Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[274]

 

 

 

 

Sabato Ndani ya Kuran

 

(Toleo La 2.0 19981212-19990921-20110406)

 

Jarida hili linaoabato ilivyotajwa na kuelezewa kwenye maandiko ya kitabu cha Qur’an au Koran.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 (Hati Miliki © 1998, 1999 Dr. Thomas McElwain na Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Sabato Ndani ya Kuran


 


Utangulizi

Lifuatalo ni somo kuhusu jinsi Sabato ya siku ya saba ya juma ilivyoelezwa ndani ya kitabu cha Kuran. Inaanza na tathmini kadhaa za jinsi ilivyoandikwa na kutajwa ndani ya kitabu huki kikitumia neno la Kiarabu sabt, na ikiendelea kufafanua hivyohivyo kwa jinsi Sabato inavyotakiwa kuadhimishwa kwa kufuata mujibu wa maagizo ya Kuran. Nukuu za nakala Kuran ya Kiingereza zimechukuliwa kwenye tafsiri ya Pickthall wakati hii ya Kiswahili ilechukuliwa kwenye tafsiri maarufu na inayotumiwa na kuaminiwa na wengi kwenye mataifa yanayotumia lugha hii.

 

Kuna jambo muhimu la aina yake katika kuhalailsha juhudi hizi za kutathmini maagizo ya utunzaji wa Sabato yaliyotolewa na kitabu hiki cha Kuran. Kuran ni kitabu kilichoandikwa na kuaminika na wakazi wengi wan chi za Mashariki ya Kati, na ni maandiko yaliyoandikwa kwa mwelekeo unaofanana kwa aina yake na maandiko ya Torati. Kuna kila sababu ya kuyatarajia maandiko haya yote mawili matakatifu kuyataja mambo yanayofanana kwa mtazamo unaofanana kidesturi au mapokeo. Na zaidi sana ni kwamba kitabu hiki cha Kuran kinajiweka kwenye uhusiano wa namna fulani na Biblia kwa mambo mengi, kama ilivyo kwenye Sura ya Pili ya Kuran (au Koran) inayojulikana kama sura ya Ng’ombe ambayo inmepewa jina hili kutokana na hadithi ya mtamba au ndama wa dhahabu iliyoko kwenye sura ya 67-71 (ni uandishi wa kimashairi unaokusudia kumtaja ndama wa dhahabu aliyeandikwa pia kwenye Torati). Alama rejea iliyoandikwa imepewa herufi Q ambavyo sisi tutatumia “K” kumaanisha Qur’an (au Koran) ikifuatiwa na nambari inayojulikana kimapokeo ya Sura husika na kisha hufuatiwa na aya kama hivi: K2:42

“Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua.” (Koran Tukufu, tafsiri ya Islam International Publications Ltd., 1988.)

 

Tafsiri ya Pickthall inatafsiri kwa namna nyingine kuhusu neno sdq, kwenye K2:42

“Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua” (Kitabu hiki kinajulikana pia kama Kuran Tukufu kwenye Tafsiri ya Kimaelezo ya Marmaduke Pickthall, Dorset Press, New York).

 

Pasipo shaka kabisa, tukiyachukulia maandiko haya kwa uzuri na kwa pamoja, Koran itajikuta ikionekana ikifanya mambo yote mawili, yaani inathibitisha na kutimiliza maagizo yaliyotolewa na kuandikwa kwenye Biblia.

 

