Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[283]

 

 

 

 

Nguzo za Filadelfia

(Toleo La 1.0 20010913-20060609)

Ahadi lililopewa Kanisa hili dogo kuliko yote na lililodumu kwa kutunza uaminifu miongoni mwa Makanisa ya Mungu, ambalo ni Kanisa la Wafiladelfia, ilikuwa ni kwamba watafanywa kuwa ni Nguao kwenye Hekalu la Mungu. Na hii ina maana kuu sana n ani ahadi kuu sana kuliko hata ilivyoonekana kwa mara ya kwanza.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki ă 2001, 2006 Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Nguzo za Filadelfia

 


Kwenye maandiko ya ujumbe walioandikiwa na kupelekewa wale Malaika Saba waliokuwa kwenye yale Makanisa Saba, Kristo alikuwa na haya ya kuwaambia waumini waliokuwa kwenye Kanisa la Filadeltia.

 

Ufunuo 3:7-13

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. 8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. 9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. 10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. 11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. 12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. 13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

Maandiko hayanasema kwamba yeye ashindaye atafanywa kuwa nguzo kwenye Hekalu la Mungu wa Masihi na kwenye tafsiri ya RSV inasema: na hatatoka humo kamwe. Lakini andiko hili kwa kweli linasema: hatatoka humo kamwe (sawa na tafsiri iitwayo Marshall’s Interlinear ambayo inasema: Na hakuna kitakachomwondoa tuka humo kabisa [hakuna]kabisa).

 

Je, usemi huu unamaisa nini hasa, usemao kufanyika kuwa nguzo kwenye Hekalu la Mungu wa Masihi? Je, kinatokea nini kwenye ujumbe huu kwa Makanisa? Je, kuna jambo hapa ambalo kwalo tunaweza kujifunza nalo?

 

Kwanza kabisa, ni kwa nini jumbe hizi ziliandikwa na kupelekewa malaika badala ya kupelekwa moja kwa moja kwenye haya Makanisa? Jibu linaweza kupatikana kutokana na ukweli halisi wa habari yenyewe. Makanisa yaliyotajwa hapa kwa kweli ni yale ambayo yalikuwepo kwenye miji iliyokuwa huko Asia Ndogo na ambayo yalikuwa kwenye orodha ya kutembelewa na kuandikiwa nyaraka mbali mbali. Inadhaniwa kwamba orodha ya maeneo yaliyokuwa njiani kwa wapeleka nyaraka yalikuwa yanapitiwa kila mara na ulikuwa ni mchakato endelevu kwa Makanisa yaliyotajwa. Makanisa haya yalianzia huko Efeso na yaliendelea kwa kujipanga kwenye miji mingine iliyofuatia hadi kwenye lile lililotajwa mwishoni la Laodikia. Utaratibu wake ulikuwa ni kuanzia Efeso Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.

 

Kwa kuwa yalikuwa kwenye njia moja tangia la kwanza hadi la mwisho, ni kama yaliyojipanga kwenye safu, ilidhaniwa pia kwamba kwa kweli yalionekana kuwa yalikuwepo kwenye kipindi cha historia ya Mtawanyiko wa Kanisa jangwani. Dhtna hii kwa kweli ilikataliwa na haikukubalika kabisa na Kanisa la Rumi jambo linalomaanisha kwamba kinara hiki kilikuwa kinapita kutoka zama moja hadi nyingine na hakikudumu kutulia kwenye kanisa moja tu lililo sehemu moja kama inavyodaiwa na imani ya Wakatiliki wa Rumi. Kanisa la Orthodox lingeweza kuiona hii kama ni makosa kwa namna fulani lakiini ikichukuliwa na wao kama ni mamlaka yaliyo kwenye imani ya Kirumi ambayo imetoholewa kutoka kwao na hatimaye wakawa hawana mamlaka nayo tena. Upinzani wao kwenye mtazamo huu wa kinabii utaimarishwa kwa wanavyoendelea mbele wote kuungana tena kwa kipindi cha miaka michache ijayo. Tangu mwaka 1996, Kanisa la kimisri la Kikoptiki lilirudi nyuma kwa kuungana na Rumi baada ya mgawanyiko uliofanyika tangu mwaka 451 uliofuatia na Mtaguso wa Kalkedoni. Tukio hili lilitokea baada ya kuongezeka kwa mateso waliyofanyiwa Wamisri wenye itikadi kali (pia soma jarida la Kuanguka kwa Misri: Unabii wa Mikono Iliyovunjika ya Farao [036]; [The Fall of Egypt (No. 36)].

 

Sababu iliyopelekea jumbe zile waandikiwe wale malaika wa Makanisa yale Saba, ni kwa kuwa walikuwa wanawajibika au walikuwa na wajibu kwa kila kilichokuwa kinatokea kwenye yale makanisa na ujumbe ule ulikuwa na uzima ndani yake uliotakiwa kwa kipindi kile.

 

Mtazamo wa zama za kanisa enezi ililazimishwa na uongozi wa makanisa yenyewe kwenye kipindi cha marne chahche za kwanza. Mtume Yohana ndiye alikuwa kiongozi wa makanisa haya yote na ndiye aliyefanyakazi kubwa sana tangu kanisa la Efeso baada ya kifo cha Mtume Petro, kwa mfano aliyekuwa ni askofu wa kanisa la Antiokia na sio wa Rumi. Wafuasi wake hawa waliochukua nafasi yake baadae na ambao aliwafundisha na kuwaandaa vyema waliweka makao makuu ynke mjini Smirna. Polycarp na baadae Polycrates walikuwa ni maaskofu wa kwanza huko Ulaya na pande za Mashariki. Kwa mfano, askofu wa Lyon hadi kufikia kipindi cha Irenaeus walifunzwa na kupelekwa wakitoke Smirna na sio Rumi. Iliaminika kuwa Polycarp aliyeanzisha kanisa huko Lyon mnamo mwaka wa 120 BK (soma jarida la Nyakati Mbalimbali za Makanisa ya Mungu (Na. 30) [Timeline of the Churches of God (No. 30)].

 

Ndiyo maana Efeso lilikuwa ni kanisa la kwanza lililoongoza kwa upendo. Lilikuwa ni jipya na pia palikuwa ni mahali alipokuwa anaishi au nyumbani kwa mtume wa mwisho na aliyependwa sana na Bwana wetu Yesu Kristo. Na ndivyo ujumbe huu unavyoweza kuonekana kwa hisia hii. Mtume Yohana aliandika ujumbe huu kipindi akiwa uhamishoni kwenye kisiwa cha Patmo, takriban mwaka wa 95 wa zama hizi za kalenda ya kidunia.

 

Ufunuo 1:9-20 inasema:

Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. 10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, 11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia. 12 Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu; 13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini. 14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto; 15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi. 16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake. 17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. 19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo. 20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

 

Siku ya Bwana inayotajwa hapa sio ile inayoitwa na kujulimana leo kama siku ya Jumapili bali siku hii inayokusudiwa ni ile Siku ya Bwana inayomaanisha kuwa ni ya mwisho wa dunia (tazama jarida la Siku ya Bwana (Na. 192) [The Day of the Lord and the Last Days (No. 192)].

 

Yohana alifungwa gerezani kwa ajili ya ushuhuda huu na kwa nasibu sana aliokolewa ma kuwa hai ili aupokee ufunuo huu, ambao Mungu alimpa Yesu Kristo. Kitabu hiki kinaitwa cha Kimabii au Apocalypse (Kwa Kiyunani Ufunuo) wa Yohana kwa mtindo wa Kirumi, licha ya kuwa na ukweli kwamba huu ni Ufunuo wa Mungu kwa Yesu Kristo na ambaye hatimaye alimpa Mtume Yohana. Na hii inamaana kwamba Kristo hakuwa na ulewewa wa kila jambo, hali hii alikuwananayo hata baada ya kufufuka kwake na ategemea na makusudio ya Ufunuo huu wa Mungu na kwa hiyo hakuwa Mungu kwa kiwango na vigezo alivyokuwanavyo Baba ambaye ni Mungu wa Pekee na Milele.

 

Kwenye maandiko haya Kristo anamwambia Mtume Yohana ayaandike yale yaliyomo nay ale yatakayokuja baadae katika siku za mwisho. Anaeleza kwa kufafanua kwamba zile nyota saba ni malaika saba wa makanisa saba na kwamba vile vinara saba vya dhahabu ni makanisa saba yaliyokuwako kipindi kile.

 

Maandiko haya yanatuelezea mambo kadhaa ya muhimu:

·         Makanisa yale yote saba kila moja lina kinara chake cha dhahabu.

·         Wale malaika saba, kila mmoja wao ana nyota kwenye mkononi wake wa kuume.

·         Ujumbe ulitolewa kwa kila mmoja wao na kwa jinsi tofauti.

 

Kwa jinsi hii tunafikiri kwamba kila kanisa na kila malaika walikuwa na wajibu wa moja kwa moja kwa Yesu Kristo na hakuna uendelevu wa watu na mamlaka kutoka kanisa moja kwa linguine.

 

Kila malaika na kanisa walikuwa wanawajibika kwa Yesu Kristo aliyekuwa na upanga ukatao kuwili uliokuwa unatoka kinywani mwake ambao ni Neno la Torati ya Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo. Hatimaye tutaona kwamba tendo la kushindwa kuishika kunaadhibiwa na kuondolewa kwa mamlaka ambayo yameonyeshwa kwa kile kinara cha taa au kinara chenyewe.  

 

Ujumbe huu ulikuwa unaelezea mambo yaliyokuwa yanatokea kipindi kile na yale yaliyokuwa yanatarajiwa kutokea siku zake za usoni. Kwa hiyo, unabii huu unahusika kipindi chote cha uwepo wa makanisa yale. Mawazo yenye kuhitilafiana yanaweza kuwepo na yameendelea kuwepo kuhusiana na maeneo yale ambayo kwayo makanisa haya yalikuwa na kwa jinsi yalivyoonyeshwa kwenye unabii huu na kipindi yalichokuwa yanapata mateso na kulinganisha na jinsi ilivyotokea kwa kipindi kimoja na unabii huu. Mawazo au mtazamo huu hauungwi mkono na wala hauna mashiko yoyote na historia ya makanisa haya yenyewe yaliyo kwenye maeneo haya. Tupo kwenye zama ya makanisa ya Waefeso na Wasmirna kabisa ambacho kimewekusudiwa na ambacho kwamba taratibuza uongozi hazitaweza kubadilishana kutoka moja hadi linguine. Hatahivyo, kanisa la Waefeso halikuweza kujirudi kabisa na kutimiliza waliyokuwa wanatakiwa kuyafanya jambo linaloweza kuwa na maana yake kubwa ambayo inahitaji matendo ma unabii hapa kwenye Ufunuo huu wa Mungu aliopa Yesu Kristo. Zaidi sana ni kwamba kunaweza kuwa na ujumbe mkuu na wamuhimu sana ndani yake au unabii huu ulionekana kuwa ungeweza kutimia katika kuchukulia kwa jujuuu au hata kupuuzia unabii uliotolewa kwa makanisa kwa vipindi vyote.

 

Tunapaswa kutathimini jumbe na historia ili kuweza kujaribu utendaji kazi wake na uhusiano wake kwenye historia na umuhimu wa nabii hizi.

