Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[248]
Fundisho la Asili ya Dhambi
Sehemu ya 2
Kizazi cha Adamu
(Toleo
La 1.0 19980627-19980627)
Mstari wa kizazi cha Adamu kupitia kwa Sethi na Kaini unamaana na umuhimu
wa namna yake katika Mpango wa Wokovu jambo ambalo halieleweki kwa jmla na
kuelezeka kinagauubaga. Mwonekano wa mipangilio miwili ina maana inayoelezeka
na hadithi inayoelezeka ya Mpango wa Mungu na inaitangaza kutoka mwanzoni.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1998 Wade Cox and Storm
Cox)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Kitabu cha
Mwanzo kinaelezea juu ya anguko la mwanadamu lililotokea kwenye Bustani ya
Edeni, ambalo tumeliongelea sana kwenye jarida la sehemu ya 1 ya mlolongo huu.
Baada ya kufukzwa kutoka Edeni, na kulaaniwa kwa ardhi kwa ajili ya dhambi ya
kwanza, Adamu aliifanya kazi aliyoagizwa na kaminiwa na Mungu. Kazi yake ya
kwanza ilikuwa ni kijaza nchi.
Mwanzo 4:1-26 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata
mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. 2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili
alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
Andiko hili hapa
linasema Nimezaa mwanaume kutoka kwa
Bwana lakini andiko lenyewe asilia hasa halisemi mwanaume kutoka kwa Bwana bali linamaanisha hasa mwanaume hata Yahova (kwa Kiebrania ‘ith ‘esh Yahova sawa na isemavyo Companion Bible n. to v. 1). Neno akamjua mke wake lililotumika hapa linamaana
sawa na kusema Alimjua mkewe ambalo Rashi
anaamini kwa linamaana kabla hawajafkzwa
bstanini (sawa na Soncino n. to v. 1). Kwa hiyo kuna mambo muhim machache
hapa, ambayo hayajaelezewa kwa maelekezo na fafanzi za kina na watoa fafanuzi
marabi au Soncino Chumash.
Nia ya Hawa
hapa inaonekana kuwa kumuweka Yahova, kama Shetani alivyojaribu kufanya au
kujifanya kuwa kama sawa nay eye. Nia yake hasa na iliyo wazi imeelezwa kwa
inakusu diaa hapa, ni kumzaa elohim hata Yahova. Rashi anashikilia kuamini
andiko hili kwamba:
Ni yeye peke yake ndiye aliyetmba
sisi sote, lakini kwenye uumbaji wa mtoto huyu sisi watatu tuliswhiriki (Soncino).
Nachmanides anaonekana
kupanua maana yake zaidi akisema
Mtoto huyu atakuwa mali ya Bwana,
ambaye kama tutakufa anaweza kumtumikia (alivyosema Soncino ibid.).
Andiko hili
limechkliwa pia kutoka kwa Rambam akisema kwamba
Huyu (kichanga) wa kiume atakuwa milki
na mali yangu kwa faida ya Mungu, kama vile alimtoa wakfu mwana wake ili
afanyike kuwa ni mtumishi wa Mungu baada ya yeye na Adamu kufariki (cf. Stones
Chumash).
Tafsiri hii ina
ugumu kimatazamo wa harakati zilivyo kwenye andiko hili.
Watoto hao
wawili walikuwa ni Kaini (milki) na Abeli (au Hebel katika Soncino) kuashiria kwamba chochote anachokipata mtu
hapa duniani ni ubatili (hebel).
Nachmanides anaamini kwamba:
Hakupenda kulifanya tumaini hili
kirahisi, kwa hiyo Maandiko Matakatifu hayakutoa tafsiri ya jina hili la Abeli
kama yalivyofanywa kwa jina la Kaini pia (anasema Soncino).
Tafsiri ya Strong
inasema kwamba Abeli inamaanisha mpito au mapito.
Hakuna hata
moja katika vitabu vya ufafanuzi vya marabi vilivyoweza kuridhisha usuluhishi
wa tatizo hili kubwa la andiko hili hapa linalomunye Zekaria 12:8 linasema
kwamba watu wale watakuwa elohim na linamaanisha Malaika wa Yahova ambaye
kichwa chake ni kama elohim pia.
Zekaria 12:8 Katika siku hiyo
Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao
atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama
malaika wa Bwana mbele yao.
Kwa kuongezea, Rashi
anaonyesha kuwa kijisemi ishara kinachosema eth
mbele ya maneno Kaini, ndugu yake na Abeli ni ya nyongeza, yanayoonyesha ama
kuashiria mapacha wa kike waliwazaa.
Rashi anazidi
kuelezea kwa kina kwamba neno lisemalo mchngaji
wa kondoo linalomtabulisha kazi ya Abeli linamaana kwamba:
Aliacha ana alijiepusha kuilima
ardhi kwa kwa ilikuwa imelaaniwa (sawa na Soncino).
Hii inaonekana
kashiria mawazo au mtazamo wa vizazi ziwili tofauti. Mtazamo huu pia inaonyesha
kuashiria kitu kilichowiana na nia aliyokwa nayo Hawa kutokana na andiko hili.
Ikawa hatimaye Kaini
akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. 4 Habili naye
akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana
akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini
hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake
ukakunjamana.
Abeli alileta
dhabihu au sadaka na mafuta yake kwa Bwana, na Bwana akaikubali. Kaini akatokea
akiwa na sadaka ya mazao aliyoyapata kutoka ardhini na inaonekana alikuwa
anailazimisha ardhi impe kitu. Mazao yaliyotoka kwenye ardhi ilikuwa ni sadaka
ya kiwango cha chini ukilinganisha wanyama kwa sababu nyingi sana. Ilikwa ni ya
kiwango cha chini kwa sababu ardhi ilikuwa imelaaniwa. Kaini alikuwa anafanya
kosa la kuleta mazao yanayotokana na ardhi iliyolaaniwa wakati ambapo ni kweli
kabisa alijua kwamba sadaka ya damu ndiyo iliyokwa inahitajika. Zaidi ya yote
ni kwamba sadaka ya Abeli ilitokana na malimbuko sawa kabisa na ilivyohitajika
kufanyika kwa mujibu Torati. Sadaka ya Kaini haikuwa ya malimbuko (kwa
Kiebrania: minchah). Habari sadaka
hii ya Kaini inaonekana pia kwenye waraka wa Yuda 11.
Yuda 11 inasema: Ole wao! Kwa
sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo
kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.
Maelezo yote
kwa kuelewa utaratibu na utoaji wa malimbuko vilijulikana vyema tangu mwanzoni.
Kila kipengele cha mpango wa Mungu na Amri Kumi chini ya sheria au torati
vilijulikana tangu zama za mwanzoni za kitabu cha Mwanzo. Hata jina la Yahova
na pia dhana ya Amri ya Tatu ilijulikana sana tangu nyakati za Adamu na Sethi
(tazama aya ya 26) na sio kama inavyodaiwa kufundishwa kimakosa au kwa uwongo
wakati ilipotolwa na kpewa Musa pale Sinai.
Kukataliwa kwa
Kaini kulisababishwa na nia hii hii ambayo tunamuonanayo Shetani akikataliwa kutokana
na uroho wake kwa kujilimbikizia na kufanya biashara au kujitafutia faida (sawa
na inavyosema Ezekieli sura ya 28 na Isaya 14). Hapa wazo hili la kutenda
dhambi na kukataliwa linawekwa ndani ya moyo wa Kaini.
Bwana akamwambia
Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda
vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa
uishinde.
Dhambi hapa zinajidhihirisha
kwa Kaini. Kukataa kwake Mngu sadaka ya Kaini na kuikubali kwake ile ya Abeli hakuwa
ni mtu asiyefuata utaratibu au mtu holelaholela. Hapa Kaini hakuwa na haki ya
kuona wivu. Zaidi sana ni kwamba alitakiwa kurekebisha makosa na mambo yake
yaliyokwa kwenye uwezo na mikononi mwake Kaini (anasema pia Sforno; Soncino).
