Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

 

 

[225]

Utangulizi kuhusu Ukristo [225]

(Edition 1.0 19990315-19990315)

 

Kristo alikuwa Myahudi. Alitunza au kuzishika Amri za Mungu na alizitii katika hali zote. Aliishi maisha yasiyo na dhambi, na dhambi maana yake ni uasi au uvunjaji wa Sheria. Alizitunza Sabato kama zilivyo katika Biblia na kulingana na mujibu wa maongozi ya kalenda iliyotumika wakati ule wa Kristo; kadiri ilivyotumika Hekaluni katika Yerusalemu na ilivyokuwa inatumika miongoni mwa Wasamaria.

 

Kalenda ya kisasa ya Kiyahudi haikwepo hadi mwaka 385BK na ilipelekea na kuahirisha kwa Siku Takatifu za Mungu kulingana na mapokeo yao (tazama jarida la Kalenda ya Mungu [156] na Sheria ya Amri ya Nne [256]). Kanisa lilikuwa haliabudu siku ya Jumapili hadi kati kati mwa karne ya  pili na kutoka Rumi (tazama jarida la Wajibu wa Amri ya Nne katika Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayoitunza Sabato [170]). Halikuiadhimisha sherehe na sikukuu ya Easter ambayo ni ya kipagani hadi wakati wa machafuko (Quarto Decimal) katika miaka ya 152 na 190BK (tazama jarida la Chimbuko la Maadhimisho ya  Christmas na Easter [235]).

 

Yesu Kristo siyo jina halisi la mtu tunayemjua kama mwana wa Mungu (tazama jarida la Maana ya Neno Mwana wa Mungu, [211]. Aliitwa Yahoshua au Yoshua (tazama jarida la Yoshua Masihi, Mwana wa Mungu [134]). Alikuwa na idadi kadhaa ya ndugu wa kiume na wa kike ambao walikuwa na majukumu maalumu katika kanisa baada ya kifo chake. Majina ya ndugu zake yameandikwa katika Biblia na pia yametunzwa katika maandishi ya kanisa la awali (tazama jarida la Mababa wa Waliokuwapo kabla ya Mtaguso wa Nikea). Watu wa ukoo wao waliuawa wakati wa uchochezi wa utawala wa kaniza la Kirumi kuanzia katika Karne ya Nne (tazama jarida la Bikira Mariamu na Ukoo wa Yesu Kristo [232]). Kristo hakuwahi kamwe kwa wakati na mahali popote hakudai kuwa yeye ni Mungu. Wala Kanisa halikuwahi hata mara moja kumhesabu yeye kuwa ni yule Mungu wa kweli au hata kumfananisha kuwa sawa na Mungu hawakufanya katika kipindi kile chote cha karne mbili za kuwepo kwao (tazama jarida la Teolojia ya Mwanzo Kuhusu Uungu [127] Hapakuwa na Mtume yeyote aliyeamini imani ya Utatu. Imani ya Utatu Mtakatifu haukuanzishwa wala kuwepo katika Mtaguso wa Baraza la Nikea mnamo mwaka 325BK. imani hii ilianzishwa na kupitishwa rasmi katika Mtaguso wa Baraza la Contantinople mnamo mwaka 381BK (tazama majarida ya imani juu ya Mungu Mmoja na Imani ya Utatu [076],  Kupewa Uweza na Baba [081] na lile la Roho Mtakatifu [117]).

 

