Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[277]
Malumbano ya Wakwortodesiman
(Toleo
La 2.0 19990407-19990528-20071203)
Malumbano ya Wakwortodesiman yqlionekana kuwa
kama jambo muhimu katika kuamua Imani ya Kikristo. Kulikuwa na mchakato miwili
ya uvumbuzi kuwahi kutokea kwenye Kanisa la Kikristo na huenda ni ya muhmu
zaidi. Baada ya ibada za Jumapili kuanzishwa kutoka Roma katikati ya karne ya
pili, imani ya Kirumi waliyoianzisha ilisababisha kuwepo na kuiadhimisha
sikukuu ya kipagani ya Easter na kuiadhimisha badcala ya Pasaka. Mwaka 664 BK
huko Whitby Uingereza , hatimayhe wa.ifanikisha mkakati huu kwa shuruti na kwa
nguvu za kijeshi katika kulifanya Kanisa la Uingereza au la Kiseltiki wakubali
kuiadhimisha sikukuu hii ya Easter.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1997, 2007 Wade Cox)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Utangulizi juu
ya Malumbano ya Wakwortodesiman
Zaidi ya kipindi
cha miaka elfu mbili iliyopita kwenye Makanisa yanayotunza Sabato na hasa
kwenye Kanisa zima, hakujawa na mdahalo wenye maana kuhusu ni usiku gani ambao
Wayahudi walishiriki kuila Pasaka, dini ya Kikristo mara zote wamekuwa
wakielewa kuijua tarehe hii kuwa ni kitendawili kikubwa. Mara zote imekuwa
ikieleweka tu kuwa wanakondoo walikuwa wanachinjwa majira ya jioni ya siku ya
14 ya mwezi wa kwanza na kuliwa siku ya 15 yake. Jambo hili, na baadhi ya mikanganyiko
na upotoshaji unazingira ukweli huu, na imeelezewa kwa kina kwenye jarida la Pasaka (Na. 98) [The Passover (No. 98)]. Mjadala ulioko kwa Wakristo umetuama
kwene dhana ama wazo la kama Ushitika wa Meza
ya Bwana, unalazimu kufanya tendo la kuoshana miguu au la, na kwamba ulaji
wa mkate na unywaji wa divai pia na kwamba maadhimisho haya yote yafanyike kwa
pamoja siku ya 14 ya mwezi wa Abibu au wa Nisani (siku moja kabla ya mlo wa
Pasaka ya kawaida) au kama mapokeo au desturi ya maadhimisho ya Ijumaa Kuu ya maadhimisho ya Easter ilivyo.
Wasamaria
waliadhimisha kwa siku mbili, siku ya 14 na ya 15 ya mwezi wa Kwanza, walimchinja
mwana kondoo wa Pasaka alasiri ya siku ya 14 na kumla jioni ya siku ya 15 ya
mwezi huu wa Abibu au Nisani. Walishinda kipindi hiki chote kwenye Mlima wa Gerizim
huku wakikesha na walikuwa wanafanya hivi kila mwaka – wakati walipokuwa
wanaweza kufanya hivyo kiimwili – kwa kipindi cha mwisho cha takriban miaka elfu
mbili na mia sita. Maskani yao huko Mlimani Gerizim yaliharibiwa na John
Hyrcanus wakati wa kipindi cha Wamakabayo katika karene ya pili KK, lakini
vinginevyo dini yao ingebaka ikidumu pasipo kuingiwa kati. Jambo hili
limefafanuliwa kwa kina kwenye jarida la Usiku wa Kuuangaliwa na Kuuadhimisha
Sana(Na. 101) [The Night To Be Much Observed (No. 101)].
Mkanganyiko huu
mkubwa ambao kwa kweli ni kiini cha Imani, uliibuka katika karne ya pili. Viongozi
wa (walioongoza) watu mahiri au nguli walikuwa ni Maaskofu wa Roma, kina Anicetus
na baadae Victor au Victorinus, na Polycarp na mrithi wake, Polycrates. Swali
lilifahamika lakini vigezo vyake havikuwa vikieleweka kabisa au vilipotoshwa na
Wakrito wa siku hizi. Angalia maandiko yaliyoko hapo chini, utaiona Easter ikitajwa kana kwamba ni neno la
Kikristo.
Ingawa uadhimishaji
wa Easter ulikuwepo tangu nyakati za kale sana na za mwanzoni wa kuawepo kwa
kanisa la Kikristo, utetezi mkubwa unaotumiwa hadi leo kwa maadhimisho yake mara
tu baada ya kuibuka kwa Wakristo na Wayshudi na wale walio na asili ya
kipagani, ambao wamepelekea kuwepo kwa mkanganyiko mkubwa na wa siku nyingi.
Kitu kilichojiri kilikuwa ni kwamba wakati mfungo wa saunu ulionekana kuwa ni
lazima waksa Pasaka ilipokuwa inafikia mwisho. Kwa Wakristo wa jamii ya Kiyahudi
ambao wazo lao kuu lilikuwa ni kifo cha Kristo kuwa ndiyo maana ya Mwanakondoo
wa Pasaka, ufungaji saumu uliishia wakati ule ule mmja na ule wa Wayahudi,
ambao ni siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza jioni, na sikukuu ya Easter
ilifuatia mara moja, pasipo kujali ni siku gani ya juma. Wakristo wanaotoka
kwene Umataifa kwa upande mwingine hawakustahili.kuachwa huru mbali na desturi
za Wayahudi, wakiitambua siku ya juma kuwa ni ya Ufufuo na wakaichukulia siku
iliyotangulia ya Ijumaa kuwa ni ya maadhimisho ya kusulibiwa kwake, bila kujali
ni siku gani ya mwezi huo" (Encyclopedia
Britannica, 11th edition, article ‘Easter’).
Jambo hili ndilo
lilikuja kujulikana kama Malumbano ya Wakwortodesiman au wanaoamini maadhimisho
ya Pasaka siku ya 14 ya mwezi wa kwanza na, usemi wa kihistoria umekuwa ni
mgongano na mkanganyiko mkubwa uliogubika kuhusu ni wakati gani hasa Ushirika
wa Meza ya Bwana unastahili kuadhimishwa.
Neno Kwortodeciman maana yake ya Kumi na Nne na mkanganyiko uliopo ni
mabishano ya maamuzi ya siku ya kuadhimisha Pasaka. Hakukuwa na mabishano
makubwa kwa kweli kuhusu jinsi ya kuhesabu ili kupata Pasaka mbali na ukweli
kwamba Wayahudi walianzisha utaratibu kuahirisha baadae. Mchakato wa kuhesabu
ulihusisha tofauti ya wakati wa kuhesabu sikukuu zilizo kwenye Biblia na zile
za ibada za kipagani za mungu Attis magharibi mwa Roma, na za mungu Adonis kwa
upande wa Mashariki tangu Ugiriki ha ulimwengu ulioingiziwa imani ya Kihellena.
Sikukuu hii pia illitwa na ulimwengu wa Waango-Saxon kuwa ni Easter, neno linalotokana
na jina la mungu Ishtar au Ashrorethi. Jambo hili limeelezewa kwa kina kwenye
majarida ya Dume la Kondoo wa Dhahabu (Na. 222); Chimbuko la Easter na Krismas (Na. 235) na Utakaso na Tohara (Na. 251) [The Golden Calf (No.
222); The Origins of Christmas and Easter (No. 235) and Purification and Circumcision (No. 251)]. Jambo linalosikitisha sana ni kwamba neno
linalotumika na Wakristo wa zama hizi linataja kitu ambacho hakina maana yoyote
na imani ya Kikristo bali linaonekana wazi kabisa kwamba linaonyesha au
kutambulisha imani na ibada za mungu Baali/Ashtorethi au Ishatar/Astarte,
Anath/Athargatis na ‘Ate au Derketo au Ceto, nguva au mungu mke mwenye umbo la
samaki na kwa wao, samaki na njiwa au huwa walikuwa ni viumbe watakatifu (kwa
habari zaidi soma jarida la Painata (Na. 276) [The Piñata (No. 276)].
Tendo la
Kusulibiwa halikufanyika siku ya Ijumaa na wala Ufufuko wake haukufanyika siku
ya Jumapili. Bali Alisulibiwa siku ya Jumatano ya tarehe 5 Aprili 30 BK (kujua
hilo zaidi soma jarida la Nyakati za Kusulibiwa na Kufufuka Kwake (Na. 159)
[The Timing of the Crucifixion and the Resurrection (No. 159)].
Pasaka yenyewe
ilikuwa ni muhimu katika kuamua mwezi Kwanza wa mwaka.
Kanuni ambayo
kwayo mwezi wa Kwanza wa mwaka ulikuwa unaamuliwa kuanza na kuona kama unakuwa
mrefu au sivyo ni rahisi sana.
Sikukuu ya Pasaka inaadhimishwa wakati mwezi unapokuwa kamili katika mwezi wa kwanza za Abibu au Nisani (siku ya 14 Nisani), na ni lazima kila mara iangukie baada ya ikwinoks ya majira ya baridi [meta isemerian earinen] ... Anatolius, kwenye kitabu chake cha maeneo yenye umuhimu mkubwa kwenye historia ya kalenda ya Kiyahudi aliyachukua maneno ya Eusebius HE vii 32, 16-19, akiuchukulia huu kuwa ni mtazamo usiojulikana sana kwenye uongozi mzima wa Wayahudi...Maneno waliyosema Philo na Josephus pia yanashabihiana na haya. Iwapo kama ilijulikana au kuchukuliwa kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka na kwamba Pasaka ingeangukia kabla ya ikwinoks ya majira ya baridi, basi ongozeko la siku la mwezi kabla ya Nisan ingepigwa marufuku au ingepingwa (Schürer, ibid., p. 593).
Schürer
anaiingiza "(14 Nisan)" hapa
kwenye maandiko yanayoegemea kwenye sehemu ya muhimu ya Anatolius, ambayo
anasema inaonyesha kuwa 14 Nisan ni lazima iangukie baada ya ikwinoks (sawa na
inavyosema. Ante-Nicene Fathers [ANF], Vol. VI, pp. 147 ff.). tumelifafanua
jambo hili kwenye jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156) [God’s Calendar (No. 156)]. Imekubalika kwenye karne ya ishirini kwamba 14
Nisan ingeangukia kwene ikwinoks lakini hii haiwezi kuwa ni sababu. Jambo la
muhimu linaonekana kuwa na Anatolius, kwamba kutolewa dhabihu mwishoni mwa siku
ya kumi na Nne lazima kuzingatiwe hali ya mwezi kuwa mkamilifu; na hapo
anaiongelea ikwinoks ya majira ya baridi inayotangulia utoaji dhabihu wa saa 9
alasiri mwishoni mwa siku ya 14 Nisan na mwanzo wa usiku wa siku ya kumi na
tano wa mwezi wa kwanza. Jambo hili lina maana sana kwa mchakato wa mwanzo wa
mwaka. Anatolius pia anafanya kosa kubwa kwenye maandiko yanayohusiana na kuanza
na mwisho wa idi ya Mikate isiyotiwa Chachu ambayo imekanganywa na vyanzo vya
Biblia na kwa Wasamaria na matendo mengineyo (soma tena ibid.). Kutokana na
usomaji wa makini wa Anatolius, kanuni ni kwamba kipindi cha ikwinoks ni lazima
kianzie kabla ya utoaji wa dhabihu ya saa 9 alasiri ya 14 Nisan. Kama haitakuwa
hivyo, basi mwaka ni lazima uwe mrefu. Hii iko hivyo na ilikuwa inahesabu miezi
na miaka kwanza.
