Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[251]
(Toleo La 1.0 19990313-19990313)
Sheria
kuhusu Utakaso wa Wanawake na Tohara kwa Wanaume inauhusiano mtambuka kwenye
imani na ni sehemu ya Sheria zilizoagizwa kwenye Torati ya Mungu. Jarida hili linatathimini
kukuhu uhusiano uliopo kwenye imani za Kiyahudi, Ukristo na Uislamu pamoja na
kweli nyingine zinazovutia na hatima yake.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hatimiliki ã 1999, 2016 Wade Cox)
(Tr.
2009; rev. 2016)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Utakaso na Tohara
Ukataso wa Wanawake
Kuna mambo mngine
magumu sana yanatojitokeza kwenye ya utakaso wa wanawake. Sayansi imefundisha
kuhusiana na vyakula kwa njia nyingi sana mbalimbali, hususan kuhusu umuhimu na
thamani yake ya kisaikolojia na ya kiafya. Matokeo yake tunaweza sasa kujua kwa
nini vyakula vingine fulani fulani ni ‘safi’ na vingine ni najisi na kwamba
hata tumekatazwa kuvitumia (Tazama jarida la Sheria ya Vyakula (Na. 15).
Hata hivyo, kwenye kizazi cha tunaokuwa tukiifuata sharia hizi za vyakula kwa
sababu Mungu ametuamuru tufanye hivyo. Tunajua kwamba Mungu alitupatia sheria hizi
kwa kusudi maalumu la kutufanya tuwe na afya iliyo thabiti, tuwe na uwiano
mzuri, na tuwe na maisha na umri uliokusudiwa. Sheria zinazohusiana na wanawake
havijasomwa na kufundishwa kwa namna hiyihiyi, kwa hiyo, yatupasa kufanya kama
tufanyavyo siku zote. Tutegemee kwenye ukweli kwamba kama Mungu amesema hivyo na
kamba ni faida yetu njema kufanya hivyo. Mambo haya pia yanakubalika na kwa mambo
yake ya kiroho, kwa kadiri yanavyohusiana na Masihi.
Neno “mwanamke najisi au mchafu” linawezakuwa
linawakwaza watu wengi. Laonekana kuwa ni kama linakera na kuchukiza hivi,
lakini sivyo. Bali ni wakati wa kutenganisha kwa kuwa mwanamke unahitaji
mapumziko na maelewano. Neno ‘najisi au mchafu’ linafanana sawa na kumwita mtu
kuwa ‘mdhambi’. Utakaso kisayansi ni wakati wa kujisafisha au kujitenga kwa muda
wa siku saba. Ni kitendo cha kimwili na cha kimwili cha kuelekea usawa wa
tumbo, ili lisiweza kupokea yai la kurutubisha mimba kwa hiyo mchakato wa
utungaji wa mimba unashindikana wakati wa mwanamke kuwa kwenye siku zake za
kuona damu. Kwa kawaida ni
kipindi cha siku saba kwa kila siku 28. Mchakato huu wa usafishaji unawezesha
mwendelezo wa mwanadamu, ambaye kwamba sheria hii kwa njia nyingine ni kwa
namna iliyosawa kama wengine ni baraza kutoka kwa Mungu (Mwanzo 1:28). Utimizaji
au ushikaji wa sheria umefungamanishwa na maisha ya kila siku ya binadamu.
Sheria ya Mungu inashinikizwa kutumika kikamilifu kwa namna zote mbili, yaani kiroho
na kimwili (2Wakorintho 7:1). Kwa Wayahudi, ni kawaida kwa wanawake kwenye siku
zao kujitenga au kujitakasa kwamba walifana mambo yafuatayo:
·
Hakujihusisha na usomaji wa neno la Mungu au Maandiko
Matakatifu.
· Hakuhudhuria au kujihudhurisha Kanisani
· Hakujihusisha na mabo ya kimapenzi kwa wakati huo
Haya ni mapokeo
na detsuri za Kiyahudi.
Walawi 15:19-30. Nayo nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba, na kuketi humo salama. 20 Na kama mkisema, Je! Mwaka wa saba tutakula nini? Angalieni hatutapanda mbegu, wala kukusanya maongeo yetu; 21 ndipo nitawaamria baraka yangu iwe juu yenu mwaka wa sita, nayo utazaa matunda hesabu ya miaka mitatu. 22 Na mwaka wa nane mtapanda mbegu, na kuyala yale matunda, akiba hiyo ya zamani, hata mwaka wa kenda, hata matunda yake yatakapoletwa ndani, mtakula hiyo akiba ya zamani. 23 Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wasafiri wangu. 24 Nanyi mtatoa ukombozi kwa ajili ya nchi, katika nchi yote ya milki yenu.
Aya hizi zimahusiana na masuala ya kiafya ya mzunguko wa kawaida na wa
asili wa mwanamke ha ya kawaida wa kipindi cha hedhi cha mwanamke. Ilikuwa kitu
cha muhimu sana kwamba mwakamke alipewa wakati aliouhitaji katika kipindi ili
kujisafisha na cha kuwa na mapumziko na cha kutuliza mawazo na akili ambavyo
ndivyo hali anayoihitaji ili kulinda afya yake. Kwa vipindi na miaka mingi
wanaume walihitaji kipindi hiki cha mpito ni kwa sababu tu ya kuwezesha amani
na utulivu kama huu uenee kwa wanawake zao. Hakuwa na vifaa tulivyonavyo siku
hizi vya kutumiwa ili kufanyia matendo ya kujijengea afya njema. Hata hivyo, hoja hiyo inahusiana pia na
ulaji wa nyama ya nguruwe. Kuhusiana na matendo au mazoezi ya kisasa ya afya kwa
kufuga nguruwe, nasi bado tumekatazwa kwa sababu fulani maalumu za kisayansi.
Mtu anaweza pia kudhania kwamba sharia za makatazo au karantini walizopewa wanawake
zina msingi wa muhimu na bado zinatenda kazi au zinatumika. Ilijitokeza kutuama
kwenye lile tunachokijua kuwa ni misingi ya kisayansi ya sheria za vyakula,
iliyo zaidi ya kuwa ni ya kiafya tu, peke yake ikihushishwa na yatupasa tufanye
kama tulivyofanya kwa tulivyofanya kwa vizazi na vizazi vilivyopita. Fanya kama
alivyosema Mungu na yatupasa tutende. Tunatenda kwa imani.
Aya zingine zinazofuata inahusiana na utokaji wa damu usio wa kawaida. Tunaona
kwamba msingi wa dhana yenyewe ni kwamba utokaji huu wa damu ni budi uchukuliwe
kama unajisi, hadi itakapothibitika kuwa kuwa inatoka kwa mazingira ya hedhi
kwa kukoma kwake. Kwa hiyo, sheria ya karantini inatuama nyuma ya kanuni ya
utakaso. Wanawake, na wanaume walijumuika nao, ni wale walioamriwa na sheria kushughulikia
na suala hili la utoaji wa damu nyingi.
Aya za 25-30 Kwamba nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye. 26 Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa; 27 ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki yake. 28 Lakini asipoweza kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa mkononi mwake huyo aliyeinunua, hata mwaka wa yubile; na katika yubile itatoka, naye atairejea milki yake. 29 Tena kwamba mtu anauza nyumba ya kukaa, iliyo ndani ya mji wenye kuta, ndipo ana ruhusa kuikomboa katika mwaka mmoja mzima baada ya kuiuza; atakuwa na amri ya kuikomboa muda wa mwaka mzima. 30 Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika yubile.
Sheria ya karantini
kwa mwanamke ni ya muhimu kwa ajili ya kulinda maisha yake mwenyewe. Pale
ambapo ugonjwa hauwezi kupona ndipo mara nyingi suala la kwamba mwanamke anafaa kutengwa na wengine kwa amani.
Utakaso Wakati Wa Kujifungua
Walawi 12 inatoa
mwongozo wa kufuatwa na wanawake wanapokuwa wanajifungua. Sheria inayohusiana
na kujifungua kwa mtoto inatoa vipindi maalumu vya utakaso kwa kutegemea na
kama mtoto aliyezaliwa ni wa kiume au wa kike.
Mambo ya Walawi 12:1-8 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto mume, ndipo atakuwa yu najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi, ndivyo atakavyokuwa najisi. 3 Siku nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake. 4 Na huyo mwanamke atakaa katika damu ya kutakata kwake siku thelathini na tatu; asiguse kitu kilicho kitakatifu, wala asiingie mahali patakatifu, hata siku hizo za kutakata kwake zitakapotimia. 5 Lakini kwamba amezaa mtoto mke ndipo atakuwa najisi juma mbili, kama katika kutengwa kwake; naye atakaa katika damu ya kutakata kwake muda wa siku sitini na sita. 6 Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mwana, au kwa ajili ya binti, ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani; 7 na yeye atawasongeza mbele za Bwana, na kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atatakasika na jicho la damu yake. Hii ndiyo amri yake huyo azaaye, kwamba ni mtoto mume au mke. 8 Kama mali yake huyo mwanamke haimfikilii mwana-kondoo, hapo ndipo atakapochukua hua wawili, au makinda mawili ya njiwa; mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na wa pili kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.
