Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[260]

 

 

Torati na Amri ya Saba ya Mungu

 (Toleo Na. 2.0 19981009-19990525-20120430)

Imeandikwa: Usizini. Jarida hili linauelezea utaratibu wote wa amri zilizoko kwenye Torati ya Mungu, na kama zinavyoenda sambamba kwenye Amri yake kwa jinsi ilivyoelezwa na kufafanuliwa na manabii na jinsi zinavyoendana na Maagano yote na jinsi zinavyohusiana na sheria ya usomaji wa Torati katika miaka ya Sabato.

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 1998, 1999, 2012  Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Torati na Amri ya Saba ya Mungu

 


Imeandikwa: Usizini. Jarida (Kutoka 20:14; Kumbukumbu la Torati 5:18).

 

Tendo la ngono na zinaa

Kufanya ngono limeruhusiwa kwa mujibu wa amri ya Mungu na ni tendo la kiasilia la kufanya ngono na lengo lake ni kuufanya ulimwengu ujae na kuongezeka na kuwaongeza wanadamu au viumbe watakaofanyika hatimaye kuwa ni wana wa Mungu, na watakaoyafuata mapenzi ya Mungu aliyompa Adamu (Mwanzo 1:28; 9:1).

 

Dunia inaongezeka na kuwa na pilikapilika zake zote zilizo kwa mujibu wa amri za Mungu.

Mathayo 5:17-18 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie.

 

Kwa hiyo imetokea kwamba kusudi la kufanyika kwa tendo hili la ngono limetafsiriwa na udhibiti wa kiwango cha kutenda ngono limetakiwa lifuatane na mujibu wa sheria za Mungu. Kwa hiyo, amri hii ya saba linaelekeza na jinsi mataifa wanavyofanya na kulichukulia tendo hili la mahusiano ya kingono. Sheria zote zinazohusika na matendo ya ngono zimepanuliwa kutokana na amri hii ya saba, na ikidhibitiwa na ile ya tano na ya sita, na nyingine zote zinafuatia tu amri hii.

 

Familia kama wadhamini

Familia ikiwa imejiunga pamoja kwenye utaratibu wa amri ya tano na mara nyingi sheria ni mdhibiti au mdhamini wa tendo hili la mahusiano ya kindoa au ngono (soma Mithali 1:8-9; 6:20; 14:1). Mke mwema hutoka kwa Bwana naye amwoaye hujipatia kibali machoni mwa Bwana (Mithali 18:22; 19:14). Mwanamke mwema ni taji kwa mumewe (Mithali 12:4).

 

Inafuatia na kuelezewa kutoka kwenye torati kwamba hali ya mwanaume kuwa mseja ni tendo lisilo la kawaida, na wala halipendezi wala kwendana na mujibu wa uhusiano asilia wa familia ikiwa ni chombo au kifaa kitumikacho kutimiliza mapenzi na mpango wa Mungu. Maisha haya ya useja hayawezi kabisa kutimiliza kusudi lililowekwa lenye nia ya kutimiliza lengo la kwanza lililokusudiwa kutimizwa kupitia maisha ya ndoa. Historia ya imani ya useja au waasetisiki kwenye Ukristo pamoja na mapokeo mengine vimeelezewa kwenye jarida la Uvijiteriani kwenye Biblia (Na. 183) [Vegetarianism and the Bible (No. 183)].

 

Mtume Paulo ameandika jambo hili kwenye waraka wake 1Wakorintho 7:1-5, lakini amesisitiza kuwa nilazima lifanyike pasipo kufanya matendo ya uasherati: kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Anasema kwamba hakuna amri toka kwa bwana kufanya hivyo kwenye aya ya 6. Jamba analokisema hapa ni kwamba kuwe na hali ya kujitoa kwa Mungu kikamilifu na kwamba hilo ndilo jambo la muhimu sana na la kwanza na kwamba ni vema watu waoe ili kuzuia hali ya uasherati. Historia ya kanisa linalowataka watu wake kuishi maisha ya useja imepitia kwenye vipindi vya kulaumiwa kwa kutoweza kwao kuishi sawa na mfumo huo. Mtume Paulo anakazai kwamba vijana wakike wote heri waolewe, ili wazao watoto na kuzisimamia nyumba zao (1Timotheo 5:14).

 

Wanadamu ni wageni na wapitaji hapa duniani na ardhi ni mali ya Bwana. Familia na maeneo mengine ni vitendea kazi tu kwenye mpango wa Mungu (Mambo ya Walawi 25:23).

 

Mwanzo 30:20 Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni.

 

Katika tendo lolote la kindoa, ngono, haipaswi ndilo jambo la kwanza au la kulifanya kwa mwasho wa kitamaa kwa mujibu wa amri ya kumi. Na wala haitakiwi tendo hili la ngono na uzaaji watoto haifai ziwe ndiyo msingi au chanzo cha matendo ya tamaa za mwili zenye kupelekea kutamani mwanamke, na wala ndoa yenyewe kutumiwa tu kwa kuzitimiza tamaa za mwili (soma. 2Samweli 11:1-12:24; 1Wafalme 21:1-19).

 

Ngono kwenye ndoa

Kwa mujibu wa Torati au Sheria za Mungu limeagizwa kufanyika kwenye maisha husiano ya kindoa, kwa mwamke aliyefanywa kutoka kwa mwanaume na kukabidhiwa mwanaume ili wawe mwili mmoja kwa lengo la kukamilisha kusudi alilolikusudia Mungu tangu mwanzo wa uumbaji (Mwanzo 1:26-28; 2:15.18-25). Utaratibu wote huu umetokana na mpangilio kutoka uumbaji na haumkuhusisha na Malaika (Mathayo 22:30). Malaika walishindwa na wakaivunja amri hii na wakafukuzwa kutoka kwenye sehemu waliyokuwako kwanza (Yuda 6).

 

Ndoa ndiyo tendo au taasisi ililoanzishwa kutoka kwenye uumbaji na inawakilisha uhusiano wa Kristo na Kanisa.

Waefeso 5:22-33 inasema: Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. 24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. 25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. 28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. 30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. 31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. 32 Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. 33 Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.

 

Mfumo mzima wa familia umetuama kwenye mahusiano haya na utakatifu wake. Na wakati inapoharibika au kufanyiwa usaliti haiwezi kurejeshwa tena. Kiroho, bibi arusi anaweza kutubu na kumrudia Kristo. Israeli walipewa fursa ya kumrudia Bwana (Yeremia 3:1,7) lakini kama taifa walikukuwa wameishapewa Hati ya Kutalikiwa. Kristo atakapokuwa anakuja ndipo atalioa Kanisa litakalokuwa kama Israeli wa kiroho, ambaye yeye atakuwa ndiye Bwana arusi wake.

 

Mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanaume na kichwa cha kila mwanaume ni Kristo, na kichwa cha Kristo ni Mungu. Kila mwanaume asimamapo na kumuomba Mungu akiwa emefunika kichwa chake anakiaibisha kichwa chake (ambacho ni Kristo). Nywele ndefu ni aibu kwa mwanaume. Mwanamke mwenye kichwa kilichonyolewa nywele anapaswa akifunike kwa kilemba anapofanya maombi, kwaa kuwa nywele ndefu ni utukufu kwake, hapaswi kuzifunika zaidi ya zinavyojifinika hizo nywele zenyewe tu (1Wakorintho 11:1-16).

 

Somo hili la jinsi Torati inavyotuamuru kufunika nywele ni la muhimu sana na limekuwa likieleweka vibaya. Na mwanamke aliyetekwa vitani kutoka mataifa mengine aliamuriwa kunyolewa kichwa chake ikiwa ni kutimiza sheria ya utakaso wake. Mwanamke anatakiwa kuwa na mamlaka kwa mambo yahusuyo kichwa chake kwa kuwa kwa ajili ya malaika (1Wakorintho 11:10). Kwa hiyo, nywele ndefu za mwanamke ni ishara ya uweza na mwanamke mmataifa anatakiwa kujinyenyekesha kwenye mamlaka iliyokuu ya malaika walioasi. Mwanamke mmataifa aliyetekwa vitani kwa nguvu alitakiwa kunyolewa kichwa chake na kisha aanze kuzikuza tena akiwa kwenye nchi hiyo. Mapokeo yanayohusu tendo la kunyolewa kichwa kwa mwanamke akiwa kwenye ndoa linapingana pia na maana hii.

 

Walawi pia walitakiwa kunyoa nywele zote zilizoota miilini mwao ikiwa ni ishara ya kutengwa kwao na kutakaswa wanapokuwa wametengwa kuwa makuhani wa Iaraeli (Hesabu 8:7). Tendo hili lilihusisha moja kwa moja na uhusiano waliootakiwa wawenao wakiwa kama mabibi arusi wa Malaika wa Yahova walipokuwa wanamuabudu Eloa ambaye ni Mungu. Tendo hili lia lilikuwa ni taswira ya uhusiano amba wateule walitakiwa kuwa nao kwa Masihi akiwa kama Kuhani Mkuu aliye mfano wa Melkizedeki. Uhusiano huu pia ulionekana kwenye nadhiri za Wanazarayo (Hesabu 6:5,18). Kichwa cha mwanamke hakikutakiwa pia kifunikwe wakati alipokuwa anatoa sadaka ya wivu (Hesabu 5:18). Maana yake ilikuwa ni kwamba alikuwa anaonyeshwa mbele za Mungu na hakuwa kwenye ulinzi na wala kwenye matazamio. Ndipo Mungu alikuwa anamwangalia hadi moyoni mwake na ndipo alikuwa anamgundua kama ni mwuovu au hana hatia.

 

Kuhani Mkuu alikuwa anavaa kifuniko cha dhahabu kufuani mwake (Kutoka 28:36-38). Mfano huu ulikuwa unamlenga Masihi ambaye alipaswa avalishwe taji akiwa ni mfalme wa Israeli. Kanzu za watoto wa Kuhani (Kutoka 28:40) zilikuwa ashirio la taji za wateule watakazovaa wakiwa kama wafalme na makuhani kwenye Ufalme wa Mungu wakiwa kama wana wa Mungu. Kwa hiyo, kuna ukuhani wa kifalme na taifa takatifu (1Petro 2:9). Ishara hizi zote zinawalnga wateule kama mabbi arusi wa Kristo, kwenye Hekalu la Mungu na warithi pamoja na Kristo.

 

Uhusiano kati ya Kristo na Kanisa, na Kanisa na Kristo, na wa mwanamke kwa mwanaume umeelezewa kwa kina kwenye Mithali 31 na kwenye Wimbo Ulio Bora (pia kwenye majarida ya Mithali 31 (Na. 114) na Wimbo Ulio Bora (Na. 145) [Proverbs 31 (No. 114) and Song of Songs (No. 145)]. Uzinzi kwenye familia ni kitu sawa tu na kufanya ibada ya sanamu kwenye Hekalu la Mungu (soma jarida la Torati na Amri ya pili (Na. 254) [Law and the Second Commandment (No. 254)].

 

Maisha ya mke mmoja

Mtindo uliokusudiwa tangu zama za uumbaji ni ule wa kila mwanaume kuwa na mke mmoja tu. Mwanamume na mwanamke waliumbwa ili wawe mwili mmoja (Wanzo 2:18-24; Mathayo 19:5). Maaskofu wote wa kanisa wanatakiwa na kuamriwa wawe ni waume wa mke mmoja tu  (1Tim. 3:2). Uhusiano wa kimitala ulioko kwenye mataifa ya dunia hii uliruhusiwa kwa mababa zetu na ambao walioa wake wengi.

 

Mfalme hakuruhusiwa kujitwali wake wengi (Kumbukumbu la Torati 17:17) ingawaje Daudi na Sulemani walikuwa na wanawake wengi kwa mamia, na kikomo kilichowekwa na baraza la kimapokeo la kidini maarufu kama Talmudi linaonekana kuweka kikomo cha wake wa nane kwa mfalme na wane au watano kwa mtu wa kawaida. Hata hivyo, la msingi tu ni kwamba kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwana mke na awe na mume wake mwenyewe (1Wakorintho 7:2). Msimamo wenye mwelekeo mwema kwa wateule ni ule wa mke mmoja. (Soma jarida la Ndoa (Na. 289) [Marriage (No. 289)].

