Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[254]

 

 

 

Torati na Amri ya Pili ya Mungu

 (Toleo Na. 3.0 19981006-20050718-20120512)

 

Imeandikwa: Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia. Jarida hili linakwenda kuifafanua Amri hii ya Pili ya Mungu, kwa jinsi ilinavyotenda kazi kwenye maagano yote mawili, yaani kwenye Agano la Kale na kwenye Agano Jipya, na kuelezea umuhimu wake kwenye taratibu zetu za kisheria, kwenye kanuni zetu za kijamii na makosa na jinsi ya kutoa hukumu kwa jinsi inavyotakikana kuwafanyia watu wote.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 1998, 1999, 2005, 2012 Wade Cox et al, ed Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org


Torati na Amri ya Pili ya Mungu

 


Amri hii ya Pili ya Mungu imeandikwa hivi ifuatavyo:

Kutoka 20:4-7 inasema: 4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. 7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

 

Kumbukumbu la Torati 5:8-10 inasema:

8 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. 9 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 10 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

 

Mari hii imetiliwa mkazo pia kwenye Agano Jipya kama ifuatavyo:

1Petro 4:3-5 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; 4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. 5 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.

 

Wagalatia 5:19-21 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

 

Warumi 1:21-25  kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. 22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; 23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. 24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.

1Wakorintho 8:4-6 Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu. 5 Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; 6 lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo.

 

1Wakorintho 10:14  Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.

 

1Yohana 5:21 Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.

 

Ni kama ilivyo amri ya tano, amri hii ya pili pia inajumuisha ahadi za hata kama ni za uovu au rehema (kama ilivyo kwenye Kutoka 20:4-7 hapo juu na kwenye Kumbukumbu la Torati 5:1-10 hapo chini).

 

Amri hii ya pili pia inatuama kwenye kivuli cha ile Amri ya Iliyokuu na ya Kwanza ambayo imetajwa kwenye kitabu cha Mathayo 22:36-37 na pia kwenye Kumbukumbu la Torati 6:5.

Mathayo 22:36-38 inasema: Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza

 

Kumbukumbu la Torati 6:5  Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

 

Amri hii Kuu na ya Kwanza inahusisha Amri zote na Manabii (Mathayo 22:40).

Analotaka Mungu tulifanye

Mungu ametuopa maelekezo mengi sana kuhusu mambo anayotaka sisi tuyafanye, na anafanya hivyo sio kwa faida yake, bali ni kwa faida yetu. Anasema kwamba ni kwa faida yet una sio kwa faida yake, kama alivyokwisha elezea tayari manufaa yake (Mathayo 19:17).

Kumbukumbu la Torati 10:12-13 Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; 13 kuzishika amri za Bwana na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?

 

Mambo ya Walawi 18:4-5 Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 5 Nanyi hapo mtakapomchinjia Bwana sadaka ya amani mtaisongeza ili kwamba mpate kukubaliwa.

 

Mambo ya Walawi 19:37 Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi Bwana.

 

Mambo ya Walawi 19:1-2 Bwana akanena na Musa, akamwambia, 2 Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu.

 

Mambo ya Walawi 20:7-8 Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 8 Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.

 

Mungu emetuahidi kwamba kama tutazishika amri zake na sheria zake atatubarikia na kutupa afya njema.

Kutoka 15:26 Akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.

 

Kumbukumbu la Torati 7:15 Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao.

 

Kwa hiyo tunaona sasa kwamba kitu anachokitaka Mungu tuwenacho sana ni utii. Tunaona pia kwamba kuna ahadi ambazo Mungu ametuahidia za kuwapa afya njema wana wa Israeli kama watakaza kumtii.

Kumbukumbu la Torati 26:16 Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.

 

Kumbukumbu la Torati 5:1-7 Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuangalia kuzitenda. 2 Bwana, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu. 3 Bwana hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai. 4 Bwana alisema nanyi uso kwa uso mlimani, toka kati ya moto; 5 (nami wakati ule nalisimama kati ya Bwana na ninyi, ili kuwaonyesha neno la Bwana; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani); naye akasema, 6 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 7 Usiwe na miungu mingine ila mimi.

Sanamu za Kuchonga

Makatazo ya kujifanyia sanamu za kuchonga yametolewa na amri hii inawakataza matendo ya kujitengenezea sanamu kwa matumizi ya kuziabudu. Hatupaswi kujifanyia sanamu hizi kama wanavyofanya wapagani wamataifa na kuzipigia magoti na kuziabudu. Kuna sanamu zilizokuwa zimetengenezwa kwa amri ya Musa za vitu vya aina zote mbili, za mambo yaliyoko mbinguni na vya duniani na havikukatazwa kabisa. Amri hii haikatazi kuchonga au kuwa na sanamu kwa nia ya kuweka mapambo au kwa matumizi mengineyo, bali isiwe ni kwa matumizi ya ibada, ba ijulikane pia kwamba tendo la kuabudu kitu kingine chochote nje ya Mwenyezi Mungu, Baba yetu ni ibada ya sanamu na imekatazwa kabisa. Tunaona kuwa hakuna sura wala mfano wowote wa Mungu Baba yetu mahali popote, na sura yake haijawahi kuonekana na mwanadamu yeyote mwenye mwili. Kwenye uandishi wa andiko hili hasa kwenye Tafsiri Mpya ya Mfalme Yakobo (NKJV) inasema hata wataalamu wa mambo ya kale na uchimbuzi wamakubaliana kuwa hakujawahi kuonekana wala kuvumbuliwa kitu chenye kuashiria umbo la Mungu hata katika kazi yao ya uchimbuzi wa mambo kale kwenye vifusi vya kwenye miji ya huko Israeli. Hii inatupa uhakika wa jinsi hata mambo ya kale yanavyokubaliana pia na inavyosema amri hii ya pili, na kwa vile tunaendelea kuona jisi mabaki ya miungu mingine yanavyoendelea kuvumbuliwa hata hadi kwenye siku za hivi karibuni.