Mwanamke anakuwa
najisi kwa siku saba kufuatia akizaa mtoto wa kiume na siku kumi na nne akizaa
mtoto wa kike. Mtoto wa kiume ni lazima atahiriwe ifikapo siku ya nane. Siku hii
ya saba hapa ni muhimu sana, kwa kuwa ndipo wakati damu inajizatiti kushikamana.
Kisha inafuatiwa na kipindi kingine zaidi cha utakaso cha siku nyingine saba
jumuisha na siku thelathini na tatu ambazo jumla zinakuwa siku arobaini kwa mtoto
wa kiume na kumi na nne jumlisha na sitini na sita ambazo ni jumla ya siku
themanini ka mtoto a kike.
Kwenye maandiko
haya hadi aya ya 5 kwenye Bibilia ya Companion, Billinger anasema kwamba kipindi
kinachoongezwa kwa mtoto wa kike kilikuwa ni cha kuhakikisha uchache wa
wazaliwa wa kike. Sababu halisi ni za muhimu sana kama tunavyokwenda kuona.
Mtindo wa
kujitolea umeisha lakini sheria ingali inasimama bado. Sababu za kimwili au kisayansi
za sababu inayofanya kuwe na tofauti ya nyakati zinazohusika kati ya kuzaliwa
kwa mwanaume na mwanamkehazijulikani. Je, ni suala tu la tofauti ya homoni? Je,
siyo kwamba ni kwa sababu kuna viwango vya jamayomo vilivyoko? Au inawezekana
sana kuwa ni suala tu la uwezo wa kujikinga na maradhi? Tunajua kuwa sayansi ya
dawa inashauri na kupendekeza unyonyeshaji kwa maziwa ufanyike katika miezi kadhaa
ya kwanza ambapo mtoto atakuwa anaendeleza uwezo wake wa kujikinga na maradhi kwa
kupitia mamake kwa njia tofauti. Kipindi cha kutenganishwa kitawafanya wote wawili,
yaani mama na mtoto kupata nguvu na kuendeleza uwezo wa kupambana na kustamili papasi
wengi na virusi vinavyozaliana kwenye ulimwengu wa kisasa. Pia kuna utofauti wa
kitofauti sana kwenye mtazamo kuhusu mtoto wa kiume na wa kike. Mtoto wa kiume
anatahiriwa na anapewa kipindi kifupi cha kutengwa kwake. Mtoto wa kike angepewa kipindi kirefu cha kutengwa
kwake kwa sababu hakuwa anafanyiwa tohara na kwamba ukweli huu ulionyesha pia kuweka
tofauti kwenye nyakati za kutengwa kwake. Kuna sababu zingine ambazo zimeonyeshwa
hapo chini.
Katika andiko la
Walawi 12:4 tunaona neno lisemalo usikiguse kitu kilicho kitakatifu. Kwenye
maneno haya tunaona maana inayolingana, ambayo ni sawa na kuwatenganisha wateule
na utakaso. Tofauti hii ilikuwepo hadi kwenye ujio wa Kristo. Dhana yenyewe
ilikuwa ni kwamba mwanamke akiwa kwenye nyakati zake za hedhi angekitia unajisi
kile kilicho safi. Hata hivyo, kile kilicho kitakatifu kingeuweza kukitakasa
kile kilichokuwa kwenye mazingira ya utakaso. Kwa sababu hii mwanamke aliyekuwa
kwenye mtoko wa damu na akihitaji kupona alitakaswa kwa kwa kulishika kwake tu
vazi la Kristo. Hii haikumfanya Kristo awe najisi, bali zaidi tu ni kwamba Roho
Mtakatifu alipitia kwake ili kumfanya mwanamke yule awe safi.
Mathayo 9:20-22 Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. 21 Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. 22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.
Kitendo hiki
kilionyesha mambo makuu mawili. La kwanza ni kwamba Kristo alikuwa ni Kuhani Mkuu
mpya ambaye upindo wake ulitengwa kipekee tokea Kutoka 28:33-34 39:25-26 na kuwa
kilemba chake kilikuwa ni Utakatifu pia kwa Bwana (Kutoka 28:36; 39:30).
Fundisho la pili lilikuwa
ni kwamba kwa kupitia imani kupitia Roho Mtakatifu, usafi na utakaso
viliwafikia wagonywa na waliodhaifu. Hii imenurudiwa tena kwenye Mathayo kwamba
tunaweza kuona umuhimu wa kuwepo kwa Kristo kwa utendajikazi wa Sheria au
Torati na manabii na uponywaji wa wagonjwa na wadhaifu na walio najisi .
Mathayo 14:34-36 Na
walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti. 35 Na
watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo
kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi; 36 nao
wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu; na wote waliogusa wakaponywa
kabisa.
Kwahiyo, kile kilichokuwa
ni kitakatifu kijikigusa kile kilichokuwa kichafu au najisi na kukifanya kiwe kitakatifu.
Hii haijawahi kuwa imezekana hadi atakapokuja Masihi kama tunavyoona kutoka kwa
manabii.
Haggai 2:11-19 Bwana wa majeshi asema hivi, Waulizeni sasa makuhani katika habari ya sheria, mkisema, 12 Mtu akichukua nyama takatifu katika upindo wa nguo yake, naye akagusa kwa upindo wake mkate, au ugali, au divai, au mafuta, au chakula cho chote, je! Kitu hicho kitakuwa kitakatifu? Makuhani wakajibu, wakasema, La. 13 Ndipo Hagai akasema, Kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti, akigusa kimojawapo cha vitu hivi, je! Kitakuwa najisi? Makuhani wakajibu, wakasema, Kitakuwa najisi. 14 Ndipo Hagai akajibu, akasema, Hivyo ndivyo walivyo watu hawa, na hivyo ndivyo lilivyo taifa hili mbele zangu, asema Bwana; na hivyo ndivyo ilivyo kila kazi ya mikono yao; na kitu hicho wakitoacho sadaka huko ni najisi. 15 Na sasa nawaomba, tafakarini; tangu siku hii na siku zilizopita; kabla halijatiwa bado jiwe juu ya jiwe katika nyumba ya Bwana; 16 katika wakati huo wote, mtu alipofikia chungu ya vipimo ishirini, palikuwa na vipimo kumi tu; na mtu alipofikia shinikizo apate kuteka divai ya vyombo hamsini, palikuwa na divai ya vyombo ishirini tu. 17 Naliwapiga kwa ukavu, na ukungu, na mvua ya mawe, katika kazi zote za mikono yenu; lakini hamkunielekea mimi, asema Bwana. 18 Tafakarini, nawaomba; tangu siku hii ya leo na siku zijazo; tangu siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kenda, naam, tangu siku hiyo ulipowekwa msingi wa hekalu la Bwana tafakarini haya. 19 Je! Mbegu ingali ghalani? Naam, huo mzabibu, wala mtini, wala mkomamanga, wala mzeituni, haikuzaa kitu; tangu siku hii ya leo nitawabariki.
Kwa hivyo kutokan
na Sheria au Torati, kile ambacho hakikuwa kisafi na kilicho najisi hakikuruhusiwa
kukigusa kilicho safi. Jambo hili waliulizwa makuhani na jibu lilipatikana. Tena
kwa sheria yake Mungu mwenyewe na unabii, hali kama hiyo hiyo iliashiria kipindi
ambacho Mungu alimwaga Roho wake kwa wote wenye mwili na kumfanya awe Mtakatifu
ndani ya sheria yake na akaindika ndani ya mioyo yao. Jambo hili ilihitimishwa au
kukamilishwa na Masihi.
Kwa hiyo, kila
mwenye mwili alifanyika kuwa mtakatifu kwa njia ya Roho na alitakaswa kwa
kupitia Masihi katika Roho Mtakatifu. Sheria ya utakaso iliashiria kwenye utakaso
wa mwanamke mzazi kama ilivyo Israeli Kanisa na Bibi arusi wa Kristo na mama wa
taifa jipya.
Kutokana na hali
hii tunaona kwamba mama ametakaswa na anaweza kushiriki mlo wa Meza ya Bwana na
Pasaka akiwa kama mmoja wa wateule waliotakaswa katika Roho Mtakatifu. Kwa
kuhesabiwa na kuzaliwa kwa mtoto kwa kama ilivyo tu kunahitaji maandalizi na
ushiriki wa Pasaka ya pili ndipo hali kama hiyo inapojitokeza.
Tohara
Ni muhimu kwa
kipindi hiki kuongelea kuhusu tohara.
