Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[192]
Siku ya Bwana
Na
Siku za Mwisho
(Toleo
La 2.0 19970208-20070824)
Maneno haya
yanayosema kwamba Siku ya Bwana na Siku za Mwisho au Nyakati za Mwishoni mara nyingi yanachanganya na yanatafsiriwa
kimakosa kwa ujumla. Kwenye Maandishi na Majarida mbalimbali ya Kikristo. Hapa
tunafafanua maneno haya kwa mtazamo na maana ya kibiblia na kuona jinsi
maandiko kadhaa zinazoelezea kuhusu dhana hii ya Siku ya Bwana tutaona kuwa
haina maana ya Siku ya Bwana inayopigiwa upatu na kutafsiriwa kuwa ni siku ya
Jumapili inayotumiwa kwa ibada za Wakristo wa mrengo huu wa Jumapili. Badala
yake tutaiona kuwa ni kipindi cha fadhaa na kamsa ambacho kitafuatia Kurudi kwa
Masihi na kuweka kipindi maalumu cha uingiliaji wa kimbinguni kwenye mambo ya
mwanadamu. Pia tutajionea maana ya neno Siku
za Mwisho au Nyakati za Mwisho Siku
Iliyo Kuu ya Mwisho zinazojiri na kipindi chote cha Zama ya Masihi ambacho
kimeelezewa vema sana kwenye unabii hadi kwenye kusudi lake kuu na mwisho wake.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1997, 2007 Wade Cox)
(Tr. 2013)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Siku ya Bwana na Siku za Mwisho
Mojawapo ya maneno yanayokosewa kueleweka maana yake kwenye Biblia ni usemi wa Siku ya Bwana, likifuatiwa kwa karibu na maneno mengine ya Siku za Meisho au Nyakati za Mwisho.
Dini kongwe za Kikristo yanajaribu kuichanganya Siku ya Bwana na Siku ya kumfanyia ibada Bwana na wanalitumia neno hili katika kuipa mashiko siku ya Jumapili kuwa ni ya kumfanyia ibada. Baadhi ya watunza Sabato wanalielewa neno hili kimakosa na wanalifanya utendaji kazi wake kuwa ni wa siku moja fulani tu na maalumu.
Siku za Mwisho
Maneno haya, Siku za Mwisho au Nyakati za Mwisho maranyingi yamechukuliwa kuwa yanahusiana na kipindi cha wakati fulani mahala fulani kilichokuwa mwishoni mwa karne ya ishirini au hata siku za mbele yake. Hata hivyo, hii sio maana iliyokusudiwa na Biblia kuhusu maneno haya.
Kusudi la kuandika jarida hili ni kuelezea na kufafanua maana ya maneno haya na kisha kuelezea vipindi husika vinavyojiri maneno haya.
Kuna awamu tatu za uumbaji wa viumbe. Awamu ya kwanza ilikuwa ni ya Adamu hadi Nuhu ambacho kiliishia kwenye kipindi cha Ibrahimu. Awamu ya pili kilikuwa ni cha Ibrahimu na Israeli ambacho kimeishia kwa Masihi. Awamu ya mwisho ni ya zama ya Masihi. Awamu hii inadumu kwa kipindi kilichokusudiwa kuwa ni cha miaka elfu mbili. Awamu hizi tatu zinadumu kwa jumla ya Yubile arobaini kwa wastani—na kufanya vipindi vitatu vyenye jumla ya miaka elfu mbili kila kimoja. Vipindi hivi vitatu
vilifanywa kwa mifano katika siku za nabii Musa kikiwa ni kipindi cha miaka arobaini mara tatu katika maisha yake. (tazama majarida ya Musa na Miungu ya Misri (Na. 105) na Pentekoste ya Sinai (Na. 115) [Moses and the Gods of Egypt (No. 105) and Pentecost at Sinai (No. 115)]. Musa alikuwa ni mfano wa Masihi, na maisha yake yaliwakilisha majukumu ya Masihi katika uumbaji.
Unabii wa Biblia unatuambia kwamba Siku za Mwisho au Nyakati za Mwisho zilianza kutoka kwenye huduma ya Masihi, na zilianzisha kipindi au zama za Masihi ambacho ndicho kilichoshuhudia adhimisho la kwanza la Pentekoste ya zama zake tuionayo kwenye Matendo 2:14-36.
Matendo 2:14-36 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake,
akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni
jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa,
kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa
kinywa cha nabii Yoeli, 17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia
watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu
wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi
wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri. 19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na
ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi. 20 Jua litageuka
kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na
iliyo dhahiri. 21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana
ataokolewa. 22 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya:
Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na
ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe
mnavyojua; 23 mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu
lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono
ya watu wabaya, mkamwua; 24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu
wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. 25 Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona
Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume,
nisitikisike. 26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu
ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.27 Kwa maana
hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone
uharibifu. 28 Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa
uso wako. 29 Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa
ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa,
na kaburi lake liko kwetu hata leo. 30 Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa
Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha
mmoja katika kiti chake cha enzi; 31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya,
alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu,
wala mwili wake haukuona uharibifu. 32 Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu
mashahidi wake. 33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume
wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki
mnachokiona sasa na kukisikia. 34 Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye
mwenyewe anasema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti upande wa mkono wangu wa
kuume. 35 Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.
36 Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya
kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.
Kwenye andiko
hili, Mtume Petro alinukuu nabii Yoeli na pia alijuza kwamba mchakato ulikuwe
kwamba, kabla ya kuja Siku ya Bwana, Mungu
angefanya kitu kilichotabiriwa kupitio nabii Yoeli. Mungu alimfanya Yehoshua
kuwa Bwana na Masihi, au Kristo, kwa kumfufua kutoka kwa wafu na kupaa kwake
mbinguni.
Siku hii ya Bwana inatkuwa ni ya kamsa na maafa na sio siku ya
kuabudu. Ni mwisho na kikomo cha zama ya Masihi. Maandiko haya yamenukuliwa
kutoka kwenye 2:28-31.
Yoeli 2:28-31 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba
nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake,
watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; 29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake,
katika siku zile, nitamimina roho yangu. 30 Nami
nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara
ya moshi. 31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa
damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.
Andiko lililo
kwenye Matendo ya Mitume linaendelea kwa kuinukuu Zaburi 16:8-11.
Zaburi 16:8-11
Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa. 9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nao utukufu wangu
unashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini. 10 Maana
hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu. 11 Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha
tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
Kwa hiyo, zama za
Masihi ilichukuliwa kuwa ni kipindi kilichojulikana kama Siku za Mwisho na ambacho kilianzia kwenye tukio la Pentekoste,
kama ilivyoelezwa na Mtume Petro.
Siku hizi za
Mwisho zilitajwa kwanza kwenye Mwanzo 49:1. Ahadi hii ya Yakobo ilikuwa
itimilike kwa Israeli katika Siku za
Mwisho sawasawa na makabila yao. Kwa hiyo ahadi ya uzaliwa wa kwanza iliyo
kwenye Mwanzo 49 ambayo ni zama za Masihi.
Mwanzo 49:1-2 Yakobo akawaita wanawe, akasema,
Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. 2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo,
Msikilizeni Israeli, baba yenu.
