Makanisa ya Kikristo ya Mungu

 

[253]

 

 

 

Torati na Amri ya Kwanza

(Toleo La 3.0 19981005-20050522-20120805)

 

Jambo la kwanza katika hii Amri Iliyokuu nay a Kwanza ni kwamba tunaijua kuwa ni Amri ya Kwanza ya Mri hizi Kumi za Mungu. Sheria au Torati imeendelezwa na muundo mzima wa kanuni inayopelekea kufanyika ukamilifu wa Torati ya Mungu.

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hakimiliki © 1998, 2005, 2012 Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Torati na Amri ya Kwanza



Amri ya Kwanza kwenye kanuni

Tunaona kwamba Amri Kuu ya Kwanza imetajwa kwenye amri ya kwanza. Imani yote imefungamaneishwa kwenye tendo la kumcha na kumuabudu Mungu wa Pekee na wa Kweli. Anajufunua mwenyewe kupitia sheria au torati yake aliyoitoa pale Sinai kupitia Malaika wa Yahova, ambaye alikuwa ni elohimu kichwani mwa Israeli (Zekaria 12:8).

Kutoka 20:18-21 Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo akatetemeka, wakasimama mbali. 19 Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa. 20 Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi. 21 Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza kuu Mungu alipokuwapo.

Kwa hiyo, uweza wa Mungu ulikuwa kati yao kama mfano kwa kuwa hawakuwa na Roho Mtakatifu, kwa hiyo, wakiwa kama binadamu hawakuenenda kwa imani peke yake.

 

Neno lisilogawanyika

Neno la Mungu haligawanjyiki, linaenda kupima na linaipa haki kweli iliyokusudiwa (Mambo ya Walawi 19:36, 37). Tunapaswa kuzishika amri zake zote, kwa kuwa yeye ndiye Bwana atutakasahe, na ametuchagua tuwe watu wake hasa (pia soma Mambo ya Walawi 20:8; 22:31-33; Kumbukumbu la Torati 7:6-8; 10:14-17; 11:1-8; 13:18; 26:16-19).

Kumbukumbu la Torati 8:1-18 inasema: Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki. 2 Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. 3 Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana. 4 Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini. 5 Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo. 6 Nawe uzishike amri za Bwana, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha. 7 Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima; 8 nchi ya ngano na shayiri, na mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali; 9 nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake yafukuka shaba. 10 Nawe utakula ushibe, utamshukuru Bwana, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa. 11 jihadhari, usije ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo. 12 Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; 13 na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; 14 basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; 15 aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, 16 aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako. 17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. 18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

 

Bwana Mungu wet uni moto ulao na anatutangulia mbele yetu ili atuokoe na kutulinda. Israeli walienda na kuingia nchi ya Misri wakiwa ni watu sabini, na sasa sisi tu wengi na tusiohesabika hapa duniani (Kumbukumbu la Torati 9:1-6; 10:21, 22).

 

Sheria za uanachama wa maagano

Sheria za uanachama wa maagano zimefungamanishwa, au zimeansdikwa kwenye Maandiko Matakatifu yafuatayo:

Mwanzo 9:5-6; 15:1-21; 17:1,9,14; 18:17-19; Kutoka 4:22-23; 9:29; 12:1-51; 13:1-16; 20:1-3; 23:18; 36:3-7; 40:12; Mambo ya Walawi 12 (hususan aya ya 3); 15:1-33; 16:26,28; 17:11,15; 22:4,6,21; 23:10,17; Hesabu 9:1-14; 19:8; Kumbukumbu la Torati 10:14,16; 14:23; 15:19-22; 16:3-4; 23:8; 26:1-11; Zaburi 24:1; 49:7-8; Isaya 53:12; Yeremia 4:4; 6:10; 31:31-34; Ezekieli 36:25-26; Marko 10:45; Luka 1:59; 2:21,24; 22:37; Yohana 10:17-18; 15:13; Matendo 20:28; Warumi 2:28-29; 4:9-12; 6:23; 8:13,23; 11:16; 1Wakorintho 5:7-8; 10:26; 11:27-30; Wagalatia 2:3; Wafilipi 3:5; Wakolosai 2:11-13; Ufunuo 14:4 (pia soma jarida la Agano la Mungu (Na. 152) [The Covenant of God (No. 152)]

 

Amri ya Kwanza na Shema Israeli

Sikia Ee, Israeli Yahova Elohenu (ni) Yahova Echad (Kumbukumbu la Torati 6:4). Yahova Elohenu ni Yahova Mmoja; ambaye ni wa kwanza n ani mmoja tu saiye na mshirika, Mfalme Yahova (pia soma Kamusi ya Kiebrania maarufu kama Strong’s Hebrew Dictionary SHD 259).

 

Ili tuweze kuwa wana wa maagano tunapaswa kujitenga nafsi zeetu tunapoabudu sawa na alivyofanya Ibrahimu ambaye alilazimika kufanya hivyo (Mwanzo 12:1). Tunapaswa na kutakiwa kumuabudu yeye tu peke yake (Kumbukumbu la Torati 10:12,13; Mathayo 22:37; Marko 12:30; Luka 10:27). Mungu ni mfalme wetu, lakini tunafungwa kwenye sheria na amri zake na hatutakiwi tufanye yale yanayoonekana kuwa ni mema machoni mwetu tu (Waamuzi 17:6; 21:25; Kumbukumbu la Torati 12:8). Kumtumikia Mungu kupitia Mwana wake kumeagizwa na Maandiko Matakatifu (Zaburi 2:11, 12). Bwana ni Mungu wa milele na habadiliki na wala hana kigeu geu (Malaki 3:6).

 

Tunavaa utepe wa wa rangi ya bluu kama ishara ya kukumbuka sheria na amri za Mungu n ani ishara ya uaminifu wetu kwa Mungu. Sheria za Mungu zinatakiwa zikae kwa wingi mioyoni mwetu, na ziwe kama utepe machoni mwetu na mikononi mwetu (Kumbukumbu la Torati 11:18-20), bali za zisiwe kama tu ishara za kimwili tu. Torati inapaswa kusomwa kikamilifu na kwa kuirudia rudia. Bwana nim pole na si mwepesi wa hasira bali hatamsamehe mkosaji yeyote yule. Yeye ni Mungu mwenye wivu (Nahumu 1:1-3; Warumi 13:4)

 

Usimjaribu Bwana Mungu wako (Kumbukumbu la Torati 6:16; Mathayo 4:7, 10). Mche Mungu; na utamtumikia yeye peke yake (Kumbukumbu la Torati 10:20). Ametulisha kwa mana (Kumbukumbu la Torati 8:3) na neno litokalo kinywani mwake kwenye mapito yetu yote (Mathayo 4:4; Kutoka 17:1-7).

Kutoka 17:1-7 inasema: Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama Bwana alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe. 2 Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu Bwana? 3 Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? 4 Musa akamlilia Bwana, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe. 5 Bwana akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe; na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende. 6 Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli. 7 Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa sababu ya mateto ya wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu Bwana, wakisema, Je! Bwana yu kati yetu au sivyo?

 

Torati inatufanya tufikie kiwango ambacho hakuna mtu atakayeweza kuiabudu au kuitumikia miungu mingine inayofanywa kwa namna ya uchawi na afanyaye hivyo hawezi kuishi.

Kutoka 22:18 Usimwache mwanamke mchawi kuishi.

 

Kutoka 22:20 Mtu atakayemchinjia sadaka mungu ye yote, isipokuwa ni yeye Bwana peke yake, na angamizwe kabisa.  

 

Uchawi unahusisha imani potofu inayoamini kuwa roho za waliokufa zinaweza kuwasiliana na kushirikiana na walio hai. Inafanya kazi pia kwa mtazamo wa kama imani na mfumo wa kipagani wa ibada. Bali sisi tumekatazwa hata kutaja majina ya miungu yao na hata kuitaja miungu mingine tunapokuwa tunazungumza.

Kutoka 23:13 Yaangalieni hayo yote niliyowaambia; wala msitaje kabisa majina ya miungu mingine, wala yasisikizwe kutoka kinywani mwako

 

Anayepaswa kuabudiwa ni Yahova, wa Majeshi ambaye pia ni Eloa. Viumbe vyote vyenye roho vinavyomtukuza yeye huamtukuza vikilitumia jina hili la Yahova; kwa namna yoyote ile, ni Eloa na hakuna mwingine anayepaswa kuabudiwa. Viumbe wote wa aina zote mbili, yaani kiroho na kimwili, wanaomtumikia yeye wote haw ani elohimu, ambao ni mwendelezo wa Mungu huyu wa Pekee na wa Kweli, Eloa, Elohim. Hakuna anayetakiwa kumuasi huyo elohim au vinginevyo atawalaani.

Kutoka 22:28-31 Usimtukane Mungu, wala usimlaani mkuu wa watu wako. 29 Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao waume utanipa mimi. 30 Nawe utafanya vivyo katika ng'ombe zako, na kondoo zako; utamwacha siku saba pamoja na mama yake; siku ya nane utanipa mimi. 31 Nanyi mtakuwa watu watakatifu kwangu mimi; kwa hiyo msiile nyama yo yote iliyoraruliwa huko kondeni na mnyama wa mwitu; mtawatupia mbwa nyama hiyo.

 

Sambamba na hilo ni malimbuko ambayo yanatakiwa yatolewe haraka, kama ni kitu kinachotolewa kwa Mungu. Kwa jinsi hii, inaendelea hadi kwenye amri nyingine inayoonekana ikitokea kutoka kwenye amri ile ya kwanza. Sawa na hilo, Sikukuu na taratibu zake zote zinalenga kumfanyia ibada Mungu huyu wa Pekee na wa Kweli (soma Kutoka 23:17).

Kutoka 23:17 Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU.

 

Malaika wa Bwana

Mungu alimsimamisha Malaika wa Yahova mbele yao na waliamriwa wamtii. Na iwapo kama walimtii na kumuabudu Mungu wa Pekee na wa Kweli peke yake ndipo angelinda na kuwabarikia.

Kutoka 23:20-33 inasema: Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. 21 Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. 22 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao. 23 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali. 24 Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande. 25 Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. 27 Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao. 28 Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako. 29 Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. 30 Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi. 31 Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hata bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako. 32 Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao. 33 Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni tanzi kwako.

Hapa aliahidi kwamba atangewapa ardhi kutoka Bahari ya Shamu hadi kwenye mto Frati na kutoka bahari ya Mediterannia hadi Jangwani. Pia wangekuwa ni watu waliotukuka kama elohim, na kama malaika vichwani mwao (Zekaria 12:8).

 

Malaika wa Bwana anayehusika ametajwa kwenye Maandiko matakatifu yafuatayo: Mwanzo 16:10,13; 18:2-4,13-14,33; 22:11-12,15-16; 31:11,13; 32:30; Yoshua 5:13-15; 6:2; Isaya 63:9; Zekaria 1:10-13; 3:1-2. Kwenye Agano Jipya ametajwa kwenye sitabu cha Matendo 5:19; 12:7-11; 1Wakorintho 10:9; Ufunuo 22:18-19.

 

Mungu na Moleki

Migonmgano mikuu ya msingi ilikuwa ni kati ya taratibu mbili za kiibada, nazo ni jinsi ya kumuabudu Mungu na jinsi ya kumuabudu Moleki, jambo ambalo linaendelezwa hadi leo kwenye ibada za wanaojiita Wakristo na ibada zao za Easter.

 

Maandiko Matakatifu yameuelezea mgongano huu kwenye kitabu cha Mambo ya Walawi 18:21; 19:26,31; Kumbukumbu la Torati 12:29-32; 13:1-4; 18:9-22; 1Wafalme 11:7-8,33; Isaya 8:18-19; 47:10-14; Yeremia 32:35; 49:1,3; Zefania 1:4-5; 1Samweli 8:7-18; 15:10-35; 28:1-25; Mwanzo 9:4-6; Mambo ya Walawi 17:10-14; Kumbukumbu la Torati 12:15-16,23; Matendo 15:20; 1Wakorintho 10:16; Waefeso 2:13; Waebrania 9:14,22; 10:19-20; 1Petro 1:2; 1Yohana 1:7; Ufunuo 7:14; 12:11; Kumbukumbu la Torati 13:1-18; 18:13-22; Mambo ya Walawi 11:44; 19:2-4; 20:26; 2Wakorintho 7:1; 1Wathesalonike 4:7; 1Petro 1:15-16.

 

Zaka

Mungu ameweka utaratibu wa utoaji wa zaka katika ukamilifu wake ikiwa kama ishara ya kurudi kwetu na uaminifu wetu kwake (soma Malaki 3:7-12 na pia jarida la Zaka (Na. 161) [Tithing (No. 161)]. Wana wa Yuda hawakuingia ndani yake kwa ajili ya kuto kuamini kwao (Waebrania 4:6). Hata hivyo, Mungu (elohim) alijaribiwa na kukubalika na Mababa zetu wa imani wa kale (Mwanzo 28:20-22).

 

Utaratibu wa kutoa zaka uliendelea hadi kwenye masuala ya kodi na uliharibiwa na vita (Hesabu 31:25-54). Utaratibu wa kutoa zaka uliwekwa ili kuwezesha utaratibu wa ibada ufanyike na uende vyema (Kumbukumbu la Torati 14:22-29) na ili kuwalinda masikini (Kumbukumbu la Torati 26:12-15). Makabila yanatakiwa kutenga mahali patakapotumika kufanyia maadhimsho ya Sikukuu, kipindi ambacho hawatakiwi kula vitu malangoni mwao (Kumbukumbu la Torati 12:6,7,17,18; pia soma Kumbukumbu la Torati 16:2,7). Sikukuu alizoziamuru Mungu kuzitunza ziko tatu kwa ujumla wake (Kumbukumbu la Torati 15:3, 10-16), na utaratibu wake umetuama au umefungamanishwa kwenye utaratibu wa utunzaji wa Yubile (Mambo ya Walawi 25:1-7; Kutoka 23:11). Yote tunayoyafanya kwa ajili ya Mungu ni kwa mujibu wa utayari wa mapenzi na nia na sawa sawa na vile tunavyoweza. Kunatakiwa kuwe na utendaji wa kila jambo lililo kwenye mfumo wake ili kuthibitisha wito wetu (2Wakorintho 8:12; pia soma Malaki 3:7-12).

 


 

 

Sehemu ya II



Agano la kufanyika kuwa kama Mungu kwenye Hekalu la Mungu

Kutoka 24:1-18 inasema: Kisha Bwana akamwambia Musa, Kweeni wewe, na Haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini wa wazee wa Israeli, mkamfikilie Bwana; mkasujudie kwa mbali; 2 na Musa peke yake ndiye atakayekaribia karibu na Bwana; lakini hao hawatakaribia karibu; wala hao watu hawatakwea pamoja naye. 3 Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda.  

Hapa mpatanishi aliwekwa asimame kati ya Mungu na watu wake, na Musa aliwakilisha katika mwonekano na usemi wa kibinadamu na akafanya majukumu yake kama mpatanishi wa kiroho. Ngozo kumi na mbili za makabila kumi na mawili yaliwakilisha nguvo kumi na mbili za Hekalu la Mungu, wakati wale waamuzi kumi na wawili walikuwa ni mahakimu watakao zihukumu zile nguzo kumi na mbili, ambao ni Mitume wake Masihi.

