Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[281]

 

 

 

Raheli na Torati

(Toleo La 1.0 19981211-19990625)

 

Historia ya Raheli imejaa mambo mengi ya kushangaza yanayoonekana pengine kama maigizo, na ni mojawapo ya uthibitisho kwamba Amri ya Kumi ilipewa mkazo wake hata kabla ya kipindi cha kutolewa kwake huko Sinai. Hapa tunashughulika na idadi kadhaa ya mambo yaliyotendeka na uhusiano wake ulio sambamba na habari ambayo kwa kawaida inaepusha mtazamo. Hadithi hii ina maana kuu sana kwa Kanisa na dhana ya upendo wa Mungu na uhusiano wake maishani mwetu.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 1998, 1999 Christian Churches of God; ed. Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

 


Raheli na Torati

 


Historia ya Raheli imejaa mambo mengi ya kushangaza yanayoonekana pengine kama maigizo, na ni mojawapo ya uthibitisho kwamba Amri ya Kumi ilipewa mkazo wake hata kabla ya kipindi cha kutolewa kwake huko Sinai. Hapa tunashughulika na idadi kadhaa ya mambo yaliyotendeka na uhusiano wake ulio sambamba na habari ambayo kwa kawaida inaepusha mtazamo. Hii ni somo linalotu sura iliyo kwenye Biblia ni mgodi wa dhahabu wenye tutuonyesha mambo ya kushangaza na yenye thamani kuu kimasomo au kimafudisho.

 

Ingawaje hadithi ya Raheli ni mojawapo ya zile zinazopendwa sana na watoto, bali watu wazina nao wanapaswa kujisomea hadithi kila mara, na wafanye kwa kumaanisha kujifunza kit una wasisome kwa mtindo wa kujisomea hadithi tu kikawaida.

 

Baada ya Yakobo kumwibia haki ya uzaliwawake ndugu yake Esau, kwa kumdanganya baba yake Isaka, mahali wapokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani hapakuwa salama tena kwa yeye kuendelea kuishi na ndipo Yakobo alilazimika kukimbilia sehemu nyingine ili kujiponya nafsi yake.

 

Mwanzo 27:41 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.

 

Hapa kunaona mawazo aliyokuwanayo Esau kwa Yakobo kuwa yalikuwa sawa tu na vile alivyokuwa akiwaza ndugu yake, ni sawa na Kaini alivyokuwa akimuwazia ndugu yake Abeli. Rebeka akasikia maneno ambayo mtoto wake mkubwa Esau aliyoyatamka akimnuia mdogo wake. Ndipo akamuita Yakobo na kumuonya akimbie kabla mambo hayajawa makubwa na hajachelewa. Akamshauri aondoke na aende nchi ya mbali ya Harani, mahali alipokulia yeye na aliamini kuwa huko kungekuwa mahali salama kwake. Pia aliamini kuwa hatimaye hasira za Esau zingetulia na kisha angeweza kurejea baada ya kitambo hapo mbeleni baada ya siku nyingi kupita.

 

Mwanzo 27:42-44 Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akapeleka mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zako Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua. 43 Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani; 44 ukae kwake siku chache, hata ghadhabu ya ndugu yako igeuke;

 

Woga aliokuwanao Rebeka wa kutokea uwezekano wa kuwakosa wanawe wote wawili kwa tendo lile lililotokea ulikuwa sio wa kawaida. Kitendo cha kuuawa Yakobo na Esau kingefuatiwa na kuuawa kwa Esau na wenye kulipiza damu aliyoimwaga ya ndugu yake, kama isemavyo Torati. Ni hii ndiyo sababu iliyomfanya Kaini akimbilie mbali baada tu ya kumuua ndugu yake Abeli.

 

Mwanzo 4:10  Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

Mwanzo 4:13-14  Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.

 

Tunaona mkazo umewekwa na kuwa muhimu hapa kwa kuwa kulikuwa na malipizo ya damu kwa mtu anayeua, hasa kwa anayemuua ndugu yake. Hapa kunaonekana wazi kwamba amri ya sita ilikuwepo tangu siku za Adamu.

 

Amri hii ilirudiwa na Nuhu:

 

Mwanzo 9:5b-6  kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu. 6 Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.

 

Hapa tunajioea wazi mkazo ulivyowekwa kwenye amri ya sita na maana au sababu zake. Pale Sinai ilisisitizwa na kurudiwa kwa maneno machache:

 

Kutoka 20:13 Usiue

 

Rebeka alimwendea Isaka na kumuomba amruhusu Yakobo aondoke na kwenda zake mbali na uso wa Esau, na akamkabili kwa namna ya werevu wa hali ya juu sana, akijifanya kumtaka mawazo yake Isaka juu ya hali ile.

 

Mwanzo 27:46  Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidia nini?

 

Esau aliwaoa binti za Kanaani na hawakupata kibali au idhini na kupendwa wazazi wake.

 

Mwanzo 26:34-35 Esau alipokuwa mwenye miaka arobaini, akamwoa Yudithi, binti Beeri, Mhiti, na Basemathi, binti Eloni, Mhiti. 35 Roho zao Isaka na Rebeka zikajaa uchungu kwa ajili yao.  

 

Ilikuwa pia ni kinyume na mapenzi ya Mungu kuwaoa binti za Kannani na kuwafanya wakeze, au kumtoa binti na kuwapa Wakanaani ili aolewe nao, na kulikuwa na sababu za msingi kutofanya kwao hivyo.

 

Kumbukumbu la Torati 7:1-4  Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; 2 wakati Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao; 3 binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. 4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.

 

Baada ya Esau kugundua kwamba ndugu yake Yakobo ameondolewa aende mbali, na tena akiwa amebarikiwa, na akatafute mwanamke asiye wa Kikanaani, ndipo alijarubu kujifariji kwa kuweka sana hali hii kwa kumuoa wanamke wengine zaidi wa Kikanaani, lakini kutoka kwenye familia zinazohusiana:

 

Mwanzo 28:6-9 Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usitwae mke wa binti za Kanaani, 7 na ya kuwa Yakobo amewatii babaye na mamaye, akaenda Padan-aramu. 8 Esau akaona ya kuwa binti za Kanaani hawakumpendeza Isaka, baba yake. 9 Basi Esau akaenda kwa Ishmaeli akamtwaa Mahalathi, binti Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, ndugu wa Nebayothi, kuwa mkewe pamoja na wakeze aliokuwa nao.

 

Makabila lililotokana na Ishimaeli, mwana wa Ibrahimu, ni watu wanaofanananao tu na hawako kwenye nasaba ya dam una Wakanaani.

 

Isaka alimpeleka Yakobo huko Padan-aramu ili kufanya mwanawe akajitwalie mke kwa binti za Labani:

 

Mwanzo 28:1-2  Basi Isaka akamwita Yakobo, akambariki, akamwagiza akamwambia, Usitwae mke wa binti za Kanaani. 2 Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.

 

Isaka alimpa Yakobo amri ya kumuoa mmoja tu kati ya binti zake Labani. Isaka alikuwa ni mume wa mke mmoja tu, na alimshauri mwana wake afanye vivyohivyo. Lakini kulingana na mazingira yalivyokuwa Yakobo alishindwa kutii agizo hili la baba yake.

 

Jambo la muhimu hapa hata hivyo ni kwamba, Isaka alimsababishia pia manawe Yakobo kutenda dhambi. Baada ya kugundua madhara ya dhambi hii, Yakobo alishindwa kukataa ushauri wa baba yake kuhusu jambo hili. Dhambi yenyewe ilikuwa ni tendo la kwenda kujipatia mke na kuoa ndugu wa karibu ndani ya familia yao:

 

Mwanzo 28:2 Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.

Pale Sinai amri hii ilitiliwa mkazo na kufafanuliwa kwa kina zaidi:

 

Mambo ya Walawi 18:4-5  Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 5 Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi Bwana

 

Kwa kujua kile ambacho kinamwezesha mtu kuishi kwacho, ndipo sheria hii iliwekwa kwa haraka na mara moja kwa upesi:

 

Mambo ya Walawi 18:6 Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana

 

Hili ni jambo lililo wazi, na lilikuwa likitenda kazi kwa siku zile za Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Kama itavunjwa sheria hii kunaweza kusababisha mmwanamke au mke kuwa mgumba. Hukumu au adhabu ile itaweza kuifanya isiwezekane kuitii amri inayotutaka kuzaana na kuongezeka na kunapelekea kuchanganyikiwa kwingi na matatizo kutokea kwenye maisha ya ndoa. Tunaanza na Ibrahimu na Sara, ambao walikuwa wamekosa mtoto kwenye ndoa yao na hawakuweza kuwa na mwana. Walikuwa ni ndugu wa karibu kutoka kwenye ukoo mmoja, wakiwa ni ndugu-mabinamu.