Tafsiri ya aya hii
imefafanuliwa na kuandikwa vema kwenye kitabu cha Targum (Rashi) kama
ifuatavyo:
Kama utazirekebisha njia zako,
dhambi zako zitafutwa; bali kama hutazirekenisha njia zako, dhambi zako zinakusubiri
kwa siku ya kiyama na hukumu, kwa kuwa hakika utahukumiwa kama hutatubu; bali kama
utatubu, utasamehewa wewe (anasema Soncino).
Swali hapa ni
kuhusu kiumbe hiki kikatili kuinuliwa juu yule aliyekuwa ameanguka (ansema
Rashi). Nachmanides anaamini kuwa inamaanisha kwamba angeinuliwa juu zaidi
kuliko ndugu yake kwa kuwa alikuwa mzaliwa wa kwanza (anasema Soncino). Sforno anaamini
kuwa habari hii inamaanisha kuwa angefikia kina kirefu cha kutukuzwa. Mtazamo
wa marabi ni kwamba kumtii Mungu ni chanzo au mlango wa kupendwa na kukubalika
naye.
Kijisemi
kisemacho wewe nndiye chaguo lake kwa
ajili ya dhambi kama inavyoelezewa na Soncino ni kiambisho kinachovutia na kupendeza.
Tafsiri ya The KJV inalielezea andiko hili hivi:
Kama ukitenda vyema,
hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo
inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Neno la Kiyahdi
kuhusu dhambi ni chat’a (sawa na inavyosema Comp.
Bible) kumaanisha dhambi. Neno danganya
linalotaja jinsia ya kiume, sadaka ya
dhambi ni la kike. Kiebrania inasomeka Kwenye
mlango pa kuingilia [wa kiume] anadanganya, sadaka ya dhambi. Marabi
wanaamini kuwa mlango ni mlango wa
kaburi (ambako hukumu inakungojea Rashi).
Nachmanides anaamini kuwa inasimama mlangoni ikitafuta kumsababisha mtu aanguke.
Sforno anaamini kuwa inammanisha kwamba dhambi
inakungojea na utaongeza zaidi ya hiyo liyokwisha kuifanya. Kijisemo cha tama yako itakwa kwake kwa mtazamo wa
Soncino unachukuliwa kumaanisha kuwa Mvuto
tapenda kukuvutia wewe (Rashi). Abraham ibn Ezra anafanya mrejesho kuhusu
maana yake hata hivyo kwa kusomeka Dhambi
itakupelekea kushindwa kama utaipenda.
Huenda huu ni
mwanzo wa fmbo. Tafsiri ya KJV inajaribu konyesha maana mbalimbali na tofauti: Tamaa yake itakuwa kwako nawe utakmtawala. Hii
ni tafsiri iliyo kinyume kati ya Malaika waasi na viumbe walio wa uzao wa
Adamu. Ilifikia kiwango chake cha juu au kilele chake kwa jaribio alilolifanya
Shetani kumjaribu Masihi alipompeleka kwene kilele cha Mlima na kumhakikishia kuwa
angevipata vitu vyote iwapo kama tu angemsujudia huyo Shetani. Andiko hili
kuhusu uongozi ama mamlaka limeonekana pia kwenye Mwanzo 3:16. Maandiko haya
pamoja na husiano wake yanavyosema kwenye heshima kamili ya mapenzi au mawazo
ya mwanadamu ni uadui kwa Mungu na kwenye mfumo wa mambo yake alyojiwekea hapa
duniani kupitia kwa wana wa Adamu. Makosa yalijitokeza mara moja. Kaini
hakuweza kutubu na kurejea kwa Mungu. Wazo la kwamba mwanaume alilalia kwenye
mlango kama sadaka ya dhambi ilikuwa inamuashiria Masihi akiongea na Kaini kama
Yahova elohim.
Halafu Kaini kama
wote walivyofanya hapo mwanzoni. Kaini akaongea na Abeli na kisha akamuua. Namna uovu unavyotenda kazi zake
ni kujihesabia haki na kutafuta makosa. Wakati kunapotokea kosa halionekani,
unageukia kwenye fujo au machafuko. Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Kristo na
kufatia mateso ya kanisa. Wateule kwa uwepo wao wanasimama kama mashahidi dihi
ya ulimwengu. Abeli (au Hebeli) alisimama kama shahidi dhidi ya Kaini. Kaini
akamuua Hebeli akiwa kama dini Kongwe zenye wafuasi wengi zilivyowatesa na
kuwaua wateule.
Kaini akamwambia
Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia
Habili nduguye,akamwua.
Rashi anaamini
kwamba Kaini alianza majadiliano na Abeli ili kumchokoza aingie kwenye malumbano
na ugomvi. Kipindi hiki walikuwa mbali na walipokuwa wazazi wao (anasema Sforno;
sawa na anavyosema pia Soncino). Neno ilinenwa
ni ‘kiambisho ambacho kwa Kiebrania
ni lazima ifuatiwe na maneno yaliyonenwa (kama ilivyopingana na dabar) lakini maneno haya yamefutwa
kwenye tafsiri ya Biblia ya the Masoretic Text (MT). Maneno halisia ya Kaini
yamehifadhiwa kwenye Torati ya Wasamaria inayojulikana kama Septuagint (LXX), ya
Kisyria, ya Vulgate, ya Targum, ya Jerome, na ya MSS ambazo maneno yameandikwa hebu na twende uwandani. Tafsiri ya\MSS ambayo
haina maneno haya inaviashiria vinavyoonyesha kuwepo uwezekano wa kuruka
maandiko haya (sawa na inavyosema Comp.
Bible n. to v. 8).
Kwamba ndipo
alipouawa ambavyo ni kwa mpito (au kama ilivyokuwa kama upepo na ndipo pia ubatili au matumaini).
Kuna maana yake
muhimu kwa mtu kitwa Hebeli. Kwa kuwa hilo ndilo hasa lilikwa jina lake (SHD
1893 ambalo ndilo lilikwa sawa na ilivyo kwenye SHD 1892). Amani ktoka kwa
Adamu haikudumu kati ya wana wa Adamu sambamba na dhambi.
Bwana akamwambia
Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu
yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu
yako inanililia kutoka katika ardhi..
Yahova elohim aliuliza
maswali ili kumpafursa Kaini ya kukiri dhambi yake na kutubu (Rashi).
Neno damu lililotumika hapa ni la uwingi
kwenye lugha ya Kiebrania. Uwezekano unaonekana kwanza kabisa wa kuwa kwamba
damu ya Abeli na damu ya vizazi vyake ilikuwa inamlilia (sawa na Mathayo
23:35). Rashi anaamini ilikuwa ni kwa sababu alikuwa ameumizwa mara nyingi kwa
mauaji ya kikatili ambayo Kaini hakujua kuwa ingemsababishia madhara au maafa (Soncino).
1 Yohana 3:12 inaonyesha sababu ya kumuua kwake ikisema:
Basi sasa,
umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu
yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa
mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Laana ilitokana
na ardhi ikiashiria kwamba isingeweza kukoma mapatilizo yake. Hapa ardhi ilitumika
ili kufichia uovu wa mauaji aliyoyafanya na ambayo kwayo tokea hapo ingetumika kama
chombo au kifaa cha kumuadhibia (wanasema kina Nachmanides na Sforno; Soncino).
Bullinger anaamini kuwa lafudhi au usemi wa Kiebrania unaoonekana mbele ya neno
laana inaonyesha kuwa ilikuwa ni
laana iliyo zaidi ya kulaaniwa kwa ardhi (kama kwenye sura na aya zifuatazo:
3:17; hadi aya ya 11 kwenye Comp. Bible).
Wazo ni kama hilo
la haki kwenye adhabu. Uhai ulichukuliwa na uhai ndiyo pekee uliochukuliwa
kuwezeshwa tu kwa njia ya kufanya kazi nguvu.
Kaini akamwambia
Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama,
umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami
nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye
ataniua.