Mamlaka ya mapokeo yajulikanayo kanuni za kuthibitisha na kuyakubali maandiko wakati wote yametuama kwenye uanzishaji wa dini. Wakati mtu anapokabiliwa na swali kuhusiana na uwepo wa kanuni na uvuvio kunakuwa na ukabiliwaji wa dhahiri na swali kuhusu uwezekano wa kubadilisha misingi ya imani au ya mafundisho makuu yaliyofunuliwa kwenye Biblia. Mabadiliko kama haya yamekuwa yakiathiriwa na tafsiri na pia na mapokeo za marabi wa Kiyahudi yaliyoegemea kwenye mitizamo ya Mafarisayo na ambayo yalishutumiwa sana Bwana wetu Yesu Kristo. Mabadiliko mengine kama vile ya mafundisho ya kizushi yaliyoingizwa kwa kupigiwa kura kwenye vikao vya Mabaraza ya Mitaguso ya Makanisa ya Kikristo. Ni mchakato huohuo ndio uliofanyika kwenye maandishi ya Hadithi (au vitabu vya mapokeo) kwenye dini ya Kiislamu. Suala la kanuni mamlaka ya uwekaji wa kanuni ni ni la kweli kabisa na ni swali la muhimu sana. Maelezo rejea ya kibiblia nikama haya yafuatayo. Torati na manabii zote mbili zilifunuliwa na Mungu kupitia kwa malaika aliyehudumu kati yao na Mungu. Malaika wa Yahova alimkabidhi Musa aliyewasomea na kuwapa Torati hii Waisraeli. Mungu alifunua mapenzi yake kwa kupitia malaika wake waliosimama kati yake na manabii kupitia kwa Roho Mtakatifu. Ufunuo wowote unatakiwa kwenye msingi wa kwamba lazima uwe na uhusiano au ufanane na maagizo ya Torati na Ushuhuda. Kama nabii haneni sawasawa na maagizo ya Torati na Ushuhuda, basi nuru haipo ndani yake (Isaya 8:20). Kwa hiyo, ugunuo wa Agano Jipya ni lazima usimame kwenye uhusiano na Torati na Unabii wa Agano la Kale, na wala usipingane nao. Na ndivyo ilivyo pia kwamba ili Kuran ikubalike kuwa imevuviwa, ni lazima ikubaliane na kuwa chombo kinachoitafsiri Biblia na kanuni zake na sio ipinganeriayo.

 

Kwa hiyo kila Maandiko Matakatifu yaliyole0wa yanakuwa ni kigezo cha kulinganishwa na tathimini ya mapwa mengine

.

Karibu ulimwengu wote wa kidini uko kwenye mkanganyiko mkubwa wa kuielewa Biblia wakijaribu kuyaona Maandiko yaliyotangulia kuwa ni utangauji wa Maandiko Matakatifu ya zamani. Kwa kuzitathimini Biblia na Koran kwa maelekezo haya ya mapenzi yaliotolezwa na Mungu kuwaonyesha kuwa wanategemeana wao wenyewe na kwa kila mmoja na mwenzake, na hivyo kuwepo. Maandiko mengine yaliyofuatia yalionyesha kuunga mkono na kuyaongezea nguvu Maandiko yaliyopita yakifafanua hali mpya ambayo ingeweza kuwa imetokea kutiwa giza kutokana na mabadiliko ya kitamaduni, mapokeo na lugha na kutokana na kujitikeza kwa hali ya uasi na ukengeufu. Kwa hiyo tunafanya mabadilio haya kwa kufuatana na maelekezo yaliyopo kwenye Isaya 8:20 kwamba ni kwa Torati na Ushuhuda. Nabii anapaswa kunena sawasawa na isemavyo Torati na Ushuhuda, vinginevyo hakuna nuru ndani  yake. Kwa hiyo, Maandiko yoyote Matakatifu na Kuran yaliyotathiminiwa na kutafsiriwa pasipokuzingatia mahudhui ya Torati ambayo ndiyo Amri za Mungu, yatakuwa hayana runu ndani yake.

 

Wakati Kuran ilipofunuliwa, ilibeba ujumbe wa ushuhuda kwa Wayahudi juu ya mamlaka ya Yesu ambaye walikuwa wamemkataa kipindi cha nabii wake. Kwa Wakristo ilishuhudia kuwa Kristo hakuwa ni nafsi ya pili wala ya tatu ya Utatu ambalo ni fundisho la uwongo ambalo limeanzishwa na kufundishwa na kuaminiwa sana na ambalo kwamba pia lilikuwa ni fundisho geni kwenye mafunuo ya mafundisho ya Kuran. Hawa wote wawili yaani Wayahudi na Wakristo wangefanya vema sana kama wangeichukulia Kurani kwa kumaanisha.