 

Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu. 12 Naye kweli ni ndugu yangu, binti wa baba yangu ila siye mwana wa mama yangu, ndipo akawa mke wangu.  (Mwanzo 20:11-12)

 

Kwenye aya kadhaa chache, tunajionea zaidi kwamba inawezekana kabisa kwamba hali ya ugumba  inaweza kuwa hukumu kwa ajili ya dhambi iliyotendwa.

 

Mwanzo 20:17-18 Ibrahimu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana. 18 Maana Bwana alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Ibrahimu.

  

Udugu kama iliokuwepo kwenye ndoa kati ya Ibwahimu na Sara haukuruhusiwa, na umetajwa kinaga ubaga na bayana:

 

Mambo ya Walawi 18:11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wako

 

Kwa ajili ya adhabu ya kwenye ndoa kwa ajili ya uhusiano huu wa damu uliokuwepo kati ya Abrahamu na Sara, basi walikosa kuzaa mwana na akawa tasa:

 

Mwanzo 16:1 Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.  

 

Mungu aliwaahidi Ibrahimu na Sara mtoto. Kipindi kikapita na Sara akapoteza imani yake kabusa.

 

Mwanzo 18:10-14 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake. 11 Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 12 Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? 13 Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? 14 Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.

 

Tunaona hapa kwamba ingawa ilikuwa ni vigumu sana kwa mwanadamu, lakini haikuwa vigumu kabisa kwa Mungu, na kwa uweza uaio wa kawaida kwa miujiza, aliwaondolea ule utasa..

 

Mwanzo 21:1-3 Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema. 2 Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.

 

Halikuwa jambo jambo lisolo la kawaida kwa Isaka kumtuma mwanawe Yakobo aende Padan-aramu ili akajitwalie mke huko. Baba yake alimpa mtumishi wake agizo kwa kumuapia kwamba akamtafutie mwanamke sahihi kwa ajili ya mwanawe Isaka.

 

Mwanzo 24:1-4 Basi Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, na Bwana alikuwa amembariki Ibrahimu katika vitu vyote. 2 Ibrahimu akamwambia mtumishi wake, mzee wa nyumba yake, aliyetawala vitu vyake vyote, Tafadhali uutie mkono wako chini ya paja langu, 3 nami nitakuapisha kwa Bwana, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao; 4 bali enenda hata nchi yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu Isaka mke.

 

na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu Isaka mke. Hapa tunamwona Abrahamu akiangukia kwenye chimo lile lile kama yeye mwenyewe alivyoangukia huko nyuma. Alimpa mtumishi wake amri ya kwenda kumtafutia mke mwanawe Isaka kwenye ukoo wake mwenyewe. 

 

Mwanzo 24:15 Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Ibrahimu, naye ana mtungi begani pake

 

Mwanzo 24:50-51 Ndipo Labani na Bethueli wakajibu wakasema, Neno hili limetoka kwa Bwana, wala sisi hatuwezi kukuambia neno jema wala baya. 51 Tazama, huyo Rebeka yuko mbele yako, umchukue, ukaende zako awe mke wa mwana wa bwana wako, kama alivyosema Bwana.

 

Mwanzo 24:67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake.

 

Ndoa hii iliandaliwa na mtumishi wa Abraham. Na bado huko mwanzoni ndoa hii ilikuwa ya utasa, kama Rebeka alivyokuwa tasa. Yeye alikuwa ni wa ukoo mmoja na Isaka. Mungu anaweka wazi kabisa sheria hii na amri na maagizo haya.

 

Kutoka 20:5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

Tendo la kuufunua utupu wa mababa (Kufanya matendo maovu yaliyofanywa na mababa huko nyuma)  [visiting of the iniquity of the fathers] sio t uni kuivunja amri ya pili, bali inatenda kazi pia kwenye Torati yote, kama Mtume Yakobo anavyoonya:

 

Yakobo 2:10  Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

Hata hivyo, kwenye hali kama hii Isaka alikuwa na nia njema. Alimuomba BWANA, na Mungu akayasikia maombi yake. Huu ni mfano mkubwa sana mmojawapo wa nguvu za maombi. Alisomama imara na pamoja kati ya baba yake Ibrahim na mwanawe Yakobo kwa imani ndogo na kicho cha Mungu (Mwanzo 31:42). 

 

Mwanzo 25:19-21 Na hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka. 20 Isaka akawa mwenye miaka arobaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake. 21 Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.

 

Ndoa kati ya Isaka na Rebeka ilikuwa ni ya utasa, bila mtoto katika kipindi cha miaka ishirini ya kwanza. Tunaona tena hapa kwamba ililazimu Mungu aingilie kati kimiujiza kwa Rebeka, ni kama alivyofanya pia kwa Sara. Hatuna kumbukumbu kutoka kwenye Biblia inayoonyesha kwamba Ibrahimu aliomba ili mke wake Sara aondolewe na ule utasa. Zaidi sana alimnung’unikia Mungu kwa ajili hii (Mwanzo 15:2-3).

 

Tunaona hali waliyokuwanayo wake za Yakobo.

 

Mwanzo 28:5 Basi Isaka akampeleka Yakobo, naye akaenda Padan-aramu, kwa Labani, mwana wa Bethueli, Mshami, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.

 

Mwanzo 29:1-10 Kisha Yakobo akashika njia yake, akafika nchi ya wana wa mashariki. 2 Naye akaangalia, na tazama, kiko kisima kondeni, na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu nacho, kwa sababu katika kisima kile hunywesha makundi; na palikuwa na jiwe kubwa juu ya kinywa cha kisima. 3 Makundi yote hukusanyika huko, watu wakafingirisha hilo jiwe katika kinywa cha kisima wakawanywesha kondoo, na kulirudisha jiwe juu ya kinywa cha kisima mahali pake. 4 Yakobo akawauliza, Ndugu zangu, watu wa wapi ninyi? Wakasema, Tu wa Harani sisi. 5 Akawauliza, Je! Mnamjua Labani, mwana wa Nahori? Wakasema, Tunamjua. 6 Akawauliza, Je! Hajambo? Wakasema, Hajambo; tazama, Raheli binti yake anakuja na kondoo. 7 Akasema, Tazama, ukali mchana bado, wala sio wakati wa kukusanya wanyama; wanywesheni kondoo, mwende kuwalisha. 8 Wakasema, Hatuwezi, hata yakusanyike makundi yote, watu wakafingirishe jiwe katika kinywa cha kisima, ndipo tunapowanywesha kondoo. 9 Hata alipokuwa akisema nao, Raheli akaja na kondoo za baba yake, maana aliwachunga. 10 Ikawa Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mamaye, na kondoo za Labani, ndugu wa mamaye, Yakobo akakaribia, na kulifingirisha lile jiwe litoke katika kinywa cha kisima, akawanywesha kondoo za Labani, ndugu wa mamaye.

 

Yakobo alifurahishwa sana na mwonekano au umbo la Raheli, na alichukua hatua kwa haraka kuwapa maji ile mifugo ya baba yake binti huyu. Akampenda sana binti huyu.

 

Mwanzo 29:11 Yakobo akambusu Raheli, akainua sauti yake akalia

 

Jw, ni kwa nini Yakobo alilia kwa sauti kuu? Je, hii ilitokana na uppendo aliokuwanao kwa yule binti, au ilisababishwa na mawazo yake kwamba kuoa mtu aliye wa jamaa yake wa karibu kungeleta kizuizi kumpata binti huyu aliyempenda sana? Linekuwa ni tatizo la kifamilia. 

 

Mwanzo 29:12 Yakobo akamwarifu Raheli ya kuwa yeye ni ndugu wa babaye, na ya kuwa ni mwana wa Rebeka. Basi akapiga mbio akampasha babaye habari.

