Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[282A]

 

 

 

 

Tawala za Wafalme Sehemu ya I: Sauli

(Toleo La 1.0 19990114-20060617)

Kipindi cha Tawala wa Wafalme tangu Sauli, hadi Daudi na Sulemani kina maana na ashirio za mifano maalumu ya kinabii ambayo yanahusiana pia na mpango wa wokovu. Kuna ujumbe wa muhimu kwenye mchakato huu, tawala na matendo ya wafalme hawa watatu wa Israeli.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 1999, 2000, 2006 Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Tawala za Wafalme Sehem ya I: Sauli


 


Tunaweza kujionea Tawala za Wafalme wa Israeli mfano wa migongano na migawanyiko iliyohusiana na moango wa wokovu kwene muundo wake na kwa njia ileile na ule wa maisha ya Musa na muundo wake uliodumu kwa miaka mia moja na ishirini.

 

Umri huu na mfano wake vinaendana na kipindi chote cha maisha ya Modekai na pia cha maisha ya Zerubabeli, ambacho kinaonekana kuhusiana na Masihi na pia cha Ujenzi wa Hekalu (sawa na maoni ya jarida la Ufafanuzi wa Kitabu cha Esta (Na. 63) [Commentary on Esther (No. 63)].

 

Tutaona kwamba kwa kweli, ina uhusiano na Masihi na kazi zake hapa duniani na ujenzi wa Hekalu.

 

Wafalme Watatu waKwanza wa Israeli

Wafalme watatu wa kwanza wa Israeli walitawala kwa kipindi cha miaka arobaini kila mmoja wao. Sauli alitawala kwa miaka arobaini na alirithiwa na Daudi ambaye alitawala miaka saba huko Hebroni na thelathini na tatu huko Yerusalemu. Kwa hiyo, huyu naye alitawala kwa miaka arobaini. Alipozeeka, Daudi alimrithisha mwanae Sulemani. Daudi hakuruhusiwa kulijenga Hekalu la Mungu. Kazi hiyo aliachiwa mwanae Sulemani ambaye ndiye aliijenga nyumba hii ya Mungu kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini (2Mambo ya Nyakati. 8:1), ambayo ni namba ya kimungu ya ukamilifu, jumlisha moja ikiwa kama tumaini la siku zijazo (sawa na isemavyo tafsiri ya Companion Bible kuhusu sura na ayah ii ya 8:1). Alitawala miaka arobaini huko Yerusalemu. Baada ya kufa kwake, ufalme aligawanyika chini ya mwanae Rehoboamu kukatikea falme mbili, yaani moja ya Yuda na nyingine ya Israeli, ambazo zilitawala tangu Yerusalemu na halikadhalika, Samaria (soma 2Mambo ya Nyakati 10:1-11:12).

 

Hatimaye pia tutaiona tarakimu hii ya ishirini au kwenye miaka au kwenye yubile ikitokea tena na tena kama kiwango cha ubora wa karne kadhaa, na yubile za ujenzi wa Hekalu la kiroho.

 

Muundo wa tarakimu arobaini tatu

Musa alidumu maishani mwake kwa vipindi vyenye awamu tatu. Kila awamu ilikuwa na jumla ya miaka arobainiya urefu wake. Waliishi miaka arobaini huko Misri akiwa kama mwana mfalme na jemadari wa kijeshi. Aliikmbia Misri  baada ya kuhadharidhwa kuwa amegundulika kuwa na nasaba ya uzaliwa wa Kiisraeli na kugundua kwamba

siri hii ilikuwa imegundulika.

 

Alikimbilia Midiani na akaishi maisha ya kuchunga mifugo kwa muda wa miaka arobaini. Huko aliandaliwa kuwaongoza Israeli jangwani wakiwa kama wana wa agano. Alirudi tena Misri baada ya miaka hii arobaini na akawaongoza Israeli walipotolewa Misri na Malaika wa Uwepo wake.

 

Musa alitumia miaka yake arobaini ya mwisho ya maisha yake jangwani akiwa kama kiongozi wa wana wa agano. Hakuweza kuingia nao kwenye Nchi ya Ahadi, bali alikufa akiwa na umri wa miaka 120 baada ya kuwaleta hadi kwenye Nchi ya Ahadi na kuwapa Torati ya Mungu.

 

Maisha yake yanaweza kutumiwa kama mpango au mfano wa kuigwa katika mpango wa Mungu, katika miaka hiyo 120 tunajionea mpango wa wokovu wa yubilee 120 ya uumbaji tangu kufungwa kwa Bustani ya Edeni.

 

Miaka yake arobaini ya kuwakwake huko Misri iliwakilisha yubile arobaini za kwanza za mpango wa Mungu tangu wakati wa Adamu hadi wa Ibrahimu. Katika kipindi hiki tunaona dunia imeharibiwa kutokana na dhambi za viumbe na Wanefili zilizofanywa na Malaika waasi. Waliangamizwa kwa gharika ya Nuhu. Hatahivyo, Nuhu aliokolewa kwa kupitia safina kuelekea kwenye mwisho wa hukumu. Musa aliokolewa kwa kisafina kidogo pia utotoni kwake ili aweze kuwaokoa kwa kuwatoa Israeli nje ya mazingira ya dhambi kama Nuhu alivyofanya kabla yake. Utaratibu ulianza kwa ukamilifu wa Adamu kuendeleza kwenye uharibifu na maangamizo. Wakiwa na Musa ilianzia na utumwa dhambi zikapungua na iliendelea kwa kuanzishwa kwa taifa la Israeli.

 

Awamu ya miaka arobaini ya pili huko Midiani, ambayo iliuwa ni mwendelezo wa kipindi ambacho ambacho angependa kushinda na Wana wa Israeli, ilikuwa ni sawa na cha kabla ya gharika kuu. Kipindi hiki kilitangulia kutoka Shemu akiwa kama kuhani wa Mungu, wa baada ya gharika kuu na kupitia kwa watoto wake hadi Ibrahimu ha kwenda chini hadi kwa Kristo. Kwa kipindi hiki chote, wana wa kimwili wa Ibrahimu walitengwa na kuwekwa mbali na hatimaye kutumiwa knzisha kuwepo kwa mafundisho na na unabii ambao ungcweka utaratibu wa mpango wa Mungu. Maandalizi ya Biblia wakati wa zama za Kristo ulioonyeshwa kwa mfano wa matendo ya \Kitabu cha Ayubu na maandalizo yake na masimulizi wakati wa kipindi hiki cha Wamidiani.

 

Wakati utaratibu huu wa kimwili na wawazi ukiendeleza matendo yake na hitimisho kamili ya muundo huu ulikuwa wazi katika Yesu Kristo utaratibu wa kimwili ulijaribiwa na kuharibiwa.

 

Kipindi cha pili cha miaka arobaini cha kuwepo kwake jangwani kiliwakilisha taswira ya Kanisa la Mungu kuwa Jangwa la Sini chini ya maongozi ya Yesu Kristo. Ni Malaika wa Uwepo wa Mungu aliyeonekana kwenye Nguzo ya Moto na Wingu. Ndiye aliyewapa Torati wana wa Israeli. Kwa kufufu kwwake, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, aliwaongoza watu wa Mungu. Torati au sheria ziliandikwa mioyoni mwao na akilini mwao kwa kipindi cha zaidi ya yubile arobaini, au miaka elfu mbili kuanzia Mwaka Uliokubalika wa Bwana au yubile hadi kwenye timu nyingine ya pili iliyokamili kwa Miaka arobaini Iliyokubalika ya Bwana. Ndipo kwa hiyo anaposalia kuwa ni mfalme mshindi na mtawala wa Yerusalemu. Yubile ya mwisho itafupishwa ili kuwaokoa wale wanaomngoja kwa hamu kubwa Masihi.

 

Baada ya kufa na kufufuka kwa Kristo na kumpokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, Yuda walipewa miaka arobaini ya kutubu na kisha Hekalu la kimwili liliangushwa na kuharibiwa kabisa, na Yuda walitawanywa huku na kuondoka wote kwa utimilifu wa kipindi cha yubile arobaini.

 

Maskani iliyojengwa au kusimamishwa jangwani ilikuwa ni mfano au mpango wa kile kinachokuja na wa Maskani ya mbinguni. Waebrania 8:5 inaonyesha kuwa huu ulikuwa ni mfano.

Waebrania 8:5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.

 

Mfano huu ulifanywa ili kwamba Mungu awe ametuandaa kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu kama mitume walivyotuambia sisi.

Waebrania 8:8-13 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; 9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana. 10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu. 11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao. 12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena. 13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.

 

Ahadi ya agano la dhabihu ilitoa njia ya ahadi ya kipawa cha Mungu katika Roho Mtakatifu kwa kupitia dhabihu iokoayo ya Kristo.

 

Pasipo Roho Mtakatifu wa Mungu, Torati na muundo hauwezi kutunzwa na kuwa isiwezekane kuishi maisha ya ukweli na utauwa.

 

Maisha mfano haya yanaonekana pia kwenye maisha ya wafalme.

 

Historia ilivyokuwa wakati wa Wafalme

Kipindi au wakati ambao Israeli walipewa wafalme kilikuwa ni cha chini ya mateso makali kutoka kwenye vyanzo kadhaa mbalimbali. Kila mara walipokuwa sio waaminifu kwa Mungu walikwenda utumwani. Wakati Israeli walipomtubia Mungu ,maliwainulia nabii au kiongozi wa kuwaongoza vitani ili awaokoe kutoka utumwani.

 

Hili ni fundisho endelevu la wakati ulioelezewa kwenye Kitabu cha Waamuzi. Wa mwisho kati ya watu hawa mashuhuri alikuwa ni Samweli aliyechukua nafasi yake kutoka kwa Eli, ambaye alikuwa ni mwamuzi na kuhani wa Israeli.

 

Watu tunaowajua leo kama Wafilisti kutoka kwenye Maandiko Matakatifu na kutajwa au kujuliakana pwengine kama Wapereseti au Watu wa Bahari walikuwa ni kundi la waabudu sanamu ambao walichukua nafasi zao kwenye kipindi hiki cha mchanganyiko wa mgongano za watu waliochaguliwa na kutengwa mbali na Mungu. Walifanya mengi ya kazi hizohizo za mfumo na utaratibu wa dunia kama walivyofanya Wanefili wakati wa kabla ya gharika kuu. Kwenye andiko hili tunaweza sasa kumuona Sauli.

 

Sauli

Kulikuwapo na Sauli wa Wana wa Ufalme wa Edomu wa wana wa Esau aliyewatawala Waedomu. Alikuwa anatoka huko Rehobothi pembeni mwa mto Frati.

 

Mwanzo 36:37 Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake.

 

Mwanzo 36:38 Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake.

 

Mstari wa uzao wa Sauli wa Israeli ulikuwa ni wa Wabenyamini aliyezaliwa na Neri na Kishi.

1Mambo ya Nyakati 8:33 Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali. (sawa na 1Mambo ya Nyakati 9:39)

 

Sauli alifanyika kuwa mfalme wa Israeli. Watu walimkataa Mungu kuwa mfalme na kiongozi wao. Hii ilijulikana kama misingi wa Kanisa la Agano Jipya.

Matendo 13:21 Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini.

 

Waamuzi wa Israeli alichaguliwa na kuinuliwa na Mungu. Watu wa Israeli waliujua na kuuelewa ukweli ule lakini si Eli wala Samweli, waamuzi wa mwisho wa Israeli aliowakataza au kuwazkuia watoto wake kama walivyopaswa kufanya.

 

1Samweli 8:4-9 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; 5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote. 6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana. 7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. 8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. 9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.

 

Samweli pia aliwaambia ukweli huo wa kumkataa kwao Mungu wakati alipomtawadha Sauli kuwa mfalme.

 

1Samweli 10:17-19 Basi Samweli akawakusanya watu mbele za Bwana huko Mispa 18 akawaambia wana wa Israeli, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Naliwatoa Israeli kutoka Misri, nami naliwaokoa ninyi na mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea; 19 lakini leo mmemkataa Mungu wenu, naye ndiye awaponyaye katika misiba yenu yote na shida zenu; nanyi mmemwambia, Sivyo, lakini weka mfalme juu yetu. Basi, sasa, hudhurieni mbele za Bwana, kwa kabila zenu na kwa elfu zenu.

 

Samweli aliwaonya pia kuhusu matokeo mabaya ya kumkataa kwao Mungu na kile kingalichoweza kutokea kwao.

1Samweli 8:10-22 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana. 11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. 12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake. 13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji. 14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake. 15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake. 16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe. 17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake. 18 Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; Bwana asiwajibu siku ile. 19 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu; 20 ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu. 21 Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa Bwana. 22 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake.

 

Watu waliamua kuchagua kuwa na mfalme na kitendo hiki kuliwafanya wajue kanuni za kuanzisha ufalme katika Israeli, ambao ungeweza kabisa kuwaongoza kwenye ufalme wa Masihi. Kwa mtazamo huu ufalme ulikuwa umekwisha ahidiwa tayari kwa Yuda kwenye ahadi za uzaliwa wa kwanza zilizotolewa kwene Mwanzo 49:10. Hata hivyo, Mungu hakuwaletea ahadi ile ikamilike kwa haraka. Alitangulia kwanza kushughulika kwa jinsi watu wanavyodhania na pia kuonyesha kuelekea kwenye ahadi nyingine. Alimchagua kutoka kwenye kabila la Benyamini. Kabila hili lilishagawahi kufutiliwa mbali lakini kwa wnaume 600 kutokana na dhambi zao, na kwa hiyo walipewa wanawake kutoka kwenye makabia meingine ili wazae nao na kulianzisha na kuliendeleza kabila lao. Ukweli huu ulikuwa unaonyesha ishara ya kuelekea uanzishaji wa kuunganisha ufalme chini ya Masihi kwa kuwatumia wana wa ahadi na makabila ya Israeli.

 

Tendo hili lilikuwa linalenga uongofu wa matgaifa na uanzishwaji wa ukuhani wa mfano wa Melkizedeki chini ya Masihi (sawa na isemavyo Ufunuo 7:3-8). Tutaona jambo hilo baadae.

1Samweli 9:1-27 Basi, kulikuwa na mtu mmoja wa Benyamini, jina lake akiitwa Kishi, mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini, mtu shujaa, mwenye nguvu. 2 Naye alikuwa na mwana, aliyeitwa jina lake Sauli, kijana, tena mzuri; wala katika wana wa Israeli hakuwako mtu mzuri kuliko yeye; tangu mabega yake kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wote. 3 Na punda za Kishi, baba yake Sauli, walikuwa wamepotea. Kishi akamwambia Sauli mwanawe, Haya basi, twaa mtumishi mmoja pamoja nawe, uondoke, uende ukawatafute punda hao. 4 Naye akapita kati ya nchi ya milima milima ya Efraimu, akapita na kati ya nchi ya Shalisha, lakini hawakuwaona; kisha wakapita kati ya nchi ya Shaalimu, wala huko hawakuwako; wakapita kati ya nchi ya Wabenyamini, lakini hawakuwapata. 5 Hata walipofika nchi ya Sufu, Sauli akamwambia yule mtumishi aliyefuatana naye, Haya, na turudi, baba yangu asije akaacha kufikiri habari za punda akatufikiri sisi. 6 Naye akamwambia, Tazama, katika mji huu mna mtu wa Mungu, naye ni mtu mwenye kuheshimiwa; yote asemayo hutukia kweli kweli; basi, twende huko; labda yeye aweza kutuambia habari ya safari yetu tunayoiendea. 7 Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, Lakini angalia, kama tukienda, tumpelekee mtu huyo kitu gani? Maana chakula kimekwisha vyomboni mwetu, wala hapana zawadi ya kumpelekea mtu wa Mungu; tuna nini sisi? 8 Yule mtumishi akamjibu Sauli, akasema, Tazama, mkononi mwangu nina robo ya shekeli ya fedha; nitampa huyo mtu wa Mungu fedha hiyo, atuambie njia yetu.

 

Wakati wa Sauli watu waliwatumia waonaji kama alivyofanya kila mtu aonavyo vyema machoni pake mwenyewe. Mungu alinena kwa kupitia waamuzi, lakini waonaji walikwenda kuulizwa mambo. Ilikuwa ni kawaida kwenda kumuuliza mwonaji siku ya Miandamo ya Mwezi, ambazo zilikuwa siyo siku za kufana biashara kama zilivyokuwa siku za Sabato.

1Samweli 9:9 (Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.) 10 Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu. 11 Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko? 12 Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu; 13 mkiingia mjini tu, mara mtamwona, kabla hajakwea kwenda mahali pa juu ale chakula; maana, watu hawatakula hata yeye atakapokuja; kwa sababu yeye ndiye anayeibarikia dhabihu; kisha hao watu walioalikwa hula. Basi, kweeni sasa; maana wakati huu ndio mtakapomwona. 14 Nao wakakwea kwenda mjini; nao walipokuwa wakiingia mjini, tazama, Samweli akawatokea, kwenda mahali pa juu.

 

Mungu alikuwa macho kuangalia tendo hili na kuchaguliwa kwa Sauli. Hii iko wazi kutoka kwenye maandiko yaliyo kwenye aya za 15 na kuendelea.

