Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[259]

 

 

 

Torati na Amri ya Sita

(Toleo La 3.0 19981009-20050810-20120804)

 

Imeandikwa: Usiue. Jarida hili linaelezea muundo mzima wa Torati au Sheria ya Mungu na jinsi inavyoendana na Amri zake, na jinsi inavyoelezewa na manabii na Agano na uhusiano wake na agizo la Usomaji wa Torati katika mwaka wa Sabato.

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hatimiliki © 1998, 1999, 2005, 2012  Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Torati na Amri ya Sita

 


Imeandikwa kwenye Kutoka 20:13 na Kumbukumbu la Torati 5:17: “Usiue”.

 

Hali ya kulinda au ulinzi wa maisha unaendelea hadi kwenye ulinzi wa mwili. Inahusika na hali ya kutilia maanani utakatifu na kujitakasa kwa mtu binafsi yake. Kama tunavyoendelea kwenye amri ya tano, ambayo inahusika na mambo ya familia na taifa, kwa hiyo ni sawa pia na ulindaji wa familia na taifa inayofungamana na amri ya sita.

 

Kuwaombolezea wafu kwa mtindo unavyofanywa na mataifa mengi hakupaswi kuwa hivyo kwenye familia za wana wa Israeli (Mambo ya Walawi 19:28). Kifo cha asili cha mtu yeyote ni tukio linqlotokea kwa mujibu wa Mpango wa Mungu, na kinamtazamo tarajiwa na tukio la ufufuo wa wafu, na Israeli watawekwa kwenye nchi yao wenyewe (soma Ezekieli. 37:1-14; Ufunuo 20:1-15).

 

Israeli wanapaswa wasiwe na doa wala kunyanzi na ngozi zao hazitakiwi zichanjwe chale au kuwekwa alama yoyote. Kwa hiyo, mtindo wa kujichora michoro na kuweka alama nyingine kwa makusudi kwenye mwili kumekatazwa. Tendo la kumruhusu mtumwa akubali kuchomwa kwa umma sikioni mwake kwa dhumuni la kuweka alama lilionekana kama ni ishara ya uduni na udhaifu.

 

Kiini au chanzo na Muundo wa Taifa

Uweza wa kuishi na kufa unamtegemea Mungu kama tulivyojionea kwenye jarida la Torati na Amri ya Tano (Na. 258) [Law and the Fifth Commandment (No. 258)].

 

Mungu ameanzisha familia kama msingi ambao Nchi inajengwa juu yake. Ameweka mamlaka ya juu sana na uweza wote hutoka kwake yeye Mungu.

Warumi 13:1-7 inasema: Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 6 Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. 7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.  

 

Mungu ametoa mamlaka yake kwa kupitia kwenye vibao vilivyoandikwa torati, ambazo alimpa Musa (Kumbukumbu la Torati 9:11). Kwa hiyo, wafalme wote wanapaswa kuwa na nakala yao wenyewe ya torati hii na waisome na kuielewa hata kabla hawajaanza kuwa wafalme.

Kumbukumbu la Torati 17:18 Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi;

 

Mungu aliwaweka wazee katika Israeli kwenye nchi yao na walipewa hekima kupitia Roho Mtakatifu, sawa na kama Musa alivyompokea na alipopewa uweza.

Hesabu 11:16-17 Kisha Bwana akamwambia Musa, Nikusanyie watu sabini, miongoni mwa wazee wa israeli, ambao wewe wawajua kuwa ndio wazee wa watu hawa, na maakida juu yao; ukawalete hata hema ya kukutania, wasimame huko pamoja nawe. 17 Nami nitashuka niseme nawe huko, nami nitatwaa sehemu ya roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao; nao watachukua mzigo wa watu hawa pamoja nawe, ili usiuchukue wewe peke yako.

 

Kwa mujibu wa Hesabu 11:26, Mungu pia aliwaweka akiba manabii wawili nje ya Maskani ya Israeli. Mungu hafanyi kitu chochote mbali ya kile alichokisema kupitia kwa watumishi wake manabii, ambao ni yeye mwenyewe ndiye aliyewachagua kutoka miongoni mwa watu wake. Na ndivyo ilivyo kwamba waamuzi au mahakimu wanatoa hukumu kwa ajili ya Bwana Mungu (2Nyakati 19:5-7).

 

Mfalme anateuliwa pia na kupewa mamlaka ya Roho ili waeeze kuwatawala Israeli (soma 1Samweli10:1-7). Viongozi au wazee wanaosimamia huduma za kiroho wa Israeli walichaguliwa kwa kupigiwa kura (Matendo 1:26). Matendo 6:3-6 inaonyesha kwamba mashemasi na wazee walichaguliwa kutoka miongoni mwa wapendwa. Viongozi wenyewe wanachaguliwa kwa kutiwa mafuta kama wafalme au waamuzi, na kwa kupigiwa kura kwa uchaguzi (soma Hosea 1:11; Luka. 14:28 na sawa na ilivyoandikwa kwenye Biblia iitwayo Companion Bible also).

Kumbukumbu la Torati 1:9-14 Nami wakati ule niliwaambia, nikasema, Siwezi mimi mwenyewe kuwachukua peke yangu. 10 Bwana, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi. 11 Bwana, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabarikia, kama alivyowaahidi. 12 Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na mateto yenu? 13 Jitwalieni watu wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya kabila zenu, nami nitawafanya wawe vichwa juu yenu. 14 Nanyi mkanijibu, mkaniambia, Jambo ulilonena ni jema la kufanya.

 

Kwa yote haya hakuna hata mzigo miongoni mwa watu, waamuzi, au wanyama, au kiumbe yeyote, au kwa msingi wa torati yenyewe (soma Kumbukumbu la Torati 22:10).

 

Torati hii ya Mungu haipaswi kufungiwa nira pamoja na sheria za mataifa, wala hazitakiwi kumwagiliwa maji ili kuzizima au kuzidiwa na sheria za kimataifa. Utaratibu wa Torati hii ya Mungu, kalenda yake na namna yake ya kumuabudu hazipaswi kufungamanishwa na mifumo yeyote ile ya mataifa wasioamini (2Wakorintho 6:14). Mfumo wa kimaongozi na kimahakama wa wana wa maagano wote ni wa mwelekeo ashirio wa wanaoiamini Torati ya Mungu.

 

Viumbe wote wanatunzwa kwenye nchi iliyoumbwa kikamilifu. Hakupaswi kuwa na machafuko kati ya viumbe wa Mungu tangia mwanzo, kama ilivyokuwa katika uumbaji wa viumbe aina ya nyumbu na wale wa damu mchanganyiko (Mambo ya Walawi 19:19); hizi zimelatazwa kwa mujibu wa sheria za Mungu. Tunatakiwa tuwe ni watu safi na watakatifu kwa ukamilifu na kuzitunza sheria takatifu. Hii pia ni kanuni moja wapo katika kulinda maisha.

 

Wala mtumishi wa Mungu asishitakiwe kwa kuzifundisha na kuzikazia sheria, na kwa kuzisimamia na kuzizimamia kwa kutochangamanisha na kazi au shughuli za kila juma. Wala kusiweko na mnyama au mwanadamu mwenye kuzuiwa kufurahia matunda mema yatokanayo na kazi zake za utumishi.

Kumbukumbu la Torati 25:4  Ng'ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa.

 

Je, hapa Mungu anaongelea habari za punda peke yake? (soma 1Wakorintho 9:9; 1Timotheo 5:18; sawa na Ayubu 38:41; Mathayo 6:26; 10:29). Vitu vyote vimetokana na sheria za Mungu, ikiwa mataifa watazitii (Mambo ya Walawi 5:5-7). Sadaka ya upatanisho na za dhambi zimefungamanishwa kwenye dhabihu bora aliyoitoa Masihi.

 

Haki inajiri kwa Watu wa Mataifa na kwa adui, na pia kwa ndugu yako (Kumbukumbu la Totari 22:1-4; Mambo ya Walawi 20:22-24).

Kutoka 23:4-5 Ukimwona ng'ombe wa adui wako, au punda wake, amepotea, sharti umrudishie mwenyewe tena. 5 Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie..

 

Kama tunavyotakiwa tuwe watakatifu sisi wenyewe, na ndvyo pia hata wale wanaoketi kati yetu wanavyotakiwa wawe watakatifu, kwa kuwa sisi sote tumefungiwa nira kwa sheria za Mungu katika Roho Mtakatifu.

2Wakorintho 6:14-18 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,

 

Imeandikwa: “Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. 18 Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana.

Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu. 34 Mgeni akaaye pamoja nawe atakuwa kama mzalia kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. (Mambo ya Walawi 19:17-18,33-34; Kutoka 22:21 RSV).

 

Amri hii ya sita sio tu kwamba inakataza tu tendo la kuua, bali ni katazo linalolinda uhai na kumfanya mtu kuwa mtakatifu kwa Bwana, kwenye sheria za Mungu aliye Hai. Uhai hauwezi kupunguzwa kiwangochake cha thamani au uzani wake wa ubora kwa kutumia udhalimu au dhuluma au kwa tendo la kuwapendelea watu. Kwa hiyo, muundo wa amri hizi unaendana na dhana ya kumshambulia au kumnyag’anya mtu na raslimali.

 

Matoleo kwa kuivunja amri ya sita

Kumbukumbu la Torati 19:1-13 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Wakati taifa la Israeli lilipoanzishwa, lilipangiliwa na kutengwa miji mitatu ya makimbilio ambayo ilitumika kwa kuikimbilia mtu yeyote aliyemuua mwenzake bila kukusudia, ili kwamba kisasi kisimfike kwa kipindi hiki na akadhuriwa na wenye hasira. Ili kusiwe na mauaji ya mtu asiye na hatia na kuimwaga damu yake. Amri hii ilipaswa itunzwe na kuangaliwa na hatimaye, miji mingine mitatu zaidi iliongezwa. Hata hivyo, kukitokea na mauaji yaliyofanywa kwa makusudi (yaani kosa la mauaji) nandipo mtu yule alitakiwa akabidhiwe kwa walalamikaji na ashitakiwe, na akikutwa na hatia hukumu yake ilikuwa ni kifo.

 

Kwa hiyo, uvunjaji wa sheria hii kwa marudio ulilindwa na Nchi iliyo kwenye moja ya miji hii ya makimbilio, ikiwa kama jambo hilo halitapewa kipindi cha matazamio kwenye mazingira ya kawaida ya kabila husika. Ni wajibu wa kila mmoja aishie kwenye Nchi kuwahakikishia ulinzi wa wakazi au wananchi wote.

 

Upotoshaji na ubadilishaji wa sheria za kibiblia uliofanywa na Yuda

Kwa hiyo, mgeni na mpitaji wanapaswa pia wapewe ulinzi huu wa kila mmoja kwenye jamii, na kupewa msaada kunapotokea hali ya hatari. Upotoshaji wa sheria za kibiblia ulitokea na kufanywa kwa kiasi kikubwa na jopo la Kiyahudi lililojulikana kama Talmud ambacho kilisimamia kwenye chimbuko au kiini cha Torati ya Mungu. Tutajionea jinsi upotoshaji uliofanywa kwa mafundisho ya marabi iliyofanywa kwa nukuu zilizochukuliwa kutoka kwenye ya Kitorati yaliyojulikana kama Maimonides’ Mishneh Thorah Murderer 4,11: inayosema:

Kwa watu wa mataifa ambao hatumo kwenye vita wala mapigano nao …kifo chao hakipaswi kisababishwe, bali imekatazwa ili kuwaokoa wanapokuwa kwenye kipindi au kiwango cha kufa, ikiwa, kwa mfano, iwapo kama mmoja wao ataangukia baharini, na iwapo kama haitawezekana kabisa kumuokoa, kwa kuwa imeandikwa ' wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako' [Mambo ya Walawi 19:16] lakini (Mmataifa) sio mwenzako"

 

Kitabu cha Soncino hakionyeshi uhusisiano wa kiuandishi na tafsiri za kibiblia kwenye maandiko yake kwa kuwa ukukaji na upotoshaji huu wa Maandiko Matakatifu usio sawa wala haki ni kiwango kinachoelezewa. Nukuu halisi zinaonekana kama ifuatavyo.

Mambo ya Walawi 19:16  Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi Bwana.

 

Andiko hili (hususan aya ya 16b) linaeleweka kama kushindwa kutoa usaidizi wa kuokoa maisha. Kitabu maarufu cha fasiri cha Stone’s Chumash kinakubaliana na maana hii na kinasema: “Iwapo kama maisha ya mtu yakiwa hatarini unalazimika kufanya jitihada zako zote ili kumuokoa...”Kwenye mapokeo yao, Wayahudi kipindi cha Kristo kwa mapokeo walitafsiriwa jambo hili wakimaanisha kwamba neno jirani lilimaanisha Myahudi, na hili lilipelekea matendo ya baadae ya Wayahudi kuwa kama ifuatavyo:

Kuinajisi Sabato kunafanika hata ikiwa mtu anafanya kazi ya kuokoa maisha ya Myahudi mwenzao italazimika kuhitajika kufanyika. Tatizo la kuyaokoa maisha ya Mmataifa siku ya Sabato hayakuelezewa kwenye kanuni na imani ya hawa Talmud wala haikuelezewa kuwa ni kitu muhimu, kwa kuwa lilikuwa kwa sababu yeyote ile limekatazwa kufanywa hata kwa siku za wakati wa katikati ya juma (ndivyo walivyoamini.).

 

Tafsiri hii kuhusu watu wa Mataifa huenda ni marejeo mabaya zaidi kuliko yote kupotosha kile ambacho Maandiko Matakatifu yalikikusudua. Na hii ni sababu iliyomfanya Kristo atumie mfano wa Msamaria Mwema, kwa jinsi mtazamo huu ulivyoingia na kupata nafasi kwenye imani ya Kiyahudi na hata kipindi cha Hekaluni katika karne ya kwanza ya zama zetu za sasa.

 

Kile kinachoitwa mapokeo ya Sheria Zinazofundishwa pasipo maandiko yznzyodaiwa kuwa yalifasiriwa au kuwa na ushawishi na Masihi ambayo yalitumiwa na vikundi vyote viwili yaani vya Watalmud wa Yerusalemu na Wakibabelonia ambayo waliyachukua, na kwa kweli yalikuwa ni nakala zilizoandikwa za tafsiri. Ziliandikwa kwa lengo la kusaidia kuzipa mashiko ya kuthibitisha mapokeo yanayoanzisha yaliyoanzishwa katika kipindi zama cha mapema ya miaka ya 160 KK. Hayakuwepo wala kueleweka kabisa kwenye historia ya Israeli, na wala hayakutokana na Musa, kama Biblia yenyewe inavyotuonyesha. Israeli mara nyingi wamesahau hata sheria zilizoandikwa, na kuziacha kabisa zile zinazojulikana kama mapokeo ya Kitamaduni ya sheria. Mapokeo haya kwa sehemu kubwa yalikuwa yanachanganya na kupingana na mengi yao yalikuwa ni ya kupotosha na ya uwongo yakilinganishwa na Maandiko Matakatifu.

Luka 10:25-37 inasema: Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? 26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? 27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. 28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. 29 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? 30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang'anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. 31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando. 32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando. 33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, 34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. 35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa. 36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang'anyi? 37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.

 

Hakuna mahali pengine popote ambapo mapokeo haya ya Kiyahudi yanapotosha sheria asilia zaidi ya mfumo huu dhanifu wa jinsi ya kuelewa maagizo ya kulinda uhai au maisha na kumtendea mabaya mtu asiye na makosa.

 

Kumuonea mtu asiye na hatia

Kumhukumu kwa maonevu mtu asiye na hatia kumekatazwa na Biblia na hakuna mtu anayepaswa kuuawa au kuadhibiwa kwa kosa ambalo halikushuhudiwa na mashahidi watu wawili au watatu. Ni kwa mujibu wa Biblia kwa namna yoyote ile waliyoifasiri wenyewe, ndipo waliitumia kuiwekwa sheria ijulikanayo kama Mishna ambayo inaendana kinyume kabisa na Mgawanyo wa Nne : Mari ya Kuvunja baraza la Sanhedrin 4:1 E(2) (Fourth Division: The Order of Damages Sanhedrin 4:1 E(2)] inayosema:.

Kwa mabo yahusuyo mali walianza [mabishano] kwa ajili ya masuala yahusuyo ama kuachiliwa ama kusamehewa au kwa ajili ya kutiwa hatiani, wakati kwenye matukio mengi makubwa walianzia tu na masuala ya msamaha na sio ya kutia hatiani au tuhuma

(sawa na anavyosema Jacob Neusner, kwenye kitabu chake cha Tafsiri Mpya ya Mishna, iliyochapishwa kwenye Chuo Kikuu cha Yale,huko New Heaven na London, mwaka 1988, ukurasa wa 589 (The Mishnah A New Translation, Yale University Press, New Haven and London, 1988, p. 589)

 

Katika mambo yote, tendo la kumuonea au kumdhulumu mtu asiye na hatia linahitaji kwamba mashitaka yafanywe, kisha yasikike na kutolewa kwa ushuhuda wa mashahidi wawili. Kwa hiyo, mshitakiwa anapaswa apewe muda muafaka wa kujitetea mahakamani ya hakimu aliyeteuliwa kusikiliza, ambaye hatayumbishwa kwa namna yoyote ile katika kutoa hukumu na kuwa hatajaribiwa kuonyesha upendeleo au kumuogopa mtu. Katika kipindi cha huduma za Hekalu, mashitaka yanayohusu umiliki wa malia yalisikilizwa na kundi la mahakimu watatu na kila mashitaka makubwa yalisikilizwa na mahakimu wasiopungua ishirini na tatu wa baraza la Sanhedrin, kama inavyoonyesha nakala ya Mishna (kwenye sehemu yake ya D (1)). Kwa hiyo, kila maamuzi yaliyohusiana na mambo ya mali na raslimali yaliwasilishwa mahakamani, kama yatawasilishwa kwenye usikilizaji wa mwanzo au mahakama ya mwanzo. Mashitaka yote makubwa yalipaswa kusikilizwa na wasikilizaji wasiopungua ishirini na tatu kutoka kwenye baraza la Sanhedrin lenyewe, kwa kuwa inawapelekea kwenye hukumu ya kifo. Kipindi cha kukata rufaa kiliruhusiwa kwa suala la mashahidi na ushahidi pia kutokana na vipindi hivi vya mwanzo (Mishnah, hiyohiyo inasema pia).