Mfano wa kwanza
wa uingizaji wa imani ya Easter kwenye Ukristo, kwa mujibu wa Irenaeus, inaonekana
kuwa mapema sana hata kabla ya kipindi cha Sixtus huko Roma yapata mwaka 120 BK
(sawa na kitabu cha Catholic Encylcopedia,
Vol. V, article ‘Easter’, p.
228).
Polycarp, mwanafunzi
wa Yohana na mwalimu wa Irenaeus, alikuja kutoka Roma yapata mwaka 150-152 kumshawishi
Anicetus. Hakufanikiwa, na imani hii Easter ya kipagani ilikuja kuimarishwa zaidi
kipindi kile. Kanisa la Uingereza lilipaswa kuendelea kuadhimisha kwa kuufuata
mfumo wa Kwortodesiman kwa kipindi cha karne kadhaa hadi huko Whitby mwaka 664 ingawaje,
na kwa taratibu kuuwezesha hata hapo, wakati ilipoenda kwa chinichini.
Kama tulivyosema,
malumbano haya yalikuja kujulikana kama ni Malumbano ya Wakwortodesiman, na kihistoria
tunaweza kusema kwamba, huu imekuwa ni mgongano mkubwa kupita mingine yote
uliowahi kujitokeza katika nyakati zote wakati ushiriki wqa Meza ya Bwana
unapokuwa unafanyika. Mchakato wa kuivunja Pasaka ya Kikristo mbali na Wayahudi
ulitokea huko Roma. Schaff anayaona malumbano haya kama yalitokea huko na
kwamba Makanisa ya Asia yaliadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Kristo siku ya 14
Nisan, katika siku ileile waliyoiadhimisha Wayahudi Pasaka na Idi ya Mikate
Isiyo na Chachu. Aliona kuwa malumbano haya yalikuwa na mambo matatu. Mjadala
wa kwanzaulikuwa ni ujio wa Polycarp, askofu wa Smyrna, hadi Anicetus, askofu
wa Roma, kati ya miaka ya 150 hadi 155 BK. Mtazamo wa Irenaeus, mwanafunzi wa
Polycarp, mwanafunzi wa Yohana ni wa muhimu sana.
Wakati mbarikiwa Polycarp aliposafiri kutembelea huko Roma kipindi au siku za Anicetus, na walikuwa na tofauti ndogo wa kimawazo au mtazamo sambamba na vigezo vingine, shuruti ilikuja kwa uelewa wenye amani kwenye kichwa hiki [kuadhimisha kwa Easter], kukosa upendo kwa pande mbili za malumbano. Basi na hata kama Anicetus alimshawishi Polycarp kutoiadhimisha, ni dhahiri sana kwamba yeye [Polycarp] alikuwa mara zote akiiadhimisha pamoja na Mtume Yohana, mwanafunzi wa Bwana wetu, pamoja na mitume wengine ambao alikuwa akishirikiana nao; wala Polycarp hakumshawishi Anicetus kuiadhimisha (JZD,Ç<), aliyesema kwamba alilazimika kurekebisha desturi ya wazee waliokuwa tegemezi kwenye imani ya kanisa (= maaskofu) mbele yao. Mambo haya yakiwa hivyo, walishiriki kwa pamoja na kanisani na Anicetus alimpa Polycarp, pasipo heshima na bila shaka sherehe au maadhimisho ya ekaristi (J¬< ,ÛP"D4FJ\"<), na walijitenga kwa amani, makanisa yote yakiwa kwenye amani, yote mawili, yaani wale waliokuwa wanaadhimisha na wale waliokuwa hawaadhimishi [siku ya kumi na nne ya Nisan], ili kuweka amani (kwa mujibu wa Schaff, History of the Christian Church, Eerdmans, Michigan, 1987, Vol. II, p. 213).
Irenaeus aliutumia
muda wake mwingi akijaribu kupatanisha na kuweka sawa malumbano haya na
kuyazuia malumbano kati ya Mashariki na Magharibi. Bila shaka kwamba tatizo
lilijitokeza na lilindelea huko Roma.
Mnamo mwaka 170
BK, mkanganyiko ulijitokeza huko Laodikia. Mkanganyiko huu unaweza kuonekana tu
kutokana na uelewa wa itikadi ya Ukwortodesiman (au Wakwortodesiman (Schaff)) wenyewe.
Ukristo wa siku hizi haulielewi yale yaliyokuwa yanabishaniwa hu o Laodikia.
Malumbano yalifika huko Asia na lnaonekana kuwa yalikuwa miongoni mwa waliokuwa
wanaamini Ukwortodesiman wenyewe. Eusebius tu ndiye alitaja kuwa Melito wa
Sardi aliandika vitabu viwili kuhusu Pasaka (H.E. IV. 26). Vitabu hivi
vimepotea kama vilivyopotea vitabu alivyoandika Clement wa Alexandria vyenye
kicha hichohicho cha maneno, pamoja na kuachilia sehemu chache kwenye Chronicon
Paschale (soma kitabu cha Schaff, p.
214). Chanzo kikuu cha habari ni kutoka kwa Claudius Apolinarius (Apollinaris),
askofu wa Hierapolis huko Phrygia, kutoka sehemu mbili zilizobakizwa kwenye Chronicon
Paschale.
Hawa ni baadhi kwa
sasa kati ya wale ambao kutokana na ujinga walipenda mgogoro kuhusu vitu hivi,
wakitiwa hatiani kwa hili kwa machukizo yaliyosamehewa, kwa ujinga
hawakustahili kabisa kulaumiwa bali walihitaji kuambiwa. Na wanasema kwamba siku ya kumi na nne [ya Nisan] Bwana ndiye mwanakondoo wa Pasaka [*] na malumbano haya pamoja na wanafunzi
wake, na lakini yeye mwenyewe aliteseka katika siku kubwa ya mikate isiyo na
chachu [kama vile. Siku ya kumi na
nne Nisan]; nakumuelewa au kumchukulia Mathayo kuwa alikuwa amependezewa na
mtazamo w ao kutokana na kile kilichoonekana kuwa mtazamo wao haukubaliani na
sheria au torati, na kwamba injili inaonekana, kwa mtazamo wao kuwa
inatofautiana.
Maadhimisho ya siku ya kumi na nne ndiyo Pasaka ya
kweli ya Bwana, dhabihu
kuu, Mwana wa Mungu mahala pa Mwanakondoo…aliyeinuliwa juu katika pembe za mnyama…na
ambaye alizikwa siku ya Pasaka na jiwe likawekwa mdomoni mwa kaburi lake (Schaff,
ibid.).
* sawa na yanavyosema majarida ya Pasaka (Na. 98) na Nyakati za Kusulibiwa na Kufufuka (Na. 159) ]The Passover (No.
98) and Timing
of the Crucifixion and the Resurrection (No. 159)].
Kutoka kwenye bangokitita (footnote) ya kitabu cha 5, Schaff haionekani kueleweka asili ya makosa, ingawaje aliona kiusahihi (fn. 6) kwamba mtazamo wa Apolinarius ulikuwa ni kwamba Kristo alikufa siku ya 14, siku ya halisi na iliyoruhusiwa.
Malumbano haya
yanaweza kuonekana vyema Wakwortodeciman. Kwa kweli, ni malumbano yaleyale
yanayoelzea hizi siku za 14-15 Nisan mkanganyiko ulioelezewa kwa kina kwene
jarida la Pasaka (Na. 98) [The Passover (No. 98)] na hapa pia. Mabishano yaliyokanushwa na Apolinarius
yalikuwa ni kwamba Kristo alikula mlo wa Pasaka siku ya 14 Nisan na kwamba kifo
chake kilitokea katika Siku Takatifu ya kwanza ya Mikate Isiyo na Chachu. Kifo
cha Kristo, kutokana na ukweli huu kwa hiyo hakikufuata mujibu wa Torati. Wale
walio kwenye makosa huuchukulia mtazamo huu kutoka kwenye Injili tatu
Zinazofanana, kama uandishi wa Mathayo unavyoonekana kukanganyana na ule wa
Yohana na Luka, haya ni mabishano yaleyale yanayotafuta kudai kwamba Kristo
aliula mlo wa Pasaka majira ya jioni ya 14 Nisan na kwamba Wayahudi kwa kweli
walikuwa wamechelewa kwa siku moja, wakiishika taratibu yao ya kutoa dhabihu ya
Pasaka kaika Siku Takatifu ya Kwanza ya Mikate Isiyo na Chachu. Mtazamo huu
ulichukuliwa kuwa ni moja ya ukosefu wa kiuelewa aliokuwanao Apolinarius.
Inaonyesha kwa
kweli kutoijua kwake Torati na umuhimu wa Masihi kuwa Mwanakondoo wa Pasaka.
Kwa hiyo, malumbano yaliyoibuka kutokana na ujinga katika karne ya ishirini
yalijitokeza kutokana na hali hii ya kukosa uelewa na kuiacha au kutoijali Torati
katika karne ya pili. Watetezi wa Easter wanatafuta kudai kutoka kwenye hii
kulikuwa na mkanganyiko katika kuikubali hii Pasaka ya siku ya 14 Nisan kwala ya
Easter. Hii siyo sahihi kabisa. Schaff mwenewe anaonekana kudhania kwamba
ukweli wa jambo hili hautegemei na jinsi tukio la waakati wa kusulibiwa na
aadhimisho ya Pasaka ya Wayahudi. Schaff, kama walivyo Watrinitarian wengi,
hakubaliani na dhana hii ya kwamba Masihi klfo chake kililazimu kufuata kanuni
zote za Torati na manabii ili aweze kufilikiza yaliyoagizwa. Schaff anajua kwa
ukamilifu wote kwamba uhusiano uliopo kati ya Pasaka na Kusulibiwa ulibidi
uvunjwe ili kulinda utata wa kipindi kifupi cha Ijumaa-Jumapili cha maadhimisho
ya Easter kwa kuwa ilikuwa imeingizwa kwenye Ukristo. Schaff anakubali na
kukiri dhana ya kuwa huenda Apolinarius alikuwa anapingana na wa upande wa
Magharibi na Warumi au msimamo wa Wakwortodeciman. Maelezo haya yaliyoko kwny
ukurasa wa 215 yanaonyesha kwamba alikuwa amepotoka kabisa kutoka kwenye ukanushaji
wa Apolinarius, inayoonekana wazi kabisa machoni ake.
