Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[261]

 

 

 

Torati na Amri ya Nane ya Mungu

 (Toleo Na. 2.0 19981010-19990525-20120430)

 

Imeandikwa kuwa: Usiibe. Jarida hili mlinqafafanua mfumo mzima wa Torati ya Mungu, na jinsi unavyoendana na Amri zake jinsi zilivyofafanuliwa na manabii na jinsi Agano lilivyoekwa na kwenda pamoja na Usomaji wa Torati katika mwaka wa Saba ambao pia ni wa Sabato.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hakimiliki © 1998, 1999, 2012  Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Torati na Amri ya Nane

 


Imeandikwa kuwa: Usiibe (Kutoka 20:15; Mumbukumbu la Torati 5:19).

Mambo ya Walawi 19:11 Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo.

 

Mali ambayo ni milki ya Mungu

Vitu vyote kwa ujulma wake ni mali ya Mungu. Mungu ameweka sheria zinazohusiana na umulikaji sahihi na utunzaji wa sehemu inayozidi ya mali zake. Mungu amegawanya viumbe vyake kwa makundi mbalimbali kuhusu mali tunazoweza kuzitumia, na vitu ambazo havitakiwi tuzitumie. Mungu amefanya makundi akitilia maanani ya sheria alizoziweka ambazo kwazo tunapaswa kuzifuata.

 

Kuna sheria zinazohusu utunzaji wa mazingira ambazo tunaruhusiwa kuzifanya, na kuna sheria zihusuzo ulaji wa aina au makundi ya vyakula ambavyo na vile ambavyo tunaruhusiwa kula, na kuna sheria zinazohusu aina ya mavuno au mazalio yanayopatikana au kuvunwa kwenye ardhi ambazo tumeeruhusiwa kula na baadhi yake ambazo zimetengwa maalumu kwa matumizi muhimu kwa Mungu katika kuendeleza mwenendo wa uumbaji wake.

 

Amri ya Kwanza na utoaji zaka

Ulimwengu wote na uumbaji umetuama na kumtegemea Mungu wa Pekee na wa Kweli na kwa hiyo amri ya kwanza inaendana na amri hii ya mali na milki, ambazo Mungu amazichukulia kama ni yake kwa pale anapotumia usemi wa Kutoa Zaka (soma jarida la Utoaji wa Zaka (Na. 161) [Tithing (No. 161)]. Tendo la kutotoa zaka kwa kufuata utaratibu aliouweka Mungu ni sawa na wizi.

Malaki 3:1-12  Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. 2 Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; 3 naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki. 4 Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani. 5 Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi. 6 Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. 7 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani? 8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. 12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.

 

Mungu ameweka utaratibu ambao unahitaji kutoa zaka kwa ajili ya kukamilisha hitaji au sharti la ibada, kuwapa masikini, na kuwafanya watu wake waashiriki vyema bila uhitaji wowote wanapokwenda kuadhimisha Sikukuu zilizoamriwa na waendapo kuziadhimisha Sabato zake.

 

Sadaka inayotakiwa kumtolea Mungu inabidi iwe haina dosari kwa kuwa anazichukulia sadaka zilizo na dosari kuwa ni machukizo makubwa mbele zake.

Kumbukumb la Torati 17:1-4 Usimchinjie Bwana, Mungu wako, ng'ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako. 2 Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, 3 naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi; 4 ukiambiwa hayo nawe umeyasikia, ndipo utafute kwa bidii, na tazama, ikiwa ni kweli lina hakika jambo lile, kuwa yafanywa machukizo kama hayo katika Israeli

 

Sharti hili la kuhakikisha kuwa sadaka inayotolewa ni kamilifu na haina mawaa wala kunyanzi lolote linafananishwa na hali ambayo wanatakiwa kuwa wateule na wanadamu wote waliochaguliwa na kukukusudiwa tangu mwanzo kutoka kwa wanadamu wote.

 

Tena huenda sawa na dhamani ya zaka, kiwango cha kutoa ili kuwahesabu Israeli kilitolewa pia na kutofanya hivyo pia ni sawa na wizi.

Kutoka 30:11-16 Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 12 Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapompa Bwana kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapowahesabu. 13 Nacho watakachotoa ni hiki, kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini;) nusu shekeli kwa sadaka ya Bwana. 14 Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka ya Bwana. 15 Matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua, katika hiyo nusu shekeli, watakapotoa hiyo sadaka ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu. 16 Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
 

Sadaka hiii ya ondoleo la dhambi ililipwa na Masihi, nah ii ndiyo maana kwa sasa hakuna anayewahesabu Israeli, na wala hakuna mtu anayejua kiini cha imani kwa kuwa kwa sasa wokovu ni kwa wote, yaani Israeli na pia kwa Mataifa, na kwa sasa wote wanakuwa ni sehemu ya Hekalu la Mungu (1Wakorintho 3:17). Kuna hitimisho la muhimu kuhusu hilo hapa, kama Masihi alivyotununua kwa thamani, hatuna haki ya kujifanya sisi wenyewe kuwa ni Hekalu.

 

Wale wanaofanya kazi za Hekaluni wana haki ya kula vitu vya Hekaluni.

1Wakorintho 9:9-14 Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya ng'ombe? 10 Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake. 11 Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? 12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo. 13 Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? 14 Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.

 

Thawabu yetu ni kama tunavyoona kwenye Malaki na kkutoka kwenye Mithali, ni uaminifu.

Mithali 3:9-10 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. 10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.

 

Mithali 11:24-26 Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. 25 Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. 26 Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake.

 

Kuna idadi kadhaa ya maelekezo yanayoendana na baraka na sehemu yake kwenye jamii.

 

Torati yote ya Mungu imeelekezwa kwenye neema na haki. Huduma za Hekalu si za bure na wala sio hotuba zisizo na maana an mapokeo, bali zinahusu mambo ya adili na haki na utakatifu.

Mathayo 23:23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

Kwa mujibu wa taratibu za Melkizedeki, Hekalu lilipokea zaka kutoka kwa Walawi. Masihi atakapokuja Walawi watafanya taratibu mpya za huduma za kikuhani kwa jinsi iliyotakiwa au kustahili kuwa. Lawi alitoa zaka kwa Melkizedeki (jina hili maana yake ni Mfale Wangu ni Mwenye Haki na Mtakatifu) na kama ni cheo anachostahili mfalme wa Salemu au wa Urusalaimu. Jina na cheo hiki lilichukuliwa pia kama sawa na Adomu-Sedeki ambayo maana yake ni Bwana Wangu ni Mtakatifu au Bwana wa Haki na Utakatifu (Yoshua 10:1). Ni unabii uhusuo mjumuisho wao kwenye agizo jipya na imani.

Waebrania 7:1-10 Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; 3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. 4 Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara. 5 Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu. 6 Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi. 7 Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa. 8 Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yu hai. 9 Tena yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi; 10 kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.

Jambo hili limefafanuliwa vizuri kwenye jarida la Melkizedeki (Na. 128) [Melchisedek (No. 128)].

 

Mungu anataka na ameagiza sheria na kanuni iliyo kwenye Kumbukumbu la Torati 14:28 ishikwe na kwamba zaka ya mwaka wa tatu iletwe mbele zake Bwana.

Kumbukumbu la Torati 14:28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;

 

Zaka hii ya mwaka wa tatu wa mgawanyo huu wa kila miaka saba itakiwa ichukuliwe hadi mahali ambapo Sikukuu inafanyika katika nchi yetu. Mchakato mzima wa zaka ya pili itakayopatikana huenda kwa makuhani ili wawape maskini ufikapo mwaka wa saba wa mapumzikoya ardhi.

 

Amosi anaongelea pia jambo hili. Sadaka za daima ilikomeshwa kwa kuangamizwa Hekalu. Katika umaliziaji wa Hekalu aliloonyeshwa nabii Ezekieli kwenye maono yake, ni sadaka ya asubuhi peke yakendiyo iliyoonekana kutilewa. Mwonekano huu unatuelezea historia ya Hekalu na uvunaji unaoendelea. Hapa nabii Amosi aanalielezea kipindi cha maangamivu ya nchi yao yaliyofanyika mwaka 70 BK.

Amosi 4:4 Njoni Betheli, mkakose; njoni Gilgali, mkaongeze makosa; kaleteni dhabihu zenu kila asubuhi, na zaka zenu kila siku ya tatu;

 

Mungu anasema kwamba amewapa Israeli “meno yenye ganzi” katika maskani kwao, lakini bado hwajamrudia yeye. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, aliwatesa kwa njaa lakini bado walikaza shingo zao na wasimrudie yeye (soma Amosi 4:1-13). Wale waliowadhulumu maskini na kuwaonea wahitaji walifukuzwa kwa umbali kiasi hiki kwa ajili ya maonevu yao na hawakumrudia Mungu. Kila moja linaendana kwa pamoja. Iwapo kama watamwibia Mungu, pia walionekana wakiwadhulumu watu wake na maskini na yatima.

 

Tunapaswa kuwa makini ili kutofautisha kati ya kilicho cha Kaisari na cha Mungu (Mathayo 22:21; Marko 12:17; Luka 20:25). Kwa hiyo mamlaka yote yanatoka kwa Mungu na wote wanalazimika kushughulikia na mamlaka mbali mbali kama yalivyowekwa na Mungu.

Warumi 13:1-10 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 6 Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. 7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. 8 Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. 9 Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 10 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.  

 

Watu wenye imani wana utaratibu wa mambo yaliyo kipaumbele chao kwa yale wanayopenda ama kukusudia kumfanya Mungu na kwenye Huduma yao na kwa mamlaka ambayo wanawajibika kwayo.

 

Mfumo wa watu wenye kutarajia mema unamaongozi ya moja kwa moja na manabii wa Mungu katika Israeli. Maongozi ya kifalme yalianzishwa kama kitu cha pili na ukiwa ni mfumo ghali sana kuliko katika kuuhudumia.

1Samweli 8:10-18 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana. 11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. 12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake. 13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji. 14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake. 15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake. 16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe. 17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake. 18 Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; Bwana asiwajibu siku ile.

 

Bwana hatawasikiliza Israeli wakiwa kwenye mzigo au utumwani na ambao unatakiwa kulipwa.

 

Kutotoa fedha kwa wakati mwafaka au Kuficha ni Wizi

Sadaka na zaka havikutakiwa kushikiliwa na wenyewe pasipo kutoa.

Kutoka 22:29-30 Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao waume utanipa mimi. 30 Nawe utafanya vivyo katika ng'ombe zako, na kondoo zako; utamwacha siku saba pamoja na mama yake; siku ya nane utanipa mimi.

 

Siku ya nane ya kuzaliwa kwao, watoto wote katika Israeli wanatakiwa kutolewa ili kuwekwa wakfu kwa Mungu, makinda ya wanyama na watoto walitakiwa wakatahiriwe na kuwekwa wakfu pia.

 

Kutoka 23:17-19 Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU. 18 Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi. 19 Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake

 

Kushindwa kujihudhurisha mbele za Bwana kwenye matukio haya matatu ya sikukuu ili kumtolea sadaka, ni uasi na ni wizi.

 

Kutoka 34:19-20 Kila kifunguacho mimba ni changu mimi; na wanyama wako wote walio waume, wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe na wa kondoo. 20 Na mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; tena kwamba hutaki kumkomboa, ndipo utamvunja shingo. Wazaliwa wa kwanza wote wa wanao utawakomboa. Wala hapana atakayehudhuria mbele zangu mikono mitupu.

Haikuruhusiwa mtu kutokea mbele za Bwana akiwa mikono mitupu. Pia tendo la kunyimana vitu katika Israeli ni wizi.

 

Kutoka 34:23-26 Mara tatu kila mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele za Bwana MUNGU, Mungu wa Israeli. 24 Kwa kuwa mimi nitazitupa nje taifa za watu mbele yako, na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu ye yote atakayeitamani nchi yako, hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za Bwana Mungu wako mara tatu kila mwaka. 25 Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu; wala hiyo sadaka ya sikukuu ya pasaka haitasazwa hata asubuhi. 26 Vitu vya kwanza vya malimbuko ya nchi yako utavileta na kuvitia ndani ya nyumba ya Bwana Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

 

Hesabu 18:20-32 Kisha Bwana akamwambia Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lo lote kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli. 21 Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania. 22 Mwanzo wa sasa wana wa Israeli wasikaribie hema ya kukutania, wasije wakachukua dhambi, nao wakafa. 23 Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi. 24 Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote. 25 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka. 27 Na sadaka yenu ya kuinuliwa itahesabiwa kwenu, kama ndiyo nafaka ya sakafu ya kupuria, na kama kujaa kwake kinu cha kushindikia zabibu. 28 Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana. 29 Katika vipawa vyenu vyote mtasongeza kila sadaka ya kuinuliwa ya Bwana, ya wema wake wote, hiyo sehemu yake iliyowekwa takatifu. 30 Kwa ajili ya hayo utawaambia, Mtakapoinua humo hayo yaliyo mema, ndipo yatahesabiwa kuwa ya Walawi, kama kuongea kwake sakafu ya kupuria nafaka, na kama maongeo ya kinu cha kushindikia zabibu. 31 Nanyi mtakula hayo kila mahali, ninyi na watu wa nyumbani mwenu; kwa kuwa ni thawabu yenu badala ya utumishi wenu katika hema ya kukutania.
32 Nanyi hamtachukua dhambi kwa ajili yake, hapo mtakapokwisha kuinua humo hayo mema yake; lakini msivitie unajisi vile vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, ili msife.
 

 

Sadaka zinatakiwa ziwe za vitu vizuri na sio za vitu najisi au visivyofaa. Kitendo cha kutia unajisi sadaka ya mwingine, au kutotoa sadaka inayotakiwa ni wizi au kuonyesha dharau kwa Mungu. Sio tu kuwa umetokea uharibifu usiokusudiwa, kama inavyoonekana, kwa kuwa ni kwa faida au jambo jema au ridhaa kutoa sadaka kamilifu, na hakuna udhuru unaokubalika kwa mtu kusema atatoa sadaka dhaifu kwa kuwa ile kamilifu imeibiwa, na ndivyo hata kwa sadaka ya kitu kibovu pia haitakiwi.

 

Kumbukumb la Torati 14:22-29 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima. 24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako; 25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; 26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; 27 na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe. 28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; 29 na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.

Zaka ya pili inatenmgwa maalumu kwa ajili ya kuitumia kwenye maadhimisho ya Sikukuu za Mungu ambazo ni za lazima kuzitunza. Kama mahala ilipowekwa kambi ni mbali na nyumbani ndipo zaka hii inaweza kubadilishwa kuwa fedha na vitu muhimu hununuliwa tunapofika huko. Siku hizi watu hawachukui mazao na kwenda nayo kwenye kambi hizi; na badala yake wanachukua fedha na kwenda nazo badala yake ambazo wanazitumia kununulia vitu vyote vinavyotakiwa kwenye kambi kwa ajili ya kuvitumia kipindi chote cha sikukuu. Kwa hiyo umuhimu wa watu masikini kulishwa chakula hauonekani kwa wazi sana. Fedha za sadaka, kama ilivyo kwa mazao hutolewa majira ya jioni ya siku ya kukusanyika majira yaliyo kabla ya majira ya jua kuchwa ambayo yanachukuliwa kuwa ni majira ya kuanza kwa maadhimisho ya Sikukuu hizi, nah ii inamaana ya kuwawezesha watu wote wanaohusika na matumizi ya sadaka hii ama wahitaji wawezeshwe kujiandaa ama na kuzifanya zitumike kununulia mahitaji kabla ya kuanza kwa Sikukuu. Kutotoa sada siku hii au kutowasaidia masikini na wahitaji kunahesabiwa pia kuwa ni wizi.

 

Tendo la kufanya unyimi na kutotoa zaka ni dhambi na wizi pia. Mtu akitaka kuikomboa zaka aliyoitoa ili aitumie yeye mwenyewe, ndipo ukombozi wa zaka hiyo utaendana na malipizi. Ikiwa kama zaka yoyote itakombolewa, malipizi yake ni kwamba mtu anayeitaka imrudie tena kwake atatakiwa aongeze sehemu ya tano zaidi yake. Na pengine atalazimika kuongeza asilimia ishirini kwenye zaka yoyote itakayotumika kwa kusudi lolote lile.

 

Majira na kalenda

Mungu ameiweka kalenda kwa kutumia vitu vilivyoko juu mawinguni. Inafanya kazi kwa kuendana na mwenendo wa Mwezi mwandamo, na inajulikana sana na kwa uwazi na utaratibu wa kuhesabu wa wataalamu wa mambo ya nyota na anga wanaojua sana mwandamo wa Mwezi Mpya. Tendo la kutoifuata kalenda hii kama ilivyokuwa hapo zamani kwa sili yake (na sio kama walivyojifania Wayahudi kwa kalenda yao inayojulikana kama ya Hilleli) ni sawa na kufanya dhambi ya kumuibia Mungu.