 

Kwa upande mwingine ni kwamba kama tunavyokwenda kuona, inaweza kabisa kuwa kwamba Waislamu nao wangefanya vizuri sana kama wangeyatathimini kwa upya maagizo ya Kuran yanayowataka kuishika Sabato. Imani na mapokeo ya Wasuni yanasema kuwa mtume alikuwa na tabia ya kufanya kwa kusujudu kifudifudi mara mbili na maombi ya kawaida ya Dua za dani ya Kaba ya msikiti siku za Jumamosi asubuhi na alikuwa anafanya hivyo tu siku za Jumamosi asubuhi pekee. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba Mtume alikuwa anazishika Sabato. Kuna maelezo yakihistoria pia yanayosema kuwa hata Mahalifa wake waliokuwa pamoja naye nao pia walifanya hivyohivyo. Waislamu wa madhehebu ya Sunni hawaziamini wala kuzifuata sunna za Mtume, lakini mapokeo na desturi za Washia yanaichukulia Sabato kuwa kuwa ni mustahab au kitu muhimu na cha kistaarabu kukifanyia funga au saumu (ambayo kama mtu hatafanya hivyo au akivunja haina hukumu yoyote atakayopewa) na kwamba kipindi chote hiki kitu chochote kitakacoweza kufarywa kitakuja kurudiwa maranyingine huko mbeleni. Kwa hiyo, sherehe za arusi, shughuli za mazishi, na ukataji wa nywele vilikatazwa kufanyika siku za Sabato kwenye imani ya Washia.

 

Utajwaji wa kwanza wa Sabato unakutikana kwenye sura ya pili ya kitabu hiki.

“Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu walio ivunja Sabato,(siku ya mapumziko, Jumaa Mosi) na tukawaambia: Kuweni manyani wadhalilifu 66. Kwa hivyo tukayafanya hayo kuwa onyo kwa wale walio kuwa katika zama zao na walio kuja baada yao, na mawaidha kwa wachamngu..” (K2:65,66)

 

 Andiko hili wanaandikiwa Wayahudi. Mazingira yaliyopelekea kuandikwa kwake hapa ni wazo la jumla kwa watu wote na ni kwa sababu zilezile na zilizoelezewa hapo baadae kwenye Sura ya Saba (K7:163). Ilikuwa ni uvunjifu wa kanuni za kupata chakula, ambao ulipelekea waende kuvua samaki siku ya Sabato kama ilivyoelezewa kwenye Kutoka 16.

 

Adhabu ya tendo hili la uasi ilikuwa ni kulaaniwa kwa laana ambayo watu waligeuka kuwa manyani. Laana hii imeenea na kuelezewa tena kwenye K5:60:

“Sema: Je! Nikwambieni yule ambaye ni mwenye malipo mabaya zaidi kuliko hayo mbele ya Mwenyezi Mungu? Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani na amemkasirikia, na amewafanya miongoni mwao manyani na nguruwe, na wakamuabudu Shet'ani. Hao ndio wenye mahali pabaya na wamepotea zaidi njia iliyo sawa.”

 

Hawa waliobadilika na kuwa manyani sio kwamba walizivunja Sabato peke yake, bali kwa kufanya hivyo waliabudu na kuzitumikia sanamu. Neno lililotumika kuelezea sanamu au vinyago hapa nimeandikwa Taghut, linalomaanisha mtu aliyezidi na kubobea kwenye vifungo au kujikita kufanya jambo fulani; na kwenye jambo hili inamaanisha kuvuka mipaka au kuvunja mipaka ya maadhimisho ya Sabato. Lakini neno hili kwa ujumla linamtaja Shetani, na watu wengine wanaowageuza watu kutoka kwenye usahihi na kuwapotosha kwa kuwaongoza wakaabudu sanamu kwa ujumla. Kitendo cha kuzivunja Sabato ni ibadaya ya Shetani, kufuata mwelekeo mpotofu na ni ibada ya sanamu.

 

