Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[244]
Mwanzo 22, Imani ya Kiyahudi, Uislamu na Sadaka ya Isaka
(Toleo
La 3.0 19980407-20000425-20110504)
Andiko la jarida hili linaelezea mabishano yaliyopo kuhusiana na sadaka
iliyotolewa ya Isaka yaliyoendelezwa na Rabi E. Ben-Yehuda na pia imefanyiwa
tathminiwa kwa kujibu sawa na ilivyoandikwa kwenye Biblia na Qur’an au Koran.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki ©
1998,
2000 Thomas McElwain, ed. Wade Cox)
(rev. 2011)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na
kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au
kufuta maneno. Jina la
mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe
pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote
atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja
ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Mwanzo 22, Imani
ya Kiyahudi, Uislamu na Sadaka ya Isaka
Kwenye Taasisi ya
Watafiti wa Ukristo wa Kiyahudi, Toleo la 1, la Novemba 1986, Rabi E.
Ben-Yehuda alichapisha jarida lene kichwa cha habari Sadaka ya Isaka [The Sacrifice of Isaac].
Mwandishi ametoa
dhumuni moja tu lililoelezewa kwa kuelezea jambo hili.akisema. “Mjibu au miitikio yote ya Kiyahudi
yametokana kipindi kifupi kabla ya Wakristo kudai kwamba upotovu au makosa
makubwa ya kitoaji dhabihu wa Yesu Kristo pale msalabani umeifanya kuonyesha
umuhimu wa dhahiri kwa Wayahudi wote kukubaliana na jukumu hili la Masihi pamoja
na hadhi yake ya kimbinguni. Ubatilishaji uliofuatia unajaribu kuonyesha kuwa Wayahudi
walikuwa na nasibu kwenye historia yao muda mrefu kabla ya kuanza kuhesabu kipindi
ch Mateso ambayo yalikuwa na matokeo sawa kwa mtazamo wa Wayahudi” (ukurasa
1). Ushawishi pekee ulioelezewa ni “kuja kwenye kuling’ang’ania au
kulishikilia” jambo hili.
Kitendo cha
kuondoka ni wazo la kwamba kuna udhaifu kwenye imani ya kiyahudi iwapo kama kusingekuwa
na utoaji wa dhambihu kwa ajili ya dhambi ambayo kwayo Mungu huitumia
kuwarehemia watu. “Kwa kuwa sadaka
haitolewi tena kwenye imani ya Kiyahudi, ni wapi utakapotarajia tena kukutana
na rehema za Mungu?” (ukurasa wa 2). Marabi wamekuta msingi uliachwa na
kupungua wa neema mahali alipokuwa amefungiwa Isaka. “Kwenye liturjia, tunaelezea tena na tena kuhusu “kufungwa kamba kwa
Isaka” kama sababu ya Mungu ili kusamehe kwa mara moja dhambi za wana
waliotokana na uzao wa Isaka” (ukurasa wa 2).
Baada ya
kujitambulisha kwao, rabi wlikuta ushahidi ufuatao wa kwmba Isaka alitolewa
sadaka kweli kama ilivyoelezwa kwenye Mwanzo 22, na kisha hatimaye alifufuka
kutoka kwa wafu. Inaleta mwaswali kwamba Mungu mwenye sifa ya kujua kila jambo
lililopita, lililoko na lijalo angehitaji “kumjaribu” Ibrahimu. Alama aminika za N-S badala ya N-S-H ni
neno lililotumika kwa kweli. Kwa hiyo tafsiri iliyotumiwa ya “kujaribu” ni
kutolielewa andiko. Ingepaswa zaidi iwe “tangazo” au “mfano” badala ya
“kujaribu” (ukurasa wa 2). Kwa nini kitendi hiki cha kufungwa tu kwa Isaka kiwe
ni tukio lililoleta gumzo kubwa duniani kama liturjia ya kiyahudi inavyoonyesha?
(ukurasa wa 2).
“Kitabu cha fafanuzi n fasiri cha Kiyahudi kinasema
‘Mungu mwenyewe aliiamuru iwepo hii sadaka ya Isaka – lakini kama Ibrahimu
angemruhusu mataika yeyote ashindane na Muumba wake?’” “Ufafanuzi unaelezea
kwamba, ‘malaika alisema akmwambia Ibrahimu na Ibrahimu akkataa kusimama,
alisem kuwa Mungu amemuamuru, na ni yeye tu ndiye anayeweza kunizuia mimi” (ukurasa wa 2). Amri iliyotolewa ya
kutomdhuru au kumchinja Isaka ilimaanisha kwamba alipaswa kutolewa sadaka yote
mzima na pasipo kuumizwa (ukurasa wa 3). Maneno haya yanaweza kutafsiriwa kama ‘kondoo
mwingine’ au ‘kondoo atafutwaye’ (ukurasa wa 3). Tahat bno linamaana ya chini ya mwanae kuliko maana
ya mwanae (ukurasa wa 3). “Kitu hiki” na “hukumuachilia mtoto wako” kwenye
Mwanzo 22:15-17 linaashiria kuwa Isaka alitolewa sadaka (ukurasa wa 3). Andiko
linaarifu kwamba wote wawili, yaani Isaka walipanda kwenda, lakini ni Ibrahimu
peke yake ndiye aliyerejea (ukurasa wa 3). Abraham alikwenda moja kwa moja huko
Be’rsheba. Mwanzo 23:2 linaripoti kuwa Sara alifariki huko Kirjath-arba. Kwa hiyo
Ibrahimu hakuonana uso kwa uso na Sara baada ya sadaka hii ya Isaka, na Sara alifariki
kwa huzuni baada ya kusikia kuwa Isaka alikuwa amefariki (ukurasa wa 3).
Mwanzo 23:2 inaripoti
kuwa Ibrahimu “alikuja” kuomboleza kifo cha Sara, lakini hakuna taarifa
iliyofanywa kuhusu Isaka (ukurasa wa 3). Mwanzo 24 inaeleza kuhusu alivyompatia
mke “Isaka”, ambavyo kwamba, Ibrahimu alikiinua kizazi kwenye jina la Isaka. Hakuna
msisitizo kuhusu Isaka, lakini Rebeka anaulizwa kama angeafiki. Rebeka alistushwa
kumkuta Isaka akiwa hai kwa hiyo alijiinamisha kwenye ngamia wake na kujifunika
uso wake (ukurasa wa 3). Isaka akaja kutoka kwenye njia inayoelekea kisimani lahay roi’, kisima cha Uhai cha Yeye
anionaye, ambalo ni jina la yeye kuwa amefufuka (ukurasa wa 4). Utajaji kuhusu
ufufuko kwenye maombi ya Kiyahudi yaliyo katika siku hizi (ukurasa wa 4). Isaka
alifarijiwa baada ya kifo cha mama yake kwa kumuoa kwake Rebeka miaka mitatu
baada ya tukio hili, akionyesha kwamba alikuwa amejifunza tu jambo hili wakati
alipofufuka (ukurasa wa 4). Matendo ya Kiyahudi ya Kidush Hashem yanatuama
kwenye kifo na ufufuko wa Isaka (ukurasa wa 4).
Kila moja kati ya
malumbano haya yamefafanuliwa kwa utaratibu.
Inashangaza na ni
jambo la kujiuliza kwamba Mungu mwenye sifa za kujua kila kitu ahitaji
“kumjaribu” Ibrahimu. Inadaiwa na wenye imani kali kuwa kwa kweli lilitumika
neno N-S badala ya N-S-H. kwa hiyo, tafsiri ya neno “kujaribu” ni matokeo ya kutolielewa
andiko. Ingekuwa kwa zaidi mna tu ya jinsi ya ”bango” au “mfano”, badala ya
“jaribu” (ukurasa wa 2).