 

Efeso

 

Mtume Yohana aliambiwa kuliandikia kanisa hili ambalo na yeye mwenyewe alikuweko.

 

Ufunuo 2:1-7

Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. 2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; 3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. 4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. 5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. 6 Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. 7 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.

 

Kwenye kanisa hili la kwanza tunakuwa karibu na matukio yaliyotokea kwenye kipimdi chake Mtume Yohana. Matukio makuu nay a kustaajabisha au ya kutisha yaliyoandikwa na Mtume Yohana kwenye nyaraka zake zilizotangulia huko nyuma zinayahusu mabishano haya yaliyoendelea hadi kipindi hiki cha kufunuliwa kweke Ufunuo huu. Hiki ndicho kipindi kilichokuwa kinalengwa kuwa kitakuwa kama kilivyo. Wakosoaji wa siku hizi9 wanadaia kwamba andiko hili linayalenga matendo na matukio ya huko Rumi yaliyotokea katika nyakati za utawala wa Nero, lakini hii sio sahihi.kanisa la kwanza liliukubali na kuuchukulia huu kuwa ni unabii kwa kipindi cha mamia ya miaka. Maandiko haya yaliandikwa kwa mtazamo uliokuwa unadhaniwa ungetokea mwishoni mwa karne ya kwanza na walidhaniwa kuwa wangeelewa lakini matukjio haya yaliyotajwa au kuelezewa yalikusudiwa kutimilika kwa kipindi cha zaidi ya millennia ya mbele yake.

 

Umuhimu wa Efeso na Antiokia kwa Kanisa hauwezi kulinganishwa na wala usipuuzwe. Ingawaje kanisa la Antiokia ambalo lilikuwa linaongozwa na Mtume Petro na wasaidizi walioliongoza baada ya kifo chake halitajwi kabisa kwenye orodha ya makanisa yaliyotajwa kwenye unabii huu. Maeneo ambako lilikuwa likihudumu shughuli au huduma yake ya kiuaskofu haikutajwa pia kabisa.

 

Ukengeufu au kuachana na upendo wake wa kwanza kulikotokea kipindi hiki cha zama hii na kwa kanisa kunaonekana kwa dhahiri na kiurahisi sana na wala sio jambo la kupinga. Kile kilichoko kwenye swali kinaendana sambamba na kipindi zama chenyewe na maeneo yaliyovyo ya Makanisa ya Mungu.

 

Efeso ulikuwa ni mji wa bandari kubwa kwenye pwani ya Asia Ndogo. Palikuwa ni mahala muhimu sana kibiashara na kitovu cha kidini na Mtume Paulo alifanya kazi ya kuhubiri hapa kwa kipindi kirefu. Kitabu cha Matendo 19:8,10 kinasema kwamba alifushisha kwenye sunagogi kwa kipindi cha miezi mitatu na pia kwenye ukumbi au darasa la Tirano kwa kipindi cha miaka miwili. Matendo 20:31 inatoa jumla ya kipindi cha jumla ya miaka mitatu cha kipindi cha jumla cha kuwepo kwake huko. Jina la Waefeso linaonekana kwenye Salamu za Mwanzoni mwa Uandishi wa waraka kwa Waefeso 1:1 (A,D,G na hatimaye kwenye familia ya Koine au Byzantine). Efeso inaonekana pia kwenye Matendo 18:27 kwenye D au maandiko rejea na ya chini ya Waarkleani Wasyria. Waefeso wanaonekana pia kwenye Matendo 19:28, 34,35). Trofimo Muefeso anatajwa pia kwenye Matendo 21:29.

 

Kanisa la Efeso bila shaka yoyote ile ni kwamba lilikuwa kwenye kitovu muhimu na cha kwanza cha kanisa la kwanza.   

 

Kaskazini mwa Esefo kulikuwa ni mdomo wa Mto Hermus ambao ulikuweko mji wa Smirna na kaskazini yake kulikuwako tena bonde la Mto Caicus ambako ndiko ulikuweko mji wa Pergamo (aambao pia huitwa Pergamos). Jina hili lilitokana na neno la kale lenye maana ya ngome au mji wenye boma.

 

Kwa mujibu wa Strabo (XIV. 632,640), watu wa mwanzoni huko walikuwa ni Wakariani na Walege. Walifukuzwa na kuondolewa huko na Androcolese mwana wa mfalme wa Athene ambaye aliwaongoza Waionia na kuweka utawala wa kikoloni wa Wayunani huko, kipindi kilekile cha kufa kwake mfalme Sulemani na mgawanyiko wa taifa la Israeli. Androcolese anachukuliwa kuwa ni mwanzilishi wa Efeso. Hata hivyo, kulikuwa na dini nyingine ya kipagani ya Artemi huko Efeso miaka mingi zaidi kabla yake. Hekalu la kwanza la Artemi lilijengwa na Mwandisi Mkuu aambaye jina lake ni Chersiphron (Strabo XIV 640). Mji huu uliwekwa wakfu wote kwa mungu huyu Artemi na ulizingirwa na Walydian wakiongozwa na Croesus takriban mwaka 560 KK wakati alipoanza mchakato wake wa kuyapiga na kuyatwaa mataifa yote yaliyokuwa magharibi mwa Mto Halys. Baada ya hapo, Croesus mwenyewe alichangia au kutoa sadaka ya dume la ng’ome wa dhahabu kwenye hekalu hili na kuchangia idadi kubwa ya nguzo za kujengea hekalu hili (soma Kamusi iitwayo Interpreter’s Dictionary of the Bible, Vol. 2, p. 115).

 

Jemadari Koreshi alimshinda Croesus mwaka 546 KK. Na kisha Kamanda wake, Jemadari Harpagus akaishinda na kuitwa miji ya Waaionian (Herodotus 162) na bilashaka hii ilikuwa ni pamoja na Efeso. Hekalu hili kuu la Efeso lilichomwa moto na kuteketezwa siku ya kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa mfalme Iskanda Mkuu.

 

Mnamo mwaka 334 BK Iskanda (Alexander) aliwashinda na kuwateka Waajemi kwenye Mto Grancus na hekalu likajengwa tena kule kwa muda mfupi tu uliofuatia kitambo. Waefeso wakaikataa hisani hii ya Iskanda (au Alexander) ya kuwalipia au kugharamia ujenzi huu.

 

Jemadari wa Iskanda (Alexander) aliyeitwa Lysimachus anaaminika na kuchukuliwa kuwa ni mwanzilishi wa Efeso ya leo wakati ilipopitia kwake kwa sehemu kubwa ya Asia Ndogo. Aliijengwa kwenye uwanda wa juu wa eneo la kiwanja pamoja na kuta zake na minara inayoonekana kwa wazi na dhahiri hata leo ikionekana kwenye kilima hiki.

 

Wakati Lysimachus aliposhwambuliwa na kushindwa vita hadi kuuawa kwa kuchinjwa na Jemadari Seleucus 1, Efeso, pamoja na Dola yote ya Asia ya Lysmachua, ndipo iliwekwa chini ya uangalizi na utawala wa mwanawe Antiochus 1 na ndipo hatimaye ikawa ni sehemu ya Dola ya Seleucid (Pausanius I. 16.2). Mwaka 190 KK mfalme wa Seleucid, Antiochus Mkuu III, alishindwa vitani na kupokwa utawala wake na Warumi huko Magnesia karibu na Sipylus na miji ya Asia Ndogo ikaangukia mikononi mwa utawala wa Warumi (hii ni kwa mujbu wa kitabu cha Livy XXXVII. xxxvii- xlv). Kwenye Vita au mapigano ya Magnesia Eumenes II wa Pergamo aliyewasaidia Warumi, na hatimaye walimpa milki nyingi za Antiochus ukiwemo mji wa Efeso.

 

Wakati mtawala wa mwisho wa Wapergamo aliyeitwa Attalus III Philometor alipokufa mnamo mwaka 133 KK, alitoa husia kwamba ufalme wake uwe kwa Warumi na ndipo Efeso ilipoangukia kuwa chini ya utawala wao tena (soma kamusi ya Interpreter’s Dict., ibid.). hadi kufikia mwaka 64 KK, Warumi walikuwa wameangusha na kukomesha kabisa kila upinzani uliokuwa maanisha kwa kujikita sana huko nae neo lote likawa kwenye ushawishi na mamlaka ya Warumi.Chini ya mfalme Augustus amani ya jumla ilifaidiwa na hadi kufikia mwaka 29 KK mji wa Efeso uliwekwa wakfu na kuwa kwenye milki ya Warumi, na kwa mjibu wa Cassius Dio (LI, xx, 6) Efeso ilichukua sehemu kubwa muhimu ya eneo lote la Asia na kamusi ya Interpreter’s Dictionary inasema:

Kwenye karne iliyofuatia au ya pili kulifaidiwa utukufu mkubwa smbsvyo kwamba uharibifuwake unaendelea kushuhudia hadi sasa (ibid.).

 

Hekalu la Artemis la Efeso lilichukuliwa au kuhesabiwa miongoni mwa maajabu saba ya ulimwengu wa kale na hatimaye kwenye zama zilizofuztia za Ukristo umuhimu wake uliendelea au kuonekana na wale wenye Imani ya Mungu mmoja au wa Unitaria na Wagothis wenye imani kali ambazo hatimaye ziliteketezwa kwa moto na kufanya zikaribie kuteketezwa kabisa kwa Hekalu mnamo mwaka 262 BK.

 

Hekalu la mfalme Domitian (mwaka 81-96) lilijengwa au kusimamishwa huko Efeso na hekalu la mungu wa Wamisri Serapis lilijengwa kwenye karne ya pili. Hiki kilikuwa ndicho kipindi ama huenda ndicho cha wakati wa Mtume Yohana. Domitian alilitesa Kanisa na alikuwa ndiye adui mkuu. Efeso hata hivyo iliendelea mbele na hali yake ya kuwa mahala palipogubikwa na imani ya Kikristo kwa kipindi cha karne nyingi. Vijiji na vilima vyake vilichoko kwenye maeneo ya majimbo ya Artemission (hekalu la Artemi) iliyoitwa Aysoluk likichukuliwa kutokana na jina ‘Agios Theologos ambalo lilikuwa ni cheo alichopewa Yohana na Makanisa ya pande za Mashariki (soma kamusi ya Interp. Dict., ibid., pp. 117-118).

 

Ilikuwa bado ikifanya kazi kwa karne nyingi na hekalu kubwa (basilica) lilijengwa hapo huenda ilikuwa ni katika karne ya nne. Kati ya uwanja wa michezo na bandari kuna maganjo ya jingo linguine kubwa la kanisa tunalolijua kuwa linaitwa Kanisa la Bikira Mariamu, na ndipo mahali ulipofanyika ule Mtaguso wa Efeso wa mwaka 431.

 

Hii inatufanya tuwe na mtazamo wa wazi juu ya umuhimu wa mji huu wa Efeso tukihusianisha au kulinganisha na miji mingine. Tunakabiliwa pia na ukweli ilikuwa kwenye maangamivu makubwa kwa karne nyingi hadi pale ilipoanza kufukuliwa kwa kuchimbwa na mwanahistoria aliyeitwa J.T. Wood tarehe 2 Mei, 1863.

