Makanisa ya Kikristo
ya Mungu
[262]
Torati na Amri ya
(Chapisho
La 2.0 19981011-19990525-20120510-20120822)
Imeandikwa: Usiseme uwongo. Jarida hili linaelezea muundo mzima wa Torati ya Mungu, na jinsi inavyowiana na Amri jinsi zilivyoelezewa na manabii na Maagano yatokanayo na agizo la usomaji wa Torati katika mwaka wa Sabato.
Email: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1998, 1999, 2012 Wade
Cox)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu
Jarida hili linapatikana Ulimwenguni
kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Torati na Amri ya Tisa
Imeandikwa:
Kutoka 20:16 Usimshuhudie jirani yako uongo
Kumbukumbu la Torati 5:20 Wala usimshuhudie jirani yako uongo
Amri ya Tisa inashughulika kumuelezea mwandamu kuwa ni kiumbe wa Mungu na Israeli kama mashahidi wa Mungu, na hawa wote wakiwa ni wawakilishi na mawakala wa Mungu ambaye ndiye aliyeweka na kuiamuru Sheria. Haki au wema (tsedek) wowote vinakubalika kwa kutegemea ushahidi wa kweli na ndiyo maana vitendo vyovyote vya uwongo vinaendana kinyume kabisa na Sheria au Torati ya Mungu. Shetani, ambaye ni mshitaki wetu ndiye baba wa huo uwongo (Yohana 8:44). Mambo yake yako kinyume kabisa na amri zilizo kwenye Sheria na amri za Mungu na hizi zake zimeegama kwenye uwongo tu.
Ushahidi wa Mungu na utaratibu wake
Taifa ni mwendelezo wa mfumo wa Mungu.
Isaya 43:1 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Tumeitwa ili tufanyike kuwa mashahidi wa Mungu aliye Hai, yaani sisi sote, yaani wateule na taifa.
Isaya 43:10 Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine.
Kwa hiyo inatunapasa tuwe ni mashahidi tunaoishuhudia imani ya Mungu.
Umuhimu na ulazima wa sheria kwa ulimwengu wote
Sheria ni jambo linalowahusu watu wote na inawahusu watu wote wanaoishi na walio sehemu ya taifa.
Hesabu 15:13-16 Wote ambao wamezaliwa kwenu watafanya hayo yote kwa kuandama mfano huo, katika kusongeza sadaka kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana. 14 Tena kwamba mgeni amekaa kwenu, au mtu ye yote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye yuataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa Bwana; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo. 15 Katika huo mkutano, kutakuwa na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye pamoja nanyi; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kama ninyi mlivyo, na mgeni atakuwa vivyo mbele za Bwana. 16 Itakuwa sheria moja na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye nanyi.
Sheria inasimama kwa
namna moja, yaani kwa taifa na kwa watu wote. Mwanadamu anaweza kutenda dhambi
iwe ni kwa kutokujua au hata akiwa anajua kabisa
sheria, bali hukumu hufanyika kwa kila mmoja peke yake kwa mujibu wa sheria
hiyohiyo moja.
Hesabu 15:29-30 Mtakuwa na
sheria moja kwa huyo afanyaye neno lo lote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa
kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati
Hukumu hiyohiyo hutolewa kwa wotel.
Kumbukumbu la Torati 10:18-19 Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 19 Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
Utakaso chini ya sheria
Tumekwisha takaswa sote kwa
mujibu wa sheria za Mungu tukiwa
Kumbukumbu la Torati 7:6-11 Kwa maana wewe u taifa
takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako,
amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa
nchi. 7 Bwana hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua
ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache
kuliko watu wote; 8 bali kwa sababu Bwana
anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu,
ndiyo sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya
utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. 9 Basi
jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano
lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu; 10 naye huwalipa wamchukiao mbele ya uso wao, kuwaangamiza.
Hatakuwa mlegevu kwake yeye amchukiaye, atamlipa mbele ya uso wake. 11 Basi zishike amri, na sheria, na hukumu ninazokuamuru
leo, uzitende
Utakaso wetu unatokana na
Agano letu na Mungu kupitia kwa Masihi. Kwa jinsi hii tumejengwa na kuwa watu wakatifu na tulio kwenye familia yake Mungu na
tusio na waa wala kunyanzi (Mambo ya Walawi 19:2; 22:17-25; pia soma jarida la Torati na Amri
ya Tano (Na. 258) [Law and the Fifth Commandment (No. 258)].
Kwa mujibu wa neno la Mungu ambalo ni ushahidi wa
kweli, ndipo tunaongozwa na kweli (Zaburi 119:105)
Maongezi ya utani au mzaha
Kwenye ushuhuda wa Mungu hakutakiwi kufanya mizaha, kwa kuwa kwenye mizaha kuna mazungumzo na ushahidi wa uwongo, na tutatoa hesabu kwa kila neno la lisilo na maana tulilolisema.
Shetani ndiye baba
wa uwongo (Yohana 8:44) na wale wasio wa imani
huwazonga wateule kwa uwongo na chuki na hupingana na sisi bila sababu (Zaburi
109:3). Wale wanaoiacha imani hufanyika kuwa wapiga porojo na
wenye mahangaiko mengi (1Tim. 5:13). “Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake;
(Mithali 11:9)
Mathayo 12:35-37 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na
mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.
36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana,
watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno
Maranyingi tumekuwa tukiwahukumu wengine kabla hatujajihukumu wenyewe na kwenye hukumu ile potofu tunafikia kiasi cha kusema uwongo.
Mathayo 7:1-5 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. 2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. 3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? 4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Tumaini letu linapaswa liwe ni kwa Mungu na kwenye kweli yake, na sio kwenye nguvu zetu sisi wenyewe.
Zaburi 52:1-5 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa
Mungu upo sikuzote. 2 Ulimi wako
watunga madhara,
Tunatakiwa tuongee mambo yaliyo sawa na mafundisho yenye uzima yanavyosema.
Tito 2:1-3 Lakini wewe nena mambo yapasayo
mafundisho yenye uzima; 2 ya kwamba wazee wawe wenye
kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na
katika upendo na katika saburi. 3 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe
wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;
Mashitaka na shutuma zote vinatoka kwa yule muovu, ambaye pia ni
mshitaki wetu. Ufalme wa Mungu wetu unakuja pale
ambapo mshitaki wandugu zetu ametupwa chini. Watakatifu – wale wazishikao amri
za Mungu na “wasioyapenda maisha
Dhana potovu kuhusu uhuru na maisha yasiyozingatia sheria
Uhuru wa mataifa yote ulimwenguni unatokana na sheria za Mungu ambazo ni ushahidi wa kweli. Uhuru usio na sheria ni uhuru mpotovu na uvunjifu wa sheria. Neema na kweli vinatoka kwa Yesu Kristo (Yohana 1:17)….waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu (Yohana 4:23, 24). Ni kweli tu ndiyo itakayotuweka huru (Yohana 8:32).
Ushuhuda dhidi ya mtu na kwa malaika walioasi
Tumetakiwa tufanye mambo yetu katika ukweli, kwa kuwa imeandikwa:
Kumbukumbu la Torati 6:16 Msimjaribu Bwana, Mungu wenu,
Tunapaswa kuishi kwa kila neno litokalo kwenye kinywa cha Mungu.
Mathayo 4:3-10 Mjaribu akamjia akamwambia,
Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya
yawe mikate. 4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu
hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo
katika kinywa cha Mungu. 5 Kisha Ibilisi akamchukua
mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, 6 akamwambia,
Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana
imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije
ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 7 Yesu
akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno,
akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka
kunisujudia. 10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako,
Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu
wako, umwabudu yeye peke yake.
Kristo alimuabudu Mungu na
alimkanusha Shetani kwa neno: “imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu
yeye peke yake.” Iwapo kama Kristo hakuwa na mwingine
wa kumuabudu ila Mungu peke yake, basi tutawezaje kuwa ni mashahidi iwapo
Kumjaribu Mungu
Uwongo wa kwanza aliutoa Shetani na kumuongopea Hawa na uwongo ule ulikuwa ni kuhusu dhana ya maisha ya umilele ambao alisema: “Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, (Mwanzo 3:4).
Mwanzo 3:4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika
hamtakufa,
Na kwa ushahidi huo wa uwongo wakajikuta wote wawili wakijaribu Mungu na wote wawili yaani mwanamke na huyu Aliyejifanywa kuwa Kerubi (yaani Shetani) ndpo wakajikuta wanahukumiwa kifo (Mwanzo 3:1-24; Isaya 14:12; Ezekieli 28:1-19).
