Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[282C]

 

 

Utawala wa Wafalme

Sehemu ya III:

Sulemani na Ufunguo wa Daudi

(Toleo La 1.0 20000315-20060717-20070906)

Awamu ya mwisho ya Mpango wa Mungu kama ulivyoonyeshwa kwenye utawala wa wafalme wa Israeli ni ile ya Mfalme Sulemani. Mwandamano huu wa matukio ulikuwa unamuashiria au kumuonyesha Kristo na uanzishaji wa Kanisa likiwa kama Hekalu la Kiroho la Mungu.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki ©  2002, 2006, 2007 Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Utawala wa Wafalme Sehemu ya III: Sulemani na Ufunguo wa Daudi


 


Kupewa Mamlaka kwa Sulemani

Ni kama tulivyoona, Mungu alimchagua Sulemani awe Mfalme, kama al;ivyomchagua Daudi achukue nafasi ya Sauli’ kila mmoja wa watawala hawa watatu walichaguliwa kwa malengo na makusudi fulani na maisha yao yalikuwa na kielelezo chenye maana kwenye Mpango wa Mungu kwenye kipindi cha miaka 6,000 ya uumbaji tangu Adamu na kufungwa kwa Bustani ya Edeni na kuendelea hadi kwenye kipindi cha Milenia kuu ya mapumziko na Yesu Kristo.

1Wafalme 2:1-46 Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema, 2 Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume; 3 uyashike mausia ya Bwana, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako; 4 ili Bwana afanye imara neno lake alilonena kwa habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli. 5 Na zaidi ya hayo, umejua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kuimwaga damu ya vita wakati wa amani, akautia damu ya vita mshipi uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake. 6 Kwa hiyo ufanye kama ilivyo hekima yako, wala usimwachie mvi zake kushukia Ahera kwa amani. 7 Lakini uwafanyie mema wana wa Barzilai Mgileadi, wawe miongoni mwao walao mezani pako; kwa jinsi walivyonijilia nilipokuwa nimekimbia mbele ya Absalomu, ndugu yako. 8 Hata, angalia, yuko pamoja nawe Shimei, mwana wa Gera, Mbenyamini, wa Bahurimu, ndiye aliyenilaani kwa laana kuu siku ile nilipokwenda Mahanaimu; lakini akashuka kunilaki kule Yordani, nami nikamwapia kwa Bwana, nikamwambia, Mimi sitakuua kwa upanga. 9 Basi kwa hiyo usimwachilie, kwa kuwa wewe u mtu wa akili; nawe utajua ikupasayo umtendee, na mvi zake utazishusha Ahera pamoja na damu. 10 Basi Daudi akalala na babaze, akazikwa mjini mwa Daudi. 11 Na siku alizotawala Daudi juu ya Israeli zilikuwa miaka arobaini; huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.

 

Daudi alikuwa ameyaona matatizo yaliyosababishwa na wale waliomuathiri yeye, kama vile Yoabu na Shimei Mbenyamini, na alimuamini Sulemani kuwa ataweza kuwaadhibu kwa damu yao. Sulemani aliaminiwa na kupewa ufalme na alikuwa na kazi fulani maalumu. Tangu wakati ule alipewa hekima pia ya kupambanua na mfano wake wa kwanza tuliouona ulikuwa ni ule wa kumhukumu Adonia.

12 Basi Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha Daudi baba yake; na ufalme wake ukawa imara sana. 13 Ndipo Adonia mwana wa Hagithi akaja kwa Bath-sheba mamaye Sulemani. Naye akasema, Je! Umekuja kwa amani? 14 Naye akajibu, Kwa amani. Tena akasema, Nina shauri ninalotaka kukuambia. Naye akamwambia, Sema. 15 Basi akasema, Wajua ya kwamba ufalme ulikuwa wangu, na Israeli wote wakaniwekea nyuso zao ili nimiliki mimi; walakini sasa ufalme umegeuka kuwa wake ndugu yangu; kwa maana ulikuwa wake kutoka kwa Bwana. 16 Basi sasa nina haja moja ninayokuomba, usinikataze hiyo. Naye akamwambia, Sema. 17 Akasema, Nena, nakusihi, na Sulemani, mfalme, (kwa kuwa hawezi kukukataza neno), kwamba anioze Abishagi, Mshunami. 18 Naye Bath-sheba akasema, Vema; nitasema na mfalme kwa ajili yako. 19 Basi Bath-sheba akaingia kwa mfalme Sulemani, aseme naye kwa ajili ya Adonia. Naye mfalme akainuka kwenda kumlaki, akamwinamia, akaketi katika kiti chake cha enzi; kisha akaagiza awekewe kiti cha enzi mamaye mfalme; naye akaketi mkono wake wa kuume. 20 Ndipo akasema, Haja moja ndogo nakuomba; usinikataze. Mfalme akamwambia, Omba, mama; kwa kuwa siwezi kukukataza neno. 21 Naye akasema, Nataka Adonia, ndugu yako, aozwe Abishagi, Mshunami. 22 Akajibu mfalme Sulemani akamwambia mamaye, Na mbona wamtakia Adonia Abishagi, Mshunami? Umtakie na ufalme pia; kwa kuwa yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, umtakie yeye, na Abiathari kuhani, na Yoabu mwana wa Seruya. 23 Ndipo mfalme Sulemani akaapa kwa Bwana, akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, isipokuwa Adonia amenena neno hili juu ya uhai wake mwenyewe. 24 Basi kwa hiyo, Bwana aishivyo, aliyenithibitisha na kunikalisha katika kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, akanifanyia nyumba, kama alivyoahidi, hakika atauawa leo hivi Adonia. 25 Mfalme Sulemani akatuma kwa mkono wa Benaya mwana wa Yehoyada: naye akampiga, hata akafa. 

 

Sulemani aliyasamehe maisha na uhai wa watu hawa kwa masharti maalumu na ilitegemea tu mwenendo wao jinsi utakavyokuwa na uadilifu wao. Ombi la Adonia linaonyesha nia yake ya kukipata kiti cha ufalme baada ya kufanikisha ndoa yake na Abigaili Mshunami, na kama alivyokuwa ni mshirika wa mwisho wa Daudi na aliyechukuliwa kuwa mwenye kuheshimika sana. Ingetoa mwanya wa ambao kwamba Adonia angetaka kuchukua kiti cha ufalme tena.

 

Sulemani aliyaponya maisha na uhai wa Abiathari kuhani, kwa kuwa alilibeba Sanduku la Agano mbele ya Daudi. Hata hivyo, alimfukuza na kumhamishia huko Anathothi. Huko ni nyumbani kwa nabii pia.

 

26 Tena, mfalme akamwambia Abiathari kuhani, Enenda Anathothi mashambani kwako; kwa kuwa wastahili kufa; ila leo sikuui, kwa sababu wewe ulichukua sanduku la Bwana mbele ya Daudi baba yangu, na kwa sababu wewe uliteswa kwa mateso yote ya baba yangu. 27 Hivyo Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa Bwana; ili alitimize neno la Bwana, alilonena juu ya nyumba ya Eli katika Shilo. 28 Tena, habari zikamfikia Yoabu; kwa maana Yoabu alikuwa amemfuata Adonia, ingawa hakumfuata Absalomu. Yoabu akakimbilia Hemani kwa Bwana, akazishika pembe za madhabahu. 29 Akaambiwa mfalme Sulemani ya kwamba, Yoabu amekimbilia Hemani kwa Bwana, naye, tazama, yuko madhabahuni. Ndipo Sulemani akamtuma Benaya, mwana wa Yehoyada, akisema, Enenda, umpige. 30 Basi Benaya akaja Hemani kwa Bwana, akamwambia, Mfalme asema hivi, Njoo utoke. Naye akajibu, La, sivyo; ila nitakufa papa hapa. Naye Benaya akamletea mfalme habari, akisema, Hivi ndivyo alivyonena Yoabu, na ndivyo alivyonijibu. 31 Mfalme akamwambia, Fanya alivyonena, umpige, ukamzike; ili uniondolee mimi na nyumba ya babangu damu aliyoimwaga Yoabu bure. 32 Naye Bwana atamrudishia damu yake kichwani pake mwenyewe, kwa kuwa aliwapiga watu wawili wenye haki, na wema kuliko yeye, akawaua kwa upanga, wala babangu Daudi hakujua habari hiyo; yaani Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa, mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda. 33 Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa Bwana. 34 Ndipo Benaya, mwana wa Yehoyada, akapanda, akampiga, akamwua; naye akazikwa katika nyumba yake mwenyewe iliyoko nyikani. 35 Kisha mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yehoyada, mahali pake juu ya jeshi; na Sadoki, kuhani, mfalme akamweka mahali pa Abiathari. 36 Tena, mfalme akatuma watu akamwita Shimei, akamwambia, Ujijengee nyumba humu Yerusalemu, ukae ndani yake, wala usitoke humo kwenda mahali po pote. 37 Kwa kuwa siku ile ya kutoka kwako, na kuvuka kijito Kidroni, ujue hakika ya kwamba kufa utakufa; damu yako itakuwa juu ya kichwa chako mwenyewe. 38 Naye Shimei akamwambia mfalme, Neno hili ni jema; kama alivyosema bwana wangu mfalme, ndivyo atakavyofanya mtumwa wako. Basi Shimei akakaa Yerusalemu siku nyingi. 39 Ikawa miaka mitatu ilipokwisha, watumwa wawili wa Shimei wakatoroka kwenda kwa Akishi, mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi. Wakamwambia Shimei, wakasema, Angalia, watumwa wako wako huko Gathi. 40 Shimei akaondoka, akatandika punda wake, akaenda Gathi kwa Akishi, ili kuwatafuta watumwa wake. Akaenda Shimei, akawaleta watumwa wake toka Gathi. 41 Naye Sulemani akaambiwa, ya kwamba Shimei alikuwa ametoka Yerusalemu kwenda Gathi, na kurudi tena. 42 Basi, mfalme akatuma watu, akamwita Shimei, akamwambia, Je! Sikukuapisha kwa Bwana, na kukushuhudia, kusema, Siku ile ya kutoka kwako ukienda mahali po pote, ujue hakika ya kwamba kufa utakufa? Nawe ukaniambia, Neno hili nililolisikia ni jema? 43 Mbona basi hukukishika kiapo cha Bwana, na amri niliyokuagiza? 44 Tena, mfalme akamwambia Shimei, Umejua uovu wote uliouona moyoni mwako, uliomtenda Daudi baba yangu; basi kwa hiyo Bwana atakurudishia uovu wako kichwani pako mwenyewe. 45 Ila mfalme Sulemani atakuwa amebarikiwa, na kiti cha enzi cha Daudi kitathibitika mbele za Bwana hata milele. 46 Basi mfalme akamwamuru Benaya, mwana wa Yehoyada; naye akatoka, akampiga, hata akafa. Nao ufalme ukawa imara mkononi mwa Sulemani.

 

Shimei, Mbenyamini, hakuweza kuaminiwa kwa kuwa alifanya uasi na alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo tena. Alipewa masharti ili kwamba kama atayavunja, kama alivyopuuzia masharti hayo ya mfalme hapo mwanzoni, basin a auawe pasipo lawama.

 

Kisha Sulemani alianza mchakato wa kuanzisha ushirikiano wa kibiashara kwa kuwaoa binti za watawala majirani zake. Kitendo hiki kilimpelekea kujikwaa na kuugawanya ufalme kipindi cha motto wake. Mungu hakulifanya hilo kipindi cha uhai na utawala wake kwa kuwa Mpango wa Mungu ukipaswa ufunuliwe kwa huo, na haukupaswa kuparaganyika kwa namna yoyote ile kwa kuwa ulikuwa unafanya taswira ya utawala wa Kristo na Kanisa, ambao utawala wa Sulemani ndiyo ulikuwa ni taswira yake. Mlolongo huu wote ulikusudiwa kuanzisha mpango wa wokovu, uliojulikana kama Ufunguo wa Daudi, na unapaswa ubakie umekamilika hadi marejesho mapya ya Siku za Mwisho.

 

Sulemani akamuoa binti wa Farao kabla ya kujengwa kwa Hekalu. bilashaka hii ilifanyika kwa lengo la kuweka amani na Misri hadi alipokamilisha kujenga Mahekalu.

 

Farao nayeongelewa hapa alikuwa ni wa Kizazi cha 21 cha Tanite kilichoitawala Misri tangu takriban mwaka 1070-945 KK. Farao huyu huenda alikuwa ni Psusennes II Titkheprure (takriban mwaka 976-962), na alirithiwa na Siamun Nutekhepere (mwaka 962-945). Sulemani alitawala miaka arobaini hadi takriban mwaka 933 KK. Kwa hiyo, ndugu zake huko Misri waliishi salama kwa kipindi chake chote cha utawala wake na amani ilikuwa ni ya uhakika sana. Kizazi cha kifalme cha Tanite kiliishia kwa kurithiwa na Kizazi cha 22 (945-730 KK), ambacho kilianzishwa na Sheshonq I.  Alitokea kwa wafanyakazi au wanajeshi wa Kilybia, Wameshwesh. Alimsaidia Yeroboamu dhidi ya Rehoboamu mfalme wa Yuda, huenda ni kwa sababu ya ushirikiano wa kindoa aliokuwanao baba yake Rehoboamu ambao ni uhusiano na ushirika wa Sulemani na ndoa aliyoifanya ya kumuoa binti mfalme wa Tenite. Alifanya kampeni huko Palestina yapata mwaka 930 na akakusanya kodi katika Yuda.

 

Kwenye andiko hili la 1Wafalme 3 tunaona hekima aliyopewa Sulemani kama alivyoiomba, na ilionekana kwenye hukumu na maamuzi yake.

 

1Wafalme 3:1-28 Huyo Sulemani akafanya ujamaa na Farao, mfalme wa Misri, akamwoa binti yake Farao, akamleta mjini mwa Daudi, hata alipokwisha kuijenga nyumba yake, na nyumba ya Bwana, na ukuta wa kuuzunguka Yerusalemu. 2 Ila watu walikuwa wakichinja dhabihu katika mahali pa juu, kwa sababu haikuwapo nyumba iliyojengwa kwa jina la Bwana, hata siku zile. 3 Sulemani naye akampenda Bwana, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu. 4 Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile. 5 Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe. 6 Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo. 7 Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. 8 Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. 9 Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? 10 Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. 11 Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; 12 basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe. 13 Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote. 14 Nawe ukienda katika njia zangu, na kuyashika mausia yangu, na amri zangu, kama baba yako Daudi alivyokwenda, basi nitazifanya siku zako kuwa nyingi. 15 Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la agano la Bwana, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote. 16 Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake. 17 Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani. 18 Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu. 19 Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. 20 Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu. 21 Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa. 22 Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme. 23 Ndipo mfalme akasema, Huyu anasema, Mtoto wangu yu hai, na mtoto wako amekufa. Na huyu anasema, Sivyo hivyo; bali mtoto aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu. 24 Mfalme akasema, Nileteeni upanga. Wakaleta upanga mbele ya mfalme. 25 Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu. 26 Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme kwa maana moyoni mwake alimwonea mtoto wake huruma, akasema, Ee bwana wangu, mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue kamwe. Lakini yule mwingine akasema, Asiwe wangu wala wako; na akatwe. 27 Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe huyu wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake. 28 Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.

 

Kilikuwa ni kipindi cha kuuona moyo au kiini cha jambo lenyewe, na kuona moyo wa mtu kwa hukumu hii na iliyomtukuza Sulemani. Nia ya Adoniya ilikuwa wazi, kama ilivyokuwa nia iliyokuwa kwa huyu kahaba ambaye alipenda kumuona mtoto akiuawa. Hakuna mzazi hasa mama wa kweli wa mtoto angaliyekubali kufanyika kwa hilo hata kwa yeyote angaliyeweza kudhania kiuhalisia na uhakika kabisa kuwa mtoto ni wake kuliko hata mama wa mtoto. Moyo aliokuwanao mwanamke huyu aliyependa kuona mtoto huyu akikatwa vipande viwili ulitaka kumfanya Yule mwenzake asikijikie vizuri ukitikisa mawazo na nia ya moyo, na ndipo Sulemani aliweza kuijua mia iliyokuwa miyoni mwao na uhakika wa jambo lilivyo kwa kutumia mtihani mdogo sana na jibu lake. Watu wengi karika Israeli walilisikia jambo hili, na kama walivyojua kwamba hukumu yake kwenye mambo makubwa angewezakugundua kwa kupitia aina yoyote ya hila au ujanja na udanganyifu wao wakifanya.

 

Baraka za Sulemani zimeandikwa pia kwenye kitabu cha Mambo ya Nyakati.

 

2Mambo ya Nyakati 1:1-17 Basi Sulemani, mwana wa Daudi, alithibitishwa katika ufalme wake, naye Bwana, Mungu wake, alikuwa pamoja naye, akamtukuza mno. 2 Sulemani akasema na Israeli wote, na maakida wa maelfu, na wa mamia, na waamuzi, na kila shehe wa Israeli wote, wakuu wa nyumba za mababa..

 

Kipindi hiki, Sulemani alikazia kwa moyo wote kumuabudu Mungu na kuwa mtiifu na mkamilifu kwake kwa bidii yake yote.

2Mambo ya Nyakati 1:3-6 Basi Sulemani akaenda mahali pa juu pa Gibeoni, na kusanyiko lote naye; kwani ndipo ilipokuwako hema ya kukutania ya Mungu, aliyoifanya Musa mtumishi wa Bwana jangwani. 4 Lakini sanduku la Mungu, Daudi alikuwa amelipandisha kutoka Kiriath-yearimu mpaka mahali Daudi alipolitengenezea; maana amelitandia hema katika Yerusalemu. 5 Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanyiza Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya Bwana; Sulemani na kusanyiko wakaiendea. 6 Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za Bwana, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.

 

Matokeo ya utiifu na unyenyekevu wake Sulemani alitakiwa na Elohim (tumjuaye kama Yesu Kristo leo) aombe lolote alitakalo.

7 Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe 

 

Sulemani hapa anaomba hekima na matokeo yake alipokea zaidi yake.

2Mambo ya Nyakati 1:8-17 Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. 9 Basi sasa, Ee Bwana Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. 10 Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi? 11 Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao; 12 basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo. 13 Akaja Sulemani kutoka mahali pa juu pa Gibeoni, toka mbele ya hema ya kukutania, mpaka Yerusalemu; akatawala juu ya Israeli. 14 Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu na mia nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu. 15 Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi. 16 Nao farasi, aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi; kila kundi na thamani yake. 17 Nao hupandisha, na kuleta kutoka Misri gari kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi kwa mia na hamsini, vivyo watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.

 

Andiko hili linaonyesha kwamba wafalme wa Wahiti na wafalme wa Syria waliungana na kushirikiana na Sulemani na walipewa magari na farasi kwa ajili ya majeshi yao yaliyokuwa kaskazini mwa Israeli, wakati washirika wa Sulemani na walioanza kulinda mpaka wake na Misri wakati wa Kizazi cha ufalme cha 21 (cha Tanite), na ambacho kilikuwa kinamiliki ufuo wa Delta ya Nile na kaskazini mwa Misri. Wasyria au Washamu walizishikilia nchi za maeneo ya Frati na walihakikisha kuwa na amani upande wa Kaskazini na Mashariki. Wakati ule, washirika wa Wahiti wa Hati na Kalti (Waseltiki) walienea tangia kaskazini mwa ile ijulikanayo leo kuwa ni Lebanoni, hadi kaskazini mwa Uturuki, hadi kwenye mipaka ya nchi za Mesheki na Tubali kaskazini na kuelekea upande wa mashariki mwa Kaspiani. Walienea kwenye maeneo yaliyobakia ya uliokuwa zamani ufalme wa Wilusia na mji wa Troy, ambalo liliangamizwa kwenye miaka ya mwisho ya utawala wa Eli akiwa kama mwamuzi wa Israeli. Walichanganyika na Waisraeli kwenye ushirikiano na mshikamano tangu hapo hadi kufikia baada ya kipindi cha Israeli kwenda utumwani mnamo mwaka 722 KK. Waashuru walipeleka Makabika Kumi kaskazini katikati yao na Waseltiki wakiwa kama ngao ya kujilinda. Waisraeli waliporudi walijichanganya na waliunda sehemu ya ushirikiano na Waparthi Waseltiki huko Scythia kwa sababu ya hawa washirika wa zamani sana. Hatimaye waliingia Ulaya katika karne ya pili BK.

 

Siku hizi wapo kwenye makundi ya watu wenye lugha mbalimbali walioenea maeneo yote ya Kaskazini-Magharibi mwa Ulaya, walitofautishwa tu kwa vipimo vyao vya nasaba vya YDNA Makundi ya Haplo au Haplogroups lakini yanamwingiliano wa kidamu kwa upande wa nasaba ya mwanamke ijulikanayo kama mtDNA. Waselkiti Wahiti na Makabila Kumi Yaliyopotea au Yaliyotawanyika sasa ni yote wana wawili wote wa Ibrahimu (soma majarida ya Chimbuko la Kijenetiki la Mataifa (Na. 265) na  Vita Vya Hamon-Gogu (Na. 294) [The Genetic Origin of the Nations (No. 265) and War of Hamon-Gog (No. 294)].

 

Uongozi katika Utawala wa Sulemani

1Wafalme 4:1-34 Basi mfalme Sulemani akawa mfalme juu ya Israeli wote. 2 Na hawa ndio wakuu aliokuwa nao; Azaria mwana wa Sadoki, kuhani, 3 Elihorefu na Ahiya, wana wa Shausha, waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe; 4 na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya jeshi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani; 5 na Azaria mwana wa Nathani alikuwa juu ya maakida; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki wake mfalme. 6 Na Ahishari alikuwa juu ya nyumba; na Adoramu mwana wa Abda alikuwa juu ya shokoa. 7 Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli wote, walioleta chakula cha mfalme na nyumba yake; kila mtu alikuwa na mwezi mmoja katika mwaka kuleta chakula.

 

Kwahiyo, makabila haya kumi na mbili yalifundishwa jinsi ya kutoa mali zao ili kuitegemeza nyumba hii iliyokuwa huko Yerusalemu kwa utaratibu wa kuwapangia kila kabila moja kwa mwezi mmoja. Kwa namna hiyohiyo, makuhani na Walawi waligawanywa kwenye makabila kwa msingi wa migawanyo miwili kwa kila kabila, na hawa walipokea zaka pia kutoka kwa makabila hayo na walitoa zaka ya zaka kwenye Hekalu la Yerusalemu, amazo zilikuwa chini ya Sadoki.

 

Sehemu za nyingeza za 1 na 2 za jarida hili inaelezea Kizazi cha ufalme wa Misri kinachohusiana na maandiko ya Biblia na kwenye vipindi maalumu  vya Ufunguo wa Daudi. Sehemu nyongeza ya 3 na 4 vinaelezea maana ya Ukuhani wa Walawi uliowekwa kuanzia au ndani ya Hekalu, na pia pamoja na Watu Mashuhuri au Wakuu wa Israeli, walifikia idadi ya thelathini na saba na uongozi.

 

Haya ni majina ya wale maafisa kumi na mbili wa wakusanya changizo wa kila kabila.

8 Na haya ndiyo majina yao. Mwana wa Huri, mlimani mwa Efraimu. 9 Mwana wa Dekari, kutoka Makasi, na Shaalbimu na Bethshemeshi na Elon-beth-hanani. 10 Mwana wa Hesedi, katika Arubothi; na Soko ilikuwa kwake na nchi yote ya Heferi. 11 Mwana wa Abinadabu katika Nafath-dori yote; ndiye aliyekuwa naye Tafathi binti Sulemani kuwa mke wake. 12 Baana mwana wa Ahiludi, katika Taanaki na Megido, na Beth-sheani yote, iliyo kando ya Sarethani, chini ya Yezreeli, tangu Beth-sheani mpaka Abel-mehola, hata kupita Yokmeamu. 13 Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba. 14 Ahinadabu mwana wa Ido, katika Mahanaimu. 15 Ahimaasi, katika Naftali; naye ndiye aliyemwoa Basemathi binti Sulemani. 16 Baana mwana wa Hushai, katika Asheri na Bealothi. 17 Yehoshafati mwana wa Parua, katika Isakari. 18 Shimei mwana wa Ela, katika Benyamini. 19 Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, na Ogu mfalme wa Bashani; naye alikuwa akida wa pekee katika nchi hiyo. 20 Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi, wakila, na kunywa, na kufurahi. 21 Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake. 22 Na vyakula vya Sulemani vya siku moja vilikuwa kori therathini za unga wa mzuri, na kori sitini za ngano. 23 na ng'ombe kumi walionona, na ng'ombe ishirini za malisho, na kondoo mia, pamoja na ayala, na paa, na kulungu, na kuku walionona. 24 Kwani alikuwa akitawala nchi yote upande huu wa Mto, toka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa Mto; naye alikuwa na amani pande zake zote. 25 Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani. 26 Tena Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi arobaini elfu kwa magari yake, na wapandao farasi kumi na mbili elfu. 27 Na maakida wale wakaleta chakula kwa mfalme Sulemani na kwa wote walioijia meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake, kisipunguke kitu. 28 Shayiri pia na majani kwa farasi, na kwa wanyama wenye mbio, wakaleta mahali walipokuwapo, kila mtu kwa kadiri ya kazi yake. 29 Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani. 30 Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri. 31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. 32 Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. 33 Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. 34 Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake.

 

Ndipo Sulemani aliandika Kitabu cha Mithali na idadi kamili na kwa hiyo vilikuwa elfu tatu.

 

Kwa hiyo Sulemani m-botania na ni mtaalamu wa mambo ya wanyama, ndege warukao na samaki. Alifanyika kuwa mtaalamu kwenye utaratibu na kuendelea kwenye uumbaji.

 

Alipofanyika kuwa Mfalme, Hiramu wa Tiro aliazimu kuanzisha uhusiano wake na Sulemani kama alivyokuwa na Daudi. Hivi ndivyo alivyotaka kufanya Daudi na Waamoni, lakini walipumbazika sana kwa ujinga na wakamtukana na kumchokoza Daudi. Sulemani hakufanya hivyo kwa Hiramu. Badala yake alimuorodheshea na kumtumia mahitaji ya vifaa alivyokuwa anavihitaji kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu. Hapa tunaona pia kwamba Wamataifa wanaorodheshwa kwenye ujenzi wa Hekalu la Kiroho, ambalo ni Kanisa la Mungu.

