Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[282D]

 

 

 

Utawala wa Wafalme

Sehemu ya IIIB:

Mtu Kama Hekalu la Mungu

 

(Toleo La 1.0 20120326-20120326)

 

Kwenye Sehemu ya III (A) tuliona Ufunguo wa Daudi na nafasi ya Sulemani kwenye Hekalu la Mungu na nafasi yake katika ujio wa Masihi. Kwenye sehemu hii tutaona HeKalu la Kiroho la Mungu ndani ya mwanadamu na jinsi linavyohusiana na mfumo wa nasaba damu ujulikanao kama DNA wa wanadamu na uhusiano wa vitabu vya Biblia katika kuelezea mpango wa Wokovu na Hekalu la Mungu likiwa kama uumbaji wa mwanadamu.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 2012 Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Utawala wa Wafalme Sehemu ya IIIB: Mtu Kama Hekalu la Mungu



Utangulizi

Kwenye jarida la Utawala wa Wafalme Sehemu ya III; Sulemani na Ufunguo wa Daudi (Na. 282C) hekalu na Ufunguo wa Daudi vimeelezewa na kufafanuliwa lakini muundo wa Hekalu ama utaratibu wake kama Nguvu za Kiroho ndani ya Mwanadamu haikuelezewa na hata haikuelezewa kuhusu jukumu la Biblia kama neno la Mungu haikuelezewa pia. Jarida hili linachukua Sehemu ya III katika kuelezea kuhusu Hekalu la Kiroho na linafafanua kuhusu Biblia na uhusiano wake na Hekalu.

 

Biblia kama Neno la Mungu

Biblia imetengenezwa kwa mjumuisho wa vitabu 66 vilivyogawanywa kwa sehemu mbili kuu zinazojulikana kama Agano la Kale na Agano Jipya ingawa hapo mwanzoni ilichapishwa kwenye tafsisiri ya KJV katika migawanyo sita ambazo ni tarakimu ya kibinadamu.

 

Muundo wa Biblia ni:

 

Agano la Kale

Mgawanyo wa Agano la Kale unajumuisha vitabu 12 kutoka kitabu cha Mwanzo hadi 2Wafalme, kisha vitabu vingine 14 na 1 na 2Mambo ya Nyakati. Idadi hii ina maana yake katika kufanya migawanyo miwili ya saba inayokamilisha idadi na kufanya jumla ya 14.

 

Marejesho ya utaratibu wa maongozi ya Torati yalikuwa yamekwisha kamilika kwenye kitabu cha 15 na cha 16 vilivyoandikwa na Ezra na Nehemia. Utaratibu wa ukamilishaji wa Hekalu ulikuwa kwenye kitabu cha 22 kinachoishia kwenye Wimbo Uliobora. Alfabeti za Kiebrania ziko 22 zinazomaanisha hitimisho.

 

Kitabu cha 23 kilikuwa cha nabii Isaya. Kwenye Isaya 53:4-5 tumepewa utaratibu na maana ya Masihi ambaye ndiye alikuwa Mwanzilishi wa Hekalu la Kiroho na Kuhani wake Mkuu. Lilikuwa ni andiko hili ambalo Towashi wa Kihabeshi alikuwa akilisoma na likafafanuliwa maana yake na Filipo na kisha akabatizwa na akapewa uweza wa kumpokea Roho Mtakatifu. Hatimaye Filipo akatwaliwa na kutoweka machoni pake kimiujiza.

 

Tarakimu au nambari hii inafikia kuonysha maana ya mwanadamu kwenye Nyanja za uumbaji. Ni kitabu cha 23 kwenye Biblia na kinauhusiano wa kitarakimu na ya Kromosomu kwenye mwili wa mwanadamu na inafanya mrejesho wa DNA ya mfumo wa Mwanadamu ambayo kwayo mwanadamu aliumbwa kwayo ili aweze kumpokea Roho Mtakatifu kwa kupitia dhabihu aliyojioa Kristo na inajumuisha vipengele 46 za mateso ya Kristo ambazo ni idadi ya pea za mfumo wa DNA ya Mwanadamu na inawakilishwa kwa Nguzo za Hekalu la Mungu kama tutakavyojionea hapo chini.

 

Agano hili la Kale linaendelea kwa kutukumbusha Manabii Wakuu pamoja na Yeremia na Maombolezo na pia vitabu vya Ezekieli na Danieli ambali waliongelea sana kuhusu muundo wa Uumbaji na ukamilishaji wa sehemu au awamu ya Kwanza hadi kwenye Ufufuo wa wafu wa Kwanza ambapo ni Naos au Patakatifu pa Patakatifu. Hivyo ni vitabu 27 hadi kufikia mahali hapa. Awamu inayofuatia kwenye Manabii Wadogo 12 wanaoshughulika na mwisho wa awamu ya Kwanza na ujenzi wa Hekalu la Milenia litakalotumika kipindi cha Masihi. Kwa hiyo, Agano la Kale linahitimika kwa jumla ya vitabu 39 vya kazi iliyovuviwa vyote.

 

Agano Jipya

Agano Jipya ni mjumuisho wa Injili Nne na Kitabu cha Matendo ambazo ni vitabu vitano vinavyotangulia hadi kufikia siku watu walipompokea Roho Mtakatifu wa Neema kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, na kuanzishwa ramsi kwa Kanisa la Mungu kama Hekalu la Mungu.

 

Kisha kuna nyaraka nyingine za Makanisa Saba zinazohitimisha idadi ya vitabu vinane zinazoonyesha mwingiliano wa kimahusiano na Makanisa Saba ya Mungu.

 

Nyaraka za Wakorintho na Wathesalonike kama kazi mbili zinafanya kuwa na jumla ya vitabu tisa. Waraka wa 1Wakorintho ni kitabu cha 46 ambacho kinatueleza sisi kuwa sisi tu Naos au Hekalu la Mungu. Tarakimu ya 46 ni kipimo cha Nguzo za Hekalu la Mungu na pia ni tarakimu ya pea kwenye vijino vya DNA na inaonyesha ukweli wa kuumbwa kwa mwanadamu akiwa na kipimo nasaba kamili cha mfumo wa DNA kama Hekalu la Mungu na inatuonyesha kusudi la uumbaji wa wanadamu wote. Nguzo mbili zinaonyesha aina mbili za DNA na kipomo X na Y cha nasaba ya ute au kromosomu: X kwenye kipima nasaba cha mtDNA cha mwanamke na Y cha mfumo YDNA ya mwanaume.

 

Sehemu au mgawanyo wa mwisho ni ule wa Vitabu Kumi na Viwili vya mfuatano wa nyaraka walizoandikiwa watu binafsi tangu nyaraka za I na II za Timotheo, Tito, Filemoni, Waebrania, Yakobo, I na II Petro, I, II na III Yohana, Yuda ambazo zinafanya kuwa na jumla ya vitabu 65. Yuda alikuwa ni Ndugu yake Kristo na ndiye aliyeelezea juu ya Imani Iliyotolewa Mara Moja tu ambayo ndiyo makusudi au malengo ya maandiko yaliyovuviwa na ndiyo iliyofanya waraka wa kumi na mbili wa watu binafsi. Kumi na mbili ni tarakimu ya ukamilifu.

 

Kitabu cha Ufunuo ni cha 27 kwenye Agano Jipya na ni cha 66 cha vitabu vya maandiko yaliyovuviwa zikimaanisha ukamilifu wa uumbaji wa mwanadamu. Kumi na Tatu ni tarakimu inayomaanisha au kuashiria Uasi na kitabu hiki cha Ufunuo ni cha nne katika vitabu alivyoviandika Mtume Yohana, ambapo wakara wa IYohana unaanza kwa kuionyesha Nuru na ushirikiano wa mwanadamu na Mungu na Kristo ambaye alikuwa ni mtetezi kwa Baba wa watenda dhambi wote. Sura ya 2 inaelezea umuhimu wa kuzishika amri za Mungu na kwa mtu kama huyo upendo wa Mungu unakamilika na dhambi za ulimwengu zinashindwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu ambaye ni mwalimu wa watu wote. Sura ya 3 inaonyesha kwamba kwa kupitia ushindi huo sasa tunakuwa wana wa Mungu na ulimwengu hautujui. Kwenye kifungu cha sura ya 3:4 tunaambiwa kwamba dhambi ni kile kitendo cha kuzivunja amri na hatutaweza kujiepusha na dhambi hadi pale tutakapozishika sheria na amri hizi. Mtume Yohana anaelezea kwenye nyaraka zake akutuandaa sisi kwa ajili ya Siku za Mwisho. Ufunuo ambao ni kitabu cha Kumi na Tatu kwenye mlolongo huu na ni kitabu cha mwisho kina idad ya Uasi huu. Ufunuo ni ujumbe ulioandikwa kwa ajili ya Makanisa Saba ya Asia. Kinatuonyesha kuwa sisi tumefanyika kuwa wafalme na makuhani kwa Mungu wetu. Kinamtaja kuwa ni Alfa na Omega, Bwana aliyeelezewa kwenye maandiko (soma jarida la  Ustadi wa Kazi ya Uumbaji wa Mungu kama Alfa na Omega (Na. 229) [Arche of the Creation of God as Alpha and Omega (No. 229)]. Sura za 2 na 3 zinashughulikia matatizo yaliyojitokeza kwenye Makanisa Saba, yakwa kama kielelezo cha tangu wakati huo hadi kuja kwa Masihi. Tangu sura ya 4 tunakiona kiti cha Enzi cha Mungu na roho saba za Mungu ambazo ni miongoni mwa makanisa saba. Vitabu vya Mihuri Saba ndipo sasa vinafunguliwa na Mwanakondoo anaonekana kuwa ndiye anayestahili kuzifungua Siri za Mungu, na athari mbaya za Dini ya Uwongo zinafunuliwa kutoka kwenye ile Mihuri Saba hadi kwenye Mhuri wa Tano na Ujio wa Masihi kuja kuwaokoa wanadamu kutoka kwenye yenyewe na kuanza kwa Utawala au Ufalme wa Mungu kupitia kwa Roho Mtakatifu chini ya Masihi nao unaelezewa kwa kina. Uasi unaotokana na uangamivu mkubwa na kuangamia kwa wale waliokuwa kwenye uasi na Ufunuo 12:17 na 14:12 inatuonyesha kwamba wateule wa Mungu ni wale wanaozishika Amri au Sheria za Mungu na Ushuhuda au Imani ya Yesu Kristo. Imani potofu ya dini ya uwongo ya mfumo wa Kibabeli ya siri na ambayo ndiyo unatawala dunia pamoja na uharibifu wake imeelezewa kwenye sura za 18 na 19 tunaziona, kutoka kwenye uangamivu wake, mwendelezo na kuziabudu mbingu kwenye Ufalme wa Mungu na Karamu ya Arusi ya Mwanakondoo, ikifanywa na wateule wakiwa wametengwa mbali na kutokuwa na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza wa wafu. Kwenye Sura ya 20 mwandamano wa matukio ya ufufuo wa Kwanza na wa Pili nay a Kiti cha Enzi, Kikubwa Cheupe cha Hukumu vinaelezewa na mwandamano wa matukio haya unaishia kwenye Sura za 21 na 22 kwa kuonyeshwa Mji wa Mungu na madhumuni au malengo ya uumbaji wa kila kilichoko duniani yanafunuliwa kwenye fumbo au Siri za Mungu. Mchakato wote mkamilifu unafunuliwa kwenye Sura ya 22 kwa Roho Mtakatifu kutufanya sisi sote kuwa ni wana wa Mungu pamoja na Malaika wa Mbinguni na uumbaji wa vitu vyote vya kimwili unaishia kwa vitabu hivi 66 na nia yake yote ikiwa imeelezewa. Mlolongo unaofuatia haujaelezewa bado kama unavyokwenda kuwa kwenye uumbaji na Viumbe wa Kiroho jinsi utakavyokuwa na kuenea ukiwa kama ni mchakato wa Saba kwenye sehemu nyingine kumi na mbili ambazo hazijaandikwa bado ukiwa kama mambo ya mwisho ya Ufunguo wa Daudi kwenye Hekalu la Kiroho la kwenye Mji wa Mungu.

