Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[271]

 

 

 

PAULO:

Sehemu ya 1 Paulo na Torati

(Toleo La 1.0 20090909-20090909)

 

Jarida hili ni ya kwanza kati ya mlolongo wa majarida kati ya yale yanayohusika na nafasi ya Paulo na mtazamo wa yale aliyokuwa akiyafundisha na kipindi zama cha kihistoria alichohudumu. Paulo alikuwa ni baba mwanzilishi wa kanisa la sasa. Kiongozi mahiri, aliyeteswa mara nyingi na kushambuliwa kwa ajili ya mafundisho yake, aliliongoza kanisa katika kipindi cha misukosuko. Kama isingekuwa mafundisho ya Paulo na miongozo yake, wengi wasingeweza kuelewa utata uliopo wa asili ya kustaajabisha ya asili ya Mungu na ya asihi mwana wake aliyemtuma kwetu. Kwenye jarida hili tunashughulika kumuelezea Paulo na msomamo wake kwenye Torati.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 2009 Storm Cox and Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Paulo na Torati

 



Huyu Paulo Ni Nani

Juna asilia la Paulo hapo mwanzo lilikuwa ni Sauli ndlo alilopewa.

Matendo 13:9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema...

(Tafsiri ya RSV ililitumia mahali pengi ila pale tu ilipokuwa lazima ndipo hailitumii.)

 

Matendo 9:11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;

 

Sehemu ya kwanza kulitaja jina hili la Sauli ni kwenye kitabu cha Matendo, mapema kabla ya kuongoka kwake kwenye tukio la kuuawa kwa kupigwa mawe kwa Stefano.

Matendo 7:58 wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli

 

Matendo 8:1a inasema “Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake”.

 

Akitokea kabila ya Benyamini, Paulo alilelewa akiwa ni Muisraeli. Alikuwa ni wa madhehebu ya Mafarisayo.

Wafilipi 3:4b-5 Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. 5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,

 

Paulo alifundishwa kazi ya utengenezaji wa wa mahema.

Matendo 18:1-3 Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho. 2 Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akila, mzalia wa Ponto; naye amekuja kutoka nchi ya Italia siku za karibu, pamoja na Prisila mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi, naye akafikilia kwao; 3 na kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema.

 

Paulo alikuwa na uraia wa Taso ya Kilikia, na alisomea mjini Yerusalemu (Matendo 26:4).

Matendo 22:3 Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; (pia nsoma atendo 9:11; 21:39)

 

Alikuwa na hati ya uraia wa Rumi pia.

Matendo 22:25-27 Hata walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye hajakuhumiwa bado? 26 Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi. 27 Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo. (sawa na inavyosema pia matendo 16:37)

 

Pia alikuwa ni mwanachama wa Baraza la kidini la Wayahudi.

Matendo 26:10 10 nami nikayafanya hayo Yerusalemu; niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na wakuu wa makuhani; na walipouawa nalitoa idhini yangu.

 

Paulo alilitesa na kulitawanya kanisa na wengi walitiwa gerezani.

Matendo 8:1b,3 Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume. 2 Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu. 3 Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.

 

Matendo 9:1-2 Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, 2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.

 

Matendo 22:4-5 nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake. 5 Kama Kuhani Mkuu naye anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipokea barua kwao kuwapelekea ndugu wale, nikaenda Dameski, ili niwalete wale waliokuwa huko hata Yerusalemu, hali wamefungwa, ili waadhibiwe.

 

Paulo alikuwa mtu mwene bidii sana kwenye mapokeo ya dini ya Kiyahudi ambayo yalienezwa na dhehebu la Mafarisayo na ambalo Kristo alikuwa akilishutumu.

Bilashaka hii ilikuwa ndiyo sababu kwa yeye kuwachukia Wakristo kwa kuwa dini hii ilikuwa inashutumu imani hii ya Mafarisayo hasa kuhusiana na mapokeo yaliyokanganya kwa kiasi kikubwa tafsiri halisi ya Kiroho la Torati ya Mungu.