Viambishi hivi N-S-H
imetumika takribam mara 36 kwenye Maandiko Matakatifu ya Kiebrania karibu
wakati wote kwa namna iyiyo wazi inayomaanisha “kutia majaribuni”. Mifano yake
ipo kama kwenye Kutoka 15:25; 1Samweli 17:39 na 1Wafalme 10:1. Mwanzo 22:1 haionekani
kuondoka kwenye matumizi haya ya wazi. Hata hivyo, kama neno jaribu kwa kweli
likiwa linamaanisha kuwa Mungu “alifanya mfano” wa Ibrahimu, zaidi ya kuwa
“alimtia majaribuni”, matokeo yake hayawezi kuwa ni kama alionekana kabisa kuwa
ni mtoto wa kambo tafsiri yoyote ijulikanayo ya kutolewa sadaka kwa Isaka.
Haiashirii kuwa Isaka kwa hiyo alitolewa sadaka kwa kweli zaidi ya kuwa
alifungwa tu madhabahuni.
Kwanini kitendo hiki
cha kufungwa tu kwa Isaka kiwe ni tukio linalotiliwa umuhimu mkubwa kama
liturjia ya Kiyahudi inavyotaka? (ukurasa wa 2).
Kama kuna maelezo
endelevu kwenye ufungaji kamba wa Isaka kwenye machapisho ya Kiyahudi, hii
haisaidii kwa kuzipa mashiko nukuu znisemazo there is a continual reference to
the binding of Isakwamba uzoefu wa Isaka ulikuwa na maana kubwa kwenye imani ya
Kiyahudi. Haifuatii kwamba Isaka kwamba kwa hakika Isaka alitolewa sadaka. Na
hata hivyo haifuatiwi kuwa imani ya kwamba Isaka alitolewa sadaka haikuenea
kabisa kwenye imani ya Kiyahudi. Maelezo ya kiliturjia yalinukuu maneno “kufungwa
kamba”, na sio sadaka yenyewe. Na kwa hiyo inaeleza mambo yaliyo kinyume na
mtazamo wa rabi huyu.
“Kitabu cha fafanuzi cha Wayahudi kinasema ‘Mungu
mwenyewe ndiye aliamuru kutolewa sadaka kwa Isaka – lakini je, Ibrahimu
angemruhusu malaika kupingana na Muumba wake?” “Kitabu hiki cha fafanuzi
kinaendelea kufafanua, ‘malaika alimwambia Ibrahimu na Ibrahimu alikataa
kusimamisha mchakato, akisema kuwa Mungu ameniamuru, ni yeye tu ndiye mwenye
uwezo wa kunisimamisha mimi nisifanye hivi.’” (ukurasa wa 2).
Malumbano
yametuam kwenye mgongano kati ya jumbe za Mungu, Elohim kwenye Mwanzo 22:1-2 na
ule wa malaika wa Bwana ulio kwenye Mwanzo 22:11-12. Kinachoonekana ni kwamba
Ibrahimu alipokea hayo yote kama amri mbili zinazopingana, zikitokea kutoka
kwenye vyanzo viwili tofauti, na akaamua kumtii Mungu na Elohim wake kama ndiye
mwenye mamlaka kuu zaidi kuliko malaika wa Bwana.
Tatizo lililopo
kwene tafsiri hii ni kwamba hakuna kitangulizi kingine kwenye Maandiko Matakatifu
ya Kiyahudi kuonesha kwamba malaika huyu wa Bwana alipingana na Mungu. Kwa
kweli, malaika wa Bwana alikuwa ni mwakilishi wa karibu wa YHVH ambaye wakati
mwingine hunena akiwa kama nafsi ya kwanza, Mimi YHVH, kama ilivyo kwenye
Mwanzo 18 ambapo viumbe watakatifu hawakuw wanaitwa malaika kabisa, ila ni
wanadamu na YHVH, waliokuwa wanatenda mambo na kuenenda kama wanadamu. Shauri
hili lingeweza kufanyika, ni kama kwenye Mwanzo 18 na Mwanzo 22:12, ambako YHVH
alinena maneno kumuelezea kama malaika wa Bwana (YHVH). Kwenye Mwanzo 19 watu hawahawa
wanaendelea kuitwa malaika.
Mwanzo 22:12 inaweka
makubaliano kati ya Mungu, Elohim na mlaika wa Bwana. Inasema kwa kuwa najua
kwamba unamtii na mumcha sana Mungu. Kiidadi, andiko hili halisaidii kuonyesha
mgongano kati ya Mungu na malaika wa Bwana (soma majarida ya Malaika wa YHVH (Na. 24); Wateule Kamas Elohim (Na. 1) na Uwepo wa Yesu Kristo Kipindi cha Kabla ya Kuzaliwa Kwake
Kimwili (Na. 243)).
Amri iliyotolewa
kuwa asimdhuru Isaka ilimaanisha kwamba alitakiwa atolewe sadaka akiwa mzima na
asiumizwe (ukurasa wa 3).
Hoja hizi
zinakubaliana na makubaliano yaliyopo kati ya malaika wa Bwana na Mungu. Maneno
ya malaika kwa tafsiri hii hayakatazi kutolewa sadaka kwa Isaka, lakini zaidi
ni kwamba yanakataza asimuumize Isaka anapomtoa sadaka. Umuhimu wa maneno kwa
hiyo yangekuwa kwamba Isaka alitakiwa awe kwenye hali kamilifu wakati anapotolewa
sadaka.
Kwa kuwa hoja hii
inapingana na hoja ya tatu, tafsiri moja au nyingine yapasa ichaguliwe. Zote
mbili hazikubaliki. Kama tutakubali uwezekano wote wa aina mbili wa nusu ya kwaza
ya aya ya 12, nusu ya pili inayofuatia itaweka sawa kile ambacho hakipo.
Kutokana na hoja ya nne, maana ya andiko yangeweza kusomeka hivi: “Usimchinje Isaka, kwa kuwa sadaka inatakiwa
isiwe na waa: kwa hiyo sasa najua ya kuwa unamcha na kumtii sana Mungu, kwa
kuwa hukumzuia mwana wako wa pekee, mwana wako wa pekee uliyempata kutoka
kwangu.” Hakuna muunganiko wenye mashiko kati ya aya ya kwanza na nusu ya
pili ya ayah ii. Kwa mujibu wa tafsiri za kimapokeo, maana au nia ya ayah ii ingesomeka
hivi: “Usimdhuru Isaka au kumtoa sadaka
kwenye mashindano: kwakuwa sasa naona kuwa unamcha na kumtii Mungu, kwa kuwa
hukumzuilia mwana wako, mwanao wa pekee kunitolea mimi.” Kwenye jambo hili,
andiko linaambatana au linaendana. Nusu ya kwanza inaingilia utoaji wa sadaka,
na nusu ya pili inaashiria kwamba jaribio limeisha, kwa kuwa Ibrahimu
hakumkatazia mwanae (sawa na jarida la Malaika na Sadaka ya Ibrahimu (Na. 71)).
Maneno yanaweza
kutafsiriwa kama “kondoo mume mwingine” (ukurasa wa 3). Ishirio ni kwamba
kondoo mume ni sadaka ya nyongeza kwenye sadaka ya Isaka, kwa kuwa ni
“nyingine” au “baada”. Biblia ya KJV inatafsiri “nyuma yake” pamoja na matamshi
ya maandiko mlalo, kuonyesha kuwa imeongezewa. Tafsiri hii ya KJV imeliacha
neno lote, ikisema “pale kichakani alimuona kondoo mume aliyenasa kwenye pembe
zake.”
Kwa mtazamo huu
rabi yuko sahihi. Uelewa mwngi wa mashiko ya kiliturjia ya maneno haya ni
kondoo mume mwingine; ni sahihi pia kwamba Isaka ni mtu pekee ambaye ngekuwa ni
kondoo mume wa kwanza, kwa kuwa ilikwisha wekwa wazi kwamba hakuna mnyama
mwingine aliyetolewa kwenye Mwanzo 22:7. Haifuati, hata hivyo, kwamba Isaka kwa
hiyo alitoewa sadaka. Inafuatia tu kuwa alikuwa ni kondoo mume ndiye
aliyetakiwa kutolewa sadaka. Kondoo aliyekamatwa kichakani alikuwa ni sadaka
nyingine.