 

Mungu alijua kwamba wanadamu watafikia kiasi cha kuchonga sanamu za watu maarufu wao au viumbe mashuhuri na hatimaye watawaabudu. Mfano wa jambo hili ni jinsi Kanisa Katoliki lilivyofanya kwa kujichongea sana za wale wanaowaita wenyewe kuwa ni watakatifu. Ni kwa makusudi kabisa Mungu aliuficha mwili wa Musa kwa kuepusha jambo hilohilo. Basi na tusiruhusu tuangukie kwenye makosa haya na ndiyo maana tunajitahidi kujiepusha kuwa na sanamu za malaika, Kristo au za viumbe wengine wa mbinguni kuwa navyo majumbani mwetu.

 

Amri hii inayotuzuia tusijifanyie au kujitengenezea aina yoyote ya sanamu—au aina yoyote ya kitu chochote kinachofanana na kitu chochote kilichoko mbinguni au duniani chini kwa nia ya kukiabudu—inatokana na tabia aliyonayo Mungu ya kuwa ni Mungu mwenye wivu. Tabia ya wivu inayotajwa hapa sio ile ya aina iliyokatazwa kwenye maandiko matakatifu, bali ni aina ya wivu wa haki ambao inatokana na upendo alionao Eloa Baba yetu kwetu sisi. Na sio aina ya wivu unaotokana na ubinafsi, ambao ni wivu ulioko kwa wanadamu. Ijulikane pia kwamba Mungu hataki sisi tujichanganye, bali anamtaka kila mmoja wetu awe ni mkamilifu na mtakatifu (Mambo ya Walawi 20:7). Hapendi sisi tujitie kwenye makundi ya kikahaba na kuitafuta na kuiabudu miunbu mingine ambayo ni ya uwongo na kutufanya tushindwe kuipata thawabu aliyotuahidia sisi watoto wake kama alivyosema :

Kumbukumbu la Torati 4:15-40 Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile Bwana aliyosema nanyi kutoka kati ya moto; 16 msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke, 17 mfano wa mnyama ye yote aliye duniani, au mfano wa ndege ye yote arukaye mbinguni, 18 au mfano wa kitu cho chote kitambaacho juu ya ardhi, au mfano wa samaki ye yote aliye majini chini ya nchi; 19 tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. 20 Bali Bwana amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuu ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo leo hivi. 21 Tena Bwana alinikasirikia kwa ajili yenu, akaapa ya kwamba sitavuka Yordani, na ya kwamba sitaingia nchi ile njema, awapayo Bwana, Mungu wenu, iwe urithi. 22 Lakini mimi nitakufa katika nchi hii, sina ruhusa kuvuka Yordani; bali ninyi mtavuka, na kuimiliki nchi ile njema. 23 Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la Bwana, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu cho chote ulichokatazwa na Bwana, Mungu wenu, 24 kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, ni moto ulao, Mungu mwenye wivu. 25 Utakapozaa wana, na wana wa wana, mkisha kuwa katika nchi siku nyingi, mkajiharibu na kufanya sanamu ya kuchonga kwa umbo la kitu cho chote, mkafanya ambayo ni maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, na kumtia hasira; 26 nawashuhudizia mbingu na nchi hivi leo, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa. 27 Na Bwana atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu kidogo hesabu yenu kati ya makabila, mtakakopelekwa mbali na Bwana. 28 Na huko mtatumikia miungu, kazi za mikono ya watu, miti na mawe, ambao hawaoni, wala hawasikii, hawali, wala hawanusi. 29 Lakini huko, kama mkimtafuta Bwana, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote. 30 Na wakati uwapo katika mashaka, ukiisha kupatwa na mambo haya yote, siku za mwisho, utamrudia Bwana, Mungu wako, na kuisikiza sauti yake; 31 kwa kuwa Bwana, Mungu wako, ni Mungu wa rehema; hatakukosa wala kukuangamiza, wala hatalisahau agano la baba zako alilowaapia. 32 Maana uliza sasa siku zilizopita, zilizokuwa kabla yako, tangu siku ile Mungu aliyoumba mwanadamu juu ya nchi, na toka pembe hii ya mbingu hata pembe hii, kwamba kumetukia neno lo lote kama neno hili kubwa, au kwamba kumesikiwa habari ya neno kama hili? 33 Je! Watu wakati wo wote wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, wasife? 34 Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu? 35 Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa Bwana ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye. 36 Kutoka mbinguni amekusikizisha sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonyesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake toka kati ya moto. 37 Na kwa sababu aliwapenda baba zenu, kwa sababu hiyo aliwachagua wazao wao baada yao, akakutoa katika Misri kwa kuwako pamoja nawe, kwa uweza wake mwingi, 38 ili kufukuza mbele yako mataifa, walio wakubwa, wenye nguvu kukupita wewe, ili kukuingiza, na kukupa nchi yao iwe urithi, kama ilivyo leo. 39 Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa Bwana ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine. 40 Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo Bwana, Mungu wako, milele.

