Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[268]
Vita Vya
Waunitariani Na Watrinitariani
(Toleo
La 2.0 19980918-20000115-20040709)
Wakati Constantine alipoingia madarakani kuwa mfalme alijaribu kuiunganisha
Dola ya Rumi iwe na mfumo na imani moja na alitaka kufanya hivyo kwa kuutumia
Ukristo. Kile alichoshindwa kukigundua ni kwamba utendaji kazi wa Warumi
haukuwa umeeleweka na kujikita miongoni mwa watu wengi kwa kuwa haukujulikana
tangu kale na kwamba mafundisho ya Kanisa yalikuwa yamechanganywa kiutata
kutokana na wale waliokuwa kwenye kanisa la kwanza asilia. Mchanganyo huu ulipelekea
kuwepo kwa mlolongo wa mapigano kadha wa kadha katikati ya utendaji kazi wake
ambao pia ulipelekea kuwepo kwa makosa ya kimafundisho. Matokeo ya mwisho
yaliyotokana na makosa haya ya kimafundisho na tama ya kuchukua maongozi ya
kisiasa kwa kutumia dini yalikuwa ni mwendelezo wa vita visivyokoma na mateso
yaliyodumu kwa miaka mia saba sasa. Makosa haya pamoja na migongano yake
vitapelekea kuwepo kwa uharibifu mkubwa sana na maangamizo makubwa ya hii dunia.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1998, 2000, 2014 Wade Cox)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Vita Vya Waunitariani na Watrinitariani
Mabishano
ya Waathanasi na Waariani Kutoka Nikea
Baada ya Tangazo au
Azimio la Uvumiliano la Milan la mwaka 314, mfalme Constantine alitanza mbinu
za kuutumia Ukristo kwa malengo ya kisiasa na hasa akilenga au kukusudia kuutumia
ili kusaidia matendo na shughuli za Kirumi, ambao hatimaye ulikuja kukubaliana
na mafundisho ya Athanasius na hatimaye yale ya Wakapadokiani. Imani iliyopo na
kukubalika na Kanisa ilichanganika na kunajisika na imani na matendo ya
Wanostiki, ikiwa na ushawishi mkubwa wa dini za imani za sirisiri zisizoelezeka
vizuri. Constantine aliwasaidia na kuwaunga mkono Waathanasius na imani yao kwa
dhana aliyokuwanayo kimakosa kwamba walikuwa wengi na imani yao inaumaarufu
mkubwa huko Roma, na ilikuwa ni dini na imani kubwa iliyokuwa kinume ikipingana
na Waarius ambayo ilishika dau kwa wengi keenye Sinodi ya Alexandria mgongano
uliopelekea kuvuka vita ndani ya dola yake dhidi ya mtawala mweza wake
aliyeitwa Licinius na kuzuka ma mapambano kwenye miaka ya 322-323 BK.
Baada ya kumshindwa
Licinius na kujitangaza mwenyewe kuwa ni Mfalme
wa Dola yote nzima, aliitisha Mtaguso wa Baraza lake huko Nicea mwaka 325
BK, mtaguso uliolenga kuirasmisha na kuiongezea nguvu imani hii ya Waathanasiani
(ambayo hatimaye ilikujakuwa ndiyo hii ya Ukatoliki). Msingi wa Ukiri wa Imani
ilitungwa na kurasmishwa kwenye Mtaguso huu wa Baraza la Nicea na kujulikana
kama ni Ukiri wa Imani wa Nicea, lakini kipindi cha kutangazwa kwake rasmi na
kupigwa marufuku aina nyingine zote za imani kiliongezwa hadi walipoitisha
Mtaguso mwingine wa Baraza huko Constantinople mwaka 381, lakini kwa kwa ni kwa
juhudi kubwa waliupa taswira potofu na endelevu. Mtaguso ule wa Baraza la Nicea
ulijulikana kama wa Ukristo unaoamini Utatu. Mwaka 318 Constantine aliitisha
kikao cha baraza la maaskofu wote waliokuwapo huho Roma na kutoka maeneo
mengineyo na wadesposyni; maaskofu hawa walikuwa wanatoka kwenye familia ya
Yesu Kristo. Mwitikio uliotokana na Kanisa la Roma ulikuwa ni wa kukomesha (tazama
na soma jarida la Bikira Mariamu na Familia ya Yesu Kristo (Na. 232) [The Virgin Mariam and
the Family of Jesus Christ (No. 232)].
Kile kilichoitwa
Kanuni ya Mtaguso wa Nicea kikakomeshwa. Hatimaye ikaanzishwa myingine
iliyosema kuwa ziwepo 20 tu ambazo zilitanguliwa na kuanzishwa kwa ukengeufu kama
vile sheria za maisha na taratibu za nyumbani zilizohusu uhusiano na huduma za
wazee au makasisi wanaoishi na wanawake, kama vile aheria za maisha ya useja,
mateso yanayotokana na kuingizwa kwa sheria za kuwaadhibu wanaopingana na imani
ya Utatu (ambao waliitwa kimakosa Waarians) na wale waliokuwa wakimsaidia Licinius;
kuanzishwa kwa utaratibu wa kuweka dayosisi na usimamiwaji wake na makasisi na
makato kwa makasisi kudai riba; na kuanzishwa kwa maombi ya kufanywa watu
wamesimama na ibada za siku ya Jumapili na “Majira ya Pasaka” (ambayo kwa kweli
ulikuwa ni mwanzo wa kuanzishwa kwa maadhisho ya Easter badala ya Pasaka). Tamko
hili la Ukiri wa Imani ulianzishwa hukohuko Constantinople, na ndiyo huohuo
uliofanyika chimbuko la imani ya Ubinitarianism na ambao ni muhimu sana na
unatumiwa na watu wanapoanza kuchukua hatua ya kuwaingiza watu kwenye itikadi
ya Utatu na ulianzisha imani ya ukengekfu kwamba Kristo alikuwa ni “mwana wa
pekee wa Baba” na ambayo indiye aliyehat Christ was the "only begotten of
the Father" anaodoa ahadi ya wateule kama wana wa pekee wa Mungu. Athanasius
anasema (kwenye kitabu chake cha Ad Afros) kwamba walikuwepo maaskofu takriban 318
waliohudhuria. Arius alionywa na ndiye aliyekuwa mlengwa kwenye Baraza la Mtaguso
huu ulioanza takriban tangu tahere 20 Mei 325 BK ulioitishwa na Hosius
Muathanasius wa Cordova. Constantine alijiunga kwenye kikao cha Baraza hili
tarehe 14 Juni. Ili kufikia muafaka na kuwapndeza, Constantine alienda kwenye
divisheni ya Warumi na kuwatia mbaroni maaskofu hadhaa na kuwafukuza kina Arius,
Theonas wa Marmarica na Secundus wa Ptolemais na kuwapeleka huko Illyrica. Maandiko
ya Arius hatimaye yalichomwa moto na wote watatu walisomea dua ya kuwalaani.
Iliazimiwa kuwa siku ya ukumbusho mfano wa Tamko hili la Ukiri wa Imani
ufanyike kila siku ya tarehe 19 Juni. Kikao cha Baraza hili la Mtaguso
kiliishia tarehe 25 August kwa sherehe na karamu yenye mbwe,mbwe iliyoandaliwa
na Constantine mwenyewe akishirikiana na maaskofu waliokuwepo.
Miezi mitatu baada
ya kwisha kwa Mtaguso huu, Eusebius wa Nicomedia
na Theognius wa Nicea, ambao walilazimishwa kutia saini Tangazo hili la Ukiri wa
Imani chini ya shinikizo kubwa/na kutishwa kwa kuttiwa mbaroni na kufukuzwa kwa
sababu ya kufuta usemi au kumpinga Theodotus wa Laodicea, ambaye pia alitia
saini kwa kushinikizwa na vitisho na kumpinga, akakubali kuachahanayo kuliko
kujiunganao.
Mwaka 328 BK
Constantine baada ya kugundua kuwa kumbe Waathanasius hawakuwa ni kundi kubwa
na kwamba walikuwa ni chanzo cha migawanyiko na mateso kwenye Dola yake na
akawakumbuka na kuwaita viongozi watano wa Kiunitariani. (Inadhaniwa kuwa miongoni
mwao alikuwepo Constantia, mjane wa Licinius. Hata hivyo inawezekana sana
kwamba yeye alikuwa ni muumini tu mashuhuri wa imani hii ya Kiunitariani
aliyekuwa wa mrengo wa Eusebian au Arian). Tatizo lililopo kwenye imani hii ya
Ukristo wa Kiyunitariani ni kwamba ulifuata misingi ya imani ya Biblia na haikuwa
inahusisha na mchakato wowote wa kutawala mataifa. Kila taifa lilikuwa pekeyake
na liliwajibika kwa viongozi wake lenyewe na kwenye mfumo na imani yao ya
kidini waliopo kwenye taifa lile na uhusiano wao ulikuwa ni kati yao na Mungu
na kama taifa walimcha na kumtii Mungu na hivyo walibarikiwa. Dola ilijiri na
mambo yanayohusu na utawala wa dunia na waongofu wa kanisa la Roma pia
walijengwa na mawazo hayo. Kwa hiyo wakaanzisha shirika la kidini lililokusudia
kutamalaki mamlaka au utawala wa dunia na isiyovumilia upinzani wowote wa imani
na utawala ule. Matokeo yake, imani ya Kanisa la Roma ikachukua na kuingiza
imani nyingi za kipagani zilizokuwa zinafundishwa na kutumiwa kwenye dini za
mungu jua zz Waariani na uziingiza kwenye Ukristo, ambazo kwamba hakuna mtu
anayeiamini Biblia anneweza kufuata imani zote mbili. Na hiki ndicho kiini cha
tatizo. Na hii ndiyo sababu iliwafanya waihakachue maandiko ya Biblia kwenye
maandiko muhimu na kusababisha utata wa kitafsiri hadi leo na kuharibu ukosoaji
wa kisomi, kama ilivyofanyika kwenye mauaji ya halaiki ya Holocaust.
Constantine mwenyewe
hakuwa amebatizwa kama Mkristo wa imani hii ya Kiathanasian na kwa kweli
alikuja kuwa Mkristo kwenye kipindi cha mwisho wa maisha yake, akibatizwa kama
Myunitariani na Eusabius wa Nicomedia, ndugu wa Julian, ambaye alikujakuwa ni
msaada wake mkubwa mwaka 329 BK. Hakukuwa na kitu kama hicho kwa Wakatoliki wa Roma au kweenye Kanisa Katoliki la Roma katika siku hizo
wakati kila mmoja wao alikuwa ni mkatoliki
au mdunia kwa kulinganisha na hali ya
kanisa. Uyunitariani ulikuwa ni mtindo na imani ya kizamani sana na ndiyo yalikuwa
nidiyo mafundisho ya kwanza ya kanisa la mitume na ukwali huo hautaweza
kusahaulika kamwe. Makasisi waliokuwa wanapinga maazimio ya Mtaguso wa Nicea (ANF) wote walikuwa ni Wayunitariani na
walidumu wakiamini hivyo kwa karne kadhaa mbele (soma jarida la Teolojia ya Mwanzo ya Uungu (Na. 127) [Early Theology of the Godhead (No.