 

Uhusiano wa kindugu kwenye familia ni wa muhimu sana. Hata hivyo, walipaswa kushukuriwa kila mara kwa mambo mema. Historia hii inaeleweka. 

 

Mwanzo 29:13-16  Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote. 14 Labani akamwambia, Ndiwe kweli mfupa wangu na nyama yangu. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja. 15 Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini? 16 Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni Lea, na jina la mdogo ni Raheli.

 

Maandiko haya yanaotoa dokezo kwamba Labani anamtafutia kwa bidii kitu chema huyu ndugu wa jamaayake wa karibu. Tabia na hulka za Labani, hatahivyo zilikuwa ni uchoyo (Mwanzo 24:29-30, 53) na Yakobo alikuja pia kugundua kwenye miaka iliyofutia baadae.

 

Mwanzo 29:17 Naye Lea macho yake yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso.

 

Hapa tunajionea ulinganifu kati ya Lea na Raheli, ni kwamba Lea alikuwa haoni vizuri kwa kuwa macho yake yalikuwa dhaifu. Tafsiri ya Mfalme Yakobo (KJV) inalielezea jambo hili kwa namna nyingine.

 

Mwanzo 29:17 Naye Lea macho yake yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso.

 

Hapa inaelezea kwamba macho ya Lea yalikuwa ni ya makengeza. Hii inaonekana tena kuwa ni hitilafu, na ilikuwa ni kinyume kabisa na jinsi alivyoonekana Raheli. Jamieson, Fausset, anatoa maelezo mengine kwa kusema:

 

Ni kwamba, macho yalikuwa ni ya kibluu nyepesi-yaliyodhaniwa kuwa na chongo au kilema

(Jamieson, Fausset, Brown Commentary Old Testament Vol. 1, 1991, Ages, Albany OR)

 

Na kwa kuwa macho ni mvuto wa moyo, basi ni kitu muhimu sana kwa mwanadamu. Macho yanawezakuwa ni ya kibluu na dhaifu au chongo. Basi hakuna sababu ya kudhania kuwa Lea hakuwa mwanamke mzuri, kama alivyokuwa mdogo wake. Bali ilikuwa ni kwenye familia iliyojaliwa kwa wanawake kuwa wazuri kiasi cha kwamba hata kwa wanawake wenye umri mkubwa kwao, wanaonekana kuwa bado tu ni wazuri, kiasi cha kuwafanya hata waumezao wahofir maisha yao. 

 

Na hili ndilo lililomtokea Sara, mke wa Ibrahim, wakati alipokuwa na umri wa takriban miaka 65.

 

Mwanzo 12:10-15 Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi. 11 Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso; 12 basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai. 13 Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako. 14 Basi ikawa Abramu alipofika Misri, Wamisri wakamwona huyo mwanamke ya kwamba yeye ni mzuri sana. 15 Wakuu wa Farao wakamwona, nao wakamsifu kwa Farao; basi yule mwanamke akachukuliwa nyumbani mwa Farao.

 

Ni mtindo huo huo wa kuongopa ulijitokeza ambao ulisababishwa na woga kwa Isaka ba Rebeka.

 

Mwanzo 26:6-9 Isaka akakaa katika Gerari. 7 Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso. 8 Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akamwona Isaka anacheza-cheza na Rebeka mkewe. 9 Abimeleki akamwita Isaka, akasema, Yakini huyu ni mkeo, mbona ulisema, Ni ndugu yangu huyu? Isaka akamwambia, Kwa sababu nalisema, Nisife kwa ajili yake.

 

Labani alikwenda kufanya matano na Yakobo kwa ajili ya mshahara wake, na kwa ajili ya uroho, akamuuza binti yake Raheli kwa Yakobo. Yakobo akaukubali mshahara huu na kuuona ulistahili kwa kipindi cha miaka saba ya utumishi wake wa kuchunga mifugo.

 

Mwanzo 29:18-20 Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. 19 Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. 20 Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda.

 

Yakobo alikuwa anampenda sana Raheli, na kuda ulikuwa umechelewa sana kwake. Hata hivyo, baada ya miaka saba kupita aliomba apewe huyo Raheli na awe mke wake.

 

Mwanzo 29:21 Yakobo akamwambia Labani, Nipe mke wangu, maana siku zangu zimetimia; niingie kwake.

 

Tunaona hapa kwamba kicha ya upendo wake uliokuwa unawake kwa kipindi cha zaidi ya miaka saba, Yakobo hakumtaka Raheli afanyenaye tendo la ngono hata kidogo. Alikuwa ni bikira bado, jaambo ambalo kwa kawaida za ulimwenguni tunaoishi siku hizi ni jambo lisilotarajiwa wala kufikirika kubakia kuwa hiyyo. Hapa kuna mfano tunaouona na ambao unatakiwa kufuatwa au kuigwa.

 

Licha ya tumaini la haki na uaminifu aliokuwanao na taraja la kumpata mke kwa siku zake za usoni, bali kile kilichofanyika kilikuwa ni kinyume kabisa na Sheria za Mungu na ilikuwa ni uvunjaji wa imini. Dadayake Lea kwa hila na udanganifu uliopagwa kwa makusudi kabisa akampiku Raheli na kuchukua mahala pake kwenye ndoa. Inaonekana kabisa kwamba Labani alikubaliana na binti yake Lea wamdanganye Yakobo na kumuamuru Raheli asijitambulishe na abakie kimya au aende mbali kabisa na asiwe karibu napo.

 

Kwa kukosa kwake uaminifu Lea pamoja na udhaifu wake alijikuta akiingia kwenye jaribu hili la udanganyifu, tendo ambalo lilimuathiri mdogo wake na mume wake kwa kipindi chote kizima kilichobakia cha maisha yao na ambacho kilisababisha machungu kwenye familia yao. Alizivunja amri nyingi za Mungu. Baada yake, hali aliyoiwekeza toka moyoni mwake na mwa baba yake na kaka yake ya hila na udanganyifu ilikuwa na uchungu ulioendelea hadi kumuathiri mdogo wake na mume wake. Na iliendelea pia hadi kuathiri masuria na msingi mzima wa makabila ya Israeli.

 

Mwanzo 29:22-26 Labani akakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu. 23 Ikawa wakati wa jioni akamtwaa Lea, binti yake, akamletea Yakobo, naye akaingia kwake. 24 Labani akampa Lea mjakazi wake Zilpa, awe mjakazi wake. 25 Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda? 26 Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa;

Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea: Ni lazima tu kulikuweko mawazo na mazingira yenye uchungu mkubwa wakati Yakobo alipomtazama na kuyaona macho dhaifuya bluu ama ya makengeza ya Lea, badala ya kuyaona yale meusi ya Raheli. Kwa kuwa walikuwa ni ndugu inawezekana walikuwa na umbo linalofanana. Kwa hiyo Yakobo hakuweza kugundua tofauti yoyote pale gizani. alikoseshwa na kutapeliwa na Labani. Hata hivyo, tapeli huyu Labani alimweleza sababu ya kumfanyia vile, na kumruhusu aanze tena kwa huyu mwingine ambaye alikuwa ni kwa ajili yake, ambaye alifanya ushauri wa maana na akampa Raheli kwa mara ya pili kwa sharti la Yakobo amtumikie tena kwa kipindi kingine cha miaka saba cha mshahara wake.

 

Mwanzo 29:26-28  Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa; 27 timiza siku zake saba, nasi tutakupa huyu naye kwa utumishi utakaonitumikia, miaka saba mingine. 28 Yakobo akafanya hivi, akatimiza siku zake saba. Naye akampa Raheli binti yake kuwa mkewe.

 

Akatimiza siku zake saba. kilikuwa ni kipindi cha kawaida cha fungate au sherehe ya ndoa. Ndoa hii ya Lea ilikuwa ni ya kinyume na maagizo ya Torati.

 

Mambo ya Walawi 18:6 Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana.  

Kisha baada ya juma moja kupita, alimuoa Raheli. Ni sawa tu na ile ya kwanza, ndoa hii aliyoifunga na Raheli ilikuwa ni kinyume na maagizo ya Torati na dhambi iliendelea kufanyika:

 

Mambo ya Walawi 18:18 Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai

 

Mwanzo 29:29-30 Labani akampa binti yake Raheli mjakazi wake Bilha, awe mjakazi wake. 30 Akaingia kwa Raheli naye, akampenda Raheli kuliko Lea, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine.