 

Kwa sababu hii madai ya uwongo ya kila kinachojulikana kama sheria za Nuhu, ambazo dini ya Kiyahudi inajaribu kuanzisha kutoka kwenye Talmud, yanayoruhusu mtu kutiwa hatiani kwa ushahidi wa hata mtu mmoja tu, ambao ni kinyume kabisa na haki na Sheria za Mungu. Dhana hii na utekelezaji wake vina madhara sana, sii ya kibiblia na hayana haki ndani yake. Dhana hii hii potofu na isiyozingatia haki inapingana na ile iliyo kwenye mfumo wa kisheria wan chi za Ulaya, ambao unamtia mtu hatiani pale anapokutwa na na kuthibitishwa ana hatia. Orodha ya watuhumiwa inaweza kukusanywa na kufungwa bila kushitakiwa, au uthibitisho, au kuzingatia namna yoyote ya haki. Nchi ya uingereza imeiga na kuchukua uovu huu na kuuingiza kwenye utaratibu unaokazia sheria zake bila manung’uniko. Matokeo yake na marejesho ya Vita ya Kiraia ya Waingereza na mara nyingi wamepotea bila kuwa na watetezi mtazamo na fikra zao za kipuuzi. Watu wanaohusika na masuala ya mafaili wanaweza kuwakomoa adui zao, na kuathiri uwepo wa haki. Kwa sababu hii ndipo mauaji dhuluma viliruhusiwa, na Dola Takatifu ya Rumi ikaanguka, na Mapinduzi au mageuzi yakaigeuza Ulaya kwenye miaka ya 1850 (soma kitabu cha Malachi Martin, kiitwaco Mafundisho ya Kuanguka kwa Kanisa la Rumi. Kilichoandikwa na Secker na Warburgh, huko Londoan mwaka 1982, kurasa za 250-256, nk. (The Decline and Fall of the Roman Church, Secker and Warburg, London, 1982, pp. 250-256, et seq.). kwa ajili hii, Ukristo umezigeuza sana sheria au kwa kiwango kikubwa sana kuliko kile cha marabi wa kiyahudi. Sheria za Mungu hazikutiliwa mkazo kabisa kwa nia na uaminifu, isipokuwa tu katika kipindi cha Musa na cha Daudi na kwa kipindi cha marejesho mafupi yaliyotokea mara chache. Imani ya Kikristo haijawahi kabisa hata kujaribu tu, bali iliachilia mali zijaribiwe tu.

 

Ni kwa jinsi hiyohiyo, wakati Muhammed alipojaribu kufundisha tena Torati ya Mungu, na Mahalifa wake Wanne Wenye haki na Waliolindwa na kuheshimika sana, walipojaribu kuzifundisha, zilipuuzwa na kuharibiwa. Uislamu ulionekana kudumu kwa kitambo tu, sawa kama ulivyodumu kwa kipindi kifupi Utawala wa Daudi. Imani asilia ya Kiislamu iliharibiwa na mafundisho yaliyojulikana kama Hadithi, kwa mtindo ule-ule ambao Mabaraza ya kidini yalivyoiharibu imani asilia ya Kikristo na mapokeao, na Talmud zilivyoiharibu Torati na mahala pake kuendeleza imani au itikadi ya Kiyahudi. “Babeli” imetawala kwa kipindi cha maelfu ya miaka, na ni dini ya mungu wa dunia hii, atakayetawala hadi marejesho yanayokuja.

 

Wajibu katika kusababisha kuishi

Kwenye dhana au mafundisho ya sheria ya udhibiti wa maisha au uhai, sisi pia tunamafundisho yasemayo kuendeleza au kutoa uhai au kusababisha kuishi.

Kumbukumbu la Torati 32:39 Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,

Mungu ni mmoja na hana mungu mwingine mdogo wa kuambatana naye, bali ni yeye tu peke yake ndoye aliye Mungu naye ndiye atoaye uzima na kuutwa uhai. Mkono wake unashikilia hukumu zote. Kwahiyo, kitendo cha kutwa uhai wa kiumbe kutokana na kushindwa au kuanguka kwake kunachukuliwa kama kuyatoa maisha kwa ufufuko (soma majarida ya Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya 1 Bustani ya Edeni (Na. 246) na  Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya 2 Kizazi cha Adamu (Na. 248) na Ufufuo wa Wafu (Na. 143) [Doctrine of Original Sin Part 1 The Garden of Eden (No. 246) and Doctrine of Original Sin Part 2 The Generations of Adam (No. 248) and The Resurrection if the Dead (No. 143)]. Kwa hiyo Mungu ndiye mlengwa kwenye sheria zake na anafanya ukombozi katika matendo yote aliyoyafanya, au aliyoyaamuru kuwepo kwenye mchakato wa uumbaji wake.

1Samweli 2:6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.

(pia soma Isaya 43:13)

 

Yahova-elohim alimpulizia Adamu pumzi ya uzima kwenye mianzi ya pua zake (Mwanzo 2:7). Kwa hiyo hwa huyo elohim pia tunapokea pumzi za Roho Mtakatifu (soma Yohana 20:22-23).

 

 Mungu huwahukumu watu kwa ahdhabu ya kifo kwa kufanya kwao dhambi na uvunjaji wao amri zake. Na ndipo tunapojionea kwamba uvunjaji wa amri hii ya sita kunapelekea mtu kuhukumiwa kifo, jambo ambalo linaonekana kutokea kwenye mifano kadhaa ya kila inapotokea hivyo kwenye kila uvunjifu wa amri hizi za Mungu unapotokea. Hukumu kubwa itolewayo kwa makosa ya uvunjaji wa mri hizi ni kifo, tangia uvunjifu wa amri ya kwanza hadi kwa ile ya mwisho na ya kumi (Kutoa 22:22-24; Kumbukumbu la Torati 24:14-17). Amri hizi zimewekwa msingi wake kwenye ukombozi na marejesho, bali hukumu kwa ajili ya uvunjaji unayofanywa kwa kurudiwa na kukaidi kuzitii, ahdabu yake ni kifo kwa namna yoyote ile.

 

Taifa linawajibika kumtunza na kuangalia ustawi na uzima wa kila raia wake aliyezaliwa kwenye nchi yao, sambamba na wageni na wapitaji wapitao nchini mwao.

Mambo ya Walawi 19:9-10  Na mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala usiyakusanye masazo ya mavuno yako; 10 wala usiyakusanye masazo ya mizabibu yako, wala usiyaokote matunda ya mizabibu yako yaliyopukutika; uyaache kwa ajili ya maskini na mgeni; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Aheri hizi pia zinamlinda mlemavu dhidi ya matendo ya kudhalilishwa na dhidi ya vitendo vyote viovu ambavyo anaweza kufanyiwa vikiwemo vya kudhulumiwa.

Mambo ya Walawi 19:14  Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi Bwana.

 

Ulindaji wa maisha na familia

Mambo ya Walawi 25:35-43 Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri. 36 Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe. 37 Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida. 38 Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu. 39 Tena kwamba nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimtumikishe mfano wa mtumwa; 40 kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hata mwaka wa yubile; 41 ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake. 42 Kwa kuwa hao ni watumishi wangu, niliowaleta watoke nchi ya Misri; wasiuzwe mfano wa watumwa. 43 Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako

 

Utozaji riba ni tendo linalopigwa vita na ni la haramu kwa kila imani ya kidini, kwa kuwa kwa kutenda hivyo tunafanya tendo baya la kudhulumiana. Sisi sote tumenunuliwa kwa gharama na thamani yetu ni moja, hivyo basi, tunapaswa sisi sote tumtukuze Mungu kwa kutulinda kila mmoja wetu (1Wakorintho 6:20; sawa na Kutoka 22:21), kwa kuwa Mungu ni elohe wa elohim, au Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana (adonai wa adonimu) (Kumbukumbu la Torati 10:17-19, kama ilivyoandikwa kwenye Biblia iitwayo Companion Bible).

 

Taifa na mwanadamu wanapaswa kutunzwa uzima na uhai wao kwa uhuru chini ya sheria za haki.

Kutoka 21:1-6  Basi hukumu utakazoziweka mbele ya watu ni hizi 2 Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure. 3 Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye. 4 Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake. 5 Lakini huyo mtumwa akisema waziwazi, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; sitaki mimi kutoka niwe huru; 6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote.

Mfuniko huu wa tundu ni alama ya ashirio la aibu. Ikifika miaka saba mtumwa aatakiwa aachiliwe huru, na bwana wake anatakiwa amwachilie huru na kumruhusu aondoke na mke wake pia. Haijalishi ni kwa kiasi gani alimtumikisha na kumdhulumu mtumwa wake huyu, bali anatakiwa ampe ujira wake anaostahili kuondoka nao (Kumbukumbu la Torati 15:12-15).

 

Itawezekanaje ujihesabu umemtendea haki kwa kumwachilia huru mtumwa wa kiume huku ukiendelea kuwashikilia wattoto wake na mke wake? Hii ni mari inayohitaji kutenda kwa haki na marejesho yaliyo na haki. Jambo linalotakiwa kufanywa hapa ni kwamba hali ya utumshi kwenye maisha haya ya utumwa ni ya lazima, na bwana wake hawezi kuadhibiwa kwa kukosa au kufanya kwake ukarimu uhusuo zawadi zake alizotoa hapo mwanzo, iwapo kama alikuwa kwenye kipindi hiki cha utumishi wake. Sheria hizi zinaweka kikomo, lakini ni kwa mtazamo wa jumla kwenye karne hii. Mtu kuwa mjakazi na utumwa vilikuwa ni kawaida hadi kwenye karne ya kumi na tisa.

 

Sheria inafanya kazi kwa watu wote wanaishi kwenye nyumba na kwa taifa, na wajibu ni wa watawala na wamilikaji wa mali katika kuwapa haki na mahitaji yanayohitajika kwa watu wote wanaishi kwenye maeneo yao.

Kutoka 23:10-11 Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake; 11 lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni.

Kwa hiyo, tujiepushe na matendo ya mauaji ya makusudi au kuwanyima chakula katika ardhi yetu yote (soma Mambo ya Walawi 19:9-10).

 

Wajibu wetu ni kuwatunza hai watu wote waishio kwenye jamii yetu, na kwenye masuala yahusuyo ushawishi wa kila mmoja. Agizo la kumpenda jirani kama nafsi ni amri inayoendelea kwa watu wote walio kwenye maeneo yetu yanayotuhusu na tunayoishi (soma fundisho la mfano wa Msamaria Mwema  katika Luka 10:30-37).

 

Wajibu wa kuwasaidia majirani zetu unatakiwa uendelee hadi kwamba hali yetu ya kudharau ichukuliwe kama ni tendo la kumsaidia masikini.

Kumbukumbu la Torati 24:19-22 Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili Bwana, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako. 20 Utakapochuma matunda ya mizeituni yako, usirudi kuchuma mara ya pili; yaliyobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane. 21 Uchumapo zabibu katika shamba lako la mizabibu, usichume mara ya pili; zilizobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane. 22 Nawe kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.

 

Linganisha pia na hadithi iliyo kwenye kitabu cha Ruthu sura ya 2.

 

Mungu aliwalinda Israeli kipindi chao chote cha kutangatanga kwao jangwani na akawalinda na kuwatunza hai ili wawe mfano wetu sisi. Musa anaelezea mzunguko wa kutangatanga kwao Israeli kwenye Kumbukumbu la Torati 1:1-46. Mungu anawahakikishia kwamba wote watapewa vitu vingi kwenye makao yao na anawabarikia sawa na vile watakavyokuwa watii kwake wakiwa kama taifa. Mifugo na masazo yote vilichukuliwa, isipokuwa pale tu ambapo Mungu aliwapa amri ya haraka dhidi ya matendo yele (Kumbukumbu la Torati 2:1-37). Watu hawakutakiwa kuogopa, kwa kuwa maadui zao wangeshindwa na kuangamizwa kabisa (Kumbukumbu la Torati 3).

 

Israeli wote waliatakiwa makabila yote yaliyokuwa kwenye milki yao yote na wachukue urithi wao. Hakuna kabila lililotakiwa lijitenge na kubadia nyuma bila kutoa msaada kwa mauaji yoyote ya haki na yaliyoamriwa na Mungu na yaliyofanyika kwa amri na maagizo yake, na yenye lengo la kulisimamisha taifa la Israeli. Hakuna mtu aliyekataa kumsaidia mwenzake kwenye makabila yao na akabakia kuwa hai, na hakuna mtu aliyefanya matendo ya dhuluma au udanganyifu au kumkatisha tama na kumchanganya mwenzake. Hakuna mtu aliyedhulumu maisha ya mwingine kwa kumtoza riba au kumdhulumu kwa namna yoyote ile.

 

Haki ya kuishi nay a kuua ilikuwa ni ya Mungu

Mungu ndiye aliweka uweza na mamlaka yote. Mahakimu wa mahakama wanashikilia upanga kwa mapenzi ya Mungu (soma Warumi 13:1-7).

Tito 3:1-3 Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; 2 wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. 3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.

 

Tunalazimika kulipa kodi na kuwatiti wale wote ambao Mungu amewainua na kuwapa mamlaka na kwa wale ambao wanastahili kuogopwa na kuheshimiwa. Taifa kwa namna yoyote ile lina haki ya kulinda maisha dhidi ya dhuluma inayofanyika kwa sheria zisizo na haki (soma Kutoka 11:1-10).

 

Kifo ni mfano, na damu inatumika kuonyesha ujio wa Masihi, ambaye kwa damu yake iliyomwagika iliwafanya watu wote wawe hai na wazima. Mfumo wa utoaji wa dhabihu ulianzishwa ili kuonyesha ashirio la kuanzishwa kwa mfumo wote kwa wanaomtii Mungu. Kama taifa la Israeli lilivyotunzwa na kubakia hai na salama na hatimaye likakombolewa kutoka Misri kwa kupitia dhabihu ya damu ya Mwanakondoo wa Pasaka, na ndivyo kwa jinsi hiyohiyo, ulimwengu umebaki salama kwa ajili ya dhabihu aliyoitoa Masihi. Dhabihu hii sio ile anayoitaka Mungu katika kutimiliza msamaha wake kwa waitoao, bali ni zaidi sana kwamba ni jaribio la utashi wa sehemu ya mambo wanayotakiwa kuwanayo watoto wake ambao wanapaswa kuyatoa maisha yao kwa kuhudumiana na kutumikiana kila mmoja na mwingine.

Kutoka 29:11-12 Kisha utamchinja huyo ng'ombe mbele ya Bwana, mlangoni pa hema ya kukutania. 12 Kisha twaa baadhi ya damu ya ng'ombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu.

 

Masihi aliiingia Patakatifu pa Patakatifu mara moja tu na kwa ajili ya wote akiwa na damu yake mwenyewe. Kwa hiyo alitufanyia njia sisi sote ya kuingia na kufanywa kuwa wana wa Mungu kwa nguvu ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, tukiwa ni warithi pamoja na Kristo (soma Warumi 1:4; Waebrania 9:12 na sehemu nyingi nyingine). Maskani ilikuwa ni mfano na uwakilishi wa ile iliyoko mbinguni. Hekalu lilikuwa ni ishara iliyotuelekea sisi ambao ni Hekalu la kiroho, ambalo ndivyo tulivyo leo (1Wakorintho 3:16-17).

 

Israeli walitembea jangwani kwa kipindi cha miaka arobaini, na wo wote miongoni mwao ambao hawakuwa tayari kupenda kuirithi ahadi yake walikufa jangwani. Ni Kalebu na Yoshua tu ndio walifanikiwa kufika hadi mwisho. Ukweli huu unatuonyesha wale Israeli ambao hawakuweza kuifikilia ile ahadi makabila walikula mana kwa kipindi hiki chote, na walikunywa kutoka kwenye mwamba wa kiroho ambao ulikuwa ni Kristo. Aliwatokea akiwa kama Amiri wa Jeshi la Bwana ili kuwaimarisha mioyo yao katika imani na tumaini la kuiteka na kuimiliki nchi ya ahadi, na aliwatokea huko Yeriko baada ya tohara yao waliyoifanywa huko Gilgali.

 

Jingo la Hekalu lilijengwa mwishoni hadi pale Masihi na hatimaye lile la kujengwa litoe nafasi kwa lile la kiroho. Kanisa lote lililo kwenye kipindi cha kupita jangwani kwa kipindi cha zaidi ya yubile arobaini, halina dhabihu nyingine zaidi ya ile ya wateule. Wale 144,000 walikuwa ni dhabihu ya kutolewa siku za Sabato, Mwandamo wa Mwezi Mpya na Sikukuu Takatifu zilizoamriwa. Sadaka za kila siku ni ashirio la wale makutano makubwa, na majira ya usiku unaofuatiwa kabla ya kupambazuka, jioni kabla ya asubuhi. Na ndiyo maana kuna dhabihu moja tu kwenye Hekalu aliloonyeshwa nabii Ezekieli, kwa kuwa sehemu kubwa ya mavuno yamekwisha kufa tayari, bali ni kwa ufufuo wa kwanza wa wafu tu ambao watafufuliwa. Kuna mavuno mengi zaidi yanakuja (Ufunuo 20:4-15). Sadaka ya jioni imeishaanzjshwa na kujulikana tayari. Kadhalika na dhabihu ya jioni imekwisha anzishwa na kutolewa tayari kama makutano makuu ya ufufuo wa kwanza (Ufunuo 7:9 nk). Kwa hiyo, dhabihu ya asubuhi ambayo pia ni ya mapambazuko ya siku yaliyo chini yake yeye Nyota ya Alfajiri, ni moja pekee kati ya mbili ya dhabihu hizi za kila siku zinazoendelea kwenye utaratibu wote wa kipindi cha milenia (soma Ezekieli 46:13-15). Usiku mrefu umeishapita tayari. Na hii ndiyo sababu inayofanya kusiweko na sababu ya kutoa dhabihu na kutoruhusiwa kufanya hivyo katka kipindi hiki chote cha usiku mrefu cha yubile ya arobaini ya kutangatanga jangwani, kwa kuwa mchakato wa kuvuno ni endelevu na wote ni mawe yaliyo hai ya Hekalu katika kipindi kile.

Ezekieli 46:13-15 Nawe utatengeneza mwana-kondoo wa mwaka wa kwanza, mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana kila siku; kila siku asubuhi utamtengeneza. 14 Nawe utatengeneza sadaka ya unga pamoja nayo kila siku asubuhi, sehemu ya sita ya efa moja, na sehemu ya tatu ya hini moja ya mafuta; kuchanganya na unga ule mzuri; sadaka ya unga kwa Bwana daima, kwa amri ya milele. 15 Hivyo ndivyo watakavyomtengeneza mwana-kondoo, na sadaka ya unga, na mafuta, kila siku asubuhi, kuwa sadaka ya kuteketezwa ya daima.

 

Utaratibu wa utoaji dhabihu unalenga kwenye kila kitu kinachohusiana na neema ya Mungu inayookoa kwa ukombozi wa dhabihu ya Masihi. Hakukuwa na siku hata moja ambayo dhabihu haikutolewa katika kipindi chote cha kudumu kwa Hekalu. Wakati Hekalu hili lilipohusuriwa, bado kulikuwa na mahala fulani huko Elephantine nchini Misri wakati wa utumwa wa babeli. Mji wenyewe wa. Elephantine ulikuwa umehusuriwa pia na hatimaye utoaji wa sadaka ulikuja kukoma baadae. Pia Hekalu lilijengwa na Onias IV huko Leontopolis ulioko kwenye mji wa kale wa Gosheni, na hii ilifanyika ili kutimiza unabii uliotolewa na nabii Isaya 19:19 kuhusu kufuru kubwa ya kinajisi itakayoanza kufanyika hadi kuangamizwa kwa Yerusalemu mnamo mwaka wa 70 BK. Hekalu katika Leontopolis lilifungwa kwa amri ya mfalme Vespasian mwaka 71 BK (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)].