127)]. Ubinitariani
ulikuwa ni imani mpyua ambayo ilikuwa na mafundisho mapya na uliendeleza
mafundisho yaliyochukuliwa kwenye chimbuko la teolojia ya kipagani ya mungu wa
Utatu aliyetokana na ibada za mungu Attis wa Roma na Adonis wa Wayunani. Watrinitariani
na imani ya Utrinitariani haikuwepo hapo mwanzoni hadi ulipofika mwaka 381. Constantine II na Constantinius wote hawa
walikuwa ni Wayunitariani walioitwa pia kama “Waariani” au “Waeusebiani” na
wale waliokuwa baadae Watrinitariani. Vikundi hivi vilipewa majina hayo na
Waathanasius, ambao waliwaita Waariani au Waeusabius, majina ambayo wao
hawakupenda kuitwa hivyo. Inaonekana kuwa ilikuwa ni mbinu chafu tu ya
Waathanasius kuwaita hawa kuwa ni Waarius kutokana na msimamo wake alioutangaza
kwa lengo la kuwapunguza nguvu na kuidhalilisha imani yao isikubalike na watu
japo ilikuwa ni ya zamani zaidi na ilikuwa kubwa kuliko ile ya Waathanasius.
Kama ni kweli kwamba
kikundi hiki kiliamini kwamba Kristo ndiye alimuumba Roho Mtakatifu basi hilo
litakuwa ni kosa na upotofu mkubwa, ila jambo hili halina ushahidi wowote kwa
kuwa hakuna hata andiko lao lolote linaloonyesha kuwa waliamini na kufundisha
hivyo. Inawezekana kuwa huenda liliingia kwnye imani au kundi wa Wagoths kama
makosa na ni katika kipindi cha baadae sana, likiwa ni matokeo ya makosa ya
kuandishwa kisynkretiki ,na imani ya Wakatoliki wa Roma wa kundi la Filioque ya
huko Toldeo katika jamii ya wa Visigoths.
Mabishano haya ya
Waathanasian/na Waarian yalipoeleweka vyema, ndipo walipouunda Ukristo ambao
ulifanya kuwepo na tofauti kubwa na uliotegemea muundo wa kiujuzi na ujanja wa
kifalsafa. Sayansi ya kibinadamu na elimu ya kimaboleo ya tamaduni za watu
ulimwenguni maarufu kama anthropoloji ya kipaleo vilifanyika vieleweke vizuri
na watu na huenda viliendelezwa kwa amani na ukimya sana, ili kuzuia vipindi
vyote viwili, yaani vya Zama ya Giza na zama za watu Mateso ya Kidini kwa
wasiokubaliana na mafundisho. Hebu na tuyatathmini mabishano haya kama
ifuatavyo.
Wahuasika wakuu au
watunguli walikuwa ni Alexander na Athanasius, maaskofu wa Alexandria tangu
mwaka 312-328 na 328-373 aliyeheshimiwa sana na kukubalika na Waathanasians; na
Waarius (256-336), Asterius wa imani ya Sophist (yapata kama mwaka 341), na
Eusebius wa Nicomedia (takriban mwaka 342), kwa Waarians au Waeusebians.
Bahati mbaya,
kutokana na kushundwa kwa Waarians huko Hispania, historia imeandikwa na
Waathanasians, na kwa mtindo wa kulalia upande mmoja na kwa upendeleo mkubwa
kuwa haiwezekani kabisa. Hata hivyo, Robert C. Gregg na Dennis E. Groh wameandika
kazi nzuri nay a maana san a kwenye kitabu kijulikanacho kama Early Arianism: A View of Salvation[Waariani
wa Zamani na Mtazamo wao Kuhusu Wokovu] (Fortress Press, Philadelphia, 1981). Kutoka
kwenye kitabu hiki tunaweza kuanzisha utafiti wa kimetafizikia au uchunguzi, na
inaweza kuwa dhahiri kuwa imani zote mbili zilikosea.
Kuandikwa upya kwa
walichokiita Thalia ya Arius kulichukuliwa kutoka kwenye maandiko ya wapinzani
wao na hivyo yalikuwa na makosa ya jinsi yalivyoandikwa kwenye nakala halisi.
Mapishano haya yanatuama kuonekana kama Waathanasians walivyopenda iwe kwa
kuzingatia yafuatayo:
Wokovu wa wale
walioshiklia itikadi kali ililazimu kwenye umuhimu wa jinsi alivyo Mwana na
Baba: kwamba ndio uliowajumuisha Mungu na Kristo kwenye uumbaji uliodhaniwa au
kuchukuliwa kuwa ni mwili wenye asili ya kimbinguni. Wokovu wa Waariani
umeathiriwa na uthibitisho wa Mwana na viumbe wengine: na ambao unamjumuisha
Kristo na viumbe wengine wa Mungu unathibitika kwa mapenzi yake (Gregg & Groh
p.8).
Kwa kukubali kwao
Waathanasians, tafsiri ya kibayolojia ya mwana, waliendeleza uhusiano wa
kiantolojia kati Mwana na Mungu, ambao waliaminkuwa ndicho kilimuwezesha Kristo
kuwa ni neno halisi au Logos wa Mungu na Hekima, na ambaye amemfanya Mwana awe
na weza wa kimungu wa kuelewa kila kitu (ibid., Ep.9).
Kutokana na Mtaguso
huu ni dhahiri kabisa kwamba imani ya Kiyunitari ilikuwa na nguvu kubwa. Ni
kweli kwamba waliongoka kutokana na kitendo kile tu cha kuwashinda wafuasi wa Salien
Franks ambao waliitisha mdahalo uliopangiliwa vizuri. Waliwashinda na
“kuoingiza” upande wao kwa shuruti kupitia na maslahi binafsi ya viongozi wao
wa jamii za Goths, Vandals, Heruli, Burgundians na Lombards na vikundi vingine
vilivyotajwa kwa ufupi tu kama Teutons, kwenye mwendelezo na mchakato endelevu.
Waingereza waliongoka na kujiunga kwenye makubaliano na muafaka uliofanyika
huko Whitby mwaka 664 BK kwa mkataba au makubaliano ya lazima kutoka kwa wa Anglo‑Saxons,
baada ya wongofu au makubaliano yaliyofanyika baadae mwaka 597 (soma kitabu cha
Stephen Neill, Anglicanism, Pelican,
London, 1965).
Mgongano ulionekana
kwa mtazamo rahisi na makabila haya kama yalivyokuwa wanamueleza bayana mmoja wa Wafalme wa Waariani Gundobald wa
jamii ya Burgundian, aliyekataa kuabudu miungu
watatu (Encyc. Of Religion and Ethics
(ERE), Vol. 1, p.782). Tafsiri hii rahisi ilikuwa ni kiini cha mambo, na matendo
ya Waathanasians yaliingizwa na kukataliwa kwa walei ambao kwayo walilazimisha
kufufua hisia na wazo la aina ya Uungu. Foakes‑Jackson alukubali makosa
ya mawazo yake ya zamani (imeelezewa
vema kwenye kitabu cha Cambridge
Theological Essays, p.500) cha udogo au uduni wa wa Teolojia ya Waarian wa
Barbarians. Alidai baadae kwamba imani ya Uariani ya jamii ya Visigoths,
Lombards, Vandals, nk, haikuwepo tena zaidi ya kuwa t uni kifungu kwenye utaratibu
wa makasisi katikati ya mawazo ya Kikristo tu wa Wateutonic na Warumi (ibid.,
p.783). Hili ni jambo kubwa ambalo halijatathminiwa vizuri. Chimbuko la Wateutons
huko Mahariki ya Kati, hususan baada ya kuanguka kwa Dola ya Wapurthian, hakujawa
na utafiti wa wazi au kufafanuliwa na wanahistoria kwa sababu ya mkanganyiko wa
Watrinitariani waliotoka shule yenye kiwango cha juu cha ufundishaji.
Kile kilichoenguliwa
kwenye majaribio ya Mabishano ya Waathanasiua dhidi ya Waariani ni kwamba
kanisa sasa limekuwa na mjumuisho wa imani mbili ambazo zimepingwa sana na
ambazo zimejumuishwa na mitizamo ya kisiasa na likapelekea kusalitiana na
kutesana. Waathananius waliwa wameweka makao yake huko Roma ambao muorodhesho
wake wa uweza waliokuwanao wafuasi wa Salien Franks kisiasa na kijeshi na jinsi
walivyofanikiwa kwa kipindi kirefu kilichofuatia. Dini hizi mbili zote kwa kweli
zilizikataa imani kwa ajili ya kupenda kwao madaraka. Mchakato wa mfuatano wa
matukio ya kumbania na vuguvugu la makabila yaliyohusishwa ni ya muhimu kwenye
uelewa wa asili na msimamo wa watu waliohusika.
Uyunitariani,
Makabila ya Wateutoniki na Wagoths
Huku ikikabiliwa na
mkanganyiko wa kuwa ni dini rasmi ya taifa na ikiendelea kufanya matendo ya
nguvu za kiutawala katika jamii nay a kijeshi, kinyume kabisa na maelekezo ya
Kristo, mafundisho yalienezwa na mlinganisho mkubwa wa kwanza wa biblia
tulionao unaoruhusu matumizi wa nguvu za kijeshi yakajitokezwa kwenye maandishi
au vitabu vya Augustine, wanatafakari wa Afrika Kaskazini, waliobatizwa kwenye
Ukristo kama walivyoelimishwa huko Punic, maandiko mbalimbali ya Kiebrania,
pamoja nay a Kilatini. Tangu mwaka 373-383 BK, walikuwa ni wanafalsafa wa Kimanichean
na Kiplatoni, aliokuwa na suria aliyezaa mtoto mwaka 372 BK. Alibatizwa mwaka 387
kuwa muamini wa mrengo wa Kiathanasian. Ambrose wa Milan, pamoja na Theodosius,
walichukua mamlaka ya uongozi wa Kanisa la Roma na kulipeleka upande wa Waathanasian
na mambo yao mwaka (381 BK) na uhusika wake na Augustine alikuwa ni kifaa
kwenye uchukuliwaji wa baadae wa amri ile, ambapo kwa wakati uliokuwepo kwake,
kitu cha busara.
Malumbano ya Waathanasian
na Waarian yalipelekea mateso makubwa na pande zote mbili za Waathanasians na zaidi
sana baadae kwa Waarians. Wagoths na Wavandals walioitwa kama “Waarians” (Biblia
ya Wagothiki inasema ilikuwa kuanzia mwaka 351). Malumbano yaliibuka hata
wakati Mtawala Mwanamke Placidia aliwatumia msaada Wagoths, na Wavandals, kuzuia
maasi ya Jimbo la Boniface hapa Afrika mwaka 427. Walisaidiwa na kuungwa mkono
na Maximinius, Myunitariani (walioitwa Waarian)
Askofu. Augustine alilazimika kuwapigania na kuinda kwa wazi kabisa dini ya Waathanasian
mwaka 428.
Mnamo mwaka 330 BK, Constantine
alilitoa kabila dogo la Wavandals upande wa Ujerumani Mashariki (au Silingi)
wan chi ya Pannonia ukanda wa kuume wa Danube. Mnamo miaka ya 166-181 waliishi
huko Silesia na waliwapigavita Waaurilian mwaka 271, wakiwa kwenye upande wa
katikati ya Danube. Yale yan yoitwa kuwa ni makabila ya Kijerumani yaliwajumuisha
wa Vandals, Alans, Sarmations, Suevians na Alamanni upande wa Mashariki na wa
Franks (su Wafaransa), wa Burgundians (ambao kwa kweli hawakuwa Majerumani) na
Lombards au Longobards upande wa Magharibi. Parsons,
Masalia wa kaila la Yafethi (1767) anamnukuu Procopius akisema kwamba Waalans
walikuwa ni Wagoths kama walivyokuwa Wasauromatae na Wamelancleni na kwamba Wavandals
wana ukawaida wa asili na Waostrogoths (p.73).