Tunatakiwa pia
kuchagua mtu ambaye tunajifunza mafundisho yake au kujifunza kweli kwake, kama tulivyoelekezwa na maandiko tutofanya kuwa “Msiwape
mbwa kilicho kitakatifu, wala mtupe lulu zenu kwa nguruwe,” Kristo alinena kwa
kutumia mifano
Tunamwabudu Mungu kwa kweli na uwazi wa kuongea ama kushuhudia. Maombi yetu
hayapaswi kuwa
Mathayo 6:5-8 Tena msalipo, msiwe
Mungu anatusik8ia sisi kwa kuomba kwetu kimyakimya na kusema kwa wazi na sio kwa mtindo wa kupayuka payuka ambao ulikuwa ikifanywa na desturi za makuhani wa Baali (1Wafalme 18:28). Tunakuwa mashahidi wake Mungu kwa njia ya matendo yetu kwa jinsi tunavyofuata na kuzitenda amri na sheria zake (Zaburi 2:1,2).
Unabii wa uwongo
Unabii wa uwongo utaondolewa atakaporudi Masihi. Na manabii wake waliokuwa wanatabiri wataangamizwa katika kipindi hiki cha kuhumu ambacho kitafuatiwa na kipindi cha milenia na ufufuo wa pili wa wafu.
Kumbukumbu la Torati 18:15 Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii
miongoni mwa ndugu zako
Nabii aliyetajwa kwenye kumbukumbu la Torati 18:15 alikuwa ni huyu Masihi ambaye neno lake ni la kweli, na nabii yule aliyetajwa kuthubutu kulitaja jina la Bwana visivyostahili na hakuagizwa, “nabii yule hakika atauawa.” Kwa hiyo, manabii hawa wote watauawa na kuingia kwenye kundi la watakaohukumiwa kwenye ufufuo wa pili wa wafu.
Kumbukumbu la Torati 18:20-22 Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. 21 Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana? 22 Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope
Iwapo kama tutamgundua nabii kuwa ni wa ueongo, hatopaswi kumuogopa, kwa kuwa Mungu atamshughulikia. Nabii hawezi kuzuiwa kuifanya kazi yake hadi pale Mungu atakapoona kuwa imekwisha.
Yeremia 11:21-23 Basi, kwa hiyo, Bwana asema hivi,
juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa
jina la Bwana, usije ukafa kwa mkono wetu. 22 Kwa
sababu hiyo Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaadhibu watu hawa; vijana
watakufa kwa upanga; wana wao na binti zao watakufa kwa njaa; 23 wala hapatakuwa na mtu atakayesalia kwao; maana nitaleta
mabaya juu ya watu wa Anathothi, mwaka wa kujiliwa kwao.
Ishara au alama ya kumjua nabii wa kweli ni kwa vile anavyokuwa mwaminifu kwenye utunzaji na kufundishaji wa Sheria na amri za Mungu (Yeremia 23:9-40). Nabii mkuu kuliko wote alifanya miujiza kwa nguvu na uweza wa Bwana Mungu, kwa kuwa dunia yote ni mali ya Bwana Mungu ili ayafanye na kuyaonyesha mapenzi yake, na anakaribia kumponda kichwa Shetani na kumseta chini ya miguu yetu (Kutoka 9:29; Kumbukumbu la Torati 10:14; Warumi 16:20).
Manabii hawahawa
Ushuhuda wa Mungu kwa
kupitia mabanii na Masihi
Mungu alinena kupitia manabii tangu siku za mababa na kuendelea. Na hafanyi kitu chochote pasipo kwana kuwafunulia watumishi wake manabii.
2Wafalme 17:23 hata Bwana akawaondoa Waisraeli wasiwe mbele zake,
(sawa na Amosi 3:7}
Na ndivyo Mungu alivyoongea na Yuda kupitia kwa Masihi. Kuhani mkuu alirarua nguo zake na kusema “Je, tunataka nini zaidi ya kuwa mashahidi?” Ingawa
hakuwa ameelewa kikamilifu maana ya kitendo alichokuwa anakifanya na kusema. Na kisha wakamhukumu Yoshua na
Masihi hukumu ya kifo (Marko 14:63). Alikuwa ni
shahidi mwaaminifu na mfalme wa wafalme wa duniani, na mwanzo wa uumbaji wa (Ufunuo
1:5-6; 3:14). Unabii kuhusu kurudi kwa Masihi umekuwa
ukitolewa kwa kipindi kirefu
Kumbukumbu la Torati 18:16-19
Masihi alimshuhudia Baba
yake aliye mbinguni. Hatumwiti mtu baba hapa
duniani kwa kuwa tuna Baba mmoja tu aliyeko mbinguni (Mathayo 6:9; 23:9). Wala hakuna
aliyewahi kumuona Mungu, basin a umtumikie yeye aliyewahi kuwa na Mungu. Kwa kupitia ushuhuda wa
Kristo, yeye aliyezaliwa elohimu peke yake, na yule ambaye Baba alitufunua sisi
(Mathayo 11:27; Yohana 1:18; 6:46; 10:15). Iwapo kama
tutazifanya kazi za Mungu ndipo tutakuwa mashahidi wa kweli na tunaweza kuaminiwa (Yohana 10:34-38). “Amwaminiye
Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona
uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.” (Yohana 3:36). “Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na
Mwana awahuisha wale awatakao.” (Yohana 5:21).
Hili ndilo lengo la kumshuhudia Masihi, alikuja kumdhihirisha Baba. Kwa hiyo inafuatiwa, shahidi wa kweli anabakia kwenye imani.
Ushahidi wa uwongo kwenye jamii zetu
Ushuhuda wa uwongo na ulimi wa uwongo
Mungu anauchukia ushuhuda wa uwongo na ulimi wa uwongo, na haya yamesababisha magomvi na matengano yatokee kati ya ndugu hata miongoni mwa waaminio.
Mithali 6:16-19 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. 17 Macho
ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; 18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo
myepesi kukimbilia maovu; 19 Shahidi wa
uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
Mithali 12:22 Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana;
Mithali 19:5 Shahidi wa
uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka.
Hukumu kwa ajili ya kumdanganya Roho Mtakatofu ni kifo, na wakati mwingine inatokea happhapo na kwa mara moja na kwa dhahiri.
Matendo 5:3-5 Petro akasema, Anania, kwa
nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa
siri sehemu ya thamani ya kiwanja? 4 Kilipokuwa kwako,
hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa
katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia
uongo mwanadamu, bali Mungu. 5 Anania aliposikia
maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia
haya.
Mtume Paulo alituambia tusijidanyanye kwa kudhani tumeuvua utu wa kale na matendo yake (Wakolosai 3:9)
Kristo aliwashangaa
Wayahudi wenzake kwa kutaka kwao kumuua. Walitaka
kumuua kwa kuwa neno
Kristo ameitwa mwaminifu na mkweli kwa kuwa ni mwaminifu na mkweli. Anapanga vita kwa haki na kwa kweli (Ufunuo 19:11).
1Wafalme 22:18-28 ni kifungu cha maandiko kinachoshangaza, inapoonekana kuwa Mungu aliiagiza na kuielekeza roho ya uwongo iingie kwenye vinywa vya manabii. Jibu linalotolewa kwa tukio lile ni kumfanya mfalme aelewe kwamba manabii wa Israeli walikuwa wamepewa roho wa udanganyifu. Wakamdanganya mfalme na nabii wa kweli akaonekana kuwa ndiye nabii wa uwongo. Unabii ulikuwa unasema: “Nenda [Ramothi-Gileadi] kwa kuwa Yahova ataiokoa nchi hii ya mfalme” (1Wafalme 22:6). Tatizo lilikuwa ni kwamba mji huu ulikuwa unakwenda kukombolewa kutoka kwenye mikono ya mfalme wa Ashuru, na sio kwa mfalme wa Israeli.
Hata hivyo, Mungu alikuwa amempeleka nabii wake wa kweli Mikaya, na alipoulizwa aseme kweli alisema hiyo kweli (1Wafalme 22:19-23). Kitendo cha kuomba maelekezo pasipo kuzifuat sheria na amri za Mungu ni machukizo na kinakaribisha maafa. Kwenye andiko hili tunajionea kwamba Mungu anaijaribu roho pia kwa kupitia jambo hili.