 

Sasa tutarejea kwenye Sehemu ya III (A) ili kutathmini sehemu ya Hekalu la Sulemani.

 

Hekalu la Kwanza

“Daudi alimuamuru Sulemani katika mwaka wa Kwanza wa Yubile ya 61. Maandalizi yalianza ili kwamba Hekalu liweze kujengwa kwa ajili yha Usomaji wa Torati uliotarajiwa kufanywa kwenye Yubile ile. Iligharimu muda wa miaka takriban ishirini kukamilisha ujenzi wa Nyumba ya Bwana na nyumba ya Mfalme na nyumba nyingine zilizojiri (tazama hapo chini). Ukamilishaji wake hii yote ulifanyika katika mwaka wa 25 wa yubile ya 61.

 

Hekalu lilianza mnamo mwaka wa Arobaini wa utawala wake Sulemani, ambao ni mwaka wa 968 KK.

 

Ujenzi wote na kuikamilisha Nyumba ya Mungu kwa kumalizia majengo mengine yaliyohitajika kulikamilika mnamo Mwezi wa Saba ulioitwa mwezi wa Ethanimu, au wa Tishri, na Sikukuu iliadhimishwa kwa siku 14.”

 

Maskani yenyewe asilia na utoaji wa sheria vilifanyika kwa zaidi ya miezi sita na Musa alikuwa na kazi kubwa ya kupanda mlimani na kushuka mara sita na aliimaliza kazi yake yote mnamo mwishoni mwa mwezi wa Eluli ili kwamba mwezi wa Ethanimu utakaswe na kubakia kuwa Mtakatifu tangu Siku ya Upigaji wa Baragumu. Mwezi wa Siwani uliwakilisha mwanzo wa utoaji wa sheria na ilikuwa imekamilika katika mwezi wa Eluli. Idi ya Ukumbusho wa kuzipiga Baragumu ilikuwa ni taswira ya Ujio wa Masihi katika Mwezi wa Saba ili kuja kuanzisha Milenia ya Saba tangu Uumbaji (soma pia jarida la     Upangaji Mlimani wa Musa (Na. 070) [The Ascents of Moses (No. 070)].

 

Hekalu la Kwanza hata hivyo lilikuwa halijaisha bado hadi kufikia Sikukuu ya Vibanda.

 

Kuendelea kutoka Sehemu ya III (A)

 

“Ni kama tuonavyo hapo chini, ujenzi halisi wa je jengo lenyewe ulichukua miaka saba na miezi saba na ulikamilika katika mwezi Nane wa mwaka wa Kumi na moja wa utawala wa Sulemani. Kwa hiyo ukamilishaji wake haukuwa kipindi muafaka kwa maadhimisho ya Sikukuu ya Vibanda ya mwaka ule. Kwa hiyo, kuna maana nyingine kwa ajili ya kipindi hiki. Hekalu lilifuatia baada ya Idi ya Pasaka, katika mwezi wa Pili wa mwaka wa Nne wa Sulemani na liliisha mwezi wa Nane wa Buli, au wa Heshavan (katikati ya Octoba/Novemba ya mwaka wa 487 tangu kipindi cha Kutoka kwao utumwani, ukiwa ni mwaka 961 KK).”

 

Mwandamano huu wa kipindi maalumu unaunda pia sehemu ya ufunguo wa Daudi. Vipindi maalumu vilivyotajwa kwa kuvitenganisha pia vina maana yake kwa ajili ya kipindi cha Siku za Mwisho cha tangu kurudi kwa Masihi na kuanzisha Hekalu la Kiroho, na hitimisho la mwisho la utawala wa kimwili na utaratibu wa Hekalu huko Yerusalemu.”

 

Kwa hiyo, Ufungua wa Daudi ni sehemu pia ya mlolongo wa kipindi na taswira ya Ujenzi wa Hekalu la kimwili na la Kiroho linaloelekea kwenye wongofu wa watu wa Mataifa na kuona jinsi watakavyopata nafasi sawia au kukubalika kwenye Hekalu ambalo ni Kanisa la Mungu.

 

“Katiika mwaka wa 28 na wa yubile, Torati ilisomwa kwenye Nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Kipindi chote kizima cha ujenzi kilijiri miaka 21 ya Utakaso wa Hekalu, na mwaka wa Sabato ulikuwa tayari. Mwaka wa 29 ulipelekea kwenye Yubile na ambao taifa lilikuwa limetakasika kwa kipindi kile chote pia. Kwa hiyo ilikuwa ni miaka elfu tatu hadi kuanzishwa kwa utawala wa millennia wa Yesu Kristo katika Yubile ya 120 ya tangu uumbaji kutoka ilipofungwa Bustani ya Edeni ambao ni aawa na mwaka 2027BK.

 

Yubile 60 ziliyosuatia ziliweka taswira ya ujenzi wa taratibu wa kimwili wa Kanisa na wa utawala wa serikali ya Mungu. Ni wazi kwamba Mungu anajishughulisha kipekee kwenye utaratibu wa Yubile na anavitumia vipindi vya Yubile kwa mgawanyo wa kitarakimu wa 10, 20 na 40.

 

Kutoka kwenye maandiko ya Agano la Kale ni wazi sana kwamba Masihi alipaswa kuinuliwa kwenye Yubile ya mwaka 27BK na huduma yake ianze rasmi mwaka 28BK. Ilimpasa afe ili awaokoe wenye dhambi. Ni sawa tu na ilivyo wazi kabisa kwamba ilimpasa kufanya Upatanisho na kisha arusi tena akiwa kama Mfalme Masihi. Kipindi hiki maalumu kilipasa kichukue miaka elfu sita ya uumbaji wa Mungu na kuishia na Yubile ya 120 mnamo mwaka 2027.

 

Tangu wakati ule, kipindi cha Utawala wa Masihi kingeanza tangu mwaka 2028 hadi mwaka 3027, kipindi kijulikanacho kama ni mapumziko ya Sabato ya Masihi. Baada ya kipindi hicho kitafuatiwa na cha Hukumu itakayofuatiwa na Ufufuo wa Pili wa wafu au wa Wote waliokufa Mautini.

 

Maandiko yanasomeka yakisema hivi:

1Wafalme 6:1-38 Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya Bwana. 2 Nayo nyumba hiyo mfalme Sulemani aliyomjengea Bwana, urefu wake ulikuwa mikono sitini, na upana wake ishirini, na kwenda juu kwake mikono thelathini. 3 Na ukumbi mbele ya hekalu la nyumba, urefu wake ulikuwa mikono ishirini, kadiri ya upana wa nyumba; na upana wake mikono kumi mbele ya nyumba. 4 Akaifanyia nyumba madirisha ya miangaza yenye kimia. 5 Nao ukuta wa nyumba akauzungushia vyumba, kushikamana na kuta za nyumba kote kote, za hekalu na za chumba cha ndani; akafanya vyumba vya mbavuni pande zote. 6 Chumba cha chini kilikuwa mikono mitano upana wake, na chumba cha katikati kilikuwa mikono sita upana wake, na chumba cha tatu kilikuwa mikono saba upana wake; kwa kuwa upande wa nje akaupunguza ukuta wa nyumba pande zote, ili boriti zisishikamane kutani mwa nyumba. 7 Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba. 8 Mlango wa vyumba vya chini ulikuwapo upande wa kuume wa nyumba; mtu hupanda madaraja ya kuzunguka mpaka vyumba vya katikati, na kutoka vile vya katikati mpaka vile vya tatu. 9 Basi ndivyo alivyoijenga nyumba, akaimaliza; akaifunika nyumba kwa boriti na mbao za mwerezi. 10 Akavijenga vyumba mbavuni mwa nyumba yote, kwenda juu kwake kila kimoja kilikuwa mikono mitano; vikaitegemea nyumba kwa boriti za mwerezi.

 

Mawe ya kujengea Hekalu yalikuwa yanachongwa au kuandaliwa sehemu nyingine mbali na uwanja linapojengewa na yaliletwa kwenye eneo la ujenzi. Na ndivyo ilivyo kwamba mawe yaliyohai yamekwisha tengenezwa tayari kutoka maeneo yaliyo mbali na Yerusalemu na yanaletwa huko ili kuanzishwa kwa Hekalu la Kiroho wakati atakaporejea Kristo. Yako alisia na makamioifu na hayahitaji kuchongwa tena yajapo kwenye uwanja wa ujenzi, kisha yajengewe na takataka zikiwa zimejichanganya pamoja nayo.

 

Kwahiyo kuna aina mbili za ujenzi ; moja ni kwenye uanzishaji wa haya Mawe yaliyo Hai; na mwingine ni ule wa utaratibu wa maongozi ya kimwili wa chini ya maongozi ya Torati kutoka Yerusalemu.”

 

Mambo mawili tofauti ya utaratibu au muundo yalikuwa ni wa kimasharti ya mtu kuwa mtiifu kwenye neno la Mungu ambalo lenyewe tu kama lilivyo lilitaswirisha uumbaji na lengo la uumbaji huo kwa mionekano ya namna mbili, ya vitabu 66 vya neno la Mungu ambalo ndilo lengo ambalo Kristo alikuja kwa muonekano wa namna mbili, mmoja kama Malaika wa Uwepo wake au Memra na mwingine ni kama Mwana wa Adamu akiwa ni Neno au Logos anayeonekana kimwili. Tunaendelea mbele kwenye Sehemu ya III (A).

 

“Kwenye ukenzi wa Hekalu neno la Mungu ndipo alipewa Sulemani, aweke agano imara kwa Israeli kulikuwa ni lazima katika kuonyesha kwake utii.

 

11 Neno la Bwana likamjia Sulemani, kusema, 12 Katika habari ya nyumba hii unayoijenga, kama ukienda katika sheria zangu, na kuzifanya hukumu zangu, na kuzishika amri zangu zote na kwenda katika hizo; ndipo nitakapolithibitisha neno langu kwako, nililomwambia Daudi baba yako. 13 Nami nitakaa katikati ya wana wa Israeli, wala sitawaacha watu wangu Israeli. 14 Basi Sulemani akaijenga hiyo nyumba akaimaliza. 15 Akazijenga kuta za nyumba ndani kwa mbao za mwerezi; toka sakafu ya nyumba hata boriti za juu, akazifunika ndani kwa mti; akafunika sakafu ya nyumba kwa mbao za mberoshi. 16 Akajenga mikono ishirini pande za nyuma za nyumba toka chini hata juu kwa mbao za mwerezi; naam, ndani akaijengea chumba cha ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu. 17 Nayo nyumba, ndiyo hekalu la mbele, ilikuwa mikono arobaini. 18 Na ndani ya nyumba, mlikuwa na mwerezi ulionakishiwa maboga na maua yaliyofunuka wazi; mlikuwa na mwerezi mahali pote; wala mawe hayakuonekana. 19 Akaweka tayari chumba cha ndani katikati ya nyumba ndani, ili atie humo sanduku la agano la Bwana. 20 Na ndani yake chumba hicho cha ndani mlikuwa na nafasi, mikono ishirini urefu, na mikono ishirini upana, na mikono ishirini kwenda juu kwake; akaifunika na dhahabu safi. Akaifunika madhabahu nayo kwa mwerezi. 21 Hivyo Sulemani akaifunika nyumba ndani kwa dhahabu safi. Akaitenga kwa mikufu ya dhahabu mbele ya chumba cha ndani; akapafunika na dhahabu. 22 Akaifunika nyumba yote kwa dhahabu, hata ilipokwisha nyumba yote; tena madhabahu yote iliyokuwa ya chumba cha ndani akaifunika kwa dhahabu. 23 Akafanya ndani ya chumba cha ndani makerubi mawili ya mzeituni, kwenda juu mikono kumi. 24 Na bawa moja la kerubi lilikuwa mikono mitano urefu wake, na bawa la pili la kerubi mikono mitano; mikono kumi toka mwisho wa bawa moja hata mwisho wa bawa la pili. 25 Na kerubi la pili lilikuwa mikono kumi; makerubi yote mawili walikuwa ya cheo kimoja na namna moja. 26 Kwenda juu kwake kerubi moja kulikuwa mikono kumi, na kerubi la pili vivyo. 27 Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani; na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko; mabawa yao yakagusana katikati ya nyumba. 28 Akayafunika makerubi kwa dhahabu. 29 Akazinakshi kuta zote za nyumba kwa nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, pande za ndani na nje. 30 Na sakafu ya nyumba akaifunika na dhahabu ndani na nje. 31 Akayafanyia maingilio ya chumba cha ndani milango ya mzeituni; kizingiti na miimo ilikuwa ya pande tano. 32 Hivyo akafanya milango miwili ya mzeituni; akanakshi juu yake nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, akaifunika kwa dhahabu; akatia dhahabu juu ya makerubi, na juu ya mitende. 33 Ndivyo alivyoyafanyia maingilio ya hekalu miimo ya mzeituni, yenye pande nne; 34 na milango miwili ya mberoshi; mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa za kukunjana, na mbao mbili za mlango wa pili za kukunjana. 35 Akanakshi juu yake makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi; akazifunika kwa dhahabu iliyonyoshwa juu ya machoro. 36 Akaijengea behewa ya ndani safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi. 37 Katika mwaka wa nne nyumba ya Bwana ilitiwa msingi, katika mwezi wa Zivu. 38 Hata katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, na sharti zake zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.