 

Kuna jambo lingine linaloelekezwa na Torati ambalo lilikuwa limevunjwa, ambalo ni kwamba hairuhusiwi mtu kuoa tena kwenye kipindi cha ndani ya mwaka mmoja wa ndoa (Kumbukumbu la Torati 20:7). Tatizo sio kwa inavyotokea vita tu, bali ni kulinda umilkaji na uzao. Ilivunjwa mara ya kwanza kwa tendo la kumuibia haki yake Raheli. Na ikavunjwa kwa tukio la pili kwa kuzima na kuyakiuka matarajio ya Lea. Hata hivyo, ilisemekana na wengi kuwa aliyasababisha haya yeye mwenyewe.

 

Hali hii ya utata kwenye ndoa ilisababisha na mgongano na upotevu wa mshikamano kati ya Yakobo na wake zake, na kati ya wake zake wenyewe. Hii ilihitaji achukue hatua muhimu katika kuweka mtengamano na maelewano ya kifamilia kwa kipindi kingine kilichofuatia. Mahusiano yalikuwa ni ya matatizo zaidi, kipindi ambacho wakezake wote walipokuwa hawazai, jambo lililosababishwa na kufanya ndoa hizi za ndugu wa karibu ambazo zimeharimishwa.

 

Mwanzo 29:31 Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.

 

Mungu akaingilia kati utasa wa Lea, kwakuwa Yakobo hakumpenda. Alikuwa hajaingilia kati bado utasa wa Raheli. Licha ya ukweli kwamba Lea alimzalia watoto Yakobo, bali alikuwa hampendi tu bado na kidogokidogo Lea akaanza kupoteza imani kwamba Yakobo ataweza kuja kumpenda, na hatimaye akamshukuru BWANA, Mungu.

 

Mwanzo 29:32-35  Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa Bwana ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda. 33 Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa Bwana amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni. 34 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi. 35 Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa.

 

Sasa kwa mara ya kwanza tabia za Raheli zikafunuliwa. Hazikuonekana kuwa zilikuwa njema kabisa, na hatimaye zilifanana tu na zile za baba yake Labani kwa mambo mengi aliyoyafanya. Alikujakuwa ni mwanamke mwenye wivu na uchungu sana kwa dada yake Lea na kwa kizazi zhake zhote na akamlaumu Yakobo kwa utasa wake.

 

Mwanzo 30:1 Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.

Ingawa Yakobo alijua vema kuwa Raheli alikuwa tasa kwa ajili ya ukaribu wake wa kindugu kati yao, na kwamba BWANA anaweza kuwahurumia na kuingilia kati kwa niaba yao, hakufuata mfano wa imani ndogo ambayo kwayo baba yake Isaka aliifuata kipindi cha majaribu ya utasa wa Rebeka. Hakumuombea, bali alikasirishwa na hali ile. Hii ilionekana kwa Raheli ambaye aliamua kufanya tendo lilelile alilolifanya Sara la kumpa Ibrahimu suria wake Hajiri awe mkewe ili amzalie wana. Raheli akamtoa mtumwa wake Bilha na kumpa Yakobo kkwa lengo lilelile la kumzalia wana. Ili kukamilisha mzunguko, Lea naye akamtoa suria wake Zilpa na kumpa Yakobo ili awe mke wake pia atakayemzalia wana.

 

Mwanzo 30:2-13 Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba? 3 Akasema, Yuko mjakazi wangu, Bilha, uingie kwake ili kwamba azae juu ya magoti yangu, nami nipate uzao kwa yeye. 4 Basi akampa Bilha mjakazi wake kuwa mkewe. Yakobo akaingia kwake. 5 Naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana. 6 Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani. 7 Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. 8 Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali. 9 Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe. 10 Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana. 11 Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi. 12 Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili. 13 Lea akasema, Ni heri mimi, maana wanawake wataniita heri. Akamwita jina lake Asheri.

 

Mazingira yote haya hayawezi kuonyesha kuwepo kwa uhusiano wa kawaida wa kifamilia na ulio imara. Hatimaye Yakobo alifanyika kuwa mwanasesere wa wanawake wanne na kwa watoto wake.

 

Kilichofuatia baada ya hapo ni mfululizo wa matukio ya kusikitisha yakutumia mbinu za kumvutia mwanaume hadi kuanza kutumia matunda yaliyojulikana kama tunguja au maepo ya kuvutia mpenzi. Tunaona hapa utumiaji wa tunguja kwa wanawake kama yalivyokuwa yanatumika kwa wanawake waliokuwa kwenye dini za kipagani, na ambayp yalionekana pia kwenye shughuli za kishirikina. Biblia imeweka bayana sana msimamo wake kuhusu matendo haya ya kishirikina au uchawi.

 

1Samweli 15:23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme

 

 2Nyakati 33:6  Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.

 

Hizi Tunguja (Tunguja za mvuto au dawa ya mvuto wa kimapenzi kama ijulikanavyo kwa Kimombo Mandragora officinarum L.) chanzo chake hasa yanatoka pande za mashariki mwa Mediterranean na Magharibi ya Asia. Wayunani wa kale na Wamisri walianza kuyatumia haya kama ni dawa ya nusukaputi. Inaweza kuonekana pia kwenye madawa yaliyotumiwa kupuliziwa kwenye Mapiramidi ya Wamisri. Akinamama walikuwa wanapewa mataji ya “epo za upendo” wakiwa njiani kuelekea kwenye ufalme wa mauti. Matunda haya ya tunguja—maepo ya upendo—yametajwa pia kwenye Biblia.. yalikuwa yanatumika kwa namna mbalimbali na kwakuchanganya ili kuongeza maumivu hasa ya uchunguau utungu na mamba. Ni sehemu ya matunda au mboga za dawa na yaliaminika kuwa na utajiri wa miujiza na zilisaidia kufanyika kwa mambo yaliyokuwa magumu kutendeka na yanaweza kumfanya mtu awe na uweza wa aina fulani usio wa kawaida au apandishwe hata cheao. Lilikuwa ni kitu kinachoonekana na kuaminiwa na wengi kuwa na uweza wa kimazingaombwe na kimiujiza kwa vile lilivyokuwa linaumbile linalofanana na umbo la mwanadamu. Watu waliokuwa wanamiliki hizi tunguja walichukuliwa kama ni watu wenye bahati nzuri—na ilimhakikishia mtu mwenye nayo kuwa atakuwa na maisha mema. Mtu aliweza kuyauza tu ingawa lingeonekana kuwa limekufa na kwa thamani iliyokuwa ya chini kuliko ile iliyonunuliwa kwalo. Mtu aliyelipata bure hakuweza kuthubutu kujitoa mwenyewe kwenye mikono ya Shetani. (peruzi kwenye wavuti hii: www.members.xoom.com, 1998, Bewitching Herbs, Mandrake)

 

Mwanzo 30:14-16 Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao. 15 Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang'anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao. 16 Yakobo akaja kutoka kondeni jioni, Lea akatoka kumlaki, akasema, Lazima uje kwangu, kwa sababu nimekuajiri, kwa tunguja za mwanangu; akalala kwake usiku ule.

 

Yakobo alikuwa amezidiwa akili na wake zake na aliuzwa kwa Raheli kwa kupewa tunguja ambazo zilimvuta hadi akubali kulala naye Lea, siku ile. Maandiko hayatuambii kama mmojawao yeyote, kati ya Lea au Raheli alikuwa anatumia ushirikina kwa kutumia hizi tunguja.

 

1Samweli 15:23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme

 

Lakini binti hawa wa Labani inaonekana walikuwa na ushawishi fulani kwenye mambo haya yaliyo sawa na ibada za sanamu, kwa jinsi tunavyowaona wakitumia tunguja na mboga kwa ajili ya kurutubisha au uzazi. Hata hivyo, tunguja hizi hazikumsaidia Raheli lea akaendelea kumzali Yakobo watoto wengine

 

Mwanzo 30:17-18 Mungu akamsikia Lea, naye akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana wa tano. 18 Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari.