.
Kitendo cha
kutahiri watoto chaweza kuwa ni moja ya desturi iliyodumu kwa kipindi kirefu
nay a kale zaidi kuziliko zote kwenye historia ya ustaarabu wa mwanadamu. Inakutikana
kwenye karibu jamii na makabila yote na maeneo mengi sana duniani. Inakutikana
kutoka Australia hadi Afrika na katika Mashariki ya Kati. Kwenye makala ya James
Frazer (ya kitabu chake cha The Golden Bough [Tawi la Dhahabu], Vol.1,
Macmillan, 1976, pp. 96ff.), inaonyesha kuwepo na uzekano mkubwa kunafanyika
tathmini kubwa kwanza kabla ya kukitenda kitendo chenyewe. Tohara ina matokeo yenye faida kubwa hasa
kwenye mazingira ya joto. Mbali na matokeo hayo, chanzo cha kwanza cha tohara
yaonekana kuwa kulikuwa na utofauti na dhana iliyojitokeza baadae ya kuhusisha
kitendo hiki na mchakato wa kuzaliwa tena kwa mtoto na kutahiriwa tena. Tangu
nyakazi za mwanzo kabisa, govi ya mwanaume aliye tahiriwa iliwekwa mahali maalumu
kwa kufuata kulielekea moja kwa moja jiwe la gumegume la kutahiria ama kwenye miti
au miamba au popote alipofaa. kutokana na kile tunachoweza kukielezea kuwa
inaonekana kuwa kitendo cha kutahiri kinahusiana zaidi na tukio la kuzaliwa kwa
mtu kutoka kwenye miili ya wazazi wake..Hii inaonekana kama inachukuliwa kwenye
mawazo ya watu wa makabila yote ya zamani, na inachukuliwa kwenda sambamba na
dhana ya uwongo ya dhambi ya asili ijulinanayo maarufu kama hakika hutakufa.
Inaonekana kwamba
kwa kutoa sheria ya tohara kwa Ibrahimu kuwa ni lazima ifanyike ifikapo siku ya
nane, kwa kweli Mungu alikuwa anaingalia kati na kutoa kwa moja kwa moja na kwa
mjumuisho kwenye matendo yaliyokuwepo ya kipagani. Mungu alikua anasema, Mimi ni jiwe lako la gumegume na ndiye
mwenye kuwafufua na kuwapa maisha endelevu na ya milele. Kwa hiyo kitendo
hiki cha tohara kiliamriwa kifanyike siku ya nane na siyo kwenye kipindi cha
kukaribia kubalehe bdipo liondolewe kwa kutahiriwa au kwenye kipindi cha mtu
mwenyewe akiwa ukubwani, na kukifanya kuwa ni kama zawadi ya bure aliyoitoa
Menyezi Mungu, ksa aliye kwenye nasaba ya taifa la Waisraeli. Kwa njia hii pia
Mungu alikuwa anasema kwamba Ishimaeli aliingizwa kwenye kabila kwa wakati
mmoja kama Isaka na kwa kweli kwa kupitia agano la uanachama au ushirika kama
aliokuwana Ibrahimu mwenyewe.
Mungu alikuwa
anauadhibu uwongo wa nafsi na mafundisho potofu ya mzunguko wa kurudiarudia
kuzaliwa upya ambayo ni mafundisho ya Mashetani nay a Mungu Sin na ya imani ya
Ishtar (sawa na kama inavyoelezewa kwenye majarida ya Ndama wa Dhahabu (Na. 222) na lile la Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235). Matendo haya yalionekana
pia yakijumuiswa pia na matendo mengine ye Jaribio kama hili itambatanishwa na
zingine kama ungoaji wa neno. Neno yalitolewa au kuangushwa na matendo mengine yajulikanayo
kama uchongaji wa meno. Meno yaliondolewa kwa kung’olewa wakati huu wa tohara
kwenye makabila yaliyoshikilia tamaduni za kikale sana. Frazer anadhania kwamba
matendo haya huenda yalichukuliwa na kuingizwa kutoka dhana ya kudumu mda mrefu
kwa jino kwenye fuvu baada ya kufa na hivyo lilitumika kama alama ya baada ya kipindi
cha kuishi. Tunajua kwa uhakika kwamba Waaustralia wa zamani walifanya matendo
haya kwa kipindi cha takriban milenia na wanaume mashuhuri wa maeneo ya Ziwa la
Nitchie walijihusisha na utendaji wa matendo haya, huenda ni kipindi cha tarehe
za nyuma za nyakati za kabla ya gharika kuu.
Waaustralia wengi
wa kisasa pia waliyatenda matendo mapotofu ya desturi ya kuchanja chale au ya
kujichora michoro ili kujionyeha makabila wanayotoka. Inaonekana kwamba malendo
haya hapo zamani sana yalitumika ili kujionyesha ishara ya miungu na kwamba wale
waliokuwa na alama hizo waliweza kuiomba na kuitangaza miungu hiyo. Matendo
haya yalikatazwa kufanywa katika Israeli (Walawi 19:28, sawa na sura ya 21:5,
Kumbuka la Torati 14:1). Ilijulika hapo zamani kwa Waarabu na kila kabila walijulikana
kwa kupitia alama zao (nembo au wasm) kwa mifugo (kwa mujibu wa kitabu
cha Encyclopedia of Region and Ethics
[Ensaikolopedia ya Dini na Maadili] (ERE, vol. 2, pp. 326ff.). Kwa mujibu wa
Lucian, Wasyria wote walikuwa na michoro yenye maana za kidini kwenye viuno na
shingoni mwao (ibid.). Herodotus anatuambia kwamba wakimbizi watumwa waliokimbilia
huko Haraculeum kule kwenye mdomo wa mkondo wa mto Nile walichorwa kichoro na
wakafanywa kuwa miungu na hivyo hawakuwa wametakiwa au kurudishwa tena kwa
matajiri wao. Kwa hiyo ndipo katazo hili lilikuwa ni rejea ya wazi yenye maana
ya uondoaji wa ibada za sanamu katika Israeli. Kwa Wasemiiti, nembo zote zilizo
za aina kama hiyo zilichapwa au kuchorwa kwa kuhisianisha na miungu yao au na
za wenzao (ibid.). Kwa hiyo, mchoro wa mtu aliyemlalia mwenzake alichorwa kama
bundi sikio lake ikiwa ni ishara ya kukosa imani kwa Mungu ambaye ndiye alikuwa
Bwana wa kweli. Alama za michoro hii huenda yote ilikwenda nyuma kwenye mawe ya
gumegume ya mwanzoni asilia na yaliyokuwa ya kawaida na yakijulikana sana.
Matendo ya “kunyoa
kwa ajili ya wafu” yalikuwa ni mojawapo ya matendo haya ya kizamani ya kuwabudu
mababu, ambayo pia yalikuwa na uhusiano na imani ya kiumbe kupitia kwenye
mchakato wa kuzunguka zunguka katika kuzaliwa hapa na pale kwa mababu. Imani
hii pia ilienea kwa Waceltiki walioipata kutoka kwenye chanzo hichohicho kimoja.
Tunajua pasipo shaka kuwa Wacaucasian, wanaoonekana kuwa ni wa jamii ya Waceltiki
wa Kiaryan, walifanya matendo ya kuasiliana au kuwaomba wafu pia.
Tuna ushahidi
sasa kutokana na masalio yaliyokutikana kwenye kile kingalichoweza kulingnishwa
au kuelezewa kama Scythia ya Kale. Masalia ya maiti zilizozikwa zilipatikana
huko Urumchi (au Urunqi) kwenye ile inayojulikana sasa kuwa ni Uchina kwenye
jimbo la Tien Shan kwenye Dini ya Kienyeji nay a Wenyeji ya Uygur karibu na
mpaka wa Kazakhstan. Ina umri wa takriban maelfu kadhaa ya miaka na inadhaniwa
ilizika kwenye kipindi cha takriban miaka 1000 KK katika wakati wa zama za
Daudi za mashambulizi ya mara kwa mara ya Waaryan wa India.
Maiti hizi za watu
mashuhuri na zilizotiwa dawa bado zingalipo bado kwenye mikono na utunzaji wa
serikali ya Uchina, ambazo walizificha ili zisitumiwe na wadadisi wa mambo ya
hadhara ya kijamii kwa ajili ya taarifa za dhahiri za Wacauscasian ambao ni
dhahiri sana kuwa zinafanana na Waceltiki, wakiwa kwenye Scythia ya Kale au
Uchina ya sasa. Tuna kumbukumbu ya nyakati za Daudi na vita vya Wascythia dhidi
ya Wamesheki na Tubali na ya makumi wa Kadari (Zaburi 120:5-7). Somo hili litatathiminiwa
kwa kina kwenye mkururu wa maandiko ya majarida ya historia ya mataifa (sawa na
asemavyo E.J.W. Barber, kwenye kitabu chake cha The Mummnies of Urumchi
[Masalia ya Maiti za Kale za Umrichi], W.W Norton, 1979).