Mapokeao kama
ushuhuda wa uwongo
Kristo aliyakemea
Mathayo 15:1-14 inasema: Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema, 2 Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa
maana hawanawi mikono walapo chakula. 3 Akajibu,
akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa
ajili ya mapokeo yenu? 4 Kwa kuwa Mungu alisema,
Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba
yake au mama yake kufa na afe. 5
Mafarisayo
na Waandishi walilifanya neno la Mungu lionekane kuwa
sio la muhimu kwa ajili ya mapokeo
Kutoka 1:17-21 Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu,
wasifanye
Ulinzi wa watu wote unategemea na jinsi wanavyomcha Mungu. Wale walioitwa na kuchaguliwa wanafanyika wote kuwa ni nyumba au vyumba kwenye Hekalu la Mungu wetu.
Mambo ya Walawi 19:14; 17-18 Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele
ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi Bwana. 17 Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea
jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. 18 Usifanye
kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani
yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana
Mfumo mzima wa haki umewekwa kwa kufuata kweli na pasipo kuwaogopa au kuwapendelea watu, nah ii ahaimaanishi kuwa kwenye ujinga.
Haitakiwi kuweka upendeleo kwa watu fulani inapotolewa hukumu (cf. Kumbukumbu la Torati 1:17).
Shahidi wa kweli anatakiwa atathminiwe na watu wa Mungu kwa kila jambo maishani mwake. Kunatakiwa kusiwe na shahidi wa uwongo kwa jambo lolote lihusulo utendaji kazi wake, wala kwa maongozi yake, au kwenye haki, au kwenye biashara kwenye matumizi ya mzani, au vipimo, au nakala.
Mambo ya Walawi 19:35-36 Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. 36 Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri.
Udanganyifu
Kudanganya (au uzushi) ni
wizi
Kwa tabia hii ya kudanganya au uzushi
tunaiba tabia ya mwingine na kwa hiyo tunawaua. Maisha
Waongo na wazushi wamekataliwa na Mungu.
Yeremia 6:27-30 Nimekuweka uwe mnara na ngome kati ya watu
wangu; upate kuijua njia
Mungu anatuonyesha matokeo ya mwisho ya uvunjaji huu wa sheria kupitia kwa nabii Yeremia.
Yeremia 9:1-6 Laiti kichwa changu kingekuwa
maji, na macho yangu kuwa chemchemi ya machozi, ili
nipate kulia mchana na usiku kwa ajili
Ushahidi wa uwongo unawazuia watu wasimjue Mungu. Watu wanabeba silaha ili wakamwage damu (Ezekieli 22:9).
Kutoka 23:6-7Usipotoe hukumu ya mtu maskini katika neno
lake. 7 Jitenge mbali na neno uongo; wala wasio hatia na wenye
haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu
Haki na isipimwe kwa kuangalia idadi au utajiri. Ukweli usipingwe au kukanushwa kwa kufuata mtazamo wa watu wengi.
Mambo ya Walawi 19:16 Usiende huko na huko
katikati ya watu wako,
Usengenyaji au utesi unaua watu na unaharibu familia. Ni ishara na alama ya taifa lisilo na maadili mema.
Uwongo na udanganifu kwenye familia
Mwamaume anayejisingizia kuwa ni msafi na
hajawahi kulala na mwanamke na kufanya ngono akimdanganya hivyo mkewake,
anabidi afanyiwe uchunguzi na wazee wa mji ule, sawa na anavyofanyiwa mwanamke
mjinga asiyeiheshimu ndoa yake (soma Kumbukumbu la Torati 22:13-21; na majarida
ya Torati na
Amri ya Tano (Na. 258) na Torati na Amri ya Saba (Na. 260) [Law
and the Fifth Commandment (No. 258) and Law and the Seventh Commandment (No. 260)].
Wanaume wote wanapaswa kuwapenda wake zao
Tabia ya udanganyifu kwenye familia ni jambo lililokatazwa kabisa.
Zaburi 50:19-20 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila. 20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia.
Ugndanganyifu
unapofanana na wizi
Tumejionea kwamba tabia ya udanganyifu inaiba tabia ya mtu mwingine. Tunatakiwa kuuvua utu wa kale na kuuvaa utu upya, ambavyo ni kuzifanya upya nia yetu iliyo sawa na taswira ya Mungu (Wakolosai 3:9-10).
Wakolosai 3:9-10 Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa
utu wa kale, pamoja na matendo yake;
10 mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu
sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba
Mtu mpya ni Roho Mtakatifu katika Yesu Kristo, ambaye ni “mfano wake
yeye aliyemuumba.” Hii ni mojawapo ya nukuu rasmi tatu
(soma Waebrania 3:2; Ufunuo 3:14) kwa kulinganisha na uumbaji wa Masihi na ni
mmoja tu peke yake ambaye hajawahi kukasirika
Inampaswa kila mtu achukie na kuiacha tabia ya udanganyifu na badala yake aanze kusema kweli kwa jirani yake (Waefeso 4:25; sawa na Mithali 11:9). Tunaonywa hivi:
Waefeso 4:29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia
Tito 3:1-3 Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa
kila kazi njema; 2 wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi,
wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. 3 Maana
hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa,
huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na
husuda, tukichukiza na kuchukiana.
Inatupasa kuziheshimu sheria na tusimnene mabaya mtu yeyote.
Yakobo 4:11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
Tusijihukumu wenyewe na kujidhania wajinga kwa kuzitumia ndimi zetu wenyewe.
Mithali 10:18 Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo, Na yeye asingiziaye ni mpumbavu.
Mungu amesema kile atakachowafanyia wadanganyifu na wenye kujivuna.
Zaburi 101:5 Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamharibu. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitavumilia naye.
Sehemu ya II
Mfumo wa Haki
Misingi ya sheria za
asili
Mambo ya Walawi 24:22 Mtakuwa na sheria moja tu, kwa huyo aliye mgeni, na kwa mzalia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Kanuni za haki za asili zinamtaka kila mtu aijue sheria zilezile. Kila mtu anapswa kujua mashitaka yaliyo dhidi yake kwa kwandishi na anapaswa kupewa fursa kujua anachotakiwa kufanya. Mtuhumiwa au mdaiwa anatakiwa kupewa usikivu wa haki na asiwe na aina yoyote ya shinikizo, na hukumu yake iwe ya haki na sio ya kupindisha au ya kumpendelea mtu.
Kwa sababu hii ndiyo maana Mungu ametupatia sheria zake kwenye maandiko
na mashitaka yanayofanywa dhidi yetu yanafanywa na
manabii na yamewekwa kwenye maandiko. Tumepewa muda wa
kutafakari mashitaka, na Mungu hafanyi haraka kutoa hukumu akikusudia kwamba
asiwepo mtu wa kupotea. Utaratibu huo huo wa kisheria
ulioko kwenye jamii yetu na ambao unafanya kazi zhini ya sheria au Torati ya
Mungu, pamoja na aunzishwaji wa mahakama yanayofanya kazi kwa niaba ya Mungu mwenyewe.
Tumepewa namna nyingi za majaribu ambayo kwayo tunajaribiwa imani zetu. Wateule wako hukumuni sasa na hukumu inaanza kwenye myumba ya Mungu.
1Petro 4:17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?
Sehemu nyingine yote iliyobakia ya dunia haitahukumiwa sasa hadi kwenye ufufuo wa pili wa wafu, wakati watu wote watakapokuwa wamefufuka, na kisha kurekebishwa kwenye hukumu na kupewa fursa ya kuokolewa (Ufunuo 20:4-15).
Kutenda jambo kwa kuamrishwa na mwingine
Ni uvunjifu wa sheria asilia ya haki na Amri ya Mungu kuitendea kazi amri ya mtu mwingine kwa niaba ya mtu mwingine. Kristo alitekeleza hukumu kwa namna alivyokuwa amepewa mamlaka na Mungu. Hakuja hapa ulimwenguni kuhukumu bali kuja kuufundisha ulimwengu jinsi unavyopasa kuhukumu. Wale waliompokea na kumkubali na kuwa sehemu ya Nyumba ya Mungu wangehukumiwa tangia hapo hadi sasa na ufufuo wa kwanza wa wafu (1Petro 4:17). Wale ambao hawakumpokea watahukumiwa katika siku za mwisho, kwa ajili hii ambayo inamaanisha ufufuo wa pili wa wafu uliotajwa kwenye Ufunuo 20:11-15.
Yohana 12:46-48 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi
asikae gizani. 47 Na mtu akiyasikia maneno yangu,
asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu
ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. 48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno
Masihi hakutumwa ili auhukumu ulimwengu, bali alitumwa ili auokoe. Siku za meisho ni kipindi cha miaka elfu tangu Marejeo ya Masihi na ufufuo wa pili wa wafu mwishoni mwa kipindi cha Milenia (soma Ufunuo 20:1-14; pia tazama jarida la Siku ya Bwana na Siku za Mwisho [The Day of the Lord and the Last Days (No. 192)].