 

Baraka ya mwisho ya Yakobo kwa mwanae Isakari iliashiria mazingira ya kuzaliwa kwake na hatima yake itakavyokuwa:

 

Mwanzo 49:14-15 Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo; 15 Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.

Soma tena kwenye wavuti ya: www.members.xoom.com, 1998, Bewitching herbs, Mandrake

Baada ya kuzaliwa kwake Isakari, Lea alimzaa Zabulon na Dina

 

Mwanzo 30:19-21 Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa sita. 20 Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni. 21 Baadaye akazaa binti, akamwita jina lake Dina.

 

Raheli alijifunza njia ngumu na akamwangalia Mungu akihitaji msaada wake. Kwanza alimlaumu Yakobo kwa kukosa kwake kuzaa mtoto. Yakobo almkemea sana na kumwambia kuwa yeye hakuwa Mungu. Hii ilipelekea wazo la kujaribu kutafuta njia ya kufidia kwa kupata mtoto kwa kupitia mjakazi wake Bilha. Hatimaye, kwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo lake na tunguja zake alizozinunua alumudu kumuajiri Yakobo alale zamu kwake siku ambayo angelala kwa ndugu yake. Na matokeo yake yalikuwa ni kwamba Lea alipata mamba na kuzaa watoto wengine watatu zaidi. Hatimaye, alitafuta msaada wa Mungu, na kama alivyoelewa sasa kwamba huenda ile ilikuwa ni dhambi ndiyo iliyosababisha utasa wake na kwamba ni Mungu tu ndiye anayeweza kuingilia kati na kumsaidia kama alivyomfanyia Lea kwa dhambi yake aliyoifanya ya usiri na hila.

 

Mwanzo 30:22-24 Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo. 23 Akapata mimba, akazaa mwana, akasema, Mungu ameondoa aibu yangu. 24 Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana aniongeze mwana mwingine.

 

Baada ya miaka hiyo yote ya kujaribu kupita njia zilizo kinyume na mapenzi ya Mungu, ndipo Raheli akautafuta msada wa Mungu, na akajipa moyo kwa kutoangalia makosa na maovu yake. Raheli akampa Mungu utukufu kwa hili, na akamuomba haraka ampe mwana mwingine. Na baada ya miaka kadhaa (yapata kama miaka sita), Mungu alimpa mtoto mwingine

 

Yakobo aliichukulia ile kama miaka aliyofanya kazi kwa Labani imeisha na inatosha na sasa ni wakati muafaka kwake kurejea nyumbani kwake. Tutaona hapo chini kwamba ilikuwa ni kipindi cha takriban miaka ishirini.

 

Mwanzo 30:25-26 Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu. 26 Nipe wake zangu na watoto wangu, niliokutumikia, niende zangu, maana umejua utumishi wangu niliokutumikia.

 

Labani mroho hakulipenda wazo hili la kumpoteza mchungaji mzuri wa mifugo yake na mtu mwadilifu na shujaa, na akajaribu kuzinunua huduma za Yakobo tena kwa kukiongeza kipindi kingine cha utumishi wake kwake. Mara hii Yakobo alimzidi maarifa.

 

Mwanzo 30:27-43 inasema: Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba Bwana amenibariki kwa ajili yako. 28 Akasema, Sema mshahara wako utakao, nami nitatoa. 29 Akamwambia, Umejua jinsi nilivyokutumikia, na jinsi wanyama wako walivyokuwa kwangu. 30 Maana mali yako ilikuwa haba kabla sijaja, nayo imezidi kuwa nyingi, Bwana akakubariki kila nilikokwenda. Basi sasa, nitaangalia lini mambo ya nyumba yangu mwenyewe? 31 Akamwuliza, Nikupe nini? Yakobo akasema, Usinipe kitu; ukinifanyia neno hili, nitalisha wanyama wako tena na kuwalinda. 32 Nitapita katika wanyama wako wote leo, na kutoa huko kila mnyama aliye na madoadoa na marakaraka, na kila mnyama mweusi katika hao kondoo, na aliye na marakaraka na madoadoa katika mbuzi; nao watakuwa mshahara wangu. 33 Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa. 34 Labani akasema, Tazama, na iwe hivi kama usemavyo. 35 Basi akatoa siku ile mbuzi waume walio na milia na madoadoa, na mbuzi wake walio na madoadoa na marakaraka, kila aliye na doa jeupe, na kondoo wote waliokuwa weusi, akawatia mikononi mwa wanawe. 36 Akajitenga na Yakobo mwendo wa siku tatu; naye Yakobo akachunga wanyama wa Labani waliosalia. 37 Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo fito. 38 Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wanywe; wakachukua mimba walipokuja kunywa. 39 Wanyama wakapata mimba mbele ya hizo fito, wakazaa wanyama walio na milia, na madoadoa, na marakaraka. 40 Na Yakobo akawatenga wana-kondoo, akazielekeza nyuso za makundi zielekee wale waliokuwa na milia, na kila aliyekuwa mweusi katika wanyama wa Labani. Akaweka kando wanyama wake mwenyewe, wala hakuwachanganya pamoja na wanyama wa Labani. 41 Ikawa kila walipopata mimba wanyama wenye nguvu, Yakobo akaziweka zile fito mbele ya macho ya hao wanyama katika mabirika ili kwamba wachukue mimba kati ya zile fito, 42 lakini wanyama walipodhoofika hakuziweka zile fito. Basi wale dhaifu walikuwa wa Labani, na wenye nguvu walikuwa wa Yakobo. 43 Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.

 

Kwa ongezeko hili la haraka la mshahara ndani ya miaka sita, kwa gharama za Labani, na ndipo alibadili mtazamo wake kinyume na Yakobo kwa kuwa haikuwa kama alivyotarajia Labani na watoto wake.

Mwanzo 31:1-2 Basi Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema, Yakobo amechukua mali yote ya baba yetu; na kwa mali ya baba yetu amepata fahari hii yote. 2 Yakobo akaona uso wa Labani, ya kuwa hakumtazama vema kama jana na juzi.

 

Ndipo Yakobo alipoambiwa na BWANA ajiandae kurejea nyumbani kwake. Ndipo Yakobo akawaita wake zake Lea na Raheli na kuwaeleza sababu inayomfanya aondoke na kurudi kwao.

 

Mwanzo 31:3-13 Bwana akamwambia Yakobo, Urudi mpaka nchi ya baba zako na kwa jamaa zako, nami nitakuwa pamoja nawe. 4 Yakobo akatuma watu, akawaita Raheli na Lea waje nyikani kwenye wanyama wake. Akawaambia, 5 Naona uso wa baba yenu, kwamba hanitazami vema kama jana na juzi. Lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami. 6 Nanyi mmejua ya kwamba kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu. 7 Na baba yenu amenidanganya, akabadili mshahara wangu mara kumi; lakini Mungu hakumwacha kunidhuru. 8 Aliposema, Walio na madoadoa watakuwa mshahara wako, wanyama wote wakazaa madoadoa. Aliposema, Walio na milia watakuwa mshahara wako, ndipo wanyama wote wakazaa wenye milia. 9 Hivi Mungu akamnyang'anya mali yake baba yenu, na kunipa mimi. 10 Ikawa, wakati wale wanyama walipochukua mimba, naliinua macho yangu nikaona katika ndoto, na tazama, mabeberu waliowapanda hao wanyama walikuwa na milia, na madoadoa, na marakaraka. 11 Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. 12 Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani. 13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.

 

Tatizo la Raheli na Lea lilikuwa wazi sana. Walijiona pia kama wameachwa na baba yao wakiuzwa kama wageni. Na huenda walionysha hali ya kutoeleweka, na huenda hawakumuonyesha heshima yoyote kabisa. Hata hivyo, kwa kufanya kwao hivyo walikuwa wanaivunja amri ya tano.

 

Kumbukumbu la Torati 5:16  Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

 

Mwanzo 31:14-16 Raheli na Lea wakajibu, wakamwambia, Je! Imetubakia sehemu au urithi katika nyumba ya baba yetu? 15 Hakutufanya kama wageni, maana ametuuza, naye amekula fedha zetu kabisa? 16 Maana mali yote ambayo Mungu amemnyang'anya baba yetu, mali hiyo ndiyo yetu na ya wana wetu. Basi yo yote Mungu aliyokuambia, uyafanye.