15 Basi Bwana alikuwa amemfunulia Samweli, siku moja kabla Sauli hajamwendea, akisema, 16 Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia. 17 Hata Samweli alipomwona Sauli, Bwana akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu. 18 Ndipo Sauli akamkaribia Samweli langoni, akasema, Tafadhali, uniambie, nyumba ya mwonaji iko wapi? 19 Samweli akamjibu Sauli, akasema, Mimi ndimi mwonaji; tangulia mbele yangu ukwee mpaka mahali pa juu, kwa maana mtakula pamoja nami leo; kisha, asubuhi nitakuacha uende zako, nami nitakuambia yote uliyo nayo moyoni mwako. 20 Na wale punda zako waliopotea siku hizi tatu, usijiudhi kwa ajili yao; maana wameonekana. Na yote yaliyotamanika katika Israeli amewekewa nani? Si wewe, na nyumba yote ya baba yako? 21 Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila ya Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo? 22 Naye Samweli akamtwaa Sauli na mtumishi wake, akawaleta ndani sebuleni, akawaketisha mahali pa heshima kati ya watu walioalikwa, nao jumla yao walikuwa kama watu thelathini. 23 Samweli akamwambia mpishi, Lete ile sehemu niliyokupa, hiyo niliyokuambia, Iweke akiba. 24 Basi mpishi akatwaa paja, na nyama iliyokuwa juu yake, akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, Iliyowekwa akiba ndiyo hiyo! Iweke mbele yako ule, kwa sababu umewekewa hiyo wewe hata wakati uliokusudiwa, maana nalisema, Nimewaalika watu. Basi Sauli akala pamoja na Samweli siku hiyo. 25 Hata waliposhuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, akaongea na Sauli darini. 26 Nao wakaamka alfajiri; kisha ikawa, kulipopambazuka, Samweli akamwita Sauli darini, akisema, Inuka, nikupeleke kwenu. Basi Sauli akainuka, nao wakatoka wote wawili, yeye na Samweli. 27 Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu.

 

Tendo hili linaonyesha kuwa wateule wanastahili kuhesabiwa kwenye baraza la elohim, na kwa maneno mengine, ni kuwa hata miongoni mwa wale thelathini, kwa kupitia mwaliko wa manabii wa Mungu. Mwendelezo wa habari ni kuonyesha umuhimu wa wateule kuurithi Ufalme wa Mungu. Hii inaonyesha pia namna ambayo mapepo wangalivyoweza pia kumpokea Roho Mtakatifu kwa mpango wa Mungu. Jambo hili lenye maana ya mpango wa Mungu kumtumia Sauli kuwa ni mfalme haukueleweka. Mungu huwatia mafuta watumishi wake kwa njia ya Roho Mtakatifu.

1Samweli 10:1-27 Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake. 2 Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu? 3 Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai; 4 nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. 5 Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri; 6 na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine. 7 Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe. 8 Nawe utatelemka mbele yangu mpaka Gilgali; nami, angalia, nitakutelemkia huko, ili kutoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja sadaka za amani; siku saba utangoja, hata nitakapokujia, na kukuonyesha yatakayokupasa kuyafanya. 9 Ikawa, alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu akambadilisha moyo; nazo ishara zile zote zikatukia siku ile ile. 10 Basi, walipofika Gibea, tazama, kikosi cha manabii wakakutana naye; kisha roho ya Mungu ikamjilia kwa nguvu, naye akatabiri kati yao. 11 Ikawa, wote waliomjua zamani walipoliona jambo hilo, kwamba, tazama, huyo anatabiri pamoja na manabii, ndipo watu wakasemezana, Ni nini hilo lililompata mwana wa Kishi? Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii? 12 Naye akajibu mtu mmoja wa mahali hapo, akasema, Na baba yao n'nani? Kwa hiyo ikawa mithali, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?

 

Kutokana na andiko hili tunaona kwamba mikate miwili ilitengwa kando kwa ajili ya Sauli na alipokea Roho Mtakatifu na akatabiri. Mikate miwili ya siku ya Pentekoste inawakilisha upokeaji wa Roho Mtakatifu. Mvinyo unaokunywa pamoja nayo na mbuzi wawili vinawakilisha dhabihu wa Pasaka na za Siku ya Upatanisho. Siku ya Upatanisho, mbuzi mmoja anapelekwa jangwani kwa mikono ya mtu hodari. Hii inaashiria mfano wa kufungwa kwake Shetani na malaika mwenye nguvu na hodari kweenye kipindi cha utawala wa millennia wa Kristo (sawa na lisemavyo jarida la Azazeli na Upatanisho (Na. 214) [Azazel and Atonement (No. 214)]. Hakuna kilichoandikwa kuhusu manabii miongoni mwa wana wa Benyamini lakini kulikuwa na manabii wakuu wengi Benyamini, na sio mdogo miongoni mwa mitume alivyokuwa ambaye ni Paulo ambaye alikuwa hapo mwanzoni akiitwa pia Sauli wa Taso, na pia ni Mbenyamini (Wafilipi 3:5). Kitendo cha kumuingiza Sauli kuwa mbadala miongoni mwa manabii ulichukuliwa kwa maelezo kama hayohayo wakati Sauli huyu alipobadilika na kuwa Paulo na akafanyika kuwa mtume. Kwa siku hii hii majadiliano na uthabiti alishambuliwa na mitume wa Kiyahudi na wenye itikadi ya dini ya Kiyahudi kwa namna hiyohiyo. Dokezo ni pia kwamba Mungu sio baba yao.

 

13 Naye alipokwisha kutabiri, alipafikilia mahali pale pa juu. 14 Basi babaye mdogo akamwuliza Sauli na mtumishi wake, Je! Mlikwenda wapi? Naye akajibu, Tulikwenda ili kuwatafuta hao punda; na tulipoona ya kwamba hawakuonekana, tulimwendea Samweli.15 Babaye mdogo Sauli akasema, Tafadhali uniambie, huyo Samweli aliwaambiaje? 16 Lakini Sauli akamjibu babaye mdogo, Alituambia waziwazi ya kuwa hao punda wamekwisha onekana. Lakini habari ya ufalme, ambayo Samweli alimwambia, hakuitaja habari hiyo.

 

Mungu anamtenga na kumuweka mbali mtiwa mafuta wake na halifunui kkuliweka wazi jambo hili hadi utakapokuja wakati wa kuliweka wazi. Wakati unapofika muda wake, Mungu hufanya mambo kwa kupitia watumishi wake manabii. Kwenye jambo hili alichagua kwa kura, ambalo ni tendo la kawaida kwa watu wa Mungu.

17 Basi Samweli akawakusanya watu mbele za Bwana huko Mispa 18 akawaambia wana wa Israeli, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Naliwatoa Israeli kutoka Misri, nami naliwaokoa ninyi na mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea; 19 lakini leo mmemkataa Mungu wenu, naye ndiye awaponyaye katika misiba yenu yote na shida zenu; nanyi mmemwambia, Sivyo, lakini weka mfalme juu yetu. Basi, sasa, hudhurieni mbele za Bwana, kwa kabila zenu na kwa elfu zenu. 20 Basi Samweli akawaleta kabila zote za Israeli karibu; na kabila ya Benyamini ikatwaliwa. 21 Kisha akaileta kabila ya Benyamini karibu, kwa jamaa zao; jamaa ya Wamatri ikatwaliwa. Akaileta jamaa ya Wamatri karibu, mtu baada ya mtu; kisha Sauli, mwana wa Kishi, akatwaliwa; lakini walipomtafuta hakuonekana.

 

Sauli alijaribu kujificha na kukwepa kazi au majukumu yaliyowekwa juu yake. Mungu atakufanya ufanye kile alichokiweka mbele zako. Nabii Yeremia alichaguliwa na kazi yake ikawekwa, hata kabla hajatungwa mimba tumboni mwa mama yake. Hii ni kawaida kwa manabii wote wa Mungu. Huwezi kujificha.

22 Basi wakazidi kumwuliza Bwana, Amebaki mtu asiyekuja huku bado? Naye Bwana akajibu, Tazama, amejificha penye mizigo. 23 Basi wakaenda mbio wakamleta kutoka huko; naye aliposimama kati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu wote, tangu mabega yake kwenda juu. 24 Samweli akawaambia watu wote, Mnamwona mtu huyu aliyechaguliwa na Bwana, ya kuwa hakuna mtu mfano wake katika watu wote. Ndipo watu wote wakapiga kelele, wakasema, Mfalme na aishi!

Mungu alimchagua na kumtia mafuta Sauli baada ya namna ambayo watu wanaona na kuhukumu. Kisha Mungu akawaambia jinsi ufalme unavyokuwa na jinsi mambo yake yatakavyokuwa. Hii ilipunguzwa kwenye Maandiko Matakatifu na kuwekwa kwene Maskani.

 

25 Kisha Samweli aliwaambia watu madaraka ya ufalme, akayaandika katika kitabu, akakiweka mbele za Bwana. Samweli akawaruhusu watu wote, waende kila mtu nyumbani kwake. 26 Sauli naye akaenda nyumbani kwake huko Gibea; na pamoja naye wakaenda kikosi cha watu, ambao Mungu alikuwa ameigusa mioyo yao.

 

Mungu alimtenga Sauli mbali na mikono ya watu ambao moyo wake uliguswa na Roho Mtakatifu. Shetani alijua jambo au tendo hili mara moja.

27 Walakini wengine wasiofaa kitu wakasema, Huyu je! Atatuokoaje? Nao wakamdharau, wasimletee zawadi.

 

Sauli akashikilia amani yake. Matukio haya yalikuwa na mapatilizo yake baadae. Kisha Mungu alianza mchakato wa kuanzisha na kuweka mazingira ambayo kwamba chaguo lake liweze kuwepo huko Israeli.

1Samweli 11:1-15 Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi, Mwamoni ,akakwea na kupanga marago juu ya Yabesh-gileadi;na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi,na sisi tutakutumikia. 2 Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hii mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kuume; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia. 3 Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, Tuachie siku saba, ili tutume wajumbe waende mipakani mwote mwa Israeli; kisha, ikiwa hakuna atakayetuokoa, tutakutokea. 4 Hivyo wajumbe wakafika Gibea ya Sauli, wakasema maneno hayo masikioni mwa watu; na watu wote wakainua sauti zao wakalia. 5 Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi. 6 Na roho ya Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, hapo alipoyasikia maneno yale, na hasira yake ikawaka sana. 7 Naye akatwaa jozi ya ng'ombe, akawakata-kata vipande, kisha akavipeleka vile vipande mipakani mwote mwa Israeli kwa mikono ya wajumbe, kusema, Ye yote asiyetoka nyuma ya Sauli na Samweli, ng'ombe zake watatendwa vivi hivi. Basi utisho wa Bwana ukawaangukia wale watu, wakatoka kama mtu mmoja.

 

Kisha Mungu akampa Roho wake Sauli na Sauli akagundua pia kwamba Mungu alikuwa pamoja na Samweli. Mfalme alikuwa pamoja na manabii na alimtegemea Samweli kuwa ni nabii wa Mungu

8 Naye akawahesabu huko Bezeki; Waisraeli walikuwa mia tatu elfu, na Wayuda thelathini elfu. 9 Nao wakawaambia hao wajumbe waliokuja, Waambieni watu wa Yabesh-gileadi, Kesho, wakati wa jua kali, mtapata wokovu. Basi wale wajumbe wakaenda, wakawaarifu watu wa Yabeshi; nao walifurahiwa. 10 Kwa hiyo watu wa Yabeshi walisema, Kesho tutawatokea, nanyi mtatufanyia yote myaonayo kuwa ni mema. 11 Ikawa, kesho yake, Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu; nao wakaingia katikati ya marago kwenye zamu ya asubuhi, wakawapiga Waamoni hata wakati wa jua kali; kisha ikawa wale waliosalia wakatawanyika, hata wasiachwe wawili wao pamoja.

Kwa jinsi hiyohiyo Gideoni aliyashinda mataifa kwa vikosi vitatu na ndivyo Sauli pia alivyoyagawa majeshi yake makundi matatu. Gideoni alikuwa na wanajeshi mia tatu elfu wa Israeli. Jeshi hili lilikuwa na nguvu mara elfu zaidi ya lile lililokuwa kwenye kamadi ya kawaida lililoundwa chini ya Gideoni na lilijumuisha majeshi ya Yuda. Simba hawa wa Israeli walinenwa haabade kwenye unabii. Sasa tunaon a matokeo ya watu waliomdhihaki Mtiwa Mafuta wa Bwana. Haikutokea kwao kuwa Sauli alikuwa ni mtiwa mafuta wa kweli na walimdhihaki. Alinyamaza kimwa lakini mara baada ya kuimarisha nguvu zake na umaarufu wake katika Israeli aliwashughulikia sawasawa na mashauri ya Mungu katika Roho Mtakatifu. Watu walitaka watu wale wauawe. Walakini Sauli hakukubali shauri hilo akawazuia ili afanikishe kuuimarisha ufalme na kuunganisha na ndipo Samweli akachukua fursa hii.

12 Ndipo watu walipomwambia Samweli, Ni nani yule aliyesema, Je! Huyo Sauli atatutawala? Walete watu hao, ili tuwaue. 13 Lakini Sauli akasema, Hakuna mtu atakayeuawa leo, maana leo Bwana amefanya wokovu katika Israeli. 14 Kisha Samweli akawaambia watu, Haya! Na twendeni mpaka Gilgali, ili tuuimarishe ufalme huko mara ya pili. 15 Nao watu wote wakaenda Gilgali; wakamtawaza Sauli mbele za Bwana huko Gilgali; wakachinja sadaka za amani mbele za Bwana; na huko Sauli na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.

 

Maendeleo kutoka kipindi cha waamuzi hadi kwenye ufalme kiliwekwa kwa utaratibu na kwa mujibu wa makusudi na malengo ya Mungu. Mungu aliutumia udhaifu wa watu ili kurejesha mtangamano mpya na kuweka utaratibu mpya chini ya uongozi wa Masihi kayika Israeli. Licha ya dhambi na udhaifu, Mungu aliweka utaratibu ambao ungeweza kushinda. Alitangaza mwisho wake tangu mwanzo wake.

1Samweli 12:1-24 Kisha Samweli akawaambia Israeli wote, Angalieni, nimeisikiliza sauti yenu katika hayo yote mliyoniambia, nami nimemtawaza mfalme juu yenu. 2 Basi sasa, angalieni, mfalme anakwenda mbele yenu; na mimi ni mzee, mwenye mvi; tena, tazameni, wana wangu wapo pamoja nanyi; nami nimekwenda mbele yenu toka ujana wangu hata leo. 3 Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za Bwana, na mbele ya masihi wake,nalitwaa ng`ombe wa nani? au nalitwaa punda wa nani? au ni nani niliye mdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi. 4 Nao wakasema, hukutudhulumu, wala hukutuonea, wala hukupokea kitu kwa mkono wa mtu awaye yote. 5 Akawaambia, Bwana ni shahidi juu yenu, na Masihi wake ni shahidi leo, ya kuwa hamkuona kitu mkononi mwangu. Nao wakasema, Yeye ni shahidi.

 

Manabii wa Mungu hawakutafuta kitu cha kuwanufaisha na watu walishuhudia ukweli huu.

 

Ndipo Samweli akaanza kuwakumbusha tena haki na utakatifu wa Mungu.

6 Samweli akawaambia watu, Ni yeye Bwana aliyewaweka Musa na Haruni, ndiye yeye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri. 7 Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za Bwana, kwa kutaja matendo yote ya haki ya Bwana, aliyowatendea ninyi na baba zenu. 8 Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia Bwana, ndipo Bwana akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa. 9 Lakini wakamsahau Bwana, Mungu wao, naye akawauza na kuwatia katika mikono ya Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori, na katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya mfalme wa Moabu, nao wakapigana nao. 10 Nao wakamlilia Bwana, wakasema, Tumefanya dhambi, kwa kuwa tumemwacha Bwana, na kuwatumikia Mabaali na Maashtorethi; lakini sasa utuokoe na mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia wewe. 11 Bwana akawatuma Yerubaali, na Baraka, na Yeftha, na Samweli, akawaokoa ninyi na mikono ya adui zenu pande zote, nanyi mkakaa salama. 12 Hata mlipomwona Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, amekuja kupigana nanyi, mliniambia, Sivyo, lakini mfalme atatutawala; ingawa Bwana, Mungu wenu, ni mfalme wenu. 13 Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, Bwana ameweka mfalme juu yenu.

Ndipo Mungu aliyaweka mazingira ya muhimu kwa Israeli kwa wakati wote. Masharti haya yanaendelea kutuhitaji hadi leo pasipo kujali ni nani anatawala sasa huko Israeli na tuko kwenye taifa lipi.

14 Kama mkimcha Bwana, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya Bwana, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata Bwana, Mungu wenu, vema! 15 Bali msipoisikia sauti ya Bwana, mkiiasi amri ya Bwana, ndipo mkono wa Bwana utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu. 16 Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, Bwana atakalolitenda mbele ya macho yenu. 17 Leo je! Si mavuno ya ngano? Nitamwomba Bwana, kwamba apeleke ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu ni mwingi sana, mlioufanya machoni pa Bwana, kwa kujitakia mfalme. 18 Basi Samweli akamwomba Bwana, naye Bwana akapeleka ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa Bwana sana, na Samweli pia. 19 Watu wote wakamwambia Samweli, Utuombee sisi watumwa wako kwa Bwana, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme. 20 Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata Bwana, bali mtumikieni Bwana kwa mioyo yenu yote. 21 Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili, 22 visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe. 23 Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka 24 Mcheni Bwana tu, mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote; maana, kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu.

Na ndivyo ilikuwa ni watu wale walitahadharishwa kuhusu dhambi zao lakini waliendelea kuzitenda hadi kilipokuja kipindi cha Shilo kilipokuja hadi kufikia kipindi ufalme nah ii haikuchukua mkondo wake. Masihi amekuja kama Masihi Kuhani lakini mara nyingine ijayo atakuja kama mfalme. Hadi kufikia wakati ule sisi bado tutakuwa chini ya utaratibu huu na ni kwa sasa tu ndipo utaratibu huu umeondolewa na wafalme, makuhani na manabii (sawa na maoni ya jarida la Kulipima Hekalu (Na. 137) [Measuring the Temple (No. 137)].

