Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[287]

 

 

 

Maadhimisho ya Siku za Kuzaliwa

(Toleo La 1.0 20000101-20000101) Imerekodiwa kwenye Tepu

Hizi sherehe za Siku za Kuzaliwa zinamaana gani hasa? Chanzo na msingi wake uko kwenye Kalenda ya Juan a haina uhusiano wowote na maagizo ya Biblia au kalenda iliyowekwa na Mungu. Watazamaji wa nyakati mbaya za Nyota wanazitumia sana katika kulinganisha na mbahatisho wa kinyota na wameuita kuwa ni fungu la nyota za bahati ya kinyota ya kuzaliwa zinazowazunguka na mahala ambapo mafungu au makundi ya nyota hujitokeza wakati wa kuzaliwa. Ni wapi basi maadhimisho haya ya Siku ya kuzaliwa yanatoka na kuna falsafa gani iliyoko nyuma ya maadhimisho haya.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 2000 Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Maadhimisho ya Siku za Kuzaliwa


 


Bilia haijaweka kumbukumbu yoyote ya kuzaliwa kwa Kristo wala hakuna kwenye ashirio lolole la uandishi wa Biblia. Na kwa kweli, Biblia inasema kwamba siku ya kufa mtu ni bora kuliko siku ya kuzaliwa kwake.

Mhubiri 7:1 Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.

 

Kwa makusudi kabisa Biblia haijaandika kuhusu tarehe aliyozaliwa kwa Yesu Kristo, ambaye ni mlengwa wa muhimu kuliko wote kwenye Biblia zaidi ya Mungu. Kwa kweli tunaweza kusema kwa hali namna fulani kwamba haikuwa siku hii inayijulikana leo kuwa ni tarehe 25 ya mwezi Desemba tunayoijua na ambayo inauhusiano na imani ya kale nay a kipagani.

 

Ni kwanini maadhimisho haya ya kuzaliwa kwa Kristo yamekuwa ni ya muhimu sana kwa baadhi ya watu? Ni kwa nini basi kwa makusudi kabisa wameianzisha siku inayoshabihiana na sikukuu ya kipagani na kuzaliwa kwa mungu Jua Asiyeonekana? Jibu lake ni rahisi sana kulijibu. Imani au dini ya Kipagani inauhusino wa karibu sana na ibada ya Mungu wa Utatu na ni mungu aliyeenea kama ugonjwa wa mlipuko na kujulikana na Waariyani kama ni ibada za Mashetani. Waabudu Shetani waliigeuza Dini ya Kikristo kupitia kwenye Dini za Usiri na imani potofu za kuabudu Juan a wakamfanya Kristo kuwa ni kitovu cha imani na ibada za kidini hizi. Kwa hiyo ilihitajika sana kwamba yeye awe na siku yake kuzaliwa kwake kwa kuwa maadhimisho haya ya siku za kuzaliwa ni kitovu cha imani yao ya dini ya shetani. Walifanya hivyo kwa sababu hizohizo kama walivyoibadili siku takatifu ya Sabato na kuwa Jumapili (soma jarida la Jukumu la Amri ya Nne Kwenye Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayozishika Sabato (Na. 170) [The Role of the Fourth Commandment in the Historical Sabbath-keeping Churches of God (No. 170)].

 

Falfasa yake ni rahisi sana. Mapezi yaliyo nje ya Mapenzi ya Mungu ni kuamini miungu wengi. Shetani ameweka utaratibu au mfomo wa kiibada ulio nje ya mapenzi ya Mungu na Sheria zake na kwa hiyo hali hii ni sawa na kuamini miungu wengi. Malaika wote wa Mbinguni wanajitahidi iwezekanavyo ili wafikie kiwango cha kuwa elohimu au kiungu wadogo wakiwa ni sehemu ya viumbe na kuwa kwenye mapenzi ya huyu Mungu mmoja, wa pekee na wa kweli (soma jarida la Wateule Kama Elohimu (Na. 1) [The Elect as Elohim (No. 1)]. Kwa jinsi hiyo, Mungu anakuwa ni Yote Ndani ya Yote (Waefeso 4:6) (soma majarida ya Jinsi Mungu Alivyofanyika Kuwa Familia (Na. 187) na Kufanyika Washirika Pamoja na Baba (Na. 81) [How God Became a Family (No. 187) and Consubstantial with the Father (No. 81)].