Tafsiri ya Biblia ya Revised Standard Version (RSV) inaiweka siku hii kama siku zijazo, bali maana yake ni Siku za Mwisho, kama ilivyotafsriwa
hapa.
Nukuu-andishi
kwenye Matendo 2:17 ilivyofanywa kwenye tafsiri ya New Oxford Annotated RSV
inasema kwamba kipawa cha Roho Mtakatifu kwa wote wenye mwili, na sio ni kwa
wateule mmoja mmoja, ni ishara ya zama za Masihi. Maana halisi ni kwamba
Wamataifa walikubaliwa kuwa makuhani wa wateule pasi kujali nasaba zao.
Kitabu cha
Waebrania kiliandikwa katika Siku za
Mwisho.
Waebrania 1:1-2
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na
kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana,
aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Kwa hiyo ni jambo
lisilo na shaka kuamini kwamba Biblia inataja kwamba Siku za Mwisho zilianzia tangia kuzaliwa na kufufuka kwake Masihi.
Mtume Petro alijua Siku hizi za Mwisho
kuwa zilianzia tangu kipindi hiki sawa na tunavyojjonea kwenye 1Petro 1:20,
akiita kama utimilifu wa nyakati na
mchakato wake ni mwendelezo uliofichika (1Petro 1:5).
Mtume Yohana
alisema kwamba ilikuwa ni nyakati za
mwisho au siku ya mwisho.
1Yohana 2:18 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile
mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi
wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.
Neno hili
limeandikwa kama eschate õra (tazama
kamusi ya Marshall’s Greek-English
Interlinear). Hakuna makala kwenye kifungu hiki; kwa hiyo, makala nyingine
zinapaswa zitathiniwe na kuonyesha kuwa “saa
la mwisho”. Kwa hiyo Siku za Mwisho
zilionekana kama ni mgawanyo wa nyakati. Matukio na kazi za Mpinga au
Wapingakristo zitafanyika ndani ya kipindi cha migawanyo hii.
Nyakati zenyewe
zinaonekana kuwa zitakuwa za hatari na za kutisha sana.
2Timotheo 3:1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za
mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
Mtume Yakobo,
aliyekuwa ndugu yake Kristo, anaonysha kwamba hii itakuwa ni mabadiliko kamili
kuipata dunia iliyopo leo na mfumo wake na taratibu zake za kiuchumi katika Siku hizi za Mwisho, na ambayo inaelekea
hadi kupelekea kwenye kipindi cha kurudi kwake Masihi na anguko la mfumo ulioko
leo (Yakobo 5:3-11).
Yakobo 5:3-11 Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo
itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. 4 Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna
mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao
waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. 5 Mmefanya anasa katika dunia, na
kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. 6 Mmehukumu
mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi. 7 Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake
Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa
ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. 8 Nanyi
vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. 9 Ndugu, msinung'unikiane, msije
mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. 10 Ndugu,
watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya,
na wa uvumilivu. 11 Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia
habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi
wa rehema, mwenye huruma.
Kupinduliwa na
anguko la utawala na mifumo iliyoko duniani leo kutafanya na mfumo mwingine
ulio tofauti na mfumo wa kiuchumi uliozoeleka wa kimashirika ya leo na
utakaomilikiwa na kutawaliwa na Mungu mwingine—atakayetoa Sheria, na ndiye yeye
huyu aliyempa nabii Musa kwa mkono wa Kristo alipokuwa kama malaika hajazaliwa
katika mwili.
Yuda 18 inarudia
maneno ya kwenye 2Petro 3:3, akilionya Kanisa.
Usemi Siku ya Mwisho ndio neno la mwisho
linalohitimisha kipindi hiki kinachoitwa cha Siku za Mwisho au Nyakati za
Mwisho. Kutokana na mtume Yohana. Kristo anaonyesha kuwa hiki ni kipindi
nyakati kinachojiri kwenye tukio la ufufuko wa wafu.
Yohana 6:39-44 Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya
kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya
mwisho. 40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana
na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 41 Basi Wayahudi wakamnung'unikia, kwa sababu
alisema, Mimi ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni. 42 Wakasema, Je! Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu,
ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?43 Basi Yesu akajibu, akawaambia,
Msinung'unike ninyi kwa ninyi. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa
na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Kwa hiyo, Siku ya Mwisho inayotajwa hapa ni ile ya
Ufufuko wa Wafu ambacho ni cha Ufufuo wa watakatifu. Hata hivyo, kipindi hiki
chote sio ni cha mchakato cha Ujio wake na kuwa hakina uhusiano wowote na
Ufufuo wa Kwanza wa wafu.
Ufufuko wa wote
wenye mwili pia unaitwa ufufuo wa Siku ya
Mwisho.
Yohana 11:24-27
Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi,
ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa
kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? 27 Akamwambia,
Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule
ajaye ulimwenguni.
Hapa Kristo
alikuwa anasema kwamba Lazaro alikuwa anapewa ufufuo katika Kristo mbali na ule
ulikuwa unatarajiwa na Yuda. Watu waliomkataa Kristo bado watahukumiwa ifikapo Siku ya Mwisho.
Yohana 12:48 Yeye
anikataaye mimi, siyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo
nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
Kwa hiyo, Siku ya Mwisho inajiri kipindi cote cha
ufufuo, ambacho ni cha miaka efu (Ufunuo 20:4-14) kujumlisha miaka mia moja
mingine (Isaya 65:20).
Ufunuo 20:4-14 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu
yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya
ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule
mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso
zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka
elfu. 5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile
miaka elfu. 6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni
yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina
nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye
hiyo miaka elfu. 7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani
atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio
katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu
yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi,
wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka
mbinguni, ukawala. 10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa
katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao
watateswa mchana na usiku hata milele na milele. 11 Kisha nikaona
kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu
zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu,
wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu
vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao
wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa
na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na
Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu
kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa
la moto. Hii ndiyo mauti ya
pili, yaani, hilo ziwa la moto.
Kwa hiyo miaka
mingine mia ya Ufufuo wa Pili inatokea.
Isaya 65:20
Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana
mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka
mia atalaaniwa.
Kipindi hiki cha
miaka hii mia moja ni sehemu ya mchakato wa hukumu ya mwisho. Siku ya Mkutano
wa makini ni sikukuu yenye umuhimu mkubwa sana. Hiki ni kipindi tofauti na kile
cha Milenia, bali ni sehemu bado ya Siku
ya Bwana.
Usemi usemao Siku za Misho au Nyakati za Mwisho unaelelezea pia mcakato mzima wa utawala wa
millennia wa Masihi.
Mika 4:1-2 Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya
kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa
juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. 2 Na mataifa mengi watakwenda na kusema,
Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye
atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika
Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.
Kipindi hiki
kinaonekana wazi sana kuwa kitakuwa kwenye ufufuko wa wote wenye mwili. Neno
linalotumika hapa ni Nyakati za Mwisho,
lakini kwenye tafsiri ya KJV inasomeka kuwa Siku
ya Mwisho na aya yenyewe inamaanisha kuwa ni mwishoni mwa siku zote (ukitazama Biblia ya Companion Bible utaona hivyo, sawa na hivyo, pia kwenye Mwanzo 49:1
(aya hiyohiyo moja); Hesabu 24:14; Isaya 2:2 nk., Ezekieli 38:8,16; Hosea 3:5).