 

Kipindi ch Hekalu kilikoma tangu ujenzi wake uliofanywa na Sulemani kwa kipindi cha miaka elfu, hadi kujakwake Masihi akiwa ni Kuhani Mkuu na Kanisa likiwa ndio wakala wake wa huduma za kikuhani mfano wa Melkizedeki. Miaka hii elfu ilikuwa ni kipindi cha yubile ishirini zinzofananishwa na dhabihu za jioni. Kwa hiyo, Kanisa likapitia kipindi cha usiku mrefu wa kutangatanga jangwani na ambacho kilikuwa hakina jingo la Hekalu na dhabihu yake ilikuwa ni wale 144,000, wakiongezwa watu sabini na wawili kila mwaka (wakilinganishwa au kugawanishwa na idadi ya sadaka au dhabihu za kila juma, kila mwezi na za Siku Takatifu zilizoamriwa) ambao wamechukuliwa na kutolewa kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu mbili au yubile arobaini. Wateule walikuwa ndiyo sadaka iliyo hai, na mkutano mkubwa unaosimama na wao (wanaoonekana kwenye Ufunuo 7:1-17) ambako sadaka za daima ambazo hakuna mtu anayeweza kuwahesabu. Ambao “wamelala” katika Bwana wakingojea ufufuo wa kwanza wa wafu, ambao wanaoneshwa hapa.

 

Dhabihu ya asubuhi iliyoonyeshwa ikitolewa kwenye Hekalu aliloliona Ezekieli linawakilisha mwonekano wa kipindi cha mwisho cha utawala wa milenia wa Yesu Kristo na wateule wake. Kipindi hiki cha mwisho cha yubile ishirini au cha miaka elfu moja, kinafanya jumla ya kipindi cha miaka elfu nne ya Hekalu, kinachoishia kwenye ufufuo wa pili wa wafu na cha hukumu na cha kuja kwa Mungu wetu aliye wa Pekee na wa Kweli kwa Utukufu wa Mji wake Mungu (sawa na Mambo ya Walawi 1:1-17 na majarida ya Mwelekeo wa Ratiba ya Nyakati (Na. 272) na Mji wa Mungu (Na. 180) [Outline Timetable of the Age (No. 272) and The City of God (No. 180)]. Dhabihu hizi zote zilitakiwa ziwe za wanyama, (kondoo, mbuzi au mafahali ya ng’ombe) au ya makinda ya ndege wasio na mawaa, na sadaka zinatakiwa zitolewe kwa hiyari na moyo wa kupenda, pasipo kulazimishwa. Makuhani ndio waliokuwa wanazitoa kwa Bwana na kuzitumia.

 

Lingine linalotakiwa kufanywa na wateule ni kutoa dhabihu kwa kuhudumiana, hakuna dhabihu iliyoruhusiwa kutolewa kwa kipindi chote cha miaka elfu mbili. Hekalu liliharibiwa kwa mpango maalumu sana wenye makusudi na maana ma maelekezo ya Mwenyezi Mungu, na dhabihu zilikoma kabisa kutolewa. Kila aliyekuwa anajaribu kurudisha utaratibu huu wa kutoa dhabihu hizi aliuawa, au kupelekwa utumwani. Mpango wa wokovu ni kwa wote wawili, Wayahudi ama Israeli na Wamataifa. Wale wanaojaribu kuwadhulumu Wamataifa wanaadhibiwa kwa kuitumia torati wanaadhibiwa na kuangamizwa.

 

Utaratibu wa kumtolea Bwana dhabihu (Mambo ya Walawi 2:1-16) haupo tena wa jinsi ya ukuhani wa Haruni bali huu wa sasa ni wa mfano wa Melkizedeki (soma Zaburi 110:4); huu haufuatani na nasaba ya kuzaliwa, hauendani na utaratibu wa kufuata uzawa, wa upande wa mama au baba, bali ni kuhani wa milele ulio chini ya Kuhani Mkuu ambaye ni Masihi (soma Waebrania 7:1-22).

 

Dhabihu zilikuwa ni kwa ajili ya wanaotoa huduma ya kikuhani kwenye utaratibu wa siku za kale (Mambo ya Walawi 3:1-17; 4:1-35). Lakini kwenye utaratibu mpya, dhabihu ni makuhani wenyewe.

 

Tumefanyika sote kwa dhabihu ya Masihi. Sheria imeandikwa ndani ya mioyo yetu (Waebrania 8:8-13), na sadaka zetu ni marejesho kwa kuwa Kuhani wetu Mkuu ameketi mkono wa kuume wa Mungu (Waebrania 8:1). Vitu vyote vinavyochinjwa, vinachinjwa kwa mamlaka na ruhusa ya Mungu. Vyote viishivyo ni mali ya Mungu, kwa kuwa ng’ombe wote ni wa Mungu, na vyungu vitakavyokuwa mjini Yerusalemu kipindi cha marejesho mapya vitakuwa vitakatifu kwa Bwana, kama itakavyokuwa kwa kila chenye uhai ni yeye mwenye mamlaka ya kuamuru kichichinjwe ama kiuawe. Dhabihu ya Masihi na sadaka ya hatia vilikuwa ni vitu muhimu kutolewa katika utaratibu mzima wa shughuli na huduma za kikuhani. Hakuna mtu anayeweza kuwa kuhani isipokuwa kwa sadaka hii ya hatia ya dhambi ya Masihi. Yeye ndiye aliye sadaka ya amani ambayo tumefanyiwa sisi mara moja na Mungu, kama inavyoonyeshwa kwenye Mambo ya Walawi 7.

 

Kwa hiyo, huduma hii ya kikuhani inatakaswa kwa kwa njia ya sadaka, na haya yote yanamlenga Masihi. Inampasa kuhani aoshwe kwenye maji ya ubatizo, akiwa amevalishwa vazi jeupe na lisilo na mawaa wala doa lililooshwa kwa damu ya mwanakondoo, na kwa hiyo wameandaliwa kama makuhani. Kuhanin alikuwa ametakaswa hapo mwanzoni na Musa (Mambo ya Walawi 8:1-36), ambaye alisema kwamba nabii atakayetokea “atakuwa kana yeye.” Kupitia kwa nabii huyu wa mwisho, watu wote kutoka kwenye aina yoyote ya maisha na makabila ya watu waliweza kuwa hai. Kutoka kwa Masihi, ndipo huduma ya kikuhani iliandaliwa na kuwekwa mahala pake. Hili ndilo Musa alilolitarajia na kuliongelea, na ndilo lililotimilika kwenye kanisa.

 

Utakaso wa makuhani unafanyika kwa namna sawasawa na ule wa kulitakasa Hekalu (soma jarida la Utakaso wa Hekalu (Na. 241) [The Sanctification of the Temple (No. 241)]. Wao ni watu wasio na chachu, walio mbali na aina yeyote ya chachu ya uovu na udhaifu, na wanangojea donge jipya la chacu ya Roho Mtakatifu. Tangia Mwanzo wa mwezi wa Kwanza unaoitwa wa Abibu au Nisani, hadi siku ya saba ya mwezi huo huo wa Kwanza, makuhani na wateule wote wanalitabaruku Hekalu, na kuzitubia dhambi zilizofanywa pasipo kujua au kwa kupotoshwa, tendo ambalo linaishia siku ya mwisho (ambayo ni ya saba ya mwezi huu). Kuhani ni.Hekalu lililomfano wa Melkizedeki.

 

Desturi ya kuadhimisha siku ya Mwaka Mpya katika siku ya kwanza ya mezi wa Saba, inaoitwa Rosh Hashanah, unapingana na agizo lililotolewa na Mungu kwenye kitabu cha Torati, na tendo au mafundisho haya hayakuingia kwenye imani ya Kiyahudi hadi ilipofika karne ya tatu ya zama zetu, kama ilivyoelezwa na rabi mmoja anayeitwa Rabi Kohn, aliyekuwa Rabi Mkuu wa Budapest (soma kitabu cha Wasabato wa Transylvania cha mwaka 1894, [The Sabbatarians in Transylvania, (1894}] na ambacho kimechapishwa upya na W. Cox, kikitafsiriwa na T. McElwain na B. Rook, 1998, CCG Publishing, pp. v. et seq.). Rosh Hashanah ilikuwa haiadhimishwi kabisa katika zama za kipindi cha Hekalu. Maana shirio mazima ya Utakaso wa Hekalu hayahusishi na dhana nzima kama hii.

 

Mambo ya Walawi 9:1-24 inasema: Basi ilikuwa siku ya nane, Musa akawaita Haruni na wanawe, pamoja na wazee wa Israeli; 2 akamwambia Haruni, Twaa wewe mwana-ng'ombe mume awe sadaka ya dhambi, na kondoo mume wa sadaka ya kuteketezwa, wakamilifu, ukawasongeze mbele ya Bwana. 3 Nawe utawaambia wana wa Israeli, ukisema, Twaeni mbuzi mume awe sadaka ya dhambi; na mwana-ng'ombe, na mwana-kondoo, wote wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, kwa sadaka ya kuteketezwa; 4 na ng'ombe mume, na kondoo mume, kwa sadaka za amani, ili kuwachinja mbele za Bwana; na sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta; kwa maana, Bwana hivi leo atawatokea. 5 Nao wakayaleta hayo yaliyoagizwa na Musa wakayaweka mbele ya hema ya kukutania; kisha mkutano wote ukakaribia wakasimama mbele za Bwana. 6 Kisha Musa akasema, Neno aliloliagiza Bwana kwamba mlifanye ni hili; na huo utukufu wa Bwana utawatokea. 7 Musa akamwambia Haruni, Ikaribie madhabahu, uitoe sadaka yako ya dhambi, na sadaka yako ya kuteketezwa, ukafanye upatanisho kwa ajili ya nafsi yako, na kwa ajili ya watu; nawe uitoe hiyo dhabihu ya watu, ukafanye upatanisho kwa ajili yao; kama Bwana alivyoagiza. 8 Basi Haruni akakaribia madhabahuni, akamchinja huyo mwana-ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliyekuwa kwa ajili ya nafsi yake. 9 Kisha wana wa Haruni wakamsongezea Haruni ile damu; naye akatia kidole chake katika damu, na kuitia katika pembe za madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu; 10 lakini mafuta, na figo, na kitambi kilichotoka katika ini ya hiyo sadaka ya dhambi, akaviteketeza juu ya madhabahu, kama Bwana alivyomwagiza Musa. 11 Na nyama, na ngozi akazichoma moto nje ya marago. 12 Naye akaichinja sadaka ya kuteketezwa; na wanawe Haruni wakamsongezea ile damu, naye akainyunyiza katika madhabahu pande zote. 13 Nao wakamletea sadaka ya kuteketezwa kipande kwa kipande, na kichwa; naye akaviteketeza juu ya madhabahu. 14 Kisha akaosha matumbo, na miguu na kuiteketeza juu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. 15 Kisha akaisongeza dhabihu ya watu, akamtwaa mbuzi wa sadaka ya dhambi aliyekuwa kwa hao watu, na kumchinja, na kumtoa kwa ajili ya dhambi kama yule wa kwanza. 16 Kisha akaisongeza sadaka ya kuteketezwa, na kuitoa sawasawa na sheria. 17 Kisha akaisongeza sadaka ya unga, na kutwaa konzi humo, na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi. 18 Huyo ng'ombe mume naye akamchinja, na huyo kondoo mume pia, dhabihu ya sadaka za amani, zilizokuwa kwa ajili ya watu; na wanawe Haruni wakamsongezea ile damu, naye akainyunyiza katika madhabahu pande zote, 19 na mafuta ya ng'ombe; na ya kondoo, mkia wake wa mafuta, na hayo yafunikayo matumbo, na figo zake, na kitambi cha ini; 20 nao wakayaweka hayo mafuta juu ya vidari, naye akayateketeza mafuta juu ya madhabahu; 21 na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kuume, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya Bwana; kama Musa alivyoagiza. 22 Kisha Haruni akainua mikono yake na kuielekeza kwa hao watu, akawabariki; kisha akashuka akisha isongeza sadaka ya dhambi, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani. 23 Kisha Musa na Haruni wakaingia ndani ya hema ya kukutania, kisha wakatoka nje, na kuwabarikia watu; na huo utukufu wa Bwana ukawatokea watu wote. 24 Kisha moto ukatoka hapo mbele za Bwana, na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na yale mafuta juu ya madhabahu; watu wote walipouona huo moto wakapiga kelele wakainama kifudifudi.

 

Tangia utakaso na kuwateua na kuwatenga kando wateule, watu wamebarikiwa tena kwa namna nyingi. Taifa na dunia haviwezi kudhurika hadi mteule wa mwisho atakapokuwa amebatizwa, ametiwa mhuri na kutengwa mbali, na ndipo ule mwisho utakapokuja (Ufunuo 7:3-4).

 

Aina yoyote ya uuaji ni amri yake Bwana Mungu, na kisasi cha damu ni lazima kilipwe kwa damu, kisipifanywa kwa mapenzi matakatifu ya Bwana Mungu.

Mambo ya Walawi 17:1-6  Bwana akamwambia Musa, akisema, 2 Sema na Haruni, na wanawe, na wana wote wa Israeli, ukawaambie; Neno hili ndilo aliloliamuru Bwana, akisema, 3 Mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli atakayechinja ng'ombe, au mwana-kondoo, au mbuzi, ndani ya marago, au atakayemchinja nje ya marago, 4 wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, ili amtoe kuwa matoleo kwa Bwana mbele ya hema ya Bwana; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake; 5 ili kusudi wana wa Israeli walete sadaka zao, wazichinjazo mashambani, naam, wazilete kwa Bwana, mpaka mlango wa hema ya kukutania, kwa huyo kuhani, ili wazichinje ziwe sadaka za amani kwa Bwana. 6 Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya Bwana, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za Bwana

 

Kwa hiyo, mambo yote yanafanywa kwa utukufu mkubwa wa Mungu. Shughuli za machinjioni au za kuchinja za mchinjaji zinatakiwa pia kuwa na uangalizi wa kuhani. Kwenye kipindi cha marejesho ya mfumo wa dunia, shughuli zote za uchinjaji wa wanyama zitafanyika kwa dhumuni la kutoa sadaka takatifu kwa Bwana tu, na vyombo vitakuwa vitakatifu kwa Bwana (Zekaria 14:20-21; pia soma jarida la Imani ya Kutokula Nyama au Uvujitariani Kwenye Biblia (Na. 183) [Vegetarianism and the Bible (No. 183)].

 

Tendo la kuchukua uhai linafanyika kwa mamlaka na ruhusa ya Mungu. Kwa hiyo damu ina uhai ndani yake na inapaswa imwagwe chini kwenye ardhi.

Kumbukumbu la Torati 12:20-28 Bwana, Mungu wako, atakapoongeza mpaka wako, kama alivyokuahidi, nawe utakaposema, Nataka kula nyama, kwa kuwa roho yako yatamani kula nyama; waweza kula nyama, kwa kufuata yote inayotamani roho yako. 21 Na mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, apaweke jina lake, pakiwa mbali nawe mno, ndipo utakapochinja katika kundi lako la ng'ombe na kondoo alilokupa Bwana kama nilivyokuagiza, nawe utakula ndani ya malango yako, kwa kufuata yote inayotamani roho yako. 22 Kama vile aliwavyo paa na kulungu, ndivyo utakavyoila nyama hii; asiyekuwa tohara na aliye tohara wataila pia. 23 Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama. 24 Usiile; imwage juu ya nchi kama maji. 25 Usiile; ili upate kufanikiwa, na watoto wako baada yako utakapofanya yaliyoelekea machoni pa Bwana. 26 Ila vitu vyako vitakatifu ulivyo navyo, na nadhiri zako, uvitwae ukaende mahali atakapochagua Bwana; 27 nawe zisongeze sadaka zako za kuteketezwa, nyama na damu, juu ya madhabahu ya Bwana, Mungu wako; na damu ya dhabihu zako uimwage juu ya madhabahu ya Bwana, Mungu wako, na wewe utakula nyama yake. 28 Maneno haya nikuagizayo yote yatunze na kuyasikiza, ili upate kufanikiwa na watoto wako baada yako milele, hapo uyafanyapo yaliyo mema na kuelekea machoni pa Bwana, Mungu wako.

 

Haki ya Jamhuri kutwaa uhai wa mtu

Haki ya kutwaa uhai wa mtu imepewa Jamhuri lakini imepewa tolewa kwa mtu binafsi pia kwa mazingira fulani fulani. Kwa mujibu wa Torati, kuna Goel aliyeteuliwa kama mlipiza kisasi cha damu, au mkombozi wa Israeli aliye kama mlipa makosa. Mfano wa kwanza uko kwenye Mwanzo 48:16 tunapojionea Malaika wa Ukombozi, ambaye alikuwa ni elohim wa Israeli. Mwonekano wa pili wan eno hili ni kwenye Kutoka 6:6 na 15:3, pale ambapo Masihi alikuwa ni mkombozi na mtu wa vita dhidi ya wale waliokuwa sio Waisraeli. Na neno lililotumika hapa kumuelezea ni mlipa kisasi cha damu chini ya sheria kwenye Hesabu 35:12,19 (pia soma Hesabu 35 hapo chini). Kazi yake kwa kawaida ilielezewa kwa kina kwa ndugu wa pili au ndugu wa karibu kwa mtazamo wa kikabila, lakini inaonekana kuwa alikuwa ni Masihi na ni elohimu wa haki aliyetoa mamlaka kwa mauaji ya nchi nzima kama ilivyotakiwa. Hakuna mzaliwa anayepaswa kuuawa hadi atakaposimama mbele ya kusanyiko kwa ajili ya hukumu. Kwa utaratibu huo ndivyo inavyotakiwa kufanywa na kufuatwa, kunatakiwa iwepo miji ya makimbilio na mahali ambapo mtu anaweza kujihakikishia usalama wake na kuletwa kwenye mashitaka.

 

Udhibiti wa uhai kwa amani

Sheria zote zinazohusika na masuala ya usafi zimetolewa ili kuyalinda maisha yetu. Ujinga au kutojua hakumfanyi mtu akubalike anapotoa udhuru kwa kuvunja shiria.

Mambo ya Walawi 5:2-3 au kama mtu akigusa kitu kilicho najisi, kama ni mzoga wa mnyama wa nyikani aliye najisi, au kama ni mzoga wa mnyama wa mfugo aliye najisi, au kama ni mzoga wa mdudu aliye najisi, naye jambo hilo linamfichamania, akapata kuwa najisi, ndipo atakapochukua uovu wake; 3 au kama akiugusa uchafu wa binadamu, uchafu uwao wote ambao kwa huo amepata unajisi, na jambo hilo linamfichamania, hapo apatapo kulijua, ndipo atakapokuwa na hatia. 

 

Baadhi ya mambo yanayotolewa dhabihu yalitolewa pia kwa kina na Bwana. Tendo hili ni adhabu na litarudishwa upya tena kama adhabu kipindi cha utawala wa milenia. Jambo hili linaweka tofauti kati ya sheria ya usafi, ambayo ni sehemu ya maagizo ya torati ya sheria ya uzima au maisha—yaani kuyafanya yome au kumfanya aishi.

