine pale alipoleta miti iliyotakiwa kujengea Hekalu la Bwana (2Nyakati 2:8-10,15). Ni jambo lisilofikirika wala kuwa namashiko kabisa kuamini kwamba Hiram alijisikia kutosheka na kuinywa tu juisi ya zabibu. Kwa siku chache ingeweza kubadilika na kuwa mvinyo tu kwa namna yoyote ile.

 

Tafsiri ya the Companion Bible ina idadi kubwa sana cha maneno ya nyomngeza au Appendix 27 ya maneno haya:

Kwa data hizi itaonekana kwamba uelezeaji wa siku hizi wa “mvinyo usiochacha” ni mgongano tu wa maneno. Kama ulikuwa ni mvinyo na kuitwa hivyo, basi ni lazima ulikuwa umechachuka. Na kama haukuwa umechachuka na kuwa wakulevya, basi haujakuwa mvinyo, bali ni aina nyingine tu ya kinywaji baridi.

 

Hamira ni donge linalo chachusha, na sio mvinyo. Ni hii hamira ndiyo inayosababisha mchachuko. Inawezekana kusiwe na chachu baada ya mchakato wa mchachusho unapikwisha au kukoma.

 

Mjadala huu pia ni wa muhimu kama unavyoendelezwa na wale wasio na habari kujua kuwa mvinyo ni zao la chachu na kwa hiyo, mvinyo uliochacha na kulevya hauwezi kutumiwa kwenye maadhimisho ya Pasaka kwa ajili ya makato waliyonayo dhidi ya kutumia kitu chenye hamira au kulevya. Makato yaliyoko ni dhidi ya kileo. Makatazo yaliyoko ni kuhusu kutumia mkate wenye chachu na kuondoa kila aina ya chachu na hamira majumbani mwetu wakati wa maadhimisho ya idi hii. Mvinyo sio mkate na mara tu mchakato wa kuchachuka unapofikia mwisho unakuwa ni bidhaa iliyokamilika. Biblia imesema wazi sana kwamba mvinnyo unaruhusiwa kutumika wakati wa maadhimisho ya sikukuu hizi tatu zilizoamriwa kuadhimishwa mara tatu kila mwaka, na inasema wazi kabisa kwamba vinywaji baridi visivyo na kileo havimo miongoni mwa vitu vya kutumiwa kwenye shughuli rasmi za maadhimisho ya Sikukuu au idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kinywaji cha bia kimeharamishwa pia kutumiwa kwenye kipindi hiki cha Idi ya Mikate Isiyotiwa na mamlaka ya kikuhani inachukulia marufuku hii kwenye mikazio ya mapokeo yao. Mtazamo huu umeathiri pia tafsiri njema iliyokusudiwa ya nakala kadhaa za kale kutoka kwenye uandishi upya wa maandiko kutoka kwenye nakala asilia za magombo ganjo ya kale wakati wa kuhamishia kwenye nakala za uandihsi za zama za kati maarufu kama Elephantine kuhusu maadhimisho ya Pasaka. Wameingiza mayai kwenye mtengani9sho kuwa ni kama makatazo ya unywaji wa bia kutoka kwenye mtazamo huu kama ilivyonukuliwa na Ginsberg kwenye maandiko ya chini na fafanuzi kwenye tafsiri na andiko Near East: An Anthology of Texts and Pictures, Princeton, 1958, p. 278). Kwenye maandiko haya ya chini ya ufafanuzi 5, H. L. Ginsberg anaandika kwamba:

… marejesho ndiyo pekee yaliyo sahihi iwapo kama mapokeo ya Hananiah kama sheria za huduma ya Marabi zingejumuishwa kwenye “chachu” iliyokolea kileo lakini sio matunda yaliyochacha (mvinyo). Wasamaria wanachukulia mtazamo mkali. 

 

Sheria hii ya marabi iliruhusu mvinyo lakini sio unywaji wa bia. Hakuna ushahidi popote pale katika historia unaoonyesha kuwa mvinyo uliochachauka ulitumika kama kitu muhimu na lazima kutumiwa kwenye maadhimisho ya Pasaka. Louis Ginsberg (1873-1941) aliruhusu kutokana na taarifa rejea za wote wawili, yaani Wababelonia na kundi la Talmud wa Yerusalemu, kwamba mivinyo isiyochacha au kulevya huenda ndiyo ilitumiwa na kuchaguliwa (lekatehillah) katika uwekaji wakfu na kuzitakasa sikukuu au sherehe kwa maana ya kuitwa kwake kikombe cha mvinyo (Kiddush) na maadhimisho au sherehe nyingine za kidini ziliyofanyika nje ya Hekalu (kwa mujibu wa mwandishi Louis Ginsberg “A Response to the Question Whether Unfermented Wine May Be Used in Jewish Ceremonies”, American Jewish Year Book 1923, p. 414 cf. Bacchiocchi, ibid., p. 50).