Hosea 3:5 baada ya
hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme
wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho.
Wakati
Israeli watakapokaa salama katika Siku au
Nyakati za Mwisho, majirani wao wa kaskazini yaaani Gogu na Magogu wataletwa ili kupigana na Israeli.
Hii ndiyo maana inaitwa Nyakati za Mwisho,
na tunaona kwenye Ufunuo kwamba itatokea mwishoni mwa millennia pamoja na
kipindi chote cha mwanzoni (sawa na Ezekieli 38:1-23).
Ezekieli 38:1-23
inasema: Neno la Bwana likanijia, kusema, 2 Mwanadamu, kaza
uso wako, umwelekee Gogu, wa nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali,
ukatabiri juu yake, 3 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu
yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, na Mesheki, na Tubali; 4 nami nitakugeuza
na kutia kulabu katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote,
farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa
sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga; 5 Uajemi, na
Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo; 6 Gomeri, na
vikosi vyake vyote; nyumba ya Togarma, pande za mwisho za kaskazini, na vikosi
vyake vyote; naam, watu wengi pamoja nawe. 7 Ujiweke tayari,
naam, jiweke tayari, wewe na majeshi yako yote waliokukusanyikia, nawe uwe
jemadari wao. 8 Na baada ya siku nyingi utajiliwa; katika miaka ya
mwisho, utaingia nchi iliyorudishiwa hali yake ya kwanza, baada ya kupigwa kwa
upanga, iliyokusanywa toka kabila nyingi za watu, juu ya milima ya Israeli,
iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini imetolewa katika kabila za watu, nao watakaa
salama salimini wote pia. 9 Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani,
utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila
nyingi za watu pamoja nawe. 10 Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika
siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya; 11 nawe utasema, Nitapanda juu niiendee nchi yenye vijiji visivyo na maboma;
nitawaendea watu wanaostarehe, wanaokaa salama, wote wakikaa pasipo kuta, ambao
hawana makomeo wala malango; 12 ili kuteka mateka, na kuwinda mawindo;
uugeuze mkono wako juu ya mahali palipoharibika, ambapo sasa panakaliwa na
watu, na juu ya watu waliokusanyika toka mataifa, waliopata ng'ombe na mali,
wakaao katikati ya dunia. 13 Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa
Tarshishi, pamoja na wana-simba wake wote, watakuambia, Je! Umekuja kuteka mateka?
Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua
ng'ombe na mali, kuteka mateka mengi sana? 14 Basi,
mwanadamu, tabiri, umwambie Gogu, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile watu
wangu, Israeli, watakapokaa salama, hutapata habari? 15 Nawe utakuja
kutoka mahali pako, kutoka pande za mwisho za kaskazini, wewe, na watu wa
kabila nyingi pamoja nawe, wote wamepanda farasi, kusanyiko kubwa, na jeshi
kuu; 16 nawe utapanda juu uwajilie watu wangu, Israeli,
kama wingu kuifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na
nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya
macho yao. 17 Bwana MUNGU asema hivi; Je! Wewe ndiwe niliyemnena
zamani za kale, kwa vinywa vya watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri
siku zile kwa muda wa miaka mingi, ya kwamba nitakuleta upigane nao? 18 Itakuwa katika siku hiyo, Gogu atakapokuja kupigana na nchi ya Israeli,
asema Bwana MUNGU, ghadhabu yangu itapanda katika mianzi ya pua yangu. 19 Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena,
Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli; 20 hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu
vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi,
watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge
yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini. 21 Nami nitaita
upanga, uje juu yake katika milima yangu yote, asema Bwana MUNGU; nao upanga wa
kila mtu utakuwa juu ya ndugu yake. 22 Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu;
nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na
kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.
23 Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha,
mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Kutoka kwenye aya
hii tunona kwa wazi kwamba miaka ya mwisho inahusika na mchakato huu unaoitwa siku moja.
Tunaona kutoka na
mwenendo huu kwamba Mungu alianza kufanya kazi na Israeli na Yuda wakati
alipowapeleka kwanza huko utumwani. Kipindi chote cha Masihi kinahusiana na
muingilio kati wa Mungu kwenye mambo na shughuli za wanadamu. Mungu akaiteua
Yerusalemu kuwa ni kituo au kitovu cha ibada kwa nyakati zote mbili, yaani
kipindi cha Hekalu lake la nyakati za mwisho na kwa kile cha marejesho mapya
cha Masihi ambacho kwamba Mungu ataifanya upya dunia kwa kufanya kazi na
wanadamu kwenye kipindi chote cha millennia.
Yohana Mbatizaji
na Masihi walikuwa ni mashahidi wawili huko Yerusalemu na Yuda watakuwa kwenye
mwanzo wa kipindi cha zama za Masihi. Kwa hiyo Kanisa lilisimama kama shahidi
dhidi yao kwa kipindi chote cha miaka arobaini ya Ishara ya Yona. Mtume Yakobo
aliuawa shahidi mwaka 63 BK na Kanisa likakimbilia huko Pella tangu kipindi
hiki. Mnamo siku ya 1 Nisan
70 BK, Yerusalemu ulizingirwa na jeshi la Warumi. Kwa hiyo ukahusuriwa kwa
maangamizo yaliyopangiliwa kwa makini kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja hadi
kufikia Siku ya Upatanisho ya mwaka 70 BK.
Mchakato huu
umeelezewa na kuandikwa kwenye kitabu cha nabii Ezekieli tangia sura ya 4 na
kuendelea. Ulijikuta ukizingirwa na Wababelonia kama maonyo, lakini maonyo
yaliyotolewa kwa unabii na Ezekieli hayajawahi kutimilika hadi ilipofikia
mzingiro wa mwisho.
Mchato huu
uliendelea kwa kipindi cha miaka elfu mbili nab ado unaendelea.
Kwanza kabisa
Ezekieli aliwataja wateule tangia kwenye sura ya 5:1-4.
Ezekieli 5:1-4 Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie,
ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya
kupimia, ukazigawanye nywele hizo. 2 Theluthi ya hizo utaiteketeza katikati ya
mji, siku za mazingiwa zitakapotimia; nawe utatwaa theluthi, na kuipiga kwa
upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo, nami nitafuta
upanga nyuma yake. 3 Nawe twaa nywele chache katika hizo, na kuzifunga
katika upindo wa mavazi yako. 4 Nawe utatwaa tena baadhi ya hizo, na
kuzitupa katikati ya moto, na kuziteketeza katika moto huo; kutoka nywele hizo
moto utakuja na kuingia katika nyumba yote ya Israeli.
Wateule ni
masalio yaliyounguzwa na moto, na kati yao utakuja moto utakaoiunguza nyumba
yote ya Israeli katika Nyakati za Mwisho.
Ndipo Mungu
ataanza kufanya kazi pamoja na taifa lenyewe la kimwili akiongoza kutoka
Yerusalemu.