Hoja kwamba Kristo ni Mungu kama sehemu ya mmoja wapo wa wahusika katika mambo ya kimungu kwa mtazamo wa kuwa yeye ni Mwana pekee ilitokana na mafundisho ya ibada ya mungu Atis ambaye alikuwa ni mungu wa Lydia na alikuwa amemwamini mungu huyu aliyekuwa ameshika hatamu ya umarufu na kufuatwa na wengi huko Rumi. Ilikuwa ni aina nyingine ya ibada za miungu Ishta au Easter au Asarte au Ashtarothi. Mwanzoni mwa karne ya Nne makuhani wa Attis walilalamika kuwa Wakristo wameiba mafundisho yao yote (tazama jarida [235] na la Utakaso na Tohara [251]). Hoja kuwa Kristo angekuwa Mungu kama Mungu na alikuwa Mungu, kwa kweli ilitokana na falsafa za Kiyunani kutokana na upungufu uliokuwepo katika lugha yao. Hawakuwa na neno linaloezea upendo wa Mungu hivyo waliazima neno la Kiebrania linaloitwa ahabah kwa mtazamo huu ambalo walibadilisha kuwa agape. Walisema kuwa ni Mungu pekee ndiye anayeweza kufanya upatanisho kati ya watu na yeye mwenyewe. Kama Yesu asingekuwa Mungu angewezaje kufanya upatanisho huo? Wazo hili halikuwa sahihi, lakini yalipokewa na Wayunani ambao walipewa kusimamia makanisa ya mashariki na kuwaondoa ndugu zake Kristo ambao waliitwa "Desposyni" (tazama ibid [232]). Hili kwa kweli hatimaye liliunganishwa na mfumo wa zamani wa kipagani wa Mungu wa Utatu (tazama majarida ya Maendeleo ya Utaratibu Uplatoni-Mamboleo [017] na Lengo la Uumbaji na Dhabihu ya Yesu Kristo [160]).

 

Kama matokeo ya vita vya watu wa Ariani na kubadili dini kwa Wafrank na  Waingereza wa asili maarufu kama Anglo-saxon, wa Kanisa linalotunza Sabato ambao walikandamizwa na utendaji wa Kiutawala wa Kirumi uliokuwa unaamini imani ya Utatu (tazama majarida ya Migawaniko Mikuu ya Makanisa Yanayoitunza Sabato [122]; ibid. [170] na lile aliloandika Cox-Kohn, Watunza Sabato katika Transylvania, toleo linalojulikana kama CCG Publishing, 1998 pp.i-xxvii).

Watunza Sabato, pamoja na kukandamizwa huko Ulaya, walisababisha kuanzishwa kwa Mageuzi katika Uprotestanti ambayo hata hivyo yalishindwa kurudisha imani ya kweli (tazama jarida la Usociniani, Uariani na Uunitariani [185]). Yaani ni imani tatu kila moja pekeyake, ya kwanza ni wale wasioamini mafundisho ya Utatu, uungu wa Kristo na upatanisho (Socinianism), wale wanaoamini mafundisho ya Arius yaliyokuwa yanakataa uungu wa Kristo (Arianism) na wale wanaoamini juu ya Mungu mmoja tu mwenye kustahili sifa zote za uungu na kuyakataa mafundisho ya Utatu (Unitarianism).

 

Wayahudi waliamini kuwa Mungu kamwe hakujidhihirisha kwa mwanadamu na kuwa Sheria za Torati zililetwa kwao kupitia kwa Malaika Mkuu wa Yehova ambaye pia aliitwa Yehova; ambaye alikuwa Mungu wa Pili wa Israeli. Ambaye alitenda na kunena kwa niaba ya Mungu na alikuwa pamoja Israel katika nguzo ya moto na wingu kama inavyoonekana ama kuandikwa katika kitabu cha Kutoka. Msimamo huu ndio waliokuwanao hata mitume na kanisa la kwanza vile vile (tazama majarida ya Malaika wa YHVH [024]; Zaburi 45 [177]; Zaburi 100 [178]; Elimu ya Asili ya Jina la Mungu [220] na Isaya 9:6 [223]). Kanisa liliamini kuwa mungu wa dunia hii ni Shetani (tazama jarida lisemalo Lusifa: Mbeba Nuru na Nyota ya Alfajiri [223]). Kanisa halikuamini kuhusu mbinguni na kuzimu na lilikataa mafundisho ya Roho isiyokufa na kwamba inaweza kuishi milele na kuyahesabia kuwa ni mafundisho ya uongo na makufuru (tazama majarida ya Roho [092] na Kuhusu Hali ya Kutokufa [165]). Watu waliomimi kuwa ulipokufa ulikwenda mbinguni walikuwa walikuwa ni Wagnostiki na walilingiza mafundisho mengine mengi ndani ya kanisa (tazama majarida ya Biblia na Sheria ya Mboga-mboga [183]; Divai katika Biblia [188] na Wanikolai [202]).