Agano la Damu
Kitendo cha kuwachapa
au kuweka alama watu wa Uarabuni kilifanywa kama agano na hiki mwanzo wake
kilihusu kati ya mwanadamu na Mungu na hatimaye ikawa baina ya mwanadamu kwa
mwanadamu (ERE ibid.). Alama hizi zilifuatiwa na ukusanyaji wa damu na ilinywewa
kama ishara ya agano. Kitendo hiki kilikuwa na msingi wa kiroho nyuma yake,
dhidi ya katazo lililotolewa la ukatazaji kunywa damu kwenye Biblia. Kuna madhara
makubwa sana ya kiafya pia yanayoibuka kutokana na kitendo hiki. Kwa hiyo
Kristo alitoa agizo kwamba yawapasa wainywe damu yake na kuula mwili wake kama
sehemu ya agano.
Desturi za Kizamani na Mavuguvugu Yake
Kwa hiyo tohara ilikuwa
kama ishara ya agano kati ya Yahova na watu wake. Mwanzoni tohara ilikuwa
imeenea kila mahali na inaonekana kuwa ilikuwepo hata nchini Misri na baada ya
tukio la Kutoka na hata zama za kabla ya tukio hili, na inadhaniwa kuwa
kilikuwa ni kitendo kilichotumika kufanywa tangu mwanzoni mwa kuanzishwa kwa
taifa la Israeli. Mungu aliwapa Israeli maana halisi ya ishara hii. Malaika waasi
wakiongezwa na Azazeli wanaonekama kuwa wamepewa mfano na alama hii kuwa ni
kama alama ya wanaojikinga na kupatwa magonjwa na kama kujipa uwezo wa
kutopatwa na madhara wala nafsi kutokufa na imani ya waamini mageuzi ya
kuzaliwa tena na tena kwa mwanadamu. Mengi yamefanywa na Waaborigines wa Australia
kuwa ni wa arobaini au wa maelfu ya miaka isiyoweza kuelezeka umri wake na
kuhusu kuingia na kuanza kwao kuishi Australia kwenye makundi manane kwa miaka
elfu chache tu.
Profesa Berndt
anashikilia kuamini kwamba walikuwa wanauhusiano na Wamisri wa kale kabila la wa
Dravidians wa India. Tabia zao, na kutokana na udadisi juu ya mila na desturi
zao yaonyesha kuunga mkono mawazo haya. Baadhi ya ushahidi na nadharia ya
wataalamu wa elimu ya mila na desturi za kijamii huwajumuisha na aina ya kale
zaidi iliyokutikana kwenye Pango la Juu la Choukoutien huko Uchina ambapo pia palijumuisha
aina tatu ya matabaka ya watu kwenye kundi moja la “Wamongoloid wa kale, na
aina ya Wamelanesoid na Waeskimoid.” Birdicell alinukuliwa na Hoolen, pia kuhusiana
na Wamurrayian au Waarchaic Weupe au Cauicasoid au uhamiaji wa kundi la pili wa
mafuvu kama ni kutoweza kufanana na Mtu wa Zamani au Mzee wa Pango la juu la Choukoutein
(kwa mujibu wa kitabu cha R.M. na C.H. Berndt, cha Aboriginal Man in
Australia [Mwanaume wa Kiaborijini wa Australia], Angus and Robertson,
1965, pp. 29-31). Weidenreich alisema kwamba:
Waanyakazi wengine (wataalamu
wa elimu ya sayansi ya makazi na tamaduni za jamii) wamechukulia Waabojini wa
Australia kama ni kizazi cha moja kwa moja cha Wazungu watokanao na mtu kutoka Nyanda
za Juu za Paleolithiki na mhamiaji wa nyakati za karibuni kutoka Ulaya au Asia ya
Kati na kuja Australia (ibid., pp. 29-31).
Kile kilicho muhimu
pia ni kwamba mchepuko huu wa aina ya kimatabaka ulikutikana kwenye kundi moja
na strata la kule Choukoutien kule Uchina, inayoonyesha huenda ni tukio la
mtawanyiko wa kawaida kwa aina ya matabaka ya Asia na/au ni wimbi la asili moja
ya damu na uzao la wakati wa ule kwenye anga.
Kwa karne kadhaa makuhani
wa Kibudha watakapokuwa kwenye sherehe za kuwekwa wakfu, walikuwa na malundo
matatu ya ubani yaliyochomwa kwenye vipaji vya nyuso zao na tendo hili
lilirudiwa rudiwa kwa kadiri walivyokuwa wanapanda juu ya madaraja ya vyeo hadi
itakapokuwa kuna makovu tisa kwenye vipaji vya nyuso zao (ERE, ibid. 2, p.
327). Kwenye sherehe za kabla ya kuweka wakfu za Watheravadin hata leo, miungu
na maroho huitwa na kuwashukia kwa njia ya viwango vitano kwenye madhabahu ya
matoleo. Ndipo mungu huabudiwa na makuhani wanatiwa chapa sawa na mstakabala husika
ulivyo.
Kwa hiyo Mungu
alitoa katazo kuwakataza Israeli wasijifunze kutenda mambo hayo. Hata hivyo,
hapo zamani sana tatika Israeli manabii yaonekana kuwa walikuwa na aina fulani
ya alama au chapa kwenye vipaji vya nyuso zao kama wengine wanavyozichukulia
kutoka kwenye andiko lililoko kwenye Wafalme wa Kwanza (yaani 1Wafalme
20:35-43, sawa na ilivyo kwenye ERE, Vol. 2, p. 327).
Musa anaonekana
kuwa aliyashuhudia matendo haya ya kujitia alama yakifanywa na Wamidiani na
wana wa Ibrahamu. Ayubu mwana wa Isakari (Mwanzo 46:13) katika nyakati za kabla
ya tukio la Kutoka huko Midiani anaonekana kuwa alikuwa na alama iliyomfanya
awe wakfu kwa Yahova. Maandiko
asilia ya Ayubu 31:35 yanasema:
Laiti ningekuwa na
mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu); Laiti
ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu!
Hii imerukwa
kwenye tafsiri ya KJV lakini kwa kweli ipo hapo na inahusiana na alama
aliyokuwanayo Ayubu. (sawa na tafsiri ya Green’s Interlinear Bible na ERE ibid.). Hii ilichukua mbadala wa Sheria ya
Mungu kama kumbukumbu katikati ya macho na mkononi ikiwa imeandikwa mioyoni.
Wakati wote ilimwashiria Roho Mtakatifu aliyepewa jukumu la kuziandika Sheria
za Mungu mioyoni mwetu na mawazoni mwetu na kwenye matendo yetu.
Wayahudi walivaa vishada
vya rangi ya samawi nyakati za Kristo ikiwa ni ishara ya kuwa wanazishika
Sheria za Mungu, lakini walikuwa wanajivunia na kuwadharau wengi na kuwatia
kiburi.
Uchoraji wa alama
kwa Wayahudi waukuweko hadi wakati wa Mkataba
au Azimio la Omari (yapata kama mwaka wa 640BK) ambapo kwenye nchi za Kiislamu
au za wafuasi wa Muhammedi Wayahudi walishurutishwa kuvaa vilemba vya manjano
kwenye nguo zao. Huko Misri katika karne ya kumi na nne Wayahudi walivaa
vilemba vya rangi ya manjano. Baada ya Mtaguso wa Nne wa Baraza la Lateran la
mwaka 1215 huko Roma uliamuru kwamba Wayahudi wote pamoja ma Waislamu ni sharti
wote wavae mavazi maalumu yenye utambulisho wa namna tofauti. Ilikuwa imekwisha
tumika tayari ilipofikia mwaka wa 1208 huko Ufaranza kwa Wayahudi. Kanisa ya
Roma lilitumia hii kama sababu ya kuzuia uoaji wa kuchanganyana na wajakazi wa
Kikristo. Huko Ufaransa alama ya utambulisho ilikuwa ni manjano lakini psnde za
mashariki ilikuwa nyekundu. (yaani ni kama kufuatiwa na Baraza la Buda).
Sheria ya tohara
ilikuja kuonekana kuwa ni kama ya kwanza ikiashiria au kumpelekea mtu kwenye
ubatizo na ndiyo maana kwenye Makanisa ya Matengenezo watoto wagodo
“walibatizwa” wakiwa na siku nane kama tohara vile inavyohitaji na hatimaye
ilichukuliwa kama kigezo kwa kuwekewa mikono na askofu. Soma jarida la Toba
na Ubatizo (Na. 52).