 

Kutoka 34:17 Usijifanyizie miungu ya kuyeyusha.

 

Mambo ya Walawi 19:4 Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Mambo ya Walawi 26:1 Msifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Israeli wenyewe walikuwa hatengenezi kabisa sanamu za kuchonga na kuziabudu kwma walivyofanya wamataifa, wapagani, na ndivyo wanavyotakiwa kufanya hata Israeli wa kiroho leo. Wakristo hawatakiwi kuabudu aina yoyote ya sanamu, wala taswira au picha wala kitu chohote kilichochongwa na wanadamu, wala malaika wa mbinguni na vingine vyote vilivyokatazwa kuabudiwa. Ni Mungu peke yake ndiye anayepaswa kutumikiwa na kuabudiwa!

Mambo ya Walawi 17:7 Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi.

 

Kumbukumbu la Torati 11:16-17 Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu; 17 hasira za Bwana zikawaka juu yenu, naye akafunga mbingu kusiwe na mvua, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo Bwana.

 

Kumbukumbu la Torati 12:29-32 Bwana, Mungu wako, atakapoyakatilia mbali hayo mataifa mbele yako, huko uingiako kuyamiliki, nawe ukawatwaa, na kuketi katika nchi yao; 30 ujiangalie, usije ukanaswa ukawafuata, wakiisha kuangamizwa mbele yako; wala usije ukauliza habari za miungu yao, ukisema, Mataifa haya waitumikiaje miungu yao? Nami nifanye vivyo. 31 Usimtende kama haya Bwana, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa Bwana, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto. 32 Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.

 

Kutakuja kipindi ambacho kwamba manabiina pengine hata watumishi wa Mungu wengine watatuambia tuende tukaiabudu miungu mingine, wakidhania kwamba hakuna ubaya na inakubalika tu kufanya hivyo. Mungu anasema kwamba jambo hilo linaweza kutokea, ila litatokea hivyo kwetu ili kutujaribu roho zetu ili aone kama tumampenda kweli Bwana Mungu wetu kwa mioyo yetu yote na roho zetu zote na akili zetu zote.

Kumbukumbu la Torati 13:1-4 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.

 

Jinsi ya kushinda kwa sisi kama Wakristo ni iwapo kama tutakuwa na uelewa wa kutosha katika amri na kanuni za Mungu. Na hii ndoyo sababu tunaisoma torati peke yake kwenye mwaka wa Sabato: jambo linalotusaidia kurejesha uelewa wetu kwa kile tunachotakiwa kukifanya. Na hii ndiyo ilikuwa sababu kwa wafalme wa Israeli waliamriwa kuiandika torati kwa mikono yao wenyewe. Walitakiwa WAIELEWE vema Torati ili waweze kutoa hukumu ya haki kwa watu. Ili tuwe wanyenyekevy na watiifu, tunatakiwa kuijua torati hata sisi pia.

 

Tumeamriwa kuziharibu aina yoyote ya sanamu popote tunapoziona, vinginevyo tutaangamia hata sisi, kama yale mataifa ambayo Mungu aliyaangamiza kipindi kile cha utawala wa wafalme.

Kumbukumbu la Torati 8:19-20 Lakini itakuwa, kama ukimsahau Bwana, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka. 20 Kama vile mataifa yale ambayo Bwana anawaangamiza mbele yenu, ndivyo mtakavyoangamia; kwa sababu hamkutaka kuisikiliza sauti ya Bwana, Mungu wenu.

 

Kumbukumbu la Torati 7:16 Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa Bwana, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani litakuwa ni mtego kwako jambo hilo.

 

Wengi wataiona hii kama tendo la kikatili. Unadhani ni kwa nini Mungu huyu mwenye upendo awaamuru Israeli kuwangamiza wengine? Jibu ni kwamba, alijua kwamba Israeli wangeangukia kwenye ibada hizi za sanamu kama wangepewa mwanya wa kuziacha sanamu hizi ziendelee kuonekana kati yao. Kanisa la Kikrisro limeangukia kwenye ibada hizi za sanamu kwa namna hiyohiyo. Walitamani kuwa na wafuasi wengi na wakawaruhusu wafuasi hawa wapya waje na sanamu zao na matendo yao ya kipagani kanisani. Mungu atawatapika watoke kinywani mwake kwa ajili ya kuendekeza kwao matendo haya yanayochukuliwa kuwa ni ibada za sanamu.

 

Kutoka 23:24 Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande.

 

1Mambo ya Nyakati 5:25 Nao wakamwasi Mungu wa baba zao, wakaenda kufanya uasherati na miungu ya watu wa nchi, ambao Mungu alikuwa amewaangamiza mbele yao.