Mambo ya Walawi 7:21-27  Kisha mtu awaye yote atakapogusa kitu cho chote kilicho najisi, uchafu wa binadamu, au mnyama aliye najisi, au machukizo yo yote yaliyo najisi, kisha akala nyama ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo ni za Bwana, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake. 22 Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 23 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yo yote, ya ng'ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi. 24 Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa ajili ya matumizi mengine; lakini msiyale kabisa. 25 Kwani huyo mtu atakayekula mafuta ya mnyama, ambaye ni katika wanyama ambao watu husongeza sadaka kwa Bwana kwa moto, mtu huyo atakayekula mafuta hayo atakatiliwa mbali na watu wake. 26 Tena msiile damu yo yote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote. 27 Mtu ye yote alaye damu, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.

Madhara ya muda mrefu yatokanayo na ulaji wa mafuta na damu kwa sasa yanajulikana vizuri. Matendo haya yamekatazwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazofundisha mbinu za kuishi maisha marefu.

 

Aina yoyote ya mqauaji na hasa uchinjaji vinapaswa vifanyike kwa lengo la kufanya kitoweo kwenye chakula tu, na kulinda uwiano au kwa ajili ya mali na ni lazima ufanyike kwa kuzingatia maelekezo ya torati. Ulinzi wa mazingira ni jambo la muhimu sana pia na ni wajibu wa kila mmoja akama ilivyo kwenye kuwalinda wengine kutokana na kupuuzia masuala ya mali au ujenzi.

Kumbukumbu la Torati 22:6-8 Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda; 7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi. 8 Utakapojenga nyumba mpya, fanya ukuta kando-kando ya dari lako, usije ukaleta damu juu ya nyumba yako, mtu akianguka huko.

 

Damu ya kila kiumbe iko juu ya yule aliyehusika kukitoa uhai wake. Kuna miiko inayowataka watu kuwalinda wengine au wenzao dhidi ya kupoteza maisha yao au kuumia kutokana na kazi au zana ngumu. Kwa jinsi hii, vizuizi vinavyowekwa kwenye mapaa ya nyumba, na hata tunapoweka kuzungushia kwenye kuta za bwawa la kuogelea kwa lengo la kuwalinda watoto wadogo, ni hadhari ya muhimu sana. Kwa jinsi hiyo hiyo, kupuuzia kumpa msaada mtu anayeuhitaji na aliye matatizoni ni mojawapo ya uvunjifu wa maagizo ya torati, hata hivyo, hakuna ulazima kwa mtu kujitaabisha au kupoteza uhai wake kwa ajili ya kutimiza jambo hilo. Kinyume na walivyofundisha marabi ya Kiyahudi, kuna ulazima wa kujitahidi na kujaribu iwezekanavyo kuokoa maisha.

 

Magonjwa

Udhibiti wa magonjwa ni sehemu muhimu sana kwenye mkakati huu wa kuzuia vifo na kulinda maisha ya watu. Amri hii ya sita inaelezea kuhusu mauaji yanayosababishwa na maambukizi ya magonjwa. Kila mtu anawajibu wa kuhakikishwa kwamba hamsababishia mwenzake hatari kwa kukosa kwake kuzizingatia taratibu na kanuni zilizowekwa ambazo kwazo wanaweza kuishi kwa usalama. Kuzaliwa kwa motto ni jambo linalowafanya wastahili haki ya kitaifa ya uzawa. Chini ya maagano na kwa mujibu wa sheria na kanuni ya utakaso (Mambo ya Walawi 12:1-8).

Mambo ya Walawi 12:1-8 inasema: Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto mume, ndipo atakuwa yu najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi, ndivyo atakavyokuwa najisi. 3 Siku nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake. 4 Na huyo mwanamke atakaa katika damu ya kutakata kwake siku thelathini na tatu; asiguse kitu kilicho kitakatifu, wala asiingie mahali patakatifu, hata siku hizo za kutakata kwake zitakapotimia. 5 Lakini kwamba amezaa mtoto mke ndipo atakuwa najisi juma mbili, kama katika kutengwa kwake; naye atakaa katika damu ya kutakata kwake muda wa siku sitini na sita. 6 Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mwana, au kwa ajili ya binti, ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani; 7 na yeye atawasongeza mbele za Bwana, na kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atatakasika na jicho la damu yake. Hii ndiyo amri yake huyo azaaye, kwamba ni mtoto mume au mke. 8 Kama mali yake huyo mwanamke haimfikilii mwana-kondoo, hapo ndipo atakapochukua hua wawili, au makinda mawili ya njiwa; mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na wa pili kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.

 

Sheria za utakaso zinaweka tofauti kati ya motto wa kimume na wa kike. Tendo hili halijafanyiwa uchunguzi na wana sayansi peke yao bali pia linapelekea kuwa na msingi mzuri na wenye mwelekeo madhubuti. Kama vilivyo Sheria nyingine zote, kuna kiini msingi cha kuwekewa sheria. Sababu ya kuwekwa kanuni inaweza kuwa ni kukusudia kuwalinda mama au mtoto dhidi ya aina mbalimbali za madhara ya kikemikali, ambayo yanaweza kudumu na kuleta maafa au udhuriko mkubwa kwa kuwa ni sehemu ya ugonjwa. Masuala yote yanayohusika na utakaso wa wanawake yametolewa ufafanuzi wake kwenye jarida la Utakaso na Tohara (Na. 251) [Purification and Circumcision (No. 251)].

 

Kuweka karantini ni sehemu ya muhimu sana katika maisha. Ni jukumu la jamii mzima na kwa kila mmoja. Sheria inayohusu ukoma inatuonyesha umuhimu na ulazima wa kuweka mkakati madhubuti wa marufuku na karantini. Ingawaje siku hizi tunaweza kuutibu ukoma, lakini sheria bado inasimama na mkakati wa kuweka karantingi na kuwatenga waathirika ni wa muhimu.

 

Mambo ya Walawi 13:1-59 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Sura hii inaelezea jinsi ya kutambua nakanuni za kushughulikia aina mbalimbali ya vipaku vinavyoonekana kwenye ngozi na kwa nguo zilizoathirika kwa kuguswa na mtu mwenye madhara haya. Utaratibu wa kuorodhesha majina ya magonjwa ni rahisi pia kwa watu wa kawaida. Upigaji marufuku na utekelezaji wake, na kwa usemi wa kisasa wanaita hali hii kuwa Torati yasingekuwako tena, bali utaratibu na kanuni zake zingebakia kuwa ni zile zile.

 

Mambo ya Walawi 14:1-57 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Mambo ya Walawi 14 inauelezea ogonjwa wa ukoma, na dhabihu anayotakiwa aitoe yule aliyeponywa, pia inaelezea juu ya nguo iliyochafuliwa na nyumba iliyonajisika.

 

Mambo yote yanayohusu na utiwaji najisi wa maeneo yameongelewa kwa kina kwenye sheria hizi. Iwapo kama sheria hizi zingekuwa zinaadhimishwa leo, basi majongwa ya kuambukizwa na mikakati ya kuzuia maambukizi hospitalini vingepungua au kukomeshwa kabisa. Tunajua sababu za maambukizi haya siku hizi kwa msingi wa kisayansi zaidi) kuliko katikwa kipindi kingine chochote lilichopita, lakini nia yetu na mtazamo wa kuweka karantini na kuwatenga wengine mbali haitendeki kikamilifu sawa na inavyopaswa kuwa. Hafungi wadi za kulala wagonjwa kwa ajili ya gharama ilivyo wala kukosekana kwa vitanda, kwa mahali ambapo kunaupinzani au vikwazo vya mazuio au marufuku vimeenea. Watu hufia hospitalini kwa sababu ya kuzivunja sheria za kibiblia hata leo.

Kumbukumbu la Torati 24:8-9 Angalia katika pigo la ukoma, utunze kwa bidii, kwa kufanya mfano wa yote watakayowafundisha makuhani Walawi; tunzeni kwa kuyafanya vile vile kama nilivyowaamuru wao. 9 Kumbukeni na Bwana, Mungu wako alivyomtenda Miriamu katika njia mlipotoka Misri.

 

Ugonjwa wa ukoma ni adhabu pia kwa ajili ya uasi. Siku hizi, suala la mbingu kuingilia kati hakuchukuliwi na kutiwa maanani kabisa.

 

Mambo ya Walawi 15:1-33 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Sura hii kwanza kabisa inaelezea kuhusu ogonjwa uliosababishwa na mtu kutokwa na shahawa (ni sawa na magonjwa yanayotokana na matendo ya zinaa, UKIMWI, mafua na aina nyingine ya magonjwa yanayoweza kuambukiza kwa urahisi). Kisha inaelezea jinsi ya kuitendea nguo iliyopatwa na kipaku cha maambukizi haya, iliyoguswa na uume, na iliyoguswa na machafu yaliyotokana na tendo la ngono na damu ya uke wa mwanamke aliye kwenye kipindi chake cha hedhi.

 

Sheria za usafi na karantini zimewekwa wa lengo kuu la kuzuia maambukizi. Sasa tunaelewa sababu ya magonjwa kwa kina zaidi na kwa upana zaidi kuliko tulivyokuwa huko nyuma, bali tunaona pia kwamba sheria za kupiga marufuku na karantini bado ni za muhimu na zinaendelea kutenda kazi.

Hesabu 5:1-4 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma maragoni, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya wafu; 3 mtawatoa nje wote, waume kwa wake, mtawaweka nje ya marago; ili wasiyatie unajisi marago yao, ambayo mimi naketi katikati yake. 4 Wana wa Israeli wakafanya vivyo, wakawatoa na kuwaweka nje ya marago; kama Bwana alivyonena na Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.

 

Kwa hiyo, kuweka karantini kwa magonjwa ya kuambukiza yanapotokea ni muhimu (Hesabu 9:6-11).

 

Maadhimisho yajulikanayo Pasaka ya pili yaliwekwa kwa wale wote walioshindwa kwa sababu mbalimbali na bahati mbaya kuitunza ile ya kwanza, kwa kuwa walikuwa wamesafiri, au kama kulikuwa na karantini fulani au kama kulijitokeza tatizo fulani lolote lile. Haikuwekwa kwa ajili ya uchaguzi wao wa hiyari kuchagua waiadhimisheje au lini.

 

Mahusiano ya sadaka hizi ni kumlingana Mungu kuwa ni kiini na chanzo cha uzima na maisha na uponyaji wetu. Uponyaji ni tendo la kisayansi, na mponyaji anayetenda kazi kwenye taifa anapaswa afanye kazi yake hii kwa mujibu wa sheria na amri za Mungu. Wanapaswa kuifanya kazi hii kwa uaminifu mkubwa kama wanavyofanya kwa maelekezo ya Mwenyezi Mungu na kwa sheria na Amri zake.

 

Kumbukumbu la Torati 23:1-8 Aliyejeruhika konde, au aliyekatika tupu yake, asiingie mtu huyo katika mkutano wa Bwana. 2 Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana. 3 Mwamoni wala Mmoabi wasiingie katika mkutano wa Bwana; wala hata kizazi cha kumi mtu wao asiingie katika mkutano wa Bwana milele; 4 kwa sababu hapo mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo Mesopotamia, aje akuapize. 5 Lakini Bwana, Mungu wako, hakukubali kumsikiza huyo Balaamu; Bwana, Mungu wako, aliyageuza yale maapizo kuwa ni baraka, kwa vile alivyokupenda Bwana, Mungu wako. 6 Usitafute amani yao wala heri yao siku zako zote, milele. 7 Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake. 8 Wana wao watakaozaliwa kizazi cha tatu na waingie katika mkutano wa Bwana.

Sehemu hii sheria, tunajionea kwamba ulinzi wa taifa unahusiana moja kwa moja na ulinzi wa familia ulivyo ndani ya maisha ya ndoa. Aina hii ya makundi ya watu yamekatazwa kuingia kwenye mkutano wa Bwana kama mfano kwa Israeli. Watu hawa walifia dhambini kwa mujibu wa sheria na amri za Mungu.

 

Ilikuwa ni tabia na imani ya wapagani pia kuwaoona mahuhani wao wakiishi maisha ya useja bila mke, au kuwafanywa wawe matowashi. Sheria iliwekwa pia ili kuzuia au kukataza matendo haya. Wapagani na wengine wote wanaoijua vema sheria hii maranyingine wanawaona na kuwafananisha wateule na matowashi ili kukanganya kile kinachosemwa na sheria hii, na kuwafatenga kiujanja na kwa hila kuwa hawastahili kuingia kwenye masunagogi yao wala kwenye makutaniko yao. Agano Jipya linathibitisha matendo haya na maamuzi yalifanywa baadae (sawa na zinavyosema nakala zinazoaminiwa kuwa ni za Katiba ya Mitume au kwa Kiingereza ni Apostolic Constitutions, ANF, Vol. VIII, pp. 479 et seq.) ambayo iliwaruhusu watu aina hii kuwa maaskofu au wazee.

 

Masihi alikufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Wokovu sasa ni kwa Wamataifa, na dhambi za mababu zetu waliotutangulia hazihesabiwi tena kwa watoto na wajukuu zao. Hili ni agano jipya ambao kwao sheria zimeandikwa ndani ya mioyo ya watu, na kila mtu anawajibika kwa dhambi zake mwenyewe. Hii ndiyo maana ya kutimilizwa kwa jinsi lilivyokuwa agano (soma Yeremia 31:29-34).

 

Utaratibu mzima wa Agano Jipya chini ya Masihi ulikusudia kushughulika na dhambi (soma Mathayo 26:28; Waebrania 8:8-12; 10:16-17). Fafanuzi tafsiri za Marabi zimeshindwa kuelezea kile kilichobadilishwa kwa usahihi (soma kitabu cha fasiri kijulikanacho kama. Soncino Commentary hadi kwenye aya ya 30). Kwa kweli Israeli watabakia waaminifu kwa Mungu, bali ile hali ya kuzichukua dhambi kutoka kwa baba hadi kwa mtoto imekomeshwa na kuondolewa kabisa kwenye mfumo wote huu kabisa wa mapatilizo ya dhambi za asili zilizofanywa na mababa kwenye kipindi cha Agano la Kale. Kile kinachojulikana siku hizi kuwa ni Ukristo kinaeneza ujumbe ulio kinyume kabisa na ule uliokusudiwa na Masihi.

 

Mapatilizo kwa ajili ya uchafu uliofanywa kwenye taifa kipindi cha vita yanaelezewa pia kwenye kifungu hiki cha maandiko. Taifa la Israeli halikupaswa kufanya mambo yake sawa na wanavyofanya Mataifa wapagani, na wala hawakuruhusiwa kujitia unajisi na Wamataifa.

Kumbukumbu la Torati 23:9-14 inasema: Utakapotoka kwenda juu ya adui zako nawe u katika marago, jilinde na kila neno baya. 10 Akiwa kwenu mtu awaye yote asiyekuwa ni tohara kwa ajili ya yaliyomtukia usiku, na atoke nje ya kituo, wala asiingie ndani ya kituo; 11 lakini na iwe ikaribiapo jioni, yeye ataoga maji; na jua likiisha kuchwa ataingia ndani ya kituo. 12 Tena uwe na mahali nje ya kituo, kwa kutokea nje; 13nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho; 14 kwa kuwa Bwana. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha.

 

Bwana Mungu wetu anatembea katikati yetu, na tunapaswa kuwa watakatifu kwa vipindi vyote, yaani cha amani na cha vita. Mungu anakaa kati yetu na sisi tu Hekalu la Mungu.

 

Sheria ya Vyakula

Sheria inayohusiana na vyakula inakusudia kurefusha maisha yetu na kuilinda sayari yetu hii ya dunia, pia zinaweka hakika ya mnyororo wa vyakula na kupunguza maambukizo au mashambulizi ya magonjwa. Misingi ya kisayansi ya sheria ya vyakula imeelezewa kwa kina katika jaarida la Sheria ya Vyakula (Na. 15) [The Food Laws (No. 15)]. Ukengeufu dhidi ya kuzishika sheria za vyakula, mafundisho ya kiasetiki yanayofundisha kutokula nyama bali kula mbogamboga peke na ukengeufu unaoenenda nayo vimeelezewa kwa kina kwenye majarida ya Uvijiteriani Na Biblia (Na. 183), Mvinyo Katika Biblia (Na. 188) na Uwiano (Na. 209) [Vegetarianism and the Bible (No. 183); Wine in the Bible (No. 188) and Balance (No. 209)]. Itikadi ya Kutokula nyama au Uvijiteriani na useja na mafundisho ya kujinyima kutofanya tendo la ndoa kwenye ndoa yameelezwa kuwa ni mafundisho ya mapepo yatakayoshika kazi siku za mwisho (1Timotheo 4:3; sawa na Matendo 15:20; Mathayo 3:4)

 

Kujilinda dhidi ya magonjwa kwa kutumia mbinu za kuyashika maelekezo yaliyomo kwenye sheria za vyakula na uchinjaji kwa uangalifu, na kuacha kula wanyama walioraruliwa na wanyama wakali wa porini kama ilivyoelezewa na kuagizwa kwenye amri na sheria za Mwenyezi Mungu (kama ilivyoandikwa kwenye Kutoka 22:31). Pia malimbuko yatokanayo na malimbuko ya kwanza yamewekwa wakfu kwenye Nyumba ya Mungu (Kutoka 34:26). Bwana aliwaongoza Israeli kwa kuwa hawakuwa na mungu mgeni katikati yao. Walikula mema ya nchi, ingawaje siku zote za Sulemani hadi alipotenda dhambi, na maovu yaliletwa kwenye nchi hii (Kumbukumbu la Torati 32:14; sawa na Mithali 27:27; 1Wafalme 4:22-23).

 

Sheria hii ya vyakula imeandikwa kwenye Mambo ya Walawi sura ya 11.