 

Waabudu Shetani wanatafuta jinsi ya kuwa miungu na wanashikilia kuwa sawa na Baba, jambo ambalo Kristo hakuwa hata kujaribu kulifanya na ni kama ilivyo imani ya Kristo na wateule hawajawahi kamwe kujaribu kuwa hivyo.

 

Wateule wamefanyika kuwa wana wa Mungu kwa ajili ya utii wao wa kuzitii na kuzishika amri za Mungu (Ufunuo 12:17; 14:12). Kristo hakutafuta wala kujifanya kuwa sawa na Mungu bali alijinyenyekeza na kuchukua mwili na umbo la kibinadamu na kuwa mtii hadi kufa, naam, mauti ya msalaba (Wafilipi 2:5-8).

 

Dhana ya kwamba mwanadamu anaweza kufanyika kuwa mungu mdogo, pasipo kumtii Kristo na kuwa mteule wa huyu Mungu wa Pekee na wa kweli na kuiamini na kuishika Torati yake, ni sehemu ya uwongo wa shetani usemao hakika hutakufa. Shetani alimwambia hivyo Hawa pale bustanini (Mwanzo 3:4) (soma jarida la Fundisho la Chanzo cha Dhambi (Na. 246); [The Doctrine of Original Sin Part I The Garden of Eden (No. 246)]; soma pia majarida ya Torati na Amri ya Kwanza (Na. 253) na Torati na Amri ya Tano (Na. 258) [Law and the First Commandment (No. 253) and Law and the Fifth Commandment (No. 258)].

 

Kwa hiyo, Lakenda ya Shetani ya Jua ambayo dini na madhehebu ya waamini Utatu yameiamini na kuikumbatia kuwa kitovu cha imani yao, inamwelekeo wa kumfanya mtu awe mungu na kuwa hatakufa hakika. Maadhimisho haya ya siku za kuzaliwa ni mwanzo na ni uwongo mkubwa unaoonekana kama mtakatifu na mashuhuri sana kwenye imani hii potofu na danyanyifu.

 

Biblia inayotumika kwenye ibada za dini ya Shetani (kwa mujibu wa kitabu cha Anton Szandor LaVey, (Air [Anga]) Book of Lucifer – The Enlightenment [Kitabu cha Lusifa], Avon Books, 1969, Ch XI, Religious Holidays [Sikukuu za Kidini], ukurasa wa 96) inasema yafuatayo kuhusu maadhimisho haya ya siku za Kuzaliwa:

Siku KUBWA ZAIDI kati ya sikukuu zinazotukuzwa kwenye dini ya Shetani ni ile ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa mtu. Siku hii ni mkanganyiko wa moja kwa moja wa siku takatifu zilizo takatifu sana za dini yao ambayo inamtukuza mungu aliyeumbwa kwa umbo la kianthropomofikia ya maumbile yao wenyewe, ambayo ni kuonyesha kuwa utu wao haujazikwa bado.