Kabila la Lombards walikuwa
mfanano wa karibu sana na makabila ya Anglo-Saxons katika uvaaji wao na matendo
yao kuliko walivyokuwa Wajerumani na wanaonekana kufanana zaidi na wa Anglo–Saxons
wakiwa kama kabila dogo. waliishi na kuenea nchini Austria hadi Katikati ya
Italia na waliungana na makabila ya Waceltiki na ya wa Ostrogoths, ambao pia waliishi
kwenye nchi inayoitwa leo Croatia na majimbo yaliyo jirani yake. Waburgundians (mwaka
443 BK) waliishia mara ya mwisho upande wa Magharibi ya Cantons huko
Switzerland, waliishi pande zote mbili za Jura, ziwa la Geneva, huko Valais, na
kwenye kingo za Rhone na Saone (kwa mujibu wa kitabu cha Historians History Vol. XVI pp. 534ff.). Sehemu yake kubwa
ilijiunga na nchi inayoitwa siku hizi Ufaransa na vilevile upande wa Kaskazini
mwa Italia. Dola ya kwanza ya Waburgundian iliyoishia mwaka 534 BK iliweka
msukumo kwa kiasi kikubwa na ugomvi au migogoro ya kifamilia na uliwasaidia
wafalme wake (ibid., p. 535). Dola ya Waostrogothi iliishia kipindi kinachofanana
na hikihiki baad ya kuwakosa wafalme wapatao watano wa kuwarithi kwenye vita
hivi viwili vyote na nchi zao. Thibert, Mfalme wa Franks, aliutumia vizuri
udhaifu wao, kwa kuirejesha mikononi mwake Rhaetia mwaka 536 BK na tangu hapo
alilichukua na kulimiliki eneo lote la Rhaetia na Helvetia, eneo lililoitwa Uswizi
au Switzerland (ibid.).
Waalemanni waliishi
upande wa Kasakazini mwa Switzerland au Uswizi, Alsatia na Baden-Wurtemburg na walitwaa
maeneo na lijichanganya kwa kujiita kuwa wao ni watu wenye uasilia wa
Gallo-Celtic, waliokuja wakitokea maeneo hayohayo yaliyo karibu na Bahari
Nyeusi hadi huko Danube. Wafaransa ambao walishindwa na kuwatumikia Waalemanni,
walifanya mambo yao sawa tu na Wacimbri, Gauls na Celts ambao kwa sasa wako
pande za Kaskazini mwa Ufaransa. walombards waliwafuatia Waostrogos Kuitawala Italia,
ila walikuwa ni wachache idadi yao baada ya kuanzisha ufalme wa kaskazini ambao
mji wake mkuu ulikuwa ni Pavia na upande wa kaskazini mwa Duchy ya Benevento,
ambao walipigwa na kushindwa na Wafaransa mwaka 774. Kusini mwa Duchy
walidumisha uhuru kwa kipindi cha takriban karne mbili zaidi. (ibid., vol. IX
p. 18). Was axons walitengwa kutoka jamii ya Wascandinavia na wakafukuziwa
kwenye muungano wa Ujerumani na Charlemagne (miaka ya 768-814) kama
walivyofanya Wafaransa. Inatosha tu kusema kuwa hii Helvetia ilikuwa ni koloni
au nchi iliyokaliwa na Wakatoliki Warfaransa wakiongozwa na Clotaire II na mwanae
Dagobert aliyemrithi baadae yapata mwaka 628, ilikuwa kwa ujumla Maaskofu
waishi kwenye ndoa kama walei waliowachagua na baadae walikubalina na
kuthibitika na mfalme (ibid., p. 535). Kwa
hiyo, haya baada ya kuchelewa kiasi hiki cha zamani, utawa na useja vilikuwa ni
aina ya maisha iliyokataliwa na haikukubalika kabisa kwenye maeneo mengi ya
Wakristo wa Ulaya.
Mtawala au Mfalme Valens
(364-378) alifanya kazi kubwa kuwajumuisha Wavandals na kuwaingiza kwenye imani
ya Ukristo wa Kiuyunitarian (ulioitwa pia kuwa ni Uarian). Na walipoongoka na
kuwa Wakristo hawakuwa wabishi au wagumu wa kupigwavita, kwa kuwa waliyajua
makatazo na marufuku aliyoyatoa Constantine aliyoyaweka na kuipa dini mamlaka
au uweza wa kijeshi. Wagoths waliingia imani ya Kikristo kipindi kirefu zaidi
kle, na wakaonekana kutoka kwa Wakristo katika makabila na kutoka kwenye barabara.
Kanisa la Sabato la Kiyunitarian liliendelea
katikati ya makabila na watu wa Ufaransa, Kaskazini mwa Italia na Ulaya kwa
ujumla kwa sababu mbalimbali. Sababu ya
kwanza ni kwamba, baada ya Mtaguso wa Baraza la Nicea wa mwaka 325 BK Mfalme
Costantine aliwapendelea Waathanasius ambao hatimaye walikuja kufanyika kuwa ni
waanzilishi wa Kanisa Katoliki la Roma
mwaka 381 BK. Aliitishna mkutano mkuu wa Wadesposyni, waliokuja huko
Roma mwaka 318 BK, ili kuungana na kujadiliana na askofu wa Roma. Ndugu hawa wa
damu na Kristo walidai marejesho ya maagizo Torati, kukiwemo na utunzaji wa Sabato
pamoja na maadhimisho ya Siku zote zilizoamriwa ambazo ni Sikukuu za BWANA,
Miandamo ya Mwezi pamoja Siku nyingine zote Takatifu kama zilivyoandikwa na
kuagizwa kwenye Maandiko Matakatifu. Pia walitaka kuwa Yerusalemu iteuliwe kuwa
ni mahali zitakapotunziwa zaka ndipo askofu au papa (maaskofu wote wakuu
inaonekana waliitwa papa kwa kweli
hasa ilipokuwa neno hilo linatumika kwa mambo ya kidini) ndipo akiwa na mamlaka ya
Roma, aliamuru kufanyike mauaji ya kuwakomesha na kampeni hii ya mauaji haya
ililengwa hasa kwa ndugu wa karibu wa familia ya Kristo, hujuma iliyoanza tangu
mwaka 318 na kuendelea (soma jarida la Bikira Mariamu na Familia ya Yesu Kristo (Na. 232)
[The Virgin Mariam and the Family of Jesus Christ (No. 232)].
Haratati na vuguvugu la imani ya Kuyunitarian hata
hivyo chini ya usimamizi wa Eusebius na akiwa kama msemaji wao, ilirudishwa
nyuma kiushawishi miaka miwili na zaidi baada ya Mtaguso huu wa Nicea hasa
tangia 0mwaka 327. Mafundisho yao yakajakuitwa baadae na kujulikana kama Uarianism, lakini Arius alikuwa pia ni
mzee-mwangalizi na hakuwepo hata kwenye Mtaguso huo wa Nicea. Hata hivyo
alikuwa anatajwatajwa sana na wataalamu wa uchabuzi wa imani za dini.
Mafundisho aliyoyashikilia na kuyafundisha hatimaye yalipewa jina la Uarianism,
yaliyoitwa kutokana na uumbaji wa Roho Mtakatifu na Kristo, hayakuimarika kutoka
kwenye maandiko yoyote ya Arius au kwenye harakati zake (soma jarida la Usocianism, Uarianism na Uyunitarianism (Na. 185) [Socinianism, Arianism
and Unitarianism (No. 185)].
Mfalme Constantine alibatizwa katika imani ya
Kiyunitariani na Eusebius alipokuwa taabani kifoni kitandani kwake. Alikuwa
amekwishafanikiwa harakati zake za kuliunganisha taifa lote likawa upande wake,
akiwa ni mfalme wa dola yote nzima na kukiweka kiti chake cha enzi cha ufalme
wake huko Constantinople mwaka 331. Alifariki mwaka 337. Watoto wake watatu,
yaani Constantine II, Constantius II na Constans, waligombania urithi wa ufalme
wake na Constantine II aliuawa vitani huko Aquileia, alipokuwa anapigana na
ndugu yake Constans, mwaka 340. Ndipo dola ikagawanyika tena vipande viwili,
upande wa Magharibi ikatawaliwa na Constans na Constantius akawa Mfalme wa
upande wa Mashariki tangu mwaka 340.
Mwaka 360 Wahuns aliishambulia
Ulaya, wakashambulia maeneo yanayojulikana siku hizi kama Urusi mwaka 376. Mwaka 361 Julian mkengeufu alijaribu kuyapokea
mafundisho ya kipagani au kile linachojulikana kama upagani kwenye Dola ya Rumi
lakini alishindwa.
Wahuns
baadae walikuwa ni wa Scythian Horde. Waliiharibu Asia Ndogo baada ya kifo cha Theodosius
mwaka 395, na wakati huo huo wakiwa kama wa Visigoths chini ya Alaric aliyeinuka
kutoka Moesia na Thrace. Alaric akafanyika kuwa Liwali wa Mashariki ya
Illyricum mwaka 398 (soma kitabu cha H.H., Vol. VII, p. 6). Katika karne ya 9,
Wahuns waliingia Ulaya wakiingia kupitia Danube ambapo Waslavs wakawasukumia upande
wa kaskazini (ibid., p. xvii). Baadhi ya watu hawa walijichanganya na
Wajerumani wa asili ya Kiasia huko Ulaya kama tabaka la jamii kuu ya Waariani,
na pamoja na Wagoths, ‘kabila’ linguine la Waarian (huenda lilitokana na mchanganyiko
wakiwemo Waguti wa kwenye Biblia) walioenea maeneo mengi ya wakazi wa Ulaya na
makabila yake pamoja na yale ya maeneo ya Mesopotamian.
Horde wa
Wascythian haikuwa taifa moja, bali ulikuwa ni mjumuisho wa makabila mengi
mbalimbali. Uundwaji wa mataifa ya Wascythian ni somo linguine tofauti. Etzal (au
Attila) waliyakusanya mataifa haya yaliyokuwa na woga mkubwa mwanzoni mwa karne
ya 5 na wakaishi maeneo ya ukanda wa kushoto wa Danube na hatimaye upande wote
wa Kaskazini mwa Ulaya. Hata hivyo Wahuns waliondoka Ulaya kwenye karne ya tano
na wakalenga waweke makazi yao tena Mashariki mwa Ulaya mwanzoni mwa karne ya
tisa, na waungane na makabila mengine zaidi ya upande wa mashariki.
Mwaka 364 nusu ya upande wa Mashariki mwa
Dola ya Kirumi, kutoka Danube hadi mpaka wa Uajemi, ilikuwa chini ya Mfalme
Valens, ambaye alikuwa ni Myunitarian. Wakati huu, kile kinachojulikana sasa
kuwa ni Kanisa la Katoliki au la Kidunia na la Kiafidhina lilikuwa ni la
Kiyunitarian, isipokuwa tu kuwa liligubikwa na matendo na imani za kipagani
huko Roma na na likayakumbatia matendo ya kipagani ya imani na ibada za Wahellena
waliokuwa wanamuabudu na kumtumikia mungu Attis upande wa Magharibi na Adonis
upande wa Mashariki wakiwaita kwa kutumia kivuli cha jina la Yesu Kristo (soma
jarida la Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235) [The Origins of Christmas and
Easter (No. 235)]. Nusu ya upande wa magharibi tangia Caledonia
hadi kaskazini magharibi ya Afrika zilikuwa chini ya Valentinian I. Valens anasemekana
kuwa alikuwa anaainhiza makabila ya kaskazini kwenye Uyunitarian (iliyoitwa
Uarianism), lakini mwaka 378 alishindwa vita na kuuawa na Wavisigoths huko Adrianople
huko Thrace. Nafasi yake ya ufalme ilichukuliwa na mzaliwa wa Hispania
aliyeitwa Theodosius, ambaye alikuwa ni Muathanasian wa kwanza au Mbinitarian
aliyewahi kuwa mfalme ambaye hatimaye alikuja kuwa ni Mtrinitarian kuwahi
kuketi kwene kiti cha enzi cha ufalme akiwa amechaguliwa na Gratian.