Msimamo wa Kanisa Kuhusu Tohara
Kwenye Kanisa la
Kwanza, utata kuhusu tohara iliibuka ambapo kwa wale wanaoitwa wa mrengo wa Kihelleni
walikataa au kuipinga na wa mrengo wa Kiyahudi waliulazimisha uendelee (soma
Matendo ya Mitume 11:2; 15:1,5; 21:21). Mtume Paulo yeye mwenyewe akiwa
ametahiriwa, na, kwa shinikizo la Wayahudi, alimtahiri Timotheo (Filemoni 3:5; Matendo
ya Mitume 16:3). Aliuchukulia
kama alama ya kupata huruma ya kimungu ya mataifa (Warumi 3:1ff.). hata hivyo,
kwa suala la waongofu wa Mataifa ilichukuliwa kuwa siyo muhimu (Matendo ya
Mitume 15:9ff., sawa na Wagalatia 5:2-4).
Paulo aliuchukulia
uwepo au kutokwepo kwa tohara ya kimwili ni sawa tu na isiyo na uhusiano na
utajiri kwenye agano la kati ya mtu mzima na Mungu (Warumi 3:30f.; 4:9ff.; 1Wakorintho
7:18ff., Wagalatia 5:6; 6:12f; Wakolosai 3:11). Kwa njia ya imani Torati imetolewa na kuwepo na
utakatifu kupitia imani. Kwa kuwa, wao wenyewe ambao wametahiriwa hawazishiki
sharia, bali anajaribu kutukuza katika mwili kwa sisi tunaozishika sharia waheshimu
sheria. (Wagalatia 6:12ff.).
Kwa kuwa tohara
pekee ya kweli ni ile ya kiroho (Warumi 2:25ff.; Filemoni 3:3ff.; Wakolosai
2:11ff.). Kwenye mafundisho
haya Paulo anamnukuu tena Yeremia (Yeremia 4:4; 6:10; 9:26; sawa na Kumbukumbu
la Torati 10:16; 30:6). Anaruhusu kwa mchakato epushika kwenye mazingira tofauti
tofauti (kwa mujibu wa Matendo ya Mitume 16:3 pamoja na Wagalatia 2:1ff.).
Alishikilia
kwamba angetumia uwezekano wowote awezavyo ili kuwaokoa wengine (1Wakorintho
9:19ff.). Lililo la muhimu ni uaminifu wa mtu binafsi na kuguswa na lile lililo
sahihi kwa kila mtu binafsi yake (sawa na Wagalatia 2:11ff.). Paulo
alijichukulia mwenyewe kuwa ni mtu mwaminifu na anayeaminiwa na mwenye injili
ya tohara, wakati ambapo Petro alikuwa ameaminiwa kwa injili ya tohara
(Wagalatia 2:7-9). Kwa hiyo misheni au mkakati wa Petro ulikuwa ni kwa ajili ya
kuwafuatilia Wayahudi waliokuwa kwenye nchi za utawanyiko na pia kwa Waisraeli.
Petro hakuwa na wala hajawahi kuwa askofu wa Roma. Na haijawahi kuwa kazi yake
kabisa hiyo.
Wasiouna umuhimu
wa kutariwa walishinda na mara nyingi inadaiwa kwamba ni madhehebu tu fulani
machache na madogomadogo na ambayo yalichukuliwa kama wapotoshaji ndio waliendelea
kushikilia sharia hii ya tohara. Mmoja ya hayo lilikuwa ni la Wayahudi wa Kiebioni
ambao waliichukulia tohara kuwa ni kama “ishara na mhuri wa manabii na wa
utakatifu” kama ilivyokuwa kwa Kristo mwenyewe wakiyawekea msingi wa matendo yao
hayo kwenye Mathayo 10:25 (kwa mujibu wa ERE 3, pp. 665f; sawa na Iren Adv.
Her. xxx. 26). Cenrithus pia alichukuwa mtazamo kama huohuo na kwa hiyo mara
nyingi anachukuliwa ni kama Mnostiki wa Kiyahudi (ERE ibid.). tutaona ni kwa
nini hapo chini.
Mtaguso wa Tatu
wa Toledo (wa tarehe 8 Mei 589) uliwakataza Wayahudi wasiwanunue watumwa Wakristo
na kurasimisha kwamba Myahudi yoyote anayemtahiri mtu kama huyo kwa msingi au
kisingizio cha andiko la Mwanzo 17:12f. ni lazina limepotea. Mzimamo huu ulikuwa
pia umeingizwa kwenye sheria na Recared kwenye kanuni yake iliyojulikana kama Leges Visigothorum [Sheria za Wavisigoths] (ed. Zeumer, Hanover, 1894, p. 305 [=XII.
ii. 12]) inayosema: ‘ille autem qui
Christianum mancipium circumciderit, omnem facultatem amittat et fisco
adgregetur.’ (kwa mujibu wa ERE
ibid., p. 664).
Kwa hiyo,
madhehebu ya wasioamini Utatu, au waliojulikana kama madhehebu wa Arian waliungana
na kukubaliana na waamini Utatu kwa jambo hili siokuwa na trinitaria au
inayoitwa Arear sects walikuwa kwa maelewano na trinitaria kwa jambo hii. Watrinitarian
au Wakatoliki walichukuwa uongozi muda mfupi baada ya hii mnamo mwaka wa 590 na
wakaanzisha kile kilichojulikana kama Dola Takatifu ya Roma. Eugene IV alitoa
tangazo rasmi la Kanisa Katoliki la Roma kwenye Tangazo lake rasmi lijulikanalo
kama Cantate Domino (tarehe 4 Februari
1441). Alichukulia kwamba umuhimu au uhitaji na maadhimisho ya Sheria au
Torati, hata hivyo ni sahihi kwa muda, wakati zilipotanguliwa kwa ujio wa
Kristo na sakramenti za Agano Jipya. Kwa hiyo ubatizo ulionekana kama unachukua
nafasi au mahala pa tohara.
Kwenye Kanisa la
Kikoptiki si kwamba tu kwamba ubatizo ulichukuliwa kama mbadala wa tohara. Vijana
walibatizwa wakiwa na umri wa siku 40 na watoto wa kike walibatizwa wakiwa na
umri wa siku 80. Mchakato huu uliashiria moja kwa moja kwamba sharia ya utakaso
na tohara kwa wanaume ilibakia kuwa muhimu kwa ujumla (kwa mujibu wa ERE, vol.
4, p. 119).
Koptiki lilikuwa moja
ya Kanisa la zamani sana la Kikristo la huko Afrika Kaskazini nchini Misri.
Walijitenga kutoka kwa lile linaloitwa Kanisa la Kihafidhina, maarufu kama
Orthodox Church mnamo mwaka 451 ikiwa ni matokeo ya kuibuka kwa mafundisho ya
kutoka Costantinople (381) na Kalkedon (451). Inaweza kuhojiwa kwa usahihi sana
kutokana na ushahidi wa Wakoptiki, kwamba ubatizo haukuonekana kuwa unachukua
nafasi ya tohara, kwa kuwa kinyume chake Wakoptiki waliuingiza ubatizo a watoto
wachanga uliofanyika kwa kutofautisha utakaso wa wanaume/wanawake, wanaume
walikuwa bado wanatahiriwa, kama yakiwa ni matendo kwenye utamaduni wa Israeli
ya kale. Na kwamba wanaume na tohara yenyewe ilionekana kuwa ni kama jambo la
tofauti, ambayo inaweka taswira ya tofauti za kibiblia.
Tunaweza kuhitimisha
kutokana na matendo ya Kanisa la zamani la Kikoptiki, ambayo pia yalikuwa yakifanywa
miongoni mwa dini za Kisabato huko Ulaya na maeneo ya Asia Ndogo, na kwamba
tohara ya watoto wachanga ilichukuwa kuwa ni ya muhimu na ni kama sehemu ya
imani ya Waisraeli na ya Kanisa. Wakati walipoingia Kanisani, Wamataifa watu
wazima waliwatahiri watoto wao, ni kama alivyofanya mtu yeyote mwingine yule. Kitendo
hiki kilikuwa ni cha wote na hakikupigwa marufuku rasmi kwenye imani ya Kikatoliki
hadi ilipofika karne ya Kumi na Tano.
Tohara ilienea
hadi kwa Wahindi wekundu wa Marekani na Lewise Spence (kwenye kitabu chake cha ERE,
vol. 3, p. 670) aliichukulia hii kuwa ni kama kitendo ambacho kinajumuisha
kutoka, na kilianzisha utoaji kafara ya wanadamu. Mfano ulioandikwa na Frazer
na jinsi alivyoungwa mkono na Spence inaonyesha kuwa na uhusiano, siyo tu kuhusu
dhana ya kiumbe kuzaliwa tena na tena mara nyingi, bali ni kwa kuzaliwa tena na
tena kwa maroho duniani, ambazo tunaziona kwenye Dini za washika Krismas na
Easter za kipagani (sawa na lisemavyo jarida la Chimbuko
la Krismas na Easter (Na. 235).