 

1Wafalme 5:1-18 Ndipo Hiramu, mfalme wa Tiro, akawatuma watumishi wake kwa Sulemani; kwani alikuwa amesikia ya kwamba wamemtia mafuta awe mfalme mahali pa baba yake. Kwa maana Hiramu alikuwa akimpenda Daudi siku zote. 2 Basi Sulemani akatuma watu kwa Hiramu, akasema, 3 Umemjua Daudi baba yangu jinsi asivyoweza kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata Bwana alipowatia watu chini ya nyayo zake. 4 Ila leo Bwana, Mungu wangu, amenipa amani kila upande; hakuna adui, wala tukio baya. 5 Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu. 6 Basi uamuru wanikatie mierezi ya Lebanoni; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni. 7 Ikawa, Hiramu aliposikia maneno yake Sulemani, alifurahi sana, akasema, Na ahimidiwe Bwana leo, aliyempa Daudi mwana mwenye akili juu ya watu hawa walio wengi. 8 Hiramu akatuma watu kwa Sulemani, akasema, Nimeyasikia yale uliyoniletea; nami nitafanya kila ulitakalo katika habari ya miti ya mierezi, na miti ya miberoshi. 9 Watumishi wangu wataishusha toka Lebanoni mpaka baharini; nami nitaiendesha baharini, ikifungwa pamoja, mpaka mahali utakaponiagiza, huko nitaifungua ili wewe uichukue; ndivyo utakavyoitimiza haja yangu, ukiwapa chakula watu wa nyumbani mwangu. 10 Basi Hiramu akampa Sulemani miti ya mierezi na miti ya miberoshi kadiri alivyotaka.11 Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano, chakula cha watu wake, na kori ishirini za mafuta safi. Ndizo Sulemani alizompa Hiramu mwaka kwa mwaka. 12 Bwana akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanyana maagano pamoja hao wawili. 13 Mfalme Sulemani akafanya shokoa ya Israeli wote; nayo shokoa hiyo ilikuwa ya watu thelathini elfu. 14 Akawatuma Lebanoni kwa mwezi, elfu kumi kwa zamu. Mwezi mmoja walikuwako huko Lebanoni, na miezi miwili wakawako kwao. Na Adoramu alikuwa juu ya shokoa. 15 Sulemani alikuwa na wachukua mizigo sabini elfu, na wakatao miti themanini elfu milimani; 16 mbali na maakida yake Sulemani waliokuwa juu ya kazi, elfu tatu na mia tatu, wasimamizi wa watu waliotenda kazi. 17 Mfalme akaamuru, nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani, ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa. 18 Na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.

 

Utaratibu tu wa kushughulika na Hiramu ulikuwa ni tofauti kutoka kwenye njia mbalimbali ambazo zilikuwa ni kwa kuwatumia wafalme wenye nguvu zaidi waliokuwepo wakati huo kuwaelekea wajirani wadhaifu. Njia ya kawaida ilikuwa ni kuwadhulumu na kuwakandamiza, lakini Sulemani alimfanyia rafiki wa baba yake kwa heshima na kwamba Wamataifa wa Mataifa yote waweze kuuingia Ufalme wa Mungu, wa kuongezewa kwenye Hekalu la Mungu. Kwa jinsi hiyohiyo Wahiti wa kaskazini walijichanganya na Israeli katika miaka iliyofuatia na wakaenea Ulaya kote.

 

(Mwisho wa tepu 282C1)

 

Ufunguo wa Daudi

Kuna maandiko maalumu kuhusu masuala ya Ufunguo wa Daudi. Imeelezwa kuwa inamaanisha Kanisa la Wafiladelfia. Ahadi imefanywa na Kristo kwamba yeye ndiye mwenye huo Ufunguo wa Daudi na kwamba atautoa na kulipa Kanisa la Wafiladelfia.

Ufunuo 3:7-8 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. 8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.

 

Sasa ni kitu kimoja cha kudai kwenye jina la Kanisa la Wafiladelfia na kusema unao Ufunguo wa Daudi, na ni kitu kingine kabisa cha kuenenda kama Wafiladelfia na kutendea kazi Ufunguo na kuelezea uweza wake na maana yake. Kwa hakika, Kanisa linalibeba jina la Mungu na limepewa mlango uliofunguliwa kwa uweza wa Mungu. Hakuna mtu anayeweza kulikomesha Kanisa kutoka kwenye utendaji kazi wake. Linaitangaza jins Imani na nguvu au uweza wa Eloa kuwa ni Mungu Mmoja, Wapekee na wa Kweli.

 

Kwenye Ufunuo 3:7, tunaona kwamba Mungu anajifunua mwenyewe kuwa yeye ni Mtakatifu, nay eye aliye wa kweli, na ni yeye aliye na Ufunguo wa Daudi. Kwa hiyo, ni kwa kumuabudu yeye pekee anayeweza kuutoa Ufunguo wa Daudi. Kwenye Ufunuo 1:4, tunaona kwamba unatoka kwa Mungu, aliyekuweko na aliyeko na ajaye, na kutoka roho saba za Mungu zilizo mbele ya Kiti chake cha enzi, ambacho kimetolewa na ufunuo.

 

Kuanzia sura ya 4 ndipo kitabu hiki cha Ufunuo kinaendelea kuutangaza utakatifu wa Mungu pamoja na maneno mengine kumi na saba yaliyo kwenye Ufunuo 4:8,11; 5:9-10,12-14; 7:10,12; 11:15,17-18; 12:10-12; 14:13; 15:3-4; 19:1-8.

 

Utakatifu wa Mungu umetangazwa mapema kabla ya kuhumu iliyoandikwa kwenye Ufunuo 4:8, na kama tunavyoona kwenye Zaburi 93, 97, 99 na Isaya 6:3.

 

Kwa hiyo, ni nini hasa huu Ufunguo wa Daudi? Na una umuhimu gani kwenye kazi ya Kanisa la Siku za Mwisho?

 

Kuna mambo yaliyowazi sana kwa kweli kuhusu maisha ya Daudi ambayo yanahusisha na ufunguo na kazi yake ya Mpango wa Mungu kama unavyohusiana na Kanisa. Ufunguo ule unafungua Siri za Mungu kwa Kanisa katika Siku za Mwisho, na Kanisa la Wafiladelfia limepewa mlango ule uliofunguliwa wa kulifundisha hili, na la kuzifanya kazi za Mungu kupitia kwa Yesu Kristo na Roho Mtakatifu katika Siku za Mwisho.

 

Daudi alikuwa kigezo cha ufunguo kwenye historia ya Utawala wa Wafalme. Alizaliwa wakati wa utawala wa mfalme Sauli na akakua hadi kufanyika kuwa ni Mtiwa Mafuta wa Bwana. Alipofikia umri wa miaka thelathini aliwekwa kwenye mchakato wa kuwa mfalme na alitawala kwa kipindi cha miaka arobaini. Alimwachia ufalme wake Sulemani na kwa hiyo alikuwa hai na kushuhudia tawala zote tatu.

 

Jambo kubwa alilolifanya maishani mwake lilikuwa ni kuwaunganisha Israeli na kwa amani, na kuwakusanya kwa mkusanyo mkuu wa vifaa vya ujenzi wa Hekalu. Alipanga ujenzi wake na kuziandika Zaburi kwa ajili ya ibada. Jambo kuu lililofanyika kwenye utawala wa Daudi ni kipaumbele wake wa kulijenga Hekalu. Ingawaje yeye mwenyewe hakulijenga hilo Hekalu, lakini hata hivyo lilikuwa ni jukumu lake kwenye mchakato ule na ndio unaofanya ufunguo wa kuuelewa Mpango wa Mungu. Kulijua jukumu la Djukumu la Daudi, na maana ya wafalme kwenye mchakato ule, ndipo tunaujua Mpango wa Mungu kwenye utawala wa Yesu Kristo na kwa Makanisa ya Mungu.

 

Kuuelewa mpango na mlolongo huu wamepewa watu walioaminiwa na jambo hili na Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli, Eloa, kwenye muda aliouamua au kuupanga kuzifunua Siri za Mungu ulimwenguni. Kwa hiyo Mungu Mmoja Wapekee na wa Kweli, Eloa, ndiye anayepaswa kuabudiwa kwenye Kanisa la Wafiladelfia. Kwa hiyo wahawezi kuwa ni watu wa imani ya Kiditheist, au Wabinitariani, zaidi ya kuwa ni Wayunitariani.

 

Mungu anawapa uwezo wa kuuelewa Ufunguo huu wa Daudi watumishi wake manabii, na tunaona hilo kutoka kwa manabii kile kilichokusudiwa kwenye Ufunguo huu.

 

Nabii Isaya aliuelezea Ufunguo huu wa Daudi kwa wazi kabisa.

 

Isaya 22:17-25 Tazama, Bwana atakutupa kwa nguvu, kama mtu mwenye nguvu; naam, atakuzonga-zonga. 18 Hakika atakukunja na kukutupa kama mpira, mpaka nchi iliyo mbali; huko utakufa, na magari ya utukufu wako yatakuwa kuko huko, ewe uliye aibu ya nyumba ya bwana wako. 19 Nami nitakusukuma na kukutoa katika mahali pako, naye atakushusha utoke hapa usimamapo. 20 Na itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia; 21 nami nitamvika vazi lako, nitamtia nguvu kwa mshipi wako, nami nitamkabidhi yeye mamlaka yako; naye atakuwa baba kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa nyumba ya Yuda. 22 Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua. 23 Nami nitamkaza kama msumari mahali palipo imara; naye atakuwa kiti cha utukufu kwa nyumba ya baba yake. 24 Nao wataangika juu yake utukufu wote wa nyumba ya baba yake; wazao wake na watoto wao, kila chombo kidogo tangu vyombo vya vikombe hata vyombo vya makopo vyote pia. 25 Katika siku ile, asema Bwana wa majeshi, ule msumari uliokazwa katika mahali palipo imara utalegea; nao utakatwa na kuanguka chini, na ule mzigo uliokuwa juu yake utakatiliwa mbali; maana Bwana amesema haya.

 

Ufunguo wa Daudi kwa hiyo ni kitu kilichoelezewa kwenye unabii na kuuelewa mchakato wa Serikali ya Mungu.

 

Huhu mtu anayetajwa hapa kwenye 2Wafalme 18:18-26. Kwahiyo, Ufunguo wa Daudi aliaminiwa kupewa Eliakimu, mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa ni mkuu wa watu wa nyumbani mwake wakati wa utawala wa Hezekia wakati Waashuru walipokuja kuupiga mji wa Yerusalemu. Walipomuita Hezekia, Eliakimu alitoka nje akiwa na Shebna mwandishi na Yoa (mwana wa Asafu) aliyerekodi kama mpasha habari. Eliakimu alivirarua nguo zake wakati alipomueleza Hezekia maneno aliyoyasema Rab-shakeh mjumbe aliyetumwa na mfalme wa Ashuru, na Hezekia aliyararua mavazi yake pia na akamtuma kwa Isaya, mwana wa Amozi, nabii.

 

Isaya akayasema maneno ya unabii wa Bonde la Maono kwenye sura ya 22. Kwenye sura hii anautaja Yerusalemu na “Bonde la Maoo”, ambalo lilikuwa ni eneo ambalo karibu maono yote muhimu yamekuwa yakionyeshwa kwanza na Ibrahimu (Mwanzo 22:2,14; sawa na jina Yahova Yire; na pia ile ya Daudi kwenye 1Nyakati 21:16,28; na maono makuu ya Isaya 1:1; 6:1-4; Tafsiri ya The Septuagint inasema Sayuni). Shebna alianza kuwa mtunza hazina na alipaswa kwenda utumwani. Anaweza sana kuwa alikuwa ni mgeni au Myahudi Mmataifa. Alikengeuka na Mungu alisema kwamba atamuondolea mbali kutoka makazi yake na kumuondoa kabisa (Isaya 22:17-19).

 

Kwa hiyo kuuondoa ukengeufu na mtu wake kulihitajika katika kumuweka Eliakimu mahali pa Shebna mkengeufu.

 

Shebna ndiye aliyedhania kuwa alikuwa ni msumari kwenye nyumba ya Bwana pamoja na ufunguo wa Daudi. Hatahivyo, alipinduliwa na kuondolewa na mtumishi wa kweli wa Mungu akawekwa. Unabii unaelezea utaratibu ambao utawekwa, na manabii wa kweli wa Mungu  (ambao watakao simamishwa kama Ufunguo wa Daudi) kama walivyowekwa tangu mwanzo. Kwahiyo, manabii wa kweli wa Mungu watawekwa mahali kwenye awamu ya mwisho kabla Mashahidi hawajachukua nafasi zao (soma jarida la Mashahidi (Na. 135)). Imani ya Kanisa ambayo ilikuwa kabla yake imeingizwa, na Injili inaenea kwa mara nyingine tena na kwa wote. Mfumo na imani ihusuyo Mpango wa Wokovu na Siri za Mungu vimefunuliwa kwa ulimwengu wote kama shahidi, na hatimaye ndipo ukamilifu wa dahari utawasili.

 

Andiko hili lilikuwa linahusu utumwa na kisha marejesho ya Hekalu huko Yerusajemu chini ya nabii mwenye uelewa mkubwa, ambaye aliweza kurejesha tena taratibu za Hekaluni na kushughulika na Siri zote.

 

Kutokana na andiko hili tunaona kwamba kulitakiwa kuwe na mitawanyiko miwili na awamu mbili za marejesho ya taratibu za Hekalu. Na ndipo Ufunguo wa Daudi ueleweke vyema wakati mitawanyiko hiyo na marejesho zinapotokea na jinsi zitakavyochukuliwa. Ni wazi sana pia kwamba Marejesho ya kwanza yalipaswa kuwa ni ya Yuda chini ya kuhani aliyechaguliwa. Hezekia alihusika na marejesho haya lakini ndivyo alivyokuwa pia Yosia, na pia baada ya mtawanyiko au utumwa kulikuwa na kina Nehemia na Ezra, kama tunavyoona hapa pamoja na Hezekia na Eliakimu. Marejesho yaliyofanyika hadi kuzaliwa kwa Kristo yameelezewa kwenye jarida la Pasaka Kuu Saba za Biblia (Na.107).

 

Kwahiyo kulikuwa na Mahekalu mawili; moja lilikuwa la kipindi cha Sulemani hadi kipindi cha Utumwa wa Babeli, na Hekalu la Pili ni la kuanzia ujenzi uliofanywa na utawala wa Dario II akiwatumia kina Ezra na Nehemia hadi Kubomolewa kwake mwaka 70 BK (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Tena wa Hekalu (Na. 13)).

 

Marejesho ya mwisho yatakuwa ni ya Hekalu la Tatu na la Mwisho. Awamu hii itakuwa kwenye kipindi ambacho Kanisa itakuwa likihudumu katika Siku za Mwisho. Utaratibu wa Wafiladelfia unaelezea mchakato wa mapema kabla ya kurudi kwa Masihi na hatimaye litauendeleza hadi kuja kwa Masihi atakapokuja kuanzisha Ufalme wa Mungu hapa Duniani. Kutakuwa na awamu mbili za marejeshonhaya kwa namna zote mbili, yaani ya Hekalu la Kiroho na kisha marejesho ya kimwili ya Hekalu la Kimwili huko Yerusalemu, na uanzishwaji wa mfumo wa kidini kwa utawala wa hii dunia kama ilivyotabiriwa na nabii Ezekieli.

 

Tunaona jinsi Ufunguo wa Daudi kuwa ni kufunguliwa kwa Siri za Mungu zihusuao Hekalu, na ujenzi wake wote likiwa kama nyumba au hekalu ya kiroho ambalo ni Kanisa la Mungu ambamo Mungu hufanya makao kwa uweza na nguvu za Roho Mtakatifu.

 

Tutajionea sasa maana ya siku na mlolongo wa matukio yaliyo kwenye ufunuo wa Mungu.

 

Hekalu Linaanzishwa

Tunaona kwamba katika mwaka wa 480 baada ya wana wa Israeli kuja kutoka Misri ndipo Hekalu lilisimikwa. Israeli walikuwa kwenye nchi yao kwa kipindi cha miaka 440 (au mizunguko kumi na moja ya vipindi vya toba) nab ado Hekalu lilikuwa halijaanza kujengwa bado. Lilianza kujengwa mwaka 968/7 KK katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Mfalme Sulemani.

 

Israeli walitangatanga kwa kipindi cha miaka 40 jangwani na tena miaka 436 ya kuwa chini ya Waamuzi (soma jarida la Samsoni na Waamuzi (Na. 73)), na kisha wakawa chini ya Sauli na Daudi; na sasa miaka minne chini ya Sulemani.

 

Jinsi inavyofanana na Kutoka

Tukio la Kutoka kutoka utumwani Misri lilitokea mwaka 1448/7 KK. Kama tukichukua kronolojia ya mwanzoni kabisa inavyosema kwamba kungemfanya Farao aliyekuwepo kipindi cha Kutoka, aitwaye Amenhotep II (1450-1412 KK). Kama tutaichukulia kronolojia ya kusema au kuitaja Oxford kisha Farao huyu ni Thumoses III. Sanamu ya Karnak Stele iliyosimamishwa na mtoto wa Amenhotep II aliyeitwa Thutmose IV anayeongelea kuhusu kampeni ya mwaka wa 2 wa utawala wa baba yake (1448 KK angekuwa kwa mwaka ule wa utawala wake uliochegama kwenye kronolojia ya zamani au mwanzoni kabisa). Pale alinukuliwa kuwa na ushindi dhidi ya Asiatics, lakini rekodi ya mateka ni jambo linaloumiza sana (walikuwa wepesi kwa kupiga pinde au mishale, nk.) na ni janga la wazi kwao. Inaonekana kuwa alizirudisha tu nyuma vilivyopotea vichache.

 

Huyu Karnak Stele anasema aliwateka watu 18 na farasi 16. Katika mwezi wa tisa wa Wamisri wa mwaka wa 2 aliteka farasi 2, gari la vita 1, koti la masanduku. pinde 2 na podo ya mishale na koseleti na kitu kisichojulikana kisicho na umuhimu.

 

Kisha, kwenye mwezi uliofuatia, alikumbana na uasi alipokuwa anarudi eneo la Misri ya kati miongoni mwa na askari walinzi wa mji wa watu wachanga kwa wale waliokuwa wanaishi humo. Ananukuu hili kama ushindi pia, lakini alikuwa ni Thutmoses IV ambaye alifanya hivyo baada ya kifo cha baba yake. Mtazamo huu unafanana na tukio la Kutoka utumwani lilivyokuwa. Matukio haya hayana maana ya kuwa ni rekodi ya ushindi.

 

Baada ya kukumbana na uasi alijaribu kuokoa sura yake. Inaonekana ni kana kwamba hatimaye aliishambulia Gaza baada ya tukio la janga la Kutoka na aliwarudisha wanaume 550, na wake zao wapatao 240, na pia nyingine kilogramu 612 za dhahabu na tani 45 za shaba.

 

Hii imetuama kwenye kronolojia ya mwanzoni zaidi. Hata hivyo, mtazamo huu sasa unapingwa. Haifanyi utofauti wowote kwa namna yoyote kama alivyofanya Farao kwenye tukio la Kutoka kwa tawala zao zote mbili zingejumuisha tukio la Kutoka utumwani kwa jinsi zinavyojulikana na wao.

 

Jila Musa linatokana na familia ya Kizazi cha Kifalme cha 18 cha Misri. Inaonekana, kwa nyaraka za kumbukumbu za zamani, kwamba Amenhotep II alimridhi baba yake katika mwaka wa 39 wa kipindi cha Musa kutorokea huko Midiani. Musa alikuwa na umri wa miaka 79. Baba wa Amenhotep alikuwa Thutmoses III Mekhepere.

 

Mama mlezi wa Musa alikuwa ni binti wa Ahmose I Nebpehtyre (mnamo mwaka 1570-1546) mwanzilishi wa Kizazi cha Kifalme cha 18, na kwamba Musa alipewa jina hilo kwa ukweli huo. Musa alizaliwa mwaka 1528 KK. Kutegemea kronolojia iliyotumika, ilikuwa ama kwenye utawala wa Amenhotep I Djesekare (tarehe za mwanzoni za takriban mwaka 1546-1527) aliyekuwa mjomba mlezi wa Musa, au kwenye utawala wa Amosis I, ambaye anaonekana kuwa ni mtajwa sahihi kwenye kronolojia. Kwa hiyo angekuwa amekwisha kufa wakati Musa akiwa karibu na umri wa miaka miwili. Thutmose I Akheperkare alirithi na alirithiwa na Thutmose II Akheperence. Alimrithi Malkia Hatshepsut Maakare (soma Jarida la Nyongeza 1 kwa kupata ufafanuzi zaidi). Alitawala kama mtawala mwenza na mpwa wake kijana aliyeitwa Thutmose III baada ya kufa kwa Thutmose II mwaka 1498. Mambo yaliyowekwa kwenye kabrasha tangu miaka ya 1960-1970 zinasema kwamba Thutmose III alitawala kwa pamoja kishirikisho na Thutmose II tangu mwaka 1504 hadi 1498 KK. Hii ilituama kwenye utawala dhaifu wa miaka 35 wa Thutmosis IV (ibid.). kronolojia ya kisasa inasema kwamba Thutmose III alitawala tangu mwaka 1479-1425.

 

Ni kwa hiyo ni kiinimacho kabisa kudai kwamba Musa alimjua Farao wa kipindi cha Kutoka kabisa kuliko kwa kwa jina, hadi alipojitokeza mbele zake. Ukweli huu na mchakato wake unaweza kupunguzwa kutoka kwenye kina chake iliyotolewa hapa kuhusu Hekalu, kwa kuwazidisha na kupatikana kwa wataalamu wa mambo kale wa sasa.

 

Hekalu lilianza kujengwa katika mwezi wa Pili wa Zivu au wa Iyari wa mwaka wa 480 tangu kipindi cha Kutoka kwao utumwani. Mwezi wa Pili ulihitajika kwa ajili ya mchakato wa kulitabaruku au kuliweka wakfu Hekalu katika Mwezi wa Kwanza kama inavyohitajika kwa mujibu wa Torati.

 

Tukio la Kutoka lilitokea mwaka wa 26 wa Yubile ya 51. Huu ulikuwa ni mwaka wa tano wa mzunguko wa Yubile, mwaka wa Neema wakati Torati ilipotolewa pale Sinai.

 

Hekalu lilianza mwaka wa Sita wa mzunguko wa kwanza wa Yubile ya 61 tangu kufungwa kwa bustani ya Edeni, mwaka wa Yubile ya mwaka 3974 KK. Kipindi chenyewe kilikuwa ni cha miaka 3006 kamili ya tangu kufukuzwa kwa Adamu na hatimaye kufuatiliwa na Yubile kwenye alama ya nusu njia ya utawala wa Shetani. Hii ni kufanya au kuweka alama ya marudio ya uumbaji kwenye Mpango wa Mungu. Kwa jinsi ya kwamba, hii ni kukebehi utukufu wa jinsi ya kumuabudu Mungu Jua ambapo kwenye majira ya solisaiti ambapo jua linaanza kucha kwake katika kuabudu kwenye Dini ya Siri ya Shetani.

 

Kwahiyo, miaka 480 inafanya kuwa ni mwanzo wake. Ilichukua miaka ishirini kukamilisha kazi ya kulijenga Hekalu na nyumba ya mfalme, na kazi iliisha kwa kipindi cha miaka 500 tangu tukio la Kutoka utumwani. Ilichukua miaka saba na miezi saba kukamilisha ujenzi wa Hekalu lenyewe, lakini ni miaka ishirini kwa ujumla. Kwahiyo, kipikuwa ni kipindi cha Yubile kumi kamili tangu kuondolewa kwa Israeli wakiwa kama taifa teule la Mungu kutoka Misri hadi kukamilika kwa Hekalu la kwanza la kimwili, na kuanzishwa kwa taifa la Israeli kuwa ni kituo muhimu cha ibada huko Yerusalemu.

 

Kilikuwa ni kipindi hikihiki maalumu tangu kurejeshwa upya chini ya Ezra na Nehemia hadi kwenye kutanngazwa kwa mwaka wa Yubile chini ya Kristo, na kuanzishwa kwa Kanisa kutoa Yerusalemu.

 

Majuma Sabini ya Danieli 9:25 na kuendelea ilienda kwenye ujenzi wa Hekalu hadi kwenye kubomolewa kwake na mtawanyo mwishoni mwa miaka 490, na Yubile iliona miaka 497 ya mzunguko wake (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13)).

 

Siku 1263.5 za Mashahidi zimeongezwa kama kifungu cha kipindi hiki mwishoni mwake. Hivi ni vile vinara viwili vya dhahabu vinavyosimama mbele za mungu wa Dunia hii.

 

Tangu kipindi cha Ezra hadi Kristo na kwenye Milenia ni Yubile 49, kinaishia mwaka 2027.

 

Huduma ya Kristo, kama mwana wa Daudi, ilianza mwaka wa 28 BK na ni Yubile Arobaini zilizopewa dunia kwa ajili ya toba inayoishia kwenye Yubile ya 120 ya mwaka 2027. Mapema kabla ya kipindi hiki, Mashahidi watafanya kazi hapa Duniani huko Yerusalemu liliko Hekalu. Watahubiri kwa kipindi cha siku 1260 na watauawa na maiti yao kulazwa mjini humo kwa siku tatu na nusu, baada ya hapo watafufuliwa. Hii ni alama ya mwisho kutokea kabla ya kuja kwa Masihi na kuanza utawala wake kwa utukufu.

 

Mwaka 2028 utakuwa ni mwanzo wa Yubile ya Hamsini au Yubile ya Dhahabu, ambayo ni Yubile ya Yubile pia ya tangu Kujengwa Tena kwa Hekalu likiwa kama Hekalu la kimwili kujengwa huko Yerusalemu.

 

Kwahiyo Yubile ya Dhahabu ni Yubile ya Kwanza ya utaratibu wa millennia. Kipindi kile kinatumika kwa kuanzisha tena Hekalu la kimwili na miongozo ya Torati ya Mungu itakayotoka huko Yerusalem. Ulimwengu utakuwa karibuni kuangamizwa wote mnamo mwaka wa 2027. Yubile ya kuanzia mwaka 2028 hadi 2077 itaishuhudia Dunia ikirejeshwa upya kwenye utukufu wake wote, pamoja na maongozi ya kambi ya watakatifu huko Yerusalemu.

