Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[229]
Mwanzo
wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na Omega
(Toleo La 1.0 19971217-19971217)
Malumbano na hoja
za Wakristo wa siku hizi kuhusu Kristo yana mambo mengi yanayotokana na falsafa
za Kiyunani na imani na matendo yaliyokuwa kwenye dini za kale yanayoenenda
kinyume kabisa na mafundisho ya Biblia. Baadhi ya maandiko ya aya za biblia za
Kiingereza yamepotoshwa kitafsiri ili kutimiza malengo na mwelekeo wa mwenendo
wa kiimani na jinsi ya kuyachukulia maneno kwa kuwa yanakusudiwa yaendane na
mwelekeo wa imani na teolojia ya waamini Utatu. Maana wanayoyachukulia neno la
Mwanzo, Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, chimbuko na mwisho wake.
Yamefafanuliwa kwa kina ikitiliwa maanani kujumuisha maandiko mengine kadha wa
kadha.
Christian Churches of God
Email: secretary@ccg.org
(Hatimiliki ©
1997 Wade
Cox)
(tr.
2016)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na
tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia.
Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala
yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Mwanzo wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na
Omega
Kwenye majarida mbalimbali
yanayohusu Mungu na Masihi, tumeshughulika na mambo mawili ya kwanza ya dhana
iliyopo kuhusu Uungu, kwa wale wanaoitwa Mungu Baba, na Yesu Kristo kama Mwana
wa Mungu. Muhtasari wake unapatikana kwenye ya kwanza ya jarida letu la Matamko
ya Msingi wa Imani ambapo Mungu Baba anaonekana wazi sana kuwa ndiye Mungu wa
pekee na wa kweli, na kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na kwamba kwa kujua
na kuelewa hivyo ni sharti muhimu katika kuupata uzima wa milele (Yohana 17:3).
Mungu Baba
Muweza wa Mambbo
yote na Muumbaji wa Ulimwengu huu ni Mungu. Yeye ni Mwenye Uweza na guvu zote, Muumbaji
na ndiye Aliyezifanya au Kuziumba Mbingu, nchi na vitu vyote vilivyomo ndani
yake (Mwa. 1.1; Neh. 9:6; Zab. 124:8; Isa. 40:26,28; 44:24; Mdo. 14:15;
17:24,25; Ufu. 14:7). Yeye peke yake ndiye hawezi kufa wala kupatwa na madhara
yoyote (1Tim. 6:16). Yeye ndiye Mungu wetu na Baba yetu, na ndiye Mungu na Baba
wa Yesu Kristo (Yn. 20:17). Yeye ndiye Mungu Mkuu na Aliye Juu Sana (Mwa.
14:18; Hes. 24:16; Kum. 32:8; Mk. 5:7) na ndiye Mungu wa Pekee na wa Kweli (Yn.
17:3; 1Yoh. 5:20).
Yesu Mwana wa Mungu
Yesu ni mzaliwa wa
kwanza (prototokos) kati ya viumbe vyote
(Kol. 1:15) ambaye ni mwanzo (arche) wa
kuumba kwa Mungu (Ufu 3:14). Yeye ni mzaliwa wa pekee (monogene) Mwana wa Mungu (Mt. 3:17; Yn. 1:18; 1Yoh. 4:9), aliyetungwa
mimba yake kwa uweza wa Roho Mtakatifu na akazaliwa na bikira, Mariamu ambaye
anaitwa kimakosa Maria au Mary kwa Kiingereza (Lk. 1:26-35). Yeye ni Kristo au
Masihi (Mt. 16:16; Yn. 1:41), aliyetumwa kutoka kwa Mungu ili awe Mwokozi na
Mkombozi wetu (Mt. 14:33; Yn. 8:42; Efe. 1:7; Tit. 2:14).
Maelezo
yaliyo kwenye Ufunuo 3:14 kwamba Kristo ni mwanzo wa kuumba kwa Mungu yana
maana kubwa sana. Hatuelewi kwa ujumla leo kwa nini Yesu Kristo alimwambia Yohana awaambie Kanisa la
Walaodikia, akikazia kuwa, “mwambie malaika wa kanisa lililoko
Laodikia kuwa mimi ni mwanzo wa
kuumba kwa Mungu”. Sasa, sababu iliyofanyika hivyo ilikuwa ni kwa sababu, kwenye kanisa la
Walaodikia, malumbano yaliibuka kwa namna zote mbili, yaani kanisani na kwa
zama zile kwamba Kristo hakuwa mwanzo wa
kuumba kwa Mungu. Malumbano haya yalituama karibu kwenye suala la umilele na
uwepo wa Mungu kwenye mambo yote.