Schaff anaona
kwamba malumbano haya yameibuka kati ya Polycrates, askofu wa Efeso na mwanafunzi
wa Polycarp, na Victor wa Roma kwenye oja ya madaraja yao ya vteo na machafuko
yanayotokana na kutovumiliana (na Roma). Hii ilikuwa ni hatua ya tatu ya utata
katikati ya miaka ya 190 na 194 BK, ambayo yalienea kwenye Kanisa lte na
kuzikumba sinodi nyingi na naraka za kisinodi.
Askofu wa Roma Victor, ni mtu wa tofauti sana kutoka kwa mtangulizi wake Anicetus, aliyewataka Waasiatics, kwenye mdundo wa kifalme, kuachana na imani na matendo ya Kikwortodeciman. Kinyume cha hili, Polycrates, askofu wa Efeso alilipinga kwa wazi kabisa akitumia jina la sinodi aliyokuwa anaisimamia, na kumchukulia kama alikuwa anaingiza kupanga safu ya mamlaka kutokana na desturi zao za kizamani (Schaff, ibid., p. 216).
Waraka wa Polycrates
kwa Victor, Askofu wa Roma, inakadiriwa kuwa uliandikwa katika miaka ya 190 na
194 BK na ulimlinda Eusebius (V. 24), kuwa ni mwenye shauku. Inaleta busara
kwene asili ya utata huu na ni majaribu ambayo Kanisa limeyavumilia kwa karne
kadhaa sasa.
“Sisi0, aliandika askofu wa Waefeso kwa papa wa Roma na kanisa lake akaendelea kusema,
“Tunaadhimisha siku halisi, pasipo kuongeza wa kupunguza. Kwa kuwa katika Asia nuru kuu imekufa, na ambayo itaangaza tena katika siku ya ujio wa Bwana ambayo yeye atakuja nayo pamoja na utukufu kutoka mbinguni. Na itawaamsha na kuwafufua watakatifu wote. Filipo mmoja wa mitume kumi na wawili, aliyelala huko Hierapolis, na mabinti zake mabikira wanaolingana umri wao; na binti yake mwingine pia aliyeishi maisha yanayovuatia ya Roho Mtakatifu nao wote wanapumzika huko Efeso; na zaidi sana Yohana aliyepumzika katika kifua cha Bwana wetu, ambaye alikuwa ni kuhani pia, na akiwa na sahani ya kasisi, akiwa na mambo yote mawili, mfia dini na mwalimu, amezikwa Efeso. Pia Polycarp wa Smyrna,mwenye yote mawili, yaani askofu na mfia dini na Thraseas mwene yote mawii, askofu na mfia dini wa Eumenia, ambaye amelala huko Smyrna. Kwanini nimtaje Sagaris, askofu na mfia dini wa aliyelala huko Laodiki; zaidi ya yote wabarikiwa na wenye heri Papirius na Melito, matoashi [walioishi waseja], walioishi pamoja kwenye mvuto wa Roho Mtakatifu, ambao sasa wanapumzika huko Sardi, wakimngojea askofu kutoka mbinguni, ambaye atafufuka toka kwa wafu. Wote hawa waliiadhimisha Pasaka ya siku ya kumi na nne ya Nisan sawasawa na inavyosema Injil, waliacha upendeleo na heshima, lakini wakafuata kanuni ya imani.
Zaidi ya yote, Mimi Polycrates, ambaye ni mdogo sana kwenu, kwa mujibu wa desturi za ndugu na wazazi wangu, ambao nimewafuatiia baadhi yao. Kwa kuwa saba kati ya ndugu zando walikuwa ni maaskofu, an Mimi ni wa nane; na hawa ndugu zangu wote waliiadhimisha siku ambayo Wayahudi waliachana kabisa na ulaji wa vitu vilivyochanganywa au kutengenezwa na chuchu na pia waliondoa kabisa chachu isiwemo majumbani mwao. Na mimi, kwa hiyo ndugu zangu, nina miaka sitini na tano nikimtumikia Bwana ambaye nimekuwa tunu ya ninyi wapendwa ndugu zangu ulimwenguni kote na nikidumu kujisomea Maandiko yote Matakatifu, sistushwi na mambo hayo ambayo ninatishwa nayo, mniige na mnifuate mimi. Kwa kuwa ni makubwa kuliko nilivyosema ‘tunapaswa kumtii Mungu kuliko kuwatii wanadamu’… ningeweza pia kuwataja maaskofu waliokuwepo, ambao mliniomba niwaambie ama kuwahutubia, na wale ninaowaita; ambao majina yao yangefanya idadi kubwa, lakini wanaouona mwili wangu mwembamba kuwa amekubaliana na waraka, na mnajua kwamba sijawa na mvi bado kichwani mwangu kwa kuwa si muhimu, bali kile nilichokifanwa wakati wote ni kuyatoa maisha yangu yote kwa Bwana Yesu” (kutoka kwenye kitabu cha Phillip Schaff, History of the Christian Church, Vol. II, “on the Quartodeciman disputes” [juu ya malumbano ya Ukwortodeciman].)
Irenaeus anadaiwa
na Schaff kuwa alipingwa na Victor kwa majivuno yake, ingawaje anadaiwa kukubaliana
na Victor kwenye kiini cha malumbano haya. Irenaeus alisema kuwa Mitume
waliamuru kwamba tusimhukumu mtu yeyote kwa kula nyma au vinywaji, au kwa mambo
yahusuyo siku za kuadhimisha Sikukuu au Miandamo ya Mwezi au Sabato (Wakolosai
2:16). Ndipo yeye alisema:
Ya nini mapigano au vita hivi? Ya nini haya mabishano na makano haya? Tunaishika sikukuu lakini kwa pamoja na chachu ya uovu kwa kuligawanya kanisa la Mungu kwa kuadhimisha kitu kilicho nje ya maagizo, huku tukikikataa kile kilicho cha maana, imani na mshikamano (kitabu cha Schaff, ibid., p.218).
Kuna mashaka
kidogo kuhusu maelezo haya ambapo kama Irenaeus aliishika Idi ya Mikate Isiyo
na Chachu, kama alivyofanya mwalimuwa wake. Imani ya Warumi hata hivyo
ilishinda iliingizwa kwa shuruti na Baraza la Mtaguso wa Nicaea mwaka 325 BK kwa shinikizo la kijeshi la mfalme Constantine. Baraza
Kuu la Mtaguso wa Nicaea lilianzisha upotofu
huu wote wa kusherehea Easter. Waliichukua yote kama ilivyokuwa:
… kutokuwa Wakristo kufuatia kuwatumia maadui wasioamini wa Wayahudi, na waliamuru kuwa Easter iadhimishwe kila mara katika Jumapili ya kwanza ya baada ya mwezi mkamilifu unaofuatia baada ya ikwinoks ya majira ya baridi (Machi 21), na mara nyingi huwa baada ya kuadhimishwa kwa Pasaka ya Wayahudi; kama mwezi huu mkamilifu utakuwa hivyo siku ya Jumapili, ndipo siku ya Easter itakuwa kwenye Jumapili inayofuatia. Kwa mpangilio huu iyohiyo fter the Jewish Passover. If the full moon occurs on a ,SEaster inaweza kuwa mapema zaidi, kabla ya tarehe Machi 22, au itachelewa hadi Aprili 25. Hapa ndipo Wakwortodeciman walichukuliwa wanafana maadhimisho kizushi na makosa makubwa na waliteswa na kuuawa baadhi yao kwa ajili hii. Wamontana na Wavatiasi walishitakiwa pia pamoja na maadhimisho ya hawa Wakwortodeciman. Dalili zake za mwiso ilipotea katika karne ya sita [tazama hapo juu].
Lakini hamu na nia ya usawa katika kusheherekea Easter bado ilizuiwa na tofauti iliyopo katika kuichukulia Jumapili ya Easter kwa mujibu wa kanuni ya mwezi ikwinoks ya majira ya baridi, ambayo Waalexandrian waliiweka katika tarehe 21 ya Machi, nay a Warumi ya tarehe 18; ili kwamba katika mwaka 387, kwa mfano, Warumi waliishika Easter tarehe 21 Machi, na Waalexandrians wakiwa bado hadi tarehe 25 Aprili. Upande wa magharibi pia utaratibu ulibadilika na kusababisha kurudiwa kwa utata wa easter kwenye karne ya sita na y a saba. Wakristo wa zamani wa huko Uingereza, Ireland na Scotland, na wamisionari wa Kiairishi wa Bara lile walishikamana na mzunguko wa miaka ishirini na nne, huku wakipingana mzunguko uliokuja baade wa Wadionysian au Warumi wa miaka themanini na tano, na hivyo walifananishwa na “Wakwortodeciman” na wapinzani wao Waanglo-Saxon na Warumi, ingawa ni kwa dhihaka, kwakuwa walisherehekea Easter wakati wote kwenye Jumapili iliyo katikati ya tarehe 14 na 20 ya mwezi (kwa Warumi ni katikati ya tarehe 15 na 21). Mtindo wa maadhisho ya Warumi ulishinda. Lakini Warumi waliibadilisha tena kalenda chini ya Gregory XIII. (A.D. 1583). Hivyo basi, hata sasa, makanisa ya Kimashariki yanayoiamini kalenda ya Julian na kuikataa kalenda ya Gregory, yanatofautiana na Waakristo wa Magharibi kuhusu wakati wa kuiadhimisha Easter (Schaff, op. cit., pp. 218-219).
Kumbuka kuwa Schaff
anadai ukomeshaji huu mapema, lakini utata huu unaonekana kuwa ni makosa na uwongo
wa wazi. Ulikuwepo hata na Wapaulicians na pia hata na Waweldensians na
makanisa ya Wahungari yaliyotokana kwao. Yalionekana pia kwenye Mpito wa
Wacarpathia. Ilionekana pia kutumiwa kimakosa na Wasabato (kimakosa kama
walivyofanya Wacarthars). Kwa ufupi, maadhimisho yake yanaonekana yamekoma (soma
jarida la Jukumu la Amri ya Nne Katika Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayoshika
Sabato (Na. 170) [The Role of the Fourth Commandment in the Historical Sabbath-keeping
Churches of God (No. 170)] na jarida la Cox.Kohn, Wasabato wa Transylivania, [iku Takatifu na, Cox/Kohn The Sabbatarians in Transylvania, CCG
Publications, 1998)].
Schaff anaonekana
kupuuzia ukweli wa kwamba kanisa la Uingereza lilikuwa ni la watunza Sabato
kipindi hiki chote. Makanisa ya Waceltiki yalikuwa ya wasomi wazuri wa Biblia
na walikuwa wanaziadhimisha Siku zote Takatifu na, “hata sheria ya ulaji wa
vyakula ya Agano la Kale waliichukulia kama ni sheria au Tprati ya Mungu”
(David L. Edwards, Christian England [Wakristo wa Uingereza], Vol. I, p. 27).