Basi Musa akayaandika maneno yote ya Bwana, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli, 5 akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za amani za ng'ombe. 6 Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu. 7 Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii. 8 Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote

Agano hili linaashiria agano la damu, aambayo ilikuwa ni damu ya Masihi, ambaye kwaye agano jipya limefanyika baada ya kuwekwa lile la kwanza (soma jarida la Agano la Mungu (Na. 152) [The Covenant of God (No. 152)].

Ndipo akakwea juu, Musa, na haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini miongoni mwa wazee wa Israeli; 10 wakamwona Mungu wa Israeli; chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi, kama zile mbingu zenyewe kwa usafi wake. 11 Naye hakuweka mkono wake juu ya hao wakuu wa wana wa Israeli; nao wakamwona Mungu, wakala na kunywa. 12 Bwana akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa mbao za mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe. 13 Musa akaondoka na Yoshua, mtumishi wake, Musa akapanda mlimani kwa Mungu. 14 Akawaambia hao wazee, Tungojeeni hapa, mpaka tutakaporudi kwenu; na tazameni, Haruni na Huri wapo pamoja nanyi; kila mtu aliye na neno na awaendee. 15 Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima. 16 Na huo utukufu wa Bwana ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu. 17 Na kuonekana kwake ule utukufu wa Bwana kulikuwa kama moto uteketezao, juu ya mlima machoni pa wana wa Israeli. 18 Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arobaini, mchana na usiku.

Maskani au Hekalu la Mungu lilipaswa lijengwe kutokana na sadaka iliyotolewa kwa moyo wa hayari, na wapewe wale wote waliopenda kushiriki ujenzi. Hii ilikuwa ni ashirio la jinsi tunavyotakiwa kujitoa kwa hiyari kuwa ni sadaka ya hiyari ya kila mmoja wetu, kwa wote wanaopenda kuwa ni sehemu ya Hekalu la Mungu, Hekalu ambalo ni sisi (1Wakorintho 3:17).

 

Kutoka 25:1-40 [INATAKIWA ISOMWE YOTE NA KIKAMILIFU]

Andiko hili linahusu ujenzi wa Maskani, na utoaji wa sadaka ya hiyari ambazo zililenga kwa mahitaji ya ujenzi wa jingo hili. Maelekezo ya ujenzi wa Hekalu hili yalikuwa wazi na yalihusika na mapambo, na maelekezo haya yalitakiwa yafuatwe kwa uangalifu mkubwa na bila kukosea.

 

Maelekezo ya kuweka mapazia kumi uliaonekana tena kwenye vinara kumi vilivyowekwa kwenye Hekalu la Sulemani. Mapazia kumi yakipaswa yawekwe na yaende hadi yafike kwenye Utawala wa mwisho wa Mungu. Mwenendo huu unamuashiria Masihi, Makanisa Saba na Mashahidi wawili, ambao kila mmoja wao ana kinara kimoja cha taa. Ile ya kumi na moja inatokana na zile kumi, na inamaanisha kurudi kwa Masihi na atakavyokuja kuanzisha Ufalme wa Mungu utakaodumu kwa kipindhi cha milenia.

 

Kutoka 26:1-37 [ISOMWE YOTE NA KIKAMILIFU]

Hapa kunatolewa maelekezo makamilifu yanayohusiana na yale mapazia na ewepo wake kwenye ile Maskani. Idadi yake na rangi zake vinaelekezwa na ukamilifu na vipimo vyake kamili na mapambo yake halisi yametolewa, pamoja na maelekezo ya jinsi vitakavyoweza kupangiliwa kwa kufungwa sehemu zake muafaka, na malighafi zitakazotumika. Hata mabaki ya mapazia haya yatakayosalia yalitakiwa yatumike. Tendo hili kwa kweli liliashiria ujenzi wa nyumba au hekalu la kiroho, ambalo hakuna hakuna kitakachoachwa, kupotea, au kucha pasipo kutumiwa.

 

Mwonekano waliokuwanao wale makerubi na jinsi majukumu yao yalivyo kwenye pande zote nne za dunia. Viumbe wale waliohai wanne wanaoonekana kwenye Ufunuo sura ya 4 na 5 ni makerubi walio kwenye maeneo yao (soma Ezekieli 1:1ff.).

 

Kutoka 27:1-21 [ISOMWE YOTE NA KIKAMILIFU]

Mgawanyo wa Maskani na nguzo huashiria nguzo za Hekalu la Mungu kwa idadi yao, na idadi kamili huashiria utawala wa Mungu.

 

Vazi la kikuhani linamaana pia na ujio wa Roho Mtakatifu, ambako kuko kwenye maziwa ya kifuani kwa kuhani, ni kama ilivyo Urimu na Thumimu zilivyokuwa kwenye mfuko wa Kuhani Mkuu.

 

Kutoka 28:1-43 [ISOMWE YOTE NA KIKAMILIFU]

Sura hii inelezea kwa kina vazi la Haruni na wanawe. Kila kitu kinaelezewa na kutolewa maana yake jinsi itakavyovaliwa. Mavazi haya ni matakatifu na yanatakiwa yashonwe na watu walio na mioyo yenye busara na waliojazwa na Roho Mtakatifu.

 

Mawe kumi na mawili yanawakilisha makabila kumi na mawili na umoja wa kitaifa. Ukuhani wa wateule katika Roho Mtakatifu ni matokeo ya mwisho ya Hekalu. Ukuhani wa Hekalu wenyewe unaelekea kwenye ukuhani wa wateule, wakiwa kama Hekalu la kiroho la Ufalme wa Mungu. Limejengwa kwa mgawanyo wa tangia mawe talilo hai na tawala za dunia kwa Roho Mtakatifu katika kipindi cha utawala wa milenia wa Yesu Kristo. Atatawala kwa niaba ya Baba yake.

 

Kutoka 29:1-46 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

 

Andiko hili linahusu kuwekwa wakfu kwa Haruni na wanawe. Sadaka inayohitajika imeelezwa pia na jinsi sherehe itakavyokuwa.

 

Masihi amewatakasa na kuwaweka wakfu wateule wake wote kwa sadaka ya damu yake, kwa shuke ya taji ya miiba na misumari aliyopigiliwa miguuni vidoleni. Yeye etutakasaye na wale wanaotakaswa wote wana asili moja tu. Wote wanalipwa kwa dhabihu ya Masihi nah ii ndiyo maana ya ile nusu shekeli iliyoagiizwa au kuamriwa kutolewa: isingeweza kulipwa na.

 

Kutoka 30:1-38 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Kwenye sura hii ya Kutoka, Haruni anaelekezwa ajenge madhabahu. Madhabahu itakayotumika kuteketeza uvumba wenye harufu nzuri milele na isitumiwe kwa kufukiza aina yoyote ya uvumba wa kigeni au kwa sadaka ya kuteketezwa au nyma au sadaka ya kinywaji. Haruni, kama Kuhani Mkuu, aliambiwa afanye upatanisho hapo mara moja kwa mwaka.

 

Wateule ni makuhani wa kifalme awanapaswa kutiwa mafuta wakiwa watakatifu kwa mafuta ya Roho Mtakatifu. Mungu anawaita wateule wake wote kwa majina yao na amewatenga kwa ajili ya kazi yake Bwana katika kulijenga Hekalu lake.

Kutoka 31:1-11 inasema: Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; 3 nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, 4 ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, 5 na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. 6 Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza; 7 yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema; 8 na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba; 9 na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake; 10 na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani; 11 na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.

 

Uaminifu wa Israeli inageuka geuka au kubadilika badilika na watu wameyumbishwa kwa kuwa Mungu alimchelewesha mtiwa mafuta wake Musa, sawa na kama alivyomchelewesha mtiwa mafuta wake Masihi. Na watu wakajikuta wameingia kwenye ibada za sanamu hatimaye kama wafanyavyo leo.

 

Kutoka 32:1-35 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Imani na taratibu za miungu iliyokuwa zama za kabla ya Kutoka kwao utumwani ilifantizwa kwa vito au pete ambavyo umbo lake lilifanyizwa kwa mwonekano uliowakilisha mwonekano wa miungu. Vito hivi ambavyo ni pete vilitendenezwa kwa dhahabu na ndivyo vilimtoa yule ndama wa dhahabu ambaye kwaye walisababishiwa kuondolewa kutoka kwenye milki za Israeli. Ndama huyu wa dhahabu alikuwa ndiye taswira ya mfumo wa kidini wa zama za kale, na alikuwa na uhusiano na ibada za mungu mwezi aliyejulikana kama Sin na alikuwa anaonekana au kuchongwa kwa mwonekano aina mbali mbali. Dini hii pia ilikuwa na uhusiano wa ibada za oak na kufungamanishwa na sikukuu za Krismas na Easter ambazo zilikuwa ni kilele cha ibada za Kipagani (soma jarida la Ndama wa Dhahabu (Na. 222) na Chanzo cha Krismas na Easter (Na. 235) [The Golden Calf (No. 222) and The Origins of Christmas and Easter (No. 235)].

 

Kutoka 33:1-23 inasema: Bwana akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii; 2 nami nitamtuma malaika aende mbele yako; nami nitawafukuza Mkanaani, na Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi; 3 waifikilie nchi imiminikayo maziwa na asali; kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia. 4 Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hapana mtu aliyevaa vyombo vyake vya uzuri. 5 Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa vueni vyombo vyenu vya uzuri ili nipate kujua nitakalowatenda. 6 Basi wana wa Israeli wakavua vyombo vyao vyote vya uzuri, tangu mlima wa Horebu na mbele. 7 Basi desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya marago mbali na hayo marago; akaiita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa Bwana, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya marago. 8 Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake, akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani. 9 Ikawa Musa alipoingia humo hemani, ile nguzo ya wingu ikashuka, ikasimama mlangoni pa ile hema; naye Bwana akasema na Musa. 10 Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake. 11 Naye Bwana akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani. 12 Musa akamwambia Bwana, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Walakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu. 13 Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. 14 Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. 15 Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. 16 Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi? 17 Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako. 18 Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. 19 Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu. 20 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. 21 Bwana akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba; 22 kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita; 23 nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana.

Hapa Bwana anamwambia Musa aondoke na kwenda kwenye Nchi ya Ahadi. Malaika atawatangulia mbele yao na maadui zao watasukumwa na kuondolewa watoke. Musa alisimika Maskani nje ya hema, na hapo ndipo Musa alionhea na Bwana. Aliomba Uwepo wa Mungu uende pamoja naye. Musa akaambiwa kwamba hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wake na akaishi; hata hivyo Musa akaruhusiwa kuuona utukufu wake tu na sehemu yake ya nyuma. Masihi ndiye huu Utukufu wa Bwana. Hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu huyu Mkuu, na wala hakuna aliyewahi kuliona umbo lake, na wala hakuna aliyewahi kuisikia sauti yake wakati wowote ule (Yohana 1:18; 5:37; 1Timotheo 6:16; 1Yohana 5:20).

 

Kutoka 34:1-35 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Mawe mawili ya Torati yamewekwa, na Musa anaomba kwa ajili ya msamaha wa watu. Mungu atawaondoa au kuwafukuzilia mbali maadui zao bali hawatakiwi kufanya agano la namna yoyote ile na watu wan chi au wenyeji wan chi wanayoiendea, bali wanapaswa kuziharibu na kuziteketeza madhabahu, na kuvivunja vinyago au sanamu na ashera wanazozikuta huko (Kumbukumbu la Torati 16:21-22). Waliamriwa kuwa wasiabudu miungu mingine. Pia waliamriwa wasiwaoe watu wa makabila haya mengine, kwa kuwa watashawishika kuiabudu na kuitumikia miungu yao. Pia waliamriwa wasijitengenezee mingu mingine ya namna yoyote ile.

 

Idi ya Mikate isiyo na Chachu inapaswa kuadhimishwa. Wazaliwa wote wa kume ni wa Bwana, ieipokuwa mzaliwa wa kwanza wa farasi, ambaye anaweza kubadilishwa kwa mwana kondoo, au vinginevyo, shingo lake livunjwe. Wazaliwa wa kwanza wote wa wanadamu ni lazima wakombolewe na hakuna anayeruhusiwa kuja mbele za Mungu akiwa mikono mitupu. Sabato, idi ya majuma na Sikukuu ya Kukusanya au ya Vibanda ni lazima ziadhimishwe. Ni mara tatu kila mwaka wanaume wote na wajitokeze mbele za Bwana Mungu wa Israeeli. Kisha, Mungu atayasukuma au kyaondoa mataifa na kuipanua mipaka ya Israeli, na kuilinda nchi yake. Agano lililopo kati ya Mungu na wanadamu limefanywa kwa ajili hii. Musa alifunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipokuwa akiandika Amri hizi Kumi za Mungu na agano hili (Kumbukumbu la Torati 10:1-11).

Kumbukumbu la Torati 10:1-11 inasema: Wakati ule Bwana akaniambia, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, kisha uje kwangu huku mlimani, ukajifanyie na sanduku la mti. 2 Nami nitaandika juu ya hizo mbao maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, ulizozivunja, nawe uzitie ndani ya hilo sanduku. 3 Basi nikafanya sanduku la mti wa mshita, nikachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, nikakwea mle mlimani, na zile mbao mbili mkononi mwangu. 4 Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi, alizowaambia Bwana huko mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano; Bwana akanipa. 5 Basi nikageuka nikashuka kutoka mlimani, nikazitia mbao ndani ya sanduku nililofanya; nazo zimo humo kama alivyoniamuru Bwana. 6 (Wana wa Israeli wakasafiri kutoka visima vya Bene-Yaakani kwenda Mosera; Haruni akafa huko, akazikwa huko; na Eleazari mwanawe alitumika utumishi wa ukuhani badala yake. 7 Wakasafiri kutoka huko kwenda Gudgoda; wakatoka Gudgoda wakaenda Yotbatha, nayo ni nchi ya vijito vya maji. 8 Na wakati huo Bwana aliitenga kabila ya Lawi ili walichukue lile sanduku la agano la Bwana, wasimame mbele ya Bwana kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo. 9 Ndipo asiwe na fungu Lawi, wala urithi pamoja na nduguze; Bwana ndiye urithi wake, kwa mfano wa vile alivyomwambia Bwana, Mungu wako.) 10 Nikakaa mle mlimani kama hapo kwanza, siku arobaini usiku na mchana; Bwana akanisikiza wakati huo nao; asitake Bwana kukuangamiza. 11 Bwana akaniambia, Ondoka, ushike safari yako mbele ya watu; nao wataingia waimiliki nchi, niliyowaapia baba zao ya kuwa nitawapa.   

 

Andiko hili linatuonyesha kuwa ridhaa ya Mungu kwa ufunuo binafsi wa mtu au kujifunua kwa mtu binafsi yake, na kwamba jambo hili ni mchakato endelevu kwa wale ambao amewaita na kuweka mamlaka yake. Utaratibu huu unaashiria kwa Masihi na matendo au kazi zake za tangu Mwanzo wa kuwepo kwake.

 

Kutoka 35:1-35 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Musa aliwaelekezwa watu kwa kupitia torati. Bwana anawaamuru kutolewe sadaka kutoka kwa wale wanaotoa kwa moyo wa mkunjufu na wakupenda peke yao. Kwenye ujenzi wa Hekalu utoaji wa hiyari ndio ulitumika kwa watu kuleta mahitaji yote yaliyotakiwa kwa kazi ya Mungu, wakati kwamba wale waliokuwa wametunukiwa vipawa na Roho Mtakatifu walifanya kazi za ufundi kwa mambo yote yalikuwa yamehitajika kwa moyo wa kupenda na ushiriki wa hiyari na sio kwa shuruti.