Ingawa andiko hili lilielekezwa kwa Wayahudi, andiko linguine au aya inatueleza kuwa fundisho hili halikuwa kwa ajili yao tu. Bali lilikuwa kwa ajili ya vizazi vinginevyovyote vinavyofuatia. Na kizazi hiki kinachofuatia kilikuwa kwanza ni kile cha Wayahudi, na lakipi pia ni cha watu wote wamchao Mungu. Fundisho lililoko hapa ni kwa kila mtu amchaye Mungu, ambaye ni kwamba yeyote aliye na juhudi ya kuiendea njia sahihi. Wengi wa wale waliojikita kufafanua maana yake wanakubaliana kwamba inamaanisha wale wote walioasi na kutotii ndiyo fundisho linapolenga na haijikitu tu kwenye adahbu inayotokana na kuvunja Sabato peke yake. Kwa hiyo, amri ya kuitunza Sabato ilitolewa kwa Wayahudi, na sio kwa wengineo. Lakini ieleweke kwamba hakuwezi kuwa na fundisho lolote kwa kuadhibu wakosaji kama hakuna amri iliyowekwa. Kuna mawili yafuatayo kuyachakua kutoka kwenye tafsiri hizi: ama kuamini kuwa fundisho hili linahusiana na adhabu kwa kuvunja Sabato, au linahusu adhabu kwa kuzivunja amri nyingine tu zilizoandikwa. Lakini ukweli unabakia dhahiri tu kwamba ni adhabu kwa ajili ya kuvunja Sabato na ambayo ni onyo kwa wacha Mungu wa kizazi chetu. Kama tutadhani kuwa amri hii haituhusu sisi na wala adhabu hii haituhusu sisi, basin a tuamini na kusema kuwa mjumuisho wa wacha Mungu pia hautuhusu sisi pia. Lakini kama tunadai kuwa sisi ni wacha Mungu, ndipo tujue kuwa amri na agizo hili la kuishika Sabato vinatuhusu, sambamba na adhabu iliyotolewa kwa watakaozivunja itatuhusu pia.

 

Kunamabishano kati ya wanazuoni kuhusu kama ubadilikaji huu wa kuwa manyani ni wa kivitendo kimwili au ni wa namna ngingine vinginevyo. Matokeo yake ni sawasawa tu, kama ni mabadiliko ya kimwili au ni wa kiakili. Sabato imetolewa kwa maendeleo ya kiroho inayofanyika kwa njia ya unyenyekevu kwa amri ya mbinguni na kwa njia ya maombi, kusikiliza na kusoma vitabu vitakatifu ibadani. Kushindwa kujinyenyekeza kwa Mungu na kupuuzia Baraka zilizofunuliwa na kuahidiwa kwa kuzitunza Sabato, ni kujifanya kuwa nyani mwenyewe. Kwa hiyo, ni kujifanya mtu mwenyewe awe mtiifu ni kujinyenyekesha kwa maigizo au kujifanya na kujionyesha na bila uelewa wowote ule wa kiroho. Hakuna shaka kabisa kuamini kwamba nyani wanatimiliza sifa za Muumbaji, na wala aya hii haiwakebehi wao. Kutokana na mtazamo na uelewa wa kibinadamu, nyani wananachukuliwa kuwa wanajua kutofautisha au kupambanua wale wanaojifanya kiuigizaji. Kuwa nyani pia kunamaana ya kuwa na mwonekano wa kiuanadini lakini pasipokuwa na uwezo wa kupambanua kiroho. Haya ni matokeo pia yanayotokana na kitendo cha kuzipuuzia Sabato.

 

Utajwaji wa pili wa Sabato upo kwenye sura ya nne.

“Enyi mlio pewa Kitabu! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni, au tukawalaani kama tulivyo walaani watu wa Sabato (Jumaamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifanyike Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa.” (K4:47,48)

 

Aya hii pia inaongelea tukio hilihili kama lilivyoelekezwa, na hii inaelezea vizuri na kwa wazi sana kwenye sura ya saba ijayo. Inaonyesha au kuitaja aya nyingine iliyotangulia inayoelekezwa kwa Wayahudi na kwa Wakristo pia. Tumeona jinsi kuabudu miungu ya uwongo kunauhusiano mkubwa na tendo la kutozishika Sabato, na hapa uhusiano wake unaonekana tena kwa uwazi sana. Kwa hii imeongeza dhambi ya tatu, ambayo nl kuipuuzia Kuran. Kwa hiyo, Kuran inatoa msisitizo kuhusu umoja wa Mungu na agizo au ulazima wa ulimwenguni kote wa kuishika Sabato ikiwa ni ushuhuda unaoonyesha kuwa Kuran ni ufunuo wa kweli. Kitendo cha kuikataa na kuipuuzia Kuran ni kujitakia laana waliyoahidiwa kukumbwa nayo wavunja Sabato. Na hivyohivyo, kitendo cha kuikubali Kuran kunaonyesha kuwakubali mashahidi hawa kwenye kweli yake: agizo la kuishika Sabato na kuwataja au kuwaonyesha au kuwataja washiriki (kwenye uungu) na kwa Mungu kwenye Utrinitari.