 

Akiwa ameweka sawa mambo ya wake zake, na kufanikisha kuweka ushirikiano mzuri nao, Yakobo alijiandaa na kuondoka zake na kila alichokuwanacho, pasipo kumuarifu Labani.

 

Mwanzo 31:17-19a Ndipo Yakobo akaondoka, akapandisha wanawe na wakeze juu ya ngamia. 18 Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa ameyapata, na wanyama aliowapata katika Padan-aramu, ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani. 19 Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake,  

 

Ndipo mambo yalipojileta penyewe:

 

Mwanzo 31:19b … na Raheli akaviiba vinyago vya babaye.

 

Raheli aliiba miungu ya nyumbani mwao, sanamu—na kwa lugha ya Kiebrania., Teraphim. Hii inaonyesha kwamba vinyago vya Babeli na ibada zake vilikuwa bado vinatumika na kuabudiwa kwenye familia ya Labani. Na kwa kufanya kwao hivi, basi Raheli hakuwa mwaminifu sio kwenye amri hizi za Mungu tu, bali pia kwa wenzake wote.

 

Kama tunavyowaona watu wote waliokuwa kwenye nyumba ya Labani, aliivunja amri ya kwanza kwa kuwa na miungu mingine, ya vinyago vya kuchonga.

 

Kumbukumbu la Torati 5:7 Usiwe na miungu mingine ila mimi

 

Yeye na wenzake wote mara hiyo waliivunja amri ya pili kwa kuwa na miungu ya kuchonga:

 

Kumbukumbu la Torati 5:8-10 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. 9 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 10 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu

 

Raheli, kama alivyo Lea alivyokuwa kabla ya kuolewa kwao, aliivunja amri ya tatu, kwa jinsi alivyokuwa analitumia jina la BWANA bure au kwa mambo ya uwongo (Mwanzo 31:16) na alikuwa na hatia.

 

Kumbukumbu la Torati 5:11 Usilitaje bure Jina la Bwana, Mungu wako; maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina lake bure.

 

Raheli na Lea waliivunja amri ya kwanza. Huenda hata sisi tunaweza kufikiri, kama matokeo yake, wao pia waliivunja amri ya nne kwa kushindwa kwao kuishika japo kidogo kitakatifu. Amri hii ya nne ni mhuri na alama wa wale wanaomuabudu Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli.

 

Kutoka 20:8-10 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.

 

Isaya 56:1-8 Bwana asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. 2 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote. 3 Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu. 4 Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu; 5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. 6 Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; 7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. 8 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.

 

Raheli aliiba miungu iliyokuwa kwenye nyumba ya baba yake. Kwa ajili ya hasira, alishindwa kumheshimu baba yake wa hapa duniani kwa kuwa myoni mwake alimuona ni kama mtu aliyewauza. Lea alikuwa na mtazamo kama huo huo pia na tunaweza kudhania kuwa walikuwa wanawaza mamoja bali huenda haikuwa hivyo kwa ujumla. Hakuziheshimu mali za Lea, ingawaje yeye na Lea waliziona kuwa ni haki yao ambazo kwazo ndizo waliweza kutokanayo. Raheli alishindwa pia kumheshimu Baba yake wa mbinguni kwa vile alivyozivunja amri zake aote, kama alivyofanya Lea huko nyuma.

 

Kumbukumbu la Torati 5:16 Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

 

Raheli, kama alivyofanya Lea huko nyuma, aliivunja pia amri ya sita kwa dhambi zake na moyo wake usio na toba. Alikuwa anajiwekea kitanzi cha kujiua kiroho au kujinyonga kiroho.

 

Kumbukumbu la Torati 5:17  Usiue

 

Raheli aliivunja pia amri ya saba. Na kama alivyofanya Lea, aliyefanya udanganyifu na kulala na Yakobo alipoamini kuwa alikuwa ni mwanamke mwingine na mke wake wa halali, na ndivyo pia Raheli alivyoivunja Sheria hii kiroho. Ingawaje hakuoneshi kuwa na uzinzi wa kimwili, bali aliufanya kiroho, kwa kuabudu sanamu, na kuzifanya kuwa ni miungu mingine.

 

Ezekieli 23:36-38 Tena Bwana akaniambia, Mwanadamu, utawahukumu Ohola na Oholiba? Basi uwahubiri machukizo yao. 37 Maana wamezini, na damu imo mikononi mwao, nao wamezini na vinyago vyao; tena wana wao walionizalia wamewapitisha katika moto ili waliwe nao. 38 Tena wamenitenda haya; wamepatia unajisi mahali pangu patakatifu, siku ile ile, nao wamezitangua sabato zangu.

 

Kumbukumbu la Torati 5:18 Wala usizini.

 

Ni wazi kabisa kwamba Raheli aliivunja amri ya nane kwa kuiiba ile miungu.

 

Kumbukumbu la Torati 5:19 Wala usiibe

 

Raheli hakumwambia Yakobo kwamba alikuwa amefanya hivyo, kama tunavyosoma kwenye Mwanzo 31:32. Lea alikuwa ameiba pia haki ya Yakobo na ndugu yake kwa kuwadanganya. Na hata kama Raheli alikuwa aidha ana mimba au ni mgumba, bali alikuwa anamdanganya baba yake kuhusu hali yake kwa wakati ule, kwenye Mwanzo 31:35, na pia alikuwa ameivunja amri ya tisa:

 

Kumbukumbu la Torati 5:20 Wala usimshuhudie jirani yako uongo

 

Na ndivyo pia Lea alitoa ushahidi wa uwongo kwenye jambo hilo hapo juu. Raheli alikuwa na hatia ya kuivunja amri ya kumi kwa kutamani, kama alivyofanya Lea huko nyuma kabla ya ndoa yake. Kwa kweli, uvunjaji wa amri hii unapelekea uvunjifu wa amri zote nyingine. Inatawala na kudhibiti mawazo yetu yote, na mienendo yet una matendo yetu kwa uzuri na ubaya.

 

Kumbukumbu la Torati 5:21 Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani yako

Tumeona kwamba kwa wizi na udanganyifu wa Raheli na Lea hatimaye walifikia kwenye hatia ya kuzivunja amri zote Kumi za Mungu. Yakobo pia hakuwa mbali na tendo hili la wizi.

 

Mwanzo 31:20 Yakobo akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia.

 

Inajulikana sana kwamba wakati Labani alipogundua kuwa Yakobo alikuwa ameiba pamoja na wake zake, watoto na mifugo yake, ndipo huenda alitafuta msaada kwa vile vinyago kwa namna ya kupiga ramri ambavyo alisema, au huenda alitazama vitu vyake vyenye dhamani tu, na ndipo aligundua kuwa vimeibiwa. Huku akiwa amejaa uchungu na hasira alitoka nje ili kujilipiza kisasi. Ndipo Mungu akijua hatari itakayosababishwa na mawazo haya, akamtokea Labani kwenye ndoto na kumuonya asifanye tendo lolote lenye madhara.

 

Mwanzo 31:22-31 Hata siku ya tatu Labani akaambiwa ya kwamba Yakobo amekimbia, 23 akatwaa ndugu zake pamoja naye, akamfuata mwendo wa siku saba. Akampata katika mlima wa Gileadi. 24 Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari. 25 Labani akamfikia Yakobo, na Yakobo alikuwa amepiga hema zake katika mlima, na Labani na ndugu zake wakapiga hema zao katika mlima wa Gileadi. 26 Labani akamwambia Yakobo, Umefanya nini? Umenihadaa, ukawachukua binti zangu kama mateka waliotwaliwa kwa upanga. 27 Mbona umekimbia kwa siri ukanihadaa, wala hukuniambia, nipate kuagana nawe uende zako kwa furaha, na nyimbo, na ngoma, na kinubi? 28 Wala hukuniacha niwabusu wanangu, na binti zangu; basi umetenda upumbavu. 29 Ninao uwezo mkononi mwangu wa kukufanyia madhara; lakini Mungu wa baba yako usiku huu ameniambia, akisema, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari. 30 Basi sasa, umetoka kwa sababu umetamani sana nyumba ya baba yako. Mbona basi umeiiba miungu yangu? 31 Yakobo akajibu, akamwambia Labani, Kwa sababu naliogopa, nikasema, Usije ukaninyang'anya binti zako kwa  

 

Hapa tunaona uweza wa Mungu wa Isaka kwa Labani, na akayatii maneno aliyoyasema. Lakini licha ya yote haya bado alidai kurusi kwenye ibada na tumaini lake kwenye sanamu. Haya yalikuwa ni mazingira ya ajabu sana. Yakobo aliamini kabisa kwamba hakuna aliyeiba vile vinyago kati yao na akafanya kiapo kukubwa sana kwa ajili ya jambo hili, nay ule aliyekuwa anamsogelea kwa mbali akaashiria kuachana nalo.