 

Kurudi kwao kutoka Babeli chini ya Ezra na Nehemia kwa ajili ya Usomaji wa Torati, na marejesho mapya ya mji wa Yerusalemu kwa ajili ya Hekalu la Pili, kulifanya mwanzo wa mchakato wa kuelekea kipindi na huduma ya Kristo kwa namna hiyohiyo kama ilivyotokea kwenye tukio la Kutoka kulikofanya mwanzo chini ya Musa hadi kwenye kukamilisha kwa Hekalu la Kwanza huko Yerusalemu. Kipindi hiki kilishuhudia kubomolewa au kuangamizwa kwa Hekalu la kimwili na mgawanyiko wake.

 

Zitakuwa ni Yubile hamsini kamili tangu Marejesho yaliyofanywa na kina Nehemia na Ezra hadi kwenye kipindi cha uanzishwaji wa utawala wa millennia chini ya Kristo na ujenzi wa Hekalu la Milenia. Kuna Yubile ya arobaini na tisa hadi kufikia mwaka 2027. Yubile ya Hamsini itakuwa mwaka 2028 hadi 2077. Kwenye Yubile hiyo ujenzi wa Nyumba za ibada na utawala mpya uataanza rasmi huko Yerusalemu. Hekalu la Milenia, au Nyumba ya Kumuabadia Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli katika utawala wa Masihi amoja na elohim ambao ni wateule litakuwa limeisha wakati wa Yubile hiyo.

 

Kutendo cha kuyatiisha mataifa na kuyatakasa kitafanyika kwa kipindi cha miaka 21 ya mwisho ya yubile ya 120, ambacho ni tangu mwaka 2006 hadi kwenye Idi ya Upatanisho ya mwaka 2027 (soma jarida la Utakaso wa Mataifa (Na. 77)).

 

Marejesho ya utawala yatafanyika tangu kipindi hiki, Kristo ataudi mapema kabla ya kipindi hiki ili kuja kuwaokoa wateule. Na kama hatarudi kipindi hiki ili kukifupisha, hakutakuwa na hata mwenye mwili atakayeokoka au atakayekutwa akiwa hai (soma majarida ya Miaka Thelathini ya Mwisho: Pambano la Mwisho (Na. 219) na Miaka Arobaini Iliyotolewa kwa Ajili ya Toba (Na. 290)).

 

Hekalu la Kwanza

Daudi alimwachia utawala wake Sulemani katika mwaka wa Kwanza wa Yubile ya 61. Maandalizi yalianza ili kwamba Hekalu liweze kujengwa kwa matayarisho ya Usomaji wa Torati katika Yubile ile. Iligharimu miaka ishirini kuumaliza ujenzi wa Nyumba ya Mungu na nyumba ya Mfalme pamoja na nyumba nyinginezo (tazama hapo chini). Kukamilika kwake zote kulifanywa katika mwaka wa 25 wa Yubile ya 61.

 

Hekalu lilianza kujengwa katika mwaka wa Arobaini wa utawala wa Sulemani, ambao ni mwaka 968 KK.

 

Ujenzi wote na umliziaji wa Nyumba ya Mungu na nyumba majengo mengine shirika kulikamilika katika mwezi wa Saba uitwao wa Ethanimu, au Tishri, na Sikukuu ilifantika kwa muda wa siku 14.

 

Ni kama tulivyoona hapo chini, ujenzi wenyewe hasa wa jengo lenyewe ulichukua miaka saba na miezi saba na ulikamilika mwezi wa Nane wa mwaka wa Kumi na Moja wa utawala wa Sulemani. Ukamilishaji huu ulikuwa wa kwamba sio wakati wa Sikukuu ya Vibanda ya mwaka ule. Kwa hiyo, kuna maana nyingine kwa kuwepo kipindi hiki. Hekalu lilifuatia baada ya Pasaka, katika mwezi wa Pili wa mwaka wa Nne wa Sulemani na liliisha katika mwezi wa Nane wa Buli au wa Heshavan (Oktobea/Novemba ya mwaka wa 487 tangu Kutoka kwao utumwani, mwaka 961 KK).

 

Kipindi hiki chenye mlolongo kinafanya pia sehemu ya ufunguo wa Dausi. Vipindi maalumu vilivyoelezwa kwa kutenganishwa pia vina maana yake kwenye kipindi cha Siku za Mwisho cha tangu kurudi kwa Masihi hadi kujengwa kwa Hekalu la Kiroho, na ukamilishaji wa mwisho wa muundo wa kihandisi wa Hekalu ka huko Yerusalemu.

 

Mnamo mwaka wa 28 wa Yubile, Torati ilisomwa kwenye Nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Kipindi chote cha ujenzi kilichukua miaka 21 cha Utakso wa Hekalu. Mnamo mwaka wa Sabato ndipo ilikuwa tayari. Mwaka wa 29 ulifuatia miaka mingine 21 ya kipindi kilichoelekea kwenye Yubile, na ndipo taifa lilitakaswa katika kipindi kile pia. Kwa hiyo ilikuwa ni miaka elfu tatu hadi kuanza kwa utawala wa millennia wa Yesu Kristo kwene Yubile ya 120 ya uumbaji na tangu kufungwa kwa bustani ya Edeni, ambapo ni sawa na mwaka 2027 BK.

 

Yubile ntingine 60 zinazofuatia zilikuwa ni za ujenzi wa mfumo wa kimwili na mpito wake wa kuelekea kwenye utaratibu wa kiroho wa Kanisa na wa serikali ya Mungu. Ni dhahiri sana kwamba Mungu anafanya mambo yake kwa kuutilia maanani mfumo huu wa Yubile na anavitumia vipindi vya Yubile kwa kuendana na tarakimu za miaka ya 10, 20 na 40.

 

Kutoka kwenye mandiko ya Agano la Kale ni wazi sana kwamba Masihi alipaswa kuhudhuria na kujulikana katika Yubile ya mwaka 27 BK na huduma yake kuanza rasmi mwaka 28 BK. Alipaswa afe ili kuwaokoa wenye dhambi. Ni sawa kabisa kwamba ilimpasa kufanya Upatanisho na alipaswa kurudi akiwa kama Masihi Mfalme. Kipindi kile maalumu kilichukua kipindi chote cha miaka elfu sita ya uumbaji wa Mungu na kuishia kwenye Yubile ya 120 ambayo ni mwaka 2027.

 

Tangu wakati ule kipindi cha Utawala wa Masihi kingefuatia tangu mwaka 2028 hadi 3027, yakiwa ni mapumziko ya Sabato ya Masihi. Baada ya kipindi hicho itafuatia Hukumu ya wote ikifuatiwa na Ufufuko wa Wote au wa Wafu.

 

Maandiko yanasomeka hivi:

1Wafalme 6:1-38 Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya Bwana. 2 Nayo nyumba hiyo mfalme Sulemani aliyomjengea Bwana, urefu wake ulikuwa mikono sitini, na upana wake ishirini, na kwenda juu kwake mikono thelathini. 3 Na ukumbi mbele ya hekalu la nyumba, urefu wake ulikuwa mikono ishirini, kadiri ya upana wa nyumba; na upana wake mikono kumi mbele ya nyumba. 4 Akaifanyia nyumba madirisha ya miangaza yenye kimia. 5 Nao ukuta wa nyumba akauzungushia vyumba, kushikamana na kuta za nyumba kote kote, za hekalu na za chumba cha ndani; akafanya vyumba vya mbavuni pande zote. 6 Chumba cha chini kilikuwa mikono mitano upana wake, na chumba cha katikati kilikuwa mikono sita upana wake, na chumba cha tatu kilikuwa mikono saba upana wake; kwa kuwa upande wa nje akaupunguza ukuta wa nyumba pande zote, ili boriti zisishikamane kutani mwa nyumba. 7 Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba. 8 Mlango wa vyumba vya chini ulikuwapo upande wa kuume wa nyumba; mtu hupanda madaraja ya kuzunguka mpaka vyumba vya katikati, na kutoka vile vya katikati mpaka vile vya tatu. 9 Basi ndivyo alivyoijenga nyumba, akaimaliza; akaifunika nyumba kwa boriti na mbao za mwerezi. 10 Akavijenga vyumba mbavuni mwa nyumba yote, kwenda juu kwake kila kimoja kilikuwa mikono mitano; vikaitegemea nyumba kwa boriti za mwerezi.

 

Habari za Hekalu zilifanywa tayari mahali pengine pote na zililetwa kwenye uwanja wa ujenzi. Kwa jinsi hiyohiyo habari za kuishi au kuwepo zilifanywa tayari mbali kutoka Yerusalemu na kuletwa kule kwa ajili ya kuanzishwa kwa Hekalu la Kiroho atakaporudi Kristo. Ni wakamilifu na hawahitaji kujengwa kwenye uwanja fulani wakiwa kama matofali ya jengo yaliyounganishwa pamoja.

 

Kwa hiyo kuna michakato miwili katika ujenzi: mmoja ni kwenye ujenzi wa Mawe yaliyo Hai; mwingine ni ule wa utaratibu wa kimwili ulio chini ya maongozi ya Torati kutoka Yerusalemu.

 

Katika ujenzi huu wa Hekalu ndipo neno la Mungu lilimjia Sulemani, akafanya agano na Israeli ambalo sharti kale lilikuwa ni utiifu.

 

11 Neno la Bwana likamjia Sulemani, kusema, 12 Katika habari ya nyumba hii unayoijenga, kama ukienda katika sheria zangu, na kuzifanya hukumu zangu, na kuzishika amri zangu zote na kwenda katika hizo; ndipo nitakapolithibitisha neno langu kwako, nililomwambia Daudi baba yako. 13 Nami nitakaa katikati ya wana wa Israeli, wala sitawaacha watu wangu Israeli. 14 Basi Sulemani akaijenga hiyo nyumba akaimaliza. 15 Akazijenga kuta za nyumba ndani kwa mbao za mwerezi; toka sakafu ya nyumba hata boriti za juu, akazifunika ndani kwa mti; akafunika sakafu ya nyumba kwa mbao za mberoshi. 16 Akajenga mikono ishirini pande za nyuma za nyumba toka chini hata juu kwa mbao za mwerezi; naam, ndani akaijengea chumba cha ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu. 17 Nayo nyumba, ndiyo hekalu la mbele, ilikuwa mikono arobaini. 18 Na ndani ya nyumba, mlikuwa na mwerezi ulionakishiwa maboga na maua yaliyofunuka wazi; mlikuwa na mwerezi mahali pote; wala mawe hayakuonekana. 19 Akaweka tayari chumba cha ndani katikati ya nyumba ndani, ili atie humo sanduku la agano la Bwana. 20 Na ndani yake chumba hicho cha ndani mlikuwa na nafasi, mikono ishirini urefu, na mikono ishirini upana, na mikono ishirini kwenda juu kwake; akaifunika na dhahabu safi. Akaifunika madhabahu nayo kwa mwerezi. 21 Hivyo Sulemani akaifunika nyumba ndani kwa dhahabu safi. Akaitenga kwa mikufu ya dhahabu mbele ya chumba cha ndani; akapafunika na dhahabu. 22 Akaifunika nyumba yote kwa dhahabu, hata ilipokwisha nyumba yote; tena madhabahu yote iliyokuwa ya chumba cha ndani akaifunika kwa dhahabu. 23 Akafanya ndani ya chumba cha ndani makerubi mawili ya mzeituni, kwenda juu mikono kumi. 24 Na bawa moja la kerubi lilikuwa mikono mitano urefu wake, na bawa la pili la kerubi mikono mitano; mikono kumi toka mwisho wa bawa moja hata mwisho wa bawa la pili. 25 Na kerubi la pili lilikuwa mikono kumi; makerubi yote mawili walikuwa ya cheo kimoja na namna moja. 26 Kwenda juu kwake kerubi moja kulikuwa mikono kumi, na kerubi la pili vivyo. 27 Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani; na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko; mabawa yao yakagusana katikati ya nyumba. 28 Akayafunika makerubi kwa dhahabu. 29 Akazinakshi kuta zote za nyumba kwa nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, pande za ndani na nje. 30 Na sakafu ya nyumba akaifunika na dhahabu ndani na nje. 31 Akayafanyia maingilio ya chumba cha ndani milango ya mzeituni; kizingiti na miimo ilikuwa ya pande tano. 32 Hivyo akafanya milango miwili ya mzeituni; akanakshi juu yake nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, akaifunika kwa dhahabu; akatia dhahabu juu ya makerubi, na juu ya mitende. 33 Ndivyo alivyoyafanyia maingilio ya hekalu miimo ya mzeituni, yenye pande nne; 34 na milango miwili ya mberoshi; mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa za kukunjana, na mbao mbili za mlango wa pili za kukunjana. 35 Akanakshi juu yake makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi; akazifunika kwa dhahabu iliyonyoshwa juu ya machoro. 36 Akaijengea behewa ya ndani safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi. 37 Katika mwaka wa nne nyumba ya Bwana ilitiwa msingi, katika mwezi wa Zivu. 38 Hata katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, na sharti zake zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.

 

Huu ulikuwa ni mchakato wa kwanza wa ufunguo wa Daudi na unahusiana na utaratibu wa kwanza, ambao ni Nyuma au Maskani ya Mungu na Mawe yaliyo Hai; na mlolongo ule unahusiana na kurudi kwa Masihi na hitimisho lake kwa Mataifa.

 

Nyumba ya Sulemani

Nyunba ya Sulamani ilijengwa kwa kipindi cha miaka kumi na tatu, kisha aliijenga Nyumba ya Misitu ya Lebanoni pia. Hekalu ndiyo ilikuwa juhudi yake kubwa na ilichukua miaka ishirini kuimalizia. Pia alimchukua binti Farao na kumleta nyumbani mwake.

 

Mlolongo huu, kama tunavyouona, ulichukua miaka saba na miezi saba kujenga Nyumba ya Mungu na kisha miaka kumi na tatu kuijenga Nyumba ya Mfalme na Ukumbi wa kutolea Hukumu, na Nyumba ya Misitu ya Lebanoni.

 

1Wafalme 7:1-51 Naye Sulemani alikuwa katika kuijenga nyumba yake mwenyewe miaka kumi na mitatu, akaimaliza nyumba yake yote. 2 Kwa kuwa aliijenga nyumba ya mwitu wa Lebanoni; mikono mia urefu wake, na mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake, juu ya safu nne za nguzo za mwerezi, na mihimili ya mwerezi juu ya nguzo. 3 Ikafunikwa juu kwa mwerezi juu ya mihimili arobaini na mitano, iliyokuwa juu ya nguzo; kumi na mitano kwa safu. 4 Na madirisha yalikuwako safu tatu, mwangaza kuelekea mwangaza katika madaraja matatu. 5 Na milango yote na miimo ilikuwa ya mraba, ilivyoangaziwa; na mwangaza kuelekea mwangaza katika madaraja matatu. 6 Akaifanya baraza ya nguzo; mikono hamsini urefu wake, na mikono thelathini upana wake; na ukumbi mbele yake; na nguzo na mihimili minene mbele yake. 7 Akaifanya baraza ya kiti cha enzi, ili ahukumu ndani yake, ndiyo baraza ya hukumu; nayo ikafunikwa mwerezi tangu sakafu mpaka dari. 8 Nayo nyumba yake atakayokalia, katika behewa nyingine iliyokuwa ndani kupita baraza, ilikuwa ya kazi kama hiyo. Tena akamjengea nyumba binti Farao, (ambaye Sulemani alikuwa amemwoa), mfano wa ile baraza. 9 Hizi zote zilikuwa za mawe ya thamani, mawe ya kuchongwa, sawasawa na cheo, yaliyokatwa kwa misumeno, ndani na nje, tangu msingi hata mawe ya juu, na nje vile vile hata behewa kuu. 10 Nao msingi ulikuwa wa mawe ya thamani, mawe makubwa, mawe mikono kumi, na mawe ya mikono minane. 11 Na juu kulikuwa na mawe ya thamani, mawe ya kuchongwa, sawasawa na cheo, na mierezi. 12 Na behewa kubwa pande zote ilikuwa na safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi; mfano wa behewa ya ndani ya nyumba ya Bwana, na ukumbi wa nyumba.

 

Hiramu alisaidia kazi hii ya ujenzi. Huyu Hiramu ambaye pia ni Mfalme wa Tiro alikuwa nusu ni Muisraeli. Baba yake alikuwa ni mtu wa Tiro na mama yake alikuwa ni mjane wa kabila la Naftali. Na zaidi sana ni kwamba alikuwa ni mshirika wa kuaminika na mataifa ya Israeli leo kama tunavyojionea kwenye maandiko yaliyotajwa hapa.

13 Mfalme Sulemani akatuma watu kumleta Huramu kutoka Tiro. 14 Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila ya Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, mstadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikilia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote. 15 Kwa maana alizifanyiza zile nguzo mbili za shaba, mikono kumi na minane kwenda juu kwake kila moja; na uzi wa mikono kumi na miwili kuizunguka nguzo hii au hii. 16 Akafanya taji mbili za shaba iliyoyeyushwa za kuwekwa juu ya vichwa vya nguzo; kwenda juu kwake taji moja mikono mitano, na mikono mitano kwenda juu kwake taji ya pili. 17 Kulikuwa na nyavu kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa taji zilizokuwako juu ya vichwa vya nguzo; saba kwa taji moja, na saba kwa taji ya pili 18 Hivyo akazifanya nguzo; na kulikuwa na safu mbili za kuzunguka juu ya wavu mmoja, zifunike taji zilizokuwako juu ya vichwa vya nguzo; akafanya vivyo hivyo kwa taji ya pili. 19 Na taji zilizokuwa juu ya nguzo ukumbini zilikuwa za kazi ya mayungi, mikono minne. 20 Kulikuwako tena taji juu ya nguzo mbili, karibu na uvimbe uliokuwako kando ya wavu; na makomamanga yalikuwa mia mbili, safu safu pande zote juu ya taji ya pili. 21 Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kuume, akaiita jina lake Yakini; akaisimamisha nguzo ya kushoto ,akaiita jina lake Boazi. 22 Na juu ya nguzo kulikuwa na kazi ya mayungi; hivyo mambo ya nguzo yakatimia. 23 Tena akaifanya bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ikaviringana, na mikono mitano ilikuwa kwenda juu kwake; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa. 24 Na chini ya ukingo wake kulikuwa na maboga yaliyoizunguka, kwa mikono kumi, yakiizunguka bahari; kulikuwa na safu mbili za hayo maboga, yakafanywa kalibuni hapo bahari ilipofanywa. 25 Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani. 26 Na unene wake ulikuwa nyanda nne; na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu mbili. 27 Akayafanya yale matako kumi ya shaba; mikono minne urefu wa tako moja, na mikono minne upana wake, na mikono mitatu kwenda juu kwake. 28 Na kazi ya matako ndiyo hii; yalikuwa na papi; na papi zilikuwa katikati ya vipandio; 29 na juu ya papi zilizokuwa katikati ya vipandio kulikuwa na simba, na ng'ombe, na makerubi; na juu ya vipandio kulikuwa na tako; na chini ya simba na ng'ombe kulikuwa na masongo ya kazi ya kupembeza. 30 Kila tako lilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vipini vya shaba; na miguu yake minne ilikuwa na mataruma; chini ya birika yalikuwako mataruma ya kusubu, yenye masongo kila moja mbavuni. 31 Na kinywa chake ndani ya taji na juu yake kilikuwa mkono mmoja; na kinywa chake kikaviringana kama kazi ya tako, mkono mmoja na nusu; tena juu ya kinywa chake kulikuwa na nakshi, na papi zao zilikuwa za mraba, wala hazikuviringana. 32 Na magurudumu manne yalikuwa chini ya papi; na mikono ya magurudumu ndani ya tako; na kwenda juu kwake gurudumu moja mkono mmoja na nusu. 33 Na kazi ya magurudumu ilikuwa kama kazi ya gurudumu la gari; mikono yake, na maduara, na matindi, na vipande vya ndani, vyote vilikuwa vya kusubu. 34 Kulikuwa na mataruma manne katika pembe nne za tako moja; mataruma hayo ni kitu kimoja na tako lenyewe. 35 Na juu ya tako kulikuwa na duara nusu mkono kwenda juu kwake; na juu ya tako mashikio yake na papi zake vilikuwa vya namna iyo hiyo. 36 Akachora juu ya mabamba ya mashikio yake, na juu ya papi zake, makerubi, na simba, na mitende, moja moja kama ilivyokuwa nafasi, na masongo pande zote. 37 Hivyo akayafanya yale matako kumi; yote yalikuwa ya kalibu moja, na cheo kimoja, na namna moja. 38 Akafanya birika kumi za shaba; birika moja huingia bathi arobaini; na kila birika ilikuwa mikono minne; birika moja juu ya tako moja, katika yale matako kumi. 39 Akayaweka yale matako, matano upande wa kuume wa nyumba, na matano upande wa kushoto wa nyumba; akaiweka ile bahari upande wa kuume wa nyumba upande wa mashariki, kuelekea kusini. 40 Tena Huramu akazifanya birika, na majembe, na mabakuli. Hivyo Huramu akazimaliza kazi zote alizomfanyia mfalme Sulemani katika nyumba ya Bwana; 41 zile nguzo mbili, na vimbe mbili za taji zilikuwa juu ya nguzo; na nyavu mbili za kuzifunika hizo vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo; 42 na makomamanga mia nne ya zile nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuzifunika hizo vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo; 43 na yale matako kumi, na birika kumi juu ya matako; 44 na ile bahari moja, na ng'ombe kumi na wawili chini ya ile bahari; 45 na masufuria, na majembe, na mabakuli; hata vyombo hivyo vyote, Huramu alivyomfanyia mfalme Sulemani, katika nyumba ya Bwana, vyote vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa. 46 Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sarethani. 47 Sulemani akaviacha vyombo vyote visipimwe kwa kuwa vilikuwa vingi mno; wala uzito wa shaba haukujulikana. 48 Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Bwana; madhabahu ya dhahabu, na ile meza iliyokuwa na mikate ya wonyesho juu yake ilikuwa ya dhahabu; 49 na vinara vya taa, vitano upande wa kuume, na vitano upande wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu safi; na maua, na taa, na koleo ya dhahabu; 50 na vikombe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu safi; na bawaba za dhahabu, za milango ya nyumba ya ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu, na za milango ya nyumba, ndiyo hekalu. 51 Hivyo ikamalizika kazi yote Sulemani mfalme aliyoifanya katika nyumba ya Bwana. Sulemani akaviingiza vile vitu alivyovitakasa Daudi baba yake, yaani, fedha, na dhahabu, na vyombo; akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Bwana.

 

Majina ya nguzo za Hekalu yametokana majina ya Waisraeli wawili. Mmoja wao ni Yakini wa kabila la Simeoni, na ni baba wa Wakini. Wapili alikuwa ni Boazi wa kabila la Yuda. Habari za huyu Boazi zinajulikana sana. Alikuwa ni mume wa Ruthu na baba yake Obedi na Yese na Daudi na hatimaye Masihi (soma jarida la Ruthu (Na. 27)). Jina lake la Boazi (SHD 1162) linatokana na chanzo kisichojulikana wala kutumika na lenye maana fulani na anaonekana tu kuwa alihusiana na mtu huyu, babu wa Daudi. Kwa vokali mbalimbali inaweza kuhusiana na kuwa aliyetiwa nguvu.

 

Jina la Yakini (Yachin, SHD 3199) maana yake ni Yeye atakayefanya au Yah (au kwa ukamilifu zaidi ni Yaho[va]) atafanya na anaweza kuwa tayari sana kuona kama kigezo cha maana ya jina katika Mungu kuwa ni kama Mmoja atakayeanzilisha.

 

Ingawa hatuwezi kuondoa ukwell wa kwamba kama Wasimeoni walivyotawanyika katika Israeli, anaweza pia kuwa na baba wa Daudi, na kwamba Daudi aliziita nguzo zote mbili kwa majina ya mababa imara na hodari wa mstari wake wa kiuzao wakiwa kama mifano ya Imani.

 

Ni sawa kabisa na kwamba mfano wa majina huonyesha na kushiria jambo kwenye jkumu la Mungu kwenye ujenzi wa Hekalu la Kirohola Mungu.

 

Huku wakati jina la Boazi kiliwa halina maana iliyo wazi sana, inaelezewa pia na kazi yake ya ukombozi kwenye hadhithi ya Ruthu. Kwa hiyo, nguzo hizi mbili zilizo kwenye lango la kuingilia Hekaluni zinamaana ya: Yeye atiaye nguvu (Bullinger anasema: katika yeye au ndani yake kuna nguvu) na anawezesha au anafanya. Maana hizo zinaonyesha kwenye kiini cha matendo yenyewe ya ujenzi ya Hekalu la mwisho la Mungu.

 

Pia yana maana yake maalumu na vipimo vyake vimepewa kwa tofauti mbalimbali kwenye idadi kadhaa ya maandiko. Huku sio kujikanganya au sio mkanganyiko, bali zaidi sana ni kwamba ni tofauti ya jinsi ya zilivyokuwa zimepimwa.

 

Kwenye 1Wafalme 7:15-16, nguzo hizi mbili zinaelezewa kupimwa mikono 18 kwenda juu, na mikono kumi na mbili mzunguko wake. Zile kubwa za katikati zilikuwa na mikono 5.

 

Jumla ya nguzo na zile kubwa kwa hiyo ziilikuwa mikono 23 kwenda juu na mikono 12 duara

 

Tunadhani kwamba nguzo zote mbili ya kulingana na linaitwa tu kama kuonyesha vipimo vya urefu na duara kwa nguzo zote mbili. Yeremia 52:21-22 inatoa kikamilifu urefu huohuo kwa nguzo na egemezo zake. 2Wafalme 25:17 inasema nguzo hizi zilikuwa 18 kwenda juu, pamoja na mikono 3 kwa zile kuu. Kipimo kwa mibahatisho yote zisizojumuisha urembo wa jani, ambalo lilikuwa aina ya lili kama ilivyoelezewa kwenye maandiko (1Wafalme 7:22).

 

Andiko lililo kwenye 2Nyakati linazipa nguzo kipimo cha pamoja mikono 35 na dhira mikono 5 kwa zile kubwa. Kwa hiyo, nguzo zilikuwa mikono 35 kwa mikono 17.5 kila moja na nusu mkono kwa kuungakila moja na nusu mkono kwa kiungo, nakiwiko au kiegemezo zilikuwa mikono 5.