Neno mwanzo maana yake ni kuanza. Neno
lililo kwenye Ufunuo 3:14 linaonekana kuhusiana na mjadala wa kifalsafa ambao
ulishika kasi sana huko Mashariki ya Kati kutoka kwa Philo kwa kupitia Imani ya
Kiplatoni ya zama za Kati. Hoja ilituama kwenye suala la theori kuhusu chanzo
au mwanzo wa dunia. Yakupasa kuelewa kuhusu hoja hizi kwa kuwa maana yake
inaelekea kwenye Vuguvugu la Mkakati wa Zama Mpya. Utaelewa au kujua pia kuhusu
Kufuru ya mkakati huu wa Vuguvugu la Zama Mpya. Na pia utajua kuwa ni unabii wa
Yesu Kristo kwamba hoja hizi zingeweza kuibuka kwenye kanisa katika siku za
mwisho na kwamba kanisa la Walaodikia lingetiwa unajisi na vuguvugu hili na
kuondolewa sehemu yake kwenye ufufuo wa kwanza wa wafu. Mwanazuoni wa
kiteolojia Clement wa Alexandria aliyachukulia malumbano haya kama ni mtindo au
aina ya Ukostiki (Nostis au Gnosis maana yake ni ujuzi au maarifa wakati kwamba Unostiki
au Gnosticism ulikuwa ni mchakato ambao kwamba mwangaza uliowezeshwa na kutolewa).
Kuna viwango viwili vilivyopo; vya kukubalika na Unostiki. Makuhani kwa kweli walifanyika
kuwa na asili ya Unostiki. Walidaiwa kuwa wana maarifa ya siri na hii haki ilipewa
kiwango cha chini cha ujuzi au maarifa. Haya kiutendaji yalifanyika kuwa
mafundisho ya Wanikolai ambapo makuhani walioelimishwa au kusomeshwa
waliaminiwa kuwa walikuwa na maarifa na uelewa ambao hii haki hawakuwanayo, au
hawakumudu kuwanayo kiasi cha kuwafanya wakubalike kujumuishwa kwenye imani za
kisirisiri na za fumbo zilizohusiana nayo. Kristo alisema kwamba anayachukia
mafundisho ya Wanikolai na mafundisho ya Balaamu ya kufundisha kwa ajira.
Mafundisho ya Balaamu yanaendana mkono kwa mkono na mafundisho ya Wanikolai na
mafundisho haya, na kwa kweli, ni ya Mpingakristo moja kwa moja. Yanahuia au
kuzuia nafasi ya Roho Mtakatifu kukua ndani ya mtu. Yatupasa kujua uhusiano na
utendaji kazi wake katika Roho Mtakatifu. Mafundisho haya yamefafanuliwa vizuri
kwenye majarida ya Wanikolai (Na. 202) na pia lile la Mafundisho ya Balaamu na Unabii wa Balaamu (Na. 204).
Clement alimfuatia mwandishi
wa Kiyahudi aliwate Philo kwenye kuutafsiri mwanzo uliotajwa kwenye kitabu cha
Mwanzo kwa kutuama kwenye tofauti iliyopo kati ya Uplatoniki kati ya mguso
hisia na uashawishi wa kiakili ya dunia ya wenye akili. Maneno ya kiraslimali
na yasiyo ya kiraslimali kimsingi yaliendelezwa sambamba na mistari ya
Kiplatoniki. Kwa hiyo, alikuwa akibishana pia na upande wa Uplatoniki ambao pia
ulichukuliwa kuwa ni ulimwengu wenye kuvutia kama nakala yenye mashiko.
Salvatore Lilla (kwenye kitabu chake cha Clement
of Alexandria [Clement wa Alexandria], Sura ya III, Oxford University
Press, 1971, p. 192) analiona hili na kwenye ukurasa wa 230 anasema:
Fundisho
lililohusika la Clement, kama Philo na Uplatoni wa Kati, yaonekana kuamini
kwenye dhana ya kuwepo kwa kiumbe siku za kabla ya kuzaliwa rasmi na
kuichukulia hii kubadilisha aina yoyote na kiwango chochote (sawa na ilivyo
kwenye Sura ya III, ukurasa wa 226).
Makubaliano yalikuwa ni sehemu
tu kwa kama alivyokataa Clement mtazamo wa nadharia hii ya Kiplatoni kwa mujibu
wa jambo ambalo kwamba mtu anaweza kuwa archai
– uwingi wa mwanzo chimbuko au chanzo cha dunia. Clement alisema kuwa
isingeweza kuwa; lakini wao walisema ilikuwa hivyo, na jambo hilo ni halisi. Clement
anatetea kwamba Mungu ndiye mwanzo pekee
na wa kweli na mwanzo mwingine wowote
mwingine unafuatiwa kutoka kwa Mungu. Sasa Kristo alikuwa anasema kwamba yeye
alikuwa ndiye mwanzo wa uumbaji wa
Mungu kwa kuwa aliumbwa kuwa mwakilishi kutoka kwa Mungu. Huo ndio msimamo wa biblia,
na ndiyo maana Yesu Kristo alisema hivyo. Clement aliamini baadae, kwamba Mungu
ndiye mwanzo pekee wa uumbaji, jambo
ambalo ni kweli kutokana na Ufunuo 4, ambapo vitu vyote vimeumbwa kwa mapenzi
ya Mungu. Lakini Waplatoni walikuwa wanasema kuwa yeye mwenyewe tu ndiye
alikuwa ndiye mwanzo. Clement
aliamini uwepo wake mapema ya mwanzo wa dunia. Kwa maneno mengine, yeye alikuwa
na uwepo au uzima wa ndani kwa ndani yake mwenyewe kabla ya kuumbwa kwa dunia.
Hii ni sawa tu na suala la kipigo kikubwa.