 

Kutokana na nukuu hizi, tunaondoa uwezekano wa namna mbili zifuatazo:

Kwanza, tunaondokana na uwezekano wa kuona kwamba andiko lililoko kwenye Ufunuo lilikuwa ni ujumbe kwa kanisa endelevu ambalo hatima yake litaishia kipindi cha kuja kwake Masihi.

 

Kutokana na historia, kunaacha uwewekano ambao kwamba umuhimu wa makanisa ulipitia kutoka kipindi kimoja hadi kingine kwa hali mpishano.

 

Umuhimu wa Smirna kwa kweli ulikua na maaskofu wake walikuwa mashuhuri kwenye mabishano au utata kuhusu siku ya kumi na Nne ya Kila Mwezi (Quartodeciman) uliojitokeza mwishoni mwa karne ya pili (soma jarida la Utata na Mabishano ya Siku ya Kumi na Nne ya Kila Mwezi (Na. 277) [The Quartodeciman Disputes (No. 277)]. Hata hivyo, hatuwezi kuhitimisha kwa kusema kwamba Pergamo, ambalo kwa kweli hatimaye lilikuwa ni la kiaskofu na ndilo lilisemekana kwamba lilichukua mahala pa umashuhuri wake na kuwa kanisa la tatu na liliendelea kuwa hivyo haki kipindi kanisa la Thiatira lilipochukua nafasi yake.

 

Haikuwa uparesheni endelevu zama za kanisa nab ado maneno yaliyo kwenye maandiko kutoka Thiatira na kuendelea yanaashiria kwamba hilo lilikuwa ni jambo muhimu.

 

Kwa kweli maandiko yanakuwa hayana maana ikiwa tunadhania na kuendelea kuzishikilia hadi kuja kwa Masihi wakati Makanisa hayo yakiwa yamekufa kwa kipindi cha karne kadhaa na kwakweli sio hata kipindi cha zama za Ukristo.

 

Mabishano ambayo yaliandikwa kipindi cha Nero yalihusu matukio ambayo hususan hasa yalikusudiwa kukikomesha Kitabu cha Ufunuo kutokana na kazi yake ya kiunabii na kisha kuziondoa na kukomesha nabii zake zinazohusika na unabii wa Siku za Mwisho.

 

Kwa mfano, Efeso ilizikwa kwa karne kadhaa na iliachwa umbali wa maili saba au zaidi kwa upande wa bara katika kipindi kile ulipochimbuliwa. laodikia ambao ulikuwa unadaiwa kuwa hai anapokuja Masihi, umekuwa kwa hizi karibuni ukichimbuliwa.

 

Efeso kwa kweli ulianza kufanya mnyororo wa matukio ambayo yalikuwa yaendeleee hadi kuja kwake Masihi na unabii huu kwa kweli unahusiana na zama kazisa. Tutaona hapo mbele kile wanachomaanisja kadiri tunavyoendelea kwenye miaka ya mbele.

 

Smirna

 

Smirna kama tulivoona ilikuwa upande wa kaskazini tu mwa Eferso. Ni mji wa kisasa wa Izmiri. Hadi siku hizi umebakia kuwa ni mji wenye shughuli nyingi na kitovu cha biashara na huenda ni mji mkubwa kuliko yote ya Asia Ndogo.

 

Ulifanywa kwenye sehemu ya mji wakati Antigonus na Lysimachus katika kipindi cha mwishoni mwa karne ya nne na mwanzoni mwa karne ya tatu KK na kuzungushiwa ngome. Tangia mwaka 195 KK Smirna ilijiunga na Rumi na ikaanzisha dini ya kipagani iliyoenziwa na wenyeji wa mji wa Rumi. Mji huu ulilindwa na kuenziwa kwa zawadi kwa namna ya kipekee sana wakati Trebonius, mmojawapo wa wauaji wa Kaisari Yulio au Julius Caesar, alipokimbilia huko na Dolabella alipouchua au kuuteka mji na kumuua Trebonius (soma kitabu cha Interp. Dict., Vol. 4, p. 393).

 

Smirna ulitunukiwa “fursa njema” mwaka wa 23 KK, kati ya miongoni mwa miji kumi na moja, kwa kujengewa hekalu na Mtawala au Mfalme Tiberius kwa kile kinachoonekana kama historia yake ndefu ya rekodi nzuri ya utii na uaminifu wake kwa Rumi (Kwa mujibu wa kitabu cha Tac. Ann. IV.55-56). Kamusi maarufu ya Interpreter’s Dictionary inasema kwamba:

Ilionekana na kuchukuliwa kwamba Efeso na Pergamo kwa cheo cha mji wa  kwanza katika Asia (ibid.).

 

Kulikuwa na dini za aina mbalimbali katika Smirna zikiwemo zile dini za kifalme. Dini iliyojulikana kuwa ni ya Mama wa Sipylus ambayo Filson anasema alikuwa na aina au namna ya mtindo sawa na wa kumwabudu Cybele (ibid.) pia uliingizwa.

 

Heshima kuu na ya kutukuka pia litolewa kwa Homer na kwa hiyo ukubalifu wa Kihekalu cha kuabudia miungu yote cha Kihomeriki. Mji huu pia ulikuwa na idadi kubwa ya Wayahudi na ambao walikuwa na juhudi kubwa sana ya kuupiga vita Ukristo na wafuasi wake.

 

Kufika kwa imani ya Kikristo huko Smirna hakujulikani. Dalili ya kwanza yake inatokana na kitabu cha Ufunuo kwenye aya hizi. Tunaona kwamba Mtume Yohana anapewa taarifa kuhusiana na kile kitakachotokea huko Smirna katika siku za mbele yake na wakati huu alipokuwa akiyaandika mambo haya kulikuwa hakujawa na “kinara cha taa” cha aina au namna yeyote ile. Hakuna taarifa wala habari nyingine zaidi ya ile iliyo kwenye kitabu hiki cha Ufunuo kwa kanisa lililoko Smirna hadi kufikia mwishoni mwa karne ya kwanza.

 

Ufunuo 2:8-29

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. 9 Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. 10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. 11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

 

Maandiko haya yanaelezea juu ya mateso yatakayolikumba kanisa hili la Smirna. Kanisa hili la Smirna kwa kweli lilichukua pahala pa uongozi kutoka kwa lile la Efeso baada ya kufariki kwake Yohana na mwanafunzi wake Polycarp alichukua huduma ya kuliongoza Kanisa hili kutoka pale  na kuanzisha makanisa mengine hadi maeneo ya mbali huko Lyon iliyoko Gaul ambayo kwa sasa imo miongoni mwa miji iliyoko pande za Kusini mwa Ufaransa tangu mwaka 120 BK.

 

Unabii wa siku hizi kumi kwa kweli ulikuwa unahusu mateso makubwa ya mtawala Diocletian, ambayo yalidumu kwa kipindi cha miaka mitatu upande wa Magharibi, na lakini yakaendelea kwa jumla ya miaka kumi pande za Mashariki tangia mwaka 303 hadi 313 BK. Mateso haya yalifikia tamati yake mnamo mwaka 314 kwa azimio la Milan lililojulikana kama Azimio la Kuvumiliana lililotangazwa na mfalme Constantine ambaye pia alijaribu kuingiza ibada na imani ya Ukristo kwenye Dola yake ya Rumi. Wayahudi waliendelea kulipigavita Kanisa na kuwatesa watu wake kipindi hiki cha Wasmirna na wakaendelea kufanya hivyo hadi mwishoni mwa zama za tawala za kifalme za Waarabu wenye nasaba ya Kitahudi, ambazo zilikomeshwa katika kipindi cha kuanzishwa kwa dini ya Kiislamu. Ushawishi wa Wayahudi katika kipindi hiki ulikuwa umeongezeka na kushika hatamu na kuenea hadi barani Afrika ukipitia kwenye pembe ya bara hilo hadi huko Uhabeshi au Ethiopia. Ni katika kipindi hiki ndipo mfumo mapokeo wa marabi wa Kiyahudi walianzisha Kalenda ya Hilleli na kubadili tarehe wakaweka ileiliyokuwa imafuata mfumo wa zamani uliopita wa Hekalu na ambao ulifuatana na mapokeo ya marabi. Kalenda ilibadilishwa mwaka 358 BK mwa mamlaka ya Rabi Hilleli II ambayo ilifuatana na mfumo na utaratibu wa mawazo ya hesabu ya Kibabeli ambayo yaliwezeshwa na marabi wawili wa Kibabeli mwaka 344 BK (soma jarida la Kalenda ya Mungu [156] [God's Calendar (No. 156)].

 

Kanisa la Wasabato la Smirna liliteswa hadi kupungua waumini wake, kwa mateso yaliyofanywa na hawa waamini Utatu au Watrinitaria na ambao pia wanaadhimisha sikukuu za kipagani za Easter/Kristmas ambazo zilianzishwa na kushika hatamu pale mwishoni mwa karne ya nne. Kwa hiyo, Wasabato walisukumiwa pande za mbali za mashariki kwa muda kitambo (soma jarida la Chanzo cha Siku ya Krismasi na Pasaka [235] [The Origins of Christmas and Easter (No. 235)].

 

Pergamo

 

Pergamo ni mji ulioko huko Misia, Magharibi ya Asia Ndogo na ulikuwa maarufu kipindi cha nyakati za itikadi ya Kiheleniki.

 

Iko umbali wa takriban maili kumi na tano au kilometa ishirini na tatu pande za bara za Bahari ya Aegean, kiasi cha takriban maili mbili upande wa kaskazini mwa Mto wa zama kale wa Caicus ambao unajulikana siku hizi kama Bakiri. Caicus ulikuwa ni mpaka uliokuwa kati ya majimbo ya kale ya  Misia na Lydia. Ulijengwa mlimani katika mwonuko wa juu wa maelfu kadhaa ya futi katikati ya miji miwili ya tozo za kodi ya Caicus, wa Selinus kwa upande wa Magharibi na Cetius kwa upande wa Mashariki.

 

Ulikuwa ni mji wa kipindi cha nyuma ya historia ambao kwao jina la kipindi cha nyuma cha Wayunani unaonekana kuwa maana yake ni Ngome au mji uliozungushiwa boma, ambalo ni neno hilohilo lililotumika ngome ya Troy au tola ya kale. Uhusiano wake na wakoloni wa Kiyunani ulianza mnamo mwanzoni mwa kipindi cha zama za kale lakini maelezo machache yameandikwa kuhusu jambo hili hadi kilipofikia kipindi cha Wahellenisi (Kwa mujibu wa Kamusi ya Biblia iitwayo Interpreter's Dictionary of the Bible, article ‘Pergamum’, Vol. 3, p. 733).

 

Xenephon na masalio ya maelfu yake waliweka makazi yao ukiwa ni mji mashuhuri wa Misia (kwa mujibu wa Anabasis VII. 8.8, cf. ibid.). Mji huu ulianza matumizi ya sarafu katika karne ya tano KK.