 

Wafafanuzi wanatathimini tu nia ya andiko. Namba arobaini ni tarakimu ya toba, na nguzo zinaashiria ukombozi wa Mungu na uanzilishi kwa kipindi cha toba kilichotolewa kwa kila mmoja. Nguzo zinawakilisha naendeleo ya mwanadamu kwa uingiliaji kati wa Mungu. Kiwango cha kipimo cha chokaa ya kujengea kilikuwa kila nguzo ni 1 kwa 6 jumlisha 2/3, ambayo ni kipimo cha kibinadamu kwa mwili hadi kichwani, kwa karibia 1 ya 7.

 

Kombe za nguzo zimetofautiana kivipimo. 1Wafalme 7:20 inasema kwamba makomamanga yaliyowekwa kwenye kombe za nguzo yalikuwa ni mia mbili kwenye mistari zikizunguka sura zote. Nguzo iliyokuwa upande wa kuume ilikuwa Yakini na ile ya upande wa kushoto ilikuwa Boazi. Inazidi kwenda chini kwenye aya ya 42 inasema zilikuwa mia mbili ili kuonyesha kuwa mia mbili hizi zilichukuliwa kwa kila kuu (soma pia 2Nyakati 4:13). Kwenye 2Nyakati 3:16 waliitwa mia moja, maana yake, walikuwa mia moja kwenye kila mstari. Yeremia 52:23 inasema kwamba mistari hadi kwenye Ruach au chamchela (kama ilivyofunuliwa) ni 96.

 

2Nyakati pia inaendelea mbele kwa kusema kwamba uwa ulikuwa wa mikono 120, kwa kutumia me’ah (SHD 3967) na 'esriym (SHD 6242). 1Wafalme 6:2-3 inasema kwamba Hekalu lilikuwa mikono 60 urefu, mikono kumi na mbili upana wake na mikono thelathini kwenda juu. Inasema pi kwamba uwa ulikuwa na mikono 20 urefu, na kwa mujibu wa upana kwa upande wa mbele ya nyumba (kama vile kuingia kwenye uwa) ulikuwa mikono 10. Ipo kimya kama kwenye urefu wa kwenda juu kwake wa uwa, na watu hudhani kwamba ulikuwa na urefu ule ule kama umbo la Hekalu lakini maandiko yanasema urefu wake ulikuwa mara nne urefu wa kwenda juu wa umbo Hekalu. Uwa uliokuwa na mikono 120 uliashiria kipindi cha kuwepo kwa uumbaji wa kimwili kwa zama hizi uliopimwa kwa Yubile. Tarakimu ile ilimaanisha pia maisha ya Musa kama tulivyojionea kwenye vitabu vya Torati. Maisha ya Musa yaligawanyika kwa sehemu tatu ya miaka arobaini arobaini, na yalionelana pia kwenye awamu tatu za Utawala wa Wafalme. Tarakimu ya “thelathini” yenye umbo kuu inaashiria serikali ya ndani ya Mungu, na pia umri wa kumudu kuufikia kabla ya mtu hajapewa majukumu ya huduma yam zee wa kusanyiko la Mungu.

 

Vidato sita vya kuingilia vinaashiria mizunguko sita ya kwanza kwenye maisha ya mwanadamu. Kidato cha saba, ambacho kilikuwa ni umbo la Hekalu lenyewe, kilishiria mzunguko wa mwisho wa Sabato ya Yubile aliyopewa mwanadamu. Inampasa mwanadamu awe na umri wa miaka ishirini ndipo ahesabiwe kuwa ni mtu mzima na aweze kwenda vitani. Inampasa mtu awe na umri wa miaka ishirini na tano ndipo aruhusiwe kuzifanya huduma za Hekaluni, na miaka thelathini ahudumu kama mzee kwenye mkutano wa Mungu.

 

Mwanadamu amepewa Yubile moja akiwa mtu mzima ya kuendeleza karama na tabia za Roho Mtakatifu. Musa aliishi na kuziona Yubile mbili. Daudi alifariki akiwa na umri wa miaka sabini, ikiashiria kupungua kwa kipindi cha kuziona Yubile na hadi kuwa moja tu. Alimkabidhi mamlaka yake Sulemani kabla hajafa, ikiwa ni ishsra ya utaratibu wa mwendelezo wa mamlaka kwa Mtiwa Mafuta wa Bwana.

 

Patakatifu pa Patakatifu palikuwa ni Naos, ambayo iliwakilisha mwaka wa mwisho wa maisha ya mwanadamu na wakati mtu amejipatia kuwa ushirika na Mungu. Ndipo Naos iliwakilisha hatua ya mwanadamu kuendelea wakati Mungu alipoingia kwa mwanadamu kwa Roho Mtkatifu na kumuinua juu ili kuwa elohim. Na ndiyo maana Agano Jipya linatuita sisi kuwa ni Naos, “ambao ni Naos yulivyo” (1Wakorintho 3:17).

 

Meza na mikate ya uwonyesho, na vile vinara kumi vya taa vilisimama kwa maendeleo ya Kanisa la Mungu kwa kipindi chote lilicopewa Kanisa kwenye hatua au awamu zake saba likiwa chini ya malaika wa makanisa saba.

 

Wale wengine watatu waliwakilisha vinara ambavyo vilikuwa ni Masihi na Mashahidi Wawili (soma jarida la Mashahidi (Na. 135)).

 

The Holy of Holies contained the Ark of the Covenant and the Law of God, where the Law was enshrined in the hearts of men who had become the Temple of God.

 

Birika la bahari la Hekaluni lilikuwa na kipimo cha mikono thelathini mzunguko wake na mikono kumi ya kotekote na kwa hiyo Mungu alikionyesha kipimo cha ukubwa wa kizingo (1:3) kwenye ukubwa. Ilikuwa nje ya Nyumba ya Mungu kama ilivyokuwa madhabahu, ili kuashiria kwamba Kristo alikufa nje ya kambi akiwa ni sadaka au dhabihu na ni mara moja tu na kwa wote ili sisi sote tupate kutakasika na kukombolewa kwa Mungu.

 

Ukubwa wa kipimo vha Hekalu ulionyesha pango wa Wokovu na ukombozi wa mwanadamu kwa Mungu. Mchakato wa ujenzi wake uliendana na mpango ule na uliionyesha hii kwenye kila kipande cha maendeleo yake. Ufunguo wa Daudi ni kitendo cha kuzielewa au kuzijua na kuzifundisha Siri za Mungu kwa mujibu sawa na utaratibu wa Yubile uliotplewa kwayo, na kuwsza kutabiri sawasawa na mafundisho yenye uzima, na sawasawa na Torati na Ushuhuda.

 

Kuliweka Sanduku la Agano Hekaluni

Mara tu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Hekalu, Sanduku la Agano lililetwa na kuingizwa Hekaluni, ili kwamba Mungu aonekane akiwa katikati yao. Lililetwa katika mwezi wa Ethanimu ambacho ni kitendo kinachoashiria Ujio wa Masihi na Mfalme na Mtawala wa hii Dunia akiwa kama Nyota ya Asubuhi.

 

1Wafalme 8:1-66 Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni. 2 Wakakutana mbele ya mfalme Sulemani watu wote wa Israeli wakati wa sikukuu, katika mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi wa saba. 3 Wazee wote wa Israeli wakaja, nao makuhani wakajitwika sanduku. 4 Wakalipandisha sanduku la Bwana, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwa katika ile Hema; vitu hivyo makuhani na Walawi wakavipandisha. 5 Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli waliokutanika kwake, walikuwako pamoja naye mbele ya sanduku, wakichinja sadaka kondoo na ng'ombe, wasioweza kuhesabiwa wala kufahamiwa idadi yao kwa kuwa wengi. 6 Makuhani wakalileta sanduku la agano la Bwana hata mahali pake, katika chumba cha ndani cha ile nyumba, patakatifu pa patakatifu, naam, chini ya mbawa za makerubi. 7 Kwa maana makerubi yalinyosha mbawa zao, juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu. 8 Na ile miti kwa kuwa mirefu, ncha za miti zilionekana katika mahali patakatifu, mbele ya chumba cha ndani; lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo. 9 Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili za mawe ambazo Musa aliziweka ndani huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka katika nchi ya Misri.

 

Kwa hiyo bao za Torati ziliwekwa kwenye Sanduku la Agano ili kuashiria ukweli wa kwamba Mungu alikuwa ameziweka Sheria zake kwenye mioyo ya watu wote na waiifantika kuwa kituo cha katikati cha mahali pa makao yake kama Naos au Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu la Mungu. Na ndiyo maana ilibidi Sanduku hili la Agano lisiletwe tena, kama ni Sanduku lililo mioyoni mwa wateule walio kwenye Makanisa ya Mungu.

 

10 Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya Bwana ikajaa wingu; 11 hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya Bwana ilikuwa imejaa utukufu wa Bwana. 12 Ndipo Sulemani akanena, Bwana alisema ya kwamba atakaa katika giza nene. 13 Hakika nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele. 14 Mfalme akageuza uso wake, akawabariki mkutano wote wa Israeli; na mkutano wote wa Israeli wakasimama. 15 Akasema, Bwana, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena na Daudi baba yangu kwa kinywa chake akalitimiza kwa mkono wake, akasema, 16 Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wo wote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nalimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli. 17 Basi ilikuwa moyoni mwake Daudi, baba yangu, kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 18 Lakini Bwana akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako. 19 Lakini wewe hutanijengea nyumba hiyo; ila mwanao atakayetoka katika viuno vyako, yeye ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu. 20 Basi Bwana amelitimiza neno lile alilolinena; nami nimesimama mahali pa Daudi baba yangu, na kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama Bwana alivyoahidi, nami nimeijenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 21 Na humo sanduku hili nimelifanyizia mahali, ambalo ndani yake mna maagano ya Bwana, aliyoyafanya na baba zetu, hapo alipowatoa katika nchi ya Misri. 22 Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana, machoni pa mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake mbinguni. 23 Akasema Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni juu wala duniani chini; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa mioyo yao yote. 24 Umemtimizia mtumishi wako, Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia; naam, ulinena kwa kinywa chako, ukayatimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo. 25 Na sasa, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, umfikilizie mtumishi wako, Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia, ukisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli machoni pangu, kama watoto wako wakiangalia njia zao, ili kuenenda mbele zangu kama wewe ulivyoenenda. 26 Sasa, Ee Mungu wa Israeli, nakusihi, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako, Daudi, baba yangu. 27 Lakini Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga! 28 Walakini uyaelekee maombi ya mtumwa wako, na dua yake, Ee Bwana, Mungu wangu, uisikilize sauti na maombi ya mtumwa wako, aombayo mbele zako leo. 29 Macho yako yafumbuke na kuielekea nyumba hii usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa. 30 Uisikie dua ya mtumwa wako, na ya watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, sikia huko mbinguni, makao yako; nawe usikiapo, samehe. 31 Ikiwa mtu amemkosa mwenzake, na kupewa sharti ya kiapo aapishwe, naye akija na kuapa hapa mbele ya madhabahu yako, katika nyumba hii; 32 basi, usikie huko mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumwa wako; ukimpatiliza mtu mbaya, kwa kuleta njia yake juu ya kichwa chake; na kumpa mwenye haki haki yake, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake. 33 Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea tena kwako, na kulikiri jina lako wakikuomba na kukusihi katika nyumba hii; 34 basi, usikie huko mbinguni, ukawaachilie watu wako Israeli dhambi yao, ukawarejeze tena katika nchi uliyowapa baba zao. 35 Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, wakati ule utakapowatesa; 36 basi, usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; unapowafundisha njia iliyo njema, iwapasayo kuiendea; ukanyeshe mvua juu ya nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi wao. 37 Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao; au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote; 38 maombi yo yote au dua yo yote ikifanywa na mtu awaye yote, au na watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu maradhi ya moyo wake, na kuikunjua mikono yake kuielekea nyumba hii; 39 basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukatende, ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote); 40 ili wakuche wewe siku zote watakazoishi katika nchi uliyowapa baba zetu. 41 Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako; 42 (maana watasikia habari za jina lako kuu, na za mkono wako ulio hodari, na za mkono wako ulionyoshwa); atakapokuja na kuomba kuielekea nyumba hii; 43 basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukatende kwa kadiri ya yote atakayokuomba mgeni huyo; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe kama watu wako Israeli, nao wajue ya kuwa nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa jina lako. 44 Ikiwa watu wako watoka kwenda kupigana na adui zao, kwa njia yo yote utakayowapeleka, wakikuomba, Bwana, kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 45 basi, uyasikie huko mbinguni maombi yao na dua yao, ukaitetee haki yao. 46 Ikiwa wamekutenda dhambi, (maana hakuna mtu asiyetenda dhambi), hata ukawaghadhibikia, ukawatia katika mikono ya adui zao, wawachukue mateka mpaka nchi ya adui zao, iliyo mbali au iliyo karibu; 47 basi, wakijirudia nafsi zao katika nchi ile watakayochukuliwa mateka, wakitubu, na kukusihi katika nchi ya hao waliowachukua mateka, wakisema, Tumekosa, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu; 48 watakaporejea kwako kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya adui zao, waliowachukua mateka, wakikuomba, kwa kuikabili nchi yao, uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 49 basi, uyasikie maombi yao na dua yao, huko mbinguni, makao yako, ukaitetee haki yao; 50 ukawasamehe watu wako waliokutenda dhambi, na makosa yao yote waliyokukosa; ukawape kuonewa huruma mbele yao waliowachukua mateka, ili wapate kuwahurumia. 51 Kwa kuwa ni watu wako, na urithi wako, uliowatoa katika Misri, toka katikati ya tanuu ya chuma. 52 Macho yako na yafumbuke, na kuielekea dua ya mtumwa wako, na dua za watu wako Israeli, ukawasikilize kila wakati watakapokulilia. 53 Kwa maana uliwatenga na watu wote wa dunia, wawe urithi wako, kama ulivyonena kwa mdomo wa Musa, mtumishi wako, hapo ulipowatoa baba zetu katika Misri, Ee Bwana MUNGU. 54 Hata ikawa, Sulemani alipokwisha kumwomba Bwana maombi hayo, na dua hiyo yote, akasimama na kuondoka hapo mbele ya madhabahu ya Bwana, hapo alipokuwa amepiga magoti, na kuikunjua mikono yake kuelekea mbinguni. 55 Akasimama, na kuwabariki mkutano wote wa Israeli kwa sauti kuu, akasema, 56 Na ahimidiwe Bwana, aliyewapa watu wake Israeli kustarehe, vile vile kama yote aliyoyaahidi. Halikukosa kupatikana neno lo lote katika ahadi yake njema, aliyoahidi kwa mkono wa Musa, mtumishi wake. 57 Bwana, Mungu wetu, na akae nasi, kama alivyokaa na baba zetu; asituache, wala asitutupe; 58 aielekeze mioyo yetu kwake, ili tuende katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na sheria zake, na hukumu zake, alizowaamuru baba zetu. 59 Na maneno yangu haya, niliyoyaomba mbele za Bwana, na yawe karibu na Bwana, Mungu wetu, mchana na usiku, ili aitetee haki ya mtumishi wake, na haki ya watu wake Israeli, kwa kadiri ya haja zao za kila siku. 60 Watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa Bwana ndiye Mungu; hakuna mwingine. 61 Mioyo yenu na iwe kamili kwa Bwana, Mungu wetu, kuenenda katika sheria zake, na kuzishika amri zake, kama ilivyo leo. 62 Ndipo mfalme, na Israeli wote pamoja naye, wakatoa sadaka mbele za Bwana. 63 Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea Bwana, ng'ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Bwana. 64 Siku ile ile mfalme akaitakasa behewa ya katikati iliyokuwa mbele ya nyumba ya Bwana; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za Bwana ilikuwa ndogo, haikutosha kuzipokea sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na mafuta ya sadaka za amani. 65 Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, kutoka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, mbele za Bwana, Mungu wetu, siku saba na siku saba, yaani siku kumi na nne. 66 Hata siku ya nane akaagana na watu, nao wakambarikia mfalme, wakaenda hemani kwao, wakifurahi na kuchangamka moyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi mtumishi wake, na Israeli watu wake.

 

(Mwisho wa Tepu 282C2)

 

Agano ililowekwa na Sulemani

Malaika wa Mungu, mjumbe wa Mungu wa Israeli tumjuaye leo kama Kristo (Zaburi 45:6-7; Waebrania 1:8,9), alimtokea Sulemani na akaliweka Agano la Mungu pamoja naye na kwa Taifa zima lote. Agano hili lilikuwa na masharti yake fulani. Waliambiwa kuwa wangeadhibiwa iwapo kama wangeliacha na kulivunja.

 

1Wafalme 9:1-28 Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya, 2 basi, Bwana akamtokea Sulemani mara ya pili kama alivyomtokea huko Gibeoni. 3 Bwana akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote; 4 na wewe, ukienda mbele zangu kama alivyokwenda Daudi, baba yako, kwa ukamilifu wa moyo, na kwa adili, kufanya hayo yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, 5 ndipo nitakapokifanya imara kiti cha ufalme wako juu ya Israeli milele; kama nilivyomwahidia Daudi, baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Israeli. 6 Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, tena mkienda na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, 7 basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote. 8 Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini Bwana ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya? 9 Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu Bwana ameleta mabaya haya yote juu yao. 10 Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alizijenga zile nyumba mbili, nyumba ya Bwana na nyumba yake mfalme, 11 (basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya. 12 Naye Hiramu akatoka Tiro kuitazama hiyo miji Sulemani aliyompa; wala haikumpendeza. 13 Akasema, Miji gani hii uliyonipa, ndugu yangu? Akaiita nchi ya Kabuli, hata leo. 14 Hiramu akamletea mfalme talanta sitini za dhahabu. 15 Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, na Megido, na Gezeri. 16 Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda akautwaa Gezeri, na kuuteketeza kwa moto, akawaua Wakanaani waliokaa mjini, akampa zawadi binti yake, mkewe Sulemani. 17 Naye Sulemani akaujenga Gezeri, na Beth-horoni wa chini, 18 na Baalathi, na Tamari ulio nyikani, katika nchi; 19 na miji yote ya hazina iliyokuwa yake Sulemani; na miji ya magari yake, na miji ya watu wake wapandao farasi, na kila alichopenda kujenga Sulemani huko Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake. 20 Kwa habari ya watu wote waliosalia, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi, wasiokuwa wa wana wa Israeli; 21 watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo. 22 Lakini wa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu shokoa; ila ndio watu wa vita, na wangoje wake, na wakuu wake, na akida zake, na wakuu, wa magari yake, na wa wapanda farasi wake. 23 Hao maakida wakuu, waliokuwa juu ya kazi yake Sulemani, walikuwa mia tano na hamsini, waliowaamuru watu watendao kazi. 24 Lakini binti Farao akapanda toka mji wa Daudi, mpaka hiyo nyumba yake Sulemani, aliyomjengea; kisha, aliijenga Milo. 25 Na mara tatu kila mwaka Sulemani alikuwa akitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu aliyomjengea Bwana akafukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu iliyokuwako mbele za Bwana. Hivyo akaimaliza nyumba. 26 Tena, mfalme Sulemani akaunda merikebu huko Ezion-geberi, ulioko karibu na Elothi, pwani ya Bahari ya Shamu, katika nchi ya Edomu. 27 Naye Hiramu akatuma merikebuni watumishi wake, wanamaji wenye kuijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani.28 Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.

 

Kwa hivyo ndivyo ilivyo pia lwamba andiko la kwenye kitabu cha Nyakati linaelezea mchakato wa Hekalu na Agano hili lilivyowekwa na Taifa.

 

2Mambo ya Nyakati 2:1-18 Basi Sulemani alikusudia kujenga nyumba kwa jina la Bwana, na kuujengea ufalme wake nyumba. 2 Sulemani akahesabu watu sabini elfu wawe wachukuzi wa mizigo, na watu themanini elfu wawe wachongaji milimani, na elfu tatu na mia sita wawe wasimamizi wao. 3 Sulemani akatuma watu kwa Hiramu mfalme wa Tiro,akisema ,kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, na kumletea mierezi , ajijengee nyumba ya kukaa ,unitendee na mimi. 4 Angalia, najenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wangu, ili kumfanyia wakfu, ya kufukizia mbele zake fukizo la manukato, na ya mkate wa wonyesho wa daima, na ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na za siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa za Bwana, Mungu wetu. Hili ni agizo la milele kwa Israeli. 5 Nayo nyumba nitakayoijenga ni kubwa; kwa sababu Mungu wetu ndiye mkuu juu ya miungu yote. 6 Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba, ikiwa mbingu hazimtoshi, wala mbingu za mbingu? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya kufukizia fukizo mbele zake? 7 Unipelekee basi mtu mstadi wa kazi ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya urujuani, na nyekundu, na samawi, mwenye kujua kuchora machoro, pamoja na wastadi walioko Yuda na Yerusalemu pamoja nami, aliowaweka baba yangu Daudi. 8 Niletee tena mierezi, na miberoshi, na miti ya msandali kutoka Lebanoni; maana najua ya kwamba watumishi wako hujua sana kuchonga miti Lebanoni; na tazama, watumishi wangu watakuwa pamoja na watumishi wako, 9 ili wanitengenezee miti kwa wingi; kwani nyumba nitakayoijenga itakuwa kubwa ajabu. 10 Na tazama, nitawapa watumishi wako, wachongaji wakatao miti, kori ishirini elfu za ngano iliyopondwa , na kori ishirini elfu za shayiri , na bathi ishirini elfu za mvinyo,na bathi ishirini elfu za mafuta. 11 Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akajibu kwa waraka, aliompelekea Sulemani, Ni kwa sababu Bwana awapenda watu wake, amekufanya uwe mfalme juu yao. 12 Hiramu akasema tena, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, aliyezifanya mbingu na nchi, ambaye amempa mfalme Daudi mwana wa hekima, mwenye busara na akili, ili amjengee Bwana nyumba, na nyumba kwa ufalme wake. 13 Na sasa nimemtuma mtu mstadi, mwenye akili, yaani, Hiramu baba yangu. 14 mwana wa mwanamke wa binti za Dani, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, ajuaye sana kazi ya dhahabu, na ya fedha, ya shaba, ya chuma, ya mawe, na ya mti, ya urujuani, ya samawi, na ya kitani safi, na ya nyekundu; tena mstadi wa kuchora machoro yo yote, na wa kufikiri fikira yo yote; apate kuagiziwa kazi pamoja na watu wako wastadi, tena na wastadi wa bwana wangu Daudi baba yako. 

 

Kama Hiramu alikuwa nusu ni Muisraeli, ndivyo pia walivyokuwa wale mafundi na waimbaji aliowaleta. Baba yake alikuwa pia ni Hiramu na mbunifu alikuwa ni mtu wa baba yake. Mtu Yule alikuwa ni kutoka mwanamke wa kabila la Dani, na ni mtu wa Tiro. Kuhusika kwa wanawake wa Israeli lakini ni mwingiliano wa kindoa au kuoana na Wamataifa waliosababisha kuingia kwa Wamataifa kwenye shughuli za ujenzi wa Hekalu. Ukweli huu ulikuwa unaashiria asili ya aina ntingi ya Israeli katika Siku za Mwisho na kwamba wokovu ulikusudiwa kwa Wamataifa.

 

15 Basi sasa hiyo ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, aliyonena bwana wangu, na wapelekewe watumishi wake; 16 nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaichukua Yerusalemu. 17 Ndipo Sulemani akawahesabu wageni wote waliokuwamo katika nchi ya Israeli, sawasawa na hesabu aliyowahesabu Daudi baba yake; wakatokea mia hamsini na tatu elfu, na mia sita. 18 Akaweka katika hao sabini elfu wawe wachukuzi wa mizigo, na themanini elfu wawe wachongaji milimani, na wasimamizi elfu tatu na mia sita, ili wawatie watu kazini.

 

Kulikuwa na wageni 153,600 katika Israeli na waliwekwa kwenye kazi ya ujenzi kama wakusanya michango. Wanaume elfu saba walikuwa ni wabeba mizigo, 80,000 walikuwa wachonga mawe milimani na 3,600 walikuwa manyapara au wasimamizi. Kwa hiyo Wamataifa wote waliokuwa ndani ya Israeli walitumiwa kwenye shughuli za ujenzi. Ndipo wokovu ulienea hadi kwa Wamataifa ulimwenguni kote.

 

2Mambo ya Nyakati 3:1-17 Ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, juu ya mlima Moria, pale Bwana alipomtokea Daudi babaye alipotengeza mahali pale alipoagiza Daudi, katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi. 2 Akaanza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa kutawala kwake. 3 Basi hii ndiyo misingi ya majengo ya nyumba ya Mungu aliyoiweka Sulemani. Urefu wake kwa mikono ya cheo cha kwanza ulikuwa mikono sitini, na upana wake mikono ishirini. 4 Na ukumbi uliokuwa mbele yake, urefu wake kadiri ya upana wa nyumba ulikuwa mikono ishirini, na kwenda juu kwake mia na ishirini; akaufunikiza ndani kwa dhahabu safi. 5 Nayo nyumba kubwa akaifunika miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, akaifanyizia mitende na minyororo. 6 Akaipamba nyumba kwa vito iwe na uzuri; nayo dhahabu ilikuwa dhahabu ya Parvaimu. 7 Tena, akaifunikiza kwa dhahabu nyumba, na boriti, na vizingiti, na kuta zake, na milango yake; akachora makerubi kutani. 8 Akaifanya nyumba ya patakatifu pa patakatifu; urefu wake kadiri ya upana wa nyumba, ulikuwa mikono ishirini, na upana wake mikono ishirini; akaifunikiza kwa dhahabu safi, ya talanta mia sita. 9 Na uzani wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Akazifunikiza orofa zake za juu kwa dhahabu. 10 Na ndani ya nyumba ya patakatifu pa patakatifu akafanyiza makerubi mawili ya kuchonga; wakayafunikiza kwa dhahabu. 11 Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili. 12 Na bawa la kerubi la pili lilikuwa mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la kwanza. 13 Yakaenea mabawa ya makerubi hayo mikono ishirini; yakasimama juu ya miguu yao, na nyuso zao ziliielekea nyumba. 14 Akalifanya pazia la samawi na urujuani na nyekundu, na kitani safi, akaifanyizia makerubi. 15 Tena akafanya mbele ya nyumba nguzo mbili za mikono thelathini na tano kwenda juu kwake, na taji iliyokuwa juu yake moja moja ilikuwa mikono mitano. 16 Akafanya minyororo ndani ya chumba cha ndani, akaiweka juu ya vichwa vya nguzo; akafanya makomamanga mia, akayaweka juu ya hiyo minyororo. 17 Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kuume, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kuume Yakini, na jina la ile ya kushoto Boazi.