Aliwafukuzwa Wapicts na Wascoti na kuwatoa huko Uingereza mwaka 370, lakini
mwaka 383 majeshi ya Warumi yalianza kuichukua nchi ya Uingereza. Wakiwa chini
ya uongozi wa mfalme Magnus Maximus majeshi yalivuka mpaka na kuitwaa Gaul na
Hispania.
Hakukuwa na mfalme Mtrinitarian kuwahi kuketi
kwenye kiti cha enzi cha ufalme hadi ulipofika mwaka 381, wakati imani ya Utatu
ilipoanzishwa huko Costantinople kwa shinikizo na mateso makubwa yaliyofanywa
na mfalme Theodosius. Walikuwa wote Wayunitariani hadi mwaka huu wa 381 mali ya
kipindi cha Julian na ukengeufu wake.
Ukiri huu wa imani ya Kiyunitarian umetuama kwenye teolojia iliyoelezewa
kwenye Zauri 45:6-7 na Waerania 1:8-9. Wateteadini wa mwanzoni kama vile kina
Irenaeus wa Lyons aliishikilia na kuiamini hadi karne ya pili. Teolojia hii
iliaminiwa na kukubaliwa na Wagoths, Wavandals,
Waalans, Wasuevi, Waheruli, Waingereza, Walombards, Wajerumani na makabila yote
ya upande wa kaskazini (soma pia jarida la Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake
Duniani (Na. 243) [The Pre-Existence of Jesus Christ (No. 243)] kuhusu ukiri wa imani ya Wagoths). Ilitokana na mafundisho ya wanateolojia
na wanafunzi wa mitume ambao walikuwepo kipindi cha karne nyingi tayari kabla
ya Mtaguso wa Halmashauri Kuu ya Nicea mwaka 325 BK, wakati wengi wa maaskofu
hawa walikuwepo. Mafundisho ya kizushi ya Wabinitariani yalitangulia kipindi
cha kuitishwa kwa Mtaguso huu.
Mwaka 381 Utrinitariani ulitangazwa rasmi kwenye Mtaguso wa Costantinople
kutokana na teolojia ya Basili Mkapadokian, Gregory wa Nyssa na Gregory wa
Nazianzus. Kuharibiwa kwa imani kulikofanywa na Wayunani na Warumi ulikuwa umeanza
kuchukua mkondo wake. Watrinitarian kwa makosa na bila kujali uadilifu waliuita
ukiri huu wa imani kuwa ni Uarianism, wakikusudia kuashiria kwamba mafundisho
yao yalikuwa ni ya zamani zaidi na kuwa mafundisho haya yalianzishwa tu na
Arius katika karne ya nne. Watrinitarian hatimaye walifanya mbinu chafu za
makusudi za kuwaita wasaidizi wa mafundisho ya Uyunitarian (Uarianism) na
hatimaye Eusebius wa Nicomedia (Ueusebianism) na maaskofu wengine waliokuwa wa
cheo kikubwa sana na Arius (ambao hata hawakuwepo huko Nicea, ili wamshuhudie
tu kwa kumzidia umahiri wa kimashiko wa imani yake). Watrinitariani
wakawashutumu Waarians kwa kushikilia
kuwa Roho ndiye aliyemuumba |Mwana, ambavyo kwamba haya ni mafundisho ya Wafillioque yaliyoendelezwa kutoka
kwenye Mtaguso wa Toledo, na Wakatoliki wenyewe katika karne ya sita. Hata
Wayunani yalikataa na kupuuza mafundisho haya. Watu waliyoyaita mafundisho haya
kuwa ni ya Arian, basi wanawezekana kuwa wamefanya hila za makusudi au basi
huenda hawaelewi vya kutosha kukijua kile wanachokisema.
Theodosius
Mkuu (392-395) aliiunganisha tena dola, ile iligawanyika tena na warithi wake kina
Honorius na Arcadius mwaka 395.
Mwaka 382 Theodosius I aliwaruhusu tena
kuishi kwenye dole yake watu wa kabila la Visigoths ila walikuwa bado ni
Wayunitarian. Ilidhaniwa sana kuwa wafalme, hasahasa Valens, aliyeyaingiza
makabila ya kaskazini kwenye Uyunitariani na sio kwenye Utrinitarian. Makabila
ya Goths, Vandals, Alans, Suevi, Heruli, wote walikuwa ni Wayunitarian kama
yalivyokuwa makabila ya Wateutons na kulikuwa na idadi ya maskofu kadhaa kutoka
makabila yaliyokuwa wanaamini Uyunitarian huko Nicea. Wahemunduri wa Kijerumani
walibakia kuwa Wayunitarian hadi kwenye karne ya nane.
Wahermunduri walikuwa
ni kabila la Kijerumani (baadae waliitwa Wathuringians tangu mwaka 420 BK) na
walilimiliki eneo kubwa la Ujerumani ya kati. Ukristo wa Kiyunitaria ulilifikia
kabila hili ukiletwa na wa Visigoths na Frisians. Walipinduliwa na Wafaransa mwaka
531 na waliingia kwenye Ukatoliki mwaka 742 na Boniface, Muanglo-Saxon kutoka
kwenye juhudi za kwanza za Wakatoliki Wafaransa. Hatimaye Boniface aliuawa na
Wafrisians (754), alipokuwa anatembelea mara yake ya tatu, huenda ni kwa ajili
ya uzushi wake, kama walivyoikaataa kabisa teolojia ya Kitrinitarian kwa mara
yake ya kwanza (716) jaribio lake la pili (719).
Lakuvutia sana ni
kwamba kabila hili lilichukua jina lake kutoka kwenye kabila la kale la
Wakaldayo waliokuwa na mapokeo au utamaduni wa Kibabeloni. Waliitwa Wahermunduri,
maana yake ni “watu wa Her au Er", ambalo limechukuliwa moja kwa moja
kutoka kwene Hadithi za mwanzoni za Er kutokana na kuabudu kwenye imani ile.
Kitecho cha kuwaita watoto wa Herman ni alama ya watu hawa hata leo, kama
lilivyo tendo la kuwaita wanaume Malcolm kutoka Milcolm, Mungu Moto au wa Moto
wa Wawakanaani ambaye anaendelea bado kujulikan a kwa Waceltiki. Tunaweza
kuwaita watu hawa kuwa “watu wa Uru”. Kwa hakika wao ni watu waliomchanganyiko
wa Waashuru na Waajemi, waliorithi kwa kuzaliwa imani ya dini ya Kibabeli,
ambayo hatimaye ilikubalika kwenye itikadi syncretikia ya kidini huko Roma,
ambayo imerokea kwenye chanzo kimoja. Licha ya Wajerumani kuwa ni kabila dogo
la Waajemi kama Waherodotus walivyotunza kumbukumbu yao, wanaonekana kuwa ni
mmeguko mkubwa wa Waashuru na Wakaldayo au watu wa Uajemi. Waanglo-Saxon na makabila
yaliyokuja pamoja nao kutoka Maashariki ya Kati wanaonekana kuwa ni masalio ya
Dola Kuu ya Waparthian ambao walishirikiana na Yuda na yakawa katikati ya Waajemi
na Dola za Warumi, hadi karne ya pili ya zama hizi. Wanaonekana kuwa walikuwa ni
wa nasaba ya Kiaebrania na wanadai kuwa wao ni miongoni mwa yale Makabila Kumi
Yaliyopotea ya Israeli ambayo yalikwenda kuishi hapo, kaskazini mwa Araxes, mwaka
722 na Waashuru. Hawa wanaoitwa Mamajusi kwenye maandiko ya Agano Jipya huenda
walitokana na watu hawa.
Wagoths
na Wavandals: Shinikizo mbaya
Alaric
akawa mfalme wa Wavisigoths na mnamo mwaka 396 aliishambulia Ugiriki. Kwa ajili
ya kuziheshimu sheria za biblia, alizibomoa sanamu za miungu ya kipagani zilizokuwepo
huko na halafu anadhaniwa kkuwa aliuteka
pia mji wa Athens na hatimaye pia Balkans mwaka 398. Mwaka 401 waliishambulia
Italia kwa mfululizo hadi mwaka 403. Mwaka 406 Gunderic (406-428) akatawazwa
kuwa mfalme wa Wavandals. Katika mwaka huohuo Ufalme wa Waburgundian wa Worms ulianzishwa.
Makabila ya Wateutonic yote yalikuwa ni ya Wayunitarian. walombards wanaonekana
kuwa na uzao unaohusiana na Waango-Saxons na walitawanyika kutoka kwao upande
wa kaskazini waliendelea kuelekea upande wa Ulaya, wakielekea upande wa kusini
kuelekea ukanda wa kaskazini mwa Danube yapata takriban mwaka 500. Walienea kutoka
huko kutokana na vita, wakahamia pia kwenye maeneo ya kaskazini mwa Italia.
Waostrogoths
walijaribu kushambulia, lakini walisimamishwa ama kuzuiwa na Stilicho mwaka
406. Hata hivyo, Wavisigoths wakiwa chini ya Alaric waliuteka na kukamia mji wa
Roma, lakini alikufa alipokuwa njiani
kuelekea kusini na alizikwa pembezoni mwa Mto Busento karibu na Cosenza. Tendo
hili hatahivyo, liliyalazimisha majeshi yaliyosalia ya Warumi yaondoke kutoka
Uingereza ili yakailinde Italia mwaka 410.
Wagoths walishamiri upande
wa Mashariki au Ostrogoths na upande wa Magharibi au Visigoths, na kwa pamoja
walikuwa ni sehemu ya Waguti (au ni |Wamassagetae?) Goths Mkuu zaidi. Watu wa Guta
au Waguta hapo mwanzoni waliishi maeneo ya karibu na Tigri na kaskazini mwa
Akkadia. Makundi ya Waguti na walio na nasaba ya makabila haya ni jambo lisilo
bayana. Mwelekeo wao wa kuelekea Ulaya utajadiliwa baadae mahali penyinepo,
kusema kwamba watu wengine wenye asili ya Wagoths walielekea upande wa kusini
mwa Caspian na waliweka wachukue mahala pa Wamedi. Dini za kale huko Danube
zinaonekana kuwa ni za wale waliojulikana kama Wayunani wa Hyperboreans, wakiwa
ni wakoloni wa kwanza kabisa wa Kiscythian wa Ulaya "mbele ya pepo za
kaskazini". Istlahi za majina ya Celts
na zama kale za Wahiti kama Wahatinau Wakalti waliojulikana kama Wayunani na
Wacelti kama Wakeltoi hawakufanyika hivyo kwa nasibu. Jambo hili litaelezewa
kwa kina kwenye jarida linalowatathimini hawa Waceltiki [amoja na historia yao na
chimbuko lao. Pia Wadanes na Waswedes nao kwa kipindi cha karne kadhaa wamekuwa
wakijulikana kama Wadanea waliotokana na Wagoths wa huko Scandinavia, ambao jina
lao linatokana na Dan mwana wa Humelus.
Hawa Ostrogoths pia
waliishi kwenye maeneo au nchi inayojulikana siku hizi kuwa ni Yugoslavia baada
ya kifo cha Valens mwaka 378 na hatimayhe walihamia Roma. Mwaka 395 Visigoths
ambayo ilikuwa imejiunga au kuungana na Dola ya Rumi, waliasi wakiwa chini ya Alaric
huko Moesia na Thrace na Alaric akafanyika kuwa liwali wa Mashariki mwa Illyricum
mwaka 398 (soma kitabu cha H.H, Vol. VII p. 6). Walizuiwa na Stilicon Mvandal akisaidiwa
na Dola, lakini ilikuwa inaongozwa na Waathanasius, kwa kipindi hiki na
Theodosius mzaliwa wa Uhispania, aliyekufa mwaka 395 huku aliwa amejitwalia
ma,laka ya kuitawala Dola ya Rumi na Kanisa. Mnamo mwezi Desemba 31, 406 BK ndipo
Vandals, Sarmatians, Alans, Suevians na Alemanni, pamoja na Huns wakiwa
wanarudi nyumbani. Walivuka Rhine na Vandals wakiongozwa na Suevians kutoka Pannonia,
wakipitia njia yha Gaul iliyoko Hispania ambako waliweka kambi na kuishi mwaka 411
katika Galicia na Asturia. Hispania iligawanywa kwa kupigiwa kura na Suevian mwenye
mchanganyiko wa Teutons akashinda Galicia na sehemu kubwa ya Leon na Castille.