 

Kisha Sauli akaliandaa jeshi la usimamizi la watu elfu tatu alipokuwa ametawala kwa kipindi cha miaka miwili. Elfu mbili walikuwa pamoja naye huko Mikimashi na Betheli. Elfu wengine walikuwa pamoja na mtoto wake Yonathani huko Gibea ya Benyamini. Kisha Mungu aliweka mpango wa kuwaangamiza maadui wa Israeli ili kuliwezesha taifa liwepo.

1Samweli 13:1-23 Sauli alikuwa na umri wa miaka kadha wa kadha hapo alipoanza kutawala;naye akatawala miaka kadha wa kadha juu ya Israeli. 2 Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini; nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake. 3 Yonathani akaipiga hiyo ngome ya Wafilisti, iliyokuwako huko Gibea, nao Wafilisti wakapata habari. Naye Sauli akapiga tarumbeta katika nchi yote, huku akisema, Na wasikie Waebrania. 4 Waisraeli wote wakasikia habari ya kwamba Sauli ameipiga hiyo ngome ya Wafilisti, na ya kwamba Waisraeli wamepata kuwa makuruhi kwa Wafilisti. Basi hao watu wakakusanyika pamoja kumfuata Sauli huko Gilgali. 5 Nao Wafilisti wakakusanyana ili wapigane na Waisraeli, magari thelathini elfu, na wapanda farasi sita elfu, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.

Kwa sababu hiyohiyo ndivyo walitaka kuwa na mfalme na sasa wanaogopa. Walipungukiwa na imani.

6 Hata Waisraeli walipoona ya kuwa wa katika dhiki, (maana watu walifadhaishwa), ndipo hao watu wakajificha katika mapango, na katika vichaka, na katika miamba, na katika mashimo, na katika mabirika. 7 Hata baadhi ya Waebrania walivuka Yordani, wakaingia nchi ya Gadi na Gileadi; lakini Sauli alikuwa akaliko huko Gilgali, nao watu wote wakamfuata wakitetemeka.

Kwa hiyo Sauli akapewa maelekezo sawasawa na neno la Samweli na alijaribiwa na kushindwa. Mungu alikuwa amemsimamisha au kumuinua na kumruhusu au kumfanya ajiimarishe. Hata hivyo, aliliasi neno la Mungu na kukumbwa na mapatilizo yake.

8 Akangoja siku saba, kwa kadiri ya muhula uliowekwa na Samweli lakini Samweli hakuja Gilgali; na hao watu wakatawanyika mbali naye. 9 Sauli akasema, Nileteeni hapa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani. Akaitoa sadaka ya kuteketezwa. 10 Hata mara alipokwisha kuitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, kumbe! Samweli akatokea. Naye Sauli akatoka kwenda kumlaki na kumsalimu. 11 Samweli akasema, Umefanya nini? Naye Sauli akasema, Ni kwa sababu naliona ya kuwa watu wanatawanyika mbali nami, na wewe hukuja siku zile zilizonenwa; nao Wafilisti wamekusanyika pamoja huko Mikmashi; 12 basi nikasema, Wafilisti watanishukia sasa mpaka Gilgali, kabla sijaomba fadhili za Bwana; kwa hiyo nalijishurutisha, nikatoa sadaka ya kuteketezwa. 13 Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya Bwana, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele.

 

Kuzishika Amri za Mungu ni muhimu katika kuendeleza ufalme wa wateule. Mfano huu huu hapa ni mfano ambapo Mungu alimpa Amri zake Yesu Kristo. Kanisa pia lilianzishwa na lilizifuata Sheria za |Mungu na halafu ndani ya kipindi cha miaka mia moja walianza kuabudu siku za Jumapili kinyume kabisa na maagizo ya Torati ya Mungu. Kwa hiyo ufalme wao uliondolewa. Lakini waliruhusiwa kutawala kwa kipindi cha miaka yubile arobaini kama Sauli alivyotawala kwa miaka arobaini. Hii ilitokea kwanza na Adamu na uharibifu, na pia kwa Kanisa chini ya Masihi. Tutajione zaidi kuhusu hii baadae.

14 Lakini sasa ufalme wako hautadumu; Bwana amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye Bwana amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile Bwana alilokuamuru. 15 Basi Samweli akaondoka, akapanda kutoka Gilgali mpaka Gibea ya Benyamini. Naye Sauli akawahesabu watu waliokuwapo pamoja naye, wapata kama mia sita. 16 Naye Sauli, na mwanawe Yonathani, na watu waliokuwapo pamoja nao, wakakaa huko Geba ya Benyamini; lakini Wafilisti wakatua katika Mikmashi. 17 Nao watekaji wa nyara wakatoka katika marago ya hao Wafilisti, vikosi vitatu; kikosi kimoja kikageukia njia iendayo Ofra, mpaka nchi ya Shuali; 18 na kikosi kingine kikageukia njia iendayo Beth-horoni; na kikosi kingine kikageukia njia ya mpakani ielekeayo bonde la Seboimu upande wa nyika.

Wafilisti walishambulia pia kwa vikosi vitatu. Walichukua tahadhari kwa kufuata sera au mbinu ya kuifanya Israeli isijimudu kwa vita. Na hii ndiyo inayojitokeza hata sasa kuizuia Israeli kuukomesha mfumo na imani iliyopo ya mungu wa dunia hii katika siku hizi za mwisho.

19 Basi, hakuonekana mhunzi ye yote katika nchi yote ya Israeli; kwa kuwa Wafilisti walisema, Waebrania wasije wakajifanyizia panga au mikuki; 20 lakini Waisraeli wote hushuka kwa Wafilisti, ili kunoa kila mtu jembe lake, na mundu wake, na shoka lake, na sululu yake; 21 ila walikuwa na tupa za kunolea sululu, na miundu, na mauma, na mashoka; na kwa kuinoa michokoo. 22 Hivyo ikawa, siku ya vita, haukuonekana mkononi mwa mtu ye yote, miongoni mwa watu waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani, upanga wala mkuki; isipokuwa Sauli mwenyewe na mwanawe Yonathani walikuwa navyo. 23 Na jeshi la Wafilisti wakatoka hata mwanya wa Mikmashi.

 

Israeli haikuwa na ulinzi mwingine isipokuwa ni Mungu peke yake. Uwezo wa kulijenga jeshi unashambuliwa sasa ili kuyafanya mataifa yadhoofike na uwezo wa kuwa na majeshi na shughuli zake yenyewe.

 

1Samweli 14:1-52 Basi ikatukia siku moja, ya kwamba Yonathani, mwana wa Sauli, akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na tuwavukie Wafilisti ngomeni, pale ng'ambo ya pili. Walakini hakumwarifu babaye. 2 Naye Sauli alikuwa akikaa katika upande wa mwisho wa Giba, chini ya mkomamanga ulioko kwenye uga; na hao watu waliokuwa pamoja naye walipata watu mia sita; 3 na Ahiya, mwana wa Ahitubu nduguye Ikabodi, mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa Bwana huko Shilo, mwenye kuvaa naivera. Tena hao watu hawakujua ya kwamba Yonathani ameondoka. 4 Na katikati ya mianya, ambayo Yonathani alitaka kuipitia ili kuifikilia hiyo ngome ya Wafilisti, palikuwa na genge la jabali upande huu, na genge la jabali upande huu; jina la moja liliitwa Bosesi, na jina la pili Sene.

Bozez (SHD 949) maana yake ni kung’ara na limechukuliwa na neno (kwa mujibu wa SHD 948) kuwa salama au mweupe au kung’ara kwa weupe.

 

Jiwe nyingine lenye ncha kali Seneh (SHD 5573) ambalo maana yake ni mwiba au kitu cha kuchoma lililochukuliwa kutoka kutoka mwiba wa porini. Namna ya kuamua ni kati ya usafi na miiba.

 

5 Hilo genge moja limesimama upande wa kaskazini, mbele ya Mikmashi, na hilo la pili upande wa kusini, mbele ya Geba. 6 Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na twende tukawavukie ngomeni hao wasiotahiriwa; yamkini Bwana atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia Bwana asiokoe, kwamba ni kwa wengi au kwamba ni kwa wachache. 7 Naye huyo mchukua silaha akamjibu, Fanya yote yaliyomo moyoni mwako; angalia, mimi hapa ni pamoja nawe, moyo wangu ni kama moyo wako. 8 Ndipo Yonathani akasema, Tazama, sisi tutawavukia watu hawa, na kujidhihirisha kwao. 9 Nao wakituambia hivi, Ngojeni, hata sisi tuwafikilie; ndipo tusimame pale pale mahali petu, tusiwapandie. 10 Lakini wakisema hivi, Haya! Ninyi, tupandieni sisi; hapo ndipo tutakapopanda; kwa maana Bwana amewatia mikononi mwetu; na hii itakuwa ndiyo ishara kwetu. 11 Basi, hao wote wawili wakajidhihirisha mbele ya ngome ya Wafilisti, na wale Wafilisti wakasema, Kumbe! Wale Waebrania watoka katika mashimo walimojificha! 12 Nao watu wa ngomeni wakamjibu Yonathani na mchukua silaha zake, wakasema, Haya! Ninyi, pandeni juu hapa tulipo, na sisi tutawaonyesha jambo. Yonathani akamwambia yule aliyezichukua silaha, Haya! Panda nyuma yangu; kwa kuwa Bwana amewatia mikononi mwa Israeli. 13 Basi Yonathani akapanda kwa mikono na miguu yake, na mchukua silaha nyuma yake; na hao watu wakaanguka mbele ya Yonathani; na huyo mchukua silaha zake akawaua nyuma yake. 14 Na uuaji huo wa kwanza walioufanya Yonathani na mchukua silaha zake, ulipata kama watu ishirini, katika nafasi kama nusu ya kiwanja kiwezacho kulimwa katika siku nzima. 15 Kukawa na tetemeko katika marago, na katika mashamba, na katikati ya watu wote; watu wa ngomeni, na watekaji wa nyara, wakatetemeka nao; hata na nchi ikatetemeka pia; basi kulikuwa na tetemeko kubwa mno.

Kwenye udhaifu huu, walikuwa ni Sauli peke yake na Yonathani walikuwa na jeshi lenye nguvu, Mungu akamchagua Yonathani awashide idadi kubwa ya wanaume kupitia imani na hivyo kulifanya jeshi lirudi kwenye mkondo wake.

16 Nao wale walinzi wa Sauli huko Gibea ya Benyamini wakaangalia, na tazama, mkutano ule ulikuwa ukitoweka, na watu walikuwa wakienda huko na huko. 17 Ndipo Sauli akawaambia watu waliokuwa pamoja naye, Haya! Hesabuni sasa, mkaone ni nani aliyeondoka kwetu. Nao walipokwisha hesabu, tazama Yonathani na yeye aliyechukua silaha zake hawapo. 18 Basi Sauli akamwambia Ahiya, Lilete hapa sanduku la Mungu. Kwa kuwa hilo sanduku la Mungu wakati huo lilikuwapo pamoja na wana wa Israeli 19 Ikawa Sauli alipokuwa katika kusema na kuhani, hayo makelele katika marago ya Wafilisti yakaendelea na kuzidi; basi Sauli akamwambia kuhani, Rudisha mkono wako. 20 Naye Sauli na watu wote waliokuwapo pamoja naye wakakusanyika, wakaenda vitani; na tazama, huko upanga wa kila mtu ulikuwa juu ya mwenziwe, kukawa fujo tele kabisa.

Wakati Israeli walipopewa mfano wa kurudi na ushindi muhimu wa kile kilichotokea kuwa ni jeshi lenye nguvu, Waebrania waliokuwa kinyume nao walirudi na kuungana nao na woga wote waliokuwa nao uliisha.

21 Basi na wale Waebrania waliokuwa pamoja na Wafilisti tangu zamani, wale waliopanda pamoja nao mpaka maragoni toka nchi iliyozunguka; watu hao nao wakageuka kuwa upande wa Waisraeli waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani. 22 Na vile vile watu wote wa Israeli waliokuwa wamejificha katika nchi ya milima milima ya Efraimu, waliposikia ya kwamba Wafilisti wamekimbia, hata hao nao wakawafuatia mbio vitani.

Na ndipo ilionekana kwamba Bwana aliwaokoa Israeli siku ile. Sauli alipewa pia amri ambayo ilikuwa ni ya ukali sana na isiyozingatia hali halisi. Iliwatisha na kuwakatisha tamaa na kuwafadhaisha Israeli asipo sababu na iliwasababishia kutenda dhambi.

23 Hivyo Bwana akawaokoa Israeli siku ile; na vita vikapita mbele karibu na Beth-aveni. Wakati huo mbele ya wana wa Israeli. 24 Nao watu wa Israeli walisumbuka sana siku ile; lakini Sauli alikuwa amewaapisha watu, akisema, Na alaaniwe mtu awaye yote alaye chakula cho chote hata jioni, nipate kujilipiza kisasi juu ya adui zangu. Basi hakuna mtu miongoni mwa watu aliyeonja chakula. 25 Nao watu wote wakaingia mwituni; na humo mlikuwa na asali juu ya nchi. 26 Na hapo watu walipokwisha kuingia mwituni, tazama, hiyo asali ilikuwa ikidondoka; walakini hakuna mtu hata mmoja aliyetia mkono wake kinywani; kwa sababu hao watu walikuwa wakikiogopa kile kiapo. 27 Ila Yonathani hakusikia, hapo babaye alipowaagiza watu kwa kiapo; basi yeye akainyosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake, na kuichovya katika sega la asali, kisha akatia mkono wake kinywani; na macho yake yakatiwa nuru. 28 Ndipo mmojawapo wa watu akamjibu, akasema, Baba yako aliwaagiza watu sana kwa kiapo, akisema, Na alaaniwe mtu alaye chakula leo. Na hao watu walikuwa wamepungukiwa na nguvu. 29 Ndipo Yonathani akasema, Babangu ameifadhaisha nchi; tafadhali, angalia jinsi macho yangu yalivyotiwa nuru, kwa sababu nalionja asali hii kidogo. 30 Je! Si zaidi sana, kama watu wangalikula na kushiba leo katika nyara hizi za adui zao walizoziteka? Kwa maana haukuwa uuaji mkuu sasa katikati ya Wafilisti. 31 Nao wakawapiga watu miongoni mwa Wafilisti siku ile kutoka Mikmashi mpaka Ayaloni; na hao watu walikuwa wamepungukiwa sana na nguvu. 32 Basi watu wakazirukia zile nyara, wakatwaa kondoo, na ng'ombe, na ndama, na kuwachinja papo hapo juu ya nchi, nao wale watu walikuwa wakiwala pamoja na damu. 33 Ndipo wakamwambia Sauli, wakisema, Angalia, watu hao wanakosa juu ya Bwana, kwa jinsi wanavyokula pamoja na damu. Naye akasema, Ninyi mmefanya kwa hiana; vingirisheni kwangu leo jiwe kubwa. 34 Kisha Sauli akasema, Haya! Tawanyikeni katikati ya watu mkawaambie, Nileteeni hapa kila mtu ng'ombe wake, na kila mtu kondoo wake, mkawachinje hapa na kula; wala msikose juu ya Bwana, kwa kula pamoja na damu. Nao watu wote wakaleta kila mtu ng'ombe wake pamoja naye usiku ule, nao wakawachinja hapo. 35 Naye Sauli akamjengea Bwana madhabahu; hiyo ndiyo madhabahu ya kwanza aliyomjengea Bwana.

Kosa hili lilifanya asogee karibu kwa Mungu na alijenga madhabahu yake ya kwanza ili kusahihisha makosa ya watu.

 

Sauli alitaka kufuatia ushindi wake lakini wakati alipomtafuta Mungu hakujibiwa. Sababu ya kosa hili halikupnyeshwa kikamilifu kwake bado.

36 Kisha Sauli akasema, Haya! Na tushuke kuwafuata Wafilisti wakati wa usiku, na kuwateka nyara hata mapambazuko, wala tusiwaache hata mmoja wao. Nao wakamjibu, Fanya yo yote uyaonayo kuwa ni mema. Ndipo yule kuhani akasema, Na tumkaribie Mungu hapa. 37 Basi Sauli akataka shauri kwa Mungu, Je! Nishuke ili kuwafuatia Wafilisti? Je! Utawatia mikononi mwa Israeli? Lakini hakumjibu neno lo lote siku ile. 38 Ndipo Sauli akasema, Karibieni hapa, enyi wakuu wote wa watu; mjue na kuona dhambi hii ya leo imekuwa katika kosa gani. 39 Kwa maana, aishivyo Bwana, awaokoaye Israeli, ijapokuwa i katika Yonathani, mwanangu, kufa atakufa. Lakini miongoni mwa watu wote hakuna mtu ye yote aliyemjibu. 40 Ndipo akawaambia Israeli wote, Ninyi mtakuwa upande mmoja, na mimi na mwanangu Yonathani tutakuwa upande wa pili. Basi wakamwambia Sauli, Fanya uonayo kuwa ni mema. 41 Kwa hiyo Sauli akamwambia Bwana, Mungu wa Israeli, [Kwani usimjibu mtumishi wako leo? Ikiwa dhambi i ndani yangu, au ndani yake Yonathani mwanangu, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, utoe Urimu; bali ukisema hivi, Dhambi i katika watu wako Israeli,] utoe Thumimu ,Basi Yonathani na Sauli wakatwaliwa,lakini watu wakapona. 42 Basi Sauli akasema, Sasa piga kati ya mimi na mwanangu Yonathani, [naye awaye yote ambaye Bwana atamtwaa, atakufa. Nao watu wakamwambia Sauli, La! Sivyo hivyo; lakini Sauli akawaweza watu. Nao wakapiga kati ya yeye na mwanawe Yonathani,] 43 Ndipo Sauli akamwambia Yonathani, Niambie ulilolifanya. Basi Yonathani akamwambia, akasema, Ni kweli, mimi nalionja asali kidogo kwa ncha ya fimbo ile iliyokuwa mkononi mwangu; na tazama, imenipasa kufa. 44 Naye Sauli akasema, Mungu anifanyie hivi, na kuzidi; kwa kuwa hakika utakufa, Yonathani.