 

Maskani iliwekwa tangu siku ya Kwanza ya mwezi wa Kwanza. Kipindi hiki ni ashirio la la utakaso wa wateule kwa mujibu wa Kalenda Takatifu, inayoanzia na utakaso wa Hekalu ya mwezi wa Kwanza. Tendo la watu wa Yuda la kuuweka Mwaka Mpya kuwa unaanza mwezi wa Saba na pengine hata mwezi wa Nane linakanganya uanzishaji huu na mchakato wake. Matendo yajulikanayo kama Rosh Hashanah ni ya desturi au mapokeo ya marabi walioishi kipindi cha zama za baadae baada ya kujengwa hekalu, na ulioingizwa kutoka Babeli na ulianzishwa tabgia karne ya tatu ya zama zetu za leo. Haikuwa ikitumika kamwe katika kipindi cha Hekalu hadi kipindi cha kuteketezwa kwake mnamo mwaka wa 70 BK (soma jarida la Utakaso wa Hekalu la Mungu (Na. 241) [Sanctification of the Temple of God (No. 241)] na pia kitabu cha R. Samuel. Kohn, kijulikanacho kama Wasabato wa Transylvania (The Sabbatarians in Transylvania), ed. Cox, tr. McElwain and Rook, CCG Publishing, 1998, cf. Foreword p. v).

 

Kutoka 40:1-38 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Wakati Hekalu litakapojengwa, Utukufu wa Bwana utaifunika Maskani. Wana wa Israeli watalindwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu chini ya Masihi, ambaye ni Nguzo ya Moto na Mawingu.

 

Dhanihu na Sadaka

Maandiko yafuatayo yanaelezea juu ya dhana au fundisho la kumtolea Mungu dhabihu likiwa ni tendo la ibada katika utaratibu wa Amri ya Kwanza.

Mambo ya Walawi 1:1-17 inasema: Bwana akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia, 2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea Bwana matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng'ombe na katika kondoo. 3 Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya Bwana. 4 Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake. 5 Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Bwana; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kando-kando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania 6 Kisha atachuna sadaka ya kuteketeza na kuikata vipande vyake. 7 Kisha wana wa Haruni, watatia moto juu ya madhabahu, na kuzipanga kuni juu ya moto, 8 kisha wana wa Haruni, makuhani, watazipanga kuni zilizo juu ya moto uliopo juu ya madhabahu; 9 lakini matumbo yake, na miguu yake, ataiosha kwa maji; na huyo kuhani ataviteketeza vyote juu ya madhabahu, ili iwe sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana. 10 Na matoleo yake kwamba ni katika kundi, katika kondoo, au katika mbuzi, kuwa sadaka ya kuteketezwa; atatoa mume mkamilifu. 11 Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za Bwana; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote. 12 Kisha atamkata vipande vyake, pamoja na kichwa chake, na mafuta yake; kisha atavipanga vile vipande juu ya kuni zilizo juu ya madhabahu; 13 lakini matumbo yake, na miguu yake, ataosha kwa maji; na huyo kuhani atavisongeza vyote na kuviteketeza juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana. 14 Na matoleo yake atakayomtolea Bwana kuwa sadaka ya kuteketezwa, kwamba ni katika ndege, ndipo atakapoleta matoleo yake katika hua au katika makinda ya njiwa. 15 Kisha kuhani atamleta karibu na madhabahu, naye atamkongonyoa kichwa, na kumteketeza kwa moto juu ya madhabahu; na damu yake itachuruzishwa kando ya madhabahu; 16 kisha atakiondoa kile kibofu chake, pamoja na taka zake, na kukitupa kando ya madhabahu upande wa mashariki, mahali pa majivu; 17 kisha atampasua na mabawa yake, lakini asimkate vipande viwili; kisha kuhani atamteketeza juu ya madhabahu, juu ya kuni zilizo juu ya moto; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.

 

Kwenye andiko hili, sadaka inatakiwa itolewe kutoka kwenye mifugo au wanyama. Inatakiwa iwe ya dume la mnyama na asiwe na mawaa, na atolewe kwa moyo wa hiyari na kupenda kwa Bwana. Sadaka ya kuteketezwa inatakiwa pia iwe ya ndege, ambaye ni ya kinda la njiwa au njiwa ndogo.

 

Mambo ya Walawi 2:1-16 inasema: Na mtu atakapomtolea Bwana matoleo ya sadaka ya unga, matoleo yake yatakuwa ya unga mwembamba; naye ataumiminia mafuta, na kutia na ubani juu yake; 2 kisha atauleta kwa wana wa Haruni, hao makuhani; naye atatwaa konzi moja katika huo unga mwembamba, na katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha kuhani atauteketeza kuwa ndio ukumbusho wake juu ya madhabahu, ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana; 3 na huo uliosalia wa ile sadaka ya unga utakuwa ni wa Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. 4 Tena, utakapotoa matoleo ya sadaka ya unga uliookwa tanuuni, yatakuwa mikate isiyotiwa chachu, ya unga mwembamba uliokandwa na mafuta, au maandazi yasiyochachwa yaliyopakwa mafuta. 5 Tena matoleo yako kwamba ni sadaka ya unga wa kaangoni, yatakuwa ya unga mwembamba usiotiwa chachu, uliokandwa na mafuta. 6 Utaukata-kata vipande, na kutia mafuta juu yake; ni sadaka ya unga. 7 Tena matoleo yako kwamba ni sadaka ya unga ya chunguni, yataandaliwa kwa unga mwembamba pamoja na mafuta. 8 Nawe utamletea Bwana sadaka ya unga iliyofanywa ya vitu hivyo; nayo italetwa kwa kuhani, naye ndiye atakayeisongeza madhabahuni. 9 Kisha kuhani atatwaa humo huo ukumbusho wa sadaka ya unga, naye atauteketeza juu ya madhabahu; ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana. 10 Na hicho kitakachosalia katika sadaka ya unga kitakuwa cha Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. 11 Sadaka ya unga iwayo yote itakayosongezwa kwa Bwana isitiwe chachu kabisa; kwa kuwa hamtateketeza chachu, wala asali iwayo yote, kuwa ni sadaka ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. 12 Vitu hivyo mtavisongeza kwa Bwana kuwa ni malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza. 13 Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote. 14 Nawe kwamba wamtolea Bwana sadaka ya unga ya malimbuko, utatoa hiyo ngano katika masuke yake iliyochomwa motoni, ngano iliyopondwa ya masuke mabichi, ndiyo utakayoleta kuwa sadaka ya unga ya malimbuko yako. 15 Nawe utatia mafuta juu yake, na kuweka ubani juu yake; ni sadaka ya unga. 16 Huyo kuhani atauteketeza ukumbusho wake, yaani, sehemu ya ngano iliyopondwa ya hiyo sadaka, na sehemu ya mafuta yake, pamoja na ule ubani wake wote; ni kafara ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.

Maagizo haya yanahusiana na maelekezo ya sadaka ya nyama. Kikomo cha torati kuhusiana na malimbuko imekuwa ni jambo linalovunjwa kila mara na watu wasio kwenye imani ya kweli na maadui wa Torati au sheria za Mungu.

 

Mambo ya Walawi 3:1-17 inasema: Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya Bwana. 2 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. 3 Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo, 4 na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na hicho kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa. 5 Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana. 6 Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia Bwana, kwamba ni katika kundi la kondoo; mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu. 7 Kama akimtoa mwana-kondoo kuwa matoleo yake, ndipo atakapomtolea Bwana; 8 naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemsongeza, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. 9 Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani dhabihu kwa Bwana, itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yake, na mkia wenye mafuta mzima, atauondoa kwa kuukata hapo karibu na mfupa wa maungoni; na mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo, 10 na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa. 11 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. 12 Na matoleo yake, kwamba ni mbuzi, ndipo atakapomtoa mbele za Bwana; 13 naye ataweka mkono wake kichwani mwake, na kumchinja hapo mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. 14 Naye atasongeza katika sadaka hiyo matoleo yake, dhabihu kwa Bwana kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo, 15 na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini pamoja na hizo figo mbili; hayo yote atayaondoa. 16 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya Bwana. 17 Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa. 

Haya ni maelekezo yahusuyo sadaka za amani. Wanaweza kutokana na majike au madume ya wanyama au mifugo na wanapaswa wawe wasio na mawaa. Ni agizo la milele kuwa hakuna damu wala mafuta yanayotakiwa kuliwa (pia soma Kutoka 20:24-26).

 

Mambo ya Walawi 4:1-35 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Hapa ndipo dhambi inayofanywa kwa kvunja Amri kwa kutokujua inaposhughulikiwa. Upatanisho unalenga kwa Yesu Kristo, bali imeonekana ikiendelea kama ni wajibu wa watawala nay a kila mmoja binafsi yake.

 

Kwenye maandiko yafuatayo, dhambi inayofanywa kwa kuvunja amri amri pasipo kujua inashughulikiwa. Upatanisho unalenga kwa Yesu Kristo, bali ilionekana ikiendelea kama ni wajibu wa watawala na ya kila mmoja binafsi

Mambo ya Walawi 5:14-19 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 15 Mtu awaye yote akiasi na kufanya dhambi naye hakukusudia, katika mambo matakatifu ya Bwana; ndipo atakapomletea Bwana sadaka yake ya hatia, kondoo mume mkamilifu katika kundi lake; sawasawa na hesabu utakayomwandikia katika shekeli za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu, kuwa sadaka ya hatia; 16 naye atalipa kwa ajili ya hilo alilolikosa katika kitu kile kitakatifu, kisha ataongeza na sehemu ya tano, na kumpa kuhani; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa huyo kondoo mume wa sadaka ya hatia, naye atasamehewa. 17 Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia vivyo, naye atachukua uovu wake. 18 Naye ataleta kondoo mume wa kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, amsongeze kwa huyo kuhani; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya jambo hilo alilolikosa pasipo kukusudia, asilijue, naye atasamehewa. 19 Ni sadaka ya hatia; hakika yake ni mwenye hatia mbele za Bwana.

 

Andiko hili linahusika na dhabihu itolewayo kwa ajili ya dhambi zilizofwanywa bila kukusudiwa au pasipo kujua dhidi ya vitu vitakatifu vya Mungu. Hapa sadaka inayotolewa ni ya mwana kondoo asiye na mawaa na marekebisho yanatakiwa yafanywe kwa kuongeza sehemu ya tano. Tendo la kuvunja sheria za Mungu pasipo kujua bado inakuwa ni uvunjifu tu na usio na udhuru na kunahitajika ukombozi. Kutojua hakuwezi kuwa ni sababu yenye kumfanya mtu kusamehewa, na taifa linabakia likilaumiwa kwa kufanya kwake hivyo.

 

Mambo ya Walwi 6:8-30 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Maelekezo ya kina zaidi yanatolewa kuhusu sadaka ya kuteketezwa. Moto hautakiwi kabisa uwake madhabahuni, na haitakiwi uchukuliwe au kutolewa nje kabisa.

 

Mambo ya Walawi 7:1-38 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Mwendelezo wa maelekezo yahusuyo dhabihu na sadaka umetolewa hapa. Utakaso wa kuhani unaffanyika kwa sadaka na upako ulio kwa mujibu wa mapokeo au ratatibu zilivyo, ambazo zinamlenga mteule. Sheria zote za mambo ya utoaji wa sadaka na dhabihu zilikuwa zinamlenga Masihi na utaratibu pya na mkuu wa Israeli uliokuwa chini ya utaratibu wa kikuhani uleoendelezwa.

 

Mambo ya Walawi 8:1-36 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Andiko hili linahusu kuwekwa wakfu kwa Haruni na wanawe.

 

Maamuzi ya jinsi ya kutoa sadaka yanafanywa na Mungu. Yeye humuita yule anayependezwa naye na hakatai au kuzuia matumizi ya madaraka kwenye mfumo wake na sheria zake.

 

Mambo ya Walawi 10:1-20 inasema: Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana, ambao yeye hakuwaagiza. 2 Kisha moto ukatoka hapo mbele za Bwana, nao ukawala, nao wakafa mbele za Bwana. 3 Ndipo Musa akamwambia Haruni, Jambo hili ni hilo Bwana alilolinena, akisema, Nitatakaswa mimi katika hao wanikaribiao, nami nitatukuzwa mbele ya watu hao wote. Haruni akanyamaza kimya. 4 Musa akawaita Mishaeli na Elisafani, wana wa Uzieli mjombaye Haruni, na kuwaambia, Njoni karibu, mwachukue hawa ndugu zenu, mkawaondoe hapa mbele ya maskani, mwende nao nje ya marago. 5 Basi wakaja karibu, na kuwachukua, hali wamevaa nguo zao, wakawachukua nje ya marago; kama Musa alivyosema. 6 Kisha Musa akamwambia Haruni na wanawe Eleazari na Ithamari, Msiache wazi nywele za vichwani mwenu, wala msiyararue mavao yenu; ili kwamba msife, tena asiukasirikie mkutano wote; lakini ndugu zenu, nyumba yote ya Israeli, na waomboleze kwa ajili ya hicho kichomo alichowasha Bwana. 7 Wala hamtatoka nje mlangoni mwa hema ya kukutania, msije mkafa; kwa sababu mafuta ya kutiwa ya Bwana ya juu yenu. Nao wakafanya kama hilo neno la Musa. 8 Kisha Bwana akanena na Haruni, na kumwambia, 9 Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu; 10 kisha, mpate kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na hayo yaliyo ya siku zote, na kati ya yaliyo najisi na hayo yaliyo safi; 11 tena mpate kuwafundisha wana wa Israeli amri hizi zote ambazo Bwana amewaambia kwa mkono wa Musa. 12 Kisha Musa akanena na Haruni, na Eleazari, na Ithamari, hao wanawe waliobaki, Twaeni hiyo sadaka ya unga iliyosalia katika kafara za Bwana zilizotolewa kwa moto, mkaile pasipo kutiwa chachu, pale karibu na madhabahu; kwa kuwa ni takatifu sana; 13 nanyi mtaila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni haki yako, na haki ya wanao, katika hizo kafara zisongezwazo kwa Bwana kwa moto; kwani ni hivyo nilivyoagizwa. 14 Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe; kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wa Israeli. 15 Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha kutikiswa, Watavileta pamoja na dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto, za hayo mafuta ili kuvitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana; kisha vitakuwa ni vyako wewe, na vya wanao pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama Bwana alivyoagiza. 16 Kisha Musa akamtafuta sana huyo mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye, tazama, alikuwa amekwisha kuchomwa moto; naye akawakasirikia hao Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni, hao waliobaki, akawaambia, 17 Kwa nini hamkula hiyo sadaka ya dhambi katika mahali patakatifu, kwa kuwa ni takatifu sana, naye amewapa ninyi ili kuuchukua uovu wa mkutano, na kuwafanyia upatanisho mbele za Bwana? 18 Angalieni, hiyo damu yake haikuletwa ndani ya mahali patakatifu; iliwapasa kuila ndani ya mahali patakatifu, kama nilivyowaagiza. 19 Haruni akamwambia Musa, Angalia, hivi leo wamesongeza sadaka yao ya dhambi, na sadaka yao ya kuteketezwa, mbele za Bwana; kisha mambo kama haya yamenipata; tena kama ningalikula hiyo sadaka ya dhambi hivi leo, je! Lingekuwa ni jambo la kupendeza mbele za macho ya Bwana? 20 Naye Musa aliposikia hayo, yakampendeza.

Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, waliwasha moto wa kigeni mbele za Bwana na wakafa. Unywaji wa mvinyo au pombe kali mapema kabla ya kuhudumu kwa Bwana Hekaluni mwake umekatazwa  pia.

 

Dhabihu zinatakiwa ziliwe mahali patakatifu na Haruni na wanawe na binti zake, na maeneo maalumu waliyoruhusiwa yameelekezwa. Utaratibu wote wa kutoa dhabihu na kuchinja umeruhusiwa na Mungu; kwa hiyo, uchinjaji wa wanyama pasipo kuruhusiwa na Mungu, wenyewe tu ilikuwa ni dhambi.

Mambo ya Walawi 17:7-9 Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi. 8 Nawe utawaambia, Mtu awaye yote katika nyumba ya Israeli, au miongoni mwa wageni, wanaokaa nao, atoaye sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, 9 wala haileti mlangoni pa hema ya kukutania, ili aisongeze kwa Bwana basi mtu huyo atatengwa na watu wake

 

Tendo la kula nyama ambayo haijatolewa na kuwekwa wakfu kwa Mungu sio dhambi, wakati kwamba tendo la kuua wanyama kwa kiwango kisochomilikika au stamilika na mtu (soma jarida la Uvijiterania na Biblia (Na. 183) [Vegetarianism and the Bible (No.183)].

Mambo ya Walawi 19:5-8 Nanyi hapo mtakapomchinjia Bwana sadaka ya amani mtaisongeza ili kwamba mpate kukubaliwa. 6 Italiwa siku iyo hiyo mliyoichinja, na siku ya pili yake; na kama kitu cho chote katika sadaka hiyo kilisalia hata siku ya tatu kitachomwa moto. 7 Kwamba sadaka hiyo yaliwa hata kidogo siku ya tatu ni machukizo; haitakubaliwa; 8 lakini kila mtu atakayekula atauchukua uovu wake mwenyewe, kwa sababu amekinajisi kitu hicho kitakatifu cha Bwana; na nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.  

Uwekaji kikomo umewekwa kwenye taratibu zote kwa jumla za utoaji wa dhabihu kwa kadiri inayoendana na kuieleleza dhabihu ya Masihi.

 

Mambo yote yahusuyo uumbaji yanatakiwa yawe safi na matakatifu kwa Bwana Mungu, n ani wajibu wa wateule kuhakikisha kuwa inakuwa hivyo.

Mambo ya Walawi 19:19 Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja.  

 

Mambo ya Walawi 19:21-22 Na huyo mume ataleta sadaka yake ya hatia aitoe kwa Bwana, hata mlangoni pa hema ya kukutania; kondoo mume kwa hiyo sadaka ya hatia. 22 Kisha huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa huyo kondoo mume wa sadaka ya hatia mbele za Bwana, kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya; naye atasamehewa hiyo dhambi yake aliyoifanya

 

Mungu anadhibiti ulaji wa viumbe vyake na ameweka sheria au amri zinazolinda mazingira na mambo ya muda mrefu ya kila mmoja wetu.

Mambo ya Walawi 19:23-25 Nanyi hapo mtakapoingia nchi ile, mkiwa mmepanda miti ya namna zote kwa ajili ya chakula, ndipo mtayahesabu matunda yake kama ni kutotahiriwa; muda wa miaka mitatu miti hiyo itakuwa kwenu kama kutotahiriwa; matunda yake hayataliwa. 24 Lakini mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa ni matakatifu, kwa ajili ya kumpa Bwana shukrani. 25 Na katika mwaka wa tano mtakula katika matunda yake, ili ipate kuwapa maongeo yake; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Utakatifu miongoni mwa watu wa Mungu

Mungu alimwambia Abrahamu kwamba yeye ni Mungu Mwenyezi na akamuamuru aenende mbele zake na awe mkamilifu (Mwanzo 17:1). Alijulikana kuwa jina lake ni Yahova (Kutoka 6:3). Viumbe wote wanaitii mamlaka iliyo juu yao, nasi tumechaguliwa kuwa watu wake (soma Warumi 13:1-6).

 

Utaratibu wa kuishi na ibada inapaswa umlenge Mungu wa Pekee na wa Kweli, ulio kwenye kalenda yake na kwa mujibu wa sheria.

Mambo ya Walawi 19:26 Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.

 

Hatupaswi tu kushughulikia roho za kurithi za kiukoo au wapigaji ramli na kutiwa unajisi nao.

Mambo ya Walawi 19:31 Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu

 

Mambo ya Walawi 20:27 Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.

 

Kumbukumbu la Torati 18:9-14 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. 14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.  

 

Maelezo yako wazi kabisa kwamba wanajimu wanaotumia maono ya njota, waonaji au wenye maroho ya urithi ya kiukoo vyote vimekatazwa, na hukumu yake ni kwenda utumwani au ukimbizi. Hakuna ishara ya utaratibu wa ibada walizonazo mataifa mengine ya kigeni inayotakiwa ionekane kwetu.

Mambo ya Walawi 19:27 Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.

 

Mambo ya Walawi 19:28 Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.

 

Hatupaswi kuwatolea sadaka wake wanaoitwa miungu au kushiriki kwa kujiingiza kwenye aina yeyote ya matendo na imani za kidhalimu, zilizooneka zikiwatoa sadaka wanadamu au watoto na matendo ya ulaji wa nyama za wanadamu wanazozifanya wao (soma majarida ya Ndama wa Dhahabu (Na. 222), Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235) na Ujumbe wa Ufunuo 14 (Na. 270) [The Golden Calf (No. 222); The Origins of Christmas and Easter (No. 235) and The Messages of Revelation 14 (No. 270)].

Mambo ya Walawi 20:1-7 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe. 3 Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu. 4 Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yo yote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue; 5 ndipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na jamaa zake, nami nitamkatilia mbali, na hao wote wamwandamao katika uzinifu, ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao. 6 Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake. 7 Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Watu wetu na makuhani wetu wanapaswa kuwa watakatifu.

Mambo ya Walawi 21:1-24 inasema: Kisha Bwana akamwambia Musa, Nena na hao makuhani, wana wa Haruni, uwaambie, Mtu asijinajisi kwa ajili ya wafu katika watu wake; 2 isipokuwa ni kwa ajili ya jamaa yake wa karibu, kwa ajili ya mama yake, na kwa ajili baba yake, na kwa ajili ya mwanawe, na kwa ajili ya binti yake, na kwa ajili ya nduguye mwanamume; 3 na kwa ajili ya umbu lake aliye mwanamwali, aliye wa udugu kwake, ambaye hajaolewa na mume; ana ruhusa kujitia unajisi kwa ajili yake huyo. 4 Asijitie unajisi, ijapokuwa ni mkubwa katika watu wake, hata akajinajisi. 5 Wasijifanyie upaa kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje chale katika miili yao. 6 Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za Bwana kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu. 7 Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake. 8 Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi Bwana niwatakasaye ninyi ni mtakatifu. 9 Na binti ya kuhani ye yote atakapojitia unajisi kwa ukahaba, amemtia unajisi baba yake; atachomwa moto. 10 Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake; 11 wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake; 12 wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake u juu yake; mimi ndimi Bwana. 13 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake. 14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe. 15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye. 16 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 17 Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake. 18 Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili, 19 au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono, 20 au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu; 21 mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za Bwana kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake. 22 Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu. 23 Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye. 24 Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.

 

Mambo ya Walawi 21:10 inasema: Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;”. Ukweli wa kwamba Kuhani Mkuu kukodisha vazi lake ili ashughulike na Yesu Kristo ilikuwa ni kuonyesha kuwa huduma ya Ukuhani Mkuu ilikuwa imeraruliwa kutoka kwa Walaawi na kupewa Masihi na wateule, kwa uitaratibu wa Melkizedeki (soma Mathayo 26:65; Marko 14:63).

 

Masakani na mkate wa uwonyesho

Ashirio lote la uwepo wa Maskani lililenga mwelekeo wa uhusiano wa kiroho kazi za Kanisa kwa Mungu kwa Roho Mtakatifu katika siku za mwisho (soma jarida la Siku ya Bwana na Siku za MWisho (NA. 192) [The Day of the Lord and the Last Days (No. 192)]. Yuda hawakujua ashirio la ukweli huu na kwa hiyo walishindwa kuingia kwenye mchakato wa uongofu kwa kipindi cha takriban milenia mbili, isipokuwa ni kwa msingi wa kila mtu mmoja mmoja.

 

Mambo ya Walawi 24:1-9 inasema: Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Waagize wana wa Israeli kwamba wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima. 3 Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele za Bwana daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu. 4 Atazitengeza hizo taa katika kile kinara kilicho safi mbele za Bwana daima. 5 Nawe utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja. 6 Nawe iweke mistari miwili, mikate sita kwa kila mstari, juu ya hiyo meza safi, mbele za Bwana. 7 Nawe utatia ubani safi juu ya kila mstari, ili uwe ukumbusho kwa hiyo mikate, sadaka ya kusongezwa kwa Bwana kwa moto. 8 Kila siku ya Sabato ataipanga mbele za Bwana daima; ni kwa ajili ya wana wa Israeli, agano la milele. 9 Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zisongezwazo kwa Bwana kwa moto, kwa amri ya milele.

Taa za Hekaluni zinapaswa ziwake wakati wote. Ni kazi na jukumu la Kuhani kuhakikisha kuwa inakuwa hivyo. Mikate ya wonyesho inawekwa mezani kwa mistari miwili zikiwa na uvumba. Kila Sabato, mikate hii ya wonyesho iliwekwa kwa mpangilio mbeke za Bwana mezani kwa mistari miwili zikiwa pamoja na uvumba, na zinabakia kuwa ni ukumbusho kwa taifa lililoundwa kwa makabila chini ya viongozi katika kujiandaa kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Maadhimisho haya ilichukuliwa kwa mwelekeo wa ushahidi uliko kwa Roho Mtakatifu kwa wateule, walio miongoni mwa makabila ya Israeli, wakiwa kama Hekalu la Mungu.

 

Mungu aliamuru unyenyekevu na alikataza kuwatolea sadaka sanamu au vinyago (soma jarida la.Torati na Amri ya Pili (Na. 255) [Law and the Second Commandment (No. 255)]. Neno la Mungu aliye hai linaelezea hukumu itakayotolewa kwa ajili ya kosa hili la kuvunja agano lake. Kutozishika amri za Mungu na kuacha kumuabudu yeye kutapelekea kuadhibiwa kwa janga la magonja, njaa, tauni, vita na utumwa.

Mambo ya Walawi 26:1-46 inasema; Msifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 2 Zishikeni Sabato zangu, na kupastahi patakatifu pangu; mimi ndimi Bwana. 3 Kama mkienda katika amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyafanya; 4 ndipo nitazinyesha mvua zenu kwa nyakati zake, na nchi itazaa maongeo yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. 5 Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuketi katika nchi yenu salama. 6 Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala wala hapana atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu. 7 Nanyi mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele zenu kwa upanga. 8 Na watu watano wa kwenu watawafukuza watu mia, na watu mia wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi; na adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga. 9 Nami nitawaelekezea uso wangu, na kuwapa uzazi mwingi, na kuwaongeza; nami nitalithibitisha agano langu pamoja nanyi. 10 Nanyi mtakula akiba ya zamani mliyoiweka siku nyingi, tena hayo ya zamani mtayatoa, ili myaweke yaliyo mapya. 11 Nami nitaiweka maskani yangu kati yenu; wala roho yangu haitawachukia. 12 Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu. 13 Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawaendesha mwende sawasawa. 14 Lakini msiponisikiza, wala hamtaki kuyafanya maagizo hayo yote; 15 nanyi mkizikataa amri zangu, na roho yenu ikichukia hukumu zangu, hata ikawa hamtaki kuyafanya maagizo yangu yote, bali mwalivunja agano langu; 16 mimi nami nitawatenda jambo hili; nitaamrisha uje juu yenu utisho, hata kifua kikuu na homa, zitakazoharibu macho yenu, na kuidhoofisha roho; nanyi mtapanda mbegu yenu bure, kwa kuwa adui zenu wataila. 17 Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye. 18 Tena ikiwa baada ya hayo hamtaki kunisikiza, ndipo nitawaadhibu zaidi mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. 19 Nami nitakivunja kiburi cha uwezo wenu; nami nitazifanya mbingu zenu kuwa kama chuma, na nchi yenu kuwa kama shaba; 20 na nguvu zenu mtazitumia bure; kwa kuwa nchi yenu haitazaa mazao yake, wala miti ya nchi haitazaa matunda yake. 21 Nanyi ikiwa mwaenenda kinyume changu, wala hamtaki kunisikiza; nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, kama dhambi zenu zilivyo. 22 Nami nitaleta wanyama wakali kati yenu, ambao watawanyang'anya watoto wenu, na kuwaharibu wanyama wenu wa kufugwa, na kuwapunguza muwe wachache hesabu yenu; na njia zenu zitakuwa ni ukiwa. 23 Tena kama hamtaki kurejezwa upya kwangu mimi kwa mambo haya, bali mwaendelea kunishikia kinyume; ndipo mimi nami nitaendelea kuwashikia ninyi kinyume; 24 nami nitawapiga, naam mimi, mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. 25 Nami nitaleta upanga juu yenu, utakaopatiliza kisasi cha hilo agano; nanyi mtakutanishwa ndani ya miji yenu; nami nitaleta tauni kati yenu; nanyi mtatiwa mkononi mwa adui. 26 Hapo nitakapovunja tegemeo lenu la mkate, wanawake kumi wataoka mikate yenu katika tanuu moja, nao watawapa mikate yenu tena kwa kupima kwa mizani; nanyi mtakula, lakini hamtashiba. 27 Tena ikiwa baada ya hayo yote hamtaki kunisikiza, bali mwaenenda kwa kunishikia kinyume; 28 ndipo nami nitakwenda kwa kuwashikia ninyi kinyume katika ghadhabu yangu; nami nitawaadhibu mara saba kwa dhambi zenu. 29 Nanyi mtakula nyama ya miili ya wana wenu, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila. 30 Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia. 31 Nami nitaifanya miji yenu iwe maganjo, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo. 32 Nami nitaitia hiyo nchi ukiwa; na adui zenu watakaokaa huko wataistaajabia. 33 Nanyi nitawatapanya-tapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ni ukiwa, na miji yenu maganjo. 34 Hapo ndipo nchi itakapozifurahia Sabato zake, wakati itakapokuwa hali ya ukiwa, nanyi mtakapokuwa katika nchi ya adui zenu; ndipo nchi itakapopumzika, na kuzifurahia Sabato zake. 35 Wakati wote itakapokuwa na ukiwa, itapumzika; ni hayo mapumziko ambayo haikuwa nayo katika Sabato zenu, hapo mlipokaa katika nchi hiyo. 36 Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatilia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye. 37 Nao wataangukiana wenyewe kwa wenyewe, kama mbele ya upanga, hapo ambapo hapana afukuzaye; wala hamtakuwa na nguvu za kusimama mbele ya adui zenu. 38 Nanyi mtaangamia kati ya mataifa, na nchi ya adui zenu itawameza. 39 Na watu wa kwenu watakaobaki watafifia kwa ajili ya uovu wao, katika hizo nchi za adui zenu; tena watafifia kwa ajili ya uovu wa baba zao, pamoja nao. 40 Nao wataukiri uovu wao, na uovu wa baba zao, katika maasi yao waliyoasi juu yangu, tena ya kuwa kwa sababu wameendelea kunishikia kinyume, 41 mimi nami nimeendelea kuwashikia kinyume wao, na kuwatia katika nchi ya adui zao; lakini hapo, kama mioyo yao isiyokuwa tohara ikinyenyekea, nao wakubali adhabu ya uovu wao; 42 ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Ibrahimu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo. 43 Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu, naam, ni kwa sababu wamezikataa hukumu zangu, na roho zao zimezichukia amri zangu. 44 Lakini pamoja na hayo yote, watakapokuwa katika nchi ya adui zao, mimi, sitawatupa, wala sitawachukia, niwaangamize kabisa, na kulivunja agano langu pamoja nao; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao; 45 lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano la baba zao, niliowaleta watoke katika nchi ya Misri mbele ya macho ya mataifa, ili kwamba niwe Mungu wao; mimi ndimi Bwana. 46 Hizi ni amri na hukumu na sheria, Bwana alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.