 

Kutoitunza na kuiadhimisha Sabato na kujitoa kwa Mungu ni sawa na kumuibia Mungu muda wake. Kila mtu anatarajiwa kuwa atazitunza siku hizo ili ajifunze kumcha Mungu aliye Hai na utaratibu wake. Kila miaka saba tunapokutanika kwenye Sikukuu katika Mwaka wa Sabato, kunatakiwa isomwe Torati. Kushindwa kuzitunza au kuziadhimisha Sabato zote na kuisoma Torati ni sawa na kumuibia Mungu muda wake na kuvunja kanuni za ibada zake. Mungu anawataka wote wanao mwabudu yeye wamwabudu katika roho na kweli.

 

Hekalu la Mungu

Mungu amewapa watu wote ujuzi afya ili kwamba wazitumie staid zao na baraka kwa ajili ya utukufu wake mkuu. Kutozitumia staid na ujuzi aliotupa Mungu kwenye ibada na utaratibu wake ni dhambi iliyo sawa na wizi.

Kutoka 36:1-38 Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye Bwana amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote Bwana aliyoyaagiza. 2 Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye Bwana alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kuifanya kazi hiyo; 3 nao wakapokea mkononi mwa Musa matoleo yote, ambayo hao wana wa Israeli walikuwa wameyaleta kwa ajili ya huo utumishi wa mahali patakatifu, ili wapafanye. Kisha wakamletea matoleo kila siku asubuhi kwa moyo wa kupenda. 4 Na hao watu wote wenye hekima, waliotumika katika kazi yote ya mahali patakatifu, wakaenda kila mtu kutoka katika kazi yake aliyokuwa akiifanya; 5 nao wakasema na Musa, na kumwambia, Watu waleta vitu vingi sana zaidi ya hivyo vitoshavyo kwa ajili ya utumishi wa hiyo kazi, ambayo Bwana aliagiza ifanywe. 6 Basi Musa akatoa amri, nao wakatangaza mbiu katika marago yote, wakisema, Wasifanye kazi tena, mtu mume wala mwanamke, kwa ajili ya matoleo kwa mahali patakatifu. Basi watu wakazuiwa wasilete tena. 7 Kwani vile vitu walivyokuwa navyo vilikuwa vyatosha kwa kuifanya kazi hiyo yote, kisha vilizidi. 8 Basi kila mtu mwenye moyo wa hekima miongoni mwa hao waliofanya kazi, akaifanya hiyo maskani ya mapazia kumi; ya nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, na nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu; pamoja na makerubi, kazi ya fundi stadi; ndivyo alivyoyafanya. 9 Urefu wa kila pazia ulikuwa ni dhiraa ishirini na nane, na upana wa kila pazia ulikuwa ni dhiraa nne; mapazia yote yalikuwa ya kipimo kimoja. 10 Naye akaunganisha mapazia matano hili na hili; na mapazia matano mengine akayaunganisha hili na hili. 11 Kisha akafanya matanzi ya rangi ya samawi katika ncha za pazia moja, katika upindo wa kiungo chake; akafanya vivyo katika ncha ya pazia lililokuwa upande wa nje katika kiungo cha pili. 12 Akafanya matanzi hamsini katika pazia moja, na matanzi hamsini katika upindo wa pazia lililokuwa katika kiungo cha pili; hayo matanzi yalikuwa yakabiliana hili na hili. 13 Kisha akafanya vifungo hamsini vya dhahabu, na kuyaunganya hayo mapazia hili na hili kwa vile vifungo; hivi ile maskani ilikuwa ni moja. 14 Kisha akafanya vifuniko vya singa za mbuzi kuwa hema ya kuifunika hiyo maskani; akafanya mapazia kumi na moja. 15 Urefu wa kila pazia ulikuwa ni dhiraa thelathini, na upana wa kila pazia ulikuwa ni dhiraa nne; hayo mapazia yote kumi na moja yalikuwa ya kipimo kimoja. 16 Naye akaunganya mapazia matano mbali, na mapazia sita mbali. 17 Kisha akafanya matanzi hamsini katika upindo wa pazia lililo upande wa nje katika kile kiungo, naye akafanya matanzi hamsini katika ncha ya pazia lililokuwa upande wa nje katika kiungo cha pili. 18 Kisha akafanya vifungo hamsini vya shaba aiunganye ile hema pamoja, ili iwe hema moja. 19 Kisha akafanya kifuniko kwa ajili ya hiyo hema cha ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu; tena juu yake akafanya kifuniko cha ngozi za pomboo. 20 Kisha akafanya mbao za mti wa mshita kwa hiyo maskani, zilizosimama. 21 Urefu wa kila ubao ulikuwa ni dhiraa kumi, na upana wa kila ubao ulikuwa ni dhiraa moja na nusu. 22 Kila ubao ulikuwa na ndimi mbili, zilizounganywa pamoja; ndivyo alivyozifanya hizo mbao zote za maskani. 23 Naye akazifanya hizo mbao kwa ajili ya hiyo maskani; mbao ishirini kwa upande wa kusini kuelekea kusini; 24 naye akafanya matako ya fedha arobaini yawe chini ya hizo mbao ishirini; matako mawili chini ya ubao mmoja kwa hizo ndimi zake mbili, na matako mawili chini ya ubao mwingine kwa ndimi zake mbili. 25 Na kwa upande wa pili wa maskani upande wa kaskazini, akafanya mbao ishirini, 26 na matako yake ya fedha arobaini; matako mawili chini ya ubao mmoja, na matako mawili chini ya ubao mwingine. 27 Na kwa upande wa nyuma wa hiyo maskani kuelekea magharibi akafanya mbao sita. 28 Naye akafanya mbao mbili kwa pembe za maskani upande wa nyuma. 29 Nazo zilikuwa mbao pacha upande wa chini, vivyo zilishikamana pamoja hata ncha ya juu kufikilia pete ya kwanza; ndivyo alivyofanya zote mbili katika hizo pembe mbili. 30 Hivyo zilikuwa mbao nane, na matako yake ya fedha, matako kumi na sita, matako mawili chini ya kila ubao. 31 Kisha akafanya mataruma ya miti ya mshita; matano kwa mbao za upande mmoja wa maskani; 32 na mataruma matano kwa mbao za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa hizo mbao za maskani zilizokuwa upande wa nyuma kuelekea magharibi. 33 Naye akalifanya hilo taruma la katikati lipenye kati ya hizo mbao kutoka upande huu hata upande huu. 34 Naye akazifunika hizo mbao dhahabu, akazifanya zile pete zake za dhahabu ziwe mahali pa hayo mataruma, akayafunika dhahabu hayo mataruma. 35 Kisha akafanya hilo pazia la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri zilizosokotwa; akatia na makerubi kazi ya fundi stadi, ndivyo alivyofanya. 36 Naye akafanya kwa ajili yake nguzo nne za mti wa mshita, akazifunika dhahabu; na kulabu zake zilikuwa za dhahabu; naye akasubu kwa ajili yake matako manne ya fedha. 37 Kisha akafanya pazia la sitara kwa ajili ya mlango wa Hema, la nguo ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na nyekundu, na nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, kazi ya mwenye kutia taraza, 38 na nguzo zake tano pamoja na kulabu zake; naye akavifunika dhahabu vichwa vyake na vifungo vyake; na matako yake matano yalikuwa ya shaba.

 

Hekalu lilijengwa kwa vitu vilivyotolewa kwa moyo wa hiyarei, na lililenga kufanana na utaratibu wa kiroho ambapo kwamba watu wanapaswa kujitolea na kutoa vitu vyao kwa moyo wa hiyari na kujitoa wenyewe. Kiini cha Hekalu na utaratibu wa ibada kilikuwa ni Sanduku la Agano. Jambo hili lililrnga kwenye mfumo mpya ambao kwamba Torati ya Mungu ingewekwa ndani ya mioyo ya watu ili kwamba hatimaye wafanyike kuwa ni Sanduku la Agano. Kwa ajili hii ndipo ilipaswa Sanduku hili liondolewe na kufichwa (soma jarida la Sanduku la Agano (Na. 190) [The Ark of the Covenant (No. 196)]. Ili kulifanya kuwa lisifikiriwe mawazoni mwa watu tena.

 

Kutoka 37:1-29 Kisha Bezaleli akalifanya lile sanduku la mti wa mshita, urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake ulikuwa dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa moja na nusu; 2 akalifunika dhahabu safi, ndani na nje, akafanya na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote. 3 Naye akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili yake, katika miguu yake minne; pete mbili upande wake mmoja na pete mbili upande wake wa pili. 4 Akafanya na miti ya kulichukulia, ya mti wa mshita akaifunika dhahabu. 5 Naye akaitia hiyo miti katika zile pete zilizokuwa ubavuni mwa sanduku, ili kulichukua hilo sanduku. 6 Kisha akafanya kiti cha rehema cha dhahabu safi; urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu na upana wake ulikuwa dhiraa moja na nusu. 7 Kisha akafanya makerubi mawili ya dhahabu; akayafanya ya kazi ya kufua, yawe katika miisho miwili ya kiti cha rehema; 8 kerubi moja mwisho huu, na kerubi moja mwisho huu; alifanya hayo makerubi mawili ya kitu kimoja na hicho kiti cha rehema katika miisho yake miwili. 9 Na hayo makerubi yakayanyosha mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zilikuwa zaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zilikuwa zikielekea kiti cha rehema. 10 Kisha akafanya hiyo meza ya mti wa mshita; urefu wake ulikuwa ni dhiraa mbili, na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja, na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa moja na nusu; 11 naye akaifunika dhahabu safi, akaifanyia ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 12 Kisha akaifanyia upapi wa upana wa shibiri kuizunguka pande zote, akauzungushia ukingo wa urembo wa dhahabu ule upapi. 13 Naye akasubu vikuku vinne vya dhahabu kwa ajili yake, akavitia vile vikuku katika pembe nne, katika miguu yake minne. 14 Vile vikuku vilikuwa karibu na ule upapi, ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza. 15 Naye akaifanya hiyo miti ya kuichukulia, ya mti wa mshita, akaifunika dhahabu, ili kuichukua hiyo meza. 16 Kisha, vile vyombo vilivyokuwa juu ya meza, sahani zake, na miiko yake, na bakuli zake, na makopo yake ya kumiminia, akavifanya vya dhahabu safi. 17 Kisha akakifanya kile kinara cha taa cha dhahabu safi, akakifanya kile kinara cha taa cha kazi ya kufua, tako lake, na mti wake; vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vilikuwa vya kitu kimoja nacho, 18 nacho kilikuwa na matawi sita yaliyotoka ubavuni mwake; matawi matatu ya kinara yalikuwa upande huu, na matawi matatu ya kinara yalikuwa upande huu; 19 vikombe vitatu, vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi vilikuwa katika tawi moja, tovu na ua; na vikombe vitatu, vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, katika tawi la pili, tovu na ua; yalikuwa ni vivyo hivyo yale matawi sita yaliyokuwa katika hicho kinara. 20 Katika kinara mlikuwa na vikombe vinne, vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake na maua yake; 21 kisha chini ya matawi mawili mlikuwa na tovu iliyokuwa ya kitu kimoja nacho, na chini ya matawi mawili mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho, tena chini ya matawi mawili hayo mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho; kwa ajili ya hayo matawi sita, yaliyotokana nacho. 22 Hayo matovu yake na matawi yake yalikuwa ya kitu kimoja nacho; kinara hicho kizima chote pia ni kazi moja ya kufua ya dhahabu safi. 23 Kisha akafanya taa zake saba, na makoleo yake, na visahani vyake, vya dhahabu safi. 24 Akakifanya cha talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo vyake vyote. 25 Kisha akafanya hiyo madhabahu ya kufukizia uvumba ya mti wa mshita; urefu wake ulikuwa ni dhiraa moja, na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja, ilikuwa mraba; na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa mbili; na pembe zake zilikuwa za kitu kimoja nayo. 26 Naye akaifunika dhahabu safi, upande wa juu, na mbavu zake pande zote, na hizo pembe zake; akaifanyia na ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 27 Naye akaifanyia vikuku viwili vya dhahabu na kuvitia chini ya ukingo wake, katika mbavu zake mbili, katika pande zake mbili, viwe ni mahali pa hiyo miti ya kuichukulia. 28 Kisha akafanya hiyo miti kwa mti wa mshita, na kuifunika dhahabu. 29 Kisha akayafanya hayo mafuta matakatifu ya kutiwa, na ule uvumba safi wa viungo vya manukato vizuri, kwa kuandama kazi ya mtengezaji manukato.

 

Na hakuna kitu kama hicho kinachojulikana kama Kiti cha Rehema. Ni Kifuniko na Kifuniko kilikuwa na Makerubi wawili juu yake katikati ya Hekalu na Kiti cha Enzi cha Mungu. Moja ya Makerubi haya mateule Yaliyofunika alikuwa ni Shetani (soma Isaya sura ya 14; Ezekieli sura ya 28). Mwingine anayeonekana inaonekana kuwa ni kama alikuwa malaika Mkuu Mikaeli au Masihi akiwa kama Yahova-elohim (soma kitabu cha Yuda aya ya 9).

 

Kutoka 38:1-31 Kisha akafanya hiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, ya mti wa mshita urefu wake ulikuwa dhiraa tano, na upana wake ulikuwa dhiraa tano, ilikuwa mraba; na kwenda juu kwake kulikuwa dhiraa tatu. 2 Naye akazifanya pembe zake katika ncha zake nne; hizo pembe zilikuwa za kitu kimoja nayo; naye akaifunika shaba. 3 Kisha akafanya vyombo vyote vya madhabahu, yaani sufuria zake, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote akavifanya vya shaba. 4 Naye akaifanyia madhabahu wavu wa shaba, akautia chini ya ukingo kuizunguka pande zote, ukawa katikati ya hiyo madhabahu. 5 Naye akasubu vikuku vinne kwa kutiwa katika pembe nne za huo wavu wa shaba, viwe mahali pa kutia ile miti ya kuichukulia. 6 Naye akaifanya hiyo miti kwa mti wa mshita na kuifunika shaba. 7 Naye akaitia ile miti katika vile vikuku vilivyokuwa katika mbavu za hiyo madhabahu, ili kuichukua; akaifanya yenye mvungu ndani, kwa zile mbao. 8 Kisha akafanya hilo birika la shaba, na tako lake la shaba; shaba hiyo ilikuwa ni ya vioo vya wanawake wenye kutumika, waliokuwa wakitumika mlangoni mwa hema ya kukutania. 9 Naye akafanya ule ua; upande wa kusini kwa kuelekea kusini, chandarua ya ua ilikuwa ya nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, kiasi cha dhiraa mia; 10 nguzo zake zilikuwa ishirini, na matako yake yalikuwa ishirini, yalikuwa ya shaba; kulabu za nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. 11 Upande wa kaskazini ulikuwa ni dhiraa mia vivyo, nguzo zake ishirini na matako yake ishirini, yalikuwa ni ya shaba; kulabu za nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. 12 Upande wa magharibi mlikuwa na chandarua ya dhiraa hamsini, nguzo zake zilikuwa ni kumi, na matako yake kumi; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. 13 Upande wa mashariki kuelekea mashariki dhiraa hamsini. 14 Chandarua ya upande mmoja wa lango ilikuwa dhiraa kumi na tano urefu wake; na nguzo zake tatu, na matako yake matatu; 15 ni vivyo upande wa pili; upande huu na huu langoni mwa ua mlikuwa na chandarua ya dhiraa kumi na tano urefu wake; nguzo zake zilikuwa ni tatu, na matako yake matatu. 16 Chandarua za nguo zote za ule ua zilizouzunguka pande zote zilikuwa za nguo ya kitani nzuri iliyosokotwa. 17 Na matako ya zile nguzo yalikuwa ya shaba; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha; na vichwa vya zile nguzo vilikuwa ni vya fedha; na nguzo zote za huo ua ziliungwa kwa vitanzi vya fedha. 18 Na hilo pazia la lango la ua, lilikuwa ni kazi ya mwenye kutia taraza, lilikuwa la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; lilikuwa na urefu wake dhiraa ishirini, na kutukuka kwake katika huo upana wake kulikuwa dhiraa tano, kupatana na ile chandarua ya ua. 19 Na nguzo zake zilikuwa nne, na matako yake manne, yalikuwa ya shaba; kulabu zake zilikuwa za fedha, na vichwa vyake na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. 20 Na vigungi vyote vya maskani, na vya ua ulioizunguka pande zote vilikuwa vya shaba. 21 Jumla ya vile vyombo vilivyofanywa kwa ajili ya hiyo maskani, hiyo maskani ya ushuhuda ni hii, kama vilivyohesabiwa, kama maagizo ya Musa yalivyokuwa, kwa ajili ya utumishi wa Walawi kwa mkono wa Ithamari, mwana wa Haruni, kuhani. 22 Na Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda, akafanya yote Bwana aliyomwagiza Musa. 23 Na pamoja naye alikuwa na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani, aliyekuwa fundi wa kuchora nakshi, mfanyaji wa kazi mwerevu, naye alikuwa mwenye kutia taraza za nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri. 24 Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya hiyo kazi, katika kazi hiyo yote ya mahali patakatifu, hiyo dhahabu ya matoleo, ilikuwa ni talanta ishirini na kenda, na shekeli mia saba na thelathini, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu. 25 Na fedha ya hao waliohesabiwa, watu wa huo mkutano ilikuwa talanta mia, na shekeli elfu moja na mia saba na sabini na tano kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu; 26 kichwa beka, maana, nusu shekeli, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu, kwa ajili ya kila mtu aliyepita kwa wale waliohesabiwa, aliyekuwa wa umri wa miaka ishirini au zaidi, kwa ajili ya watu waume sita mia na tatu elfu, na mia tano na hamsini (603,550). 27 Na hizo talanta mia za fedha zilikuwa kwa kusubu yale matako ya mahali patakatifu na matako ya hilo pazia; matako mia kwa hizo talanta mia, talanta moja tako moja. 28 Na kwa hizo shekeli elfu moja na mia saba, na sabini na tano, akafanya vifungo vya hizo nguzo, na kuvifunika fedha vile vichwa vyake, na kufanya vitanzi vyake. 29 Na hiyo shaba iliyoletwa ilikuwa ni talanta sabini, na shekeli elfu mbili na mia nne. 30 Naye akafanya ya hiyo shaba matako kwa ajili ya lango la hema ya kukutania, na hiyo madhabahu ya shaba, na ule wavu wa shaba kwa ajili yake na vyombo vyote vya hiyo madhabahu, 31 na matako ya ua kuuzunguka pande zote, na matako ya lango la huo ua, na vigingi vyote vya maskani, na vigingi vyote vya huo ua uliozunguka pande zote.