 

Wagalatia 1:14 Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. (sawapia  na Wafilipi 3:5; Matendo 22:3; 23:6; 26:5)

 

Kristo alikuwa na maneno haya ya kusema kuhusu mapokeo haya ya wazee ambayo yaliendelezwa na Waandishi na Mafarisayo kwa kusema: “Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,  basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu. Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.  Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.” (Mathayo 15:3; Marko 7:6-7; Isaya 29:13). Mungu alisema kupitia nabii Isaya kwamba atayakomesha mapokeo haya. Paulo hakuwa ameelewa bado madhumuni au nia ya Mungu kupitia kwa Yesu Kristo na Kanisa. Kwa ajili hii, na makosa ya kimafundisho, alilitesa na kulidhulumu kanisa kinyume kabisa na maagizo ya Torati ya Mungu huku akidhani kwamba yu sahihi kwa mujibu wa Torati ya Mungu. Usemi na dhana ya kwamba “hakuwa na hatia kwa mujibu wa totati” kumtenga mbali kunaonyesha vilevile kwamba hakuwa anaelewa alikuwa anakiuka maagizo ya torati. Yeye ni kama Wayahudi wengi wengine leo ambao wanadhania na kujiona kuwa hawana hatia kwa mujibu wa torati lakini huku wakitenda dhambi na kumkana Kristo aliyewaokoa. Wakati alipoitwa aje kwenye utumishi, ndipo alipouelewa wito wake. Alijiona kuwa hakuwa na dhambi wala hatia chini ya torati lakini hatimaye akagungua kwamba alikuwa ameihalifu torati kwa kupitia mapokeo na akayachukia. Jambo hili aliliona na kulionyesha wazi kwenye mafundisho yake kwenye Warumi 3:9,10,19,20,23 na Wagalatia 3:10-12.

 

Hata hivyo, kila ilipombidi Paulo alitumia mkazo wake kwa kutumia mapito yake ya Kifarisayo aliyoyapitia huko nyuma.

Matendo 23:6 Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu.

 

Wongofu wa Paulo

Wongofu wa Paulo haukuwa wa kuongoka kunakoeleweka kwa kuigeukia Torati na kuikiri ili kuanza kuishika na uiona umuhimu wake. Yeye alikuwa ni mtu anayeishika kwa bidii na moyo wake wote, pamoja na mapokeo yote, lakini alipaswa kuonyehswa uhusiano uliopo kati ya imani na sheria nah ii ilikuewa ndiyo sababu kuu ya kuandika na ndiyo hasa ujumbe au maana kuu ya maandiko au waraka kwa Wagalatia.

 

Wongofu wake ulikuwa ni kwa ajili ya kujua mamlaka na maagizo makuu ya kiroho kwenye imani. Kusudi kuu na la kwanza na la mwisho la Sheria yote ya Mungu ulielekezwa kwenye Amri Kuu Mbili.

 

Mathayo 22:37-39 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

 

Paulo anaelewa lengo hili. Kusudi la huduma hii, na kwa hiyo ndiyo yetu, ilikuwa ni kuzihubiri amri hizo mbili zote kwa kuwa kama tutazishika hizo zote, hatutaweza kutenda dhambi na sheria ndipo haitatuhusu sisi.

 

Kama hatutamwibia jirani yetu kwa kuhofia kutiwa mbaroni na kufungwa jela, bado tunakuwa wezi, lakini ni kwamba tu hatufanyi hivyo kimatendo. Bali kama tutampenda jiraji yetu, hatutaweza kufikiria kumuibia kwa kuwa hatutapenda kuwataabisha na kuwaona wakipata mateso. Kwa hiyo kama tutampenda jirani yetu, sheria inayohusu wizi, udanganyifu au usingiziaji, kutamani na kumfanyia maovu, nk, haitatuhusu tena kwa kuwa hazijaingia mawazoni wala aikilini mwetu. Na ndiyo maana ya usemi alioutoa wa “wamekufa kutokana na sheria”.

 

Watu wengi wanapenda kujipa haki wanapovunja sheria wakisingia kwamba Paulo aliacha kushika sheria na wanawafundisha wengine wafanye hivyo. Watu hawa wanahatia ya makosa makubwa.

 

Paulo na Sheria

Matendo 20:5-16 inasema:

Ila watu hao wamekwisha kutangulia wakamngojea Troa. 6 Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba. 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane. 8 Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika. 9 Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa. 10 Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake. 11 Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hata alfajiri, ndipo akaenda zake. 12 Wakamleta yule kijana, yu mzima, wakafarijika faraja kubwa sana. 13 Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukaabiri kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimu kwenda kwa miguu. 14 Alipotufikia huko Aso, tukampakia, kisha tukafika Mitilene.15 Tukatweka kutoka huko, na siku ya pili tukafika mahali panapokabili Kio; siku ya tatu tukawasili Samo, tukakaa Trogilio, siku ya nne tukafika Mileto. 16 Kwa sababu Paulo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka, akitaka kuwahi Yerusalemu siku ya Pentekoste, kama ikiwezekana.

 

Hapa tunamuona Paulo na wenzake wakiadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu kisha akasariri akirudi Yerusalemu ili akaishike Sikukuu ya Pentekoste huko. Hii ilikuwa safari ya kupendeza kwa mtu anayenenewa kuwa amefundisha kuiondoa sheria!