 

Watu wanaojiunga na Kanisa wanapaswa waamue kujiepusha na kuzikana ibada za sanamu na wajiepushe na matendo ya aina yoyote ya kuabudu na kuvipigia magoti vitu vingine vyovyote. Hii ikiwa ni pamoja na malaika na viumbe vyovyote viliovyoko mbinguni. Yatupasa kujua kwamba hakuna kiumbe yeyote aliye sawa na Mungu Baba yet una hakuna mwigine tunayepaswa kumuabudu, ila ni yeye peke yake.

1Wathesalonike 1:9 Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;

Makatazo kuhusu miungu mingine

Mungu hakuacha kitu anapofikiri mambo tunayopaswa kuwafanyia hawa miungu ya sanamu za kuchonga au miungu ya kusubu. Amri aliyoitoa Kungu ni kuiharibu kabisa na kuzivunjavunja kabisa na kusiweko na ukumbusho wowote uliobakia.

Kutoka 34:12-13 Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako. 13 Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao.

 

Kumbukumbu la Torati 7:25-26 Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako; 26 na machukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni kitu kilichoharimishwa.

 

Kumbukumbu la Torati 12:1-4 Hizi ndizo amri na hukumu mtakazotunza kuzifanya katika nchi aliyokupa Bwana, Mungu wa baba zako, uimiliki, siku zote mtakazoishi juu ya nchi. 2 Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; 3 nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo. 4 Wala msimfanyie hivyo Bwana, Mungu wenu.

 

Hesabu 33:52 ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunja-vunja mahali pao pote palipoinuka;  

 

Mungu amewakataza Israeli na wale walio Israeli wote wa Mungu ambao ni Hekalu la Kanisa, kuwa wasiwaoe mataifa wapagani, yaani watu walio kwenye umataifa wa kipagani na wenye imani na ibada za sanamu mioyoni mwao.

 

Biblia imewanukuu watu waliotoka kwenye mataifa mengine na waliowaoa Israeli na kwenye Kanisa, bali kila mara walikuwa kwenye mabishano na mijadala na kulionekana kuwepo kwa mwendelezo wa kutanuka hali ya kuwafikia mataifa Wapagani na kuwaokoa. Hatupaswi kufungiwa nira pamoja na waabudu sanamu.

 

Musa alimuoa mwanamke wa Kimidiani, binti wa kuhani wa Midiani aliyetokana na mwana wa Ibrahimu aliyemzaa kwa Ketura, lakini tunaona bado kwamba Wamidiani waliangamizwa na kufutiliwa mbali miaka arobaini iliyofuatia baadae kwa ajili ya dhambi yao hii ya kuabudu sanamu. 

Kumbukumbu la Torati 7:1-5 Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; 2 wakati Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao; 3 binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. 4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi. 5 Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.

Ibada za kuwatoa watoto wao sadaka kwa miungu ya uwongo

Wakati wowote inapotolewa sadaka kwa miungu mingine badala ya kumtolea Mungu Mmoja na Wapekee wa Kweli inahesabiwa kuwa hiyo ni ibada ya sanamu. Kwa ufafanuzi ni kwamba utoaji wa sadaka ni kitendo sawa na kufanya ibada au kuabudu. Kwa hiyo, utoaji wa sadaka ni tendo la kuabudu ambalo linaambatana na utoaji wa sadaka.

 

Katika siku za zama za uandishi wa Biblia, Moleki au Moloki ndiye alikuwa mungu maarufu wa Wakanaani ambaye aliabudiwa kwa kumtolea sadaka za wanadamu (hususan watoto wadogo) ndio waliokuwa wanatolewa. Aina hii ya dhabihu au sadaka imekatazwa kabisa na Mwenyezi Mungu, na adhabu kwa mtu afanyaye hivyo ni kifo.

Mambo ya Walawi 18:21 Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana.

 

Mambo ya Walawi 20:2-5 Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe. 3 Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu. 4 Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yo yote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue; 5 ndipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na jamaa zake, nami nitamkatilia mbali, na hao wote wamwandamao katika uzinifu, ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao.

 

2Wafalme 16:3 Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.

 

Yeremia 7:31 Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni; jambo ambalo mimi sikuliagiza, wala halikuingia moyoni mwangu.

 

Yeremia 19:5  nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu;

 

Kumbukumbu la Torati 12:31 Usimtende kama haya Bwana, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa Bwana, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto

 

Kumbukumbu la Torati 18:9-10 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

Desturi za mataifa wapagani

Tumeamriwa kuwa tusizifuate kwa sababu yoyote ile desturi na machukizo ya watu hawa wa mataifa ambao tunaketi kati yao, na hasa kwa desturi au mila zile zinazopingana na maagizo au mapenzi ya Mungu wetu.

Kutoka 23:32 Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao.

 

Kutoka 23:33 Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni tanzi kwako

 

Mambo ya Walawi 18:3 Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msiende katika amri zao hao.  

 

Mambo ya Walawi 18:26-30 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao. 30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Mambo ya Walawi 20:23 Nanyi msiende kwa kuziandama desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia.

 

Kumbukumbu la Torati 6:14 Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;

 (sawa na inavyosema Kumbukumbu la Torati 12:29-31 hapo juu)

 

Kumbukumbu la Torati 18:9-14 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. 14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.  