Waabudu hawa wa Shetani hujisikia kwamba: ‘Kwa nini tusiwe wa kweli hasa na kama unakwenda kujifanya kuwa ni mungu mdogo anayefanana nawe, na basi ni kwanini usimfanye mungu huyo awe kama ulivyo wewe mwenyewe?” kila mtu ni mungu mdogo iwapo tu kama anaweza kujitambua kuwa ndivyo alivyo. Na ndipo waabudu mashetani hufanya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa mtu na kuifanya kuwa ni kama siku muhimu sana ya kuiadhimisha na kuisherehekea katika mwaka. Baada ya wote ndipo iwe ni wewe tu usiyeonyesha furaha kuu kwa ukweli wa kwamba wewe ulizaliwa na kuliko kipindi cha kuwa karibu na kuzaliwa na kukutana na mtu ambaye hujawahi hata kukutana naye? Au kwa jinsi hiyo, licha ya kuwa ni sikukuu ya kidini, bali ni kwa nini basi ulipe gharama au usababishiwe kulipa kodi kubwa kwa ajili tu ya kuzaliwa kwa rais au kwa siku tu iliyowekwa kwenye historia zaidi ya vile tufanyavyo kwenye siku tuliyoletwa kwenye ulimwengu huu mkubwa kuliko zote?

Licha ya ukweli wa kwamba baadhi yetu tunaweza kuwa hatukutakiwa au huenda twawezakuwa hatukuwa tumepangiwa kuwepo kwetu, basi tungefurahi, hata kama hakuna mwingine yeyote aliyekuwepo pale! Basi ulipaswa kujipongeza mwenyewe kwa kujipigapiga mgongoni, na kujinunulia chochote ukipendacho, na kujiburudisha au kujipa raha mwenyewe kama mfalme (mungu mdogo) ambavyo ndivyo ulivyo, na kwa hiyo usheherekee maadhimisho haya ya siku ya kuzaliwa kwa kurukaruka na nderemo na kuserebuka.

 

Mwandamano wa mambo yanayofanyika kwenye maadhimisho haya ya Sikukuu za Shetani yanaonyesha jinsi imani hii illivyojipenyeza na kuingia kwenye Ukristo. Mara nyingi wanafanya hivyo wakati wanapofanya onyesho la wao kuwa ni sehemu ya jambi hili na kisha wanayaiga majina ya watu na kuyaweka au kuwachukua hatu hao na kuwaweka kwenye orodha yao ya Watakatifu wanaowatangaza kwenye imani zao wanazoziita kwa kujichanganya kuwa ni za Kikristo, ingawaje hata wao wenyewe kwa kweli walikuwa ni waabudu Shetani wakubwa. Kwa jinsi hii, familia ya Kiingereza ya Biniface ilipeleka Ukristo bandia na wa uwongo huko Ulaya na kuudharau kwa kuupotoa Ukristo wa kweli na halisi wan Wafrisians wa Ujerumani. Hebu na tuiangalie familia hii inayojulikana kama ya Mtakatifu Boniface na walivyofanya kwa hivi yunavyotafakari juu ya sikukuu nyingine muhimu zaidi na zenye mashiko kwenye Kalenda ya Shetani. Biblia ya Shetani inazitaja sikukuu hizi nyingine na zinazofuatia kuwa ni zile za Walpurgisnacht na Halloween.

Baada ya sherehe ya kuzaliwa kwa mtu, sikukuu nyingine mbili kubwa za Shetani ni zile za Walpurgisnacht na Halloween (au za Kumtukuza Hawa).