 

Uhusiano wa Kiplatoniki na Daudi

Wakati Daudi alipokuwa mzee alipewa mwanamke wa kumapasha moto aliyeitwa Abishagi Mhunami ili amhudumie, lakini hakuweza kushiriki ngono naye. Hatahivyo, hii ilichukuliwa kuwa ni uhusiano wa kawaida kama wakati Adonia alipoomba kumuoa Abishagi ambaye alikuwa ni wa Sulemani kaka yake mkubwa, jambo ambalo lilimfanya Sulemani amuue bila huruma wala kusita. Kwa namna zote mbili tunaweza kusoma kuwa huenda Sulemani alihofia kuipoteza nafasi yake iwapo kama ndugu yake mkubwa angepewa kumuoa Abishagi na kuwa mkewe, na inasimama pia kwamba angejisikia vibaya iwapo kama mwanamke huyu angemfanyia mambo kama suria wa baba yake, na ndipo kwamba Adonia angekuwa amezivunja amri za Mungu zinazokataza uhusiano wa kingono kufanyika kwa watu wa jamaa moja. Hata hivyo, hii ingemfanya aondolewe tu (soma 1Wafalme 2:13-25).

 

Mitala

Uhusiano wa kwanza wa kimitala ulifanywa na wana wa Kaini wakati Lameki alipojitwalia wake wawili Ada na Sila (Mwanzo 4:19). Ufafanuzi kwa kile kinachotokea kwenye kitabu cha Mwanzo upo kwenye jarida la Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya 2 Kizazi cha Adamu (Na. 248) [Doctrine of Original Sin Part 2 The Generations of Adam (No. 248)].

 

Kwa mujibu wa Torati, ndoa za wake wengi zimeruhusiwa. Israeli mwenyewe alikuwa na wake wawili na masuria kadhaa, na watoto wake wote tunaona kuwa walikuwa halali na hakuna aliye wa haramu hata mmoja na ni warithi wa ahadi ya agano. Ndivyo ilivyokuwa pia kwa Samweli mtiwa mafuta wa Bwana, ambaye alizaliwa kwenye ndoa ya aina hii hii ya wake wengi (1Samweli 1:1-2).

Kumbukumbu la Torati 21:15-17  Akiwa mtu yuna wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa; 16 ndipo itakapokuwa ya kwamba siku atakayowarithisha wanawe alivyo navyo, asimweke mwana wa ampendaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana wa asiyempenda, naye ndiye mzaliwa wa kwanza huyu; 17 lakini amkubali mzaliwa wa kwanza mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo; kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake; haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.

 

Kwa hiyo ni jambo lisilo pingika kuamini kwamba torati inaruhusu ndoa hizi za mitala na mababa zetu hawa ndiyo watakaokuwa wa kwanza kwenye ufufo wa wafu. Maisha ya usuria tunayaona kuwa yakiwa ni mtindo wa kilale zaidi kuwepo hapa duniani: mataifa yote yaliuruhusu na kuukubali mtindo huu wa maisha. Ilichukuliwa kuwa sio jambo la aibu kwa mtu kumchukua suria kwa dhumuni la kumzalia wana wa kiume, na huu ndiyo umebakia kuwa mtazamo wa Wachina unaobebwa na mafundisho ya Wakonfyusiani hata leo. (Soma jarida la Mitala kwenye Biblia na Korani (Na. 293) [Polygamy in the Bible and the Koran (No. 293).]

 

Suria alikuwa na haki chache kuliko mke wa ndoa na mara nyingi walichukuliwa kwa lengo la kuzaa nao watoto hasa wa kiume tu, na walilipwa stahili zao. Makabila waliiiga kutoka kwenye uhusiano huu mchanganiko na Israeli likichukulia kama mtindo wa kitaifa, linachukulia mashiko yake kutoka kwenye mahusiano ya namna hii, hadi kwamba hata tendo la kuhasili watoto limechukuliwa kutoka kwenye mtazamo huu. Israeli ni mwana wa Mungu na Mataifa wamefanyika kuwa wana wa Mungu pamoja na Israeli kwa nguvu za ufufuo wa wafu, wakiwa ni warithi pamoja na Kristo (soma Warumi 1:4; 8:17).

 

Esau alioa wanawake pia: Yudithi aliyeitwa pia Aholibama na Bashemathi aliyeitwa pia Ada  (soma Mwanzo 26:34-35 na 36:2). Andiko linasema kwamba jambo hili liliwahuzunisha sana wazazi wake, hasa kwa kuwa walikuwa ni wanawake wa Kihiti. Mmoja wao alikuwa ni Mhivi ambalo ni tawi la Wakanaani (Mwanzo 28:8). Kisha aliendelea kwa kumuoa Bashemathi (ambaye pia aliitwa Mahalathi), ambaye alikuwa ni binti wa Ishmaeli na dada wa Nebayothi (Mwanzo 28:9; 36:3). Tendo hili linaonyesha kuwa walikuwa wamependezwa sana kuwaoa Wakanaani ambao walikuwa wanaabudu mungu wa uwongo na kwa hiyo walikuwa chini ya laana. Hii ilikuwa ni ndoa nyingine iliyofanyika kwa ndugu wa karibu (ya kindugu).

 

Kwa mara nyingine tena, hapa somo lilikuwa ni kutuonyesha vile tulivyo kwenye mahusiano yetu na Mungu hayazuii kutenda tunatakayo au kuyatenda ya wazazi wetu yanayoweza kutuponya na magonjwa na makosa yao. Fundisho liliendelea hadi kwa Ishmaeli, Esau, Moabu, Amoni na hadi kwa wana wa Ketura ili kusiwepo na mtu wa kujitukuza kwa mambo ya mwili au nyama na damu.

 

Mlolongo wa uzao wa Daudi ambao ndio wa Masihi pia, una jumuisha wanawake wanne wa mafaifa, ambao watatu kati yao walifanya dhambi mbaya sana ya uzinzi (soma jarida la Mlolongo wa Uzao wa Masihi (Na. 119) [Genealogy of the Messiah (No. 119)]. Kwa hiyo, wokovu ulikuwa wa Mataifa wapagani kutoka kwa waliokuwa wa uazao kabisa wa Yudana Israeli.

 

Kuachana na kuoa tena

Torati inaruhusu kuachana na kuoa tena, bali hairuhusu kumuoa tena mwanamke yuleyule baada ya kuolewa na mwanaume mwingine. Anaweza kuolewa na mwanaume huyohuyo tena iwapo tu kama atakuwa hajaolewa na mwanaume mwingine kipindi cha kuachana kwao.

Kumbukumbu la Torati 24:1-4 Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake. 2 Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. 3 Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; 4 yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za Bwana; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi.

 

Sheria hii ilikusudia kuilinda familia na pia kulinda maadili na kiwango cha maadili ya taifa lao. Maana yake yako wazi. Ikiwa mwanaume ataolewa tena na akakuta kwamba mume wake wa kwanza alikuwa ni bora zaidi kuliko huyu wa pili, au anagubu na magomvi kuliko yule wa zamani, ndipo maana ya kuwa na ushirikiano wa pili utafanyika kuwa mhanga wa kuwa na uwezekano wa hatari ya kuachana tena zaidi kwa ajili ya kupenda kumrudia na kuoana tena na mwanaume wake wa kwanza au wa zamani. Nia nzima ya kufanya hivyo ni kuzuia kuwa na na ndoa za kituo cha muda ambacho kitatumika kama mahala pa kujipumzisha tu wakati anajipanga kurukia kwingine na ndiyo maana torati ilikataza maisha aina hii. (Ikumbukwe kwamba uchafuko kama unaotajwakwenye Kumbukumbu la Torati 24:1 umetajwa kuwa ni dhambi ya mbaya kabisa; soma Kumbukumbu la Torati 22:14; Mathayo 19:19; 5:32.)

 

Uaminifu kwa wateule, wake wa waume, ni jambo linalotokana na jinsi mawazo yake alivyoyaweka na ndivyo linavyokuwa hata kwenye hali ya mwilini kwa mwingiliano wa Roho Mtakatifu na kuiheshimu Amri ya Kumi.

Mathayo 5:27-32  Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. 30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. 31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

(soma Marko 10:10-12; Luka 16:18).

 

Mtume Paulo alisema pia kuhusu jambo hili na akasema kwamba ndoa na watoto wanatakaswa na mwamini. Tendo la kuachana halipaswi kuchuliwa kirahisi hata kama mwezi wa ndoa hiyo sio muumini.

1Wakorintho 7:12-17 Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. 13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. 14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu. 15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani. 16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo? 17 Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aenende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote.

 

Kristo alitamka maneno mazito sana kuhusu tafsiri ya sheria alipokuwa anaongea na mwanamke Msamaria pale kisimani.

Yohana 4:7-29 inasema: Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. 8 Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. 9 Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.) 10 Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. 11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? 12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? 13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; 14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka. 16 Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. 17 Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; 18 kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. 19 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! 20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. 21 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. 25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote. 26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye. 27 Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye? 28 Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, 29 Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?

 

Mfumo huu unaonyesha fundisho lifuatalo kuhusu ndoa. Kwanza kabisa, ni kuhusu mwanamke aliyeolewa mara tano kwa kufuata mujibu wa torati na kila ndoa ilikubalika na kuchukuliwa kuwa ya halali na Masihi. Na kwa kipindi hiki alikuwa anaishi na maisha ambayo talikuwa hayakubaliki kuitwaa kuwa ni ndoa na Masihi. Ndipo Masihi alipofanya fundisho lake kutokana na hali hii. Alizitambua ndoa zote tano kwa kuwa mwanamke huyu hakuwahi kuwa mjane hata mara moja kati ya mara hizi tano za maisha yake. Na kwa kweli, torati inaruhusu kuoa na kuolewa tena kama tulivoelezea hapo juu. Jambo la pili ni kwamba Kristo alionyesha hapa kuwa ndoa zote zilikuwa halali na zisizo na kipingamizi cha kuzitangaza kuwa ni ndoa halali.

 

Ndoa katika mataifa inategemea au kuendana na sheria zilizo kwenye nchi zao na hazihusiani ma sakramenti za Kanisa au kanuni za Kanisa. Kwa ajili hii mataifa yote yana sheria zake za ndoa na watoto wake ni ni halali kama wana halali wa Adamu. Kuna sakramenti mbili tu za Kanisa, ambazo ni Kubatizwa na Kushiriki Mlo wa Bwana (soma jarida la Sakramenti za Kanisa (Na. 150) [The Sacraments of the Church (No. 150)].

 

Ndoa ni muungano wa kimaandiko wa wawili kuwa mwili mmoja. Kristo alikuwa na mengi sana kuongea kuhusu hili, na alifanya mlinganisho mkuu sana kwa wateule kuhusu ndoa na talaka.

Mathayo 19:1-12 inasema: Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng'ambo ya Yordani. 2 Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko. 3 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? 4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? 6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. 7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? 8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. 9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. 10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa. 12 Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

 

Kuna watu waliojitoa kwa ajili ya utukufu wa Mungu, na hapa Kristo alikuwa anasema kuwa alikuwa yeye mwenyewe amejitoa kikamilifu. Mitume wote walikuwa wameoa pia na hata Paulo inaonekana kwamba alikuwa ameoa kipindi cha huduma yake. Lingekuwa ni jambo lisilofikirika kama Kristo angekuwa ameona, sio tu kwa kuwa ilikuwa imejulikana kuwa atauawa kipindi kifupi tu kijacho na kwamba hakupenda amwache mjane, bali ni kwa kuwa yeye ni Bwana arusi wa Kanisa na mfano huu haukupaswa kuingiliwa na kuharibiwa na kitu kingine. Iwapo kama angekuwa amewaacha watoto, basi maana halisi na muhimu yangeondoka. Na kwa kweli ndivyo ilivyotokea pale ndugu zake wa kimwili waliozaliwa kwenye ukoo wake kama wapwaze na binamu zake – ndugu wa kimwili –hadi kipindi walichotokomezwa kabisa na utawala wa Warumi. Kanisa tangia karne ya nne na kuendelea (soma jarida la Bikira Mariamu na Familia ya Yesu Kristo (Na. 232) [The Virgin Mariam and the Family of Jesus Christ (No. 232)].

 

Kuachana kwenye ndoa za wateule ni jambo lisilo kubalika na Kristo, isipokuwa kana kumekutikana na matendo ya uzinifu (soma Mathayo 5:32). Pia wanatakiwa kudumu na wenzi wao ambao sio waumini iwapo kama mwenzi huyu asiyeamini atakubali kuishi naye. Bali iwapo kama mwezi huyu asiyeamini hakubali kuishi naye, ndipo inaporuhusiwa kutolewa hati ya talaka na wanaweza kuachana. Kwa kweli kuna sababu nyingine zinazopelekea wenzi kuruhusiwa kuachana, au kutanguliwa ndoa zao, kwa mambo kama vile uganaganyifu, udugu wa kinasaba, dhuluma au kutendea vibaya, bali mambo ya jinsi hii yamekuwa kwa kiasi kikubwa (na mara nyingi) hutumiwa vibaya na mataifa na mifumo ya makanisa yao.