Tafsiri iliyoko
kwenye KJV na ile iliyo kwenye Soncino ni tafsiri iliyofanywa na Abraham ibn
Ezra. Hata hivyo, Rashi anaiwekea maswali yafuatayo: Je, dhambi yang uni kubwa sana kuweza kuibeba? na Nachmanides anaiweka
hii kwa usemi wa kwamba lakini dhambi
yang uni kubwa sana kuweza kusamehewa (Soncino). Je, uovu wangu ni mkubwa sana kuweza kusamehewa? Inatokana na
uandishi wa nakala za Septuagint, Vulgate, Syriac, Arabic, Targum wa Onkelos,
Torati ya Wasamaria(Samaritan Pentateuch) na ya Kiyunani na ya makasisi wa Kilatini.
Ni tafsiri iliyofuatia baadae ya MT inakubaliana nayo, au inaweka msingi wa ile
ya KJV unapoisoma (sawa na Comp. Bible sura hiyohiyo hadi aya ya 13). Dhana
iliyoko hapa kwenye aya ya 14 ni kwamba aliondolewa mbali na usoni pa nchi na
kutoa uhai wa mtu mwingine. Aliondolewa au kukatiliwa mbali kutoka kwenye uwepo
wa Mungu na uwezekano way eye kutoa sadaka kwa aibu (inasema Nachmanides).
Hapa kuna
mlolongo wa matatizo yanayoshangaza. Kila mtu atakayekutana na Kaini atamuua ni
maneno mageni kusikika na hasa kwa kuwa ilijulikana kwamba ni watu wawili tu
wanaume ambao ni yeye Kaini mwenyewe na Adamu baba yake ndio waliokuwepo eke
yao juu ya uso wa dunia kipindi kile. Ni wazi sana kwamba kulikuwa na kitu
kingine zaidi kilichokuwepo kuendelea pia. Nachmanides na Rashi waliliona
tatizo fulani kwa dhahiri kwenye mchakato wa uumbaji na wakaitafsiri ayah ii
kumaanisha kitu chochote na kuichukulia aya ya 15 kuwa ilikuwa inawaongelea
wanyama wa porini.
Mtazamo wa Nachmanides
ulikuwa ni kuwa, Kaini hakujenga nyumba kwa ajili ya kujilinda na pasipo ulinzi
wa Mungu angeuawa na wanyama wa porini.
Usemi usemao wataniua ulichukuliwa kama unaashiria
adhabu iliyokuu zaidi ya hukumu iliyotangazwa (Nachmanides na Sforno)
Maneno
yaliyotamkwa na Yahova elohim hapa yametafsriwa kwa namna hiyo na marabi wa
Kiyahudi, ambayo inaashiria kuwa ndiyo mtazamo ulioelezwa kwenye Agano Jipya.
Bwana akamwambia,
Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana
akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Aya ya 15 imetafsiwa
na Rashi kama ifuatavyo:
Kwahiyo yeyote atakaye muua Kaini ataadhibiwa (kifungu na usemi huu unabakia ukiwa
haujafafanuliwa vizuri); kama ulikuwa unamhusu Kaini mwenyewe, kuwa kisasi kitafanywa
juu yake baada ya vizazi kadhaa vilivyomfuatia (atakapouawa, lakini hadi
kutakapokuwa hakuna aliyemdhuru). Ibn Ezra, Nachmanides na Sforno wanaandika
namna inayofanana lakini Sforno imeandikwa vipindi vitatu vya sabini na mbili au
sabini na mbili mara tatu, sawa na baada ya vizazi kumi na nne. Vizazi kumi
na vinne vimetolewa kutoka kwa Ibrahimu kwenye mlolongo wa vizazi vitatu kwenye
kitabu cha Mathayo. Lakini vizazi kumi na vinne kutoka Adamu vinaangukia kwa Sila
baba wa Eberi na kwa mtazamo huu Waebrania walitajwa lakini kulikuwa hakuna
kanuni yoyote kwa mlolongo huu wa vizazi kumi na vinne. Kwa hiyo Sforno hayuko sahihi. Vizazi saba vina
umuhimu sana. Sforno angekuwa sahihi kama ingechukuliwa kwa kuashiria kwamba
vizazi saba vimetajwa kwenye mistari miwili ya uzao wa Sethi na Kaini pekee.
Kaini akatoka mbele
za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni. 17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba,
akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe.
Kwa hiyo, Kaini
akaishi katika nchi ya Nodi au nowd (SHD
5113) ambayo ni nchi iliyo upande wa mashariki mwa Edeni. Ni sawa kama
ilivyoandikwa kwenye kamusi ya SHD 5112 na inamaanisha vuruvuru au tangatanga. Hii
ina maana iliyo kinyume na SHD 5115 na 5116 navah
maana yake kupumzika na kwa hiyo ni nyumbani au makao na pia kuliendeleza au kulipanua hekalu la Mungu na pumziko
lake. Maana lengwa ya maneno haya ni kukatiliwa mbali kutoka kwa Mungu na kwa
lugha ya Kiebrania inaliendeleza kwa kina wazo hili wakati kwenye Kiingereza
hakifanyi hivyo. Dalili iliyoko hapa kuhusu nchi ya kutangia tangia ni muhimu
katika kulipa wazo kuwafikiria viumbe wengine kuwepo duniani. Alipigwa chapa au
alama kwenye kipaji cha uso wake na mamlaka mbalimbali za marabi zimetafsiri
hii ikimaanisha kwamba alama iliyowekewa inaweza kuwa ni herufi za jina lake.
Rashi anadhania kuwa Mungu aliweka woga wa kiasilia ya mwanadamu kwa wanyama
kufuatia wazo la kwamba walikuwa ni wao waliomtisha. Ibin Ezra anaamini kuwa
Bwana alimuwekea alama Kaini ili kila atakayekutana naye asimpige na kumdhuru
au kumuua. Kwa hiyo, tunaona kwamba walikuwapo watu wangalioweza kumpiga na
kumuua Kaini angali badi hai hata wakati ule. Ni nani basi hawa?
Kaini alitoka
na kuondoka zake kutoka machoni au mbele za Bwana. Andiko linasema kwa kifupi
tu kwamba alimjua kewe baada ya kuondoka kwake na kuelekea nchi ya Nodi. Alipata
uzao au watoto. Baada yam tota ke Enoshi kuzaliwa, Kaini aliujenga mji na na
akauita kwa jina la mwanae, Enoshi. Enoshi maana yake fundisho au chuo; kwa
hiyo maana yake inakuwa ni ni mwanafunzi
wa au kufundisha. Majina yanayohusu mji ni: alikuwa anajenga kwa maneno mengine ni
mchakato endelevu. Alikuwa amelaaniwa na kwa hiyo aliuita mji ule kwa jina la mwanae
na inaonekana kuwa alikuwa anajaribu kujiondolea laana (sawa na asemavyo
Nachmanides; Soncino).
Bullinger anaamini
huu kuwa ni mji uliokutikana chini ya uwanda wa matofali ulioko huko Nip[p]ur upande
wa Kusini mwa Babeli uliojengwa (sawaa na sura hiyohiyo hadi aya ya v. 17 kwenye
Companion Bible). Bullinger anaamini
kuwa ugumu wa Kaini inatoka kwenye Kizazi
cha Mbinguni na Duniani waliozaliwa baada ya kuuawa kwa Abeli.
Henoko akamzaa
Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli
akamzaa Lameki.
Majina yaliyo
kwenye orodha hii yanamaana kubwa sana. Iradi maana yake mkimbizi (SHD 5897 sawa
na 6166). Bullinger anauona huu kama Mji
wa Mashahidi lakini hana uhakika na hilo. Mpangilio wa miji ya makimbilio
kama unavyoonekana kwenye totati unaweza kuwa ni mapema sana kabla ya matendo
au matukio haya ya Kaini.
Hii kwa hiyo
ingeashiria kiwango cha sheria au kanuni zikiwepo kwenye ukamilifu tangu
mwanzo. Kutoka nje ya mji wa mafunzo au
kuhitimisha, kumtenganisha na Mungu, akawa mkimbizi.