Neno Tahat bno maana yake ni “chini” ya
mwanae kuliko kuwa “badala ya” mwanae (ukurasa wa 3).
Ni kweli kwamba
neno tahat maana yake ni chini.
Limetumika kama hivyo kwenye Mwanzo 1:7. Hata hivyo, neno hili linamaanisha pia
badala ya, kama lilivyotumika kweye
Mwanzo 2:21 “Bkisha akatwaa ubavu
wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,”. Ingekuwa hakuna maana
kutafsiri chini kwa maelezo haya. Neno limetumika badala ya kwenye Mwanzo 4:25; 30:15; Mambo
ya Walawi 14:42; 2Samweli 19:14. Imetumika kama chini kwenye Mwanzo 7:19; Kutoka 32:19; na inawezekana sana kwenye 1Nyakati
29:34. Limetumika kwa maana ya kwa ajili
yake kwenye Kutoka 21:26. Limetumika kwa
matumizi ya kwenye Zaburi 66:17. Limetumika wakati kwamba kwenye Isaya 60:15. Hatimaye kabisa, limejumuisha na
sehemu nyingine nyingi kwa matumizi mengine kwenye kitabi cha Yeremia. Tofauti
kubwa ya maana ya neno, na ukweli kwamba limetumika kwa maana haya ya chini
kwenye uchache wa matukio ya kibiblia, inaelezewa kinyume na mtazamo na fikra
ya rabi. Hatimaye, dhana ya “chini” haina mashiko yoyote kabisa. Kama kondoo
huyu alitolewa sadaka chini ya Isaka, basi angewekwaje pale, kwa karidi kwamba
Isaka alikuwa alikuwa amekwisha fungwa kamba tayari pale madhabahuni? Na kama
huyu kondoo alikuwa ametolewa dhabihu chini ya Isaka, ndipo itaonekana kuwa
huyu kondoo sio wa mbadala/mwingine/wa pili, bali ni wa kwanza. Tafsiri ya
kwamba ni badala yake ni tafsiri
pekee ambayo inafanya kuwe na mitizamo inayopingana.
“Kitu hiki” na “hukumzuia
mwanao” kwenye Mwanzo 22:15-17 vinaashiria kwamba Isaka alitolewa sadaka (ukurasa
wa 3).
Rabi anaelezea maelezo
yaliyo kwenye Mwanzo 22:16 hukumzuilia
mwanao kuonyesha kuwa Isaka alitolewa sadaka. Maelezo hayohayo yasemayo, loo chasakhtaa eth binkhaa, yanakutikana
kwenye Mwanzo 22:12. Kwenye Mwanzo 22:12 Ibrahimu ni wazi kabisa kwamba alikuwa
hajamtoa sadaka Isaka, na lakini alikuwa amekwishatimiza tayari kila
kilichotakiwa asikizuilie. Kwa kuwa maelezo haya kwa wazi kabisa hayaelezi kuwa
alichukua sadaka ya kuteketezwa kwenye Mwanzo 22:12, basi hakuwa sababu
kudhania kuwa inaelezea kuwa ilichukuliwa na kuletwa sadaka ya kuteketezwa
kwenye Mwanzo 22:16.
Andiko linaripoti
tu kwamba wote wawili, Ibrahimu na Isaka walikwenda kwenye Mwanzo 22:8, lakini
ni kwamba Ibrahimu tu ndiye alitudi nyumbani kwenye Mwanzo 22:19 (ukurasa wa
3).
Ripoti ya rabi kuhusu
andiko ni ya hakika. Ukweli, hta hivyo, ni kwamba, wote wawili wametajwa kwenye
safari yao ya kurudi nyumbani, haimaanishi kuwa Isaka hakurudi. Kwenye Mwanzo 12:14
inasema kuwa Abramu alipanda kwenda Misri. Haisemi kuwa Sarai alikwenda pamoja
naye. Kwa kweli, aya zinazotangulia zinaonyesha kuwa Abramu aliogopa kumchukua
mke wake kwendanaye Misri. Kwa kutumia
utaratibu wa rabi huyu wa kutafsiri, tungeweza kuona kutokana na hili kwamba kwenye wakati wake wa mwisho
waliamua kuwa asiende, badala ya kuongopa kuhusu uhusiano wao. Lakini licha ya
ukweli kwamba andiko hili linasema tu kuwa Abramu alikwenda Misri, lo, na sasa
tazama, aya hiyohiyo inaendelea kwa kusema “Wamisri wakamuona kuwa mwanamke
uule alikuwa ni mzuri sana”. Kama isingekuwa ile aya ya kumi na saba, ambako
jina la Sara limetajwa, tungehitimisha hat kwa kwa kutumia mtindo wa rabi wa
kutafsiri, kwamba Abramu alikuwa na mke mwingine wa kujishikizia aliyekwenda
nye Misri.
Mwanzo 22:19 inahitimisha
kwamba walikwenda pamoj hadi Beer Sheba. Ingawaje wavulana wanatajwa pia, tuna
haki zaidi ya kuhitimisha kwamba Isaka alifuatana nao kama tunavyohitimisha
kwamba Sarai alishukia kwenda huko Misri kwenye Mwadzo 12.
Ibrahimu alikwenda
moja kwa moja hadi Be’re Sheva. Mwanzo 23:2 inatuambia kuwa Sara alifariki
akiwa huko Kirjath-arba. Kwa hiyo Ibrahimu asingeweza kumuona Sara baada ya
kumtoa dhabihu Isaka, na alikufa kwa huzuni na kihoro aliposikia kuwa Isaka ameuliwa
(ukurasa wa 3).
Rabi huyu
anadhani kuwa Ibrahimu alikwenda Beer Sheba badala ya kurudi kwa Sana. Lakini
Mwanzo 21:33, ni aya mbili tu kabla ya ile amri ngumu iliyotolewa ya kumtoa
sadaka Isaka, aliyombiwa Ibrahimu alipokuwa bado yungali aliishi huko Beer
Sheba. Ingawa andiko halisemi hivyo, isingeweza kwa kiasi kikubwa kudhania kuwa
mke wake Sara alikuwa anaishi kule na yeye. Mwanzo 21:34 inaashiria kuwa
Ibrahimu aliishi huko Beer Sheba kwa kipindi kirefu. neno hili ‘siku nyingi’
halina mkanunisho kama ulivyo kwenye lugha ya Kiingereza la majuma machache tu.
Ni sawasawa na maelezo yasemavyo kwenye Zaburi 23:6, ilitafsiri kwa ilivyo kwenye
zote mbili, yaani biblia za KJV na NIV kama milele. Kuna kikomo kwenye
maelekezo yaliyo kwenye Mwanzo 22:1, kwa hiyo inawezekana kudhania kwamba
Ibrahimu alikuwa anaishi kwenye kipindi cha sehemu zilizojulikan. Lakini ukweli
kuwa Mwanzo 22:19 inasema kuwa alikwenda Beer Sheba inadhaniwa kwa kiwasi kikubwa
alianza nje kutoka pale, na kwamba Sara alikuwa anamngojea pale, isipokuwa kwa
kweli alikuwa anamngojea akiwa na vijana wa kiume. Andiko halimtaji tu Sara
kabisa, na udadisi na mtazamo wa rabi huyu, kama tutakavyojione, kuwa
ingemaanisha kabisa kuwa alikuwa amekwisha kufa, na kufufuka na kuf tena kwenye
Mwanzo 23.
Njia bora ya
kulielewa andiko ni kudhania kwamba Ibrahimu na Sara walikuwa wanaishi huko Beer
Sheba kwa karibu kipindi cha kufungwa kwa Mwanzo 22:19. Kuna kikomo kingine
kwenye maelezo ya Mwanzo 22:20, ambapo panaendelea hadi mwanzoni mwa Mwanzo 23.
Kwa hiyo, hakuna sababu ya kimaandiko ya kudhania kuwa Ibrahimu alikuwa
anamkwepa Sara.