 

Kipindi kuku na muhimu cha Pergamo kilianza na warithi waliochukua madaraka ya mfalme Iskanda. Ilikuwa ni sehemu ya mamlaka ya kidola yaliyotwaliwa na Antigonus. Mnamo mwaka 301 akiwa anakufa, Lysimachus alitwaa mamlaka upande wa Magharibi mwa Asia Ndogo. Aliwekeza raslimali huko yenye thamani ya talanta 9,000 na kuiweka chini ya uangalizi wa Phyleterus, mmoja wa maafisa wake. Phyleterus akaasi na kuungana na Seleucus dhidi ya Lysimachus mnamo mwaka 282 KK. Baada ya kifo cha Lysimachus vitani mwaka 281 KK na kifo cha Seleucus, Pergamo uliendelea na harakati zake kutoka kuwa chini ya milki ya Seleucid hadi kujipatia uhuru na kuwa tawala ya kifalme uliyokuwa chini ya kizazi cha utawala au cha kifalme kilichoanzishwa na Phyleterus (283-263). Ulihusishwa na harakati zake dhidi ya Wagalatia walioishambulia Asia Ndogo kutokea Ulaya tangu mwaka 278 KK. Ulikuwa ni rafiki na Roma na ukiwa chini ya wafalme wake ulifanyika kuwa ni kituo muhimu na chenye kujulikana cha shughuli za sanaa na mafunzo.

 

Phyleterus alikuwa ni mfalme wa kwanza wa Wapagamene kufanikiwa kuwashinda Wagalatia kwenye mapigano. Mpwawake Eumenes I (263-241) alishauri na kutaka kuwalipa fidia wakati alipoanza kipindi chake cha utawala. Lakini Attalus I 241-197) alifanikiwa kupata ushindi mkubwa sana wa kijeshi dhidi yao. Kwa hiyo, mji wa Statues ulisiwekwa kwenye makundi yote mawili ya Pergamo na Athens. Eumenes II (197-159) alipata ushindi mwingine mnamo mwaka 167.

 

Pergamo uliisaidia Roma kivita dhidi ya Makedonia chini ya Attalus I. Eumenes aliendeleza sera kuisaidia Roma dhidi ya Antiochus III wa Syria. Licha ya kuwa na sera za zamani kuhusu Warumi, umuhimu wake ulipungua kipindi cha warithi wake Attalus II (159-138) na Attalus III (138-133). Eumenes II alichangia kwa kiasi kikubwa ukubwa na umashuhuri wake na maktaba yake ilikuwa ni ya pili kwa ukubwa ikitanguliwa na ile ya Alexandria (ibid., p. 734). Mji huu ulifurahia uzalendo wake wa kidesturi na mila ukiwa na kizazi endelevu cha kiutawala hadi ilipounganishwa na Roma kufuatia wosia uliotolewa baada ya kifo cha Attalus III.

 

Mali na raslimali za Pergamo zilipelekwa Roma kwa madhara au hasara yake na upinzani kwa Roma yaliyoongezeka hadi kufikia kiwango cha kufuata mari za Mithradite na mauaji makuu ya Warumi yaliyofanyika humo mjini mwaka 88 KK. Pergamo ilipoteza uhuru wake kwa ajili hii lakini ilimudu kuurejesha upya tena chini ya Kaisari mwaka 47-46 KK.

 

Chini ya Dola ya Kirumi, na ingawaje haikuwa ni kitovu cha biashara, ilifanikiwa kurejesha hali yake ya ustawi na utajiri na kufanyika kuwa ni kitovu au makao makuu ya dini iliyofanya ibada za kumwabudu Mfalme. Dini ya Kirumi na Augusta ilianzishwa hapo chini ya mfalme Augustus. Hatimaye helaku la Trajan lilijengwa kwenye mji wa ngome na linguine kwa ajili ya Caracalla lilijengwa na kusimamishwa kwenye uwanja maarufu wa michezo. Kwa hiyo ukawa mji unaojulikana kuwa ni wa “mji ulioruzukiwa mahekalu matatu” wa dini hii ya mfalme na pakawa ni kituo ama kitovu muhimu cha kidini kwenye jimbo lote la Asia (ibid.).

 

Ulipoteza maktaba yake baada ya Antony kuitoa kama zawadi yake kwa Cleopatra wa Alexandria. Sanamu kubwa la fedha la Wagalatia lilichukuliwa na kupelekwa Roma kwa amri ya Nero. Ulipendeza kwa kuwa mji wake ulijengwa kwenye mwinuko.

 

Ulipambwa kwa mapambo mazuri na ya kupendeza kwa kupambwa kwa michoro ya kisanaa kwenye madhabahu yake kuu iliyojengwa kwenye mwinuko wa juu, kwa urembo ulioshiria mapogano kati ya miungu na majitu. Sanamu hii ilichukuliwa kuwa ni ya muhimu sana kwa kazi zote za kisanii iliyofanywa na ambayo inautambulisha na kuulinda mji wa Pergamo (ibid.).

 

Maana yake haijajulikana bado. Bali ndiyo iliyopelekea kuambiwa kuwa kuna kiti cha enzi cha Shetani kwenye Ufunuo 2:13 ambapo kunadhaniwa kutokuwa na uhusiano sana na madhabahu hii ambayo pengine ingeweza kuonekana kuwaamisha hivyo. M. J. Mellink (kamusi yake ya The Interpreter's Dictionary, ibid.) anadhani kuna uwezekano mkubwa sana kuwa inahusiana na dini hii ya kumuabudu mfalme iliyoanzishwa hapa Pergamo.

 

Mwinuko ulioko upande wa kaskazini mwa madhabahu unajumuisha hekalu la Athena, ambako kumepangwa safu ya nguzo za uwa ambazo zinafanya mlango wa kuingia kwenye maktaba kubwa na ambako ukumbi wake ulikuwa umepambwa na sanamu za Wagalatia walioshindwa vitani.

 

Mji ulipanuliwa hadi Kusini katika zama za Warumi na mtaa uliofunika kwa upande wa magharibi ulikuwa na mteremko ulioelekea hadi kwenye kihekalu cha Asclepius ambapo Galen alifanya kazi katika karne ya pili BK.

 

Mellink anaamini na kuchukulia kwamba kanisa la kwanza la Pergamo na juhudi zake za kupambana dhidi ya dini hii ya kumuabudu mfalme kumeelezewa kwenye Ufunuo 1:11; 2:12. Hakuna ushahidi uliodhahiri wa kihistoria kwenye karne ya kwanza BK.

 

Mji wa Kirumi ulituama kwenye mji wa kisasa wa Bergama.

 

Katika kipindi cha Wabyzani wakati Pergamo iliwa kwenye zama yake ya kihistoria, wakazi wake waliondoka na kweda kwenye maboma na kujenga kuta mpya zilizojulikana na kusifikana zilizojengwa kwa matofali ya zama za kale yaliyochukuliwa kutoka kwenye makaburi za mapambo au nakshi za madhabahu.

 

Hakuna ushahidi au uthibitisho wa kweli kuwa mji huu ulifanikiwa kupata mamlaka ya kuurithi mji wa Smirna kimaongozi ya Kanisa, iwe kwa mtindo imani ya Kiutatu au Utrinitari au kwa imani ya wafuasi wa Paulo ya kuamini Mungu mmoja au ya Kiunitari. Hitimisho ni kuwa kwamba ujumbe huu wa kwenye Ufunuo ni kwa ajili ya makosa na sio kwa ajili ya Kanisa la Pergamo hasa. Hata hivyo, mtu anaweza kujipatia somo kutoka kwenye maneno yanayoashiria kutegemea kwenye mikono kama maboma yanavyoonekana kuwa na utegemezi Fulani kwenye ujumbe ambao Kristo anao kwa Kanisa. Tutaona kwamba hii kwa kweli ni kitu cha kuangalia au kuzingatia.

 

Ili kuhakikisha kwamba jumbe hizi zilikuwa ni kwa makanisa saba hapa yaliyokuwa kwenye maeneo haya ya Asia Ndogo na sio jumbe kwa ajili ya mlolongo wa makanisa yaliyopitia vipindi mbalimbali vya kihistoria, maneno yasemayo “yaliyoko Asia” yaliongezwa kwenye maandiko haya ya Ufunuo 1:11 kwenye nakala za Receptus na Tafsiri ya Mfalme Yakobo, maarufu kama KJV. Namna hii ya kughushi bilashaka ilikusudiwa kuifanya ionekane kwa namna fulani kwamba kwa kweli maneno haya yaonekane yalikuwa yaihusu miji hii saba lakini ukweli ni kwamba ikumbukwe kwamba maneno haya hayapo na wala hayanekani kwenye nakala za kale (soma kamusi ya Companion Bible fn. to Rev. 1:11). Kwa hiyo, hitimisho linapaswa kuwa kwamba inahusiana na mlolongo wa vipindi makanisa yaliyoko kwenye mamlaka ya Mungu katika Krosto katika Kanisa la kweli.

 

Kipindi hiki cha pili kilichofuata cha Kanisa katika unabii kinahusishwa kama cha Zama ya Wapergamo. Kipindi hiki kinatanguliwa tangia mwisho wa kipindi cha Smirna na kuinuka au kuanza kwa Wapaulisia katika Asia Ndogo ambao hatimaye walijiunga majeshi mapya ya Kiislamu dhidi ya matesaji wao waliokuwa na itikadi asilia za pande za Mashariki ya Rumi. Uislamu wenyewe uliinuka ama kutokea kutoka kwenye tawi la Kanisa la Mungu lililokuwa huko Uarabuni. Kuna mfululizo wa jumbe kwa kanisa hili kwa kuwa linatuamanisha kipindi kirefu na lina idadi kubwa ya matatizo ya kimafundisho na pia lilikuwa lenye kupenda vita. Na hii ndiyo maana Kristo aliongelea juu ya upanga ukatao kuwili. Wapaulicia walikuwa huko kwenye Milima ya Taurus ma kwenye maeneo ya jumla ya Mesopotamia, ambayo yalikuwa na mfumo wa kidini wa Kibabeloni mwanzo wake. Imani ile ilikuwa ni ya Kishetani asilia na chanzo chake.

 

Ufunuo 2:12 inaendelea:

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. 13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. 14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. 15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. 16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. 17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

 

Tendo la kumtaja Antipa limefanywa kimfano na mwandishi maarufu Bullinger anasema hivyo ili kuelezea ashirio la mashahidi wajao huko mbeleni, akionyesha kana kwamba hakuwemo kipindi cha uandishi wa Biblia mtu mwenye jina hilo. Kwa hiyo, andiko hilo linakuwa ni la kinabii na linaelezea matukio n na sio kwa ajili ya matukio ya kihistoria yaliyotokea kipindi cha karne ya kwanza. Antipas anayetajwa hapa ni mfano wa jumla wa watu wote wanaopingana SGD 473) au "mahala pa" au "kwa sababu ya" na waliochanganyika (SGD 3962) ikimaanisha "baba." Kwa hiyo ni jina la kinasaba linalochukua maana hiyohiyo kama Wapinga mchanganyiko. Kwa ajili hii, inamaanisha neno la kitaaluma lenye maana ya waliouawa kwa kufi dini kwa sababu ya mababa. Kwa kweli haya ndiyo yalikuwa mazingira yaliyokuweko katika zama za Wapergamo. Mauaji ya kidini yalishika kasi huko yaliyofanywa na watesaji waliokuwa wakiamini imani ya Utatu au Watrinitaria dhidi ya Waamini Mungu Mmoja au Waunitaria wa Kipauliciani waliokataa kujiunga na imani ya Utatu au ya Kitrinitaria iliyolazimishwa kwa nguvu na utawala wa Wabyzani ambao hujulikana pia kama Byzantine.