 

Wapinzani wa Paulo wanatafuta kutumia andiko hili kuonyesha kwamba Paulo alikuwa anaabudu siku ya Jumapili, lakini yana maana gani hasa maandiko haya?

Tafsiri ya Biblia ya King James inasema kwene Matendo 20:7 hivi:

Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.

 

Toleo hili liliaandikwa ili kuonyesha kwamba hili lilikuwa na uhusiano mkutaniko wa kanisa na kwamba Paulo alikuwa anahubiri na kwamba uke umegaji wa mkate ulikuwa ni ibada ya ushirika wa komunio takatifu. Hata hivyo, neno linalotumika hapa kuelezea kuhubiri ni neno la Kiyunani mjadala au majadiliano linalomaanisha pia majadiliano yanayoendana na kujibu maswali kati ya watu wawili au zaidi katika kuwafundisha na kujibu maswali yao.

 

Usemi uliotumika kuelezea kuwa waliumega mkate ulimaanisha tendo la kula chakula cha kawaida tu. Neno lililotumika kuelezea juma au wiki ni sabbaton ambayo inaweza kuwa siku nyingine yoyote ndani ya kipindi hiki cha siku saba. Kwa hiyo, ni kwamba Paulo alikula nao chakula siku ya Jumapili jioni akiwa pamoja na wanafunzi wake na mazungumzo yao yaliendelea hadi usiku wa manane, kwa kuwa alikuwa anaondoka asubuhi iliyfuatia.

 

Watu wanajaribu kudai kwamba kwakuwa Paulo hakuwalazimisha waongofu wapya kutahiriwa, basi alihubiri akipinga tohara na sheria pia; lakini je, Paulo anasemaje kuhusu madai yao hayo?

 

Matendo 21:17-26

Tulipofika Yerusalemu wale ndugu wakatukaribisha kwa furaha. 18 Hata siku ya pili yake Paulo akaingia kwa Yakobo pamoja nasi, na wazee wote walikuwako. 19 Na baada ya kuwaamkua, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyoyatenda katika Mataifa kwa huduma yake. 20 Nao waliposikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati. 21 Nao wameambiwa habari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika Mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi. 22 Basi, ni nini? Bila shaka watasikia kwamba umekuja. 23 Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na nadhiri. 24 Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati. 25 Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati. 26 Ndipo Paulo akawatwaa wanaume wale, na siku ya pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza habari ya kutimiza siku za utakaso, hata sadaka itolewe kwa ajili ya kila mmoja wao. Tulipofika Yerusalemu wale ndugu wakatukaribisha kwa furaha. 18 Hata siku ya pili yake Paulo akaingia kwa Yakobo pamoja nasi, na wazee wote walikuwako. 19 Na baada ya kuwaamkua, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyoyatenda katika Mataifa kwa huduma yake. 20 Nao waliposikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati. 21 Nao wameambiwa habari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika Mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi. 22 Basi, ni nini? Bila shaka watasikia kwamba umekuja. 23 Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na nadhiri. 24 Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati. 25 Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati. 26 Ndipo Paulo akawatwaa wanaume wale, na siku ya pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza habari ya kutimiza siku za utakaso, hata sadaka itolewe kwa ajili ya kila mmoja wao.

 

Hapa tunamuona Yakobo, ndugu wa kuzaliwa na Kristo, pamoja na Wazee, waliomba kwamba Paulo afanye utakaso Hekaluni kwa mujibu wa Torati ili awathibitishie Wayahudi kwamba bado yungali anashika Torati. Habari na tukio hili ni mojawapo ya ushahidi mkubwa na wenye nguvu unaoonyesha mwendelezo wa ushikaji wa sheria kwenye Agano Jipya.

 

Kanisa halikuachwa huru kutoka kwenye umuhimu wa kuzishika na kuzitii sheria kwa kifo cha Kristo, bali ni ile tu kanuni ya utoaji dhabihu za wanyama ndiyo ilitimilizwa nay eye. Ishara ya Yona ilikuwa bado inatenda kazi au inaelea kwa miaka 40 tangu Yohana Mbatizaji na kwene huduma ya Kristo na iliishia pale Hekalu lilipobomoshwa kwa ajili ya kuasi kwao Yuda na kushindwa kwao kufanya toba kwa dhambi waliyoifanya kwa kuendelea kwao kuivunja na kuitia unajisi torati kwa ajili ya kuyatukuza mapokeo yao baada ya miaka 40 ya neema waliyopewa. Utaratibu wa Hekalu katika Yuda ulikoma kwa kuangamizwa kwake Hekalu mwaka 70 BK.