Mambo ya Walwi 11:1-47 inasema: Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2 Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi. 3 Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala. 4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 6 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. 8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu. 9 Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao. 10 Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu, 11 watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu. 12 Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu. 13 Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; 14 na mwewe, na kozi kwa aina zake, 15 na kila kunguru kwa aina zake; 16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 17 na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa; 18 na mumbi, na mwari, na mderi; 19 na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo. 20 Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo kwenu. 21 Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi; 22 katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake. 23 Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu. 24 Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni; 25 na mtu awaye yote atakayechukua cho chote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni. 26 Kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, naye hana kwato mbili, wala hacheui, huyo ni najisi kwenu; kila agusaye wanyama hao atakuwa ni najisi. 27 Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni. 28 Na huyo atakayechukua mzoga wa wanyama hao atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni; hao ni najisi kwenu 29 Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake, 30 na guruguru na kenge, na mjusi na goromoe, na lumbwi. 31 Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; awaye yote atakayewagusa, wakiisha kufa, atakuwa ni najisi hata jioni. 32 Tena kitu cho chote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; kwamba ni chombo cha mti, au nguo, au ngozi, au gunia, chombo cho chote kitakachoangukiwa, ambacho ni chombo cha kufanyia kazi yo yote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hata jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi. 33 Na kila chombo cha udongo, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, kila kilichomo ndani yake kitakuwa ni najisi, na hicho chombo kitavunjwa. 34 Kila chakula kilichomo, ambacho ni kuliwa, hicho ambacho maji hutumiwa juu yake, kitakuwa ni najisi; na kila kinyweo ambacho ni cha kunywewa, kilichomo katika chombo kama hicho, kitakuwa ni najisi. 35 Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande cho chote cha mizoga yao kitakuwa najisi; kwamba ni tanuru, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu. 36 Pamoja na hayo, chemchemi, au shimo, ambamo maji yakusanyika, vitakuwa ni safi; lakini hicho kitakachogusa mizoga yao kitakuwa ni najisi. 37 Na kipande cho chote cha mzoga kikiwa kimeangukia mbegu za kupandwa zitakazopandwa, zitakuwa safi. 38 Lakini kwamba hizo mbegu zilitiwa maji na cho chote cha mizoga yao kuziangukia, ni najisi kwenu. 39 Kama akifa mnyama awaye yote, ambaye mna ruhusa kumla, yeye anayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hata jioni. 40 Na yeye atakayekula nyama ya mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; yeye atakayeuchukua mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni. 41 Na kila kitu kitambaacho juu ya nchi ni machukizo; hakitaliwa. 42 Kila aendaye kwa tumbo lake, na kila aendaye kwa miguu minne, na kila aendaye kwa miguu mingi, maana, ni vyote vyenye kutambaa vitambaavyo juu ya nchi, hamtavila, kwa kuwa ni machukizo. 43 Msifanye nafsi zenu kuwa ni chukizo kwa kitu cho chote chenye kutambaa, kitambaacho, wala msifanye nafsi zenu kuwa ni najisi kwa vitu hivyo, mkajipatia uchafu kwa hivyo. 44 Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi. 45 Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu. 46 Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi; 47 ili kupambanua kati ya hao walio najisi na hao walio safi, na kati ya kiumbe kilicho hai ambacho chaliwa, na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi.

 

Ikumbukwe kwamba tafsiri ya Biblia ya Mfalme Yakobo (KJV) inatumia neno swan kumtaja nguruwe na haikujumuishwa kwa kulinganisha wanyama walio kwenye kundi la bata salili na bata bukini kwenye ile aya ya 18. Neno lililoko hapa kwa kweli halimaanishi kutaja swan na hawekwi kwenye mjumuisho wa kundi la hawa bata salili na bata bukini. Neno lililotumika la tinshemes linamjumuisha popo (Rashi; Chizkuni) au mwewe (Ralbag; kama isemavyo Stone’s Chumash) au mwewe mkubwa (kwa mujibu wa Soncino), au tanshemes (SHD 8580) inavyomtaja kuwa ni kuku wa majini.

 

Kumbukumbu la Torati 14:1-21 inasema: Kisha Ninyi mmekuwa wana wa Bwana, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa. 2 Kwa kuwa u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, na Bwana amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi. 3 Usile kitu cho chote kichukizacho. 4 Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, 5 kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima; 6 na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla. 7 Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu; 8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse. 9 Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula; 10 na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu. 11 Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi. 12 Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu; 13 na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake; 14 na kila kunguru kwa aina zake; 15 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 16 na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa; 17 na mwari, na nderi, na mnandi; 18 na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo. 19 Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale. 20 Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi. 21 Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.

Kwa hiyo, ndiyo maana kuna umuhimu wa kuwa na uzao mkamilifu wa wanyama wafugwao na sio waliochanganyika aina mbalimbali, au kuwa na wanyama wa aina moja, na wala tusizae mavazi au nguo zenye sufi iliyochanganyikana na hariri (Mambo ya Walawi 19:19) mbali na ile anayoivaa Kuhani Mkuu.

 

Mambo ya Walawi 20:25 inasema: Kwa ajili ya hayo mtapambanua kati ya mnyama aliye safi na mnyama aliye najisi, na kati ya ndege aliye tohara na ndege aliye najisi; nanyi msizifanye nafsi zenu kuwa machukizo kwa njia ya mnyama, au kwa njia ya ndege, au kwa njia ya kitu cho chote ambacho nchi imejaa nacho, niliowatenga nanyi kuwa ni najisi.

Tofauti hizi za vitu fasi na najisi zipo pale ili kuwalinda watu.

 

Mambo ya Walawi 22:1-33 inaelezea matumizi au ulaji wa vitu vitakatifu. Vitu hivi havitakiwi vitiwe unajjsi.

 

Sheria hizi hapa zimewekwa ili kuwalinda Makuhani na huduma yao na ilikuwa inawalenga wateule. Kama sheria hii isingekuwepo ili kuwalinda makuhani na aina ya wanyama wanaotolewa sadaka, basi Walawi wangekula vitu vilivyonajisi au unajisi wan chi, na meza au madhabahu ya Bwana ingekuwa imenajisika. Sadaka au dhabihu zilizotolewa zilikuwa na makusudio makuu mawili yafuatayo: sadaka zilikuwa ni takatifu kwa Bwana na ni zilizokuwa njema tu ndizo zilitolewa, na pia sadaka za dhambi zilikuwa ni adhabu waliyopaswa kuito, na itaendelea kuwepo tena kipindi cha milenia. Daudi alikula mkate wa wonyesho, ambao haukuruhusiwa kuliwa na mtu kama yeye, bali alikuwa anaweka welekeo wa Masihi na Kuhani mpya anayekuja kupitia kwenye mlolongo wa uzao na kwenye nyumba yake Daudi.

 

Maandiko yaliyo kwenye Hesabu 19 yanaelezea kutolewa kwa sadaka ya mtamba mwekunbu na jinsi ya kuwafanyia waliokufa.

Hesabu 19:1-22 inasema: Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2 Hii ndiyo amri ya sheria Bwana aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng'ombe mke mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado; 3 nanyi mtamleta kwa Eleazari kuhani, naye atakwenda naye nje ya kambi, na mtu mmoja atamchinja mbele yake; 4 kisha Eleazari kuhani atatwaa katika damu yake kwa kidole chake, na kuinyunyiza damu yake kuelekea upande wa mbele wa hema ya kukutania mara saba; 5 kisha mtu mmoja atamchoma moto huyo ng'ombe mbele yake; ngozi yake, na nyama yake, na damu yake, pamoja na mavi yake pia atachoma moto; 6 kisha kuhani atatwaa mti wa mwerezi, na hisopo, na sufu nyekundu, na kuvitupa katika huo moto unaomchoma ng'ombe. 7 Ndipo kuhani atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, kisha baadaye ataingia kambini, naye kuhani atakuwa najisi hata jioni. 8 Na huyo aliyemchoma moto ng'ombe atazifua nguo zake majini, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa najisi hata jioni. 9 Kisha mtu mmoja aliye safi atayazoa majivu ya huyo ng'ombe, na kuyaweka yawe akiba katika mahali safi nje ya kambi, nayo yatatunzwa kwa ajili ya mkutano wa wana wa israeli, kuwa ndiyo maji ya farakano; ni sadaka ya dhambi. 10 Na yeye ayazoaye majivu ya huyo ng'ombe atazifua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; na jambo hili litakuwa amri ya milele, kwa wana wa Israeli, na wa mgeni akaaye kati yao. 11 Mtu agusaye maiti ye yote atakuwa najisi muda wa siku saba; 12 naye atajitakasa kwa yale maji siku ya tatu, na siku ya saba atakuwa safi; lakini kama hajitakasi siku ya tatu, ndipo na siku ya saba hatakuwa safi. 13 Mtu awaye yote agusaye maiti wa mtu aliyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ukali juu yake bado. 14 Hii ndiyo amri, mtu afapo ndani ya hema; kila mtu aingiaye ndani ya hema hiyo, na kila mtu aliye humo hemani, atakuwa najisi muda wa siku saba. 15 Na kila chombo kilicho wazi, kisichofungwa na kifuniko, ni najisi. 16 Kisha mtu ye yote huko nje shambani atakayemgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga, au mfupa wa mtu, au kaburi, atakuwa najisi muda wa siku saba. 17 Na kwa huyo aliye najisi watatwaa katika majivu ya kuchomwa kwake hiyo sadaka ya dhambi, na maji ya mtoni yatachanganywa na majivu katika chombo; 18 kisha mtu mmoja aliye safi atatwaa hisopo, na kuitia katika hayo maji naye atayanyunyiza juu ya hema, na juu ya vyombo vyote, na juu ya watu waliokuwapo, na juu yake yeye aliyeugusa mfupa, au mtu aliyeuawa, au mzoga, au kaburi; 19 na yule aliye safi atamnyunyiza huyo aliye najisi siku ya tatu, na siku ya saba; na katika siku ya saba atamtakasa; naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa safi jioni. 20 Lakini mtu atakayekuwa najisi, naye hataki kujitakasa, mtu huyo atakatiliwa mbali katika mkutano, kwa sababu amepatia unajisi mahali patakatifu pa Bwana; hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake; yeye yu najisi. 21 Nayo itakuwa amri ya sikuzote kwao; na yeye anyunyizaye maji ya farakano atazifua nguo zake; naye ayagusaye hayo maji ya farakano atakuwa najisi hata jioni. 22 Na kitu cho chote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hata jioni.

Utaratibu au kanuni ya utakaso ulifanya kazi kuu mbuli: ilihusika na kutimiliza kanuni au utaratibu wa kutakasa au kusafisha kwa ajili ya mazingira ambayo yalikuwa yanahatari ya kuwapelekea kuitia unajisi sheria, na ilikuwa pia inaelekeza kanuni na utaratibu wa utakaso wa Hekalu la wateule. Kwa kuwa kanisa potovu halikuzielewa sheria za Agano la Kale lenye maagizo haya, na kwa ajili hii, mamilioni ya watu wamekufa kabla ya kipindi chao cha kuzaliwa kwa ajili ya kuzivunja sheria na amri hizi, vifo vilivyotokana na ujinga na magonjwa.

 

Kumbukumbu la Torati 22:9-11 Usipande shamba lako la mizabibu aina mbili za mbegu; yasije yakaondolewa matunda yote, mbegu ulizopanda na maongeo ya mizabibu yako. 10 Usilime kwa ng'ombe na punda wakikokota jembe pamoja. 11 Usivae nguo iliyochanganyikana sufu na kitani pamoja.

Sheria hizi zinazohusu usafi wa mbegu na aina zake zimeelezewa kwa kina kwenye jarida la Torati na Amri ya Tano (Na. 258) [Law and the Fifth Commandment (No. 258)].

 

Ukiukaji wa sheria hii kwa kundandikiza wanyama au kupanda mbegu za aina mbalimbali ni jambo linaloleta mkanganyiko. Mikakati ya makusudi ya kufanya mambo haya na kufanya mambo mengine mengi kunafanyika sana siku hizi.

 

Makatazo dhidi ya ulaji wa damu

Kwa hiyo damu ni uhai na ulaji wa damu ni jambo linalohatarisha uhai kwa kiasi kikubwa sana.

Mambo ya Walawi 17:10-16  Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake. 11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. 12 Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aketiye kati yenu asile damu. 13 Mtu ye yote aliye wa wana wa Israeli, au wa hao wageni wakaao kati yenu, ambaye amemshika mnyama, au ndege ambaye huliwa, katika kuwinda kwake; atamwaga damu yake, na kuifunika mchanga. 14 Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali. 15 Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi. 16 Lakini kwamba hazifui, wala haogi mwili, ndipo atakapochukua uovu wake.

Tendo la kushindwa kudumu su kuzitii Sheria za Mungu kunapelekea mtu huyo kupata adhabu.

 

Masuala makuu ya sheria hizi huashiria aina ya ibada ambayo ilikuwa inafanyika kwenye ulimwengu wa kipagani wa kale. Tunajua na kujionea sasa kwamba imani au dini inayokumbatia mafundisho ya Utatu ya Wadruidi, Wacelti na Waaryan kwa ujumla wao, ambapo utoaji sadaka za wanadamu ulikuwa unafanyika na grovusi zilikuwa zinachafuliwa, au kuvaliwa na korodani za wanadamu na damu (soma jarida la Chanzo Cha Krismas na Easter (Na. 235) [The Origin of Christmas and Easter (No. 235)]. Itikadi ya kizodiaki, kama dini au imani inayojihusisha ma masuala ya kuadhimisha au kutazama nyakati, haiku kwenye utaratibu au maagizo ya kalenda ya Biblia. Dhana na kazi ya wapiga bao iko tofauti sana na ile ya Urimu na Thumimu, na ilikuwa ni mojawapo ya kazi za kichawi ama ulozi.

 

Uasi

Mungu anatutaka tutii na anapenda tufanye hivyo, na wala hapendezwi na sadaka. Kuasi kunafananishwa na dhambi ya uchawi (1Samweli 15:22-23) kwa kuwa kunaanzisha hali ya kupinga mapenzi ya Mungu, kama tunavyoona kwenye Hesabu 16:1-50. Andiko hili linaelezea kuhusu uasi wa Kora, na ambalo limefafanuliwa kwa kina kwenye jarida la Torati na Amri ya Tano (Na. 253) [Law and the First Commandment (No. 253)].

 

Mungu aliushughulikia uasi huu kwa namna mbili. Hatua ya kwanza haikusilikizwa wala kuogopwa, na umaarufu au umuhimu wake ulikuwa hatarini kuharibiwa miongoni mwa watu. Huduma yote ya kikikuhani ilitengwa mbali wakati huu, hadi alipokuja Masihi na huduma ya kikuhani ya Melkizedeki. Na ndipo wateule watahudumu huduma hii ya kikuhani milele baada ya amri ya Melkizedeki, na Mungu amesema kwamba kutakuwa na miungu wadogo, wana wa Yeye Aliye Juu, na wote miongoni mwao, na Maandiko Matakatifu hayawezi kutanguka (Zaburi 82:6-7; Yohana 10:35).

 

Kwenye Hesabu 17 tunaona Haruni akichaguliwa kufanya huduma ya kikuhani katika makabila kumi na mawili na akitumika chini ya Masihi, na kisha Lawi anafanya mahala pake kama sehemu ya ukuhani mkuu kwa Wamataifa, na ulimwengu mzima wote utakuwa ni sehemu ya kufanyia ibada za Waisraeli (Ufunuo 7:4-8).

 

Mfumo wa maagizo ya sheria za Mungu umeanzishwa kwenye taifa ambalo kiongozi wake ni kama mwakilishi wa Mungu. Kiongozi ana wawakilishi zaidi, na mikononi mwao kuna sheria na hukumu zilizowekwa.

 

Kuanzishwa kwa utaratibu na mfumo wa makosa ya jinai na humuku zake

Kila moja ya sheria hizi imewekewa hukumu ya kifo kwa anayeivunja, na adhabu au hukumu hii haileti madhara au matokeo yanayopendelea au ubaguzi wa kihukumu. Mungu anapendezwa na rehema na haki. Kristo alionyesha jinsi hukumu hizi zilivyopaswa kusimamiwa. (Yohana 8:7). Hukumu haifai ifanyike kwa machafuko na mzozo wa kundi kubwa la watu. Na wala haipaswi hukumu ya kifo itolewe kwa upendeleo au kimaonevu, kama tunavyojionea kwenye amri alizotupa Masihi kwa mfano aliotuomysha kwa kesi ya mwanamke aliyefumaniwa na uzinzi (Yohana 8:1-11).

 

Kwenye mfano huu, Masihi anaonyesha tafsiri halisi ya sheria. Ni kwa kuzivunja mara nyingi sheria hizi ndipo hukumu ya kifo itekelezwe, au wakati amri ya sita inapokuwa imevunjwa kwa mazingira fulani na mahsusi, kwa kuwa torati inaruhusu kuyakatiza maisha ya mtu kwa sababu fulani na kwa mazingira yake fulani muafaka.

 

Utoaji mimba

Tendo la kutoa mamba ni dhambi inayotokana na kuvunja amri ya sita, isipokuwa ni kwa mazingira fulani. Mazingira yanayoongelewa hapa ni yale yanayoonekana kusababisha uvunjifu wa sheria nyingine hasa inavyodhihirika kwamba kitoto kichanga kinaweza kusababisha madhara ya mzazi, ndipo kitoto hiki kichanga kinaweza kuidhinishiwa kifo.

 

Hii inaashiria amri ya sita, na amri ya sita inafuatia baada ya ile ya tano nah ii inaitafsiri ile ya juu yake, yaani ya tano. Kwa hiyo, motto hawezi kuruhusiwa amuue mzazi wake, jambo ambalo lingekuwa ni kinyume kabisa na Amri za Mungu. Mri sita za kwanza zinahusika na kumpa mtu wajibu wake kwa Mungu na kwenye familia za kwenye jamii yake, akiwa ni muumbaji wa wazazi. Amri nyingine tano za mwisho zinahusika na uhusiano au mwingiliano katika jamii. Hakuna mtoto anayeruhusiwa kumdhuru au kumsababishia kifo mzazi wake kwa kumdhuru kwa namna yoyote ile.

Kutoka 21:15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.

 

Kwa ajili hii ndopo utoaji mamba unaporuhusiwa kwa mujibu kabisa wa sheria au Torati ya Mungu kwa lengo la kuokoa uhai wa mama yake.

 

Madhara ya kuharibika mimba

Adhabu ya kutoka au kuharibika kwa mamba yanayotokana na machafuko yanayodaiwa kuwa ni kuharibika, kama ilivyoelekezwa kwenye mahakama ya chi husika.

Kutoka 21:22-25 Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema. 23 Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai, 24 jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, 25 kuteketeza kwa kuteketeza, jeraha kwa jeraha, chubuko kwa ajili ya chubuko.

 

Tendo la kukataa kuja mahakamani, na utengenezaji wa mazingira ya kutoka kwa mambo mengine yote yanayofuatiia, yanapaswa yaclukuliwe kwa kuhukumiwa kwa hukumu ya haki ya mtu aliyeiharibu. Kwa hiyo, sehemu zote mbili zinapaswa zifungamanishwe na mahakama na maamuzi yake, na utoaji wowote uliosababishwa ama na sehemu ya adhabu itahukumiwa kama ni adibisho sawa na uharibifu uliotokea. Hii ni kwa mujibu wa sheria za nchi husika kwa kuwa imeandikwa: “usimtukane elohim wala kumnenea mabaya mkuu wa watu wako.”

 

Uuaji au Kuua

Tendo la kuchukua uhai wa mtu pasipo sababu za kisheria ni uuaji. Torati inaelezea kwa kutoa mifano kadhaa na mazingira na sababu ambazo kwazo mtu anaweza kuuawa. Aina yoyote ya utekelezaji wa kuchukua uhai wa mtu kinyume cha sheria ni uuaji, ambao unaelezewa na kukatazwa na amri hii ya sita kwa kusema kuwa “Usiue,” na ni jambo linalojulikana vema na maana yake kuwa ni “Usiue”

 

Tendo hili la kutwaa uhai wa mtu sio tu kwamba limekatazwa, bali limeharamishwa kabisa kwa mujibu wa sheria na kwa mifano kadhaa ya namna fulani, kama inavyoonyeshwa hapo juu. Zaidi sana ni kwamba, aina ya makosa haya ya kihalifu yanaendana na viwango vyake fulani vya kutendea kazi kwa mujibu wa sheria. Kuivunja amri hii ya sita hukumu yake ni kuuawa, wakati kwamba kama mtu atakuwa anarudiarudia kuzivunja kwa makusidu amri nyingine zilizobaki ndipo anaweza kuhukumiwa adbabu hii ya kifo, lakini ni kwamba sio kila amri hizi zinaendana na hukumu hii ya kifo kwa anayeivunja kwa mujibu wa mfano wa mwisho (soma Hesabu 15:32-36).