Mehuyaeli (kwa
Kiebrania Mehijael sawa na Soncino;
SHD 4232 sawa na 4229, 410) maana yake Aliyepigwa
na Eli, au Mungu. Hii hatimaye
kumtangulia Methusela (SHD 4967 sawa na 4962) maana yake Mtu ambaye ni Eli au Mungu.
Somo la
kujifunza hapa linaonekana kuwa ni maswali ya kujihoji yanayopelekea mtengano
na kisha kujifunza katika muundo ambao ulipelekea yeye kuwa mkimbizi. Kwa
uumbaji wa Mungu mwanadamu anaweza kutembea chini ya maelekezo ya Mungu.
Kwa hiyo
mchakato ulimtoa Lameki. Lameki ni wa saba kwenye mlolongo wa uzao wa Adamu.
Lameki, kwa mujibu wa SHD 3929 Lemek ni
mtu asiyezoeleka na kiini cha kabila la Waebrania kwa maana isiyo rasmi.
Inataja mababa wawili, mmoja kutoka kila upande kutoka Adamu. Kwenye upande wa
Kaini, Lameki ndiye wa saba kwenye
mlolongo wa uzao wao toka Adamu. Kwenye mstari mwingine, Enoshi ndiye alikuwa
wa saba ambaye anaitwa kwa jina lenye maana ya kizazi cha tatu na motto wa
Kaini. Kwa hiyo, ujumbe ni kwa mlolongo na usawa wa mafunzo kama yote
yanavyomaanisha kufundishwa au kuwezeshwa na kufanywawa wanafunzi. Mmoja, Enoko alikuwa mtakatifu na wengine
hawakuwa hivyo. Kwa hiyo, kipindi na mchakato wa mafunzo ni lililo gumu kulijua.
Lameki kwenye
mlolongo wa uzao wa Kaini ni mtu wa
kwanza kuandikwa kuwa na wake wawili. Rashi anaamini anapolinganisha na andiko
hili kwamba tendo la kawaida la kizazi cha gharika kuu kilijulikana kuwa ni
watu walioishi na mke mmoja kwa kusudi la kuzaa watoto na wengine ni kwa ajili
ya kuendeleza makazi yao (sawa na anavyoamini Soncino). Huenda hii inatokana na mtazamo wa marabi
unaotokana na majina yalivyo.
Lameki akajitwalia
wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.
Kwa mujibu wa
Rashi, Ada anaonekana kurudi nyuma na
kwa hiyo alikuwa kwa ajili ya kuzaa watoto na aliruhusiwa aendelee kuwa mbaya
na mume wake aliachana naye au alimuacha (sawa na anavyosema Soncino). Maana ya
neno lake kwa mujibu wa Strong linamaanisha kinyume chake. Jina hilo kwa mujibu
wa SHD 5711, linadhaniwa kumaanisha Manukato
na limechukuliwa kutoka kwenye SHD 5710 ‘âdâh ambayo inamaanisha kuendelea na kwa hivyo inamaanisha kupitisha au kuendelea na kusababisha kuondoa’
hasa inamaanisha kurembesha au kuinukiza manukato na kwa hiyo inaweza
kumaanisha kupamba, kuremba mtu mwenyewe,
kupitiwa, au kuchukulia mbali.
Sila (au Tsillâh SHD 6741) anachukuliwa na Rashi kuwa alikuwa ni wa kustarehe naye
tu na hivyo kumfanya wakati wote kwenye matukio yake ama kuwa karibu naye (tsêl
au kuwanaye pamoja). Kwa hiyo, jina lake linamaanisha kivuli (soma Soncino). Jina hili ni la kike, kwa mujibu wa SHD 6738
tsêl ambalo linaaminika kumaanisha kivuli lakini linaweza pia kumaanisha ulinzi. Kwa hiyo majina yanaweza
kumaanisha shambulio na ulinzi au kinga njema kwa maana iliyotolewa na Rashi. Hii ina zaidi ya
kufanya kwenye matatizo ya kiroho ya malaika, ambayo yalipelekea maangamizo ya
gharika kuu na yanapaswa kufumbuliwa. Jambo hili linapelekea kwa maana maneno
ya watoto.
Ada akamzaa Yabali;
huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama. 21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba
yao wapigao kinubi na filimbi.
Yabali (SHD
2989) alikuwa ni baba yao wapiga filimbi na aliishi hemani na wao pamoja na
mifugo. Hii inaweza kuwa vigumu kupata maana rahisi kama Abeli alikuwa ni mfugaji
wa kwanza kama tulivyojionea hapo juu na alitoa sadaka yake kwa Bwana, ambayo
ilikubalika sana kuliko ile aliyoitoa Kanini ya nafaka. Neno linalotumika
kulitaja hema hapa linamaana moja na ile ya hekalu za sanamu na Midrash anatangaza
kuwa alikuwa wa kwanza kujenga hekalu za kuabudia sanamu na kuwatolea sadaka.
Ndipo tunaona kwamba Ada ana kanuni ya kupamba
kwa mtindo tofauti na sanamu na ndipo akapitiwa
au hakuachwa au hakurudi nyuma (soma jarida la Mwanzo wa Kuvaa Bangili na Vito vya Dhahabu Katika Zama za Kale (Na. 197)
[The Origin of the Wearing of Earrings and Jewellery in Ancient Times (No. 197)].
Jina Yubali
(SHD 3106) baba wa wote wanaopiga vinubi na filimbi alitokea kuwa kutoka SHD
2986 na inamaanisha kijito. SHD 2987 inamaanisha
kuleta au kubeba na ni sawa na 2986. Hii ina maana sawa na kiini kama Yubali
(SHD 2989) ambalo lina maana sawa na ile ya SHD 2988 chanzo cha maji au kijito.
Rashi anafuatia
kutoka kwenye maelezo ya mwanzo na anasema kwamba alikuwa wa kwanza kuutambulisha
(kuuleta au kuubeba) muziki kwenye ibada za sanamu.
Maelezo yaha na
ufafanuzi wake vimeelezwa kwa kina kwenye majarida ya Chanzo cha Krismas na Easter (Na. 235) na Fundisho la Chanzo cha Dhambi Sehemu ya 1
Bustani ya Edeni (Na. 246) [The Origins of Christmas and Easter (No. 235) and The Doctrine of Original Sin Part I The Garden of Eden (No. 246)] tunaona kwamba imani ya Utatu ilikuwa ni mtindo wa kale zaidi ya ibada za sanamu.
Ilichukuliwa kutoka kwa ulimwengu wa kipindi cha kabla ya gharika kuu sawasawa
na tutakavyojionea kutoka kwa mabaki yao, kama vile yale ya Stonehenge.
Ufafanuzi na
maelezo ya Rashi yanaangukia kusema kuwa Sila alikuwa na watoto pia na jina
lake la kiume aliitwa Tubalkaini ingawa haonekani kuona vyema yeye mwenyewe.
Rashi na Ibn
Ezra wameandika mghushaji kama kinoleo (sawa na Soncino).
Sila naye akamzaa
Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake
Tubal-kaini alikuwa Naama.
Tubal-kaini aliendeleza
vema (tabal) kazi ya Kaini, akiandaa silaha
kwa kuulia watu au umwagaji wa damu (kila
chombo chenye makali au cha kukatia)
kwa mujibu wa Rashi, ambayo inamaanisha majambia na visu (anasema Soncino). Kitabu
cha Soncino kimeandikwa kuwa andiko hili kama mtengenezaji wa kila chombo cha kukatia chenye makali cha shaba ba
chuma. Tafsiri ya KJV na maandiko mengine yanaonyesha kwamba kulikuwa na watu
wengine waliofundishwa na yeye. Nachmanides analichukulia andiko hili kama
lilivyo na kuongeza maelezo ya Targum kwamba neno baba yao linamaanisha alikuwa
wa kwanza kutengeneza vifaa hivis (sawa na Soncino). Hili ni sawa na
tunavyosema kuwa Shetani ni baba wa uwongo kuwa ni sababu inayotokana nay eye
kuwa wa kwanza kusema uwongo na kuwafundisha wengine kufanya hivyo. Inaweza
kuchukuliwa kumaanisha kuwa Tubalkaini alikuwa ni chombo katika kutengeneza silaha
za vita kwenye ulimwengu wa zama za kabla ya gharika kuu.