Kanisa lisingeweza kuanza kutawala hadi ufufuo wa kwanza utakapokuwa umetimia na wangetawala sayari ya dunia yetu hii kwa kipindi cha miaka elfu moja chini ya Masihi na halafu baadaye kushiriki katika ufufuo wa pili na kuiandaa sayari ya dunia yetu tayari kwa Mji wa Mungu (tazama majarida ya Milenia na Kunyakuliwa [095] na lile la Mji wa Mungu [180]).

 

Kristo alikuwa na jukumu maalumu la kufanya katika uumbaji. Yeye hakuwa ni yule Mungu wa pekee wa Kweli. Alitumwa na Mungu mmoja wa pekee na wa Kweli na katika kulijua hili, ni muhimu katika kuwa na uzima wa milele (Yoh 17:3), (tazama jarida la Majukumu ya Masihi [226]). Hata hivyo hakuwa yule Mungu Aketiye Mahali pa Juu Palipoinuka, yaani Eloi, ila yeye alikuwepo tangu mwanzo (tazama jarida la Kuwepo Tangu Mwanzo kwa Yesu Kristo [243]). Alikuwa miongoni mwa wana wa Mungu wakiwepo wakati wa uumbaji kwa mtazamo wa wingi wa neno elohim. Kanisa lilielewa na kufundisha kwa karne nyingi kwamba wateule watakuwa wana wa Mungu (elohim) kama Malaika wa Yehova katika vichwa vyao (tazama Zekaria 12:8 na jarida la Wateule Kuwa Elohim [001]).

Uingizaji au uvamizi wa mafundisho ya uongo yahusuyo dhana ya Mungu wa Utatu au kuwa amegawanyika katika nafsi tatu ulipelekea kuanzishwa kwa dini ya Kiislamu ambayo ilipinga dhana hii moja kwa moja na kwa uwazi. Muhamad na mahalifa wa kwanza wanne ambao walijulikana kama wenye msimamo sahihi, walikuwa viongozi pekee ambao walikuwa na mafundisho sahihi ya Kiislamu. Baada ya wao Uislamu ulisambaratika na kupotoshwa na desturi kama ilivyotokea kukumbwa katika dini za Kiyahudi na Ukristo ilivyotokea kabla yao (tazama majarida ya Krisot na Korani [163] na Sabato ndani ya Korani [274]).

 

Kristo hakuwa ni yule Mungu wa pekee wa Kweli ambaye hakuna mwanadamu aliyewahi kumwona na kwamba hakuna mtu anayeweza kumuona na ambaye ni yeye pekee ambaye anaishi milele na hawezi kufa (tazama 1Timotheo 6:16, na jarida la Kristo na Uungu [237]). Kristo alikuwa Kiinii cha Uumbaji wa Mungu na alikuwa na kusudi maalum katika uumbaji (tazama jarida la Kiini cha Uumbaji wa Mungu kama Mwanzo na Mwisho [229]). Uumbaji una mpango maalum unaoshabihiana katika sikukuu zilizoandikwa katika Biblia (tazama jarida la Sikukuu za Mungu Kama Zinavyohusiana na Uumbaji [227]). Ni hivi karibuni tu Masihi atarudi kuwaokoa wale ambao wanamngojea kwa hamu; na kuanzisha mfumo wenye kuzifuata Sheria za Mungu na mfumo wa utawala katika sayari hii (tazama majarida ya Jedwali la Ratiba ya Nyakati [272]; Sheria za Mungu [L1] na Mafuatano ya Amri za Mungu [252]).

 

Kanisa ni kundi dogo lililochaguliwa na kuitwa litoke nje ya maisha na mwenendo wa ulimwengu huu kwa kipindi cha miaka hii elfu mbili iliyopita na limeandaliwa kwa utawala wa Mungu kwa miaka elfu yaani wa Milenia. Wao ni Hekalu la Mungu na wametakaswa na kutengwa kwa matendo na juhudi zao husaidia katika kazi ambazo Mungu alimpatia Masihi ili azikamilishe (tazama majarida ya Utakaso wa Hekalu la Mungu [241], Kupimwa kwa Hekalu [137]; Utawala wa Mungu [174] na Mungu na Kanisa [151]).

 

 

 

 

(Copyright Ó 1999 Christian Churches of God)

(Tr. 2005)