Kujaribiwa kwa mateso
Bwana ameanzisha utaratibu wa aina hiyohiyo wa kujaribiwa kwa mateso makali kwa sababu fulani maalumu za kisaikolojia kwenye nchi. Mambo haya yote yamefanywa ili kulinda familia isitatizwe.
Hesabu 5:11-31 inasema: Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 12 Nena na wana wa israeli, uwaambie, kama mke wa mtu ye
yote akikengeuka, na kumkosa mumewe, 13 na mtu mume akalala
naye kwa uasherati, na jambo hilo likamfichamania mumewe, likawa jambo
lisilojulikana, na huyo mwanamke akawa najisi, wala hapana shahidi
aliyeshuhudia juu yake, wala hakufumaniwa; 14 kisha
mumewe akashikwa na roho ya wivu, akamwonea wivu mkewe, naye akawa najisi huyo
mwanamke; au kama akiingiwa na roho ya wivu, akamwonea wivu mkewe, naye hakuwa
na unajisi huyo mke; 15 ndipo huyo mume
atamchukua mkewe, aende naye kwa kuhani, naye ataleta sadaka yake kwa ajili
yake, yaani, sehemu ya kumi ya efa ya unga wa shayiri; asitie mafuta juu yake,
wala asitie ubani juu yake; maana, ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga
ya ukumbusho ya kukumbukia uovu. 16 Basi kuhani atamleta
mwanamke akaribie, na kumweka mbele za Bwana; 17 kisha
kuhani atatwaa maji matakatifu katika chombo cha udongo; kisha kuhani atatwaa
katika vumbi lililo pale chini ya maskani, na kulitia katika hayo maji; 18 kisha kuhani atamweka mwanamke mbele za Bwana, naye
atazifungua nywele za kichwani mwa huyo mwanamke, kisha atampa hiyo sadaka ya
unga ya ukumbusho mikononi mwake, ambayo ni sadaka ya unga ya wivu, naye kuhani
atakuwa na hayo maji ya uchungu yaletayo laana mkononi mwake; 19 tena kuhani atamwapisha huyo mwanamke, naye atamwambia
mwanamke, Kwamba hakulala mtu mume pamoja nawe, tena kwamba hukukengeuka
kuandama uchafu, uli chini ya mumeo, maji haya ya uchungu yaletayo laana
yasikudhuru;
20 lakini kwamba umekengeuka uli chini ya mumeo, na kwamba
u hali ya unajisi, na mtu mume amelala nawe, asiyekuwa mumeo; 21 hapo ndipo kuhani atamwapisha mwanamke kwa kiapo cha
kuapiza, kisha kuhani atamwambia huyo mwanamke maneno haya, Bwana na akufanye
wewe uwe laana na kiapo kati ya watu wako, hapo Bwana akufanyapo paja lako
kupooza, na tumbo lako kuvimba; 22 na maji yaletayo
laana yatakuingia matumboni mwako, na kukuvimbisha tumbo, na kukupoozesha paja
lako; na mwanamke ataitika, Amina, Amina. 23 Kisha
kuhani ataziandika laana hizo ndani ya kitabu, na kuzifuta katika maji ya
uchungu; 24 kisha atamnywesha mwanamke hayo maji ya
uchungu yaletayo laana; nayo maji yaletayo laana yataingia ndani yake, nayo
yatageuka kuwa uchungu. 25 Kisha kuhani
ataitwaa hiyo sadaka ya unga ya wivu, kwa kuiondoa mkononi mwa huyo mwanamke,
naye ataitikisa sadaka ya unga mbele ya Bwana, na kuisongeza pale madhabahuni; 26 kisha kuhani atatwaa konzi moja ya sadaka ya unga, kuwa
ni ukumbusho wake, na kuuteketeza madhabahuni, baadaye atamnywesha mwanamke
hayo maji. 27 Kisha hapo atakapokwisha kumnywesha maji,
ndipo itakapokuwa, kama amekuwa hali ya unajisi na kumkosa mumewe, hayo maji
yaletayo laana yatamwingia ndani yake, nayo yatakuwa uchungu, na tumbo lake
litavimba, na paja lake litapooza; na huyo mwanamke atakuwa laana kati ya watu
wake. 28 Na kama mwanamke hakuwa na unajisi lakini
yu safi; ndipo ataachiliwa, naye atazaa wana. 29 Hii
ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na
kupata unajisi; 30 au, roho ya wivu ikimwingia mtu mume,
naye akamwonea wivu mkewe; ndipo atakapomweka huyo mwanamke mbele za Bwana, na
kuhani atatenda juu yake sheria hii yote. 31 Na
huyo mume atakuwa hana uovu, na mwanamke atauchukua uovu wake.
Sheria hizi ni kwa
ajili ya kuzilinda familia na kila mtu kutokana na vishawishi au matamanio ya
watu walio kwenye nyumba husika. Tunajionea
Tabia ya udanganyifu au
uzushi na uvuruga nyumba vinatozwa faini na hairuhusiwi kuchukuliwa kuwa ni
jambo linalostahili kuwaachanisha watu kwa kipindi hicho na kwa siku za mbele,
hata kama uamuzi huu wa kuachana utaonekana kama unafaa au watu wanaupendelea
kwa kigezo cha kuwepo wa ushahidi wa dhahiri. Shahidi wa
uwongo kwenye suala la lonaloathiri ushuhuda au sifanjema ya mtu kwa siku za
usoni ndvyo ilivyo pia kwa suala la uaminifu wa mwanamke aliyeolewa.
Eheria hii inayohusika na ushahidi
wa uwongo ina namna nyingi
Torati au sheria ya Mungu ni ushuhuda kwa ulimweng.
Warumi 3:9-23 inasema: Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo.
Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani
ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi; 10
Hakuna mtu anayehesabiwa haki kwa sheria, bali ni kwa ushuhuda wa Totati na manabii na ndipo Mungu anaonekana kuwa ni mwenye haki. Uumbaji wenyewe unaonekana kwa ni jaribu lenye mateso, na wote wametenda dhambi na wote wamepugukiwa na utukufu wa Mungu.
Kuanzishwa kwa mfumo au utaratibu wa kimahama na mahakimu au waamuzi
Mamlaka yote yamewekwa na
Mungu. Maamuzi yote yanapaswa yafanyike kwa kulingana
na maagizo ya Torati ya Mungu
Sheria zinatendakazi kwa kufuata sheria zilizo kwenye biblia zinapaswa zisiwadhuru
watu wengine. Sheria ndogondogo zinapaswa zianzishwe ili
itimiwe na jamii kama udhibiti umefanyika kwenye taifa
Hakuna kinachoweza kuongezwa kwenye Ushuhuda au kuondolewa kutoka na vile ilivyo. (soma Ufunuo 22:18-19). Maana ya andiko hili imefungwa hadi kwenye nyakati za mwisho na sasa Roho Mtakatifu anaoweka wazi kwa wale watakao msikiliza. Hakuna sheria itakayoenda kinyume au kupunguzwa maana yake kwa ajili ya dhana hii ya uhuru na utaratibu uliowekwa kwenye hii Torati ya Mungu.
Sheria za dunia hii zinaweza kupingana na sheria zilizo kwenye Torati ya Mungu
Hakuna taifa linalopitisha sheria ambayo uwepo wake unaenda kinyume au unapingana na Torati ya Mungu. Wala hakuna kikundi kinachoanzisha mapokeo yanayogeuza au kubadili au kupuinguzia nguvu zake Torati ya Mungu. Hali kadhalika, hakuna Kanisa linaloweza kuipitisha sheria ambayo inaibadili au kuigeuza Torati ya Mungu au Kalenda yake ambayo kiini chake ni mpangilio wa kimbingu na maelekezo ya Biblia. Kanisa kuu la Kikristo la kidunia limekuwa likiwaua watu kinyume kabisa cha sheria hasa wale waliokataa au kupinga kuyatii mapokeo na maamrisho haya yaliyotungwa na kuwekwa na wanadamu na yaliyo kinyume na maandiko ya Torati ya Mungu, kuliko hata mfumo au dini yoyote ile hapa duniani. Kwa kweli wamelewa kwa damu za watakatifu na wafia dini (Ufunuo 17:4-6).
Matendo 5:29 Petro na mitume wakajibu,
wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
Mahakumu na
wajibu wao
Kungu ameanzisha utaratibu wa mahakimu au waamuzi kwenye sheria (Kutoka 18:13-26). Umuhimu wa mahakimu umeandikwa na kuelezewa kwenye kumbukumbu la Torati 16:18.