 

Sauli aliandaliwa kumtoa kafara Yonathani hapa, lakini watu waliingia kati.

45 Walakini watu wakamwambia Sauli, Je! Atakufa Yonathani, ambaye ndiye aliyeufanya huo wokovu mkuu katika Israeli? Hasha! Aishivyo Bwana, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa kichwa chake; kwa maana ametenda kazi pamoja na Mungu leo. Hivyo hao watu wakamponya Yonathani, asife.

Kutoka wakati huu Sauli alianza kuuimarisha ufalme wake. Mungu alimuacha awe kiongozi ingawaje alikuwa amekosa sifa muhimu ya kuwa na haki hiyo.

46 Ndipo Sauli akakwea kuacha kuwafuata Wafilisti; nao Wafilisti wakaenda zao kwao. 47 Basi Sauli alipokwisha kuutwaa ufalme juu ya Israeli, alipigana na adui zake zote pande zote, juu ya Moabu, na juu ya wana wa Amoni, na juu ya Edomu, na juu ya wafalme wa Soba, na juu ya Wafilisti; na po pote alipogeukia, akawashinda. 48 Naye akatenda kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na kuwaokoa Waisraeli katika mikono yao waliowateka nyara. 49 Basi, wana wa Sauli walikuwa ni hawa, Yonathani, na Ishvi, na Malkishua; na majina ya binti zake wawili yalikuwa haya; jina lake wa kwanza aliitwa Merabu, na jina lake mdogo aliitwa Mikali; 50 na jina lake mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu, binti Ahimaasi. Tena, jina la jemadari wa jeshi lake aliitwa Abneri, mwana wa Neri, aliyekuwa baba mdogo wa Sauli. 51 Na Kishi, babaye Sauli, na Neri, babaye Abneri, walikuwa wana wa Abieli. 52 Tena, kulikuwa na vita vikali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu ye yote aliyekuwa hodari, au mtu ye yote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.

 

Waamaleki

Mara nyingi adhabu za Sauli zilipimwa. Hapa anamuasi tgena Mungu kwa Waamaleki.

 

1Samweli 15:1-35 Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya Bwana. 2 Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. 3 Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. 4 Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari waliopanda farasi mia mbili elfu, na watu wa Yuda kumi elfu.

Tunaona tena kwamba Yuda walihesabiwa kwa ajili ya Jeshi. Walijua kwamba fimbo ya kifalme ilikuwa ni yao kutokana na haki ya uzaliwa wa kwanza lakini bado walimfuata Mungu.

5 Sauli akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. 6 Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Enendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. 7 Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri, unaokabili Misri. 8 Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. 9 Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa. 10 Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, kusema, 11 Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha. 12 Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia ukumbusho, akageuka, akapita, akatelemkia Gilgali. 13 Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na Bwana, nimeitimiza amri ya Bwana. 14 Samweli akasema, Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? 15 Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa. 16 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia Bwana usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. 17 Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha kabila za Israeli? Naye Bwana akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. 18 Kisha Bwana akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia. 19 Mbona, basi, hukuitii sauti ya Bwana, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana? 20 Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. 21 Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali. 22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. 23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme. 24 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya Bwana, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. 25 Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu Bwana. 26 Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la Bwana, Bwana naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. 27 Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. 28 Basi Samweli akamwambia, Leo Bwana amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe. 29 Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute. 30 Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu Bwana, Mungu wako. 31 Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu Bwana. 32 Ndipo Samweli akasema, Nileteeni hapa Agagi, mfalme wa Waamaleki. Basi Agagi akamwendea kwa utepetevu. Naye Agagi akasema, Bila shaka uchungu wa mauti umeondoka. 33 Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za Bwana huko Gilgali. 34 Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli. 35 Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye Bwana akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.

Kitendo cha kumfana Sauli kuwa mfalme halikuwa ni kosa la kimtazamo la \Mungu. Kwa uweza wake Mungu wa kujua kila kitu ulimfanya aone ama ajue umuhimu wa kuwa na mfalme wa Yuda. Neno lililotumika hapa halimaanishi kuwa moja ya masahihisho ya makosa bali linamaanisha tu kuweka kikomo cha jambo lililotokea kimatendo amacho kimekwisha patwa na matokeo yake mabaya. Matukio na m kakati ya Waamaleki inaonekana pia kama vita inayoendelea kwa vita ili kumfanya Hagagi awe baba wa watu wa jamii na kabila au taifa la Wahagagi. Kwenye Kitabu cha Esta kutoka kwenye utumwa wa Babeli adui wa Yuda alikuwa ni wa kizazi cha Hagagi aliyeitwa jina lake Hamani Mhagagi. Nabii Ezekieli pia anawaweka Waamoni na Gogu kwenye kundi moja. Gogu wanaitwa pia Agogu au Agagu. Jambo hili limeelezewa pia kwenye jarida la Vita ya Hamon-Gogu (Na. 294) [War of Hamon-Gog (No. 294)].

 

Wafalme Katika Yuda

Hatimaye Mungu aliweka mpango wa kukamilisha ahadi aliyoitoa kwene kabila la Yuda.

1Samweli 16:1-23 Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. 2 Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu. 3 Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako. 4 Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani? 5 Naye akasema, Naam, kwa amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye dhabihu. Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu. 6 Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake. 7 Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo. 8 Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, Bwana hakumchagua huyu. 9 Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala Bwana hakumchagua huyu. 10 Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.

Hii ilikuwa ni kito cha kuelekea kwa Masihi ajaye kutoka kwenye mstari wa uzao wa Daudi, na ukweli wa hapa ni kwamba ilipasa itokee au ifanyike kwenye kipindi fulani kabla hata mfalme wa kweli hajatokea.

11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. 12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. 13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama. 14 Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. 15 Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua. 16 Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona. 17 Basi Sauli akawaambia, Vema, nitafutieni mtu aliye stadi wa kupiga kinubi, mkaniletee. 18 Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye Bwana yu pamoja naye. 19 Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe, akasema, Nipelekee Daudi mwanao, aliye pamoja na kondoo. 20 Yese akatwaa punda, wa kuchukua mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, akampelekea Sauli kwa mkono wa Daudi mwanawe. 21 Basi Daudi akamwendea Sauli, akasimama mbele yake, naye akampenda sana; naye akapata kuwa mtu wa kumchukulia silaha zake. 22 Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana ameona kibali machoni pangu. 23 Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.

 

Kwa hiyo, mstari wa mtiwa mafuta ulipitia kwenye kabila la Yuda na kwenye mstari wa Bethelehemu Efrata.

Ruthu 4:17 Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.

 

Ruthu 4:22 na Obedi akamzaa Yese; na Yese akamzaa Daudi

 

Hadithi ya kumuua Goliathi na Daudi imeelezewa kwa kina kwenye jarida la Daudi na Goliathi (Na. 126) [David and Goliath (No. 126)]. Kukusanyika kwa majeshi ya Wafilisti dhidi ya Israeli kumeelezewa kwa kina kwenye kitabu cha 1Samweli 17:1-58.

 

Daudi na Yonathani walikuwa marafiki wa karibu sana licha ya uadui na chuki za Sauli. Pia kuna hadithi kwenye haki yao wenyewe ya uchumba wa Daudi kumchumbia Mikali. Mahari aliyotakiwa kulipa inahusiana pia na wateule Kanisani na mataifa ya Israeli.

1Samweli 18:1-30 Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe. 2 Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. 3 Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. 4 Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake. 5 Basi Daudi akatoka kwenda kila mahali alikotumwa na Sauli, akatenda kwa akili; Sauli akamweka juu ya watu wa vita; jambo hili likawa jema machoni pa watu wote, na machoni pa watumishi wa Sauli pia. 6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. 7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. 8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? 9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. 10 Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake. 11 Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili. 12 Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja naye, ila amemwacha Sauli. 13 Kwa ajili ya hayo Sauli akamwondosha kwake, akamfanya awe akida wake juu ya askari elfu; naye akatoka na kuingia mbele ya watu. 14 Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye Bwana alikuwa pamoja naye. 15 Sauli alipoona ya kwamba alitenda kwa busara sana, yeye alimwogopa. 16 Lakini Israeli wote na Yuda wakampenda Daudi; kwa kuwa alitoka na kuingia mbele yao. 17 Kisha Sauli akamwambia Daudi, Tazama, binti yangu mkubwa, Merabu, huyu nitakupa wewe ili umwoe; ila na wewe uniwie hodari wa vita, na kuvipiga vita vya Bwana. Maana Sauli alisema moyoni mwake, Mkono wangu usiwe juu yake, bali mkono wa Wafilisti na uwe juu yake. 18 Naye Daudi akamwambia Sauli, Mimi ni nani, na jamaa zangu ni akina nani, au mbari ya babangu, katika Israeli, hata mimi niwe mkwewe mfalme? 19 Lakini ikawa, wakati ule, ilipopasa Daudi apewe Merabu, binti Sauli, aliolewa na Adrieli, Mmeholathi. 20 Walakini Mikali, binti Sauli, alimpenda Daudi; watu wakamwambia Sauli, na neno hilo likampendeza. 21 Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa mkwe wangu. 22 Naye Sauli akawaagiza watumishi wake, Zungumzeni na Daudi kwa siri, na kusema, Angalia, mfalme anakuridhia, na watumishi wake wote wanakupenda; haya basi! Na uwe mkwewe mfalme. 23 Nao watumishi wa Sauli wakanena maneno hayo masikioni mwa Daudi. Daudi akasema, Je! Ninyi mwaona kuwa ni shani mimi kuwa mkwewe mfalme, nami ni maskini, tena sina cheo? 24 Na hao watumishi wa Sauli wakampasha habari, wakisema, Ndivyo hivyo alivyosema Daudi. 25 Naye Sauli akasema, Mwambieni Daudi hivi, Mfalme hataki mahari yo yote, ila anataka govi mia za Wafilisti, ili ajilipize kisasi adui za mfalme. Basi Sauli alidhani kumwangamiza Daudi kwa mkono wa Wafilisti. 26 Na watumishi wake walipomwambia Daudi; maneno hayo, ilimpendeza Daudi sana kuwa mkwewe mfalme. Na siku zilikuwa hazijaisha bado; 27 basi Daudi akainuka, akaenda yeye na watu wake, akaua katika Wafilisti watu mia mbili; na Daudi akazileta govi zao, wakampa mfalme hesabu kamili, ili awe mkwewe mfalme. Naye Sauli akamwoza Mikali, binti yake. 28 Sauli akaona na kutambua ya kwamba Bwana alikuwa pamoja na Daudi; na huyo Mikali, binti Sauli, akampenda. 29 Naye Sauli akazidi kumwogopa Daudi; Sauli akawa adui yake Daudi sikuzote. 30 Wakati huo wakuu wa Wafilisti wakatoka; kisha ikawa, kila mara walipotoka, Daudi akatenda kwa busara zaidi ya watumishi wote wa Sauli hivyo jina lake likawa na sifa kuu.

Ilikuwa ni lazima kwa mtu anayetaka kuwa na utaifa wa Israeli atahiriwe. Wafilisti walikuwa wamekufa katika dhambi zao kwa kumtumikia mungu wa uwongo Dagoni na imani ya Atargatis (sawa na maoni yaliyo kwenye jarida la Daudi na Goliathi (Na. 126 [David and Goliath (No. 126) ibid)].

 

Daudi akiwa kama mwakilishi wa ufalme mpya na kiongozi wa nyumba mpya, alitakiwa kwa imani na utaratibu wa zamani za agano la kale kuwatahiri Wamataifa.

 

Hapa Daudi aliambiwa kuleta govi mia moja. Yeye akaleta mia mbili, au mara mbili ya zile alizotakiwa kuzileta ili apate mke kutoka kwenye familia ya kifalme. Alichaguliwa na kupewa upako na kisha akaruzukiwa kumchumbia mwanamke aliyekuwa wa damu ya familia ya kifalme. Kwa namna zake mwenyewe zilizoonyeshwa kwenye maandiko ya Zekaria 12:8 na kuchaguliwa kwa nyumba ya Daudi kama elohimu. Imeandikwa: Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia. (Zaburi 82:6; Yohana 10:34-35). Mikali (SHD 4324) ni neno lenye maana ya kijito au mto mdogo lililochukuliwa kutoka kwenye kamusi ya SHD 4323 linamaana ya kontaina na kwa hiyo ni kama kijimto kidogo au matatizo. Kwa namna nyingine twaweza kusema kuwa limetokana na neno yakawl (SHD 3201), ambalo linamaana ya kushinda au kumudu kujipatia.

 

Sauli alitafuta jinsi ya kumuua Daudi lakini Daudi alipata upendeleo machoni mwa Yonathani na ingawa Daudi alikuwa jasiri na matatizo kwenye ufalme, Yonathani alimpigania kumuokoa Daudi.

1Samweli 19:1-24 Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi. 2 Lakini huyo Yonathani, mwana wake Sauli, alikuwa akipendezwa sana na Daudi. Basi Yonathani akamwambia Daudi, akasema, Sauli, baba yangu, anatafuta kukuua; basi, nakusihi, ujiangalie sana asubuhi, ukae mahali pa siri na kujificha; 3 na mimi nitatoka nje na kusimama kando ya babangu huko shambani ulipo wewe, nami nitazungumza na babangu habari zako; nami nikiona neno lo lote nitakuambia. 4 Naye Yonathani akamsifu Daudi kwa Sauli, babaye akamwambia, Mfalme asikose juu ya mtumishi wake, yaani, juu ya Daudi kwa maana yeye hakukosa juu yako, tena matendo yake kwako yamekuwa mema sana. 5 Kwa kuwa alitia uhai wake mkononi mwake, na kumpiga yule Mfilisti, naye Bwana akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure? 6 Sauli akaisikiliza sauti ya Yonathani; naye Sauli akaapa, Aishivyo Bwana, yeye hatauawa. 7 Basi Yonathani akamwita Daudi, naye Yonathani akamjulisha mambo hayo yote. Kisha Yonathani akamleta Daudi kwa Sauli, naye alikuwa akihudhuria mbele yake, kama kwanza.

Kitendo hiki cha kumuokoa Daudi kilifantika na kufanikiwa kwa mema na hatimaye Daudi akashirikiana Sauli kupigana na Wafilisti. Sauli alipata tabu pia akisumbuliwa na mapepo, na kwenye andiko hili tunaambiwa kuwa tunashughulika ma maroho ambayo bado yalikuwa yanajitokeza kwenye vikao vinayofanyika kwenye Kiti cha Enzi cha Mungu na kujifanya kazi kwa mamlaka. Hii ni masalia ya viumbe au uumbaji wa awamu ya kwanza ya uumbaji kwenye yubile arobaini za tangu Adamu hadi Ibrahimu na kupitia tukio la gharika kuu ya wakati wa Nuhu.

8 Baada ya hayo kulikuwa na vita tena; naye Daudi akatoka, naye akapigana na Wafilisti, naye akawaua kwa uuaji mkuu; nao wakakimbia mbele yake. 9 Tena ikawa, roho mbaya kutoka kwa Bwana ilimjilia Sauli, hapo alipoketi ndani ya nyumba yake, akiwa na mkuki wake mkononi mwake; naye Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake. 10 Sauli akajaribu kumpiga Daudi hata ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule. 11 Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa. 12 Basi Mikali akamtelemsha Daudi dirishani; naye akaenda akakimbia na kuokoka. 13 Ndipo Mikali akakitwaa kinyago, na kukilaza kitandani, akatia na mto wa singa za mbuzi kichwani pake, na kukifunika kwa nguo. 14 Naye Sauli alipotuma wajumbe ili kumkamata Daudi, yeye alisema, Hawezi. 15 Basi Sauli akawatuma hao wajumbe ili wamtazame Daudi, akisema, Mleteni kwangu juu ya kitanda chake, nipate kumwua. 16 Nao wajumbe walipoingia, kumbe! Kuna kinyago kitandani, na mto wa singa za mbuzi kichwani pake! 17 Sauli akamwambia Mikali, Mbona wewe umenidanganya hivi, na kumwacha adui yangu aende, hata ameniponyoka? Naye Mikali akamjibu Sauli, Yeye aliniambia, Niache niende zangu; kwa nini nikuue? 18 Hivyo Daudi akakimbia, akajiponya, akamwendea Samweli huko Rama, akamwambia hayo yote Sauli aliyomtenda. Kisha yeye na Samweli wakaenda na kukaa katika Nayothi. 19 Naye Sauli akaambiwa, kusema, Angalia, yule Daudi yuko katika Nayothi, huko Rama. 20 Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, roho ya Mungu ikawajilia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri. 21 Naye Sauli alipoambiwa, alituma wajumbe wengine, wao nao wakatabiri. Naye Sauli akatuma wajumbe tena mara ya tatu, na wao pia wakatabiri. 22 Kisha yeye mwenyewe akaenda Rama, akafika kunako kile kisima kikubwa kilicho huko Seku; akauliza, akasema, Je! Wako wapi Samweli na Daudi? Na mtu mmoja akajibu, Tazama, wako Nayothi, huko Rama. 23 Basi akaenda Nayothi huko Rama, na roho ya Mungu ikamjilia yeye naye, akaendelea mbele, huku anatabiri, mpaka kufika Nayothi huko Rama. 24 Naye akavua nguo zake, akatabiri mbele ya Samweli, akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha siku ile. Kwa hiyo watu husema, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?

Roho Mtakatifu anaonyesha na kuelekeza kinachotaka kutokea. Iliendelea hadi kwenye matumizi ya kila kilichohusika, hata kwa Sauli, na pia kwa manabii, na kwa wote wawili, yaani Daudi na Sauli walijazwa kwa Roho ya Unabii na wakatabiri.

 

Kwa sababu hii Daudi asingeweza kuuinua mkono wake dhidi ya Mtiwa Mafuta wa Bwana. Kwanza alifadhaishwanna kushangazwa.