 

Maskani kule jangwani ilijengwa kwa michango au sadaka zilizotolewa na kwa utaratibu wa kuwahesabu Israeli. Sadaka hii inaashiria hali ya Kanisa lililo jangwani, na ukweli wa kwamba Hekalu lilijengwa kwa sadaka iliyofanywa kwa kuwahesabu wana wa Mungu ambao walikuwa wamekombolewa na Masihi na kuwekwa ndani yake.

 

Madhabahu na pambizo zake zilifumikwa na sahani zake zilifanywa shaba iliyosuguliwa, zikitumiwa na vioo vya wanawake waliokusanyika. Jambo hili lilikuwa linaashiria pia sehemu ya wanawake kwenye Hekalu la Mungu wakiwa kama wana wa Mungu walio jangwani. Wazee wa kabila zote mbili yaani ya Yuda na Efraimu, ambao walikuwa ni Kalebu na Yoshua na walioheshimika sana, walitengwa kando na kuahidiwa kuingia kwenye Nchi ya Ahadi katika kipindi chao cha mwisho.

 

Kutoka 39:1-43 Na zile nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyafanya hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa. 2 Naye akaifanya hiyo naivera, ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa. 3 Nao wakaifua hiyo dhahabu hata ikawa mabamba membamba sana, kisha wakaikata iwe nyuzi, ili wapate kuifuma pamoja na hizo nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyuzi nyekundu na za kitani nzuri, kazi ya fundi stadi sana. 4 Nao wakafanya na vipande vya mabegani kwa ajili yake, vilivyoungwa pamoja; viliungwa pamoja kwa ncha zake mbili. 5 Na huo mshipi wa kazi ya werevu, uliokuwa juu yake ili kuifunga mahali pake; ulikuwa wa kitu kimoja, na wa kazi moja na naivera ya dhahabu, na rangi ya samawi, na rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa. 6 Nao wakavitengeza vile vito vya shohamu, vilivyotiwa katika vijalizo vya dhahabu, vilivyochorwa mfano wa kuchora kwake muhuri, kwa majina ya hao wana wa Israeli. 7 Naye akavitia katika vile vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli, kama Bwana alivyomwagiza Musa. 8 Naye akafanya kile kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi, kama hiyo kazi ya naivera; ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa. 9 Kilikuwa mraba; wakakifanya kile kifuko cha kifuani kwa kukikunja; urefu wake ulikuwa shibiri, na upana wake ulikuwa shibiri, tena kilikuwa ni cha kukunjwa. 10 Nao wakatia safu nne za vito ndani yake, safu moja ilikuwa ni akiki, na yakuti ya rangi ya manjano, na baharamani, vilikuwa ni safu ya kwanza. 11 Na safu ya pili ilikuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi. 12 Na safu ya tatu ilikuwa ni hiakintho, na akiki nyekundu, na amethisto. 13 Na safu ya nne ilikuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi: vito hivyo vilikuwa vimetiwa katika vijalizo vya dhahabu, kila kimoja mahali pake. 14 Na hivyo vito vilikuwa vyaandama majina ya wana wa Israeli, kumi na mawili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora muhuri, kila moja kwa jina lake, kwa zile kabila kumi na mbili. 15 Nao wakafanya katika kile kifuko cha kifuani mikufu mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa ya dhahabu safi. 16 Nao wakafanya vijalizo viwili vya dhahabu, na pete mbili za dhahabu; nao wakazitia hizo pete mbili katika ncha mbili za hicho kifuko. 17 Nao wakaitia hiyo mikufu miwili iliyosokotwa katika hizo pete mbili zilizokuwa katika ncha mbili za hicho kifuko. 18 Na ncha hizo mbili nyingine, za hiyo mikufu miwili ya kusokotwa, wakazitia katika vile vijalizo viwili, na kuvitia katika vile vipande vya mabegani vya naivera, upande wa mbele. 19 Nao wakafanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake, ulio upande wa naivera ulio ndani. 20 Nao wakafanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi. 21 Nao wakakikaza kile kifuko kwa pete zake kwenye naivera kwa ukanda wa rangi ya samawi, ili kikae pale juu ya mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi, na ya kwamba kifuko cha kifuani kisiachane na naivera; vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa. 22 Naye akafanya hiyo joho ya naivera ya kazi ya kusuka, rangi ya samawi yote; 23 na hilo tundu lililokuwa katikati yake, mfano wa tundu lililo katika kanzu ya chuma, na utepe wake kulizunguka hilo tundu, ili lisipasuke. 24 Nao wakatia katika upindo wa joho makomamanga ya nyuzi za rangi ya samawi, na rangi ya zambarau, na rangi nyekundu, na kitani iliyosokotwa. 25 Nao wakafanya njuga za dhahabu safi, na kuzitia hizo njuga kati ya hayo makomamanga pande zote, kati ya hayo makomamanga; 26 njuga na komamanga, njuga na komamanga katika pindo za joho kuizunguka pande zote, ili kutumika kwa hiyo; vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa. 27 Nao wakafanya hizo kanzu za nguo ya kitani nzuri ya kufumwa, kwa Haruni, na kwa wanawe 28 na hicho kilemba cha nguo ya kitani nzuri, na zile kofia nzuri za kitani, na hizo suruali za nguo ya kitani nzuri iliyosokotwa, 29 na huo mshipi wa nguo nzuri ya kitani iliyosokotwa, na rangi ya samawi, na rangi ya zambarau, na nyekundu, kazi ya fundi mwenye kutia taraza; vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa. 30 Nao wakafanya hilo bamba la hiyo taji takatifu la dhahabu safi, na kuandika juu yake andiko, mfano wa kuchorwa kwa muhuri, MTAKATIFU KWA Bwana. 31 Nao wakatia ukanda wa rangi ya samawi ili kulifunga katika hicho kilemba upande wa juu; vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa. 32 Basi ndivyo ilivyomalizwa kazi yote ya maskani ya hema ya kukutania; na wana wa Israeli walifanya kama yote Bwana aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya. 33 Nao wakamletea Musa hiyo maskani; yaani Hema, na vyombo vyake vyote, vifungo vyake, na mbao zake, na mataruma yake, na nguzo zake, na matako yake; 34 na kifuniko chake cha ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na kifuniko cha ngozi za pomboo, na pazia la sitara; 35 na sanduku la ushuhuda, na miti yake, na kiti cha rehema; 36 na meza, na vyombo vyake vyote, na mikate ya wonyesho; 37 na kinara cha taa safi, na taa zake, hizo taa za kuwekwa mahali pake, na vyombo vyake vyote, na mafuta ya taa, 38 na madhabahu ya dhahabu, na mafuta ya kutiwa, na uvumba mzuri, na pazia kwa mlango wa hema; 39 na madhabahu ya shaba, na wavu wake wa shaba, na miti yake, na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake; 40 na ukuta wa nguo wa ua, na nguzo zake na matako yake, na pazia la lango la ua, na kamba zake, na vigingi vyake, na vyombo vyote vya kutumiwa katika utumishi wa maskani, kwa hiyo hema ya kukutania, 41 na mavazi ya kazi nzuri kwa utumishi katika mahali patakatifu, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani. 42 Sawasawa na yote Bwana aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyoifanya hiyo kazi yote wana wa Israeli. 43 Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama Bwana alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo; basi Musa akawaombea heri.

 

Kazi ya kikuhani iliwekwa chini ya Kuhani Mkuu, ambaye alisimama kwa ajili ya makabila yote ya Israeli, na juu ya sahani za maziwa kuliwekwa mawe kumi na mawili, ambayo ni misingi kumi na mbili iliyowekwa kwa mpangilio wa mistari minne, kila mstari ukiwa na mitatu mitatu. Mgawanyo huu wa miatari minne kwa mitatu unaashiria mgawanyo wa robo ulio chini ya wenye uhai wanne. Wawili kati ya viumbe hawa wanachukua mahala pa elohim ambaye anaonekana pia kwenye makerubi yanayoonekana kwa umbo la kichwa cha simba na mwanadamu ukutani kwenye maono ya Hekalu aliloonyeshwa nabii Ezekieli simba was set under a High Priest, who stood (Ezekieli 41:19). Mawe ya misingi kumi na miwili ni vichwa kumi na viwili vya makabila kumi na mawili kwenye Mji wa Mungu (soma jarida la Mji wa Mungu (Na. 180) [The City of God (No. 180)]. Mawe haya yameorodheshwa kitofauti sana kwenye Ufunuo 21:19-20. ndani ya mfuko wa ile sahani ya maziwa wa Kuhani Mkuu kulikuwa na Urimu na Thumimu ambazo zilikuwa ni mawe wawili ya kufanyia Utabiri wa Kumwuliza Mungu (soma jarida la Kutaka Mashauri kwa Mungu (Na. 184) [The Oracles of God (No. 184)]. Makabila yenyewe yamewekewa pahala pao kwenye ufalme kwa kupewa majukumu ya namna mbali mbali na mahala pao. Mungu anaandaa makazi kwenye Ufalme wa Mungu na amempa Kristo ayaandae na kuyathibitisha.

 

Uumbaji

Uumbaji wote—yaani wa dunia na ukamilifu wa viumbe vyake vyote—ni mali ya Mungu. Amempa mwanadamu mamlaka ya kuvitawala viumbe vyote na vitu vyote vilivyoko ndani yake ili avitiishe, na kuviangalia na kuvilinda kwa mujibu wa mpango wa Mungu (Mwanzo 1:26-31; Zaburi 24:1; 50:12; 1Wakorintho 10:26-28).

Kutoka 9:29 Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia Bwana mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya Bwana.

 

Mataifa hawakumtii Mungu na hawakukuchukua milki zao kama ilivyotakiwa (soma Kutoka 9:29-35; na jarida la Musa na Miungu ya Misri (Na. 105) [Moses and the Gods of Egypt (No. 105)].

 

Mwelekeo wetu ni kufanyika miungu midogo au elohim, lakini kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu na sio kwa kuiba. Wazo hili lilikuwa ndilo lililokuweko mioyoni mwa Adamu na Hawa na ndilo lililowapelekea kuanguka kwao (Mwanzo 3:5). Mafundisho ya dini ya Mambo fumbo ya Mysticism, au mafundisho yanayofundisha watu kuwa na sawa na Mungu na wao kuwa kama Mungu, ni kosa lilelile lililofanywa na Hawa alipokuwa anahojiana na Shetani. Sisi sote tumekududiwa tangu mwanzo na tukachaguliwa, kuitwa, kuhesabiwa haki na kutukuzwa (Warumi 8:29-30). Tumemuweka mtu mpya tunapomwalika Mungu, kwa kuzifanya upya nia zatu. Ni hali tuliyopewa bure, lakini haiwezi kupatikana kwa kuiba (Wakolosai 3:10).

 

Matendo 2:41-47 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. 43 Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. 44 Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, 47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

 

Uumbaji na viumbe wanangoja kufunuliwa kwake mwana wa Mungu.

Warumi 8:19-23 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; 21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. 22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. 23 Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

Wateule hawako kama wale wanaoliharifu au kulighoshi neno la Mungu bali, ni wanaoyanena mapenzi ya Mungu kwa moyo wa unyofu na wanaomnena machoni pake Mungu, Yeru Kristo (2Wakorintho 5:17). Hapa duniani – wengi – wamelighoshi neno la Mungu na wamebadili majira na sheria zake. Wameyaondoa Maagano kutoka kwenye taratibu zao au mapokeo ya dini zao na wamejaribiwa kukiiba kipawa cha uzima wa milele ambacho kimetolewa bure kabisa kwa wale ambao Mungu amewaita kwa makusudio yake.

 

Mungu anapendezwa na utii zaidi kuliko sadaka.

Kutoka 19:5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,

 

Je, ni nini Mungu anachokihitaji kwetu?

Kumbukumbu la Torati 10:12-17 Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; 13 kuzishika amri za Bwana na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri? 14 Tazama, mbingu ni mali za Bwana, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo. 15 Tena, Bwana aliwafurahia baba zako, na kuwapenda, akawachagua wazao wao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo. 16 Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu. 17 Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa.

Tunatakiwa kuzishika amri zake, pasipo kuzigeuza au kuzibadilisha, na kwa kadri zilivyo kikamilifu. 

 

Mazao na mifugo

Mifugo ni mali ya Bwana lakini wanaweza kutumika na wanadamu. Utaratibu unaofanya kazi umefanywa ili kuwalinda wasiharibiwe (soma Kutoka 21:28-32; na pia soma jarida la Torati na Amri ya Sita (Na. 259) [Law and the Sixth Commandment (No. 259)].

 

Wizi huu hutokea kwa kuficha au kunyima kama tulivyojionea. Mfumo huu unaendela toka kwa Mungu hadi kwa makuhani na hadi kwenye utawla na kwa viumbe wote wakiwemo wanyama. Imenadikwa imeandikwa: usimfunge kinywa punda apurapo nafaka: je, mungu anaongelea jambo la punda hapa? (soma Kumbukumbu la Torati 25:4; 1Wakorintho 9:9; 1Timotheo 5:18).

 

Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini. (1Timotheo 5:8). Aaina yote ya kutojali ni dhuluma au wizi.

 

Jinsi Wizi unavyohusiana na sheria ya vyakula

Sheria ya vyakula imewekwa kwenye nafasi yenye nia ya kumrekebishia mtu uratatibu wa mzunguko wa vyakula na mazingira yake. Suala hili la sheria ya vyakula limefafanuliwa kwa kina kwenye majarida ya Sheria ya Vyakula (Na. 15) na Torati na Amri ya Sita (Na. 259) [The Food laws (No. 15) and Law and the Sixth Commandment (No. 259)].

 

Kitendo cha kula chakula najisi sio tu kuwa ni cha kukosa busara kwa masuala la kiafya, bali pia ni kuiba kwenye utaratibu aliouweka Mungu katika mfumo wa kisayari. Kumekuwa na wazo lililo wazi kabisa na kisilo na shaka kuhusu msingi wa kisayansi na kipindi kinachohusika na sheria za vyakula. Wanyama walio safi wanakula vyakula kutoka kwenye mlolongo wa vyakula vinavyoelekezwa kulindwa. Ubadhilifu na uozeshaji huu wa sayari yetu ni matokeo ya moja kwa moja ya kumuibia Mungu tulikokufanya na viumbe vyake kwa matendo yetu ya kula vitu ambavyo hatujaruhusiwa kuvila.