 

Ndo kama Mfano wa Uhusiano wetu wa Kiroho na Masihi

Israeli wameolewa na Mungu. Kanisa limeolewa na Masihi kama Tahova, Elohim wa Agano la Kale. Mataifa yote yatakuja na kuungana na Israeli wakiwa kama Hekalu lijalo la Mungu wakiwa na Kuhani wao Mkuu, ambaye ni Elohim wa Israeli (soma Zaburi 45:6-7 na Waebrania 1:8-9). Mafundisho haya yote ya mifano yanafanya taswira ya wokovu wa dunia kwa Mungu kama gari lake lililounganishwa vema kwa Roho Mtakatifu.

Yeremia 3:1-9 Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? Asema Bwana. 2 Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pa wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako. 3 Kwa sababu hiyo manyunyu yamezuiliwa, wala hapakuwa na mvua ya vuli; hata hivyo ulikuwa na kipaji cha uso cha kahaba, ulikataa kutahayarika. 4 Je, tokea wakati huu hutanililia, Ee Baba yangu, wewe u kiongozi wa ujana wangu? 5 Je! Ataishika hasira yake hata milele? Ataishika hata mwisho? Tazama, umesema hivyo, bali umetenda mambo mabaya, umefuata njia yako mwenyewe. 6 Tena, Bwana akaniambia siku za mfalme Yosia, Je! Umeyaona aliyotenda Israeli mwenye kuasi? Amepanda juu ya kila mlima mrefu, akafanya huko mambo ya ukahaba, tena, chini ya kila mti wenye majani mabichi. 7 Nami nalisema baada ya yeye kuyatenda hayo yote, Atanirudia mimi, lakini hakurudi; na dada yake, Yuda mwenye hiana, akayaona hayo. 8 Nami nikaona, wakati nilipokuwa nimemwacha Israeli mwenye kuasi, nikampa hati ya talaka kwa sababu hiyo ya kuzini, dada yake, Yuda mwenye hiana, hakufanya hofu; bali yeye naye akaenda akafanya mambo ya ukahaba. 9 Hata ikawa, kwa sababu alikuwa mwepesi wa kufanya ukahaba, nchi ikatiwa unajisi, naye akazini na mawe na miti.

 

Mazingira yanayopelekea wanandoa kuachana na junsi ya kurudiana ni muhimu ili kuzuia uwezekano wa kuwa na mwanaume mwingine anayeingilia, kes kues uhusisno ksms huo utschukuliws kuwa ni sawa na ibada ya sanamu na uingiliaji wake kwenye uhusiano na Mungu.

 

Kwenye ufufuo tutakuwa kama malaika walivyo Mbinguni, na maisha ya ndoa yanafikia kikomo wakati mwenzi mmojawapo anapokufa.

Mathayo 22:23-33 Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, 24 wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. 25 Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. 26 Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba. 27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. 28 Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye. 29 Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. 30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. 31 Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema, 32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. 33 Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake.

 

Hatima yetu ya mwisho inafungamanishwa kwenye ufufuo wa wafu na wote wataamka kwa hukumu, bsli hukumu ya wateule imeshaanza tayari na yao itakuwa kwenye Ufufuo wa Kwanza atakaporudi Masihi.

 

Ndoa Mchanganiko

Kanuni au utaratibu wa kuchangamana kwenye ndoa umewekwa kwa lengo la kuyatakasa mafundisho na hauhusiani na mambo ya damu peke yake (soma Yeremia 3:8-10; Isaya 50:1-10). Ilikuwa ni Masihi ndiye aliyewapa waliomchubua mgongo wake kama ilivyoandikwa kwenye Isaya 50:6. Bwana hana mzabuni ambaye kwake angeweza kutuuza kwake au kututalikia kwake. Je, iko wapi hati ya talaka ya mama yetu? Binti za mfalme hula kwenye nyumba ya baba yao na hakuna mgeni anayekula humo (soma Mambo ya Walawi 22:13; Kutoka 34:12-16).

 

Taifa la Israeli lilifanya dhambi kubwa wakati wa Marejesho mapya waliyoyafanya kina Ezra na Nehemia. Ndipo walilazimika kuachana na wanawake zao waliokuwa waabudu sanamu (Nehemia 9:2; 13:23-31). Jambo husianifu hapa ni lile alilolifanya Sulemani.

Nehemia 13:23-31 Tena siku zizo hizo nikawaona wale Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake wa Ashdodi, na Amoni, na Moabu; 24 na watoto wao wakanena nusu kwa lugha ya Ashdodi, wala hawakuweza kunena kwa Kiyahudi, bali kwa lugha ya watu hao mojawapo. 25 Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe. 26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye. 27 Basi, na sisi, je! Tuwasikilize ninyi kutenda neno hili baya, hata kumhalifu Mungu wetu kwa kuwaoa wanawake wageni? 28 Na mwana mmoja wa Yoyada, mwana wa Eliashibu, kuhani mkuu, alikuwa mkwewe Sanbalati, Mhoroni, basi nikamfukuza kwangu. 29 Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, jinsi walivyounajisi ukuhani, na agano la ukuhani na la Walawi. 30 Hivyo nikawatakasa na kila kitu kigeni, nami nikawaagizia zamu makuhani na Walawi, kila mtu kazini mwake; 31 na matoleo ya kuni nyakati zilizoamriwa, na malimbuko. Nikumbuke, Ee Mungu wangu, ili unitendee mema.

 

Ibada za sanamu zilikuwa zinawalazimisha watoto wasahau lugha yao, ambayo ilikuwa ni ya muhimu kwa kuwafundishia Biblia na na kwa kuyaelewa maandiko matakatifu na makuhani walikuwa wanayanajisi.

 

2Wakorintho 6:14-18 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,

 

Mwenzi asiyeamini anawajibika kuisaidia ndoa yake. Tunabakia kwenye halia ambayo kwayo tuliitwa.

1Wakorintho 7:20-24 Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. 21 Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia. 22 Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo. 23 Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu. 24 Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo.

 

Mwenazi anayeamini anaweza kuwa ni chanzo au sababu ya kumwokoa mwingine. Kwa hiyo wito wa wokovu usiwe kigezo cha watu kuachana.

 

Ngono nje ya ndoa

Mungu anasheria mahsusi inayohusika na mtu anayefanya ndono nje ya ndoa yake. Matendo YOTE ya ndoa nje ya muungano wa wanandoa, au kufanya na suria (tangu zama za Mababa waliokuwa wanafanya kwa lengo la kujipatia watoto) ni machukizo, haijalishi ni umri gani au wadhifa gani alionao mtu. Uanzishaji wa ndoa ulianza siku za Adamu na unaendelea hadi leo (Mwanzo 5:3-5).

 

Uaminifu kwenye ndoa ni wa muhimu sana.

Mithali 5:1-23 inasema: Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu; 2 Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. 3 Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; 4 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. 5 Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; 6 Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. 7 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. 8 Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. 9 Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; 10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; 11 Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; 12 Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; 13 Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! 14 Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko. 15 Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. 16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? 17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. 18 Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. 19 Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima. 20 Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni? 21 Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya Bwana, Na mienendo yake yote huitafakari. 22 Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. 23 Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.

 

Uzinzi ni tendo baya na ni dhambi, na msamaha wake haupatikani kiurahisi licha ya zawadi na wajinga wamepotoshwa kwenye vita na mauti (soma Mithali 6:20-35; 7:1-27; Malaki 2:14). Imeandikwa:

Mambo ya Walawi 18:20 Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.

 

Zinaa

Watu WOTE walio kwenye imani wanatakiwa kujiepusha na aina ZOTE za matendo ya zinaa (Matendo 15:20, 29; 21:25).

1Wakorintho 5:1-13 inasema: Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. 2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. 3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. 4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; 5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu. 6 Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? 7 Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; 8 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli. 9 Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. 10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. 11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye. 12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani? 13 Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.

 

Kufanya zinaa na mke wa baba zetu au meme zetu wadogo au wa kufikia sio tu kuwa ni zinaa, bali ni zinaa inayoambatana na ndugu wa karibu. Adhabu aliyostahili mtu kupewa na hasa kwa tukio hili ilikuwa ni kumwondoa atoke Kanisani hadi atakapotubu. Hii ilikuwa kwa sababu kwamba uhai wa mzinifu uweze kuokolewa siku za mwisho, kama tunavyoona kwenye aya ya 5 hapo juu.

 

Wale walio Kanisani na ambao hawako katika roho wako chini ya mamlaka ya mungu wa dunia hii na wanatarajiwa kwenye ufufuo wa pili. Kwa walioko Kanisani, tendo la kushindwa kuzitubia dhambi humaanisha ni kujiondoa kuwepo kwao kwenye ufufuo wa kwanza na kujiweka kwenye uwezekano wa kuwepo kwenye ufufuo wa pili ambao ni wa hukumu. Kwa kadiri inavyofanywa kwa haraka sana ndipo msamaha wake unapofanyika kwa haraka sana pia, basi kwa mkosaji na anayetenda hivyo, fursa nzuri ni ile ya kufanya toba, kwa ama kipindi cha sasa au au ni kuamua kuwa hivyo ili aingie kwenye ufufuo wa pili na wa hukumu.

 

Miili hii ni ya Bwana, na sisi ni Hekalu lake tu Mungu.

1Wakorintho 6:12-20  Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote. 13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. 14 Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. 15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! 16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. 18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

 

Mungu atawahukumu waasherati makahaba wote na wazinifu.

Waebrania 13:4  Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

 

Torati hii ya Mungu Kanisani imewekwa kwenye kiwango cha juu kwa wateule zaidi ya sheria iliyo katika taifa (soma Mathayo 5:27-32 hapo juu).

 

Ubatizo unawezesha mtu kumpokea Roho Mtakatifu, anayetuwezesha sisi kuyafanya mambo kwa mujibu wa inavyotutaka Torati yake na kuipa kipaumbele kikubwa zaidi ya vile inavyofanywa kwa sheria za mataifa. Kipaumbele hiki kinategemea na jinsi nia zetu zilivyo na na uhusiano wetu wa kiroho tulionao kwa Mungu; vinginevyo inakuwa ni vigumu sana kufika kwenye kiwango hiki. Mtu asiitumie sheria ya talaka kwa kuwa inamsababishia mwingine kuwa mzinifu, jambo litakalomfanya kuwa ni vigumu sana kwake kuuingia ufalme wa Mungu. Inasababisha migogoro na kuachana kwenye familia na Mungu anachukia machafuko na kuachana (Malaki 2:10-17).

Malaki 2:10-17  Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu? 11 Yuda ametenda kwa hiana, na chukizo limetendeka katika Israeli, na katika Yerusalemu; maana Yuda ameunajisi utakatifu wa Bwana aupendao, naye amemwoa binti ya mungu mgeni. 12 Bwana atamtenga mtu atendaye hayo, yeye aliye macho, na yeye ajibuye, atamtenga na hema za Yakobo, pia atamtenga yeye amtoleaye Bwana wa majeshi dhabihu. 13 Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya Bwana kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia. 14 Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. 15 Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. 16 Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana. 17 Mmemchokesha Bwana kwa maneno yenu. Lakini ninyi mwasema, Tumemchokesha kwa maneno gani? Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa Bwana, naye huwafurahia watu hao, au, Mungu mwenye kuhukumu yuko wapi?

 

Matendo ya zinaa na ndugu wa karibu

Sheria kuhusu matendo ya zinaa kwa ndugu wa karibu au wa nasaba moja imeandikwa kwenye Mambo ya Walawi 18. Ni tendo lililokatazwa kabisa kutendwa kwa sababu zozote zile, kama tunavyoona ilivyoandikwa hapa chini.

Mambo ya Walwi 18:1-18 inasema: Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 3 Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msiende katika amri zao hao. 4 Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 5 Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi Bwana. 6 Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana. 7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. 8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. 9 Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. 10 Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. 11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. 12 Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. 13 Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu. 14 Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako. 15 Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. 16 Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo. 17 Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. 18 Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai.  

 

Kumbukumbu la Torati 22:30  Mtu mume asimtwae mke wa baba yake, wala asifunue ncha ya mavazi ya baba yake.