 

Hii ni hatua ya kwanza ya mafuatano ya Ufunguo wa Daudi na inahusiana na utaratibu wa kwanza, ambao ni Nyumba ya Mungu iliyojengwa kwa Mawe Yaliyohai, na mlolongo ule unahusiana na kurudi kwa Masihi na hitimisho lake kwa Mataifa.”

 

Nyumba ya Sulemani

“Nyumba ya Sulemani ilijengwa kwa kipindi cha miaka kumi na mitatu; kisha akajenga nyumba kutokana na miti iliyotoka kwenye Misitu ya Lebanoni pia. Hekalu ndilo lilikuwa juhudi yak kubwa alipoiweka na hadi kukamilika kwake lilijengwa kwa jumla ya miaka ishirini. Na pia alimchukua binti wa Farao na kumuweka nyumbani mwake mwenyewe kama mke wake.

 

Mlolongo huu wa matukio kama tunavyouona, ulichukua miaka saba na miezi saba kwa Nyumba ya Mungu na kisha miaka mingine mitatu kwa ajili ya Nyumba ya Mfalme, Ukumbi wa kutolea Hukumu, na Nyumba ya Misitu ya Lebanoni.

 

1Wafalme 7:1-51 Naye Sulemani alikuwa katika kuijenga nyumba yake mwenyewe miaka kumi na mitatu, akaimaliza nyumba yake yote. 2 Kwa kuwa aliijenga nyumba ya mwitu wa Lebanoni; mikono mia urefu wake, na mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake, juu ya safu nne za nguzo za mwerezi, na mihimili ya mwerezi juu ya nguzo. 3 Ikafunikwa juu kwa mwerezi juu ya mihimili arobaini na mitano, iliyokuwa juu ya nguzo; kumi na mitano kwa safu. 4 Na madirisha yalikuwako safu tatu, mwangaza kuelekea mwangaza katika madaraja matatu. 5 Na milango yote na miimo ilikuwa ya mraba, ilivyoangaziwa; na mwangaza kuelekea mwangaza katika madaraja matatu. 6 Akaifanya baraza ya nguzo; mikono hamsini urefu wake, na mikono thelathini upana wake; na ukumbi mbele yake; na nguzo na mihimili minene mbele yake. 7 Akaifanya baraza ya kiti cha enzi, ili ahukumu ndani yake, ndiyo baraza ya hukumu; nayo ikafunikwa mwerezi tangu sakafu mpaka dari. 8 Nayo nyumba yake atakayokalia, katika behewa nyingine iliyokuwa ndani kupita baraza, ilikuwa ya kazi kama hiyo. Tena akamjengea nyumba binti Farao, (ambaye Sulemani alikuwa amemwoa), mfano wa ile baraza. 9 Hizi zote zilikuwa za mawe ya thamani, mawe ya kuchongwa, sawasawa na cheo, yaliyokatwa kwa misumeno, ndani na nje, tangu msingi hata mawe ya juu, na nje vile vile hata behewa kuu. 10 Nao msingi ulikuwa wa mawe ya thamani, mawe makubwa, mawe mikono kumi, na mawe ya mikono minane. 11 Na juu kulikuwa na mawe ya thamani, mawe ya kuchongwa, sawasawa na cheo, na mierezi. 12 Na behewa kubwa pande zote ilikuwa na safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi; mfano wa behewa ya ndani ya nyumba ya Bwana, na ukumbi wa nyumba.  

 

Hiramu alimsaidia kwenye ujenzi huu. Huyu Hiramu alikuwa nusu Muisraeli. Baba yake alikuwa ni mtu wa Tiro na mama yake alikuwa ni mjane kutoka kabila la Naftali. Kwa hiyo yalikuwa ni mataifa rafiki na yanayoshirikiana pia na washirika wa kuaminika wa Israeli na leo ni kama tunavyojionea kwenye maandiko yaliyotajwa hapa chini.

13 Mfalme Sulemani akatuma watu kumleta Huramu kutoka Tiro. 14 Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila ya Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, mstadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikilia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote. 15 Kwa maana alizifanyiza zile nguzo mbili za shaba, mikono kumi na minane kwenda juu kwake kila moja; na uzi wa mikono kumi na miwili kuizunguka nguzo hii au hii. 16 Akafanya taji mbili za shaba iliyoyeyushwa za kuwekwa juu ya vichwa vya nguzo; kwenda juu kwake taji moja mikono mitano, na mikono mitano kwenda juu kwake taji ya pili. 17 Kulikuwa na nyavu kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa taji zilizokuwako juu ya vichwa vya nguzo; saba kwa taji moja, na saba kwa taji ya pili 18 Hivyo akazifanya nguzo; na kulikuwa na safu mbili za kuzunguka juu ya wavu mmoja, zifunike taji zilizokuwako juu ya vichwa vya nguzo; akafanya vivyo hivyo kwa taji ya pili. 19 Na taji zilizokuwa juu ya nguzo ukumbini zilikuwa za kazi ya mayungi, mikono minne. 20 Kulikuwako tena taji juu ya nguzo mbili, karibu na uvimbe uliokuwako kando ya wavu; na makomamanga yalikuwa mia mbili, safu safu pande zote juu ya taji ya pili. 21 Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kuume, akaiita jina lake Yakini; akaisimamisha nguzo ya kushoto ,akaiita jina lake Boazi. 22 Na juu ya nguzo kulikuwa na kazi ya mayungi; hivyo mambo ya nguzo yakatimia. 23 Tena akaifanya bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ikaviringana, na mikono mitano ilikuwa kwenda juu kwake; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa. 24 Na chini ya ukingo wake kulikuwa na maboga yaliyoizunguka, kwa mikono kumi, yakiizunguka bahari; kulikuwa na safu mbili za hayo maboga, yakafanywa kalibuni hapo bahari ilipofanywa. 25 Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani. 26 Na unene wake ulikuwa nyanda nne; na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu mbili. 27 Akayafanya yale matako kumi ya shaba; mikono minne urefu wa tako moja, na mikono minne upana wake, na mikono mitatu kwenda juu kwake. 28 Na kazi ya matako ndiyo hii; yalikuwa na papi; na papi zilikuwa katikati ya vipandio; 29 na juu ya papi zilizokuwa katikati ya vipandio kulikuwa na simba, na ng'ombe, na makerubi; na juu ya vipandio kulikuwa na tako; na chini ya simba na ng'ombe kulikuwa na masongo ya kazi ya kupembeza. 30 Kila tako lilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vipini vya shaba; na miguu yake minne ilikuwa na mataruma; chini ya birika yalikuwako mataruma ya kusubu, yenye masongo kila moja mbavuni. 31 Na kinywa chake ndani ya taji na juu yake kilikuwa mkono mmoja; na kinywa chake kikaviringana kama kazi ya tako, mkono mmoja na nusu; tena juu ya kinywa chake kulikuwa na nakshi, na papi zao zilikuwa za mraba, wala hazikuviringana. 32 Na magurudumu manne yalikuwa chini ya papi; na mikono ya magurudumu ndani ya tako; na kwenda juu kwake gurudumu moja mkono mmoja na nusu. 33 Na kazi ya magurudumu ilikuwa kama kazi ya gurudumu la gari; mikono yake, na maduara, na matindi, na vipande vya ndani, vyote vilikuwa vya kusubu. 34 Kulikuwa na mataruma manne katika pembe nne za tako moja; mataruma hayo ni kitu kimoja na tako lenyewe. 35 Na juu ya tako kulikuwa na duara nusu mkono kwenda juu kwake; na juu ya tako mashikio yake na papi zake vilikuwa vya namna iyo hiyo. 36 Akachora juu ya mabamba ya mashikio yake, na juu ya papi zake, makerubi, na simba, na mitende, moja moja kama ilivyokuwa nafasi, na masongo pande zote. 37 Hivyo akayafanya yale matako kumi; yote yalikuwa ya kalibu moja, na cheo kimoja, na namna moja. 38 Akafanya birika kumi za shaba; birika moja huingia bathi arobaini; na kila birika ilikuwa mikono minne; birika moja juu ya tako moja, katika yale matako kumi. 39 Akayaweka yale matako, matano upande wa kuume wa nyumba, na matano upande wa kushoto wa nyumba; akaiweka ile bahari upande wa kuume wa nyumba upande wa mashariki, kuelekea kusini. 40 Tena Huramu akazifanya birika, na majembe, na mabakuli. Hivyo Huramu akazimaliza kazi zote alizomfanyia mfalme Sulemani katika nyumba ya Bwana; 41 zile nguzo mbili, na vimbe mbili za taji zilikuwa juu ya nguzo; na nyavu mbili za kuzifunika hizo vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo; 42 na makomamanga mia nne ya zile nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuzifunika hizo vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo; 43 na yale matako kumi, na birika kumi juu ya matako; 44 na ile bahari moja, na ng'ombe kumi na wawili chini ya ile bahari; 45 na masufuria, na majembe, na mabakuli; hata vyombo hivyo vyote, Huramu alivyomfanyia mfalme Sulemani, katika nyumba ya Bwana, vyote vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa. 46 Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sarethani. 47 Sulemani akaviacha vyombo vyote visipimwe kwa kuwa vilikuwa vingi mno; wala uzito wa shaba haukujulikana. 48 Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Bwana; madhabahu ya dhahabu, na ile meza iliyokuwa na mikate ya wonyesho juu yake ilikuwa ya dhahabu; 49 na vinara vya taa, vitano upande wa kuume, na vitano upande wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu safi; na maua, na taa, na koleo ya dhahabu; 50 na vikombe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu safi; na bawaba za dhahabu, za milango ya nyumba ya ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu, na za milango ya nyumba, ndiyo hekalu. 51 Hivyo ikamalizika kazi yote Sulemani mfalme aliyoifanya katika nyumba ya Bwana. Sulemani akaviingiza vile vitu alivyovitakasa Daudi baba yake, yaani, fedha, na dhahabu, na vyombo; akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Bwana.

 

Majina ya nguzo za Hekalu yamechukuliwa kutoka kwenye majina ya Waisraeli wawili. Mmoja ni  Yakini, wa kabila la Simeoni, wa uzao wa Wayakini. Wapili ni Boazi, alikuwa ni wa kabila la Yuda. Habari za Boazi zinafahamika sana. Alikujakuwa ni mume wa Ruthu na baba wa Obedi, baba yake Yese,baba yake Daudi na kisha hadi kufikia kwa Masihi (sona jarida la  Ruthu (Na. 27)). His name Boaz (SHD 1162) is from an unused root of uncertain meaning and was only applied to this man, the ancestor of David. With different vowels it may relate to being strengthened.