Dada yake
alikuwa Naama (SHD 5279) ikimaanisha wa kuipendeza ambalo ni la mrengo wa
kike SHD 5277 Na’am maana yake burudani au kupendeza. Rashi anasema kuwa Naama alikuwa ni mke wa Nuhu (sawa
na Soncino). Jina hili linaonekana hatimaye tena kwa Waamoni. Madiu ya kuwa
alikuwa ni mke wa Nuhu bila shaka yametolewa ili kuelezea matatizo ya Wakanaani
na ndugu zao. Inaonekana hakumaanishi kujumuishwa kwake hapa zaidi ya
kumuunganisha na matatizo yaliyojitokeza kutokana na ibada potofu
zilizojitokeza kutokana na imani ya mungu wa Utatu na miungu Mwezi, Jua na sayari ya Venus, Utatu uliofanyizwa kutokana
na imani za Kibabeloni (sawa na jarida la Ndama wa Dhahabu (Na. 222) [The Golden Calf (No. 222)]. Alama ya sayari pia inafuatia utaratibu huu
unaohusiana na Mjumuisho wa msalaba wa jua kwa dunia ukionekana hivi Å, pamoja na Venus akiwa mwanamke na Mars kama
mwanaume (sawa na sehemu ya 1 na jarida la Msalaba: Chanzo Chake na Maana Yake (Na. 39) [The Cross: Its Origin and
Significance (No. 39)]. Mlolongo huu unawakilisha mgawanyo wa
pande robo ya ulimwengu na kwa hiyo serikali inawekwa duniani.
Lameki akawaambia
wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni
usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua; 24 Kama Kaini
akilipiwa kisasi mara saba, Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba.
Andiko hili
tata lina uwezekano mdogo. Mapokeo ya marabi yanasema kuwa Lameki alikuwa
kipofu na alikuwa anaongozwa na Tubalkaini. Siku moja Tubalikaini alipomuona
Kaini, alimwambia Lameki kuwa kulikuwa na paa mbele yake na akamuomba ampige
kwa mkuki ambao ulimuua. Ndipo Lameki alipogundua kuwa alikuwa amenuua mtoto
wake. Hii iliwachukiza wake zake ambao walijitenga naye. Rashi anasema kwamba
hatimaye alijaribu wakurejesha kwake. Wengine kama vile Nachmanides na Sforno, wanaamini
kuwa wale wakeze waliogopa kuwa huenda angeuawa naye akawahakikishia usalama wao
(sawa na Soncino).
Mlolongo huu ndipo
unaendelea tangu Adamu hadi Lameki kupitia kwa Kaini kama vizazi saba kilichokatiliwa
mbali na Mungu na hatimaye Kaini aliuawa na kizazi hiki cha saba kutoka Kaini
kilichoitwa cha Tubalkaini. Kwa hiyo, mlolongo ulirudiwa tena. Lameki alikuwa
kwenye juhudi kubwa ya kujiona hana hatia na hatimaye akalipizwa kisasi mara
sabini na saba zaidi. Muono wa marabi ni kwamba lilikuwa ni swali nyeti na
halikuhitaji uwajibikaji kwa mauaji yale ambayo Lameki alimuua Kainni kwa
bahati mbaya. Utata ulioko ni kwamba kwa namna yoyote ile Kaini alikuwa na alama
ya ulinzi aliyowekewa na Mungu na kwa hiyo Yule aliyemuua alipaswa kuadhibiwa
mara saba ya sabini.
Lameki bila
shaka alichukua mahala pa hukumu ya Mungu. Hii ni namna nyingine ya kuitendea
kazi sheria inayohusiana na amri ya tano. Soncino inaamini kwamba kwa maelezo
na fafanuzi zote, mwanadamu anaonekana
kuwa alimdanganya Lameki na kijana wa
kiume kwa Tubalkaini. Hata hivyo, hii inaonekana kuwa ni upuuzi. Mtazamo ni
kwamba mtu aliyeuawa kwa kumchubua au kujeruhi Lameki alikuwa Kaini na mtu
aliyemchubua alikuwa Tubalkaini. Lameki aliumizwa kwenye mnyororo wa uzao wao
kwa kukatiliwa mbali na Mungu na kuchubuliwa kwa kuwa mtoto wake mwenyewe ndiye
alikuwa ni mhusika way eye kumuua Kaini. Kizazi cha saba cha Adamu kilikuwa ndicho
kimemuua Kaini na mchokozi aliuawa pia.
Rashi anaamini
kuwa ni hatua muhimu sana kuhusianisha na andiko hili. Anasema kwamba
inamaanisha kwamba kama hukumu ilicheleweshwa kwa vizazi saba kwa Kaini ndipo
kwa jambo hili lingecheleshwa kwa vizazi sabini na saba. Gharika kuu ikatokea
sio mbali sana tangu hapo na hakuna maelezo mengine ya kina kutolewa kuhusu
kizazi hiki cha Lameki hadi kufikia watoto hawa waabudu sanamu wa Ada.
Dini ya uwongo
ya Utatu kwa kweli iliingia hadi katika kizazi hiki cha sabini na saba na
hatimaye ilipata mwanya zaidi kwenye Ukristo miaka elfu tatu iliyofuatia baadae
kwenye karne ya saba ya ya nane ya zama hizi tulizonazo. Dokezo linaloonekana
kuchukuliwa hapa kuhusu imani za dini hizi za uwongo. Kwa hakika, mstari wa
uzao wa Kaini wa Wanefili walifutiliwa mbali kwenye gharika kuu. Hakuna kitu
kilichosemwa zaidi hapa kuhusu upande wa uzao wa Kaini hadi tunapokutana na
maandiko yanayowataja Wanefili kwenye Mwanzo 6:4. Madai ya kwamba Naama na Nuhu
walikuwa mke na mume huenda yanaweza pia kutuama kwenye unabii huu uwe na msingi
fulani kwa kweli.
Mstari wa uzao wa Sethi
Tunarudi nyuma
tena hadi kwa Adamu na kuzaliwa kwa Sethi.
Adamu akamjua mke
wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema,
Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.
Sethi (SHD 8352
Shêth) maana yake ni aliyechukua nafasi
mbadala na linatokana na SHD 7896 shîyth
linalomaanisha kufidia (Huenda hii
ndiyo sababu pia ya neno la Kiingereza sheath
(ngao) kwa ajili ya silaha).
Sethi naye akazaa
mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la
Bwana.
Tangu kipindi
hiki watu walianza kuliitia jina la Yahova/ kwa hiyo, madai ya kwamba jina hili
lilikuwa halijulikani hadi walipofika Sinai ni ya uwongo. Torati au sheria ilitolewa
na kupewa wanadamu tangu mwanzoni na Yahova alikuwa ni sehemu mfumo na
utaratibu uliotolewa. Ile inayojulikana kama Sheria za Nuhu ni uwongo wa marabi
tu ili kuhalalisha na imehalalisha dini za Wababeli na Talmud. Zinapaswa kuwa
na msimamo wa njia panda kati ya kukosewa, mapokeo yasiyo wezekana na dhana
nyinginezo maarufu, wanaosoma Biblia lakini bado wapo kwenye ushawishi wa imani
ya Utatu.
Madai ya kwamba
ilikuwa ni baada ya vizazi viwili ndipo walipoanza kuliitia jina la Bwana
yanaonyesha kukusudia kutenganisha na Mungu na umuhimu wa kufanya hivyo kupitia
majaribu na mateso.