 

Katazo mojawapo ni lile linaloonysha dhahiri kukataza mtu kumuoa dada yeke. Iwapo kama dada mmoja anaishi bado, hairuhusiwi kumchukua ndugu yake mwingine na kumfanya kuwa mkeo, bali anaweza kufanya hivyo ikitokea kuwa yule dada yake aliyekuwa mkewe amefariki. Yakobo aliivinja sheria hii kwa kuwachukua Lea na Raheli kwa pamoja. Alikuwa na muda na sababu bado ambazo kwazo angeweza kumuacha Lea na kumchukua Raheli aliyempenda na kumchagua, lakini yeye hakufanya hivyo. Huu ulikuwa ni mfano pia wa Kristo aliyewachukua Yuda na Israeli kuwa wake zake kwa pamoja na kisha akawachukua Israeli na Wamaifa kuwa wakeze kwa pamoja, wakiwa ni sehemu ya yale makabila kumi na wawili.

 

Dhambi hizi ni sehemu ya laana zilizowafanya kupatilizwa Israeli (Kumbukumbu la Torati 27:20, 22, 23). Lakini pamoja na dhambi hizi, bado Mungu aliwafanya kuwa taifa. Na zaidi ya yote ni kwamba Musa mwenyewe na Haruni aliyekuwa Kuhani, ni watoto waliozaliwa kutoka kwenye ndoa ya mtindo huu wa uhusiano wa watu wa nasaba moja.

Kutoka 6:20 Huyo Amramu akamwoa Yokebedi ndugu ya baba yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia na thelathini na saba.

 

Na ndivyo ilivyotokea pia kwa wana wa Ibrahim na Sara (Mwanzo 20:12) na wale waliowatangulia (Mwanzo 5:4).

 

Ilifanyika hivi kiasilia ili kuwafanya makuhani waone hivyo pia, na manabii wa Mungu kwa kupitia sheria au torati ya Musa ambayo kwa kweli ni kwa rehema itendayo kazi ya Yesu Kristo na kwa wao wenyewe wasiweze kuupata wokovu. Na hii ndiyo sababu Masihi alizaliwa kwa kupitia kwenye mlolongo wa kiuzao wa sehemu zote mbili, kutoka Daudi akapitia kwa Nathani na kutoka Lawi kupitia kwa Shimei. Ni kwa jitihada za Mungu tu na kwa tendo la Yesu Kristo la kukubali kuachilia hali yake ya uzaliwa wake wa kabla ndipo wokovu ulipowajia wanadamu.

 

Sheria ya Kilawi

Sheria nyingine ya pekee ya aina yake ni ile inayoelezea kuhusu iwapo mwanaume atakufa bila kuzaa motto: kuwa mke wake anaweza kutolewa na kupewa ndugu yake ili amzalie wana kwa niaba ya ndugu yake aliyekufa, kwa lengo la kulinda urithi au milki ya ndugu yake na kulinda hali ya familia. Motto huyo atahesabiwa kuwa ni wa yule ndugu aliyekufa na kuwa anakuwa kwenye uzao wake. Kiutendaji, mtoto huyu au watoto hawa hawakuhesabiwa ama kuchukuliwa kuwa miongoni mwa walio kwenye uzao wa yule aliyewazaa na walihesabiwa nje kabisa ya yule ndugu wa karibu aliyekuja kuzalia kimsaada, kama tunavyoona ilivyotokea kwa Ruthu na Boazi. Wao walioana.

Kumbukumbu la Torati 25:5-12 Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe. 6 Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli. 7 Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu. 8 Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu, 9 ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi. 10 Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu. 11 Washindanapo waume wao kwa wao, akakaribia mke wa mmojawapo, ili kumwokoa mumewe katika mkono wa ampigaye, yule mke akatoa mkono wake, na kumkamata tupu yake; 12 umkate ule mkono wake, lisiwe na huruma jicho lako.

 

Hivi ndivyo sheria ya kurithi mke ilivyoanzishwa, huyu ndugu alikuwa haruhusiwi kumuoa bali alikuwa analazimika kumchukua kuwa mke wake mke huyu aliyeachwa kuwa mjane na ndugu yake. Mahudhui ya aina ya ndoa hii yalikuwa ni kwamba ilikuwa ni kumchukua mjane aliyefiliwa na mume wake ambaye ni ndugu na huyu anayemchua sasa ili kuwa ni urithi tu na sio mkewe halisi asilia.

 

Kwenye Gombo za maandiko yakale ya Hammurabi, yalieezea kuwa ndilo tendo alilolifanya Abrahamu kwenye tukio linaloonekana kwenye kitabu cha Mwanzo 15:2-3, mwanaume asiye na motto alimchukua na kumfanya kuwa suria mjakazi wake ambaye alichukuliwa kama mmoja wa watu wa nyumbani mwake na kuwa angeweza kuwa mrithi wa milki zake. Mazingira ya jambo hili hayakuwa kwenye sheria ya Mungu sana, bali yalitokana na kushindwa kwake kubeba majukumu yake ambayo kwayo yalimsabishia Onani auawe (soma jarida la Dhambi ya Onani (Na. 162) [The Sin of Onan (No. 162)].

 

Ilitokana na sheria yake na pia ni kutokana na kurutubisha uzao (IVF) kunakoweza kufanyika wakati wezi wa ndoa wakijulikana kuwa hawana mtoto na hakuna uwezekano wa kuzaa watoto. Ndipo utaratibu huu unaweza kufanywa kwa mujibu wa sheria na ndugu wa karibu anaweza kuchukua mahala, iwapo kama mwanamke ataaminika kuwa na mayai na kama hana anaweza kutiwa kwa mtu yeyote aliye kwenye familia yao. Motto atakayezaliwa kutoka kwenye familia hiyo atakuwa na wasifa sawa na ndugu wa kiume na wa kike wa familia hii kwa mujibu wa sheria au torati.

 

Ushahidi wa uwongo na chuki kwenye ndoa

Kumbukumbu la Torati 22:13-29 inasema: Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia, 14 kisha akamshitaki mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke huyu, nami nilipomkaribia sikuona kwake alama za ubikira; 15 ndipo babaye yule kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee wa mji langoni; 16 na baba yake yule kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu nilimpa binti yangu awe mkewe, naye amchukia; 17 angalieni, amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira. Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji. 18 Basi wazee wa mji ule na wamtwae yule mtu mume na kumrudi, 19 wamtoze shekeli mia za fedha, wampe babaye yule kijana, kwa kuwa amemzulia jina baya mwanamwali wa Israeli; naye awe mkewe; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote. 20 Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira; 21 na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. 22 Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli. 23 Pakiwa na kijana aliye mwanamwali ameposwa na mume, na mwanamume akimkuta mjini, akalala naye; 24 watoeni nje katika lango la mji ule, mkawapige kwa mawe hata wafe; yule kijana, kwa kuwa hakupiga ukelele, naye yu ndani ya mji; na yule mume, kwa kuwa amemtweza mke wa mwenzake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. 25 Lakini yule mtu mume kama akimkuta kondeni kijana aliyeposwa, naye mume akamtenza nguvu, akalala naye; yule mtu mume aliyelala naye na afe pekee; 26 lakini yule kijana usimfanye neno; hana dhambi yule kijana ipasayo kuuawa, kwa kuwa ni mfano wa mtu kumwondokea mwenzake akamwua, ni vivyo lilivyo jambo hili; 27 kwani alimkuta kondeni; yule kijana aliyeposwa akalia, pasiwe na mtu wa kumwokoa. 28 Mtu mume akimwona kijana aliye mwanamwali ambaye hajaposwa, akamshika na kulala naye, wakaonekana; 29 yule mtu mume aliyelala naye na ampe baba yake yule kijana shekeli hamsini za fedha, kisha na awe mkewe, kwa kuwa amemtweza; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote.

 

Tendo la kushuhudia ushuhuda wa uwongo dhidi ya mke na kumtenganisha na mumewe kunasababisha hatimaye kupoteza haki zake kwa mume wake anapoachika na kupewa talaka. Kwa kuwa anawajibika kwake katika maisha yake yote. Yeye asiyewatunza watu wa nyumbani mwake mwenyewe anakuwa ameikana imani na ni mbaya kuliko yule asiye amini.

 

Adhabu aliyostahili kupewa mwanaume anayembaka mchumba wake au mke wa mtu ni kifo, kama tunavyoona hapa. Na iwapo kama mwanamke amechukuliwa kwa nguvu kutoka mjini na hapigi kelele ndipo nay eye atauawa pia. Na iwapo kama ametwaliwa kwa nguvu na akapiga makelele ndipo mwanaume tu ndiye atakaye uawa. Tendo la kumtwaa mwanamke kwa kumtorosha kutoka mashambani ambaye hakuolewa, hukumu yake ni kutozwa mahari na atatakiwa kumuoa (kama watakutwa wote wawili wanafanya tendo la zinaa), na mwanaume mhusika hataruhusiwa kumuacha kwa sababu nyingine yoyote ile. Na iwapo kama mzazi atamkatalia kumpa binti yake mwanaume huyu ili amuoe, ndio atapewa adhabu tu ya kutoa mahari badala yake. Matendo yoyote yale ya kumbaka mwanamke au kumchukua kwa nguvu adhabu yake hayo yote ni kifo.

 

Sadaka ya Wivu

Hesabu 5:12-31 inasema: Nena na wana wa israeli, uwaambie, kama mke wa mtu ye yote akikengeuka, na kumkosa mumewe, 13 na mtu mume akalala naye kwa uasherati, na jambo hilo likamfichamania mumewe, likawa jambo lisilojulikana, na huyo mwanamke akawa najisi, wala hapana shahidi aliyeshuhudia juu yake, wala hakufumaniwa; 14 kisha mumewe akashikwa na roho ya wivu, akamwonea wivu mkewe, naye akawa najisi huyo mwanamke; au kama akiingiwa na roho ya wivu, akamwonea wivu mkewe, naye hakuwa na unajisi huyo mke; 15 ndipo huyo mume atamchukua mkewe, aende naye kwa kuhani, naye ataleta sadaka yake kwa ajili yake, yaani, sehemu ya kumi ya efa ya unga wa shayiri; asitie mafuta juu yake, wala asitie ubani juu yake; maana, ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho ya kukumbukia uovu. 16 Basi kuhani atamleta mwanamke akaribie, na kumweka mbele za Bwana; 17 kisha kuhani atatwaa maji matakatifu katika chombo cha udongo; kisha kuhani atatwaa katika vumbi lililo pale chini ya maskani, na kulitia katika hayo maji; 18 kisha kuhani atamweka mwanamke mbele za Bwana, naye atazifungua nywele za kichwani mwa huyo mwanamke, kisha atampa hiyo sadaka ya unga ya ukumbusho mikononi mwake, ambayo ni sadaka ya unga ya wivu, naye kuhani atakuwa na hayo maji ya uchungu yaletayo laana mkononi mwake; 19 tena kuhani atamwapisha huyo mwanamke, naye atamwambia mwanamke, Kwamba hakulala mtu mume pamoja nawe, tena kwamba hukukengeuka kuandama uchafu, uli chini ya mumeo, maji haya ya uchungu yaletayo laana yasikudhuru; 20 lakini kwamba umekengeuka uli chini ya mumeo, na kwamba u hali ya unajisi, na mtu mume amelala nawe, asiyekuwa mumeo; 21 hapo ndipo kuhani atamwapisha mwanamke kwa kiapo cha kuapiza, kisha kuhani atamwambia huyo mwanamke maneno haya, Bwana na akufanye wewe uwe laana na kiapo kati ya watu wako, hapo Bwana akufanyapo paja lako kupooza, na tumbo lako kuvimba; 22 na maji yaletayo laana yatakuingia matumboni mwako, na kukuvimbisha tumbo, na kukupoozesha paja lako; na mwanamke ataitika, Amina, Amina. 23 Kisha kuhani ataziandika laana hizo ndani ya kitabu, na kuzifuta katika maji ya uchungu; 24 kisha atamnywesha mwanamke hayo maji ya uchungu yaletayo laana; nayo maji yaletayo laana yataingia ndani yake, nayo yatageuka kuwa uchungu. 25 Kisha kuhani ataitwaa hiyo sadaka ya unga ya wivu, kwa kuiondoa mkononi mwa huyo mwanamke, naye ataitikisa sadaka ya unga mbele ya Bwana, na kuisongeza pale madhabahuni; 26 kisha kuhani atatwaa konzi moja ya sadaka ya unga, kuwa ni ukumbusho wake, na kuuteketeza madhabahuni, baadaye atamnywesha mwanamke hayo maji. 27 Kisha hapo atakapokwisha kumnywesha maji, ndipo itakapokuwa, kama amekuwa hali ya unajisi na kumkosa mumewe, hayo maji yaletayo laana yatamwingia ndani yake, nayo yatakuwa uchungu, na tumbo lake litavimba, na paja lake litapooza; na huyo mwanamke atakuwa laana kati ya watu wake. 28 Na kama mwanamke hakuwa na unajisi lakini yu safi; ndipo ataachiliwa, naye atazaa wana. 29 Hii ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na kupata unajisi; 30 au, roho ya wivu ikimwingia mtu mume, naye akamwonea wivu mkewe; ndipo atakapomweka huyo mwanamke mbele za Bwana, na kuhani atatenda juu yake sheria hii yote. 31 Na huyo mume atakuwa hana uovu, na mwanamke atauchukua uovu wake.  