Mtakatifu Walpurgis.—au Walpurga, au Walburga, kutegemea na wakati na mahali ambapo mtu anamtaja au kumtamka mwanamke huyu—alizaliwa huko Sussex yapata mwishoni mwa Saba au mwanzoni mwa Karne ya Nane, na alisomeshwa huko Winburn, Dorset, ambako baada ya kuchukua au kuweka nadhiri, alibakia kwa miaka ishirini na saba. Naye kisha kwa msisitizo wa mjomba wake Mtakatifu Boniface, na kaka yake Mtakatifu Wilibald, waliondoka pamoja na watawa wengine kwenda kutafuta nyumba za kidini huko Ujerumani. Makazi yake ya kwanza yalikuwa huko Bischofsheim kwenye dayosisi ya Mainz, na miaka miwili baadae (754 BK.) akafanyika kuwa ni gombera wa jumba la watawa wa Kibenedictine huko Heidenheim, kwenye dayosisi ya kaka yake Wilibald wa Eichatadt huko Bavaria, ambako kaka yake mwingine, Winebald, kwa wakati huohuo alifanywa kuwa ni mkuu wa nyumba ya watawa. Na alipofariki Winebald mwaka 760 alichukua wadhifa wake wa kuwa kiongozi, akishughulika na uangalizi wa nyuma zote mbili hadi kufa kwake mnamo Februari 25, 779. Mabaki ya kifupa yake yalielezewa na Eichstad kuwa; pale alipolazwa kwenye mwamba wa jiwe takatifu, hatimaye kulitokea mafuta ya aina ya lami, ambayo baadae yalikuja kujulikana kama mafuta ya Walpurgis, na ambayo yalichukuliwa au kuaminika kuwa yalikuwa na miujiza fulani ya nguvu ya kuwaponya watu na magonjwa yao. Pango la kaburi lake likafanywa kuwa ni mahali pa kutembelea wahujaji, na kanisa kubwa sana lilijengwa mahala hapo wakati huohuo. Anaadhimishwa kwa kukumbuka kwa nyakati mbali mbali na kila mara lakini hasahasa ni tarehe 1 Mei, siku yake hii ilichukuliwa kutoka kwenye sherehe na sikukuu za kizamani za Kipagani. Lakushangaza sana ni kwamba, mchakato wote huu uilionekana kuwa ni ya muhimu na lazima kwa ajili ya kuupuuzia au kufumbia macho mwendelezo wa sikukuu iliyokuwa muhimu sana ya Kipagani ya kila mwaka—iliyofanyika kama hitimisho kuu la ikwinoks ya majira ya baridi! (La Vey, ibid. pp. 96-98)

 

Tunaona hapa nia halisi hasa iliyoko katika kuziiga na kuziingiza sikukuu za Utatu wa Kipagani na jinsi wanavyozigeuza na kuzifanya kuwa ni sikukuu za Kikristo. Kwa njia hii ilifanywa kwa kupitia utendaji kazi wa familia au jumuia ya kishetani iliyokuwa inafanya kazi ndani ya imani ya Kikatoliki. Kanisa hili la Katiliki limefanyika kuwa ni wakala mzuri na wa kuaminika katika kuieneza imani na dini hii ya uwongo na ya kishetani kwenye maeneo yote ya Ulaya Kaskazini.

 

Walifanikiwa sana kwa kuwa Wajerumani na wakazi wengine wa maeneo hayo maarufu kama Teutons walikuwa ni sehemu ya waumini na wafuasi wa imani hii ya zama kale sana iliyokuwa ikihitimisha ibada zake kwa kuwatoa kafara watoto wao na imekuweko huko kwa muda mrefu ikitokea Mashariki ya Kati, zamani sana hata kabla hawajahamia Ulaya. Wamekuwa waumini wa dini hii ya Kisirisiri na tata kwa kipindi cha Milenia wakiwa cihini ya imani nyingine nyingi ambazo ziliibuka kutoka Babeli pamoja na kwa Waashuru na Wahiti; Wababelonia na Wamedi na Waajemi na hatimaye kwa Waparthiani wa Kiisraeli (soma jarida la Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235) [The Origins of Christmas and Easter (No. 235)]; soma pia Muhtasari ulioandikwa kwenye machapisho ya W. Cox kwenye kitabu kilichoandikwa na R. S. Kohn; cha The Sabbatarians in Transylvania, [Wasabato wa Transylvania] CCG Publishing, USA, 1998).

 

Wazungu walikuwa ni sehemu ya imani hii ya kale ya kuiabudu miungu ya machanganyiko wa Waashuru na Wababeloni ambayo msingi wake ulikuwa ni kumuabudu Mungu wa Utatu na ni imani ambayo ilijipenyeza na kukubalika huko India na ulimwenguni kote (soma jarida la Ndama wa Dhahabu (Na. 222) [The Golden Calf (No. 222)].