1Samweli 20:1-42 Kisha Daudi akatoka Nayothi huko Rama, akakimbia, akaenda kwa Yonathani, akasema mbele yake, Nimefanya nini? Uovu wangu ni nini? Dhambi yangu mbele ya baba yako ni nini, hata akaitaka roho yangu? 2 Naye akamwambia, Hasha! Hutakufa; angalia, baba yangu hatendi neno kubwa wala dogo bila kuifunulia mimi, na baba yangu ana sababu gani ya kunificha jambo hili? Sivyo usemavyo. 3 Daudi akaapa, akasema, Baba yako anajua sana ya kuwa nimeona kibali machoni pako, naye asema, Yonathani asilijue neno hili, asije akahuzunika; lakini ni kweli, aishivyo Bwana, na iishivyo roho yako, iko hatua moja tu kati ya mimi na mauti. 4 Ndipo Yonathani akamwambia Daudi, Kadiri roho yako itakavyo, nitakutendea. 5 Naye Daudi akamwambia Yonathani, Tazama, kesho ni mwandamo wa mwezi, nami hainipasi kukosa kuketi chakulani pamoja na mfalme; lakini niache nijifiche bondeni hata siku ya tatu jioni. 6 Baba yako akiona ya kuwa sipo basi sema, Daudi alitaka sana nimpe ruhusa, aende upesi Bethlehemu, mji wake, kwa maana iko huko dhabihu ya mwaka kwa ajili ya jamaa yake yote. 7 Basi, akisema, Ni vema, mimi mtumishi wako nitakuwa na amani; bali akikasirika, ujue ya kuwa amekusudia kutenda jambo baya. 8 Basi, unitendee mema mimi mtumishi wako; kwa sababu umenitia mimi mtumishi wako katika agano la Bwana pamoja nawe, lakini ikiwa mna uovu moyoni mwangu, uniue wewe mwenyewe; kwa nini kunileta kwa baba yako? 9 Naye Yonathani akasema, Haya na yawe mbali nawe, kwa maana kama ningejua ya kuwa baba yangu amekusudia kukutenda neno baya, je! Singekuambia? 10 Basi Daudi akamwambia Yonathani, Ni nani atakayeniambia, ikiwa baba yako amekujibu maneno makali? 11 Yonathani akamwambia Daudi, Twende zetu nje mashambani. Wakatoka wote wawili, wakaenda mashambani. 12 Naye Yonathani akamwambia Daudi, Bwana, Mungu wa Israeli, na awe shahidi; nitakapokuwa nimekwisha kumwuliza baba yangu, kama wakati huu kesho, au siku ya tatu, angalia, kama liko neno jema la kumfaa Daudi, je! Nisikupelekee habari na kukufunulia neno hili? 13 Bwana anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukupeleka uende zako kwa amani; na Bwana awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu. 14 Nawe utanionyesha fadhili za Bwana, ili nisife, si wakati huu tu maadamu mimi ni hai; 15 lakini pamoja na hayo, hata jamaa yangu pia hutawaondolea kabisa fadhili zako; la, hata wakati ule Bwana atakapokuwa amewaondoa kabisa adui za Daudi wote pia katika uso wa nchi. 16 Basi Yonathani akafanya agano na jamaa yake Daudi, akisema, Bwana naye atayataka mkononi mwa adui zake Daudi. 17 Naye Yonathani akamwapisha Daudi mara ya pili, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake; kwa maana alimpenda kama alivyoipenda roho yake mwenyewe.

Jakamoyo na uadui na migngano ililjitokeza kwenye Nyumba za Kifalme katika Israeli hayakuwa ya lazima na ni kama wote wangekuwa kama Daudi na Yonathani tungekuwa na amani. Na hasa kwenye Makanisa ya Mungu yangekuwa na amani.

 

Kwenye awamu iliyofuatia tunaona pia utendaji kazi wa kalenda na ikitumika mnamo takriban mwaka 1000 KK (sawa na majarida ya Kalenda ya Mungu (Na. 156) na Mwezi na Mwaka Mpya (Na. 213) [God’s Calendar (No. 156) and The Moon and the New Year (No. 213)].

18 Kisha Yonathani akamwambia, Kesho ni mwandamo wa mwezi, nawe utakosekana, kwa sababu kiti chako kitakuwa hakina mtu. 19 Nawe ukiisha kungoja siku tatu, shuka upesi ufike kuko huko ulikojificha, siku ya shughuli ile; nawe kaa karibu na kile kichuguu kule. 20 Nami nitapiga mishale mitatu kando-kando yake, kana kwamba ninapiga shabaha. 21 Kisha, angalia, nitamtuma mtoto na kumwambia, Nenda ukaitafute mishale. Hapo nikimwambia yule mtoto, Tazama, mishale iko upande wako huu, itwae; basi uje, maana iko amani kwako, wala hapana hatari, Bwana aishivyo. 22 Bali nikimwambia yule mtoto, Tazama, mishale iko huko mbele yako; basi enenda zako, kwa maana Bwana amekuamuru uende zako. 23 Na kwa habari ya neno lile tulilonena, wewe na mimi, angalia Bwana yu kati ya wewe na mimi milele. 24 Basi Daudi akajificha shambani; na mwezi ulipoandama, mfalme aliketi kula chakula. 25 Mfalme aliketi kitini mwake kama sikuzote, katika kiti kilichokuwa karibu na ukuta; Yonathani alikuwa mbele yake; Abneri naye akaketi karibu na Sauli; lakini mahali pake Daudi palikuwa hapana mtu. 26 Lakini Sauli hakusema neno siku ile; maana alidhani ya kuwa, Amepatikana na neno, hakutakata; hakosi yeye hakutakata. 27 Hata siku ya pili baada ya mwandamo wa mwezi, mahali pake palikuwa hapana mtu; basi Sauli akamwambia Yonathani mwanawe, Mbona mwana wa Yese haji kula chakula, jana wala leo? 28 Naye Yonathani akamjibu Sauli, Daudi alitaka sana nimpe ruhusa aende Bethlehemu; 29 akasema, Tafadhali nipe ruhusa niende; kwa maana jamaa yetu wana dhabihu mjini mwetu; na ndugu yangu ameniamuru niende; basi sasa, kama nimeona kibali machoni pako, nakuomba, niondoke; nikawatazame ndugu zangu. Ndiyo sababu hakuja mezani pa mfalme. 30 Basi hasira yake Sauli ikawaka juu ya Yonathani, akamwambia, Wewe, mwana wa mke mkaidi, asi, je! Mimi sijui ya kuwa umemchagua huyo mwana wa Yese, kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako. 31 Maana wakati mwana wa Yese akiwa hai juu ya nchi, wewe hutafanikiwa, wala ufalme wako. Basi, sasa peleka, ukamlete kwangu, maana hakika yake atakufa huyu. 32 Yonathani akamjibu Sauli, baba yake, akamwambia, Auawe kwa sababu gani? Amefanya nini? 33 Sauli akamtupia mkuki wake ili kumpiga; basi Yonathani akajua ya kuwa baba yake ameazimu kumwua Daudi. 34 Basi Yonathani akaondoka pale mezani, mwenye hasira kali, wala hakula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi sana, na kwa sababu baba yake amemwaibisha. 35 Hata asubuhi Yonathani akatoka kwenda shambani wakati ule alioagana na Daudi, na mtoto mdogo alikuwa pamoja naye. 36 Akamwambia mtoto wake, Piga mbio, ukaitafute mishale niipigayo. Na yule mtoto alipokuwa akipiga mbio, akapiga mshale, ukapita juu yake. 37 Na mtoto alipofika penye ule mshale alioupiga Yonathani, Yonathani akampigia mtoto kelele, akasema, Je! Mshale si huko mbele yako? 38 Yonathani akampigia mtoto kelele, Haya! Hima! Usikawie. Mtoto wa Yonathani akaikusanya mishale, akaenda kwa bwana wake. 39 Lakini yule mtoto hakujua lo lote. Yonathani na Daudi ndio walioijua habari yenyewe. 40 Naye Yonathani akampa mtoto silaha zake, akamwambia, Nenda, ukazichukue mjini. 41 Basi mara alipokuwa amekwisha ondoka yule mtoto, mara Daudi akatoka mahali pale karibu na kile kichuguu, akaanguka kifudifudi, akajiinama mara tatu; nao wakabusiana, wakaliliana, hata Daudi akazidi. 42 Naye Yonathani akamwambia Daudi, Enenda kwa amani; kwa maana sisi sote wawili tumeapiana kwa jina la Bwana ya kwamba, Bwana atakuwa kati ya mimi na wewe, na kati ya uzao wangu na uzao wako milele. Daudi akaondoka, akaenda zake; Yonathani naye akaenda zake mjini.

 

Agano na patano hili lilipaswa lidumu na kuheshimiwa na Daudi.

 

Kuula Mkate wa Wonyesho

1Samweli 21:1-6 Basi Daudi akaenda Nobu kwa Ahimeleki, kuhani. Ahimeleki akaenda kumlaki Daudi, akitetemeka, akamwambia, Kwani wewe kuwa peke yako, wala hapana mtu pamoja nawe? 2 Daudi akamwambia Ahimeleki, kuhani, Mfalme ameniagiza shughuli, akaniambia, Asijue mtu awaye yote habari ya shughuli hii ninayokutuma, wala ya neno hili ninalokuamuru; nami nimewaagiza vijana waende mahali fulani. 3 Kuna nini basi, chini ya mkono wako? Nipe mkononi mwangu mikate mitano, au cho chote ulicho nacho hapa. 4 Yule kuhani akamjibu Daudi, akasema, Hapana mikate ya sikuzote chini ya mkono wangu, ila mikate mitakatifu; ikiwa wale vijana wamejitenga na wanawake. 5 Naye Daudi akamjibu kuhani, akamwambia, Hakika tumejitenga na wanawake siku hizi tatu; napo nilipotoka, vyombo vya vijana hawa vilikuwa vitakatifu, ingawa ilikuwa safari ya sikuzote; basi leo je! Vyombo vyetu havitakuwa vitakatifu zaidi? 6 Ndipo kuhani akampa ile mikate mitakatifu; kwa maana hapakuwa na mikate ila ile ya Wonyesho, nayo imekwisha kuondolewa mbele za Bwana, ili itiwe mikate ya moto siku ile ilipoondolewa.

Haikuruhusiwa na Torati kwa Daudi kuula Mkate wa Wonyesho, lakini ulitolewa na kupewa yeye na watu wake kwa kuwa uliashiria pia kuchaguliwa kwa nyumba yote ya Daudi kwenye Kanisa na kufanyika kuwa elohim (Zekaria 12:8; Zaburi 82:6).

 

Upanga wa Goliathi

Tunaona hapa pia silaha ya adui yake zikitolewa na kukabidhiwa yeye ili kuiendeleza kazi ya Waisraeli. Hii ilimhusu pia Daudi kujifanya kama anawazimu alipokuwa katikati ya Wafilisti.

 

1Samweli 21:7-15 Basi siku ile palikuwapo na mtu mmoja wa watumishi wa Sauli, amezuiwa hapo mbele za Bwana jina lake akiitwa Doegi, Mwedomi, mkubwa wa wachungaji wa Sauli. 8 Tena Daudi akamwambia Ahimeleki, Na hapa chini ya mkono wako, je! Hapana mkuki, au upanga? Kwa maana sikuleta upanga, wala silaha zangu, kwa sababu ile shughuli ya mfalme ilitaka haraka. 9 Yule kuhani akasema, upanga wa Goliathi, yule Mfilisti, uliyemwua katika bonde la Ela, tazama, upo hapa, umefungwa ndani ya nguo nyuma ya naivera; ukipenda kuuchukua, haya! Uchukue, maana hapa hapana mwingine ila huo tu. Daudi akasema, Hapana mwingine kama ule; haya! Nipe. 10 Basi Daudi akaondoka, akakimbia siku ile, kwa hofu ya Sauli, akamwendea Akishi, mfalme wa Gathi. 11 Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, Je! Huyu siye yule Daudi, mfalme wa nchi? Je! Hawakuimbiana habari zake katika ngoma zao, kusema,Sauli amewaua elfu zake,Na Daudi makumi elfu yake. 12 Naye Daudi akayatia maneno hayo moyoni mwake, akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi. 13 Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye wazimu mikononi mwao, akakuna-kuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake. 14 Ndipo huyo Akishi akawaambia watumishi wake, Angalieni, mwaona ya kuwa mtu huyu ana wazimu; basi, maana yake nini kumleta kwangu? 15 Je! Mimi nina haja ya watu wenye wazimu, hata mmemleta kiumbe hiki ili aonyeshe wazimu wake machoni pangu? Je! Huyu ataingia nyumbani mwangu?

 

Hatimaye alionekana kuwa sio tishio kwao na ndipo aliachiwa hai na ndipo alipotoroka. Kwenye tofauti ya machoni mwa Daudi ilikuwa ni sehemu nzuri ya kupata silaha na ala kwa wakati huu. Cha kwanza kufanya kilikuwa ni kuilinda familia yake dhidi ya mfalme wa Wamoabu. Huu ulikuwa ni mpangilio rahisi kwa kuwa iliwafanya Wamoabu wampende Daudi kama angeshinda. Daudi alikuwa amekusanya kila kadhia na wanaodai madeni kwenye taifa ambalo lingechukua upanga. Sauli aliogopa sana hil na alijua kwamba hata mwanae mwenyewe hakukubaliana na mapatano ya Daudi. Kwa hiyo Sauli aliogopa sana.

1Samweli 22:1-23 Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. 2 Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walipata kama watu mia nne. 3 Kutoka huko Daudi akaenda Mispa ya Moabu; akamwambia mfalme wa Moabu, Tafadhali ukubali baba yangu na mama yangu watoke huko waliko, wakakae kwenu, hata nitakapojua Mungu atakalotenda kwa ajili yangu. 4 Akawaleta mbele ya mfalme wa Moabu, nao wakakaa pamoja naye wakati wote Daudi alipokuwa ngomeni. 5 Kisha nabii Gadi akamwambia Daudi, Usikae hapa ngomeni; ondoka, ukaende mpaka nchi ya Yuda. Ndipo Daudi akaondoka, akaenda zake, akakaa katika msitu wa Herethi. 6 Kisha Sauli akasikia ya kwamba Daudi ameonekana, na wale watu waliokuwa pamoja naye. Basi Sauli alikuwa akikaa Gibea, chini ya mkwaju katika mahali palipoinuka, naye alikuwa na mkuki wake mkononi, na watumishi wake wote wakimzunguka. 7 Naye Sauli akawaambia watumishi wake waliomzunguka, Sikieni sasa, enyi Wabenyamini; je! Huyu mwana wa Yese atawapa ninyi kila mmoja mashamba, na mashamba ya mizabibu, atawafanya kuwa maakida wa watu elfu, na maakida wa watu mia; 8 hata ninyi nyote mkafanya fitina juu yangu, wala hapana mtu anifunuliaye habari hii mwanangu afanyapo agano na mwana wa Yese, wala hapana mmoja wenu anayenisikitikia, wala kunifunulia ya kuwa mwanangu amemwondokesha mtumishi wangu juu yangu, anivizie kama hivi leo?

Kwa ajili hii pia Doegi, Muedomu (tunamuita Doug siku hizi) aliona namna ya kujitanua na kuongezeka. Alikaa kwa mtumishi wa Sauli. Hatimaye Waedomu wangemudu kuishi ndani ya nyumba yote ya Yuda na kumudu kuvuruga mpangilio na mkakati wao waliojiwekea kwa ajili ya pande za nchi ya kusini mwa Yudea wakati wa Kristo. Kwa hiyo makuhani wakaadhibiwa kwa kumsaidia Daudi.

9 Ndipo akajibu Doegi, Mwedomi, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akasema, Mimi nalimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu. 10 Naye akamwuliza Bwana kwa ajili yake, akampa vyakula, akampa na ule upanga wa Goliathi, Mfilisti. 11 Ndipo mfalme akatuma watu waende kumwita Ahimeleki, kuhani, mwana wa Ahitubu, na jamaa yote ya baba yake, hao makuhani, waliokuwako huko Nobu; nao wakaenda kwa mfalme wote pia. 12 Sauli akasema, Sikia sasa, Ewe mwana wa Ahitubu. Naye akaitika, Mimi hapa, bwana wangu. 13 Sauli akamwuliza, Mbona mmefanya fitina juu yangu, wewe na mwana wa Yese? Kwa maana umempa mikate, na upanga, nawe umemwuliza Mungu kwa ajili yake, ili aniondokee na kunivizia kama hivi leo? 14 Basi Ahimeleki akamjibu mfalme, akasema, Katika watumishi wako wote ni nani aliye mwaminifu kama Daudi, aliye mkwewe mfalme, tena msiri wako, mwenye heshima nyumbani mwako? 15 Je! Mimi nimeanza leo tu kumwuliza Mungu kwa ajili yake? Hasha! Mfalme asinidhanie mimi, mtumishi wake neno hili, Wala jamaa yote ya baba yangu, kwa maana mimi, mtumishi wako siyajui hayo yote, yaliyopungua au yaliyozidi. 16 Naye mfalme akasema, Kufa utakufa, Ahimeleki, wewe na jamaa yote ya baba yako. 17 Kisha mfalme akawaambia askari walinzi waliosimama karibu naye Geukeni, mkawaue hao makuhani wa Bwana, kwa sababu mkono wao u pamoja na Daudi, na kwa sababu walijua ya kuwa amekimbia, wasiniarifu. Lakini watumishi wa mfalme walikataa kunyosha mkono na kuwaangukia makuhani wa Bwana. 18 Basi mfalme akamwambia Doegi, Geuka wewe, ukawaangukia hao makuhani. Basi Doegi, Mwedomi, akageuka, akawaangukia makuhani, akaua siku ile watu themanini na watano wenye kuvaa naivera ya kitani. 19 Kisha akaupiga Nobu, mji wa makuhani, kwa makali ya upanga, wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, na ng'ombe, na punda, na kondoo. 20 Na katika wana wa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu, akaokoka mtu mmoja tu, aliyeitwa jina lake Abiathari, akamkimbilia Daudi. 21 Naye Abiathari akamweleza Daudi ya kwamba Sauli amewaua makuhani wa Bwana. 22 Daudi akamwambia Abiathari, Siku ile alipokuwako Doegi, Mwedomi, nalijua yakini ya kuwa atamwambia Sauli; mimi nimewapatia watu wote wa jamaa ya baba yako kifo. 23 Kaa wewe pamoja nami, usiogope; kwa maana yeye atafutaye roho yangu, ndiye atafutaye na roho yako; nawe utakaa kwangu salama.