Baetica iliangukia kwa Vandals na ilipewa tena jina la Vandalusia. Magharibi
mwa Alans, waliojiunganao tena huko ni Uhispania, ikaishinda Lusitania, lakini
hatimaye uliangamia na kujumuishwa na Vandals na jina lao likapotea. Wasuevi
walipigana na Vandals na wote wakaungana kupigana na Goths, wakati Wagoths
Waarians walipigana wa Wakatoliki/Waroman
Wafaransa na pia Waburgundians. Makabila yaliyokuwa kwenye mrengo wa Kiyunitarian
huko Hispania yalipigana na Waheruli (wa Ostrogoths) na wenyewe kwa wenyewe.
Wasuevi wakaishi maeneo ya Galicia na sehemu ya Leon na Ureno baada ya kupigwa
na kushindwa na Wagoths. Wareno ndiyo hawa wa Teutons (wanaoitwa Germanic) wa
Vandal Alans Kusini na Suevi upande wa Kaskazini akitiwa nguvu na Carthagineans
Mfoenike ambaye ni Myunitarian wa kwanza na ambaye hatimaye mapokeo ya Kiislamu.
Wasuevians wametofautiana na Waallemani kwa kuwa waliishia kuwa kama
makundi mawili ya kitaifa. Wasuevans walikuwa na asili ya Waalleni (pia
Waalemani). Kabila lilikuwa na uasili wa Wasuevian hadi miaka ya 201-211,
wakati walipokutana pamoja kama “Wanaume wote” baadae kwa Waallemani. Gibbon
(Vol 1, p. 104, col. 2) anasema:
“Jeshi la haraka la
wanajeshi wa kujitolea liliungana kidogokidogo kwenye taifa kubwa na kudumu, na
kama lilivyoundwa kutokana na makabila mengi mbalimbali, waliojiita la
Waalemanni, au Watu wote:..”
Kundi la magharibi ndipo lilikwenda huko
Hispania na kuweka makazi yake huko Ureno, ambako Waalan ambao walikuwa ni
kundi linalohusiananao walikwendaa pia. Sehemu ya watu wa Ukoo wa Ufalme wa
Yuda walifanya makao yao pia huko. Jambo hili linaelezwa kwa kina kwenye
jedwali la vizazi lililpo kwenye wavuti wa http://www.ccg.org/_domain/Abrahams-Legacy.org/.
Kuongeza kwa wanaume wa kazi za kujitolea walioongezwa kwenye kabila hili
waliokwenda pia huko Uswizi na wakaunda chimbuo la Waswizi. Hili kwa kweli ni
masalia ya kabila la Benyamini lililoongezwa na ambalo hatimaye liliunda
muungano wenye nguvu kupitia mstari wa damu ya wanawake.
Wavandals waliweka kamazi yao huko Hispania, na
Wahispania walikuwa ni Wayunitasrian. Wavisigoths waliushinda ufalme wa Vandali
huko Hispania mwaka 416. Kwa hiyo maeneo yote ya kaskazini na magharibi
walikuwa ni Wayunitarian. Ilisemekana pia kwamba Italia ilikuwa ni ya mrengo
huu wa Kiyunitarian. Mnamo mwaka 418 Wafaransa waliishi kwenye sehemu fulani ya
Gaul. Na katika mwaka huohuo, Theodiric I akafanika kuwa mfalme wa Visigoths.
Mnamo mwaka 425 hawa wanaoitwa wababarians ambao kwa kweli walikuwa ni
Wayunitarian walioishi maeneo karibu yote, waliweka makazi yao kwene majimbo ya
Warumi. wavandals walikuwa kusini mwa Uhispania, Wahuns walikuwa huko Pannonia,
Waostrogoths (na hatimaye Waheruli) walikuwa huko Dalmatia na Wavisigoths na
Wasuevi waliishi kaskazini mwa Ureno na Hispania. Wahuns wa Ulaya walibakia
huko Pannonia hadi mwaka 470 walipjiondoa kutoka
Ulaya.
Kama tulivyoona hapo juu, Wahuns wanaonekana kuwa
waliondoka na kuhamia kwenye kingo na kujiunga ushirika na Wakhazars, na
wakasalia kule hadi walipoutamalaki Pannonia tena baada ya 800, pamoja na wale
ambao ni kirasmi waliwasaidia Wayahudi na Wakhazars. Uwezekano hauwezi
kukanushika kuwa kwamba Wasabato wa
Transylvania kwa hakika walikujakuwa ni sehemu ya horde ya Wahuns kutoka
Khazaria na Levedia na zilikuwa ni sehemu ya Makanisa yaliyoanzishwa upande wa
Mashariki tangu mwanzo na mitume kupitia dola ya Parthian (sawa na kitabu cha
Grun, The Timetable of History, 3rd
ed., Touchstone, 1991, p. 30) (pia sawa na nukuu za bango kitita
yaliyochukuliwa na Cox kutoka kwa R. Samuel Kohn, na kuandikwa kwenye jarida la
Wasabato wa Transylvania, [1894], CCG Publishing, 1998)
Mwaka 425, Valentinian III akafanyika
Mfalme wa upande wa Magharibi mwa Dola ya Roma chini ya uangalizi wa mama yake
Galla Placidia. Gaiseric (428-477) akafanyika kuwa malme wa Vandals mwaka ule.
Mwaka 429 Wapicts na Wascots walifukuzwa kutoka
kusini mwa Uingereza na Waangles, Saxons na Jutes. Mwaka 457, kwenye mapigano
ya Crayford, Wajutes wakiongozwa na Hengest waliwashinda Waingereza na kuikalia
Kenti ambako wapo hadi sasa. Mnamo mwaka 429 Aetius waziri mkuu wa mfalme
Valentinian III akafanyika kuwa mtawala halisi wa upande wa Magharibi mwa Dola
ya Rumi (429-454). Mwaka huohuo, Gaiseric alianzisha ufalme wa Vandal wa
Kaskazini mwa Afrika. Mwaka 443 akaichukua sehemu ya mwisho ya dola ya Warumi
upande wa Kaskazini mwa Afrika na Afrika ikawa chini ya utawala wa
Wayunitariani tena.
Mwaka 433 Attila (d. 453) akafanyika kuwa kiongozi
na mtawala wa Wahuns. Mwaka 436 majeshi ya mwisho ya Warumi yaliondoka
Uingereza. Na mwaka huohuo Wahuns wakauangusha na kuuhusuru kabisa Ufalme wa
Waburgundian wa Worms. Waburgundians walikuwa ni sehemu kuondolewa kwao
kikatili huko Ulaya, kazi iliyofanywa na Waanglo-Saxons na Walombards na
makabila mengine yanayoonekana kama ya horde za Waparthians.
Mwaka 443 Waalemanni Wakijerumani (Wajerumani wa
Kisiwzi) wakaweka makao yao huko Alsace.
Mwaka 453 Attila wa Huns alifariki na
Theodoric II (453-466) akawa mfalme wa Wavisigoths hadi alipouawa na ndugu yake
Eric (466-484) ndiye alimrithi. Hii ilifuatiwa na kushambulia au mashambulio ya Roma mwaka 455 na Wavandals.
Ukweli wa mambo ulikuwa ni kwamba Wavandals walikuwa ni Wayunitarian.
Walizivunja sanamu za kipagani zilizopewa majina yanayoitwa ya Kikristo
wakionssa mambo hayo kuwa ni machikizo na uvunjaji wa amri ya pili ya Mungu. Neno
la Uvandalism linatokana na kitendo
hiki. Kitendo cha kuzivunja na kuzibomoa kwa kweli kilikuwa ni agizo la
kibiblia lililoagiza tuvivunje na kuharibu vinyago na sanamu zote za kipagani.
Theodoric Mkuu alifanyika kuwa mfalme wa Ostrogoths
tangu mwaka 471-526.
Mashariki mwa Doma ya Rumi, kwa wakati
ule, walikuwa ni Theodosius II (d. 450), Marcian 450-457), Leo I (457-474). Mwaka
457 Childeric I (457-481) akafanyika kuwa mfalme wa Salien Ufaransa. Mwaka 460 Wafaransa
wakautwaa mji wa Cologne. Wavandals pia waliungamiza manowari ya Warumi wa Cartagena
kwenye mwaka huohuo.
Migongano iliyojitokeza Ulaya kote kwa kweli
chanzo chake kilikuwa ni kuhusu kabila gani litakalokuwa limezungushiwa maeneo
gani ya Ulaya. Ingawa walikuwa ni Wayunitarian, lakini bado waliongozwa na watu
walafi na haya ndiyo yalikuwa wasiyokuwa wanayafanya.
Wafalme wa mwisho kutawala upande wa Magharibi mwa
Roma katika kipindi cha tangu mwaka 461 walikuwa ni Severus (461-465); Athemius
(to 467); Alybrius (to 473); Glycerius (to 474); Julius Nepos (hadi 475); na
Romulus Augustulus (hadi 476). Dola ya Magharibi ilifikia mwisho wake kutokana
na udhaifu wa wafalme wake. Mjerumani Odoacer (433-493) alimkamata na kumuua Orestes
huko Placentia na hatimaye akamuua mtoto wake Romulus Augustulus na akatangazwa
kuwa mfalme wa Italia.
Kwa hiyo, Dola ya upende wa Magharibi ya Roma
ililetwa karibu, pasipo kuanzishwa kwa Kanisa Katoliki na bila ya sera
inayojulikana kwa Ulaya.
Kukomeshwa
kwa Dini za Kimagharibi
Mwaka 474 Zeno alifanywa kuwa Mfalme wa Magharibi
ya Dola ya Roma (474-491). Shule za Watrinitarian
zilikuwa zimeendelezwa sana na kuwezeshwa upande wa Magharibi mwa Dola tangu
kipindi hiki, na Uplatonist Mamboleo ulianzishwa na Proclus akafanyika kuwa
kiongozi au mkuu wa chuo cha Kiplatonist huko Athens mwaka 476. Imani ya
Utrinitarian ilianzishwa na kurekebishwa kwene Mtaguso wa Chalcedon mwaka 451. Mgawanyiko
uliopelekea kuanzishwa kwa Kanisa la Wacoptic wa Misri ulianzia wakati huu.
Mwaka 483 Papa Simplicius alirithiwa na Felix III (-492). Mwaka 484 kwenye
tukio la kumtenga kutoka kwenye ushirika Patriarch Acacius wa Constantinople kulipelekea
mafarakano ya kwanza wa makanisa yaliyoamini Utrinitarian ya upande wa
Magharibi na Mashariki (484-519).
Mwaka 489 Mfalme Zeno wa upande wa Mashariki
aliiangamiza shule ya Kikristo ya Wanestorian ya huko Edessa na akalijenga
kanisa la Mt. Symeon Stylites karibu na mnara wake. Mwaka 491 kanisa la Waarmenian
lililazimishwa kufanya uhusiano wa karibu na Byzantium na Roma na mwaka 498 Wanestorians
waliweka makazi yahoo huko Nisibis iliyoko Persia. Kanisa lililokuwako kutoka Yerusalemu
hadi Armenia halikuwa la Kitrinitarian
Diphysite na lilikuwa ni la watunza Sabato. Pia lilikuwa ni hazina na la kutegemeka,
huko Edessa, na maandiko ya Kiaramu na liliuwa na Biblia ya toleo la Kipeshitta,
hadi lilipokomeshwa. Utunzaji wa Sabato na mafundisho yake vilienea hadi kufika
mbali huko Uchina na kanisa la kwanza kutoka upande wa mashariki (soma jarida
la Mgawanyo Mkuu wa Makanisa Yanayozishika Sabato (Na. 122) [General
Distribution of the Sabbath-keeping Churches (No. 122)].