 

Ukristo ulirithi kwa kiasi kikubwa au kwa kiasi fulani kukomesha ibada za kutoa kafara wanadamu huko Ulaya lakini wenyewe ulijitoa mhanga kushika mchakato unaoendelea wa kalenda na wa sikukuu zake kutokana na matumizi yaliyoanzishwa na Waaryani na ukengeufu wa kanisa lililojichanganya kiimani na lililojiingiza kwenye mambo ya kisiasa.

 

Imani Iliyo na Mchanganyiko wa Kiashuru na Kibabeloni

Jambo geni kama itakavyoonekana kwenye utaratibu wetu wa upimaji wa masaa na mahali pa mwanadamu na ni kwenye wakati ule wa kipimo vinatokana na kipimo cha umri wa miaka ya uzeeni cha Wababelonia, kilicho sawa na tarakimu ya sitini. Ndipo kwamba kulikuwa na dakika sitini kwenye saa moja na sekunde sitini kwenye dakika moja. Waashuru na Wababeloni walipenda kulinganisha mchakato huu kwa kuhakikisha uzao unachukua mahala pake kwa wakati muafaka pasi kutofautiana kwenye mzunguko wa jua. Siku za kuzaliwa ziliendana sawia na mwonekano wa mwezi mwandamo na kwa hiyo inaonekana na hesabu za awamu zilizowekwa kwenye meza kama tunavyoziona leo (soma kitabu cha fasihi cha The Encyc. Of Religion and Ethics (ERE), art. Birth (Assyro-Babylonian), Vol. 2, p. 643). Hesabu hizi zinaonekana kutuama kwenye ibada za Mungu mke aitwaye Ishtar au Easter. Meza hizi zinaonyesha michoro mbalimbali ya tarakimu au hesabu za mambo ya juani na horoscopes za jua zilizopangiliwa kutokana na siku za kuzaliwa pamoja na uwekaji wa michora ya kupatwa kwa jua (soma kitabu hichohicho). Mwezi mwandamo ulikuwa wa muhimu na sio muhimu sana kuliko Ishtar au Venus na anaonekana tofauti moja tu na mke wa Merodach, Zer-panitum aliyechukua jina la Eru’a au mtungo. Kwa mtazamo wa namna mbili wa Uumbaji anaonekana kama Aruru likimaanisha yeye aliyefanya, pamoja na Merodach muumbaji wa vitu vyote, mbegu ya mwanadamu.

 

Akiwa kama Ishtar-Zer-panitum (akiitwa Zer banitum), aliitwa pia Mah au Mami alikuwa ni mbegu muumaji wa kike ambaye mara nyingi hubadilika kuwa Sar-panitum ambaye maana yake ni Mwenye Kung’aa au Mwenye nuru (ambaye ni Venus). Alikuwa ni mungu-mke wa urutubisho aliyejulikana kwa majina ya wadhifa mbalimbali kama vile mama anayefungua vio vya uzazi (Amu-du-bat=ummu pitat burki); Nagar-Sagar, mbunifu wa uumbaji wa kijusi kinachokuwa mwanadamu; Sasuru, mungu mke wa kijusi, Nintur, mwanamke mwenye tumbbbo au mimba, Nin-zizna=belit binti, mwanamke wa uzazi; Nin-Dim, mwanamke wa uzazi mwingi, nk. Hii inaonyesha jinsi ambavyo mungu huyuhuyu mmoja anavyoweza kuwa na majina tofauti tofauti kutoka sehemu moja hadi nyingine nab ado akichukuliwa kuwa ni mungu yuleyule mmoja, kama vile anavyoitwa majina mbalimbali Diana wa Efeso alivyokuwa anatwa na kujulikana shughuli zake kwenye hekalu la mungu wa urutubisho kule.