Spence anaichukulia tohara kwa aina mbili; moja, ni kama dhabihu ya mifano ya kingono
na tama, na nyingine ni kama dhabihu halisi, mfano wa dhabihu ya viumbe wote
kwa mungu asiyejulikana (ibid.).
Tohara ya Wamisri
inarejelewa nyuma hadi kwenye Kizazi cha VI, kutokana na ushahidi uliokutwa
huko Saqqarah, na ushahidi halisi wa kitendo kama hicho katika nyakati za kale ambao
ulionewa mashaka kwanza na mamlaka mkuu (kwa mujibu wa ERE, ibid., 3, 671ff.).
Tohara inakutikana,
kama ilivyokuwa imetarajiwa, na dini ya kale ya ilioitwa ya Bene Israeli, Waisraeli
wa zamani waliita “Wanaume wa Mafuta wa Jumamosi” na huko India ikaenea Kusini
mwa Bombay na Konkan kote (kwa mujibu wa ERE, vol. 2, p. 471ff.). Tohara wakati
wote ilifanywa majumbani hadi wakati wa Geonim. Kati ya karne ya sita na ya kumi
na moja ilihamishiwa kwenye sinagogi na kufanywa hadharani kama sherehe ya kidini
mbele ya kundi la waumini. Matendo yote ya kimaombolezo kwenye ibada
yaliahirishwa katika siku hizi.
Tangu wakati wa
Kristo kwenye maanfiko ya Kitalmudi ya Kiyahudi, mtoto alipewa jina haraka sana
baada ya sherehe. Ndipo tunapoona kwamba utoaji wa majina wa baada ya ubatizo
ulianzia kutokana ma sherehe hizi zaidi ya kutokana na ubatizo wenyewe tu. Aina
nyingi za ubatizo wa watoto wachanga ilikuja kuingizwa mahala pa sherehe za
tohara. Kwenye Talmudi ya Kiyahudi, sherehe hizi zilijumuisha mambo matatu
yafuatayo:
1)
Milah kuikatilia mbali sehemu ya nje ya govi
ambako kulifanya kwa kisu kikali na kilichonolewa vizuri.
2)
Peri’ah uchanaji wa sehemu ya ndani ya maji wa
ngozi ya ndani ya govi ambavyo inafanywa kwa kucha ya kidole gumba na kidole
kilichokaribu na kidole cha shahada.
3)
au kuiminya
na kuikamua damu kutoka kwenye kidonda (kitendo hiki kinapingana na sheria ya
biblia).
Tohara haikuchukuliwi
kuwa ni sakramenti ya Wahahudi (au ya Waisraeli a zamani) kwa namna sawa na kama
ya Ubatizo na Ushirika wa Meza ya Bwana ni Sakramenti mbili za Imani ya Kikristo
(soma jarida la Sacramenti za
Kanisa (Na. 150); sawa na ERE, vol. 3, p. 680). Wanamatengenezo wa Kiyahudi
tangu mwaka 1843 wamefanya juhudi kubwa ya kukomesha ufanyaji tohara na
hawakufanikiwa. lakini tangu mwaka wa 1892 Wanamatengenezo hawa wa Kiyahudi huko
Marekani hawakuihitaji kabisa washurutishwe waongofu wanaoingia imani hiyo kwa
kigezo cha kuona kuwa ni ukatili wakati wanapofanyiwa watu wazima.
Tohara katika Israeli
ni ishara ya kimaadili na utaratibu au kanuni ya kidini ya moyoni na kifikra,
ambayo inawafanya waongofu wote wa kiroho akiwa ni sehemu ya washirika wa Israeli
(kama isemavyo Kumbukumbu la Torati 30:6; Yeremia 4:4; mambo ya Walawi 26:41;
Warumi 2:28; Wakolosai 2:11). Philo 38d aliiona hii kama kutoka kwa El ambaye
alijitahiri mwenyewe na watu wake (kwa mujibu wa ERE, vol. 9, p. 896).
Herodotus (ii
104) anasema kuwa Wafoenike na Wasyria waliichukua desturi hii ya tohara kutoka
Misri.
Moja ya kanuni za
kidini za zamani za waabudu mungu Ashtarte au Ishtorethi au Athargatis kutegemea
na eneo lililopo huku Mashariki ya Kati, ilikuwa ni ile ya kuwa mwanana. Vijana
walijitahidi kujitengenezea kwa wazimu mubwa sana kutumia muziki na matendo
mengine ya kidini na hatimaye walijihanithisha wao wenyewe. Tangu hapo na
kuendelea walizitumia nguo za wanawake. Walilibeba sanamu la mungumke, ambaye
walikuwa wanamuabudu kwenye ibada au karamu na matamasha ya porini. Walirukiana
na kujikatakata wenyewe. Walikuwepo pia wanawake waliokuwa anatumika kwa kujitolea
Hekaluni na matendo ya kifisadi yalifanyika. Kulikuwa na rejea ya samaki katikati mwa Hierapolis
na Bambce. Tunaweza pia kufikiri kwamba kwa hiyo samaki alikuwa ni alama ya
Easter au Attis na hakikuwa na uhusiano wowote ule na Ukristo. Sherehe hizi pia
zilihusisha matendo mengine, ambayo yameingizwa kwenye Ukristo. Sherehe ya kubeba
sanamu la tatu (Ate) kwenye fukwe za
bahari na kisha kuchukua majagi ya maji na kurudinayo kwenye hekalu na
kuyamiminia kwenye shimo lililo kwenye majimbo yake ziliadhimishwa pia. Sherehe
ya majira ya machipuko iliyojumuisha na kukusanya matawi pamoja na kuyalundika
pamoja na bidhaa na mali na kisha kuyachoma mbele ya miungu ya Syria, ambao
wote walikusanywa Hekaluni kwa ajili ya kuendeleza na mchakato mingine zaidi.
Wanyama na pengine hata watoto walitolewa kafara pia kwa namna hii hii. Mahujaji
kila mara walinyoa vichwa vyao walipokuwa wanakuja hekaluni kwa njia hii na
vijana wa kiume na wanawake walitoa sadaka nywele zao kwenye makasha ya dhahabu
au ya fedha kabla ya kuoa au kuolewa. Kujichora michoro kwa heshima ya mungu
kilikuwa pia ni jambo la kawaida (kwa mujibu wa ERE, article Atargatis vol. 2, pp. 166-167). Kutokana
na haya tunaweza kuona uhusiano ibada au matendo ya Waarabu wa zamani kama
ifuatavyo, Lewis Paton anaona kwamba miungu ya Lydia Attis inaweza kuwa ni aina
nyingine ya jina la Atargatis au
Ishtar kwa umbo la ‘Ate (soma kitabu cha ERE, ibid., ‘Ate, vol. 2, p. 168). Attis alikanganywa na Rhea na kisha akaendelea
na kuvaa mavazi ya wanawake. Lucian atatoa sababu mbili kwa kitendo hiki. Anasema
kuwa kilikuwa ni cha kumuenzi na kumpa heshima Ate au Attis na pia ni cha kumpa
heshima Combabus ambaye alijizidisha mwenyewe ili kusimamisha kitendo cha
kujichanganya yeye mwenyewe na Malkia Stratonice (ERE ibid). Imani na utaratibu
huu wa kidini ambavyo tunavikuta kwenye Biblia kwa mazingira yaliyorudiwa
rudiwa, na bilashaka ndiyo sababu chanzo cha kuwepo kwa makatazo ya Bibilia kuhusu
matendo haya. Ni rahisi pia kuona uhusiano uliopo kati ya Ishtar au Easter na
miungu anayekufa Attis ambaye alijitolea kafara kwa kutundikwa juu ya msonobari
(soma jarida la Mslaba: Chimbuko Lake na
Maana Yake (Na. 39). Ibada za mungu Attis ziliendelea na kuenea huko Roma
katika mwanzo wa nyakati za sasa.
Makuhani wa Attis
waliendelea kufanya kupinga kwa maandamano kila mara katika karne ya nne waklalamikwa
kuwa Wakristo walikuwa wamewaibia mafundisho yao yote. Imani iliyopo sasa ya
kidini ya dini za mungu Jua imefikia hata kiasi cha kulitumia jinaa la Easter
kwenye ibada za imani zao na pia zinaadhimisha sikukuu na kutumia sanamu kubwa
za mungu mke na ya mungu wa uwongo. Tertallian anasema kuwa Atargatis alikuwa ni
miungu mke wa Wasyria. Macrobius anasema waliita jua kuwa Hadard na dunia kuwa ni Atargatis.
Kwa hiyo ben Hadadi maana yake ni Mana au mtoto wa Jua. Talmud inamuita kuwa
Tar’atha. Kule Armenia yeye anaitwa Tharatha. Yeye ni kama aina ya mungu mke
wa Wasemitiki Ishalar. Athtar au kwa ilivyo tu kwa lugha ya Kianglo Saxon ni Easter.