 

Sheria ya ndoa

Taifa linahesabiwa kwa ajili ya vita, kwa mujibu wa sheria (Hesabu 26:2).

 

Mfalme anayechaguliwa kuwaongoza Israeli anatakiwa atoke miongoni mwa ndugu zao na asiwe mgeni. Pia anatakiwa asijifanyie farasi wake kuwa wengi, na wala asiwe mwenye kuwafanya ndugu zake arudi Misri ili wakamchukulie farasi wengi na kumlimbikizia. Na pia asiwe ni mtu mwenye kujikusanyia na kujilimbikizia wake wengi, au mtu asiyeyajua au kupenda kuyashika maneno ya Torati hii ya Mungu (Kumbukumbu la Torati 17:14-20; Mhubiri 5:9; Isaya 32:17; pia soma jarida la Torati na Amri ya Tano (Na. 258) [Law and the Fifth Commandment (No. 258)].

 

Mfalme atatawala sawa na maagizo na mapenzi ya Mungu hata katika kipindi cha utawala wa Masihi, ambacho itakayotawala itatoka Sayuni.

Isaya 2:2-5 Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. 3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. 4 Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. 5 Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.

 

Maisha yote yanaendana kwa kufuatana na kutii Torati ya Mungu (soma Kumbukumbu la Torati 7:1-5).

 

Mamlaka na uhalali wa kuandaa vita

Mamlaka ya kuandaa vita yamewekwa kwa viongozi wan chi, na viapo vya mataifa vinahusika na jambo hili na vinafungamanishwa. Mungu alisababisha mapatilizo kwa ajili ya kushindwa kwao kupandilia vita kwa utaratibu mzuri na unaotakiwa (soma Hesabu 21:1-5).

 

Kutotii na kutoamini au ukosefu wa imani katika taifa kuliwasababishia kufanya makosa ya serafi wa shaba aliyejulikana kama njoka. Serafi huyu au njoka wa shaba aliwekwa ili kuwasaidia kuinua kiwango cha imani yao Israeli ilipokuwa imepungua au kuyeyuka, lakini hakukuwa na msukumo wa kimwili na hakukuhitajika kitu kama hicho.

 

Mara nyingi Bwana hulazimisha maamuzi ili kwamba adui aweze kutiwa kwenye mikono ya taifa, ingawaje hawapendi kwenda vitani, na ndivyo itakavyokuwa hata katika siku za mwisho. Mataifa watajikusanya kwenye bonde la kukata maneno wakisimama kinyume na Masihi, na huko ndiko wataangamizwa.

 

Hesabu 31:1-54 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Sura hii inaelezea vita na mapigano zaidi na matayarisho mazuri nay a umakini yaliyoweka tahadhari ya kukiuka mipangilio yake na adhabu kwa atakayefanya hivyo.

 

Watu pekee waliomudu kuingia kwenye mkutano wa Israeli walikuwa ni wanawake elfu thelathini na mbili ambao walikuwa hawajawahi kumjua mwanaume bado. Mfano kama huu tunauona ukitendeka pia kwa Gideoni, wakati idadi kama hii hii ilijitokeza kutoka kwa watu wengine kuchujwa na akabakia na zaidi ndogo tu ya watu mia tatu waliochaguliwa wakapigane vita na mataifa. Hakuna aina yoyote ya unajisi iliyotakiwa ili watu waweze kuingia kwenye mkutano wa Israeli, wala hakuna aina yoyote ya miungu wa uwongo na wala hakuna magonjwa, bali ni walio katika hali ya uwanawali tu. Mifano hii yote ni ashirio la watu wote kutoka mataifa yote walioyafua mavazi yao na kuyafanya meupe kwa damu ya mwana kondoo ambao pia ni wanawali mabikira wa kiroho, ambao wanamjua Mungu Mmoja tu na ambao ni mabibi arusi wa Kristo.

 

Huduma ya vita na utaratibu wa kuhesabu askari

Hakuna mtu aliyelazimishwa kwenda vitani akiwa kwenye kipindi cha mwaka mmoja cha ndoa yake, na wala hakulazimishwa kwenda kupigana wakati akiwa hapendi kwenda na akiwa hana utashi moyoni mwake (soma Kumbukumbu la Torati 20).

Kumbukumbu la Torati 24:5 Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yo yote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.

 

Na hakuna aliyeruhusiwa kujiunga na mapigano au jeshi akiwa na umri wa chini ya miaka ishirini, na hakuruhusiwa hata kupelekwa vitani akiwa hapendi.

 

Hesabu 1:1-46 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Sura hii inaelezea juu ya jinsi ya kuwahesabu Israeli, zoezi ambao lilifanyika siku ya kwanza ya mwezi wa Pili katika mwaka wa pili baada ya kuondoa kwao nchini Misri.

 

Wale waliohesabiwa na wakawa hawataki kwenda vitani ni sehemu ya wenyeji ambao hawamo kwenye makundi yaliyoorodheshwa hapo juu na ambao waliachwa nje ya mchakato wa mapigano, na ambao wanaweza kutumika kwa kutumikishwa kazi zote za shokoa na hasa kwa zile zinazohusika na ubebaji wa makusanyo ya michango, inayochangwa kwa ajili ya kumpelekea mfalme au zilizoamriwa na dola (soma 1Wafalme 5:13ff.). Israeli wote ni lazima wajihudhurishe wakati inapopigwa mbiu ya kuwataka kufanya kazi na viongozi wao. Wana namna fulani na maalumu ya kupita na amri ya vita.

 

Hesabu 10:1-36 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Tarummeta zilitengenezwa kwa ajili ya kuzipiga mbiu za namna mbalimbali ili kuwafanya Israeli wakusanyike pamoja kwa ajili ya kusudi lolote litakalohitajika. Fungu hili la maandiko linaelezea pia utaratibu wa jinsi ya kupita mbele kufanywa na makabila yote. Taifa la Israeli lilikuwa chini ya usimamizi na uangalizi wa Malaika wa Bwana, Masihi wao, kwa usiku na kwa mchana, kama inavyoonekana kwenye Hesabu 13; na tumeifafanua vizuri kwenye jarida letu la Torati na Amri ya Kwanza (Na. 253) [Law and the First Commandment (No. 253)]. Wanaume walitumwa wakaipeleleze Nchi ya Ahadi ya Kanaani. Ripiti waliyoileta ilisema kwamba nchi ilikuwa ni njema mno nay a ajabu, ila walikuwa wanawaogopa wenyeji wanaoikaa nchi hiyo. Bwana Mungu aliwapa ushindi bali wakuu wa makabila yao walipoteza haki yao ya kuingia kwenye Nchi ile ya Ahadi kwa ajili ya woga na kutokuamini kwao.

 

Oparesheni za kawaiada za vita

Imeruhusiwa kuua kwa ajili ya kulilinda taifa lake mtu na kuihami nyumba au familia yake. Mungu humsaidia yule anayejilinda mwenyewe. Kunaorodha ya aina mbalimbali ya watu walioondolewa na wasiohesabiwa (soma jarida la Kumbukumbu la Torati (Na. 201) [Deuteronomy 20 (No. 201)].

Kumbukumbu la Torati 20:1-20 inasema: Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri. 2 Na iwe, msongeapo mapiganoni, kuhani na akaribie na kusema na watu, 3 awaambie, Sikizeni, enyi Israeli, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu mioyo yenu na isizime; msiche, wala msiteteme, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao; 4 kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi. 5 Na maakida na waseme na watu, na kuwaambia, Ni mtu gani aliye hapa aliyejenga nyumba mpya, wala hajaiweka wakfu? Aende akarudi nyumbani kwake, asije akafa mapiganoni, ikawekwa wakfu na mtu mwingine. 6 Ni mtu gani aliye hapa aliyepanda shamba la mizabibu, wala hajatumia matunda yake? Aende akarudi nyumbani kwake asije akafa mapiganoni, yakatumiwa na mtu mwingine matunda yake. 7 Ni mtu gani aliye hapa aliyemposa mke wala hajaoa? Aende akarudi nyumbani kwake asije akafa mapiganoni, huyo mwanamke akaolewa na mume mwingine. 8 Tena maakida na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake. 9 Itakuwa hapo watakapokwisha wale maakida kusema na watu, na waweke majemadari wa majeshi juu ya watu. 10 Utakaposongea karibu ya mji kwenda kupigana juu yake, ndipo utakapowapigia ukelele wa amani. 11 Itakuwa utakapokujibu kwa amani, na kukufungulia, ndipo watu wote watakaoonekana humo watakufanyia kazi ya shokoa, na kukutumikia. 12 Na kwamba hautaki kufanya amani nawe, lakini utafanya vita juu yako, ndipo uuhusuru; 13 na Bwana, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga; 14 lakini wanawake na watoto, na wanyama wa miji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka kwako; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana, Mungu wako. 15 Utaifanyia vivyo miji yote iliyo mbali sana nawe, isiyokuwa miji ya mataifa haya. 16 Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho; 17 lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru Bwana, Mungu wako; 18 wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya Bwana, Mungu wenu. 19 Wewe utakapohusuru mji siku nyingi kwa kufanya vita juu yake, upate kuutwaa, usiangamize miti yake kwa kupeleka shoka juu yake, kwani utaweza kula matunda yake; wala usiiteme, kwa maana huo mti wa kondeni, je! Ni mtu, hata ukauzuie? 20 Ila miti uijuayo si miti ya kuliwa iangamize, na kuitema; ukajenge maburuji juu ya mji ufanyao vita juu yako, hata uanguke.

 

Nchi lazima ilindwe na mazingira yanapaswa yalindwe pia. Ni wale wanaoabudu miungu mingine tu (mbali na Bwana Mungu wa Israeli) ndio wanatakiwa waangamizwe kabisa na pasipo na huruma.

 

Maovu na makosa ya jinai vitani

Tendo la kuwaangamiza waabudu sananmu halimo nwenye orodha ya makosa ya jinai ya kivita, kwa mujibu wa torati ya Mungu. Wanapaswa kuonywa kwanza na kupewa muda ambao utakuwa ni fursa yao ya kutubu, na kisha ndipo waangamizwe kama wakikataa kutubu. Iwapo kama tumepewa amri ya kuitwaa na kuikalia nchi yao, au kama hatupendi kufanya mahusiano nao au kuwashughulikia kwa kuwaangamiza wakiwa kama taifa, basi tunatakiwa tuwaache wawe peke yao kabisa.

 

Iwapo kama hatutawaangamiza na badala yake tunaishi kwenye nchi yao pamoja nao, ndipo sisi kama taifa kunauwezekano mkubwa sana wa kulazimika kuingia kwenye mtindo na imani yao ya kuabudu sanamu na kulisababishia taifa letu liangamizwe kwa hasira kali ya Mungu. Ibada ya sanamu ni jambo lililokatazwa na kuharimishwa kabisa kufanywa na Israeli na hata kwa mgeni aliye kwenye malango yao, na ni chukizo kuu sana mbele za Mungu (Kumbukumbu la Torati 7:22-26).

 

Wakati taifa linapokuwa linatubu linatakiwa kitendewe kama ndugu na kwa hiyo linatakiwa lijinyenyekeshe kwa Mungu.

 

Waamaleki na vita kati ya mataifa

Unabii wa Balaamu ulionyesha hatima ya mataifa yanayoinuka kinyume na Israeli. Amaleki walikuwa ni wa kwanza kukutananao kati ya mataifa mengine yaliyofuatia, lakini mwisho wake ilikuwa ni kuangamia milele, kama ilivyotokea kwa Wakeni ambao pia waliangamia milele. Kipindi chao cha mwisho kilikuwa cha matatizo ya jinsi ya kujiokoa kama tunavyoona wakati Balaamu aliposema pia kwamba “Ninani atakayeishi (auu kumudu kuishi) wakati Mungu akifanya hivi?” (soma Hesabu 24:20-24). “Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu, Nazo zitamtaabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha, Yeye naye atafikilia uharibifu” (aya ya 24). Kwenye nakala za maandiko ya Waashuru, na maandiko ya baadae yaliyoandikwa mapema kwa Kiebrania cha kale sana yanayoelezea mambo ya uzao na nasaba ya mataifa, yanamtaja Kitimu kuwa mwana Yavani, mwana wa Yafeti, (Mwanzo 10:4). Hapo mwanzoni nchi ya Kitimu/Shitimu ilijulikana kama Cyprus na ilikuwa ukanda wa pwani ya kaskazini mwa bahari ya Mediterranean. Watu waake walichanganyika pia na Wafoeniki, ambayo ilikuwa ni pia ni sehemu ya kale ya Bahari ya Mabwana (Sea Lords) aambao walitawala pia kutoka Cyprus.

 

Vita hivi vya siku za mwisho ni masalio ya vita vilivyopiganwa kati ya Israeli na Amaleki siku za kale hata kabla hawajaingia kwenye Nchi ya Ahadi (Kutoka 17:8-16).

Kutoka 17:8-16 inasema: Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. 9 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. 10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. 11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. 12 Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. 13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. 14 Bwana akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. 15 Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi; 16 akasema, Bwana ameapa; Bwana atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.

 

Amaleki waliwapiga watu dhaifu na wasiojiweza na hawakuwa na hofu ya Mungu kabisa (Kumbukumbu la Torati 25:17-19).

 

Muungano wowote unasimama pamoja kwenye Zaburi 83. Matawi yote ya mataifa haya walijiunga pamoja na kufanya hila wakinuia kuwaangamiza Israeli. Kulikuwa na jumla ya mataifa kumi kwa ujumla wao, ambao waalifanya muungano wa wafalme. Waedomu na Waishimaeli, Wamoabu na Wahagiri, Wageba na Waamoni na Waamaleki, Wafilisti na wenyeji wa Tiro, na Waashuru walijiunga nao (Zaburi 83:5-8). Mungu akawaamuru wafanye maangamizi mzkuu (soma 1Samweli 15:2,3; 28:18), lakini haikufanyika hivyo, na badala yake ilikuwa ni nusura kabisa waangamize Yuda (soma Esta 3:7-9, 10). Kwa yote haya, busara –kama ya kuzishika amri za Mungu –ambazo ni ufunguo au chanzo cha kuyarefusha maisha, na ni kwa uweza wa Mungu tu Israeli wanalindwa (soma Mithali 4:1-27).

 

Jinsi ya kumtendea mateka wa kike

Mwanamke aliyetekwa vitani anaweza pia kuchukuliwa na kufanywa kuwa mke na anahesabiwa kuwa ni sehemu ya taifa la Israeli, haipaswi watumiwe kwa shughuli za kikahaba, au kuwatumia kwa matumizi mengine yasiyomema na stahiki. Na iwapo kama atachukuliwa na kufanywa mke hairuhusiwi kumuuza awe mtumwa.

Kumbukumbu la Torati 21:10-14  Utakapokwenda vitani kupigana juu ya adui zako, na Bwana, Mungu wako, awatiapo mikononi mwako, nawe uwachukuapo mateka, 11 ukaona kati ya mateka mwanamke mzuri, ukafanya tamaa kwake, ukawaza kumtwaa kuwa mkeo; 12 ndipo umchukue kwenu nyumbani kwako, naye atanyoa kichwa, akate na kucha; 13 avue na mavazi ya uteka wake akae nyumbani mwako, awakalie matanga babaye na mamaye mwezi mzima, kisha uingie kwake uwe mumewe, naye awe mkeo. 14 Tena utakapokuwa huna furaha naye, mpe ruhusa aende atakako; lakini usimwuze kabisa kwa fedha, usimfanye kama mtumwa, kwa kuwa ulimtweza.

 

Jinsi ya kuigawa Nchi

Hesabu 33:1-56 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Safari ya kutoka Misri ndiyo inayoelezewa hapa.

 

Hesabu 32:1-42 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Kwa hawa Manase wa pili, Reubeni na Gadi walipewa urithi nje ya milki ya Israeli, ila bado walitarajiwa kuwa watakuwa wanajiunga ma wenzao kupigana inapotokea vita. Na hivi ndivyo itakavyotokea pia siku za mwisho wakati makosa ya kutoshiriki yatakapotoa taswira yenye maana sawa na kutengana na Israeli chini ya utawala wa Masihi.

 

Hesabu 34:1-29 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Mipaka ya nchi imeelekezwa kwa kina kwenye sura hii. Ardhi au nchi imegawanywa kwa kupigiwa kura kwa umilikaji wa makabila haya. Kwa hiyo mgawanyo wan chi unaendana kwa mujibu sawa na uongozi ulivyo wa kila kabila, na inafanyika kwa kuzingatia na idadi ya makabila yalivyo. Mipaka ya nchi imepanuliwa katika siku za mwisho hadi kufika kwenye Mto Mkubwa wa Frati na kuelekea upande wa mashariki kutoka palestina. Mataifa ya Yordani yamemezwa na kujumuishwa na taifa la Israeli, au limefanyika kuwa ni moja ya majimbo yake (Isaya 11:1-16).

 

Milki na alama ya mipaka

Suala la umiliki na alama ya mipaka ni moja ya mambo yanayohusika na usalama wa maisha ya familia na makabila. Ni laana kuiondoa, au kuongeza vipimo vyake kwa kusogeza mbele, au kuingia na kulitwaa shamba la yatima, “Kwakuwa Mwokozi wao yu Mwenyenguvu na atawapigania” (Kumbukumbu la Torati 27:17; Ayubu 24:2; Mithali 22:28; 23:10,11; Hosea 5:10). Mambo haya yanashughulikiwa na kufafanuliwa kwa kina kwenye majarida yetu ya Torati na Amri ya Nne (Na. 256) pia na lile la Torati na Amri ya Tano (Na. 258) [Law and the Fourth Commandment (No. 256) and also Law and the Fifth Commandment (No. 258)].

 

Miji ya Walawi ya kujipatia riziki zao

Makuhani walipaswa kupewa miji ambayo kwayo wangeishi na kujipatia riziki zao, na utoaji wa miji hii utakuja fanyika tena kwenye kipindi cha marejesho mapya kitakapokuja. Sambamba na hilo, Dani watachukua milki yao ambayo itakuwa ni huduma ya uhakimu kuwahukumu Israeli (Mwanzo 49:16), na wataathiri pia ugawanyaji huu.