Mwanzo 23:2 inaripoti
kuwa Ibrahimu “alikuja” kumuombolezea Sara, lakini hakuna kitu kinachoelezea
kuhusu Isaka (ukurasa wa 3).
Rabi huyu
anadhani kwamba Isaka inawezekana kabisa alikuwa amekwisha kufa kwa kuwa
haelezewi kaisa kuwa alikuwepo kwenye mazishi ya mama yake Sara. Tena hitimisho
kama hilo kutokana na kile ambacho andiko halisemi hakithibitiki, kama
tulivyokwisha kujionea tayari. Ni wazi kwamba Sara alishuka kwenda Misri,
ingawaje andiko linasema tu kuwa ni Ibrahimu ndiye aliyeshuka kwenda huko. Ni
wazi sana kwamba Sara alikuwa yungali hai bado kipindi hiki kilichoelezewa
kwenye Mwanzo 22, ingawaje halisemi kuwa alikuwepo kwenye shughuli hii muhimu
iliyo kwenye kifungu hiki cha kutolewa sadaka kwa mwanawe Isaaka. Ni wazi pia
kwamba kutoka kwene andiko kwamba Isaka alikuwa yu mzima wakati alipofariki
mama yake. Alikuwa angali hai bado kwenye Mwanzo 22:12 na Mwanzo 24:6.
Mwanzo 24 inaelezea
kuhusu alivyopewa mke “Isaka”, ili kwamba Ibrahimu ajipatie uzao kutokana na
jina la Isaka. Hakukuwa na la kumuuliza Isaka, ila Rebeka aliulizwa kama
anakubaliana. Rebeka alishangazwa kukuta kuwa Isaka alikuwa mzima, ndipo
alijiinamisha juu ya ngamia wake na kujifunika uso wake (ukurasa wa 3).
Wazo la kwanza la
huyu rabi ni kwamba Ibrahimu alimuokoa Isaka, ambaye alikuwa amekufa, kwa
kuipanda tena mbegu kwa kumpa Isaka mke. Hoja hii imekosa mashiko kwa ukweli
kwamba kwenye Mwanzo 24:6 Ibrahimu anaamuru watumishi wake wasimchukue mtoto wake
na kumrudisha kwenye nchi ya uzaliwa wake. Maana ya tendo hili iko wazi sana
kwamba Isaka alikuwa mzima na kwamba Yule mke alikuwa ni kwa ajili yake
mwenyewe kabisa.
Sababu y pili ya huyu
rabi ni kwamba kwakuwa haoinyeshi kuwa Isaka alishauriwa au kushirikishwa,
wakati mawazo na ushauri wa Rebeka unaonekana ulifanyika kwa karibu sana. Kwa
hiyo anaamini kuwa Isaka alikuwa amekwisha kufa. Hata hivyo, hakuna sababu ya
kuelezea kuhusu ushirikishwaji wa Isaka, kwa kadiri tunavyoona ni salama zaidi
kudhania kuwa akipofikia umri wa utu uzima wa miaka arobaini alikuwa yu tayari
sana kuoa. Ushirikishwaji wake unatakiwa uelezwe tu kwa mambo yaliyo kinyume.
Kuulizwa kiukaribu kwa mawazo na ushauri wa Rebeka hakupingani na kitendo cha
maandalizi ya ndoa au kwa utaratibu wa viwango vya ufungaji ndoa wa eneo la
Mashariki ya Kati. Kudhania kuwa ni kinyume ni tabia tu ya ubaguzi wa
Kimagharibi.
Sababu ya tatu ya
huyu rabi ni kuwa kitendo cha Rebeka cha
kuinamia kwenye ngamia na kujifunika shela kinaashiria mshangao wake kumuona
Isaka amefufuka. Mwanzo 24:64 inasema kuwa alishuka kutoka mgongoni mwa ngamia.
Shina la neno hili ni N-P-L ambalo kwa kweli ni lilitumika kwa kawaida
likimaanisha kushuka chini kutoka mlimani au kutoka kwenye gari, hata hivyo.
Limetumika sana kama hivyo kwenye 2Wafalme 5:21 pamoja na kwenye Mwanzo 24:64.
Tafsiri ya huyu rabi huenda rni wa maana ya kiliturjia ambao sio wa lazima.
Kitendo cha mwanamke kushuka kutoka mgongoni mwa ngamia, ambapo ni juu sana
kuliko mgongo wa farasi, kungelazimu zaidi sana kuliko kumsaidia tu kumvua
shela yake. Kwenye maeneo ya nchi za Mashariki ya Kati leo bado kuna utamaduni
huu wa mwanamke kushuka kutoka kutoka mlimani juu kama atakutana na mwanaume
anamjongelea akija kwake barabarani. Hakuna mashiko yoyote kuamini kuwa Rebeka
alifanya hivyo kwa ajili ya kushangaa. Katika nchi ile, tabia yake ile ilikuwa
ni ya kawaida, ambayo inaelezea au kuonyesha kinyume sana na matokeo ya msituko
au mshangao.
Isaka alitokea
kwenye njia ya kisima cha lahay roi’,
kisima ch Uzima way eye anionaye, ambalo ni neno linaloashiria kuwa alikuwa
amefufuka (ukurasa wa 4).
Rabi alitafsiri
kitendo cha Isaka kuja akitokea kwenye njia ile ya kisima cha lahay roi’ kama ushahidi wa kuwa yeye
alikuwa amefufuka. Hata hivyo, maneno haya hayana maana hii ya kiulinganisho
kwenye maandiko haya. Yanaelezea kuwa ni kisima tu cha kawaida cha maji ambacho
kiliipewa jina hilo na Hajiri kwenye Mwanzo 16:13-14. Maana isemayo Mungu aonaye imetokana na matatizo
aliyokutananayo Hajiri, na sio Isaka. Halina maana ndogo kwa kumaanisha
kufufuka kwa Isaka.
Kutajwa kwa
ufufuo kwene maombi ya Wayahudi bado kunaendelea hadi sasa (ukurasa wa 4).
Rabi huyu
anahitimisha kuwa kutajwa kwake kwenye maombi ya Wayahudi wakimuombapo Mungu
awafufue wafu, kwa kuwa yalikuwa yanafundishwa hata leo, kwa namna yoyote
inavyomaanisha kutokana na hiyo, kwa kuwa hakuna kitenzi kiashiriacho tendo
kufanyika kila siku kwenye lugha ya Kiebrania, kunamaanisha kuwa Mungu bado
yupo hata sasa akiwafufua wafu. Kwa kuwa Mungu bado yupo hata sasa akiwa ni
mfufuaji wa wafu, basi angeweza pia kumfufua Isaka. Kama tunakubaliana na hoja
za rabi, kwamba Mungu tayari yupo hata sasa akiwa ni mfufua watu kutoka kwa
wafu, basi haiashirii kuwa Isaka ni miongoni mwa hao waliofufuliwa. Kuna jinsi
inavyotejwa kwenye biblia kwa watu wengine waliowahi kufufuliwa kwa wafu, kama
lile tukio la mtoto wa mjane wakati wa Eliya (1Wafalme 17:17 nk.), na mtoto wa
mwanamke Mshunami wakati wa Elisha (2Wafalme 4:8ff.).
Ingawa maombi ya
Wayahudi yanaashiria kitu fulani muhimu kwene maisha ya Wayahudi, ambalo ndilo
lilikwa kusudi la mafundisho ya rabi sehemu ya kwanza, hawawezi kutoa ushahidi wa
kwamba andiko hili la Mwanzo linaripoti au haliripoti kwa kweli dhana hii ya
kufufuka kwake au kama haisaidii. Isaka alifarijika baada ya kifo cha mama yake
kutokana na kuoa kwake mwanamke huyu Rebeka miaka mitatu baada ya tukio,
ikionyesha kuwa alikuwa amejifunza kwa uhakika jambi hili wakati akiwa
amefufuka (uurasa wa 4).
Haifuati. Inawezekana
kabisa kwamba yawezekana kuwa Isaka alimuombolezea mama yake kwa kipindi cha takriban
miaka mitatu, kwa kiasi kwamba ndoa yake ilimfariji sana. Hakuna ushahidi wa
kifo cha Isaka na kufufuka kwake hapa.