Ezekieli 5:5-12
Bwana MUNGU asema hivi; Huu ndio Yerusalemu; nimeuweka kati ya mataifa, na nchi
zauzunguka pande zote. 6 Nao umeasi hukumu zangu, kwa kutenda mabaya kuliko
mataifa hayo, nao umeasi sheria kuliko nchi hizo ziuzungukazo; maana
wamezikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika sheria zangu. 7 Basi, kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu ninyi mmefanya ghasia
kuliko mataifa wawazungukao ninyi, wala hamkuenda katika sheria zangu, wala
hamkuzishika hukumu zangu, wala hamkutenda kama kawaida za mataifa
wawazungukao; 8 basi, Bwana MUNGU asema hivi; Angalia, mimi, naam,
mimi, ni juu yako; nami nitafanya hukumu kati yako machoni pa mataifa. 9 Nami nitakutenda nisiyoyatenda zamani, wala sitafanya tena mambo kama hayo,
kwa sababu ya machukizo yako yote. 10 Kwa sababu hiyo baba za watu watawala wana
wao kati yako, nao wana watawala baba zao; nami nitafanya hukumu ndani yako, na
hao wote waliosalia kwako nitawatawanya kwa pepo zote. 11 Kwa sababu hiyo, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa kuwa
umepatia unajisi patakatifu pangu, kwa matendo yako yote niyachukiayo, na kwa
machukizo yako yote, kwa sababu hiyo mimi nami nitakupunguza; wala jicho langu
halitaachilia, wala sitaona huruma. 12 Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa
njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako
zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma
yao.
Yerusalemu
uliingiliwa na walioushinda mara 24 kwa mujibu wa historia yake, na watu wake
waliwekwa kwenye mazingiwa na kutekwa. Vitisho vya waliowazingira Yuda
vinaonekana hapa. Utawanyiko wa wakazi wake uliosababishwa na mzingiro wa tatu
ambao waliokoka kwa kufuatwa na upanga. Hii ina maana fulani katika Nyumba ya
Mungu. Kwa kipindi cha karne kadhaa, wateule wamekuwa wakijaribiwa kwa moto
usiokoma. Mungu aliendelea kuuonya mji wa Yerusalemu tangu kwenye Ezekieli
5:13-17.
Hatua ya pili
katika kuliadhibu taifa la Israeli ni kwenye kipindi ambacho Israeli ilikuabwa
na na hali iliyolisababishia kuwa kama taifa lililoparaganyika au milima. Wakajitia unajisi kwa kuabudu
sanamu na miungu ya uwongo, na miji yao ilifanyika kuwa maganjo kwa ajili ya
kuabudu kwao miungu ya uwongo.
Ezekieli 6:1-7 Neno
la Bwana likanijia, kusema, 2 Mwanadamu, uelekeze uso wako uitazame
milima ya Israeli, ukaitabirie, 3 ukisema, Enyi milima ya Israeli, lisikieni
neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi milima na vilima, na vijito na
mabonde; Tazama, mimi, naam, mimi, nitaleta upanga juu yenu, nami nitapaharibu
mahali penu palipoinuka, 4 Na madhabahu zenu zitakuwa ukiwa, na
sanamu zenu za jua zitavunjika; nami nitawatupa wana wenu waliouawa mbele ya
vinyago vyenu. 5 Nami nitaiweka mizoga ya wana wa Israeli mbele ya
vinyago vyao; nami nitaitawanya mifupa yenu pande zote za madhabahu zenu. 6 Kila mahali mkaapo miji itaharibika, na mahali palipoinuka patakuwa ukiwa;
ili madhabahu zenu ziharibiwe, na kufanywa ukiwa, na vinyago vyenu vivunjwe, na
kukoma, na sanamu zenu za jua zikatwe, na kuangushwa, na kazi zenu zifutwe kabisa.
7 Na hao waliouawa wataanguka katikati yenu; nanyi
mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana
Taifa la Israeli
lilipaswa lipelekwe utumwani na kutokomelea huko wakati lilipoangukia kwenye
kwenye mkazo wake wa kuabudu na wajibu wake kwa Mungu. Baadhi yao hata hivyo
waliachwa na kunusurika hai wakiwa kama masalia watakaomrudia Mungu.
Ezekieli 6:8-10
Lakini nitasaza mabaki; maana mtakuwa na baadhi ya watu watakaoukimbia upanga
kati ya mataifa, mtakapokuwa mmetawanyika katika nchi za watu. 9 Na hao wa kwenu watakaookoka watanikumbuka kati ya mataifa,
watakakochukuliwa mateka, jinsi nilivyoiponda mioyo yao ya kikahaba,
iliyoniacha, na macho yao, yaendayo kufanya uasherati na vinyago vyao; nao
watajichukia nafsi zao machoni pao wenyewe, kwa sababu ya mabaya yao yote,
waliyoyatenda kwa machukizo yao yote. 10 Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana;
sikusema bure kama nitawatenda mabaya hayo.
Wakati wenyeji
hawa wa Yerusalemu walipopelekwa utumwani kwenye hatua yao ya mwisho mwaka 70
BK, ilionekana haikuchuma ubani kwa vinyago. Walipelekwa utumwani kwa kuwa
iliziasi na kuzibadili Sheria za Mungu kwa mapokeo yao. Bali walikuwa bado
wanaendelea kwa uaminifu sana kumuabudu Mungu huyuhuyu wa kweli, ila walikuwa
wameziasi na kuigeuza Torati yake kwa kuyatukuza mapokeo ambayo yaliwapelekea
wenyewe kuangukia imani na dini za Kibabeloni. Walikuwa bado wanaziadhimisha
Sikukuu na Siku zote Takatifu bali walikuwa wanayageuza maana yake na ibada na
walikuwa wameanza kuitumia Kalenda iliyoanzishwa kwa mujibu wa mapokeo yao.
Baada ya
kumshuhudia Masihi, ndipo Yuda walianza kulitesa Kanisa kiasi cha kuwaua
wateule wake. Yakobo, ndugu yake Yesu, alikumbwa na maafa kama hayahaya kama
Masihi, na ndivyo walivyowafanyia Mitume wote isipokuwa Yohana. Kutopka kipindi
hiki, Mungu alianza kuwaletea maangamizi kwenye itikadi na imani ya Yuda katika
Yerusalemu. Ugumu huu wa mioyo wa Yuda utaishia na kufikia kikomo chake
itimiapo miaka elfu mbili. Mwishoni wataongoka. Hata hivyo watakuwa wamebobea
kwenye mapokeo yao kwa kipindi chote kizima. Kwakweli, walikuwa wameyashinikiza
mapokeo haya kiasi kwamba inaonekana kuwa ni vigumu kushika imani ya kale
asilia kwa kuyashika mapokeo yao na mfumo wao wa kalenda. Muundo mzima wa
Wayahudi walioko Ulaya ulikuwa karibu ukomeshwe kabisa kwenye mauaji ya Kimbari
maarufu kama Holocaust yaliyofanyika kwenye Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Vita vya
karne ya ishirini ilikuwa na maonyo kwa wote wawili, yaani Israeli na Yuda, ila
hawakuweza kabisa kuyajali wala kuyatilia maanani maonyo haya. Tunapaswa
kukumbuka kwamba Mungu alisema kwamba: Hakuna laana inayokuja pasipo sababu
(Mithali 26:2).