 

Merodach mwenyewe alionekana pia kuwa ni kama mungu wa uzazi pamoja na mshiriki wake ama mke wake, huenda kwa kuwa alichukuliwa mwanzo wa miungu. Hatahivyo, kitabu cha fasihi cha ERE kinachukulia kwamba dhana na nguvu zinazoonekana inaweza kuwa ni sahihi zaidi kwa kuwa Merodach alipata jina hili la kiwadhifa baada tu ya Babeli ambaye alikuwa ni somo wake, ilipoibuka na kupata nguvu za kutawala na miungu yake ya kale kuwa ni udhihirisho wake. Anajulikana kwenye mfano huu kama Tutu (ajulikanaye kama mullid ilani, mudil ilani (ERE, ibid.). Kwa kusahihisha uzazi Wababeloni pia alitumia vidonge vya kurutubishia mbegu na uzuiaji wa mimba na mimea na mawe (haya yapo kwenye kitabu hichohicho).

 

Tunajua asipo shaka kabisa kutokana na vibao vilivyoandikwa tarehe zilizofuatia baadae kwamba saa ya kuzaa ilikuwa inawekewa umuhimu wake na kupewa uzito wa juu wa aina yake na kuagua kwa kutumia jinsi nyota zilivyojipanga anapozaliwa mtoto na zilipigiwa kura, ikichukuliwa kwa kunukuliwa au kukumbukwa kwa ziada ya aina yake na kufanyiwa sherehe za kidini au ibada takatifu. Kutokana na kibao cha udongo kilichojulikana kama K 1285, tunajulishwa kwamba sherehe hizi zilikuwa zikifanyika kwenye Hekalu la mungu Ishtar, au Istar (Easter), kwa watoto wa watu walioandikishwa. Kwenye kibao hiki ametajwa kuwa Malkia wa Ninawi (soma kitabu hichohicho, uk. 644).

 

Siku fulani za mwezi zilikuwa heri au zenye bahati na tangu kipindi cha kizazi cha kifalme cha Babeli (yapata mwaka 2000 KK) majina kama vile mwana wa siku ya ishirini (Mar-umi-esra) yalikutikana. Tunajua kwamba siku ya 20 ya mwezi ilikuwa ni siku ya sherehe ya mungu jua iliyoitwa Samas au Shamash ambayo ndiyo kwayo jina Shamus limetokea. Hii inaonekana kuhusiana na Mng’ao wa Ushindi wa jua (unaoonekana hasa baada ya kwisha kwa matukio ya kupatwa jua).

 

Matukio ya Maadhimisho Siku za Kuzaliwa Kwenye Biblia

Desturi hii ya kuadhimisho siku za kuzaliwa ilijipenyeza na kuingia katika Yuda kutoka kwenye maisha tandawazi yaliyoingiza desturi mchanganyiko wa Kiashuru na Kibabeloni na zilisherehekewa katika Misri ya Kale kwa kuandaliwa tafrija kubwa, kama tunavyoona jinsi alivyoadhimisha Mfalme Farao kwenye Mwanzo 40:20. Kwenye tukio hili muoka mikate wake aliuawa.

 

Tukio jingine ni lile la Yohana Mbatizaji alipouawa kwenye sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Herode (Mathayo 14:6).

Mathayo 14:6- Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode. 7 Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba. 8 Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. 9 Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe;

Jinsi walivyokuwa wanafanya kwenye utaratibu huu wa kale ilifungamanishwa na utaratibu au imani ya kutoa kafara za wanadamu, kwa utaratibu na imani yote na maadhimisho haya ya siku za kuzaliwa yalikuwa ni sehemu ya ibada na imani hiyo. Tutaliona hilo kwa kina kwenye jarida lenye kichwa cha habari: Siku za Kutoa Kafara za Wanadamu.

Msimamo wa Biblia kuhusu maadhimisho haya ya Siku za Kuzaliwa umetolewa wazi kabisa kwenye Kitabu cha Ayubu.

Ayubu 1:1-12 Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. 2 Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu. 3 Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki. 4 Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. 5 Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote. 6 Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. 7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. 8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. 9 Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? 10 Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. 11 Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. 12 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.