 

Mahala pa tatu ilipotajwa Sabato kwenye Kuran pia kunaonekana kwenye sura ya nne.

“Na tukanyanyua mlima juu yao kwa kufanya agano nao. Na tukawaambia: Ingilieni mlangoni kwa unyenyekevu. Na tukawaambia: Msiivunje Siku ya Sabato (Jumaa mosi). Na tukachukua kwao ahadi iliyo madhubuti..” (K4:154)

 

Andiko hili pia linawaambia Wakristo kama aya iliyotangulia inavyoonyesha. Inatoa sehemu ya mwitikio kwa Wakristo ambao walikuwa wanadai kuwa Mtume aliyesababisha kitabu kishuke kutoka mbinguni machoni pao. Jibu ni kwamba Mungu amekwishatoa tayari Amri zake Kumi kwenye Mlima wa Sinai. Na kwakuwa bado zipo, basi hakuna “kitabu” kingine chochote tena kitakachokuja kushushwa chini machoni mwa wanadamu. Aya hii inahitimisha Amri hizi Kumi kwa migawanyo ya makundi mawili ya amri. Ya kwanza ni amri ya maombi kwenye kusujudu, ambayo ni ufafanuzi wa amri ya pili kwa mtazamo chanya. Amri inayokataza kutofanya sanamu na kuziabudu ina mwelekeo chanya ambayo ni kujiinamisha kwa namna ya kusujudu kifudifudi kwa Mungu. Amri ya pili iliyotajwa ni ile inayohusiana na utunzaji wa Sabato. Kinachoashiria ni kwamba maandiko yote ya Torati yamefungamanishwa kwenye amri hizi mbili, na kwamba zina uhusiano wa kivitendo kati yake. Kwa hiyo, kusujudu kwa kuanguka kifudifudi mbele za Mungu siku ya Sabato ni amri na agizo na muhimu sio tu kwenye amri hizi mbili, bali pia kwa kumi zote. Hii haitafuti kubadilisha ule usemi wa Amri Kuu Mbili, bali ni kuelezea mambo mawili kuhusu Amri Kuu ya Kwanza.

 

Fungu la nne lililoitaja Sabato ni lile lililo kwenye sura ya 7:163.

“Na waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu.”

 

Tukio la kuzivunja Sabato limeelezewa kwa kina zaidi hapa. Kwa mujibu wa mapokeo, hii ilifanyika kwenye jamii ya kiyahudi iliyokuwa upande wa nyanda za chini za bahari kipindi cha Daudi. Kwa ajili ya ukatili wao na dhuluma Mungu aliwapa majaribu. Alisababisha samaki watokee kwenye mapumziko yao siku ya Sabato na sio kwenye siku nyingine zozote zile. Na kama wasingekuwa kwenye mapumziko yao siku za Sabato, basi hii isingeweza kutokea. Kwa kufanya kwao hivyo walimkasirisha Mungu na kumsababisha awaadhibu. Wakati huohuo, Mungu aliwajaribu maadhimisho yao ya Sabato kwa kuwaletea samaki siku hizo peke yake. Asingeweza kuwafanyia hivyo kama wangekuwa watiifu kwake.

 

Watu wengi hudai kwamba maadhimisho ya Sabato ni jambo lisilowezekana. Imekuwa vigumu kwao kuiadhimisha kwa kuwa tangu mwanzo wamekuwa wamekataa kuishika. Na kwa kukosa kwao kuishika wanakuwa wamepoteza uwezo wa kiroho na nia ya kuitunza.

 

Sehemu ya mwisho iliyotaja Sabato ni kwenye sura ya 16.

“Hakika siku ya Sabato (Jumaamosi) waliwekewa wale walio khitalifiana kwa ajili yake. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana. (K16:124)

 

Tafsiri nyingine mbili zinasema hivi:

“Hakika siku ya Sabato (Jumaamosi) waliwekewa wale walio khitalifiana kwa ajili yake. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana.” (Kuran Tukufu, Islam International Publications Ltd., 1988.)