Imani ya Wayahudi
ya Kidush Hashem yanatokana na kifo na kufufuka kwa Isaka (ukurasa wa 4).
Ingawa imani
kwenye kifo na kufufuka kwa Isaka inaweza kuwa na athari ya ushawishi kwa
baadhi ya Wayahudi ili kuwafanya wawe waaminifu kwenye imani yao ya kuifia
dini, imani ile ni ya muhimu sana kwenye uaminifu kama huo. Uamifu kama huo sio
ushahidi ama kwenye imani ya kifo.na ufufuo wa Isaka au kwa ukweli wa tukio
lenyewe.
Kwa hoja hii
inawezekana kufanya tathmini ya jumla ya somo. Tatizo la kwanza ni nia ya rabi
na hoja zake. Nia yake inakuwa imepotoshwa, kwa hiyo matokeo yake hayawezi kusaidia
ila imekuwa imepotoshwa. Nia sahihi pekee kwa kujisomea andiko ni kujitafuti
ukweli, ukweli wa kile kilichomaanishwa hapo mwanzoni na maandiko na jinsi inavyoweza
kusaidia kwenye imani ya mtu binafsi na uzoefu wake. Rabi huyu hapendi kutafuta
ukweli, lakini kwa maneno yake mwenyewe, anapendezwa na hamu ya kupata utenzi wa
Wakristo kwenye imani ya \Kiyahudi. Anataka kukuta mbadala wa bandia wa kifo
cha Yesu mtini kama njia ya neema ya mbinguni. Kwa nia hii moyoni, anakomelea kwenye
sadaka ya Isaka.
Hoja yake
imebakia bila kuonekana. Hoja ni kwamba kumuamini mtu aliyeuawa shahidi au
kufufuka kutafanya kwa yenyewe tu isiwekane kwa Mungu kusamehe dhambi. Ingawa
hoja hii inakubalika na imani za Kikristo, mwanazuoni wa Kiyahudi anawajibu wa
kuonyesha uwepo wake. Rabi hafanyi juhusi yoyote ya kufnya hivyo. Anakubaliana
tu na mtazamo huu wa Wakristo na kuanzia kutoka hapa. Huu ni mwendelezo au
mtiririko uliomaanisha sana wa kimethodolojia.
Kuna aina kadhaa
za udhaifu kwenye hoja hizi za rabi. Kwanza kabisa, kuna makosa yakimkanganyiko.
Ni kana kwamba utendaji wa kompyuta imepokonya watafiti wa msingi wa uwezo wake
wa kutofautisha lugha mbalimbali. Kuchagua maana moja y neno na kuitenda mbele
ya baraza kunaanzisha utendaji kazi wa juujuu wa kiufundi na ukosefu wa
uadilifu wa kitathimini ambao ungeweza kutofikirika mbele ya kizazi cha
watafsiri wa mambo ya kiufundi. Methodolojia kama hiyo inakutikana kwenye njia
ya rabi ya jinsi anavyolitumia maneno ya tahat
(badala ya) na tippol (alishuka chini).
Matumizi ya maneno haya ni makosa mkubwa ya kitafsiri.
Kuna matatizo
mengine ya kilugha pia. Tafsiri ya kialama haikubaliki wakati andiko likiwa
wazi na maana isiyohitaji kutafsiriwa vingine. Rabi anafanya makosa haya katika
kushughulikia vyema naelezo au usemi walahay
roi’. Kosa linguine la kilugha ni kutoa maelezo yaleyale kwenye dhana yenye
maana tofauti, isipokuwa ile dhana inayohitajika na muhimu. Rabi alifanya hivyo
kwa maelezo kwamba hukumzuilia mwanao, yanayojitokeza
mara mbili kwenye kifungu kinachojadiliwa. Hatimaye, rabi anaelezea mjadala wa
kilugha ambao haufanani na nasaha kama walivyokuwa navyo, kama kwenye utendaji
kazi wa huduma ya kirabi N-S-H.
Kuna makosa ya
kimashiko pia. Rabi anatoa tafsiri inayopimgana ya maana iliyo kwenye Mwanzo 22:12
kama ushahidi kwa tafsiri hiyohiyo ya sadaka ya Isaka. Hii haiwezekani kabisa
na inadhoofisha sana hoja yake. Rabi anafanya hitimisho lisilo na mashiko na
kueleweka kutoka na vitu vilivyoachwa bila kuezewa vizuri kwenye maandiko: kwamba
Isaka hakurudi pamoja na Ibrahimu baada ya utoaji ule wa sadaka, kwamba Isaka
hakuhudhuria mazishi ya mama yake, na kwamba Isaka hakuhusishwa kwenye mipango
ya ndoa yake. Hoja zilizotuama kwenye kitu kisichoeleweka hayawezi kustahili
zaidi ya kuwa hakuna. Mwishoni kabisa, rabi anafanya makosa kimashiko kwa
kufana hitimisho kutoka kwenye maelezo yaliyo kwenye andiko. Anafanya hitimisho
la kuw Sara alikuwa huko Kiriath-arba wakati Ibrahimu alipokuwa huko Beer-Sheba
kwa msingi wa ukweli kwamba alifariki huko. Data zilizo kwenye andiko hazitoshelezi
kufanya hitimisho lile.
Rabi anafanya hitimisho
kutumia makosa ya kidesturi na kwa mawazo ya kisaikolojia. Anakosea kwa kufanya
udadisi au upelelezi kuhusu hisia ya mwanamke aliyependa wala kutamani mambo ya
kuolewa au ndoa iliyoandaliwa. Anakosea kwa kudhania kuwa Isaka hakumuombolezea
mama yake kwa kipindi stahiki cha miaka mitatu.
Kuna yapata dosari
kubwa kwenye mafundisho ya rabi. La kwanza ni linalotokana na kutegemea tofauti
iliyopo kati ya Elohimu, Mungu na malaika wa Bwana. Hakuna kinachotangulia kati
yake kutok kwenye Maandiko Matakatifu, la pili halihitajiki, na inaleta mambo
yenye matatizo ya kiteolojia ambayo kwayo rabi anayajua na kuyataja. Wazo la
mgongano uliopo kati ya Elohimu Mungu na malaika wa Bwana haikubaliki kabisa
kama msingi wa andiko la biblia.
Kosa kubwa la
pili dosari au makosa makubwa ni kushindwa kwa rabi kuyatilia maanani maandiko haya,
ambayo yanapinga kwa wazi kabisa juu ya kufa n kufufuka kwa Isaka. Miongoni mwa
hayo kwenye Mwanzo 24:6, panaposema kuwa Isaka alikuwa hai wakati ule kiasi
kwamba kwa mujibu wa dhana alikuwa hajafufuka bado.
Somo hili
linakanganya pia kutokana na kushindwa kwake kuyatilia maanani maandiko yaliyo
kwenye kifungu, ambayo kwa kweli yanaleta au kusababisha matatizo. Mahali
panapoonekana wazi kuhusu jamho hili ni kwenye Mwanzo 22:2 na Mwanzo 22:16, ambapo
Isaka anaitwa kuwa ni mwana wa pekee wa Ibrahimu. Hakukuwa na wakati wowote
mwingine ambao Isaka aliitwa kuwa ni mwana pekee wa Ibrahimu. Hili ni kosa
mojawapo la kihistoria ambalo linahitaji kutilia maanani sana, na twaweza
kumshukuru Rabi Ben-Yehuda kwa kuanzisha mjadala huu.
Sehemu kubwa ya
masomo haya yatatathimini au kufafanua maandiko ya biblia, lakini kwa nia ya
kufafanua kile kinachoonekana kutoendelea ndani yake. Wazo la msingi ni kwamba
tafsiri ya Masoretic Text ya Biblia ya Kiebrania, hasa kama ilivyo kwenye
Mwanzo 22 imehusika, imeimarika na inajitosheleza sana kikamilifu kwa kuwiana
yenyewe kwa yenyewe.