Waanglo-Saxons waliingia
kwenye Ukatoliki tangu mwaka 597 BK kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini na
“na kwa makamio makuu mahakama iliagizwa kwamba wasiachiliwe hadi pale
watakapokubaliana kuingia kwene upagani huu” (Edwards, ibid., p. 45). Kuingia huku
kulitanguiwa na Ethelbert mfalme wa Saxons huko Kent. Imani ya Ukatoliki na na
mapokeo ua desturi zake havikuwahi kuwepo huko Uingereza hadi ulipofika mwaka 597
BK na kisha inaonekana kuwa ilikuwa ni kwa sababu za kisiasa. Kwa hiyo maelezo
ya Schaff yanaonekana kuwa ni ya hatari sana kwa ufupi sana. Schaff anasema
kuwa haya yote ni malumbano batili ya
sheria za kidini (sic.) yangeweza kuepukwa iwapo kama yangefanika kuifanya
sikukuu isiepukwe. Hapa Schaff anakosa pointi yote ya Pasaka na Mavuno au
Mganda wa Kutikiswa. Kuweka kwao mbadala wa mazao na mzunguko wa mwezi
vinafanya mfano ashirio wa Mpango wa Wokovu, ambao imani ya kihafidhina
(orthodox) haiujui.
Mwandamo wa Mwezi Mpya na Sikukuu
Mwandamo wa Mwezi
Mpya ulikuwa ni jambo la muhimu sana katika kujua miezi ua mwezi ulopo.
Mwandamo wa Mwezi Mpya wa Nisan ulichukuliwa kuwa ni mwanzo wa hesabu ya miezi
ya mwaka kuliko ulivyo mwezi wa Tishri, kama inavyoadhimishwa kwenye dini ya
Kiyahudi tangu karne ya tatu ya zama hizi au baadakuzaliwa kwa Mwokozi. Ile
inayoitwa Rosh HaShanah, kwa mfumo wake uliopo siku hizi wa kuamua, haiwezi
kuchukuliwa kama ni maadhimisho ya kibilia au ya kipindi cha Hekalu, au kuwa imekuwa
ni maadhimisho sahihi ya Wakristo wa Kiyahudi.
Philo wa Alexandria (kitabu chake cha The Special Laws [Sheria
Mahsusi], II, xi, 41, Loeb Classical Library, Harvard University Press,
Cambridge, MA, 1937, tr. by F.H. Colson) anatuambia kuwa: “[Sikukuu] ya tatu ni
mwandamo wa mwezi mpya inaayofuatiwa na kipindi cha kutoonekana mwezi na jua”. Na:
“Huu ni Mwandamo wa Mwezi Mpya, au mwanzo wa mwezi mwandamo, unaotokea kipindi
cha katikati ya kipindi cha kutoonekana mwezi na cha pili chake, na urefu ambao
kinahesabiwa kikamilifu kwenye shule za elimu ya anga” (ibid., II, xxvi, 140).
Yapasa ikumbukwe pia kwamba toleo la Machapisho maarufu la ya Hendrickson [Hendrickson
Publishers edition (1993)] la tafsiri ya C.D. Jonge ya mwaka 1854 halina taarifa
kwamba tafsiri ya Colson inatoa. Yanayoashiria
ni kwamba vipindi vya kutoonekana mwezi kilichukuliwa katika kuamua siku ya
Kwanza ya mwezi.
Wasamarita na Masadukayo
makundi yote mawili yaliamua kalenda yao kwa kufuata kipindi hiki cha
kutoonemana mwezi, maadhimisho ya sikuu yalipangwa kwa kuafuata kpindi hiki cha
kutoonekana mwezi kwa imani za wote wawili kipindi cha kuwepo kwake Hekalu,
isipokuwa tu kwa Essene ambao walikuwa na kamilifu na isiyobadilika, ambayo
siku ya 14 Abibu iliangukia siku ya Jumatano klla mwaka, na ongezeko lake kwenye
mzunguko wake usiobadilika. Wasamaria waliona kuwa Mwandamo wa Mwezi unaanza
kutegemeana mbadilishano ya siku hii (soma jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156) [God’s Calendar
(No. 156)’.
Wasamaria walianzisha
makosa kwenye kalenda, wakati kwamba waliamua kwamba Mwandamo wa Mwezi Mpya wa
Mwaka wa Kwanza ni lazima kila mara uangukie kwenye ikwinoks au baadae; na
ikwinoks yenewe ikiangukia tarehe 25 Machi. Hesabu za (1988-2163 BK) kama
ilivyoonyeshwa na Kuhani Eleazar ben
Tsedeka, zimejumuishwa kwenye kitabu cha maombi ya Pasaka na Mazzot, Knws
tplwt hg hpsh whg hmswt (Holon, 1964, pp. 332-336; sawa na asemavyo
Reinhard Pummer kitabu chake cha Mapokeo ya Kidini ya Wasamaria [Samaritan
Rituals and Customs], pp. 681-682, fn. 201 in Alan D. Crown (Ed.), The
Samaritans, 1989, J.C.B. Mohr (Paul Siebeck) Tübingen). Ukweli huu pia inaashiria
kwamba tunaangalia kwenye chanzo cha zama kale cha kawaida, ambayo ina msingi
kwenye kalenda inayotumika wakati ikwinoks ilikuwa tarehe 25 Machi. Tarehe hii
kwa muda mrefu ilitanguliwa na kipindi cha Kristo na iliwekwa uwiano wake
kwenye kalenda ya Kaisari Julius (sawa na maoni ya David Ewing Duncan, The
Calendar, 4th Estate London, 1998, p. 81).
Hii inaashiria
chanzo fulani cha makosa. Zamani hapo kale uamuzi wa kipindi cha kutoonekana
mwezi kilikuwa ni tarehe 25 Machi na inaonekana imetokana na kipindi cha Kwanza
na cha Pili cha Hekalu na inaashiria kwamba huenda tunaangalia kwenye asili
halisi ya kalenda ya Yeroboam (soma jarida la Yeroboam na Kalenda ya Hileli (Na. 191) [Jeroboam
and the Hillel Calendar (No. 191)]. Kwa hiyo, kitendo cha kuiadhimisha Sikukuu Mwezi
wa Nane kama kilivyokemewa na Biblia, kingetokea tangia kitendo cha kuuweka
mwezi wa Mwezi Mpya ambacho mara nyingi knatokea kabla au baada ya ikwinoks. Hii
inaonekana kuwa haikubadilishwa na kwa suala ya Wasamaria tangu kuanguka kwa
taifa la Israeli. Kwa sababu hii, waliangukia kwenye laana na wamekuwa ni
masalia pekee ya Israeli ambao hawajabarikiwa na ahadi ya uzaliwa wa kwanza ya
Yusufu. Hesabu au tarakimu ya Wasamaria zilitunza kiusiri, huenda ilitokana na
sababu hii. Hata hivyo, wao pamoja na Masadukayo kilamara waliamua kalenda
kutokana na muunganiko, jambo ambalo lilikuwa ni la kawaida wakati wa kuwepo
kwa Hekalu.
Kalenda ua ‘Ukristo’
Wasomaji
wanapaswa kujua kwamba hakukuwa na sheria ya uhairisho kwenye Kanisa la kwanza.
Waandishi wa kwanza walikuwa wavumilivu na maamuzi tunayoyafanya kuhusu mambo
haya ya kufanyia maamuzl kuhusu ni kalenda gani ambayo Wakristo wanapaswa
kuitumia. Tunaporudi nyuma kufanya rejea kwenye maandiko ya zamani ya Wayunani,
tunaona kuwa tafsiri za Kiingereza bado zinatumia neno hili la kipagani la Easter wanaolitafsiri neno Pasaka. Neno
Easter ni upotoaji wa watafsiri wa kipindi cha baadae wa Kitrinitarian walioitafsiri
Biblia. (kama vile kwenye
Matendo 12:4) na maandishi ya Kanisa la kwanza kwenye Kiingereza.
Hippolytus (170-236 CE), kwenye kitabu chake cha Makanuso ya Uzushi Wote [The Refutation of All Heresies], VIII, xi (ANF, Vol. V, p. 123), aliandika:
Easter [Pasaka] inapaswa iadhimishwe siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, sawasawa na maagizo na amri za Torati, wa siku yoyote inayoangukia (katika mwezi) itakapotokea.
Anatolius wa Alexandria (yapata miaka ya 230--ca.280 BK) alisema kwenye kitabu chake cha The Paschal Canon [Kanuni ya Kuadhimisha Pasaka] (ANF, Vol. VI, pp. 146-147):
(I) Ni kama [Isodore, Jerome, Clement] walivyotofautiana
pia kwenye lugha na kamwe hawakufikia muafaka kila mmoja wao na kwa namna kuu
ya kuchukuliana kisawasawa na siku ya Easter [Pasaka] na mwezi wake na wakati
wa kukutanika kwa mujibu wa kuupa heshima kuu ufufuko wa Bwana. Lakini Origen pia,
na mtu mgumu kuliko wote na aliyejitahidi kufanya majumuisho ya kihesabu, .... amekchapisha
kwa namna ya kujiamini sana na kwa majivuno kijitabu kidogo kinachoielezea
Easter. Na kwenye kijitabu hiki ,manapokuwa akitangaza kwa heshima zote siku ya
Easter, kwamba haghari inapaswa itolewe sio tu kwenye chanzo cha mwandamo wa
mwezi na mwenendo wake kwenye ikwonoks bali pia kifungu cha jua, (II) Kwa hiyo,
katika mwaka wa kwanza mwezi mpya wa mwezi wa kwanza, ambao ndiyo mwanzo wa
kila mzunguko wa miaka kumi na tisa, kwenye siku ya sita nay a ishirini ya mwezi
ambao unaitwa na Wamisri wa Phamenoth. Lakini kutokana na miezi ya Makedonia.
Lakini kwa mujibu wa miezi ya Wamakedonia, ilikuwa ni siku ya pili na ya
ishirini ya Dystrus. Na kama
ulimwengu wa Warumi unavyosema, ni siku ya kumi na moja kabla ya Wakalends [siku
ya kwanza] ya Aprili. (III). Na hii inawezakuwa walijifunza kutoka kwa Philo, na
Josephus, na Musaeus wameandika Waagothobuli wawili, ambao walikuwa ni moja ya
wale sabini na mbili waliopewa majina ya kuwa ni Mabwana, na kwa haraka Aristobulus,
ambaye alikuwa ni mmoja ya wale Sabini waliotafsiri Maandiko Matakatifu ya
Kiebrania kwa Ptolemy Philadelphus na baba yake.... waandishi hawa, kwa kutatua
baadhi ya maswali yanayoinuka kuhusu kitabu cha Kutoka, wote wanatakiwa kutoa
dhabihu ya Pasaka kipindi cha baada ya ikwinoks ya majira ya baridi katikati ya
mwezi wa kwanza. Na hi inakutikana wakati jua linapozama upande wa magharibi
mwa ncha ya dunia, au kama wengine wanapoita hali hii kuwa ni mzingo wa kupunga
jua magharibi. (IV) Lakini huyu Aristobulus pia anaongeza, kwamba kwa habari ya
sikukuu ya Pasaka ilikuwa muhimu sio tu kwa jua kupita tu juu ya nyakati za
ikwinoks, bali mwezi mwandamo pia.