Hesabu 35:1-8 inasema Kisha Bwana akanena na Musa katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko, akamwambia, 2 Uwaagize wana wa Israeli wawape Walawi miji wapate mahali pa kukaa, katika milki yao; pamoja na malisho yaliyoizunguka hiyo miji kotekote mtawapa Walawi. 3 Hiyo miji watakuwa nayo ili wakae humo, na malisho watakuwa nayo kwa wanyama wao wa mifugo, na kwa mali zao, na kwa wanyama wao wote. 4 Na yale malisho ya miji mtakayowapa Walawi, ukubwa wake utakuwa tangu ukuta wa mji kupima kiasi cha dhiraa elfu pande zote. 5 Nanyi mtapima hapo nje ya mji upande wa mashariki dhiraa elfu mbili, na upande wa kusini dhiraa elfu mbili, na upande wa magharibi dhiraa elfu mbili, na upande wa kaskazini dhiraa elfu mbili, huo mji ulio katikati. Hayo ndiyo yatakayokuwa kwao malisho ya miji. 6 Na hiyo miji mtakayowapa Walawi, itakuwa miji sita ya makimbilio, mtakayoweka kwa ajili ya mwenye kumwua mtu, ili akimbilie huko; pamoja na hiyo mtawapa miji arobaini na miwili zaidi. 7 Miji yote mtakayowapa hao Walawi jumla yake itakuwa miji arobaini na minane; mtawapa miji hiyo pamoja na malisho yake. 8 Tena katika miji mtakayotoa ya hiyo milki ya wana wa Israeli, katika hao walio wengi mtatwaa miji mingi; na katika hao walio wachache mtatwaa miji michache; kila mtu kama ulivyo urithi wake atakaourithi, atawapa Walawi katika miji yake. (pia soma Mambo ya Walawi 25:32-34)

 

Mauaji na miji ya makimbilio

Hesabu 35:9-15 inasema: Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, 11 Ndipo mtajiwekea miji iwe miji ya makimbilio kwa ajili yenu; ili kwamba mwenye kumwua mtu, pasipo kukusudia kumwua, apate kukimbilia huko. 12 Na hiyo miji itakuwa kwenu kuwa makimbilio, kumkimbia mwenye kutwaa kisasi, ili asiuawe mwenye kumwua mtu, hata atakaposimama mbele ya mkutano ahukumiwe. 13 Na hiyo miji mtakayowapa itakuwa kwenu ni miji sita ya makimbilio. 14 Mtawapa miji mitatu ng'ambo ya pili ya Yordani, na miji mitatu mtawapa katika nchi ya Kanaani; miji hiyo itakuwa ni miji ya makimbilio. 15 Miji hiyo sita itakuwa miji ya makimbilio kwa ajili ya wana wa Israeli, na kwa ajili ya mgeni, na kwa ajili ya huyo aketiye kati yao hali ya ugeni; ili kila amwuaye mtu, naye hakukusudia kumwua, apate kukimbilia huko.

Mauaji yanayofanywa kwa ajali na pasipo kukusudia ndiyo sababu ya kutengwa kwa miji hii, na watu wanatakiwa kulindwa dhidi ya mwenye kujilipiza kisasi kwa kumuua. Hata hivyo, kunapofanyika mauaji yaliyipangwa tangu mwanzo, kuuawa kwa muuaji ndiyo tukio la mwisho linalopaswa kufanyika na ndivyo ilivyogizwa ifanyike na Torati.

Hesabu 35:16-21 inasema: Lakini kama alimpiga kwa chombo cha chuma, akafa, ni mwuaji huyo; mwuaji hakika yake atauawa. 17 Na kama alimpiga kwa jiwe lililokuwa mkononi mwake, ambalo kwa hilo humkini mtu kufa, naye akafa, yeye ni mwuaji; huyo mwuaji lazima atauawa. 18 Au kama alimpiga kwa chombo cha mti kilichokuwa mkononi mwake ambacho kwa hicho humkini mtu kufa, naye akafa, ni mwuaji huyo, mwuaji lazima atauawa. 19 Mwenye kutwaa kisasi cha damu ndiye atakayemwua mwuaji; hapo atakapokutana naye, atamwua. 20 Tena kwamba alimsukuma kwa kumchukia, au kwamba alimtupia kitu kwa kumvizia, hata akafa; 21 au akampiga kwa mkono wake kwa kuwa ni adui, naye akafa; yeye aliyempiga lazima atauawa; yeye ni mwuaji; mwenye kutwaa kisasi cha damu atamwua mwuaji, hapo atakapokutana naye.

 

Mauaji yaliyotokea kwa bahati mbaya

Hesabu 35:22-34 inasema: Lakini ikiwa alimsukuma ghafula pasipo kumchukia; au akamtupia kitu cho chote pasipo kumvizia, 23 au kwa jiwe liwalo lote, ambalo kwa kupigwa kwalo humkini mtu kufa, asipomwona, akamtupia hata akafa, naye hakuwa adui yake, wala hakumtakia madhara; 24 ndipo mkutano utaamua kati ya huyo aliyempiga mtu na huyo atakayetwaa kisasi cha damu, kama hukumu hizi zilivyo; 25 nao mkutano utamwokoa yule aliyemwua mtu na mkono wa mwenye kutwaa kisasi cha damu; tena mkutano utamrejeza katika mji wake wa makimbilio, aliokuwa anaukimbilia; naye atakaa humo hata kifo chake kuhani mkuu, aliyepakwa mafuta kwa mafuta matakatifu. 26 Lakini kama mwenye kumwua mtu akienda wakati wo wote kupita mpaka wa huo mji wa makimbilio, alioukimbilia; 27 na mwenye kutwaa kisasi cha damu akamwona, naye yu nje ya mpaka wa mji wake wa makimbilio, na mwenye kutwaa kisasi cha damu akamwua huyo mwuaji, hatakuwa na hatia ya damu; 28 kwa sababu ilimpasa kukaa ndani ya mji wake wa makimbilio hata kifo chake kuhani mkuu lakini kuhani mkuu atakapokwisha kufa huyo mwuaji atarudi aende nchi ya urithi wake. 29 Mambo haya yatakuwa ni amri ya hukumu kwenu, katika vizazi vyenu vyote, katika makazi yenu yote. 30 Mtu awaye yote atakayemwua mtu, huyo mwuaji atauawa kwa vinywa vya mashahidi; lakini shahidi mmoja hatashuhudia juu ya mtu hata akafa. 31 Tena, msipokee fidia kwa ajili ya uhai wa mwuaji, ambaye amekuwa na hatia ya mauti; Lakini lazima atauawa. 32 Tena hamtapokea fidia kwa ajili ya huyo aliyeukimbilia mji wake wa makimbilio, apate kwenda tena kuketi katika nchi, hata kifo cha kuhani mkuu. 33 Hivi hamtaitia unajisi nchi ambayo mwakaa; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi; wala hapana sadaka itoshayo kwa ajili ya nchi, kwa ajili ya damu iliyomwagwa ndani yake, isipokuwa ni damu ya huyo aliyeimwaga. 34 Kwa hiyo msiitie unajisi nchi muiketiyo, ambayo naketi nami kati yake; kwa kuwa mimi Bwana nakaa kati ya wana wa Israeli.

Mtu akikimbilia na kufika kwenye mji wa makimbilio, ataishi humo kwa kipindi chote cha uhai wa kuhani aliye kwenye mji ule, ni sharti muhimu na la lazima kwa kila aliyeua bila kukusudia. Anapofariki kuhani aliyekuwa anasikiliza kesi na kuhukumu, au mwenye mamlaka ya kutoa hukumu kwenye mji huo wa makimbilio, ndipo yule muuaji ataruhusiwa kurudi kwenye makazi yake asilia. Kesi na mashitaka haya hayawezi kutolewa kikombozi chochote.

 

Tunajionea pia kwamba jambo lingine kuhusu suala hili limeandikwa kwenye kitabu cha Kutoka.

Kutoka 2:11-15 Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake. 12 Basi akatazama huko na huko, na alipoona ya kuwa hapana mtu, akampiga Mmisri yule, akamficha ndani ya mchanga. 13 Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, Mbona unampiga mwenzako? 14 Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana. 15 Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.

 

Tendo la kumuua mtu kwa kimvizia na pasipo kupewa ruhusa au mamlaka ya kufanya hivyo ni uvunjaji wa amri hii pia. Mji wa makimbilio uliwekwa na Musa ukiwa kama adhabu, na ni mtindo ulio sawa tu na kama ilivyoagiza Sheria ya Mungu au Torati. Hakudumu kubakia huko hadi kufikia kifo cha kuhani (kwa kuwa Yethro alikuwa ndiye kuhani wa Midiani) bali Mungu alimuita Musa na kumtuma aende Misri. Na kwa hiyo Musa alikuwa kila mara mnyenyekevu kwenye sheria na amri za Mungu, hata alipokuwa huko Misri, hata hivyo, alisamehewa kwa ajili ya kutozikua kwake vizuri kwa muda kitambo.

 

Kifo kilichotokana na sababu zisizojulikana

Kumbukumbu la Torati 21:1-9 inasema: Aonekanapo mtu ameuawa katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, kuimiliki, amelala kondeni, wala haijulikani ni nani aliyempiga; 2 na watoke nje wazee wako na waamuzi wako, nao wapime hapo mpaka miji iliyomzunguka huyo aliyeuawa; 3 na iwe, mji ulio karibu na yule aliyeuawa, wale wazee wake mji huo watwae mtamba katika kundi la ng'ombe, ambaye hajafanya kazi, wala hajakokota jembe la nira; 4 wazee wa mji huo na wamshushe yule mtamba mpaka bonde lenye maji ya mtoni, lisilolimwa wala kupandwa, wakamvunje yule mtamba shingo yake humo bondeni; 5 nao makuhani wana wa Lawi wasongee karibu, kwa kuwa ndio aliowachagua Bwana, Mungu wako, wamtumikie, na kubariki katika jina la Bwana na kila neno lishindaniwalo, na kila pigo, litakuwa kwa kufuata maneno yao; 6 na wazee wote wa mji ule, ulio karibu sana na yule aliyeuawa, na waoshe mikono yao juu ya huyo mtamba aliyevunjwa shingo yake humo bondeni; 7 na wajibizane kwamba, Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuiona. 8 Ee Bwana, samehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwao. 9 Ndivyo utakavyoondoa damu ya asiye makosa katikati yako, utakapofanya yaliyo sawa machoni pa Bwana.

Kutokana na maandiko haya tunaona na kujua kwamba kila mtu mmoja mmoja anawajibu mkubwa na wa aina yake machoni pa Mungu katika kuilinda haki isiharibiwe ama kupotea, na kulinda maisha na kuisimamia sheria isipindishwe ama kuhalifiwa kwenye maeneo yake. Ndio maana kuna mazingira ya kumfungamanisha mtu ndani ya sheria.

 

Ukombozi au marejesho

Ukombozi au marejesho sio matendo tu ya masuala yaliyo kwenye amri hii ya sita tu, na ambayo inawafanya watu kuielewa sheria. Hata hivyo, damu hulipwa kwa damu kwa mujibu wa amri hii ya sita. Bali kutakuwa na kipindi cha marejesho ya vitu vyote, nah ii itatokea katika kipindi cha utawala wa Masihi, ambaye mbingu ilimpokea hadi kipindi hicho. Kila roho ambayo itakuwa haijasikia unabii huu itaangamizwa wa kutolewa mbali na watu wake (Kumbukumbu la Torati 18:15-19; Matendo 3:21-23). Mesihi anafuatiwa na wanafunzi wake ambao pia ni mitume watakaoketi kwenye viti vya enzi kumi na viwili (Mathayo 19:28).

 

Ukomboaji ulifanywa kwa ajili ya uvunjaji wa amri hizi nyingine, na iwapo kama hii haitendeki ndipo huyo mwizi au mtuhumiwa aliyekamatwa atauzwa kwa ajili ya kukopmboa kitu husika. Na tangu hapo atafanyika mtumwa kwa ajili ya kufidia. Na kwa hiyo, Taifa linalazimika kutoa ajira yenye malipo ili kurejesha fidia ya mali iliyoibiwa kimakosa. Na iwapo kama mkosaji haiatumikia kifungo hiki, ndipo uhai wake utaamriwa kwa mujibu wa jinsi sheria au amri zinavyosema. Faini kwa ajili ya kukufuru au kumnenea vibaya Bwana Mungu inaendana pia na kundi (soma Kutoka 22:1-17; Kumbukumbu la Torati 22:19, 29; Hesabu 5:6-8: Mambo ya Walawi 5:14-19; 2Wafalme 3:4). Maelezo zaidi kuhusiana na mambo haya ya tozo za faini yanapatikana kwenye maandiko mengine ya sheria, kama vile majarida yetu ya.Torati na Amri ya Saba (Na. 260) na Torati na Amri ya Nane (Na. 261) [Law and the Seventh Commandment (No. 260) and Law and the Eight Commandment (No. 261)].

 

Jinsi ya kuitenda kazi Torati

Kuna sheria moja tu kwa wote.

Hesabu 15:29-31 Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lo lote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao. 30 Lakini mtu afanyaye neno lo lote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake. 31 Kwa sababu amelidharau neno la Bwana, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake.  

 

Kitendo cha kudharau mahakama na kuidharau Torati ya Mungu kunempelekea mtu kuhukumiwa kifo kwa mujibu wa mfano tuliouona mwishoni.

Kumbukumbu la Torati 17:12-13 Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia Bwana, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli. 13 Na hao watu wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena kwa kujikinai

 

Hukumu ya kifo

Mwanadamu aliumbwa kwa haiba ya mfano wa  Mungu, na yeyote atakayeimwaga damu ya mwanadamu, basi damu hiyo itadaiwa kwake na atailipa (Mwanzo 9:5-6). Hukumu ya kifo imelengwa kutolewa kwenye mazingira yake fulani (soma Mambo ya Walawi 20:1-27; 24:10-23; Hesabu 15:29-31; Kumbukumbu la Torati 17:12-13).

 

Mambo yaha yote yanafanyika ili kwamba tujifunze kumcha Mungu na kuzitii Sheria na amri zake, ili tuwe ulinzi wetu na haki yetu, na pia zifanyike kuwa ni agano letu kwenye Hekalu lake (Kumbukumbu la Torati 8:6; Kutoka 12:15-19; Mwanzo 17:14; Kutoka 3:14; Mambo ya Walawi 17:8).

 

Mtu akimlaani baba yake au mama yake hufa bila kuzaa mtoto, na hivyo kumfanya kizazi chake kinakatiliwa mbali au atakubwa na mauti (Mithali 20:20; Mathayo 15:4; Marko 7:10).

 

Hukumu ya kifo hutolewa kwa makosa yafuatayo:

·         Utekaji wa nyara kwa manufaa fulani (Kumbukumbu la Torati 24:7);

·         uzininzi (Kumbukumbu la Torati 22:22-24);

·         kumbaka kwa nguvu mwanamke aliyechumbiwa au kuolewa (Kumbukumbu la Torati 22:25-27);

·         vitendo vya ufiraji (Lev. 20:13);

·         uchawi au ushirikina au machukizo ya kutoa sadaka kwa miungu wa uwongo (Kutoka 22:18-20);

·         kuwaasi na kutowatii wazazi (Kumbukumbu la Torati. 21:18-21);

·         kuivunja Sabato (Kutoka 35:2; Hesabu 15:32-36);

·         kutoa unabii wa an mafundisho ya uwongo yanayodharau umuhimu wa kuishika na kuiheshimu Torati na amri za Mungu (Kumbukumbu la Torati 13:1-10);

·         kuidharau mahakama kwa kutotumikia hukumu zake (kumbukumbu la Torati 17: 8-13);

·         mwana aliye mwizi au mvunjaji wa maagano, au mtu aliye mwabudu sanamu, mzinzi, anayewadhulumu maskini na wahitaji, afanyaye machukizo kwa kudhulumu na ufisadi, au anayechukua riba au aina hiyo ya mapato ya aibu (Ezekieli 18:10-13).

 

Mashahidi na Mtego wa fumanizii

Hairuhusiwi mtu kutiwa hatiani hadi kuweko mashahidi wawili au watatu walioshuhudia jambo likitokea (Kumbukumbu la Torati 17:6). Hairuhusiwi kumhukumu mtu kifo na kumuua kwa ushahidi uliotolewa na mtu mmoja tu, na wala hairuhusiwi shahidi mmoja tu kutoa ushahidi dhidi ya dhambi za mwenzake na akachukuliwa kuwa ni kweli (soma Kumbukumbu la Torati 19:15). Mikono ya mashahidi ndiyo itakuwa ya kwanza kumpatiliza, au kwa maneno mengine ni kwamba, mashahidi wanatakiwa wawe ni sehemu ya wale wanaotoa mapatilizo ya hukumu ya mkosaji (Kumbukumbu la Torati 17:7).

 

Kutokana na dhana hii kwenye maandiko yanayoelezea utumiaji uwongo ili kufanikisha kumtia mtu hatiani au kukamata wengine, tunaona kwamba tendo la kumuwekea mtu mtego ni baya au machukizo kabisa, sawa tu na ilivyo kwa usingiziaji. Ni mambo yaliyotofauti kabisa na ni matedo ya namna ile ile ya dhambi inayokusidia kumchafua au kumharibia sifa zake mtu kwa kutumia mbinu ya namna nyingine.

 

Aina ya hukumu za kifo

Kuna aina mbalimbali kadhaa zinazotumika katika kumuua mtu zilizoelekezwa kwenye Bbilbia:

·         Kuchoma moto (Mambo ya Walawi 20:14; 21:9).

·         Kupiga mawe (Mambo ya Walawi 20:1, 27; 24:14; Kumbukumbu la Torati 21:21).

·         Kunyoka hadi kufa (Kumbukumbu la Torati 21:22, 23; Yoshua 8:29).

·         Kuua kwa Upanga (Kutoka 32:27, 28).

 

Utaratibu wa kutekeleza hukumu hii ya kifo inatakiwa itekelezwe hadharani ili iwe fundisho kwa wengine, na haikuwa lazima kumhukumu mtu hivi kwa kosa la kwanza, isipokuwa ni kama tu itakuwa inahusiana na uvunjifu wa amri hii ya sita.

 

Kutumia vibaya kanuni ya utoaji wa ushahidi na uendekezaji wa mapokeo ya kifarisayo ni uvunjifu na ukiukaji wa amri na sheria za kibiblia. Kwa mfano, Biblia inasema kwamba mtu asihukumiwe kifo na kuuawa kwa ushahidi wa mtu mmoja tu, lakini mapokeo haya yanasema kuwa ushahidi wa mtu mmoja unatosha kuutolea hukumu. Kila anayeyaendekeza mapokeo ya Watalmudi na kuyatumia ili kupinga maelezo yaliyotokewa wazi ya Biblia kwa ajili ya jambo hili anakuwa ametenda dhambi kubwa sana na uovu.

 

Utekelezaji usio sahihi wa hukumu hii ya kifo

Agizo au amri ya kuua, ikitolewa kwa lengo potofu tu la kuwaangamiza watu wetu, inapaswa kuligomea na kutoitekeleza.

Kutoka 1:15-16 Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; 16 akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.

Sera hii zimewahi kufanywa na baadhi ya imani fulani za kidini katika karene hii, kwa sehemu zote mbili yaani za Ulaya na Asia.

Kutoka 1:22 Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.