 

2Mambo ya Nyakati 36:14  Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya Bwana aliyoitakasa katika Yerusalemu.

 

2Wafalme 21:1-7 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na mitano katika Yerusalemu, na jina la mamaye aliitwa Hefziba. 2 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli. 3 Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. 4 Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu. 5 Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. 6 Akampitisha mwanawe motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. 7 Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo Bwana alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele;

 

Ezekieli 20:31-32 Tena mtoapo matoleo yenu, na kuwapitisha watoto wenu motoni, je! Mnajitia unajisi kwa vinyago vyenu vyote hata leo? Na mimi je! Niulizwe neno nanyi, Enyi nyumba ya Israeli? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi. 32 Na haya yote yaingiayo katika nia zenu hayatakuwa kamwe; ikiwa mmesema, Sisi tutakuwa sawasawa na mataifa, sawasawa na jamaa za nchi nyingine, kutumikia miti na mawe.

Uchawi na Ulozi ni Ibada ya Sanamu

Tendo la kuwaendea wachawi, walozi, au aina yeyote ile ya watambuzi kama wanavyojulikana leo kuwa ni wataalamu wa utambuzi wa mambo yaliyoko moyoni mwa mtu (psychs) au wanajimu, ni tendo lililo sawa tu na ibada hii ya sanamu na itapelekea mtu kukatiliwa mbali atoke kwa watu wake, au kwa maneno mengine ni kwamba auawe. Aina hii ya dhabihu ni machukizo kwa Bwana Mungu wetu.

Mambo ya Walawi 19:26 Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.

 

Mambo ya Walawi 19:31 Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Mambo ya Walawi 20:6 Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.

 

Mambo ya Walawi 20:27 Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.

(sawa na inavyosema Kumbukumbu la Torati 18:9-14 hapo juu)

 

Kutoka 22:18 Usimwache mwanamke mchawi kuishi. 19 Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.

 

2Mambo ya Nyakati 33:6 Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.

 

Isaya 47:13-15  Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata. 14 Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao. 15 Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.

 

Kupotea kwa watoto wetu na kinamama kuwa wajane kunaweza kuwa ni matokeo ya ulozi tunaoufanya na kujipendelea sisi wenyewe.

Isaya 47:9-14  lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno. 10 Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi. 11 Kwa sababu hiyo ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua. 12 Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda. 13 Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata. 14 Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao.

 

Yeremia 27:9 Lakini, katika habari zenu, msisikilize manabii wenu, wala wabashiri wenu, wala ndoto zenu, wala watambuzi wenu, wala waganga wenu, wanaowaambia, ya kwamba, Hamtamtumikia mfalme wa Babeli;

 

Mika 5:12 nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana;

 

Malaki 3:5 Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.

 

Matendo 13:6-11 Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; 7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. 9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? 11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.

 

Wagalatia 5:16-21 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. 19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.  

 

Uasi ni moja wapo ya ibada ya sanamu pia. Machoni pa Mungu, uasi na ibada ya sanamu ni kitu kumoja na vinaenda pamoja. Tendo la kulikataa neno la Mungu pia ni ibada ya sanamu na mtumishi anayeshindwa kufundisha kweli ya Mungu ana hatia ya kuwapeleka wafuasi wake kwenye ibada hizi za sanamu. Kwa sababu hii ndio maana mfalme sauli alikataliwa na Mungu asiwe mfalme wa Israeli.

1Samweli 15:23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.

Sanamu na vinyago: Ni kazi ya mikono ya wanadamu

Wale wanaoabudu sanamu, hata kama ni zile zilizotengenezwa kwa mawe, miti au mali ghafi nyingine yoyote, kwa kweli wanafanya ibada ya kujipotezea, isiyo na maana yoyote. Sanamu hizi zenyewe tu zinahitaji mtu wa kuzitengeneza na kuzisogeza mahali fulani kwa kuwa haziwezi kusogea, wala kuongea wala kufanya jambo lolote, na wale waliozitengeneza sanamu hizi nao ni kama vinyago hivyo vyenyewe walivyo na ndivyo walivyo wale wote wanaovitumainia vinyago hivyo hufanana navyo (Kutoka 20:22-23).

Zaburi 115:1-8 Ee Bwana, kutukuza usitutukuze sisi, Bali ulitukuze jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako, Kwa ajili ya uaminifu wako. 2 Kwa nini mataifa kusema, Yuko wapi Mungu wao? 3 Lakini Mungu wetu yuko mbinguni, Alitakalo lote amelitenda. 4 Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. 5 Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, 6 Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu, 7 Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake. 8 Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia.