 

Maadili ya kimazingira

Kuna mlolongo wa sheria unaohusika na yale tunayoweza kuchukua na kile ambacho hatutakiwi kuua kwa ajili ya mazingira yake yalivyo. Sheria inayohusu jinsi tunavyoweza kuua na vile ambavyo hatupaswi kuviua, kama vile vilevyohusiana na wanyama na ndege na watoto wao, vimeelezewa kwa ufafanuzi kwenye jarida la Torati na Amri ya Sita (Na. 259) [Law and the Sixth Commandment (No. 259)]. Kushindwa kuyatilia maanani makatazo haya yanayohusu asili na watoto wake, Sabato, na utunzaji wa mazingira wa muda mrefu ni tendo sawa na wizi na unatakiwa kulipwa kwa kadiri hiyo hiyo ilivyo. Ardhi itazifurahia Sabato zake bila ya kuwepo kwa mwanadamu (tazama hapo chini).

 

Milki au mali za umma

Kwa kuongezea kuhusu wazo hili la mazingira huru ulio chini ya maelekezo yaliyo kwenye Torati ya Mungu kuna dhana ya mali zinazomilikiwa na umma au jamii yote. Dhana hii kuhusu mali za umma ina sehemu kuu mbili.

 

Mali ya Umma na Sheria Zilizozoeleka kawaida

Jambo la kwanza ni lile la mali inayomilikiwa na dola kwa sababu zake yenyewe. Jambo la pili ni lile la mali za kawaida inayomilikiwa na umma kwa kiasi kikubwa, zinazopatikana kwenye jamii. Dhana hii ya mali ya kawaida inafanya mtazamo wa kwenye Biblia kwa kuorodhesha vilivyoko mitaani. Mali hizi ni kama ardhi zilizo kwenye miji ya Walawi na wanyama walioweza kuchungwa kwa kawaida. Dhana hii kila mara ilijumuishwa kwenye kile kilichokuwa kinaitwa Sheria ya Kawaida iliyoko kati ya watu wetu. Jinsi ya kuweka mambo sawa kwa kulinganisha na masuala ya Kidola ya maeneo yaliyo na haki nay ale ya watu wa kawaida ni wizi, sawa tu na kama ilivyo kwa watu binafsi. Kwa hiyo, kunatakiwa kuwepo na uhakiki wa mali kwa kuyataja na kuweka kumbukumbu zake. Pia kunatakiwa kuwe na mpangilio wa kimiji kwa ardhi ya kawaida inayoyagawa maeneo ya nyumba. Hii ni kile kinachojulikana kama viunga vya kweli vya miji kwa usemi wa kibiblia.

 

Mali za mtu binafsi

Haki ya kila mmoja imefungamanishwa kwa kiasi kikubwa sana na dhana yenye mtazamo wa kuwa ni mali za kibinafsi. Haki ya umiliki imeonyeshwa kwenye sheria zilizo kwenye Biblia.

 

Mali zimegawanyika pia kwenye makundi makuu mawili: Halisi na Binafsi. Haki halisia inaanzia moja kwa moja kutoka kwa umilikaji na kutenda kazi kwake rasilimali au nyuma.

 

Mambo haya kwa kawaida yanaonekana ki rahisi sana, na wizi kwa kawaida inahusisha matendo ya moja kwa moja ya kimwili na kuondolewa kwa mambo ya kimwili. Mambo haya yanafungamanishwa na thamani ya umiliki na kupoteza kwa mambo kwa kuweka au tathmini ya thamani ya fidia.

 

Kwa hiyo migawanyo inaendelea hadi kuwa ni mali zinazohamishika na zisizohamishika. Kupotea kwa mali inayohamishika kunaweza kuhusishwa na sifa njema ya mtu, nia njema, kiwango cha maisha, upendo na athari, ubunifu na usanii, haki zake na kadhalika wa kadhalika. Mambo haya kwa kiasi fulani ni vigumu kuamua na uthaminisho, na ni mara nyingi ni mambo haya haya ambayo watu huona hakuna madhara ya kuharibu kwa chuki, kuteta na kuchonganisha, na tama ya mwili.

 

Haki ya kumiliki

Kila mmoja ana haki ya kumiliki mali unaoelezewa kama ni kupendana kila mmoja na mwingine kama tulivyojionea hapo juu.

Warumi 13:8-10 Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. 9 Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 10 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

 

Kila mmoja anapaswa kuwa salama na hakuna anayetakiwa kuwa tishio na kuwaogopesha (Mambo ya Walawi 26:6).

 

Wakati dhana na wazo hili lilipoanzisha haki ya kwa milki zao, zilifanywa kwa mpaka na utafiti. Tendo la kuondoa alama ya mpaka ni wizi pia.

 

Kumbukumbu la Torati 19:14 Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki.

 

Harakati hii ilisababisha kuwepo kwa sheria ya ukombozi kwa mazao yaliyoibiwa, ikiwa ardhi haijarejeshwa milele. Tendo hili linasababisha laana (Kumbukumbu la Torati 27:17; pia soma Ufunuo 22:28; 23:10).

 

Tendo la kuondoa alama za mpaka na kuchukua shamba la yatima ni wizi au ni dalili ya kukusudia kuiba. Mungu atawatetea yatima, lakini mahakimu wa mahakama wanawajibika kushughulikia jambo kama hilo kwa mujibu wa vile zinavyosema sheria zao. Ayubu alimlaumu Mungu kwa kuwa mambo haya yalimpata (Ayubu 24:2); na Mungu bado anaona na kuhukumu.

 

Kikomo cha umiliki kwa mfumo ulio ndani ya yubile

Mambo ya Walawi 25:1-11 Kisha Bwana akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia, 2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya Bwana. 3 Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake; 4 lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu. 5 Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizitunde; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi. 6 Na hiyo Sabato ya nchi itakuwa chakula kwenu; kwako wewe, na kwa mtumwa wako, na kwa mjakazi wako, na kwa mtumishi aliyeajiriwa, na kwa mgeni wako akaaye pamoja nawe; 7 na kwa hayawani wako, na kwa wanyama walio katika nchi yako; maongeo yote yatakuwa ni chakula chao. 8 Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. 9 Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. 10 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. 11 Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.

 

Haya ni mwajibiko wa mambo yanayohusiana na umiliki wa ardhi ambayo iliyolewa yote na Mungu. Kwa matumizi ya ardhi kuna pia mambo ya kuwajibika kwayo.

 

Mambo ya Walawi 25:23-28 Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wasafiri wangu. 24 Nanyi mtatoa ukombozi kwa ajili ya nchi, katika nchi yote ya milki yenu. 25 Kwamba nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye. 26 Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa; 27 ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki yake. 28 Lakini asipoweza kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa mkononi mwake huyo aliyeinunua, hata mwaka wa yubile; na katika yubile itatoka, naye atairejea milki yake

 

Ardhi iliyo nje ya miji yenye “kuta au maboma” haitakiwi ichukuliwe kuwa milki ya milele. Pia kulikuwa na kikomo kwenye utaratibu umiliki wa ardhi, nah ii hubadilika kutokana na wajibu wake.

Mambo ya Walawi 25:29-34 Tena kwamba mtu anauza nyumba ya kukaa, iliyo ndani ya mji wenye kuta, ndipo ana ruhusa kuikomboa katika mwaka mmoja mzima baada ya kuiuza; atakuwa na amri ya kuikomboa muda wa mwaka mzima. 30 Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika yubile.31 Lakini nyumba za vijiji, ambavyo havikuzingirwa na kuta, zitahesabiwa pamoja na mashamba ya nchi; nazo zina ruhusa ya kukombolewa, nazo zitatoka katika yubile. 32 Pamoja na hayo, miji ya Walawi, nyumba za miji ya milki yao, Walawi wana ruhusa ya kuzikomboa majira yo yote. 33 Tena kama mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa, ndipo nyumba iliyouzwa, na mji wa milki yake, itatoka katika yubile; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli. 34 Lakini konde la malisho ya miji yao lisiuzwe kwa kuwa ni milki yao ya daima.

 

Tofauti kati ya miji yenye maboma na ile isiyozungushiwa na kuta au boma hufanya kuwe maamuzi kwa kiwango cha kukombolewa kwake na jinsi ya kuwa na sehemu kwenye utaratibu wa kukombelewa na kurejeshewa wamiliki asilia inapofika yubile. Ni miji ile iliyo kwenye kuta au boma tu ndizo zinaweza kuuzwa na bila kurudishwa kwa wenyewe milele. Miji ya Makuhani inayoonekana kuonekana kujumuishwa na miji ya makimbilio, pia haikuruhusiwa kuuzwa kuwa milki ya milele bali inaweza kukombolewa wakati wowote na makuhani. Hakuna mfumo wowote wa ardhi iliyokuwa nje ya miji yenye boma au kwenye vijiji vilivyo kwenye nchi au miji isiyo na maboma au kuta ambazo zinaweza kuondolewa kwenye mfumo wa yubile. Tofauti hii inaenda hadi kwenye sheria inayohusu marejesho na ukombozi na umiliki. Mtu aliye kwenye mji uliouzwa milele anaweza kuukomboa mali yake kwa kipindi cha mwaka mmoja wa tangu kuuzwa kwake. Vinginevyo itakuwa ni mali ya aliyekinunua milele. Hakuna milki nyingine iliyo kama jimbo inayoruhusiwa kuuzwa milele kwa namna rahisi na huru tu.

 

Uaminifu wa mtu

Kwa kipindi cha zama na zama sasa wanadamu wamekuwa wakiuzwa kwa wenzao na pia kuchukuliwa na wachuuzi hawa makwao kwa kuwatumikisha kwa shughuli za kitumwa na kutumikishwa kwa kuodishwa kibiashara kwa kutumikishwa kwa kazi za shokoa ki mikataba. Wachezaji wa mpira wa miguu ni mfano uliobakia wa mfumo huu wa kutumikishwa kwa kazi hizi ngumu za shokoa, bali wao wamekuwa wakilipwa wenyewe kipato kikubwa japo huwa wanauzwa na wenzao.

 

Mara nyingi watu wanaangukia kweenye vipindi vigumu na wanataabika kwenye jambo hilo. Kuna vipengele kadhaa vya sheria zinazotutaka sisi kumlinda kila mmoja, na kushindwa kufanya wajibu wetu kwa kila mmoja wetu huwa ni sehemu ya wizi au dhuluma.

Mambo ya Walawi 25:35-43 Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri. 36 Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe. 37 Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida. 38 Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu. 39 Tena kwamba nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimtumikishe mfano wa mtumwa; 40 kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hata mwaka wa yubile; 41 ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake. 42 Kwa kuwa hao ni watumishi wangu, niliowaleta watoke nchi ya Misri; wasiuzwe mfano wa watumwa. 43 Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako.

 

Kwa hiyo, mtu akiwa kwenye nchi yake mwenyewe anaweza kuwa mtumwa au anaweza kutumikishwa kwa kazi ngumu za shokoa. Hiki ndicho kitu kibaya zaidi na kilichopo leo lakini Wamataifa wamewekwa huru na kuwa na sehemu kwenye Ufalme wa Mungu. Wale wanaokataa kuwa ni sehemu ya taifa na kanisa wanaweza kushurutishwa kwa sheria za kidunia.

Mambo ya Walwi 25:44-46 Tena katika habari za watumwa wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando-kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi. 45 Tena katika wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu. 46 Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumwa wenu katika hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli, wenyewe kwa wenyewe.

 

Sheria hii inaonyesha faida ya maamuzi ya uraia kwenye taifa la Israeli.

 

Mambo ya Walawi 25:47-55 Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni; 48 baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa; 49 au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu awaye yote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kwamba yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe. 50 Naye atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa yubile; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo; atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo. 51 Kwamba ikali imesalia miaka mingi, kama hesabu yake ilivyo ndivyo atakavyolipa bei ya ukombozi wake, katika hiyo fedha ambayo alinunuliwa kwayo. 52 Tena kwamba imesalia miaka michache tu hata mwaka wa yubile, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake. 53 Kama mtumishi aliyeajiriwa mwaka hata mwaka, ndivyo atakavyokuwa pamoja naye; asitawale juu yake kwa nguvu mbele ya macho yako. 54 Tena kwamba hakukombolewa kwa njia hizi mojawapo, ndipo atatoka katika mwaka wa yubile, yeye, na watoto wake pamoja naye. 55 Kwa kuwa wana wa Israeli ni watumishi; ni watumishi wangu niliowaleta watoke katika nchi ya Misri; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Kitendo cha kushindwa kuutumia muda na kazi kwa haki ni sawa na dhuluma. Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kutenda kwa haki hambo ya kikazi na sheria ya nguvu kazi au viwanda inayotokana na amri za Mungu. Munbu, ndiye anaowamiliki Israeli na wala sio mwanadamu awayeyote, na ni wa Waisraeli wote, wa aina zote mbili, yaani wale waliozaliwa hivyo na wale waliofanywa kuwa hivyo kwa wongofu kutoka kwenye Umataifa, hawa wote ni mali ya Bwana na wala sio watumwa. Na wala hawawezi kuuzwa kuwa watumwa na mtu yeyote au na taasisi yoyote iliyoko nchini au kwa namna yeyote ile.

 

Sheria hii itakuja rejeshwa upya tena katika Israeli na mfumo wa Yubile utakuja kurejeshwa upya kwa mujibu wa neno la Bwana ambalo Mungu alimwambia mtumishi wake nabii Yeremia (Yeremia 32:6-44).

 

Mwanakondoo amewakomboa wanadamu kwa Mungu na atawalinda kwenye Makao yake Matakatifu, kama tunavyoona kwenye kitabu cha Wimbo wa Bwana (Kutoka 15:1-19).

Kutoka 15:1-19  Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. 2 Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. 3 Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake. 4 Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu 5 Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe. 6 Bwana, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo, Bwana, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui. 7 Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea, Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu. 8 Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. 9 Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza. 10 Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu. 11 Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu? 12 Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi ikawameza. 13 Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu. 14 Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika. 15 Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka. 16 Hofu na woga umewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee Bwana, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua. 17 Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Mahali pale ulipojifanyia, Ee Bwana, ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara, Bwana, kwa mikono yako. 18 Bwana atatawala milele na milele. 19 Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, Bwana akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.

 

Naye Bwana atakuwa pamoja nasi kati yetu, yeye ambaye haanguki jangwani; Kwa hiyo msiitie unajisi nchi muiketiyo, ambayo naketi nami kati yake; kwa kuwa mimi Bwana nakaa(Hesabu 35:34; 20:22-24).

 

Basi na tusishindwe kumtolea Bwana sadaka zetu (Hesabu 15:1-12). Iwapo kama tulishindwa kumtolea pasipo kujua, ndipo upatanisho utafanywa (Hesabu 15:17-28). Hata hivyo, hakuna awezaye kumkomboa ndugu yake, bali ni Kristo tu ndiye awezaye hilo (Zaburi 49:6-7).

 

Dhana ya usawa

Katika sheria zote kuna dhana ya usawa kwenye kabila na familia zetu; ambavyo huweka majukumu ya watu na familia zao kwenye taifa lao.

 

Kwa hiyo kunafuatiwa na Mafundisho yanayofundisha Haki za Msingi yanayosema kuwa hakuna haki za mtu peke yake, na Mafundisho ya Sheeria na makatazo. Jamii yoyote inayoweka haki za watu kwenye mwonekano wa wasatani hushindwa kuweka mkakati fanikishi wa kimlingano kwa kipindi kijacho. Kwa hiyo sheria aote za kibiblia zimetuama kwenye mafundisho haya ya makatazo au miiko ya kwenye familia na kwenye taifa na yanatuama kwa kiasi kikubwa sana na miiko iliyawekwa na Mungu. Kwa jinsi.hiyo hiyo, jamii ina mambo yaliyokatazwa au kuharamishwa yasifanyike kati yao. Kwa hiyo, mfumo mzima wote wa usawa unaendana na kama miiko iliyoamriwa kwenye Amri Kuu ya Kwanza na ya Pili.   

 

Kuharibiwa kwa Mtu na Mali

 

Mtu asiyejali kumharibu mtu

Kutoka 21:18-19 17 Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa. 18 Watu wakigombana, na mmoja akimpiga mwenziwe kwa jiwe, au kwa konde, asife, lakini yualazwa kitandani mwake; 19 atakapoinuka tena na kuenenda nje kwa kutegemea fimbo, ndipo hapo yule aliyempiga ataachwa; ila atamlipa kwa ajili ya hayo majira yake yaliyompotea, naye atamwuguza hata apone kabisa.

 

Uharibifu hapa unatokana na mkusanyiko au mchango wa kudharau uliofanywa na pande zote mbili. Hakuna madai kwa makosa yaliyofanywa kwa ajili ya uharibifu auliochangiwa kufanywa na pande zote mbili. Hata hivyo, upande ulioumizwa unapaswa kurejeshewe upotevu wa muda na afya uliosababishwa na kwa upande ule ambao umesababisha maumivu haya.

 

Uharibifu uliofanywa kwa kudharau au kwa makusudi kama ulivyokusudiwa na upande wa tatu unabidi ulipwe sawa na uharibifu huo ulivyofanyika kama itakavyoonekana na kuamriwa na mahakama (Kutoka 21:22). Malipo kwa uharibifu uliofanywa na wanyama au matendo yaliyofanywa na upande wa tatu yameelezewa kwenye kitabu cha Kutoka 21:28-33. Malipo kwa ajili ya uhai uliopotea kwa uzembe yalifanywa kwa kufuatana na vile mahakama yatakavyoona, na hukumu yake inaweza kuwa ni kifo.