 

Rehema na haki

Utekelezaji wa sheria hizi unapaswa kuzingatia kanuni njema ya rehema na haki, na Kristo alituonyesha kwa bayana jinsi sheria hizi zinavyotakiwa kutekelezwa. Hukumu ya kifo—kwa mfano, inatokana na tabia ya uzinifu—haikuwa lazima, bali ilitekelezwa baada ya kuona kwamba tabia hiyo ilikuwa inarudiwa rudiwa na kwa mwonekano usioashiria kuwa mtu huyu anahofu tena na maagizo au maelekezo ya torati.

 

Kila amri inapelekea hukumu ya kifo ili kuonyesha usawa wa mamlaka ya sheria kwa kila jambo. Ni kwenye hii amri ya sita tu ndiko hukumu hii ya kifo ni ya lazima na kwa kosa la kwanza, lakini ni kwenye mazingira na hali ileile.

 

Maneno ya Kristo yanaonyesha kuwa hili ndiyo ilikuwa kusudi la sheria (Yohana 8:7). Sheria hizi zinapaswa zitekelezwe kwa kuzingatia rehema na haki, na ili kusiweko na mauaji ya kidhalimu au maonevu, au kwa kuwaendekeza wale wanaomvizia mwenzao au kumvizia ili wamkamate.

 

Kuabudu sanamu na ushiriki wa ibada zake ni mambo waliyokatazwa kabisa Israeli, au kufanywa na wageni waliowatembelea malangoni mwao wote walikatazwa kufanya hivyo na ni machukizo makuu kwa Mungu wao.

Kumbukumbu la Torati 7:22-26  Naye Bwana, Mungu wako, atayatupia nje mataifa yale mbele yako kidogo kidogo; haikupasi kuwaangamiza kwa mara moja, wasije wakaongezeka kwako wanyama wa mwitu. 23 Ila Bwana, Mungu wako, atawatoa mbele yako, atawatia mashaka, mashaka makuu, hata waishe kuangamizwa. 24 Na wafalme wao atakutilia mkononi mwako, nawe utalipoteza jina lao litoke chini ya mbingu; hapana mtu atakayeweza kusimama mbele yako, hata utakapokwisha kuwaangamiza. 25 Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako; 26 na machukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni kitu kilichoharimishwa.

 

Hukumu kwa dhambi zifanywapo na haki ya maisha au uhai kwa mujibu wa Torati

Hakuna mtoto au mwana atakayeuawa kwa ajili ya dhambi zilizofanywa na baba yake, bali kila mtu atauawa kwa ajili ya dhambi alizozitenda mwenyewe (Kumbukumbu la Torati 24:16,17; 2Wafalme 14:6).

 

Mtumwa aliyemudu kumtotoka bwana wake haikuruhusiwa kumrejesha kwa bwana wake tena. Wakimbizi wanapaswa wapewe sehemu ya kuishi ndani ya malango ya miji, mahala wanapopachagua, na haipaswi waonewe au kubughudhiwa. Wanastahili kupewa msaada wa kuishi na ulinzi kwa mujibu wa Torati na sheria nyingine nyingi za Mungu (Kumbukumbu la Torati 23:15, 16).

 

Ushuhuda wa sababu asilia ya hukumu hii ya kifo

Hukumu ya kifo ni ya lazima kunapotokea matukio ya mauaji yaliyopangwa na kufanyika kwa kukusudia, na kutengwa kwa miji ya makimbilio ni muhimu kwa ajili ya kukimbilia mtu aliyeua pasipo kukusudia, ambaye ataishi humo kipindi chote cha maisha ya kuhani aliye ndani ya mji huo wa makimbilio.

 

Kwa makosa ya mauaji, kuuawa kwa muuaji ni tukio la mwisho na ndivyo inavyoagiza sheria kuwa ifanyike.

Hesabu 36:13 Haya ndiyo maagizo na hukumu, ambayo Bwana aliwaagiza wana wa Israeli, kwa mkono wa Musa, hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko

 

Mazingira ambayo kuua kunakua sio uhalifu

Haiwi uhalifu mtu anapoua iwapo kama atakuwa anatekeleza maagizo aliyopewa na Mungu kupitia Torati yake, kama tulivyosema huko nyuma.

Kutoka 4:24 Ilikuwa walipokuwa njiani mahali pa kulala, Bwana akakutana naye akataka kumwua.

Mungu anaonyesha nia yake hapa kwa vile alivyotaka kumuua Musa kwa kutolitii agano linalomtaka awatahiri watoto wake wa kiume.

 

Mungu alisababisha vifo vya watu ili iwe mfano kwetu kwa kipindi cha zaidi ya karne kadhaa zilizopita. Hakuna dhambi katika tendo lenyewe la kuua liifanywa kwa mujibu wa sheria za Mungu zinzzohusiana na jinsi ya kutekeleza hukumu ya kifo, sawa na ilivyo kwa mtu aliyeihalifu Sheria ya Mungu kwa ajili kumuua Masihi ambaye hakutenda dhambi yoyote.

 

Ulinzi wa Maskani na haki na utumishi wa kutoa huduma kumtumikia Mungu ni sehemu ya sheria pia.

Hesabu 18:22 Mwanzo wa sasa wana wa Israeli wasikaribie hema ya kukutania, wasije wakachukua dhambi, nao wakafa.  

Maagizo haya yanayolenga Hekalu jipya na kuwateuwa wateule kwa utumishi ulio wa mfano wa Melikizedeki katika jamii. Marekebisho ya sheria ya kuiondoa moja kutoka kwenye ile ya kwanza na kuifanya ya pili ifufuke. Hekalu liliondolewa na Hekalu jipya ni mawe yaliyo hai.

 

Mtu anaweza kuuawa kwa lengo la kulinda mali pia, au kwa kutekeleza amri ya hukumu iliyotolewa na mahakama na ambayo inaendana sawa na sheria kwa ajili ya makosa ya uhalifu alioufanya mtu na ambao unampelekea kuaawa. Hukumu hii ya kifo inaweza kutekelezwa kwa makosa au ya utendaji dhambi au kwa ajili ya kuivunja amri hii ya sita.

 

Miji ya makimbilio na sheria inayohusika na mauaji yaliyofanywa kwa bahati mbaya na mtu asiyekusudia kumuua mwenzake, haviwezi kumuokoa muuaji, hata kama mtu aliishikilia pembe ya madhabahu ya Mungu. Haiwezi kumsaidia kwa kuwa haiweki zuio kwa mtu aliyeua kwa kukusudia na ambaye anakabiliwa na hukumu ha kuuawa kwa haki.

Kutoka 21:12-14  Mtu awaye yote ampigaye mtu, hata akafa, hana budi atauawa huyo. 13 Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonyesha mahali atakapopakimbilia. 14 Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe.

 

Marufuku iliyowekwa kwa ajili ya kumtumia ng’ombe maksai kwa chakula kama akigonga na kumuumiza mtu yeyote ni kuiachqa nyama yake isitumiwe, na inasaidia kuwavunja watu mioyo yao wasipende kufuga au kuwatumia wanyama wakali na hatarishi. Iwapi kama mmiliki atakuwa anafuga mnyama mkali na wa hatari kwa makusudi, ndipo hata mfugaji huyo atakuwa na hatia na atashitakiwa. Sheria hii ilihusu pia katika ufugaji wa mbwa na wanyama wengine wa nyumbani. Wanyamapori wanaofugwa kwenye bustani ya wanyama maarufukama zuu ni suala lingine, iwapo kama kusudio lake litakuwa ni kwa ajili ya kuwaua kwa kitoweo au kama ni kwa ajili ya kuwalinda ili wasiuawe. Kitu cha kuangalia kwa jambo hili ni kuhusu kifo cha yule mnyama na kuzuia uharibifu..

Kutoka 21:28-36 inasema: Ng'ombe akipiga pembe mtu mume au mtu mke, nao wakafa, huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng'ombe ataachiliwa. 29 Lakini kwamba huyo ng'ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa. 30 Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa. 31 Akiwa ng'ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo.

 

Kushindwa au kutolipa gharama ilioyotokana na uharibifu ni kutoyatendea haki maisha na kudharau uthamani wake. Uharibifu unaendelea hadi kwenye mali ya mtu binafsi, ambayo ni “kitu chochote kilicho kwenye milki yake” na alichopewa akimiliki.

 

32 Ng'ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng'ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe.

Hasara au kuumizwa kunakoelezewapa ni kwa thamani ya mtumwa ambayo fidia yake ni vipande thelathini vya fedha. Fedha hizi alipewa bwana wa mtumwa yule, ambaye anajukumu la muda mrefu wa kumtunza na kumhudumia yule mtumwa. Hata hivyo, malipo haya hayamfanyi yule mkosaji ajitoe na kujiweka mbali na wajibu wa kumhudumia. Kwa ajili hii, jamii inawajibika kwenye masuala yote yanayohusiana na mahitaji na usalama wa watu wake.

 

Kwa masuala yahusuyo uharibifu, kila mmoja wetu anao wajibu kwa matendo yake mwenyewe yanapoharibika.

33 Kwamba mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng'ombe au punda kutumbukia humo, 34 mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake.

 

Gharama hii inafidiwa kwa mnyama aliyekufa. Mwenye kubeba wajibu wa lawama kwa ajili ya kuondolewa au kutoweka kwake huwa ni juu ya yule aliyekutwa na hatia. Kwa hiyo juhudi zote za kuonyesha kutojali jambo hili linachukuliwa kwa kutolewa hukumu inayostahili.

 

35 Ng'ombe wa mtu akimwumiza ng'ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng'ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng'ombe aliyekufa pia watamgawanya. 36 Au kwamba ilijulikana ya kuwa ng'ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng'ombe kwa ng'ombe, na huyo ng'ombe aliyekufa atakuwa ni wake.

 

Tunaona hapa kwamba kuna aina kuu mbili za uuaji. Namna ya kwanza ni ile ya uhatarisho wa kawaida, yaani iwapo kwma wanyama watajulikana kuwa walikuwa wanapigana na hovyohovyo, na ndipo hasara yake itakuwa sawa na kuharibu uzazi wote. Wakati mfugo unapojulikana kuwa unaleta matatizo, ndipo lawama yote atapewa yule mmiliki wake. Na hii ndivyo ilivyo kwa nyakati zetu hizi za leo wakati ng’ome anapopita barabarani na uharibifu wake unawaathiri wengine.

 

Mambo ya Walawi 24:17-21 Na mtu ampigaye mtu hata akafa, lazima atauawa; 18 na atakayempiga mnyama hata akafa atalipa; uhai kwa uhai. 19 Na mtu akimtia mwenziwe kilema; vile vile kama alivyofanya, naye atafanyiwa vivyo; 20 jeraha kwa jeraha, jicho kwa jicho, jino kwa jino; vile vile kama alivyomtia mtu kilema, naye atalipwa vivyo. 21 Na mtu amwuaye mnyama atalipa; na yeye atakayemwua binadamu atauawa

 

Aina hii ya tozo za faini au adhabu za kisheria ziliwekwa ili kukomesha uharibifu na maovu yenye kuleta madhara, vifo, sisasi cha jicho kwa jovho, jino kwa jino, nk. Uharibifu na fujo zinakwisha na kukoma katika kati ya watu. Tukio la uharibifu unaotokea kwa bahati mbaya  pasipo kukusudia ni jambo lingine, na hapa hasara iliyotokea inafidiwa kwa njia ya kupatiliza kulingana na ukubwa wa jambo lenyewe ulivyo.

 

Suala ya usiri au kuficha uharibifu wa makusudi unampekelea mkosaji kulaanika. Na watu wanatakiwa wakuli jambo hili kwa kusema Amina (au ukweli au kweli auna iwe hivyo),  wanaposimama mbele ya mahakama. Adhabu utatolewa, lakini laana itakuwa juu yake.

Kumbukumbu la Torati 27:24-25 Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina. 25 Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina. 26 Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.

 

Sheria iko wazi ili kufanya kusiweko na majonzi au kujihisi kuonewa na machungu kwa suala la mauaji na maovu ya aina hiyo.

Kumbukumbu la Torati 19:21 Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu

Sheria zinataka kwamba kusiwe na mtu anayeendelea kuwambwa juu mtini na kubakia hapo kwa usiku mzima akiwa bado anaendelea kuwa juu ya mti, bali anatakiwa azikwe siku ile ile anayowambwa. Shria hii mara nyingi ilikuwa inavunjwa na Wayunani na Warumi na desturi hii ya kuwaacha watu wakining’inia juu ya mti usiku kucha ilijipenyeza hata kwenye ulimwengu unaojiita kuwa ni Wakikristo.

Kumbukumbu la Torati 21:22-23 Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti; 23 mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako.

Nchi haipaswi kulaaniwa kwa ajili ya ushenzi na ukatili huu. Kwa hiyo unyongaji ulichukuliwa kuwa ni jambo la kawaida la kumwua mtu. Mazishi yalipaswa yafanyike siku ile, nia ikiwa ni kuliokoa taifa kutokana na ushenzi na ubadhirifu, kwa wakati mmoja.

 

Mungu amemuinua mwokozi kwa wakati huu.

Hesabu 25:7-9  Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake; 8 akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. 9 Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao.

 

Fineasi alihukumiwa kwa haki kwa kuuawa kwa hawa watuhumiwa, wakati taifa liliposimama kivivu na maafa ya tauni yaliwaangamiza kwa ajili ya wivu huu. Somo lilikuwa ni kwamba Usiandamane na mkutano kutenda uovu(Kutoka 23:2), au hukumu ya mashindano.

 

Ibada ya sanamu husababisha kuwepo na ulazima wa kutolewa hukumu ya kifo.

Kumbukumbu la Torati 13:11-18 Na Israeli wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako. 12 Ukisikia yasemwa habari ya miji yako mmojawapo, akupayo Bwana, Mungu wako, ukae humo, ukiambiwa, 13 Kumetoka katikati yako mabaradhuli kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua; 14 ndipo nawe uulize na kutafuta, ukiuliza kwa bidii; nawe angalia, ikiwa kweli, na jambo lile halina shaka, kwamba machukizo mfano wa haya yafanyika katikati yako; 15 hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo, na wanyama walio humo, kwa makali ya upanga. 16 Na nyara zake zote uzikusanyie katikati ya njia yake; na mji uuteketeze kwa moto, na nyara zake zote, kuwe sadaka kamili ya kuteketezwa kwa Bwana, Mungu wako; nao utakuwa magofu milele; usijengwe tena. 17 Kisishikamane na mkono wako kitu cho chote katika kitu kilichoharimishwa; ili ageuke Bwana na ukali wa hasira zake akurehemu, akuonee huruma, na kukufanya kuwa wengi, kama alivyowaapia baba zako; 18 utakaposikiza sauti ya Bwana, Mungu wako kwa kushika maagizo yake yote nikuagizayo leo, ufanye yaliyoelekea machoni pa Bwana, Mungu wako.

 

Sulemani alitenda dhambi na akafa kifo cha kimeili. Thawabu yake hata hivyo itategemea kama alitubu.

 

Hukumu ya kifo inaendelea kwa kipatiliza familia, na wazazi wanawajibika kwa matendo ya watoto wao.. kwa hiyo, uharibifu uliofanywa na watoto ni wajibu wa familia hadi watakapofikia umri wa ujibu wa mzazi wake pia, na wanatakiwa wamtoe na kumleta mbele ya mashitaka ili ashitakiwe.

Kumbukumbu la Torati 21:18-21 Mtu akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi, 19 ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake; 20 wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi. 21 Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.

 

Sambamba na hilo imeandikwa: “Msiwachokoze watoto wenu na kuwakasirisha” (Waefeso 6:4; Wakolosai 3:21). Muundo wa amri hii ya tano umetokana na dhana iliyo kwenye amri ya sita. Haitakiwi mtoto achokozwe hadi kumkasirisha kwa mujibu wa amri hii ya tano, kiasi cha kumsababishia ahukumiwe kifo au auwawe kama zinavyoagiza amri za tano na ile ya sita. Mzazi analaumiwa kwa mujibu wa amri ya sita kwa kumsababishia ahukumiwe kifo kama inavyoagiza amri ya tano. Kwa hiyo tunaiona tafsiri ya mtume Paulo kwenye kitabu cha Waefeso na Wagalatia.

 

Umuhimu wa kuwatii viongozi unaofundishwa kwenye familia na inashhinikizwa na mfumo wa sheria za nchi, kama tunavyojionea kwenye Hesabu 14:1-45. jambo hili limefafanuliwa kwa kina kwenye jarida letu la Torati na Amri ya Kwanza (Na. 253) [Law and the First Commandment (No. 253)].

 

Kuyatii Mapenzi ya Mungu

Bwana anapendezwa na utii zaidi kuliko sadaka au dhabihu.

Kumbukumbu la Torati 11:1-32 [ISOMWE YOTE NA KWA UKAMILIFU]

Kwa hiyo, Bwana hutoa maisha na hurefusha siku zetu na kuilinda dunia kama tu tutaendelea kumtii. Kwa namna yoyote ile ilivyo, jukumu la kuua kiumbe cha Mungu amepewa mwanadamu (soma Kumbukumbu la Torati 12:15).

 

Kuyatii mapenzi ya Mungu ni jambo muhimu na lazima kwa ajili ya kuishi. Taifa limekuwa likifanyiwa marejesho mapya kwa mara nyingi. Mungu amekuwa akiliadhibu pia mara nyingi, ila bado limekuwa halisikii. Wakati Israeli walipopewa fursa ya kuupata wokovu, lakini hao hawakufanya hivyo, na Mungu akaondoka kati yao na kuwaacha, na ndipo haqtimaye wakataka wafanye hivyo kwa matakwa na juhudi zao. Kwa kipindi cha miaka arobaini Israeli walitangatanga jangwani kwa ajili ya dhambi zao, na wakafia jangwani. Ni watoto wao tu ndio waliobakia na kuingia kwenye Nchi ya Ahadi. Na ndivyo ilivyotokea pia kwamba hata watu kutoka makabila ya Lawi na Benyamini walifia jangwani kwa kipindi cha yubile arobaini. Sawa na ilivyo, makabila ya Israeli waliobakia hawajaongoka walikufa. Wote walikabiliwa na hukumu ya kifo, sawa na kama mababa zao walivyokufa (isipokuwa Kalebu kutoka kabila la Yuda na Yoshua kutoka kabila ya Efraimu) na watakuwa na sehemu kwenye ufufuo wa pili wa wafu kwa ajili ya kutokutii au kuasi kwao. Wengi kutoka kabila la Efraimu na wa makabila mengine walimkubali na kumpokea masihi na walikuwa ni sehemu ya wale 144,000. Mitume wote katika wale kumi na wawili walikuwa ni kutoka makabila ya yuda na Lawi waliotoka katika jimbo la Galilaya, wakati Mtume Paulo alikuwa ni wa kabila la Benyamini.

 

Torati na amri ya sita pamoja nayo inaweka ulazima wa kutoa uhai na kuyalinda. Kutochukua hatua kwa mujibu wa amri hii kunapelekea kusababisha kuharibika kwa jamii. Sheria inapaswa itekelezwe kwa rehema na haki, hata hivyo, haki inapaswa haipaswi icheleweshwe. Haki haipasw pia ikataliwe kwa ajili ya kushindwa kuiua haki kwa udhaifu. Rehema na uvumilivu sio udhaifu, na haki haipaswi ichanganywe kwa wanaoipuuza sheria.

q