Mwanzo 5:1-32 Hiki
ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya
Mungu alimfanya; 2 mwanamume na mwanamke aliwaumba,
akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.3 Adamu
akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake,
akamwita jina lake Sethi. 4 Siku za Adamu baada ya
kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. 5 Siku zote
za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
Kwenye andiko
hili tunajionea urefu wa kipindi cha Mababa ukionekana. Adamu alikuwa hai
wakati wa kuzaliwa kwa Sethi na mtoto wa Sethi na mtoto wake na kadhalika kwa
vizazi vyake kadhaa. Zaidi ya yote, uwezo wa kuwachunga wanawake pia uliongezeka
kwenye kipindi hiki kirefu. Wana
na binti waliozaliwa na Adamu na Hawa ia wameongezeka. Hawa alimchukua mtoto
kipindi kirefu cha nyuma wakati alipokuwa na umri wa miaka 130 na kwa kweli
alipokuwa na umri wa miaka.
Sethi akaishi miaka mia na mitano,
akamzaa Enoshi. 7 Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi
miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake. 8 Siku
zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.
Ni sawasawa tu na
Sethi aliishi kipindi kimoja na “Adamu” baba yake na mama yake kwa miaka mamia.
Sethi alikuwa ni wa mbadala au alichukua mahala pa Abeli kiumbe aliyeishi kipindi
kifupi cha mpito na aliyeuawa. Enoshi alikuwa ni mtoto wa kwanza wa Sethi na
jina lake maana yake ni mwenye kufa (sawa
na Strong’s HD 582 ‘enôwsh na 583) na
haina heshima kuliko ile ya kwenye SHD 120 Adamu
maana yake pia ni mwanadamu. Kwa hiyo
kuna mabadiliko kwenye daraja la mstari wa kizazi cha Adamu kwa ajili ya chanzo
cha dhambi.
Enoshi akaishi miaka tisini,
akamzaa Kenani. 10 Enoshi akaishi baada ya kumzaa
Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake. 11 Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.
Kanaani (SHD
7018 Qêynân) alikuwa mtoto Enoshi.
Jina lake linatokana na kamusi hiihii ya SHD 7064 imerekebishwa na 7077 maana
yake kusimamisha kwenye mtazamo wa ujenzi au kumiliki kama kiota.
Kenani akaishi miaka sabini,
akamzaa Mahalaleli. 13 Kenani akaishi baada ya kumzaa
Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake. 14 Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.
Mtoto wake aliitwa
Mahalaleli ambalo ni mjumuisho wa maneno mawili SHD 4110 mashuhuri au sifa na 410 el au Mungu. Hivyo basi jina hili maana
yake ni msifu Mungu. Tunaona hali bhapa kwamba kutoka kwenye usimamishaji mzuri
wa nyumba na kumlea kijana kumsifu Mungu ndiko kunatakiwa kuanzishwe kiusahihi.
Mahalaleli akaishi miaka sitini
na mitano, akamzaa Yaredi.16 Mahalaleli akaishi baada
ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake. 17 Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na
mitano, akafa.
Yaredi alikuwa
mtoto wa kwanza wa kiume wa Mahalaleli. Jina lake Yered (SHD 3382) maana yake
ni heshima au mwenye kuheshimika. Ingawa njia sahihi ya kuilea nyumba na
familia kwa heshima na marejesho ya Mungu yawe yanawezekana.
Yaredi akaishi miaka mia na
sitini na miwili, akamzaa Henoko. 19 Yaredi akaishi
baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. 20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na
miwili, akafa.
Yeredi akamzaa Enoshi
ambaye tumeona maana yake kuwa ni kufanyizwa
au kufundiswa (SHD 2585 Chanowk ambalo linatokana na kamusi ya
SHD 2596 kubananisha maana yake ni kushamirisha au kuadibisha). Kwa hiyo, kupitia na heshima ya Mungu kufundisha mwenendo
wa mwanadamu kufanya iwezekane. Ndipo mwanadamu akamilike. Hii ni tofauti na
kuweka kitu mbadala ya jina la wana wa Kaini ambao Enoshi alikuwa wa damu moja
na Kaini kupitia kukamatwa na kumilikiwa na Mungu. Hii ndiyo tofauti iliyopo
kati ya mistari hii miwili. Kwa Mungu mmoja alijieneza mwenyewe kwa kupenda
ajifunue na kuwainua watu kwa ajili yake mwenyewe. Kwa upande mwingine ni
kusema kwamba Kaini alitafuta kushikilia masharti yale na akaua kufanya hivyo.
Hii ndiyo tofauti iliyoko kati Kristo na Shetani kwenye Wafilipi 2:5-8.
Wafilipi 2:5-8 Iweni
na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye
hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya
mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena,
alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti,
naam, mauti ya msalaba.
Adamu na mstari
ule kupitia kwa Sethi pia walikuwa
kwenye maisha ya ucha Mungu bali hawakujihesabia kuwa sawa na Mungu ni kitu cha
kukishikilia. Huu ulikuwa ni mwanzo wa dhambi bali haikuwa ni dhambi ya Adamu
peke yake. Dhambi ile ilifanywa na Shetani ambaye hatimaye alimshawishi Hawa
kuifanya kwa muktada kama ule ule. Naye akamshawishi Adamu kuitenda. Ndipo mstari
wote mzima ukaathirika na kuwa dhaifu kuliko ungalivyokuwa. Ni pale tu kwenye mstari
ulio kwenye mchakato mpya ndipo mwanadamu angeweza kufanikiwa na kwamba kupitia
kwenye uzao na mwingilio kati wa Yahova-elohim ambaye hatimaye akifanyika kuwa
mwanadamu kwa maongozi ya Mungu Aliye Juu Sana, Eloa, Mungu wa Pekee na wa
Kweli aliyemtuma Masihi aje kuwakomboa wanadamu (soma Yohana 17:3). Uzoefu huu
uliofichika wa dini siri inayotuama kwenye imani zisizo wazi zilizoshika nyoyo
za Wababeloni ni kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu na ufunuo wake mwenyewe.
Inatafuta na kulenga kujiinua juu na kujiunganisha na Mungu katika uholela na
imani yenye usiri au msingi wa kihisia.
Henoko akaishi miaka sitini na
mitano, akamzaa Methusela.22 Henoko akaenda pamoja na
Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. 23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na
mitano. 24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye
akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
Henoko
alitembea na Mungu na ndipo Mungu alimtwaa. Henoko alionyeshwa mchakato wa
mwisho na alichukuliwa akafanye shughuli nyingine. Na ndivyo alivyofanywa Eliya
pia na hawa ndio wanadamu wawili peke yao waliotwaliwa pasipo kuona mauti. Ibin
Ezra anakiona kitendo hiki kama tunu ya heshima.
Lakini watakufa
hatimaye kama ilivyoandikwa kwamba watu wote lazima wafe mara moja (Waebrania
9:27 sawa na jarida la Mashahidi (PAmoja na Mashahidi Wawili) (Na. 135) [The Witnesses (including
the Two Witnesses) (No. 135)].
Henoko alionyesha kwa
namna hii kama Masihi ni sawa pia kama alivyofanya Eliya. Henoko alikuwa pia
baba yake Methusela. Kwa mujibu wa mapokeo, mke wake alikuwa anaitwa Edna (sawa
na kitabu cha M. A. Knibb, kinachoitwa The
Ethiopic Book of Enoch, 85:2, Vol. 2, [Kitabu
cha Historia ya Henoko cha Waethiopia] Oxford Clarendon 1982 p. 195).
Methusela (SHD 4968 methûwshelach) maana
yake ni mtu wa kukurupuka. Limechukuliwa
kutoka mjumuisho wa 4962 na 7973. 4962 Math
(kutokana na maana hiyohiyo kama ilivyo kwenye 4970) inayomaanisha mtu mzima kutoka kwenye dhsns ys kufikis urefu kamili. Alifikisha urefu
kamili wa miaka. Neno lililo kwenye 7973 shelach
linamaana ya mzinga wa kushambulia kama
vile mkuki. Kwa hiyo ni mtu wa kukurupuka. Hii ingetatanisha kama
isingekuwa na ukweli kwamba inamaanisha pia kuwa chipukizi likualo kwa wazo hilohilo linalomaanisha mkuki wa mmea na
ndipo inamaanisha Tawi na pia ni
ukurupukaji au ukuaji. Pia inamaana ya mtu
mwenye Tawi. Kwa hiyo maana yake inapelekea kuwa na maana mpya tunapogundua
kuwa Kristo alikuwa ni mtumishi wa Mungu ambaye ni Tawi (SHD 6780 tsemach maana yake ni kuchipuza au kupiga au chipukizi).