Kwenye Mwanzo
22:2 (na kwenye Mwanzo 22:16), Isaka anaitwa mtoto wa pekee wa Ibrahimu. Hii haijitoshelezi
na ripoti iliyo kwenye Maandiko ya Masoretic katik Mwanzo 16:15 ambapo inasema
kuwa Hajiri alimzalia Abramu mtoto wakiume aitwaye Ishimaeli. Kwenye Mwanzo 17:17-19,
ni dhahiri sana kwamba Ishimaeli alikuwa yupo na mzima kabla ya kuzaliwa kw Isaka.
Mwanzo 21:2-3 inatumbia kuhusu kuzaliwa kwa Isaka baada ya kutahiriwa kwa Ishimaeli
akiwa na umri wa miaka kumi na tatu (Mwanzo 17:25). Mwisho kabisa, Mwanzo 25:9 inasema
kuwa Ishimaeli alikuwepo na alikuwa mzima bada ya tukio lililo kwenye Mwanzo
22. Isaka kwa hiyo hakuwepo kwa mujibu wa andiko lisemalo mwana wa pekee
Ibrahimu wakati wa tukio hili kwenye Mwanzo 22 au kipindi kingine chochote
kilichopita kwao.
Kuna matatizo
mengine kwenye habari iliyo sambamba na kilichoandikwa kwenye andiko hili. Imani
ya Kiyahudi kwa ujumla inaitafsiri habari hii kuwa ni kama ufunuo kwa Ibrahimu
tu kwakuwa Mungu haukubali wala kuipokea sadka ya mwanadamu. Wakristo wanaitafrisi
hadithi hii kiujumla wakisisitiza somo la utiifu. Kwahiyo Wakristo wanakabiliwa
na mgano wa kiteolojia kuhusu amri hii ya kumtoa sadaka mtoto huyu kama sadaka
ya kuteketezwa. Amri kama hii inapingana na amri iliyo kwenye Kutoka 20:13, Usiue.
Ingawa wanateolojia wanaweza kuleta ufumbuzi wa jambo hili kwa kiasi fulani
kwenye mawazo yao na mitizamo yao wenyewe, Wakristo wengi wanaachwa kwenye
mshngao au njia panda. Hawawezi kuelewa jinsi Mungu anavyoweza kumuamuru mtu yeyote
kwa kwli amuue mtoto wake mwenyewe.
Kama tutaielewa
hadithi hii kama ilivyo kwa ujumla – kwamba ni kweli kuwa Mungu alimuamuru Ibrahimu
amuue mwanae wa pekee – kisha kuna matatizo fulani ya kimaelezo kwenye hadithi
hii kama yanavyoonekana kwenye Biblia. Mazungumzo yaliyo kwenye Mwanzo 22:7-8 hayakithi
haja kwenye sababu ya ya tukio ambalo kwamba Ibrahimu alikusudia kbisa kumuua Isaka.
Isaka akauliza ni wapi alipo mwanakondoo, kana kwamba mwanakondoo ndiye
anayekwenda kutolew sadaka na sio Isaka. Zaidi ya yote, hkuna ushahidi
unaofuatia wa kwamba Ibrahimu alimuarifu Isaka baadae kuhusu hali halisi ya
jinsi sadaka itakavyokuwa, halafu Isak akahiyari na kujua kuwa ni mshiriki
wakati wote huu.
Kile ambacho
Biblia inakielezea ni tukio ambalo kwalo baba anamchukua mwanae, akaenda mahala
pasipojulikana wakiwa kama kikundi cha wanaume watupu lililoachwa kwenye zamu,
akijitenga mwenyewe mbali na mwanae, akitoa sadaka ya dhihaka au mfano ya
mwanae, kisha akamtoa mnyam sadaka kama sadaka ya kuteketezwa, na akarudi
nyumbani peke yake bila mtoto.
Kipindi hiki
chote ch mchakato huu, Isaka bado anaitwa mwana wa pekee. Na haitwi mahala
pengine popote kwenye miito yote ya kitabu cha Mwanzo. Ukweli huu unaendana na
tukio hili. Tukio hili linajumuisha matendo ya utoaji wa sadaka na mfuatano wa
maelezo au maswali na majibu. Kifungu hiki kinajionyesha chenyewe kama kipo,
licha ya hitilafu au tofauti ya baadhi ya hotuba au semi. Andiko linapuuzia
matatizo ya kiteolojia ya majiribu kutoka juu mbinguni na sadaka ya mwanadamu,
kana kwamba hii siyo jambo la muhimu.
Kwa jinsi hii
tunakuwa tumezipunguza au kupingana na taarifa za biblia. Ni muhimu kuangalia
ufafanuzi wa mambo yaliyo nje ya andiko lenyewe. Kuna ukweli kadhaa wa
kuuangalia. Ikiwezekana, kutaweza kukuta mifano ya sadaka ya mzaha ya vijana na
baba zao au mamlaka nyingine zilizofuatia na sadaka iliyochuua mbadala ya
mnyma. Matukio haya ya utoaji wa sadaka yalijumuisha mlolongo wa hotuba au
semi, ambayo yangepuuzia au kukataza hali yenyewe halisi.
Mwaka 1909,
A. van Gennep alitambulisha kwa wazi aina hii ya jambo kwenye kitabu
chake cha Les rites de passage. Sheria
au kanuni za kifungu cha namna hii inafanyika kwa vijana wa umri fulani, ingawa
kuna kanuni kama hizohizo kwenye baadhi ya jamii zinazowahusu wasichana pia. Sheria
hizi mara zote zimehusiana na jinsi ya kutoa hotuba au semi kwenye kile kinachoitwa
kuwa ni mfumo shinikizo. Kuna igizo la kumuua kijana, kutimilizia sadaka ya
mnyama badala yake, na mfano wa kufufuka wa kijana. Mara nyingi ni kipindi cha
kujitenga kutoka kwenye jinsia tofauti. Mwishoni mwa sheria hii, kijna anakuwa
amepita umri wa utoto na kuingia umri wa utu uzima, na anaweza kuoa au kubeba
majukumu mengine ya kiutu uzima au mwenendo wa utu uzima, au anakuwa amepita
kutoka kwenye umri mmoja hadi mwingine kwenye maisha yake ya utu uzima.
Ingawa lirutjia
au sheria za kidini za kanuni au sheria za kifungu kwa kawaida inaonekana kuwa
ni jamii isiyojua mabo ya uandishi, kuna mifano ya maandiko yenye miundo
shinikivu kwenye maandiko mbalimbali ya madara ya kidini ya ulimwengu. Moja ya
hizi ni sehemu ya kwanza ya Kathopanishad, moja ya Vedic Upanishads inayojulikana
sana kwenye Maandiko muhimu kwenye daraja za Kihindu. Kuna mwendelezo fulani
kwa muundo shinikizo kwenye maandiko ya dini za kale kutoka ulimwenguni kote,
na hakuna sababu yoyote kabisa ya kwa nini tusiweze kuukuta mmoja kwenye
Biblia. Ni wazi kuwa hadithi ya kutolewa sadaka kwa Isaka inakuwa na mambo yote
muhimu ya namna hiyo sheria na kanuni ya utoaji dhabihu.
Kama hadithi
inaelezea kanuni au sheria ya kifungu cha liturjia, hotuba itafanywa kuwa ni
hotuba inayohusiana na taratibu zake. Kwa kweli zilitolewa kama zilitokea kwa
kipindi chake maalumu na kwa mahala maalumu na mtu maalumu aliyehusishwa, ila
yawapasa wajue kuwa zikitokea kwa mumhusu kila kijana wa kiume kwenye utamaduni
uliotolewa wakati ilipohitajika jinsi iliyo muafaka.