 

Mwanzo 31:32  Awaye yote utakayemwona kuwa nayo miungu yako, yeye asiishi. Mbele ya ndugu zetu ukitambue kilicho chako kwangu, ukakichukue. Maana Yakobo hakujua ya kwamba Raheli ameiiba.

 

Bila kujua Yakobo akamlaumu mkewe kipenzi sana Raheli kuwa afe kama amechukua vinyago hivyo.

 

Mwanzo 31:33-35 Labani akaingia katika hema ya Yakobo, na hema ya Lea, na hema ya vijakazi wawili, wala hakuiona. Akatoka katika hema ya Lea, akaingia katika hema ya Raheli. 34 Basi Raheli alikuwa amevitwaa vile vinyago ameviweka katika matandiko ya ngamia, na kuvikalia. Labani akapapasa hema yote wala hakuviona. 35 Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.

 

Baada ya Labani kushindwa kuviona hivyo vinyago, ilikuwa ni nafuu kubwa kwa Yakobo, na alijisikia kupata nguvu kuu sana kwa jambo hilo na akasema maneno makuu sana kwa Labani.

 

Mwanzo 31:36-43 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N'nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii? 37 Umepapasa-papasa vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu. 38 Miaka hii ishirini nimekaa kwako; kondoo zako wala mbuzi zako wake hawakuharibu mimba wala waume katika wanyama wako sikuwala. 39 Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku. 40 Hii ilikuwa hali yangu; mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi ukanitoka machoni mwangu. 41 Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi. 42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu. 43 Labani akajibu, akamwambia Yakobo, Hao binti ni binti zangu, na wana ni wanangu, na wanyama ni wanyama wangu, na yote uyaonayo ni yangu; nami naweza kuwatendea nini leo binti zangu na wana wao waliowalea?

 

Sasa Labani akagundua kwamba amepoteza sababu na akajaribu kuuokoa uso wake kwa weledi mkubwa kama alivyoweza kwa kupendekeza wafanye agano na kasha waachane.

Mwanzo 31:43-55 Labani akajibu, akamwambia Yakobo, Hao binti ni binti zangu, na wana ni wanangu, na wanyama ni wanyama wangu, na yote uyaonayo ni yangu; nami naweza kuwatendea nini leo binti zangu na wana wao waliowalea? 44 Haya! Na tufanye agano, mimi na wewe, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe. 45 Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo. 46 Yakobo akawaambia ndugu zake, Kusanyeni mawe. Wakatwaa mawe, wakafanya chungu, nao wakala huko karibu na ile chungu. 47 Labani aliiita Yegarsahadutha, lakini Yakobo aliiita Galedi. 48 Labani akasema, Chungu hii ni shahidi kati ya mimi na wewe hivi leo. Kwa hiyo likaitwa jina lake Galedi, 49 na Mispa, maana alisema, Mungu avizie kati ya mimi na wewe, wakati tusipoonana. 50 Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe. 51 Labani akamwambia Yakobo, Tazama chungu hii utazame na nguzo niliyoitia kati ya mimi na wewe. 52 Chungu hii na iwe shahidi, na nguzo hii na iwe shahidi, ya kuwa mimi sitapita chungu hii kuja kwako, wala wewe hutapita chungu hii na nguzo hii uje kwangu, kwa madhara. 53 Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu. 54 Yakobo akachinja sadaka katika mlima, akawaita ndugu zake waje wale chakula, nao wakala chakula, wakakaa usiku kucha mlimani. 55 Labani akaondoka asubuhi na mapema, akawabusu wanawe na binti zake, akawabariki; kisha Labani akaenda zake, akarudi kwao.

 

Tunaacha matukio mfululizo ya Yakobo na Esau, Penieli na Dina, hadi kwenye mtangamano wa kila mahali na mwendelezo wa historia ya Yakobo alipokuwa huko Betheli ambako Yakobo aliviondoa vinyago vyote kutoka kwenye nyumba yote.

 

Mwanzo 35:1-3 Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako. 2 Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu. 3 Bwana akamwambia Yakobo, Urudi mpaka nchi ya baba zako na kwa jamaa zako, nami nitakuwa pamoja nawe.

 

Kipindi kinachofuatia ni lazima kiwe ni cha mshtuko mkubwa sana kwa Yakobo, kwa kuwa miungu yote ya kigeni alikuwanayo yeye. Hii ni pamoja na vinyago vilivyoibiwa na Raheli. Lazima ilimshangaza na kumtetemesha sana na kuogopa baada ya kugundua kwamba Raheli alikuwa ameviiba kweli vile vinyago na alikumbuka vile viapo alivyokuwa ameviweka akisema kwamba mtu yeyote yule miongoni mwetu atakayeonekana kuwa navyo hivyo vinyago hemani mwake ni sharti auawe na asiishi kabisa. Katika kipindi hikihiki, Raheli alikuwa na mimba kwa uzao wa pili baada ya miaka hii yote

 

Mwanzo 35:4 Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu.

 

Sababu ya kweli ya kuichukua miungu ile migeni inaweza kuwa kwamba malighafi iliyotumika kutengeneza vinyago vile haikuwa ni udongo wa kawaida wa mfinyanzi, bali kwa kweli ilitengenezwa kwa vitu vya dhahabu na fedha (sawa na Waamuzi 18:14). Tunaweza kudhania jambo hili pia kwa majibu waliyokuwa wakijibizana kina Lea na Raheli, binti za Labani na mawazo aliyokuwanayo Labani kwa Yakobo kama tulivyojionea hapo juu. Kulikuwa na hali halisi ya uchungu kwenye upande wa wana wa Labani na mjukuu wake kwa matendo aliyowatendea, na wote walijisikia kudanganywa. Kwa matendo haya aliwasababishia wote wazivunje amri. Labani ndiye aliyeanza kufanya udanganyifu na wizi na binti yake wa kwanza, Lea, aliyekubali kufanya kitendo kisicho cha haki. Kwa makusudi kabisa yeye aliingia kwenye tendo la uvunjifu wa amri na kumdanganya mume wake na mdogo wake, ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kujaribu na kumdanganya mume wake na haki ya uzaliwa ya mtoto wake. Kwa vyovyote, hii ilimjumuisha baba yake. Wizi huu haukuheshimiwa na Mungu, ambaye mwishowe aliihamisha haki hii ya uzaliwa kwa wana wa Raheli kupitia kwa Yusufu. Reuben mzaliwa wa kwanza alimvunjia heshima baba yake, kwa kulala na Bilha suria wa baba yake (Mwanzo 35:22), na alisaidia kufanya madhara ya kuhamisha kwake. Jambo hili lilikuwa na madhara ya mbali ya urithi na haki ya uzaliwa wa kwanza ya makabila, na lilihukumiwa sawasawa.

 

Janga hili la kuzivunja Sheria, linahusika pia na uvunjaji wa majukumu yaliyo chini ya Sheria na maelekezo ya Torati, ambayo inahusisha pia na uvunjifu wa wajibu ulio chini ya Sheria ambayo inabidi ifuatwe na kwenye Agano Jipya, itokanayo na hali ya kutolitendea kazi au kulidharau Agano la kale. Nasaha iliyoko ni kwamba “msiwachokoze watoto wenu,” (Eph. 6:4; Col. 3:21).

 

Kupitia kwa Mikali, Daudi pia alipaswa ahusishwe na utumiaji wa kinyago nyumbani mwake. Hata hivyo, vilifanya kazi yake kwa kuyaokoa maisha yake (1Samweli 19:13). Kwa kujifunza maana ya miungu migeni na vikuku vya masikioni, basi jisomee majarida ya: Chanzo zha Uvaaji wa Ndewe Masikioni & Vito vya Dhahabu Siku za Kale (Na. 197) na Ndama wa Dhahabu (Na. 222) [The Origin of the Wearing of Earrings & Jewellery in Ancient Times (No. 197) and The Golden Calf (No. 222)].