Kama Henoko, Kristo
alikubalika kwa Mungu na Mungu alimchukua. Uzao wake, Kanisa ambalo walikuwa wanaume wa kurupuka au chipukizi au tawi. Dunia haitaanoch Christ was acceptable to God and God took higamizwa
hadi kanisa litakapokuwa limetimiliza siku zake na wale 144,000 watakapopigwa
mhuri nao na wengine wengi watakapotolewa watoke duniani. Ndipo ule mwisho utakapokuja.
Maana yaje ni
kwamba hii inampendeza Mungu na kukubalika na inaongeza siku za mtu za kila
mzawa/ kanisa ni familia na uzao wa wateule. Kwa hiyo maezi ya watoto hayamaanishi
lazima kuufikia wokovu. Wateule hata hivyo, wanatakiwa wawalee na kuwafundisha
warithi wao na kulisaidia taifa. Mchakato huu unauhusiano wa moja kwa moja na
kanisa. Ile dunia waliyokuwamo wao kama
ilivyojulikana haikuangamizwa hadi Methusela alipotimiliza siku zake na mwaka
aliokufa ndio gharika kuu ilipokuja. Kitabu
cha Waethiopia cha Historia ya Henoko kinaonekana kufanana na historia
nzima yote hadi kipindi cha nyuma cha anguko la malaika na uingilianaji
uliojitokeza wa malaika na wanadamu na kinataja Meli nyeupe na meli nyingine
kumi na mbili (moja iliyotolewa kwa majeshi menguine, kama ya Yuda) na kukiwa
na meli nyingine nyingi zilizotawanyikana hapo. Hii inaonekana wazi kuwa
alikuwa anaonyeshwa kanisa (Knibb ibid., p. 195-202ff.).
Methusela akaishi miaka mia na
themanini na saba, akamzaa Lameki. 26 Methusela
akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa
wana, waume na wake. 27 Siku zote za Methusela ni
miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
Methusela
akamuacha wanae Lameki. Maana ya jina Lameki yatakuwa yamepotea kwenye uovu.
Wote wawili wanaonekana kama kwa vyovyote vile ni wakomeshaji wa ulimwengu wa
zama za kabla ya gharika kuu. Huyu Lameki wa Methusela alikuwa ndiye baba wa
Nuhu na Lameki wa mstari wa Kaini pia ni baba wa Naama, ambaye Rashi anaamini
kuwa alikuwa ni mke wa Nuhu na kwa hiyo anaunganisha pande zote mbili. Wana wakengeufu
na waabudu sanamu wa Ada wanaaminika kuwa walikufa na ni yeye tu peke yake
kutoka upande ule aliyeokoka. Huenda haya ni mafundisho tu ya marabi ya Roshi
akielezea kilichotokea baada wa Wanefili baada ya gharika kuu.
Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili,
akazaa mwana. 29 Akamwita jina lake Nuhu, akinena,
Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika
nchi aliyoilaani Bwana. 30 Lameki akaishi baada ya
kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake. 31 Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba,
akafa. 32 Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu
akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.
Siku za Lameki
ni jumla ya miaka mia saba na sabini na saba ambao ni mlolongo kamili na
timilifu na unasimama kwenye mkanganyo wa moja kwa moja ulio kinyume na
tarakimu ya mnyama au ya Shetani ya mia sita sitini na sita. Mchakato wa
kitarakimu ya Kiutatu au ya mnyama haupo tu kuwa ni kitu kilichoanzishwa katika
kaanisa la karne ya kwanza. Mkanganyo na tofauti iliyopo ni ile inayosimama
kama Shetani na itikadi yake dhidi ya kanisa na imani halisi ya Mungu chini ya
Masihi. Matokeo ya mwisho ya mlolongo ule wa uzao ulikuwa ni mwandamano kamili
wa wana wa Mungu.
Kama
alivyofanya kwa suala la gharika kuu, Mungu atafanya maangamizo kuiangamiza
dunia katika siku za mwisho na ndipo hadithi yote itafikia kkomo chake kutoka
mwanzo hadi mwisho wake na kueleweka kirahisi kwa mafundisho ya manabii wa siku
za mwisho na Kanisa. Mchakato wa muda hata hivyo unahitimisha mpango wa uumbaji
wa jumla ya kipindi cha millennia saba.
Anguko la Malaika
Kuelewa Anguko
la la Malaika ni jeraha kubwa sana kwa undani sana hakika katika uumbaji wa
wanadamu na mwingiliano wa kingono waliouliofanya na binti za wanadamu. Hii
imeelezewa kwa kina kwenye jarida la Wanefili (Na. 154) [The Nephilim (No. 154)] lakini imeelezwa hapa katika uhusiano na maandiko
ya kitabu cha Mwanzo na maandiko mengine ya marabi na inavyoonekana kwenye
Fundisho la Asili au Chanzo cha Dhambi.
Mwanzo 6:1-8 Ikawa wanadamu
walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni
wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 Bwana
akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni
nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 4 Nao
Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu
walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu
hodari zamani ,watu wenye sifa. 5 Bwana akaona ya kuwa
maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni
mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa
amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 Bwana
akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na
mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba
nimewafanya. 8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa
Bwana.
Andiko lililoko
kwenye Mwanzo 5:32 linaonyesha kuwa Nuhu alikuwa na umri wa miaka mia tano
alipowazaa kina Shemu, Hamu na Yafethi. Kuna maelezo yanayotolewa na marabi
kuhusu sababu mbalimbali kuhusu kuchelewa kuzaa kwa Nuhu. Moja wapo nay a
muhimu kuhusu kuchelewa kwake ilikuwa ni kwa sababu za kusafisha uzao chafu
uliokuwepo kati ya mpya wa kwake na ule wa zamani pamoja na imani zao na
uadilifu wao wa matendo yao yaliyokuwa nyakati za Nuhu. Rashi anaamini kwamba
wakati Yafethi alikuwa mzaliwa wa kwanza, Shemu ametajwa kwanza kwa kuwa
alikuwa ni mtu mwenye haki na inasemekana kwamba alizaliwa akiwa ametahiriwa
(sawa na anavyosema Soncino). Hii ni ishara inayoonyesha agano la Ibrahimu na
inaonyesha kwamba uhusiano ulijulikana na marabi kabla ya gharika kuu. Na ndiyo
maana kwa mtazamo huu tunaona kwamba imani kuhusu Sheria za Nuhu sio sahihi (sawa
na linavyosema jarida la Melkizedeki (Na. 128)).
Kwenye andiko
la Mwanzo 6:1 tunaona kwamba mafundisho ya marabi yana rahibu kwa namna yoyote
ile. kwenye aya ya kwanza Rashi anafafanua kuhusu hawa wana wa Mungu ambao wana
wa elohim na kwa mtazamo huu Rashi anaona hawa kuwa ni wana wa wafalme na wakuu
ambao elohim anaonyesha kusimama
imara na Mungu na kwa hiyo kuwa ni uongozi au mamlaka na inafanya rejea yake
kwenye Kutoka 4:16; 7:1. Walipaswa kuilinda imani lakini walifanya machafuko ya
dhahiri. Nachmanides anakubaliana na mtazamo huu (sawa na Soncino). Haya ni matumizi ya Elohim ambapo kila
misimamo ni imara kwa Eloa. Jambo la kuelewa ni hili, kwamba elohim ni jina la
uwingi la mjumuisho wa jamaa ya Mungu.