 

Tafsiri mpya ya Kuran iliyotafsiriwa na  Muhammad Zafrulla Khan, Curzon Press, 1971, inatoa maana ifuatayo:

“Hakika siku ya Sabato (Jumaamosi) waliwekewa wale walio khitalifiana kwa ajili yake. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana..”

 

Maneno “adhabu” na “hukumu” mwanzoni mwa aya yametenganishwa na watafsiri kwa kuwa yanaashiria kuwa na maana sawa na neno ju’ila. Maana ya aya hii ni kwamba kuna adhabu au hukumu kwa wanaoivunja Sabato, bali inapasa kuchukuliwa nje na wale wanaopinga amri na agizo hili la kuitunza Sabato. Zaidi ya yote, imehitimishwa kwenye andiko kuwa hakuna adhabu kwa kuivunja Sabato itakayotolewa kabla ya Siku ya Hukumu.

 

Huu ni mfano bora sana wa jinsi Kuran inavyounga mkono na inavyohitimisha Biblia. Kwenye Biblia tunakabiliana na matatizo mawili. La kwanza ni kwamba hukumu ya anayeivunja Sabato ni kifo. Kimatendo, hii haifanyiki katika siku zetu hizi.

 

Tafsiri ya Torati kikamilifu inaonyesha kwamba Sabato ni kitu endelevu na ni ya kushinikiza kwa hukumu ya kifo. Kristo alionyesha mfano wa jinsi sheria za Agano la Kale zilivyopaswa kutafsiriwa. Hakufanya kile Wakristo wanachodai kuwa alizitangua. Na muhimu sana ni kwamba Agano la Kale linaonyesha kwamba Sabato itatambulishwa na kutuzwa tena kwenye kipindi cha utawala wa millennia wa Yesu Kristo. Tunalijua hilo kupifia Zekaria  14:16-21 ambako inaonyesha kuwa sikukuu zitaadhimishwa kipindi hiki na kwamba hukumu kwa wanaozivunja itakuwa ni mvua kutonyesha kwa wakati wake muafaka ambayo itasababisha kuhukumiwa kwa vifo vitakavyotokea kwa baa la njaa litakalosababishwa na ukosefu wa mvua.

 

Isaya 66:18-24 inaonyesha kwamba katika kipindi kile Mwandamo wa Mwezi Mpya utakuwa unaadhimishwa pia na wote wenye mwili hapa duniani sambamba na maadhimisho ya Sabato. Torati haibadiliki. Ili kuwa sehemu ya Israeli na kuwa na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza wa wafu, mtu anapaswa kuzishika Sabato ili asiweze kuingia hukumuni.

 

Wakati wa hukumu ya walio kwenye nyumba ya Mungu ni sasa. Ilianza kanisani tangu zama za mitume (1Petro 4:17).

 

Kurani inafanya tafsiri inayotafsiri matendo yaliyopo nyakati hizi. Imekuwa ikipotoshwa sana na kutafsiriwa vibaya na zile zinazoitwa Hadithi na makundi au dini zote mbili, yaani Wayahudi na Wakristo. Hakuna hukumu ya kimwili iliyomaanishwa kutolewa kwa anayeivunja Sabato. Hii inaweza kuwa kweli nap engine inaweza kutokea mara moja hapo kwa hapo. Kama mtu hatatubu na kubatizwa na kama hazishiki Sabato, kama alivyofanya mtume na wale Mahalifa Wanne Walioambatana na Mtume, hataweza kuingia rahani mwake. Kwa hiyo watangojea Ufufuo wa Pili wa wafu utakaotokea mwishoni mwa Milenia. Ufufuo wa Kwanza wa wafu ni ule ambao Kuran inauelezea kwa kuulinganisha na maisha kwenye Bustani ya Paradiso. Ufufuo wa Pili inautaja kama Bustani au Paradiso ya Pili. Matukio ya Ufufuo huu wa kwanza na wa pili yatafanyika kwa zama mbili tofauti na yatatofautiana kwa kipindi cha miaka 1,000 tangia wa kwanza hadi wa pili (Ufunuo 20:4-13).

 

Maandiko ya Hadithi yameharibu na kupotosha lengo hasa lililokusudia uandishi wa Kuran (au Koran) na uelewa aliokuwa amepewa Mtume.