Hapa tunaona kuwa Ayubu alikuwa amebarikiwa, lakini watoto wake tunawaona kuwa walikuwa wamezifuata njia na desturi hizi za mchanganyiko wa Kishuru na Kibabeli walipoanza kuadhimisha nyakati au kusherehekea siku za kuzaliwa (soma nakala ya Companion Bible fn. to v. 4). Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho Waisraeli walikuwa Misri na Ayubu aliorodheshwa kuwa mwana wa Isakari (Mwanzo 46:13). Inaonekana kuwa tukio hili alisimuliwa Musa wakati alipokuwa huko Midiani na akaliandika kwa vili kuwaelimisha kizazi cha baadae cha Israeli, wakati walipokuwa wakiondoka toka utumwani kwenye kitabu cha Kutoka.

 

Ayubu alitoa sadaka ili kuwatakasa watoto wake wakati walipokuwa wakienda kuziadhisha sherehe hizi kwenye hizi siku zao, aliwaombea msamaha kama walikuwa wamefanya dhambi, lakini wakati Ayubu alipotolewa kwenye mikono ya Shetani, watoto hawa wote waliuawa kwa ajili ya dhambi zao. Maneno ya Ayubu kwenye Ayubu 3:3 yanaonekana kuthibitisha jambo hili. Mungu aliwatoa kwa Wana wa Mungu chini ya Shetani ili kuwaua na kummpepeta Ayubu kama ngano. Hawakuweza kutakaswa na Ayubu kutokana na maovu yao. Hivi ndivyo jinsi Mungu anavyolichukulia jambo hili kwa uzito mkubwa kuwa ni dhambi na uovu mkubwa. Somo la kujifunza hapa ni kwamba hii ni dhambi na uovu mkubwa na matokeo yake ni kifo kwa wateule na matokeo yake ni kujumuishwa kwenye ufufuo wa pili wa wafu amoja na watu wengine wote kwa hukumu (soma jarida la Ufufuko wa Wafu (Na. 143) [The Resurrection of the Dead (No. 143)].

 

Maadhimisho ya Siku za Kuzaliwa na Kafara za Wanadamu

Mitaabisho au jakamoyo linalojitokeza la kutolewa kwa kafara za wanadamu si vyema ikaachwa pasipo kuelezewa pia.

 

Herodotus anatuonyeshansisi kwamba maadhimisho haya ya Siku za Kuzaliwa yaliendana na mlo mahsusi na maalumu kwa Waajemi (Vitga vya I vya Waajemi 333 [Persian Wars I, 133]). Kuhusu habari za mfalme kulikuwa na tafrija ya kifalme iliyoadhimishwa kila mwaka ambayo iliandamana na utoaji zawadi zinazoendana na hadhi ya sherehe yenyewe (ix, 110).

 

Kipindi cha kabla ya Wahelleniki wa Kiyunani walisherehekea siku za kuzaliwa kwa miungu na za watu mashuhuri (kwa mujibu wa Kitabu cha fasihi kiitwacho The International Standard Bible Encyclopedia (ISBE), art. Birthday, Vol. 1, p. 515). Maneno ya \kiyunani ya genéthlia yalikusudia kuziita sherehe hizi kuwa ni genésia zilizowakilisha sherehe za siku ya kuzaliwa kwa mtu muhimu au mashuhuri ambaye sasa alikuwa anaugua magonjwa.

Kwenye kitabu cha 2Makabayo 6:7 panaitaja sherehe hii ya kila mwezi ijulikanayo kama genéthlia ya Antiochus IV, kipindi ambacho Wayahudi walilazimishwa kuila sadaka hii. Josephus (kwenye kitabu chake kiitwacho Vita Vya Wayahudi [Wars of the Jews, vii. 3. 1]) anaitaja sherehe aliyoifanya Tito aliyoifanya kwa ajili ya kuadhimisha siku za kuzaliwa kwa ndugu yake na baba yake (genéthlia) kwa kuwachinja wafungwa au mateka wa Kiyahudi.