Kuja kwake
kutafanyiza marejesho mapya ya mfumo mzima wa kiibada na imani ya kweli ya
Torati ya Mungu. Mapokeo yote pamoja na imani na mafundisho yote ya uwongo ya
wote wawili, yaani Wayahudi na dini potofu za kale za Ukristo wa uwongo
vitafutiliwa mbali kipindi hiki. Masihi alisema kuwa maandiko hayawezi
kutanguka (Yohana 10:35), na manabii wamesema kwamba utaratibu wote wa utunzaji
wa Sabato, kukiwepo na Miandamo ya Mwezi Mpya na Sikukuu, vitaanzishwa kutoka
mjini Yerusalemu.
Kipindi cha
kuanzia Ujio wa Masihi akiwa kama Mfalme-Masihi wa Israeli hadi ufufuo wa wote
wa wafu utakapotokea na kuirudisha Siku
ya Mwisho, ambayo ni Mwisho wa Siku
zote ambayo pia ni Siku ya Bwana.
Siku ya Bwana
Neno sahihi na
halisi la kwanza la Siku ya Bwana lipo
kwenye Isaya 2:12.
Isaya 2:12 Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa
majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka;
nayo yatashushwa chini.
“Yatashushwa
chini” linamaanisha kubadilisha
sheria iliyopo leo hapa duniani kama tunavyoona kwenye Ufunuo na Yakobo 5 (hapo
juu).
Hii ni ya kwanza
kati ya maonekano ishirini ya neno hili kwenye Biblia. Kutoka kwenye matumizi
haya tunaona kwamba inaonyesha mwingiliano wa mambo ya hapa sayarini, ambayo ni
Ujio wa Masihi na kuyatiisha mataifa. Hili litafanyika kwa kuongeza muda.
Tumejionea kutoka hapo juu kwamba neno lipo kwenye kipindi cha muunganiko na
neno Siku ya Mwisho, ambacho kinadumu
kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu moja.
Mtume Petro
anatuambia jambo hili anapoongelea kuhusu uvumilivu wa Mungu na suala la muda
machoni pa Mungu.
2Petro 3:8 Lakini,
wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu,
na miaka elfu ni kama siku moja.
Kwenye matukio
kumi na sita neno hili limeandikwa yom
Yahovah au siku ya Yahova (Isaya
13:6,9; Ezekieli 13:5; Yoeli 1:15; 2:1,11; 3:14 (sawa na Waebrania 4:14); Amosi
5:18,20; Obadia 15; Sefania 1:7,14 (mara mbili); Malaki 4:5).
Isaya 13:6-9 Pigeni
kelele za hofu; maana siku ya Bwana i karibu; itanyesha kama maangamizi
yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. 7 Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na
moyo wa kila mtu utayeyuka. 8 Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na
maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana
macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto. 9 Tazama, siku ya
Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa
ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
Kipindi hiki pia
kitakuwa na vita.
Ezekieli 13:5
Hamkupanda kwenda mahali palipobomolewa, wala hamkuitengenezea nyumba ya
Israeli boma, wapate kusimama vitani katika siku ya Bwana.
Yoeli 1:15 Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya Bwana
inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.
Siku hii ya Bwana ni ya mapigano ya mwanzo wa kipindi cha mwanzo wa
millennia kilichotabiriwa na kwenye Yoeli 2:1-11.
Yoeli 2:1-11 Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu
mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya Bwana inakuja.
Kwa sababu inakaribia; 2 siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza
kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye
nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika
miaka ya vizazi vingi. 3 Moto unakula
mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na
bustani ya Adeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna
aliyeokoka asipatikane nao. 4 Kuonekana kwao
ni kama kuonekana kwa farasi; na kama wapanda farasi ndivyo wanavyopiga mbio. 5 Kama mshindo wa magari ya vita juu ya
vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto ilapo mabua
makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita. 6 Mbele yao watu
wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu. 7 Hupiga mbio kama mashujaa; huupanda ukuta
kama watu wa vita; nao huendelea mbele kila mmoja katika njia zake, wala
hawapotoshi safu zao. 8 Wala hapana mmoja amsukumaye mwenzake;
huendelea mbele kila mmoja katika njia yake; hujifanyizia njia kwa nguvu kati
ya silaha, wala hawaachi kuifuata njia yao. 9 Huurukia mji;
hupiga mbio juu ya ukuta; hupanda na kuingia ndani ya nyumba; huingia
madirishani kama aingiavyo mwivi. 10 Nchi
inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota
huacha kuangaza; 11 naye Bwana anatoa sauti yake mbele ya
jeshi lake; maana matuo yake ni makubwa sana; kwa maana yeye ni hodari
atekelezaye neno lake; kwa kuwa siku ya Bwana ni kuu, yenye kitisho sana; naye
ni nani awezaye kuistahimili?
Kwa hiyo, vita ya
Siku ya Bwana itakuwa ni kubwa sana
mwanzoni mwake na hakutakuwepo na kitu chochote kama hiki kwa vizazi vingi.
Hii inajumuisha
kipindi cha mchakato huu haiepushi na kuwa mbali na kipindi kingine cha mbele,
kama tunavyojionea kwenye maandiko.
Inapendeza kuona
aina vita na uwezo wa majeshi yakizuia uwezekano wa watu kujeruhiwa. Hii ni
aina ya vita inayopiganwa na silaha na mashine ambayo hatujawahi kabisa kuviona
hapo kabla au hata kuziwazia kwenye fikra za mavumbuzi ya kisayansi
inayoghushiwa kwenye sinema. Mungu anaruhusu utisho huu kuwaangukia wanadamu
kwa ajili ya uovu wao.
Hukumu ya itikadi
ya Mungu kwa namna mbili. Ya kwanza ni hukumu ya kimwili na itakayowatiisha
mataifa ili kuanzisha utaratibu wake. Hii inahusisha tu kuukomesha na kuuangamiza mfumo na utawala wa mataifa.
Yoeli 3:9-21 Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa
vita na wakaribie; na wapande juu. 10 Yafueni
majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi
ni hodari. 11 Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande
zote, jikusanyeni pamoja; na huko watelemshe mashujaa wako wote, Ee Bwana. 12 Mataifa na
wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana huko ndiko
nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote. 13 Haya! Utieni
mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa,
mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sana. 14 Makutano
makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku
ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno. 15 Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota
zimeacha kuangaza. 16 Naye Bwana atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti
yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa
kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli. 17 Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi
ndimi Bwana, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo
Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.
18 Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza
divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa
maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya Bwana, na kulinywesha bonde
la Shitimu. 19 Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu,
kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu
isiyo na hatia katika nchi yao. 20 Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu
tangu kizazi hata kizazi. 21 Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa;
kwa maana Bwana ndiye akaaye Sayuni.
Kitendo cha
kuyatiisha mataifa kitashuhudia pia uanzishwaji wa Yuda na Yerusalemu katika Siku za Mwisho. Ila siku hizi sio jambo
muhimu sana cha kuangalia kwenye matarajio pekee.
Amosi 5:18-27 Ole
wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza,
wala si nuru. 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika
nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru?
Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. 21 Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau,
nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini. 22 Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za
kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka
zenu za amani, na za wanyama walionona. 23 Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa
maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu. 24 Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama
maji makuu. 25 Je! Mliniletea dhabihu na sadaka jangwani muda wa miaka arobaini, enyi
nyumba ya Israeli? 26 Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya
mungu wenu, mliojifanyizia wenyewe. 27 Kwa sababu hiyo nitawahamisha, hali ya
kufungwa, mwende mbali kupita Dameski, asema Bwana, ambaye jina lake ni Mungu
wa majeshi.
[Matendo 7:43
inasema mbali na Babeli amhavyo ni
zaidi ya Damascus na inammanisha mfumo wa kidini pia. Roho Mtakatifu
amelichukua andiko la aya hii.]
Siku ya Bwana inayotajwa hapa ilikuwa ni kwa Waisraeli kwanza,
kisha kwa Yuda na hatimaye kwa mataifa. Kwa hiyo, neno hili lilitumika kama
mlolongo au mfuatano wa matukio ya Mungu kwa kipindi kizima chote cha utumwa wa
Israeli na kutiishwa kwa mataifa. Tunajionea kutokana nah ii kukamilika kwa
Mpango kama mara moja kwenye kurasa za historia, ikihusiana na mlolongo wa
matukio ya unabii wa Siku za Mwisho.
Upangiwaji wa
mataifa kwenye ahadi zaa milki zao za uzaliwa wa kwanza (kama tuonavyo hapo
juu) kunaonekana kuwa kutaitangulia hukumu ya Mungu kwa Israeli. Kitashuhudia
Baraka kuu, hawakuzitunza Sikukuu zake na katika utakatifu na haki yake. Hukumu na Haki
ni neno moja kwenye lugha ya Kiebrania la: tsedek.
Tunaona kwamba
hii inatenda kazi kwa wamataifa, kutokana na Obadia 15-17.
Obadia 15-17 Kwa
maana hiyo siku ya Bwana i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo
utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe. 16 Kwa maana kama vile mlivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, ndivyo
mataifa yote watakavyokunywa daima; naam, watakunywa na kubabaika, nao watakuwa
kana kwamba hawakuwa kamwe. 17 Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye
kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.
Mchakato huu ni
wa taratibu kwa watu wote. Vita vya karne ya ishirini ni sehemu ya nchakato huu
unaokusudia au kulenga kuvunja nguvu za watakatifu. Ni mara tu baada ya nguvu
za watakatifu zitakapokomeshwa, ndipo ule mwisho utakapokuja (Danieli 12:7).
Mchakato huu umeanza kuanzia Vita Kuu ya Pili ya Dunia na unaendelea. Kipindi
kinachojulikana kama cha Utimilifu wa
Mataifa kiliishia mwaka 1996-1997 (tazama jarida la Kuanguka Kwa Misri (Na. 36); Unabii wa Mikono ya Farao Iliyovunjika [The
Fall of Egypt (No. 36) The Prophecy of Pharaoh’s Broken Arms)].
Sefania 1:7-18
Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU; Kwa maana siku ya Bwana i karibu; Kwa kuwa
Bwana ameweka tayari dhabihu, Amewatakasa wageni wake. 8 Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya Bwana, nitawaadhibu wakuu, na
wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni. 9 Na katika siku ile nitawaadhibu hao wote warukao juu ya kizingiti, waijazao
nyumba ya bwana wao udhalimu na udanganyifu. 10 Na katika siku
ile, asema Bwana kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu
katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani. 11 Haya! Lieni,
ninyi mkaao katika Makteshi,
maana wafanya biashara wote wameangamia; hao wote waliokuwa na mizigo ya fedha
wamekatiliwa mbali. 12 Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu
kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika
mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. 13 Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam,
watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini
hawatakunywa divai yake. 14 Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I
karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; Shujaa hulia
kwa uchungu mwingi huko! 15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya
fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya
mawingu na giza kuu, 16 Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye
maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana. 17 Nami
nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda
Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. 18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu
ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana
atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.
Neno Maktesh maana yake ni chokaa au tukuza au soketi.
Inadaiwa kuwa ni jimbo au wilaya iliyo karibu na mji wa Yerusalemu, ila mtazamo
huu unawezakutokana na matumizi yake hapa. Huenda linawamaanisha wakazi wa mji.
Kama haita maanisha mahala maalumu. Kuharibiwa kwa utaratibu kijamii unaofanywa
na masuala ya kijeshi na kiviwanda ndiyo inayomaanishwa. Na hii inahusisha
kipindi kirefu na kilicho zaidi ya karne ya ishirini.
Kwahiyo, Yuda
wanatajwa hapa kama walengwa wa maangamizo ya majeshi yaliyowazunguka ya
mataifa, kama vile ya Ashuru, na kunatajwa kuangamizwa kwa mji wa Ninawi.
Mchakato huu wa kuondolewa na kuangamizwa kwa Yuda ulifanywa na Wababelonia,
waliochukua nafasi ya kutawala ya Waashuru. Kwa hiyo, hii Siku ya hasira ya
Bwana, iliyotajwa kwenye Sefania 2:1-14, inahusisha kipindi cha uharibifu na
maangamizo ya Waashuru na kinaendelea hadi kwenye kipindi chote cha utawanyiko,
na hadi kipindi cha marejesho mapya yatakayofanywa kwa lugha kamilifu na katika
marejesho mapya ya Israeli (Sefania 3:6-20).
Maana Nyingine
Kwenye vifungu
vine imeelezewa kwa kutumia neno lamed na
maana ya siku inayojulikana na Yahova
(Isaya 2:12 (angalia hapo juu); Ezekieli 30:3; Zekaria 14:1,17).
Kuangamia kwa
Misri na kusini kulionekana kuwa kama ni sehemu ya Siku ya Bwana au Siku
inayojulikana na Yahova.
Ezekieli 30:3-7 Kwa
maana siku ile i karibu, siku ile ya Bwana i karibu, siku ya mawingu; itakuwa
wakati wa mataifa. 4 Na upanga utakuja juu ya Misri, na dhiki itakuwa
katika Kushi, watakapoanguka watu waliouawa katika Misri, nao watauondoa wingi
wa watu wake, na misingi yake itabomolewa. 5 Kushi, na Putu,
na Ludi, na watu wote waliochanganyika, na Kubu, na wana wa nchi ya agano,
wataanguka kwa upanga pamoja nao. 6 Bwana asema hivi; Nao pia wanaoitegemeza
Misri wataanguka, na kiburi cha uwezo wake kitashuka; toka Migdoli hata Sewene,
wataanguka ndani yake kwa upanga, asema Bwana MUNGU. 7 Nao watakuwa
ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake itakuwamo kati ya miji
iliyoharibika.
Kwenye andiko
hili, maangamizo ya Misri yanaanza na Nebukadneza wa Babeli (Ezekieli 30:10).
Kwa hiyo. Siku inayotajwa hapa sio
ile iliyo kwenye Ufunuo bali ni ya kamsa inayoonyesha mfano unaoendana.
Aina hii ya siku inayojulikana na Bwana, inaonekana
pia kwenye Zekaria 14:1-21. Hata hivyo, kwenye andiko hili tunaona kwamba
Masihi anahusishwa na watakatifu (Zekaria 14:1-5) na kwa kweli ni kipindi cha
mwingiliano.