 

Ni kwa kupitia wokovu wa Mungu ndipo tunaingia kwenye Hekalu la Mungu. Makerubi wanakilinda kiti cha enzi cha Mungu na wanawakilisha Makerubi wa wa teule na wa aina ya Malaika. Makerubi walioonyeshwa kwenye Hekalu la nabii Ezekieli wanaonyesha kwamba ni Makerubi wawili waliowekwa au kwenye upande wa mitende ambaye ni Kristo, wanaweka mtu na kerubi mwenye kichwa cha simba wa Malaika Muasi, aitwaye Shetani na Aeon mwenye kichwa cha simba. Hawa elohim ni Ibrahimu na Musa, ambao ni Elohim wawili pekee waliotajwa kwenye maandiko ya vitabu vya Mwanzo na Kutoka.

 

Wakati kwamba Ibrahimu na Musa ni wawili peke yao waliotajwa kuwa ni Elohim, kwenye tukio la kutokewa na watu wa kale alioonyeshwa Yesu, watu wawili, walionekana ambao ni Musa na Eliya (Mathayo 17:3). Kwa hiyo tunaweza kudhania kwamba kulikuwa na takriban viumbe wanne waliohusika kwenye mwandamano huu wa matuki, ambao ni Henoko, Ibrahimu, Musa na Eliya na huenda na watu wengine wawili ambao hawajatajwa au kuonekana bado.

 

2Mambo ya Nyakati 4:1-22 Tena akafanya madhabahu ya shaba, mikono ishirini urefu wake, na mikono ishirini upana wake, na mikono kumi kwenda juu kwake. 2 Tena akaifanya bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ya mviringo, na kwenda juu kwake ilikuwa mikono mitano; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa. 3 Na chini yake palikuwa na mifano ya ng'ombe, walioizunguka pande zote ,kwa mikono kumi,wakiizunguka pande zote ile bahari. Ng`ombe walikuwa safu mbili ,wakayeyushwa hapo ilipoyeyushwa hiyo bahari. 4 Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani. 5 Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu tatu, kukaa ndani yake. 6 Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kuume, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea. 7 Akavifanya vinara vya taa kumi vya dhahabu, kadiri ya vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kuume, na vitano upande wa kushoto. 8 Akafanya na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kuume, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia ya dhahabu. 9 Tena akaufanya ua wa makuhani, na ua mkubwa, nayo milango yake, akaifunikiza kwa shaba milango yake. 10 Nayo bahari akaiweka upande wa kuume kwa mashariki, kuelekea kusini. 11 Na Huramu akayafanya masufuria, na majembe, na mabakuli. Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu; 12 zile nguzo mbili, na vimbe, na taji mbili zilizokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuzifunika vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo; 13 na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuzifunika vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo. 14 Akayafanya na matako, na mabirika akafanya juu ya matako; 15 bahari moja, na ng'ombe kumi na wawili chini yake. 16 Masufuria pia, na majembe, na nyuma, na vyombo vyake vyote, Huramu akamfanyia mfalme Sulemani kwa nyumba ya BWANA ,vya shaba iliyokatuka. 17 Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda. 18 Ndivyo alivyovifanya Sulemani vyombo hivyo vyote, vingi sana; kwa kuwa uzani wa shaba ulikuwa hautafutikani. 19 Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho; 20 na vinara na taa zake, ziwake kama ilivyoagizwa mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu iliyosafika; 21 na maua, na taa, na makoleo, ya dhahabu, ndiyo dhahabu bora; 22 na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.

 

Dhahabu haikuwa kitu adimu na haikuwa na gharama kubwa kipindi cha utawala huu. Na ndivyo ilivyo kwamba wa wateule wanapaswa kuwa watakatifu na kusafishwa na wenye kuthaminika na kufundishika.

 

2Mambo ya Nyakati 5:1 Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya Bwana. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu.  

 

Kulikuwa na vitu vilivyotakiwa kwenye maandalizi, na hizi ailipaswa kuletwa kwenye Hekalu wakati lilipokamilika. Kwa hiyo kulikuwa na vitu vilivyotumiwa kwenye ujenzi kwa ajili ya matumizi baada ya awamu ya kwanza ya ujenzi ikiwa imekamilika.

 

2Mambo ya Nyakati 5:2 Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.

 

Wakati Hekalu lilipokuwa tayari limeisha ndipo Sanduku la Agano lilipoletwa huko Yerusalemu. Kwa hiyo Sanduku la Agano linawakilisha Roho Mtakatifu aliye ndani ya wateule, ambaye anaweka makao huko Yerusalemu baada ya Masihi kuikamilisha awamu ya kwanza. Wokovu ni wa Yuda pain a Yerusalemu kwenye awamu ile, kama ulivyo kwa Israeli wote.

 

2Mambo ya Nyakati 5:3-14 3 Wakakutana watu wote wa Israeli mbele ya mfalme wakati wa sikukuu, katika mwezi wa saba. 4 Wakaja wazee wote wa Israeli, nao Walawi wakajitwika sanduku. 5 Wakalipandisha sanduku, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwamo Hemani, vitu hivyo makuhani Walawi wakavipandisha. 6 Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli, waliokutanika kwake, walikuwako mbele ya sanduku, wakichinja dhabihu za kondoo na ng'ombe, wasiohesabika wala kujumlishwa kwa kuwa wengi. 7 Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi. 8 Kwa maana makerubi yalinyosha mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu. 9 Na ile miti ilikuwa mirefu, hata ncha za miti zilionekana sandukuni mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo. 10 Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri. 11 Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala hawakuzishika zamu zao; 12 tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;) 13 hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana, 14 hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.

 

Sanduku la Agano halitaletwa na kungizwa mioyoni tena (soma jarida la Sanduku la Agano (Na. 196)). Kinachokusudiwa kuonyeshwa ni kwamba Roho Mtakatifu, ambaye anafundisha Sheria na amri za Torati ya Mungu na kuwafanya watu wazielewe, ataliweka Sanduku la Agano la kimwili na atawaongoa Yuda na Israeli katika Siku za Mwisho, lakini nitu baada ya nyuma – Kanisa la Mungu – likiwa limekwisha anzishwa tayari.

 

2Mambo ya Nyakati 6:1-42 Ndipo Sulemani akanena, Bwana alisema ya kwamba atakaa katika giza nene. 2 Lakini nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele. 3 Mfalme akageuza uso wake, akawabarikia mkutano wote wa Israeli; na mkutano wote wa Israeli wakasimama. 4 Akasema, Bwana, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena kwa kinywa chake na baba yangu Daudi, akalitimiza kwa mikono yake, akasema, 5 Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji wo wote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe humo; wala sikumchagua mtu ye yote awe mkuu juu ya watu wangu Israeli; 6 lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo; na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli. 7 Basi ilikuwa moyoni mwake Daudi, baba yangu, kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 8 Lakini Bwana akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako; 9 lakini si wewe utakayeijenga nyumba hiyo; ila mwanao atakayetoka katika viuno vyako, yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu. 10 Basi Bwana amelitimiza neno lile alilolinena; nami nimesimama mahali pa Daudi baba yangu, na kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama Bwana alivyoahidi, nami nimeijenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 11 Ndimo nilimoliweka hilo sanduku, ambalo ndani yake mna agano la Bwana, alilolifanya na wana wa Israeli. 12 Akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana, machoni pa mkutano wote wa Israeli, akainyosha mikono; 13 (maana Sulemani alikuwa amefanya mimbari ya shaba, urefu wake mikono mitano, na upana wake mikono mitano, na kwenda juu kwake mikono mitatu, na kuisimamisha katikati ya ua; akasimama juu yake, akapiga magoti mbele ya mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake kuelekea mbinguni); 14 akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni, wala duniani; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa moyo wao wote; 15 uliyemtimizia mtumishi wako Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidi; naam, ulinena kwa kinywa chako, ukayatimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo. 16 Sasa, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, umfikilizie mtumishi wako Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia, ukisema, Hutakosa kuwa na mtu machoni pangu, wa kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli; wakiwa tu watoto wako wataiangalia njia yao, ili kuiendea torati yangu, kama wewe ulivyokwenda mbele zangu. 17 Basi sasa, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako Daudi. 18 Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga! 19 Walakini umwangalie mtumwa wako anayoyaomba, na kusihi, Ee Bwana, Mungu wangu, usikie kilio na maombi anayoyaomba mtumwa wako mbele zako; 20 ili macho yako yafumbuke kwa nyumba hii mchana na usiku, mahali uliponena, ndipo utakapoliweka jina lako; usikie maombi atakayoomba mtumwa wako, akikabili mahali hapa. 21 Uyasikie atakayosihi mtumwa wako, na watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, usikie toka makaoni mwako, toka mbinguni, nawe usikiapo, samehe. 22 Ikiwa mtu amemkosea mwenzake, akitiwa kiapo, aapishwe, naye akija na kuapa hapa mbele ya madhabahu yako nyumbani humu; 23 basi, usikie mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumwa wako; ukimlipiza mwovu, kumpatilizia njia yake kichwani; ukamfanyie haki mwenye haki, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake. 24 Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea kwako, na kulikiri jina lako, wakikuomba na kukusihi nyumbani humu; 25 basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watu wako Israeli, na kuwarejeza tena katika nchi uliyowapa wao na baba zao. 26 Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, uwatesapo; 27 basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; uwafundishapo njia njema iwapasayo waiendee; ukainyeshee mvua nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi. 28 Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao, au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote; 29 yo yote atakayoyaomba na kusihi mtu awaye yote, au watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu pigo lake mwenyewe, na msiba wake mwenyewe, akiinyoshea mikono nyumba hii; 30 basi usikie huko mbinguni, ukaapo, ukasamehe, ukampatilize kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote; wewe umjuaye moyo; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu); 31 ili wakuche wewe, waziendee njia zako, siku zote watakazoishi katika nchi uliyowapa baba zetu. 32 Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii; 33 basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako. 34 Ikiwa watu wako wametoka kupigana na adui zao, utakakowatuma ko kote, wakikuomba kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako;35 basi uyasikie huko mbinguni wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao. 36 Wakikukosa, (maana hakuna mtu asiyekosa), hata uwakasirikie, na kuwatia mikononi mwa adui zao, wawahamishe, na kuwachukua mateka mpaka nchi iliyo mbali au iliyo karibu; 37 basi wakikumbuka katika nchi walikohamishwa, na kutubu, na kukusihi katika nchi ya uhamisho wao, wakisema, Tumekosa, tumetenda kwa ukaidi, tumefanya maovu; 38 wakurudiapo kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya uhamisho wao, adui walikowahamisha, wakiomba na kuielekea nchi uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 39 basi uyasikie toka mbinguni, toka makaoni mwako, wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao; ukawasamehe watu wako, waliokosa juu yako. 40 Na sasa, Ee Mungu wangu, macho yako yafumbuke, nakusihi, masikio yako yakasikilize maombi yaombwayo mahali hapa. 41 Sasa, Ee Bwana, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee Bwana, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema. 42 Ee Bwana, Mungu, usiurudishe nyuma uso wa masihi wako,uzikumbuke fadhili za Daudi mtumishi wako.

 

Uponyaji uliendelea na kuenea kwa wote kwa njia ya msamaha wa dhambi. Kwa hiyo, uwekaji wakfu wa Nyumba ya Mungu ulifanyika ili kwamba Wamataoifa pia waweze kuokolewa, na ili warudi na kumuomba Mungu jambo lolote walitakalo na wapewe.

 

Baada ya Sulemani kuomba, moto ulishuka kutoma Mbinguni na kuiteketeza sadaka yote ya kuteketezwa ikiwa kama ishara ya kwamba Mungu ameyasikia na ameyakubali maombi yao. Wana wa Israeli ndipo walikuwa na moyo mkuu na kujitoa sana na kukijua kile alichowatendea Mungu. Hii ilikuwa ni miaka mia tano baada ya tukio la Kutoka kwao utumwani, Israeli walipewa tgena ishara zihusuzo uwepo wa Malaika wa Bwana kuwa yu katikati yao akiwa kama Yahova wa Israeli, ambaye ni Yesu Kristo (Zaburi 45:6-7; Heb 1:8-9).

 

2Mambo ya Nyakati 7:1-22 Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba. 2 Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa Bwana, kwa kuwa utukufu wa Bwana umeijaza nyumba ya Bwana. 3 Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa Bwana ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele. 4 Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana. 5 Mfalme Sulemani akatoa sadaka ya ng'ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na watu wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Mungu. 6 Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao pamoja na vinanda vya Bwana, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru Bwana, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama. 7 Tena Sulemani akaitakasa behewa katikati, iliyokuwa mbele ya nyumba ya Bwana; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka za kuteketezwa, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba aliyoifanya Sulemani haikutosha kuzipokea sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta. 8 Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba. 9 Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba. 10 Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake. 11 Hivyo Sulemani akaimaliza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na yote yaliyomwingia Sulemani moyoni ayafanye nyumbani mwa Bwana, na nyumbani mwake mwenyewe, akayafanikisha.

 

Sikukuu ya mwezi wa Saba ilifanyika kwa siku kumi na nne, siku saba zikiwa kwa ajili ya kuitakasa au kuweka wakfu madhabahu, na siku nyingine saba kwa ajili ya Sikukuu ya Vibanda. Sherehe za uwekaji wakfu zilifanyika kuanzia siku ya 8 hadi ya 14 mwezi Tishri, na siku saba za Sikukuu zilikuwa ni tangia siku ya 15 hadi ya 21 mwezi Tishri. Siku ya Mkutano Mkuu wa Makini ilikuwa ni siku ya 22 Tishri, na siku ya 23 Tishri walirejea majumbani mwao. Siku Kubwa ya Mkutano wa Makini haikuhesabiwa kuwa ni Sikukuu kwenye hesabu. Siku Kubwa ya Mkutano wa Makini ni ishsra ya nyakati za mwisho ambayo ni mfano wa Kiti Kikubwa Cheupe cha Enzi cha Hukumu na haipo kwenye uhusiano na kipindi cha utawala wa millennia. Ni kipindi cha Ufufuo wa Pili wa Wafu na kinahusiana na hukumu ya ulimwengu. Kwenye mwandamano wa matukio ya mwezi wa Tishri mwishoni mwa zama hizi za leo utaendana na maadhimisho ya Yubile ya mwaka 2027. Halafu Ufufuo wa wafu utakamilika na watu watarejea kwenye nchi au watarejeshewa ardhi zao katika Israeli na ulimwenguni kote.

 

Mchakato huu pia unahusiana na siku za mwis. Siku ishirini na moja zilizotajwa za kukamilisha mchakato huu ili kufikia kwenye utawala wa millennia kama ulivyoelezewa kwenye jarida la Utakaso wa Mataifa (Na. 77). Mchakato huu una migawanyo mitatu ya siku saba kila mmoja nay a marejesho mapya ya utawala huko Yerusalemu. Kwa hiyo kipindi cha kwanza cha miaka saba ya kwanza ya Utakaso kitakuwa mwaka 2012 ambacho ni cha mwajibiko wa Kanisa. Mafundisho yake yanapaswa yawe sahihi na yakamilike na yachapishwe na kuezwa kwa mataifa yote katika kipindi hiki. Ufunguo wa Daudi limepewa Kanisa adilifu na aminifu ka Siku za Mwisho, likifundisha mafundisho asilia ya kwanza ya Kanisa la Mungu yaliyokuwa yanafundishwa tangu karne ya Kwanza. Na hii inamaana ni mafundisho juu ya Mungu Mmoja au imani ya Kiyunitariani pamoja na mafundisho yake yasiyoghoshiwa. Ikiwemo Kalenda Takatifu pamoja na Miandamo wa Mwezi Mpya. Huo ndio Ufunguo wa Daudi katika kufafanua unabii kuhusu mwandamano wa matukio ya Siku za Mwisho.

 

Kwenye awamu hii hapa, kwenye mwandamano wa mambo ya Hekaluni, Utakaso wa Madhabahu kwa kweli kwa kweli ni shughuli ya pili iliyokuwa inafanyika siku saba za mwezi wa Tishri, ikifuatiwa na siku ya Nane ya mwezi wa Tishri, au mwaka 2013 kwa hesabu za mwaka mmoja kwa siku kuelekea kwenye Yubile ya mwaka 2027. Siku saba za mwisho za mchakato wa kuwatiisha mataifa kutoka Yerusalemu chini ya Masihi tangu mwaka 2019 hadi 2026 (soma jarida la Kuanguka kwa Yeriko (Na. 142)). Yubile ya mwaka 2027 inakamilisha mchakato na mwaka 2028 ni mwanzo wa utawala Mpya wa Milenia. Mwaka huu wa 2028 Marejesho ya \utawala wa Milenia na kanuni zake yatafanyika, na utaratibu wa Hekalu na usimamizi wake na mambo yote ya kiuatawala huko Yerusalemu yatawekwa, kama nyumba za Mfalme na Ukumbi wa kutolea Hukumu. Kutoka huko ndipo hukumu zitatolewa kwa watu wote ulimwenguni.

 

12 Bwana akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. 13 Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; 14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. 16 Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima. 17 Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu; 18 ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli. 19 Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu; 20 ndipo nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote. 21 Na nyumba hii, iliyo juu, kila apitaye ataona ushangao, atasema, Mbona Bwana ameitendea hivi nchi hii, na nyumba hii? 22 Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao.

 

Sulemani alikuwa ametahadharishwa vya kutosha kwa kile kingalichotokea kama wangejiingiza kwenye ibada za sanamu, lakini hatimaye yeye mwenyewe alijikwaa kwa hilo na akafanya hivyo.

 

2Mambo ya Nyakati 8:1-18 Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani aliijenga nyumba ya Bwana, na nyumba yake mwenyewe; 2 ndipo Sulemani akaijenga miji ile Hiramu aliyompa Sulemani, akawakalisha humo wana wa Israeli. 3 Naye Sulemani akaenda Hamath-zoba, akaushinda. 4 Akaujenga Tadmori wa nyikani, na miji yote ya hazina, aliyoijenga katika Hamathi. 5 Tena akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji yenye boma, yenye kuta, na malango, na makomeo; 6 na Baalathi, na miji yote ya hazina Sulemani aliyokuwa nayo, na miji yote ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na ya anasa yote aliyopenda Sulemani kujenga humo Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake. 7 Basi kwa habari ya watu wote waliosalia wa Wahiti, na wa Waamori, na wa Waperizi, na wa Wahivi, na wa Wayebusi, wasiokuwa wa Israeli; 8 wa watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuwakomesha, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo. 9 Wala katika wana wa Israeli Sulemani hakuwafanya watumwa kazini mwake; lakini hao walikuwa watu wa vita, na wakuu wa majemadari wake, na maakida wa magari yake na wa wapanda farasi wake. 10 Na hao walikuwa maakida wakuu wa Sulemani, watu mia mbili na hamsini, waliotawala juu ya watu. 11 Sulemani akamleta binti Farao kutoka mji wa Daudi mpaka nyumba aliyomjengea; kwa kuwa alisema, Mke wangu hatakaa nyumbani mwa Daudi mfalme wa Israeli, kwa kuwa ni patakatifu, mahali palipofika sanduku la Bwana. 12 Ndipo Sulemani akamtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana, aliyoijenga mbele ya ukumbi, 13 kadiri ilivyohitajiwa huduma ya kila siku, akitoa sawasawa na amri ya Musa, siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoamriwa, mara tatu kila mwaka, yaani, sikukuu ya mikate isiyochachwa, na sikukuu ya majuma, na sikukuu ya vibanda.

 

Sulemani akaweka mkazo kwenye Torati ya Mungu na Kalenda na akazitunza Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya ma kuzisisitiza kuwa ni Siku Takatifu za Mapumziko na maadhimisho, pamoja na mkazo wa kuzishika Sikukuu; ambazo tunaziadhimisha mara tatu kila mwaka, sawasawa na vilivyo kwenye Kalenda Takatifu (soma jarida la God’s Kalenda ya Mungu (Na. 156)). Utaratibu huu wa kalenda ulipaswa ushikwe hivyo tangu mwanzo hadi kuangamizwa kwa Hekalu mwaka 70 BK. Haya hivyo, mara ningi ilikuwa haishikwi, na Sikukuu na Usomaji wa Torati mara nyingi ulikuwa haufanywi kabisa kutokana na hali ya ukengeufu na ugumu wa mioyo au wavivu.

 

Utaratibu uliowekwa na Daudi ulianzishwa na kushikwa hadi na wafinyanzi waliotengeneza malango, na kilakitu kilikuwa na maana kwa ajili ya Hekalu lijalo la kipindi cha Yesu Kristo.

 

14 Akaziamuru, sawasawa na agizo la Daudi babaye, zamu za makuhani za kutumika, nao Walawi kwa kadiri ya malinzi yao, ili kusifu, na kuhudumu mbele ya makuhani, kama ilivyohitajiwa kila siku; tena mabawabu kwa zamu zao za kila mlango; maana ndivyo alivyoamuru Daudi mtu wa Mungu. 15 Wala hawakuyaacha maagizo ya mfalme aliyowaamuru makuhani na Walawi kwa neno lo lote, wala kwa habari ya hazina. 16 Basi ikatengenezwa kazi yote ya Sulemani hata siku ya kutiwa msingi wa nyumba ya Bwana, na hata ilipokwisha. Hivyo ikamalizika nyumba ya Bwana. 17 Ndipo Sulemani akaenda Esion-geberi, na Elothi, pwani ya nchi ya Edomu. 18 Naye Hiramu akamletea merikebu kwa mikono ya watumishi wake, na watumishi waliokuwa wana-maji; nao wakafika Ofiri pamoja na watumishi wa Sulemani, wakachukua kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, wakamletea mfalme Sulemani.

 

Malakia wa Sheba

Sulemani alimkuchua mwanamke kutoka nje ya Israeli. Uchaguzi wa wanawake wa Sulemani unamaanisha mjumuisho wa Wamataifa kwenye Kanisa, na ibada za sanamu ambazo Israeli waliziona na kutaabishwa navyo ziliwakilisha kupotoshwa kwa Kanisa na hawa wanawake wa kigeni ambao ni mfano wa Makanisa ya Wamataifa. Jambo baya zaidi kutokana na hali hii ni upotovu wa mfumo uliotokana Roma.

 

1Wafalme 10:1-29 Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani juu ya jina la Bwana, alikuja ili amjaribu kwa maswali ya fumbo. 2 Akaingia Yerusalemu na wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni. 3 Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala hakukuwa na neno alilofichiwa mfalme asimwambie. 4 Naye malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani, na nyumba aliyokuwa ameijenga, 5 na chakula cha mezani pake, na watumishi wake walivyokaa, na kusimamia kwao wangoje wake, na mavazi yao, na wanyweshaji wake, na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya Bwana, roho yake ilizimia. 6 Akamwambia mfalme, Ndizo kweli habari zile nilizozisikia katika nchi yangu za mambo yako na za hekima yako. 7 Lakini mimi sikuzisadiki habari hizo, hata nilipokuja na kuona kwa macho yangu; tena, tazama, sikuambiwa nusu; wewe umezidi kwa hekima na kufanikiwa kuliko habari nilizozisikia. 8 Heri watu wako, na heri watumishi hawa wako, wasimamao mbele yako siku zote, wakisikia hekima yako. 9 Na ahimidiwe Bwana, Mungu wako, aliyependezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti cha enzi cha Israeli; kwa kuwa Bwana amewapenda Israeli milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme, ufanye hukumu na haki. 10 Basi akampa mfalme talanta za dhahabu mia na ishirini, na manukato mengi, mengi sana, na vito vya thamani; wala haukuja tena wingi wa manukato, kama hayo malkia wa Sheba aliyompa mfalme Sulemani. 11 Tena merikebu za Hiramu, zilizochukua dhahabu kutoka Ofiri, zikaleta kutoka Ofiri miti ya msandali mingi sana, na vito vya thamani. 12 Mfalme akafanya kwa mia hiyo ya msandali nguzo za nyumba ya Bwana, na za nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda vya hao waimbaji; wala haikuja miti ya msandali kama hiyo, wala haikuonekana, hata leo. 13 Naye mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba haja yake yote, kila alilotaka, zaidi ya hayo aliyopewa na Sulemani kwa ukarimu wake wa kifalme. Basi, akarudi akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake. 14 Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Sulemani mwaka mmoja, ndio talanta mia sita sitini na sita, 15 zaidi ya faida ya wachuuzi, na bidhaa ya wafanya biashara, na ya wafalme wote wa hao waliochanganyika, na ya maliwali wa nchi.

Maana yake hapa ni kwamba Mfalme wa Toro mara nyingi ni jina linalomtaja Shetani. Kiwango kamili cha uzito wa Hekalu iliyotokana kutokana na biashara ilikuwa ni talanta mia sita na sitini na sita za dhahabu, ambayo ni tarakimu ya Mnyama. Inawakilisha uovu wa mfumo wa Malaika walioasi na upotovu wa kiimani ulioanzishwa kwenye awamu ya mwisho, ambao unaliwakilisha au unamaanisha Kanisa. Unaonyesha kuelekea upotofu wa imani ya Kanisa kwa utajiri na biashara na kupelekea upotoshaji wa mafundisho kwenye awamu ya mwisho ya kipindi cha Kanisa kuwa jangwani. Wale waliotafuta utajiri walipotoshwa na Mnyama.

 

16 Mfalme Sulemani akafanya ngao mia mbili za dhahabu iliyofuliwa; kila ngao moja ilipata shekeli mia sita za dhahabu. 17 Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kila kigao kimoja kilipata mane tatu za dhahabu. Mfalme akaviweka katika nyumba ya mwitu wa Lebanoni. 18 Tena mfalme akafanya kiti cha enzi kikubwa cha pembe, akakifunikiza kwa dhahabu iliyo safi. 19 Kiti kile kilikuwa na daraja sita, na juu yake kimeviringana nyuma; na mikono huko na huko mahali pa kuketi, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono. 20 Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya daraja sita huko na huko; wala hakikufanyika kwa mkono wake katika ufalme wo wote. 21 Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani. 22 Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi. 23 Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima. 24 Ulimwengu wote ukamtafuta Sulemani uso wake, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni. 25 Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, hesabu yake ya mwaka kwa mwaka. 26 Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu na mia nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu. 27 Mfalme akafanya fedha humo Yerusalemu kuwa kama mawe, na mierezi akaifinya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi. 28 Nao farasi aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi, kila kundi na thamani yake. 29 Tena gari huja kutoka katika Misri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa mia hamsini; vivyo watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.