Kwa hiyo nadharia ya kipigo kikubwa sio
kitu kipya. Haya ni mafundisho ya Kiplatoniki. Clement alitetea lawama ya
kwamba Wastoniki, Plato, na Aristotle walichukulia uwepo huu wa mwanzoni kuwa
ni kama moja ya kanuni za kwanza. Aliliweka sawa jambo hilo ili lielezewe na
wanafalsafa hawa kama kiasilia kulikuwa tupu na hakukuwa na ubora wowote na
kukafafanuliwa na Plato kama ni mimi anayekuja
kuwepo na kuishi kwa kukubalika (upodoche)
(soma pia Timaeus 49e-50a, 50b-c), na
kuwa umbo tupu (Tim. esp. 50d-e), vigumu
kujua (51b1), maana iliyo pana zaidi kwa maana ya kutokuwa halali au kiuharamu (alikosea:
Lilla) kufikiria kwa kutoaminika kirahisi (52b2). Clement anaonekana
kukubaliana nao kabisa (Lilla, p. 193). Kwa hiyo huko tuna makanisa yanayoanza
kutunga na kuingiza dhana hizi, wakiachana kabisa na isemavyo biblia na
wakielekea kwenye Uplatoniki. Huu ni mwanzo wa kufikiria Uttinitariani na Uplatoniki
wake, safi na rahisi. Philo (wanafalsafa wa Kiyahudi akiandika kwenye kipindi
cha kabla ya Kristo) na Plutarch kwa kinyume chake kabisa alimchukulia huyu
aliyekuwako huko nyuma kuwa ni kama bado ni ousia
(Lilla, p. 230). Lilla anasema kwamba Plutarch pamoja na Waplatoni wengine wa
zama Kati kama vile akina Albinus, Apuleis na watunzi wa kitabu cha tatu wa
huko Diogenes Laertius na wa Hippolytus walimchukulia kiumbe huyu kuwa ni kama
wa milele na aliye tupu kwa kila kiwango na asiye na umbo (ibid., Ch. III, pp.
193,195-6). Kwa hiyo, walikuwa wanasema kabisa kwamba ni juu yake na yupo,
lakini hana umbo waka muonekano, bali ananing’inia
tu mahali apajuapo mwenyewe. Tuna muundo huu (umilele) unaobeba ujazo wa tabia
ya Mungu. Una umilele kwa haki yake. Kutokana na mchakato huo wa kimawazo ndipo
kumetokea imani ya Uanimisti ya Kibabeloni na kwa zaidi tu kwamba ni mwanzo wa mchakato
wa wazo au dhana hiyo. Kuhusiana na jambo akiwa kama mimi zaidi Clement anakubaliana na imani ya Upythagoreanism
mamboleo, pamoja na Plotinus, na huenda pia na Ammonius Saccas (Lilla, Ch. III,
pp. 195-196 and fn. 1, p. 226).
Kiumbe anayejadiliwa kuwa ni
kama hana umbo na wa milele au ameumbwa bila umbo. Hicho ndicho kiini na maana
ya mabishano haya. Umilele usio na umbo wa kiumbe huyu unamfanya awe kuwa ousia au mshirika na Mungu, kwa hiyo Mungu ndiye aliyefanyika kuwa mwili na
ambaye ni washirika na Mungu walikuwa ni washirika wa kimsingi. Sasa tunakwenda
mbali na zaidi ya hapo makanisani mwetu.
Ndipo swali liliibuka: Dunia
iliumbwa au haikuumbwa? Kwa maneno mengine, je, ilikuwa na uzima yenyewe au
iliumbwa? Hii inaondoa malumbano ya huko nyuma sasa ya nadharia ya viumbe
kugeukageuka yaani evolusheni na uumbaji. Kristo alikuwa anasema kwamba haikuwa
hivyo; na kwamba yeye alikuwa ndiye chanzo.
Alikuwa ndiye chombo kilichotumiwa kwenye uumbaji wa Mungu na kwamba jambo hilo
(ulimwengu) wenyewe haukuwa ni chanzo
na Mungu sio kwamba hayupo kwenye jambo, hayuko kwenye miamba, kwenye jiwe, na
kwenye nyasi. Kusema kwamba Mungu yupo kwenye jambo, kwa maana ya kuharibu au
kuangamiza na kuua na kwamba Mungu mwenyewe anamaovu yake kwa ndani yake, dhana
hiyo ni ya makufuru makubwa. Hivyo tunafikia kwenye hatua ambapo Shetani
alichukuliwa kuwa muovu tangu mwanzoni mwa kuumbwa kwake na kwa kweli ni mshirika
anayeandamana na uovu akimchukiza Mungu.
Ni sawa tu kabisa, kwamba
malaika ni washiriki wa Mungu, kama viumbe wapeleka ujumbe wake. Mtu anaweza
sasa kuona uovu mkubwa wa kufuru inayojitokeza. Watu wamepigwa upofu kwenye tatizo
hili. kwa kiasi kikubwa ni kwa sababu wanayafuata mafundisho na sera za
serikali ambazo hazina lolote la kulinganisha na imani ya kibiblia. Na ndiyo
maana Mungu na Kristo wake wanayachukia sana mafundisho ya Wanikolai.
Yanawapofusha watu wasiisikie wala kuona kweli. Wamepotoshwa kwa mafundisho ya Waplatoni.