Ndipo makuhani wakaungana na Daudi kwa faida binafsi za Muedomu.

 

Daudi kama chombo cha Mungu

Daudi alikuwa ni mtu anayejali na makini kujua kuwa alikuwa ametiwa mafuta na kutengwa rasmi kwa kusudi la kuwa mfalme hatimaye. Na ilikuwa kwa ajili hiyo ndipo shujaa huyu wa Israeli na kazi iliyokuwako ndani yake kuitenda ilikuwa ni kulilinda taifa hili.

1Samweli 23:1-29 Kisha wakamwambia Daudi, kusema, Angalia, Wafilisti wanapigana vita juu ya Keila na kuiba nafaka sakafuni mwa kupuria. 2 Basi Daudi akamwuliza Bwana, kusema, Je! Niende nikawapige hao Wafilisti? Naye Bwana akamwambia Daudi, Nenda ukawapige Wafilisti, na kuuokoa Keila. 3 Ila watu wake Daudi wakamwambia, Tazama, sisi tunaogopa hapa katika Yuda; je! Si zaidi tukienda Keila juu ya majeshi ya Wafilisti?

Woga wa kabila la Daudi mwenyewe ulionekana wazi pia. Hii ilimfanya Daudi kuyaonea shaka maelekezo aliyopewa mwanzoni na Bwana.

4 Basi Daudi akamwuliza Bwana tena, Naye Bwana akamjibu, akasema, Ondoka, ukashukie Keila; kwa kuwa nitawatia hao Wafilisti mikononi mwako. 5 Ndipo wakaenda Keila, Daudi na watu wake, wakapigana na hao Wafilisti, wakateka nyara ng'ombe zao, na kuwaua uuaji mkuu. Hivyo Daudi akawaokoa watu wa Keila. 6 Ikawa Abiathari, mwana wa Ahimeleki, alipomkimbilia Daudi huko Keila, alishuka na naivera mkononi mwake. 7 Kisha Sauli aliambiwa ya kwamba Daudi amefika Keila. Sauli akasema, Mungu amemtia mkononi mwangu; kwa maana amefungwa ndani, kwa vile alivyoingia katika mji wenye malango na makomeo. 8 Basi Sauli akawaita watu wote waende vitani, ili waishukie Keila, na kumhusuru Daudi na watu wake. 9 Naye Daudi alifahamu ya kuwa Sauli amemkusudia mabaya; akamwambia Abiathari, kuhani, Lete hapa hiyo naivera. 10 Ndipo Daudi akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, mimi mtumwa wako nimesikia hakika ya kuwa Sauli anataka kuja huku Keila, ili kuuharibu mji kwa ajili yangu. 11 Je! Watu wa Keila watanitoa, nitiwe mkononi mwake? Je! Sauli atashuka, kama mtumwa wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumwa wako. Naye Bwana akamjibu, Atashuka. 12 Ndipo Daudi akasema, Je! Watu wa Keila watanitia mimi na watu wangu mkononi mwake Sauli? Bwana akasema, Watakutia. 13 Basi Daudi na watu wake, ambao wapata kama mia sita, wakaondoka na kutoka Keila, wakaenda po pote walipoweza kwenda. Kisha Sauli akaambiwa ya kwamba Daudi amekimbia toka Keila; akaacha kutoka nje. 14 Basi Daudi alikuwa akikaa nyikani ngomeni, akakaa katika nchi ya milima milima kwenye nyika ya Zifu. Naye Sauli alikuwa akimtafuta kila siku, lakini Mungu hakumtia mikononi mwake. 15 Daudi akaona ya kwamba Sauli ametoka nje ili kutafuta roho yake; naye Daudi akawako katika nyika ya Zifu, huko Horeshi. 16 Ndipo Yonathani, mwana wa Sauli, akainuka akamwendea Daudi huko Horeshi, akamtia nguvu mkono wake katika Mungu. 17 Akamwambia, Usiogope, kwa maana mkono wa Sauli, babangu, hautakupata; na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli; na mimi nitakuwa wa pili wako; ndivyo ajuavyo hata Sauli, babangu. 18 Na hao wawili wakafanya agano mbele za Bwana; Daudi naye akakaa huko Horeshi, na Yonathani akaenda nyumbani kwake. 19 Ndipo wale Wazifi wakakwea kwa Sauli huko Gibea, wakasema, Je! Yule Daudi hakujificha kwetu ngomeni mwa Horeshi, kilimani pa Hakila upande wa kusini wa Yeshimoni? 20 Basi sasa, Ee mfalme, ushuke, kama utakavyo nafsini mwako kushuka; na kazi yetu itakuwa kumtia mkononi mwa mfalme. 21 Naye Sauli akasema, Na mbarikiwe ninyi na Bwana; kwa sababu mmenihurumia. 22 Nendeni, nawasihi, mkazidi kupata hakika, mkajue na kuona mahali pake anapojificha, tena ni nani aliyemwona huko; maana nimeambiwa ya kwamba atenda kwa hila nyingi. 23 Chunguzeni basi, mkayajue maficho yake yote anapojificha; kisha njoni kwangu, tena msikose, nami nitakwenda pamoja nanyi; tena itakuwa, akiwapo katika nchi, mimi nitamtafuta-tafuta katika elfu zote za Yuda. 24 Nao wakaondoka, wakaenda Zifu kumtangulia Sauli; lakini Daudi na watu wake walikuwapo nyikani pa Maoni, katika Araba upande wa kusini wa jangwa. 25 Basi Sauli na watu wake wakaenda kumtafuta. Watu wakamwambia Daudi; basi kwa hiyo akashuka mpaka mwambani, akakaa nyikani pa Maoni. Naye Sauli alipopata habari, alimwinda Daudi nyikani pa Maoni. 26 Sauli akaenda upande huu wa mlima, na Daudi na watu wake wakaenda upande huu wa mlima; naye Daudi akafanya haraka sana kwenda zake kwa hofu ya Sauli; kwa sababu Sauli na watu wake wakamzunguka Daudi na watu wake ili kuwakamata. 27 Lakini akaja mjumbe kwa Sauli, kusema, Njoo upesi, kwa kuwa Wafilisti wameishambulia nchi. 28 Basi Sauli akarudi kutoka kumwinda Daudi, akaenda kinyume cha Wafilisti; kwa hiyo wakapaita mahali pale, Selahamalekothi. 29 Naye Daudi akakwea kutoka huko, akakaa katika ngome ya Engedi.

Sauli alikuwa ameguswa na kuumizwa sana na kuuliwa kwa mjukuu wake kuliko usalama wa Israeli.

 

Ilikuwa ni Sauli ndiye alipaswa kuwandea kupigana na Wafilisti na haikupaswa jukumu hili aachiwe Daudi. Mji huu ulipaswa unamshukuru sana Daudi. Lakini kinyume chake walimkabidhi Daudi kwa Sauli. Ni nguvu za kiasi gani na kujitoa kwa Mungu kungekuwaje na sifa kwa ufalme ingekuwa iwapo kama Sauli angemtii tu Mungu.

 

Sauli na Daudi huko Engedi

1Samweli 24:1-22 Ikawa, Sauli aliporudi baada ya kuwafuatia Wafilisti, aliambiwa ya kwamba, Daudi yuko katika nyika ya Engedi. 2 Ndipo Sauli akatwaa watu elfu waliochaguliwa katika Israeli wote, akaenda kumtafuta Daudi na watu wake juu ya majabali ya mbuzi-mwitu. 3 Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, na huko kulikuwa na pango; Sauli akaingia ndani ili kuifunika miguu. Na Daudi na watu wake walikuwa wakikaa mle pangoni ndani sana. 4 Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia Bwana, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yo yote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri. 5 Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli. 6 Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA,neon hili,kuunyosha mkono wangu juu yake,kwa maana yeye ni masihi wa BWANA. 7 Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaache kumwondokea Sauli. Kisha Sauli akatoka pangoni, akaenda zake. 8 Daudi naye akainuka baadaye, akatoka pangoni, akamwita Sauli, akisema, Bwana wangu, mfalme. Na Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama uso wake hata nchi, akamsujudia. 9 Daudi akamwambia Sauli, Kwa nini unasikiliza maneno ya watu wasemao, Tazama, Daudi anataka kukudhuru? 10 Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi Bwana alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA. 11 Tena, baba yangu, tazama, tafadhali, tazama upindo wa vazi lako mkononi mwangu; maana ikiwa nimeukata upindo wa vazi lako, nisikuue, ujue, na kuona ya kuwa hakuna uovu wala kosa mkononi mwangu, wala sikukukosa neno; ingawa wewe unaniwinda roho yangu ili kuikamata. 12 Bwana atuamue, mimi na wewe, na Bwana anilipizie kisasi changu kwako; lakini mkono wangu hautakuwa juu yako. 13 Kama vile walivyosema watu wa kale katika mithali yao, Katika waovu hutoka uovu; ila mkono wangu hautakuwa juu yako. 14 Na mfalme wa Israeli ametoka ili kumfuatia nani? Unamwinda nani? Ni kuwinda mbwa mfu, au kiroboto. 15 Basi Bwana atuamue, akatuhukumu mimi na wewe, akaone, akanitetee neno langu, akaniokoe na mkono wako. 16 Ikawa, Daudi alipokwisha kumwambia Sauli maneno hayo Sauli alisema, Hii ndiyo sauti yako, Daudi, mwanangu? Naye Sauli akapaza sauti yake, akalia. 17 Akamwambia Daudi, Wewe u mwenye haki kuliko mimi; maana wewe umenitendea mema, nami nimekutenda mabaya. 18 Nawe umeonyesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani Bwana aliponitia mikononi mwako, hukuniua. 19 Maana mtu akimwona adui yake, je! Atamwacha aende zake salama? Basi Bwana na akulipe mema kwa haya uliyonitendea leo. 20 Na sasa, angalia, najua ya kuwa hakika utakuwa mfalme, na ufalme wa Israeli utafanyika imara mkononi mwako. 21 Basi sasa, uniapie kwa Bwana, ya kwamba hutawakatilia mbali wazao wangu baada yangu, wala hutaliharibu jina langu katika mbari ya baba yangu. 22 Naye Daudi akamwapia Sauli. Kisha Sauli akaenda zake kwao; lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.

Sauli aliguswa sana na haki na roho njema aliyokuwanayo Daudi na alijua kuwa Mungu alimfanya aangukie mikononi mwa Daudi. Kukilinda kizazi cha Sauli pia lilikuwa ni jambo muhimu sana na Daudi alikuwa anamlinda mmoja wa watu wa nyumba ya Sauli wakati alipofanyika kuwa mfalme.

 

Kifo cha Samweli na Nabali

1Samweli 25:1-44 Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. 2 Na huko Maoni kulikuwa na mtu mmoja, ambaye alikuwa na mali yake katika Karmeli; naye yule mtu alikuwa mkuu sana, mwenye kondoo elfu tatu na mbuzi elfu; naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo zake huko Karmeli. 3 Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso; bali yule mwanamume alikuwa hana adabu, tena mwovu katika matendo yake; naye alikuwa wa mbari ya Kalebu. 4 Basi Daudi akasikia huko nyikani ya kuwa Nabali alikuwa katika kuwakata manyoya kondoo zake. 5 Daudi akatuma vijana kumi, Daudi naye akawaambia hao vijana, Kweeni mwende Karmeli, na kumwendea huyu Nabali ili mnisalimie; 6 na hivi ndivyo mtakavyomwambia huyu aishiye salama, Amani na iwe kwako, na amani nyumbani mwako, na amani kwao wote ulio nao. 7 Nami sasa nimesikia ya kuwa una watu wanaokata manyoya kondoo zako; haya! Wachungaji wako wamekuwa pamoja nasi, wala hatukuwadhuru, wala hawakukosa kitu wakati wote walipokuwako huko Karmeli. 8 Waulize vijana wako, nao watakuambia; basi na wakubaliwe vijana hawa machoni pako; maana tumekujia katika siku ya heri; uwape, nakusihi, cho chote kitakachokujia mkononi, uwape watumwa wako na mwanao Daudi. 9 Basi walipofika vijana wake Daudi, wakamwambia Nabali sawasawa na maneno hayo yote kwa jina la Daudi, kisha wakanyamaza. 10 Naye Nabali akawajibu wale watumishi wa Daudi, akasema, Huyu Daudi ni nani? Na mwana wa Yese ni nani? Siku hizi kuna watumwa wengi wanaomtoroka kila mtu bwana wake! 11 Basi mimi je! Nitwae mkate wangu, na maji yangu, na machinjo yangu niliyowachinjia hao watu wangu wakatao manyoya kondoo zangu, na kuwapa watu ambao siwajui wametoka wapi? 12 Basi vijana wake Daudi wakageuka, wakaenda zao, wakarudi, nao wakaja wakamwambia sawasawa na maneno hayo yote. 13 Kisha Daudi akawaambia watu wake, Haya! Jifungeni kila mtu upanga wake. Nao wakajifunga kila mtu upanga wake; Daudi naye akajifunga upanga wake; nao wakapanda nyuma yake Daudi, wapata kama watu mia nne; na watu mia mbili wakakaa na vyombo vyao. 14 Lakini kijana mmojawapo alimpasha habari Abigaili, mkewe Nabali, kasema, Tazama, Daudi alituma wajumbe kutoka nyikani waje ili kumsalimu bwana wetu, naye akawatukana. 15 Walakini watu hawa walitutendea mema sana, wala hatukupata dhara, wala sisi hatukupotewa na kitu cho chote, wakati wote tulipofuatana nao, tulipokuwako mavueni; 16 watu hao walikuwa boma kwetu usiku na mchana, wakati wote tulipokuwa nao tukiwachunga kondoo. 17 Basi sasa ujue na kufikiri utakayotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya bwana wetu, na juu ya nyumba yake yote; kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi kusema naye. 18 Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliofanyizwa tayari, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda. 19 Akawaambia vijana wake, Haya! Tangulieni mbele yangu; angalieni, mimi nawafuata. Ila hakumwambia mumewe, Nabali. 20 Ikawa, alipokuwa amepanda punda wake, na kutelemka penye sitara ya mlima, tazama, Daudi na watu wake walikuwa wakishuka kumkabili; naye akawakuta. 21 Basi Daudi alikuwa amesema, Hakika ni bure nilivyokuwa nikilinda nyikani yote aliyo nayo mtu huyu, asipotewe na kitu cho chote cha mali yake yote; naye amenilipa mabaya badala ya mema. 22 Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi. 23 Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka nchi. 24 Akamwangukia miguuni pake, akasema, Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na uwe uovu; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize maneno ya mjakazi wako. 25 Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.

Nabali maana yake ni mpumbavu au muovu, mjinga au uovu. Kwa kweli ndivyo alivyokuwa, kama Daudi angewaua watumishi wake wote na kuchukua kondoo zake wote. Na ingawa hakuwa mtu wa shukurani kwa hilo bali aliwalinda watu wake badala yake.

26 Basi sasa, bwana wangu, aishivyo Bwana, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa Bwana amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali. 27 Na sasa zawadi hii, mjakazi wako aliyomletea bwana wangu, na wapewe vijana wamfuatao bwana wangu. 28 Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika Bwana atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya Bwana; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote. 29 Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na Bwana, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya teo. 30 Tena itakuwa, hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu sawasawa na mema yote aliyoyanena juu yako, na kukutawaza juu ya Israeli; 31 hili halitakuwa kwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako. 32 Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki; 33 na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe. 34 Kwa kuwa ni kweli, aishivyo Bwana, Mungu wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi. 35 Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso wako. 36 Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hata kulipopambazuka. 37 Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, mkewe alimwambia mambo hayo, na moyo wake ukafa ndani yake, akawa kama jiwe. 38 Tena ikawa, yapata siku kumi baadaye, Bwana alimpiga huyo Nabali, hata akafa. 39 Naye aliposikia ya kwamba Nabali amekufa, Daudi alisema, Na ahimidiwe Bwana ambaye amenitetea teto la shutumu langu mkononi mwa Nabali, na kumzuia mtumwa wake asitende maovu; tena uovu wake Nabali Bwana amemrudishia juu ya kichwa chake mwenyewe. Kisha Daudi akatuma watu, akamposa Abigaili ili amwoe. 40 Na hao watumishi wa Daudi walipomjia huyo Abigaili huko Karmeli, walimwambia, wakasema, Daudi ametutuma kwako ili tukutwae uwe mkewe. 41 Naye akainuka na kujiinamisha kifulifuli mpaka nchi, akasema, Tazama, mjakazi wako ni mtumwa wa kuwaosha miguu watumishi wa bwana wangu. 42 Abigaili akafanya haraka, akainuka, akapanda punda, pamoja na vijakazi watano wake waliofuatana naye, akawafuata hao wajumbe wa Daudi, akawa mkewe. 43 Tena Daudi akamwoa Ahinoamu wa Yezreeli; wakawa wote wawili wakeze. 44 Walakini Sauli alikuwa amempa Palti, mwana wa Laishi, aliyekuwa mtu wa Galimu, Mikali binti yake, aliyekuwa mkewe Daudi.