 

Kristo alisema kwenye Mathayo16:4:

Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake. Tunajua kwamba kazi ya Yona huko Ninawi iligharimu safari ya siku moja (huduma ya Yohana Mbatizaji ilifanyika kwa mwaka mmoja) na siku mbili akhubiri (huduma ya Kristo ya miaka miwili) na siku 40 za kutubu (mwaka wa 30 BK hadi 70 BK) wakati utoaji wa dhabihu za wanyama ulipokoma. Unabii wa Danieli kuhusu juma la 70 la miaka na uelekeo wa Kristo na kuashiria kwake kwenye Ishara ya Yona haukukoma hadi kuhusuriwa kwa Hekalu, kwa hiyo utaratibu ule haukuhukumiwa hadi kipindi cha neema (miaka 40) kilipowasili (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 013) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 013)].

 

Wayahudi walikuwa wanawahukumu watakatifu kwa alama onekevu kama vile tohara, ns Paulo mara moja anasema hivi: “Kama tohara inatosha, basi hatuna haja ya kuwa na Kristo”. Je, Paulo alikuwa anamaanisha kwamba tohara ilikiwa ni lazima au haina maana kuifanya? Hapana. Basi alisema tu kwamba watu wa mataifa walioitwa na kuongoka wakiwa watu wazima haikuwa lazima kwao kutahiriwa ila watoto wao waliozaliwa baada ya kuongoka kwao walipaswa kutahiriwa kama inavyoagiza torati, na ndivyo walivyofanya. Soma pia jarida la Utakaso na Tohara (Na. 251) [Purification and Circumcision (No. 251)].

 

Harakati za Yakobo Hekaluni zikukuwa sahihi na zilifuata mahudhui yote ya torati. Paulo alikuwa chini ya maelekezo ya baraza kuishika Toraati ya Mungu kwa mujibu wa sura na aya. (Matendo 21:17-40)

 

kwenye Matendo 21:24 mitume (na hasa Yakobo) walimwambia awachukue wanaume wane kisha ajifanyie utakaso pamoja nao na awalipie gharama ili wanyoe vichwa vyao (kwa maneno mengine wakamilishe au kutimiza nadhiri zao kwa mujibu wa torati, kama Paulo alivyotakiwa kukamilisha nadhiri zake alizoziweka alipokuwa Senkrae (sawa na inavyosema Matendo 18:18)). Kwa nini ilikuwa hivi? “Watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika Torati.” (RSV) (pia tazama KJV: neno Shika Sheria au Torati).

 

Mchakato wote huu ulihesabiwa kuwa anahaki na kustahili na Kristo kutoka Matendo 23:11 ambapo inasema:

Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako.

 

Kwa mtu anayenenwa na kutolewa hoja ya kwamba ameiondoa sheria, anaonekana kwa kina sana mwenyewe akiishika.

Paulo na Ndoa

Makanisa yale yanayofundisha ukasisi wa useja au wa kutooa yanapenda kumchukulia Paulo kama kigezo cha kuhalalisha hoja yao wakisema kuwa alikuwa kinyume na mambo ya kuoa ama ndoa. Watu hawa pia wanahatia ya makosa makubwa na kutokuwa sahihi. Paulo alihubiri alionyesha kutopendezewa ma hali ya mtu kuishi maisha haya ya useja na hakupenda kabisa kasisi aishi na kuhudumu akiwa hajaoa na kuweka utaratibu wa kuwa na nyumba ya wanawake wasioolewa kama bweni.

 

Kwenye waraka wa 1 wa Paulo kwa Timotheo 5:9-16 unasema hivi:

Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja; 10 naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema. 11 Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa; 12 nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza. 13 Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa. 14 Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu. 15 Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani. 16 Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.

 

Hapa Paulo anakataza kitendo cha kuwaweka mahala amoja wanawake wasioolewa wenye umri chini ya miaka 60 kwenye maisha ya nadhiri au ujane kwa kuwa watatamani kuolewa au wanaweza kuolewa tena, na kwa hiyo watakuwa wameanguka dhambini. Hii ndiyo hatia na kosa kubwa na la moja kwa moja kwenye mfumo huu wa maisha ya utawa.

 

1Timotheo iko wazi kuhusu ulazima wa kuoa kwa mtumishi apendaye kuhudumu.

 

1Timotheo 3:2 na 12

Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;  12 Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.

 

Hapa Paulo anatoa msimamo mkali sana kuhusu hili:

1Timotheo 3:4-5 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; 5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)

 

Fundisho hili ni kwa sababu nzuri. Maaskofu watahudumu makanisani mwao kwa namna hiyohiyo kwa hali sawa na tabia ile ile wanavyowatea wake zao na watoto wao. Kama wataiburuza na kuitendea vibaya familia yao ndipo watalitendea vivyoviho kanisa

 

Vivyohivyo, kama watakuwa wakizembea katika kuzisimamia familia zao kwa kuwaruhusu watoto wao wawe na uhuru wa kidunia, ndipo pia watawaruhusu ama kuwafanya watu wa kanisani wawe na mwenendo wa uhuru kama huo huo.