Mapapa kwa kipindi hiki tangu kifo cha Felix
III, walikuwa ni Gelasius (492-496); nad Anastasius II (hadi 498) na Symmachus
(hadi 514). Gelasius akakinndika na kukitambulisha Gelasian Missal, Kitabu cha maombi, na kusifu na kuelekeza au
kuongoza kwenye ibada Madhabahuni na Meza ya Ushirika. Mwaka 499 sinodi ya Roma
ilitangaza amri wakati wa uchaguzi wa papa na mwaka 500, ibada za kufukiza
uvumba zilianzishwa kwenye ibada za makanisa ya Kitrinitarian kwa mara ya
kwanza na kwenye kila kanisa la Kikristo.
Mateso
Mwaka 476 Gaiseric mfalme wa Vandals aliliuza eneo
la mashariki mwa Sicily kwa Theodoric mfalme wa Visigoths. Wayunitarians wakiwa
chini ya Hunneric mfalme wa Vandals alianza kuwa na msimamo unaopingana na wa
Wakatoliki, ambao walijiondoa kwenye muafaka wa kuvumiliana hadi leo, kukiwemo
msamaha wa wazi wa ibada za sanamu. Mabishano ya Wayunitarian na Watrinitarian sasa yakapelekea kuanza rasi kwa
mateso.
Malengo
na dhamira ya Watrinitarian au Waikatoliki/Wahathinina yalilenga kwenye wale
waliokuwa dhaifu au kuwadhoofisha na Uyunitarian ukomeshwe na kuondolewa mbali
kabisa. Hii ilikuwa ni pamoja na mkakati wa kubadilisha hali ya kuwasaidia
Wasalien wa Ufaransa. Mwaka 481 Childeric I alifariki na nafasi yake ikarithiwa
na mtoto wake Clovis (hadi 511) ambaye ndiye alikuwa mwanzilishi wa nguvu za wa
Merovingian. Mwaka 484 Hunneric mfalme wa Vandals alirithiwa na mjomba wake Gunthamund
(hadi 496). Mwaka 486 Clovis alimshinda Syagrius aliyekuwa liwali wa mwisho wa
Warumi huko Gaul. Roma haikuwa na nguvu tena huko Gaul.
Mara tu baada ya tukio hili, huko Armenia, maasi
yaliyoongozwa na Vahan Mamikonian yalitokea tangu mwaka 481-484 na ushindi huu
uliliunusuru uhuru wa kidini na kisiasa huko Armenia. Uhuru huu pia unaonekana kuwa
ni wa muhimu katika kuyasaidiwa makanisa yanayozitunza Sabato kuanzishwa na
Wapaulicians waliokuwa wakiishi kwene Milima ya Taurus. Wapaulicians walikuwa
bado wanapatikana pende za mashariki katika karne ya kumi na tisa. Kizazi chao
kinafikia idadi ya watu takriban milioni au zaidi, aliteswa na kuuawa kwenye
maeneo ya Armenia baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Walikuwa idadi
inayokadiriwa kuwa kati ya millioni moja ua mbili ya Wasabato waliuawa baada ya
uharamisho uliofanywa Bektashi Uislamu baada ya mwaka 1927. Mchakaio huu wa
mateso ma mauaji uliendelezwa kupitia mauaji ya kuangamiza maarufu kama Holocaust
huko Ulaya na mnamo mwaka 1953 na kufa kwa Stalin.
Kuunganishwa
na kuunganishwa Kwa Ulaya
Kipindi
hiki pia (487-493) Waostrogoths waamini Uyunitaria walianza harakati za kuiteka
Italia. Theodoric alimshinda Odoecer Mjerumani kwenye mapigano yaluyofanyika
kwenye Mto Isonzo na tena karibu na Verona (489). Mwaka 493 Odoace r walisalimu
amri kwa Waostrogoths na aliuawa na Theodoric ambaye hatimaye alianzisha ufalme
wa Ostrogothi wa Italia na alimuona dada wa Clovis. waostrogoths waliitamalaki Malta
tangu mwaka 494-534. Mwaka 500 Thrasamund alimuoa dada wa Theodoric ana alipewa
kutawala magharibi mwa Sicily kama mahari.
Katika mwaka huohuo wa 500 Wajerumani wa
jamii ya Marcomanni huko Bohemia waliivamia na kuishambulia Bavaria na walipokuwa
wanaivamia, Waczechs waliingia na kukaa huko Bohemia
Mwaka 493 Clovis alimuoa Clothilda, Mburgundian ambaye
alikuwa ni binti wa mfalme aliyemfanya aingie kwenye Ukristo wa mrengo wa
Kiyunitarian mwaka 496. Aliwashinda Waalemanni karibu na Strasbourg mwaka 496 na
hatimaye akabatizwa na rafiki yake Remigius, au Remy, askofu wa Rheims.
Mwaka 506 Alaric II alianzisha Sheria
iliyojulikana kama Lex Romana
Visigothorum lakini mwaka 507 alilemewa na kushindwa vita na kuuawa na Clovis
kwenye Mapigano ya Campus Vogladensis (Vouillé, karibu na Poitiers). Clovis hatimaye
wakaungana na ufalme wa Wavisigothic wa Toulouse. Ufalme wa Wavisigothi wa Castille
ya Zamani uliendelea hadi mwaka 711. Eneo hili la Toulouse lilibidi libakie
kuwa eneo kubwa la Wasabato au Kanisa la Wayunitarian wanaozishika Sabato haki
kipindi cha Vita vya Kidini au Crusade ya Waalbigensian na kipindi cha
Kudhuriwa wapinga mafundisho cha Counts wa Toulouse.
Hawa Wavisigoths
pia waliitwa Wabonosonians inaonekana
walitokea maeneo ya Bonosus ya Sardica waliofundisha (kutoka kwenye maandiko ya
Biblia na historia) kwamba Yusufu na Mariamu walikuwa na watoto wengine.
Mafundisho haya yanaonekana kuwa ni mafundisho ya kudumu ya historia ya kanisa
zima la watunza Sabato, yaliyotokana na fafanuzi za Agano Jipya na majina ya
ndugu wane wa Kristo waliojumuishwa pale na kutajwa kwa dada zake, kama ilivyo
pia kwenye historia za (Mathayo 13:55; Marko 6:3; sawa na jarida la Bikira Mariamu na Familia ya Yesu Kristo (Na. 232) [The Virgin Mariam and
the Family of Jesus Christ (No. 232)]. Tukilinganisha na Marcellus na Photius tunapata
dalili kuwa walikuwa ni watu wenye nia moja wakiwa ni watunza Sabato na Torati
(sawa na linavyosema jarida la Migawanyiko Mikuu ya Makanisa Yanayozishika Sabato (Na. 122_ [General
Distribution of the Sabbath-keeping Churches (No. 122), uk. 2)]. Mji wa Sabadell ulio kaskazini
mwa Uhispania pia ilitokana na Wasabato au watunza Sabato.
Wavisigoths waliweka
makazi yao huko Aquitaine tangu mwaka 418 kama shinikizo dhidi ya Vandals na Alans
Mwingingereza Constantinus aliyeweka makao yake huko Arles. Waingereza hawakuutarajia
Ukatoliki hadi bada ya kutangazwaau kuwekwa kwa Sinodi ya Whitby mwaka 664 BK huko
Hilda's Abbey, walipoketi mkutano wa kujadili wakisema:
"namna anayoitumia
papa kuhesabu au kupanga siku ya kusherehekea Easter ni kama ishara ya mamlaka
kamili ya jumla ya Wakristo wa Roma. Inaweza kuonekana kama maamuzi yameenda na
kufanyika kwa kuwapendelea Waceltiki au Kanisa la Wairish na maadhimisho yao ya Easter lakini
wanailinda tarehe ya kizamani ya Kiceltic kwenye sinodi ya Whitby ilikuwa na matumaini
ya kweli madogo ya kufanikiwa. Mfalme (Oswiu)
aliyekuwa kiongozi kwenye sinodi alimuoa malkia (ndinti wa Mfalme Edwin
aliyeitwa Eanfled) ambaye alikuwa amelelewa huko Kent, na ambaye alikuwa
amekwisha iadhimisha Easter ya Wakatoliki" (David L. Edwards, Christian England, vol I. p.57).
Edwards anadai
kwamba wnwo kubwa ya kusini mwa Ireland wameikubali tarehe mpya iliyowekwa ya
kuadhimisha Easter. Kwa kweli walikuwa ni Wakwato-desiman, waliokuwa wanaishika
Pasaka na Idi ya Mikate Isiyo na Chachu na jambo hili limetathminiwa kwa kina kwenye
jarida la Mwanzo wa Kanisa la Kikristo Nchini Uingereza (Na. 266) [Origin of the
Christian Church in Britain (No. 266)] (sawa
na pia ilivyoandikwa kwenye jarida la Migongano ya Kwrto-sediman (Na. 277) [The
Quartodeciman Disputes (No. 277)]. Askofu Colman alirudi
zake Iona baada ya kuachana na jambo hilo, ingawa Chqad na Cedd walimthibitisha
kama alivyofana Tuda askofu mpya wa Northumbrian, ambapo yeye mwenyewe alikuwa
ni Muairish ya Kusini, na Mueata wa Mwiingereza, Abbot wa Lindisfarne, ambaye
alifundishwa na Aidan (Edwards, ibid.). ni makosa ya kuelezea kwa mtu akisema
kwamba hay yalikuwa ni mabishano yaliyohusu tu tarehe ya kusherehekea Easter.
Mabishano yalikuwa ni kwa sababu ya kuishika ama kuiadhimisha Pasaka ya
Wakwortodesiman pamoja na mlolongo wake wote unaofuatia mazingira yake ya
kimaadhimisho ya Pasaka, ama kuchagua kuadhimisha sikukuu ya kipagani ya
Easter, iliyopewa jina lake kutokana na mungu Ishtar au Astarte au Ahtoreti, au
mungu mke wa Kikaldayo aitwaye Easter. Maadhimiso ya sikukuu hii yalijumuisha
tukio la Kifo au maombolezo ya Msiba yaliyofanyika siku ya Ijumaa, na Jumapili
iliyofuatia kuliadhimishwa tukio la Ufufuo na ilijumuishwa na sikukuu ya majira
ya baridi ya miungu waliojulikana kwa mujina ya Attis na Adonis, na mwingine
aliyejumuishwa baadae aliyeitwa Tamuzi aliyetajwahata kwenye kitabu cha nabii Ezekieli (kwenye Ezekieli
8:14).
Mabadiliko hayo
yaliyojumuisha maadhimisho ya Sabato na Sikukuu ya Vibanda pia. Na kwa kweli,
yalihusu hatima ya mabadiliko kalenda nzima yote ya Waceltiki na kuingiza
sheria ya ulaji wa cyakula. Edwards aliona kwamba waliyzshika maagizo zu desturi
zote za Wakristo wn zamani. Wairish wa kaskazini walidumu kwa kiasi kikubwa
kwenye utaratibu wa tarehe za zamani kama walivyofanywa wale wa Iona hadi mwaka
716 (ibid., sawa na majarida ya Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235); Ndama wa Dhahabu (Na. 222) na Wajibu wa Amri ya
Nne Katika Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayozishika Sabato (Na. 170) [The
Origins of Christmas and Easter (No. 235); The Golden Calf (No. 222) and The Role of the Fourth Commandment in the Historical Sabbath-keeping
Churches of God (No. 170)].