Zekaria 14:1-5 Tazama, siku moja ya Bwana inakuja, ambayo
mateka yatagawanyika kati yako.2 Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita
juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake
watatendwa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani; ila mabaki
ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali. 3 Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na
mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita. 4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya
mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa
Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi;
litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande
wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini. 5 Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la
milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam,
mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia,
mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.
Usemi na dhana ya
kusema siku moja inavyoonekana kutoka
kwenye andiko hili.
Zekaria 14:6-16 Tena
itakuwa siku hiyo, ya kwamba nuru yake haitakuwa na mwangaza na kiwi; 7 lakini itakuwa siku moja, iliyojulikana na
Bwana; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, ya kwamba wakati wa jioni
kutakuwako nuru. 8 Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba maji yaliyo hai yatatoka katika
Yerusalemu; nusu yake itakwenda upande wa bahari ya mashariki, na nusu yake
upande wa bahari ya magharibi; wakati wa hari na wakati wa baridi itakuwa hivi.
9 Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja,
na jina lake moja. 10 Nchi yote itageuzwa kuwa kama Araba, toka Geba mpaka Rimoni upande wa
kusini wa Yerusalemu; naye atainuliwa juu, atakaa mahali pake mwenyewe, toka
lango la Benyamini mpaka mahali pa lango la kwanza, mpaka lango la pembeni;
tena toka mnara wa Hananeli mpaka mashinikizo ya mfalme. 11 Na watu watakaa ndani yake, wala
hakutakuwako laana tena; lakini Yerusalemu utakaa salama. 12 Na hii ndiyo tauni, ambayo Bwana atawapiga
watu wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu; nyama ya mwili wao itaharibika,
wasimamapo juu ya miguu yao, na macho yao yataharibika ndani ya vichwa vyao, na
ndimi zao zitaharibika vinywani mwao. 13 Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba mashaka
makubwa yatokayo kwa Bwana yatakuwa kati yao; na kila mmoja wao atakamata mkono
wa jirani yake, na mkono wake utainuliwa ili kushindana na mkono wa jirani
yake. 14 Yuda naye atafanya vita juu ya Yerusalemu; na huo utajiri wa mataifa wa
pande zote utakusanyika, dhahabu, na fedha, na mavazi; vitu vingi sana. 15 Na hivyo ndivyo itakavyokuwa tauni ya
farasi, na nyumbu, na ngamia, na punda, na ya hao wanyama wote watakaokuwamo
matuoni mle, kama tauni hiyo. 16 Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu
aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Yerusalemu, atakwea mwaka
baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, na kuishika sikukuu ya
Vibanda.
Aya ya 17
inaonyesha kuwa mataifa hayo ambayo hayatawapeleks watu wake kushika sikukuu
huko Yerusalemu, vyua haitanyesha kwao kwa wakati
muafaka. Ni kusema kwamba dunia itakuwa inazishika kwa kuziadhimisha Sikukuu za
Mungu kipindi hiki cha utawala wa millennia au vinginevyo watakumbwa na baa la
njaa hadi watakapotubu au vinginevyo watakufa.
Usemi huu wa siku moja ni wa kimfano tu, kwa kuwa
itachukua kipindi cha miaka saba kuyaleta na kuyatiisha mataifa hadi yayatii
mamlaka ya Yerusalemu. Tunajionea somo hili au mchakato huu kutokana na anguko
la mataifa kwa namna mbili zote na habari ya Yeriko (tazama jarida la Kuanguka kwa Yeriko (Na. 142) na pia kutokana na vita vilivyoandikwa kwenye Ufunuo, kwenye majarida ya Mihuri Saba (Na. 140), Baragumu Saba (Na. 141)
na Miaka Thelathini ya Mwisho ya Dhiki ya Mwisho
(Na. 219) [The Fall of Jericho (No. 142), The Seven Seals (No. 140); The Seven Trumpets (No. 141) and The Last Thirty Years: the Final Struggle
(No. 219)].
Kwa hiyo
inahusika na Ufufuo wa Kwanza kutoka hapo na kuendelea. Hii siku inaonekana itakuwa kwenye kipindi
cha utawala wa millennia, na mataifa yote watajua umuhimu na kulazimika
kuitunza Sikukuu ya Vibanda kila mwaka, vinginevyo mvua haitanyesha kwao kwa
majira yake muafaka (Zekaria 14:13-21).
Sehemu nyingine
kwenye Biblia neno hili limejumuisha na maneno mengine kama vile hasira au kisasi.
Neno Siku ya Bwana limetokea mara nne kwenye
Agano Jipya (1Wathesalonike 5:2; 2Wathesalonike 2:2; 2Petro 3:10 na Ufunuo
1:10).
1Wathesalonike 5:1-4
Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. 2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile
mwivi ajavyo usiku. 3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo
uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala
hakika hawataokolewa. 4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile
iwapate kama mwivi.
Maana yake hapa
ni kwamba dunia inafikiri kwamba imeendeleza ama kuanzisha utawala wa amani na
mtangamano pasipo Torati ya Mungu, lakini hiki ni kipindi ambacho mifumo hii
yote itakuwa imekomeshwa na kuangamizwa.
Neno lililotumika
kwenye 2Wathesaloniake 2:2 ni siku ya
Kristo kwenye KJV, bali neno halisi ni siku
ya Bwana (kuriou; sawa na ilivyo kwenye Marshall’s Greek-English Interlinear). Siku hii ya Bwana ni siku iliyokuwa kwenye unabii wa Agano la
Kale uliotajwa hapo juu. Neno Siku ya
Kristo limetumika kwenye Wafilipi 1:10. Mtume Paulo anasema kwamba hii ni
Siku ya Kristo (Wafilipi 2:16) na kwamba ataifurahia, na kwamba hatakimbia mbio za bure. Kwa hiyo, Siku
ya Kristo ni namna nyingine ya kuelezea mchakato wa matukio yatakayoanza
kutokea taiga Ujio wake hadi Ufufuo wa wafuwote. Mtume Paulo anaingojea siku
hii na tukio hili kwa hamu kubwa, kwa kweli, hakujua kitu zaidi hadi ifike siku
hii.
Mtume Petro
anaonyesha kuwa Siku ya Bwana inahusika
kipindi chote cha kuanzia kuja kwake hadi kile cha hukumu na hadi cha kuangamia
kwa Dunia yote kwa moto na kuanzishwa kwa makao mapywa kwenye Mji wa Mungu. Maandiko
haya hayapingani; bali yanawaonysha wasomaji wenye bidii wa Biblia mpangilio na
Nyakati zilizo kwenye Mpango wa Mungu.