 

Haya Majina yaliyotajwa hapa yanaonyesha kwamba kikosi cha wanajeshi cha Kitimu au Tarshishi, ambayo yaliweka makao yake huko Uhispania au Tarshishi, yalikuwa ni majeshi ya Wafalme wa Zamani walioishi kwenye maeneo ya kandoni mwa Bahari. Sulemani alishirikiana na Hiramu na waliweka makao yao kwenye pwani ya Tiro na Sidoni. Ukweli huu unaonekana pia kwenye vipimo vya nasaba ya damu vya makundi ya YDNA K2 vya Wafoinike wa huko Lebanoni, na pia wa huko Malta, na kwa Wayahudi wa sasa na Wadruze (sma majarida ya Chimbuko la Urithi wa Kinasaba wa Mataifa (Na. 265) aa Vita Vya Hamon-Gogu (Na. 294)). Sasa tunajua kwamba katika kipindi hiki walikuwa wanafanya biashara na wenyeji wa Amerika ya Kusini na walikuwa wakipeleka tumbaku na mihadarati aina ya cocaine huko Misri. Majaribio ya Kiforensiki kwa mumiani wa Berlin na Uingereza yanathibitisha ukweli huo.

 

Mambo ya Nyakati inaandika pia kwa kina kuhusu Malkia wa Sheba, na kuhusu mibaraka na hekima aliyokuwanayo Sulemani.

2Mambo ya Nyakati 9:1-31 Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, mwenye wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake. 2 Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno alilofichiwa Sulemani, asimwambie. 3 Naye malkia wa Sheba alipoona hekima ya Sulemani, na nyumba aliyoijenga, 4 na vyakula vya mezani mwake, na kikao cha watumishi wake, na usimamizi wao wangoje wake, na mavazi yao; na wanyweshaji wake, na mavazi yao; na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya Bwana; roho yake ilizimia. 5 Akamwambia mfalme, Ndizo kweli habari zile nilizozisikia katika nchi yangu za mambo yako na za hekima yako. 6 Lakini mimi sikuyasadiki maneno yao, hata nilipokuja na kuona kwa macho yangu; wala, tazama, ukuu wa hekima yako sikuambiwa nusu; wewe umezidi kuliko habari nilizozisikia. 7 Heri watu wako, na heri hawa watumishi wako, wasimamao mbele yako sikuzote, wakisikia hekima yako. 8 Na ahimidiwe Bwana, Mungu wako, aliyependezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti chake cha enzi, kuwa mfalme wake Bwana, Mungu wako; kwa kuwa Mungu wako amewapenda Israeli, kuwathibitisha milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme juu yao, ufanye hukumu na haki. 9 Basi akampa mfalme talanta mia na ishirini za dhahabu, na manukato mengi mengi sana, na vito vya thamani; wala haukuja wingi wa manukato, kama hayo aliyopewa mfalme Sulemani na malkia wa Sheba. 10 Tena watumishi wa Hiramu, pamoja na watumishi wa Sulemani, walioleta dhahabu kutoka Ofiri, wakaleta miti ya msandali, na vito vya thamani. 11 Mfalme akayafanya kwa miti hiyo ya msandali madari ya nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda vya hao waimbaji; wala haijatokea kama hiyo katika nchi ya Yuda. 12 Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba haja yake yote, kila alilotaka, zaidi ya vile alivyomletea mfalme. Basi akarudi, akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake. 13 Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Sulemani mwaka mmoja, ndio talanta mia sita sitini na sita za dhahabu; 14 mbali na ile waliyoileta wachuuzi na wafanya biashara; tena wafalme wote wa Arabuni, na maliwali wa nchi wakamletea Sulemani dhahabu na fedha. 15 Mfalme Sulemani akafanya ngao mia mbili za dhahabu iliyofuliwa; ngao moja hupata shekeli mia sita za dhahabu iliyofuliwa. 16 Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kigao kimoja hupata shekeli mia tatu za dhahabu; mfalme akaviweka katika nyumba ya mwitu wa Lebanoni. 17 Tena mfalme akafanya kiti cha enzi kikubwa cha pembe, akakifunikiza kwa dhahabu iliyo safi. 18 Kiti kile kilikuwa na daraja sita, tena na kikao cha miguu cha dhahabu, navyo vilikuwa vimeshikamana na kiti; na mikono huko na huko mahali pa kuketi, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono. 19 Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya daraja sita, huko na huko; wala hakikufanyika kwa mfano wake katika ufalme wo wote. 20 Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani. 21 Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu zilizokwenda Tarshishi pamoja na watumishi wa Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi. 22 Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima. 23 Wafalme wote wa duniani wakamtafuta Sulemani uso wake, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni. 24 Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, hesabu yake ya mwaka kwa mwaka. 25 Sulemani akawa na mazizi ya farasi na magari elfu nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu. 26 Akatawala juu ya wafalme wote toka Mto hata nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri. 27 Mfalme akafanya fedha humo Yerusalemu kuwa kama mawe, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi. 28 Wakamletea Sulemani farasi kutoka Misri, na kutoka nchi zote. 29 Basi mambo yake Sulemani yaliyosalia, ya kwanza, na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe ya Nathani nabii, katika unabii wa Ahiya, Mshiloni, na katika maono ya Ido mwonaji juu ya Yeroboamu mwana wa Nebati? 30 Akatawala Sulemani katika Yerusalemu juu ya Israeli wote miaka arobaini. 31 Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa mjini mwa Daudi babaye; akatawala Rehoboamu mwanawe badala yake.

 

Katika kipindi chake cha uzee, Sulemani aligeuka na kuwa mwabudu sanamu. Hii pia itakuwa ni budi kuwa hivyo kwa nyakati za mwisho za Kanisa. Wengi watapotoshwa na mafundisho ya uwongo. Ufano wake utaweka taswira kwa Kanisa kwenye awamu yake ya muongo wa mwisho.

1Wafalme 11:1-43 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. 3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. 4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. 5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. 6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. 7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. 8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. 9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili, 10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana. 11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako. 12 Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako. 13 Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua.

 

Kwa sababu ya hali hii ya kuabudu sanamu, Mungu aliamua kumshughulikia Sulemani kwa kupitia kipimo cha ardhi. Ndipo amani iliondolewa kutoka kwake.

14 Ndipo Bwana akamwondokeshea Sulemani adui, Hadadi Mwedomi; yeye alikuwa wa wazao wake mfalme wa Edomu. 15 Kwa maana ikawa, Daudi alipokuwako Edomu, naye Yoabu, mkuu wa jeshi, amepanda awazike waliouawa, akiisha kumpiga kila mwanamume wa Edomu, 16 (kwa kuwa Yoabu alikaa huko miezi sita pamoja na Israeli wote, hata alipompoteza kila mwanamume wa Edomu); 17 yule Hadadi alikimbia, yeye na Waedomi wengine, watumishi wa baba yake, pamoja naye, waende Misri; yule Hadadi akali ni mtoto mdogo. 18 Wakaondoka katika Midiani, wakafika Parani; wakachukua pamoja nao watu toka Parani, wakafika Misri, kwa Farao mfalme wa Misri; aliyempa nyumba, akamwamria vyakula, akampa mashamba. 19 Hadadi akapendeza sana machoni pa Farao, hata akamwoza umbu la mkewe, umbu la Tapenesi aliyekuwa malkia. 20 Naye huyo umbu la Tapenesi akamzalia Genubathi mwanawe, ambaye Tapenesi alimlea nyumbani mwa Farao; naye Genubathi akawako nyumbani mwa Farao pamoja na wana wa Farao. 21 Naye Hadadi aliposikia huko Misri ya kuwa Daudi amelala na babaze, na Yoabu, jemadari wa jeshi, amekufa, Hadadi akamwambia Farao, Unipe ruhusa, niende mpaka nchi yangu. 22 Farao akamwambia, Umekosa nini kwangu, hata, tazama, unatafuta kuirudia nchi yako? Akajibu, Hakuna, lakini unipe ruhusa tu. 23 Tena, Mungu akamwondokeshea adui mwingine, Rezoni mwana wa Eliada, aliyemkimbia bwana wake Hadadezeri mfalme wa Soba, 24 naye akakusanya watu, akawa mkuu wa jeshi, hapo Daudi alipowaua hao watu wa Soba; wakaenda Dameski, wakakaa humo, na kumiliki huko Dameski. 25 Naye akawa adui wa Israeli siku zote za Sulemani, zaidi ya madhara yake Hadadi; naye akawachukia Israeli, akamiliki juu ya Shamu. 26 Na Yeroboamu wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumwa wake Sulemani; ambaye jina lake mamaye aliitwa Serua, mwanamke aliyefiwa na mumewe; yeye naye akainua mkono wake juu ya mfalme. 27 Na hii ndiyo sababu ya yeye kumwinulia mfalme mkono. Sulemani aliijenga Milo, akapafunga palipobomoka pa mji wa baba yake Daudi. 28 Na huyo Yeroboamu alikuwa mtu hodari, shujaa; Sulemani akaona ya kuwa kijana huyo ni mtu mwenye bidii, akamweka juu ya kazi yote ya nyumba ya Yusufu. 29 Ikawa zamani zile Yeroboamu alipokuwa akitoka katika Yerusalemu, nabii Ahiya, Mshiloni, alikutana naye njiani; naye Ahiya amevaa vazi jipya, na hao wawili walikuwa peke yao mashambani. 30 Ahiya akalishika lile vazi jipya alilokuwa amelivaa, akalirarua vipande kumi na viwili. 31 Akamwambia Yeroboamu, Twaa wewe vipande kumi, maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe kabila kumi, 32 (lakini yeye atakuwa na kabila moja kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi, na kwa ajili ya Yerusalemu mji ule iliouchagua katika miji yote ya kabila za Israeli); 33 kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake. 34 Walakini sitauondoa ufalme wote katika mkono wake; lakini nitamfanya awe mkuu siku zote za maisha yake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi niliyemchagua kwa maana alizishika amri zangu na sheria zangu, 35 lakini nitauondoa ufalme katika mkono wa mwanawe, nami nitakupa wewe kabila kumi. 36 Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko. 37 Nami nitakutwaa wewe, nawe utatawala kama roho yako inavyotamani, nawe utakuwa mfalme juu ya Israeli. 38 Tena itakuwa, ukiyasikia yote nitakayokuamuru, na kuenda katika njia zangu, na kutenda yaliyo mema machoni pangu, ili kuzishika amri zangu na hukumu zangu kama Daudi mtumishi wangu alivyotenda, basi, nitakuwa pamoja nawe, nitakujengea nyumba iliyo imara, kama nilivyomjengea Daudi, nami nitakupa wewe Israeli. 39 Tena nitawatesa wazao wa Daudi kwa sababu hii, lakini si daima. 40 Basi Sulemani akataka kumwua Yeroboamu, lakini Yeroboamu akaondoka, akakimbilia Misri, kwa Shishaki, mfalme wa Misri, akakaa katika Misri hata wakati wa kufa kwake Sulemani. 41 Nayo yaliyosalia ya Sulemani, mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! Hayo siyo yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani? 42 Na siku alizotawala Sulemani katika Yerusalemu juu ya Israeli wote zilikuwa miaka arobaini. 43 Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa katika mji wa Daudi baba yake; na Rehoboamu mwanawe akatawala mahali pake.

 

2Mambo ya Nyakati 10:2 Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia, (maana alikuwako Misri, ambako amekimbilia mbele ya mfalme Sulemani), Yeroboamu akarudi kutoka Misri.

 

Hapa tunaona jinsi Yeroboamu alipokimbilia Misri na kujiunga na Sishaki, au Shishiki I, mfalme wa Walybia walioingia huko Kizazi cha Kifalme cha 22 waliokuwa na vita nao au uadui nao na waliokiangamiza Kizazi cha 21 cha Kifalme cha Tanite, ambacho kilikuwa na ushirikiano na Sulemani kupitia ndoa yake aliyoifanya kwa kumchukua binti wa mfalme. Kitendo hiki kilitoa uhakika wa matatizo makubwa kuwakumba Yuda chini ya Rehoboamu wakati Wamisri walipomsaidia Yeroboamu alipokuwa anarudi na akaongeza kiwango cha utoaji kodi katika Yuda.

2Mambo ya Nyakati 12:9 Basi Shishaki, mfalme wa Misri, akapanda juu ya Yerusalemu, akazichukua hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozifanya Sulemani.  

 

Wamisri waliichukua hazina iliyokuwa kwenye Nyumba ya Mungu iliyowekwa humo na Sulemani, na haikuwa na ule utukufu teka kabisa kama ilivyokuwa huko nyuma.

 

Kutokana na maandiko yake, Sulemani anaonekana kuwa alitubia jambo hil akiwa kwenye umri wake wa uzee na kujirudi, lakini alipaswa aadhibiwe. Historia ilibidi ibakie kama ilivyo ili kwamba Kanisa lipate kujua kile kilichokuwa kimetokea kwake katika miaka yake iliyofuatia. Awamu ya mwisho ya Makanisa ya Mungu ilikuwa ni ile ya kufa kiroho kwa kupotoshwa na imani za Kibinitariani na Kiditheisim, na hasahasa na imani ya Utatu au Utrinitariani. Wengine wameichukua kalenda ya uwongo ya nyakati za baada ya utumwa wa Babeli iliyotungwa na kuanzishwa na marabi wa Kiyahudi. Walikuwa maskini, wanyonge, vipofu, na walouchi, ingawaje waonekana kuwa ni matajiri.

 

Alipofariki Sulemani, Mungu ndipo aliweka mchakato wa kuufanya ufalme ugawanyike sehemu mbili na makabila ya kaskazini yajiondoe kabisa kutoka kwenye ufalme wa Yuda.

2Mambo ya Nyakati 10:1-19 Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekuja Shekemu, ili wamfanye mfalme. 2 Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia, (maana alikuwako Misri, ambako amekimbilia mbele ya mfalme Sulemani), Yeroboamu akarudi kutoka Misri. 3 Wakapeleka ujumbe, wakamwita, Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema, 4 Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako, na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia. 5 Akawaambia, Mnirudie baada ya siku tatu. Watu wakaenda zao. 6 Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa? 7 Wakamwambia, wakasema, Ukiwa mwema kwao watu hawa, na kuwapendeza, na kuwaambia maneno mazuri, ndipo watakapokuwa watumishi wako siku zote. 8 Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana waliokua pamoja naye, waliosimama mbele yake. 9 Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, Utufanyie jepesi kongwa alilotutwika baba yako. 10 Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. 11 Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu akiwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge. 12 Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu. 13 Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana, 14 akinena, Baba yangu aliwafanyia kongwa zito, nami nitawaongezea; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge. 15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa Mungu, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni. 16 Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hawasikilizi, watu wakamjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli, kila mtu; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Daudi. Basi wakaenda zao Israeli wote hemani kwao. 17 Lakini kwa habari za wana wa Israeli waliokaa katika miji ya Yuda, Rehoboamu alitawala juu yao. 18 Ndipo mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, msimamizi wa shokoa; nao wana wa Israeli wakamtupia mawe, hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda garini mwake, ili akimbilie Yerusalemu. 19 Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi, hata leo.

 

2Mambo ya Nyakati 13:6 Lakini Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumwa wa Sulemani mwana wa Daudi, akainuka, akamfanyia fitina bwana wake.  

 

2Mambo ya Nyakati 13:7 Wakamkusanyikia watu mabaradhuli, wasiofaa kitu, waliojitia nguvu juu ya Rehoboamu mwana wa Sulemani, Rehoboamu alipokuwa kijana na wa moyo mwororo, asiweze kuwazuia.  

 

Tendo hili liliweka mtafaruku na tofauti ya wazi kwenye kipindi cha Utawala wa Wafalme na Mpango wa Mungu kama ilivyoelezewa kwenye Ufunguo wa Daudi na kwa wale waliopewa kwenye mstari wa uzao wake mwenyewe. Hatimaye Israeli waliondolewa na kwenda utumwani huko Ashuru, takriban mwaka 722 KK, kwa hiyo lingeweza kupelekwa mahali pengine popote kwene urithi wake, kama Mungu alivyoahidi kumbariki Ibrahimu.

 

Kwenye miaka 120 ya tawala za wafalme watatu, Mungu alionyesha kile kingalichoweza kutokea ulimwenguni na kwamba Kanisa la Mungu lianzishwe chini ya Masihi.

 

Yuda na sehemu ya kabila la Benyamini walibakia kwenye ufalme huu nay ale makabila ya Kaskazini yalijiondoa yenyewe. Hata hivyo, walidumu kwa miaka mitatu kabla ya kuanguka kwao kutoka kwenye neema.

2Mambo ya Nyakati 11:17 Hivyo wakaufanya imara kwa miaka mitatu ufalme wa Yuda, na kumtia nguvu Rehoboamu mwana wa Sulemani; kwa maana muda wa miaka mitatu wakaiendea njia ya Daudi na Sulemani.

 

Yuda waliendelea kubaki pale walipokuwa ili kwamba Masihi afikie mahala pake na palipokusudiwa, ili kuuoko ulimwengu kutokana na dhambi na maangamizo. Kulikuwa na marejesho yaliyofanyika mara nyingi, lakini maranyingi zilikuwa ni vipindi dha dhambi na maangamizo (soma jarida la Pasaka Kuu Saba za Kwenye Biblia (Na.107)). Marejesho haya yalikuwa na maana kubwa sana kufutaiwa na uasi na vipindi vya kwenda utumwani.

 

Nyongeza ya 1:Vizavi vya Kifalme vya Misri Kwene Biblia

Nyongeza ya 2: Muhtasari wa Maelezo ya Ufunguo wa Daudi

Nyongeza ya 3: Jarida la 282D Wanaume Mashujaa wa Israeli

Nyongeza ya 4: Jarida la 282E Makuhani wa Hekalu

q

 


 

Nyongeza 1: Vizazi vya Kifalme vya Misri kwenye Biblia

Biblia imeandikwa kwamba mabadiliko ua utawala wa Misri yalitokea na Farao aliinuka siyemjua Yusufu. Farao huyu alianza kuwatesa na kuwadhulumu Waisraeli. Sababu ya kuibuka kwa mateso haya ilikuwa kipindi hiki ambacho Waisraeli walifanikiwa sana kiutajiri kilikuwa ni cha utawala wa Hyksos, au wafalme Wachungaji ambao walikuwa ni Waasia na wa jamii ya kichungaji walioishambulia na kuiteka Misri na kuitawala kwa kipindi kifupi cha miaka mamia kadhaa tu. Habari za kuhusu Manetho na baadae waandishi zilipelekea kuwepo kwa hila ambazo za kufanana na ushirikiano na washirika wabaya na waovu na mashujaa wazawa waliokuwa wema, na kwa hiyo hawa Hyksos walifanywa wabaya mno kama waliopagawa na mapepo vile kwa kiwango ambacho sicho kilichostahili kuwa. Mahala pa Waisraeli huko Misri katika siku za mwanzoni hapana la kujiuliza wala kuonesha shaka kwa sababu ya mahala pa hawa Hyksos na chimbuko la Waisraeli wenye asili ya Kiasia na Kisemitiki. Mateso yao yalifuatia kuanguka kwa kizazi hiki cha Hyksos, au wanaweza pia kuwa ni sehemu ya utawala wa Hyksos. Kizazi cha hawa Hyksos kilitawala kwa muda wa miaka 104 na Misri iligawanyika pande mbili. Misri ya Pande za Juu ilitawaliwa na Kizazi cha 17 wakati katika kipindi hichohicho Kizazi cha 16 cha Hyksos kikitawala Misri ya Chini. Huu unaoitwa mgawanyiko unaweza pia kwamba ulianzia wakati Yusufu alipofanywa kuwa mmoja wa mawaziri au Wazirimkuu wa Misri na wana wa Israeli walipohamia huko Gosheni na kuchukua mahala pa kizazi cha 15. Hadithi ya Biblia inaungana na kusaidiana na historia ya Wamisri, ingawa wanahistoria wanajaribu kwa makusudi tu kuitenganisha Biblia ili wafanye hii kuwa ni hadithi tu ya kufikirika na isiyo rasmi.

 

Kizazi cha 18 kilitokana na kile cha 17 na mwanzilishi wake alitokana na ndoa ya kibinamu kati ya Seqenenre II na dada yake. Kwenye ndoa yake hii ya kiudugu na binamu yake. Ahmose aliwashinda na kuwatiisha Hyksos na kuchukua umiliki kamili wa dola. Kwa hiyo, Kizazi cha 18 sito Kizazi kipya bali ni rekodi ya Farao asiyemjua Yufusu, aliyewatumikisha kitumwa hata hawa Hyksos na kuuondoa utawala wa Wasemitiki katika Misri ya Chini.

 

Mafarao

 

1785-1650 KK           

Kizazi cha 13-15

Kipindi cha Pili cha Zama za Kati

1650-1554 KK           

Kizazi cha 16

Utawala wa Hyksos Kutoka Misri ya Chini

1650-1554 KK

Kizazi cha 17

Kamose Seqenenre II (Misri ya Juu)

1554-1305 KK           

Kizazi cha 18 

Ahmose (Amosis I)

Amenhotep I (Amenophis I)

Tuthmosis I
Tuthmosis II
Hatshepsut
Tuthmosis III
Amenhotep II
Tuthmosis IV
Amenhotep III
Amenhotep IV
Semenkare
Tutankhamen
Malkia Ankhesenamun
Ay
Horemhab

1305-1196 KK           

Kizazi cha 19

Rameses I

Seti I

Rameses II
Lord Ameni (Bwana Ameni)
Merenptah
Seti II
Siptah

 

Muhtasari wa Maelezo ya Kizazi cha Kifalme cha 18

 

Jina                            Maelezo                               Tarehe za Mwaka wa Juu Zaidi

 

Ahmose                       Amosis                                                           1550 – 1525

Mwanzo wa Kizazi hiki unachukuliwa na kuaminika na wengine kuwa ni mwaka 1554. Tarehe zilizoandikw na Baine na Malek kwenye kitabu kijulikanacho kama Atlasi ya Misri ya Kale [Atlas of Ancient Egypt] (Iliyodunu Hadi, 1994) inasema 1550-1307 (tazama hapo chini). Tarehe za kwenye Mtandao au Wikipidia zilizotolewa ni kama ifuatavyo.

Amenhotep I               Amenophis                                                     1525 - 1494

Thutmosis I                 Tethmosis                                                       1494 - 1482

Thutmosis II                Khebron                                                          1482 - 1479

Thutmosis III              Misphragmuthosis                                           1479 - 1425

Hatshepsut                  Amensis                                                         1473 - 1458

Amenhotep II                                                                                    1425 - 1401

Thutmosis IV              Tuthmosis                                                      1401 - 1391

Amenhotep III                                                                                   1391 - 1353

Amenhotep IV

Akhenaten                                                                                     1353 - 1335

Semenekhkare                                                                                    1335 - 1334

Tutankhamun                                                                                     1334 - 1325

Ay                                                                                                      1325 - 1321

Horemheb                   Armaios                       13                                1321 - 1307

(kumbuka kwamba hii Wikipidia inasema 1540-1307. Tarehe za Wikipidia ni zile ambazo ziko nje kabisa na mwandamano wa tarehe zilizokubalika na wengine).

 

Taarifa Zihusuzo Habari za Farao

1785-1650 KK            Kizazi cha 13                          Kipindi cha Pili cha Zama za Kati

 

1650-1554 KK                                                            Kizazi cha 16 Utawala wa Hyksos Misri ya Chini

 

1650-1554 KK            Kizazi cha 17                          Kamose Seqenenre II (Misri ya Juu)

Mfalme wa kumi na nne wa Kizazi cha Kifalme cha Theban alitawala Misri kwa wakati mmoja na Hyksos wa Kizazi cha 15 na cha 16 alikuwa ni mtoto wa Tao I na Malkia Tetisheri. Wakati Tao alipopokea neno kutoka kwa Apophis, mtawala wa Hyksos, capital huko Avaris, kwamba kulikuwa na mnyama kiboko kwenye bwawa takatifu huko Thebes alimfanya aamke pamoja na mikotomo yao, Tao aliichukulia taarifa hii kama tusi. Hawa wanyama aina ya viboko walikuwa takriban maili 400 kutoka vyumba alivyokuwa analala Apophis! Tao alitangaza vita lakini aliuawa mara moja. Mama yake alionyesha ushahidi au alama ya kupiga kelele za kuyagonganisha mashoka ya vita, mishale na fumo. Mbavu zake, pingili za uti wa mgongo na fuvu vilikatikakatika. Mrithi wake, Kamose, akachukua kiti chake cha ufalme na madaraka ya kuendeleza vita, na akashinda (kama ilivyoandikwa kwenye tovuti ya http://www.touregypt.net). Kamose alikuwa ni wa mwisho wao kwenye Kizazi hiki cha Kifalme cha 17 lakini mwanae wa kiume (ndugu yake?) Ahmose alianzisha Kizazi cha Kifalme cha 18  ambacho kilikuwa na nguvu kwa ajili ya mbinu zake za kuiunganisha Misri wakati Hyksos alipofukuzwa au kupinduliwa. Kwa hiyo utumwa wa wana wa Israeli ulikuwa ni nitu cha mahati mbaya au nasibu iliyotokea baada ya kuanguka kwa kizazi hiki cha Hyksos. Ufafanusi wenye mashiko zaidi wakati propaganda za baadae ziliposhindikana, ni kwamba uongozi wa Misri umeanzishwa au uko chini ya Yusufu na hiki ni kipindi kinachotajwa kuwa ni cha utawala wa Hyksos. Waliandikwa kuwa ni kama wakusanaji wa kodi katika Misri yote. Dhana kama hiyo ilikataliwa kwa kuwa ilidhaniwa kwamba walikuwa ni watawala wa vipindi tofauti zaidi ya kuwa ni viongozi. Mwadhiriko wa baadae ya Hyksos inaonekana sasa kuwa ni kama propaganda inayofanana.