Mungu aliwaahidi Israeli ulinzi, na kuwanyeshea mvua kwa majira yake kwa kipindi chote watakachokuwa wanazitii amri zake.

 

Gharama ya ukombozi inaamuliwa kwa muibu wa umri na uwezo. Mungu huwawezesha wote kuingia kwenye Ufalme wake kwa kulinganisha na uwezo wa kazi na huduma au utumishi wake. Yeye aliyepewa vingi atadaiwa vingi.

 

Mambo ya Walawi 27:1-34 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Andiko hisli linahusu uwekaji wa nadhiri na kuwekwa wakfu wa mtu, mnyama au ardhi kwenye utumishi au kazi za Mungu na ukombozi wa kila aina yoyote ya sadaka ya namna hii, thamani inayopaswa kulinganishwa kwayo na kuhani. Sheria za Yubile na uhusiano wake kwa ardhi iliyowekwa wakfu zimeelezwa na kufafanuliwa pia. Wazaliwa wa kwanza wa wanyama au mifugo ni wa Mungu tayari na kwa hiyo hawawezi kutakaswa. Sehemu ya tano inatakiwa iongezwe kwenye thamani ya ukombozi.

 

Mlawi hekaluni

Ukuhani ni wajibu muhimu kwaajili ya kuliangalia na kulipamba Hekalu. Wajibu huu unafanywa na makuhani wa wateule wake, ambao, kwa kazi zao ni za muhimu na wajibu kwa utunzaji wa Hekalu la mawe yaliyo hai.

Hesabu 1:47-54 inasema: Lakini Walawi kwa kuiandama kabila ya baba zao hawakuhesabiwa katika watu hao. 48 Kwa kuwa Bwana alinena na Musa, na kumwambia, 49 Hiyo kabila ya Lawi tu usiihesabu, wala usiitie hesabu yao katika wana wa Israeli; 50 lakini uwaweke Walawi wawe juu ya maskani ya ushahidi, na juu ya vyombo vyake vyote, na juu ya vitu vyake vyote; wao wataichukua hiyo maskani, na vyombo vyake vyote; nao wataitumikia, na kupanga hema zao kwa kuizunguka maskani pande zote. 51 Tena hapo maskani itakapokwenda mbele, Walawi wataishusha; tena hapo maskani itakaposimamishwa, Walawi wataisimamisha; na mgeni atakayekaribia atauawa. 52 Na wana wa Israeli watazipanga hema zao, kila mtu katika marago yake mwenyewe, kila mtu hapo ilipo beramu yake mwenyewe, kama majeshi yao yalivyo. 53 Lakini Walawi watapanga hema zao kuizunguka maskani ya ushahidi pande zote, ili zisiwe hasira juu ya mkutano wa wana wa Israeli; kisha Walawi wataulinda ulinzi wa hiyo maskani ya ushahidi. 54 Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote Bwana aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.   

 

Mteule ametengwa mbali na taifa kwa kuzaliwa na sasa wokovu ni kwa Wamataifa, ambao wameingizwa na kufanyika kuwa Israeli kama sehemu ta taifa lakini wakiwa pia ni Hekalula Mungu.

Hesabu 2:33 Lakini Walawi hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli; kama Bwana alivyomwagiza Musa.

 

Mgawanyo wa kazi za makuhani ulifanywa katika maskani au patakatifu pake Mungu kwa kufuatana na kielelezo cha Maskani yenyewe. Kila utendaji wake umehusiana na umuhimu wa uwekaji na utaratibu wa Hekalu.

 

Hesabu 3:1-51 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Hesabu 3 inaelezea vizazi vya Haruni na Musa. Idadi ya Walawi, familia na wajibu na kazi walizopewa. Walawi wote walikuwa wake, Bwana (Kumbukumbu la Torati 10:8-9). Mzaliwa wa kwanza wa Israeli alihesabiwa na makusanyo ya ukombozi wake yalichukuliwa. Ukombozi wa mzaliwa wa kwanza uliwalenga wateule ambao walikombolewa na kutolewa kwa makuhani chini ya Masihi. Lawi alifanywa kuwa ni kiini cha utumishi huu wa kikuhani kati ya makabila yote na kwa hiyo waliteuliwa kama walivyofanywa wateule ambao wameitwa, kuchaguliwa na kutakaswa kutoka kwenye uzao wao.

 

Utaratibu huu ulianzishwa ili kumuwezesha mtu aweze kutengwa na kuwekwa wakfu kama Mnazarayo, nah ii inamhusu pia mteule. Utaratibu huu kwa jinsi na kadiri ulivyo, haukuweza na haukufanikiwa kuwapatia wokovu. Ubatizo wa Yohana haukukubalika kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu ingawaje alikuwa ni Mnadhiri tangu kuzaliwa kwake, akiwa kama mwana wa Kuhani Mkuu. Sheria kuhusu Mnazarayo au Mnadhiri zimefafanuliwa vema kwenye maandiko haya.

 

Hesabu 6:1-27 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Wana wa Kohathi, Geshoni na Merari wanahesabiwa tangu wakiwa na umri wa miaka thelathini hadi hamsini, na kupewa majukumu ya kazi zao Hekaluni.

 

Hesabu 4:1-49 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Kuhani Melkizedeki hana historia ya uzaliwa wake na hana siku ya kuanza kwake wala mwaka wake wa mwisho; kwa hiyo, makuhani wateule chini ya Masihi hana nasaba ya uzawa wa mama wala baba, na hana mwanzo wala mwisho priesthood is without genealogy and without (Waebrania 7:1-10). Ukuhani huu unaendelea kudumu baada ya kufa na kufufuka, ndipo ukuhani huu wa Walawi wa kimwili utakapokoma baada ya kipindi fulani na unaelekea hadi kwenye ufufuo wa pili, usipoachiliwa kwa namna yake mahsusi na Roho Mtakatifu kwa manabii na kwa wale walio na sehemu kwenye ufufuo wa kwanza.

 

Hesabu 7:1-89 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Sura hii ya kwenye kitabu hiki cha Hesabu inaelezea sadaka zinazotolewa na makabila ya Israeli kwenye uwekaji wakfu Maskani ya kumuabudia Mungu wa Pekee na wa Kweli. Idadi ya dhabihu zinazotolewa inatoka kwenye makabila kwa kutegemea mlingano wa idadi ya Malaika walioko mbinguni, na maana ya vitu vinavyolingana na Malaika hawa wa mbinguni, na maana ya vitu ambavyo vinahusiana pia Malaika hawa. Kila dhabihu inaashiria na utaratibu, wa jinsi unavyofanyika kwa dhabihu ya kila mwaka, kila mwezi, na kila juma zinazowashiria wateule ambao idadi yao ni 144,000, pamoja na Kundi Kubwa linalowakilishwa na dhabihu au sadaka ya jioni.

 

Taa hizi ina maana yake pia kwa jinsi zinavyoonyeshwa hapa.

 

Hesabu 8:1-26 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Tendo la kuoshwa ili kusafishwa na kutakaswa kwa Walawi kumeelezewa kwenye maandiko haya. Huduma ya kumtumikia Mungu Hekaluni ilikuwa ni kazi ngumu sana na iliwefanywa na mtu mwenye umri wa miaka kati ya ishirini na mitano hadi hamsini, na hatimaye atahudumu kwa mafundisho peke yake tangu akiwa na umri wa miaka hamsini na kuendelea. Huduma ya kufundisha Hekaluni ilianzia tangu mtu anapokuwa mwenye umri wa miaka thelathini, wakati kwamba kipindi kuanzia cha miaka ishirini na tano hadi thelathini cha kuwa kwenye huduma na cha kujifunza kuwa mtumishi.

 

Mungu anawahakikishia kuwapa mahitaji watu

Kumnung’unikia Bwana, Mungu ni kitendo kibaya n ani uovu mkuu.

Hesabu 11:1-35 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Watu walinung’unika na kulalamika kwa kukosa nyma kwenye kitabu cha Kutoka, kwa kuwa wakuwa wamepewa mana peke yake. Hii inatupeleka mbele kwenye kipindi cha Yubile arobaini za jangwani ambazo kwamba mkate na maji vilikuwa ni mahitaji ya kawaida waliyohakikishiwa wateule. Musa akamuomba Mungu na kumwambia kuwa kazi ya kuwaongoza Israeli ilikuwa ni kubwa na ngumu kwake na ndipo akaambiwa awachague wazee sabini ili wamsaidie. Wazee hawa sabini wa Israeli hatimaye ndio walikuwa ni wanachama wa baraza la kidini lililojulikana kuwa ni Sanhedrin. Kuanzishwa kwa baraza la hawa sabini kwa roho iliyokuweko kwa Musa iliendelea kwa tendo alilolifanya Masihi kuwachagua wanafunzi sabini ambao hatimaye walifanyika kuwa ni wazee wa Israeli ambao walitumwa wawili wawili, na kwa wale kumi na wawili wakawekwa kwenye makundi yaliyo kwenye kitabu cha Hesabu sura 7 hapo juu (soma Luka 10:1, 17).

 

Wana wa Israeli walipewa kware waliponung’unika kwamba hawana nyama, lakini nyama ilikuwa ni nyingi sana kwao, walikuwa wachoyo, na wengi wao walikufa. Wazo hapa linatupeleka pia kwenye uweza wa Roho Mtakatifu na uwezo wa kuzijua siri za Mungu (soma jarida la Siri za Mungu (Na. 131) [The Mysteries of God (No. 131)].

 

Mungu pia aliwapa Israeli fursa ya kuingia kwenye Nchi ya Ahadi mwnzoni, lakini waliipuuzia fursa ile. Walipaswa kufanya hiivi pia katika kindi cha Masihi wakati walipopewa fursa hii. Yuda na Lawi walipuuzia hata baada ya kufufuka kwake..

 

Hesabu 13:1-33 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Wanaume kumi na wawili walipelekwa wakaione Nchi ya Ahadi na wakaleta habari. Habari waliyoleta kumi miongoni mwao ilionyesha upungufu wa imani kabisa mwa Mungu.

 

Hesabu 14:1-45 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Kutokuwa na imani kwenye mioyo ya Israeli kuliwaponza sana. Kusanyiko lote liliogopa na wakawalalamikia Musa na Haruni. Yoshua na Kalebu, ndio waliokuwa peke yao wanaimani mioyoni mwao, walishindwa kuwatuliza na kuwanyamazisha watu kwamba wanaweza au wangeweza kuirithi nchi ile kama wangeamini. Mungu akawakasirikia na ilikuwa ni kwa maombi tu ya Musa ndipo waliokoka wasiangamizwe na mahali walipokuwa. Ndipo watu waliadhibiwa kwa kufanga tanga jangwani kwa kipindi cha miaka arobaini, kwa ajili ya kuto kuamini kwao, n ani Kalebu na Yoshua tu ndio walioruhusiwa kwenda na kuiingia Nchi hii ya Ahadi.

 

Musa alijaribiwa lakini hakuanguka na kupotoka. Mungu ameweka utaratibu wake na ukuhani wake na watu wake, na alikuwa anawashughulikia ili tuweze kuelewa kwamba katika siku za mwisho kile kitakachokuja kutokea. Yuda walipewa miaka arobaini ya kufanya toba baada ya kifo cha Masihi lakini hawakutubu na kwa hiyo walipatilizwa na kupelekwa utumwani (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)].

 

Mfumo mzima wa ibada na utoaji sadaka unapaswa uwe wa namna moja, kwa wote, yaani Wamataifa na kwa wazawa asilia wa Israeli.

 

Hesabu 15:1-41 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Andiko hili linaelezea thamani au kiwango cha sadaka na dhabihu zinazoweza kutolewa wanapoingia kwenye Nchi ya Ahadi. Ahdabu kwa ajili ya kuivunja Sabato ni kifo.

 

Hesabu 16:1-50 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Uasi wa Kora unaoshughulikiwa hapa. Wote waliohusika na uasi huu walikufa, na tauni ilikoma pale tu Haruni aliposimama na kupita kati kati ya waliokufa na walio hai. Tendo hili linaonyesha maombezi ya kuhani kwa taifa, na yanalihusu Kanisa na jukumu lake na kazi zake. Uasi wa wana wa Israeli kwa kweli ulitanguliwa na kuhani na watawala wa Israeli. Ukengeufu huu ulipaswa kutokea tena katikati ya makabila kwa kiwango cha kurudia rudia, kote kuwila, yaani kwa Israeli na miongoni mwa Kanisa baada ya kutawanyika, hasa kwenye nchi iliyoko sasa.

 

Hesabu 17:1-13 inasema: Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, 2 Nena na wana wa Israeli, kisha upokee kwao fimbo, fimbo moja kwa ajili ya nyumba ya kila baba, katika wakuu wao wote, kama nyumba za baba zao zilivyo, fimbo kumi na mbili; kisha andika jina la kila mtu katika fimbo yake. 3 Na katika fimbo ya Lawi utaliandika jina la Haruni; maana, itakuwa fimbo moja kwa kila kichwa cha nyumba za baba zao. 4 Nawe utaziweka katika hema ya kukutania mbele ya huo ushahidi, hapo nikutanapo pamoja nanyi. 5 Kisha itakuwa, mtu huyo nitakayemchagua, fimbo yake itachipuka; nami nitayakomesha kwangu manung'uniko ya wana wa Israeli, wanung'unikiayo juu yenu. 6 Basi Musa akawaambia wana wa Israeli, ndipo wakuu wao wote wakampa fimbo, fimbo moja kwa kila mkuu, kama nyumba za baba zao zilivyokuwa, fimbo kumi na mbili; na fimbo ya Haruni ilikuwa kati ya fimbo zao. 7 Kisha Musa akaziweka hizo fimbo mbele za Bwana katika hema ya kukutania.

Fito kumi mbili zilizowekwa chini ya fimbo ya Haruni zilikuwa na uhusiano na migawanyo kumi na mbili ya makabila ya yaliyokuwa chini ya waamuzi, na hatimaye mitume. Msingi wa Mji wa Mungu unajengwa kwenye mitume hawa kumi na wawili na kazi zao (soma Ufunuo 21:10-14).