 

Jiwe lenye jina jipya ni ishara ya ukazi au uraia wao. Hii inawakilisha uraia wa Mji wa Mungu. Habari za Wapaulicia inakutikana kwenye majarida ya Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122]  na pia lile la Wajibu wa Amri ya Nne katika Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayoishika—Sabato [170].

[General Distribution of the Sabbath-keeping Churches (No. 122) and also Role of the Fourth Commandment in the Historical Sabbath-keeping Churches of God (No. 170)]

 

Kanisa hili lilikuwa lingaliko hai bado na linafanya kazi zake hadi katika karne ya kumi na tisa na ilipofika karne ya ishirini lilikubwa na maafa makubwa ya kuuawa watu wake kwa ajili ya imani ya kidini na watu wake waliobakia kwa kudra ya Mungu walipelekwa mafichoni au ukimbizini huko Siberia. Sio mkakati wa kuwasaka bali masalia wake bado wako huko.

 

Hii inatupeleka kwenye kipindi zama kingine cha kukichukua kutoka kile cha Wapergamo. Kipindi hicho ni kile cha Wathiatira.

 

Thiatira

 

Thiatira ni mji ulioko pande za magharibi mwa Asia Ndogo, karibu na ukingo wa kusini mwa Mto Lycus, na uko kwenye njia iliyoko kati ya Pergamo upande wa Kaskazini Magharibi na Sardi upande wa Kusini-Mashariki yake. Iko katika upande wa Kaskazini mwa sehemu ya mji wa kale wa Lydia; na kwa kipindi kile ilichukuliwa kuwa ipo upande wa kusini zaidi mwa Misia.

 

Machache tu yanajulikana kuhusu historia yake ya siku za mapema huko nyuma. Mji huu ulikuwa huku ukiwa na umaarufu hasa kwenye kipindi cha mwanzoni mwa karne ya tatu KK, na Seleucus Nicator aliuanzisha upya na, kama unavyoonekana ulikuwa na makundi ya wanajeshi Kimakedonia hapa. Haukuwa mji mukubwa sana kabisa bali ulikuwa ni mji mkubwa miongoni mwa ile ya Bonde la Lycus na uliendelea kuwa na nguvu-kazi au viwanda vyenye kuleta faida na wenye umuhimu kibiashara. Nakala la laandishi ya kale zinaonyesha kwamba kulikuwa na aina mbalimbali kadhaa za huduma za kibiashara, zikiwemo na vitu vilivyotengenezwa kwa madini ya shaba, mahema, bidhaa za ngozi, mabatiki, vitu vilivyofumwa kwa manyoya ya kondoo, na hariri na watengenezaji wake stadi walikuwepo. Usatadi kama huu ni lazima iwe umefanywe kwa sehemu na umuhimu au umashuhuri wa maisha ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kidini ya watu wa mji huo.

 

Moja ya miungu mashuhuri aliyekuwa akiabudiwa na watu wa Thiatira alikuwa Tyrimnos, ambaye alijulikana kama Apollo ambaye ni mungu-jua, na Boreitene, ambaye ni mungu mke aliyejulikana kama Artemi. Ni jambo lisilowezekana kwamba mwonekano wa uliotajwa wa Mwana wa Mungu mwenye "macho yaliyo kama mwali wa moto" na miguu "iliyo kama shaba iliyosuguliwa sana" kuwa ilikuwa inalenga kwa makusudi kwenye kile kinachodaiwa kuwa ni mwana wa mungu wa Thiatira (Ufu. 2:18).

 

Chini ya utawala wa Dola ya Kirumi ibada ya kumuabudu Apollo Tyrimnaios iliunganishwa na dini iliyokuwa inafanya ibada ya kumuabudu mfalme. Imani nyingine ya kidini ilikuwa ni ile ya Sibyl Sambathe au Sambethe ambayo kihekalu chake kidogo kilikuwa “mbele” zaidi ya kuwa ndani mji. Dhana ya kwamba Yezebeli anayetajwa kwenye Ufunuo 2:20 alikuwa kuhani mke wa kijihekalu hiki inakuwa ni vugumu sana kuaminika, kwa kuwa Yezebeli anatajwa kuwa alikuwa anachukuliana na Kanisa la Thiatira akiwa kama mshirika au mwanachama, na alikuwa anakubalika na wachache miongoni mwa Wakristo hawa na kuaminika kuwa ni nabii mke.

 

Ni jambo linalofikirika kwa kiasi kikubwa sana kwamba walikuweko walowezi wa Kiyahudi huko. Matendo 16:14 inaunga mkono hitimisho hili. Wakati huko Filipi, Paulo, Sila na Timotheo walikuwa wanatafuta mahali wanapofanyia ibada Wayahudi siku ya Sabato, wakafika “kando ya mto” “nje ya mji,” wakakutana na kundi la “wanawake” waliokutanika pale,” na mmoja wao alikuwa ni "Lydia, aliyetoka katika mji wa Thiatira na mwenyeji wa huko." Alikuwa huko kwa kuwa alikuwa ni “muuzaji wa bidhaa za rangi ya zambarau” zilizotengenezwa huko  Thiatira, na alikuwa ni “mchaji wa Mungu,” Mmataifa aliyeongokea dini ya Kiyahudi, huenda alitokana na mawasiliano yake na Wayahudi waliokuwa huko Thiatira, lakini ambaye hawajawahi kuwa waongofu bado.

 

Haijajulikana bado kwa wazi ni lini au ni nani ambaye Injili hii ya imani ya Kikristo alihubiri kwa mara ya kwanza kwenye mji huu. Uwezekano mmoj wapo ni ule unaoonekana kwenye Matendo 19:10 ambao unaonyesha kwamba kipindi cha huduma ya Mtume Paulo huko Efeso mmoja au wengi wa wasaidizi wake au waumini wake alienda huko Thiatira na kuanzisha kanisa huko. Wakati kitabu cha Ufunuo kilipokuwa kinaandikwa mnamo mwaka 95 BK kulikuwa na kanisa lenye nguvu huko (Ufu. 2:18-29). 

 

Ufafanuzi mmoja wapo ni kwamba inaonekana kwamba wakati wa utoaji wa ripoti kwa sehemu (baadhi) ya waumini wa Kanisa walikuwa wanamfuata mwanamke aliyeitwa, kwa jina la mfano Yezebeli aliyekuwa anajifanya kuwa ni nabii. Aliwafundisha na kuwapelekea wafanye matendo za uasherati na kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Alikuwa hataki kutubu na inaonekana kwamba wengi miongoni mwa waumini wa Kanisa hili walikuwa wanachukuliana naye. Mbali ya ufafanuzi tutajionea kuna mambo mengi zaidi ya kweli yenye kushawishi na yenye kuelezeka.

 

Kwa mujibu wa Kamusi maarufu ya Biblia iitwayo Interpreter's Dictionary of the Bible, maana ya mambo haya ni:

1. Mwandishi wa kitabu [cha Ufunuo] huenda anakanusha au kupingana na mafundisho yasemayo kwamba kujikana na kujinyima kimwili hakuna athari yoyte kwenye imani ya Kikristo (Matendo 15:29). Kwenye mtazamo huu mpotofu, mafundisho yanayofundisha uhuru wa kufanya ngono na kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu yanasema kwamba hakuna madhara yoyote katika imani ya Wakrito au hayamuathiri mtu kusimama na Mungu.

2. Kwa kuwa ibada ya sanamu inayoelezwa kwenye Agano la Kale pamoja na dhambi ya kuabudu miungu mingine kunafananishwa na dhambi ya uasherati au “uzinzi;” na kwa kuwa karamu za maporini na michezo ya kingono vilikuwa ni sehemu kwenye baadhi ya imani na ibada hizi za kipagani, basi huenda mwandishi alikuwa anakataza hali ya kujiachia huru na kujiburudisha kianasa pale ambapo kunatokea hali ya kujinyima kimwili wakati wa mhudhurisho wa kimatendo kwenye aina kama hii ya dini za kipagani.

3. “Yezebeli” wa Thiatira huenda alikuwa anahamasisha uvumilivu uliotatanisha na watu wa makundi mengine mengi ya dini zilizokuwa kwenye mji ule. Kila kundi la dini hizi walikuwa na mungu-somo na walikuwa na sikukuu zao, shughuli au sherehe zao za kijamii ambazo kwazo zingewafanya wawe na uchangamfu au furaha ya kimwili. Mambo haya hayakuhitaji kuyachukulia kiumakini sana kwa kuwa kila mtendakazi wa vikundi hivi alilazimika kuwa kwenye mojawapo wa vikundi hivi kwa lengo moja tu la kujipatia namna ya kuishi au kuendesha maisha yao. Kwa hiyo, aliweza kutotilia mkazo yale anayoamini kwenye dini yake na kuyachukulia kijuujuu tu na wangeweza kujifunza kujua ukweli kuhusu maisha iwapo kama tu atashirikisha au kuchanganya na masuala ya burudani au anasa na wanafanya hivyo kwa kuwa na ujuzi mkubwa ulitokana na kujifunza kwao kwa kina “mambo ya ndani sana ya Shetani”.

 

Tatizo halikujulikana au kuelekezwa huko Thiatira. Lilikutwa au kugunduliwa huko Efeso na Pergamo (Ufunuo 2:6, 14-15). Kwa hiyo makundi haya hayawezi kuhesabiwa au kujulikana yote vizuri. Itikadi ya uhuru ilikuwa ndiyo mwiba kwa imani ya Wakristo iliyofundishwa vizuri na Mtume Paulo na kuendelezwa kwenye miongo mingine iliyofuatia. Wapagani hatimaye walipungukiwa au kukosa ujuzi hasa na mwelekeo wa imani juu ya Mungu Mmoja na mfungamano ulioko kati ya imani na maisha ya kawaida ya kijamii yenye kuzingatia maadili. Nyakati zilijitetea zenyewe kwa wenye kutangatanga na miungu au mambo mawili ambao walitengwa kutoka na mambo yote ya anasa za mwili na visivyohusika na maisha ya kiroho.

 

Ilikuwa ni vigumu kwa watu walio wachache kujitenga wenyewe kutoka kwenye maisha ya kirafiki na ya kijamii yaliyodhaniwa na kuchukuliwa kuwa ni halali na sio dhambi au hatia kuamini miungu mingi na yasiyoadibisha su kuweka ukomo wa kujinyima mambo ya mwilini. Hata hivyo, imani ya Kikristo ilikuwa kwenye hatari kwa maamuzi haya, na mwandishi wa Ufunuo alionyesha umuhimu wa uvunjifu matendo juu ya miungu wengi (Soma Kamusi ya Interpreter's Dictionary of the Bible, article ‘Thyatira’, Vol.4, p.638-639).

 

Hebu na tuone kile tunachoweza kukifanya kwa ajili hii kwa kadiri tunavyozidi kuendelea mbele.

 

Ufunuo 2:18-29

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. 19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza. 20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. 21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. 22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; 23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine. 25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja. 26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, 27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. 28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi. 29 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

Mabishano kwa ajili ya Thiatira kwa zamani zake na kuhusu Yezebeli hapo chini ni jambo lililoongelewa sana.