Wateule wanapaswa kutahadharishwa na kujiepusha na makosa ya kimafundisho.
Ujumbe kwa Walaodikia umeweka wazi sana kwa kiasi fulani kutokana na
mjadala huu. Mjadala wa kifalsafa ulituama karibu kwenye utoshelezi wa kwamba
muumbaji mwenyewe ni ousia au mshirika wake yeye na kwamba Mungu alikuwa
yupo kwenye suala zima lolote. Kwa hiyo Mungu alikuwa kwenye ubao au kuni na
jiwe. Hii ni dhana au wazo la msingi nyuma ya imani ya Kianimism pamoja na ile
iliyokutikana huko Babeli, ya Ushamanism na Nadharia zote za Uhuru na Ukombozi
zinazoeneza imani ya Kibudha na imani iliyoshika dau huko Japani ya Ushintoism.
Sasa kitabu cha Sir Wallace Budge kuhusu Babeli (alichimba kwa kina kuhusu jambo
hili) kimekuwa karibu kwa kipindi kirefu. Tumekijua kwa zaidi ya miaka mia kuwa
dini ya Babeli ipo. Dini ya Kibabeli ilikuwa ya kianimistiki nah ii ndiyo hasa
dini yenyewe iliyoyasukuma karibu Makanisa mengi ya leo.
Clement, kama alivyokuwa
Philo na Waplatoni wa pande za Mashariki ya Kati – Plutarch na Atticus – walionyesha
wazi sana kupendelea kizazi. Clement, akimfuatia Philo, alitetea kwamba uumbaji
haukuwa umefanyika kwa wakati, kwakuwa wakati wenyewe unategemea moja kwa moja
na mwelekeo wa ulimwengu (Lilla, p. 230). Hii kimsingi makosa (kwa kuwa sababu
zilimetolewa hapo mwanzoni na kwenye majarida mengine) na zilichukuliwa na Augustine
kwenye kitabu chake cha Mji wa Mungu.
Kurudia kipengele cha Wakati na Hali ya
Kutokufa kutoka kwenye jarida la Uzima wa Milele (Na. 133):
Wazo au dhana ya
wakati inajitokeza tu wakati kunakuwa na uhusiano kati ya vitu. Kwa mfano, siku
inatokea kwa mzunguko au mwenendo wa dunia kwenye mhimili wake ikihusishwa na
jua. Mwaka unaotokana na mzunguko wa jua unajulikana kama mageuzi mamoja ya
dunia karibu na Jua. Kuna miaka kadhaa inayohusishwa kwenye mwenendo au
mzunguko wa mhimili, yaani Jua/Upande/Kigalaktiki. Ulimwengu una jinsi ya
kujiongeza au kujitanua ambayo inahusiana na mwenendo wa mbali na kituo cha
msingi.
Kituo cha msingi
kiliamuliwa na Penrose kuwa ni kama kipimo cha nguvu cha kumi na hadi kwa kumi
hadi kwa 123 [cha nishati]. Hivyo, kutokana na nguvu zake zote za asili za
namba hii yapasa kuwa na sababu ya mwanzo wake, na sio nyingine kwa ulimwengu.
Mienendo yake yote imeelezewa kwene dhana ya wakati ambao unahusiana na mfumo
wa mzunguko wa dunia.
Licha ya utaratibu
wa upimaji inaweza tu wakati ule ilianza kwa kuhusiana na idadi ya kitu kimoja
au zaidi kwa kila kimoja kwa kingine. Hivyo basi kipindi kingeanzia tu kwa
uwepo wavitu viwili au zaidi. Mungu alikuwepo hata kabla ya kuanza kwa muda.
Kizazi cha elohim kwa kweli ndicho kilikuwa ndiyo mwanzo wa wakati. Mwanzo wa kuumba
kwa Mungu (Ufu. 3:14). Wakolosai 1:15 inasema kwamba Kristo alikuwa ndiye
mzaliwa wa kwanza na wa pekee wa Uumbaji.
Kwahiyo Bwana Mungu
ni Alfa, kwa maana zote mbili na yupo anaishi, na ndiye mwisho wa mambo ya
matendo yale. Yeye pia ni Omega:
Ufunuo 1:8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho,
asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
(yaan wakati
anapofanyika kuwa yote katika yote na ndani ya yote (Efe. 1:23)).
Wazo la wakati lilianza kwa
uwepo wa Yesu Kristo. Kwa kuwa wakati Yesu Kristo alipoumbwa (na elohim
walipoumbwa) ndipo wakati ulianza kwa kuwa kulikuwa na uhusiano kati ya viumbe.
Ni Mungu peke yake ndiye aliishi milele pasi kufa wala kupatwa na madhara. Licha
ya masuala ya upimaji, kuna vitu viwili vinavyofanya kuwepo na muda au wakati.
Kristo ndipo anafanyika kuwa uumbaji wa Mungu kutokana na kuzaliwa kwake.
Viumbe wote wametokana na Mungu. Kwa hiyo, Mungu ndiye wa Mwanzo au Alfa kwa
namna au maana mbili zote na kwa kuwepo na ni wa mwisho kwenye utendaji. Hivyo,
yeye pia ni Omega kutokana na Ufunuo 1:8. Hivyo Kristo alilionya kanisa la
Walaodikia na tunapaswa kujua kuhusu maonyo waliyoonywa Walaodikia.