Kumbukumbu la Torati 16:18 Weka waamuzi na maakida katika malango yako yote akupayo Bwana, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki.
Torati ilitolewa na kukabidhiwa wazee sabini wa Israeli ambao walipewa majukumu na uelewa wa Roho Mtakatifu wa Bwana.
Hesabu 11:16-17 Kisha Bwana akamwambia Musa,
Nikusanyie watu sabini, miongoni mwa wazee wa israeli,
ambao wewe wawajua kuwa ndio wazee wa watu hawa, na maakida juu
Jukumu la watu
hawa lilikuwa ni kwenye umahiri wao wa kuitafsiri Torati,
kazi ambayo walipewa watafsiri, Kuhani Mkuu na baraza la Wazee wa Israeli. Tangia
hapo, waamuzi waliwekwa kwenye miji yote ya Israeli katika makabila
2Mambo ya Nyakati 19:1-7 Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi Yerusalemu nyumbani kwake kwa amani. 2 Yehu mwana wa Hanani mwonaji
akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia
waovu, na kuwapenda wamchukiao Bwana? Kwa ajili ya
hayo ghadhabu i juu yako itokayo kwa Bwana. 3 Walakini yameonekana mema ndani yako, kwa
kuwa umeyaondoa maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu. 4 Na Yehoshafati akakaa Yerusalemu; akatoka tena kwenda kati
ya watu toka Beer-sheba mpaka milima ya Efraimu, akawarudisha kwa Bwana, Mungu wa baba zao. 5 Akasimamisha
makadhi katika nchi, katikati ya miji yote yenye maboma ya Yuda, mji kwa mji; 6 akawaambia hao makadhi, Angalieni myafanyayo; kwa kuwa
hammfanyii mwanadamu hukumu, ila Bwana; naye yupo pamoja nanyi katika neno la
hukumu. 7 Basi sasa hofu ya Bwana na
iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa Bwana, Mungu wetu, hapana
uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.
Bwana yu pamoja na waamuzi wa Israeli na hakukutakiwa kuwa na upendeleo wa aina yoyote miongoni mwa watu au kupokea zawadi au kupokea rushwa nah ii ilikuwa sio kwa kuwaogopa wanadamu, bali ni kwa kumuogopa Mungu. Jambi hili limeagizwa kwenye Torati .
Kutoka 23:8 Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki.
Mambo ya Walawi 19:15 Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee
mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali
utamhukumu jirani yako kwa haki.
Kumbukumbu la Torati 24:17-18 Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala
ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;
18 bali kumbuka ya kuwa
ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo
nakuamuru kutenda neno hili.
Waamuzi waliwekwa
Kutoka 18:22-27 nao wawaamue watu hawa
sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo
wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao
watauchukua huo mzigo pamoja nawe. 23 Kwamba utafanya
jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza
kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani. 24 Basi Musa akasikiza neno la mkwewe,
akayafanya yote aliyokuwa amemwambia. 25 Musa
akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya
watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa
hamsini, na wakuu wa kumi. 26 Nao
wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno
dogo wakaliamua wenyewe. 27 Kisha Musa akaagana
na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake
mwenyewe.
Musa ndiye aliyehusika kuwachagua waamuzi watakaowahukumu Israeli.
Kumbukumbu la Torati 1:12-17 Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu,
na mzigo wenu, na mateto yenu? 13 Jitwalieni watu
wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya kabila zenu, nami
nitawafanya wawe vichwa juu yenu. 14 Nanyi mkanijibu,
mkaniambia, Jambo ulilonena ni jema la kufanya. 15 Basi
nikatwaa vichwa vya kabila zenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe
vichwa juu yenu, maakida ya elfu elfu, na maakida ya mia mia, na maakida ya
hamsini hamsini, na maakida ya kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya kabila
zenu. 16 Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu,
nikawaambia, Sikizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya
mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye. 17 Msitazame
nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso
wa mtu awaye yote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo
mniletee mimi, nami nitalisikiza.
Hata hivyo, Israeli walikuwa na matatizo ya kiimani, hata walipokuwa chini ya waamuzi.
Waamuzi walipaswa kuilinda utu, siri na heshima ya mtu, kwa namna zote mbili, yaani kwa kipindi cha mchakato wa kushughulikia hatia ya mtu hadi huku yake.
Kumbukumbu la Torati 25:1-3 Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu; 2 na iwe, ikimpasa kupigwa yule mwovu, alazwe chini na mwamuzi, na kupigwa mbele ya uso wake, kwa kadiri ya uovu wake, kwa kuhesabu. 3 Aweza kumpiga fimbo arobaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako, azidishapo kwa kumpiga fimbo nyingi juu ya hizi.
Sheria inataka kuweko na
upepelezi wa kina kuchunguza makosa ya mtu na kupata uthibitisho au kithibiti,
Kumbukumbu la Torati 21:1-9 Aonekanapo mtu ameuawa katika nchi akupayo
Bwana, Mungu wako, kuimiliki, amelala kondeni, wala haijulikani ni nani
aliyempiga; 2 na watoke nje wazee wako na waamuzi wako,
nao wapime hapo mpaka miji iliyomzunguka huyo aliyeuawa; 3 na
iwe, mji ulio karibu na yule aliyeuawa, wale wazee wake mji huo watwae mtamba
katika kundi la ng'ombe, ambaye hajafanya kazi, wala hajakokota jembe la nira; 4 wazee wa mji huo na wamshushe yule mtamba mpaka bonde
lenye maji ya mtoni, lisilolimwa wala kupandwa, wakamvunje yule mtamba shingo
yake humo bondeni; 5 nao makuhani wana wa
Lawi wasongee karibu, kwa kuwa ndio aliowachagua Bwana, Mungu wako, wamtumikie,
na kubariki katika jina la Bwana na kila neno lishindaniwalo, na kila pigo,
litakuwa kwa kufuata maneno yao; 6 na wazee wote wa mji
ule, ulio karibu sana na yule aliyeuawa, na waoshe mikono yao juu ya huyo
mtamba aliyevunjwa shingo yake humo bondeni; 7 na
wajibizane kwamba, Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuiona.
8 Ee Bwana, samehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala
usiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu
utasamehewa kwao. 9 Ndivyo utakavyoondoa
damu ya asiye makosa katikati yako, utakapofanya yaliyo sawa machoni pa Bwana.
Kwenye
tukio hili kuna tuhumu ya makosa ya kubambikizwa kati ya pande mbili
yaliyongojelewa huhukumiwa. Makosa ya
kubambikiwa ni mwiba mkubwa katika utoaji haki
inayoendeshwa kwa mujibu wa Torati ya Mungu na hasa inapotokea kwamba watu wote
wana makosa mbele ya sheria (soma jarida la .Torati na Amri ya
Sita (Na. 259) [Law and the Sixth Commandment (No. 259)].
Hata mshitaki wetu ambaye ni Ibilisi alitiwa hatiani mbele ya wakuu wa baraza kipindi ambacho Kristo alikuwa jangwani. Ni kwa damu ya Kristo ndiyo uliyotuondolea hatia yetu na kutuokoa na mauti na kutufanya tusamehewe kutoka kwenye kazi zetu mbovu na kustahili tumtumikie Mungu aliye Hai (Waebrania 9:13-14).
Wakati huhuku inapokuwa imetokewa na ushahidi kutolewa na ndipo fedha zote zinaweza kulipwa ili kufidia uhai uliopotezwa.
Kutoka 21:30-32 Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa
ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa. 31 Akiwa
ng'ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au
akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa
Samweli akiwa ni mwamuzi
mkuu
Samweli alianzisha utaratibu wa kufanya kazi hii kwa kuzunguka kwenye maeneo yote ya
Israeli na kwa hiyo inaruhusiwa kuweka mahakama za muda na kuhama
1Samweli 7:16-17 Naye huenda mwaka kwa mwaka
kuzunguka mpaka Betheli, na Gilgali, na Mispa; akawaamua Israeli mahali hapo
pote. 17 Na kurudi kwake kulikuwa mpaka Rama; maana
ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Israeli; na
huko akamjengea Bwana madhabahu.
Hukumu ilikuwa ni
juu ya viongozi wa Israeli
2Mambo ya Nyakati 6:23 basi, usikie mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumwa wako; ukimlipiza mwovu, kumpatilizia njia yake kichwani; ukamfanyie haki mwenye haki, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake.
Watu wote waliofanywa kuwa ni watumishi wanapaswa wakutwe wakiwa ni waaminifu.
1Wakorintho 4:2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa
mwaminifu.