Anatolius anaedelea
mbele zaidi kutoa maelezo mengine yanayovutia zaidi kuhusiana na hesabu ya
mwezi, na umuhimu wa ikwinoks kufanyika kabla ya wakati wa kutoa dhabihu alasiri
ya siku ya Kumi na nne; pia kwa kipindi hiki cha siku ya kumi na Nne hadi siku
ya Ishirini na moja inapaswa kuwa ni kipindi cha mwezi kuwa mkamilifu kuonekana
kwake, kwa ajili ya uhusiano wake na nuru ya ulimwengu. Malumbano hayahusiani
na maji au kitu kingine chochote kinachotakiwa kiwepo wakati wa kila Siukuu
inapofanyika na kwa hiyo kiondolewe kama ulivyo sheria ya kawaida; lakini
ilifana kazi ili kuonyesha kanuni ya kuweka mbadala wa siku ya Kumi na Nne ya
mwezi wa Abibu na ikwinoks. Malumbano haya pia yanaonesha kwamba siku za Kumi
na Nne nay a Kumi na Tano zote mbili ziliadhimishwa na kwamba zote wakati
uliweza kuhesabiwa sio tu kwa kufuatia mwezi, lakini pia ni kwa kipindi cha
siku ya ikwinoks na uhusiano wake na Mwezi wa Kwanza na mwezi mkamiIifu.
Kutoka kwa
Anatolius, tunaona kuwa msingi wa kuhesabu ulikuwa ni kwamba ikwinoks inapaswa
iangukie katika Siku ya Kumi na Nne, lakini sio zaidi ya saa 9 alasiri, au
sadaka ya saa za usiku, kama ilivyokuwa baadae. Kwa hiyo, malumbano yaliyoko
sasa kwamba ile Pasaka ya mlo aliokula Kristo haina msingi wala uhusiano na
ukweli wa mambo ya kihistoria. Wasamaria bado wanashika wa siku mbili na hilo
limeelezewa kwa kna kwenhe jarida la Usiku wa Kuuadhimisha Sana (Na. 101) [The Night To
Be Much Observed (No. 101)].
Asili iliyohusiswa na mabishano ya wataalamu wa mambo ya anga inaonyesha
kwamba walikuwa na uwezo wa kufanya utata huu wa kimahesabu, na walifanya hivyo,
wakati malumbano kuhusu uadhimishaji wa siku ya mwandamo wa mwezi kwa Wayahudi
wa siku hizi na Kairites inaonekana kuwa si kitu muhimu wakilenga kuupa mashiko
utaratibu wao unaojulikana kama wa ahirisho, na mbaya.
Anatolius anafanya
makosa pia kwenye utaratibu wa Mikate Isiyo na Chachu, ambao unaweza kuonwa na
kuigwa kutoka kwenye Biblia na pia kwenye matendo na imani ya Wasamaria (cf. ANF,
Vol. VI, pp. 146-151).
Anasema kwenye makala
yake isemayo ‘Meza ya Pasaka’ kwamba Pasaka ilizunguka kwa miaka zaidi ya
mzunguko wa miaka kumi na nane kati ya siku ya 6 kabla ya Kalends ya Aprili na
siku ya 9 ya kabla ya Kalends ya Mei (ibid., p. 150). Kwa hiyo Pasaka
iliangukia kati ya tarehe 24 Machi na 21 Aprili. Wazo la kwamba Pasaka ingeweza
kutokea tarehe 25 Aprili haliwezekani, iwe ni kwa kihstoria au kwenye imani ya
siku hizi ya Kiyahudi. Ilitokea tu kwenye utaratibu au mfumo wa kuadhimisha Easter,
kama tulivyojionea hapo juu.
Anatolius anaithaminisha
pia kwa kuonyesha kuwa siku ya Kumi na Tano ilianza di ya Mikate Isiyo na Chachu, na kwamba Pasaka hii inaweza na
iliwezekana kwenda hadi siku ya Ishirini ya mwezi, na kuendelea hadi mwishoni
mwa Mikate Isiyotiwa Chachu kwa sababu ya kuiiingiz Jumapili badala yake (ambayo
yeye aliita kuwa ni Siku ya Bwana), ambayo pia ni Siku ya Mganda wa
Kutikiswa (ibid., XI, p. 149). Ni dhahiri
kabisa kwa kipindi hiki kwamba mkazo ulikuwa ni kwenye kipindi cha kuanzia siku
ya 14 Abibu hadi siku Jumapili ya Mganda wa Kutikiswa, wakati wowote inapoangukia
– bali pia waliishika Idi ya Mikate Isiyo na Chachu kwa kipindi cha siku saba
mfululizo. Inaonekana kwamba, kutokana na makosa ya kimahesabu, wangweza kuila
Mikate Isiyo na Chachu kwenye jioni ile tu ya Siku Takatifu ya mwisho, lakini
malumbano ni ujinga. Anatolius, hata hivyo, anasema kuwa Sikukuu haiwezi
kusherehekewa siku ya 22 au ya 23 ya mwezi huu (ibid., VII, p. 148). Kwa hiyo, siku ya Ishirini na moja
ni ya mwisho kwa maadhimisho ya Sikukuu na Mganda wa Kutikiswa au Siku ya Bwana
ni lazima iangukie siku hii au kabla ya siku ya 21 Abibu, mwezi wa Kwanza.
Utaratibu wa
kuhesabu hii inayoitwa Easter ulifanyika kwa kutokana na Mtaguso wa Baraza Kuu
la Nicaea mwaka 325 BK. Kutokana na Mtaguso wa Barz hili kipaumbele kilitolewa
kwa Alexandria na papa au askofu wa Alexandria alikuwa na jukumu la kuweka
utaratuibu wa kimahesabu. Desturi au mapokeo ya kijadi yalishinda na
kuchukuliwa huko Roma na pia huko Anthiokia (cf. ANF, Vol. 2, p. 342).
Imani hi ya kipindi
cha baada ya mtaguso wa Nicaea iliwekwa baadae na mfalme Constantine I (306-337
BK), unaweza kuonyesha kwa kina zaidi aina ya matatizo ya kikalenda ambayo
tunakabiliwa nayo. Andiko lililo kwenye suala hili limewekwa pia kwenye jarida
la Kalenda na Mwezi: Ahirisho la Sikukuu? (Na. 195) [The Calendar and
the Moon: Postponements or Festivals? (No. 195)].
Waraka wa Constantine, wa mwezi Augusti,kwa makanisa. ...
Wakati swali lilipojitokeza kuhusiana na siku takatifu sana ya Easter, ilitangazwa kwa mtazamo wa kawaida ifae, kwamba sikuu hii inapaswa kusherehekewa siku hiyohiyo na wato wote, na pahala pote. ... ilionekana na kla mmoja kuwa ni kitu kisichostahili kwa sisi kufuata desturi Wayahudi katika kuisherehekea sikukuu hii muhimu na takatifu sana iliyoipunguzia nguvu au kuinajisi! Ikichafulia mikono yao kwa uhalifu mkuuna, kama ulivyoyapofusha nia na mioyo yao. Ni vyema kwa hiyo, kwamba kuyakataa matendo ya watu hawa, tutapangilia na kuwekea mkazo kwenye maadhimisho ya zama zijazo mbele yetu na maadhimisho ya kanuni zote, kwa utaratibu ulio halali, tulizozishika tangia siku ya kwanza ya mateso ya Bwana wetu hata kwa siku hizi. Hebu na tusiwe na kitu kingine zaidi cha kawaida zaidi ya kuwa na uadui na Wahayudi. Tumepokea mtindo na utaratibu mwingine kutoka kwa Mwokozi. Sababu nyingine ya kisheria zaidi na halisi au njema iko wazi kwenye dini yetu tukufu na takatifu zaidi. Kwa kuifuatia sababu hii kwa mtazamo usio rasmi sana, hebu na tujitoe, ndugu zangu wastahiki sana, kutoka kwene ushirika huu usio na mwelekeo. ... Kama itakuwa muhimu au lazima kwamba makosa haya yanapaswa kurekebishwa ili tusiwe na lingine kwa kawaida na kuyatumia matukio haya maangamivu na mauaji ya Bwana wetu, na hivyo kwamba utaratibu iweze kuwa muafaka zaidi unavyofanyika na makanisa yote ya Magharibi, pamoja nay ale ya upande wa kusini na kaskazini ya dunia na kwa baadhi ya yale ya Mashariki, ilihukumiwa kwa hiyo kuwa ni muhimu na sahihi sana, na mimi mwenyewe niliahidi kwamba mpangilio huu ufikilize matakwa na matarajio yenu, sambamba na desturi zinazoonekana kupendwa na kushinda kwa kishindo kwenye miji ya Roma na na maeneo mengineyo yote ya Italia, Afrika na Misri, Uhispania, Gaul, Uingereza, Lybia, Ugiriki kote, dayosisi za Asia, Ponto na Kilikia, ingependeza sana kama zilikumbatiwa na hekima na ujanja wenu, ... na kutokuwa na uhusiano na uvunjaji maagano na Wayahudi. Na kuhesabu vyote kwa maneno machache, inakubalika kwa hukumu za wote, kwamba sikukuu takatifu zaidi ya Easter inapaswa isherehekewe mara moja na kwa siku moja (kwa mujibu wa kitabu cha A Historical View of THE COUNCIL OF NICE; with a TRANSLATION OF DOCUMENTS by Rev. Isaac Boyle, D.D.; T Mason and G Lane, New York, 1839; pp. 51-54).
Sio tu kwamba tunaifikilia ngazi ya juu ya nguvu za udanganyifu au upotevu, propaganda, na imani ya kidini, bali pia tunajionea mwonekano wa kiini cha upingaUsemitiki kwenye desturi za Magharibi kutoka kwenye serikali ya kidunia ya siku zile.
Ni jambo linalostahili kuona kiasi cha mlipuko wa upinzani, katika Uingereza ukiangukia kwenye ushambuliaji ya kikalenda na kueneza ukomo wa kidini. Mwanahistoria wa Kiingereza na askofu, Bede (takriban miaka ya 672-735 BK), kwenye jarida lake la Historia ya Kanisa ua Waingereza [[Ecclesiastical History of the English People], hususan kwenye sura za 25-26 za Kitabu chake cha III, alikuwa na mengi ya kusema kuhusu sinodi na kuhusu mijadala iliyoitishwa na Mfalme Oswy (mwaka 612-670), hasahasa miaka kati ya Askofu Colman na mkereketwa wa Kirumi, Wilfred, Abbot wa Ripon, kwenye jumba la kitawa la huko Streanaeshalch, kama vile. Jumba la watawa la St Hilda ambako walidai kuwa ni Sinodi ya kihistoria (na maarufu) ya huko Whitby ya mwaka 664 BK.