 

Mafundisho ya Paulo kuhusu watu kuishi bila kuoa au kuolewa yanatakiwa yatafsiriwe kwa kuangalia kwa umakini kile alichokuwa anakusudia.

 

1Wakorintho 7:8-9

Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. 9 Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.

 

Aya hizi zinatumika na makasisi waseja kama moja ya sababu za kuwahesabia haki. Hata hivyo, sheria inasema kwamba Yule anayeshindwa kuwahudumia watu wa familia yake ni mbaya kuliko akiyeamini.

 

1Timotheo 5:8

8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini  

 

Paulo aliamini huenda kwa kuwa Kristo alikuwepo kwenye tukio la wongofu wake, ambako angeweza kusulibiwa pea kama Kristo alivyofanyiwa/ hakujua kuwa wala kudhania kuwa huduma yake ingeendelea mbele kwa kipindi kirefu kama ilivyotokea kwa kweli. Bali alidhania tu wale waliokuwa kanisani waliamriwa na |kufa na Kristo wengine wasingeweza kuuawa kwa kadiri walivyojitoa kwenye jamii zao iwapo kama walikuwa wamebahatika kukubalika na jamii iliyowazunguka na wawapo hawalaumiwi na ndugu zao kwa kujitoa kwao kuwahudumia.

 

Sio watumishi wote waliohukumiwa kuuawa kama wafia dini na walitiwa moyo kuoa kama ilivyoonekana tangu mwanzoni, na kwa kweli hii ilikuwa ni muhimu na sharti moja wapo la utumishi wao.

 

Kimsingi, Paulo alisisitiza ufungaji wan do kwa waumini wote waliokuwepo kamanisani katika hali ya utawanyiko kote walikukwenda katika nchi za wamataifa waliokoishi katika mazingira magumu sana.

 

Agano Jipya linaashiria kuonyesha kwamba huenda Paulo mwenyewe hakuwa ameoa kutokana na maneno aliyoyaandika kwenye nyaraka zake.

 

Katika Warumi 16:13, Paulo anasema: Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliye mama yangu pia”.

 

Inachukuliwa na waamini useja kwamba maneno haya yalikuwa yanahusiana na hali ya maisha aliyokuwa anaishi huyu Rufo na mama yake, bali inadaiwa tena pia kwamba Rufo alikuwa ni shemeji yake na kwamba hatimaye Paulo alioa nah ii ilikuwa ndiyo msingi wa maelezo yaliyo kwenye waraka wake kuhusu kitendi cha kusafiri pamona na mke.

 

Katika 1Wakorintho 7:39, Paulo anasema wazi kwamba mke amefungwa kwa mujibu wa sheria hadi kifo cha mume wake. Kwa wazi kabisa anashikilia na kuitaja torati ya Mungu kuhusiana na nambo ya ndoa.

 

Katika 1Wakorintho 9:1 kwa wazi sana anajitaja yeye mwenyewe kama mtume na anasema kwamba hana mashaka juu ya wito wake kama mtume wa Wakorinto. Anasema kwenye 9:3-5 kuwa: “Hilo ndilo jawabu langu kwa wale wanaoniuliza. 4 Je! Hatuna uwezo wa kula na kunywa? 5 Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?

 

Kwa wazi kabisa alikuwa anasisitiza maisha ya ndoa kama sio kwa kuoa kabisa, vinginevyo mfano wake ungekuwa hauna maana yoyote. Kefa anajulikana wazi kabisa kuwa alikuwa ameoa kama Paulo anavyosema hapa.

 

Kutoka katika aya za 6-8 anaweka wazi kabisa akihusisha na ujibu wa sheria kuunga mkono mawazo haya. Kwenye aya ya 9, anainukuu Torati ya Musa kuhusu inavyokataza kufunga kinywa punda anapopura nafaka (Kumbukumbu 25:4) kwa kukazia na kusisitizia maneno yake kuhusu sharti analotakiwa kuwa nalo Yule aliyechaguliwa kulihudumia kanisa na apendaye kufanya huduma za kiroho.

 

Umoja wa Kanisa

Maelekezo na maagizo ya biblia huhusu umoja kanisani yako wazi kabisa kutoka kwenye nyaraka za mitume. Paulo pia hatofautiani nao kwa hili.

 

1Wakorintho 1:10-17

10 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. 11 Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. 12 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. 13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? 14 Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo; 15 mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 16 Tena naliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine. 17 Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.