 

Jina la Yakini (Yachin, SHD 3199) maana yake: Yeye ataanzisha, au Yah (au kiukamilifu wake Yaho[vah]) ataanzisha na atakuwa tayari zaidi kama inavyoonekana kama rejea ya maana ya jina la Mungu kama ndiye anayelengwa kunenwa kwamba Ndiye yeye atakayeanzisha.

 

Ingawaje hatuwezi kupuuzla ukweli kwamba Simeoni walikuwa watawanyike huku na huko katika Israeli, bali angeweza pia kujionea mzao wake Daudi, na kwamba Daudi aliitwa kwa majina yote mawili, yaani nguzo za mababu imara wa uzao wake akiwa kama mfano wa Imani.

 

Inaonekana vyema sana kwamba taswira ya majina huashiria jukumu la Mungu katika uanzishaji wa Hekalu la Kiroho la Mungu.

 

Wakati kwamba jina la Boazi halionyeshi maana yake hasa kwa wazi, na pia limeelezewa kwa kazi yake ya ukombozi kwenye habari zilizo kwnye kitabu cha Ruthu. Kwa hiyo nguzo mbili zilizo kwenye lango la Hekalu humaanisha: Yeye atiaye nguvu (Bullinger anasema: Katika yeye ipo nguvu au uweza) na Yeye aanzishaye. Maana hizo zinaonyesha kiini cha matendo ya ujenzi wa Hekalu la mwisho la Kiroho la Mungu.

 

Pia yana maana nyingine tofauti maalumu na vipimo vyake vimepewa kitofauti kabisa kwenye idadi ya maandiko. Hii haikwanganyi sana, lakini sana tu kuwa ni tofauti tu kwa jinsi yalivyopimwa.”

 

Tutaona sasa jinsi uhusiano wa hizi nguzo ulivyo na jinsi tunavyotakiwa kutafsiri vipimo vyake.

 

“Kwenye 1Wafalme 7:15-16, nguzo mbili zimetajwa ili kupima vipimo vya dhiraa 18 kwenda juu kwake kwa nguzo moja, na ya pili ilikuwa na mikono kumi na mbili kwa mzunguko au duara. Zile kubwa zilikuwa na dhiraa 5.”

 

Kumbuka: dhiraa 18 huwakilisha misingi 18 ya muundo wa mfumo wa kipimo cha nasaba damu cha YDNA ya mwanadamu.

 

Idadi ya jumla ya dhiraa za nguzo zote na zile kubwa ni 23 kwenda juu na 12 kwa kuzunguka au kwa duara. Namba 12 inaonyesha hitimisho na ukamilifu wa kimuundo wa kazi ya Mungu pamoja na tarakimu nyingine ya 22. Namba 23 ni Genomu ya Mwanadamu kama tutakavyoona hapo chini.

 

Tunadhani kwamba nguzo hizi mbili zote zipo kwenye mtindo wa kisimetrikali na inashangaza sana kama inavyoonyesha kipimo cha urefu wa kwenda juu na duara kwa nguzo zote mbili. Yeremia 52:21-22 anatoa urefu wake kamili wa nguzo hizo na zile kubwa. 2Wafalme 25:17 inasema nguzo hizi zilikuwa 18 kwenda juu, pamoja na dhiraa 3 kwa zile kubwa za katikati. Kipimo hiki kwa uwezekano wote kukiwepo na mapambo ya jani, ambalo lilikuwa ni kazi ya ua kama ilivyoelezwa kwenye maandiko (1Wafalme 7:22).

 

Andiko lililo kwenye 2Mambo ya Nyakati linatoa nguzo kipimo kilivyojumuishwa cha dhiraa 35 na 5 kwa zile kubwa za katikati. Kwa hiyo, nguzo hizi ni za dhiraa 35 kwa 17.5 kila moja pamoja na nusu dhiraa kwa kuunganisha, na viwiko au egemezo za nguzo zilikuwa mikono 5.

 

Wafafanuzi wanaelezea tathmini yao kuwa tu ndiyo lengo la maandiko hayo. Tarakimu ya arobaini ni nambari ya toba, na nguzo, nguzo zinazoashiria ukombozi wa Mungu na uanzishaji wake kwa kipindi cha toba kilichowekwa kwa kila mmoja. Nguzo hizi zinaashiria maendeleo ya mwanadamu kwa kuingilia kwake Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Kipimo cha chokaa kilichotumiwa kujengea kila nguzo kilikuwa ni 1 kwa 6 pamoja na 2/3, ambacho ni kipimo cha mwanadamu cha mwili hadi kichwani, kwa karibu 1 hadi 7.”

 

Hata hivyo, vipimo hivi vinahusiana pia na kipimo cha muundo wa DNA cha Kromosomu 23 na jumla yake ni 46 kwenye pea 23 ambayo ni tarakimu ya pea za DNA. Dhiraa ni kipimo cha viumbe wote wawili, yaani cha malaika na kinaonyesha kusudi la mwisho la uumbaji kwenye Mji wa Mungu ambako mwanadamu na Malaika watakuwa viwango na hali sawa.

 

“Zile kubwa za katikati zinatofautiana kivipimo. 1Wafalme 7:20 inasema kwamba kulikuwa na komamanga kwenye zile kubwa za katikati zilikuwa mia mbili kwenye mistari inayozunguka kuhusu sura hizi. Ile nguzo iliyosimamishwa upande wa kuume ilimuwakilisha Yakini/Jachin na ile ya upande wa kushoto ni Boazi. Zaidi sana kwenye aya ya 42 inasema zilikuwa ni mia mbili ili kuzionyesha kuwa ni mia mbili zilichukuliwa kwa kila kubwa (soma pia 2Mambo ya Nyakati 4:13). Kwenye 2Mambo ya Nyakati 3:16 zimeitwa mia moja, ikimaanisha, zilikuwa mia moja kwenye kila mstari. Yeremia 52:23 inasema kwamba mistari hii ya Ruachi au kwenye mwelekeo wa upepo (yaani imefunuliwa) kuwa zilikuwa 96.”

 

Mia mbili kwenye kila zile kubwa sio hakika sana lakini zimepewa nguvu kwa kulinganishwa na idadi ya Genomu za Mwanadamu huenda inahusianishwa na DYS ndani ya YDNA zinazofanya uwezo wa kujikinga mara 400.

 

“2Mambo ya Nyakati pia inaendelea kwa kusema kwamba ukumbi moja liliuwa na kipimo cha ujazo cha 120, kikitumia me’ah (SHD 3967) na 'esriym (SHD 6242). 1Wafalme 6:2-3 inasema Hekalu lilikuwa ni la dhiraa 60 urefu, na dhiraa ishirini upana na dhiraa thelathini urefu wake kwenda juu. Inasemekana pia kuwa kila ukumbi mmoja ulikuwa wa mikono 20 urefu wake, na sawasawa na mapana ya nyumba, na mapana ya upande wa mbele ya nyumba (yaani wa kuingilia kwenye ukumbi) lilikuwa na dhiraa 10. Ipo kimya kama kwenye urefu wa kwenda juu wa ukumbi, na watu wanadhani kwamba ulikuwa ni urefu uleule wa kama mwili wa Hekalu lakini maandiko yanasema ilikuwa ngi mara nne urefu wa mwili wa Hekalu. Ukumbi wenye dhiraa 120 unaashiria urefu wa kipindi cha uumbaji wa kimwili wa zama hizi kilichopimwa kwa idadi ya Yubile. Namba hii ilikonyesha pia kipindi cha uhai na maisha ya nabii Musa kama tunavyoona kwenye vitabu vya Torati na pia kwenye kipindi cha kwanza cha maisha ya mababa. Kipindi cha uhai au maisha ya Musa yaligawanyika katika migawanyo mitatu ya miaka arobaini-arobaini na yalifanya taswira ya awamu za Utawala wa Wafalme. Tarakimu ya “thelathini” ni kiini kikubwa iliyoashiria serikali ya ndani ya Mungu, na pia umri unaofaa kufikia kipindi cha kabla mtu hajawa kiongozi wa kundi au kusanyiko la Mungu.

 

Ngazi sita za kuingilia zinaashiria mizunguko sita ha kwanza ya maisha ya mwanadamu. Ngazi ya saba na ambayo ndiyo ilikuwa ni sehemu ya Hekalu lenyewe, iliashiria mzunguko wa Sabato ya mwisho ya Yubile uliowekwa na kupewa wanadamu. Mtu anapaswa awe na umri wa miaka ishirini ndipo ahesabiwe kuwa ni mtu mzima na astahili kwenda vitani. Inampasa mtu awe na umri wa miaka ishirini na tano kabla hajaruhusiwa kufanya kazi na huduma za Hekaluni, na hadi awe na umri wa miaka thelathini ndipo awe mzee kwenye ushirika au kanisa la Mungu.

 

Mtu amewekewa au kupewa Yubile moja akiwa mtu mzima ili aweze kuendelea katika Roho Mtakatifu. Musa alipewa Yubile mbili. Daudi alifariki akiwa na umri wa miaka sabini ikimaanisha ashirio la kupungua kwa wakati hadi kufikia Yubile moja. Alimuachia madaraka ya ufalme wake Sulemani kabla hajafa, kitendo kilichoashiria utaratibu kwenye mwendelezon wa mamlaka kwa mtiwa Mafuta wa Bwana.

 

Patakatifu pa Patakatifu palikuwa ni Naos, ambayo iliashiria mwaka wa mwisho wa maisha ya mwanadamu na wakati mtu alipoupata umoja mkamilifu na Mungu. Ndipo hii Naos iliwakilisha hatua ya maendeleo ya mwanadamu wakati Mungu alipoingia kwa mwanadamu kwa kupitia Roho Mtakatifuna kumuinua yeye kwa elohm. Na hii ndiyo maana Agano Jipya linatutaja sisi kuwa ni Naos, “na ni Naos tulivyo sisi” (1Wakorintho 3:17).

 

Zile Meza, na Mkate wa wonyesho, na vinara kumi vya taa vilisimama kwa ajili ya kuliendeleza Kanisa la Mungu kwa kipindi chote lilichopewa Kanisa kwenye awamu zake saba za maendeleo likiwa chini ya malaika saba wa makanisa saba.

 

Zile tatu nyingine ziliwakilisha vinara ambazo zilikuwa ni Masihi na Mashahidi Wawili (soma jarida la Mashahidi (Wakiwemo Mashahidi Wawili) (Na. 135) [The Witnesses (including the Two Witnesses) (No. 135)].

 

Patakatifu pa Patakatifu palikuwa na Sanduku la Agano na Torati ya Mungu, ambapo Torati ya Mungu iliwekwa kwenye mioyo ya watu waliokujakuwa hatimaye kuwa ni Hekalu la Mungu.

 

Bahari iliyoyeyuka au kioo cha Hekalu vilikuwa kubiti thelathini vilivyozunguka na hivyo Mungu alifunua kiwango cha uweza wa kimazingira yake (1:3) kwenye urefu wake wa kiina na ubora. Ilikuwa ni nje ya Nyumba ya Mungu, kama ilivyokuwa madhabahu, ili kuashiria kwamba Kristo alikufa nje ya kambi akiwa kama sadaka, mara moja tu na kwa ajili ya wote ili sote tuweze kutakasika na kukombolewa na Mungu.

 

Ukubwa wa Hekalu iliashiria Mpango wa Wokovu na ukombozi wa mwanadamu unaofanywa na Mungu. Mlolongo na mpangilio wa ujenzi wake uliendana na ramani ile na ililiashiria kila kitu cha maendeleo yake. Ufunguo wa Daudi ni kuelewa na kuzifundisha Siri za Mungu kwa mujibu sawa na mpangilio wa Yubile ulivyopangiliwa na kulingana nayo, na kuweza kutabiri sawasawa na mafundisho yenye uzima, na sawasawa na inavyosema Torati na Ushuhuda.”

 

Kulikuwa na idadi kubwa ya mahekalu ambayo tutakwenda kuyaongelea habari zake hapo chini.

 

Kuwekwa kwa Sanduku la Agano Hekaluni

Ni baada tu ya kukamilika Hekalu, ndipo Sanduku la Agano lililetwa na kuingizwa Hekaluni, ili kwamba Mungu aonekane akiwa kama kiini chake. Lililetwa katika mwezi wa Ethanimu, ambao unaashiria Ujio wa Masihi na Mfalme na Mtawala wa Ulimwengu akiwa kama Nyota ya Asubuhi.