 

Dhana hii ni dhana fikirika tu. Haimo kwenye taratibu zenyewe asilia za Maadhimisho ya Wayahudi wa Kiddush, na Ushirika wa Meza ya Bwana haimo kwenye maadhimisho yaliyofanywa kwenye imani na taratibu za Wayahudi. Sio ule mlo unaoadhimishwa siku ya 15 Nisan. Bali ni mlo wa siku ya 14 Nisan, au Mlo wa Maandalio. Kristo alikufa kwa siku ya kuila Pasaka kwa kuwa alikuwa ndiye Pasaka.

 

Bacchiocchi anadai kwenye ukurasa wake wa 12 wa ufupisho wake.

Hila za kuachana kwa taratibu msimamo wa biblia unatokana na mafundisho yanayodai kuachana kabisa na matumizi ya kileo, imani na mafundisho yanayozidi kushamiri na kuongezeka kwa idadi ya makanisa yanayoamini hivyo kumesaidia sana kueneza dhana hii ya kukataza watu kutumia kileo, jambo lililopelekea matatizo makubwa siku hizi.

 

Madai na dhana hii haina mashiko wala ushahidi wowote wa kimaandiko wala kihistoria wala hata kwa namna nyingine yoyote mbali na kwenye mafundisho ya kizushi ya Montanist na Manichean pamoja na wazee wao walioanzisha na kuendeleza mafundisho haya hapo kale. Fundisho la kuwa wana kiasi limegeuzwa na kutumiwa kungeusha watu kwenye historia ya dini au imani ya waasetiki pamoja na wazee wao wa kale ambao walikuwa wanaitwa Wapuritani. Imani hii ilipata kukubalika sana huko Marekani na imesababisha kuendelea kuaminika hivyo kwenye zama hii ya makatazo ya unywaji wa vileo. Mwonekano na tabia ya uleyi ni tabia ya mtu binasfi yake na—sio makosa ya imani au dini. Matumizi mema ya unywaji pombe kwa furaha au kwa kujiburudisha tu hakuwezi kumsababisha mtu kumtendan Mungu dhambi au kukosea Kristo.

 

Hitimisho

Katika kila mfano uliotolewa tumejionea mifano ambayo kwayo neno mvinyo limetumika kwenye mambo yote mawili, yaani upande asi na chanya. Lugha ya Kiebrania ni tajiri kwa upembuzi wa maneno yanayochambua kinywaji hiki cha mvinyo. Kila neno limeonyesha sehemu ya mchakato husika kwenye utexamples we have seen, the instance where the ngenezaji wa mvinyo. Kiingereza kinatumia maneno mengine yenye maana yake halisia na lengwa katika kumaanisha maana moja hiyohiyo. Mchakato ni mtambuka na ni sehemu muhimu kwa maisha ya kila siku ya watu wote wawili. Kuamini na kufudhisha watu kuwa mvinyo ulikuwa sio kitu chenye kileo ndani yake bali ulikuwa ni juisi tu ya zabibu wkati unapotajwa kwenye matumizi matakatifu kwenye biblia ni sawa na kuwatukana watu wenye akili kwa kuwaona wajinga, jambo ambalo si jema kuwafanyia wanazuoni wenye akli wa Biblia na Maandiko Matakatifu. Mamlaka ya Kirabi waliiona hii kuwa sawa na ujinga. Mtazamo kama huu, unaotokana na imani ya Wanostiki ambao wanaitendea kazi mafundisho na imani ya waasetiki waliopitiliza hadi kufikia kuharamisha ulaji wa nyama na wao kula mbogamboga peke yake, wakitafuta kupingana na jinsi Maandiko Matakatifu yanavyosema na kutufundisha, na hawa waasetiki wanaojihesabia haki wenyewe wameonekana kama ni watu waliotengwa na imani ya Kikristo wanapolinganishwa na wa Puritani au wa Cathari na wamechukua mafundisho ya Uungu ya Watrinitariani na kuyakumbatia kwa lengo la kufanya wakubalike zaidi kuliko wa Montana na wa Manicheani waliowatangulia. Lakini kwa namna yoyote ile ijulikane tu kuwa haya ni mafundisho ya kizushi na ambayo yemekwisha kukataliwa na aina nyingine yote ya Wakristo kwa sababu ya mwonekano wake wa upotoshaji wa dhahiri wa Maandiko Matakatifu.

q