Bede anaweka hii wazi sana kwamba kuhesabu siku ya Easter halikuwa ni jambo la kimbinu tu au ni jambo lililoachwa. Vuguvugu la Easter lilikuwa ni moja wapo ya mambo mengi ambalo mabishano yake kwa jina la ishara (kama tungalivyoweza kusema, lakini ishara ni kwa sisi kujaribu kulipunguza neno siri ambalo wangelitumia kusema) lilonyesha kujawa na maana ya Easter kuwa ingeweza tu kuwa kwenye ikwinoks, kwa kuongezea siku zilizotolewa na ushindi wa Kristo dhidi ya nguvu za giza. Ilipaswa iwe kene mwezi wa kwanza wa mwaka unaoendana na mwonekano wa mwezi mwandamo, kwa kuwa huu ulikuwa ndio mwezi ambao ndio dunia iliumbwa kwao na ni ambao unapaswa ufanyiwe umbaaji wake upya. Ilitakiwa iwe kama vile mwezi unaoishilia kwa mwezi unarudi ardhini pamoja na vitu vya mbinguni [Ufunuo 12:1; Malaki 4:2; Luka 2:32; Isaya 60:1-3]. Ni kweli na dhahiri kabisa kuwa Easter inatakiwa mara zote iangukie ndani ya kipindi cha siku saba, kwa kuwa tarakimu hii sappropriate that Easter should always fall within a space of seba ilikuwa na maana ya kimungu. Kwa kutitilia maanani kutoka kwenye mtazamo wa aina nyingine, Easter inaweza kuhesabiwa kwa namna ile kama kuhitimisha Torati yote ya Wayahudi na Sheria au amri mpya ya Kristo. Kama ilisherehekewa wakati wa usiku, basi wote walikuwa kwenye mtangamano. (kwa mujibu wa kitabu cha Introduction, p. xviii, by James Campbell, who translated Bede’s The Ecclesiastical History of the English People for The Great Histories Series by Washington Square Press, NY, 1968).
Hii ndiyo sababu, kwa mfano, mwaka 1997 tuliadhimisha ibada ya Mganda wa Kutikiswa Jumapili ya tarehe 15 Nisan na kutoka siku ile tulianza hesabu kuelekea Pentekoste, na ndiyo maana mfumo wa makanisa makongwe unangoja hadi Jumapili hii au inayofuatia (ambayo ilikuwa ni siku kamili ya 22 Nisan mwaka 1997) kusherehekea Jumapili ya Easter na ambayo ndiyo hesabu kuelekea Pentekoste ilianza. Utaratibu huu umewekwa ili kuhakikiswha kwamba Kanisa la Kitrinitarian kidogokidogo lifuate Sheria za Biblia na ambayo mara nyingi ni juma moja na Pentekoste.
Kabla ya kunukuu moja kwa moja kutoka kwa Bede, hebu na tuone maandiko ya bango kitita (namba 44, kurasa za 400-401):
Wote wawili, yaani Wacelts na wapinzani wao wanakubaliana kwamba Easter ilipaswa kuhesabiwa kwa kukumbu umuhimu wa mwezi kuwa mkubwa na mkamilifu ukiwa umejitokeza au kwanza tu baada ya ikwinoks ya majira ya baridi. Lakini Waceltiki walishikilia kuwa Jumapili ya Easter kuwa ni ile inayotokea katikati ya siku ya kumi na nne ya mwezi (yaani, siku ya mwezi mkamilifu) na siku ya ishirini, zote zikijumuishwa. Hivyo ni kusema kwamba kama mwezi mkamilifu utakuwa siku ya Jumapili, waliifanya kuwa ni Jumapili ya Easter. Makanisa mengine yalikataa kuifa siku hi ya mwezi ,ka,ilifu kuwa ni Jumapili ya Easter kwa hiyo mtinda alioutumia Bede na ambao ulikujakiuwa ni wa ulimwenguni kote wa magharibi. Wakiichukulia Jumapili ya Easter kuwa ni ilw inayoangukia, sawa na ile iliyoangukia katikati ya siku ya kumi na tano na ishirini na moja ya mwezi. Kama mwezi mkamilifu utakuwa inayofuatia au inayofuatia baada ya ikwinoks inayotokea siku ya Jumapili, ndipo Jumapili inayofuatia inakuwa ni Jumapili ya Easter.
Baada ya Askofu Colman kuonyesha kwamba maadhimisho yake ya Easter yalichukuliwa kutoka kwa wazee wake na kwamba ilikuwa ni “ileile ambayo mwenyeheri Mwinjilist Yohana, mwanafunzi na hasa ni kipenzi chake Bwana, aliiadhimisha”, mwanzilishi wa Utaratibu na imani ya Wabenedictine huko Uingereza, ndipo Wilfred, alijibu:
Easter ambayo tunayoiadhimisha tumeona ikisherehekewa na watu wote huko Roma, ambako wenyeheri na wabarikiwa Mitume Petro na Paulo waliishi, wakafundisha, kuteswa na walizikiwa. Hivi ndivyo tulivyoona iliadhimishwa na wote huko Gaul na Italia wakati tulipotembelea kwa kupita huko kujifunza na kuomba. Hii tumejifunza kuwa ni matendo ya ya watu wa huko Afrika, Asia, Misri na Ugiriki, na ulimwenguni kote ambako imani ya Kristo imeenea kwa aina mbalimbali za watu, mataifa na lugha; wote wanafanya matumizi ya njia moja ya uwekaji wa tahere ya Easter. Kitu pekee cha tofauti ni watu hawa na inakalisha kwenye ubishi. Namaanisha kuwa Wapicts na Waingereza ambao (wakazi wa visiwa viwili vya mwisho vya bahari, na ni sehemu yao pekee) wamesimama kinyume na ulimwengu wote, wakijitahidi kupigania kijinga mno (ibid., pp. 160-161).
Maelezo yaliyofuatia ya Wilfred yanapumbaa, hasa wakati tunapojua kwamba wote wawili wamekosea; lakini Wilfred anaonekana kuongopa kwa dhahiri sana na anaambiwa:
Na litupitie mbali jambo hili kumbadilisha Yohana kijinga, kwa kuwa yeye aliyashika maagizo ya Torati ya Musa kikamilifu na kimatendo, kipindi kile wakati kanisa lilikuwa linafuata bado linawafuata Wayahudi kwa mambo mengi, na Mitume hawakuweza kuachana nazo kwa ghafla maadhimisho yote na ushiaji wa Torati iliyotolewa na Mungu… Kwa hiyo, kwa mujibu wa mapokeo na maagizo ya Torati alianza kuadhimisha sikuu ya Easter majira ya jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, bila kujali kama iliangukia siku ya Sabato au kwenye siku nyingineyo (pp. 161-162).
Tunaweza kujua ukweli kwamba hakukuwa na uahirisho kwenye matumizi haya hapa. Wilfred halafu anaendelea kujikanganya kutoka na kile alichosema na anaunga mkono ukiri au imani ya Kikatoliki.
Ruaya hii ya maamrisho ya kilimwengu ya kuweka hesabu na utaratibu wa namna ya kuchukulia mkanganyiko wa maadhimisho ya Pasaka/Easter yamekuwepo kwa karne nyingi. Kitabu cha fasiri kijulikanacho kwa jina la The New Catholic Encyclopedia kinaeleza:
Kwa kuwa idadi kubwa ya Wakristo wa mwanzoni walikuwa ni waongofu wa jamii ya Wayahudi, inajulikana kutokana na kuwekwa kwa kalenda ya Kikristo kulisimamiwa na ukweli wa kwamba kufa na Kufufuka kwa Kristo kumefanyika kipindi cha sikukuu kubwa ya Wayahudi, ya Paeaka iliyoadhimishwa siku ya 14 ya mwezi wa Nisan ambayo ni kipindi cha mwezi mkamilifu uliofuatia baada ya siku ya ikwinoks ya majira ya baridi. Hata hivyo, badala ya kufuata kimatendo na moja kwa moja Pasaka ya Wayahudi, kwa kuwa hii ingelazimisha maadhimisho ya Ufufuko siku nyingine ya juma kila mwaka. Desturi na mapokeo ya Kikristo (yalikatazwa na Baraza la Mtaguso wa I wa Nicaea mwaka 325; kwa ConOecDecr 2-3, n.6) yaliweka maadhimisho ya Ufufuko wa Kristo kwenye siku halisi maalumu ya wiki waliyoiteua. Matokeo yake, Easter inaangukia katika siku ya kwanza ya juma (Jumapili_ baada ya mwezi mkamilifu wa kwanza inayofuatiwa na ikwinoks ya majira ya baridi na hivyo inafanyika mapema sana baada ya tarehe 22 Machi na kama imechelewa sana haizidi tarehe 25 Aprili [wakati itakaporudia tena kuwa na mwezi mkamilifu baada ya ikwinoks] (ibid., McGraw Hill, NY, 1967, pp. 1062-1063).
Tarehe za hivi karibuni kabisa hapa hazihusiani uwekaji wa tarehe za
Pasaka za siku za 14-15 Abibu au Nisan, bali inahusiana na tarehe za hivi
karibuni kabisa ambazo Jumapili inaangukia. Na ambazo inaweza ni siku nyingi baada ya siku ya 14 ya mwezi wa
Kwanza. Tarehe za hivi karibuni kabisa zinazowezekana kuwa Pasaka inaweza
kuangukia imeonyeshwa na kanuni za zamani, ambazo pia zinasema kuwa jua lipo
kwenye mkao unaoashiria alama ya Kondoo au Aries. Jua linaondoka kwenye Aries
tangu tarehe 10-20 Aprili na ni tarehe inayoonekana kuwa muafaka kwa maadhimisho
ya Pasaka ni kabla ya tarehe 20-21 Aprili.
La muhimu zaidi
kutoka kwenye nukuu hizi hapa ni kwamba, tunaona kwamba ushawishi wa dini zote
hizi mbili, Roma (iliyofuatia baadae) nay a Kiyahudi zina haya yote, lakini zimetatizwa
kwa kutoijua Pasaka ya kweli. Muundo wa baadae wa Wahafdhina au Orthodox umeleta
matatizo na hata utata mkubwa zaidi kwa kile walichokiiga baadae kutok kwenye
dini ya Kiyahudi knachojulikana kama uahirisho na kisha hatimaye waliishika
Easter yao juma moja baada ya tarehe za Wayaduhi za 14-15 Nisan.
Kutokana na maandiko yaliyo kwenye jarida
la Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235) [The Origins of Christmas and
Easter (No. 235)], tunaona kwamba mabishano ya Nicaea yalikuwa
yanaanzishwa tu mgogoro wa mwanzo wa uingizaji na uwepo wa matendo na imani za
kipagani. Hayakuweza kutatua malumbano ya Wakwortodeciman. Tunarudia andiko
lile kwa ajili hii.