Rab. Judan anaamini
kuwa kwa kusema maneno ambayo ni haki ya ius
primae noctis ililazimishwa kuliko mtemi au chifu; aliyechukua kwa nguvu
yeyote waliyemchagua (anasema Nachmanides sawasawa na Soncino).
Mtazamo wa
marabi ulikuwa ni kwamba Mungu alitajwa kuwa ni Roho ya Kimbinguni na
asingeweza tena kabisa kuishi na wanadamu kwa ajili ya upunguzaji huu wa siku
za kuishi. Mwanadamu alipewa miaka 120 ikiwa ni kipindi cha kutubu na kumrudia.
Hivyo basi, tangu mwanzo wa kukua alikuwa na yubile mbili kamili kabla ya
maangamizo. Kipindi hiki cha mpito kitatolewa tena kwenye ufufuo wa pili wa
wafu ili kuwapa wote fursa ya kutubu (soma Isaya 65:20).
Mwanzo 6:4 kwa
hiyo inaendelea kushughulika na Wanefili na hapa mamlaka ya marabi yanafanya
mrejeo hadi nyuma kwenye uelewa alisia wa andiko linalowaelezea Malaika
walioasi. Rashi anaamini kuwa waliitwa Wanefili kwa kuwa “walianguka” (naphal) na pia waliisababishia dunia kuanguka.
Ibn Ezra anaamini pia kuwa mioyo ya wale waliowaona ilisisimka kwa mshangao kwa
kuona urefu wao wa kushangaza.
Neno
lililoambishwa kwenye siku hizo linakitaja
kizazi cha Enoshi nna wana wa Kaini. Rashi anarejea nyuma kwenye wasifa wa kale
na kwamba neno hili linahusiana na pia kwenye uharibifu wa kizazi cha Enoshi na
kile cha tatu cha dunia kiliangamizwa na bahari iliyovunja kuta na kingo zake
lakini bado hawakutubu. Ibn Ezra analifafanua andiko hili kuwa ni baada ya
gharika kuu. Nachmanides anaamini mtazamo usemao kwamba ama ni wake wa watoto
wa Nuhu wanaweza kuwa walitokana na uzao huo na ndiyo maana watoto walio wazaa
walikuwa warefu na wakupendeza au mfano wao ulikuwa ni Ogu mfalme wa Bashani
alikuwa ni mmoja wao na aliepuka gharika na wengine wengi pamoja naye (anasema
Soncino).
Nachmanides anatafsiri
kifungu hiki kuwa kinawaashiria Adamu na Hawa kuwa ndiyo alitajwa kuwa ni wana
au watoto wa Mungu pamoja na Sethi na Henoko na anashikilia kuamini kuwa
Wanefili walikuwa “watu dhaifu.” Ananukuu pia na kuthibitisha fafanuzi
zilizotolewa na R. Eliezar Mkuu, ambazo zinapatikana katika Midrash, zisemazo
kwamba Wanefili walikuwa ni malaika alioanguka kutoka mbinguni mahali ilipo
maskani yao na anaichukulia hii kuwa ni maana sahihi na inayomaanisha zaidi.
Sforno anajaibu kuyawekea ukomo maneno ya nyakati hizo hadi kwenye siku za toba.
Rashi anaamini
kuwa neno hili linalosema binti za wanadamu linamaanisha kwamba walizaa majitu
kama wao wenyewe. Usemi wa “watu hodari” unamaana kuwa walikuwa walikuwa hodari
kwenye matendo maovu na uasi kwa Mungu (wanaamini hivyo Rashi na Soncino).
Usemi wa kwamba
watu wenye sifa (shem) maana yake walikuwa
ndio watu walioleta ukengeufu na uharibifu (shemamon) duniani.
Rashi anaamini
kuwa usemi wa kwamba ilimtubia (wayinnachem)
Bwana kwenye aya ya 6 maana yake ilikuwa inamhurumia yule ambaye hakuwaumba
watu kuwa ni viumbe muhimu kana kwamba ndiye angeweza kuanzisha uasi katikati
ya malaika. Andiko hili linajulikana na wengine kuwa kama la kianthropomofia.
Korani inasema kuwa Ibilisi (Shetani) aliasi kwa sababu ya wivu wa kuumbwa kwa
mwanadamu. Mwanadamu hakuumbwa kwa umbo la kimbinguni ili kwamba Malaika
wajaribiwe kwa imani.
Nachmanides anafafanua
kwamba nexno moyoni mwake linamaana
kwamba hakumtuma nabii kuwaonya. Neno kusema wote wanadamu na mnyama
linaaminika kuwa huenda linamaanisha kwamba wanyama walikuwa pia wameharibika.
Ni Nuhu tu ndiye alipata rehema au neema machoni pa Mungu (wanasema kina Nachmanides
na Soncino).
Mamlaka za
marabi ndizo zimeendelea hadi mwishoni mwa aya ya 8 kudai kwamba Haphtarah Bereshith
imechukuliwa kutoka kwenye Isaya 42:5-43:10 kuanzia inaposema “Bwana asema
hivi.” Andiko hili ni la muhimu katika kushughulikia masuala ya wokovu na
marejesho mapya ia Israeli. Ni wazi kabisa kwenye utaratibu huu kuwa marejesho
mapya ya Israeli katika siku za mwisho yanaonekana kuwa ni jambo linaloendana
na mchakato wa kuuelewa uumbaji hadi kipindi cha gharika kuu na usafishaji wa
dunia. Jambo hili ni somo kwa haki yake yenyewe.
Tulichonacho hapa
kwenye andiko la aya za kitabu cha Mwanzo ni kwamba mnyororo mzima wa uzao wa
wana wa Adamu ulikuwa umeharibiwa na hawa Maaika walioasi na kwamba walipaswa
tu kuangamizwa na Nuhu tu ndiye alikuwa mkamilifu katika nj9ia zake kwenye
kizazi hiki chote.
Wazo lililokuwepo
hapa ni kwamba mwanamke alidanganyika na kuanguka na ataokolewa na mtoto
aliyemzaa na kumbeba.
1Timotheo 2:13-15 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa
kwanza, na Hawa baadaye. 14 Wala Adamu hakudanganywa,
ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. 15 Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika
imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
Tumeona kwamba wokovu
haujalishi wala kutegemea na kuzaa kwa mtoto hasa kwa mtu mmoja mmoja anayelitaja
kanisa na kuanzisha kwa taifa na kuwafundisha wateule walio kwenye imani ile.
Mungu ametuweka na kutufana kuwa familia (Mathayo 12:50; Waefeso 3:15).
Kunamashaka
kutoka hapa na kwenye aya za Yuda 6 na pia 1Wakorintho 11:10 (sawa na Mwanzo
24:65) malaika walijulikana kuwa waliharibu uumbaji na viumbe waliokuwemo.
Wanawake walifunikwa vitambaa kwa sababu ya dhambi hii ya kwanza ya mapema hata
kabla ya andiko hili la Mwanzo na uingilianaji wa malaika wote na viumbe
wanadamu.
Kusudi la uumbaji lilikuwa ni ili kwamba Mungu ajipanue mwenyewe na hatimaye awe ni yote katika yote na ndani ya yote kwa viumbe wote ni kama ilivyotakiwa kuenea kwenye muundo wa kifamilia pasipo mwingilio wa hawa malaika. Muundo wa dhambi ya sili uliingiliwa na kuharibiwa kwa mwanadamu na ndiyo maana Augustine wa Hippo alikosea kwenye uelewa wake kuhusu makusudi na nia ya maandiko yaliyo kwenye sura sita za kwanza za kitabu cha Mwanzo. Mlolongo wa vizazi vya Adamu unaonyesha kwamba wokovu unaoweka utaratibu kwa watu wazima unaendelea mbele hadi kwenye mchakato vizazi vilivyofundishwa vya kutosha na wana. Kwa hiyo dhana ya dhambi ya asili haiwezi kuwaokoa au kuleta wokovu kwa mtoto mdogo. Tutaandika kuelezea au kufafanua kiwango cha Mafundisho.
q