 

Paula hapa anaelezea kuhusu uwezekano wa kuwepo ama kujitokeza madhehebu au dini zinazosisitiza tofauti ya kimadaraja ya waumini wao na hali ya kuwaona wengine kuwa bora zaidi yaw engine na kuifanya hali hiyo kuwa ni kigezo cha utaratibu kanisani na kwenye jamii zetu tangu kale. Tunaona hapa kuwa Wakorintho walikuwa wanawekea umuhimu wa kimadaraja watu waliowabatiza au waliowaweka wakfu wao, huku wakiacha kuipa kipaumbele hali yao mpya ya kiroho na wakaonyesha upendeleo kwa wale waliowabatiza. Karama zinatoka kwa Mungu, na sio kwa Yule mtu aliowabatiza. Makanisa ya Mungu ya leo yameangukia kwenye mtego huu, hususan katika kipindi kisicho cha kawaida cha miaka ishirini iliyopita, kilichojitokeza tabia ya kufuata tu amri na mtazamo wa mtu mmoja na tafsiri ya mtu mmoja. Hali hii ililiathiri sana Makanisa ya Mungu tangu kuanzishwa kwa Radio Manisa la Mungu na kuathiri kabisa mafundisho au kiteolojia ya Waadventista.

 

Paulo anasema kwenye aya ya 10 kwamba sisi sote tunanena kitu kimoja na tusiwe na migongano au mashindano kati yenu. Hii inapelekea nyuma kwenye sheria.

 

Hii ingekuwa ni sababu ya migawanyiko kanisani yanachukuliwa kama unyanyapaa au ubaguzi. Umoja kwenye mwili wa Kristo ni jambo muhimu katika imani. Watu wanaougawa nwili wa Kristo kwa visingizio vya mambo ya kiuongozi wanawajibika kwa matukio kama haya. Unabii wa uwongo ni ishara ya kutokea jambo ambalo Mungu anashughulika nalo kwene mwili. Ni kweli kwamba kuna viongozi wengi lakini Bwana ni mmoja kama anavyo fundisha Paulo.

 

Kuujua mwili kumefunuliwa kwa kupitia maafisa wake na kunawezekana kupitia michakato mbalimbali ya Roho.

 

1Wakorintho, hapohapo hadi kwenye sara ya 4, inaongelea juu ya umoja wa imani katika umoja wa kimafundisho. Kuna ukweli mmoja tu. Paulo anashutumu ibada za sanamu kwenye Warumi 1:22-25.

Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; 23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. 24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.

 

Kitendo cha kumuabudu Mungu Mmoja wa pekee na wa Kweli kinaonyesha kuwa ni muhimu sana kwenye uandishi wa nyaraka za Paulo, sambamba na uasherati. Jambo la kwanza na muhimu katika imani ni ndoa ya viumbe kwa Kristo.

 

Umoja huu wa bibi arusi na bwana arusi unafanana sawa na umoja wa kimafundisho. Mtu mmoja mmoja hawezi na hataweza kuruhusu mwanya na kufanya tafsiri ya kulitawanya au kuligawa kanisa. Kristo alikazia sheria ya ndoa ili kuachana kufanyike tu kwa sababu ya zinaa au uasherati. Kristo asingeweza kuiandaa arusi akiwa kama bwana arusi na huku akitarajia kuwepo na mtengano ama kuachana na kupeana talaka. Na ndivyo ilivyo, kwamba uzinzi au uasherati ni chukizo kubwa kufanyika kwenye ndoa na ndivyo ilivyo kuwa haupaswi uvumiliwe kanisani.

 

1Wakorintho 6:9-10,13,18:

Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.

13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.

18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.

 

Wagalatia 5:19:

Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

 

1Wathesalonike 4:2-5:

Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. 3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.  

 

Kiwango chetu kwa wapendwa wetu kimwili unahusiana  moja kwa moja na uwiano wetu wa kiuwezo wa uaminifu wetu kwa Kristo. Mambo yaliyoorodheshwa hapo juu yote yanahusiana na Torati yake Mungu. Vigezo vya makatazo vinatuama moja kwa moja na sheria. Kristo alizishika sheria au torati ambayo yeye mwenyewe aliwapa Israeli pale Sinai/ hii sio Torati ya Musa, bali ni Torati ya Mungu, iliyotolewa kupitia kwa Kristo.

 

Paulo alisema kwenye 1Wakorintho 11:1 (RSV):

Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.

 

Tafsiri ya KJV imeitafsiri aya hii kwa kusema hivi:

Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.

 

Neno mimētēs (Kamusi ya Strong’s G3401) kwa kawaida limetafsiriwa kama wafuasi lakini kwenye tafsiri ya RSV limetafsiriwa kama waigaji.