 

1Wafalme 8:1-66 Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni. 2 Wakakutana mbele ya mfalme Sulemani watu wote wa Israeli wakati wa sikukuu, katika mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi wa saba. 3 Wazee wote wa Israeli wakaja, nao makuhani wakajitwika sanduku. 4 Wakalipandisha sanduku la Bwana, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwa katika ile Hema; vitu hivyo makuhani na Walawi wakavipandisha. 5 Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli waliokutanika kwake, walikuwako pamoja naye mbele ya sanduku, wakichinja sadaka kondoo na ng'ombe, wasioweza kuhesabiwa wala kufahamiwa idadi yao kwa kuwa wengi. 6 Makuhani wakalileta sanduku la agano la Bwana hata mahali pake, katika chumba cha ndani cha ile nyumba, patakatifu pa patakatifu, naam, chini ya mbawa za makerubi. 7 Kwa maana makerubi yalinyosha mbawa zao, juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu. 8 Na ile miti kwa kuwa mirefu, ncha za miti zilionekana katika mahali patakatifu, mbele ya chumba cha ndani; lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo. 9 Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili za mawe ambazo Musa aliziweka ndani huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka katika nchi ya Misri.  

 

Kwa hiyo hizi Meza ziliwekwa kwenye Sanduku la Agano ili kuonyesha ukweli wa kwamba Mungu aliziweka Sheria zake mioyoni mwa watu wote na zingekuwa mahali pa katikati pa makao yake kama Naos au Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu la Mungu. Na hii ndiyo maana Sanduku hili la Agano lilipaswa liingizwe mioyoni mwa wateule walio kwenye Makanisa ya Mungu.

 

10 Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya Bwana ikajaa wingu; 11 hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya Bwana ilikuwa imejaa utukufu wa Bwana. 12 Ndipo Sulemani akanena, Bwana alisema ya kwamba atakaa katika giza nene. 13 Hakika nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele. 14 Mfalme akageuza uso wake, akawabariki mkutano wote wa Israeli; na mkutano wote wa Israeli wakasimama. 15 Akasema, Bwana, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena na Daudi baba yangu kwa kinywa chake akalitimiza kwa mkono wake, akasema, 16 Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wo wote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nalimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli. 17 Basi ilikuwa moyoni mwake Daudi, baba yangu, kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 18 Lakini Bwana akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako. 19 Lakini wewe hutanijengea nyumba hiyo; ila mwanao atakayetoka katika viuno vyako, yeye ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu. 20 Basi Bwana amelitimiza neno lile alilolinena; nami nimesimama mahali pa Daudi baba yangu, na kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama Bwana alivyoahidi, nami nimeijenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 21 Na humo sanduku hili nimelifanyizia mahali, ambalo ndani yake mna maagano ya Bwana, aliyoyafanya na baba zetu, hapo alipowatoa katika nchi ya Misri. 22 Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana, machoni pa mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake mbinguni. 23 Akasema Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni juu wala duniani chini; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa mioyo yao yote. 24 Umemtimizia mtumishi wako, Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia; naam, ulinena kwa kinywa chako, ukayatimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo. 25 Na sasa, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, umfikilizie mtumishi wako, Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia, ukisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli machoni pangu, kama watoto wako wakiangalia njia zao, ili kuenenda mbele zangu kama wewe ulivyoenenda. 26 Sasa, Ee Mungu wa Israeli, nakusihi, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako, Daudi, baba yangu. 27 Lakini Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga! 28 Walakini uyaelekee maombi ya mtumwa wako, na dua yake, Ee Bwana, Mungu wangu, uisikilize sauti na maombi ya mtumwa wako, aombayo mbele zako leo. 29 Macho yako yafumbuke na kuielekea nyumba hii usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa. 30 Uisikie dua ya mtumwa wako, na ya watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, sikia huko mbinguni, makao yako; nawe usikiapo, samehe. 31 Ikiwa mtu amemkosa mwenzake, na kupewa sharti ya kiapo aapishwe, naye akija na kuapa hapa mbele ya madhabahu yako, katika nyumba hii; 32 basi, usikie huko mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumwa wako; ukimpatiliza mtu mbaya, kwa kuleta njia yake juu ya kichwa chake; na kumpa mwenye haki haki yake, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake. 33 Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea tena kwako, na kulikiri jina lako wakikuomba na kukusihi katika nyumba hii; 34 basi, usikie huko mbinguni, ukawaachilie watu wako Israeli dhambi yao, ukawarejeze tena katika nchi uliyowapa baba zao. 35 Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, wakati ule utakapowatesa; 36 basi, usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; unapowafundisha njia iliyo njema, iwapasayo kuiendea; ukanyeshe mvua juu ya nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi wao. 37 Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao; au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote; 38 maombi yo yote au dua yo yote ikifanywa na mtu awaye yote, au na watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu maradhi ya moyo wake, na kuikunjua mikono yake kuielekea nyumba hii; 39 basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukatende, ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote); 40 ili wakuche wewe siku zote watakazoishi katika nchi uliyowapa baba zetu. 41 Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako; 42 (maana watasikia habari za jina lako kuu, na za mkono wako ulio hodari, na za mkono wako ulionyoshwa); atakapokuja na kuomba kuielekea nyumba hii; 43 basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukatende kwa kadiri ya yote atakayokuomba mgeni huyo; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe kama watu wako Israeli, nao wajue ya kuwa nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa jina lako. 44 Ikiwa watu wako watoka kwenda kupigana na adui zao, kwa njia yo yote utakayowapeleka, wakikuomba, Bwana, kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 45 basi, uyasikie huko mbinguni maombi yao na dua yao, ukaitetee haki yao. 46 Ikiwa wamekutenda dhambi, (maana hakuna mtu asiyetenda dhambi), hata ukawaghadhibikia, ukawatia katika mikono ya adui zao, wawachukue mateka mpaka nchi ya adui zao, iliyo mbali au iliyo karibu; 47 basi, wakijirudia nafsi zao katika nchi ile watakayochukuliwa mateka, wakitubu, na kukusihi katika nchi ya hao waliowachukua mateka, wakisema, Tumekosa, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu; 48 watakaporejea kwako kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya adui zao, waliowachukua mateka, wakikuomba, kwa kuikabili nchi yao, uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 49 basi, uyasikie maombi yao na dua yao, huko mbinguni, makao yako, ukaitetee haki yao; 50 ukawasamehe watu wako waliokutenda dhambi, na makosa yao yote waliyokukosa; ukawape kuonewa huruma mbele yao waliowachukua mateka, ili wapate kuwahurumia. 51 Kwa kuwa ni watu wako, na urithi wako, uliowatoa katika Misri, toka katikati ya tanuu ya chuma. 52 Macho yako na yafumbuke, na kuielekea dua ya mtumwa wako, na dua za watu wako Israeli, ukawasikilize kila wakati watakapokulilia. 53 Kwa maana uliwatenga na watu wote wa dunia, wawe urithi wako, kama ulivyonena kwa mdomo wa Musa, mtumishi wako, hapo ulipowatoa baba zetu katika Misri, Ee Bwana MUNGU. 54 Hata ikawa, Sulemani alipokwisha kumwomba Bwana maombi hayo, na dua hiyo yote, akasimama na kuondoka hapo mbele ya madhabahu ya Bwana, hapo alipokuwa amepiga magoti, na kuikunjua mikono yake kuelekea mbinguni. 55 Akasimama, na kuwabariki mkutano wote wa Israeli kwa sauti kuu, akasema, 56 Na ahimidiwe Bwana, aliyewapa watu wake Israeli kustarehe, vile vile kama yote aliyoyaahidi. Halikukosa kupatikana neno lo lote katika ahadi yake njema, aliyoahidi kwa mkono wa Musa, mtumishi wake. 57 Bwana, Mungu wetu, na akae nasi, kama alivyokaa na baba zetu; asituache, wala asitutupe; 58 aielekeze mioyo yetu kwake, ili tuende katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na sheria zake, na hukumu zake, alizowaamuru baba zetu. 59 Na maneno yangu haya, niliyoyaomba mbele za Bwana, na yawe karibu na Bwana, Mungu wetu, mchana na usiku, ili aitetee haki ya mtumishi wake, na haki ya watu wake Israeli, kwa kadiri ya haja zao za kila siku. 60 Watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa Bwana ndiye Mungu; hakuna mwingine. 61 Mioyo yenu na iwe kamili kwa Bwana, Mungu wetu, kuenenda katika sheria zake, na kuzishika amri zake, kama ilivyo leo. 62 Ndipo mfalme, na Israeli wote pamoja naye, wakatoa sadaka mbele za Bwana. 63 Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea Bwana, ng'ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Bwana. 64 Siku ile ile mfalme akaitakasa behewa ya katikati iliyokuwa mbele ya nyumba ya Bwana; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za Bwana ilikuwa ndogo, haikutosha kuzipokea sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na mafuta ya sadaka za amani. 65 Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, kutoka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, mbele za Bwana, Mungu wetu, siku saba na siku saba, yaani siku kumi na nne. 66 Hata siku ya nane akaagana na watu, nao wakambarikia mfalme, wakaenda hemani kwao, wakifurahi na kuchangamka moyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi mtumishi wake, na Israeli watu wake.

 

Agano Liliwekwa na Sulemani

Malaika wa Mungu, msaidizi au mjumbe wa Mungu wa Israeli tunayemjua kama Kristo (Zaburi 45:6-7; Waebrania 1:8,9) alimtokea Sulemani na kuliweka Agano la Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa Taifa zima. Agano hili lilikuwa na masharti. Waliambiwa kuwa wangeadhibiwa iwapo kama hawatalishika au wakiliasi.

 

1Wafalme 9:1-28 Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya, 2 basi, Bwana akamtokea Sulemani mara ya pili kama alivyomtokea huko Gibeoni. 3 Bwana akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote; 4 na wewe, ukienda mbele zangu kama alivyokwenda Daudi, baba yako, kwa ukamilifu wa moyo, na kwa adili, kufanya hayo yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, 5 ndipo nitakapokifanya imara kiti cha ufalme wako juu ya Israeli milele; kama nilivyomwahidia Daudi, baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Israeli. 6 Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, tena mkienda na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, 7 basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote. 8 Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini Bwana ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya? 9 Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu Bwana ameleta mabaya haya yote juu yao. 10 Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alizijenga zile nyumba mbili, nyumba ya Bwana na nyumba yake mfalme, 11 (basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya. 12 Naye Hiramu akatoka Tiro kuitazama hiyo miji Sulemani aliyompa; wala haikumpendeza. 13 Akasema, Miji gani hii uliyonipa, ndugu yangu? Akaiita nchi ya Kabuli, hata leo. 14 Hiramu akamletea mfalme talanta sitini za dhahabu. 15 Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, na Megido, na Gezeri. 16 Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda akautwaa Gezeri, na kuuteketeza kwa moto, akawaua Wakanaani waliokaa mjini, akampa zawadi binti yake, mkewe Sulemani. 17 Naye Sulemani akaujenga Gezeri, na Beth-horoni wa chini, 18 na Baalathi, na Tamari ulio nyikani, katika nchi; 19 na miji yote ya hazina iliyokuwa yake Sulemani; na miji ya magari yake, na miji ya watu wake wapandao farasi, na kila alichopenda kujenga Sulemani huko Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake. 20 Kwa habari ya watu wote waliosalia, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi, wasiokuwa wa wana wa Israeli; 21 watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo. 22 Lakini wa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu shokoa; ila ndio watu wa vita, na wangoje wake, na wakuu wake, na akida zake, na wakuu, wa magari yake, na wa wapanda farasi wake. 23 Hao maakida wakuu, waliokuwa juu ya kazi yake Sulemani, walikuwa mia tano na hamsini, waliowaamuru watu watendao kazi. 24 Lakini binti Farao akapanda toka mji wa Daudi, mpaka hiyo nyumba yake Sulemani, aliyomjengea; kisha, aliijenga Milo. 25 Na mara tatu kila mwaka Sulemani alikuwa akitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu aliyomjengea Bwana akafukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu iliyokuwako mbele za Bwana. Hivyo akaimaliza nyumba. 26 Tena, mfalme Sulemani akaunda merikebu huko Ezion-geberi, ulioko karibu na Elothi, pwani ya Bahari ya Shamu, katika nchi ya Edomu. 27 Naye Hiramu akatuma merikebuni watumishi wake, wanamaji wenye kuijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani.28 Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.