 

1554-1305 KK ,           Kizazi cha Kifalme cha 18 cha                           Ahmose (Amosis I)

1554-1525                   Mfalme Amosis anadai kwamba wazazi wake walikuwa ni watoto wa mama mmoja na baba mmoja, yaani ndugu wa kuzaliwa tumbo moja, wakiwa kama mfano mzuri kwa mila zao wa ndoa ya kaka na dada wa tumbo moja. Mama wa Amosis alikuwa 'Ahhotpe, na alikuwa ni mke wa Sekenenre' Ta'o II. Katika namna zote za kudhania au mabahatisho, mama yake Terisheri alikuwa ni mke wa Ta'o I, ambaye kaburi lake, kama lilivyokuwa la Ta'o II, ilipaswa kukaguliwa wakati wa utawala wa Ramesses IX na kwa kweli alikutwa hajaoza bado. Hakuna kinachojulikana zaidi kuhusu huyu Ta'o I lakini inadhaniwa kwamba Prenomeni wake alikuwa ni Senakhtenre'.

 

1528/7 KK: Musa alizaliwa, mapema kabla ya kufariki kwa Ahmosis na aliitwa au kupewa jina lake yeye na dada yake. Kwa mujibu wa vitabu vya kumbukumbu za mambo kale za Kizazi cha Kifalme cha 18 anaweza kuwa alizaliwa kwenye utawala wa wa Amenhotep I.

 

1525-1504 KK Amenhotep I (Amenophis I)

 

1525 KK: Kifo cha Ahmose/Ahmosis I, (wengine husema mwaka 1527). Mwaka huu ulikuwa ni wa Sabato wa mzunguko wa mwisho wa Yubile ya 49. Ulikuwa ni mwisho wa mauaji ya kuwaangamiza wana wa Israeli kwene mateso yao. Ufalme Mpya, au Mfalme alijionea kwa kipindi cha zaidi ya karene moja na nusu ya mafanikio yasiyoshuka kiwango chake. Amri ya kuwangamiza Waisraeli huenda ilichochewa na hali ya wao kuonekana kuwa ni sehemu ya Hyksos anayechukiwa. Amri hizi zilitolewa na mfalme huyu ili kuanzisha Kizazi kingine cha kifalme.

“Mtoto wa kiume wa Ahmose na Malkia Ahmose Nefretiri, Amenhotep I alikuwa ni mfalme wa pili wa Kizazi cha Kifalme cha 18. Anaweza kuwa alikitaa kiti cha enzi cha ufalme cha wazazi wake akiwa na umri wa ujana, kwa kuwa kaka yake yake mkubwa alikuwa amechukuliwa kuwa ni mrithi wa pekee kwa kipindi cha miaka mitano nyuma.”

Inaonekana kuwa mtoto mkubwa na wa kwanza wa Ahmosis alikuwa amefakiri. Tunaweza kusema kwamba hii ilikuwa ni adhabu au mapigo kwa ajili ya kuwaua wana ya Israeli.

“Kwa wazi kabisa, Amenhotep alifanya matendo mengi ya baba yake, na mama yake kwa kweli alifanya wajibu wake alivyoweza na wa muhimu kwene utawala wake, akijifanya kama Mke wa Mungu, Amun. Amenhotep I anaweza kuwa alimuoa dada yake, (Ahmose-) Merytamun, ambaye alikuwa akijulikana kwa imani yao kuwa ni Mke wa Mungu, Amun, ingawa kuna madodoso madogo yaliyowazi yanayofafanua juu ya uhusiano huu. Aliyekuwa anajulikana sana ni binti wa mfalme huyu, Satamun, ambaye anajulikana kwa namna mbili kutokana na sanduku lake la jeneza lililokutikana kwenye moja ya caches za mama yake na kutoka kwenye sanamu ya huko katikati na kusini mwa Karnak” (tazama makala ya Jimmy Dunn kwenye tovuti ya http://www.touregypt.net/featurestories/amenhotep1.htm)

 

1524 KK              Yubile ya  49

 

1504-1492                                      Tuthmosis I

1492-1479                                      Tuthmosis II


1488 KK : Musa anafikia umri wa miaka 40 na anakimbilia Midiani, kipindi cha utawala wa mfalme Tuthmosis II, katika kipindi chake cha miaka arobaini ya utawala wake, baadaa ya kumuua Yule mlinzi au nyapara asimamizi wa kazi

 

1479-1458 KK                               Hatshepsut (Ma’atkare’) Malkia Regent

1473 KK                                        Hatshepsut alijitawaza mwenyewe kuwa Farao.

 

Wikipidia inatupa maelezo yenye kukanganya kidogo kuhusu huyu Hatshepsut.

 

Hatshepsut alikuwa ni binti wa kwanza kabisa katika kuzaliwa wa Thutmose I na Malkia Ahmose, mfalme wa kwanza na malkia wa ukoo wa Thutmosid wa Kizazi zha Kifalme cha 18. Thutmose I na Ahmose wanajulikana kuwa walikuja kumpata mtoto mmoja tu mwingine, binti aliyeitwa Akhbetneferu (Neferubity), aliyefariki akiwa mtoto mchanga. Thutmose I pia alliolewa na Mutnofret, huenda huyu alikuwa ni binti wa Ahmose I, na alikuwa na ndugu kambo kadhaa kwa Hatshepsut: Wadjmose, Amenose, Thutmose II, na huenda hata Ramose, kupitia muungano ule. Wote hawa wawili, yaani Wadjmose na Amenose waliandaliwa kumrithi baba yao, lakini wala hakuna hata mmoja wao aliyeishi na kufikia umri wa ujana. Akiwa kwenye umri wa utoto, inaaminika kuwa Hatshepsut alisaidiwa na Hekalu la Karnak dhidi ya kaka zake wawili—mtazamo uliopaishwa kwa propaganda zake mwenyewe. Ni hakika kabisa kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wazazi wake wote wawili, na akatunga hadithi ya propaganda ambayo kwamba, baba yake Thutmose I alikaribia sana kumtangaza yeye kuwa ndiye atakuwa mrithi wake moja kwa moja (tazama hapo chini).

Alipofariki baba yake mwaka 1492 KK, alioewa na Thutmose II na akachukua cheo cha kuitwa Mke Mkubwa wa Mfalme Thutmose II aliyetawala kwa miaka thelathini, wakati ambao kimapokeo kiliaminika kwamba Hatshepsut aliwezeshwa kupata mvuto mkubwa kwenye jamii zaidi yake.

Thutmose II alikuwa na binti mmoja aliyempata na Hatshepsut, Neferure. Hatshepsut alimfanya bwana arusi wake Neferure kuwa kama mfalme mwenye taji la kifalme, akiwaamumuru maafisa wake wa kijeshi wamvike kichwa cha uwongo na kifungo cha ujana kwa upande mmoja. Wasomi wengine wanadhani kwamba ushahidi huu wa kwamba Hatshepsut alikuwa saisi Neferure kwa ajili ya kiti cha ufalme; na huku wengine wakisema kwamba alikuwa anapanga tu Hatshepsut mwingine. Kwa namna yoyote ile, nia yake ilikuwa, haikuwa na maana yoyote kwa kuwa Neferure hakuishi hadi kufikia umri wa utu uzima.

 

Makala ya kwenye Wikipidia ndipo inaukadiria utawala wa Hatshepsut kuwa ni tangia mwaka 1503 KK hadi 1482 KK. Hata hivyo, hii inaonekana kutuama kwenye tarehe sizizosahihi za zamani au zinakanganya ndoa yake kwa Thutmose II alivyooana na Thutmose I. Inasema alifariki “mapema sana ya Februari 1482 KK au 1483 KK”. Kisha inadai pia kwamba yeye mwenyewe alimtawaza farao mnamo mwaka 1473 KK, alichukua kiti cha mfalme aliyeitwa Maatkare.

 

Maatkare Hatshepsut au Hatchepsut (mwishoni mwa  karne ya 16 KK – takriban 1482 KK) alikuwa farao wa tano wa Kizazi cha Kumi na Nane cha Misri ya Kale. Hatshepsut kwa ujumla alichukuliwa na Wataalamu wa Elimu ya Kimisri wa kisasa kama ni mmoja wa mafaro waliofanikiwa sana, akiwa ametawala kipindi kirefu kuliko mtawala yeyote wa kike wa kizazi cha kifalme cha wenyeji au wazawa asilia. Alikuwa ni mmoja ya wajenzi waliofanikiwa sana wa Misri ya Kale, akiamuru ifanyike miradi ya ujenzi kwa mamia kwa sehemu zote mbili, yaani maeneo yote ya Misri ya Juu na ya Chini na chini ya uongozi wake, mtangao wa kibiashara wa Misri ulianza kujengwa, baadawa Misri ulianza kujengwa, baada ya kuharibika na kuanguka wakati wa tawala za kizazi cha Hyksos huko Misri kipindi cha Zama au Kipindi cha Pili cha Zama za Kati. Anaaminika kuwa alitawala tangu mwaka 1503 KK hadi 1482 KK. Josephus ameandika kwamba alitawala kwa kipindi cha miaka 21 na miezi 9, wakati Africanus anauelea utawala wake kuwa uliishia miaka 22; lakini tunayemnukuu na kuamini habari zake ni Manetho. Hatshepsut anachukuliwa kitofauti sana kabisa kama kile kilichojulikana mapema sana kama utawala wa malkia kwenye historia, kama wa mwanamke wa kwanza kujulikana kuchukua cheo cha Mfalme wa Misri ya Juu na ya Chini, na ni mwanamke mkuu wa kwanza kwenye historia iliyoandikwa.

 

Lesser anatoa mwanga zaidi kuhusu jambo hili kama ifuatavyo. Aliolewa na Thutmose II yapata mwaka mmoja kabla ya kufariki kwa Thutmose I.

“Urefu wa kipindi cha utawala wa Thutmosis II umetolewa na Beckerath (1997) pamoja na [kama] miaka 12 - 14 na kwa mujibu wa Grimm na Schoske (1999) pamoja na [kama] miaka 3 tu - kisha alizikwa. Hadi sasa hakuna kaburi kwenye Bondeni la Wafalme linalodhaniwa kuwa ni lake yeye pamoja na ubahatishaji lakini baadhi ya ushahidi unaonyesha kwenye kaburi lenye alama ya KV42. Ukweli wa kwamba alama hii ya KV42 ni [kama] kaburi rahisi ambalo kwenye jeneza la jiwe pasipo maelezo yaliyokutwa inaashiria kwamba mfalme alikufa kwa mazingira ya kutatanisha sana na wala halikuwa kaburi zuri wala jeneza la kuchongwa mwambani vilivyokuwa na kiwango cha juu vilivyokutikana.

 

Kulingana na mahesabu yaliyotajwa mapema huko nyuma kuhusu umri aliokuwanao wakati anaolewa na kuhusu urefu wa kipindi cha utawala wake Thutmosis II Hatshepsut inawezekana sana kuwa alikuwa na umri wa katikati ya miaka 15 (zaidi ya Grimm na Schoske) na miaka 30 (zaidi ya Beckerath) wakati mume wake alipofariki.

Kwa kuwa kuna ushahidi mwingine kwamba Thutmosis I bado alitawala kwa kipindi cha takriban mwaka 1 baada ya ndoa yake aliyofunga na Thutmosis II Hatshepsut anawezekana kabisa kwamba alikuwa na umri wa miaka 15 – au na umri mdogo tu – kwa angau kama mume wake Thutmosis II angetawala kwa kama miaka 3 tu. Kwa hiyo, inawezekana sana kwamba mama yake Ah-mose alishika hatamu za utawala kwa kipindi fulani, kabla ya Hatshepsut na baada ya kifo cha Ah-mose – kwa makubaliano na desturi za familia ya hawa Ahmosids na historia ya Wamisri (kushika hatamu za utawala wa mfalme aliye na umri wa chini umeshuhudiwa kwa kuwa Ufalme wa zama Kale) – alishika hatamu ya utawala wa Thutmosis III aliyekuwa na umri wa chini.” (Tembelea Tovuti ya Dr Karl Lesser http://www.maat-ka-ra.de/english/maat_ka_ra/regentin.htm)

Ndoa hizi za kuonana ndugu wa karibu zilisababisha mwingiliano mkubwa wa kidamu wa tabaka la watawala au waungwana wa Kimisri. Matendo hayo yalikuwa ya kawaida katika siku hizo. Majina waliyopewa wote wazaliwa wa jinsia zote mbili, yaani wanawake na wanaume yalitofautiana na majina ya Mose au Mosis, na kiini cha chanzo cha jina hili ni Musa (au Moshe) ni dhahiri kabisa.

 

Ukitembelea tovuti ya www.touregypt.net utaona inahitimisha jambo hili kama ifuatavyo.

Hatshepsut, mtawala wa tano wa Kizazi cha 8, alikuwa ni binti wa Thutmose I na Malkia Ahmose. Kama ilivyokuwa kwenye familia za kifalme, aliolewa na binamu yake, Thutmose II, ambaye alikuwa na mtoto, Thutmose III, kwa mke wake mdogo. Wakati Thutmose II alipofariki mwaka 1479 KK. mtoto wake wa kiume, Thutmose III, alichaguliwa kwa mrithi. Hata hivyo, Hatshepsut alichaguliwa kutawala kutokana na umri wake wa ujana sana. Walitawala kwa pamoja hadi mwaka 1473 wakati alipojitangaza mwenyewe kuwa ni farao. Akajivika mavazi na taji za kifalme za wanaume, Hatshepsut alisimamia mambo ya kitaifa, kwa kusaidiwa kikamilifu na kuhani mkuu Amun, Hapuseneb na maafisa wengine. Wakati alipojenga Hekalu lake la Kupendeza huko Deir el Bahari iliyoko Thebes, aliupa ahueni uzazi wake wa kimbinguni akiwa kama ni binti wa Amun. Hatshepsut alipotea mwaka 1458 KK. wakati Thutmose III, alipokuwa anakitaka tena kukitwa kiti cha ufalme, akaongoza maasi. Thutmose alikuwa na vijihekalu au miungu yake, sanamu na alijipa ahueni kwa kuviongeza.

 

Huu ulikuwa ni mtazamo wa jumla kuhusu uongezaji wa ahueni yake lakini sisi sasa tunajiuliza mengi kuhusu mtazamo huu.

 

Baada ya kifo chake, sanamu na mapambo mengi ya Hatshepsut na maashirio yake yaliondolewa na kuharibiwa kidogokidogo au kuondolewa kabisa, yakiwemo yale ya kwenye hekalu ya mochwarie lililokuwa kubwa na lililojengwa huko Deir el-Bahri. Haya kimapokeo yamekuwa yakitafsiriwa kuwa ni ushahidi wa matendo ya damnatio memoriae (kumlaumu mtu8 kwa ajili ya kumla yeye mwanaume au mwanamke kitoka kwenye uwepo ulioandikwa) na Thutmose III. Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wanazuoni kama ule uliofanwa na kina Charles Nims na Peter Dorman umetathimini tena hakikisho hizi na kukuta kwamba matendo ambayo yangepewa tarehe au siku zake kuwa yalitokea baada ya mwaka wa arobaini na mbili wa utawala wa Thutmose. Hii inaondoa mashaka makubwa kutoka kwenye dhana mashuhuri ya kwamba Thutmose III aliamuru kuangamizwa kwao kwa ukamilifu na kamio la kujilipizia kisasi mara tu baada ya kuingia kwake madarakani. Zaidi sana ni kwamba inakubalika kila mahali leo kwamba Thutmose III anaweza kuwa aliamua kuifutilia mbali kumbukumbu ya Hatshepsut kutoka kwenye historia ya rekodi ya kihistoria ya ushupavu na uafithina wa Wamisri na mfumo wao wa madaraka ya kisiasa, ni wanaume tu ndio waliokuwa wanaruhusiwa na kuonekana wanastahili kutawala nchi wakati wanawake walikuwa wakitarajiwa kuwa watiifu kwa waume zao na kuwatunza watu walio majumbani mwao. Kwa kweli, kipindi cha kabla ya utawala wa Hatshepsut ni Mafarao wanawake wengine wawili tu wa Kimisri ndio walijulikana kuwepo: Nitocris na Sobekneferu. Ni kama alivyokuwa Hatshepsut hatahivyo, malkia hawa wawili wote walifaidi kipindi kifupi sana cha kutawala (kwa mujibu wa Wikipedia).

 

1479-1425                            Tuthmosis III

“Mrithi wa Thutmosis II alikuwa ni mtoto wake, Thutmosis III, ndiye alizaliwa na mke wake wa pili, Isis. Hivyo basi Thutmosis III alikuwa na umri gani basi wakati baba yake alipokufa na akachukua utawala na kiti cha enzi cha ufalme (mnamo mwaka 1479 KK. Kipindi cha Beckerath, 1997) hajulikani. Haya hivyo alitawala kwa takriban miaka 54 – pamoja na utawala wa Hatshepsut – na mama yake akiwa hajawa mzee sana. Kwa hiyo, inawezekana sana kuwa alikuwa mtoto mdogo sana na kwa jinsi hii sio mkubwa zaidi ya miaka 10. Kwa mujibu wa tarehe zilizotajwa hadi mwaka 42 wa utawala wake alikuwa na umri wa miaka 6 alipochaguliwa kwa ubashiri wa kuhani Amun awe mfalme. Maelezo haya kwa hakika yalikuwa yanajaribu kuuhalalisha utawala wake kwa kuwa hakuna mrithi wakiume kwenye kiti cha ufalme aiiyekuja kutoka kwene ndoa ya baba yake pamoja na Hatshepsut na kutoka kwenye upande wa mama yake hakuwa wa kustahili kuwa mfalme – hata hivyo maelezo haya yanaweza kutumika kama adidu rejea za haraka haraka na za juujuu kuhusu umri wake na uchukuaji wake madaraka” (Lesser ibid).

 

1448/7 KK: ndani ya kronolojia hii, tukio la Kutoka utumwani lilifanyika miaka kumi baada ya kifo cha Hatshepsut. Kama utawala wake na mwanae wa ambo na binamu yake alikuwa ni mjenzi mkuu sana na mwendelezaji wa Misri. Kujilimbikizia kwake madaraka ya kifalme mwaka 1473 kulipelekea hatimaye kupinduliwa na kupotea kwake mwaka 1458.

 

Menkheperre Thutmose III (pia anaandikwa kama Tuthmosis III au Thothmes III; anaitwa Manahpi(r)ya kwa mwandiko au herufi za Kiamarna) (takriban mwaka 1425 KK), alikuwa ni Farao wa sita wa Misri kwenye Kizazi cha Kumi na Nane, na kilitawala kama cha mafarao wakuu wa Misri. Alitawala tangu mwaka 1479 KK hadi 1425 KK, kwa mujibu wa Kronolojia ya zama za Kati ya Wamisri wa Kale. Machapisho ya kale zaidi ya miaka ya 1960 na 1970 yamesema kwamba huenda alitawala Misri tangu mwaka 1504 KK hadi 1450 KK lakini hii ilitegemeana kwa sehemu na mtazamo usio rasmi na usiothibitishika wa miaka 35 ua utawala wa Thutmose IV. Hata hivyo. Inajulikana kuwa Manetho alimpa Thutmose IV atawale kwa Miaka 9 na Miezi 8 tu kwenye Mfano na kifupisho chake wakati Mwaka wa Juu zaidi wa mfalme huyu ulioandikwa ni Mwaka wake wa 8 tu. Hatimaye, masanamu ya Thutmose IV yalikuwa ni madogo sana kwa kuyalinganisha na ni magodo kulinganishwa na yale ya mtoto wake Amenhotep III, ambaye alifaidi kipindi cha utawala wake wa Miaka 38. Wanazuoni wa mambo kale ya Misri wa leo wanasema kuwa Thutmose IV utawala wake ulidumu kwa takriban Miaka 10 tu na wameweka tarehe ya kutawazwa kwa Thutmose III kuwa ni mwaka 1479 KK badala yake.

Thutmose alikuwa ni mfupi sana, akiwa na urefu wa futi tano tu (sawa na mita 1.5) urefu wake, ukweli uliokuja kujulikana baadae na wanahistoria hadu lilipogunduliwa mumiani au adui yake mnamo mwaka 1881.

 

1427- 1401                                     Amenhotep II

Kama kawaida, vifaa mbalimbali vinatoa vipindi maalumu mbalimbali vya utawala wa Amenhotep II. Maandiko ya Kihistoia ya Zama za Mafarao yaliyoandikwa na  Peter A. Clayton yanasema utawala wake ulidumu kwa kipindi cha tangu mwaka 1453 hadi 1419 KK, ambacho kinamfanya kuwa ndiye Farao wa wakati wa Kutoka. Hiyo ni kwa mujibu wa rekodi za Karnak Stele kuhusiana na tukio la Kutoka lakini inawezakuwa haihusiani kabisa. Historia ya Oxford ya Misri ya Kale inakifanya kipindi hiki cha utawala kuwa ni kati ya mwaka 1427 hadi 1400 KK. Wikipidia inasema mwaka 1425 na Baines na Malek wanasema mwaka 1427-1401. Kwahiyo, baba yake Thutmose III alikuwa ni Farao wa kipindi cha Kutoka kwenye tarehe hizi za baadae za Thutmoses III.

 

Amenhotep II alikuwa mtotos wa kiume wa Thutmose III na mke mkubwa, Hatshepsut-Meryetre. Amenhotep kwa kweli alikuwa ni mdogo akitawala kwa wakati mmoja na baba yake kwa Miaka 2 na Miezi 4 kwa mujibu wa rekodi za kihistoria za wakati mmoja tangu tarehe ya kutawazwa kwake kuwa mfalme alikuwa wa "IV Akhet siku ya 1 kama ilivyoonyeshwa kwenye stela ya Semna ya Usersatet, mtoto amtumikiaye Mfalme (kama mshindi) wa Kushi chini ya Amenhotep II, wakati Tuthmose III ananukuliwa kuwa alikufa wakati wa III Peret siku ya 30 kwenye Kaburi la Wasifa wa Amenemheb (inasema Wikipidia).

 

Ukweli wa kwamba alikuwa ni mtoto wa Farao kwa mke wake mdogo unaweza kuwa ni sawa na inavyosema Biblia kwenye maandiko na kumbukumbu zake kwamba mzaliwa wa kwanza wa kiume wa farao wa wakati wa Kutoka (Thutmoses III) alikuwa ameuawa pamoja na wazaliwa wengine wa kwanza wa Misri.

 

1424 KK: Yubile ya 51

 

Amenhotep II alikuwa mtoto wa kiume wa Thutmose III na mke mdogo, Hatshepsut-Meryetre. Amenhotep alikuwa kwa kweli ni mdogo aliyeshirikishwa kutawala na baba yake kwa Miaka 2 na Miezi 4 kwa mujibu wa rekodi za kihistoria za mambo ya nyakati moja tangu kutawazwa kwake ilikuwa ni tarehe "IV Akhet siku ya 1 kama inavyoonekana kwenye stela ya Semna ya Usersatet, utumishi wa mwana wa Mfalme (kama ushindi) wa Kushi chini ya Amenhotep II, wakati kwamba Tuthmose III ananukuliwa kuwa alifariki siku ya III Peret siku ya 30 kwenye Kaburi la Wasifa wa Amenemheb. Peter Der Manuelian kwenye kitabu chake cha mwaka 1987 cha "Lakujifunza kwenye Utawala wa Amenophis II," kinatupa tafsiri ya andiko kwenye stela ya Usersatet: "Mwaka 23, IV Akhet [siku] 1, Siku ya Sikukuu au Sherehe za kutawazwa kwa mfalme" (uk.21). Amenhotep alikabiliwa na uasi mkubwa huko Shamu kwenye jimbo la vassal la Naharin katika Mwaka wake wa 3 karibu nl mara tu baada ya kifo cha baba yake na akalipeleka \Jeshi kwa wa Levant ili kuukomesha uasi huo. Mfalme alijulikana vyema kutokana na uhdaifu wake na kutokuwa na uwezo kwake na inasemekana kuwa aliuawa kwa pigo moja tu na waasi 7 wa Mfalme wa Takhsy. Baad ya kutwaa au kuteka Kadesh na ndipo kwa ufanisi mkuwa sana kuikomesha kampeni yake ya kwanza huko Shamu, mfalme aliamuru miili ya wafalme saba itundikwe kichwa chini na miguu juu kwenye mti wa meli yake—ikiwa ni adhabu uliyojulikana na ya kawaida kufanyiwa viongozi wa uasi kama agizo ya Kifalme au Kifarao huko Misri. Alipofikia kwa Thebes wote ila mmoja wa wafalme hawa walichomwa moto kwenye kuta za mji. Mwingine alichukuliwa hadi kwenye jimbo lililojulikana la uasi wa Nubia na kumtundika kwenye kuta za mji wa Napata, kama mfano wa mchakato huu wa kujiinua kinyume cha Farao na kuvunja moyo upinzani wowote kutoka kwa Wanubi waliokuwa wanayapinga mamlaka ya Wamisri huko. Amenhotep II alikuwa amefanikiwa sana kwenye juhudi zake kwa kuwa hakuna maelezo yoyote ya kufanyika kwa uasi ulioandikwa kutoka kwa Wanubi wakati wa utawala wake – kama ilivyokuwa kwa mrithi wake Thutmose IV. Amenhotep pia alishambulia kwenye kampeni yake ya pili na ya tatu kwa Washami kwenye Mwaka wa 7 na 9 wa utawala wake. Maasi haya yote mawili yalisababishwa na uasi ya majimbo ya Washami kwenye Dola ya Misri, ambayo ni kama yalichochewa na watemi wa Kimisri kwa uasi wa Mashariki ya Karibu, Mitanni. Vita ya Mwaka wa 9 vilitokea kwenye viunga vya Niy na vilipelekea au kuwasababishia Wamisri kukosa udhibiti wa eneo lote zima lililoko katikati ya mito ya Orontes na Frati licha ya mbinu za Wamisri za kulundikana huko Retenu na kuwateka wafungwa au mateka wa vita 3,600 wa Apiru. Baadabaada ya kampeni hii, hakuna migogoro mingine zaidi iliyojitokeza katikati ya jitokeza katikati ya Wamitanni na Wamisri, na amani isiyorasmi iliwekwa kati ya Amenhotep na mfaalme wa Wamitanni. Kwa hiyo, Amenhotep alijikita kwenye mambo ya nyumbani lakini alihakikisha anaufanya ufalme wa Misri uidhibiti Kanaani na mali zote za Misri.