Strabo na Hesychius wote wawili wanamjua yeye kwa jina la Athara na kwa maelezo
ya Delos wanamuita. Aphrodite (ERE ibid.) Askelon, Karnaim na Delos waliendelea
kwa kipindi kirefu kumtumikia Astarte. Akijulikana kama Derketo huko Askelon nusu
ya upande wake wa chini alikuwa samaki. Hii inaonekana kuwa ndicho chanzo cha
wazo la kumchora hivyo nguva. Lucian hamwonyeshi ala kumuelezea mungu a Wasyria
huko Hierapolis pamoja na mungu wa Ashkelon, inaonekana kwa sababu za kwamba
mungu wa huko Hierapolis aliwa na umbo lote kamili la kibinadamu na alimuita
yeye kuwa Hera, lakini anakubali kwamba anaweza kujulishwa kama Rhea. Kuna
mashaka kidogo kwamba wanaweza kuwa ni mmoja nan i mungu mmoja huyohuyo.
Wafuasi wa miungu yote miwili, yaani Atargatis na Astarte hawakuwa wanakula
samaki, na kanuni za kijinsia ziliwatambulisha miungu wakike hao wote wawili
kama ni mmoja na ni mungu huyohuyo mmoja. Mungu alitofautishwa kwa kutokana na
eneo husika nah ii ndiyo ilikuwa tofauti ya kieneo kwenye akili na mawazo ya
watu wa kawaida ni kama yeye alivyokuwa kama Ishtar kwa Wasyria wa pande zote
mbili, yaani Ninawi na huko Arbela. Jina la kienyeji la Hierapolis ni Mabog na linamaanisha
majira ya machipuko kwa Kiaramu cha
wenyeji (soma ERE, ibid.). Hiyo kuna uhusiano wa maji na maji na majira haya ya
machipuko pia.
Kutokana na 2Makabayo
12:26, Yuda Makabayo aliliendea kimyume Hekalu la Atergatis lilikopo huko Karmion mwaka 164 KK na kuwauwa watu 25,000.
Paton anahitimisha kwenye maandiko yake kwenye 1Makabayo 5:43 kuwa dini ya Waatargatis
imeenea siyo tu huko Hierapolis na Askalon, bali hata Bashan. Utofauti wa kati
ya Damascus na Bamas huko Kefir Hauwar inaonyesha kuwa hekalu lilikuwepo huko
na pia idadi ya wafuasi ilikuwepo huko Delos, ikihesabu tangia kipindi kifupi
sana kabla ya kipindi cha Ukristo, akimjulisha yeye na Hadad na pia akimtambulisha
kama Aphrodite (soma ERE, vol. 2, p.166). kwa hiyo, yeye ni mwenza na Hadad,
jua au Baali. Ni kama Rhea alivyomhanithi Attis ambaye anamtambulikana pia na
yeye.
Paton pia anasema
kuwa maandiko ya Ovid ya mwaka 17 BK yanaelezea jinsi Dercetis alivyobadilika kuwa
samaki huko Palestina. Germanicus, mnamo mwaka wa 19 BK, anamuita yeye kuwa ni
mungu mke wa Wasyria, Derceto na Atargatus na anaongeza taarifa mpya kuwa
alibadilika na kuwa samaki huko Bamboyce jina la Kiyunani la Hierapolis. Maandiko
ya Strabo ya mwaka 24 BK yanasema:
Artargate (au Artagate kwenye baadhi ya tafsiri za MSS) kuwa Wasyria wanamuita yeye kuwa ni Arthara, lakini Ctesias anamuita Derketo. Hapa Artagatus anatambulika kama “Artar (=Ashrt, Astarte), kwa namna hiyohiyo ambayo kwayo ametambulika kama Aphrodite kwenye maandiko ya na marelezo ya Delos (soma ERE ibid).
Ceto is perhaps to be regarded as the
truncated form of Derceto, but Paton says this is uncertain (ERE ibid.). Cornitus (mnamo mwaka 68 BK) anasema
kwamba samaki na njiwa walikuwa ni watakatifu kwa mungu mke Atargatis watu wa
Syria. Bilashaka hiki ndicho chimbuko halisi la kuanza kwa alama ya samaki huko
Roma katika karne yak kwanza. Wakristo hawakuwa wakijingenezea kabisa au kuweka
alama ya imani yao, yaani sanamu au kiashiria chochote kilichokuwa kikitumika
na waabudu sanamu wa huko Palestina walizokwa wanazitumia katika nyakati za
kabla na hata baada Kristo. Pliny katika mwaka 79 BK anasema kwamba Ceto
anaabudiwa huko Yafa. Wote wawili, yaani Pliny na Strabo walionyeshwa kwenye
mabaki ya mifupa au skeleton zao kwa samaki au kiumbe mkubwa wa baharini
aliyekuwa ametengenezwa na kusimamishwa huko Yafa. Huenda Ceto anachukuliwa kuwa
alikuwa wa umbo lililofupishwa na Derceto, lakini Paton anasema hii haieleweki
na haina uhakika sana (ERE ibid.). Pliny anamuona Atargatis kama Derceto na anasema
kwamba alikuwa anaabudiwa huko Hierapolis au Bambyce au Mabog. Plutarch anasema
kulikuwa na dimbwi la maji la samaki mtakatifu huko Hierapolis na anasema
kwamba mungu mke huyu aliyekuwa akiabudiwa huko alijulikana na Aphrodite na
Hera au mingu mke aliyewapatia wanyama hao wakubwa mbegu za namna zote (ERE
ibid.). uhibitisho mkubwa sana ulitolewa la Lucian mwaka 200BK na ni kama ni shahidi
wa macho, na yeye mwenyewe akiwa ni Msyria. Ni kama tulivyojionea, anapendekeza
kumtambulisha yaye kuwa ni Hera, lakini Paton akasema kuwa bila shaka alikuwa
anashuhulika na Atargatis (ERE ibid.). Kwa hiyo dini potofu ya Atargatis,
Ishtar au Astarte, Ashitaroth au Easter ni misingi ya makatazo yaliyowekwa au
kuamriwa kwenye Biblia yakihusishwa na mambo haya ya namna mbalimbali. Masharti ya utakaso yanahusiana na kuondoa
utaratibu huu wa ibada. Ilirudisha hadi kwenye tarehe au nyakati za nyuma za imani
za kuabudu Ndama wa Dhahabu kwa kutumia majina mbalimbali (soma jarida la Ndama
wa Dhahabu (Na. 222). Kwa hivyo, imani na dizi za Attis na
Easter likuwa zingaliko bado huko Syria hadi mwishoni mwa miaka ya 200 BK.
Desturi za
utakaso na tohara zilionekana kama ukomeshaji wa dini na imani hizi za
urutubisho na za waabudu jua na kuziondoa kabisa katika Israeli na kwa watoto
wa Ibraham. Tohara kila wakati ilifanyika kwa Waarabu na iliingizwa kwenye
Uislamu bila kupingwa, kwa kuchukulia kigezo cha matendo ya kale, ambayo bila
shaka yalitoholewa kutoka kwa Ibrahimu. Uislamu una mapokeo yanayofanana kabisa
kuhusiana na wanaume, na kwa hiyo ufanyaji wa tohara ulifanyika kinadharia
baada ya siku saba. Hata hivyo, mara nyingi ilicheleshwa hadi miaka mitano,
sita au zaidi. Nywele za mtoto mchanga zilinyolewa pia na kupimwa uzito wake na
uzito kwenye dhahabu au fedha zilitolewa na kupewa mafukara. Kipindi cha
utakaso ni kipindi hichohicho cha siku arobaini na mzazi anaenda kuoga wakati
huu (ERE, vol. 2, p. 660).
Matenzo ya zamani
ya kumukomboa mtoto kwenye utoaji wa kafara ili asitolewe lilitokana pia kwenye
mapokeo na desturi za Kiislamu tangu nyakati za zamani sana. Neno ‘aqiqah’ linatumika kwa maana zote mbili,
yaani kunyoa kichwa cha mtoto na kitendo cha kumchinja mbuzi kwa ukombozi
katika siku ya saba (ERE ibid.). Kwa hiyo tohara ikakanganywa na kufanywa katika
siku ya saba kutokana utendaji wa zama
za kale. Nywele hapa zina maana sawa na ile ya Mnazarayo au Mnadhiri kwa sheria
za kibibilia, kwa kumweka wakfu kwa Mungu (soma pia ERE, vol. 12, p.148a).