 

Saikolojia ya mawazo ya wivu mara nyingi inahitaji kutawaliwa kwa namna ya udhibiti wa nje au vigezo ambatanishi, abavyo kwa kawaida huwa za kimapokeo ya kimila na yenye uchungu. Baadhi ya mawazo na mitizamo hii haifai kabisa na hazina maana wala nafasi kwa wateule. Hata hivyo, tatizo hili halipaswi kupewa nafasi kutokea. Mwenendo wetu haupaswi uwe wa kuonewa mashaka bali uwe wenye kukubalika na kuaminika bila kulaumiwa.

 

“Sadaka ya wivu” ilitolewa na Masihi mara moja tu na kwa watu wote. Roho Mtakatifu anasimama mahala pa kuhani. Na mtu akimdanganya Roho Mtakatifu adhabu yake ni kifo, kama ilivyotokea kwa kina Anania na mke wake Safira (Matendo 5:1-5). Kwa wengine kifo hakitokea kipindi hikihiki; hata hivyo, ni linabakia kuwa ni jambo la hakika.

 

Kuuawa kwa Kuhani

Mambo ya Walawi 21:7-15 Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake. 8 Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi Bwana niwatakasaye ninyi ni mtakatifu. 9 Na binti ya kuhani ye yote atakapojitia unajisi kwa ukahaba, amemtia unajisi baba yake; atachomwa moto. 10 Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake; 11 wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake; 12 wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake u juu yake; mimi ndimi Bwana. 13 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake. 14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe. 15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye.  

 

Kuhani Mkuu wa Hekalu la Mungu ni Masihi, na aliingia patakatifu mara moja tu na kwa ajili ya wote, akiwa kama Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa, mnamo mwaka 30BK. Makuhani wote wanaotumika Kanisani wanafanya hivyo kwa niaba yake. Kwa hoyo wanatakiwa kuwa watakatifu kama yeye alivyo mtakatifu. Wateule kwa vyovyote vile hawapaswi kulitia unajisi Hekalu, Hekalu ambalo ni wao wenyewe. Kuhusu hali ya kunajisika kwa ajili ya wafu imeandikwa hapa chini.

 

Kukilinda kizazi dhidi ya Matendo ya Kipagani

Mkazo mzima na wenye msingi wa amri ya saba unalenga kuwezesha kuzaliwa kwa taifa takatifu, na watu safi waliojitoa kwa Mungu. Uhusiano wa kindoa haupaswi uwe ni kitu chenye kunajisika ili kwamba watu wasinajisike. Ni kwa ajili hii ndipo utakaso wa kizazi ulilindwa na matumizi yao katika kumtumikia Mungu kwenye taifa lao kulilindwa pia. Hakuna tena watoto walioruhusiwa kupitishwa kati ya moto ili kuwatoa sadaka ama wakfu kwa Moleki (cf. Mambo ya Walawi 18:21). Tendo hili la kuchukiza la ibada lililofanywa kwenye ibada za kumwabudu Moleki au Kemoshi au mungu Mwezi Sin aliyechongwa kwa umbo la Ndama wa Dhahabu ambao hata Israeli walimwabudu kule Sinai kwa jinsi alivyokuwa anaoitwa na kujulikana kwa majina tofauti tofauti lakini alikuwa ni huyu huyu mmoja, na ibada yake ilihusisha utoaji wa dhabihu na pia (hasa Waashuru) dhabihu hii ilifanywa kwa kuwala watoto wadogo na ilikuwa ni machukizo makubwa sana kwa Bwana. Ka mujibu wa utafiti uliofanywa na Abbe MacGeoghegan, ibada hii ya kumwabudu Ndama wa Dhahabu iliendelea kufanywa na watu wa kabila la Wamilesiani wa nchini Ireland wakimfanya kuwa ni mungu wa pili kwa umaarufu akitanguliwa na miungu mingine kina Oak na Mistletoe hadi kilipokuja kipindi cha zama ya Ukristo (kwa kujibu wa mtunzi MacGeoghegan-Mitchell, kitabu chake cha History of Ireland (Historia ya Ireland), Sadlier, NY, 1868, ukurasa wa 65). Dini hii inayoendana kwa imani ya miungu mitatu katika umoja yaani mungu wa Utatu wa Waashuru ilikuwa maarufu sana kwa Wafoeniki, (Phoenicians), Wakathagini (Carthaginians), Wagauli (Gauls), Wasythiani (Scythians), Wayunani (Greeks) na Warumi (Romans). Hii ndiyo sababu iliyopelekea imani ya Utatu kuanzishwa na kuingizwa kwenye imani ya kikristo na kutetewa kwa nguvu zote na Warumi na Waselti. Ibada na matendo ya kuwala watoto na mbwa viliendelea huko hadi kipindi cha kuanguka na kuangamizwa kwa Carthage. Matendo haya yaliendelea kufanywa na Wakarthagini hata siku za utawala wa Darius I, ambaye alikichukulia kitendo hiki kuwa ni cha kikatili na ushetani mkubwa.

 

Wa Milesiani wa Ki-Irish hawakuwa peke yao kwenye utoaji huu wa dhabihu na ulaji wa nyama za binadamu (mara nyingi ilikuwa kwa sababu za kishirikina). Polybius ameandika kwamba [H]Annibal alikataa wazo alilipewa akishauriwa na Gauls la kula nyama za wanadamu. Lilikuwa ni tendo walilolifanya na kuzoeleka na watu wa makabila ya Irish, Gauls, Britons, Spaniards, Scythians na mataifa meingine mengi. Strabo, (kwenye kitabu chake cha Jiografia yaani Geography) kwenya karne ya kwanza KK, aliandika kwamba hawa wa-Irish walikuwa wana wala wafu wao na hasa wazazi wao. Hii inazifanya sheria zilizo kwenye Biblia kuhusu kutojitia unajisi kwa makuhani kwa ajili ya waliokufa kuwa ni jambo lenye kuogopesha sana na la kweli na lenye maana yake kamilifu. Jerome aliwataja pia kuwa Wascotish wa Uingereza kuwa ni miongoni mwa walaji wa nyama za watu katika kipindi chake, na kwamba aliwawashuhudia mwenyewe wakifanya hivyo wa-Gaul kipindi cha mwishoni mwa karne ya nne (sona kitabu cha MacGeoghegan, ibid., ukurasa wa 67).

 

Matumizi ya alama ya mwezi mpevu pamoja na nyota ambavyo vimejipenyeza hata kwenye Uislamu vinahusiana na ibada za kale za kuabudu Mungu Mwezi aliyejulikana kwa jina la Sin (soma jarida la Ndama wa Dhahabu (Na. 222) [The Golden Calf (No. 222)]. Jones na Pennick (kwenye kitabu chao cha Historia ya Ulaya ya Kipagani [A History of Pagan Europe], Routledge, London and New York, 1995, pp. 77ff.) wanaandika kwamba ilea lama ya mwezi mpevu na nyota inayotumika na Waislamu inaashiria kuipa heshima na kuiendeleza ibada ya kumuabudu mungu mwezi aitwaye Sin ambaye tayari alikuwa ameanza kuabudiwa hapo zamani akijulikana na kuchongwa kwa umbo la miungu mitatu ya kike ambao kwa Kiarabu walijulikana kwa majina ya Al’lat, Al-Uzzah na Manat. Mfumo wa imani ya Utatu ulijulikana na kupata mashiko sana na Waashuru na ulikutikana kwa wa-Celts ukiwa na umbo hilohilo la Kiutatu na likiwa na miungu mitatu ya kike ambao nnoja alikuwa ni Bridgit (au Brigit). Mfumo huu wa Kiutatu ulikuwa pia una miungu mitatu ambao ni Esus, Taranis na Teutates. Hawa pamoja na mfumo wa Kiutatu walikuwa ni sehemu ya mfumo huo huo wa Majipu mtakatifu na mungu mwezi aitwaye Sin, ambaye aliambatanishwa pia kwenye ibada. Haya Majipu Matakatifu walichanganywa na kugawiwa watu pamoja na matumbo ya wanadamu kiasi kwamba hata wa-Druids wasiingie ndani yake kwa wakati wake fulani. Mji wa Sardinia (Sardi) ulikuwa ni ngome kuu wa imani na ibada hizi za kipagani hadi kwenye karne ya kumi na moja, na wakawahonga kwa rushwa mahakimu ili wasihumuku watu waliofanya mambo haya.

 

Imani hii ilikuwa ni ya kawaida huko Ireland na ulaji wa nyama za wanadamu lilikuwa ni jambo la kawaida tu kwa maeneo yote mawili, yaani kwa wa-Scots, waliokuja kutoka Ireland wakati ilipokuwa inaitwa Scotia. Uchimbuzi wa kwenye miamba ya kale kwenye Jimbo la Sligo unaonyesha umeonyesha kaburi kubwa la pamoja lililokuweko huko lililozikwa maelfu ya watu, kwa kiasi kingi zaidi ya kile ambacho kilipaswa kusaidiwa na nchi zilizokuwa karibu yao. Kuna watu wengi kwa mamia ya watu wa aina hii waliozikwa kwenye makaburi kama haya huko nchini Ireland lakini yaleya Sligo yanaonekana kuwa ni kubwa zaidi.

 

Wataalamu wa kuyachimbua mambo kale wamegundua hivi karibuni kuwa kuna watu waliokuwa wamechomwa moto kwa kutumia mafuta yaliyotoka kwenye miili yao wenyewe na halafu (kama mwanazuoni mmoja alivyosema radioni alipokuwa anafanyiwa mahojiano) kwamba “yaonekana ni ndugu zao ndio walifanya hivyo kwa ajili ya sikukuu au baadae kidogo”. Hitimisho la wazi kama alilolifanya Strabo kuwa tukio hili halikufanyika mapema sana bali ni kwenye karne ya kwanza, ambapo ya kale yaliweza kudharauliwa na kuyapisha yaliyokuweko kipindi hicho (kama alivyofanya MacGeoghegan wakati alipojionea mazishi yakifanywa). Waliwala wafu wao. Ukweli ni kwamba, wanadamu, na hasa watoto wadogo walitokoswa au kukaushwa kwa maumbo ya miungu, au waliteketezwa kwenye moto kwenye maeneo yote waliyokaa Waashuru na katika ulimwengu wote wa Wafoeniki. Wacelti wa Kirumi na kinamama wa Kifoeniki walilichukulia kambo hilo kama kitu ch kujivunia na la fahari kwa kujiliwaza kwamba wakifanya hivyo watawaliwaza na kuwafariji watoto wao wasijisikie vibaya walipokuwa wanawaoka wakiwa hai kwa walipojisia kulia kwa maumivu makali na kutweta kwa uchungu, kelele zao ziilifunikwa kwa kupiga ngoma na parapanda (soma kitabu cha MacGeoghegan, ibid., kurasa 65-73).

 

Dini na mila hii pia ilikutikana huko Tiro na kwa watu miongoni mwa Wafoeniki, na iliendelea kwa kitambo kirefu huko na hata kwa baadhi ya Wakanaani. Wale waliokuwa hawana watoto waliwanunua kutoka kwa watu maskini ili wasikose kuwa na kafara ya kutoa inayohitajika. Watoto hawa baada ya kutokoswa hatima yao ilikuwa ni aidha waliteketezwa kabisa kwa kuchomwa moto kwenye tanuu au waliwekwa mbele ya sanamu la Saturn, ambako waliteketezwa motoni. Kuangushwa kwa Carthage na Agathocles kuliaminiwa kuwa kulisababishwa na makosa waliyoyafanya kwa wao kuwatoa kafara watoto wao waliokuwa wa daraja la pili kwa ubora, na pia kuwa walikuwa watoto wa wageni na watumwa, na kuwa ndio waliwatoa na kumpa mungu wao aliyeundwa kwa umbo la Sarturn (ambaye ndiye Sartunalia) badala ya kuwatoa watoto wao wenyewe wanaowatoa kila mara wa daraja la kwanza kwa ubora. Ndipo walipoamua kuwatoa kafara watu wazawa wa nchi wa daraja la kwanza kwa ubora idadi ya zaidi ya mia tatu waliojitoa kwa hiyari yao wenyewe, wakajitolea wateketezwe ili kumtuliza hasira mungu wao na awasamehe makosa na uovu wote walioutenda uliofanana sawa na kumdharau (MacGeoghegan, ukurasa 67-68).