 

Kwa hiyo andiko lililo kwenye Mambo ya Nyakati linahusu mambo yanayotakiwa kufanyika Hekalu na Agano lililowekwa na Taifa. Ni kama tunavyoona kwenye 2Mambo ya Nyakati 2:1-18. Kuanzia aya ya 4 tunaona kwamba Hekalu liliandaliwa kwa utoaji wa sadaka ya kutekeezwa na hii inawakilisha maombi ya Watakatifu ya kila siku nay a Sabato na Mwandamo wa Mwezi Mpya na sikukuu zote takatifu zilizoamriwa na Bwana kama amri ya milele.

4 Angalia, najenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wangu, ili kumfanyia wakfu, ya kufukizia mbele zake fukizo la manukato, na ya mkate wa wonyesho wa daima, na ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na za siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa za Bwana, Mungu wetu. Hili ni agizo la milele kwa Israeli. 5 Nayo nyumba nitakayoijenga ni kubwa; kwa sababu Mungu wetu ndiye mkuu juu ya miungu yote. 6 Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba, ikiwa mbingu hazimtoshi, wala mbingu za mbingu? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya kufukizia fukizo mbele zake?

 

Kisha Sulemani aliwaruhusu waimbaji au watunzi waende na wakafanye hivyo na vitu vingine pia (aya za 7-14).

 

Hiramu alipeleka mwimbaji na mtunzi ambaye ni nusu Muisraeli. Baba yake alikuwa pia Hiramu na mwimbaji na munzi wa nyimbo alikuwa ni mtu wa baba yake. Mtu Yule alikuwa ni kutoka kwa mwanamke wa kabila la Dani, na ni mtu wa Tiro ushiriki wa wanawake wa Israeli kwenye mwingiliano wa kindoa na Wamataifa kwenye ujenzi wa Hekalu. Ukweli ule ulionyesha kuelekea asili ya uzawa wa Israeli katika Siku za Mwisho na Wokovu ule ulikuwa ni wa Wamataifa.”

 

Utaratibu wa kipimo cha DNA kilijumuisha Israeli na Wamataifa ili kwamba Ibrahimu afanyike kuwa Baba wa Mataifa na Agano na Mungu na Roho Mtakatifu ambaye ndiye aliziandika Sheria zile ndani ya mioyo ya wanadamu na ili iendelee kwa mfumo wote wa mwanadamu na wokovu uliendelea hadi kwa Wamataifa.

 

15 Basi sasa hiyo ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, aliyonena bwana wangu, na wapelekewe watumishi wake; 16 nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaichukua Yerusalemu. 17 Ndipo Sulemani akawahesabu wageni wote waliokuwamo katika nchi ya Israeli, sawasawa na hesabu aliyowahesabu Daudi baba yake; wakatokea mia hamsini na tatu elfu, na mia sita. 18 Akaweka katika hao sabini elfu wawe wachukuzi wa mizigo, na themanini elfu wawe wachongaji milimani, na wasimamizi elfu tatu na mia sita, ili wawatie watu kazini.

 

Idadi yao watu hawa ilikuwa ni 153,600 ambao ni wageni katika Israeli na walipangiwa kazi kwenye kazi hii ya ujenzi wakiwa kama wakusanya changizo. Wanaume elfu sabini walikuwa ni wachukuzi wa mizigo, 80,000 walikuwa wakata miti milimani na 3,600 walikuwa wasimamizi au manyapara. Kwa hiyo Wamataifa wote waliokuwa katika Israeli walihusishwa na kazi hii ya ujenzi. Wakati wokovu ulipoenea na kuwafikia Wamataifa ulimwenguni kote.

 

Mara tu baada ya vifaa vyote vya ujenzi vilipokamilika na kuletwa, ndipo Sulemani alianza kulijega (2Mambo ya Nyakati 3:-1-17).

 

2Mambo ya Nyakati 3:1-17 Ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, juu ya mlima Moria, pale Bwana alipomtokea Daudi babaye alipotengeza mahali pale alipoagiza Daudi, katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.  

 

Kwa hiyo eneo la Wayebusi ambalo lilikuwa ni mahali pa kikuhani pa Melikizedeki palifanywa kuwa ni mahali pa Hekalu na kuwa ni pa imani ile.

 

2 Mambo ya Nyakati 3:2-17 inaelezea kuhusu ujenzi ule tuliouona kwenye kitabu cha Wafalme lakini kina mengi ya kuongelea kwa kina zaidi kama vile dhahabu kuwa ni ya Parvaimu na dari yake ya afiri na ya mawe ya thamani sana kwenye Nyumba Kubwa.

 

2 Akaanza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa kutawala kwake. 3 Basi hii ndiyo misingi ya majengo ya nyumba ya Mungu aliyoiweka Sulemani. Urefu wake kwa mikono ya cheo cha kwanza ulikuwa mikono sitini, na upana wake mikono ishirini. 4 Na ukumbi uliokuwa mbele yake, urefu wake kadiri ya upana wa nyumba ulikuwa mikono ishirini, na kwenda juu kwake mia na ishirini; akaufunikiza ndani kwa dhahabu safi. 5 Nayo nyumba kubwa akaifunika miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, akaifanyizia mitende na minyororo. 6 Akaipamba nyumba kwa vito iwe na uzuri; nayo dhahabu ilikuwa dhahabu ya Parvaimu. 7 Tena, akaifunikiza kwa dhahabu nyumba, na boriti, na vizingiti, na kuta zake, na milango yake; akachora makerubi kutani. 8 Akaifanya nyumba ya patakatifu pa patakatifu; urefu wake kadiri ya upana wa nyumba, ulikuwa mikono ishirini, na upana wake mikono ishirini; akaifunikiza kwa dhahabu safi, ya talanta mia sita. 9 Na uzani wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Akazifunikiza orofa zake za juu kwa dhahabu. 10 Na ndani ya nyumba ya patakatifu pa patakatifu akafanyiza makerubi mawili ya kuchonga; wakayafunikiza kwa dhahabu. 11 Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili. 12 Na bawa la kerubi la pili lilikuwa mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la kwanza. 13 Yakaenea mabawa ya makerubi hayo mikono ishirini; yakasimama juu ya miguu yao, na nyuso zao ziliielekea nyumba. 14 Akalifanya pazia la samawi na urujuani na nyekundu, na kitani safi, akaifanyizia makerubi. 15 Tena akafanya mbele ya nyumba nguzo mbili za mikono thelathini na tano kwenda juu kwake, na taji iliyokuwa juu yake moja moja ilikuwa mikono mitano. 16 Akafanya minyororo ndani ya chumba cha ndani, akaiweka juu ya vichwa vya nguzo; akafanya makomamanga mia, akayaweka juu ya hiyo minyororo. 17 Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kuume, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kuume Yakini, na jina la ile ya kushoto Boazi.

 

Ni kupitia wokovu wa Mungu ndipo tunaingia kwenye Hekalu la Mungu. Makerubi wanakilinda Kiti cha Enzi cha Mungu na wanawakilisha Makerubi wa kundi la Malaikana wanawakilisha Makerubi wa kundi la Malaika. Makerubi walioonekana kwenye Hekalu aliloonyeshwa nabii Ezekieli wanaonyesha kwamba makerubi wengine wawili walioingizwa wa upande wao wa mtende ambao ni Kristo, wanachukua nafasi ya mtu mwanaume na kerubi mwenye umbo la kichwa cha samba cha malaika Muasi, aitwaye Shetani na Aeon mwenye kichwa cha samba. Hawa elohimu waliowekwa hapa ni Ibrahimu na Musa, ambao ni wawili pekee waliotajwa kuwa ni Elohim kwenye maandiko ya vitabu vya Mwanzo na Kutoka.

 

Wakati Ibrahimu na Musa wakiwa ni watu wawili tu pekee waliotajwa kuwa ni Elohim, kulikuwa ni wawili waliomtokea Yesu, ambao ni Musa na Eliya (Mathayo 17:3). Kwa hiyo tunaweza kudhania kwamba kunaweza kuwa na angao viumbe wane waliohusika kwenye mlolongo huu, akiwemo pia Henoko pamoja na hawa wengine kina Ibrahimu, Musa na Eliya na huenda hata na wawili wengine ambao hawajajulikana bado.

 

Madhabahu ya shaba na bahari ya kioo vilifuatiwa kujengwa. Habari zake zimeelezewa pia kwenye 2Nyakati 4:1-22. Kulisimamishwa kwa mistari miwili na maksai kumi na mbili, kila watatu wao wakiangalia upande wa Kaskazini, Mashariki, Kusini na Magharibi. Waliangalia wakiwa na waangalizi au walinzi wao ndani yake. Bahari hii ilikuwa na maafu 3000. Unene wake ulikuwa ni wa sawa na mkono mmoja tena kwa kipimo cha kazi ya mwanadamu (aya ya 5). Luva kumi za upande wa kulia na tano za kushoto ziliwakilisha pia kazi ya mwanadamu, wakati kwamba walisafishwa au kuitakasa sadaka kwa Bwana kiasi kwamba vitu vyote vilivyotolewa sadaka kwa Mungu vilikuwa vimeisha na kwa watu. Bahari yenyewe ilikuwa ni kwa ajili ya makuhani ya kunawia na shughuli hii ya kuwasafisha au kuwatakasa makuhani ilikuwa kwanza kwa Walawi lakini ilikuwa na ingepaswa kuwa ya Melikizedeki chini ya Masihi (kama ilivyo kwenye Waebrania sura ya 1 hadi 8) na Kristo ni mwombezi aliyeitoa sadaka mara moja tu kwa watu wote (sura ya 9), na atawatokea wale wanaomtafuta kwa mara ya pili pasipo kutenda dhambi kwenye wokovu (Waebrania 9:28).

 

Imeandikwa kulikuwa na vinara kumi vya taa vya dhahabu, na tena vitano upande wa kulia na vitano upande wa kushoto vilivyowekwa kwenye meza kumi na pamoja navyo mabeseni mia moja ya dhahabu (aya za 6-8).

 

Hekalu hili lilijengwa pia nyua za makuhani na Ua Mkubwa na milango ya ua. Kwa hiyo wateule walitengwa mbali na Kuhani Mkuu na kuhani aliyesimama katikati wanapokuwa kwenye kazi au huduma zao muhimu (aya ya 9). Bahari iliwekwa upande wa kuume wa mashariki mwishoni, ambako ndiko mfalme anakoingilia akija helakuni.

 

Nguzo mbili za Hekalu zilitengenezwa na Wamataifa na ziliwakilisha mfumo wa nasaba ya DNA za kipimo cha Kibinadmu cha kubits 23 na 46 na pia cha komamanga 400 kwenye shada za maua mbili na mistari mkiwili katika kila shada moja (aya za 12-13).

 

Vyombo vya shaba vilichukuliwa kwenye uwanda Yordani na vilikuwa vingi vivivyopimika au kuhesabika kama sadaka za daima za kila siku ambayo ni Makutano Makuu ya kanisa yalivyo hayana idadi (Ufunuo 7:9).

 

Vyombo vyote vilivyokuwa kwenye Nyumba ya Mungu vilitengenezwa au vilikuwa vya dhahabu kwa amri na maelekezo ya mfalme, ambaye ndiye Sulemani, ambaye ni ishara ya Masihi ambaye ndiye mwenye jumukumu kwa Kanisa la Mungu kupitia Roho Mtakatifu. Vile vinara vya taa vilikuwa ni vya dhahabu safi pia ambavyo walivitumia kuviwasha mbele za Bwana. Pia taa zote na vishikio au koleo na beseni zote na mishumaa na vijiko na vyetezo vyote hivi vilikuwa vya dhahabu na kama yalivyokuwa miaango yote ya kuingilia kwenye nyumba na milango yote mingine midogomidogo, ya sehemu zote mbili, za ndani na za Mahali Patakatifu au Naos pia na milango ya nyumba za Hekalu (aya za 21-22). Na idadi ya maandiko mengine yalioishia kwenye aya ya 22.