 

Makosa ya kuwafanyia uharibifu wa makusudi kwa watu

Makosa yenye kuleta uharibifu kwa watu yanachukuliwa kwa makundi mbali mbali. Yanaweza kufanywa na wake walioolewa (Kumbukumbu la Torati 22:13); na na wanawake ambao hawajaposwa bado (Kumbukumbu la Torati 22:28-29).

 

Tendo la kuteka na kumtorosha mtu hukumu yake ilikuwa ni kifo (Kutoka 21:16).

 

Uhalifu na dhuluma havitakiwi kumfanyia mtu yeyote na walio kwenye mamlaka (Luka 3:14; pia soma Isaya 17:14). Kudhulumiwa na wazani ni dhuluma pia na inamletea madhara yule aliyefanyiwa hivyo (Mithali 28:24).

 

Uharibifu wa makusudi wa mali

Wakati uharibifu unapotokea kwa hali tu ya kulidharau au kutotilia manani na kupuuza jambo, inatakiwa lirejeshwe kwanye ubora wake. Tunatakiwa kwenda mbali zaidi na kulifanya liwe bora kuliko lilivyokuwa hapo kabla. Kwa jinsi hiyohiyo, tunapokuwa tunalazimika kutoa huduma na kudumu kwenye uotaji wa huduma kwa bidii na hiyari (soma Mathayo 5:41; 27:32; Marko 15:21).

 

Adhabu ya makosa ya uharibifu wa makusudi

Kumbukumbu la Torati 23:24-25 Uingiapo katika shamba la mizabibu la jirani yako, utaweza kula zabibu za kukushibisha, kama upendavyo; ila usitie katika chombo chako. 25 Uingiapo katika mmea wa jirani yako waweza kuyapurura masuke kwa mkono wako; ila usisongeze mundu katika mmea wa jirani yako.

 

Hakuna mtu anayezuiwa kula au kupura masuke na mazao yaliyo mashambani anapokuwa na njaa, lakini hatakiwi au anachokatazwa ni kutovuna mavuno haya ayakutapo shambani. Kufanya hivyo ni sawa na kuiba na itachukuliwa kama ni dhuluma na wizi kwa afanyaye hivyo.

 

Uharibifu unaofanywa kwa makusudi, kuifanyia jumuia ya kidugu, kwa udanganyifu au wizi

Hatia inayofanywa kwa kuokota au kutapeli mali, au kwa kuifanyia hivyo jumuia ya kidugu, au kufanya udanganyifu, au kuiba, vyote hivi vinachukuliwa kama utapeli unaofanyika kwa namna ya kiwizi na unyang’anyi.

Mambo ya Walawi 6:1-5 Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Mtu awaye yote akifanya dhambi, na kuasi juu ya Bwana, akamdanganya mwenziwe katika jambo la amana, au la mapatano, au la kunyang'anya, au kumwonea mwenziwe; 3 au kuzumbua kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo; 4 ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang'anya, au kitu kile alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea alichokizumbua yeye, 5 au kitu cho chote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia.

 

Suala hili la kumuondoa au kumtenga mtu kutoka kwenye ushirika linafanyika pale inapofikia kiwango cha kuwa mtu amefanya wizi kwa kutumia cheo alichopewa kwa kuaminiwa. Torati ina idadi kadhaa ya mambo inayoshughulikia matukio kama hayo ya dhuluma na wizi. Katika mambo haya yote yaliyotajwa hapo juu, maamuzi yanabakia pale pale kwamba mali hiyo ni lazima irejeshwe kwa mwenyewe, na sehemu ya tano inatakiwa iongezwe juu yake. Hii kwa kuongezea kwenye gharama ya dhabihu kwa kuhani.

 

Wizi wa kawaida uliozoeleka

Mgawanyo wa kwanza na wa msingi wa amri ya nane inelezea wizi uliozoeleka na wa kawaida. Kama tunavyoona, kuna aina nyingi sana ya wizi. Aina mbili za kwanza za wizi zimeelezewa kama amri kwenye haki yao wenyewe, zinaelezewa kama wizi wa au kudhulumu maisha kwenye amri ya sita, kuiibia familia kwenye amri ya saba. Amri ya nane inahusika tu na aina duni ya dhana ya mali, inayojulikana kuwa ni mali ya kweli nay a mtu binafsi. Amri ya kumi inamhusisha mke na mali ya mtu binafsi ambazo hazitakiwi kuwakiwa tama.

 

Wizi una sura na tabia za aina mbili. Wizi wa vyakula umeharimishwa kote kuwili, yaani kwenye familia na kwenye jamii. Na ukitokea au kufanyika malipizi yake hufanywa kwa namna kadhaa mbali mbali, na haulipwi kwa kile tu kilichopotea peke yake na kilichojulikana kwa umaarufu wake.

Mithali 6:30-31 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa; 31 Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake.

(pia soma Mithali  13:11)

 

Kungu ndiye atoaye utajiri na ili kwamba asiwepo mtu atakayetaabika kwa njaa au ukosefu wa mahitaji.

Kumbukumbu la Torati 8:17-18 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. 18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

 

Marekebisho ya tabia ni jukumu la jamii katika kushughulikia suala la wizi (Waefeso 4:28).

 

Kuna kundi au aina nyingine ya wizi ambalo ni uibaji wa kitu kwa kuokota. Hakuna mtu anayeruhusiwa kuhodhi au kushikilia kitu cha mwingine, hata kitu cha adui yake, kama tulivyojionea kwenye aya za maandiko haya (Kutoka 23:4-5; Kumbukumbu la Torati 22:1-4).

 

Wizi ufanywao kwa wadhifa wa mtu

Haitakiwi kufanyika wizi kwa kutumia cheo au wadhifa wa mtu.

Ezekieli 46:18 Tena mkuu hatawaondolea watu urithi wao, hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake.

 

Kwa hiyo marudisho au utwaaji wa mali yanatakiwa kufanywa kwa wakati wake na pasipokuingilia na utaratibu wa yubile, au kwa kumwonea haya au kumpendelea mwingine (soma pia Mithali 28:19). Mamlaka ya kifalme au ya Kidola hayatakiwi yatumike kwa kunyang’anya ardhi kwa dhuluma au kwa sababu zisizo za lazima.

 

Marejesho ya mali au ardhi kwa kuzingatia Haki ni miongoni kwa mambo muhimu sana katika kulinda jamii yenye haki na huru.

 

Wizi unaofanywa kwa kutozingatia haki chini ya torati

Haitakiwi kuweko wizi kwa ajili ya kufanya mapunjo kwa kuzingatia torati.

Hesabu 15:13-16 Wote ambao wamezaliwa kwenu watafanya hayo yote kwa kuandama mfano huo, katika kusongeza sadaka kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana. 14 Tena kwamba mgeni amekaa kwenu, au mtu ye yote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye yuataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa Bwana; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo. 15 Katika huo mkutano, kutakuwa na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye pamoja nanyi; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kama ninyi mlivyo, na mgeni atakuwa vivyo mbele za Bwana. 16 Itakuwa sheria moja na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye nanyi.

 

Sawa na ilivyo kwamba kuna sheria moja tu ya upatanisho.

Hesabu 15:29-31 Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lo lote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao. 30 Lakini mtu afanyaye neno lo lote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake. 31 Kwa sababu amelidharau neno la Bwana, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake.

(soma Kumbukumbu la Torati 28:63).

 

Kwa hiyo, dhuluma inayofanywa kwa kuhukumu kwa upendeleo imekatazwa (soma Mithali 18:5, 11).

Kumbukumbu la Torati 1:17 Msitazame nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu awaye yote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.

(soma Kumbukumbu la Torati 1:11-18).

 

Kinga dhidi ya mwendelezo wa usawa wa haki za kikabila

Sheria za urithi tulizoziona zinaziendeleza zile za tano na sita zinazolinda heshima au hali ya kuaminika ya makabila na utajiri wa kitaifa. Tunajionea hilo kwenye sheria zilizo kenye kitabu cha Hesabu 27:1-11.

 

Haki ya kuhamisha au kubadilisha umiliko wa mali

Kwa namna hiyo hiyo hakutakiwi kuwa na upendeleo kwa mtu yeyote kwenye umiliki wa mali. Kufanya hivyo ni sawa na dhuluma pia, kwa mali iliyokuwa ya mababa kwenye kabila linaloheshimu sheria na kanuni ya mwaka wa yubile na haifai kufanywa hivyo kwa upendeleo.

Kumbukumbu la Torati 21:15-17 15 Akiwa mtu yuna wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa; 16 ndipo itakapokuwa ya kwamba siku atakayowarithisha wanawe alivyo navyo, asimweke mwana wa ampendaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana wa asiyempenda, naye ndiye mzaliwa wa kwanza huyu; 17 lakini amkubali mzaliwa wa kwanza mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo; kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake; haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.

 

Haki ya mzaliwa wa kwanza wa Israeli na miongoni mwa Mababu zao ulipotea kwa ajili ya dhambi, kama tunavyojionea kwa mfano wa Reubeni. Harakati hii inalenga kwenye hali ya muonekao ya wateule katika kuhitimisha mwelekeo wao wa dhambi. Haki ya mzaliwa wa kwanza inatuama kwenye nafasi au eneo linaloendeleza hali ya kuendeleza wajibu kwenye fa,ilia.

 

Kuiba kwa kutumia vipimo na mizani

Kipimo kile kile linatakiwa kitumike kwenye nyumba au kwenye biashara, na ni wizi au dhuluma kutumia vipimo na mizani ya uwongo.

Mambo ya Walawi 19:35-37 Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. 36 Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. 37 Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi Bwana.

 

Tunapaswa kutumia mizani kamili ili tuweze kuwa na maisha marefu, kama inavyosema amri ya tano, jambo muhimu na linalooweka mwelekeo na mwonekano wa utendaji wa haki na kazi ya Bwana (soma Mika 6:10-11; mithali 11:1; 16:11; 20:10, 23).

Kumbukumbu la Torati 25:13-16 Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako. 14 Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako. 15 Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. 16 Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.

 

Viwango vya uzani na vipimo vimeelezewa kwa kupitia mabii Ezekieli l.

Ezekieli 45:9-12 Bwana MUNGU asema hivi; Na iwatoshe ninyi, enyi wakuu wa Israeli; ondoeni dhuluma na unyang'anyi; fanyeni hukumu na haki; ondoeni kutoza kwa nguvu kwenu katika watu wangu, asema Bwana MUNGU. 10 Mtakuwa na mizani ya haki, na efa ya haki, na bathi ya haki. 11 Efa na bathi zitakuwa za kipimo kimoja; ili kwamba bathi ichukue sehemu ya kumi ya homeri, na efa sehemu ya kumi ya homeri; kipimo chake kitakuwa kwa kadiri ya cheo cha kawaida cha homeri. 12 Nayo shekeli itakuwa gera ishirini; shekeli tano zitakuwa shekeli tano, shekeli kumi zitakuwa kumi, na shekeli hamsini zitakuwa mane yenu.

 

Wizi unaofanyika kwa udanganyifu na dhuluma

Watu wengi hawajui kwamba tendo la kudanganya au kupunja na kudhulumu ni wizi na vinamuathiri na kumharibu mtu. Watu hawafikiri jambo jingine zaidi ya kufanya utapeli na kudhulumu kwa mfululizo wala kukoma, wakiwafanyia hivyo wenzao na kwa kawaida kwa kuwa wamechagua kuwa upande fulani au mwingine. Dini ya uwongo kwa muda mrefu sana zimekuwa ni chanzo udanganyifu mkubwa na utapeli kuliko kufanya jambi jingine lolote. Pale ambapo watu hawawezi kukanusha mabishano wanakimbilia kufanya visingizio, na pale wanapoweza wanaweza hata kuua pia. Jambo hili limeelezewa kwa kina zaidi kwenye jarida la Torati na Amri ya Tisa (Na. 262) [Law and the Ninth Commandment (No. 262)].

 

Kuiba ubora wa jina la mtu ni jambo lililo kinyume sana na Sheria au Torati ya Mungu na ni jambo lililo sawa na wizi au dhuluma iliyo mbaya sana kiaina yake.

 

Uharamu wa kushikilia mali na mshahara wa mtu

Ni kinyume na Sheria au Torati ya Mungu kumnyima mtu au kushikilia mshahara au mali ya mtu maskini, kwa vitu kama nguo na kitanda. Udanyanyifu au utapeli umekatazwa pia.

Kutoka 22:26-27 Ikiwa wewe kwa njia yo yote wapokea nguo ya jirani yako rehani, lazima utamrudishia mbele ya jua kuchwa; 27 maana hiyo nguo ni kifuniko chake, hiyo peke yake ni nguo ya ngozi yake; je! Atalalia nini? Itakuwa, hapo atakaponililia mimi, nitasikia; kwa kuwa mimi ni mwenye rehema.  

 

Mambo ya Walawi 19:13 Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang'anya mali yake; ijara yake aliyeajiriwa isikae kwako usiku kucha hata asubuhi.

 

Kumbukumbu la Torati 24:14-15 Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako; 15 mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako.

 

Mshahara wa malipo ya kila siku unatakiwa utolewe siku hiyo hiyo. Ni kinyume na sheria kushikilia mshahara wa malipo ya siku. Pia ni kinyume na sheria kushikilia ujira wa mkataba wa malipo ya siku kwa usiku kucha ua hadi asubuhi. Mkataba wa ujira unapaswa kufanyika kwa msingi wa makubaliano ya malipo ya kila juma au siku arobaini. Malipo ya ujira kwa kweli ni makubaliano yanayopaswa kukubaliana miongoni mwa pande zote mbili, yaani mwajiri na mwajiriwa.

 

Mikataba hii ya kisheria iko wazi na inaelezewa kwa wazi. Inaenda kwenye kiini cha sheria inayosema mpende jirani yako. Mtume Yakobo, ambaye alikuwa ni ndugu yake Yesu Kristo ana mengi ya kusema kuhusu jambi hili.

Yekobo 5:1-6 Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. 2 Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3 Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. 4 Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. 5 Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. 6 Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.

 

Jambo hilo hilo linaonekana kwenye waraka wa Mtume Paulo.

1Timotheo 5:18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake

(sawa na Warumi 13:7).

 

Pia Mungu alimwambia nabii Yeremia

Yeremia 22:13  Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake;

 

Mungu atawahukumu wale wote wanaotumia vibaya mamlaka yao.

Malaki 3:5 Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.

 

Mesihi alisema kuwa ujira wetu ambao utatolewa wote na kwamba utatolewa kwa mgao sawa, unaoitwa wokovu. Wale wanaowadhulumu na kuwatendea vibaya wale waliowajiri na kushikilia mashahara wao kinyume na haki hawatakuwa na sehemu kwenye Ufalme wa Mungu (soma Mathayo 20:1-16).

 

Kwa jinsi hiyo hiyo watumishi wanaohudumu kanisani hawapaswi kushikilia mshahara wa watumishi na wale wanaotumika kwenye makanisa yao. Hakuna hata mmoja miongoni mwa waaminio anayetakiwa akionekana akitangatanga kutoka nyumba hii hadi ile (Luka 10:7; 1Timotheo 5:17,18). Kila mmoja atapewa dhawabu yake sawa sawa na kazi aliyoifanya (1Wakorintho 3:8). Lakini wale walio kwenye imani wanatakiwa watumike kwa mfano wa wengine, na wanatakiwa wawasaidie na kuwalinda.

 

Udhalimu na unyang’anyi

Uchukuwaji wa zawadi mwa mtu mwenye majukumu ya kuhukumu unasababisha mwenye hekima kushawishika kupotoka na kufanya matendo yasoyo ya haki (Kutoka 23:8; Mambo ya Walawi 19:15; Kumbukumbu la Torati 16:18-20). Mungu hutoa malipo ya haki kama awezavyo (Zaburi 137:8).

 

Aina yote ya matendo yasiyo haki huiba sehemu ya kile anachokifanya asiye haki. Hili limefafanuliwa zaidi kwenye jarida la Torati na Amri ya Tisa (Na. 262) [Law and the Ninth Commandment (No. 262)].

 

Mungu atawatukuza na kuwarejesha upya wana wa watu wake.

Yoeli 3:6-8 tena watoto wa Yuda na watoto wa Yerusalemu mmewauzia Wayunani, mpate kuwahamisha mbali na mipaka yao; 7 tazameni, nitawaamsha wapatoke mahali mlipowauza, nami nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe. 8 Na mimi nitawauza wana wenu na binti zenu, na kuwatia katika mikono ya wana wa Yuda, nao watawauzia watu wa

Mambo yote hanayohusu hukumu yanapaswa yafanyike kwa haki, kwanza ni kanisani, na pilikwenye taifa (Mathayo 18:7; 1Wakorintho 6:1-8). Kushindwa kufanya mambo kwa haki kanisani ni udhalimu na dhuluma au wizi.