Sheria na kanuni
hizi zinaanzia na mchocheo wa Mungu, aliyemuita Ibrahimu kwenye Mwanzo 22:1. Jibu
la Mungu kwenye aya ya 2 ni pia limefundishwa kwenye vifungu vya tafsiri ya
kiibada. Hii inafafanua na kuelezea sababu ya kwa nini hapa Isaka amexkuwa kila
mara anaitwa mtoto wa pekee. Ni sehemu ya taratibu za kiibada. Inawezekana kuwa
wakfu ni inatajwa kwa mzaliwa wa kwanza wa kila mwanamke. Kitendo cha kumuweka
alama mzaliwa wa kwanza ni jambo endelevu kwa sehemu nyingi za Biblia. Kitendo
cha kumuweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa kila mwanamke kumeelezewa kwa mara ya
kwanza kwenye Kutoka 13 na kwenye vifungu vingine vilivyofuatia. Maelezo haya
yangechukuliwa kwa ujumla kuwa ya kweli, na yangeishia tu kwenye hali ya ndoa
ya matala, kama ilivyo kwa habari ya Ibrahimu. Bado hata katika hali hii ya ndoa
ya matala, maneno hayahaya ya kiutaratibu wa kiibada yangeweza kutumika kwenye
tukio la utoaji wa sadaka, kwa kadiri kwamba liturjia ya kimapokeo au maneno
muafaka kwa ajili ya sadaka yangeweza kutumika wakati wote
Tabia na
pambanuzi za kawida za kanuni za vifungu vinavyoshabihiana kwenye hadithi iliyo
kwenye kitabu cha Mwanzo kama hii. Makundi yote ya wanaume yaondoke kwa ajili
ya safari ngumu na ndefu ya siku tatu (Mwanzo 22:3,4). Wale ambao hawashiriki
kikamilifu wanaachwa wasubiri na kulinda (Mwanzo 22:5). Sheria nyingi za
vifungu zinajumuisha vikorokoro au zana kama hizi za kuni ya kutumia kwenye
ibada hii ya kutolea sadaka, moto, na zana au silaha (Mwanzo 22:6). Kanuni
nyingi za vifungu zinajumuisha maandiko yaliyowekewa kiwango cha hotuba na
majibu kati ya mtu aliyechukua cheo cha mwingine na uimaririsho (Mwanzo
22:7,8). Sheria nyingi za vifungu zinajumuisha maandalizi ya dhabihu na sadaka
kivuli iliyokusudiwa ambayo kwayo yeye amefungwa kamba au kufungiwa kwenye
kifungo cha gizani (Mwanzo 22:9-10). Sheria nyingi za vifungu hujumuisha sadaka
mbadala ambayo inakutikana kwenye mlolongo wa maelezo au hotuba, iliyofanyika
kuwa ni mbadala wa kilichodhamiriwa na dhabihu (Mwanzo 22:11-13). Sheria nyingi
za vifungu hujumuisha na kutaja majina ya maeneo au itendo cha kutaja
yaliyokusudiwa au mara chache sana, kupewa cheo (Mwanzo 22:14). Nyingi ya hizi
sheria zinazowekwa au kuingizwa zinaishia na kuwabariki au kuzibariki juhudi,
kuelekezea utu uzima au wadhifa na heshima stahiki (Mwanzo 22:15-18). Sheria
nyingine za vifungu huishia na kumtafuta kijana anayetafuta nyumba na njia zake
mwenyewe, kuonyesha faida yake ya wadhifa wake mpya kabisa (Mwanzo 22:19).
Andiko lililo
kwenye Mwanzo 22 limetathiminiwa kutoka kwenye mtazamo wa muundo uliorasimishwa
kama sheria ya kifungu. Hakuna isiyokuwepo au kudumu miongoni mwa dhana na wazo
hili la kitafsiri ambapo kunapatikana kwenye maandiko ya biblia.
Tafsiri nyingine
ya andiko hili kama kanuni ya andiko inafanya namna ya kuendelea kwa kiwango
chu kutoimarika mbele kwa Mwanzo 22. Tofauti au mkinzano wa hotuba, pamoja na kuendelea
kufifia mng’aro au mvuto wa kumuita Isaka kuwa ni mwana pekee wa Ibrahimu, kunaonekana
kuwa yanaendelea kuendelevu wote kabisa na sheria ya kifungu. Amrisho lenye kukinzana
la kiteolojia imepeleke utoaji wa sadaka au dhabihu ya mwanadamu kutokomea.
Jaribu la Mungu limepunguzwa kwa umhimu wa kumkomboa mzaliwa wa kwanza wa kila
mwanamke, au kuelezea kwamba Ibrahimu ni mfano kwa vizazi vijavyo.
Swali laweza
kujitokeza kama tunayo haki kulitafsiri andiko kuwa mfumo shirikishi kwa kuwa
hakuna hakuna kitu kutoka kwenye maandiko kinachosema kuwa ni hivyo. Mtu
anaweza moja kubwa dhidi ya tafsiri nyingine. Kulitafsiri andiko vinginevyo kunaweza
kutuacha na matatizo yaliyotajwa hapo juu, baadhi yake yakiwa ni ya muhimu na
baadhi yake yamefifia sana kimawazi. Tunahesabia haki kwa kuyakubali maelezo
yatolewayo kwa sababu nyingi zaidi kuliko zile zilizopo na yaliyoenezwa sana
kila mahali ulimwenguni kote na kwa karne nyingi katika Australia, Asia, Afrika
na Amerika. Ukweli ni kwamba miundo elekevu inaonekana kwenye maandiko mengine
ya kidini, kama vile Kathopanishad, ingawa mashauri fulani hayatusukomi au
kutushurutisha kuikubali hii kuhusiana na maandiko ya kibiblia. Tunakuwa salama
kwa kukubali tafsiri mahiri kwa kuwa ukombozi wa mzaliwa wa kwanza kumeamriwa
kwenye Kutoka 13, na ilivyoelezewa na kuwa alidangantika kwa mara nyingi.
Chochote kilichoamriwa na kuwa kuhadaika kunatakiwa pia kuwa matendo. Ni dhahiri pia kuwa ilielezewa kwenye Mwanzo
22.
Yapasa ielezwe
kuwa andiko hili, kutolew Sadaka kwa Isaka, kulikuwa kuna maana kubwa sana
kwenye uzoefu wa mambo ya kidini. Dhana ya kimakosa kuwa Mungu anaweza
kumuamuru mtu ajishughulishe na utoaji wa sadaka ya mwanadamu kumefungua mlango
wa kukosolewa kwa dini kwa nyingine zote kwa upande mmoja, na mambo menyine
makuu ya matendo yasiyo imara kwa meingine/ kwenye dini ya Kiyhudi, inaonekana
kuwa nia na lengo la hadithi hii ni kwamba Mungu alimfundisha Ibrahimu kwa njia
pana kwamba yeye hakuwa anaipokea sadaka ya binadamu. Ilikuwa njia ya kimatendo
kwa kuwa matendo ya kutoa sadaka za wanadamu huko Kanaani kwa namna nyingine
yangewashawishi na kuwavutia kwa namna fulani Ibrahimu na uzao wake.
Ukristo umejionea
maalidi ya hadithi kuwa ni kwamba utii wa Ibrahimu ni mfano kwa wote kuufuata’
imani zote mbili, yaani Wakristo na Wayahudi wameitumia hadithi hii kama ni
silaha ya kuikosoa imani ya Kiislamu. Kor’ani ([37]:103-106) [inadaiwa kuwa
ed.] inaelezea tukio hilohilo kwa Ishimaeli badala ya Isaka. Wanazuoni wa
Kiislamu wameona kutajwa kwa “mtoto wa pekee” kwenye Mwanzo 22:2 kama masalia ya
andiko la kweli linalomtaja Ishmaeli, ambaye alikuwa mtoto wa pekee wa Ibwahimu
kwa maisha halisi. Mwanazuoni na mtafsiri kama huyu angeshauri kuwa andiko
lilikuwa limegeuzwa na Wayahudi na kumuelezea Isaka badala yake.