 

Kwa mujibu wa taarifa inayojulikana kama ya Cornelius Walford kuhusu njaa kuu iliyoikumba dunia katika karne ya pili, ulaji wa nyama za wanadamu ulifanyika na kunukuliwa miongoni mwa wa- Irish uliofanyika katika kipindi cha njaa ya miaka ya 1588-89 na 1601-03 (soma kitabu cha Reay Tannahill’s Flesh and Blood (Damu na Nyama) kwa historia yote ya walaji hawa wa nyama za binadamu wenzao na wengine wanaofanya hivyo). Tukio la mwisho la ukoo au kabila linalikula watu lililotukia huko Uingereza lilisikika huko Western Highlands huko Scotland lililotukia mnamo karne ya kumi na saba. Kikosi cha takriban wanajeshi 400 wanaume kikiwa chini ya Mfalme James VI wa Scotland, na pia James I wa England, kilipekekwa kwa amri moja tu ya kuangamiza watu wote wa ukoo wa Sawney Beane waliokuwa wanaishi mapangoni huko Galloway. Watu walikamatwa na kuuawa huko Edinburgh bila kufanyiwa mashitaka au kupelekwa mahakamani, wanaume wakachaangwa vipande vipande na kuwekwa  chungu chungu na wanawake wakateketezwa kwa moto. Inasemekana kwamba hakuna mgeni au msafiri aliyeachwa hai na salama siku hiyo huko Western Highlands hadi jambo hili lilipohitimishwa kwa faida na maslahi ya wanadamu.

 

Matendo ya kuwinda ili kukipata kichwa cha wanadamu na ulaji wa nyama za wanadamu yaliwepo pia huko nchini Indonesia, na kwenye Bahari ya Coral na Australia yaliendelea hadi kwenye karne hii. Wanawake wa Kiaborigini pia walisemekana kuwa walikuwa wanawatoa watoto wao kwa kupeana na mtu wa pili miongoni mwa ndugu zao au na ndugu aliyekuwa kwenye ukoo wao inapotokea mambo kuwa magumu kwao. Ulaji wa binadamu uliendelea pia huko Papua-New Guinea na kwenye maeneo fulani ya Kusini Mashariki mwa Bara la Asia na huko Afrika hata baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambako ugonjwa wa kucheka (ugonjwa unaotokana na ulaji wa nyama za wanadamu) ulikuwa bado unaripotiwa kuwepo. Baadhi ya Wapagani wanaendelea bado kutoa kafara za wanadamu kwa siri hadi leo.

 

Dini hiii ya kuabudu mungu Mwezi aitwaye Sin aliyeundwa kwa mwonekano wa Ndama wa Dhahabu au Moleki, au kwa mwonekano wake wa Kiutatu ndio unaoendelea kwa mtindo wa kisasa na kimamboleo, lakini ndiyo mfumo wa dini wenye kuchukiza sana kuliko, na ni machukizo makuu sana mno. Mungu ameulaani na kuukataza sana pamoja na imani zake na mifumo yake yote, lakini bado ungali ukiendelezwa na kushikiliwa kuaminiwa hadi leo hii (soma majarida ya Chanzo cha Krismas na Easter (Na. 235) na Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya 1 Bustani ya Edeni (Na. 246) [The Origins of Christmas and Easter (No. 235) and The Doctrine of Original Sin Part I The Garden of Eden (No. 246)].

 

Mfumo wote wa dini hii umefungamana na matendo ya zinaa yanayoendana kama sharti muhimu na moja wapo kwenye Dini hii ya Kisirisiri au ya Kimisteria. Uzinifu, ulawiti, tama za mwili, utoaji wa kafara za wanadamu, na maadhimisho ya sikukuu za Krismas na Easter, yalikuwa ni mambo yanayokwenda sambamba pasipo kuyatenganisha kwenye ibada za wapagani, na ni mambo yaliyoorodheshwa na kupangiliwa kwenye ratiba za kalenda na utaratibu wao wa kuabudu na ni mambo ambayo yanaendelea hivyo hadi leo. Dunia nzima, wakiwemo Israeli, ipo kwenye mfumo huu wa mahusiano ya kiasherati kufanywa na mungu wa dunia hii lakini haijui hilo.

 

Mahusianp Mengine Yaliyokatazwa

Kuna idadi kadhaa ya aina ya mahusiano yaliyokatazwa kabisa, ambayo kwayo yanachukuliwa kwa mkazo mkubwa sana.

 

Ukahaba

Mambo ya Walawi 19:29 Usimnajisi binti yako, ili kumfanya awe kahaba; isiwe hiyo nchi kuuandama ukahaba, na nchi kujawa na uovu mkuu.

 

Kufanya ukahaba na uasherati na sanamu

Hesabu 25:1-18 inasema: Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu;  2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli. 4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli. 5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. 6 Na tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania. 7 Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake; 8 akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. 9 Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao. 10 Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, 11 Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu. 12 Basi kwa hiyo, sema, Tazama, nampa yeye agano langu la amani; 13 tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli. 14 Basi jina la Mwisraeli huyo aliyeuawa pamoja na yule mwanamke Mmidiani, aliitwa Zimri, mwana wa Salu, mkuu wa nyumba ya baba zake, katika kabila la Simeoni. 15 Na jina la huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa, aliitwa Kozbi, binti Suri; naye alikuwa kichwa cha watu wa nyumba ya baba zake huko Midiani 16 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 17 Wasumbue Wamidiani, na kuwapiga; 18 kwa sababu wao wawasumbua ninyi kwa hila zao, ambazo kwa hizo wamewadanganya ninyi katika jambo la Peori, na katika jambo la huyo Kozbi, binti wa mkuu wa Midiani, umbu lao, huyo aliyeuawa siku hiyo ya pigo katika jambo la Peori.

 

Kama tuonavyo hapo juu, matendo ya uasherati yalijumuishwa kwenye mafundisho ya dini hizi zilizoabudu miungu migeni. Haya ni matokeo ya kuyaendekeza mawazo au hisia chafu kama tunavyoona kwenye Warumi sura ya 1 (hususan aya za 18-32), kwa kuwa kuhani ni mtu anayeichukua kweli na kuwapelekea wasio haki au wasiotakasika.

 

Matendo ya Sodoma au Ufiraji

Mambo ya Walawi 18:22 Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.

 

Ufiraji ni machukizo, na kila anayetependa kufanyiwa matendo haya akiwa kama shoga au mfiraji, wote hawa hawana sehemu katika ufalme wa Mungu, isipokuwa kama tu atafanya toba na kuzaa matunda yanayofuatana na toba yake aliyoifanya.

 

Kumbukumbu la Torati 23:17-18 Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume. 18 Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili (cf. Mambo ya Walawi 20:13).

 

Katika kumbukumbu la Torati 23:18 watu hawa wanaopenda matendo haya ya kufira wametajwa kuwa ni kama mbwa wakielezewa hivyo pia kwenye Ufunuo 22:15 wakitajwa kwamba hawana sehemu katika Ufalme wa Mungu (Warumi 1:24-27).

Warumi 1:24-27 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. 26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.

 

Kulala na mnyama

Tendo la kuzini na mnyama limekatazwa na linapaswa kuepukwa kabisa na wana wa Imani, sawa na pia tendo la kubadili matumizi ya asili.

Kutoka 22:19 Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.

 

Mambo ya Walawi 18:23 Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.

(pia soma Kumbukumbu la Torati 27:21)

 

Utumwa na maangamizo ni adhabu, na ilikuwa ni kwa sababu hii pamoja na tendo la kumuabudu Ashtaroth au Easter ndipo Mungu aliwamuru wenyeji Kanaani waangamizwe. Hakuna yeyote miongoni mwa waaminio anayetakiwa kufanya moja wapo ya mambo haya, tena kwana hakuna hata taifa lolote, wala mgeni anayesafiri alipita kati yao anayeruhusiwa kufanya hivyo.

Mambo ya Walawi 18:24-30 Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; 25 na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. 26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao. 30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Adhabu kwa Dhambi hii ya Uzinzi

Uzinifu umeharibu yale ambayo ni muhimu yanatakiwa yafuatwe au kufanywa. Mazingira ya kufanya ngono yanahitajika kufanywa kwenye ndoa tu. Iwapo kama ndoa haiwezekani, au imekataliwa na baba wa binti, ndipo mahari ya mwanamwali yanapaswa kulipwa yakiwa ni fidia.

Kutoka 22:16-18 Mtu akimshawishi mwanamwali, aliyeposwa na mume, na kulala naye, lazima atatoa mahari kwa ajili yake ili awe mkewe. 17 Ikiwa baba yake huyo mwanamwali akataa kabisa kumpa, atalipa fedha kama hesabu ya mahari ya mwanamwali ilivyo. 18 Usimwache mwanamke mchawi kuishi.

 

Tendo la zinaa linalazimu hukumu. Uasherati kwa mtazamo wa kiroho. Ujulikanao kama ushirikina, ni jambo linalostahili hukumu ya kifo (aya ya 18). Kwa kuwa dhambi zote ni kinyume na mapenzi ya Mungu na sio kuwa tunamtenda dhambi Mungu tu, bali na wanadamu pia, ambao tunawaumiza. Tunamtenda dhambi Mungu na ni kwake yeye tu peke yake.

Zaburi 51:1-4 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. 2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. 3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. 4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.

 

Iwapo kama mtumwa atafanya uzinifu akiwa kwenye milki na sio huru, ataadhibiwa kwa kuchapwa bakora aumijeledi. Hii ndiyo atakavyofanyia mtu anayeiba kazini kwake kwa kisingizio cha hali ngumu ya uchumi.

Mambo ya Walawi 19:20 Tena mtu ye yote alalaye na mwanamke aliye mjakazi, naye ameposwa na mume, wala hakukombolewa kwa lo lote, wala hakupewa uhuru; wataadhibiwa; hawatauawa, kwa sababu huyo mwanamke hakuwa huru.

 

Adhabu anayopewa mzinzi ni kifo na adhabu wanayopewa waasherati wote ni kuuawa pia, sawa na zinavyosema Amri Kumi za Mungu na kanuni zake zinzosisitiza hukumu ya kifo.

Mambo ya Walawi 20:10-17 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa. 11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. 12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao. 13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. 14 Tena mtu mume akimwoa mke pamoja na mama yake, ni uovu mkuu; atachomwa moto, yeye mume na hao wanawake pia; ili kwamba usiwe uovu kati yenu. 15 Tena mtu mume akilala na mnyama, hakika atauawa; nanyi mtamwua huyo mnyama. 16 Tena mwanamke akimkaribia mnyama ye yote, na kulala pamoja naye, mtamwua huyo mwanamke, na mnyama pia; hakika watauawa; damu yao itakuwa ni juu yao. 17 Tena mtu mume akimwoa umbu lake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mume; ni jambo la aibu; watakatiliwa mbali mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa umbu lake; naye atauchukua uovu wake.

 

Abrahamu aliivunja amri hii kwa kumuoa binamu yake Sara na kwa hiyo alistahili kuadhibiwa sawa na sheria hii. Mungu aliingilia kati baada ya kipindi cha kujigeuza kwa ajili ya sheria zao. Kwa kweli, mataifa lote la Israeli limetoka kwenye familia ya naona hii, yaani iliyoivunja sheria. Pia Abrahamu alikuwa ni baba wa imani na taifa la Israeli lilikuwa ni chombo tu cha kutimiliza jambo hili. Kwa nini jambo hili liwe limeandikwa kwenye Maandiko Matakatifu na likionekana limekubaliwa? Jibu ni rahisi. Ilifanyika hivyo ili kutuonyesha tena uhusiano wa wateule kama wana kiume na wakike wa Mungu, ili kuashiria kwamba umuhimu wa mahusiano yoyote yanasimama au yanaanguka yenyewe mbele za Mungu bila kujali mazingira ua kuzaliwa kwao na dhambi zao. Mtoto aliyezaliwa kwenye mazingira yaliyo kinyume na sheria hayajalishi umuhimu wa wana wa Mungu.

 

Chini ya mfumo wa Kiutatu wa wapagani, utoaji kafara wa wanadamu na ulaji wa nyama za wanadamu ulipata nguvu sana miongoni mwao. Tofauti kati ya Torati ya Mungu na matendo ya wapagani ni mambo yaliyo dhahiri. Abrahamu alitumika ili kuonyesha jinsi Mungu hakuridhia au kuhitaji sadaka ya namna hiyo, hata kama ingetokewa kama alivyokuwa ameiihitaji. Dhabihu ya mtu mwenye imani ni kitu muhimu kuhitajika na kujinyenyekesha kwa kuyatoa maisha yake mtu katika kutumikiana ni muhimu kama Kristo alivyotuonyesha mfano wake. Sisi sote tumeitwa kwa uelewa mkubwa. Toba inatarajiwa kuonyeshwa na watu wote na jambo la mwisho au kikomo chetu ni kifo.