 

Kuran inafuatia mambo yaliyotangulia kuandikwa kwenye Maandiko Matakatifu na inafundisha kuwa hukumu inatokea mara moja. Utii wa mwamini na mnyenyekevu anayevishika Sabato (pamoja na Pasaka) atapata hukumu yake ambayo ni kuingia kwenye Bustani ya Kwanza ya Paradiso. Wale wasiofanya hivyo watatofautishwa katika Siku ya Hukumu au kwenye Ufufuo wa Pill, ambao watatakiwa waende kwa kupitia mchakato wote wa mafundisho tena na kipindi hiki wafanye hivyo kikamilifu. Ujuzi au uelewa huu ni wa zamani na ni uelewa sahihi wa kanisa la Mungu wenye chimbuko lake kwenye maandiko ya Agano Jipya ambao unawatambulisha watakatifu watakaokuwepo kwenye Ufufuo wa Kwanza wa Wafu kuwa ni wale wanaozishika Amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu (Ufunuo 12:17; 14:12; 22:14, KJV); kwa hiyo utunzaji wa Sabato unaamua ni Ufufuo gani ambao mtu ameruzukiwa nao.

 

Tatizo la pili ni kwamba hakuna udhuru au mbadala wa kuchelewa kwenye maadhimisho ya Sabato. Kama kutakuwa na kitu kinachoweza kuzuia maadhimisho ya Sabato ifikapo siku ya saba ya juma, basi hakuna ruhusa iliyotolewa kokote, iwe kwenye Torati au kwenye Maandiko mengine Matakatifu kuhalalisha au kuruhusu kuiahirisha na kupeleka mbele hadi siku inayofuatia, kama ilivyoruhusiwa kufanyika hivyo kwenye Pasaka, kwa mfano inapotokea kuna mazingira yasiyo muafaka na kwamba inaweza kuahirishwa hadi ikasogezwa hadi mwezi mwingine unaofuatia. Hii hainamaanisha kwamba kama kuna mazingira yasiyofaa kufanyika maadhimisho ya Sabato kunaweza kufanyika hivyo pia. Kama kunakitu kilichojitokeza na ambacho hakijaonekana mapema kabla na hakikukusudiwa, bado tu kwamba Sabato haiwezi kubadilishiwa siku au kuhamishiwa siku nyingine inayofuata. Inapaswa inakie tu kama ilivyo, hata kama maadhimisho yake yatakuwa ni tofauti na jinsi yalivyokusudiwa kufanywa. Kwa hiyo, hukumu imewekwa kwa wale wote waliokuwa wanapinga amri hii. Wale waliokusudia kuishika Sabato lakini maadhimisho yao kwa sababu zisizoonekana na kujulikana mapema zilishindwa kufikia malengo, hawatahukumiwa kwa kuzivunja Sabato.

 

Hii inahitimisha andiko la Kuran ambalo Sabato imetajwa kwa wazi sana. Sabato kwenye Torati hata hivyo imekaribiana kwa karibu sana na uhusiano wa kimatendo yanayofanyika siku ya sita ya juma. Kwenye hadithi ya uumbaji, siku ya sita ni siku ambayo mwanadamu aliumbwa, akabarikiwa, akapewa amri ya kuzaana na kuongezeka kuijaza nchi na kupewa mamlaka ambayo yametafsiriwa kama ni kuwa na sehemu kwenye milki ya vyakula vya ulimwenguni. Kwenye Kuran siku hii ya sita inashughuli sawa tu na vile zilivyoandikwa kwenye Torati, kuwa ni siku inayoitangulia Sabato. Ni siku ya maandalio. Ina shughuli na kazi yake maalumu, ni karibu sawa tu na jinsi inavyoelezewa kwenye Kuran, ni siku ya kuitisha mkutaniko wa maombi ya alfajiri. Pia tazama jarida la Ijum’aa: Maandalio ya Sabato (Na. 285) [The Juma'ah: Preparing for the Sabbath (No. 285)].

 

Hadi kufikia hapa tunakabiliwa na jambi linguine na somo linguine/ tazama jarida la Kurani Ndani ya Biblia, Torati na Agano (Na. 83) [The Koran on the Bible, the Law, and the Covenant (No. 83)].

q