Alfa na Omega jinsi alivyoendelea hadi kwa Yesu Kristo
Majina cheo ya
Alfa na Omega na majina mengine yaliyotumiwa hasahasa kwenye kitabu cha Ufunuo
yanajibu hamu ya kifilosofia ya Kiyunani pamoja na kuelezea ukweli wa
uwakilishi wa elohim kwa wateule kupitia kwa Yesu Kristo.
Ufunuo 1:11 kwenye
tafsiri ya KJV inataja cheo hiki cha Alfa na Omega ikimtaja na kumhusisha Yesu
Kristo. Jina hili la kicheo halipo kwenye tafsiri ya RSV na nakala za maandiko ya
kale (kama inavyosema Companion Bible angalia kwenye andiko hilo). Inaonekana
tu kwenye tafsiri ya Receptus na pia kwenye KJV.
Umuhimu wa nyongeza hii kwenye matumizi yake ili kuonyesha mtiririko ya
kile kinachotokea kwenye utendaji kazi wa jina cheo hili toka Mungu hadi kwa
Kristo kwenye mtiririko wa unabii wa Ufunuo.
Hivyo, andiko halisi
linalosomwa zaidi au lisilosomwa sana kama ilivyo tafsiri ya RSV:
Ufunuo 1:11 ikisema,
Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso,
na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
Andiko hili linatokana
na tafsiri ya KJV:
Ufunuo 1:11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo,
ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira,
na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
Uingizaji huu wa andiko
umefanywa maalumu na kwa makusudi ili kuunga mkono au kutetea imani ya Utatu au
Utrinitarian na kupuuzia maana iliyokusudiwa na sehemu nyingine iliyobakia ya
Ufunuo kwenye suala hili.
Ufunuo 1:8 inafafanua
rejea hii kuwa inamhusu Mungu ambaye Ufunuo 1:6 inasema kuwa ni Mungu na Baba
wa Kristo.
Ufunuo 1:8 Mimi ni
Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na
atakayekuja, Mwenyezi.
Tunaona tena KJV ikiitumia
tafsiri ya Receptus kuwakilisha maneno ho
theos au Mungu na ikitumia kurios peke yake au Bwana. Kwa hiyo andiko hili linabeba tofauti kubwa sana na lengo la
kupotosha na kudanganya kwa maandiko yote mawili yanayomtaja Kristo wakati Alfa
na Omega yanatofauti inayomaanisha Bwana Mungu na Baba wa Kristo na hayamaanishi
Kristo kabisa tangu mwanzo. Hii ina mengi ya kufanya na teolojia kama
ilivyoendelezwa kutokana na msukumo wa wanafalsafa wa Kiyunani na waamini Utatu
kama tuonavyo hapa. Lilikuwa ni jaribio la makusudi la kuipotosha asili ya
kweli na nafasi aliyonayo Kristo kwenye uhusiano wake na Mungu wake na kumuinua
yeye kwa kutumia imani na mfumo potofu wa Kiutatu.
Ufunuo 1:8 Mimi ni Alfa na
Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na
atakayekuja, Mwenyezi.
Aya za Ufunuo 1:17 na
2:8 havina maneno haya ya Alfa na Omega.
Zinatumia maneno protos na eschatos ambayo yanaashiria wazo
linguine linalotofautiana na maana ya Alfa na Omega.
Ufunuo 1:17 Nami
nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa
kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
Ufunuo 2:8 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.
Maneno ya protos na eschatos yanabeba dhana iliyopo kwenye Ufunuo 3:14 ambapo Kristo
anatajwa kuwa ni mwanzo au chanzo cha
kuumba kwa Mungu akiwa ni prototokos au
mzaliwa wa kwanza kama mtoto wa kiroho. Hatimaye alifanyika kuwa ni mzaliwa wa
pekee wa Mungu aliyenenwa kwenye Yohana 1:18 (akiwa kama theos au elohim au monogene theos).
Utandaji huu
umeongezweka. Atakaporudi Masihi hapa duniani na kwenye mchakato wa mwisho
kwenye tukio la kushuka kwa Mji wa Mungu, tunamuona Masihi akiwa ni Alfa na
Omega. Majinacheo haya hayakutumika kumuita yeye kimsingi, ambavyo ni nia na
mkakati ulio nyuma ya tafsiri potofu na za uwongo.
Kwenye Ufunuo
22:13-16 tunaona majina mawili yakitokana na Masihi kuwa alifanyika kuwa nuru
na nyota ya asubuhi.
Ufunuo 22:13-16 Mimi
ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14
Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na
kuingia mjini kwa milango yake. 15 Huko nje wako mbwa,
na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye
uongo na kuufanya. 16 Mimi Yesu nimemtuma malaika
wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na
Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.
Amepewa majina haya
ya kivyeo kama mtu aliyepewa uweza kutoka kwa Mungu. Akiwa kama protos wa uumbaji anafanika kuwa mmoja
na huyu Alfa. Akiwa kama eschatos wa uumbaji, anafanyika kuwa mmoja
na Omega kama Mungu alivyo yote katika
yote na ndani ya yote (Efe. 4:6).