 

Kuwa mshirika wa Kanisa kunamaanisha kwamba wewe ni mfuasi wa dhehebu au dini ile, au muunga mkono wa imani ile. Kama wewe ni muumini wa imani ya Kibudha inamaanisha kuwa wewe ni mfuasi wa Budha lakini haina maana kuwa ni lazima uwe unamuiga yeye. Unaweza kuwa kwenye Kanisa la kikristo na kwa hakika unaweza kuwa humuigi wa huishi kama yeye Kristo.

 

2Th 3:7 kwa 1063 ninyi wenyewe 846 kujua 1492 jinsi 4459 yeye apasaye 1163 kufuata 3401 sisi 2248: kwa 3754 tunaamini 812 0 siyo 3756 kukosa kwetu utaratibu 812 miongoni 1722 mwenu 5213;

2Th 3:9 siyo 3756 kwa sababu 3754 tunayo 2192 siyo 3756 uweza 1849, lakini 235 kwenda 2443 kufanya 1325 sisi wenyewe 1438 mfano 5179 juu yako 5213 kwa 1519 fuata 3401 sisi 2248.

Hbr 13:7 Kumbuka 3421 wao walio na mamlaka 2233 juu yenu 5216, yeye 3748 aliyesema 2980 kwenu 5213 neno 3056 la Mungu 2316: ambaye 3739 imani 4102 fuata 3401 , tilia maanani 333 mwisho 1545 wa mjadala [wao] 391.

3Jo 1:11 Mpendwa 27, fuata 3401 siyo 3361 kile kilicho kipotovu 2556, lakini 235 kile kilicho bora 18. Yeye atendaye mema 15 ni 2076 wa 1537 Mungu 2316: lakini 1161 yeye atendaye maovu 2554 haja 3708 0 wahi 3756 kumuona 3708 Mungu 2316.

 

Neno lililotafsiriwa kama wafuasi ni hili lifuatalo:

Kamusi ya Kiyunani ya Strong’s Greek Dictionary (SGD) 190 ni akoloutheō ambalo linamaanisha:

1) kumfuata yule aliyetangulia, jiunge naye kama mshirika wake, kujiunga naye 2) kujiunga na mtu kama mwanafunzi, kuwa au kuwa kwenye mwanafunzi wake, a) kuwa upande wake.

 

Tunaamini kama Kristo alivyoamini, tukimuiga ili kwamba wale wanaotuiga au kutufuata wamfuate Kristo.

 

Watu wanasema kwamba Paulo aliiondoa sheria. Kifungu kiki kinatuobyesha kinyume. Kristo alisema kwenye Yohana 14:15:

Mkinipenda, mtazishika amri zangu.  

 

Ni kwenye amri ipi ambayo alikuwa anataabika kwayo? Alikuwa anataabishwa na Mathayo 22:37-39 kama ilivyojadiliwa hapo juu.

 

1Wakorintho 10:1-6 (KJV)

Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. 6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.

 

Agano Jipya linasema wazi kwamba Torati ilitolewa na kupewa Musa na Kristo. Kwa hiyo tunajua kwamba Paulo na wanafunzi walikuwa wazi na sahihi kwenye uelewa wao kuhusu uwepo wake Kristo kipindi kabla ya kuzaliwa kwake ulimwenguni. Paulo anasema wazi kwamba anashika sheria hizihizi ambayo Kristo aliishika. Kristo aliishika Sabato sawa kama Paulo alivyofanya.

 

Sabato

Matendo 18:4

Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.

 

Pasaka/Mikate Isiyo na Chachu

Kristo aliishika Idi au Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu, sawa na Paulo na wengine, kwa hiyo na sisi tunapaswa kuishika.

 

Matendo 12:3

Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa.

 

Matendo 20:6

Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba.  

 

1Wakorintho 5:8

basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.

 

Miandamo ya Mwezi

Wakolosai 2:16

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

 

Kwa suala la Mwandamo wa Mwezi, hapa tunamuona Paulo akiwaambia wamataifa wasione haya kushika na kuadhimisha zile zilizokuwa zinajulikana kama Sikukuu za Wayahudi ambazo sasa ni zao pia. Kristo alitilia maanani Miandamo ya Mwezi na kuichukulia kama jambo muhimu, kwa kuwa kama Paulo angeenda kinyue na kupingana na Kristo na Paulo akaishika Miandamo ya Mwezi inaonyesha kuwa Kristo alifanya hivyo pia. Aliziishika sheria na Sikukuu, na Miandamo ya Mwezi na ziliadhimishwa kwa uaminifu mkubwa kwenye imani au dini ya Kiyahudi hadi kuangamizwa kwa Hekalu, na Kristo alikuwa ni Mfalme na ni Kuhani Mkuu aliyewekwa asiye na dhambi. Kuidai na kuamini kuwa andiko hili limeondoa umuhimu wa kuziadhimisha Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zilizoamriwa ni kutumia vibaya kabisa matumizi ya lugha zote mbili, yaani Kyunani ya Kiingereza.