 

Sardi

 

Ufunuo 3:1-6

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. 2 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. 3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako. 4 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. 5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. 6 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

Sardi ni mji uliokuweko upande wa magharibi mwa Asia Ndogo, na mji mkuu wa Lydia ya kale, ilijengwa kwenye Bonde la Hermus (kwa sasa Gediz). Mwonekano unajulikana sana ni acropolis ulioanzishwa na mwamba  uliochongoka na ambao ni kichochoro cha Timolus. Pia kuna hekalu la Artemi na uwanda wa safu ya “maelfu ya vilima" (soma Bin Tepe), mkabala na Hermus.

 

Masalio yanayoonekana hadi sasa ya kiufundi wa ujenzi ni yale Artemi, yaliyoko upande wa magharibi mwa acropolis. Dini iliyotukuka na kukubalika na wengi ni ile ya mungu mke wa Asia yote, aliyejulikana kama Artemi ambaye wakati mwingine anajulikana kwa jina la Cybele. Hekalu lake liliangamizwa na kuharibiwa kipindi cha mapinduzi ya Ionic mwaka 499 KK wakati mji wa chini wa Sardi ulipochomwa moto (kwa kujibu wa kitabu cha Herodotus V.102).

 

Historia ya Sardi inauhusiano unaofanana au kufungamanishwa na ile ya mji wa Lydia, ambao makao yake makuu yamebakia kipindi chote cha matatizo ya kisiasa yaliyotokea kwenye maeneo hayo ya kijimbo. Kuna ushahidi fulani kutoka zama za kale za kihistoria za wakazi wake; lakini nafasi yake ya kiuongozi ya mji inapaswa kuwa ni maendeleo ya kipindi cha Walydia walivyokuwa chini ya wafalme wa Kizazi cha Mermnad. Inaonekana kuwa Sardi uko miongoni mwa miji iliyo kwenye himaya ya kifalme ya Waajemi inayojulikana kama Sparda (Darius, Behistun § 6; Babylonian Sa-par-du), jina linalomaanisha nchi ya Walydia, sawa sawa na mji. Sardi ulikujakuwa ni mji muhimu sana miongoni mwa miji ya Uajemi katika Asia Ndogo. Uko upande wa Magharibi mwishoni mwa barabara kuu ya kifalme inayoenda kutoka Susa ilipitia kwenye mito na ikipita Asia Ndogo. Tawi la barabara linatoka Sardi hadi Efeso (kwa mujibu wa Herodotus V.52-54). Utajiri ulioko kwenye mji wa kipindi cha Waajemi unaweza kulinganishwa na mifano fulani kadhaa wingi wa dhahabu iliyokutikana kwenye makaburi yaliyo kwenye vitalu vya Pactolus. Miongoni mwa mapambo ya dhahabu, bangili, vidani, vikuku, na mihuri ya mawe vilivyoko kule ni mfano mzuri wa kazi za kisanii za Achaemenian.

 

Mji wa Sardi unaonekana kwenye Agano la Kale kwenye Obadia 20 ukitajwa kama Mchungaji, na kama mahali ambapo wakimbizi waliotoka Yerusalemu wamekimbilia na kuishi kipindi cha karne ya tano KK.

 

Mnamo mwaka 334 KK mji ulizingirwa na Iskanda (au Alexander), ambaye aliacha jeshi lake lililolinda ngome. Sardi pakabakia kuwa ni kituo cha maongozi kilichokuwa chini ya Kizazi cha kifalme cha Seleucid. Katika juhudi za mdhulumaji Achaeus dhidi ya Antiochus III sehemu ya chini ya mji huu ilichomwa moto (mwaka 216 KK). Sardi uliangukia mokononi mwa Warumi mwaka 189 KK na kuwa chini ya utawala wa Pergamene hadi mwaka 133 KK. Ukiwa chini ya Warumi, Sardi ulikuwa kituo cha kile kilichoitwa a conventus iuridicus, ambayo ilikuwa na idadi kubwa ya wajumbe wake kutoka miji ya Walydian. Ilifaidika sana na utajiri mkuwa kwenye kipindi chake cha karne tatu BK. Shughuli za biashara na viwanda zilishika hatamu. Baada ya tetemeko kuu la ardhi la mwaka wa 17 BK, Tiberius alifanya juhudi za kuujenga upya tena kwa ukarimu wake (Tac.Ann. II.24). Hadrian alutembelea mji huu wa Sardi mwaka 123.

 

Tangia karne ya kwanza na kuendelea imani ya kikristo ilizidi kuenea huko Sardi. Melito, askofu wa Sardi kipindi cha Marcus Aurelius, aliandika idadi kubwa ya tasnifu, moja wapo ilikuwa ni mahubiri au hotuba, ambayo kwa hivi karibuni imenonekana kurudiwa kwenye kile kinachoitwa Chester Beatty Papyri. Baada ya kuunganishwa tena kwa Asia na Diocletian mwaka 297 BK, Sardi ilifanyika kuwa makao makuu ya jimbo lililorejeshwa upya la Lydia, makao ya liwali na ya askofu mkuu wa Sardi, ambao ulikuwa ni mji wa kisasa katika hadhi na viwango vya kimataifa.

 

Waarabu waliuteka mji wa Sardi mwaka 716. Uliendelea kuwa kukaliwa hata baada ya kuangamia kwake na Tamerlane mwaka 1403. Kwa sasa umekuwa ni mahala panapoonekana kama kijiji kidogo, ambacho bado kinaendeleza kuitwa jina lake na kujulikana kama Sart.

 

Sardi linajulikana kama limekufa lakini linaendelea kufanya kazi likiwa ni kituo cha Wakristo wakati Masihi atakaporudi. Na tena hatuwezi kulinganisha na kanisa la mahali pamoja tunapopaongelea mahali hapa.

 

Filadelfia

 

Ufunuo 3:7-13

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. 8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. 9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. 10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. 11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. 12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. 13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

Mji wa Filadelfia (kwa sasa unajulikana kama Alashehir) ulikuwa kwenye jimbo la Warumi la Lydia. Mpangilio wake wa kimakazi ni miongoni mwa sababu kunzishwa kwa imani ya Kihelenisti (Hellenistic). Mtangandao wa kimawasiliano ulitakiwa sana kutoka Pergamo kupitia Sardi na hatimaye kufika Filadelfia hadi kwenye Bonde la Maeander na kwenye njia kuu ya upande wa kusini.

 

Utengenezaji wa sarafu ulianza tangu karne ya pili KK. Ngao za Wamakedonia zilionekana kuwa kwenye aina ya sarafu jambo linaloashiria kuwa ni koloni la wanajeshi wastaafu wa Kimakedonia waliishi kwenye mji huu.

 

Tetemeko luu la ardhi na lililoleta maafa la mwaka 17 BK liliupiga mji huu wa Filadelfia. Tiberius alikuja kutoa msaada, na katika kuwashukuru wakazi wa mji huu kulichukuliwa kama tendo lililoashiria kuujenga upya ambako kunaitwa Neocaesarea. Kipindi cha Vespasian cheo na alama ya Flavia ilianza kuonekana kwenye sarafu. Tangu kipindi cha Caracalla mji huu ulikuwa unaitwa Neokoros (“mwangalizi wa hekalu”) ukihusishwa na dini inayomwabudu mfalme.

 

Mambo ya liutawala au uongozi ya Filadelfia yalikuwa chini ya wilaya ya Wasardi ambayo ililinda sana hadhi yake ya kuwa mji unaoongoza katika jimbo la Lydia. Maendeleo ya mji wa Filadelfia yalitegemea kazi ya kilimo pamoja na shughuli za kutengeneza nguo na bidhaa za ngozi. Katika karne ya tano BK mji huu ulipewa jina la utani na kuitwa “Athene ndogo” kwa ajili ya wingi wa sikukuu wake na madhehebu mengi ya dini potovu.

 

Utukufu wa Filadelfia wa kuwa ni mji muhimu na imara wa Wakristo ulihuishwa siku za mashambulizi ya Seljuk na Ottoman kwenye Dola ya Wabyzantine. Filadelfia ulijihuisha wenyewe na kujiona kama mji ulio pekeyake wa Kikristo kwenye maeneo yaliyotekwa na kusimama au kuhimuli kwenye mizingiro miwili ya kishujaa. Wakati wa kuanguka kwake mwaka 1391, ulijisalimisha kwenye majeshi ya muungano ya Beyazit I na kwa waliowasaidia Wayunani waliokuwa chini ya Manuel II (kwa mujibu wa Interpreter’s Dictionary, ibid., pp. 781-2).

 

Jina hili maana yake ni ‘upendano wa ndugu’ na linakumbusha utiifu na kujitoa kwa unyenyekevu kwa Attalus II (220-130 KK) kwa kaka yake Eumenes II.

 

Mji wa Filadelfia utakuwa hai kipindi cha kurudi kwake Kristo na, ingawaje unazo nguvu kidogo, bado umesifiwa sana. Kuna mambo kadhaa yanayofanya usifiwe na umepewa ahadi kadhaa ambazo zinahitaji maelezo na ufafanuzi wa kina.

 

Laodikia

 

Ufunuo 3:14-22

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

Mji wa Laodikia (siku hizi unaitwa Pamukkale) ulikuwa ulikuwa kwenye barabara kuu ya zamani iliyokuwa inaanzia Efeso na kupitia Maeander na kwenye Mabonde ya Lycus upande wa mashariki na kuishia huko Syria. Pliny anatoa majina ya kwanza kabisa ya Laodikia kuwa ni Diospolis au Rhoas, majina ambayo huenda baadae yaliitwa badala ya kijiji cha Phrygian kilichokuwa mahala hapa. Ukiwa ni mji mkubwa Laodikia ilianzhishwa na WaseleuSidi, kipindi kinachodhaniwa takriban mwaka 250 KK na Antiochus II, ambaye aliuita kwa jina la mke wake Laodice. Kwa sababu mwelekeo wake uliopangiliwa ilimaanisha kuwa alikuwa ni ngome kuu ya huyu Seleusidi.  Mnamo mwaka 190 KK Laodikia uliangukia chini ya utawala wa Wapergamenia, jambo linaloomanisha kushuka hadhi au kudhoofika kwa mji huu. Hata hivyo, utajiri wao ilongezeka wakiwa chini ya himaya ya Warumi baada ya mwaka 133 KK wakati mji uliporuhusiwa kuendeleza uchumi wake uwezo wake wa kibiashara.

 

Utajiri wa Laodikia ulitokana na ardhi yake yenye rutuba na ardhi yake nzuri na yenye nyasi nyingi iliyofaa kwa ufugaji wa kondoo, shughuli za viwanda vya ufumaji na ujenzi wa shule za kufundisha elimu ya madawa. Utajiri wa kanda hii tajiri na yenye maendeleo ulipelekea kwenye mwendelezo wa shughuli nyingi za kifedha na za Kibenki kwenye mji huu wa Laodikia. Mji huu ulitengeneza sarafu yake wenyewe tangu karne ya pili Kabla ta Kuzaliwa Kristo na kipindi kingine kilichofuatia na kuwa kituo muhimu kilichokuwa kwenye mto uliojulikana sana kufanyiwa ibada za miungu yao na kulikoshamiri shughuli za idaba za dini zao. Idadi ya wakazi wake wakiwemo Wasyria wanaoongea lugha ya Kiyunani, Warumi, na wale waliofanyika kuwa ni wa asili ya Kirumi, pamoja na Wayahudi waarufu na matajiri walijumuishwa pamoja. Mnamo mwaka 62 KK kwa amri ya liwali Flaccus, mchango wa kila mwaka, ambao Wayahudi walimariwa wapeleke Yerusalemu, ulipokonywa na kupelekwa Roma. Haki maalumu na za msingi za Wahayudi ziliondolewa mwaka 70 BK. Haya yalikuwa ni matokeo ya uasi wa Wayahudi wa Yerusalemu na matokeo yake yalikuwa ni kuangamizwa kwa Hekalu lao. Wakristo wa kwanza wa huko Laodikia walikuwa na uhusiano na wenzao wa Kolosai na wale wa Hierapolis. Mji huu ukaangukia kwenye mateso ya vita vya Waseljuki na Waturuki na uliachwa kwa haraka sana baada ya karne ya kumi na tatu. (soma Kamusi ya Interpreter’s Dictionary, ibid., pp. 70-71)

 

Udhaifuwake mkuu ulikuwa ni upungufu wa miundombinu mizuri ya isambazaji wa maji.