Ufunuo 21:6 inaonyesha
kiwango wakati tukio hili linapotokea. Kristo anafanyika
kuwa Alfa na Omega na mwanzo na telos. Alianza kama mwanzo au wa kwanza kwenye uumbaji wa Mungu kwa mujibu wa Ufunuo 3:14.
Hapa tuna wa kwanza aliye kama mwanzo
na telos kama mwisho. Neno linalotokea ni la uwingi wa ujumla na
lisilo la kijinsia la gegonan (sawa
na ilivyo kwenye Ufunuo 16 na 17 na kwenye kamusi ya Marshall's Interlinear
RSV). Imetafsiriwa kama imefanyika. Hata
hivyo, ina maana sahihi, na Marshall anaitafsiri kama ni, imekwisha kuwa.
Ufunuo 21:6 Akaniambia,
Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji
ya uzima, bure.
Imekwisha kuwa imetafsiriwa kuwa kama ilikwisha fanyika ili kulipa mashiko wazo la kwamba mchakato huu wa
Mungu kufanyika kuwa yote katika yote na ndani ya yote uanzie kwa Kristo ambayo
hakuwa hivyo hapo mwanzoni.
Kwa hiyo
tunashughulika na wazo endelevu la utendaji wa Masihi na wateule. "Tazama,
nayafanya yote kuwa mapya".
Mungu anafanyika
kuwa yote katika yote. Hivyo basi, Mungu ni Omega au matokeo ya mwisho ya
uumbaji wake mwenyewe. watafsiri wa Kitrinitarian walioitafsiri bilbia ya KJV kwa
makusudi kabisa wameuficha ukweli huu na dhana yake nzima kwa wasomaji wake.
Kristo akiwa kama wa Kwanza kwenye mrengo wa
Kitrinitarian
Malumbano nahoja zilizotajwa
hapo juu zinachukuliwa kuwa ndiyo msimamo na kiini cha ujumbe lililopelekewa
Kanisa la Walaodikia. Kwa hiyo, hoja hizi yapasa ziwe chimbuko au chanzo cha
msingi wa makosa kwenye kanisa lile – au kosa kwa kueneza. Unabii unasema
kwamba makosa yapo. Ni makosa la msingi la kanisa la Walaodikia na sababu
ambayo Mungu anasema atalitapika kanisa la Laodikia kutoka kinwani mwake.
Kristo anasema kwamba yeye
alikuwa ni mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
Clement alimchukulia Mungu kuwa ni kama ni mwanzo
pekee wa kweli akizuia wazo la kwamba Kristo awe ni mwanzo wa utendaji kazi
wa Mungu. Hivyo ndivyo ilivyojiri. Watrinitarian hawapendi Kristo awe kwenye
wajibu ule kwa kuwa Kristo ndiye aliye kwenye nafasi ile kwa kuwa ndipo Kristo alikuwa
ndiye kazi ya Mungu zaidi ya Mungu mwenyewe kama ilivyo imani ya Wabinitarian.
Usipokuwa
ni muumini wa imani ya Kibinitarian hutaweza kujenga wazo la Utrinitarian – na
mbegu ya Utatu inarithiwa kwenye imani ya Ubinitarian. Hivyo basi, Ubinitarian
una chembe ya mbegu ya maangamizi wake wenyewe. Kinachoendana mkono kwa mkono
nayo ni mafundisho potofu kuhusu Uhai wa nafsi. Clement hata hivyo, alikuwa ni
mwanateolojia ambaye alikuwa, kwa azima yoyote ile na malengo yote, ni Mnostiki.
Aliamini fundisho hili la uhai wa nafsi na kwamba roho zinapaa kwa viwango au
madaraja saba na kwamba zinakuwa zimetoka na hazishikamani tena na hali ya kuwa
kwenye mwili na kuwa kwenye nosis (Lilla, p. 182). Hivyo, wateule walichukuliwa
kuwa wanapitia kwenye mchakato huu wa kujiwezesha au kujimudu. Kanisa lolote,
linapokuwa la Kitriitarian, litajikita kuyakumbatia mafundisho haya ya Roho
kuwa hai. Hatimaye kabisa, itabidi kuwe na imani ya ulimwengu inayoamini
fundisho hili la roho kuendelea kuishi. Mshuko wa ngazi au madaraja saba
anaouongelea Clement ni imani ya Ushamanism kabisa. Inatokana na imani ya dini
za Kibabeli na ikatoka na kuendelea hadi kwenye Steppes za Urusi kwa tukio la
utawanyiko wa watu kulikotokea baada ya gharika kuu. Ilianzisha imani za
Kishamanism wakati waumini wake walioishika wanakwenda kutoka kiwango kimoja
hadi ya pili kwa kupitia hatua saba kwa ujumla. Zinaweza kuwa ni nyingi kiasi
cha tisa hadi kumi na tatu. Kuna roho ya kimizimu au ya kipepo inayotawala (au
mungu kama wanavyoita wenewe) kila moja yah atua hizo saba hadi utakapo panda hadi
kufikia usawa wa juu zaidi.