 

Riba

Moja ya makundi ya wale walioainishwa kuwa ni watu wa Bwana ni mtu yule ambaye haweki fedha zake kwenye riba au michezo ya kamari, au kumpa zawadi asiye na kosa (Ps. 15:5).

Zaburi 15:5 Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.

 

Kinachofuatia kwa hiyo ni kwamaa riba, au kukopesha fedha kwa riba sio tu kuwa kumekatazwa, bali kunamzuia mtu asiwe na sehemu kwenye Ufalme wa Mungu.

Mithali 28:8 Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.

Jambo hili huenda lisiweze kutokea kuwa la kuzingatiwa kwenye mazingira ya kila siku, bali tunashughulika pia na kutaka tuwe na sehemu kwenye hukumu na ufufuo wa kwanza wa wafu.

 

Nabii Yeremia anaiona hii riba kama kiini cha laana.

Yeremia 15:10  Ole wangu, mama yangu, kwa kuwa umenizaa mtu wa kuteta, na mtu wa kushindana na dunia yote! Mimi sikukopesha kwa riba, wala watu hawakunikopesha kwa riba; lakini kila mmoja wao hunilaani.

 

Mungu anauonya “mji wa damu” kwa kufanya kwao dhambi hii.

Ezekieli 22:12 Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu; umepokea riba na faida; nawe kwa choyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako, nawe umenisahau mimi, asema Bwana MUNGU.

 

Mungu anaelezea tofauti hii pia kwenye Ezekieli 18:3-20. roho itendayo dhambi hakika yake itakufa. Riba imetajwa wazi hapa kuwa ni tendo linalomuondolea mtu kuwa na sehemu kwenye uzima wa milele (Ezekieli 18:8,13). Dhana ya kutoza riba inapata mashiko kwa imani ya kujiongezea faida pia na kwa hiyo imekatazwa kukipesha kwa malipo ya riba. Kufanya hivyo kunamfanya mteule asiwe na sehemu kwenye ufufuo wa kwanza na ni wizi na dhuluma pia.

 

Kipindi cha kina Ezra na Nehemia, watu walilazimishwa kukodisha ardhi zao na nyumba zao ili wamudu kununua nafaka wakati wa marejesho mapya. Nehemia aliwafanya watu waliochukua ardhi na kuimiliki tena wairudishe kwa wamiliki wake halali, kwa kuwa kukopesha fedha kwa malipo ya ziada, na hususan kwenye ukodishaji, ni wizi, jambo ambalo halitaruhusiwa kwenye Ufalme wa Mungu. Riba au kukopesha fedha kwa faida ni kinyume na inavyoelekeza Torati ya Mungu na inatakiwa isiruhusiwe kabisa.

Nehemia 5:1-13 Ndipo kukatokea kilio kikuu cha watu, na wake zao, juu ya ndugu zao Wayahudi. 2 Maana, walikuwako watu waliosema, Sisi, na wana wetu na binti zetu, tu wengi; na tupate ngano, tule, tukaishi. 3 Tena walikuwako wengine waliosema, Tumeweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu, na nyumba zetu; tupate ngano, kwa sababu ya njaa. 4 Tena walikuwako wengine waliosema, Tumekopa fedha ili kulipa kodi ya mfalme kwa kuweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu. 5 Walakini miili yetu ni kama miili ya ndugu zetu, na watoto wetu kama watoto wao; kumbe! Mnawatia utumwani wana wetu na binti zetu kuwa watumishi, na baadhi ya binti zetu wamekwisha kutiwa utumwani; wala hatuwezi kujiepusha na hayo; maana watu wengine wana mashamba yetu na mizabibu yetu. 6 Nami nilikasirika sana, niliposikia kilio chao, na maneno hayo. 7 Ndipo nikafanya shauri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na mashehe, nikawaambia, Mnatoza watu riba, kila mtu ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kushindana nao. 8 Nikawaambia, Sisi kwa kadiri ya uwezo wetu tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi, waliouzwa kwa makafiri; na ninyi mnataka kuwauza ndugu zenu, tena kuwauza ili sisi tuwanunue? Wakanyamaza kimya, wasiweze kusema neno lo lote. 9 Tena nalisema, Neno hili mnalolitenda si jema; je! Haiwapasi ninyi kwenda katika kicho cha Mungu wetu, kwa sababu ya mashutumu ya makafiri adui zetu? 10 Na mimi pia, na ndugu zangu, na watumishi wangu, twawakopesha fedha na ngano ili kupata faida? Tafadhali na tuliache jambo hili la riba. 11 Naomba, warudishieni leo hivi mashamba yao, na mashamba yao ya mizabibu, na mashamba yao ya mizeituni, na nyumba zao, na lile fungu la mia la fedha, na la ngano, na la divai, na la mafuta, mnalowatoza. 12 Ndipo wakasema, Tutawarudishia, wala hatutataka kitu kwao; tutafanya hivyo, kama ulivyosema. Kisha nikawaita makuhani, nikawaapisha, ya kwamba watafanya kama ahadi hiyo. 13 Tena nikakung'uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung'ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung'utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi Bwana. Nao watu wakafanya kama ahadi hiyo.

 

Sheria iko wazi, fedha iliyokopeshwa haitakiwi ikopeshwe kwa faida. Riba hii haipaswi kuwa ya aina yoyote ya fedha wala ya mali au rasilimali ya namna yoyote.

Kutoka 22:25 Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida

 

Kumbukumbu la Torati 23:19-20 19 Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu cho chote kikopeshwacho kwa riba; 20 mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.

 

Lakini wakili alimwambia Kristo “Ni nani ndugu yangu?” sasa wokovu umewafikia Mataifa. Hakuna mtu anayepaswa kumkopesha mwenzake kwa riba kwenye nchi. Mataifa yote yamefunguliwa sasa kwa Ufalme wa Mungu. Wasamaria na Wamisri ni ndugu wa Wayahudi kwa uthamani bora ya imani.

 

Haiwapasi Yuda kuwakopesha Waefraimu, wala Waefraimu kuwakopesha Wamanase. Hakutakuwa na utaratibu wa kukopesha fedha kwa faida kipindi cha milenia ya Mungu. Kukopesha kutakuwa ni kati ya mataifa kwa ajili ya kufanya biashara na kusaidia.

 

Ufafanuzi wa Kristo kwenye Injili ya Mathayo 25:27 naLuka 19:23 haupaswi kuchukuliwa kuwa alikuwa anahalalisha tendo hili la kuchukua riba. Tendo hili limekatazwa na Mungu kwa wazi sana kwa kupitia torati na manabii wake. Kristo alikuwa anailiza swali kutoka kwenye mazingira yaliyozoeleka. Jibu lilikuwa ni kwamba mtu yule aliyedhaniwa kuwa ni mmiliki mwenye tabia ngumu za ubahiri na ndiyo maana aliamua kuificha ile talanta. Kisha Kristo akasema huyu alikuwa ni mtumishi mbaya na mpumbavu, kwa kuwa ni heri kama angeipeleka ile fedha kwa wabadili fedha na ndipo Kristo angepokea kutoka kwake iliyo stahili yake na riba. Hata hivyo, tendo hili lilikatazwa na kuharimishwa na Mungu. Maelezo haya ni ya kimfano tu na maana yake yanalenga hali halisi katika Ufalme wa Mungu na wala hayana uhusiano wowote na masuala ya fedha.

 

Tendo la kukopesha fedha kwa kurudishiwa na faida ni kutoza riba na Mungu ameliharimisha tendo hili na amehesabu kuwa ni haramu wale wote wafanyao hivyo. Kwa masuala ya kifedha, watu wanaweza kutoza ada kwa ajili ya huduma na sio zaidi yake. Inapohusiana na masuala ya kimahesabu kwa namna ya kujipatia faida (huwa sawa na riba au wizi), basi inabidi irejeshwe, kwa mujibu wa sheria ya torati inayoelezea masuala ya wizi ambao ni uvunjaji wa amri ya tisa. Kipindi cha utawala wa Masihi kila mtu atakayekpesha kitu chochote na kupenda kurudishiwa na faida juu yake ataletwa hukumuni na kuamriwa kulipa kwa mujibu w adhabu inayohusiana na wizi huo na faida aliyoipata kiudhalimu.

 

Madeni ma maachilio

Inahusiana na kulinda makatazo dhidi ya riba ni maachilio ya mwaka wa Sabato ambao kwao madeni yote huachiliwa na kusamehewa.

Kumbukumbu la Torati 15:1-23 Kila miaka saba, mwisho wake, fanya maachilio. 2 Na jinsi ya maachilio ni hii, kila mkopeshaji na akiache alichomkopesha mwenziwe, wala asimlipize mwenziwe wala nduguye; kwa kuwa imepigwa mbiu ya maachilio ya Bwana. 3 Waweza kumtoza mgeni; lakini kila uwiacho kwa nduguyo mkono wako utamwachilia. 4 Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa Bwana atakubarikia kweli katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;) 5 kwamba utaisikiza tu kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, uyatunze maagizo haya yote nikuagizayo leo, kuyafanya. 6 Kwani Bwana, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao. 7 Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; 8 lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo. 9 Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako. 10 Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia Bwana, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako. 11 Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako. 12 Ikiwa nduguyo, mume wa Kiebrania, au mwanamke wa Kiebrania, akiuzwa kwako, naye amekutumikia miaka sita; basi mwaka wa saba mwache huru aondoke kwako. 13 Nawe utakapomwacha huru aondoke kwako, usimwache aende zake mikono mitupu; 14 umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia Bwana, Mungu wako. 15 Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, akakukomboa Bwana, Mungu wako; kwa hiyo mimi nakuamuru neno hili hivi leo. 16 Hata itakuwa, akikuambia, Siondoki kwako; kwa sababu akupenda wewe na nyumba yako, kwa kuwa yu hali njema kwako; 17 ndipo utwae uma, uupenyeze katika sikio lake uingie katika ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako milele. Na kijakazi chako naye mfanye vivyo. 18 Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na Bwana, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya. 19 Wazaliwa wa kwanza waume wote wazaliwao katika kundi lako la ng'ombe na la kondoo, uwatakase kwa Bwana, Mungu wako; usifanye kazi kwa mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wako, wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kundi lako la kondoo. 20 Utamla mbele za Bwana, Mungu wako, mwaka hata mwaka mahali atakapochagua Bwana, wewe na nyumba yako. 21 Lakini akiwa na kilema, akichechea, au akiwa kipofu, au mwenye kilema kibaya cho chote, usimsongezee Bwana, Mungu wako, sadaka. 22 Utamla ndani ya malango yako; wasio tohara na wenye tohara pia watakula, kama unavyokula paa na kulungu. 23 Pamoja na haya usile damu yake; uimwage nchi kama maji.

 

Utaratibu wote huu umewekwa ili kumsamehe kila mmoja kutokana ma madeni na kumuachilia kutoka kwenye kazi nguvu ya utumwa, amri inayotekelezwa katika kila mwaka wa saba wa mzunguko wa kalenda. Kushindwa kuitekeleza amri hii ni kunachukuliwa sawa na kufanya uovu mkuu na kudharau au kudhalilisha uhuru wa kila mtu na taifa kwa mujibu wa Torati ya Mungu. Uamuzi wa kubakia utumwani ni wa mtu binafsi yake na ni udhaifu wa mtu binafsi yake ndio utakaompelekea kukataa fursa hii muhimu anayopewa kwenye utaratibu huu.

 

Dhana nzima ni kwamba sadaka ya hiyari itolewayo ya mnyama mkamilifu na asiye na waa lolote sio sehemu ya malimbuko ya kwanza na inaweza kuliwa ndani ya malango yetu. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, hayapo kwenye sehemu ya matoleo ya zaka, ambayo kwayo yanawakilisha ashirio la wateule.

 

Kuiba vitu vya wajane, yatima na wageni

Umiliki na haki ya kumiliki huendana na matarajio. Kila mtu ana matarajio ya kuruhusiwa kwa kiasi fulani na mhimu maishani mwake. Tumejonea kwamba Wamataifa wanamatarajio ya halali ya kuwa na sehemu katika milki ya Israeli, ikiwa ni moja ya mipango yake Mungu. Wamataifa hawa watajifunza kututumainia sisi na mamlaka iliyofanywa na kuanzishwa na Mungu chini ya Masihi (sawa na inavyosema Mwanzo 39:20-23; 40:3,5; 42:16,19; Mathayo 12:21; Warumi 15:12). Hii ifatokea kwa namna ambayo siyo ya kudhalilisha mamlaka ya Mungu katika kuwashughulikia walio dhaifu na yatima, masikini na wageni.

 

Hatutakiwi kumdhulumu mgeni yeyote, au mjane, au yatima, kwa kuw Mungu atawasikia kilio chao na kuwafanya wajane wake wa wale wanaodhulumu na watoto wao kuwa yatima kwa maafa yatakayoletwa na vita (Kutoka 22: 21-24; 23:9). Hatupaswi kumtenga na kumbagua au kumchukia mgeni bali tumpende na kumruhusu akae kwenye nchi yetu na miongoni mwetu, na tunapaswa kumpenda kama mmoja wetu, kwa kuwa nasisi tulikuwa wageni kwenye nchi ya Misri (Mambo ya Walawi 19:33, 34). Mgeni atafanya upatanisho pamoja nasi (Mambo ya Walawi 16:29) au vinginevyo atakatiliwa mbali (Mambo ya Walawi 17:8,9). Wageni watajumuishwa katika taifa la Israeli, kwa kuwa walinunulwa kwa thamani na Masihi na sasa wokovu ni kwa Wamataifa. Kwa hiyo sehemu yao ni ya masharti fulani, lakini badi haiwezi kuibiwa au kuondolewa kutoka kwao. Hata hivyo, wanapaswa kwa lazima wawe ni sehemu ya utaratibu uliowekwa wa taifa hilo (Mambo ya Walawi 22:10,11,15,18). Machukizo yao yameharimishwa kwetu, bali tunapaswa kuwapenda kama nafsi zetu (Mambo ya Walawi 18:26; Kumbukumbu la Torati 10:17-22). Iwapo kama mjane yeyote au yatima ameonewa au kudhulumiwa kwa namna yoyote ile, Mungu atakisikia kilio chake (Kutoka 22:23).

 

Kuwaibia masikini kwa kuweka nadhiri au ahadi

Hatupaswi kuchukua kitu chochote kutoka kwa masikini kuwa ni poni kwa ajili ya madeni yake, kwa kuchukua vitu vinavyoyahusu maisha yake, kiwango cha maisha yao, au kulingana na mali, au usalama wao au maisha yao.

Kumbukumbu la Torati 24:10-14  Umkopeshapo jirani yako cho chote kikopeshwacho usiingie katika nyumba yake kwenda kutwaa rehani kwake. 11 Simama nje, yule umkopeshaye akuletee nje ile rehani. 12 Naye akiwa ni mtu maskini, usilale na rehani yake. 13 Sharti umrudishie rehani lichwapo jua, apate kulala na mavazi yake, na kukubarikia; nayo itakuwa ni haki kwako mbele za Bwana, Mungu wako. 14Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako;

Hapa tunalazimisha malipo ya shuruti kwa mwajiriwa na amri ionekanayo hapa haimaanishi kumfanyia dhuluma mtu huyo.

 

Kuingia kwa shuruti au pasipo kukaribishwa au kualikwa na mkopaji kwenye nyumba yake kwa nia ya kumdai kumekatazwa. Mambo yote yanapaswa yafanyike kwa mujibu wa sheria.

 

Kuwatunza au kuwahudumia masikini

Maagizo ya shetia yanaenda hadi kwenye masuala ya kuwahudumia masikini, kuliko kuwaacha tu na kukwepa au kuepuka kuwahudumia na kuwatendea vibaya.

 

Mahudhui ya torati yanaonyesha jinsi Mungu anavyowakemea wale wanalalamika kwa kukosa kufanya biashara siku za Mwandamo wa Mwezi Mpya na Sabato hadi zitakapopita. Kwa hiyo, katika siku hizi za mwisho Israeli ambayo inaonyeshwa kwa lugha picha ya kikapu cha matunda ya majira ya hari.