 8 Ilikuwa siku ya pili yake, Musa akaingia ndani ya hema ya ushahidi; na tazama, ile fimbo ya Haruni iliyokuwa kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka, imetoa michipukizi, na kuchanua maua; na kuzaa malozi mabivu. 9 Kisha Musa akazileta nje hizo fimbo zote kutoka hapo mbele za Bwana na kuziweka mbele ya wana wa Israeli wote; nao wakaangalia, na kila mtu akaitwaa fimbo yake. 10 Kisha Bwana akamwambia Musa, Irudishe fimbo ya Haruni mbele ya ushahidi, ili itunzwe iwe ishara juu ya hawa wana wa maasi; ili uyakomeshe manung'uniko yao waliyoninung'unikia, ili wasife. 11 Basi Musa akafanya vivyo; kama Bwana alivyomwagiza, ndivyo alivyofanya. 12 Kisha wana wa Israeli wakanena na Musa, na kumwambia, Angalia, sisi twafa, twaangamia, sote twaangamia. 13 Kila mtu akaribiaye, aikaribiaye maskani ya Bwana, hufa; je! Tutakufa pia sote?.  

Uovu wa patakatifu unachukuliwa na viongozi na hili ndilo hekalu halisi lililo hai.

 

Hesabu 18:1-32 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Wateule wametumwa na kwenda duniani wakiwa kama kondoo kati kati ya mbwa mwitu na mchakato wao urithi wa huduma za Walawi unaofanywa ni kama kipimo kwa wateule. Wateule ni uzao mteule, n ani Makuhani wa Kifalme n ani taifa takatifu (1Petro 2:9). Musa alizuiliwa kuiingia nchi ya ahadi kwa kuwa alikuwa ameupiga mwamba. Yeye na Haruni walikufa nje ya mipaka ya Israeli jambo linalotukumbusha kwamba tutakuwepo kwenye Ufufuo wa Kwanza na tutakuwa pamoja na Israeli na Musa tukiwa kama wanadamu wa ulimwengu kiroho (soma Kumbukumbu la Torati 10:6-7 hapo juu).

 

Maandiko Matakatifu yanatuambia kwamba Musa alikufa kwenye nchi ya Moabu (soma Kumbukumbu la Torati 34:5-6). Iwapo kama tungefia nchini Israeli tungefanya vinyago na kutunza masalio yake. Kwa ajili hii malaika mkuu Mikaeli alishindana na Shetani kwa ajili ya mwili wa Musa (Yuda 9).

 

Hesabu 20:1-13 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Tunaona kutoka kwenye maandiko yaha kwamba watu wa Bwana waliingia kwenye hukumu.

 

Hesabu 20:14-29 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Watu wa Kanaani walipatilizwa kwa hukumiwa waliyostahili iliyokywa sawa na matendo yao na kisha wakafukuzwa.

 

Hesabu 21:1-35 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Israeli waliwashinda Wakanaani bali hatimaye walikata tama na walimnung’unikia Mungu kwa mara nyingine tena. Ndipo Mungu akawatuma nyoka wakali sana ili kuwahukumu. Musa akamwomba Mungu na akafanya kile kinachojulikana kama nyoka wa shaba ili wapone. Kwa kweli kitu hiki kilikuwa ni Serafi. Serafi alikuwa ni kiumbe cha asili chenye mabawa sita, na alikuwa anafanya mambo yasiyo ya kawaida ambayo yamepotea kwenye fasiri.

 

Mungu aliwalinda Israeli na kuwaleta kwenye urithi wao. Kuondolewa kwa kufukuzwa makabila yaliyowatisha Israeli kulifanywa kwa mpangilio makinifu. Urithi wa mipaka ya Israeli ulipanuliwa hadi kuvuka kingo za Yordan kwenye mchakato huu, na sio Waisraeii walikuwa kwenye nchi ya Israeli, magharibi ya Yordani. Hii ilikuwa inaashiria pia matukio ya siku za mwisho na matendo ya wateule. Hata hivyo, Israeli waliopotoshwa kwa kuabudu na kutumikia vinyago na kuabudu miungu mingine kwa kadiri wavyofundishwa na kuongozwa na makuhani wa uwongo waliokuwa wakitumika kwa maslahi yao tu.

 

Unabii wa Balaamu

Kwenye kitabu cha Hesabu 22 tunaona kuwa Israeeli waliweka matuo kwenye uwanda wa Moabu mahala palipokuwa kati ya Yordan na Yesriko. Wamoabu wakawaogopa watu hawa, na idadi yao ilikuwa sio kubwa, bali walikuwa wachache. Ndipo Wamoabu wakamwendea Balaamu, mwana wa Peori, wakamwajiri ili awalaani Israel.

 

Hesabu 22:1-41 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Sadaka ya kumwajiria Balaamu ililenga kwa kusudi la kuwashusha hadhi na kuwalaani Israeli, ambao walikuwa wanalindwa kwa mkono wenye nguvu kupitia roho saba za Mungu ambazo zilionekana tena kwenye wale Malaika wa Makanisa Saba.

 

Numbers 23:1-30 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Unabii huu unamaanisha umuhimu wa subira na uvumilivu, kwa kuwa unahusiana na maelekezo au mwongozo wa Mungu kwa manabii wake katika kuwalinda na kuwabarikia Israeli. Unahusiana pia na itikadi ya kidini na mafundisho ya jinsi ya kuzihusisha au kuzitumia vibaya sheria za kibiblia kwa kuzitumia kwa maslahi binafsi, jambo linaloweza kumsababishia mtu kuandamwa na laana ya magonjwa ya kinasaba kwenye ukoo wa kikuhani katika Israeli, magonjwa ambayo yalipaswa kuwapata watu wa mataifa.

Hesabu 24:1-25 inasema: Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza Bwana kuwabariki Israeli, hakwenda, kama hapo kwanza, ili kutafuta uchawi, bali alielekeza uso wake jangwani. 2 Balaamu akainua macho yake akawaona Israeli wamekaa kabila kabila; roho ya Mungu ikamjia. 3 Akatunga mithali yake, akasema, Balaamu mwana wa Beori asema, Yule mtu aliyefumbwa macho asema; 4 Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho; 5 Mahema yako ni mazuri namna gani, Ee Yakobo, Maskani zako, Ee Israeli! 6 Mfano wa bonde zimetandwa, Mfano wa bustani kando ya mto, Mfano wa mishubiri aliyoipanda Bwana, Mfano wa mierezi kando ya maji. 7 Maji yatafurika katika ndoo zake, Na mbegu zake zitakuwa katika maji mengi. Na mfalme wake ataadhimishwa kuliko Agagi, Na ufalme wake utatukuzwa. 8 Mungu amemleta kutoka Misri, Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati; Atawameza mataifa walio adui zake, Ataivunja mifupa yao vipande vipande. Atawachoma kwa mishale yake. 9 Aliinama, akalala mfano wa simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha? Na abarikiwe kila akubarikiye, Na alaaniwe kila akulaaniye. 10 Hasira ya Balaki ikawaka juu ya Balaamu akayapiga makofi; Balaki akamwambia Balaamu, Nalikuita ili unilaanie adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa mara tatu hizi. 11 Basi sasa kimbilia mahali pako; naliazimu kukuheshimu sana; lakini, tazama, Bwana amekuzuilia heshima. 12 Balaamu akamwambia Balaki, Je! Sikuwaambia wajumbe wako ulionipelekea, nikisema, 13 Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la Bwana, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; Bwana atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi. 14 Basi sasa, tazama, ninakwenda kwa watu wangu; haya, nitakuarifu mambo ambayo watu hawa watakayowatenda watu wako siku za mwisho. 15 Akatunga mithali yake akasema, Balaamu mwana wa Beori asema, Yule mtu aliyefumbwa macho asema, 16 Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu. Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho, 17 Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia. 18 Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa. 19 Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini. 20 Kisha akamwangalia Amaleki, akatunga mithali yake, akasema, Amaleki alikuwa ni wa kwanza wa mataifa; Lakini mwisho wake atafikilia uharibifu. 21 Kisha akamwangalia Mkeni, akatunga mithali yake, akasema, Makao yako yana nguvu, Na kitundu chako kimewekwa katika jabali. 22 Pamoja na haya Wakeni wataangamizwa, Hata Ashuru atakapokuchukua mateka. 23 Akatunga mithali yake akasema, Ole wao! Ni nani atakayepona, Mungu atakapofanya haya? 24 Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu, Nazo zitamtaabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha, Yeye naye atafikilia uharibifu. 25 Basi Balaamu akainuka, akaondoka na kurudi mahali pake; Balaki naye akaenda zake.

 

Unabii huu ulihusiana na tumwa wa Israeli waliokwenda Ushuru na pia na maafa au maangamivu ya Eberi. Maangamivu ya siku za mwisho na vita vya mwisho vimeelezewa pia milolongo rahisi na matokeo yake yako wazi (soma jarida la Mafundisho ya Balaam una Unabii wa Balaamu (Na. 204) 9The Doctrine of Balaam and Balaam’s Prophecy (No. 204)].

Hesabu 25:1-18 inasema: Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli. 4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli. 5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. 6 Na tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania. 7 Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake; 8 akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. 9 Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao. 10 Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, 11 Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu. 12 Basi kwa hiyo, sema, Tazama, nampa yeye agano langu la amani; 13 tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli. 14 Basi jina la Mwisraeli huyo aliyeuawa pamoja na yule mwanamke Mmidiani, aliitwa Zimri, mwana wa Salu, mkuu wa nyumba ya baba zake, katika kabila la Simeoni. 15 Na jina la huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa, aliitwa Kozbi, binti Suri; naye alikuwa kichwa cha watu wa nyumba ya baba zake huko Midiani 16 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 17 Wasumbue Wamidiani, na kuwapiga; 18 kwa sababu wao wawasumbua ninyi kwa hila zao, ambazo kwa hizo wamewadanganya ninyi katika jambo la Peori, na katika jambo la huyo Kozbi, binti wa mkuu wa Midiani, umbu lao, huyo aliyeuawa siku hiyo ya pigo katika jambo la Peori.

 

Wamidiani walikuwa kwenye hatari ya kuangamia pia kwa ajili ya udanganyifu huu wa ibada za ssnamu.

 

Katika sadaka za kila siku, taa zilikuwa zinaletwa na sadaka ziliwekwa mbili mbili na watu wa Mungu wote. Kwa hiyo, lile Kundi Kubwa linaloonekana kwenye Ufunuo 7:9, linahusiana na sadaka ya kila siku.

Hesabu 28:1-31 inasema: Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Waagize hao wana wa Israeli, uwaambie, Matoleo yangu, chakula changu cha sadaka zangu zisongezwazo kwa moto, za harufu ya kupendeza kwangu mimi, mtaangalia kuzisongeza kwangu wakati wake upasao. 3 Nawe utawaambia, Hii ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto mtakayomsongezea Bwana; wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu, wawili kila siku, wawe sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote. 4 Mwana-kondoo mmoja utamsongeza asubuhi, na mwana-kondoo wa pili utamsongeza jioni; 5 pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta ya kupondwa. 6 Ni sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, iliyoamriwa huko katika mlima wa Sinai iwe harufu ya kupendeza, sadaka ya kusongezwa kwa Bwana kwa moto. 7 Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa robo ya hini kwa mwana-kondoo mmoja; hiyo sadaka ya kinywaji, ya kileo, utammiminia Bwana katika mahali hapo patakatifu. 8 Na mwana-kondoo wa pili utamsongeza wakati wa jioni; kama ile sadaka ya unga iliyosongezwa asubuhi, na kama sadaka yake ya kinywaji, ndivyo utakavyoisongeza, ni sadaka ya kusongezwa kwa moto, ni harufu ya kupendeza kwa Bwana. 9 Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo wawili, waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, pamoja na sehemu ya kumi mbili za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji; 10 hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila Sabato, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. 11 Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng'ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba; 12 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng'ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja; 13 na sehemu ya kumi moja ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwana-kondoo; kuwa sadaka ya kuteketezwa ya harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. 14 Tena sadaka zake za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng'ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo mume, na robo ya hini kwa mwana-kondoo; hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka. 15 Tena mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa Bwana itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. 16 Tena, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, ni pasaka ya Bwana. 17 Siku ya kumi na tano ya mwezi huo patakuwa na sikukuu; mkate usiotiwa chachu utaliwa muda wa siku saba. 18 Siku ya kwanza patakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; 19 lakini mtaisongeza sadaka kwa njia ya moto, sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana; ng'ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu; 20 pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta; mtasongeza sehemu ya kumi tatu kwa ng'ombe mmoja, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume; 21 na sehemu ya kumi moja utasongeza kwa kila mwana-kondoo, wale wana-kondoo saba; 22 tena mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 23 Mtasongeza wanyama hao zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, iliyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote. 24 Mtasongeza sadaka kwa mfano huu kila siku muda wa siku saba, chakula cha sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana; itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. 25 Na siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi. 26 Tena katika siku ya malimbuko, hapo mtakapomsongezea Bwana sadaka ya unga mpya katika sikukuu yenu ya majuma mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; 27 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng'ombe waume wadogo wawili, kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; 28 pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng'ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume, 29 na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo, wa wale wana-kondoo saba; 30 na mbuzi mume mmoja, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 31 Zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, mtasongeza wanyama hao (watakuwa wakamilifu kwenu), pamoja na sadaka zake za vinywaji.  

Kwa hiyo, mfuanato huu wa matukio unaendelea hadi kwenye siku za hizo na kwa hiyo, tangia wale 144,000 hadi kwenye Makutaniko Mkuu kwa kipindi cha zaidi ya Yubile arobaini.

 

Sheria ya kutwaa na kumiliki nchi

Mungu alimpa Sheria maalumu Musa kwa kupitia Yesu Kristo, na alianza kuiandika alipokuwa kwenye nchi ya Wamoabu, ng’ambo ya Yordan. Kwa hiyo, maelekezo na kanuni ya utamalaki wa kimakazi uliandaliwa hapo kabla hata Israeli hawajaingia kwenye nchi hoyo, jambo ambalo lilifanyika kwenye siku zilizofuatia baadae.

 

Kumbukumbu la Torati 1:1-46 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Mwishoni mwa kipindi cha miaka arobaini, Musa aliyatabiri mambo ambayo yalikuja tokea kipindi cha baada ya miaka ya wao kuwa jangwani. Aliwakumbusha watu kuhusu manung’uniko na akawaambia kwamba Yoshua na Kalebu ndio watakaoingia kwenye Nchi ya Ahadi, bali baba zao hawataingia kwa ajili ya kutokuamini kwao na kumtii Mungu aliye Hai.

 

Kwa hiyo ilibidi cheo cha Musa kirithiwe na Yoshua ambaye hatimaye aliwachukua Israeli na kuwaingiza kwenye Nchi ya Ahadi. Jambo hili linaashiria tena tendo la kwamba Musa alirithiwa na Masihi ambaye aliitwa Yehoshua au Yoshua, ambalo ndilo lilikuwa jina alilopewa katika Yuda. Yesu Kristo linatokana na lugha ya Kiyunani na lenye mchanganyiko na Kiaramu, ambalo linamaana halisia ya Yoshua Masihi. Kwenye tafsiri la biblia ya The Septuagint, jina hili limeandikwa Yoshua na Ičsous.