 

Amri hii inaendana na rehema na huruma, na hakuna mtu anayepaswa kuuawa bila kupewa fursa ya kutubu, kama tunavyoona kutokana mfano wa Yesu Kristo.

Yohana 8:1-11 inasema: [Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni. 2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha. 3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. 4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. 5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. 10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? 11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.

 

Mwenye kuhukumu ni Masihi, na ni kwa kupitia njia ya toba tu ndipo tunaletwa mbele ya Mungu aliye Hai tukiwa ni sehemu ya Hekalu lake (soma 1Wakorintho 5:1-13). Ni kutokana na mchakato wa mawazo haya mapotofu, ndipo hunyesha mazingira ya kilichoko rohoni (Marko 7:21).

 

Mchakato mzima wa fikra za ngono na ushoga huja kwa ajili ya kuachana na kuwa mabali na Mungu na yanatokana pia kutoka kwenye mawazo machafu yanayolingana na ibada ya sanamu. Dhumuni lote linalosemwa kwenye Warumi 1:1-32 ni kuonysha kwamba kutoka kwenye ibada za sanamu na ukweli, au hali ya kumuasi au kutomheshimu Mungu (kutoipenda au kuikana kweli ni dhambi na uasi) jambo linalotupelekea tufanye uzinifu au uasherati na kuwa na kiwango kisiocho cha kawaida cha kuvutiwa na tama za mwili, kama vile kufanya matendo ya ufiraji na ulaji wa nyama za wanadamu na uvunjifu wa kila amri ya Mungu. Ingawje uasherati na ufiraji havikutikani kwenye makatazo au hayajatajwa yakikatazwa rasmi kwenye moja ya Amri hizi Kumi lakini yanakutikana yakielezewa na kutakazwa kwenye maandiko mengine ya Torati, yakionekana kuhusiana na makatazo yaliyo kwenye zime amri Kumi lakini yakiwa yameandikwa kama kitu kinachoelezewa kipekee.

Warumi 1:28-32 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, 30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, 31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; 32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.

 

Wagalatia 5:19-21  Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu

 

Hqakuna atakayeweza kuurithi ufalme wa Mungu akiwa anaishi maisha haya ya uasherati, au kama atakuwa anayaishia aina nyingine yoyote ya uchafuko huu. Hata hivyo, tujue kwamba hatuhesabiwi haki kwa sheria au kwa kuishikilia kwetu hiyo. Utakatifu na haki yetu ni kama kitambaa kichafu (Isaya 64:6). Kinachotufanya kuokolewa sio juhudi zetu tuzifanyazo au kazi zetu tunazozifanywa kwa kufuata sheria ila ni kwa neema, na sio kwa kazi tunazozifanya kwa tohara ya miili yetu bali ni kwa tohara ya mioyo yetu katika Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:1-4). Iwapo kama tunahesabiwa haki kwa sheria, basi tuko mbali na neema. Je, hii inamaanisha kwamba tusizishike sheria? Pasipo sababu yoyote na kwa mazingira fulani inaonekana kama ni kweli, hususan kama itakuwa kwenye mapenzi ya Mungu na “hata kwenye utakaso wetu” ambao tunaupata kutokana na matendo ya uasherati (1Wathesalonike 4:3).

 

Dunia yote hiii pamoja na watu wake vitaharibiwa na Mungu aliye hai kwa kuwa hawataki kuzitubia kazi za mikono yao na uasherati wao na wizi.

Ufunuo 9:21 Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.

 

Uasherati wa dunia imetokana na mfumo wa uwongo wa mwanamke kahaba, anayefanya matendo ya uasherati na wafalme wa dunia (Ufunuo 14:8; 17:2-4; 18:3; 19:2) na kwa mfumo wa imani yake na mungu wa dunia hii ambaye amefanikiwa kuwawapofusha watu wote (2Wakorintho 4:4) na wameiendea njia ya uasherati na kufanya ukahaba (soma Hosea 4:1-19; Ezekieli 23:19-21). Mungu atawatia hukumuni wote hawa. Ameichukua mbegu ya wachawi na waasherati na watenda maovu na kuwashughulikia. Atawaondoa wenye haki na wenye rehema na hakuna atakaye liweka hili moyoni mwake, na hatimaye ataiharibu mbegu potovu au mbovu na hakutakuwa na amani (soma Isaya 57:1-21). Na hakuna atakayeweza kuokoka kwa kuwa tu eti kakulizaliwa kutokana na uasherati (Yohana 8:41-42). Ijulikane kwamba watu waliozaliwa kiharamu, yaani nje ya ndoa hawatakataliwa kuupokea wokovu.

Kumbukumbu la Torati 23:2 Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana.

 

Maana yake hapa ni kwamba inapotokea tu kuwa na mtoto wa nje ya ndoa, kutakuwa na watoto wa Mungu aliye hai.

 

Uvunjaji wa Amri unatokana na kukosekana kwa ukweli, rehema, na kumjua Mungu hapa duniani (Hosea 4:1 cf. 1mambo ya Nyakati 5:25).

 

Inatupasa pia kulindana kwa mazingira yote. Kuyaelewa kwetu mazingira ya mwanadamu kwa sasa kunafikia kwenye kiwango cha kutufanya sasa kuelewa misingi ya sayansi ya sheria hizi. Hata hivyo, kuna misingi ya kiroho kwenye kanuni zote za utakaso (soma jarida la Torati na Amri ya Sita (Na. 259) [Law and the Sixth Commandment (No. 259)].

 

Uhusiano usiozingatia usafi umeamriwa kuhumumiwa kwa mtu huyo kutengwa mbali na watu wake au kuondolewa mbali au kuuawa. Kwa hiyo, matendo kama haya yanamfanya mtu aondolewe Kanisani na kwenye imani. Hukumu iliyowekwa kwa mambo mengine ni kufa mgumba bila kuzaa mtoto.

Mambo ya Walawi 20:18-24 Tena mtu mume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amelifunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watakatiliwa mbali na watu wao. 19 Usifunue utupu wa umbu la mama yako, wala umbu la baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watauchukua uovu wao. 20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana. 21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana. 22 Basi zishikeni amri zangu zote, na hukumu zangu zote, na kuzifanya; ili kwamba hiyo nchi, ambayo nawapeleka ninyi kukaa, isiwatapike. 23 Nanyi msiende kwa kuziandama desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia. 24 Lakini mimi nimewaambia ninyi, Mtairithi nchi yao, nami nitawapa ninyi kuimiliki; nchi iliyojaa maziwa na asali; mimi ni Bwana, Mungu wenu, niliyewatenga ninyi na mataifa.

 

Jukumu la wanaume katika jamii

Kama matuo ya Israeli yalivyotakiwa yawe safi. Kutokana na amri ya tano tuliona kwamba amri hii ilikuwa kwa ajili yetu s the camp of Israel was to be kept clean so toisio ili kutufanya tuwe watakatifu. Hapa tunaona kwamba inaenelea kwenye makazi yetu na kwa watu wetu ili kwamba Mungu asikione kitu kichafu na kisichotakiwa miongoni mwetu.

Kumbukumbu la Torati 23:7-14 inasema: Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake. 8 Wana wao watakaozaliwa kizazi cha tatu na waingie katika mkutano wa Bwana. 9 Utakapotoka kwenda juu ya adui zako nawe u katika marago, jilinde na kila neno baya. 10 Akiwa kwenu mtu awaye yote asiyekuwa ni tohara kwa ajili ya yaliyomtukia usiku, na atoke nje ya kituo, wala asiingie ndani ya kituo; 11 lakini na iwe ikaribiapo jioni, yeye ataoga maji; na jua likiisha kuchwa ataingia ndani ya kituo. 12 Tena uwe na mahali nje ya kituo, kwa kutokea nje; 13nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho; 14 kwa kuwa Bwana. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha.

 

Wokovu ni wa watu wa Mataifa. Hali ya taifa la Israeli imeenea hadi kwao. Yusufu alikuwa pia Misri, akiwa kama mama wa Efraimu na Manase waliokuwa Wamisri. Kuna mnyororo wa uzao wa Wamataifa kwa wote, yaani Yuda na Israeli. Mungu anafanya kazi ndani yetu.

 

Utaratibu wa kifamilia ni mmoja na wanaume kwenye familia wamepewa majukumu kuwa ndio wanaohakikisha ustawi na hali ya mfumo wa familia, na hatimaye husababisha mafanikio ya kabila na taifa. Kwa wale waliojifanya matoashi kwa ajili ya kulitumikia Kanisa wanamajukumu ya kulifanya kanisa liendelee kufanya vizuri.

 

Majukumu ya wanawake katika jamii

Wanaume wanatakiwa kuwaheshimu wanawake.

1Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

 

Je, kwa wale ambao hawajao au kuolewa itakuwaje? Bwana ameweka wanaume na wanawake kwenye familia na kwenye Kanisa kama familia ya Mungu. Tumejionea kwamba wanawake wanatakiwa watendewe kama ndugu wapendwa na kwamba hakuna mwanamke mateka anayeweza kuchukuliwa katika Israeli kuwa mke na kunfanya asiwe na haki sawa (Kumgukumgu la Torati 21:10-14).

 

Kitabu cha Mithali kinaonyesha kwamba mwanamke ana majukumu muhimu ya kufanya. Biblia iko wazi kwa jambo moja, na hiyo inaonekana kuwa kikomo pekee cha majukumu ya wanawake ni kwamba hawawezi wala kuruhusiwa kuwa wachungaji au makuhani. Wao wameondolewa pia kwenda vitani kwa mujibu wa sheria.

 

Wotw wawili, yaani wanawake na wanaume wako sawa katika ufalme wa Mungu, ambako hakutakuwa na kuoa wala kuolewa na watafanana kama malaika wa Mungu. Roho Mtakatifu pia anakaa kwao na kuwapa uweza na kuwabadilisha kutoka kuwa watu wa mwilini na kuwa watu wa rohoni. Mwanamke amefungwa kwa mumewe kwa agano la ndoa, na haki za mwanamke kwenye ndoa zilizompelekea hadi kula kiapo cha nadhiri zimefafanuliwa kwa kina kwenye jarida la  Torati na Amri ya Tano (Na. 258) [Law and the Fifth Commandment (No. 258)] (pia soma Hesabu 30: 6-10).

 

Kuna tofauti kubwa sana kwenye masuala ya uvaaji na jinsi ya kumtofautisha mwanamke na mwanaume.

Kumbukumbu la Torati 22:5  Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.

 

Nyele ni jambo mojawapo la wazi linaloweka tufauti kama ilivyo kwenye mapambo ya uvaaji wa tunu za dhahabu, ambazo mara nyingi na kwa kiasi kikubwa ni mambo yanayotokana na asili ya wapagani (soma jarida la Asili ya Uvaaji wa Vikuku Masikioni na Vito vya Thamani Katika Siku za Kale (Na. 197) [The Origin of the Wearing of Earrings and Jewellery in Ancient Times (No. 197)].

 

Ulinzi wa wanawake kwenye ndoa au mahusiano ya kiuchumi

Nyingi ya sheria hizi zimeandikwa zikilenga kuwalinda wanawake dhidi ya mambo ya kijamii ambayo yanaonekana kuwa ni magumu sana kuliko yalivyo leo. Hata hivyo hii ni dhana fikirika tu kama inavyotiliwa chumvi na watu wa kwenye jamii zetu ambao wanaharibiwa kwa kutumiliwa mbinu kubwa na mawazo au fikra potofu ambayo ni uadui na Mungu. Upungufu wa maadili kwenye jamii zetu kwa sasa kumefikia kiwangi cha kwamba kutufanya tuwe kwenye siku mbaya za mwisho, na ambazo zimekuwa ni ngome kama ilivyokuwa siku za Sodoma na Gomora. Mungu ataingilia kati kwa haraka ili kukomeshya hali hii kabla hatujajiharibu wenyewe na Masihi atakuja kuanzisha utawala wake utakaoendana na sheria hizi za torati.