Klwa hiyo, ni kwa yule mtarajiwa tu miongoni mwa wawakilishi kwa mamlaka juu ya mashitaka magumu na wajibu wake.
Mahakama na mchakato wake
Inafuatia na uwekaji wa waamuzi ambapo mahakama na mchakato zinapaswa pia ziamuliwe chini ya mamlaka iliyo chini ya sheria. Mchakato wa uchunguzi na upelelezi vinabidi kufanyika na kutolewa matokeo yake (soma Kumbukumbu la Torati. 21:1-9 above).
Mambo yote
yanayotakiwa kusuluhishwa kati ya pande zote kwanza na
yapelekwe mahakamani tu iwapo
Mathayo 18:15-16 Na ndugu yako akikukosa,
enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia,
umempata nduguyo. 16 La,
Masuala magumu na yenye utata yanapaswa yapelekwe kwenye mahakama za juu. (cf. Kumbukumbu la Torati 17:8-11).
Wazee wa mji wanapaswa kuweka mahakama ya haki, ambazo zitachukuliwa ziwemo kwenye malango ya miji, ambazo hapo kale wazee waliketi na kutoa hukumu (Kumbukumbu la Torati 21:19; 22:15; 25:7; Amosi 5:12,15; Zekaria 8:16).
Mahakama yenye mamlaka ya Kuhukumu iliyoanzishwa na Sulemani ilitengenezwa kwa miti aina ya mkangazi au mshitana kiti cha kuhukumia kiliwekwa kwenye baraza iliyonakshiwa kwa mti wa mshita. Hii ilikuwa ni mbali na nyumba ya mfalme ambayo ilikuwa na baraza nyingine ndani ya baraza ya hukumu, ambayo ilikuwa sawa na ujenzi wa zile zingine (1Wafalme 7:7).
Mambo yote yanayolalamikiwa yanatakiwa wapunguzwe kwa maandishi (sawa na Ayubu 31:35)
Utaratibu wa mahakama
yanapaswa yashughulikiwe kikamilifu na kwa heshima,
Mungu atamuondoa Roho
wake Mtakatifu aliyekuwa akimtia nguvu Masihi na
atawapa waamuzi na watawala wa Israeli sawasawa na maombi
1Wafalme 3:5-15 Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku;
Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe. 6 Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu
fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na
katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana
umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo. 7 Na
sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi
mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi
inipasavyo kutoka wala kuingia. 8 Na mtumwa wako yu
katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala
kufahamiwa idadi
Hata Sulemani alianguka mbali na neema baada ya kupewa hekima yake yote na uweza, na kuruhusiwa kulijenga Hekalu. Na ndivyo ilivyo kwamba hata wateule wanaweza kupoteza nafasi zao kwenye ufufuo wa kwanza wa wafu kwa ajili ya ibada za sanamu au uvunjaji wa Roho ya Torati.
Ushahidi
Kuna utaratibu wa kukusanyika na kutathmini ushahidi ulioanzishwa (sawa na Kumbukumbu la Torati 19:3-13).
Hakuna mtu aliyeruhusiwa kuuawa kwa ushahidi wa mtu mmoja tu.
Hesabu 35:30 Mtu awaye yote atakayemwua mtu, huyo mwuaji atauawa kwa vinywa vya mashahidi; lakini shahidi mmoja hatashuhudia juu ya mtu hata akafa.
Shahidi mmoja hakuruhusiwa kuinuka na kumshuhudia mtu yeyote kwa dhambi yoyote.
Kumbukumbu la Torati 19:15 Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote
kumshuhudia kwa uovu wo wote, wala kwa dhambi yo yote,
katika makosa akosayo yo yote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi
wawili, au watatu.
Jambo hili linafanywa pia na wazee (1Timotheo 5:19).
Evidence should be disclosed in a hearing of both parties. There can be no withholding of evidence or of witnesses (cf. Mat. 18:15, 16).
Torati ailiyopewa nabii Musa ni kiini msingi wa sheria zote za Mungu. Ingawaje kuna Roho Mtakatifu, watu wote wanatakiwa waipokee neema.
Waebrania 10:28-29 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. 29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?
Katika siku za Waamuzi, kosa lilijulikana kwa kupigia kura na pia kwa mtu kukiri au kukubali kosa (sawa na Yoshua 7:14-26). Hakuna vitisho vilivyowahi kutumika ili kupata ushahidi chini ya mfumo wa sheria ya kibiblia. Neno lililotoka vinywani mwa manabii lilitumika mara nyingi na Mungu.
Kitendo cha kushindwa kupata ushahidi kwenye makosa yanayofanyiwa madai ni kukamililisha ukomo wa madai ya makosa (mambo ya Walawi 5:1; Zaburi 50:18).
Mambo ya Walawi 5:1 Na mtu awaye yote akifanya dhambi, kwa kuwa ameisikia sauti yenye kuapisha, naye akawa ni shahidi, kwamba aliona au kujua, asipolifunua neno lile, ndipo atakapochukua uovu wake mwenyewe;
Ushahidi wa uwongo umekatazwa.
Kutoka 23:1-3 Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu. 2 Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu; 3 wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake
Utaratibu wa Mungu ni mmoja ya kitu cha kutilia maanani kwa walio masikini na kwa kila mtu anatakiwa apewe fursa, lakini ni kwa juhudi zitokanazo na matendo yao.
Mambo ya Walawi 19:9-11 Na mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala usiyakusanye masazo ya mavuno yako; 10 wala usiyakusanye masazo ya mizabibu yako, wala usiyaokote matunda ya mizabibu yako yaliyopukutika; uyaache kwa ajili ya maskini na mgeni; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 11 Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo.
Hakuna mtu anayetakiwa ashughulikiwe au atendewe vibaya na mwingine. Umuhimu huu unaendelea hadi kwenye biashara na viwanda kwa mambo yote.
Kumbukumbu la Torati 25:13-19 Usiwe na
mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako. 14 Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika
nyumba yako. 15 Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na
kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo
Bwana, Mungu wako. 16 Kwa kuwa wote
wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa Bwana,
Mungu wako. 17 Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia
mlipokuwa mkitoka Misri; 18 jinsi alivyokukuta
katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge
nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. 19 Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana,
Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana,
Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya
mbingu; usisahau.
Tendo la kutumia vipimo vya uzito na vya ujazo vya uwongo ni ushuhuda wa uwongo pia. Tendo la kuchukua fursa ya udhaifu katika kujaribu kuliharibia sifa kundi lingine au watu wengine kwa kuvunja kwao torati ya Mungu, isipokuwa kwa wakati ilipoamriwa hivyo kimahsusi na Mungu chini ya sheria yake.
Kuficha kwa
kutoutoa ushahidi
Hatupaswi kuficha
kutoutoa ushahidi. Inapotokea kughafilika na kutokuwepo kwa ushuhuda ndipo kamosa au hatia inaweza
kugundukika. Hapo ndipo ushuhuda unabidi utolewe, hadi itakapokuwa imefanywa
hivyo kwa sadaka ya dhambi
Mambo ya Walawi 5:4-13 au, kama mtu akijiapisha, kwa kutamka haraka kwa midomo yake, kutenda uovu, au kutenda mema, neno lo lote mtu atakalolitamka kwa kiapo pasipo kufikiri, na neno hilo likamfichamania; hapo atakapolijua, ndipo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo; 5 kisha itakuwa, hapo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo, ndipo atakapoliungama jambo hilo alilolikosa; 6 naye atamletea Bwana sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake. 7 Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea Bwana hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa. 8 Naye atawaleta kwa kuhani, atakayemsongeza kwanza yule wa sadaka ya dhambi, naye atamkongonyoa kichwa shingoni mwake, lakini asimpasue vipande viwili; 9 kisha baadhi ya damu ya hiyo sadaka ya dhambi atainyunyiza katika ubavu wa madhabahu; na damu iliyosalia itachuruzishwa hapo chini ya madhabahu; ni sadaka ya dhambi. 10 Kisha huyo ndege wa pili atamsongeza kuwa sadaka ya kuteketezwa, sawasawa na sheria; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa. 11 Lakini asipowaweza hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, ndipo hapo atakapoleta matoleo yake kwa ajili ya neno hilo alilolikosa, sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, kuwa sadaka yake ya dhambi; asitie mafuta juu yake, wala ubani usitiwe juu yake; maana, ni sadaka ya dhambi. 12 Naye atamletea kuhani, na kuhani atatwaa konzi yake ya huo unga kuwa ukumbusho wake, na kuuteketeza juu ya madhabahu, juu ya sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto; ni sadaka ya dhambi. 13 Na huyo kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake ambayo katika mambo hayo mojawapo amefanya dhambi, naye atasamehewa; na unga uliosalia utakuwa wa kuhani, kama hiyo sadaka ya unga ilivyokuwa.