Utaratibu wa kuweka
tarehe ya kusherehekea 'Easter' ulibuniwa na Victorius wa Aquitane, kwa kweli
ulikuwa unaigwa tu kidogokidogo. Gaul aliuiubali imani mpya mwaka 541, huenda
inaweza kuwa ni matokeo ya kushindwa kwake na Wayunitariann pale, na Edwards
anathibitisha hilo kwenye ukurasa wa 38. Kwa kweli ilikuwa ni mkono wa chuma au
ukatili na shuruti ndiyo ndiyo uliosababisha Waceltiki wawe sasa ni waungaji
mkono wa imani ile..ambavyo walipigana kwa nguvu zote kuipinga. Kwa kweli,
Ireland ilitolewa kwa Uingereza na papa katika karene ya kumi na mbili, kwa
hila ya makusudi yas kukomesha masalia yaliyokuwepo huko ya wanaoamini katika
utunzanji wa Sabato ambayo yado ilikuwa inaadhimishwa na watu wa huko. Hali hii
kwa kiasi kikubwa ililetwa kwa kushirikiana na wafalme wa Ki-Irish wa wakati ule
na tamaa au mpano au mkakati waliokuwanao Wakatoliki wa kuachana na imani ya
kibiblia upande wote wa kaskazini. Mtu muhimu aliyetwishwa mkakati huu alikuwa
ni Malachy askofu wa Armagh (soma jarida la Papa wa Mwisho: Kama Alivyoelezewa na Nostradamas
na Malachy (Na. 288) [he Last Pope: Examining Nostradamus and Malachy (No. 288) kuhusu unabii huu mkuu)].
Kulikuwa na
makubaliano huko Whitby tu kwa kuwa patano la kukomesha vita la Waanglosaxon
lilifuatia majadiliano nao mwaka 598 kufuatia ujio wa Augustine mwaka 597 (tazama
kitabu cha Neill, S. Anglicanism,
p.11). Wangles 10,000 waliingia kwenye sherehe za Krismas huko Kent wakiongozwa
na Mfalme wao Ethelbert. Uingereza haikuwa imejikita yote kwenye Ukatoliki
kipindi hiki hadi kufikia mwaka 716 BK I ingawaje mwaka 786 papa wa kwanza alitangulia
kuwasili akikusudia kushawishi uwepo na mwendelezo wa matendo na imani za
kipagani (ibid., p. 45). Waraka uliotoka kwa Alcuin kumpelekea Etherhard, Askofu
Mkuu wa York, ulielezea kwamba baadhi ya watu walikuwa wanabeba hirizi za
kishirikina na 'kwendanazo milimani ambako wanafanyia iada, si kwa kwenda
kufanya maombi, bali kwenda kulewa na vileo' (kutoka kitabu cha Edwards ibid.).
Wakatoliki walianza
kuimiliki Hispania ya Kati. Wahispania wpte walikuwa ni Wayunitarian wengi wao
tangu wakati huu na wafalme wa Wavigothic Toledo walisaliwa washupavu kwenye
kile kinachojulikana kuwa ni imani ya Arian
au Uarianism ikiwa ni dini ya Kitaifa
na Askofu wa Taledo Primate wa Hispania. Kutoka kwenye imani ya Kiyunitarian ya
Kikristo na Uislamu, Hispania ikawa mrengo wa Watunza Sabato Wayahudi na
Wakristo pia hadi kipindi cha Inkwisisheni mnamo karne ya 13. (Udadisi wa imani
ya Waarian ulikuwa ni kwamba kalenda ilianza miaka 38 kabla ya tarehe inayoaminika
sasa na iliendelea hadi karne ya 11). Tangu mwaka 573 nchi iliweza kuwa na
maendele akuunganisha tena na wale walioitwa ama kujulikana kama Waarian wakawa
kwenye uthibiti wa Warumi na kutawaliwa nao. Mwaka 586 Wavigoths wote na kwa
kiasi kikubwa wanaingia na kuwa Wakatoliki. Mnamo mwaka 590 Roma ikajiundia
utaratibu wake wa kidini ya kifalme.
Wanahistoria wanatofautiana
na kwa kweli wamesababisha kujikanganyika kitabu cha fasiri cha Kikatoliki
kinachoitwa Catholic Encyclopedia kwa suala linalohusiana na uwekaji makazi upande
wa Afrika Kasakazini mwaka 427-429, wakiwa na wanajeshi takriban 80,000 wakiongozwa
na Genseric, lakini Malkia au Mtawala wa kike Placidia inawezekana kuwa
aliwapeleka Wavisigoths na Vandals hadi Afrika ili kupinga na kuyazima maasi ya
Count Boniface mwaka 427 BK. Walifuatana na Maximinius, Askofu wa Kiyunitarian.
Ilimpasa Augustine awatetee kwa wazi Waathanasians mwaka 428 BK. Ni dhahiri
kabisa kwamba Wayunitarian wa Goths na Vandals walikuwa vitani na Waathanasian
(ambao baadae walikujakuwa Warumi) Wakatoliki wa huko Roma isopokuwa ni kwa
ajili ya amani mwaka 435-439, tangu mwaka 429 na waliweka makazi yao huko Roma
mwaka 455. Hii ilikuwa ni dhahaka ya maombi ya Malakia au Mtawala wa kike Eudoxia,
aliyemuomba Genseric kummuweka huru kutona kwenye ndoa aliyoichukia na Mfalme Petronius
Maximus.
Kutoka uwekaji
makazi huu wamapema hawa Vandal na mwendo wao wa mapema wakipitia huko Gaul
mmoja kati ya miji yenye miungu mingi ya ajabu kwa kipindi kile, bado imani na
matendo ya Wakatoliki na Waathanasius yalijipenyeza. Wavandals walikuwa
Wayunitari na na kwa hiyo kuwa ni wapinzani na walizidharau ibada za sanamu na
vinyago zilizokuwa na imani kamilifu yenye kufanana huko Roma na uingizaji wa syncretic
na imani au sanamu za kale za kipagani na vinyago vyake. Hizi kwa kweli
zilibomolewa na hapo mwanzo na Gaul mwaka 409-411 na alipokuwa anawasili
Hispanoa, Afrika, na tena huko Roma. Walichukuliwa kuwa kama wapagani wakibarbarians
na kutokana na tendo hili ndipo neno ubabariani lilitokea, lakini kwa kweli
walikuwa ni wa wapingaji waliodharau na kuchukia ibada za sanamu za syncretics.
Walitaka kuiangamiza Roma pia kwa kile walichoichukulia kuwa ni mji wa waabudu
sanamu, lakini waliuacha kutokana na ombi la Leo la tarehe 2 Juni 455.
Kwenye kitabu chake, Dr. Peter Heylyn (History of the Sabbath[Historia ya Sabato], London 1636, Part 2, para. 5, pp. 73-74) anasema kwamba mji wa Milan ulikuwa wa Washika Sabato tangu zama za kale kufuatia na matendo ya kimashariki.
Wakati huohuo, mnamo mwaka 510 Jimbo, sehemu ya kusini magharibi mwa Ufaransa, lilienda kwa Waostrogothshadi mwaka 563. Ukweli huu unaonyesha sababu gani iliyopelekea Wasabato wote walikuwa pande za kusini mwa Ufaransa, kaskazina mwa Uhispania, na kaskazini mwa Italia. Wakristo waliitunza Sabato hadi ilipofika karne ya tano na wakati wa Jerome (yapata mwaka 420) Wakrito waliojitoa na kuwa waaminifu walifana kazi za kawaida siku za Jumapili (kwa mujibu wa Dr. White, aksofu wa Ely, kitabu chake cha Kuikomesha Siku ya Sabato [Treatise of the Sabbath Day], p. 219; sawa na kitabu cha Augustine wa Hippo, cha NPNF First Series, Vol. 1, pp. 353-354 na jarida la Mgawanyo Mkubwa wa Makanisa ya Watunza Sabato (Na. 122) [General Distribution of the Sabbath-keeping Churches (No. 122), p. 2)].
Mwaka 511 Clovis, mfalme wa Urafansa alifariki na ufalme wake uligawanyika miongoni mwa watoto wake wanne; Theodoric I (mwaka 534); Chlodomer (mwaka 524); Childebert I (mwaka 558) na Chlothar (mwaka 561) na walianzisha mahakama huko Soissons, Paris, Metz, na Orleans kwa umakini mkubwa. Kipindi hiki pia jumba la watawa ya huko St Césaire iliyoko Arles ilianzishwa pia. Maisha ya Useja au Umonastiki yalikuwa pia yameanza kuchukua mkondo wake katika kuiendeleza imani ya Utatu au Utrinitarian.
Mwaka 523 Thrasamund mfalme wa Vandals alifariki dunia na nafasi yake ilirithiwa na Hilderic (hadi mwaka 530). Mwaka 524 Sigismund aliuawa na Chlodomer, mwana wa Clovis I. Waostrogoths alijenga kile kinachojulikana kama Baptistery ya Kiarian ambayo leo inajulikana kama Bapstery ya S. Maria huko Cosmedin, Ravenna mwaka 525. Hata hivyo, mwaka 526 Theodoric Mkuu alifariki na alizikwa huko Ravenna. Binti yake Amalaswintha akawa liwali wa Italia (hadi mwaka 534).
Mwaka 527 Justinian I akaf anyika kuwa Mfalme wa Byzantine (hadi mwaka 565) na mlolongo wa matukio ya kurudi nyuma na migongano na migawanyiko ilitokea kwa Wagoths na Wavandals na ndipo kanisa la Wayunitarian lilidumu kwa muda mrefu hadi mwaka 590. Ni tukio la kustusha sana la kurudi nyuma kwa hali ya juu kuwahi kushuhudiwa katika historia ya watu wa Ulaya kuwaona Wafaransa wakijiunga na imani ya Utrinitaria, kama ukweli huu ulivyodaiwa kuwa ndiyo fursa iliyopelekea kuazishwa kwa Kanisa la Roma huko Ulaya. Kama isingekuwa Wafaransa basi kusingekuwepo na chochote. Tutaliona hilo sasa kwashuruti pasi na huruma kuendelea hadi kutangazwa kwa Dola Takatifu ya Rumi mwaka 590 na dola hii ilidumu kwa kipoindi cha miaka 1260 hadi ilipotawanyika au kuparaganyika mwaka 1850.
Vita vya Mwisho hadi
kuinuka kwa Uislamu na Dola \Takatifu ya Rumi
Mwaka 529 Justinian aliifunga shule ya Wanafalsafa wa Kiyunani iliyokuwa dumu kwa miaka takriban 1,000 huko mjini Athens. Kitendo hiki kilidaiwa kupata maelekezo yaliyolenga kuupa nafasi Upagani lakini kililazimisha syncretisasheni ya Waplatonists Mamboleo na iliwalazimisha kwa shuruti kubwa Maprofesa waende Uajemi na Syria ambako wawe huko, kuanzia mwaka unaofuatia na kuendelea, amri iliyotolewa na Chosroes I (531-579), waajemi wakanufaika na kitendo hiki kwa kufikia upeo wa juu zaidi wa kimasomo. Mkakati huu ulitekelezwa kwa kitovu cha masomo hadi kwenye kile kilichokuwa kinajulikana kama ulimwengu wa Kiislamu, wakati ilipounda kanre iliofuatia kwa kuonyesha muendelezo wa Utrinitarian wa Constantinople.