 

Kwa hiyo, tunaweza kujionea kwamba dhana au imani ya kwamba mji huu utakuwepo bado wakati wa kurudi kwake Masihi haiwezi kuwa kweli.

 

Maganjo ya mji huu na kuharibiwa kwake hata hivyo hakukuonekana hadi kulipofanyika uchimbuzi miaka kadhaa na michache iliyopita. Kwa hiyo unabii unapaswa kuwa uwe unaongelea vipindi-zama na sio maeneo fulani maalumu yaliyotajwa kwenye maandiko haya.

 

Kutambua Uelewa

Maandiko yanayaelezea makanisa saba. Miongoni mwa saba haya, matatu ya kwanza hayaambiwi chochote kuwa yashike walichonacho hadi atakaporudi Kristo.

 

Kristo anajitaja mwenyewe hapa kama kichwa cha kanisa na mwenye zile nyota saba za yale makanisa saba kwenye mkno wake wa kuume na kuwa ndiye anayetembea kwenye vile vinara saba vya dhahabu (vinara vya dhahabu KJV na hata Biblia ya Kiswahili). Kwa hiyo, Kristo ndiye mwangalizi wa mfumo ule wote mzima na wa wale malaika wa makanisa yale saba.

 

Efeso ni waaminifu na walikuwa hawajapotoshwa na mafundisho ya wale manabii wa uwongo, bali inasemekana kwamba wameuacha upendo wao wa kwanza. Walitakiwa watubu vinginevyo Kristo atakuja na kuwaondolea kinara chao ambacho walikuwa nacho.

 

Ahadi waliyopewa ilikuwa ni kwamba Yule atakayeshinda atakula matunda ya mti wa uzima katika Paradiso ya Mungu. Huu ndio msingi wa mafundisho ya Korani pia kuhusu fundisho la Bustani ya Paradiso.

 

Ukweli ni kwamba, mji huu na kanisa lake vilikoma na havipo leo ukomo uliofanyika tangu karne kadhaa zilizopita na kwa hiyo sisi tunakabiliwa na ukweli kwamba vitu hivi haviko tena kabisa na wala Kristo haendi kuurejesha uwepo tena hapo atakaporudi. Tunajua kuwa ni kweli kwamba Smirna ilichukua mahala pa Efeso na kuwa ni kituo cha kazi ya Mungu katika kipindi cha karne ya pili na ya tatu nay a nne.

 

Ilikuwa ni hili la Smirna ndilo lililopinga mabadiliko ya imani ya Kanisa iliyoshurutishwa kutoka Roma na lilikuwa hilihili la Smirna ndilo lililowalea na kuwafundisha wasemaji wa Kanisa waliokuwa chini ya Polycarp mwanafunzi wa Mtume Yohana, na ni mfuasi wake Polycrates wote wawili walihusika kwenye utaratibu wa kikalenda wa vipindi vya siku ya kumi na nne ya mwezi Utata Juu ya Adhimisho la Siku ya Kumi na Nne (Na. 277) [Quartodeciman Disputes (No. 277)].

 

Kristo anamwambia Malaika wa Kanisa lililoko Smirna na anajitaja mwenyewe kuwa yeye ni wa kwanza na wa mwisho na aliyekuwa amekufa na kisha akafufuka tena na kuwa hai. Ili kulielewa vyema andiko hili, soma jarida la Arche ya Uumbaji wa Mungu akiwa kama Alfa na Omega (Na. 229). [Arche of the Creation of God as Alpha and Omega (No. 229)]

 

Kwenye mlolongo huu wa mambo, makanisa yanaambiwa kuwa hayataweza kuwa na madhura ya mauti ya pili. Wale ambao waliuawa watapewa taji za uzima. Kama tulivyoona, siku kumi za dhiki na mateso zinahusu mateso ya Diocletian siku nyingi kabla ya karne ya kwanza na karne kadhaa baada ya Nero na hali iliyokuwepo kwenye ukosoaji na wapinzani walioko na wanaoendelea siku zetu hizi.

 

Kanisa hili halitajwi kuwa litakuwa hai kipindi atakachorudi Kristo.

 

Kanisa la Pergamo lilionekana kuwa ni kama lenye vita na mapambano na lilikuwa limeadhiriwa na mafundhisho ya uwongo ya Balaamu na ya Wanikolai (soma jarida la Mafundisho ya Balaamu na Unabii wa Balaamu (Na. 204) [The Doctrine of Balaam and Balaam's Prophecy (No. 204) and Wanikolai [202] The Nicolaitans (No. 202)].

 

Wanakaa mahala palipo na kiti cha enzi cha Shetani.

 

Danieli 8:23-25 inamwelezea mfalme wa mkuu ajaye inatafsiriwa kama “mfalme mwenye uso mkali na ajuaye mafumbo.” Hiki ni cheo au jina la Mpingakristo. Katika Siku za Mwisho Danieli anatueleza kuwa atawashinda Watakatifu au Watakatifu wake Aliye Juu (pia soma Danieli 7:8,22).

 

Tunajua kutokana inavyosema Ufunuo 13:2 kwamba kiti cha enzi cha Shetani amepewa kiumbe aliyeko kuzimuni ambaye ni mwingine aanayetajwa kwenye Yohana 5:43 (pia Luka 4:6).

 

Kiti cha Shetani au kiti cha enzi cha Shetani kwa hakika hakiko huko Izmir kwa kipindi cha karne hadhaa na wala sio kwenye Siku za Mwisho. Bali ni kiti hiki ndicho kitakachopokea vitasa vya makamio ya Yule Malaika wa Tano kwenye ghadhabu ya Mungu (Ufu. 16:10). Hii haiwezi kuwa na maana sawa au kulinganishwa na Izmir kwenye Siku za Mwisho na ni jambo la jumla sana.

 

Kiti hiki kiko huko Iraq na mto Frati utakauka ili kuwezesha kuwepo na njia ya wafalme wa Mashariki (Ufu. 16:10-12). Eneo hili lilikuwa ni kubwa kuliko kiti cha Smirna bali lilienea hadi kulifikia eneo hili chini ya Wapauliciani wa zama za Wapergamo. Kwa kweli sio Pergamo au mji wa Wapergamo.

 

Kanisa hili liliambiwa litubu, vinginevo Kristo atakuja kwao haraka. Kwa kuwa Wapauliciani walikuwa ni wanaoijua vita aliwaambia atawajilia kinyume na upanga wa kinywa chake, ambao ni Neno la Mungu kwa mamlaka na uweza.

 

Ahadi waliyopewa Wapergamo ni kwamba Yule atakayeshinda atapewa kula mana iliyofichwa (pia soma Yohana 6:58; sawa na Kutoka 16:14, 32-34; Zaburi 78:24-25). Mana iliyofichwa kilikuwa ni chakula cha malaika, kilichopewa jina la uweza au nguvu za Roho Mtakatifu na jiwe la uraia kwenye Mji wa Mungu.

 

Wathiatira walipewa vipindi viwili vya kufanya matendo na cha mwisho kilikua kikuu kuliko cha kwanza. Walienea huko Ulaya na waliteswa kwa muda wa karne kadhaa. Wathiatira walishuhudia zama za kufanyika au kuja kwa Matengenezo na waliteswa na Waprotestanti sawa na walivyoteswa na Wakatoliki kipindi cha nyuma kabla yao.

 

Yezebeli ni Kanisa linalofanya uzinifu na wafalme wa dunia. Yeye ndiye Yule Kahaba Mkuu aliyeandika na kutajwa kwenye kitabu cha Ufunuo kuwa na jina la Siri, Babeli Mkuu, na Mama wa Makahaba. Yeye ni kinara wa makanisa mengi ya nchi za Magharibi na ambaye ana mlolongo mkubwa wa binti zake ambao ni makanisa ya Kiprotestanti na mabinti zake hawa pia wanawakiliasha ama kukumbatia mafundisho ya Utatu au Utrinitari unaomwamni Mungu wa Utatu. Kwa kweli watakufa kabisa lakini hatima yao wataishia kurejea tu kwenye mfumo na imani ya Utrinitaria ama Utatu katika Nyakati za Mwisho pale utakapoondolewa na kuangamizwa kabisa.

 

Tatizo laweza kuwa liliepukwa kwa kudai kwamba maandiko yanaelezea kipindi cha cha Rumi kipindi cha Nero na sio kwa Kanisa kwa kipindi chake chote, lakini andiko lililoko kwenye Ufunuo linaonyesha wazi ni kanisa linalotajwa. Linaweza kuwa linaelekea kuwa na mfumo wa kiimani ya Kanisa la Kirumi na mabinti zake Waprotestanti. Tunaweza tu pia tukiongelea kuhusu kipindi cha Wanamatengenezo na tunaweza tu kuelezea kipindi cha zama za Kanisa ambacho kila kimoja kilichukua hatamu ya ubora wake kwa kipindi tofauti cha malmaka yake. Hawa wanaweza tu kuwa wapeleka nuru kwa kipindi kile na kinara kimoja.

 

Kanis hili linahukumiwa sawasawa na matendo yake na maonyo yametolewa kwa wale wote ambao wamehukumiwa sawasawa na matendo yao.

 

Wale wote wasiozijua hila za Shetani (sawa na. 2Wakorintho 2:11) hawatapewa mzigo mwingine. Hili ni kanisa la kwanza kuambiwa kushika walichonacho hata atakapokuja Kristo (Ufunuo 2:25).

 

Wale wote walio kwenye msimamo au imani hii na ambao watashinda na kuyafanya matendo ya Kristo hadi mwisho watapewa uweza na mamlaka juu ya mataifa (au Wamataifa) na watawachunga kwa fimbo ya chuma. Mataifa yatavunjika hasa pale Kristo atakapochukua mamlaka ya kiutawala kutoka kwa Baba. Ndipo kanisa hili lililokuwa kwenye majaribu makubwa ya kukomeshwa na makanisa ya Wamataifa ambayo yaliyapotosha mafundisho kwa kuyachanganya ma yale ya Dini potofu na za Uwongo, basi kanisa hili lililoshinda litapewa mamlaka juu yao na fimbo ya chuma.

 

Kristo anafika mbali kwa kusema: “Nami nitampa ile Nyota ya Asubuhi” Zawadi au thawabu hii ni ya kuitawala sayari hii yote kama Waleta Nuru kwenye sayari hii. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba watakuwa ni wafundishaji au waelimishaji wakuu kwenye sayari hii wakiwa chini ya mamlaka ya Yesu Kristo aliye Nyota Mpya ya Alfajiri kutoka kwao na kwa wengine.