 

Mungu hakufifisha nuru na alikuwa na mawazo makamilifu na mpangilio. Kwa hiyo, ndivyo tupaswavyo kuwa hihi wateule tuwe watakatifu na kutakaswa kama dhahabu na kuwa waelekevu au tunaofundishika.

 

2Mambo ya Nyakati 5:1 Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya Bwana. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu.

Hivi vilikuwa ndiyo vifaa vilivyoelekezwa kwenye maandalizi, na ndizo hatimaye zililetwa Hekaluni lilipokamilika. Kwa hiyo kulikuwa na vifaa vilivyotumika kwenye ujenzi na kulikuwa na vifaa vilivyotengwa maalumu kwa kutumiwa baada ya awamu ya kwanza ya ujenzi ilipokamilika.

 

2Mambo ya Nyakati 5:2 Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.

 

Wakati Hekalu lililokuwa tayari, ndipo Sanduku la Agano lililetwa Yerusalemu. Kwa hiyo, Sanduku hili la Agano ni ishara ya Roho Mtakatifu kuwa ndani ya wateule, ambaye anafana makao yake huko Yerusalemu baada ya Masihi kuikamilisha awamu ya kuu ya kwanza. Wokovu pia ni wa watu wa Yuda na Yerusalemu kwenye awamu ile, ni kama ulivyo kwa Israeli wote.

 

Katika mwezi wa saba wanaume wote wa Israeli walikusanyika mbele za mfalme wakati wa sikukuu. Wazee wote wa Israeli walikuja na Walawi walilibeba Sanduku la Agano mabegani mwao na maskani ya mkusanyiko wote hadi Hekaluni. Kwa hiyo vitu hivi vyote vilikuwa Wakfu na Vitakatifu kwa Bwana pamoja na wale wote waliojihudhurisha kwenye kusanyiko hili lililofanyika kwenye Hekalu la Mungu mbele za Israeli na walimtolea dhabihu Bwana Mungu. Kwa ajili hii, wateule wote wa Israeli watapanda kwenda kwa Bwana huko Yerusalemu na kujihudhurisha mbele za Bwana na mbele ya Sanduku la Agano ambalo ndilokituo au makao ya cha Naos na ni makao ya Roho Mtakatifu. Viliwekwa chini ya kerubi d ambalo ni elohim wa Ufufu wa Kwanza wa Wafu.

 

2Mambo ya Nyakati 5:3-14 Wakakutana watu wote wa Israeli mbele ya mfalme wakati wa sikukuu, katika mwezi wa saba. 4 Wakaja wazee wote wa Israeli, nao Walawi wakajitwika sanduku. 5 Wakalipandisha sanduku, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwamo Hemani, vitu hivyo makuhani Walawi wakavipandisha. 6 Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli, waliokutanika kwake, walikuwako mbele ya sanduku, wakichinja dhabihu za kondoo na ng'ombe, wasiohesabika wala kujumlishwa kwa kuwa wengi. 7 Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi. 8 Kwa maana makerubi yalinyosha mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu. 9 Na ile miti ilikuwa mirefu, hata ncha za miti zilionekana sandukuni mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo.

 

Sanduku la Agano lilikuwa ishara ya mioyo ya wateule ambao walipaswa kumpokea Roho Mtakatifu na ambao walikujakuwa elohim au wana wa Mungu. Mioyoni mwao ziliwekwa sheria za Mungu.

 

10 Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri.  

 

Kwa hiyo maelezo kuhusu Sanduku la Agano yamepunguzwa ili kuzionyesha kuwa ni sheria za Mungu tu zitakazokuwa mioyoni mwa wateule. Hatimaye wateule walifanyika kuwa ni makuhani wa Melikizedeki.

 

11 Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala hawakuzishika zamu zao; 12 tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;) 13 hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana, 14 hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.

 

Sanduku hili la Agano haliteweza kuingizwa mioyoni tena (soma jarida la Sanduku la Agano (Na. 196)). Matokeo yake ni kwamba Roho Mtakatifu, ambayefundisha Torati ya Mungu na kuwawezesha wateule kuielewa ataliweka tena Sanduku hili la kimwili la Agano na atawaongoa Yuda na Israeli katika Siku za Mwisho, lakini ni pale tu baada ya kuwa sehemu—Kanisa la Mungu–litakapokuwa limeanzishwa.

 

Yerusalemu ilichakuliwa na Hekalu lilijengwa huko ili kupafanya kuwa ni mahali ambapo Mungu atapachagua kufanya makao yake lakini palikuwa ni kwa watu wote na sio kwa ajili ya Yuda na Israeli peke yao na haikuwa ni urithi wa Yuda tangu mwanzo ila lililetwa na Daudi kwa ajili ya Hekalu na hatimaye ukafanyika kuwa ni mji wa Wayebusi kwa Israeli kama ilivyokuwa ni lengo la siku za Ibrahimu na Shemu akiwa kama Kuhani wa Melkizedeki (soma jarida la Melikizedeki (Na. 128).

 

2Mambo ya Nyakati 6:1-42 inafanya taswira ya maandiko yaliyo kwenye vitabu vya Wafalme, na Sulemani aliwabariki makutano wa Israeli na kuonyesha kuwa ndiye aliyechaguliwa miongoni mwa wana wa Daudi kulikamilisha Hekalu.

 

Ndipo Sulemani akainuliwa na kuongezeka kama mwana wa Daudi na kwa hiyo alimuwakilisha Masihi kama wana wa Daujdi. Kisha akaomba akiwa amesimama kwenye mimbari ya shaba kuwaombea Israeli wote. Andiko lililo kuanzia aya ya 12 linasema kuwa mimbari hii ilikuwa ni ya shaba na maombi yalifanyika kwenye uwa wa hekalu. Lakini haya ndiyo yalikuwa ndiyo maombi yake kwa Mungu ambayo ni fundisho kwa Wafalme.

 

2Mambo ya Nyakati 6:12-42 Akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana, machoni pa mkutano wote wa Israeli, akainyosha mikono; 13 (maana Sulemani alikuwa amefanya mimbari ya shaba, urefu wake mikono mitano, na upana wake mikono mitano, na kwenda juu kwake mikono mitatu, na kuisimamisha katikati ya ua; akasimama juu yake, akapiga magoti mbele ya mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake kuelekea mbinguni); 14 akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni, wala duniani; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa moyo wao wote; 15 uliyemtimizia mtumishi wako Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidi; naam, ulinena kwa kinywa chako, ukayatimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo. 16 Sasa, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, umfikilizie mtumishi wako Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia, ukisema, Hutakosa kuwa na mtu machoni pangu, wa kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli; wakiwa tu watoto wako wataiangalia njia yao, ili kuiendea torati yangu, kama wewe ulivyokwenda mbele zangu. 17 Basi sasa, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako Daudi. 18 Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga! 19 Walakini umwangalie mtumwa wako anayoyaomba, na kusihi, Ee Bwana, Mungu wangu, usikie kilio na maombi anayoyaomba mtumwa wako mbele zako; 20 ili macho yako yafumbuke kwa nyumba hii mchana na usiku, mahali uliponena, ndipo utakapoliweka jina lako; usikie maombi atakayoomba mtumwa wako, akikabili mahali hapa. 21 Uyasikie atakayosihi mtumwa wako, na watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, usikie toka makaoni mwako, toka mbinguni, nawe usikiapo, samehe. 22 Ikiwa mtu amemkosea mwenzake, akitiwa kiapo, aapishwe, naye akija na kuapa hapa mbele ya madhabahu yako nyumbani humu; 23 basi, usikie mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumwa wako; ukimlipiza mwovu, kumpatilizia njia yake kichwani; ukamfanyie haki mwenye haki, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake. 24 Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea kwako, na kulikiri jina lako, wakikuomba na kukusihi nyumbani humu; 25 basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watu wako Israeli, na kuwarejeza tena katika nchi uliyowapa wao na baba zao. 26 Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, uwatesapo; 27 basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; uwafundishapo njia njema iwapasayo waiendee; ukainyeshee mvua nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi. 28 Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao, au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote; 29 yo yote atakayoyaomba na kusihi mtu awaye yote, au watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu pigo lake mwenyewe, na msiba wake mwenyewe, akiinyoshea mikono nyumba hii; 30 basi usikie huko mbinguni, ukaapo, ukasamehe, ukampatilize kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote; wewe umjuaye moyo; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu); 31 ili wakuche wewe, waziendee njia zako, siku zote watakazoishi katika nchi uliyowapa baba zetu. 32 Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii; 33 basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako. 34 Ikiwa watu wako wametoka kupigana na adui zao, utakakowatuma ko kote, wakikuomba kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako;35 basi uyasikie huko mbinguni wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao. 36 Wakikukosa, (maana hakuna mtu asiyekosa), hata uwakasirikie, na kuwatia mikononi mwa adui zao, wawahamishe, na kuwachukua mateka mpaka nchi iliyo mbali au iliyo karibu; 37 basi wakikumbuka katika nchi walikohamishwa, na kutubu, na kukusihi katika nchi ya uhamisho wao, wakisema, Tumekosa, tumetenda kwa ukaidi, tumefanya maovu; 38 wakurudiapo kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya uhamisho wao, adui walikowahamisha, wakiomba na kuielekea nchi uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 39 basi uyasikie toka mbinguni, toka makaoni mwako, wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao; ukawasamehe watu wako, waliokosa juu yako. 40 Na sasa, Ee Mungu wangu, macho yako yafumbuke, nakusihi, masikio yako yakasikilize maombi yaombwayo mahali hapa. 41 Sasa, Ee Bwana, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee Bwana, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema. 42 Ee Bwana, Mungu, usiurudishe nyuma uso wa masihi wako,uzikumbuke fadhili za Daudi mtumishi wako.

 

Uponyaji ulombwa kwa wote katika msamaha wa dhambi. Kwa hiyo wakfu wa Nyumba hii ya Mungu ulikuwa ili kwamba Wamataifa waweze kuokolewa pia, na ili wamrudie na kumuomba Mungu chochote wakitakacho na wangepewa.

 

Baada ya Sulemani kumaliza maombi yake, moto ulishuka kutoka Mbinguni na kuiteketeza ile sadaka ya kuteketezwa ikiwa ni ishara kwa mba Mungu alikuwa ametasikia na kuyakubali maombi yao. Kwa hiyo Israeli walikijua sana na walijihadhari sana kwa kile Mungu alichokifana. Kwa hiyo, takriban miaka mia tano tangu kipindi cha Kutoka kwao utumwani, Israeli waliweza kuziona tena ishara zikitolewa zinazoashiria uwepo wa Malaika wa Bwana katikati yao akiwa kama Yahova wa Israeli, ambaye ndiye Yesu Kristo (Zaburi 45:6-7; Waebrania 1:8-9).

 

2Mambo ya Nyakati 7:1-22 Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba. 2 Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa Bwana, kwa kuwa utukufu wa Bwana umeijaza nyumba ya Bwana. 3 Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa Bwana ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele. 4 Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana.

 

Andiko hili linaonyesha kwamba Maskani na hatimaye Hekalu zote hizi zilijazwa na utukufu wa Bwana. Moto ulioshuka kutoka mbinguni na kuiteketeza dhabihu ilikuwa ni taswira ya Hekalu la Kiroho ambalo lingeweguswa na moto siku ya Pentekoste mwaka 30BK na wateule walianza kuwa Hekalu la Kiroho lililojazwa au lililotengenezwa kwa dhabihu ya wanadamu waliojitoa kwa Bwana Mungu na ambalo lingechukua mahala pa lile Hekalu la Kimwili la Yerusalemu na ambalo liliangushwa na kuharibiwa mwaka 70BK kama ilivyokuwa imetabiriwa kwenye Danieli 9:25 nk. Washirika wa dhabihu hii walikuwa na maana yake ya kiroho. Kila kitu kiliandaliwa tangu mwanzoni kama walivyokuwa wote zana na waimba Zaburi.