Mwaka 532 Wafaransa waliuangusha ufalme wa Burgundy, ambao ulifumika maeneo yote ya Ufaransa, Uswizi na Austria. Pia jemadari Belisarius alikiokoa kiti cha ufalme cha Justinian kwa kuyazuia na kushinda uasi wa Nika huko Constantinople. Aliukumbuka mwaka uliopita baada ya kufukuzwa kwake aliposhindwa na kufukuzwa na Waajemi. Mji wa Costantinople hatimaye ulijengwa tena. Mwaka 533 Belisarius aliupindua ufalme wa Vandal na kuifanya Afrika Kaskazini kuwa ni Jimbo la Byzantine. Mwaka 534 Toledo ulifanywa kuwa ni mji mkuu wa ufalme wa Wavisigoths ya Yunitarian huko Hispania (hadi mwaka 711). Mwaka 535 Belisarius aliutwaa ufalme wa Waostrogothis wa Italia na akabakia hadi mwaka 540. Kiendo hiki kiliruhusu Jimbo liende kutoka kwa Waostrogoths hadi kwenye ufalme wa Wafaransa na Naples ikawa sehemu ya Dola ya Byzantine.
Tangu mwaka 539 hadi 562 Dola ya Byzantine ilikuwa
vitani na Waajemi. Vita hii ilimfanya Totila wa Waostrogoths kukomesha utawala
wa Byzantine huko Italia mwaka 540 na kuwa mfalme mwaka 541 wakati alipokufa
mjomba wake Hildebad (hadi mwaka 552). Mwaka 546 Totila aliingia Roma (na
kuondoka tena mwaka 547). Katika mwaka ule, Adouin mwenyeji wa Lombard akaanzisha
kizazi kipya cha Lombard na akautadaza au kuueneza utawala wake hadi maeneo ya
mbali kwenye Mto Save. Mwaka 550
Totila aliushinda tena Roma na Wayunitariani walirudi tena madarakani. Na
katika mwaka huohuo, uingiaji wa Waturuki wa asili ya Waras upande wa Magharibi
ulianza na makabila ya Waslav yaliweka makazi yao huko Mecklenburg.
Wapoles waliishi magharibi mwa Galicia, na Waukrainians
waliishi mashariki mwa Galicia. Kwenye mwaka huohuo pia, Wawelsh waliongoka na
kuingia kwenye Ukristo kwa ushuhuda wa David na watunza Sabato wakaanza kuingia
huko Wales, ambako hawakuweza kufukuzwa kabisa huko hadi kufikia karne ya kumi
na moja. Maisha ya ndoa kwa makasisi yaliendelea hadi mnamo karne ya kumi na
mija hivi. Columban, mmishenari wa Kiairish huko Ufaransa na Italiay (550-615),
pia alihesabu tangu mwaka huu. Kengele zilitumika makanisani huko Ufaransa kwa
mara ya kwanza tangu mwaka huu pia, zikitumika kwa lengo la kuwavutia Watrinitarian
syncretic kuja ibadani huko Ufaransa.
Mwaka 543 maandiko ya Origen yalilaaniwa na
kupigwa marufuku na Justinian. Ingawa Origen alikuwa na asili ya kupenda na
kuamini Ukwasi-Nostiki, bali maandiko au vitabu vyake pamoja na Hexapla vilikuwa
muhimu pia. Tendo hili lilikuwa ni mkakati wa mafundisho ya kimapokeo ya
wapinga Sabato ambao pia ni Watrinitarian upande wa Mashariki. Mfalme Theodora alifariki
mwaka 548.
Mwaka 551 nyambizi
ya Waostrogoth ilipigwa na Wabyzantines. Totila mfalme wa Ostrogoths aliuawa
mwaka uliofuataia na wa Byzantines wakiongozwa na towashi Narses (mwaka 478-c.
573) kwenye mapigano ya Taginae. Mwaka 553 Narses ndipo alijiunga na Naples na
Roma kwa Byzantine na alimteua Exarch wa Italia, kuwa mtu wa cheo kikubwa sana
jeshini una kwenye mamlaka ya kijamii. Kiti cha ufalme cha askofu mkuu Maximian
pia kilianzishwa huko Roma katika mwaka huu.
Mwaka 558 Clothar I mwana wa Clovis aliuunganisha
tena ufalme wa Ufaransa ambao uliishia hadi ilipofikia mwaka 561 wakati
ulipogawanyika tena chini ya watoto wake Charibert, Guntram, Sigebert na
Chilperic. Mwaka 563 Mmishonari wa mrengo wa Waceltiki wa Sabato aliyeitwa
Columbia, alijitangaza kutawala Kisiwa cha Iona na alianza kuwaingiza kwenye imani
Wapicts.
Mwaka 565 Justinian I alifariki dunia na nafasi
yake ilichukuliwa na mrithi wake ambaye pia alikuwa ni mjomba wake Justin II (hadi
mwaka 578). Kisha Lombards aliwafukuza Wabyzantines kutoka kaskazini mwa Italia
waende kusini, lakini akawaacha huko Ravenna. Audoin alirithiwa na mtoto wake Alboin
aliyewasaidia Waavars, kuuangusha ufalme wa Wagothiki wa Gepidae wa nyanda za
chini za Vistula, na mnamo mwaka 568 alianzisha ufalme wa Lombard kaskazini na
katikati ya Italia.
Mwaka 567 Leovigild mfalme wa Visigoths (hadi
586) aliwafukuza Wabyzantines kutoka Magharibi ya Uhispania na kuishinda na
kuiteka Hispania yote mwaka 585. Ufalme wa Ufaransa ulikuwa pia umegawanyika
kitakaba, upande wa Waaustrasia ukijumuisha Walorraine, Ubelgiji na ukanda wa
kulia wa Rhine na Neustria (Ufaransa) na Burgundy.
Mwaka 570 Muhammad mwanzilishi wa Uislamu
alizaliwa. Mwaka 572, vita kati ya Waajemi na Wabyzantines ilianza tena na
iliendelea ikiongozwa na Chosroes II baada ya kilichodaiwa kuwa kupaa kwake
mwaka 590 hadi 628, na Uislamu alianzishwa mwaka 632. Mnamo mwaka 632 mgawanyiko
wa kisiasa ambao hatimaye utasababisha kuwepo kwa Vita Kuu ya III ya Dunia
ulianza.
Mwaka 573 watoto wa Clothar kina Chilperic na
Sigebert walienda vitani.
Mwaka 590 Authari mfalme wa Lombards alirithiwa
na Agilulf (hadi 615) na papa Pelagius II alirithiwa na papa Gregory I aliyeitwa
Mkuu. Aliitanga Roma kuwa ni Dola Takatifu. Mwaka 591 Columbanus (hadi 543) aliwasili
huko Brittany akitokea Ireland. Gregory alimtuma Augustine kuwa mmisionari huko
Uingereza mwaka 597 aliyembatiza Ethelbert huko Kent na ilifuatia kushamiri kwa
imani ya Ukatoliki huko Uingereza.
Mnamo mwaka 600 mashambulizi ya magharibi
mwa Ulaya yalifanika. Katika mwaka huu huu, Wakhazars walianzisha ufalme au
dola yao katikati ya nyanda za chini za Volga na nyanda myanda mwa Don. Waczechs
na Waslovaks waliweka makazi huko Bohemia na Moravia na Yugoslavs huko Serbia. Ulaya
ikafanyika imara na wakati huohuo dhaifu sana. Hata hivyo, matokeo mengine ya
ghafla ya “mchakato” huu yalikuwa kwamba utaratibu wa kudurufu wa Italia
ulibadilika na kuchukuliwa na muaji ya kutisha katika mwaka 600 na ugonjwa wa ndui
ukaingia kusini mwa Ulaya ukitokea India kwa kupitia Asia Ndogo.
Kwa kuiimarisha Ulaya, Watrinitarian waliweka
nguvu zao pamoja kwa kuweka mgawanyo wa vyeo na madakahuko Ulaya kwa nguvu za Wafaransa
na Waangles na ulafi au tamaa yao. Mwaka 600 Gregory aliazisha programu ya majadiliano ya amani na Wayahudi. Ndipo akaanzisha au kuamuru kiandikwe kitabu cha
mtindo wa picha ili kitumike mahala pa Biblia kwa wasiojua kusoma. Biblia ya
Wagoths inayokadiriwa kuwa iliandikwa mwaka 351. Biblia hii ilikataliwa na
haikuaminika, na hatimaye iliondolewa kabisa kutoka kwenye maeneo ya wazi ya
Roma hadi tangazo la kuifana Roma kuwa ni Dola Takatifu mwaka 1850. Mwaka 603 watu
wa Lombards walijiunga kwenye Ukatiliki wa Roma. Mwaka 609 Mantheon ya Roma
iliwekwa wakfu kuwa kanisa la Kusini S. Maria Rotunda.
Kwenye mkakati wa kuiunganisha Ulaya,
ndipo Utrinitaria ulligeuza macho yake kuitazama Asia Ndogo. Kuongezeka kwa
Ulaya na Byzantium kuliona uwezekano uliokuwepo wa kwamba matokeo yake yatakuwa
ni kuja kwa umbo la Uislamu.
Ukristo wa Kiutrinitarian ulijipenyeza hadi Urusi mwishoni mwa karne ya kumi, ukiletwa na Waorthodox wa Kiyunani wa Constantinople. Inawezekana sana kuwa huenda haya yalikuwa ni maamuzi ya kisiasa tu, ikichukuliwa kwamba Wakhazars wa kusini na kupitia Ukraine kote huko hadi Ulaya wote walikuwa ni watunza Sabato na Wayunitarian, kwa dini zote mbili, yaani Wayahudi na Wakristo. Na pia kulikuwa na Wabulgars waliofika huko kwa wakati huohuo kama walivyofika Wahuns katika karne ya kumi. Na ndivyo ilivyo kuwa kulikuwa na Wapaulicians waliokuja tena kuishi huko Trace wakiongozwa na Constantine Capronymus katika karne ya nane na baadae na John Tsimiskes katika karne ya tisa (soma jarida hilohilo (Na. 122). Kwa kweli inawezekana kabisa kuwa kwamba maamuzi yote yaliyofanyika kuhusu jinsi gani imani itakavyokuwa ya Wakristo wa Ulaya yamefanyika kwa kuzingatia mtazamo wa kisiasa na hayana uhusiano wowote na masuala ya imani iliyoanzishwa na Yesu Kristo na kama inavyoonekana au kufunuliwa kwenye maandiko ya Biblia.
Katika miaka ya 1260 tangu mwaka 590 hadi 1850 Kanisa Katoliki la Roma limejenga teolojia yake kwenye mambo ya uwongo, iliweka msingi wake kwenye Falsafa za Kiyunani na imani za kipagani za ibada na miungu. Kuchukua kwao Kalenda ya kipagani na imani zake kuliitumbukiza imani ya Kitrinitariani kwenye mgongano na kila kabila na watu waliokuwa nazo, au kusoma, au waliojifunza Biblia na Torati au Sheria za Mungu.
Matokeo yake, ili kulinda mamlaka yao, wakaanzisha mkakati wa kuwatesa watu kitaifa na kimataifa na kuwadhoofisha au kuwanyamazisgha, ambao ulipelekea kuteswa na kuuawa na kuwekwa kwa mamilioni ya sheria za usalama zinazowahusu wakazi walioko barani Ulaya na katia Asia Ndogo (na hatimaye huko Marekani). Uvamizi na mashambulizi yake huko Mashariki ya Kati kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Vita ya kuitetea Dini yaani Crusades imeshudia kusababisha muwako wa hasira na chuki dhidi ya Uislamu kiasi ambacho kwa sasa umeikumba zaidi ya nusu ya wakazi ulimwenguni. Karne ya ishirini imeshuhudia vita hivi vikiendelea dhidi ya sheria za amani zinazowazuia wakazi na wazawa wa Ulaya, kwa mauaji yaliyoratibiwa na kufanwa kwa makusudi ya kuangamiza halaiki ya watu maarufu kama genocide waliyofanyiwa Wayahudi na Wakristo watunza Sabato wa Ulaya. Jambo hili limefafanuliwa na kuchambuliwa vizuri kwenye jarida lisemalo Mauaji ya Kuangamiza Halaiki ya Watu, Siri yake Imefunuliwa (The Holocaust Revealed).
q