Hiki
ndicho alichokuwa anashauri Clement na ndivyo ilivyo kwa maana hasa ya mipando
na dini za siri za Kiplatoniki ilivyo. Na kiki ndicho wanateolojia wa
Kikapadokia walichokuwa wanadhania. Walikuwa wanaunga mkono mipando ya imani za
siri ya madaraja saba. Miungu waliyoipana na iliyowajilia haikuwa ni huyu Mungu
wa kweli. Waliokuwa ni wakimapepo. Na ndiyo imani hiyohiyo inayoendelea kwenye
imani ya kibudha leo. Kwenye sherehe za kusimikwa au kuwekwa wakfu mtu za
Kibudha za hapo kale kulikuwa na koni yenye ujazo sawia ndani yake, pamoja na
yai kwenye levo moja; zote hizi zikiashiria maana ya kuwaita maroho au mizimu
washuke kwa kupitia ngazi hizi ili wawaendee waumini wao. Yeyote Yule kwenye
imani ya Kibudha analazimika kuwa anaaimi imani ya Kishamanism. Wanawaita
mizimu waje wao na wawapagae. Utaratibu wote wa kupandisha mizimu unafanyizwa
na nguvu za mapepo na kwa kuwaita au kuwapandisha hao mizimu. Ni roho nyingine
na tofauti kabisa na Roho Mtakatifu. Na ndiyo maana ni muhimu kuelewa au kujua
kabla hatujamsoma Roho Mtakatifu.
Tofauti
ya vitu kati ya Wakristo, Waplatoni na Wanostiki kuhusu dhana ya uumbaji
inahusu mianzo ni kwamba Wanostiki
waliamini kwamba waanzilishi au archontes walikuwa kwa ujumla wao ni
nguvu ovu waliokuwa chini ya uhakimu wa Jaldabaoth wa umbo duni au dhaifu la
udongo wa duniani (soma kitabu kiitwacho Apochryphon
of John 41:12-14 na gombo liitwalo codex II Krause-Labib, II. 4-5, p. 139;
Lilla, p. 183 and fn. 5). Tofauti ya utendaji kazi umekuwa kwenye karne mbili
za kwanza. Utambulisho wa neno au Logos ilifanywa kama mshirika wa pili wa
Mungu. Clement analiona logos kama ni
mshirika wa Mungu, na sio wa kwanza
pamoja na hekima takatifu, wa kwanza kati ya viumbe walioumbwa na Mungu na
mshauri wake (Lilla, p. 208). Mshauri wa Mungu alikuwa ni hekima kutokana na
Mithali 8:22. Hii inatokana na hali ya kutoyajua majukumu ya Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu alikuwa ni nguvu ya kwanza ya Mungu aliyoitumia Mungu wakati wa
uumbaji. Roho Mtakatifu hakuja baada ya Kristo. Kimsingi anatoka kwa Mungu,
akiwa ni nguvu au uweza wake. Ni kifaa ambacho kwacho Kristo na Malaika wote wanafungamanishwa
na kuwa na ushirika na Mungu. Hoja hii ni ya muhimu sana, hivyo basi hebu isome
ili kuielewa hoja za watu hawa.
Kwa hiyo, mjadala uliotuama
karibu na falsafa unaotafuta kushindana na Maandiko Matakatifu ili kwamba
viumbe wote walioumbwa walikuwa ni washirika
au ousia wa Mungu. Washirika na ousia hawakuwa na majina sawa ya kuadibiwa. Ushirika huu unatokana na neno la Kistoiki; ousia ni neno la Kiplatoniki. Yote yanamaana na asili moja tu.
Waamini Utatu wanatumia washirika kama
wanaotokana na ousia moja. Kwa hiyo wanatumia majina mawili
kumaanisha Mungu kuwa ni kama anajumuisha washirika watatu. Ni muhimu jukua
kuwa watu hawa wanasema wakati wanapoyatumia maneno haya (soma jarida la Matumizi ya Neno Washirika (Na. 230) kwa ufafanuzi kamili wa maneno haya). Malaika ndio wanachukuliwa
kuwa ni washirika wa Mungu kama walivyo mapepo pia. Hivyo Shetani angekuwa
muovu kutoka mwanzo wa kuumbwa kwake kama ilivyoendelezwa hivi karibuni na
wanazuoni kwenye Makanisa ya Mungu. Tumejionea tayari jinsi hilo lisivyo
sahihi. Biblia inasema wazi sana kwamba Shetani alikuwa mkamilifu kutoka wakati
alipoumbwa (Eze. 28:15).
Dhana iliyopo ni kwamba: Kama
ni Mungu tu yupo ndani ya viumbe vyote ni washirika tu wa Mungu, kwa hiyo
Shetani ndiye atakuwa mshirika ambaye hana uhalisia zaidi ya kuwa tu ni
mwelekezaji wa mawazo ya Mungu. Ni sawa tu na ilivyo kuwa malaika pia ni
wanaakisi taswira ya Mungu na hawana uhalisia wa uwepo wao zaidi ya kuwa ni
washirika tu. Uwongo huu umeenea hadi kwenye uwepo wa kimaumbo kwa kupitia
mwendelezo wa falsafa za Uplatoni mamboleo. Umeenea mbali zaidi ya
Utrinitariani wa kihafidhina hadi kwenye Teolojia Mchakato iliyoendelezwa
kutoka kwenye Uplatoni mamboleo. Umekuwa ni msingi wa mfumo wa ibada za nyakati
za mwisho.