Amosi 8:1-8 Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, kikapu cha matunda ya wakati wa hari. 2 Akaniambia, Amosii, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa hari. Ndipo Bwana akaniambia, Mwisho wao umewajilia watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe. 3 Tena nyimbo za hekaluni zitakuwa vilio siku ile, asema Bwana MUNGU; mizoga itakuwa mingi; kila mahali wataitupa, wakinyamaza kimya. 4 Lisikieni hili, ninyi mnaopenda kuwameza wahitaji, na kuwakomesha maskini wa nchi, 5 mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na sabato nayo, tupate kuandika ngano? Mkiipunguza efa na kuiongeza shekeli, mkidanganya watu kwa mizani ya udanganyifu; 6 tupate kuwanunua maskini kwa fedha, na wahitaji kwa jozi ya viatu; na kuziuza takataka za ngano. 7 Bwana ameapa kwa fahari ya Yakobo, Hakika sitazisahau kamwe kazi zao hata mojawapo. 8 Kwa ajili ya hayo, je! Haitatetemeka nchi, na kuomboleza kila mtu akaaye ndani yake? Naam, itainuka yote pia kama huo Mto; nayo itataabika na kupwa tena kama Mto wa Misri

(sawa na Nehemia 5:1-13)

Kwa mtazamo huu, tendo la kuwatunza masikini ni wajibu muhimu na uliosisitizwa sana na torati.

 

Luka 6:30-34 Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. 31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo. 32 Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao. 33 Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. 34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.

 

Tuwaonapo watu wenye uhitaji, kila mmoja wetu anawajibika kumkopesha na asiulizie kuhusu lini atarudishiwa. Na vivyo hivyo, wale wanaokopa wanaowajibu wa kurejesha na kuwakopesha wengine wenye uhitaji zaidi yao.

 

Tunapakiwa kuwapenda maadui zetu pia (Luka 6:35); na kuwalinda wanaokimbilia kwetu (Kumbukumbu la Torati 23:15-16). Wale ambao hawawadhulumu masikini, au ambao hawajachukua riba au faida itokanayo na kukopesha kwao, wataishi maisha marefu (Ezekieli 18:17; sawa na Ayubu 24:2-10; Mithali 22:22, 23).

 

Kukomboa, Marejesho na Marekebisho

Kusudi la la kutolewa kwa sheria zote hizi zinazoendana na migawanyo ya Kuzuia na kisha Kukomboa, au Marejesho na Marekebisho.

Waefeso 4:28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.

 

Kwa hiyo, hata hivyo, kuna amri mahsusi zinazohusiana na adhabu na malipizi zinazohusiana na mambo ya wizi pia.

 

Matendo ya hila na ulaghai yanasamehewa pia. Kwa hiyo, tendo la kudanganya na ambalo liko kinyume na maagizo ya torati linapaswa kutubiwa.

Luka 17:4 Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.

 

Dhambi zilizofanywa bila kukusudiwa na kwa ujinga zimeorodheshwa na kufafanuliwa kwenye kitabu cha Mambo ya Walawi sura za 4 na 5. Dhumuni la kuamriwa kutolewa kwa sadaka ni kufanya toba ya wazi na faini kwa ajili ya mambo yaliyofanywa kwa mikono. Kristo alitulipia deni la adhabu kwa dhambi zetu na hii isingewezekana kulilipwa yote kikamilifu kwa damu ya wanyama. Katika siku za mwisho, utaratibu utarejeshwa tena, dhabihu zitatolewa na adhabu zitarejeshwa tena na kutumika. Kwa hiyo, hakutakuwa na jinsi yoyote ya kusimamisha matendo ya utoaji wa dhabihu kwa Kristo, bali ni kwa namna ya kutoa adhabu na kufanya toba ya dhahiri tu (sawa na Hesabu 15:28). Na itakapofanyw ahivyo, mtenda dhabi atakuwa amesamehewa.

 

Kwa wale wanaopenda sana, watasamehewa mengi; na wale wanaopenda kidogo, watasamehewa machache na Mwana wa Mungu anao uwezo wa kusamehe dhambi (Luka 7:47-48). Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila. (Zaburi 32:1-2; Warumi 4:7-8; Wakolosai 2:13).

 

Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa (Yakobo 5:15). Kwa hiyo, magonjwa ni mambo yanayotokana na dhambi. Kwa hiyo, dhambi zote zinasamehewa kwa jina tukufu la Mungu katika Yesu Kristo (1Yohana 2:12)

 

Kwa hiyo mtu anayepuuzia msamaha unaotokana na toba anafanya dhambi mbaya kama ya wizi na anazuia marejesho, na anaiba maisha ya anayetubu na wale wote waliokaribu naye.

 

Maombi au sala ya Bwana yana sehemu inayosema “Baba, utusamehe sisi kama na sisi tunavyowasamehe wale wanaotukosea.” Kusamehe ni jambo la lazima na kutofanya hivyo, yaani kutowasamehe wengine ni sawa na kufanya mambo yote mawili, yaani uuaji na wizi, na ni kuzivunja amri za sita na nane. Inatenga na kuhalifu hali ya kujiona kuwa sawa au kujihesabia haki, jambo ambalo linamwondolea mtu uwezekano wa kukubalika kuuingia Ufalme wa Mungu. Tendo hili la kujihesa bia haki mwanadamu humpeleka kwenye dhuluma au wizi na kumfanya ajisikie mkosaji maisha yake yote na kuwaletea madhara wale wote waliokaribu naye, na sharti muhimu katika kusamehe ni toba ya kweli na mwenye kufanya hivyo tu ndiye apaswaye kusamehewa. Kwa ajili ya kutokujua kwao watajikuta wakikosa kuuingia Ufalme wa Mungu wao wenyewe na wanawazuia wengine ambao huenda wangeweza kuuingia na kuurithi kama wangeweza kufanya hivyo.

 

Tendo la kumuiba mke wa mtu linahusika pia na makosa haya ya kutozwa faini. Abimeleki alijikuta akiadhibiwa ingawaje hakuwa hata amewahi kulala na Sara, bali alikuwa amemchukua tu, kwa kuwa Abrahamu alisema kuwa alikuwa ni dada yake tu. Ingawaa maneno yake yalikuwa ni ya kweli, bali yalikuwa yameficha kweli nyingine ya muhimu, na ambayo ilimsababishia Abimeleki aingie kwenye hali ambayo yeye mwenyewe pamoja na taifa lake lote lingeweza kuingia hatarini na kupata mapigo (soma Mwanzo 20:3-7). Amri ya saba ilikuwa ndiyo iliyokuwa ikishinikiza katika kipindi hiki pia na iliyoeleweka na Wamataifa. Licha ya dhambi hizi za Abrahamu, bado yeye ni nabii na Mungu aliyasikia maombi yake aliyokuwa anamuomba. Mungu amemchagua na kumtenga mbali na alishughulikia nay eye licha ya dhambi zake hizi. Kwa hiyo, Abrahamu hakuhesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake tu, bali ni kwa Neema ya Mungu peke yake (soma Mwanzo 20:3-7, 14-18). Kwa hiyo, hatimaye alimbariki Abimeleki kwa jinsi alivyomtunza na kumfanyia Abrahamu. Mungu atayalinda mataifa yote kwa njia ya imani kama alivyofanya hatimaye (Isaya 2:4). Mungu ametupa sisi huduma hii ya upatanisho (2Wakorintho 5:18)

 

Tumeona kwamba aina yoyote ya wizi ufanywao kwa kuokota au kwa kujitwalia kitu cha mtu pasipo ridhaa yake, au kwa kuchukua kwa nguvu na kukificha ni matendo mabaya yasiyokubalika na yaliyoharamishwa na sheria na kinatakiwa kirejeshwe kwa mwenyewe kikiwa na nyongeza ya sehemu ya tano ya thamani yake asilia, na gharama ya sadaka itakayotolewa kwa Mungu kupitia kwa makuhani wake itaongezewa pia kiasi kama hicho pia (sawa na isemavyo Mambo ya Walawi 6:1-5 hapo juu). Inapotokea kuwa kuna kitu kimechukuliwa au kupotea na hatimaye kuuawa, au kimeuzwa, au kimeraruliwa kwa namna nyingine yoyote ile, ndipo thamani ya kitu hicho italipwa kwa kiasi cha juu kwa ajili ya adhabu au faini. Ikitokea kutokea hayo kwa ng’ombe, basi malipo yake yatakuwa ni kutolewa watano kwa ajili ya mmoja; au kama ni kondoo atalipa wane kwa ajili ya mmoja. Iwapo kama atakutwa mikononi mwake na akiwa angali hai bado, atalipa mara mbili yake. Na iwapo kama atakutwa au kukamatwa akivunja ili kuiba mali iliyoko ndani au kwenye giza, atauawa na asitakiwe kulipa aina yoyote ya malipizo kwa mauaji aliyoyafanya. Kama atakuwa ameuawa baada ya mapambazuko, ndipo muuaji atatakiwa kulipa faini.

 

Mwizi atatakiwa kufanya marejesho kamili, vinginevyo anaweza kuuzwa kuwa mtumwa kwa ajili ya wizi wake. Tendo la kupuuzia uharibifu uliofanywa na unguzo la moto kunachukuliwa pia kama wizi, na unahitaji marejesho kamili. Iwapo kama itapotea kwa ajili ya kushukilia mali ya mtu mwingine kikiwa kwenye matunzo au uangalizi salama kunahitaji malipo maradufu.

Kutoka 22:1-15 Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng'ombe watano badala ya ng'ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. 2 Mwivi akipatikana akiwa yu hali ya kuvunja mahali, naye akapigwa hata akafa, hapatakuwa na malipizo ya damu kwa ajili yake. 3 Lakini kama jua limekucha juu yake, ndipo patakuwa na malipizo ya damu kwa ajili yake; ingempasa kutoa malipo kamili; akiwa hana kitu, na auzwe kwa ajili ya wivi wake. 4 Kama hicho kitu kilichoibwa chapatikana hai mkononi mwake, kama ni ng'ombe, au punda, au kondoo; atalipa thamani yake mara mbili. 5 Mtu akilisha katika shamba, au shamba la mizabibu, akimwacha mnyama wake, akala katika shamba la mtu mwingine; atalipa katika vitu vilivyo vizuri vya shamba lake mwenyewe, au vya mizabibu yake. 6 Ukiwaka moto, na kushika penye miiba, na ngano zilizofungwa miganda, au ngano ambazo hazijakatwa, au shamba, likateketea; yeye aliyeuwasha huo moto lazima atalipa. 7 Mtu akimpa mwenziwe amana ya fedha au vitu vingine amtunzie, na vitu vile vikaibwa katika nyumba ya mtu huyo; mwivi akipatikana, atalipa thamani yake mara mbili. 8 Mwivi asipopatikana, ndipo mwenye nyumba atakaribia mbele ya Mungu, ionekane kwamba si yeye aliyetia mkono na kutwaa vyombo vya mwenziwe. 9 Kila jambo la kukosana, kama ni la ng'ombe, au la punda, au la kondoo, au la mavazi, au la kitu cho chote kilichopotea, ambacho mtu mmoja asema ni chake, hilo jambo la watu wote wawili litaletwa mbele ya Mungu; na yeye atakayehukumiwa na Mungu kuwa ni mkosa atamlipa mwenziwe thamani yake mara mbili. 10 Mtu akimpa mwenziwe punda, au ng'ombe, au kondoo, au mnyama ye yote, ili amtunzie; yule mnyama akafa, au akaumia, au akachukuliwa mtu asione; 11 patakuwa na kiapo cha Bwana katikati ya watu hao wawili, kwamba alipeleka mkono wake kutwaa mali ya mwenziwe, na mwenyewe atakubali hayo, wala hatalipa. 12 Lakini kwamba aliibiwa mnyama huyo, sharti amlipe yule mwenyewe. 13 Kwamba aliraruliwa na mnyama mkali, na amlete uwe ushahidi; hatalipa kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa. 14 Mtu akiazima mnyama kwa mwenziwe, naye akaumia huyo mnyama, au akafa, mwenyewe asipokuwapo, lazima atalipa. 15 Kama huyo mwenyewe alikuwapo pamoja na mnyama wake, hatalipa; kama ni mnyama aliyeajiriwa, alikwenda kwa ajili ya ujira wake.

 

Sheria ihusuyo marejesho ya vitu vilivyouawa kikiwa kwenye uangalizi au kimeazimwa yanategemea jinsi ya marejesho na sheria zinazohusu uharibifu uliotokana na uzembe. Kwa hiyo masharti ya kufanya kwa ajili ya uangalizi wa mali iliyotolewa kwa mtu ili atunze ni tawi lingine la sheria au torati. Kwa usemi wa siku hizi, mtu anayehusika na uangalizi wa mali anawajibika kwa kifo au uharibifu wake, na ni lazima amfanyie mambo mema kwa jinsi alivyomsababishia upotevu mtu huyo aliye umiliki asilia na wa kweli. Hata hivyo, iwapo kama alikuwa ni mwangalizi na iliharibiwa au kuraruliwa na mnyama wa porini, atapaswa kuthibitisha ukweli wake, na kisha litaangaliwa na kuthibitishwa kwa muwajibiko unaostahili kwa jinsi linavyoweza kuamuliwa kulingana na hali halisi ilivyoonekana pasipo kujali ni nani aliyekuwa anamuangalia au kumtunza.

 

Kutengwa maalumu kwa ajili ya nadhiri au kanuni za uwajibiko

Mambo ya Walawi 27:1-34 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtu atakapoondoa nadhiri, hizo nafsi za watu zitakuwa kwa Bwana, kama utakavyowahesabia wewe. 3 Na hesabu yako itakuwa kwa mtu mume, tokea aliye na umri wa miaka ishirini hata umri wa miaka sitini, hesabu yako itakuwa shekeli hamsini za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu. 4 Kama ni mwanamke, hesabu yako itakuwa shekeli thelathini. 5 Tena akiwa mwenye umri wa miaka mitano hata umri wa miaka ishirini, ndipo hesabu yako itakuwa shekeli ishirini kwa mwanamume, na shekeli kumi kwa mwanamke. 6 Tena akiwa mwenye umri wa mwezi mmoja hata umri wa miaka mitano, ndipo hesabu yako itakuwa shekeli tano za fedha kwa mwanamume, na hesabu yako itakuwa shekeli tatu za fedha kwa mwanamke. 7 Tena akiwa mwenye umri wa miaka sitini na kuzidi; kama ni mwanamume, hesabu yako itakuwa shekeli kumi na tano, na kwa mwanamke shekeli kumi. 8 Lakini kwamba ni maskini zaidi ya kuhesabu kwako, ndipo atawekwa mbele ya kuhani, na huyo kuhani atamtia kima; kama uwezo wake huyo aliyeweka nadhiri ulivyo, ndivyo kuhani atakavyomtia kima. 9 Tena kama ni mnyama wa namna ambayo watu husongeza kuwa sadaka kwa Bwana, kila mmoja katika wanyama hao atakayetolewa kwa Bwana, na mtu ye yote, atakuwa ni mtakatifu. 10 Yeye hatamgeuza, wala kumbadili mwema kwa mbaya, au mbaya kwa mwema; kwamba atabadili mnyama kwa mnyama ye yote, ndipo mnyama huyo na yule waliobadiliwa wote wawili watakuwa watakatifu.11 Na kama ni mnyama ye yote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa Bwana, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani; 12 na kuhani atamtia kima, akiwa mwema akiwa mbaya; kama wewe kuhani utakavyomtia kima, ndivyo itakavyokuwa. 13 Lakini kwamba ataka kumkomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano juu ya hesabu yako. 14 Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa Bwana ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa. 15 Tena mtu huyo aliyeweka nyumba yake iwe wakfu kama akitaka kuikomboa, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nayo itakuwa mali yake. 16 Tena kama mtu akiweka wakfu kwa Bwana sehemu ya shamba la milki yake, ndipo hesabu yako itakuwa kama kule kupanda kwake kulivyo; kupanda kwake homeri moja ya mbegu ya shayiri, kutahesabiwa kuwa ni shekeli hamsini za fedha. 17 Kwamba anaweka shamba lake liwe wakfu tangu mwaka wa yubile, litasimama vivyo kama hesabu yako ilivyo. 18 Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya yubile, ndipo kuhani atamhesabia hiyo fedha kama hesabu ya miaka iliyobaki hata mwaka wa yubile, na kuhesabiwa kwako kutapunguzwa. 19 Na kama yeye aliyeliweka shamba wakfu akitaka kulikomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nalo litathibitishwa kwake. 20 Lakini asipotaka kulikomboa shamba, au kama amemwuzia mtu mwingine hilo shamba, halitakombolewa tena kabisa; 21 ila hilo shamba litakuwa takatifu kwa Bwana litakapotoka katika yubile, kama ni shamba lililowekwa wakfu; litakuwa mali ya kuhani. 22 Tena kama akiweka wakfu kwa Bwana shamba ambalo amelinunua, ambalo si shamba la milki yake; 23 ndipo kuhani atamhesabia kima cha kuhesabu kwako hata mwaka wa yubile: naye atatoa siku hiyo kama hesabu yako, kuwa ni kitu kitakatifu kwa Bwana. 24 Mwaka wa yubile shamba hilo litarejea kwake huyo ambaye lilinunuliwa kwake, yaani, huyo ambaye nchi hiyo ni milki yake. 25 Na hesabu zako zote zitaandamana shekeli ya mahali patakatifu; gera ishirini zitakuwa shekeli moja. 26 Mzaliwa wa kwanza tu katika wanyama, aliyewekwa kuwa mzaliwa wa kwanza kwa Bwana, mtu awaye yote hatamweka kuwa mtakatifu; kama ni ng'ombe, kama ni kondoo, huyo ni wa Bwana. 27 Na kama ni wa mnyama asiye safi, ndipo atamkomboa kama hesabu yako ilivyo, naye ataongeza sehemu ya tano ya bei yake; au asipokombolewa, ndipo atauzwa kama hesabu yako ilivyo. 28 Pamoja na hayo, hakitauzwa wala kukombolewa kitu cho chote kilichowekwa wakfu, ambacho mtu amekiweka wakfu kwa Bwana, katika vitu vyote alivyo navyo, kama ni mtu, au mnyama, au kama ni shamba la milki yake; kila kitu kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa Bwana. 29 Kila aliyewekwa wakfu, aliyewekwa wakfu na binadamu, hatakombolewa; sharti atauawa. 30 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana. 31 Na kama mtu akitaka kukomboa cho chote cha zaka yake, ataongeza sehemu yake ya tano juu yake. 32 Tena zaka yote ya ng'ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa Bwana. 33 Hataangalia kwamba ni mwema au kwamba ni mbaya, wala hatambadili; na kama akimbadili na yo yote, ndipo wote wawili, huyo na huyo waliobadiliwa watakuwa ni watakatifu; hatakombolewa. 34 Haya ndiyo maagizo, Bwana aliyomwagiza Musa kwa ajili ya wana wa Israeli katika mlima wa Sinai.