Mfumo wa kuhesabu
‘siku ya Jua’ kwenye ikwinoks ya majira ya baridi ulikuwa sawa na ule wa
kuhesabu siku ya kutoa sadaka ya Mganda wa kutikisa ya Walawi 23, lakini
haikuwa sahihi na haikulingana. Na hii ndiyo sababu kuna utofauti kidogo kati ya
maadhimisho ya Pasaka na Easter.
Kamusi maarufu ya
Universal Oxford Dictionary inatoa
utaratibu wa jinsi ya kupangilia uwekaji wa Jumapili ya Easter ai siku ya Easter,
ambayo ni siku halisi ya mungu Jua kama ilivyo Easter.
Iliadhimishwa
Jumapili ya kwanza baada ya siku ya wwezi mkamilifu kwenye kalenda, kama vile
siku ya 14 ya kwenye kalenda ya mwezi—inayotokea
tarehe 21 Machi au baadae. Wanaichukulia kuhusiana na juma linaloitangulia
Jumapili ya Easter (1964 print, p. 579).
Hii ndiyo kanuni
ya kuipangilia sikukuu ya Easter au Ishtar na sio kanuni inayotumika kuweka siku
ya kuiadhimisha Pasaka ya kwenye Biblia.
Malumbano haya
yanaonekana wazi kwenye Historia ya malumbano ya Wakwortodeciman, ambayo
yametokea tangu utawala wa Anicetus hadi ule wa Victor (au Victorinus), askofu
wa Roma tangu karne ya kati nay a pili (yapatabkama 154-190).
Kwa hiyo, kutokana
na malumbano ya Wakwortodeciman tunajua kwamba makosa haya ya utaratibu wa
kupangilia tahere ulikuwa umeanzishwa kutoka Roma katika karne ya pili, na ulipingwa
na wale waliokuwa Kanisani waliokuwa wanafundishwa na Mitume, mmojawao
alijulikana kama Polycarp aliyempinga Anicetus, na mwanafunzi wake Polycrates, akimpinga
Victor (au Victorinus). Maandishi ya baadae ya Socrates Scholasticus (yapata
mwaka 439 BK) yanaonyesha makosa yaliyofanyika kwenye historian a hayako sahihi
kwenye idadi ya maeneo, mengi yake ni yale yaliyoonyeshwa na ukusanyaji wa Makasisi (wenyewe huwaita Mababa) wa zama za
Nicene na hata wa Baada ya Nicaea (kwa mujibu wa kitabu cha NPNF 2nd series, Vol. 2, introduction to
the text[utangulizi wa maandiko]).
Socrates anakumbuka
kwamba Wakwortodeciman waliadhimisha siku ya 14 ya mwezi bila kujali kama
ilikuwa ni Sabato (ibid., Ch. XXII, p. 130). Ameandika kwamba ilikuwa ni Victor,
askofu wa Roma, aliyewatenga kwenye ushirika na alikuwa amelaumiwa kwa hili na Irenaeus
(ibid.). alijaribu kuanzisha, kwenye hatua hii ya kuchelewa, akiweka rufaa yake
kwenye maandiko na nasaha za Petro na Paulo ili vimsaidie kulinganisha matendo
ya Warumi kuhusu uadhimishaji wa Easter na matendo au msimamo wa
Wakwortodeciman wakiwa na Yohana (ibid., p. 131). Alidai kwamba hakuna upande unaoweza
kutoa ushuhuda wa kimaandishi kuthibitisha mtazamo wao. Hata hivyo, bado
tunajua kiusahihi sana kwamba Wakwortodeciman waliyachukua maandiko ya Yohana
kutokana na maandiko ya kina Polycarp na Polycrates, ambao walikuwa
wamefundishwa na Yohana. Hakuna rufani iliyofanywa kwa Petro na Paulo kusaidia
kuihalalisha Easter kwa namna iliyo makini sana. Zaidi sana, inaonekana kuwa ni
upuuzi kuamini kwamba Mitume wale Kumi na mbili wangegawanyika katika jinsi ya
kuhesabu ili kuipata siku ya Pasaka.
Socrates yuko wazi
kwa kitu kimoja, ambacho ni kwamba Kanisa na Wakwortodeciman hawakuzishika siku
maadhimisho ya Pasaka kwa mujibu sawa na
utaratibu wa kuhesabu walionao Wayahudi walioko leo (aliandika yapata mwaka 437
BK, siku nyingi baada ya kuanzishwa kwa kalenda ya Hilleli mwaka 358). Anashikilia
kwa kuwaona kuwa walikosea karibuni kwenye kila kitu (ibid., p. 131).
Kwa matendo haya
walikuwa wamuzuiwa, hawakuthibitisha kuwa walikuwa Wayahudi wa siku hizi,
waliokosea kwenye kila kitu, lakini kwa wale wa kale na kwa mujibu wa Josephus kwa
kile alichokiandika kwenye kitabu chake katika karne ya tatu juu ya hili Zama za Kale za Wayahudi.
Anataja Zama za Kale za Wayahudi, III, 10, ulionukuliwa
hapa kikamiiifu:
Katika mwezi wa Xanthicus,
tunaouitwa wa Nisan, na ni mwanzo wa mwaka, siku ya kumi na nne ya mwezi,
wakati jua linapokuwa kwenye mwonekano wa ishara ya Aries (Ndama), kwa kuwa
wakati wa mwezi huu tunaona tulikombolewa kutoka utumwa wa Wamisri, ndipo pia
alipoamuru kwamba tumtolee sadaka kwa kila mwaka dhabihu ya kama tulivyotoka
Misri, walituamuru kutoa dhabihu iliyoitwa ya Pasaka.
Ishara ya Aries iliishia
tarehe 19-20 Aprili na ambapo Pasaka isingeweza kuangukia baada ya kipindi hiki
(Anatolius anaamini ilikuwa ni tarehe 21 Aprili kama hapo juu). Hata kama
ingekuwa siku hii ya 14 ingeangukia kabla ya ikwonoks; na kwamba tuna kigezo
kwa Pasaka. Hapa tunaona kwamba Kanisa la kwanza halikufuata mapokeo ya baadae
ya Wayahudi yaliyotungwa na Hilleli. Nukuu nyingi za Socrates zinapuuzia
kipande hiki muhimu sana kwa ushahidi.
Siku ya
Maandalizi ya 14 Nisan ilikuwas ni ile iliyoonekana ya kikale zaidi kama ni
mwanzo wa Pasaka na siku ile ingeangukia kwenye ikwinoks; lakinni siku ya 15
Nisan, ambayoo ndiyo ilikuwa ni Siku Takatifu ya Kwanza na ni usiku ambao
Pasaka ilikuwa inaliwa, isingeweza kuangukia siku ya ikwinoks. Matendo ya kale
ni msingi kwa kanuni ya sasa, lakini baada ya mtawanyiko, Wayahudi
waliadhimisha siku ya 15 Nisan na sio siku zote mbili kama walivyofanya
mwanzoni, sawa na maagizo ya Kumbukumbu la Torati 16:5-7.
Tumeona pia
kutoka kwa Socrates hapa kwamba Baraza la Mtaguso wa Nicaea halikuweka wakati
maalumu wa kusherehekea Easter kama alivyodai Audiani (soma kitabu cha NPNF,
ibid., p. 131 and fn. 14 to p. 131). Tunajua iliamuliwa sawasawa na mapokeo ya
kale, ambavyo ni, kwa mujibu wa ibada za mungu Adonis na mungu Attis, wakichanganya
na mungu Ishtar au Venus na ibada za mungu Jua. Ilitatua mgogoro kwenye muundo wa imani za
kipagani za miungu Attis na Adonis. Mtaguso wa Nicaea uliichukua na kuiingiza
Eatser na kuifanya kuwa ni sikukuu rasmi wakitumia matendo na mapokeo yaliyokuwepo
ya kipagani, bali pia waliichanganya nayo. Hakikuitunga wala hawakuianzisha
sikukuu hii. Wayahudi waliianzisha na kuiendeleza kalenda potofu kabisa mwaka 358,
sio mbali baada ya Mtaguso wa Nicaea, kama tunavyoona kutoka kwa Socrates. Tukio
hili linakaribiana sana na kipindi cha karibu na wakati wake, na kwa hivo, kujulikana
kwa ufasaha zaidi.
Kwa hiyo, Pasaka
ya Wakristo ilikuwepo kabisa bali ilikuja ondolewa na upagani, ulianzisha na
kuiweka Easter au kalenda ya uwongo na potofu ya ya marabi wa Kiyahudi na
kuondoa siku za kuiadhimisha Pasaka za mwezi Nisan zinazotokana na mwezi
mwandamo. Baraza la Mtaguso wa Nicaea lilitangaza kwamba uwekaji wa siku ya
kusherehekea Jumapili ya Easter kwa kuishagua Jumapili inayofuatia mwezi
mkamilifu utokee kwanza kulifanya hii iwe haiwezekani kabisa (lakini sio sana)
kwa Jumapili ya Easter iangukie kwenye Jumapili ileile kama inavyokuwa kwa
Mganda wa Kutikiswa wakati wa Pasaka unavyoangukia siku ya 15 Nisan. Kwa hiyo,
ni karibu sana kuwa haiwezekani kuwa na Easter na Pasaka wakati mmoja na
kufanyika kuwa ni tukio linalofanyika kwa wakati mmoja. Hii ilijitokeza kinyume
na mapenzi ikilenga kuwatenga Wakristo na kuwaweka nje ya imani na itikadi za
Kiyahudi, lakini ni jambo lililo halisi katika kuamua au kuinyoesha wazi imani
ya mungu wa uwongo ili kuondoa sikukuu ya kweli na kuifanya ijulikane kwenye
ibada za miungu mingine.
Lugha iliyotumika
kwenye lugha ya Kiingereza kwa yenyewe tu inatueleza. Paska ilitajwa kuwa ni Pash kwenye maandiko ya Makanisa ya
Wakristo wa zamani. Neno Easter linatokana na muundo wa lugha ya zamani ya Kianglo-Saxon.
Kamusi maarufu
ijulikanayo kama The Universal Oxford
Dictionary inatoa maana ya Easter na kusema kuwa inatokana na neno la Kiingereza
cha zamani la éastre au jina la kike
la umoja la éastron. Inasema:
Baeda [Bede] amelichukua
neno hili kutoka kwenye neon Eostre (Northumb.
sp. of Éastre), mungu mke ambaye sikukuu
yake ilikuwa ikisherehekewa kipindi cha ikwinoks ya majira ya baridi (ibid.).
Kamusi hii inaendelea
kupuuzia dhana hii na inaendelea kushirikisha au kuifananiaha na sikukuu ya
Wakristo, baada ya kuyaonesha matumizi yake ya zamani yalivyokuwa yakifanywa na
dini za uwongo na potofu za imani ya mungu mke huyu.