Utaratibu
huu wa Teolojia Mchakato ulioendelezwa na Waplatoni mamboleo inaounda
Utrinitarian utakuwa ndiyo mfumo, utakaoijumuisha imani ya Kibudha na dini hizi
zote nyingine na kuijumisha kwenye imani na mfumo wa siku za mwisho.
Inakubalika kwenye Teolojia Huria ya Washinto nay a Wahindu. Ni itikadi
jumuishi na ni chombo cha uharibifu au cha kuliangamizia Kanisa Katoliki, na
sio cha kulikengeushia. Ni chombo ambacho atakitumia Mnyama kumgeuka Mwanamke
Kahaba na kumwangamiza. Kwa kweli sisi tunatazamia kuona dini ya nyakati za mwisho
ikianzishwa. Dini hii inajipenyeza pia ili ianze hata kwenye Makanisa ya Mungu.
Ni kutoka kwenye imani au mfumo huu ambapo yule Mtu wa Kuasi ataibukia. Imani hii
na mfumo wake, utafanikiwa kuwadanganya yamkini hata walio wateule ikiwezekana.
Dhana na imani hii ni ya
udanyanyifu na uwongo mtupu na imeingia kwenye Makanisa ya Mungu katia siku
hizi za mwisho kama alivyosema Kristo. Kristo alitoa ufafanuzi kuonyesha kwamba
alikuwa ni mwanzo au wa kwanza kwenye
uumbaji wa Mungu. Clement alikuwa sahihi kusema kwamba Mungu alikuwa mwanzo halisi kwa maana kwamba aliumba
kutokana na utashi wake na kwa mapenzi yake vitu vyote viliumbwa (Ufu. 4:11). Kwa
hiyo, Mungu ndiye muumba ila Kristo alikuwa ni chombo tu cha kuumbia na alikuwa
ni mwanzo (soma tena hapo juu).
Wazo
la kwamba hekima mtakatifu wa kimungu ndiye mshauri wa Mungu na wa kwanza kati
ya viumbe walioumbwa na Mungu ni, kwa mujibu wa Lilla, kwa tabia ya falsafa ya
Wayahudi wenye asili ya Alexandria ya
siku za kabla ya Philo. Kwa hiyo Wayahudi wa Alexandria walielewa kwamba hekima
alikuwa ndiye wa kwanza kati ya viumbe wote wa Mungu. Kwa hiyo anatangulia
kutoka kwa Mungu, na Neno wa Mungu na kisha akaishi na kujumuika pamoja na
Mungu, kwa hekima akiwa kama Roho Mtakatifu. Yeye ni yule Sophia aliyenenwa kwenye Mhubiri 1:4 na ni kiumbe wa kwanza kuumbwa
aliyenenwa kwenye Mithali 8:22. Kitabu cha Hekima ya Sulemani 9:9 inaonyesha
kuwa anamsaidia Mungu kwenye uumbaji. Kitabu cha Mwanzo kinamtaja kuwa ni Roho
ya Mungu kwenye Mwanzo 1:2. Waandishi waliokuwa kipindi cha kabla ya Kristo
walifafanua kimakosa kitu hiki ambacho ni uweza
wa Mungu kuwa ni kiumbe na kosa hili limeendelea hadi siku hizi kama dhana
kwamba Roho Mtakatifu ni nafsi au mtu. Huu ndiyo mwanzo wa upotofu r.
Kimsingi, Roho ni mwanzo wa
uumbaji wa kwanza ya Mungu, kwa kuwa uzao wa Kristo na wa elohim wngine
walifanya hii iwe na mashiko muhimu kwa hizi kuwa mahali pa kitendea kazi tu
kwa uadilifu wake kwa Mungu ili kwamba kuweze kuwa na mwonekano halisi wa imani
ya Mungu mmoja kama muunganiko mzima. Mungu ni kiini cha viumbe wote. Viumbe
wote pamoja na Malaika ni mali yake na wanaungana naye kwa njia ya Roho
Mtakatifu. Ni kwa kupitia huyo Roho ndipo asili ya Mungu na tabia zake
zinawaambukia viumbe wote, wote wawili, yaani Kristo na wateule wengine
waliobakia, na hatimaye wanadamu wote. Yeye ni kitendea kazi tu na usipoelewa
mtiririko huo kwa kweli huwezi kuelewa kinachotokea kwa Roho Mtakatifu.. Inatokea
kwa kuwa sheria ya Mungu inatokana na uwepo wa wema wa tabia ya Mungu. Kwa hiyo,
hawezi kuwa wa Kibinitarian kwa kuwa ana kiini au asili halisi ya wema, na wema
huo ni Mungu. Kristo alisema kwamba ni Mungu tu ndiye aliye mwema; kwanini unaniita mwema, ni Mungu tu ndiye
aliye mwema kwa sababu ya ukweli wa asili yake ya kijadi ya wema usio na
kifani. Hatuwezi kuwa na mfumo au imani ya kiditheist. system. Ukifikiri kwa
kina, na kwa mashiko, kunatuambia kuwa hawezi kuwa hivyo. Torati au sheria ya
Mungu inatokana na tabia ya Mungu inayosimama milele, kama alivyo Mungu
mwenyewe habadiliki, akiwa ni mwema kabisa akiwa kama kiini cha wema wote.
q