 

Kumbukumbu la Torati 2:1-37 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Kwenye maandiko haya Musa anaendelea kuwakumbusha Israeli historia iliyowapelekea wao kutangatanga jangwani, vita walivyopigana na ushimdi wao. Kwa hiyo, mataifa yote yalikusudiwa yaokolewe kutoka mikononi mwa Israeli, yawekwe chini yao kwa taratibu zao na kwa kulingana na maelekezo ya Mungu. Hii ilkuwa ni ahadi iliyowekwa kwa lengo la kuanzisha maongozi ya amri na Torati ya Mungu kufanya tahadhari ya kitaifa na kuweka mwelekeo unaoashiria kwenye utaratibu wa milenia chini ya Masihi.

 

Kumbukumbu la Torati 3:1-29 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Andiko hili linaielezea vita dhidi ya Ogu, Mfalme wa Bashani. Ushindi unaonekana mgawanyo wan nchi zilizo nje ya Nchi ya Ahadi zilizo kwenye maeneo ya makabila yaliyoko huko, na Yoshua au Yoshua ambaye hatimaye alipewa jukumu la kuwaongoza.

 

Mungu alikuwa pamoja nao Israeli kwa kipindi chote walichodumu kuwa watiifu kwa uongozi wake uliowekwa. Mfuatano huu wa matukio unaashiria siku za mwisho na kuanzishwa kwa taifa la Israeli kwenye urithi wake, pamoja na kuwekwa kwa taifa la Israeli chini ya operasheni ya kijeshi yaw a majeshi ya Bwana. Makabila yakiwa kwenye urithi wao hawakuachiliwa au kusamehewa wasibebe majukumu yao ya kiutumishi hadi kipindi chote cha kuwatiisha mataifa kimekamilika na makabila yote yawe kwenye himaya yao.

 

Israeli walikuwa na uhuru wa kuzishika amri au kuziongeza au kuzifuta. Yuda ameongezwa kwenye amri hizi za Mungu aliye Hai kwa kufuata mapokeo ya kale, yaliyothibishwa na Masihi kwa ajili ya ukweli huo na hatimaye wakaenda utumwani.

 

Kumbukumbu la Torati 4:1-39 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Kwenye andiko hili Israeli wanaonywa kwa kuamriwa kulitunza agano na amri na maagizo ya ya Mungu. Musa anawaambia hapa kwamba kama hawatafanya hivyo, basi watqatawanywa kwa kufukuzwa na kupelekwa kwenye mataifa ya mbali. Na hata Musa mwenye hakuvuka Yordan na kuiingia nchi hiyo.

 

Kumbukumbu la Torati 4:40-49 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Kwenye Maandiko haya Matakatifu Musa anaanzisha mfumo wa kimahama akiwa nje ya Nchi ya Ahadi, mashariki mwa Yordan, na hii inahusiana pia na siku za mwisho. Munbu ameongeza ahadi zake kwa Israeli, ambazo zilikuwa zinahusiana na urithi wao iliotegemeana na kazi au matendo yao (soma Mwanzo 49:1-33).

 

Uanzishwaji wa mfumo huu wa kisheria wa kimakazi ilikamilika siku za kabla Israeli hawjavuka Yordan, na ndivyo itakavyokuwa katika siku za mwisho. Mfumo mzima ulitokana na Amri Kumi, ambazo zilirudiwa mara kwa mara kwenye Kumbukumbu la Torati.

Kumbukumbu la Torati 5:1-33 inasema: Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuangalia kuzitenda. 2 Bwana, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu. 3 Bwana hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai. 4 Bwana alisema nanyi uso kwa uso mlimani, toka kati ya moto; 5 (nami wakati ule nalisimama kati ya Bwana na ninyi, ili kuwaonyesha neno la Bwana; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani); naye akasema, 6 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 7 Usiwe na miungu mingine ila mimi. 8 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. 9 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 10 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. 11 Usilitaje bure Jina la Bwana, Mungu wako; maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina lake bure. 12 Ishike siku ya Sabato uitakase, kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru. 13 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 14 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe. 15 Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa Bwana, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato. 16 Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. 17 Usiue. 18 Wala usizini. 19 Wala usiibe. 20 Wala usimshuhudie jirani yako uongo. 21 Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani yako. 22 Haya ndiyo maneno ambayo Bwana aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa. 23 Ikawa, mlipoisikia sauti ile toka kati ya giza, na wakati uo huo mlima ule ulikuwa ukiwaka moto, basi, mlinikaribia, naam, wakuu wote wa kabila zenu, na wazee wenu, 24 mkasema, Tazama, Bwana, Mungu wetu, ametuonyesha utukufu wake, na ukuu wake, nasi tunasikia sauti yake toka kati ya moto; mmeona leo ya kuwa Mungu husema na mwanadamu, naye akaishi. 25 Sasa basi, mbona tufe? Maana moto huu mkubwa utatuteketeza; tukiisikia tena sauti ya Bwana, Mungu wetu, tutakufa. 26 Maana katika wote wenye mwili ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka kati ya moto, kama vile sisi, asife? 27 Enenda karibu wewe, ukasikie yote atakayoyasema Bwana, Mungu wetu; ukatuambie yote atakayokuambia Bwana, Mungu wetu; nasi tutayasikia na kuyatenda. 28 Naye Bwana akasikia sauti ya maneno yenu mliyoniambia; Bwana akaniambia, Nimesikia sauti ya maneno ya watu hawa waliyokuambia; wamesema vema yote waliyosema. 29 Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele! 30 Enda uwaambie, Rudini hemani mwenu. 31 Lakini wewe, simama hapa karibu nami, nami nitanena nawe sheria zote, na amri na hukumu, utakazowafunza, wapate kuzifanya katika nchi niwapayo kuimiliki. 32 Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na Bwana, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kuume wala wa kushoto. 33 Endeni njia yote aliyowaagiza Bwana, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.

 

Ahadi hizi zilianzishwa ili kuwafanya waishi, sio tu wana wa Israeli, bali ni kwa watu wa ulimwenguni kote pia, kupitia kwa Israeli chini ya Masihi katika kumuabudu Mungu.

Kumbukumbu la Torati 6:1-25 inasema: Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru Bwana, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; 2 upate kumcha Bwana, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe. 3 Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali. 4 Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. 9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako. 10 Tena itakuwa atakapokwisha Bwana, Mungu wako, kukuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Ibrahimu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe, 11 na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vimefukuliwa usivyofukua wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba; 12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa. 13 Mche Bwana, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake. 14 Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao; 15 kwani Bwana, Mungu wako, aliye katikati yako ni Mungu mwenye wivu; isije ikawaka juu yako hasira ya Bwana, Mungu wako, akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi. 16 Msimjaribu Bwana, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa. 17 Zishikeni kwa bidii sheria za Bwana, Mungu wenu, na mashuhudizo yake, na amri zake alizokuagiza. 18 Nawe fanya yaliyo sawa, na mema, machoni pa Bwana; ili mpate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kuimiliki nchi nzuri Bwana aliyowaapia baba zako, 19 ya kuwa atawasukumia nje adui zako wote mbele yako, kama alivyosema Bwana. 20 Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, N'nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza Bwana, Mungu wetu? 21 Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; Bwana, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu; 22 Bwana akaonya ishara na maajabu, makubwa, mazito, juu ya Misri, na juu ya Farao, na juu ya nyumba yake yote, mbele ya macho yetu; 23 akatutoa huko ili kututia huku, apate kutupa nchi aliyowaapia baba zetu. 24 Bwana akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche Bwana, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo. 25 Tena itakuwa haki kwetu, tukitunza kufanya maagizo haya yote mbele ya Bwana, Mungu wetu, kama alivyotuagiza.

 

Israeli wamekuwa kila mara wakichukiwa na mataifa waliokuwa wanaabudu sanamu. Mfumo wa imani ya kuabudu sanamu na kuliabudu Jeshi la Mbinguni umekatazwa kwa namna na sababu zozote zile.

Kumbukumbu la Torati 4:19 tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.  

 

Uhusiano wa Torati au sheria na kalenda katika kumuabudu Mungu

Amri za Mungu zina zinaendana na maagizo, na utaratibu au mfumo wa sheria unasimama kama ulivyo (soma Kumbukumbu la Torati 4:40, inavyosema hapo juu)

 

Utaratibu wa agano la Israeli umeendelea hadi kwenye Kanisa lake Masihi na hadi kwa Wamataifa. (soma Kumbukumbu la Torati 5:1-7 hapo juu)

 

Mfumo na taratibu za Torati ya Mungu na kanuni zake vinawalikishwa na maadhimisho ya Sabato na Kalenda yeke Takatifu. (Kumbukumbu la Torati 5:14 hapo juu)

 

Israeli wanatakiwa kuyahubiri maneno yaliyo kwenye torati iliyoandikwa kwenye mawe makubwa, ni sawa na inavyotakiwa kwa kila mzaliwa au mkazi wa nyumbani mwetu azitunze Amri hizi Kumbu za Mungu. Utaratibu huu wa kuziandika kwenye mawe ni wa utumishi zikiwa kama nakala asilia ya torati kwenye taifa.

 

Kumbukumbu la Torati 27:1-26 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Andiko hili linamaonyo zaidi ya kuzitunza amri hizi. Wanaambiwa wajenge madhabahu na wayaandike maneno ya torati hii kwenye mawe.

 

Baraka na laana

Ahadi ya baraka maalumu kwa ajili ya kuyatunza maneno ya Torati na laana kwa ajili ya kutoyashika maneno ya Torati zimetolewa kwenye maandiko yayofuatia.

 

Baraka kwa Kuzitii

Kumbukumbu la Torati 28:1-14 inasema: Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. 3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. 6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. 7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. 8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. 9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake. 10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. 11 Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa. 12 Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. 13 Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya; 14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia

Ikiwa tukifuata na kuyatumikia maagizo yenye uzima yaliyotolewa na Mungu wetu wa Pekee na wa Kweli, basi baraka hizi zote zilizoorodheshwa hapo juu zitatupata na kutujilia. Tumepokea baraka hizi kwa sababu aliahidiwa Abrahamu na sisi ni uzao wake tulio na haki ya kuzipokea.

 

Laana kwa Kutozitii

Ni makosa kumdharau Mungu na kuziasi amri, sheria na hukumu zake. Wakati uovu wa mataifa ulipofikia kiwango chake cha kujaa na kukamilika, ndipo hukumu za Yahova zilipowafikia.

Kumbukumbu la Torati 28:15-36 inasema: Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. 16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. 17 Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia. 18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, 20 Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo. 21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki. 22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie. 23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma. 24 Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie. 25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani. 26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza. 27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa. 28 Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni; 29 utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa. 30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake. 31 Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang'anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa. 32 Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako. 33 Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima; 34 hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona. 35 Bwana atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa. 36 Bwana atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko utatumikia miungu mingine ya miti na mawe.
 

 

Iwapo kama tutaasi, ndipo laana zifuatazo zitaliandama taifa.

Kumbukumbu la Torati 28:37-68 inasema: Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza Bwana. 38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila. 39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu. 40 Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika. 41 Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani. 42 Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo. 43 Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini. 44 Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia. 45 Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza; 46 nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele; 47 kwa kuwa hukumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote; 48 kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza. 49 Bwana atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake; 50 taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana; 51 naye atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala maongeo ya ng'ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza. 52 Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa Bwana, Mungu wako. 53 Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa Bwana, Mungu wako; katika mazingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako. 54 Mtu mume kati yenu aliye mwororo na laini sana, jicho lake litakuwa ovu juu ya nduguye, na juu ya mke wa kifuani mwake, na juu ya masalio ya wanawe waliosalia naye; 55 hata asitake wao mmojawapo apewe katika nyama ya wanawe atakaowala, kwa kuwa hana kitu kilichomsalia kwake; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako yote. 56 Mwanamke kati yenu aliye mwororo na laini, ambaye hangehatirisha kuweka wayo wa mguu wake nchi kwa umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa kifuani mwake, na juu ya mwanawe, na juu ya binti yake, 57 na juu ya mchanga wake atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe atakaowazaa; kwa kuwa atawala kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako. 58 Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, Bwana, MUNGU WAKO; 59 ndipo atakapofanya Bwana mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana. 60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe. 61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa. 62 Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako. 63 Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi Bwana juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi Bwana juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki. 64 Bwana atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe. 65 Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini Bwana atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika; 66 na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako; 67 asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona. 68 Bwana atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena po pote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.

 

Ni kama tulivyoona hapo juu, laana zinafuatiwa na baraka ambazo zitafuatia baada ya kutii. Maonyo zaidi kuhusu uasi yanatolewa, nah ii imefafanuliwa zaidi kwenye jarida la Baraka na Laana (Na. 75) [The Blessings and the Curses (No. 75)].

 

Miujiza kwenye ulinzi

Kumbukumbu la Torati 29:1-29 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Maandiko yaliyoko hapo juu yanaonyesha kwamba Waisraeli wanakumbushwa kuhusu miujiza waliyoiona tangu walipoivuka Bahari ya Shamu, kwa mfano nguo zao na na viatu vyao havikuharibika. Waliambiwa kwamba agano lililokuwa kati yao na Mungu linabakia kuwa ni muhimu, na wanaonywa tena kuhusu madhara yatakayojitokeza baada ya kulivunja agano. Mfano huu ulikuwa ni wa kubakia kuwa kama sehemu ya Torati ya wakati wote.

Kumbukumbu la Torati 30:1-20 inasema: Tena itakuwa, mambo haya yote yatakapokujilia, baraka na laana nilizoweka mbele yako, nawe utakapozikumbuka kati ya mataifa yote, huko atakakokupeleka Bwana, Mungu wako, 2 nawe utakapomrudia Bwana, Mungu wako, na kuitii sauti yake, mfano wa yote nikuagizayo leo, wewe na wanao, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; 3 ndipo Bwana, Mungu wako, atakapougeuza utumwa wako, naye atakuhurumia, tena atarejea na kukukusanya kutoka mataifa yote, huko alikokutawanyia Bwana, Mungu wako. 4 Watu wako waliotawanyika wakiwako katika ncha za mbingu za mwisho, kutoka huko atakukusanya Bwana, Mungu wako; kutoka huko atakutwaa; 5 atakuleta Bwana, Mungu wako, uingie nchi waliyomiliki baba zako, nawe utaimiliki; naye atakutendea mema, na kukufanya uwe watu wengi kuliko baba zako. 6 Bwana, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai. 7 Na laana hizi zote Bwana, Mungu wako, atawatia adui zako na hao wakuchukiao, waliokuwa wakikutesa. 8 Nawe utarudi, uitii sauti ya Bwana, na kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo. 9 Na Bwana, Mungu wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako, katika uzao wa tumbo lako, na katika uzao wa ng'ombe wako, na katika uzao wa nchi yako; kwa kuwa Bwana atafurahi tena juu yako kwa wema, kama alivyofurahi juu ya baba zako; 10 ukiwa utaifuata sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa kuyashika maagizo yake, na amri zake zilizoandikwa katika chuo hiki cha torati; ukimwelekea Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote. 11 Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali. 12 Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya? 13 Wala si ng'ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya? 14 Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya. 15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya; 16 kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki. 17 Lakini moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikiza, lakini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia; 18 nawahubiri hivi leo hakika mtaangamia; hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukiayo Yordani, uingie kuimiliki. 19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; 20 kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.