Tendo la kuficha ukweli kwenye udhalimu pia
linafanywa
Warumi 1:18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote
na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
Hakuna Kanisa lililo na haki ya kuanzisha sheria au mafundisho yaliyo kinyume na Torati na ushuhuda wa Biblia. Kila baraza la kanisa na kila kanuni ya imani ya Kanisa zinazopingana na sheria za Biblia sio tu kwamba haziko sahihi bali pia ni machukizo kwa Mwenyezi Mungu. Na kila mtu aliyewahi kufanya uovu huu, basi amejihukumu mwenyewe kwa hukumu itakayotolewa kwenye ufufuo wa pili wa wafu pamoja na wale wote waliowafuata. Kwa kweli, hakuna mateso makuu yatakayowahi kuumiza watu zaidi ya haya ya kwenye ufufuo wa pili wa wafu, wakati ambapo mamilioni yasiyohesabika ya watu watakapogundua kuwa walikuwa wanawafuata wahubiri shupavu waliokuwa wanawahubiria uwongo nay a ukengeufu na kwamba wamewapoteza na wanatakiwa kuanza upya tena. Sio suala la kukataliwa kwao kuuingia Ufalme wa Mungu kwa watu wa aina hii ambao viongozi wao ni watumishi na vifaa kamilifu vya Joka ambaye pia ni Shetani, aliyelishawishi Kanisa na kufanya vita na wale waliokuwa wanazishika amri za Mungu na ushuhuda wa imani ya Yesu Kristo (Ufunuo 6:9-11; 12:17; 14:12; 22:14).
Agizo la kusema na kuhubiri ukweli limetolewa kwa wote. Kitendo cha kusema uwongo kwa kutojali mamlaka iliyowekwa kisheria ni sawa na dhambi ya kushuhudia uwongo.
Kuvuapa kwa uwongo
Hairuhusiwi mtu kuapa kwa uwongo.
Mambo ya Walawi 19:12 Msiape uongo kwa jina langu, hata ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi Bwana
Adabu au hukumu kwa mtu aliyeapa kwa uwongo ni ya muhimu (Mithali 19:5,9 sawa na 25:18). Mashahidi wote wa uwongo hawatakiwi waishi (Mathayo 19:17-19; Marko 10:18-19; Luka 18:19-20). Pia soma Warumi 13:8-10.
Luka 18:19-20 Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu. 20 Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.
Kwa hiyo, kila mtu aliyeshindwa kuzishika amri za Mungu ameshindwa au kuanguka kiimani na anapaswa aondolewe kutoka kwenye ushirika wa waumini hadi atakapotubu.
Ni kama tulivyojionea kwamba
kushuhudia uwongo ni dhambi mbele za Mungu.
Mambo ya Walawi 6:1-7 Bwana akanena na Musa, na
kumwambia, 2 Mtu awaye yote akifanya dhambi, na kuasi
juu ya Bwana, akamdanganya mwenziwe katika jambo la amana, au la mapatano, au
la kunyang'anya, au kumwonea mwenziwe; 3 au
kuzumbua kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo;
katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo; 4 ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata
hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang'anya, au kitu kile
alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea
alichokizumbua yeye, 5 au kitu cho chote
ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza
na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo
atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia. 6 Kisha ataleta sadaka
yake ya hatia kwa Bwana, ni kondoo mume wa katika kundi lake, mkamilifu,
sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani; 7 na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele
za Bwana, naye atasamehewa; katika jambo lo lote alifanyalo hata akapata kuwa
mwenye hatia kwalo.
Ushuhuda wote wa uwongo kuhusu dhambi iliyotendwa na ni uharibifu ambao kwamba unahitaji kufanyike marejesho.
Kumbukumbu la Torati 19:16-21 Shahidi mdhalimu akimwinukia mtu ye yote na kushuhudia juu yake ya upotoe; 17 ndipo wale watu washindanao kwa mambo yale na wasimame wote wawili mbele za Bwana, mbele ya makuhani na waamuzi watakaokuwapo siku hizo; 18 nao waamuzi na watafute kwa bidii; na tazama, yule shahidi akiwa shahidi wa uongo, naye ametoa ushahidi wa uongo juu ya nduguye; 19 ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. 20 Na watakaosalia watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako. 21 Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.
Kwa hiyo hukumu kwa ajili ya kuvunja kiapo inandana na ile ya makusudi, na ni uhalifu ambao unabidi uhukumiwe.
Hukumu
Mtume Yakobo anatuonyesha umuhimu wa Torati au Sheria.
Yakobo 2:8-13 8 Lakini
mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa,
Mpende jirani yako
Hukumu isiyozingatia rehema inakiuka misingi ya haki. Yeyote anayehukumu pasipo huruma atahukumiwa pasipo huruma (cf. Kumbukumbu la Torati 1:16).
Hakimu hauchukui upanga bure na anapata uweza wake kutoka kwa Mungu, haijalishi ni utaratibu gani.
Warumi 13:1-4 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu
Mungu huwahukumu wateule au elohimu wake (Zaburi 82:1).
Zaburi 82:8 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe
utawarithi mataifa yote
Je, tutawezaje kuwahukumu malaika ikiwa tunashindwa kuhukumu maneno yetu wenyewe?
1Wakorintho 6:3-4 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika,
basi si zaidi
Kwa kuitendea kazi hukumu wote
wanafundishwa kwa kazi hiyo ambayo imewekwa juu
Haki ni tendo la kuishi maisha yasiyo na mawaa kwa kuwa haki ni dhabihu kwa Mungu ya utauwa.
Kumbukumbu la Torati 17:1-20 inasema: Usimchinjie Bwana, Mungu wako,
ng'ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo
lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako. 2 Ikiwa
ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana,
Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako,
kwa kuvunja maagano yake, 3 naye amekwenda
kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi
la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi; 4 ukiambiwa
hayo nawe umeyasikia, ndipo utafute kwa bidii, na tazama, ikiwa ni kweli lina
hakika jambo lile, kuwa yafanywa machukizo kama hayo katika Israeli; 5 ndipo umchukue nje malangoni kwako, yule mtu mume, au
yule mwanamke, aliyefanya jambo lile ovu; ukawapige kwa mawe, wafe. 6 Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili,
au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. 7 Mikono
ya wale mashahidi na iwe juu yake kwanza kwa kumwua, kisha mikono ya watu wote.
Uondoe vivyo uovu katikati yako. 8 Ikiwa limezuka neno
lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya
daawa na daawa, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako;
ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; 9 uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku
hizo; uwaulize; nao watakuonyesha hukumu ya maamuzi; 10 nawe
fanya sawasawa na hukumu watakayokuonyesha mahali hapo atakapochagua Bwana;
nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza; 11 kwa mfano wa sheria watakayokufunza, na kwa mfano
wa hukumu watakayokuambia, fanya vivyo; usigeuke katika hukumu
watakayokuonyesha, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto. 12 Na mtu afanyaye kwa
kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia Bwana, Mungu
wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli. 13 Na hao watu wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena
kwa kujikinai. 14 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo
Bwana, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, itaweka mfalme
juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu; 15 usiache
kumweka yule atakayechaguliwa na Bwana, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke
mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye
si ndugu yako. 16 Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala
asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa Bwana
amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile. 17 Wala
asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na
dhahabu kuwa nyingi mno. 18 Tena na iwe, zamani
aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika
chuo, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi; 19 na
awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana,
Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya; 20 moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala
asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kuume wala wa kushoto; ili apate
kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya
Israeli.
Mfumo wa haki unaendana na idadi dhana zilizotajwa mapema huko nyuma.
Kumbukumbu la Torati 16:19-20 Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki. 20 Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
Hakuna mtawala aliyetawala huku akiwa hajajitengenezea nakala ya kitabu cha Torati na kujisomea, na kuiandika Torati hii na kuiteda. Tamko la hukumu ni la rehema na hukumu inapaswa ifanyike kwa kufuata maelekezo ya Torati ya Mungu, na inatakiwa ichukuliwe kikamilifu.
Jela au lokapu
Mtuhumiwa anaweza kuhukumuwa kifungo cha nje (Hesabu 15:32-36). Hukumu inatakiwa ifanyike haraka na hukumu ifanyike kulingana na kosa lenyewe lilivyofanyika.