Tunaweza
kulinganisha kutokana na uhusiano uliopo kati ya siku saba za utakaso na harakati
za tohara katika siku ya nane, na hivyo tunashughulikia mpango wa wokovu. Siku
ya saba ya utakaso inahusiana na kipindi cha mwisho cha milenia na utakasaji wa
ulimwengu wote. Siku ya nane inahusiana na ufufuo wa wafu na kufanywa upya kwa
miili duniani, kama sehemu ya taifa la Israeli na hatimaye kufanyika kuwa sehemu
ya Mji wa Mungu (sawa na Ufunuo 21:1-3) na lisemavyo jarida la Mji wa Mungu
(Na. 180). Wanawake wanatakaswa kwa Roho Mtakatifu na ndivyo watoto pia wanatakaswa
kwa kupitia wazazi wao.
Tutana hapo chini
dhana hii ya utakaso ikichukuliwa kwa viwango vya juu zaidi. Vitu vinavyotanjwa
kwenye Torati au Sheria ambavyo
vimetenganishwa kwa maana ya utakaso, tutaviona vikitakaswa na Masihi. Alama na
ishara hizi zina maana kubwa kwa wateule na haviwezi kueleweka kama vitafananishwa
na mwonekano wa kimwili ambao kwao tunaona Yuda wakinaswa nao kwa nyakati hizi.
Tohara ya
Wanawake
Utofauti uliopo kenye
sheria ya utakaso kuhusu utenganishaji ulionekana kabisa kuwa ulikusudia
kuanzisha tofauti nyingine ya wazi kuhusu kuwatofautisha kimahusiano kati ya
wanaume na wanawake. Hayo ni matendo ya unyanyasaji na yasiyo ya kistaarabu nay
a kipagani ya kutahiri wanawake, ambayo yalikuwepo kwa kipindi kirefu hata
kabla ya kuanza kwa imani za Kikristo na Uislamu na hata kabla ya kuanza kwa
imani ya Kiyahudi. Tohara ya wanawake haina uhusiano wowote kabisa na Mungu,
wla na Sheria zake na ni nyanyasaji wa kikatili na kibaradhuli tu wa kipagani,
unaotokana na desturi potofu na za kikengeufu za watu wa makabila ya Mashariki
ya Kati.
Tohara ya
wanawake inafaywa kwa kuondoa kisimi au
kigozi kinembe klichosimama kwenye
kuma, ambacho kinaunganisha pande mbili zote za duara ya kinembe. Utamaduni huu
ungali unafanywa bado na makabila ya Waarabu ya Moabu kunavyokaribia kipindi
cha kuolewa. Huenda chimbuko lake lilikuwa ni kuwatoa sadaka kwa mungu wao wa
rutuba na uzazi ili wajipatie watoto au uzao mwingi, lakini ilimaanisha kuwa
sadaka hii ni sehemu ya mtu badala ya kuwa ni mtu wote mzima, na ni kitendo
kilichokuwa kimeenea kwa Wamoabu. (soma ERE ibid.). Upanuaji na kuzidisha kwa sehemu
ya siri au kisimi kwa kumtahiri mwanamke kwa nia ya kumlinda dhidi ya wadudu ni
desturi potofu iliyotokana na baadhi ya makabila ya Mashariki ya Kati na hakuungwi
mkono kabisa na Bibilia wala na Korani.
Jinsi ya
Kuwalinda Watoto wa Kike
Moja ya desturi iliyokuwa imeenea sehemu
nyingi katika nyakati za zamani ilikuwa ni ya kuwatoa kafara watoto wadogo kwa
mungu Moleki na kwa mungu Mwezi aitwaye sin, au kama walivyoitwa jina lolote
lile kutegemea msimamo wa dini husika ulivyo alikokuwa akiabudiwa. Moja ya
desturi lililojulikana sana na kwamba ni ya kweli kutendeka kwenye mchakato huu
ni kwamba watoto wadogo walikuwa wanazikwa ili kutolewa sadaka/kafara kwa mungu
wa dunia. Kitendo hiki kilikuwa
pia cha zamani sana kama ilivyokuwa ile desturi ya tohara. Kitendo au desturi
hii ya Waarabu imeandikwa pia kwenye makala kuhusu Waarabu (wa Zamakale) (ERE,
vol.1, pp. 669ff.). Korani (Qur’an) iliandika desturi hii na kuielezea kuwa
kilifanywa kwa nia njema, kikijulikana kama cha ufukara (Sura za 5:15;17:33).
Muathirika wa
kitendo hiki aliuwawa bila kutoa damu. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba alizikwa
akiwa hai. Kitendo hiki chawezekana sana kwamba kilikuwa ni chanzo au sababu ya
kuanzishwa kwa sharia ya kuwalinda watoto wa kike. Maarifa au uwezo wetu wa
kujua kitendo hiki umeadimika sasa tangi kipindi hiki kirefu, lakini haiwezi kukosa
kujua kamba sheria ya makatazo tuliwekewa au tulipewa ikiwa kama ishara na
alama ya kumlinda toto wa kike katika Israeli na kujitoa kwake wakfu kwa Mungu
kwa kujitakasa na kujiondoa kutoka kwenye imani za kipagani za wamataifa, ambao
kwamba Israeli walikuwa wamechaguliwa na kuitwa.
Sheria ya utakaso
inaonekana pia kuwa na uhusiano na utenganishi wa Masihi, alipokuwa hajazaliwa
baso hapa duniani alipoletwa kenye huduma kwenye kipindi cha mwishoni mwa
milenia ya nne, au karne ya nne, akawa amezaliwa mwaka 5 KK. Mwanamke ambaye
alikuwa ni mwandani wa mme alitolewa nje na kuhifadhiwa sehemu nyingine akiwa ametenganishwa
kwa karne sabini kutoka zama ya Adamu hadi kwenye Ufufuo wa Kwanza wa Wafu na kisha
kwa zaidi ya miaka saba ya Milenia ya Nane. Kwa hiyo mwanaume alitahiriwa siku
ya nane, ikiwa pia ni alama ya mwishoni mwa utawala ilioonyeshwa ishara au mfano
kwa wanawake katika siku ya nane. Awamu ya mwisho ni ya bingu mpya na nchi
mpya.
Ishara au Alama ya Sheria na Dhabihu
Utaratibu wa
utoaji wa dhabihu wenyewe tu ulikuwa ni alama wa idadi kubwa ya mambo ya ibada.
Sadaka ya amani pamoja na uhusiano au ushirikiano wake na sikukuu ilionyesha
dhana ya kiushirikiano kati ya Mungu na mwanadamu. Tamid au sadaka ya daime ilionyesha madhiri ya Waisraeli wa utumishi
usiovunjika wa kumtumikia Yahova. Sadaka ya dhambi ni:
Kwa upakaji wa damu ulionyesha
kwamba moja ya masharti ya utakaso wenyewe kutokana na dhambi ilikuwa ni kujifanya
mtu mwenyewe kuwa ni mnyenyekevu zaidi mbele za Mungu (soma ERE,Vol. 12, p.148).
Tohara ilikuwa ni
alama ya kitaifa ya kujitoa kikamilifu kwa Yahova. Sabato ilikuwa ni alama au
ishara ya ukamilifu wa kazi ya uumbaji. Sabato yenyewe tu ni ishara ya utakaso
wa Israeli na wa watu wa Mungu (Kutoka 31:13).
Kwa hivyo
taratibu nyingine zozote za Sabato zinaashiria kumwabudu Mungu mwingine na kwa
mujibu wa Torati, ziwe zinaazisha ibada ya sanamu. Ni mchanganyiko wa utakaso
unaofuatiwa na utakaso wa Masihi.
Sheria yenyewe na
sheria za utakaso hazikuweza kumfanya mtu kuwa mkamilifu na kumpeleka kwenye
utawala mkamilifu ujao.
Waebrania 10:1-23: Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao. 2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? 3 Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. 4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. 5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; 6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; 7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. 8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), 9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. 10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. 11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. 12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; 13 tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. 14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. 15 Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema, 16 Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo, 17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. 18 Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi. 19 Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; 21 na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; 22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi. 23 Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu.
Kwa namna hii, tulikuwa tumetakaswa wote. Toashi na Mtu wa Mataifa, ambao
walizuiwa na Torati wasihudumu, walifanywa kuwa ni sehemu kwenye Hekalu la
Mungu kwenye dhabihu ya utumishi ya Yesu Kristo.
Matendo 8:26-40 Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. 27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, 28 akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. 29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. 30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. 32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. 33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi. 34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? 35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. 36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? 37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] 38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. 39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. 40 Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.
Kutokana na hali hii towashi hakuwa na sababu ya kuwa na mwalimu na Filipo aliondolewa ili kuonyesha miujiza katika Roho Mtakatifu, kwamba towashi alikuwa amefundisha moja kwa moja na Roho na hakuna na hitaji zaidi la mwalimu zaidi ya Kristo kwa njia ya Roho Mtakatifu akiwa ni nguvu au uweza wa Mungu ukiwa ni yote katika yote. Kile kilichokuwa kwenye dhambi kilitakaswa na kufanyika kuwa kitakatifu.
q