Ikwinoks ya
majira ya baridi ni wakati ambao siku zinaanza kuwa ndefu zaidi ya urefu wa saa
za usiku (ndipo ikwinoks: sawasawa na usiku)
na ukuaji unaanza kuwa wa haraka. Kwa hiyo, inaashiria rutuba. Kutokana na
dhana hii tunaulinganisha mfano huu na Sungura, mayai, nk. Sungura alikuwa ni
alama ya urutubisho kwenye imani za dini za zamani za Wababeloni na vimeonekana
kwenye masalia ya mambokale ya wataalamu wa uchimbuzi wa masalia ya kihistoria.
Sungura walikuwa wakitumika kwenye talasimu na mambo mengine ya kishirikina
kutoka Afrika hadi Marekani (kwa mujibu wa kitabu cha Frazer, The Golden
Bough [Majipu ya Dhahabu], i, pp. 154-155). Walikuwa wakitumika pia kwe ye
sherehe za ibada za kusimamisha au kunyamazisha mvua (ibid., i, p. 295).
Sio tu kuwa ni
Wakristo peke yao ndio walichukua na kuiiga imani hii ya alama ya mayai kwenye
taratibu na imani zao za kidini, bali pia marabi wa Kiyahudi waliiga matendo
haya ya kuonyesha ishara ya mayai kwenye Seder ya Meza kwenye Pasaka, ambapo ni
kuutia unajisi mlo wa Pasaka kwa mwaka mzima na msingi wote wa kiibada.
Wanandoa walioiiga kalenda ya Hilleli, kwa kweli hawakuiadhimisha Pasaka
wenyewe na kuwazuia wowote waliojaribu kuifuata imani yao kutokana na kufanya
kwao hivyo kutokana na mfumo mbaya wa kalenda ya uwongo waliyoianzisha.
Katekisimu
ya Kanisa Katoliki [The Catechism of the Catholic Church] (St Pauls, Libreria Editrice Vaticana,
1994, Item 1170) inasema: “Kuhusu
Mtaguso wa Baraza la Nicaea, la mwaka 325, Makanisa yote yalikubali kuwa Easter,
Pasaka ya Wakristo, na iadhimishwe siku ya Jumapili inayofuatia mwezi mkamilifu
wa kwanza (Nisan 14) baada ikwinoks ya majira ya baridi. Marejesho ya Kalenda
ya Magharibi, inayoitwa ya “Gregorian” baada ya Papa Gregory XIII (1582), yalisababisha
mkanganyiko wa siku kadhaa na kalenda ya Mashariki. Hivi leo, Makanisa ya
Magharibi nay a Mashariki yanatafuta muafaka utakaowawezesha kwa mara nyingine
tena kuisherehekea siku ya Kukuka kwake Bwana kwa siku moja”.
Ugumu unaoonekana kwenye mfano ufuatao wa
kisasa. Mnamo mwaka 1997, Makanisa ya Magharibi waliisherehekea Easter wiki
moja baada ya Jumapili, ambayo iliangukia siku ya kweli na kamili ya 15 Nisan mwezi
Machi. Imani ya Wahafdhina au Orthodox ambayo kanisa la Ukraini linakuwa ni mfano,
lilisherehekea Easter yake Jumapili ya wiki moja iliyofuatia zaidi ile ya
uahirisho ya Kiyahudi ya tarehe 27 Aprili. Ya Wayahudi ilifuatia mwezi mmoja
zaidi ya ile ya Magharibi katika mwaka wa nane na wa kumi na tisa ya mzunguko
wa kalenda. Kulikuwa na madhara zaidi, kwenye Pentekoste ile na mwishoni mwa
sikukuu ya mwaka mtakatifu (Sikukuu za Baragumu, Upatanisho na Sikukuu ya
Vibanda) ambazo ziliadhimishwa mwezi mmoja baadae.
Kingine kufanyika zaidi kilicho sawa na
uhairisho wa Wayahudi kilichukuliwa kutoka kwenye imani ya Waorthodox. Hapo
mwanzoni, sharika ya Magharibi haikukubaliwa na kanisa la Mashariki la huko
Syria la Mesopotamia, hususan lile la Antiokia. Walidumu na imani na mfumo wa
Wakwortodeciman hadi jambo hili lilipotatuliwa. Tangazo la Kanuni maarufu kama
Canon I ya Baraza la Mtaguso wa Antiokia ya mwaka 341 inaonyesha kuwa maaskofu wa
Mashariki walikubalika katika kuukubali mfumo wa imani ya Warumi kama
ilivyowekwa kutoka Alexandria (soma jarida la Yeroboam na Kalenda ya Hilleli (Na. 191)
[Jeroboam and the Hillel Calendar (No. 191) ili ujifunze kwa
kina zaidi). Warusi waliongoka na kuingia imani ya Kikristo kufuatia na ubatizo
wa Olga wa Kiev mwaka 955 BK. Mwanae wa kiume, Svyatoslav wa Kiev, akaanzisha
ufalme wa Wayahudi wa asili ya Kikhazar wa Askenaz mwaka 967. Hivyo basi,
waliingizwa ndani ya Urusi na mjukuu wa Olga ambaye jina lake aliitwa Vladimir
aliyeukubali Ukristo na akajiunga rasmi na dini mwaka 988/989 BK (kwa mujibu wa
kitabu cha Milner-Gulland na Dejevsky, cha
Cultural Atlas of Russia and the Soviet Union, [Atlasi ya Utamaduni wa
Urusi na Umoja wa Kisovieti] kitabu kijulikanacho kama Time-Life Books, 1994,
p. 8).
Ushawishi wa imani ya Wayahudi wa Kikhazar
haukuweza kueleweka. Ushawishi wa imani ya Kiyahudi kwa Waorthodox wa Kirusi ulikuwa
ni mkubwa sana kiasi cha kwamba kenye nusu ya kwanza ya karne ya kumi na tano
ilionekana kuwa ni lazima kuiingiza kwenye shinikizo kubwa (tazama kitabu cha ERE,
art. ‘Russian Church’, Vol.
10, p. 869). Hali kufikia mwaka 1480, pamoja na Ivan III Vasilievich, Urusi
ilikuwa chini ya Watartars au Mongols (ibid., p. 870) na walikuwa ni wavumilivu
nana na wanaochukuliana mno na harakati za kidini, ni kawa walivyokuwa Wakhazaria
waliokuwa kabla yao. Urusi iligawanywa kwa sehemu mbili za mgawanyo ya kisiasa,
upande wa kati katika karne ya kumi na tano na sehemu ya magharibi ulikuwa
chini ya umiliki wa Wakatoliki wenye asili mchanganyiko wa Kilithuania na
Kipoland waliowashinikiza wahafdhina au Waorthodox kwa namna zozote zile (ibid.,
pp. 869-870). Wakijumuika na nguvu za kushindwa kwa Kanisa la Kiorthodox kukubaliana
na kalenda ya Wagregorian, hii huenda inaonyesha tofauti ya tarehe za Easter.
Ni mjumuisho wa kushinwa kurekebisha makosa kwenye kalenda ili kuupa mashiko
mfumo wa ile ya Gregorian na uahirisho kwenye Mwandamo wa Mwezi unaofuata,
ambao kwa mwaka wa 1997, unahusiana na uahirisho wa Wayahudi (soma pia jarida
la Kwa Nini Pasaka Ilichelewa Sana Mwaka 1997? (Na. 239) [Why is
Passover So Late in 1997? (No. 239)].
Wakati Yesu Kristo alipokutana na Mitume kwa kile Mtume Paulo anachokiita Meza ya Bwana (1Wakorintho 11:20; tazama Yohana 13:2,4; 21:20), usiku ule ulikuwa ni nusiku uliotangulia kabla ya Pasaka ya Wayahudi. Tukio ambalo Wakristo tunapaswa kuliadhimisha lilikuwa ni la jioni ya siku ya 14 Abibu, ambapo Wayahudi waliadhimisha, ni jioni tu ya siku ya 15 Abibu, pamoja ya uchinjaji wa wanakondoo wa Pasaka wakati wa jioni na mara tu kufuatia usiku ule – ambao pia umeelezewa kwenye Kutoka 12:40-42. Ushirika wa Meza ya Bwana katika mwaka 1997 uliangukia jioni ya Ijumaa, tarehe 21 Machi (14 Abibu), kwa kuwa ikwinoks ya majira ya baridi ilikuwa ni kipindi cha kabla ya usiku wa manane wa tarehe 20 Machi. Huenda ilikuwa ni vigumu kwamba, katika mwaka huu huu, tarehe 22 Machi ilienda sambamba na sikukuu ya Kiyahudi ya Purimu. (Soka pia kitabu cha Esta 9:18-19.)
Jioni ya siku ya 15 Nisan inajulikana kama Usiku wa Kuuangalia Sana (soma jarida la Usiku wa Kuuangalia Sana (Na. 101) [The Night to Be Much Observed (No. 101)], na kwa hiyo, Waristo wanaziadhimisha jioni zote mbili; lakini mkazo umewekwa katika hii siku ya 14 Nisan na sio ya 15 Nisan na Pasaka inaendelea hadi Jumapili (kama ilivyoanukuliwa na Tertullian) bila kujali ni wakati gani au lini siku hii ya 14 Nisan inaangukia. Kwa mujibu wa Tertullian, kusulibiwa na kufa kwa Yesu kulichukuliwa kama matukio sawa na neno Paska (au Pasaka) lilimannisha maana zote mbili, 14 Nisan hadi kuwa Jumapili (ambayo ioikuwa ni siku ya Mganda wa Kutikiswa na kutokana hiyo ndipo Pentekoste ilikuwa inaanza kuhesabiwa) (sawa na kitabu cha Cath. Encyc., Vol. III, art. ‘Calendar’, pp. 159 ff.). Inapaswa ikumbukwe pia kwamba kuingizwa kwa sherehe ya Easter kulifanywa na Baraza Kuu la Mtaguso wa Nicaea, lakini hakuna kumbukumbu yoyote inayoonyesha kikanuni kutoka ikwenye Baraza lile unaoonyesha kulifanyika maamuzi hayo. Tunaamini tu kutokana na kitabu cha Eusebius kinachosema Life of Constantine [Maisha ya Costantine] (III, xxviii sq.) kwakuwa kumbukumbu za nyaraka za Constantine kwa makanisa baada ya Mtaguso ule (soma hapo juu ambazo sawa na Cath. Encyc., ibid., p. 160; cf. Turner, Monumenta Nicaeana 152; cf. Cath. Encyc., Vol. V, art. ‘Easter’, p. 228).
Easter sio Pasaka halisi, ila ni ya
kipagani. Pasaka ya Wakwortodeciman ndiyo pekee ya kweli na yenye maadhimisho
yaliyoagizwa kibiblia yafanywe kwenye Kanisa la Mungu.
q