 

1408 KK Israeli waliingia Nchi ya Ahadi na kuwatiisha Wakanaani katika mwaka wa 16 wa Yubile ya 52 kufuatiwa na kifo cha Musa.

 

1401-1391 KK                        Tuthmosis IV (Dini potofu ya Aten inaibuka na Misri wanaiga imani ya Waisraeli ya kuamini Mungu mmoja)

1391-1353 KK                        Amenhotep III

1353-1335                               Amenhotep IV “Akhenaten” (Imani bandia ya kizushi ya Kimonotheisti inaibuka kwa kiwango kikubwa na kamili.)

1335-1334                               Semenkare (Malkia?)

1334-1325                               Tutankhamen

?                                              Malkia Ankhesenamun

Ankhesenamun- Aliolewa na na Tutankhamun akiwa na umri wa miaka kumi na tatu. Mfalme Tutankhamun alioa akiwa kijana sana, huenda alikuwa mdogo wa ummri wa miaka kumi. Sababu ya kufana hivyo ilikuwa ni kwamba mfalme wa Wamisri alitarajiwa awe na mke (wakati mwingine zaidi ya mmoja ambaye mwenye kumsaidia yeye kubeba majukumu mengine ya kiofisi yanayohusiana na mambo ya kidini ya ofisi yake. Tutankhamun alimuoa Ankhesenaten, mmoja wa mabinti wa baba yake Akhenaten na mama yake wa kambo Malkia Nefertiti, kwa hiyo, alikuwa ni dada yake binamu! Alikuwa mkubwa kidogo kuliko Tutankhamun mwenyewe, baadae, Ankhesenaten alibadilisha jina lake na kujiita Ankhesenamun, "Aliishi (ankhes) kwa (en) mungu Amun (amun)". Hapo mwanzoni kabisa aliitwa Ankhesenpa'aten na alizaliwa huko 'Kipindi cha Amarna huenda kwenye mji wa Akhetaten. Wakati wa ndoa yao, aliwazaa mapacha waliokuwa hawajatimiza wakati wao wa kuzaliwa. Kuna uwezekano mkubwa kwamba watoto hawa walikufa kwa sababu ya mahusiano yao ya udugu wa karibu wa damu.

 

1323-1319                                      Ay
1319-1307/5                                   Horemhab

1305-1196 KK     Kizazi cha 19    Rameses I

1305-1290

“Mwanzoni kabisa aliitwa Paramessu, hakuwa wa uzao wa kifalme, alizaliwa kwenye familia ya waungwana kutoka kwenye jimbo la  delta ya Nile, huenda ni karibu na Hyksos ya zamani ya Avaris kuu. Alikuwa ni askari mchukuzi, ambaye hapo mwanzoni kabisa alikuwa ni mbunif au mtunzi (kazi aliyoirithi kutoka kwa baba yake, Seti), na kufanyika kuwa jemadari kamili wa majeshi. Alipata upendeleo au kuhurumiwa na Horemheb, farao wa mwisho wa kichuguu ya Kizazi cha Kifalme cha kumi na nane, aliyemchagua Ramesses awe wariri mkuu. Alihudumu pia kama Kuhani Mkuu wa Amun – kana kwamba angeweza kuchukua jukumu muhimu kwenye marejesho mapya za dini ya kale ya ikifuatiwa na mafundisho ya kizushi ya Amarna wa kizazi kilichofuatia baadae chini ya Akhenaten.

Horemheb mwenyewe alikuwa mtu muungwana kutoka nje ya jamii ya kifalme ya haraka, waliotokea kwenye kutoka kwenye daraja za vyeo la majshi ya Wamisri ahudumu kama mshauri wa mfalme na hatimaye kuwa Farao. Akiwa hana mtoto wa kumzaa yeye mwenyewe wa kuendeleza msitari wa uzao wake, Horemheb alimchagua Ramesses ili kuwa mrithi wake kwenye miaka ya mwishoni ya utawala wake kwa kudhania tu kwa kuwa Ramesses I alikuwa kwa namna zote mbili, yaani mi kiongozi awezaye na alikuwa na mtoto na mjukuu (hatima yake Ramesses II) kumrithi yeye na kujiepusha na ugumu wa kurithisha.

Alipokuwa anarithishwa, Ramesses alichukua jina la kicheo, au jina ambalo lilikuwa limeandikwa kwenye orodha ya wafalme waliomtangulia wa Wamisri hadi kulipata lililosahihi au jema. Wakati alipolitamka, jina ni mn-pḥty-r‘, ambalo kwa kawaida linatafsiriwa kama Menpehtyre, maana yake ni "Aliyewekwa kwa nguvu au uweza wa Ra". Hata hivyo, anajulikana vyema kwa nomen yake, au jina lake la binafsi. Hili linatamkwa kwa lafudhi nyingine kama r‘-ms-sw, na kwa kawaida anajulikana kama Ramessu au Ramesses, maana yake ni 'Ra alimzaa yeye'. Already mzee wakati alipotawaza kuwa mfalme, Ramesses alimchagua mtoto wake, farao aliyefuatia baadae aitwaye Seti I, ili ahudumu kama mfalme mwenza. Seti alifanya operesheni kadhaa za kijeshi wakati huu – kwa kweli, jaribio la kuwaweka pamoja na kuwarejesha mahala pao Wamisri waliopotea huko Shamu. Ramesses anaonekana kuwa alichukua majukumu na uangalizi wa masuala ya nyumbani yanayo kumhukwa sana, aliikamilisha au kuimalizia awamu/pylon ya pili ya Hekalu la Karnak, lililoanza chini ya Horemheb (soma makala ya kwenye Tovuti/Wikipidia ya http://en.wikipedia.org/wiki/Ramses_I)

 

1290-1279 KK     Seti I

Kwenye ainema ya Amri Kumi za Mungu, Farao Seti I alikuwa anadhaniwa kuwa ni Farao ambaye kipindi chake Musa alikuwa ni Jemadari wa Misri, na mwanae Rameses II anaonyeshwa kuwa kama Farao wa kipindi cha Kutoka. Seti alikuwa tayari ni baba wa Rameses II wakati Horemheb alipomchagua yeye kuwa ni mrithi wake kama ni Farao. Alikuwa ni msimamizi mwenye uwezo. Mandiko ya Biblia tarehe zake hata hivyo vinamfanya Farao huyu, kwenye vipindi maalumu vya hivi karibuni kama aliyekubalika, ni mgombea asiyewezekana kaka Musa alikuwa amekwisha kufa tayari na Israeli waliishi kipindi cha kabla farao huyu hayatawazwa kuwa mfalme. Sababu inayopelekea wazo hili ni kwa sababu wataalamu wa mambo ya wafalme wa Kimisri waiiamua kwamba ufyatuaji wa matofali na kuyafanya kama vifaa pekee na vikuu kwenye ujenzi ilikuwa ni mashuhuri kwenye kipindi cha Ramesside. Biblia hata hivyo inaliweka tukio la Kutoka kwenye miaka ya 480 kabla ya kuanza kwa ujenzi wa Hekalu katika mwaka wa Arobaini wa Sulemani na ile inafanya tarehe hii kuwa ni mwaka 1448/7 KK. Biblia inasema kwamba Waisraeli waliujenga mji wa Rameses na ndipo inadhaniwa alikuwa ni hiki Kizazi cha Kifalme cha Rameses kilichokuwa kimehusika, kama walivyoujenga Pi-Ramesse. Hatanhivyo, jina la Rameses lenyewe limekutikana pia limeandikwa kwenye rangi za makaburi waliyozikiwa tangu Farao Amenhotep III, ambaye alitawala karibia karne moja kabla ya Rameses II.

 

1279-1213 KK                               Rameses II


Bwana au Lord Ameni
Merenptah

Seti II

Siptah

 


              

Kizazi cha Kifalme cha Mke wa Sulemani

 

Kizazi cha Kifalme cha Ishirini na Moja

 

Jina                                                                 Tarehe au Miaka

Smendes                                                          1069 KK - 1043

Amenemnisu                                                   1043 KK - 1039

Psusennes I                                                     1039 KK - 990

Amenemopet                                                   992 KK - 983

Osorkon the Elder                                           983 KK - 977

Siamun                                                            977 KK - 958

Psusennes II                                                   958 KK - 943C

 

Baada ya utawala wa Ramesses III, kulikuwa na hali ya kupingua kidogo kwa nguvu za kifalme katika Misri


 

Kizazi cha 22: Washindi waliowashinda Israeli na Yuda.

 

Kizazi cha Ishirini na Mbili

Kizazi cha Kifalme cha Ishirini na Mbili cha Misri kilikuwa ni mfuatano wa Meshwesh Wafalme wa Kilibya waliotawala tangu mwaka 945 KK au 943 KK hadi mwaka 720 KK. Waliishi huko Misri tangu Kizazi cha Ishirini. Manetho anasema kwamba kizazi chenye asili au chimbuko lake huko Bubastis, lakini wafalme huenda kwa kiasi fulani walitawala tangu Tanis, ambao ulikuwa ni mji wao kuu na ni mji yalikokuwepo makaburi yaliyochimbuliwa. Kizazi hiki mara nyingi kinachukuliwa kuwa ni sehemu ya Kipindi cha Tatu cha Zama ya Kati.

Jina                         Maelezo                                                                              Tarehe au Mwaka

Shoshenq I               Anasemekana kuwa ni Shishaq wa kwenye Biblia                    943 – 922 KK

 

Osorkon I                                                                                                                   922887 KK

 

Shoshenq II             aliufaidi utawala wauhuru wa karibu miaka  2 huko Tanis kwa mujibu wa Von Beckerath     887885 KK

 

Takelot I                                                                                                                     885872 KK

 

Harsiese A               mfalme tofauti wa huko Thebes aliyetawala wakati

                                 Osorkon II na utawala wa Takelot I.                                         880860 BC

 

Osorkon II               aliwasaidia Israeli kumshinda Shalmaneser III wa Ashuru

                                 kwenye Vita ya Qarqar mwaka 853 KK.                                  872837 KK

 

Shoshenq III                                                                                                               837798 KK

 

Shoshenq                 asichanganywe na Shoshenq VI – mwenyewe asilia                 798785 KK

(IV)"mkwazi"          Shoshenq IV kwenye kipindi cha kabla ya vitabu vya mwaka-1993 na makala za jarida

                                                                                                                                   

Pami                         aliwazika Mitamba wawili wa Ng’ombe au Apis Bulls kwenye utawala wake.    Ni mfalme tu ambaye whose Habari za matendo yake zilihifadhiwa kwenye kabrasha ya Annal mwaka     785778 KK

 

Shoshenq V                                                                                                                778 – 740 KK

 

Osorkon IV             ni mfalme mwingine tofauti aliyetawala kwenye Delta iliyomeguka 740 – 720 KK

                                 Dini ya Tefnakhte wa Sais na Iuput II wa Leontopolis            

Mfalme mwingine aliyetokana na kundi hili ni Tutkheperre Shoshenq, ambaye nafasi yake halisi kwenye kizazi hiki cha kifalme kwa sasa haieleweki. Kile kinachoitwa Kizazi cha Kifalme cha Ishirini na tatu kilikiwa ni chipukizi la kizazi hiki kilichotuama maeneo ya Misri ya Juu. Wafalme wake wote walitawala Misri ya Kati nay a Juu pamoja na Chemichemi za Magharibi mwa Jangwa walikuwa ni msaada wa kimadaraka wa stela kilichokadiriwa kupewa tarehe za utawala wa 13 Takelot III imekutwa kuwa ni.0 (sawa na Wikipidia).


 

Nyongeza ya 2: Uchambuzi wa Ratiba ya Ufunguo wa Daudi

 

Mwaka 1974 KK: Yubile ya 40 tangu kufungwa kwa bustani ya Edeni. Lbrahimu akiwa anakaribia wastani wa umri wa miaka 22. Alifikia umri wa utuuzima katika mwaka wa Sitini wa Yubile ya 39.

 

1785-1650 KK

Kizazi cha 13

Kipindi cha Pili cha Zama za Kati

1650-1554 KK

Kizazi cha 16

Utawala wa Hyksos kutoka Misri ya Chini

1650-1554 KK

Kizazi cha 17

Kamose Seqenenre II (Misri ya Juu)

1554-1305 KK            E

1554-1525 KK

Kizazi cha18

(Hyksos alipinduliwa)

Ahmose (Amosis I)

 

 

1528/7 KK

Musa alizaliwa mapema kabla ya kufariki kwa Ahmosis, na aliitwa jina lake na dada yake.

1525-1504 KK

Amenhotep I (Amenophis I)

1525 KK

Kifo cha Ahmose/Ahmosis I (wengine wanasema mwaka 1527). Mwaka huu ulikuwa ni mwaka wa Sabato wa mzunguko wa mwisho wa yubile ya 49. Ilishuhudia mwisho wa mauaji ya kuuliwa kwa watoto wa wana wa Israeli kwene kipindi chao cha mateso. Ufalme Mpya au Dola ilishuhudia kipindi cha zaidi ya karne moja na nusu cha kutoporomoka kwa uchumi na mafanikio. Amri ya kuwaua watoto wakiume wa Israeli huenda ilichochewa na hali ya kuonekana kwao kuwa walikuwa ni sehemu ya kizazi kilichochukiwa cha Hyksos. Amri hizi zilitolewa na mfalme huyu ili kuanzisha na kukishamirisha kizazi cha kifalme.

1524 KK        

Yubile ya 49

1504-1492 KK

Tuthmosis I

1492-1479 KK

Tuthmosis II

1488 KK

Musa alifikisha umri wa miaka 40 na anakimbilia Midian kipindi cha utawala wa Tuthmosis II, kwenye kipindi hiki cha miaka arobaini ya utawala wake, baada ya kumuua mlinzi. Kimfano hii inamaanisha ukomo wa zama ya kwanza. (Awamu ya kwanza ya Ufunguo wa Daudi inaanza.)

1479-1458 KK

Hatshepsut (Ma’atkare’) Malkia Regent

1473 KK        

Hatshepsut anajitawazwa mwenyewe kuwa Farao.

1479-1425 KK

Tuthmosis III

1448/7 KK

Kwa hiyo, ndani ya mlolongo huu, tukio la Kutoka utumwani lilitokea miaka kumi baada ya kifo cha Hatshepsut. Akiwa anatawala na mwana wa kambo na binamu yake alikuwa ni mjenzi mkuu na mwendelezaji wa Misri. Kitendo chake cha kujilimbikizia madaraka ya kifalme mwaka 1473 kilimpelekea kupinduliwa kwake madarakani na kupotezwa mwaka 1458.

1427-1401 KK

Amenhotep II

Ukweli wa kwamba alikuwa ni mtoto wa Farao kwa mke mdogo unaweza kuwa ni sawasawa na inavyosema Biblia kwamba mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao wa wakati wa Kutoka (Thutmoses III) aliuawa pamoja na wazaliwa wengine wa kwanza wa Misri.

1424 KK

Yubile ya 51

1408 KK

Israeli wanaingia kwenye Nchi ya Ahadi na kuwatiisha Wakanaani katika mwaka wa 16 wa Yubile ya 52 iliyofuatika kifo cha Musa.

1401-1391 KK

Tuthmosis IV (Dini ya Aten inaibuka na Wamisri wanaiga imani ya Waisraeli ya kuamini Mungu mmoja au umotheism.)                            

1391-1353 KK

Amenhotep III

1353-1335 KK           

Amenhotep IV “Akhenaten” Mafundisho ya kizushi na mapotofu ya Kimonotheisti yanaibuka kwa kiwango cha juu sana.

1335-1334 KK

Semenkare (Malkia Nefertiti?)

1334-1325 KK

Tutankhamen

?

Malkia Ankhesenamun

1323-1319 KK

Ay

1319-1307/5 KK     

Horemhab

1305-1196 KK

Kizazi cha 19

1305-1290

Rameses I

1290-1279 KK

Seti I

1279-1213 KK

Rameses II

Lord Ameni

Merenptah

Seti II

Siptah

1224 KK

Yubile ya 55

1074 KK

Yubile ya 58

1054 KK

Kuanguka Troy na Wahiti wa Magharibi wa Wilusia. Ripathian Celts anahamia Uingereza na wanaungana na masalia ya Tuathan De Danaan kutoka Ireland na kuwatiisha Wamagogu huko Uingereza.

1053/2 KK

Mwisho wa kipindi cha utawala wa Waamuzi 12 pamoja na Eli na Samweli. Utawala wa Wafalme unaanza kwa utawala wa Sauli.

1024 KK

Yubile ya 59

1012 KK

Utawala wa Daudi unaanza. Anatawala miaka saba huko Hebroni.

1005 KK

Dauidi anaingia Yerusalemu. Kipindi cha nusu kamili cha uumbaji, miaka 3000 tangu Adamu. Melkizedeki anatoa njia kwa Lawi huko Yerusalemu kwa Yubile 20 au miaka 1000 hadi kuzaliwa kwa Kristo akiwa kama Kuhani Mkuu wa mfano wa Melkizedeki.

974 KK

Yubile ya 60 tangu kufungwa kwa Bustani ya Edeni. (Nusu ya kipindi cha umri wa Shetani.)

972 KK

Daudi anamrithisha ufalme wake Sulemani. (Awamu ya kwanza Inaisha)

968/7 KK

Hekalu linaanza kujengwa katika mwaka wa Arobaini wa Sulemani.

948 KK

Hekalu pamoja na Nyumba za Mfalme na Nyumba ya Misitu ya Lebanoni ziliisha.

932 KK

Utawala wa Sulemani unaishia. (Awamu ya pili ya Ufunguo wa Daudi inaisha.)

932-924 KK

Kugawanika kwa Ufalme kutokana na ibada za sanamu za Sulemani zilizoyaingia makabila ya Kaskazini.

924 KK

Yubile ya 61: miaka 1000 au Yubile 20 hadi kwenye kutangazwa na Masihi kwa Mwaka wa Bwana Uliokubaliwa mwaka 27 BK.

Jedwali la 3

724 KK

Yubile ya 65: Kuzingirwa kwa Samaria kunapelekea kuondolewa kwa Israeli kutoka kwenye ardhi zake tangu Mwaka wa Sabato, Yubile, na mwaka wa 723 KK au Mwaka wa Kwanza wa Yubile Mpya. Miaka 250 tangu Yubile ya Daudi huko Yerusalemu na kumkabidhi kwake madaraka Sulemani.

722 KK

 

722 KK

Sargon II anaingamiza Samaria baada ya miaka mitatu ya kuizingira na kifo cha Shalmaneser V.

Israeli wanachukuliwa utumwani kwa awamu tatu: Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase upande wa mashari ya Yordani chini ya Pul au Tiglath-Pileser III. Kisha walifuatiwa na Wamedi kwa Waisraeli wa makabila ya upande wa magharibi chini ya Sargon II, ambaye aliwaangamiza pia Wahiti (Hatti or Kalti) upande wa kaskazini ya Shamu, Wakaldayo wa Urartu. Yuda walifuatia baadae. (Awamu ya tatu ya Ufunguo wa Daudi.)

605 KK       

Vita vya Carchemish. Nebukadneza anaipiga na kuishinda Misri.

598/7 KK    

Utumwa wa Yehoyakini (siku ya 2 WeAdar au 14/15 Machi 597). (Awamu ya nne ya Ufunguo wa Daudi.)

594 KK       

Maono ya Ezekieli (mwaka wa 30) (Ushahidi wa 1 wa Kimaandiko).

587

Kuanguka kwa Yerusalemu. (Awamu ya tano ya Ufunguo wa Daudi.)

Yuda wanapelekwa utumwani kwa kosa la kuihalifu sheria ya kuitunza Sabato ya mapumziko ya ardhi na kalenda. (Sehemu ya sita)

574 KK

Mwaka wa Yubile ya 68

539 KK

Kuanguka na kutekwa kwa Babeli na Koreshi na Dario Mmedi, mwana wa Astyages (aliyeitwa Ahauswero na Danieli).

538/7 KK

Tangazo la Koreshi na kurudi kwa waliokwenda utumwani kwenye nchi yao ya Palestina lakini sio Yerusalemu (tarehe kamili haijulikani).

530-522 KK

Utawala wa Cambyses.

525 KK

Kutekwa kwa Misri na Cambyses (Unabii wa Mikono Iliyovunjika ya Farao unatimilika kwenye awamu yake ya kwanza (soma jarida la Unabii wa Mikono Iliyovunjika ya farao  (Na. 36); soma pia Jedwali la 5 Uchambuzi wa Jedwali la Kipindi-Zama (Na. 272)).

524 KK

Yubile ya 69

522 KK

Utawala wa Mamajusi (Magi).

521 KK

Darius I

516 KK

Unabii wa miaka saba unafikia mwisho (Yeremia 25:8-14; Danieli sura ya 9). Yerusalemu inabakia ukiwa bila kukaliwa na watu hadi kipindi hiki. Maandiko hayatanguki.

486 KK

Ahauwero I. Barua aliyoandikiwa na kupelekewa hakuna majibu yaliyonukuliwa kuwa yalifanyika (Ezra 4:6).

465

Artashasta I (jina lake halisi Cyrus pia aliitwa Macrocheir au Longimanus). anasimamisha ujenzi wa Hekalu na shughuli zote za ujenzi zinasimama hadi kipindi cha utawala wa Dario Muajemi (Ezra 4:7-24).

424 KK

Yubile ya 71

424 KK

Uhauswero II (hakuandikwa kwenye biblia).

423 KK

Dario II anatoa tangazo la kuanza ujenzi wa Hekalu mwaka 422.

Majuma Saba ya Miaka yanaanza katika mwaka wa kwanza wa Yubile va 72.

418 KK

Ujenzi wa Hekalu ulikamilika katika mwaka wa sita wa Dario, siku ya 3 mwezi Adari.

404 KK

Artashasta II

398 KK

Tangazo la kupewa mahitaji linatolewa kwa ajili ya kurudi kwa Ezra (Ezra 7:1-26).

385 KK

Tangazo la pili la Artashasta II. Nehemia anafanywa kuwa liwali wa Yudea (385-372). Kuta za Yerusalemu zinajengwa (Nehemia 5:14).

375/4 KK   

Majuma saba ya kwanza ya miaka ya mtiwa mafuta ajaye au Masihi Danieli 9:25.

374/3 KK

Mwaka wa Yubile na wa Usomaji wa Torati. (Ushahidi wa 2 wa Kimaandiko)

323/1 KK

Ezra anafariki katika mwaka mmoja huohuo aliokufa Iskanda Mkuu (Seder Olam Rabbah 30). Kile kilichojulikana kama Kanuni ya kuhakiki Biblia ilifungwa. (Awamu ya saba ya Ufunguo wa Daudi inakamilika.)

27 BK

Mesihi anaitangaza Yubile ya 80 kama Mwaka wa Bwana Uliokubalika na anaanzisha Ushahidi  wa Agano Jipya kama Awamu ya nane ya Ufunguo wa Daudi.

30 BK

Sadaka ya Kristo na kupokelewa kwa Roho Mtakatifu. Kuanza kwa Yubile ya Arobaini ya Kanisa kuwa Jangwani.

62/3 BK

Mwisho wa kipindi cha Majuma 62 ya miaka na mabadiliko makubwa ya utaratibu wa kutoa zaka hadi kwa ule wa Melkizedeki. Kuuawa shahidi kwa Yakobo ndugu yake Kristo, askofu wa kwanza wa Yerusalemu.

70 BK

Mwisho wa Juma la Saba la Miaka na kubomolewa kwa Hekalu.

73BK

Kuanguka kwa Yudea na Masada.

77 BK

Yubile ya 81.

590-1850 BK

Miaka 1260 ya Mateso ya Kanisa.

1799

Miaka 2520 ya “myakati saba” tangu utumwa wa Israeli. Israeli wote wanaingia kwenye haki ya uzaliwa wa kwanza wa nchi au ardhi zao.

1916-1948

Kuanzishwa kwa Nchi au taifa la Wayahudi.

1916-1996

Mwisho wa unabii wa Mikono Iliyovunjika ya farao kwenye awamu ya pili. (Awamu ya tisa inaisha 1996.)

1939-1945

Dola ya Mnyama na Mpingakristo wa Pili akijaribu kuliangamiza Kanisa na taifa la Yuda kwa kutumia mbinu ya mauaji makubwa ya kuangamiza Wayahudi na Watunza Sabato wa Ulaya, maarufu kama Holocaust.

1977

Yubile ya 119, mwanzo wa nyakati za mwisho. (Awamu ya tisa inaanza.)

1987

Kupimwa kwa Hekalu kunaaza. Soma jarida la Kupimwa kwa Hekalu (Na. 137)

1997

Mwisho wa Wakati au Utimilifu wa Wamataifa na Miaka Thelathini ya Mwisho wa Maombolezo ya Musa.

1998-2005

Usomaji wa Torati ulifanyika kama mwisho wa nyakati mbili za ushuhuda.

2006-2012

Utakaso wa Mataifa unaanza (soma jarida la Utakaso wa Mataifa (Na. 77).)

2012

Injili inahubirikwa kwa mataifa yote. Usomaji wa tatu wa Torati. Mwanzo wa kipindi cha Kuiwekaji wakfu Madhabahu tayari kwa marejesho mapya.

2015

Mwaka wa kutangazwa kwa Mfalme.

2019-2027

Kutiishwa kwa Mataifa wakati wa kurudi kwa Mfalme.

2027

Yubile ya 120 (Awamu ya Tisa inaishia).

2028

Milenia inaanza. Hekalu la Kimwili linaanza na utaratibu wa utawala unawekwa na unawekewa utaratibu (Awamu ya kumi ya Ufunguo wa Daudi.)

2028-2077

Dunia inafanywa upya na Torati ya Mungu inatumika rasmi kwa watu wote.

2028-3027

Milenia iliyo kama Mapumziko ya Sabato ya Yesu Kristo inaendelea. Kipindi cha Nne cha Hekalu kinaendelea.

3015

Shetani anafunguliwa tena na Vita vya mwisho vya Nyakati za Mwisho vinaanza. Yerusalemu unashambuliwa.

3027

Yubile ya 140: Ufufuo wa Pili wa Wafu. Awamu ya kumi inafikia kikomo kwa kushuka kwa Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe cha Hukumu.

3128

Mji wa Mungu Unashuka kutoka Mbinguni. Mwanzo wa Mbingu Mpya na Nchi Mpya.