Ezra 7:26 Na kila mtu asiyekubali kuitenda sheria ya Mungu wako, na sheria ya mfalme, na apatilizwe hukumu kwa bidii, kwamba
ni kuuawa, au kwamba ni kuhamishwa, au kuondolewa
Kwa hiyo, mtu anatakiwa aletwe mbele ya mashitaka pasipo kumchelewesha. Kitendo cha kulaza mtu jela bila kumfikisha mahakamani ni kinyume na Torati au sheria za Mungu.
Kifungo kinakusudiwa kurekesha harasa au
deni lililotokana na uhalifu uliofanyika, kwa kufanya
kazi, sawa na jinsi alivyohukumiwa. Fedha zitakazopatikana zinatarajiwa kutumika
kwa kulipa au kufanya ukombozi au fidia kwa uhalifu
uliofanyika iwapo kama utaifishaji wa
Hukumu ya mwili
ilifanyika nje ya makao au kambi zao Israeli (Mambo ya Walawi 24:14).
Sulemani alifanya
dhambi na akafa kifo cha kimwlili asilia. Hata hivyo,
thawabu yake haikuwa
Marekebisho na
malipizi
Kufuatia na makosa au mashitaka ya kumdhalilisha mtu au kumuaibisha, tunaendelea kwenye hukumu. Dhana au lengo la kwanza kuhusu kumhukumu mtu ni kumrekebisha. Makosa yote ni dhambi na dhambi ni uvunjifu wa sheria. Mungu anapenda kwamba kusiweko mtu yeyote atakayepotea bali wote waweze kumuona yeye, na ndio maana jambo la kwanza linalotiliwa maanani ni kutubu na marekebisho ni neema tu.
Israeli wote wanatakiwa wawe watakatifu kwa Bwana. Marekebisho ni
kuhakikisha kwamba mtu emerudi kwenye jamii na anafaa kwenye taifa
Mathayo 5:3-13 Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4 Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. 5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. 6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. 7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. 8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. 9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. 10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. 12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu. 13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Ingwa wokovu wa Kristo umeendelea hadi kwa Wamataifa na utaratibu wa hukumu ulitolewa kwa watu wa mataifa yote. Wamoabu na Waamoni walitabiriwa kuwa watajumuishwa na Yuda na kwa hiyo wataingia kwenye imani katika siku za mwisho wakiwa ni sehemu ya Israeli. Wamisri watabakia wagumu. Mataifa yoye watakuwa ni sehemu ya hekalu la Mungu aliye.
Kumbukumbu la Torati 23:3-8 Mwamoni wala Mmoabi wasiingie
katika mkutano wa Bwana; wala hata kizazi cha kumi mtu
wao asiingie katika mkutano wa Bwana milele; 4
kwa sababu hapo mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na
kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo
Hapa tunaiona dhana ya udugu ilivyo kwenye Torati ya Mungu inavyoendelea mbali zaidi kwenye makabila ya Israeli kwa wana wa Ibrahimu na kwa watu mchanganyiko wa Kisyria na Kifoenike, ambao walijumuishwa kwa waedomu (Waidumea), na Wamisri, walio na msingi wa ukarimu kwa Waisraeli. Pia imeenelea hadi kwa Waashuru ambao walifanya kazi mkono kwa mkono na Israeli watakaotokea pande za kaskazini katika nyakati za mwisho. Wokovu uliendelea hadi kwa Wamataifa.
Mwisho wa sheria ni kumhakikishia pia usalama wa kila mtu. Pale
ambapo ushahidi wa uwongo ulisababisha hasara kuliko
kutokea kwa marejesho. Hata hivyo, kwenye sheria zote kuna asili fulani ya msamaha na huruma. Mahali pasipo na msamaha, hapawezi kuwa na marekebisho makamilifu. Kila mtu anapaswa kujua kwamba amepoteza kile wanachokitarajia kukipata.
Ni vema kurejeshwa kwa ndugu yako kuliko kurejeshewa
Uhalifu unaendana na adhabu, na sio kila mara kini aiwa kwa unaendana na toba. Pasipo toba laana ya Torati inafuatia. Laana hizi zinalitesa taifa zaidi kuliko zinavyomuathiri mtu binafsi.
Kumbukumbu la Torati 28:18-19 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,
Kila mara kuna dhambi, na ukosaji na malipizo, lakini hata hivyo, Mungu huhukumu moyo wa kila mmoja.
Hesabu 5:5-10 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 6 Uwaambie wana wa Israeli, Mtu mume au mke atakapofanya dhambi yo yote, ifanywayo na binadamu, kumwasi Bwana, na mtu huyo akawa na hatia; 7 ndipo watakapoungama dhambi yao waliyoifanya; naye atarudisha kwa hatia yake, kwa utimilifu wake, tena ataongeza juu yake sehemu ya tano, na kumpa huyo aliyemkosa. 8 Lakini kwamba mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye inampasa kurudishiwa kwa ajili ya hiyo hatia, kile kitakachorudishwa kwa Bwana kwa hiyo hatia kitakuwa cha kuhani, pamoja na kondoo mume wa upatanisho, ambaye kwa huyo utafanywa upatanisho kwa ajili yake. 9 Tena kila sadaka ya kuinuliwa, ya vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, watakavyosongeza kwa kuhani, itakuwa ni yake. 10 Tena vitu vilivyowekwa wakfu na mtu awaye yote, vitakuwa ni vya kuhani; kitu cho chote mtu atakachompa kuhani, kitakuwa chake.
Kila mmoja sasa anawajibika kwa dhambi zake mwenyewe na Mungu amesema kwa kupitia manabii wake kuhusu dhambi za.
Hesabu 14:18 Bwana ni mpole wa hasira, mwingi wa
rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana
makosa kwa njia yo yote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika
kizazi cha tatu na cha nne.
Neema hii ya Mungu imetokana na Roho wake aliyemfanya akae na watu wote, ili kwamba kila mtu sasa awajibike kwa maovu yake au dhambi zake.
Ezekieli 18:19-24 Lakini ninyi mwasema, Kwani
yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana
atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika amri
zangu na kuzitenda, hakika ataishi. 20 Roho itendayo
dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa
baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa
juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. 21 Lakini
mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote
alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki,
hakika ataishi, hatakufa. 22 Dhambi
zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake
aliyoitenda ataishi. 23 Je! Mimi
ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba
aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi? 24 Bali mwenye haki atakapoghairi, na
kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote
Kusomwa na
Kukaziwa kwa Torati kila miaka saba
Torati inapaswa isomwe na kutangazwa kwa kuwekewa mkazo kila baada ya miaka saba na kwenye mwaka wa Sabato wa Yubile.
Kumbukumbu la Torati 31:10-13 Musa, akawaamuru, akasema, Mwisho wa kila mwaka wa saba, wakati wa maachilio, wakati ulioamriwa wa sikukuu ya vibanda, 11 Israeli wote wafikapo ili kuonekana mbele za Bwana, Mungu wako, mahali pale atakapopachagua, uisome torati hii mbele ya Israeli wote masikioni mwao. 12 Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha Bwana, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii; 13 na watoto wao wasiojua, wapate kusikia na kujifunza kumcha Bwana, Mungu wenu, siku zote mtakazokaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki.
Ukamilifu wa kila
mmoja na wa mfumo mzima
Matokeo ya mwisho ya sheria na
mpango wa Mungu ni ukamilifu wa Roho Mtakatifu.
Kumbukumbu la Torati 18:13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako
Tunatakiwa pia
kuwapenda adui zetu, kwa kuwa
Mathayo 5:46-48 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata
thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la
ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48 Basi
ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Lengo hili
linawezekana kulifikia wana wa Adamu. Tunapaswa kuwa wakamilifu
kana Nuhu aliyokuwa mkamilifu na
Mwanzo 6:9 Hivi ndivyo
vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda
pamoja na Mungu.
Ingawa Mungu
alimuamuru Abrahamu awe mkamilifu, ni sawa
Mwanzo 17:1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Kwa hiyo, ukamilifu katika Roho Mtakatifu sio tu kwamba unawezekana, bali pia tumeamriwa kuwa hivyo. Tumeamriwa pia kuwapenda maadui zetu na kuwarekebisha wale wote walioanguka mbali na neema. Kwa hiyo, adhabu kali zilizo kwenye sheria zinapaswa ziruhusiwe pale tu inapotolewa fusra ya mkosaji kukiri nay eye akakiri lakini asitake kutubu kabisa.
Zaburi 37:37 Umwangalie
Watu wote wanatakiwa kuenenda kwa Roho Mtakatifu kwa Sheria ya Kifalme ya Uhuru.
q