 

Sikukuu ya Vibanda

Yohana 7:2

Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.

 

Kama Kristo alivyoishika Sikuuu ya Vibanda, ndivyo pia Paulo alivyofanya na ndivyo hata sisi tunavyotakiwa kufanya.

 

Matendo 18:18-21

Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Prisila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri. 19 Wakafika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sinagogi, akahojiana na Wayahudi. 20 Walipomtaka akae wakati mwingi zaidi, hakukubali; 21 bali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso,

 

Hii ni nadhiri ambayo inapaswa ikamilike huko Yerusalemu wakati alipokwenda huko kama tunavyoona hapo juu.

 

Kwa kuwa wasomaji wengi wa Injili ya Yohana walikuwa sio Wayahudi, ilikuwa muhimu kutumia neno “Wayahudi” katika kuitja sikukuu hii kama Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi (Yohana 7:2). Matendo na mwenendo wa Kristo unaonyesha kutilia kwake umuhimu utunzaji wa Sikukuu, kama alivyo waambia na kuwasisitiza watu wa familia yake waende kuishika kwenye Yohana 7:8, na aya ya 10 tunaona kwamba yeye mwenyewe pia alikwenda kuishika Sikukuu hii. Ingawaje viongozi wa dini wa wakati ule walitafuta kumuua, hii haikumzuia Kristo kwenda kuishika na kuingia hadi ndani ya Hekalu ambako alikuwa anafundisha pia (Yohana 7:14). Ukweli huu unatuacha sisi tukwa hatuna udhuru wowote wa kutoishika au kuadhimisha siku hizi za muhimu.

 

Sikukuu ambayo Paulo alikuwa anaitaja inaweza kuwa ilikuwa ni Sikukuu ya Vibanda tu. Kupangilia upya kwa ratiba ya safari ya Paulo unaonyesha kuwa alikuwa makini kuiadhimisha. Alifika huko Korintho (Matendo 18:1) na akakaa nyumbani kwa Yusto kwa miezi 18 (Matendo 18:11). Ksha akasafiri hadi Yerusalemu, ambako aliwasili majira ya kipupwe ya mwaka 52-53 BK. Paulo kwa wazi anaona hitaji na umuhimu wa kuitunza Sikukuu ya Vibanda mjini Yerusalemu, ambako ndiko yalikuwa makao makuu ya Kanisa kwa wakati ule.

 

Upatanisho

Matendo 27:9

Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya,

 

Bullinger anasema kwenye ufafanuzi wake kuhusu aya ya 9 juu ya mfungu huu wa saumu kuwa ulifanyika siku ya kumi ya mwezi wa saba, ambayo ni Siku ya Upatanisho. Anadhani kuwa ilikuwa ni tarehe 1 Oktoba ya mwaka ule (Companion Bible).

 

I wazi kabisa kwamba Paulo alishika sheria ama torati kama alivyofanya Kristo. Tunajua kwamba Torati haikutanguliwa na yeyote kwa kuwa Kristo anasema kwenye Mathayo 5:17-18 kwamba:

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.  

 

Ufunuo 22:6

Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.

 

Hadi matukio haya yalipokuwa yanatimilika yote yalikuwa hayajatimilika

 

Dhambi ni uasi na uvunjaji wa sheria (1Yohana 3:4). Kama Paulo hakushika sheria, basi alikuwa akitenda dhambi. Na iwapo kama alizivunja sheria kwa kiufanya mambo aliyokuwa anayafanya Kristo, basi tutasema kuwa Kristo alikuwa anafanya dhambi pia. Lawama atakayopewa Paulo kwa kuishika kwake sheria ni lawama ya kumshambulia Kristo pia.

 

Ni nani hawa watakatifu wa Mungu? Hawa ni wale wanaoishika sheria au Amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12).

 

Na ni lini ilitimilika? Utimilifu wa Ufufuo wa wafu na Hukumu na kushuka kwa Mji wa Mungu ndiko kukamilika kwa mpango au mchakato huu na kufanya mwisho na hitimisho kuukomesha uasi na kuwaleta viumbe wote kwa Mungu, mbingu na dunia havitapita na sheria itasimama. Tuna kazi nginyine mbele yetu ambayo itagharimu maisha yetu na imani kuendelea katika sheria au Torati ya Mungu kama zilivyotolewa kutoka asili yake ambayo tutairithi.

 

Soma jarida la Torati ya Mungu (Na. L1) [The Law of God (No. L1)].

 

q