 

5 Mfalme Sulemani akatoa sadaka ya ng'ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na watu wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Mungu. 6 Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao pamoja na vinanda vya Bwana, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru Bwana, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama. 7 Tena Sulemani akaitakasa behewa katikati, iliyokuwa mbele ya nyumba ya Bwana; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka za kuteketezwa, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba aliyoifanya Sulemani haikutosha kuzipokea sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta. 8 Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba. 9 Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba. 10 Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake. 11 Hivyo Sulemani akaimaliza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na yote yaliyomwingia Sulemani moyoni ayafanye nyumbani mwa Bwana, na nyumbani mwake mwenyewe, akayafanikisha.

 

Sikukuu ya Mwezi wa Saba iliadheimishwa kwa siku kumi na nne, siku saba zikiwa ni kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, na siku saba nyingine zikiwa ni kwa ajili ya maadhimisho ya Sikukuu ya Vibanda. Uwekaji wakfu ulikuwa ni kuanzia siku ya 8 hadi ya 14 ya mwezi wa Ethanimu, na siku saba nyingine za Sikukuu zilikuwa tangu siku ya 15 hadi 21 Ethanimu. Siku ya Mkutano wa Makini ilikuwa ya 22 Ethanimu, na siku ya 23 Ethanimu walirejea majumbani au makaoni kwao. Siku ya Kutaniko la Makini au Iliyokuu ya Mwisho haikuhesabiwa kuwa ni ya Sikukuu kwenye hesabu hizi. Siku Iyiyo Kuu ya Mwisho iliyo kwenye nyakati za mwisho inafanya taswira ya Hukumu itakayotolewa kwenye Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe na sio sehemu ya kipindi cha utawala wa millennia. Ni siku ya Ufufuo wa Pili wa Wafu na inahusiana na hukumu ya ulimwengu na watu wake wote. Kwenye mwandamano wa matukio ya mwezi Tishri yaliyo taswira ya mwisho wa zama hizi yanahusiana na Yubile ya mwaka 2027. Kisha marejesho yatakuwa yamekamilika na watu wanarudi kwenye nchi au ardhi zao katika Israeli na ulimwenguni kote kwingineko.

 

Matukio haya pia yanahusiana na mwisho wa zama hizi. Siku ishirini na moja zilizotajwa kukamilisha kipindi cha mlolongo huu na kufikia kwenye mfumo wa kimillenia ulioelezewa kwa kina kwenye jarida la Utakaso wa Mataifa (Na. 77). Mchakato huu ni migawanyo mitatu yenye siku saba saba na marejesho ya utawala mpya huko Yerusalemu. Kwa hiyo, awamu ya kwanza ya miaka saba ya kwanza ya Utakato itatupeleka hadi mwaka 2012, ambacho ni kipindi cha kuwajibika kwa Kanisa. Mafundisho yake yanapaswa yawe sahihi na yamekamilika ya yachapishwe kwa mataifa yote kwa kipindi hiki. Ufunguo wa Daudi limepewa Kanisa aminifu na adilifu la Siku za Mwisho, linaloandika na kuchapisha au kutangaza mafundisho asilia ya Kanisa la Mungu yaliyotumika tangu karne ya Kwanza. Hii inamaana ni mfumo wa kiimani wa Waamini Mungu Mmoja na Wasiochanganya Imani na miungu Mingine au Wayuniratiani wa Kimonotheisti pamoja na mafundisho yasiyoghoshiwa, pamoja na fundisho kuhusu Kalenda Takatifu amoja na Mwandamo wa Mwezi Mpya. Huu ndiyo Ufunguo wa Daudi katika kuelezea wa mwandamano wa matukio katika Siku za Mwisho kiunabii.

 

Kwenye awamu hii hapa, kwenye mwandamano wa mambo ya Hekaluni, Utakaso wa Madhabahu kwa kweli kwa kweli ni shughuli ya pili iliyokuwa inafanyika siku saba za mwezi wa Tishri, ikifuatiwa na siku ya Nane ya mwezi wa Tishri, au mwaka 2013 kwa hesabu za mwaka mmoja kwa siku kuelekea kwenye Yubile ya mwaka 2027. Siku saba za mwisho za mchakato wa kuwatiisha mataifa kutoka Yerusalemu chini ya Masihi tangu mwaka 2019 hadi 2026 (soma jarida la Kuanguka kwa Yeriko (Na. 142)). Yubile ya mwaka 2027 inakamilisha mchakato na mwaka 2028 ni mwanzo wa utawala Mpya wa Milenia. Mwaka huu wa 2028 Marejesho ya \utawala wa Milenia na kanuni zake yatafanyika, na utaratibu wa Hekalu na usimamizi wake na mambo yote ya kiuatawala huko Yerusalemu yatawekwa, kama nyumba za Mfalme na Ukumbi wa kutolea Hukumu. Kutoka huko ndipo hukumu zitatolewa kwa watu wote ulimwenguni.

 

12 Bwana akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. 13 Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; 14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. 16 Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima. 17 Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu; 18 ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli. 19 Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu; 20 ndipo nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote. 21 Na nyumba hii, iliyo juu, kila apitaye ataona ushangao, atasema, Mbona Bwana ameitendea hivi nchi hii, na nyumba hii? 22 Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao.

 

Sulemani alikuwa ametahadharishwa vya kutosha kwa kile kingalichotokea kama wangejiingiza kwenye ibada za sanamu, lakini hatimaye yeye mwenyewe alijikwaa kwa hilo na akafanya hivyo.

 

2Mambo ya Nyakati 8:1- Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani aliijenga nyumba ya Bwana, na nyumba yake mwenyewe; 2 ndipo Sulemani akaijenga miji ile Hiramu aliyompa Sulemani, akawakalisha humo wana wa Israeli. 3 Naye Sulemani akaenda Hamath-zoba, akaushinda. 4 Akaujenga Tadmori wa nyikani, na miji yote ya hazina, aliyoijenga katika Hamathi. 5 Tena akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji yenye boma, yenye kuta, na malango, na makomeo; 6 na Baalathi, na miji yote ya hazina Sulemani aliyokuwa nayo, na miji yote ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na ya anasa yote aliyopenda Sulemani kujenga humo Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake. 7 Basi kwa habari ya watu wote waliosalia wa Wahiti, na wa Waamori, na wa Waperizi, na wa Wahivi, na wa Wayebusi, wasiokuwa wa Israeli; 8 wa watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuwakomesha, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo. 9 Wala katika wana wa Israeli Sulemani hakuwafanya watumwa kazini mwake; lakini hao walikuwa watu wa vita, na wakuu wa majemadari wake, na maakida wa magari yake na wa wapanda farasi wake. 10 Na hao walikuwa maakida wakuu wa Sulemani, watu mia mbili na hamsini, waliotawala juu ya watu. 11 Sulemani akamleta binti Farao kutoka mji wa Daudi mpaka nyumba aliyomjengea; kwa kuwa alisema, Mke wangu hatakaa nyumbani mwa Daudi mfalme wa Israeli, kwa kuwa ni patakatifu, mahali palipofika sanduku la Bwana. 12 Ndipo Sulemani akamtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana, aliyoijenga mbele ya ukumbi, 13 kadiri ilivyohitajiwa huduma ya kila siku, akitoa sawasawa na amri ya Musa, siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoamriwa, mara tatu kila mwaka, yaani, sikukuu ya mikate isiyochachwa, na sikukuu ya majuma, na sikukuu ya vibanda.

 

Kumbuka kwamba binti Farao hakuruhusiwa kuishi mahali ambapo Sanduku la Agano liliwekwa kwenye nyumba ya Daudi. Kitendo hiki kingemsababishia kuingia kwenye ibada hizi za sanamu za mataifa, jambo ambalo halikuruhusiwa kwenye Hekalu la Mungu au kwenye makao ya Naos kama Watu walio kwenye Nyumba ya Daudi ambao walipaswa kuwa ni elohim. Mwanamke huyu mwenyewe tu aliruhusiwa kujijengea madhabahu kwa ajili ya mungu wake huko Kidroni na wengine wengi.

 

Sulemani akaweka mkazo kwenye Torati ya Mungu na Kalenda na akazitunza Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya ma kuzisisitiza kuwa ni Siku Takatifu za Mapumziko na maadhimisho, pamoja na mkazo wa kuzishika Sikukuu; ambazo tunaziadhimisha mara tatu kila mwaka, sawasawa na vilivyo kwenye Kalenda Takatifu (soma jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156)). Utaratibu huu wa kalenda ulipaswa ushikwe hivyo tangu mwanzo hadi kuangamizwa kwa Hekalu mwaka 70 BK. Haya hivyo, mara ningi ilikuwa haishikwi, na Sikukuu na Usomaji wa Torati mara nyingi ulikuwa haufanywi kabisa kutokana na hali ya ukengeufu na ugumu wa mioyo au wavivu.

 

Utaratibu uliowekwa na Daudi ulianzishwa na kushikwa hadi na wafinyanzi waliotengeneza malango, na kilakitu kilikuwa na maana kwa ajili ya Hekalu lijalo la kipindi cha Yesu Kristo.

 

14 Akaziamuru, sawasawa na agizo la Daudi babaye, zamu za makuhani za kutumika, nao Walawi kwa kadiri ya malinzi yao, ili kusifu, na kuhudumu mbele ya makuhani, kama ilivyohitajiwa kila siku; tena mabawabu kwa zamu zao za kila mlango; maana ndivyo alivyoamuru Daudi mtu wa Mungu. 15 Wala hawakuyaacha maagizo ya mfalme aliyowaamuru makuhani na Walawi kwa neno lo lote, wala kwa habari ya hazina. 16 Basi ikatengenezwa kazi yote ya Sulemani hata siku ya kutiwa msingi wa nyumba ya Bwana, na hata ilipokwisha. Hivyo ikamalizika nyumba ya Bwana. 17 Ndipo Sulemani akaenda Esion-geberi, na Elothi, pwani ya nchi ya Edomu. 18 Naye Hiramu akamletea merikebu kwa mikono ya watumishi wake, na watumishi waliokuwa wana-maji; nao wakafika Ofiri pamoja na watumishi wa Sulemani, wakachukua kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, wakamletea mfalme Sulemani.

 

Kuna kazi nyingine mbili kamili pia kufanyika Hekaluni nje na Israeli huko Misri ambazo zilizofanyika wakati Hekalu la Yerusalemu lilikuwa halifanyi kazi zake kutokana na kuangamizwa kwake na Wababeloni na utumwa na pamoja kutokana na ujenzi wa Mahali pa Juu na Onias IV huko Gosheni huko Heliopolis wakati Kristo alipokwenda huko.                                      

Mahekalu yalikuwa:

1. Hekalu la Sulemani liliangamizwa na Wababeloni;                                   

2. Hekalu lililokarabatiwa kwa amri au agizo la Koreshi na Dario na II na Utoaji wa Amri wa Artashasta II (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13));

3. Hekalu lililojengwa na Herode ambalo ni miaka 46 tangu lilipojengwa hadi pale Kristo alipolitabiria kuwa litakuja kubomolewa na kwamba atalijenga tena kwa siku tatu (Yohana 2:19-20).   

 

Mungu aliruhusu Hekalu hili lijengwe tena na Herode ili kuonyesha uhusiano uliopo kati ya ujio wa Masihi na uhusiano kati ya mwanadamu kama Hekalu na makusudio makamilifu ya uumbaji na kumpokea Roho Mtakatifu kama wana wa Mungu au elohim. Mwaka wa 70 BK baada ya juma la sabini la miaka lilihusuriwa au kubomolewa ili kwamba mwanadamu awe ni Hekalu pekee au Naos lililoachwa hadi kufikia kipindi cha kurudi kwa Masihi kwa ajili ya Yubile ya mwaka 2027 BK.          

 

q