 

Isaya 44:6-20 Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. 7 Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze. 8 Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine. 9 Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike. 10 Ni nani aliyejichongea mungu mmoja, au aliyesubu sanamu isiyofaa kitu? 11 Tazama, wenziwe wote watatahayari; na mafundi, hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja. 12 Mfua chuma hufanza shoka, hufanya kazi kwa makaa, huitengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake; naam, huona njaa, nguvu zake zikampungukia; asipokunywa maji huzimia. 13 Seremala hunyosha uzi; huiandika kwa kalamu ya mate; huitengeneza kwa randa, huiandika kwa bikari, huifanza kwa mfano wa mwanadamu, sawasawa na uzuri wa mwanadamu, ili ikae nyumbani. 14 Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiriza, na mwaloni, hujichagulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje, mvua ikausitawisha. 15 Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota moto; naam, huuwasha moto, akaoka mkate; naam, huufanya mungu, akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga, akaisujudia. 16 Sehemu moja huiteketeza; kwa sehemu nyingine hula nyama; huoka chakula kiokwacho, akashiba; naam, huota moto, akasema, Aha, nimeota moto, nimeona moto; 17 na kwa sehemu iliyobakia hufanya mungu, yaani, sanamu yake ya kuchonga; husujudu mbele yake akaiabudu, akaiomba, akasema, Uniokoe; maana wewe u mungu wangu. 18 Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu. 19 Wala hapana atiaye moyoni, wala hapana maarifa, wala fahamu kusema, Nimeteketeza sehemu motoni, naam, pia nimeoka mkate juu ya makaa yake; nimeoka nyama nikaila; nami, je! Kilichobaki nikifanye kuwa chukizo? Je! Nisujudie shina la mti? 20 Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?

 

Isaya 46:5-9 Mtanifananisha na nani, na kunisawazisha naye, na kunilinganisha naye, ili tuwe sawasawa? 6 Watu wamwagao dhahabu kutoka mfukoni, na kupima fedha katika mizani, huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu. 7 Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa na taabu yake. 8 Kumbukeni haya, mkajionyeshe kuwa waume; jifahamisheni haya, ninyi mkosao; 9 kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;

Kushirikiana na waabudu sanamu

Mungu ametuamuru tusishirikiane na ndugu yeyote anayeishi maisha yaliyo kinyume na torati hii ya Mungu, na kwa kweli tumekatazwa hata kula naye mtu wa namna hii.

Zaburi 26:5 Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu

 

2Mambo ya Nyakati 19:2 Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao Bwana? Kwa ajili ya hayo ghadhabu i juu yako itokayo kwa Bwana.

 

1Wakoritho 5:9-11 Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. 10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. 11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.

 

1Wakorintho 10:19-20 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? 20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.

 

2Wakorintho 6:14-18 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,

 

2Wathesaloniake 3:6 Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.  

 

2Wathesalonike 3:14 Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari;

Hukumu kwa waabudu sanamu na taifa linaloabudu sanamu

Hukumu waliyofanyiwa waabudu sanamu ilikuwa ni kubwa sana. Mtu anayekutwa na akiabudu sanamu alihukumiwa kuuawa kwa kupigwa mawe.

Kumbukumbu la Torati 27:15  Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.

 

Kumbukumbu la Torati 17:2-5 Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, 3 naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi; 4 ukiambiwa hayo nawe umeyasikia, ndipo utafute kwa bidii, na tazama, ikiwa ni kweli lina hakika jambo lile, kuwa yafanywa machukizo kama hayo katika Israeli; 5 ndipo umchukue nje malangoni kwako, yule mtu mume, au yule mwanamke, aliyefanya jambo lile ovu; ukawapige kwa mawe, wafe.

 

Kutoka 22:20 Mtu atakayemchinjia sadaka mungu ye yote, isipokuwa ni yeye Bwana peke yake, na angamizwe kabisa.

 

Hukumu kwa taifa lililomuacha Bwana na kuabudu sanamu ilikuwa ni kupelekwa utumwani na kupatilizwa nap engine hata kufutwa kwa kizazi cha taifa hilo. Mataifa yele yalikuwa yanakazia tendo la kuivunja amri hii ya pili ya Mungu watafanywa na Mungu waende utumwani hadi watakapotubu na kukubali kulifuata agano ambalo Mungu aliliweka na wao.

 

Amosi 5:25-27 Je! Mliniletea dhabihu na sadaka jangwani muda wa miaka arobaini, enyi nyumba ya Israeli? 26 Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyizia wenyewe. 27 Kwa sababu hiyo nitawahamisha, hali ya kufungwa, mwende mbali kupita Dameski, asema Bwana, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi.

 

Kumbukumbu la Torati 29:16-18 (kwani mwajua mlivyoketi nchi ya Misri, na tulivyo kuja katikati ya mataifa hayo mliyopita katikati yao; 17 nanyi mliona machukizo yao, na sanamu zao, miti na mawe, fedha na dhahabu, zilizokuwako kwao;) 18 asiwe mtu katikati yenu, mume wala mke, wala jamaa, wala kabila, ageukaye moyo wake leo amwache Bwana, Mungu wetu, kwenda kuitumikia miungu ya mataifa hayo; lisiwe katikati yenu shina lizaalo uchungu na pakanga;

 

Waamuzi 2:1-5 Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi; 2 nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani? 3 Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu. 4 Ikawa, hapo huyo malaika wa Bwana alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia. 5 Nao wakaliita jina la mahali pale Bokimu; nao wakamchinjia Bwana sadaka huko.

 

Waamuzi 2:11-15  Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali. 12 Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika. 13 Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. 14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao. 15 Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.