 

Mwanzo 35:5-15 Wakashika njia, hofu ya Mungu ikaishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo. 6 Basi Yakobo akafika Luzu, ulio katika nchi ya Kanaani, ndio Betheli, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye. 7 Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake. 8 Akafa Debora mlezi wa Rebeka, akazikwa chini ya Betheli, chini ya mwaloni; na jina lake likaitwa Alon-bakuthi. 9 Mungu akamtokea Yakobo tena, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki. 10 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli. 11 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako. 12 Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo. 13 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye. 14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake. 15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.

 

Sasa tuko kwenye kilele cha mambo yote. Yakobo kwa mara nyingine tena anatamka hukumu ya kifo kwa Raheli, pasipo kujua, na ilibakiwa kama iliyofunikwa kwa muda. Hata hivyo, kwa kumuamuru suaria wake ajitakase, tendo hili liliashiria utimilizo kamili. Mungu alikuwa amemahidi Raheli kumpa mtoto mwingine wa pili. Alikuwa sasa mja mzito. Kwa hiyo Yakobo asingeweza kutamka hukumu ya kifo, na kichanga kilichoko tumboni kisiathirike. Wala hakutafuta hata kuweko kwa hukumu kama ile.

 

Bali hakuwa na la kufanya kwa kuitoa aina ile ya kiapo aliyoifanya bila kuzingatia sheria na kanuni kama alivyofanya Yefta (Waamuzi 11:30-35). Hata hivyo, Raheli alikufa wakati akijifungua na hukumu ile inaonekana kuwa ilitimilika kwa madhara makubwa.

Mwanzo 35:16-20 Wakasafiri kutoka Betheli, hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito. 17 Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine. 18 Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini. 19 Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu. 20 Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.

 

Ni ukatili kiasi gani ulionekana kwa Raheli kufa akiwa anajifungua mtoto. Hata hivyo tunaweza kujenga hoja kwamba ilisababishwa na mazingira halisi ya maisha yake, kwa vile alivyoshindwa kujikabidhi kikamilifu kwa Mungu.

 

Mazingira yanaweza kuwa yalimpelekea kwenye hali hii, kwa ajili ya kiapo alichokifanya Yakobo bila kufikiria vizuri, na alichokifanya pasipo sababu yoyete ya msingi. Inaweza kuchukuliwa kama funzo la maafa mabaya sana kuwahi kutokea, bali kuna fundisho kubwa sana la kiroho tunalojifunza kutokana na tukio hili na ambalo linawahusu na linaloweza kumpata mtu mwingine yeyote.

 

Ilikuwa ni kutokana na utakaso huu alioamuru Yakobo ambao ulikuwa ni neema iokoayo ya familia yake na fundisho kuu tunalojifunza kwenye andiko hili. Ni kwa kujitakasa tu na kumrudia Mungu ndipo tunawezakuwa ni sehemu taifa la Mungu, yaani Israeli. (soma pia jarida la Utarakaso na Tohara (Na. 251) [Purification and Circumcision (No. 251)]. Baada ya Yakobo kuiakasa familia yake, ambayo ilikuwa ni kiini au chanzo cha taifa la Israeli, huko Betheli, alibadilika na familia yake ilisamehewa na walichukuliwa kwenye wajibu au majukumu ya El-Betheli au El wa Nyumba ya El, ambaye ni Kuhani Mkuu au El Shaddai (sawa na Mwanzo 35:11).

 

Akaitwa jina jipya la Israeli au utatawala kama Mungu na familia yake wakabarikiwa na kutiwa nguvu.

 

Licha ya baraka hizi, wakiwa njiani wakitokea Betheli na kabla hawajafika Efrati, Raheli alikufa baada ya kumzaa mwanae wa pili. Akamuita mtoto wake Benoni (SHD 1126) ambalo maana yake ni mwana au mtoto wa huzuni yangu. Katika mtoto wake huyu wa mwisho wa Yakobo, ambaye sasa ni Israeli, safari yao sasa ilikuwa inakamilika Israeli alilibadilisha jina la mtoto wake huyu wa mwisho na kumuita Benyamini (SHD 1144), ambalo maana yake ni mwenye kutumia mkono wa kushoto, au kusini, au kuume. Hapa tunaona kipindi cha mpito cha vipawa vya Mungu kutoka kuwa kwenye hali ya dhambi na kuondolewa mbali na Mungu hadi kwenye hali ya neema kama wana wa Mungu aliye hai.

 

Ilikuwa ni kutoka kwenye mchakato huu wa kutoka Betheli, ambapo maana yake ni Nyumba ya Mungu, ambapo tunaona makusudio ya habari hii. Israeli na watu wote wa nyumbani mwake walitakaswa kwa uingilio alioufanya Kuhani Mkuu au El Bethel. Kwenye uzaliwa wa mtoto na kufa kwa mwanamke tunapata wazo la ahadi ya haki ya uzaliwa wa kwanza kwa Kanisa na ua uwana wa ahadi. Kupitia kwenye jina lile la wana wa huzuni kunabadilika na kuwa wana wa ahadi. Walipokuwa njiani kuelekea Efrath alikufa na akazikwa karibu na Bethlehemu mahali ambako alijionyesha mfano kwa wana wa ahadi na kwa mwana wa Yuda ambaye ni Masihi. Alikuja alitokea Bethelehemu ya Epratha, uliye mdogo ssana katika majumbe wa Yuda. Wana wa Lea waliungana na wana wa Raheli, kwa kuwa fimbo ya kifalme itatoka katika Yuda na haki ya uzaliwa wa kwanza wa itatoka kwa Yusufu. Wana wa ahadi wanapaswa kuwa ni wale wote walio kwenye koo za Israeli na wa mataifa yote ya dunia wanapaswa waungane nao kwa utakaso kama huo huo wa neema chini ya Masihi. F

 

Tunaweza kujifunza somo muhimu sana kutokana na habari hii.

§  Unapaswa kuwa mwangalifu kilamara unapoweka nadhiri au kula kiapo au unapokuwa unaomba. Mara nyingi kiapo au nadhiri itatiizwa sawasawa na jinsi ulivyoiweka, hata hivyo, kuwa inatokea tofauti kwenye mazingira tofauti na vile ilivyotarajiwa.

§  Kwa kuivunja amri moja tu, basi Torati yote itakuwa imevunjwa kwa mapatilizo makubwa sana.

§  Kuishika amri ya kwanza kwa mahali pa kwanza, kama hivi kutailinda nia yako kwa amri nyingine zote.

§  Kila kinachoonekana kama hadithi rahisi kwenye Biblia kina mahusiano mengi yenye maana kuhusu kuzitunza au kuzivunja Sheria za Mungu au Torati.

§  Unapaswa kila mara kuwa makini na maagizo ya Torati.

§  Fundisho kuu ni kwamba hatujahesabiwa haki kwa jinsi tujionavyo kwa macho yet una tunahukumiwa kwa matendo yetu.

§  Tunatengwa na kukosa haki yetu kwa ajili ya dhambi, lakini pia hatuhesabiwi haki kwa Sheria.

§  Tunaokolewa kwa Neema.

§  Mungu ametuahidi kupitia kwa mababa zetu wa imani kwamba hatutashindwa.

§  Tunazishika amri za Mungu kwa kumpenda yeye na kwa kuwa alijifunua kwetu sisi yeye mwenyewe kama alivyofanya, kupitia kwa El Betheli na Masihi, kwa wote wawili, yaani kwa mababa wa imani na kwa Kanisa.

 

Ufunuo 14:12  Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.

 

Jitahidi kuyajua yale yaliyotokea kwa habari kugundulika kwa familia ya makabila ya Israeli na mazingira yale ambayo yaliathiri kuendelea kuwepo kwayo, hata katika maisha ya Raheli na kuwepo kwa wana wa Israeli kwenye haki ya uzaliwa wao. Raheli aliruhusiwa afe ili kwamba sisi tuwe na mfano wa imani na ahadi kwa Israeli ya Masihi na ya Kanisa.

 

Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.   

 

q