 

Wote wawili, yaani watoto wa kiume na wakike wanaletwa kwenye agano lenye uhusiano na Israeli na kwa Mungu wa Pekee na wa Kweli. Mwanaume anatahiriwa akiwa mtoto na kisha anatengwa mbali kwa utakaso wa mama yake. Na ndivyo ilivyo kwa mwanamke, naye anatengwa mbali na kutofautishwa kwa maana utofauti (Mambo ya Walawi 12:2-5). Tofauti hizi hufanyika ili kuwalinda wanawake dhidi ya watoto wao ikiwa ni sehemu ya sheria na hawatakiwi watengwe mbali kimchezo mchezo au ki mashara. Hakuna Mmataifa mwongofu aliyelazimika kufanyiwa tohara (Matendo 15:1-30).

 

Iliwapasa wanawake kulindwa na wanaume dhidi ya mambo mabaya sana yanayoweza kutokea yanayotokea kama matokeo ya shughuli za mwanaume (Mithali 5:15-19; pia soma 18:4). Hairuhusiwi kumwingilia mwanamke akiwa kwenye kipindi cha kutumia cha kike au akiwa kwenye mazingira yanayofanana na hayo.

Mambo ya Walawi 18:19 Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake

 

Kwa hiyo, ni wajibu pia wa mwanamke kumlinda mwanaume.

 

Mwongozo wa jinsi ya kuwanunua watumwa ulikuwepo tangu mwanzo na uliwekwa na Torati ya Mungu. Hata hivyo, kulikuwa na idadi ya miongozo muhimu iliyowekwa na sheria ambazo zinapelekea masomo ya kujifunza kwetu sisi leo.

Kutoka 21:7-11 Mtu akimwuza binti yake awe kijakazi, hatatoka yeye kama watumwa wa kiume watokavyo. 8 Kwamba bwana wake hakupendezewa naye, akiwa amemposa, ndipo atakubali akombolewe; hana amri yeye kumwuza aende kwa watu wageni maana amemtenda kwa udanganyifu. 9 Kwamba amposa mwanawe, atamtendea kama desturi zipasazo binti zake. 10 Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia. 11 Kwamba hamfanyii mambo haya matatu, ndipo atatoka aende bure, pasipo kutolewa mali.

 

Hakuna mtu anayepaswa kupunzuzwa ama kuondolewa kwenye masuala ya kifedha na kiuchumi kwa kiasi cha kufanya kwamba utaifa wao au nafasi yao kulifanya suala la ndoa kuwa ni uhusiano wa kimuwasho au wa kuyatimiza mapenzi ya mwili tu na wenye ubaguzi. Hakuna mtu anayeingia kwenye ndoa kwa makubaliano ya kifedha na kwa kuyaathiri ama kuyavunja mambo anayopaswa kupewa mke kwa muda mrefu, au kwa shemejiiwa kike, au kushikilia uhuru wao.

 

Mungu ndiye awalindaye mayatima na wajane (Yeremia 49:11). Wanawake kwenye jamii wanawekwa pamoja kwa mujibu wa Torati ya Mungu kwa utaratibu mahsusi. Kile kinachoitwa siku hizi kuwa jumuia ya Kikristo na haifanyikazi na wala haijawahi kutenda kazi. Haiwezi kufanya kazi kwa kuwa haijaweka msingi wake kwenye Torati ya Mungu. Mafundisho yao yote ya msingi wa umoja wao kwa kweli yanalenga kuzigeuza Sheria au Amri za Mungu na yenye kuiharibu sayari hii. Mfumo na dini ya uwongo imeibuka na kufanya kazi yake kwa mtindo wa kisirisiri sana kwa wanadamu unasababisha kuwashushia hadhi kabisa wote wawili, yaani wanaume na wanawake, na hasa ni kwa kiasi kikubwa wanawake. Na kwa kweli mchanganyiko ambao watu waovu au mfumo wao na dini zilizokengeuka maadili umechukua mafundisho ya Kikristo lakini wakitumia mfumo wa kipagani wa mungu wa utatu, ne kuuendeleza kwa kwenda mbele kwa viwango mbali mbali wa jinsi hiyohiyo isiyokoma kwenye imani mbalimbali za Ukristo wa uwongo au kwa usahihi zaidi twaweza kuuita ni Ugnosisi uliojibadili sura tu.

 

Makosa na hukumu zake

Kutoka 21:16-27 inasema: Yeye amwibaye mtu, na kumwuza, au akipatikana mkononi mwake, sharti atauawa huyo 17 Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa. 18 Watu wakigombana, na mmoja akimpiga mwenziwe kwa jiwe, au kwa konde, asife, lakini yualazwa kitandani mwake; 19 atakapoinuka tena na kuenenda nje kwa kutegemea fimbo, ndipo hapo yule aliyempiga ataachwa; ila atamlipa kwa ajili ya hayo majira yake yaliyompotea, naye atamwuguza hata apone kabisa. 20 Mtu akimpiga mtumwa wake, au kijakazi chake, kwa fimbo, naye akifa mkononi mwake, hana budi ataadhibiwa. 21 Lakini akipona siku moja au mbili hataadhibiwa; maana, ni mali yake. 22 Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema. 23 Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai, 24 jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, 25 kuteketeza kwa kuteketeza, jeraha kwa jeraha, chubuko kwa ajili ya chubuko. 26 Mtu akimpiga mtumwa wake jicho, au jicho la kijakazi chake, na kuliharibu; atamwacha huru kwa ajili ya jicho lake. 27 Au akimpiga mtumwa wake jino likang'oka, au jino la kijakazi chake, atamwacha huru kwa ajili ya jino lake.

 

Hukumu ya matukio ya kukoseana au kufanyiana maovu ambayo yanaikumba familia na yenye kuleta madhara mara nyingi ilikuwa ni kifo. Sheria inailinda familia na kuzaa matunda kwenye ndoa.

 

Laana ya taifa inasimama na kuendelea bila kukoma.

Kumbukumbu la Torati 27:20-23  Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina. 21 Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina. 22 Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina. 23 Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.

 

Kuna adhabu anayopewa mtu kwa kuivunja amri ya saba na sheria nyingine ndogo ndogo. Baadhi ya matendo ya mahusiano haya huadhibiwa moja kwa moja na Mungu mwenyewe. Mungu aliifunga nyumba yote ya Farao kwa kuwa farao alimchukua Sara, akiwa hajui kuwa alikuwa ni mke wa Abrahamu, ingawaje ni Abrahamu aliyemsababishia kufanya dhambi hii kwa kunyamaza kwake kimya, lakini ni Farao ndiye aliyeadhibiwa.

 

Bwana atatoa hukumu yake kwa haki na kweli (Zaburi 96:11-13). Uvunjaji wa waziwazi wa amri za Mungu unapaswa ukemewe na jamii, kama tunavyomuona Masihi na yule mwanamke mzinzi, ambapo maonyo elekevu yalitosha kumfanya agundue ubaya wa kutenda dhambi.

 

Hatua ya pili baada ya kumuonya ni kumuadhibu kwa kumpiga mijeledi. Sheria inaruhusu mtu kuadhibiwa kwa kupigwa mijeledi isiyozidi idadi ya – hadi 39 – kutegemea kwa jinsi alivyoyarudia matendo haya. Hii itaamriwa na waamuzi au mahakimu wa mahakama inayosikiliza kesi hiyo.

Kumbukumbu la Torati 17:8-10 Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya daawa na daawa, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; 9 uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku hizo; uwaulize; nao watakuonyesha hukumu ya maamuzi; 10 nawe fanya sawasawa na hukumu watakayokuonyesha mahali hapo atakapochagua Bwana; nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza;

 

Hakuna kosa wala mazingiza yoyote yanayoruhusu mkosaji kupigwa zaidi ya mapigo ya mijeledi yanayozidi arobaini.

Kumbukumbu la Torati 25:1-3 Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu; 2 na iwe, ikimpasa kupigwa yule mwovu, alazwe chini na mwamuzi, na kupigwa mbele ya uso wake, kwa kadiri ya uovu wake, kwa kuhesabu. 3 Aweza kumpiga fimbo arobaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako, azidishapo kwa kumpiga fimbo nyingi juu ya hizi.

 

Adhabu ndiyo hitimisho na inapasa iendane na tendo lenyewe lilivyo bila kupendelea au kukomoa. Ili kuhakikisha kuwa kosa hili halirudiwi tena, ndiyo maana iliamriwa apigwe mapigo ya mijeledi thelathini na tisa ambayo waliambiwa watumie Waisraeli na Yuda wa hapo kale.

2Wakorintho 11:24-25 Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. 25 Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;

 

Paulo alipigwa mawe huko Listra (Matendo 14:19). Michirizi ya mapigo yake ilionyesha pia kuwa ilikuwa sio ya aina ya fimbo, ambazo Paulo alipigwa mara tatu kwa maisha yake (Matendo 16:22). Paulo hakuwa na makosa wala hakufanya uhalifu wowote, ila alihukumiwa pasipo kufuata sheria kwa kuwa hakukuweko adhabu ya kupigwa mawe katika sheria za mahakama zao. Tendo lililo kwenye Matendo 16:22 lilifanywa kwa amri ya liwali wa mahakama yao. Mchapa mijeledi alichukua fimbo (ndiyo maana limetumika neno Mbeba-fimbo na “mchapa fimbo”). Wapiga mawe walikusanyika pamoja na huyu mchapa mijeledi aliyekuwa anasikiliza shauri na kutoa hukumu. Ni kwenye masuala magumu tu ya kuendelea kukataa bila kutubu na kukubali kutii sheria za mahakama na kutowatii mahakimu ndiyo ahdabu yake ilikuwa ni kifo, na sio kwa mtumwa mwanamke, ambaye anaweza kupewa adhabu ya kupigwa tu.

 

Fidia ya kulipa fedha inaweza tu kuamriwa na mahakama kutegemeana na uzito wa kila madai. Kinachotakiwa tu ni kwamba haki itendeke tu na uovu uondolewe.

 

Uaminifu wa Mungu

Mungu ni mwaminifu na tunapaswa kuonyesha uaminifu wetu kwake. Kutokana na Amri Kuu na ya Kwanza, sisi ni mabibi arusi waaminifu wa Masihi. Kwa kuitunza Amri ya Saba tunaonyesha uaminifu wetu pia kwa mtazamo wa kimwili, ha hii ndiyo sababu wateule wanahukumiwa kwa kiwango kikubwa.

 

Kumbukumbu la Torati 5:32-33 Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na Bwana, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kuume wala wa kushoto. 33 Endeni njia yote aliyowaagiza Bwana, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.

 

Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata? (Mithali 20:6). Uasherati na ukahaba wa kidini ni mwanamke mzinifu anayefanya ukahaba na wanaume na mungu kwa uweza wake (Ufunuo 17:14). Tunapaswa kuwa waaminifu kwa Mungu na kwa kila mmoja wetu na kuwa hivyo kwa kila jambo, na ndipo Mungu atatufanya kuwa watawala kwa kweli na uaminifu (Mathayo 25:21).

 

Mungu ni mwaminifu kwetu. Tunapaswa sisi kuwa waaminifu pia (Zaburi 89:1-4) kwa kuwa sisi ni uzao wa ahadi kupitia kwa Masihi nasi tutadumu milele tukiwa ni elohim kama wa nyumbani mwake Daudi (Zekaria 12:8). Kwa kuwa fadhili na rehema zake zadumu hata milele na zinafika hata mbinguni (Zaburi 36:5-6).

 

Vifaa vyote vile vimeundwa kwa makusudi maalumu na Muumbaji na hatupaswi kuvitumia pasipo uangalifu au kuziweka mbali.

Warumi 9:14-26 inasema: Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha! 15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. 16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu. 17 Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. 18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu. 19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake? 20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi? 21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? 22 Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu; 23 tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu; 24 ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? 25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. 26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.

 

Kutofautisha kati ya Mema na Mabaya

Mti wa ujuzi wa mema na mabaya umebeba laana ndani yake (Mwanzo 3:17). Kumeonekana maara kumi kwenye kitabu cha Kumbukumbu la Torati mahali ambapo watu walilazimishwa kusema “Ameni” ili kuwazuia wasipate madhara ya ghadhabu yake Bwana, ili isiwawakie. (Kumbukumbu la Torati 11:17; Mambo ya Walawi 25:19; 26:4; Kumbukumbu la Torati 32:43; Isaya 24:4-6).

 

Kwa mujibu wa Torati, Amri zote zinatiririka kutoka kwa ile ijulikanayo kama Amri Iliyokuu nay a Kwanza, ili kuondoa uwezekano wa kuufanya mtiririko huu ulio kwenye Torati usiendelee kupotoshwa ama kuvunjwa. Jinsi pekee ya kujinasua na tama hii ya zinaa za kila namna ni kufanya toba na kudhamiria kuacha.

2Wakorintho 12:21 nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya.

 

q