 

Waamuzi 8:33-35 Kisha ikawa, mara alipokufa Gideoni, wana wa Israeli wakakengeuka tena, wakawaandama Mabaali kwa ukahaba, wakamfanya Baal-berithi kuwa ni mungu wao. 34 Kwani wana wa Israeli hawakumkumbuka Bwana, Mungu wao, ambaye ndiye aliyewaokoa na mikono ya adui zao wote pande zote; 35 wala hawakuifanyia mema nyumba ya Yerubaali, yaani Gideoni, kwa kuyafuata hayo mema yote aliyowafanyia Israeli.

Wajibu kwa kuitii Torati na Sheria za Mungu

Kuwa na uongozi dhaifu au kutokuwa na uongozi kabisa sio sababu ya kuwafanya watu wazivunje amri za Mungu, kana walivyofanya watu wengi katika kipindi cha Waamuzi wakati kulipokuwa hakuna mfalme wa kuliongoza Taifa.

Waamuzi 17:1-6 Wakati huo alikuwako mtu mmoja wa nchi ya vilima ya Efraimu, ambaye jina lake alikuwa akiitwa Mika. 2 Naye akamwambia mama yake, Hizo fedha elfu na mia moja ulizonyang'anywa, ambazo uliweka kiapo kwa ajili yake na kusema masikioni mwangu, tazama, ninazo mimi hizo fedha; ni mimi niliyezitwaa. Mama yake akasema, mwanangu na abarikiwe na Bwana. 3 Basi akamrudishia mama yake hizo fedha elfu na mia moja. Mama yake akasema, Mimi naziweka fedha hizi kabisa ziwe wakfu kwa Bwana, zitoke mkononi mwangu kwa ajili ya mwanangu, ili kufanya sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu; basi kwa hiyo nakurudishia wewe. 4 Basi hapo alipomrudishia mama yake hizo fedha, mama yake akatwaa fedha mia mbili, akampa fundi mwenye kusubu fedha, naye akafanya sanamu ya kuchonga kwazo, na sanamu ya kusubu; ambazo zilikuwa ndani ya nyumba ya Mika. 5 Basi mtu huyo Mika alikuwa na nyumba ya miungu, naye akafanya naivera, na kinyago, akamweka wakfu mmoja miongoni mwa wanawe, akawa kuhani wake. 6 Siku hizo hapakuwa na mfalme katika israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe.

 

Hata Mfalme Sulemani hakuweza kulishinda jaribu hili la kuabudu sanamu. Anguko lake la kuabudu sanamu lilianzia pale alipojichanganya na hatimaye kuzolewa na tama yake ya kuwapenda na kuwa na wake wengi waliotoka kwenye dini mbali mbali zinazofuata miungu mingi badala ya Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli. Ndipo alipoanza kuabudu miungu mingi isiyo na hesabu na akaanza kuitengenezea sanamu za kuchonga na kuzijengea vihekalu kwenye mahala pa juu. Hatimaye Mungu aliligawanya taifa la Israeli pande mbili ikiwa ni adhabu kwa matendo haya aliyoyafanya Sulamani, na limebakia katika hali hii ya ngawanyiko hadi leo.

1Wafalme 11:1-13 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. 3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. 4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. 5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. 6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. 7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. 8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. 9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili, 10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana. 11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako. 12 Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako. 13 Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua.

Kuendelea na moyo mgumu na kushindwa kumrudia Mungu kutoka kwenye matendo yao maovu wayafanyayo machoni pa Bwana kutawapelekea hukumu ya kukomeshwa na kutomezwa kabisa usoni pa nchi. Na hii ndiyo iliyomtokea kabisa Mfalme Yeroboamu ambaye aliibadiki Sikukuu ya Vibanda na kuifanya iadhimishwe mwezi wan ane na kuwachagua watu wowote tu waifanye kazi na huduma ya kikuhani, watu ambao hawakutokana na uzao wa kabila la Lawi.

1Wafalme 13:33 Baada ya hayo Yeroboamu hakuiacha njia yake mbovu, lakini akafanya tena makuhani wa mahali pa juu, wa watu wo wote.

1Wafalme 13:34 Kila aliyetaka akamfanya wakfu, ili wawepo makuhani wa mahali pa juu. Jambo hilo likawa dhambi kwa nyumba ya Yeroboamu, hata kuiharibu, na kuifuta usoni pa nchi.

 

Kuwa wachache kiidadi sio sababu ya kuwafanya muanze kuyafanya yale ambayo yanafanywa na kuaminiwa na wengi wakati tunapokuwa tayari tumejaaliwa kujua ukweli na kujua kuwa wao wanakosea. Hatupaswi kuwafuata walio kundi kubwa au waliowengi na kujiunga kwenye uovu. Haijalishi kuwa sisi tu wachache kiasi gani, Mungu yuko upande wetu pamoja nasi, kama alivyokuwa na nabii Eliya wakati aliposimama kinyume na wale manabii 450 wa Baali (1Fal. 18:22).