Daudi aliiona hekima ilyokuweko ndani mwa Abigaili na upumbavu wa Nabali. Nabali aliyajua makosa aliyoayafanya kwa kwamba Daudi alikuwa ameuelekeza uso wake dhidi yake lakini alifanya maovu tu na kisha akafa. Ngeweza kutoa pasipo kusikitika au kujutia, wala kukubaliana na adhabu ya Mungu kwa jambo lile. Alibakia kuwa hai kwa sababu ya kuingiaji kati uliofanywa na mke wake na ni yeye peke yake ndiye alimnusuru.  Hii ia ina maana yake kwa taifa ovu kuwa linaweza kulindwa na Kanisa ambalo ni mke wa mfale anayetarajiwa kuja na ambaye hajachukua kiti chake cha ufalme bado. Kanisa humuokoa mfalme mara nyingi hasa kutokana na mapenzi ya mume mkorofi aliyenaye anatarajia kufanyika kuwa mume wake wakati Masihi atakapoanza kutawala huk maovuo Yerusalemu. Israeli ni taifa maovu na ni bwana mdhaifu na muovu wakati alipokatiliwa mbali na Roho wa Mungu na Kanisa mara nyingi limekuwa likiteswa nalo.

 

Vinara vitano vinawakilisha makanisa au zama ambazo zimekubaliwa kuwa kwenye mwili wa Kristo pamoja na vingine viwili vya Wasardi na Walaodikia yaliyokataliwa na ni wachache sana na ni binafsi yao au mmoja mmoja kutoka kwenye makundi hayo watapata uwokovu.

 

Kwa mara nyingine tena Sauli alijaribu kuyachukua maisha ya Daudi. Hii tena ilikuwa kama tunavyoona wakati Kristo alipoweka Nyota ya Asubuhi, watu wa nyumbani mwake Masihi wamekuwa ni elohimu mahali pa watu walio nyumbani mwa Shetani. Ni kama Shetani alivyojaribu kuwaangamiza Watakatifu wake Kristo akiwa kama Amiri wa Jeshi la Bwana na akatupwa hapa duniani na kushindwa, na ndipo sasa alipojaribu kumuua Masihi na kuwaangamiza watu wa nyumbani mwake wote wakati alipozaliwa kimwili. Ndivyo ilivyotokea tena kama Israeli wanapoendela kushambuliwa kwa matukio yanayorudiwa rudiwa na watumishi wa Shetani lakini wamekuwa wakilindwa na Malaika kwa walio pamoja na Kristo.

1Samweli 26:1-25 Basi hao Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea, wakasema, Je! Yule Daudi hakujificha katika kilima cha Hakila, kuelekea Yeshimoni? 2 Basi Sauli akaondoka, akashuka nyikani kwa Zifu, naye alikuwa na watu elfu tatu, wateule wa Israeli, pamoja naye, ili kumtafuta Daudi katika nyika ya Zifu. 3 Naye Sauli akapiga hema katika kilima cha Hakila, kilichoelekea Yeshimoni, barabarani; lakini Daudi alikuwa akikaa nyikani, akaona ya kwamba Sauli amemfuata mpaka nyikani. 4 Basi Daudi akatuma wapelelezi, akapata habari ya hakika ya kwamba Sauli amefika. 5 Daudi akainuka, akafika mahali pale alipotua Sauli; Daudi akapaangalia mahali alipolala Sauli, na Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi lake; naye Sauli alikuwa amelala kati ya magari, na hao watu wamepiga hema zao wakimzunguka. 6 Ndipo Daudi akajibu, akamwambia Ahimeleki, Mhiti, na Abishai, mwana wa Seruya, ndugu yake Yoabu, akisema, Ni nani atakayeshuka pamoja nami kwa Sauli kambini? Abishai akasema, Mimi nitashuka pamoja nawe. 7 Basi Daudi na Abishai wakawaendea watu usiku; na tazama, Sauli alikuwapo kati ya magari amelala usingizi, na fumo lake limechomekwa chini, karibu na kichwa chake; naye Abneri na watu wake wamelala wakimzunguka. 8 Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hata nchi kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili. 9 Lakini Daudi akamwambia Abishai, Usimwangamize; kwani ni nani awezaye kuunyosha mkono wake juu ya masihi 10 Daudi akasema, Aishivyo Bwana, Bwana atampiga; au siku yake ya kufa itampata; atashuka kwenda vitani na kupotea. 11 Hasha! Nisiunyoshe mkono wangu juu ya masihi 12 Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia. 13 Kisha Daudi akaenda ng'ambo ya pili, akasimama juu ya kilima, mbali sana; palipokuwapo nafasi tele katikati yao; 14 naye Daudi akawapigia kelele watu wale, na Abneri, mwana wa Neri, akasema, Abneri, hujibu? Ndipo Abneri akajibu, akasema, U nani wewe unayemlilia mfalme? 15 Naye Daudi akamwambia Abneri, Wewe si mtu shujaa? Tena ni nani aliye sawa na wewe katika Israeli? Mbona, basi, hukumlinda bwana wako, huyo mfalme? Kwa maana mtu mmoja aliingia ili amwangamize mfalme, bwana wako? 16 Jambo hili ulilolitenda si jema. Aishivyo Bwana, mmestahili kufa, kwa sababu hamkumlinda bwana wenu, masihi*fq* wa Bwana. Haya basi! Tazameni, liko wapi fumo la mfalme, na gudulia la maji lililokuwa kichwani pake? 17 Naye Sauli akaitambua sauti ya Daudi, akasema, Hii ndiyo sauti yako, Daudi, mwanangu? Daudi akasema, Ndiyo, ni sauti yangu, bwana wangu, mfalme. 18 Akasema, Bwana wangu ananiwinda mimi mtumishi wake kwa sababu gani? Nimefanya nini mimi? Ni uovu gani nilio nao mkononi mwangu? 19 Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni Bwana aliyekuondokesha juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za Bwana; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa Bwana, wakisema, Enenda, katumikie miungu mingine. 20 Basi sasa, isianguke damu yangu chini mbali na uso wa Bwana; maana mfalme wa Israeli ametoka ili kutafuta uhai wangu, kama vile mtu awindavyo kware mlimani. 21 Ndipo Sauli akasema, Nimekosa; rudi, Daudi, mwanangu; maana sitakudhuru tena, kwa kuwa maisha yangu yalikuwa na thamani machoni pako leo; angalia, nimetenda upumbavu, nimekosa sana. 22 Daudi akajibu, akasema, Litazame fumo hili, Ee mfalme! Kijana mmoja na avukie huku, alitwae. 23 Naye Bwana atamlipa kila mtu haki yake, na uaminifu wake; maana Bwana amekutia mikononi mwangu leo, nami nalikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA. 24 Tena, angalia, kama vile maisha yako yalivyokuwa na thamani machoni pangu, kadhalika na maisha yangu na yawe na thamani machoni pa Bwana, akaniokoe katika shida zote. 25 Ndipo Sauli akamwambia Daudi, Ubarikiwe, Daudi, mwanangu; utatenda mambo makuu, tena hakika yako utashinda. Basi, Daudi akaenda zake; Sauli naye akarudi kwao.

 

Kwa hiyo, Sauli alitubu tena lakini Daudi alijua kwamba asingekuwa salama kabisa. Nia iliyomfanya Sauli akubali kufanya hivyo ilikuwa ni roho chafu. Pia Shetani alijua kuwa mstari wa uzao wa Masihi ulikuwa unapitia kwenye kabila la Yuda na kwa kupitia Daudi na sio kwa Wabenyamini kwa kupitia Sauli. Huo ndio mpango wa Mungu ulivyo na ulivyofunuliwa tayari (soma majarida ya Ruthu (Na. 27)  Mlolongo wa Uzao wa Masihi (Na. 119) na [Ruth (No. 27) and Genealogy of the Messiah (No. 119)].

 

1Samweli 27:1-12 Ndipo Daudi aliposema moyoni mwake, Siku moja, basi, mimi nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jema zaidi kwangu kuliko kukimbia mpaka nchi ya Wafilisti; naye Sauli atakata tamaa kwa habari yangu, asinitafute tena mipakani mwote mwa Israeli; hivyo nitaokoka katika mikono yake. 2 Basi Daudi akaondoka, yeye na hao watu mia sita aliokuwa nao, akamvukia Akishi, mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi. 3 Daudi akakaa huko Gathi pamoja na Akishi, yeye na watu wake, kila mtu na watu wa nyumbani mwake; Daudi naye alikuwa na wakeze wawili, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili wa Karmeli, aliyekuwa mkewe Nabali. 4 Naye Sauli akaambiwa ya kwamba Daudi amekimbia mpaka Gathi; wala hakumtafuta tena. 5 Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona kibali machoni pako na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumwa wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe? 6 Ndipo Akishi akampa Siklagi siku ile; kwa sababu hiyo huo mji wa Siklagi ni mali ya wafalme wa Yuda hata hivi leo. 7 Na hesabu ya siku alizokaa Daudi katika nchi ya Wafilisti ilikuwa mwaka mzima na miezi minne. 8 Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, hata mpaka nchi ya Misri. 9 Tena Daudi akaipiga nchi hiyo, asimhifadhi hai mume wala mke, akateka nyara kondoo, na ng'ombe, na punda, na ngamia na mavazi; kisha akarejea na kufika kwa Akishi. 10 Naye Akishi humwuliza, Je! Mmeshambulia upande gani leo? Na Daudi husema, Juu ya Negebu ya Yuda, au, juu ya Negebu ya Wayerameeli, au, juu ya Negebu ya Wakeni. 11 Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti. 12 Hivyo Akishi akamsadiki Daudi, akasema, Amewachukiza kabisa hao watu wake Israeli; kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu hata milele.

Daudi kwenye nchi ya Wafilisti na kutafuta ulinzi huko na kuendeleza mpango wa Mungu wa kuwaimarisha Israeli na kuwalinda waishi salama dhidi ya maadui zao. Wafilisti wakafanya mapatano na kushirikiana na Daudi na jeshi lake na waliwatumikia walitumia hil kuwa ni kama msingi au kigezo chao kwa majeshi yaliyoweka matuo yake dhidi ya wakazi wa kusini mwa Yuda. Kwa hiyo wakati mwingine haina maana kuwatumikia maadui zetu kwa lengo la kulilinda taifa dhidi ya maadui wa muda mrefu. Na ndipo mji wa Siklagi ukatwaliwa au kuhudishwa kwa Yuda na kutumiwa kama ngome isiyorasmi ambayo kwamba jeshi la watu wa Mungu lingfanyia mikakati yake ya mashambulizi. Kwa jinsi hii, Kanisa wakati mwingine pia linalazimika kutafuta ukimbizi nje ya Israeli kwa nia ya kulinda nafasi yake, na usalama wa Israeli kwa kipindi kirefu. Ufunuo 12:1-17 inaonyesha kuwa nchi itamlida Yule mwanamke ambaye alikuwa ni Kanisa kwa kipindi cha miaka 1260 ambacho ni cha kati ya miaka ya 590 BK hadi mwaka 1850 BK wakati wa zama za iliyokuwa inajulikana kama Dola Takatifu ya Ruma hadi walipofanikiwa kuyyatwaa maeneo au milki zilizosalia kwa ajili yao na Mungu. Waaka wa miaka hiyo, mara zote hata sisi tulikuwa chini ya mfumo huu au tuliutumikia mfumo huo kwa shuruti.

 

1Mambo ya Nyakati ina mengi ya kusema pia kwa ajili ya kipindi hiki cha Daudi alichokuwa huko Siklagi.

1Mambo ya Nyakati 12:1-22 Basi hawa ndio wale waliomjia Daudi huko Siklagi, alipokuwa akijificha kwa ajili ya Sauli, mwana wa Kishi; nao walikuwamo miongoni mwa wale mashujaa, waliomsaidia vitani. 2 Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kuume na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini. 3 Mkubwa wao alikuwa Ahiezeri, kisha Yoashi, wana wa Shemaa Mgibeathi; na Yezieli, na Peleti, wana wa Azmawethi; na Beraka, na Yehu Mwanathothi; 4 na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi; 5 Eluzai, na Yerimothi, na Bealia, na Shemaria, na Shefatia Mharufi; 6 Elkana, na Ishia, na Azaleli, na Yoezeri, na Yashobeamu, Wakora; 7 na Yoela, na Zebadia, wana wa Yerohamu, wa Gedori. 8 Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima; 9 Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu; 10 Mishmana wa nne, Yeremia wa tano; 11 Atai wa sita, Elieli wa saba; 12 Yohana wa nane, Elzabadi wa kenda; 13 Yeremia wa kumi, Makbanai wa kumi na moja. 14 Hao wa wana wa Gadi walikuwa maakida wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia, na yeye aliyekuwa mkuu, na elfu. 15 Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia. 16 Tena wakafika ngomeni kwa Daudi baadhi ya wana wa Benyamini na Yuda. 17 Naye Daudi akatoka ili kuwalaki, akajibu, akawaambia, Kama mmenijia kwa amani ili kunisaidia, basi moyo wangu utaambatana nanyi; lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu, kwa kuwa hamna udhalimu mikononi mwangu, Mungu wa baba zetu na alitazame neno hili, na kulikemea. 18 Ndipo roho ikamjilia Abishai, mkuu wa wale thelathini, naye akasema, Sisi tu watu wako, Ee Daudi; Na wa upande wako, Ee mwana wa Yese; Amani, naam, amani iwe kwako, Na amani iwe kwao wakusaidiao; Maana akusaidiye ndiye Mungu wako. Ndipo Daudi akawakaribisha, akawaweka wawe maakida wa kile kikosi. 19 Wa Manase pia wengine walimwangukia Daudi, alipokwenda pamoja na Wafilisti juu ya Sauli vitani, lakini hawakuwasaidia; kwani wale mabwana wa Wafilisti wakafanya shauri, wakamfukuza, wakisema, kwa hatari ya vichwa vyetu atamwangukia bwana wake Sauli. 20 Naye alipokuwa akienda Siklagi, wakamwangukia hawa wa Manase, Adna, na Yozabadi, na Yediaeli, na Mikaeli, na Yozabadi, na Elihu, na Silethai, maakida wa maelfu waliokuwa wa Manase. 21 Wakamsaidia Daudi juu ya kile kikosi kilichomshambulia; kwani walikuwa waume mashujaa wote, nao wakawa maakida jeshini. 22 Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.

 

Ukimwa wa Mungu na dhambi ya Sauli

1Samweli 28:1-25 Ikawa siku zile hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao waende vitani, ili kupigana na Israeli. Naye Akishi akamwambia Daudi, Jua hakika ya kuwa wewe utatoka pamoja nami jeshini, wewe na watu wako. 2 Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe kuwa mlinda kichwa changu daima. 3 Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao Israeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi. 4 Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika Gilboa. 5 Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana. 6 Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. 7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. 8 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako. 9 Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua? 10 Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili. 11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli. 12 Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. 13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. 14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia. 15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje. 16 Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako? 17 Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. 18 Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo. 19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti. 20 Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha. 21 Ndipo yule mwanamke akamwendea Sauli, akamwona ya kuwa yeye ametaabika sana, akamwambia, Angalia, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako, nami nimeutia uhai wangu mkononi mwangu, nami nimeyasikiliza maneno yako uliyoniambia. 22 Basi sasa, tafadhali, wewe uisikilize sauti ya mjakazi wako, nikakuandalie ngaa mkate kidogo; ukale, ili upate nguvu, utakapokwenda zako. 23 Lakini yeye alikataa, akasema, Mimi sitaki kula. Ila watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha; naye akaisikiliza sauti yao. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda. 24 Naye yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na unga, akaukanda, akafanya mkate wa mofa kwa unga huo; 25 kisha akamwandalia Sauli na watumishi wake; wakala. Ndipo wakaondoka, wakaenda zao usiku ule.

Ni elohim, au pepo Yule aliyekuja toka kuzimuni alinena kama Samweli, na Sauli aliadhibiwa kwa ajili ya ibada hii ya sanamu na vinago.

 

Aliyavunja maagizo ya Torati ya Mungu kwa kuwa hakumngojea na hakudumu kumtafuta Bwana wakati wote. Mara nyingi huwa hatujibiwi wakati tunapodhania kuwa tunahitaji kiru ila badala yake ni wakati inapokuwa sawasawa na kwenye mpango wa Mungu.

 

Kushindwa kwa Sauli

Sauli alikuwa amepewa kipindi maalumu na klipaswa kuwa ni kipindi kamili cha miaka arobaini ya utawala wake. Arobaini ni tarakimu muhimu inayoshabihiana na kipindi maalumu cha kufanya toba, kiwe kwa mwonekano wa idadi ya suku, majuma au miaka au yubile. Sauli aliwaongoza na kutawala Israeli kwa miaka arobaini. Mapepo walipewa kipindi maalumu cha kuitawala dunia kwa awamu tatu za miaka arobaini kila awamu moja, au cha yubile 120 au cha miaka elfu sita (soma jarida la Miaka Arobaini ya Toba (Na. 290) [Forty Years for Repentance (No. 290)].

 

Kwenye mapigano Daudi alilindwa na Akishi kwa kuwa Wafilisti walikuwa hawamuamini kwa asilimia zote.