 

Usomaji wa Torati ya Mungu

Hatimaye Musa akafikia umri wa miaka mia moja na ishirini na kipindi chake kikawa kimeisha. Anawatia moyo watu, na anamtia moyo Yoshua. Kisha Musa akaanza kuiandika torati na ikawekwa kwenye Sanduku la Agano la Bwana. Kisha Musa akawapa amri iliyotoka kwa Mungu kwamba torati yake inapaswa isomwe (Kumbukumbu la Torati 31:10-13).

Kumbukumbu la Torati 31:1-30 inasema: Musa akaenda akawaambia Waisraeli maneno haya yote.
2 Akawaambia, Mimi leo ni mwenye miaka mia na ishirini; siwezi tena kutoka na kuingia, na Bwana ameniambia, Hutavuka mto huu Yordani. 3 Bwana Mungu wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama Bwana alivyonena. 4 Na Bwana atawatenda hao kama vile alivyowatenda Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, na nchi yao, ambao aliwaharibu. 5 Naye Bwana atawatia mikononi mwenu, nanyi mtawatenda kadiri ya amri ile niliyowaamuru. 6 Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha. 7 Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi Bwana aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha. 8 Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike. 9 Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la agano la Bwana, na wazee wote wa Israeli. 10 Musa, akawaamuru, akasema, Mwisho wa kila mwaka wa saba, wakati wa maachilio, wakati ulioamriwa wa sikukuu ya vibanda, 11 Israeli wote wafikapo ili kuonekana mbele za Bwana, Mungu wako, mahali pale atakapopachagua, uisome torati hii mbele ya Israeli wote masikioni mwao. 12 Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha Bwana, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii; 13 na watoto wao wasiojua, wapate kusikia na kujifunza kumcha Bwana, Mungu wenu, siku zote mtakazokaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki. 14 Bwana akamwambia Musa, Tazama, siku zako za kufa zinakaribia, umwite Yoshua, nanyi mkajihudhurishe katika hema ya kukutania, ili nipate kumwagiza kazi. Musa na Yoshua wakaenda, wakajihudhurisha ndani ya hema ya kukutania. 15 Bwana akaonekana katika Hema katika nguzo ya wingu; na ile nguzo ya wingu ikasimama juu ya mlango wa Hema. 16 Bwana akamwambia Musa, Angalia, wewe utalala na baba zako; na watu hawa wataondoka, wataifuata kwa ukahaba miungu ya kigeni ya nchi waiendeayo kuwa kati yao, nao wataniacha mimi na kulivunja agano langu, nililofanya nao. 17 Ndipo hasira yangu itakapowaka juu yao siku hiyo, nami nitawaacha, nitawaficha uso wangu, nao wataliwa, tena watajiliwa na mambo maovu mengi na mashaka; hata waseme siku hiyo, Je! Kujiliwa kwetu na maovu haya si kwa sababu Mungu wetu hayumo kati yetu? 18 Nami nitawaficha uso wangu kwa kweli siku hiyo, kwa maovu yote waliyoyafanya, kwa kuigeukia hiyo miungu mingine. 19 Basi sasa jiandikieni wimbo huu, uwafundishe wana wa Israeli; kawatie vinywani mwao, ili uwe shahidi kwangu wimbo huu, juu ya wana wa Israeli. 20 Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu. 21 Tena itakuwa, wakiisha kujiliwa na mambo maovu mengi na mashaka, utashuhudia wimbo huu mbele yao kama shahidi, kwa maana hautasahauliwa katika vinywa vya uzao wao; kwani nayajua mawazo yao wayawazayo, hata sasa kabla sijawatia katika nchi niliyoapa. 22 Basi Musa akauandika wimbo huu siku iyo hiyo, akawafundisha wana wa Israeli. 23 Akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, Uwe hodari na moyo mkuu, kwa kuwa utawapeleka wana wa Israeli katika nchi niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja nawe. 24 Basi ikawa hapo Musa alipomaliza kuandika maneno ya torati hii katika chuo, hata yakaisha, 25 ndipo Musa akawaamuru Walawi waliokuwa wakilichukua sanduku la agano la Bwana akawaambia, 26 Twaeni chuo hiki cha torati, mkiweke kando ya sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako. 27 Kwa kuwa uasi wako naujua, na shingo yako ngumu; angalieni, mimi nikali hai pamoja nanyi leo, mmekuwa waasi juu ya Bwana; siuze nitakapokwisha kufa! 28 Nikutanishieni wazee wote wa kabila zenu, na maakida yenu, ili niseme maneno haya masikioni mwao, na kuwashuhudizia mbingu na nchi juu yao. 29 Kwa sababu najua baada ya kufa kwangu mtajiharibu kabisa, na kukengeuka katika njia niliyowaamuru; nayo mabaya yatawapata siku za mwisho, kwa vile mtakavyofanya maovu machoni pa Bwana kumtia kasirani kwa kazi ya mikono yenu. 30 Musa akasema maneno ya wimbo huu masikioni mwa kusanyiko la wana wa Israeli hata yakaisha.
 

 

Wimbo wa Musa

Mungu akaweka sheria zake na taratibu zake chini ya mtumishi wake mwaminifu. Wakati alipofanya yote ambayo Mungu alimtaka ayafanye, ndipo Mungu akamwambia Musa kwamba ulikuwa umefika sasa muda way eye kufa. Ndipo Musa na Yoshua wakaingia kwenye Hema ya kukutania na Bwana akawatokea. Akawaambia kwamba anajua kwamba watu watalivunja agano na jambo hilo litampekelea yeye kuwakasirikia na mabaya mengi yatawapata. Walitakiwa kujifunza na kuimba wimbo wa pili wa utukufu ujulikanao kama Wimbo wa Musa.

Kumbukumbu la Torati 32:1-52 inasema::Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu. 2 Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea. 3 Maana nitalitangaza Jina la Bwana; Mpeni ukuu Mungu wetu. 4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili. 5 Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka. 6 Je! Mnamlipa Bwana hivi, Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara. 7 Kumbuka siku za kale, Tafakari miaka ya vizazi vingi; Mwulize baba yako, naye atakuonyesha; Wazee wako, nao watakuambia. 8 Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao, Alipowabagua wanadamu, Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli. 9 Maana, sehemu ya Bwana ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake. 10 Alimkuta katika nchi ya ukame, Na katika jangwa tupu litishalo; Alimzunguka, akamtunza; Akamhifadhi kama mboni ya jicho; 11 Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake; Na kupapatika juu ya makinda yake, Alikunjua mbawa zake, akawatwaa, Akawachukua juu ya mbawa zake; 12 Bwana peke yake alimwongoza, Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye. 13 Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume; 14 Siagi ya ng'ombe, na maziwa ya kondoo, Pamoja na mafuta ya wana-kondoo, Kondoo waume wa Kibashani, na mbuzi, Na unono wa ngano iliyo nzuri; Ukanywa divai, damu ya mizabibu. 15 Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake. 16 Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo. 17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa. 18 Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau. 19 Bwana akaona, akawachukia, Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake. 20 Akasema, Nitawaficha uso wangu, Nitaona mwisho wao utakuwaje; Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi, Watoto wasio imani ndani yao. 21 Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu; Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo. 22 Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima. 23 Nitaweka madhara juu yao chunguchungu; Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe; 24 Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto, Na uharibifu mkali; Nitawapelekea meno ya wanyama wakali, Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini. 25 Nje upanga utawafifiliza Na ndani ya vyumba, utisho; Utaangamiza mvulana na msichana, Anyonyaye pamoja na mwenye mvi, 26 Nalisema, Ningewatawanyia mbali, Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu; 27 Isipokuwa naliogopa makamio ya adui, Adui zao wasije wakafikiri uongo, Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka, Wala Bwana hakuyafanya haya yote. 28 Maana hawa ni taifa wasio shauri, Wala fahamu hamna ndani yao. 29 Laiti wangekuwa na akili, hata wakafahamu haya, Ili watafakari mwisho wao. 30 Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa? 31 Maana, Mwamba wao si kama Mwamba wetu, Hata adui zetu wenyewe ndivyo wahukumuvyo. 32 Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma, Nao ni wa mashamba ya Gomora; Zabibu zao ni zabibu za uchungu, Vichala vyao ni vichungu. 33 Mvinyo yao ni sumu ya majoka, Uchungu mkali wa nyoka. 34 Je! Haya hayakuwekwa akiba kwangu? Na kutiwa muhuri kati ya hazina yangu? 35 Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka. 36 Kwa kuwa Bwana atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa, 37 Naye atasema, Iko wapi miungu yao, Mwamba ule walioutumaini; 38 Uliokula shahamu za sadaka zao, Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji? Na waondoke na kuwasaidia ninyi; Na wawe hao himaya yenu. 39 Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu, 40 Maana, nainua mkono wangu mbinguni, Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele, 41 Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia. 42 Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui. 43 Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake; Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake, Atawatoza kisasi adui zake, Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake. 44 Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni. 45 Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote; 46 akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii. 47 Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki. 48 Bwana akasema na Musa siku iyo hiyo, akamwambia, 49 Kwea katika mlima huu wa Abarimu, mpaka kilima cha Nebo, kilicho katika nchi ya Moabu, kuelekea Yeriko; ukaangalie nchi ya Kanaani niwapayo wana wa Israeli kuimiliki; 50 ukafe katika kilima, huko ukweako, ukusanywe uwe pamoja na jamaa zako; kama alivyokufa nduguyo Haruni katika mlima wa Hori, akakusanywa awe pamoja na watu wake; 51 kwa sababu mlinikosa ninyi juu yangu katikati ya wana wa Israeli katika maji ya Meriba huko Kadeshi, katika bara ya Sini; kwa kuwa hamkunitakasa katikati ya wana wa Israeli. 52 Kwani utaiona hiyo nchi mbele yako, lakini hutakwenda huko kuingia hiyo nchi niwapayo wana wa Israeli

 

Kuyabariki makabila

Kisha Musa akawabarikia watu wa makabila ya Israeli.

Kumbukumbu la Torati 33:1-29 inasema::Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake. 2 Akasema,Bwana alitoka Sinai,Akawaondokea kutoka Seiri;Aliangaza katika kilima cha Parani,Akaja Meribath-Kadeshi.Upande wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao. 3 Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako. 4 Musa alituagiza torati, Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo. 5 Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja. 6 Reubeni na aishi, asife; Lakini watu wake na wawe wachache. 7 Na baraka ya Yuda ni hii; akasema, Isikize, Ee Bwana, sauti ya Yuda, Umlete ndani kwa watu wake; Alijitetea kwa mikono yake; Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake. 8 Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta naye kwenye maji ya Meriba. 9 Aliyemtaja baba yake na mama yake, Mimi sikumwona; Wala nduguze hakuwakubali; Wala hakuwajua watoto wake mwenyewe; Maana wameliangalia neno lako, Wamelishika agano lako. 10 Watamfundisha Yakobo hukumu zako, Na Israeli torati yako, Wataweka uvumba mbele zako, Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako. 11 Ee Bwana, ubariki mali zake, Utakabali kazi ya mikono yake; Uwapige viuno vyao waondokao juu yake, Na wenye kumchukia, wasiinuke tena. 12 Akamnena Benyamini, Mpenzi wa Bwana atakaa salama kwake; Yuamfunika mchana kutwa, Naye hukaa kati ya mabega yake. 13 Na Yusufu akamnena, Nchi yake na ibarikiwe na Bwana; Kwa vitu vya thamani vya mbinguni, kwa huo umande, Na kwa kilindi kilalacho chini, 14 Na kwa vitu vilivyo bora vya matunda ya jua, Na kwa vitu vilivyo bora vya maongeo ya miezi, 15 Na kwa vitu viteule vya milima ya kale, Na kwa vitu vilivyo bora vya vilima vya milele, 16 Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake, Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kijiti; Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze. 17 Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase. 18 Na Zabuloni akamnena, Furahi Zabuloni, katika kutoka kwako; 19 Watayaita mataifa waje mlimani; Wakasongeze huko sadaka za haki; Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari, Na akiba zilizofichamana za mchangani. 20 Na Gadi akamnena, Na abarikiwe amwongezaye Gadi; Yeye hukaa kama simba mke, Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa. 21 Akajichagulia sehemu ya kwanza, Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria; Akaja pamoja na wakuu wa watu, Akaitekeleza haki ya Bwana, Na hukumu zake kwa Israeli. 22 Na Dani akamnena, Dani ni mwana-simba, Arukaye kutoka Bashani. 23 Na Naftali akamnena, Ee Naftali, uliyeshiba fadhili, Uliyejawa na baraka ya Bwana; Umiliki magharibi na kusini. 24 Na Asheri akamnena, Na abarikiwe Asheri kwa watoto; Na akubaliwe katika nduguze, Na achovye mguu wake katika mafuta. 25 Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako. 26 Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake. 27 Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza. 28 Na Israeli anakaa salama, Chemchemi ya Yakobo peke yake, Katika nchi ya ngano na divai; Naam, mbingu zake zadondoza umande. 29 U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.

 

Musa na wateule

Musa aliruhusiwa kuiona Nchi ya Ahadi lakini “alichukuliwa” kabla ya kuiteka na kuikalia, na ndivyo ulivyo ukweli kwa maisha ya wateule, kwamba wataiona Israeli chini ya Masihi wakiwa watu walio kwenye ulimwengu wa roho.

Kumbukumbu la Torati 34:1-12 inasema: Musa akapanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo, hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. Bwana akamwonyesha nchi yote ya Gileadi hata Dani; 2 na Naftali yote, na nchi ya Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda, mpaka bahari ya magharibi; 3 na Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari. 4 Bwana akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko. 5 Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la Bwana. 6 Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo. 7 Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka. 8 Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha. 9 Na Yoshua, mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama Bwana alivyomwamuru Musa. 10 Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso; 11 katika ishara zote na maajabu yote, ambayo Bwana alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote; 12 na katika ule mkono wa nguvu wote, tena katika ule utisho mkuu wote, alioutenda Musa machoni pa Israeli wote.

 

Mungu, akiwa ni Yahova wa Majeshi, ametutenga sisi mbali katika utumishi wake kwa kupitia manabii watumikao chini ya Yahova. Hatupaswi kuwa na miungu mingine ila Mungu peke yake, ni kama ilivyo kwamba hakuna Eloa mwingine, bali ni Eloa peke yake. Yahova ndiye elohim wetu, na tusiwe na elohim mwingine zaidi yake. Uwezo wa kuwa elohim uliwekwa na Mungu kwa kuanzia kwa Mjumbe wa Yahova kupitia kwa Roho Mtakatifu. Mjumbe huyu akafanyika kuwa Kuhani Mkuu na akatufungulia njia ili tuwe wana wa Mungu kwa uweza kama wa elohim, kama alivyo yeye, tangia alipofufuka toka kwa wafu (soma Warumi 1:4). Amefanyikwa kuwa ni elohim kama Malaika wa Yahova na kichwa chetu (Zekaria 12:8). Kwa kupitia utii wetu kwenye Torati kiasi cha kuifia, tunafanywa pia kuwa ni wana wa Mungu, na watoto wak yeye aliye juu sana na Mwenyezi na Maandiko hayawezi kutanguka (Zaburi 82:6; Yohana 10:34-35).

q