 

Dhana nzima ya utoaji wa zaka na kikombozi ni kuonyesha kwamba wale waliojitoa nafsi zao kwa Bwana wa wanyama safi wasiweze kukombolewa, kama inavyoashiria kuwa wateule ni malimbuko ya mavuno. Tendo la kukomboa zaka iliyotolewa ni uchoyo, na linagharimu mtu kuongeza sehemu ya ishirini au adhabu yake ni kuongeza sehemu ya tano ambayo ni muhimu na ni ya lazima kwa anayetaka kurudishiwa mali yake. Kwa kuwa Dhaka ni mali ya Mungu.

 

Taratibu na kanuni za kimahakama

Amri zote zinazohusiana na kumpeleka mtu kwenye mahakama ya kata au kumuweka kizuizini zinategemea jinsi mahakama inavyoamua (sawa na Mambo ya Walawi 24:12; Hesabu 15:34; 1Wafalmw 22:27). Kusiweko na ucheleweshaji wa kutoa hukumu au maamuzi bila sababu ya msingi, bali haki inatakiwa iangaliwe na kuheshimiwa.

 

Kunapaswa kuwe na viwango vya maamuzi, ili kwamba mambo yote yashughulikiwe kikamilifu na kwa haki na kwa viwango vyake halisia (Kutoka 18:12-24). Kusiweko na mtu atakayemfanyia mwenzake jambo ambalo hakustahili au hapendi kufanyiwa yeye mwenyewe (Mathayo 7:12). Thawabu ya kila mmoja itamrudia kichwani mwake mwenyewe (Obadia 15).

 

Mwaka wa Sabato ni mwaka wa maachilio pia na unapaswa uchukuliwe hivyo na kila mahakama na taratibu zake ziheshimu mahudhui yake, kwa mikataba yote na mambo yaliyosababisha uharibifu na hasara. Mambo yote yaliyosababisha hasara na gharama zake yanapaswa yahusishwe kwenye mwaka wa yubile na huu wa Sabato na hakuna zawadi inayopaswa kutolewa inayoendana na mahudhui mazima ya mwaka wa yubile na taratibu zake (soma jarida la Torati na Amri ya Nne (Na. 250) [Law and the Fourth Commandment (No. 256)].

 

Msamaha na Maachilio

Tunapaswa kuwasamehe wote wote tunaowadai madeni katika Mwaka wa Maachilio. Hatupaswi kumfanya mtu kuwa mtumwa wa kujikia katika hisia zake wala wa madeni ya fedha kwa kumfanya awe mtumwa wetu atutumikie au kwa ajili ya madeni tunayomdai (soma Kumbukumbu la Torati 15:1-18 hapo juu).

 

Katika milki za urithi wetu zote ambazo Mungu ametupa, watumishi wa kanisa au makuhani waliochaguliwa na kuwekwa wakfu wanaotutumikia, na hao wanapaswa kuhudimiwa au kupewa sehemu yao kutoka kwenye zaka na sadaka iliyotolewa kwa imani na moyo wa hiyari. Hatupaswi kuwaibia wale ambao Mungu amewateua na kuwaweka wakfu watutumikie.

Kumbukumbu la Torati 18:1-8 Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za Bwana zifanywazo kwa moto, na urithi wake. 2 Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaambia. 3 Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo. 4 Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, umpe. 5 Kwani Bwana, Mungu wako, amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina la Bwana, yeye na wanawe milele. 6 Na akija Mlawi atokaye katika malango yako mojawapo, katika Israeli yote alipokuwa akikaa, akaja kwa mapenzi yote ya nafsi yake mahali atakapochagua Bwana; 7 na atumike kwa jina la Bwana, Mungu wake, kama wafanyavyo ndugu zake wote, Walawi wasimamao huko mbele za Bwana. 8 Wawe na fungu sawasawa la kula, pamoja na haya yaliyomfikilia kwa kuuzwa urithi wa baba zake.  

 

Walawi walitengwa kando na sasa makuhani walio mfano wa Melkizedeki ndio pia wameitwa na kuchaguliwa (soma Waebrania 7:1-8:13).

Hesabu 1:47 Lakini Walawi kwa kuiandama kabila ya baba zao hawakuhesabiwa katika watu hao.

Kuhani ameteuliwa na Mungu, wakiwa ni wateule kamili wa wateule wa Mungu na makuhani.

Hesabu 8:13-19 Kisha utawaweka Walawi mbele ya Haruni, na mbele ya wanawe na kuwasongeza kwa Bwana wawe sadaka ya kutikiswa. 14 Ndivyo utakavyowatenga Walawi na kuwatoa katika wana wa Israeli; na Walawi watakuwa wangu. 15 Kisha baadaye Walawi wataingia ndani, ili wafanye utumishi wa hema ya kukutania; nawe utawatakasa, na kuwasongeza wawe sadaka ya kutikiswa. 16 Kwa kuwa nimepewa kabisa mimi watu hawa kutoka katika wana wa Israeli; badala ya wote wafunguao mimba, maana, wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wote, nimewatwaa wawe wangu. 17 Kwa kuwa wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli ni wangu, wa wanadamu na wa wanyama; siku hiyo niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri niliwatakasa kwa ajili yangu mwenyewe. 18 Nami nimewatwaa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote walio katika wana wa Israeli. 19 Nami nimempa Haruni hao Walawi wawe kipawa chake yeye na wanawe, kutoka kwa wana wa Israeli, ili watumike utumishi wa wana wa Israeli katika hema ya kukutania, kisha wafanye upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli; ili kusiwe na maradhi kati ya wana wa Israeli, hapo wana wa Israeli watakapopakaribia mahali patakatifu.

Walawi wanashughulika na mambo ya kanisa na wanawakilisha taifa zima la Israeli wakiwa ni wazaliwa wa kwanza wa Mungu. Na ndiyo maana kwa sasa kanisa ni mfano wa mzaliwa wa kwanza wa mataifa yote na wokovu wa ulimwengu.

 

Hesabu 18:15-18 Kila kifunguacho tumbo, cha wenye mwili wote watakachomsongezea Bwana cha wanadamu na cha wanyama, ni chako; lakini mzaliwa wa kwanza wa binadamu, huna budi utamkomboa, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi utamkomboa. 16 Na hao watakaokombolewa katika wanyama hao, tangu aliyepata umri wa mwezi mmoja utamkomboa, kama utakavyohesabu kima chake, kwa fedha ya shekeli tano, kwa shekeli ya mahali patakatifu (nayo ni gera ishirini). 17 Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, au mzaliwa wa kwanza wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, hutawakomboa hao; maana, ni watakatifu hao; utanyunyiza damu yao katika madhabahu, na kuyateketeza mafuta yao kuwa sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto, iwe harufu ya kupendeza. 18 Tena nyama yao itakuwa ni yako wewe, kama kile kidari cha kutikiswa, na kama mguu wa nyuma wa upande wa kuume, itakuwa yako.

 

Kwenye sheria zote za sadaka, tunatakiwa kukitumia kile kilichowekwa wakfu na Bwana kwa matumizi sahihi, na hatupaswi kukitumia vibaya kabla hakijatolewa kwa Mungu. Kumzuilia kutomtoa mzaliwa wa kwanza ni sawa na kuiba, na kwa hiyo wateule ambao wnakwenda kuwa wafalme na makuhani hawataweza kuzuiliwa na Mungu. Kwa hiyo, wanyama wenye mawaa wanaweza kuliwa, bali ni wale wasio na mawaa tu ndio wanatakiwa kutengwa ili kuwekwa wakfu kwa Mungu. Hii inaonyesha ukweli kwamba wateule wananguo zao ndefu za kanzu nyeupe kwenye damu ya mwana kondoo na wamewekwa wakfu wamtumikie Mungu kwa Kristo wake (soma Kumbukumbu la Torati 15:19-23 hapo juu).

 

Kumbukumbu la Torati 26:1-19 Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu; 2 na iwe, ikimpasa kupigwa yule mwovu, alazwe chini na mwamuzi, na kupigwa mbele ya uso wake, kwa kadiri ya uovu wake, kwa kuhesabu. 3 Aweza kumpiga fimbo arobaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako, azidishapo kwa kumpiga fimbo nyingi juu ya hizi. 4 Ng'ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa. 5 Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe. 6 Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli. 7 Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu. 8 Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu, 9 ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi. 10 Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu. 11 Washindanapo waume wao kwa wao, akakaribia mke wa mmojawapo, ili kumwokoa mumewe katika mkono wa ampigaye, yule mke akatoa mkono wake, na kumkamata tupu yake; 12 umkate ule mkono wake, lisiwe na huruma jicho lako. 13 Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako. 14 Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako. 15 Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. 16 Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako. 17 Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri; 18 jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. 19 Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.

 

Kwa hiyo, Zaka na Sikukuu kwa hiyo ni za muhimu na lazima na zinatoa ashirio la marejesho. Kutozitunza hizi Sikukuu na kutoa zaka ni wizi, na unamtenga mtu huyo mbali na ufufuo wa kwanza. Zaka na sadaka hizi hazipaswi zitumike kwa ajili ya wafu kama ilivyokuwa ni kawaida kufanywa kwenye huduma za mazishini kwa wapagani hapo zama za kale.

 

Maafikiano na uhuru

Kila mmjoa wetu amenunuliwa kwa walipo ya gharama kubwa ili kwamba tusiwe watumwa au watumishi wa mtu yeyote yule tena (1Wakorintho 7:23). Sisi sio watumwa wala watumishi wa mtu yeyote tena na hatupaswi kuwafanya wengine kuwa watumwa au watumishi wetu. Tumeamriwa kuwa tusiibe. Tendo la kuwanyang’anya watu uhuru au haki yao ya uzaliwa wa kwanza ni wizi ulio dhahiri, na unafanya mtu aliye mwizi kutokuwa na sehemu kwenye Ufalme wa Mungu. Na tusimame imara kwenye uhuru wetu ambao kwao tumewekwa huru, na kwa utii unatulinda sisi na uhuru wetu, na uhuru wa wengine pia (Wagalatia 5:1).

 

Kushindwa kuafikiana: kwa kupuuzia au kwa makusudi

Kushindwa kuafikiana na kila utaratibu wa kimahakama zinazofanana au kwendana sawa na sheria au amri za Mungu kunaweza kupelekea mtu kuhukumiwa adhabu ya kifo. Kila mtu anatakiwa ahakikishe kuwa sheria zote zinaheshimiwa. Amri ya nane haina udhuru wa kuivunja. Kukosa kushughulikia raslimali ya mwingine ni kupuuzia waraka na nia iliyo kwenye sheria.

Kumbukumbu la Torati 22:1-4 Umwonapo ng'ombe wa nduguyo au kondoo wake akipotea, usijifiche kama usiyemwona; sharti utamrudisha kwa nduguyo. 2 Na kwamba yule nduguyo hayupo karibu nawe, au ukiwa humjui, umchukue kwenu nyumbani kwako, uwe naye hata aje nduguyo kumtafuta, nawe mrudishie. 3 Tena fanya vivyo kwa punda wake; tena fanya vivyo kwa mavazi yake; tena fanya vivyo kwa kila kitu kilichopotea cha nduguyo, kilichompotea ukakiona wewe; usijifiche kama usiyekiona. 4 Umwonapo punda wa nduguyo, au ng'ombe wake, ameanguka kando ya njia, usijifiche kama usiyemwona; sharti umsaidie kumwinua tena.

 

Sambamba na hilo, agizo linabakia katika kuuweka wazi uvunjifu wa sheria (Kumbukumbu la Torati 22:24). Kushindwa kutozuia hili ni kitendo cha kkuchukiza na hata kuwafurahia au kuchukuliana na wale wanaoyatenda hayo (Zaburi 50:18; Warumi 1:32; 1Timotheo 5:22). Iwapo kama kuna mtu anayetafuta kufanya na faida kwa kutumia ushahidi wa uwongo, akumbuke kuwa itakuja kumtokea hata yeye kufanyiwa hivyo, kama alivyofanyiwa yule aliyeshitakiwa kwa mambo ya uwongo (Kumbukumbu la Torati 19:18,19). Tusifiche kutoa ushahidi wa jambo lolote tulionalo au kulijua (Mithali 24:10-12) (pia soma jarida la Torati na Amri ya Tisa (NA. 262) [Law and the Ninth Commandment (No. 262)].

 

Hakuna mtu anayerususiwa kumchukiza au kumfanyia uhalifu mwingine kwa kuvunja mojawapo ya amri hizi (Mithali 28:17; pia soma Luka 10:29-30). Kuficha kitu alichoibiwa mtu kwa hila, ndipo inaashiria kwa mwingine kuwa ni udanganyifu au utapeli, na ni aina mbaya sana ya wizi.

 

Kristo alisema kwamba Mafarusayo walitoa zaka ya jira na mnaanaa, lakini bado walikuwa kwenye hukumu kwa kutokuwa na upendo wa dhati kwa Mungu. Bali walipaswa kuyafanya haya yopte kwa pamoja (Luka 11:42).

 

Sheria za umilikaji wa mali na amri ya nane zina nia ya kumlinda mtu binafsi kwenye jamii yake, na inalinda jamii kutokana na matendo ya mtu binafsi mali sio mwisho wa kila jambo kwa ilivyo yenyewe tu, bali ni kitendea kazi ambacho kinaweza kutumiwa katika kuweka mambo sawa ya watu wetu.

 

Kupata mali kwa mtindo usio wa kufuata njia ya Mungu. Kuipata na kufanya, ili kwamba kila mtu atajirike akiwa hapa duniani kwa kuzivunja sheria zilizoelekezwa kwenye Torati na manabii.

 

Hatima ya uhalifu na hukumu

Kumbukumbu la Torati 24:7 Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwivi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Kwenye maandiko tumeona kwamba tendo la kuteka nyara hukumu yake ni kifo; hata hovyo, kuna dhana pana zaidi kwenye andiko hili linalobeba maana na dhana ya kufanya biashara kila mmoja na mwingine. Kwa hiyo mashirika yale yanayopenda kufanya kazi ya kuandikisha watu na kuwaingiza jeshini na kuwauza wengine mbali na masuala ya mtandao wa kibiashara, wote hawa wanaenda kinyume na maagizo ya Torati hii ya Mungu, na watu wanaohusika kufanya hivyo wanapaswa kutubu. Hakuna mtu anayediriki kuiba au kutwaa fedha kwa kuthamanisha maisha ya mtu mwingine ambaye anaweza kuurithi Ufalme wa Mungu.

 

Sheria ya umilikaji wa mali ni kitu pekee tuwezacho kukiona na kinachoweza kulinganishwa sheria kuu ya kiroho. Kumuibia mtu ni sawa tu na kumuibia Mungu kwa namna nyingine. Kama hatutaweza kuaminiwa kwa kuvitunza vitu tuvionavyo, tutawezaje kuaminiwa kwa mambo ya kiroho? Tunapaswa kutubu na kupendana kila mtu na mwenzake, na kuchukuliana mambo yatupatayo kila mmoja wetu kwa uhuru na usafi au moyo mweupe.

 

q