 

Dodoso lililoandikwa kwenye Mathayo 14:6 na Marko 6:21 linaonyesha wazi kwamba neno genésia lilitumika kumtaja wadhifa wa mtu mashuhuri na wa muhimu. Tafsiri ya ISBE inashikilia kwamba Herode aliadhimisha siku ya kuzaliwa kwake sawasawa na masharti desturi za Kihelleniki; na kwa kweli hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kulikuwa na maadhimisho ya siku za kuzaliwa katika Israeli kwenye kipindi cha nyuma cha kabla ya hiki cha Wahelleniki (kwa mujibu wa tafsiri hii hii ya ISBE). Jina la Siku ambalo limeingizwa na ambalo imani ya Utatu imelichukua limetoka kwenye chanzo hikihiki.

 

Mfano wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Farao ulioandikwa kwenye Mwanzo 40:20 unachukuliwa kuwa ni ushahidi wa maadhimisho ya siku za kuzaliwa za Farao huko Misri katika zama za kabla ya kipindi cha Wahelleniki. Procksh anaamini na kusema kwamba maadhimisho ya kila mwaka ya kutawazwa kuwa mfalme kwa Farao, ambayo kwayo, yalikuwa ni kama yeye alikuwa amezaliwa na kuwa kama mungu mdogo huenda ikaw ndiyo maana iliyoko nyuma ya kole kilichoelezwa kwenye Mwanzo 40:20. Hii ingemaanisha kwamba siku ya kutawazwa kwake kuwa mfalme ilikuwa ni ya muhimu sana kwa kuwa ilifanyika kuwa ndiyo iliyoleta mabdiliko kwennye hadhi au daraja la kimaisha la mtu aliyefanyika kuwa ni Farao na aliyeinuliwa juu sana zaidi ya wengine wote. Katika kipindi cha Ptolemi siku za kuzaliwa kwa Farao ziliadhimishwa kwa kufanya tukio la kuwaachilia wafungwa (kinyume na lile tendo la kuwatoa kafara kama tulivyoona huko nyuma). Hii ilikuwa bado ina maana sawa tu na dhana iliyokuwa nyuma yake ya kwamba uweza juu ya uzima au maisha na kifo uko mikononi mwa mungu ambaye anaweza kuamua kufana lolote sawasawa na jinsi anavyopenda iwe. Josephus anaitaja sherehe au maadhimisho haya (genésia) pale anapoelezea kuzaliwa kwa mtoto wa kiume wa Ptolemy (A of J, xii, 4, 7-9).

 

Hitimisho

Sherehe hizi za Siku za Kuzaliwa zina mafungamano na imani zilizo na mchanganyiko wa Waashuru na Wababeloni ambazo ziliingia kwa Wayunani na Warumi kwa kupitia kwa Wahelleniki wa Kiajemi. Hii ni siku maalumu iliyokusudiwa hasa kumfanya mwanadamu au mhusika kutukuzwa kama mungu na ni sehemu ya imani za kale zilizotumika kwenye dini za siri za Shetani na waridhi waliokuwa wanaziamini dini za Kibabeli. Zilikuwa zinahitimishwa kwa kitendo cha kutoa sadaka au kafara za wanadamu na kuwatoa uhai wao. Hazitokani na maagizo ya kwenye Biblia na zinapingana na maagizo na uweza au mamlaka ya Mungu.

 

Mungu alitupa sisi utaratimu kupitia kwenye Kalenda yake ambayo kwayo tunapat siku zake takatifu kwa kufuata utaratibu na mchakato huo (tazama jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156) [God’s Calendar (No. 156)].

 

Tutaendelea kwenye awamu inayofuatia ya uandishi ambapo tutashughulikia kuielezea kalenda ya shetani kwa ujumla na Siku za Kutoa Kafara  za Wanadamu, ambazo kwazo ndizo maana hasa ya siku hizi takatifu na utaratibu wake mzima unavyomaanisha.

 

q