1Samweli 29:1-11 Basi hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao yote huko Afeki; nao Waisraeli wakafanya kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli. 2 Nao mashehe wa Wafilisti wakapita mbele, mia kwa mia, na elfu kwa elfu; naye Daudi na watu wake wakapita wa mwisho pamoja na Akishi. 3 Ndipo wakuu wa Wafilisti wakasema, Waebrania hawa wafanyani hapa? Naye Akishi akawaambia wakuu wa Wafilisti, Je! Siye huyu Daudi, yule mtumishi wa Sauli, mfalme wa Israeli, ambaye amefuatana na mimi siku hizi, naam, miaka hii, wala mimi nisione hatia kwake, tangu hapo aliponiangukia mimi hata leo? 4 Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia; nao wakuu wa Wafilisti wakamwambia, Mrudishe huyu, apate kurejea mahali pake ulipomwagiza, wala asiende pamoja nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani; kwani mtu huyu angejipatanisha na bwana wake kwa njia gani? Je! Si kwa vichwa vya watu hawa? 5 Je! Siye huyo Daudi, ambaye waliimbiana habari zake katika michezo, wakisema,Sauli amewaua elfu zake,Na Daudi makumi elfu yake? 6 Ndipo Akishi akamwita Daudi, akamwambia, Aishivyo Bwana, wewe umekuwa mwenye adili, tena kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema machoni pangu; kwa sababu mimi sikuona uovu ndani yako tangu siku ile uliponijia hata leo; walakini hao wakuu hawakuridhii. 7 Basi sasa urudi, uende zako kwa amani, ili usiwachukize hao mashehe wa Wafilisti. 8 Naye Daudi akamwambia Akishi, Lakini mimi nimefanyaje? Nawe umeona nini kwangu mimi mtumwa wako, muda wote niliokaa mbele yako hata leo, nisipate ruhusa niende na kupigana na adui za bwana wangu mfalme? 9 Akishi akajibu, akamwambia Daudi, Mimi najua ya kuwa u mwema machoni pangu, kama malaika wa Mungu; ila hao wakuu wa Wafilisti wamesema, Huyu hatakwea pamoja nasi kwenda vitani. 10 Kwa hiyo sasa amka asubuhi na mapema, wewe na watumwa wa bwana wako waliokuja pamoja nawe; nanyi mtakapoamka asubuhi na mapema, na kupata mwanga, nendeni zenu. 11 Basi Daudi akaamka asubuhi na mapema, yeye na watu wake, kwenda zao asubuhi, kuirudia nchi ya Wafilisti. Nao Wafilisti wakakwea kwenda Yezreeli.

 

Wakati huu baadhi ya Wamanase walikwenda kwa Daudi pia.

1Mambo ya Nyakati 12:19 Wa Manase pia wengine walimwangukia Daudi, alipokwenda pamoja na Wafilisti juu ya Sauli vitani, lakini hawakuwasaidia; kwani wale mabwana wa Wafilisti wakafanya shauri, wakamfukuza, wakisema, kwa hatari ya vichwa vyetu atamwangukia bwana wake Sauli.

 

Kwenye mapigano haya alilindwa ili asitumike kinyume cha watu wake mwenyewe. Lakini Mungu alimshughulikia Sauli, na Daudi aliwekwa mbali na mapigano haya. Ni mahali hapa ndipo Akishi alisema kuwa Daudi alikuwa kwake kama malaika wa Mungu, na ndivyo hata sisi tunatakiwa tuwe ni watu tusio na lawama yoyote ile maishani mwetu.

1Samweli 30:1-30 Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto; 2 nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo wote, ila wakawachukua, wakaenda zao. 3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka. 4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. 5 Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli. 6 Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. 7 Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. 8 Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote. 9 Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikilia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa. 10 Lakini Daudi akakaza kufuata, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori. 11 Nao wakamkuta Mmisri mavueni, wakamleta kwa Daudi, na kumpa chakula, naye akala; nao wakampa maji ya kunywa; 12 kisha wakampa kipande cha mkate wa tini, na vishada viwili vya zabibu; naye akiisha kula roho yake ikamrudia; kwa maana alikuwa hakula chakula wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku. 13 Ndipo Daudi akamwuliza, Wewe u mtu wa nani; nawe umetoka wapi? Naye akasema, Mimi ni kijana wa Misri, mtumwa wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu tangu siku hizi tatu nalishikwa na ugonjwa. 14 Sisi tulishambulia Negebu ya Wakerethi, na ya milki ya Yuda, na Negebu ya Kalebu; na huo mji wa Siklagi tukauchoma moto. 15 Daudi akamwambia, Je! Wewe utaniongoza chini hata nilifikilie jeshi hilo? Naye akasema, Uniapie kwa Mungu, ya kwamba hutaniua, wala kunitia mikononi mwa huyo bwana wangu, nami nitakuongoza chini hata kulifikilia jeshi hilo. 16 Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda. 17 Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hata jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia. 18 Daudi akawapokonya wote waliokuwa wamechukuliwa na Waamaleki; naye Daudi akawaokoa wakeze wawili. 19 Wala hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala cho chote walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote. 20 Naye Daudi akatwaa makundi yote ya kondoo na ng'ombe, ambao waliwatanguliza mbele ya wanyama wale wengine, wakasema, Hao ndio nyara za Daudi. 21 Kisha Daudi aliwafikilia wale watu mia mbili, waliokuwa wametaka kuzimia, hata wasiweze kumfuata Daudi, wale waliowaacha wakae karibu na kijito cha Besori; nao wakatoka nje ili kumlaki Daudi, na kuwalaki hao watu waliokuwa pamoja naye, naye Daudi alipowakaribia hao watu, aliwasalimu. 22 Ndipo watu waovu wote na wale wasiofaa, miongoni mwa hao waliokwenda pamoja na Daudi, wakasema, Kwa kuwa watu hawa hawakuenda pamoja na sisi, hatutawapa kitu cho chote katika hizo nyara tulizozitwaa tena, isipokuwa kila mtu atapewa mkewe na watoto wake, wawachukue na kwenda zao. 23 Ndipo Daudi akasema, La, ndugu zangu, msitende hivyo katika hizo nyara alizotupa Bwana, ambaye ndiye aliyetuhifadhi, akalitia mikononi mwetu lile jeshi lililokuja kinyume chetu. 24 Tena ni nani atakayewasikiliza ninyi katika jambo hili? Kwa kuwa kama lilivyo fungu lake yeye ashukaye vitani, ndivyo litakavyokuwa na fungu lake huyo akaaye karibu na vyombo; watagawiwa sawasawa. 25 Basi ikawa hivyo tangu siku ile na baadaye; akaiweka iwe amri na agizo la Israeli hata leo. 26 Basi Daudi alipofika Siklagi, aliwapelekea wazee wa Yuda, rafiki zake, sehemu ya nyara, akasema, Angalieni, zawadi yenu katika nyara za adui za Bwana; 27 yaani, kwa hao wa Betheli, na kwa hao wa Ramoth-Negebu, na kwa hao wa Yatiri; 28 na kwa hao wa Aroeri, na kwa hao wa Sifmothi, na kwa hao wa Eshtemoa; 29 na kwa hao wa Rakali, na kwa hao wa miji ya Wayerameeli, na kwa hao wa miji ya Wakeni; 30 na kwa hao wa Horma, na kwa hao wa Korashani, na kwa hao wa Athaki; 31 na kwa hao wa Hebroni, na kwa hao wa kila mahali alipozoelea Daudi mwenyewe na watu wake.

Kwenye mapigano haya Mungu aliwatenga mbali wateule waliofuatana na Daudi ili kuilinda miji ya Siklagi na kusini mwa Yuda na kuwaangamiza maadui wengine wa Israeli. Waamaleki waliwashuhudia maadui zao wa muda mrefu na wa hatari, wakiangukia mikononi mwa Israeli (soma jarida la Ufafanuzi wa Kitabu cha Esta (na. 63) [Commentary on Esther (No. 63)]. Aliwawapa fursa njema kwa ushindi huu mkubwa.

 

Sauli anajiua mwenyewe

1Samweli 31:1-13 Basi Wafilisti wakapigana na Israeli; nao watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, wakaanguka wameuawa katika mlima wa Gilboa. 2 Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli. 3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde. 4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia. 5 Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye. 6 Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu, na mchukua silaha zake, na watu wake wote pamoja siku iyo hiyo. 7 Kisha watu wa Israeli waliokuwa upande wa pili wa bonde lile, na ng'ambo ya Yordani, walipoona ya kuwa watu wa Israeli wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.

Wakati Sauli na wanawe watatu ambao walikuwa ni mihimili ya Israeli machoni mwa watu wengi, walipouawa, watu walipoteza imani na ujasiri na wakakimbia.

8 Hata ikawa, siku ya pili yake, Wafilisti walipokwenda kuwateka nyara waliouawa, walimwona Sauli na wanawe watatu wameanguka juu ya mlima wa Gilboa. 9 Wakamkata kichwa, wakamvua silaha zake, wakapeleka wajumbe kwenda nchi ya Wafilisti pande zote, ili kutangaza habari nyumbani mwa sanamu zao, na kwa watu. 10 Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa Maashtorethi; wakakitundika kiwiliwili chake katika ukuta wa Beth-shani. 11 Na wenyeji wa Yabesh-Gileadi waliposikia habari zake, jinsi hao Wafilisti walivyomtenda Sauli, 12 wakainuka mashujaa wote, wakaenda usiku kucha, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, na kuiondoa ukutani kwa Beth-shani nao wakaja Yabeshi, na kuiteketeza huko. 13 Kisha wakaitwaa mifupa yao, na kuizika chini ya mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba. (sawa na Mambo ya Nyakati 10:4-12)

 

Na ndivyo ilivyokuwa, kwa hawa watoto wa kiume wa Sauli.

1Mambo ya Nyakati 8:33 Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali. (sawasawa na 1Nyakati 9:39)

 

Ndipo Sauli alipokufa kwa kuwa alikwnda kuomba ushauri kwa watu wenye pepo wa utambuzi na hakutaka kumngoja Bwana. Sauli aliuangukia mkuki wake mwenyewe na inaonekana kuwa maisha yake hatimaye yaliishia kwa kumaliziwa na Mwamaleki – au kama alivyosema (soma 1Samwli. 1:5 na kuendelea).

1Mambo ya Nyakti 10:13 Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake,

 

Kwa kuwa Mungu alimuamuru awalishe watu wake Israeli na alishindwa.

 

1Mambo ya Nyakati 11:2 Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyewatoa na kuwaingiza Israeli. Naye Bwana, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli.

 

Kuchagua kunaendelea

Watu mashujaa walichaguliwa chini ya matatizo ya Daudi huko Siklagi. Hawa walikuja pia, kama tulivyoona, kutoka manase na kila mahali na kufanya kikosi kikubwa cha kupigana vita cha jeshi la taifa la Israeli.

1Mambo ya Nyakati 12:1 Basi hawa ndio wale waliomjia Daudi huko Siklagi, alipokuwa akijificha kwa ajili ya Sauli, mwana wa Kishi; nao walikuwamo miongoni mwa wale mashujaa, waliomsaidia vitani.

 

Kosa kubwa alilolifanya Sauli lilikuwa ni kwamba katika miaka ya utawala wake tatizo kubwa lilitokea kwenye mambo ya ibada. Katika kipindi hiki umuhimu wa Sanduku la Agano ulikuwa haueleweki na wala hakuja aliyekuwa na habari kuhusu lilipo sanduku hili, na kwa hiyo Sheria au Torati ya Mungu ilikuwa haieleweki pia.

1Mambo ya Nyakati 13:3 nasi tujirudishie tena sanduku la Mungu wetu; maana hamkuuliza neno kwa hilo katika siku za Sauli.

Kosa hili liliashiria mwanzo wa matatizo mngine ya kipindi kile cha Sauli yaliyoendelea hadi kwene kipindi kingine cha pili cha Daudi. Undugu wa kuzaliwa wa Dauli ilibidi utumike katika kuwaandaa watu kwa ajili ya kuzijua Sheria za Mungu. Tazama kwenye mfualulizo wa majarida ya  Torati ya Mungu (Na. L1) [The Law of God (L1)] na pia maana yake.

 

Ushahidi wa Zaburi

Kwa yote haya Daudi alimtafuta Mungu na tunajionea ukweli huo kwenye maandiko ya Zaburi.

Zaburi 18:1 Wewe, Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana; 2 Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.

 

Zaburi 52:1 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote. 2 Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila 3 Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.

 

Zaburi 54:1 Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu. 2 Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu.

 

Zaburi 57:1 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hata misiba hii itakapopita.

 

Zaburi 59:1 Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu, Uniinue juu yao wanaoshindana nami.

 

Unabii

Na ndipo tunaona kwamba hadithi hii inaendelea hadi kwenye unabii na kueleweka kama una maana kwnye kipindi chote cha Israeli na cha Kanisa.

Isaya 10:29 wamevuka kivuko; wamekwenda kulala katika Geba; Rama unatetemeka; Gibea wa Sauli umekimbia.

 

Matendo 13:21 Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini.

 

Kipindi chenye maana ashirio cha utawala wa Sauli

 

Kama viumbe walivyomkata Mungu pamoja na Adamu wa kwanza, hawa pia walimkataa Mungu pamoja na mfalme wao wa kwanza. Kwa hiyo ndivyo pia, wana wa Israeli walifanya mambo yao chini ya utawala wa Sauli sawasawa na walivyofanya watu wengine wote waliowatangulia kabla yao. Sauli alipagawa na wazimu wa Wanefili na Waanaki na ni jambo lililoonekana dhahiri pia.

 

Kwa jinsi hii tunaona kuwa utawala wa Sauli ulikuwa sawasawa na unabii na kipindi cha mfano wa kiroho cha yubile aribaini za kwanza katika uumbaji hadi kwenye tukio la gharika kuu hadi Ibrahimu. Tunaweza kukitumia kipindi hiki maalumu kilichotajwa na Ussher, cha tangu kuumbwa kwa Adamu kama kilivyonyeshwa hadi mwaka 4004/5 KK na kushuka chini na hadi tukio la gharika kuu na cha kufanywa kwa marejesho tena kwa hii dunia, chini ya wana wa Nuhu na ukuhani wa Kishemu ya mfano wa Melkizedeki huko Yerusalemu. Ukuhani huu wa Melkizedeki ilibidi nindelee hadi Daudi alipoingia Yerusalemu mnamo mwaka 1005/4 KK, ni miaka elfu tatu kamili tangu uumbaji wa Adamu sawasawa na maagizo ya Biblia. Majina ya mfalme wa Yerusalemu yalikuwa ni Melkizedeki na Adonizedeki ambayo maana yake halisi ni Mfalme wangu ni mtu wa Haki au Bwana wangu ni Mtakatifu na anajulikana kama Bwana au Mfalme wa Haki na Utakatifu. Siku hii ni ina maana yake halisi ni kama kilivyo nusu kipindi cha katikati ya Ibrahimu na kuzaliwa kwa Kristo, ambacho ni cha miaka elfu nne kamili tangu kuumbwa kwa Adamu. Kipindi zama cha katikati pia kinafanya utimilifu wa nyakati za Wamataifa (sawa na maoni ya jarida la Kuichambua Ratiba ya Zama na Nyakati (Na. 272) [Outline Timetable of the Age (No. 272)]. Inaonyesha pia kipindi cha mpito cha huko Yerusalmu cha tangu ukuhani ulipowekwa huko Yerusalemu chini ya Shemu, na kufanywa upya kwa hii dunia kutakakofanywa chini ya mfano wa Melkizedeki, na kuanzishwa kwa ukuhani wa muda wa Lawi aliyetoa zaka yake kwa Melkizedeki alipokuwa viunoni mwa Ibrahimu. Ukuhani huu ulikuwa mkuu kuliko ule wa Lawi, na hata ule wa Israeli, na uliendeleza ukuhani ule hadi kwa Wamataifa bila kuwa na kizuizi cha mstari na umri, sambamba na vizuizi vinavyohuana na kupewa huduma hii watu kutoka kabila la Lawi kwa mujibu wa Torati kwenye sheria zinazohusiana na huduma za Hekaluni. Kristo alikuja ili kuendeleza ukuhani huu na kuupanua kwa upana zaidi ya mipaka ya Israeli.

 

Kipindi hiki cha mpito tangu Sauli alipoonesha kubadilishana kutoka kwa Mbenyamini mwana wa ahadi hadi  kwenye kabila la Yuda la mtiwa mafuta wa Bwana na mrithi wa ahadi ya fimbo ya ufalme au utawala. Ahadi hii ilitolewa na Mababa kwa niaba ya Mungu. Na pia inaashiria kuwa tendo hili la kubadilishana utawala na ahadi ya urithi ya Ibrahimu aliyopewa kwenye agano lake ambalo Mungu alilifanya nay eye, Ibrahimu kwa njia ya imani (kwa habari hii zaidi tembelea kwenye tovuti ya http://abrahams-legacy.org).

 

Kuondolewa kwa Sauli

Karama zote zimetolewa kwa masharti maalumu ya kutii. Sauli aliondolewa na Mungu kwa kuwa hakuwa mtiifu na hakuwa kifaa kinachofaa au kilicho imara kumudu kuiongoza Israeli. Hapa ubadilishaji wa ufalme ulifanyika na ufalme ukachukuliwa kutoka kwenye kabila la Benyamini na kupewa Daudi wa kabila la Yuda. Ni kwa namna hii hii ndipo Masihi ia alihesabiwa na kuwekwa kwenye orodha ya kabila hilihili lililochaguliwa au kuteuliwa la Yuda lililopewa fimbo ya kifalme na kwenye mstari wa uzaliwa wa Yese, na kutoka Yuda na mstari huu unamaanisha kuwa wokovu unapaswa uje kwa kupitia watu wa Mataifa (soma jarida la Mlolongo wa Uza wa Masihi (Na. 119) [The Genealogy of the Messiah (No. 119)]. Mstari wake pia ulijazwa na vipengele vingi vya ahadi na unabii wa Mungu kupitia hekaluni na ufalme wa Yuda.

 

Kwa hiyo tunaona mwisho wa kipindi cha kwanza cha miaka arobaini ya wafalme. Kipindi hiki pia inakuwa inalingana kinabii kwenye Miaka hii Arobaini ya Kwanza ya maisha ya Musa na kinawakilisha miaka elfu mbili cha uumbaji chini ya malaika walioasi na Wanefili hadi kwenye gharika kuu na hatimaye kwenye kuitwa kwake Ibrahimu.

 

q