 

Kanisa hili la Sardi linaambiwa liyakamilishe mambo yanayotaka kufa. Kanisa hili la Sardi lilijidhania kuwa liko hai na kudhania kuwa linaishi bali lilikuwa limekufa. Lilichukua nafasi ya kanisa la Thiatira kipindi ambacho kanisa la Thiatira lilip[okuwa kwenye limeteswa kwa mateso makali sana likiwa kwenye maeneo hayahaya. Matatizo yaliyoyakumba makanisa yaha yameelezewa kwa kina kwenye jarida la Wajibu wa Amri ya Nne ya Mungu kwenye Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayozishika Sabato (Na. 170) [Role of the Fourth Commandment in the Historical Sabbath-keeping Churches of God (No. 170)].

 

Kanisa hili lilianza baada ya zama za matengenezo yaliyofanyika ndani ya Kanisa la Ubatizo la Sabato lililojulikana kama Seventh Day Baptist na hatimaye kwenye Makanisa ya Mungu. Mengi ya makanisa haya yameanguka na kujichanganya na mengi yao yamo kwenye imani ya miungu mingi. Kanisa hili halijui chochote kuhusu unabii wala mahala pao katika historian a mpango wa Mungu, ni kama Kristo anavyosema kuwa hawataujua muda wa kuja kuwajilia. Wanamgojea kwa uaminifu kuja kwake na hadi atakapokuja.

 

Na hii ndiyo sababu iliyowapelekea kutoa nabii za uwongo nyingi sana (soma majarida yetu ya Unabii Wa Uongo [269] na Miaka Arobaini ya Toba [290]. [False Prophecy (No. 269) and Forty Years for Repentance (No. 290)].

 

Wale walio kwenye kanisa hili na ambao hawajayatia unajisi mavazi yao watatembea na Kristo waliwa na mavazi meupe. Msingi au kiini cha wao kutembea na mavazi meupe kunakoelezwa kwenye unabii huu kunatokana na kama ilivyoandikwa kwenye Ezekieli kulikotokana na vita ya Hamon-Gog na kufanyika kwa Matengenezo mapya ya Israeli na huduma ya ukuhani itakayowekwa ndani yake ambao watakuwa wanavaa mavazi meupe ya Hariri au bafta na ambao watamngoja Kristo (soma jarida la Vita Vya Amagadon [294] [War of Hamon-Gog (No. 294)]

 

Ahadi Kwa Wafiladelfia

 

Kanisa la Wafiladelfia ni kituo kilichodhahiri kutoka kwa Wasardi. Hao hawako kwenye mwonekano wa kazi zilizokufa au imani iliyokufa na pia hawakuwa kwenye mafundisho yaliyokufa.

 

Kristo analiambia kanisa hili kwamba yeye ni mtakatifu na wa kweli na kwamba anazo Funguo za Daudi. Anafungua na hakuna anayeweza kufunga na kwamba anafunga na hakuna awezaye kufungua. Hii inatokana na jina alilojiita mwenyewe la kuwa yeye ni Nyota ya Alfajiri, yaani, Al Tarikh. Uweza huu ni mlango uliofunguliwa ambao amewapa. Kanisa hili linamatendo ingawaje linanguvu kidogo sana. Linayashika maneno ya Kristo na wala halikulikana jina lake.

 

Kanisa hili limeijaribu imani ya Kiyahudi na ya waongofu waliotoka kwenye Umataifa na ambao wanajiita kuwa wao ni Wayahudi, bali sio, ingawaje mafundisho ya uwongo yalichukuliwa kutoka kwenye itikadi za kimapokeo ya wanadamu. Kanisa hili liliwajaribu na kuwaona kuwa ni waongo na wamepotoka na kuwagundua kuwa wanayoyashika ni ya uwongo na Kristo amewafanya waje na waabudu au waje kusujudu mbele ya kanisa hili. Ndipo kanisa hili litakuwa na sehemu muhumu ya kujifunza kutoka kwalo na mafundisho yake kwenye Siku hizi za Mwisho na Ukiri utakaopelekea kuongoka kwao Yuda.

 

Na kwa kuwa kanisa hili linalishika neno la Kristo kwa uvumilivu, ndipo Kristo atawalinda watoke saa ya kujaribiwa itakayoujilia ulimwengu wote. Imani ya Wasardi na Walaodikia haikuweza kuwaokoa.

 

Ujio wa Kristo uko karibu sana pamoja na kuwepo kwa hali hizi za imani na mambo vilivyo sasa.

 

Kanisa hili limevikwa taji na kila mmoja wao wamebarikiwa kwa namna hiyo hiyo. Kricto ameahidi kuwafanya Wafiladelfia kuwa ni nguzo ndani ya Hekalu la Mungu. Kwanza kabisa tunapolisikia jambo hili tunaona kwamba halionekani kuwa ni la namna ya mfano tu kama alivyowaahidi Wathiatira bali linaonekana kuwa ni kubwa na linanguvu zaidi kimaana yake.

 

Wafiladelfia walijaribiwa kimafundisho na wanawajibika katika kuitangaza na kuieneza Injili ya Ufalme wa Mungu katika Siku za Mwisho na kurekebisha makosa mengi yaliyo kwenye imani ya Wasardi.

 

Ni kanisa hili ndilo ambalo sauti yake inatoka kwa lengo la kuchapisha na kutangaza hatari au mateso na maonyo ya Siku za Mwisho kama yalivyotabiriwa na nabii Yeremia (Yeremia 4:15-16); pia soma jarida la Maonyo ya Siku za Mwisho (Na. 44) [Warning of the Last Days (No. 44)].

 

Watu hawa wamepewa pia jina la Mungu na jina la Mji wa Mungu. Kwa maneno mengine ni kwamba wataitwa Yahova kama Kristo alivyoitwa wakati alipoongea na Mababa wa kale. watapewa cheo cha kuitwa elohim kwa amri ya mamlaka ya juu sana pamoja na kuuingia Mji wa Mungu, ambao ni Yerusalemu Mpya, unaoshuka kutoka mbinguni. Kristo anawapa watu wa kundi hili jina lake jipya na ambalo ndiyo mamlaka yake.

 

Kwa hiyo Kristo anasema: “yeyen aliye na sikio na alisikie neno hili analoyaambia makanisa.” Hii ni kwa sababu Wasardi na Walaodikia hawasikilizi. Kanisa la Sardi limekufa na lile la Laodikia liko vuguvugu na limetapikwa kutoka kinywani mwa Mungu.

 

Alipokuwa analielezea kanisa la Walaodikia, Kristo alijiita kuwa ni “yeye ni Amin, mwaminifu na shahidi wa kweli.” Ni katika kipindi cha makanisa haya ndipo Kristo atakapokuja. Anayaambia makanisa haya kwamba Kristo atakuja. Analiambia kanisa hili kwamba yeye ni “Mwanzo wa Uumbaji wa Mungu” (Ufunuo 3:14) kwa kuwa imani hii inaanza kwa kufundisha kuwa yeye sio, bali zaidi sana inadai kuamini kwamba yeye anacheo sawa na Mungu.

 

Kosa hili lilijipenyeza hadi kwenye kanisa la Sardi kipindi cha kuwepo kwa makanisa yaliyofuatia, lakini hili la Sardi halikuwa hivyo ka kipindi cha karne nyingi za hapo nyuma.

 

Matendo yaliyotokana na imani hii yalikuwa hayako kwenye ubaridi wala moto, bali yalikuwa ni vuguvugu na kwa sababu ya kuwa kwao hivyo walitapikwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Imani hii inajifananisha na nyingine na kujiona kuwa wao ni tajiri na kuwa hawahitaji kitu chochote na wala hawajui ukweli halisi ulivyo wa hali yao ya kiroho. Wako wanyonge, wenye mashaka, na maskini, vipofu, na wako uchi.

 

Njia pekee ambayo kanisa hili linaweza kurejeshwa upya ni kwa wao kuamua kununua dhahabu iliyosafishwa kwa moto kwa uweza wa Roho Mtakatifu ili waweze kuwa tajiri na kuvaa vazi jeupe ili waweze kuificha aibu yao na asiwepo mtu wa kuuona uchi wao.

 

Limeambiwa lijipake dawa machoni mwake ili lipate kuona. Lina upofu wa kuijua kweli ya neno la Mungu na unabii na wa kufikia kwenye ujuzi wa kweli na kuujua mpango wa Mungu na kuujua muundo na mfumo wa kalenda yake.

 

Analikemea na kulitaka kanisa hili litubu kwenye nyakati hizi ambazo pia ni Siku za Mwisho akilitaka kanisa hili litubu. Yeye anasimama mlangoni na anabisha na kusema na kila mmoja peke yake. Kanisa hili linabidi pia kushughulika na kile kinachojulikana kama Al Tarikh au Nyota ya Alfajiri. Kristo ndiye naayekuja kama mwivi ajaye majira ya usiku wa manane Mgeni ajaye Usiku lakini pia ni kama mtu asimamaye mlangoni na kubisha na kusema na wale wanaoitwa na kuokolewa. Mchakato huu ni wa mwishoni kabisa na unaoitangulia ile karamu ya arusi ya Mwana Kondoo (soma jarida la Baragumu [136] [Trumpets (No. 136)].

 

Hatimaye anaendelea kutoa wito wa toba kwa Walaodikia na yeyote atakayeshinda ataketi pamoja naye katika kiti cha enzi kama yeye alivyoshinda na kuketi pamoja na Baba ambaye pia ni Mungu wake, kwenye Kiti chake cha Enzi.

 

Dhana iliyopo kuhusu usemi wa Nguzo za Filadelfia ni kwamba nguzo ni vitu vinavyofuatia kujengwa baada ya mawe ya msingi wa Hekalu, ambazo ni Mitume wa Kristo na manabii. Wamefanywa kwa matofali makamilifu yaliyochongwa vizuri na ambayo pia yamechimbiwa vizuri na kuchongwa na kuingizwa kwenye fimbo za chuma za Wathiatia na kuwekwa hapo ili ziweze kushikilia mfumo mzima wa uimarisho wa Hekalu ili liwe ni jengo lililosimama imara. Wamejengwa juu ya msingi wa Kristo na mitume na manabii na wao ni mwegamo wa katikati ya Hekalu la Mungu. Wao ni mwili wa Kristo na ambao kwa pamoja wanafanyika kuwa ni ndugu wanaopendana.

 

Imani hii itaendelea na kudumu hadi mwisho na watapata thawabu zao na Kristo atakapokuja. Haijalishi ni zama gani au mfumo gani ulioko wewe la msingi t uni kwamba unatakiwa kushinda na ufanyika kazi na kuwa na bidii katika katengenezo mapya ya imani ambayo wamepewa watakatifu mara moja tu.

 

Kuna uhusiano na dhana ya kwamba kila zama ina zama yake, bali tabia kuu za kawaida za kila zama ni zile zinazoionyesha na zama zina kawaida hiyo au inajulikana na hilo. Kila mtu anapaswa kuonywa na anapaswa kushinda matatizo yake na kuyashinda majaribu au matatizo yaliyo kwenye zama zake anazoishi kwazo.