2Petro 3:10-16
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa
mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi
zilizomo ndani yake zitateketea. 11 Basi, kwa kuwa
vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani
katika mwenendo mtakatifu na utauwa, 12 mkitazamia
hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu
zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? 13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na
nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. 14 Kwa hiyo,
wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika
amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake. 15 Nanyi
uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu
mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa; 16 vile
vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo;
katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo
watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko
mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
Mungu alimpa
Kristo unabii wa mwisho wa Ufunuo, ambao alifunuliwa na Mungu. Kristo, alikuwa
nao hadi kipindi kile, akautendea kazi kwa imani na aliendelea kuwa mwaminifu
na mtiifu hadi kifo chake kwa imani. Hatimaye Kristo akamfunulia mtume Yohana
ili uweze kuandikwa vema na kiuaminifu. Mambo mengine bado yamefichwa
hayajafunuliwa hadi kwenye kipindi chake cha mwisho ambapo yatafunuliwa kwa
manabii wa Mungu. Na ni kwa sababu hii ya kunukuu Ufunuo wa Mungu ndipo Yohana
alisalia kuwa hai, kama Kristo alivyoonyesha (Yohana 21:22-23). Ufunuo ni ufafanuzi wa unabii wa Mathayo
24 (hususan aya ya 22). Ila siku hizo
zitafupishwa inamaanisha uharibifu au maangamizi, bali sio mchakato wote
mzima.
Ufunuo 1:1 Ufunuo wa
Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba
hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa
wake Yohana;
Yohana
alichukuliwa katika Roho katika Siku ya
Bwana ili aione hatima yake na mchakato wa maangamizo ya mataifa kwa
kipindi hiki. Yohana aliyaona matukio yatakayokuwa yakiendelea kwenye kipindi
chote kizima. Kipindi hiki kilikuwa ni cha miaka elfu moja na mia moja cha Siku ya Bwana.
Siku Iliyokuu nay
a Mwisho ni Sikukuu yenye umuhumu wake kwa kuwa inatoa taswira ashirio la
kipindi hiki cha mwisho cha miaka mia moja cha mchakato wa Ufufuo wa Pili wa
wafu.
Andiko lililo
kwenye Ufunuo 1:10 limasema Siku ya Bwana
nadala ya Siku Iliyowekwa na Bwana na
waabudu siku ya Jumapili wanavyojaribu kuitafutia namna ya kuihalalisha kwa
kutumia Biblia kwa matendo yao, itikadi ambayo ukweli uliopo imetokana na ibada
za kale za waabudu Jua. Wanatafuta kwa mbinu kutokana na maneno haya kwamba
Yohana alipewa maono haya siku ya Jumapili, ambayo kwamba ndiyo aliyoiita kuwa
ni Siku ya Bwana. Huu ni uwongo
mkubwa kabisa. Tendo la kuabudu siku ya Jumapili na kufanya makutaniko ya ibada
halikuwa likifanyika hapo mwanzoni hadi ilipofikia katikakati ya karne ya
pili—na hatimaye ilifanyika huko Roma peke yake. Iliibuka kutoka na waliokuwa
wanaipinga imani ya Kisemitiki na ilitumika kama namna ya kulilinda Kanisa huko
Roma lakini haikuweza kuchukua mahala pa Sabato hata kama hivyo (tazama kiyabu
cha Justin Martyr (Martyr-Mfiadini), kiitwacho Dialogue with Trypho; cf. Bacchiocchi, From Sabbath to Sunday, pp. 231ff.).
Ufunuo 1:10-11 Nalikuwa
katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya
baragumu, 11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo,
ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira,
na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
Maandiko ya
Kiyunani yametumia neno kuriake emera
au siku ya kifalme (tazama kitbu cha Marshall’s Interlinear). Inaelezea
mchakato wote mzima au mfululizo wa mambo na matukio yaliyoandikwa kwenye
kitabu cha Ufunuo yatakayojiri kwenye kipindi cha utawala wa miaka elfu moja.
Haimaanishi kabisa na siku ya Jumapili; wala na mchakato unaohusiana na Ujio wa
Bwana siku ya kupigwa kwa Baragumu ya mwisho, kama mlolongo wa mambo yaliyo
kwenye kitabu cha Ufunuo ilivyelekezwa kwa kina sana. Mchakato mzima unaonekana
kuwa ni Siku ya Bwana. Ufufuo wa wafu
utakuwa wa awamu mbili na utachukua kipindi cha miaka elfu, kama inavyosema na
kuonekana kwenye Ufunuo 20 ambako imeelezwa kwa wazi sana. Mchakato uneoonyesha
,chakato endelevu wa Siku ya Bwana hadi
kufikia kwenye utiishaji wa mataifa ya dunia. Kwa kweli, Kristo pia anauelezea
awamu hii iliyoelezwa pia kwenye Ufunuo ambayo inaendelea kwa kipindi cha miaka
elfu moja akiifananjsha na saa oja kwenye
Yohana 5:25-29.
Yohana 5:25-29 Amin,
amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana
wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. 26 Maana kama vile
Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima
nafsini mwake. 27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni
Mwana wa Adamu. 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja,
ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda
mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Biblia ya KJV
inasema kuwa ufufuo wa hukumu na,
neno lililotumika la kiyunani ni kriseõs
na lina maana ya hukumu na, kwa hiyo usahihi (tazama kitabu cha Marshall’s Interlinear na Bibliai ya RSV). Tafsiri hii kwenye Biblia ya KJV imetolewa ili kuunga mkono
imani ya Utatu au Utrinitariani ya mafundisho kuhusu roho, ambayo ni ya uwongo
(tazama jarida la Roho (Na. 92) [The Soul (No. 92)].
Kipindi mtambuka
cha Siku za Meisho na cha Siku ya Kumuadhimisha Bwana kinatuama
jumla ya zaidi ya miaka efu tatu. Usemi huu wa saa moja linaweka neno linguine la nusu saa lililotumika kwenye Ufunuo 8:1 kwa mihuri saba zaidi
kuliko kitu kingine chochote. Nusu saa ni kipindi moja ya arobaini na nane ya
siku moja. Hesabu hii ni kipindi cha mtambuka wa miaka iliyo kwenye Yubile
inayotangulia kabla ya miaka ya mwisho ya Sabato na Yubile ya miaka. Hesabu hii
ya arobaini na nane ni mavuno ya tatu. Nusu saa iliyo kwenye maelezo haya
inamaana ya moja ya arobaini na nane au mwaka wa hamsini ya miaka elfu moja; ambayo
kwamba, ni miaka ishirini kwa kudumu kwake. Kutokana na jinsi alivyotumia
Kristo kuhusu saa, kingeweza pia
kuendelea zaidi.
Tatizo halisi
lililoko hapa ni kwamba tofauti ya maneno itategemea na mgawanyo wa vipindi
vinavyohusiana na zama za mwanadamu na uhusiano wake na sayari au dunia.
Maneno haya
yanasisitiza uingiliaji wa Mungu kupitia Masihi.
Kwa hiyo, tofauti
hii imeendelezwa na Biblia kwamba zama za leo ni siku za mwanadamu, ambayo kwamba wanadamu wanajaribu kumuondoa
Mungu kutoka kwenye uumbaji (1Wakorintho 4:3).
1Wakorintho 4:3
Lakini, kwangu mimi, si kitu kabisa nihukumiwe na ninyi, wala kwa hukumu ya
kibinadamu, wala sijihukumu hata nafsi yangu.
Siku ya Bwana ni kiondi cha haki na hukumu ya Bwana, na hiki
kinachukua kipindi cha zaidi ya miaka elfu moja cha kukamika au kuhitimishwa
kwa zama za Dunia.
q