1Wafalme 18:20-40 Basi, Ahabu akapeleka watu kwa wana wa Israeli wote, akawakusanya manabii pamoja katika mlima wa Karmeli. 21 Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno. 22 Ndipo Eliya akawaambia watu, Mimi nimesalia, mimi peke yangu, nabii wa Bwana; lakini manabii wa Baali ni watu mia nne na hamsini. 23 Kwa hiyo na watutolee ng'ombe wawili; wao na wajichagulie ng'ombe mmoja, wamkate-kate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza huyo ng'ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto chini. 24 Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la Bwana; na Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu. Watu wote wakajibu wakasema, Maneno haya ni mazuri. 25 Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. 26 Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya. 27 Ikawa, wakati wa adhuhuri, Eliya akawafanyia dhihaka, akasema, Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo; labda anazungumza, au ana shughuli, au anasafiri, au labda amelala, sharti aamshwe. 28 Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika. 29 Ikawa, wakati wa adhuhuri ulipopita, walitabiri hata wakati wa kutoa dhabihu ya jioni; lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu, wala aliyeangalia. 30 Kisha Eliya akawaambia watu wote, Nikaribieni mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhabahu ya Bwana iliyovunjika. 31 Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo, aliyejiliwa na neno la Bwana na kuambiwa, Jina lako litakuwa Israeli. 32 Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu. 33 Kisha akazipanga zile kuni, akamkata yule ng'ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni. 34 Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili. Akasema, Fanyeni mara ya tatu. Wakafanya mara ya tatu. 35 Yale maji yakaizunguka madhabahu; akaujaza mfereji maji. 36 Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. 37 Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie. 38 Ndipo moto wa Bwana ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. 39 Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu. 40 Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko.

Wale wote wanaoabudu sanamu za kuchonga na kujisifu au kujivunia sanamu wataaibika siku moja, kwa kuwa kuna Mungu mmoja tu na ambaye ndiye Mungu wa miungu mingine yote na nia anayeabudiwa na miungu mingine yote (sawa na inavyosema Zaburi 135:1-21).

 

Zaburi 97:1-12 Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. 2 Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. 3 Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani. 4 Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema, 5 Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake, Lafurahi kama mtu aliye hodari Kwenda mbio katika njia yake. 6 Kutoka kwake lautoka mwisho wa mbingu, Na kuzunguka kwake hata miisho yake, Wala kwa hari yake Hakuna kitu kilichositirika. 7 Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima. 8 Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru. 9 Kicho cha Bwana ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za Bwana ni kweli, Zina haki kabisa. 10 Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali. 11 Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu nyingi. 12 Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.

Lengo au mpango mkuu la Mungu

Kusudi na mpango mkuu wa Mungu ni yeye kuwa ni yote katika yote, na kwa hiyo sisi sote tutafanyika kuwa ni miungu midogo midogo au elohim tukiwa chini ya mamlaka na himaya yake, tukiwa kama malaika wa Yahova.

Zekaria 12:8 Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.

 

Waefeso 4:4  Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote

 

1Wakorintho 15:28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

Hitimisho

Amri za Mungu ziliwekwa tangu mwanzo wa kuumbwa kwa hii dunia. Amri hii ya pili inahusiana sana utaratibu wa kuabudu chini ya amri ya kwanza na inazuia kufanyika kwa tendo lingine lolote la kujiingiza kwenye utaratibu wa ibada za miungu mingine. Kwa ajili hii, amri ya tatu inaifuatia ile ya pili na inakataza kulitumia jina la Mungu kwa matumizi mengine yasiyosahihi, ili kwamba kusiweko na namna nyingine yoyote mbaya ya kiibada itakayofanyika kwa kulishirikisha au kulifanyia mbadala wa kumuabudu Mungu wa Pekee na wa Kweli. Amri ya nne inahusika na kuitaja siku ambayo imewekwa ya kumuabudu Mungu huyu wa Pekee na wa Kweli, na inafungamanisha kwenye kalenda inayoiweka pasipo mabadiliko siku hii ya kuabudu na kuifanya siku za Sabato ziwe ndizo siku maalumu za kumfanyia ibada. Kwa hiyo, amri ya tatu na ya nne inaipa mashiko amri hii ya pili kulikataza jina la Mungu lisitumiwe kwenye utaratibu wowote mwingine na kwenye mfumo wa lakenda nyingine yoyote ihusuyo mambo ya ibada. Mfumo au imani iliyoko leo ya kuabudu mungu Jua, na ambao unatumika kwa kufananisha na ibada ya Mungu wa Pekee na wa Kweli kwa kisingizio cha jina la Yesu Kristo linatokana na mwendlezo wa imani na dini hii hii ya kipuuzi ya waabudu sanamu na ndiyo iliyoko na kushamiri hadi leo. Amri Kuu ya Kwanza ya kumpenda Bwana, Mungu wetu imefungamanishwa kwenye amri hizi nne za kwanza, ambazo zinatoa mwongozo wa jinsi ya kuabudu. Tendo la kuivunja mojawapo ya hizi, ni sawa na kuvunja nyingine zote nne zilizobakia, na tendo la kuuvunja mfumo huu wote wa ibada unatoa mwanya wa kuanzishwa kwa dini nyingine ya uwongo.

 

Atakaporudi Masihi atakomesha kila aina yoyote iliyoko ya taratibu za ibada ambazo ni za uwongo na zisizomlenga yeye, hasa zile zote zinazotokana na Imani Fumbo au za mungu Jua zinazofungamanisha imani ya Utatu pamoja na imani zake potofu na ibada zake za vinyago au sananmu.

 

 

 

q