Kwenye mambo au
matukio yanayopigiwa chapuo, ukweli ungekuwa ni tofauti. Wote wawili, yaani
Ishimaeli na Isaka, wote wawili wakiwa ni wazaliwa wa kwanza kutoka tumboni mwa
mama zao, walipaswa kukombolewa. Dr McElwain anahitimisha andiko kwa kutoa
fafanuzi. Ukombozi wa lazima, wa kutoa kikombozi cha sadaka mbadala vilifanyika
kwa wote wawili. Mwishoni, maandiko ya biblia yanaenda pamoja, na Biblia na
Korani zote mbili ziko sahihi. Kila moja inakubali na kukiri na sisi sote tunakabiliwa na kuishi pamoja
kwa amani. Je, tunaweza kuinuka kwa jaziba kwenye changamoto ile?
Hata hivyo kuna
kosa kubwa katika kudhani au kwenye dhana kuhusu imani ya Kiislamu kuhusu
Ishimaeli. Andiko kwenye Korani Sura ya 37:103-106 haionekani kumtaja Ishimaeli
kabisa.
Dhana hii
inabakia kwenye ukweli kwamba andiko lililo kwenye Sura ya 37:112 ndipo
inaendelea mbele kuelezea kuzaliwa kwa Isaka. Ndipo wazo linapofanywa kwamba
andiko hili linamtaja Ishimaeli na kisha Isaka. Ukweli ni kwamba andiko hili
linaiezea baraka ya Isaka kama nabii wa haki kuanzia hata kabla kuzaliwa kwake.
Andiko hili linakutja kuzaliwa kwa Isaka na baraka zake na huduma yake ya
kinabii, au wadhifa wake akiwa kama nabii, miongoni mwa mwa manabii wa Biblia (pamoja
na Nuhu (37:79-82, Ibrahimu (37:83 na kuendelea), Isaka (37:112 na kuendele.),
Musa na Haruni (37:120 na kuendelea), Eliya (37:130 na kuendelea), na Yona
(37:139 na kuendelea)). alitangaziwa Ibrahimu kabla ya kuzaliwa kwake. Ukweli
wa mambo ni kwamba Sura ya 37 haina lolote la kufanya wala kuhusiano wowote na
Ishimaeli na ni marudio ya hadithi ya Mwanzo 22:2 na 25:5-6, 9, 11, 12. Ina,fanya
Isaka kuwa ni kama nabii, kama mmoja wa wale
walio kwenye vyeo akipewa hata jina la Sura hii. Sura hii inashughulika na
kukemea ibada potofu na miungu wa dunia hii ambalo kwa hakika ndiyo maana
halisi kabisa ya hadithi hii ya kutolewa sadaka kwa Isaka. Agano lililofanywa
na Ibrahimu ilikuwa ni ishara iliyotolewa badala ya sadaka ya mwanadamu kama
ilivyokuwa inatolewa kwenye imani na ibada za Moleki na kwenye imani na ibada
za Baali-Ishta. Ilikuwa ni kawaida tu huko Uarabuni na ulimwenguni kote kwa
ujumla hadi kipindi cha kumuabudu Ndama wa Dhahabu ilipokomeshwa na imani ya
Ukristo (soma jarida la Ndama wa Dhahabu (Na. 222)). Kuhusishwa kwa Ishimaeli ni jambo
lililofanywa kwa fikra tu kwamba watajwe wote kwenye kuzaliwa kwao kwenye Sura ya
37:101, 112 inawataja watoto wawili ambao ni Ishimaeli na Isaka na Ishimaeli hatajwi
kwa jina. Wazo hili ndilo ambaalo lililotolewa na kudai kuwa mgongano kati ya
Korani na andiko la kitabu cha Mwanzo. Kutokana na hili upungufu wa uvuvio
inaodaiwa kuwepo kwenye Maandiko Matakatifu na kwenye Sheria za Mungu zilizo
kwenye Torati kwa Waislamu wa siku hizi wanayoyatumia ili kuhalalisha mambo yasiyo
na uhusiano na Maandiko Matakatifu na Torati ya Mungu. Hebu na tutathimini
andiko lote zima kuwahusu Ibrahimu na Isaka:
99: Na akasema: Hakika
mimi[Ibrahimu] nahama, nakwenda kwa Mola
wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.
100. Ewe Mola wangu
Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.
101. Basi tukambashiria
mwana aliye mpole.
102. Basi
alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye [Ibrahimu], alimwambia: Ewe
mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe,
waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi,
Inshallah, katika wanao subiri.
103. Basi wote wawili walipo jisalimisha, (kwa Allah) na akamlaza juu ya kipaji.
105. Umekwisha
itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema.
106. Hakika
haya ni majaribio yaliyo dhaahiri.
107. Basi
tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu
108. Na
tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye.
109. Iwe
salama kwa Ibrahim!
110. Hivi
ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema
111. Hakika
yeye ni katika waja wetu walio amini.
112. Na
tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema.
113. Na
tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na
wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi. (Tafsiri ya Kiswahili)
Tafsiri
iliyofanywa na Arberry (iitwayo Korani Ilitafsiri
[Koran Interpreted], Oxford, 1964) anatumia maneno kisha ili kuashiria ukitambo wa muda kuendeleza malumbano haya
kwamba wote wawili, yaani Ishimaeli na Isaka wameelezewa kwenye mchakato,
lakini hii ni leseni ya mtafsiri ambayo haikuchukuliwa na Pickthall. Sale
(Warne and Co., pp. 336-337) yaonekana kubeba dhana au wazo kuhusu ukuwili wa
matangazo na kwa hiyo ndipo watoto wawili walitajwa kwenye tafsiri yake
ingawaje hakuna sababu kwa namn yoyote ile ya kufanya hivyo kutoka kwenye
maneno ya tafsiri. Kwa kweli kinyume chake ndicho kinachoonekana. Tafsiri ya Dawood
inafuatia andiko kama anavyofanya Pickthall na inafanya uandishi mwingine tena
jambo lililopo kuhusu Isaka kwenye sura ya 37:112.
Abdullah Yusuf
Ali anaanzisha malumbano makubwa kwenye kitabu chake cha fafanuzi (kiitwacho The Qur’an, Text, Translation and Commentary
[Korani, Andiko, Tafsiri na Ufafanuzi], Tahrike Tarsile Qur’an Inc, 1987
print, p. 1205) kwamba kwa miaka kumi na minne Ishimaeli alikuwa ni mtoto pekee
wa Ibrahimu. Anashikilia kuwa hoja yake ilikuja kutupiliwa mbali baadae na
imani za Kiyahudi na Kikristo ambao walimkweza Yule kijana mdogo wa familia,
aitwaye Isaka. Hata hivyo, tunajua pasi shaka kutokana na watalaamu wa elimu
kale na uchimbuzi wa siku hizi na maandiko ya kale kwamba ni maana ya kweli na
maandiko ya Maandiko Matakatifu ya kale ya wakati wa Kristo na yalikuwa ni maandiko
yanayoeleweka hata wakati wa Qasim (aliyeitwa Muhammad), na ni maandiko asilia ya
Biblia.
Andiko lililo
kwenye Qur’an (Korani) halipingani kwa namna yoyote na maandiko ya Biblia kwenye
kitabu cha Mwanzo na ni ushahidi mwingine zaidi kwamba tafsiri ya Marabi wa
Kiyahudi inayomuona Isaka kuwa ndiye aliyetolewa sadaka inakosea kabisa. Pia,
uelewa sahihi kama ulivyofunuliwa kwenye Sura kama ilivyoeleweka na Mtume ni
sawa na ilivyo kwenye maandiko ya Biblia. Na kwa kweli inapasa kuwa hivyo. Hata
hivyo, iwapo kama inadaiwa kuwa Ishimaeli anahusika, kutokana na kukarabatiwa
kwa maanndiko, ndipo kanuni ya ya muafaka wa kifungu itaondoa mgongano na inasisitiza
umuhimu wa kuondolewa kwa mifumo na imani za zama kale kutoka katikati mwa watu
wa Mungu wawe Waarabu au Waisraeli, iwe kimwili ama kiroho.
Agano la Mungu ni
la lazima na muhimu kwa ajili ya imani na kwa wana wa Ibrahimu kwenye kila
ushawishi wa kidini
.
q