Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[290]

 

 

 

 

Miaka Arobaini ya Toba

 

(Toleo La 1.0 20060610-20060610)

 

Katika kipindi cha hadi mwaka 1972 na tena mwaka 1975, Makanisa ya Mungu, hususan kanisa lililojulikana kama Kanisa la Mungu Ulimwenguni Kote, maarufu kwa Kiingereza kama “Worldwide Church of God” na Mashahidi wa Yehiva (Jehovah’s Witnesses), walitangaza kwamba Kristo atarudi katika kipindi cha vita hivi vya mwisho vilivyopiganwa miaka hii ya 1972-1975. Lakini matokeo yake ni kwamba hakuna kilichotokea mwaka huu wa 1975 na Masihi hakuja. Walitabiri kwa makosa. Je, maana ya kipindi hiki yalikuwa ni nini basi?

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

 

(Haki Miliki © 2006 Wade Cox)

(tr. 2912)

 

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Miaka Arobaini ya Toba

 


Herbert Armstrong na huduma yake, pamoja na wale wanaojiita manabii wa Mnara wa Ulinzi (the Watchtower) na idara yao inayoitwa ya Machapisho ya Vipeperushi na Biblia Kwenye Jamii (Bible Tract Society) au kwa jina lingine maarufu wanajulikana kama Mashahidi wa Yehova, watangaza kwamba Masihi atakuja kwenye kipindi cha miaka ya 1972-1975.

 

Ukweli wa kwamba Mashahidi Wawili hawajaanza kazi yao huko Yerusalemu hauwavunji moyo kwa kile walichojitangaza kuwa wao ni mashahidi walioahidiwa na kutabiriwa kwenye Ufunuo 11:3-13 (tazama jarida la Mashahidi (wakiwemo Mashahidi hawa Wawili) Na. 135 [The Witnesses (including the Two Witnesses) (No. 135)].

 

Hawakikuweza hata mara moja kufanana na manabii hao wa Mungu lakini hawakukata tamaa hata mmoja wao.

 

Kile walichofanya kwa kweli ni kutangaza vipindi vyao vya toba. Kipindi cha miaka arobaini, miezi, majuma, au siku ni vipindi vinavyojulikana kuwa ni vilivyoruhusiwa na Mungu kwa kila mtu, makundi, au mataifa kujichunguza mambo yao na kutubu ka kufikia mahala pa kuelewa na kujifananisha ma Amri za Mungu na Mpango wake wa Wokovu wa kila mtu au kikundi cha watu husika.

 

Nabii zilizotolewa na imani waliyokuwa nayo kina Armstrong, na Mashahidi wa Yehova na Waadventisata iliyotokana na hisia za mitazamo yao, ziliwapeleka kwenye makosa makubwa sana. Na kuonekana waongo (soma jarida la Unabii wa Uwongo (Na. 269) [False Prophecy (No. 269)].

 

Imani zote hizi mbili zimepotoka kuona mambo muhimu na ya msingi yatumakayo katika kuitafsiri Biblia. Huduma ya Mashahidi wa Yehova haikuwa inajua Kalenda itokanayo na Biblia, kwa kuwa hawaishiki Amri ya Nne au kuufuata mfumo wowote wa kalenda ya kibiblia na wakafundisha watu wao kwamba Mungu amezikomesha na hazina umuhimu tena Amri zake hizi. Wasabato tu ndio walioitunza Sabato na hatimaye wakajiunga kwenye imani ya Utatu ma kuwa miongoni mwao, wakiachana na uelewa sahihi waliokuwanao hapo kwanza.

 

Armstrong, ambaye alilelewa kiroho na kufundishwa kwenye Kanisa liiitwalo leo kama Kanisa la Mungu la Siku ya Saba [Church of God (Seventh Day)], na wakaiingiza Kalenda ya Hilleli kwenye Kanisa la Mungu na wakashindwa kuuelewa mfumo wa kuzipata yubile. Kwa hiyo, huduma zitokanazo mifumo hii yote miwili ilishindwa kuelewa mlolongo wa unabii kwa jinsi ulivyofunuliwa katika Mpango wa Mungu.

 

Kwa ajili hii hii, Makanisa mengine ya Mungu pia yameshindwa kuurudisha mfumo muhimu wa Kalenda na kuwafanya washindwe kuligawa neno la kweli na kupambanua kati ya ukweli na mambo bandia na ya uwongo.

 

Mengi ya yale waliyoyafanya yalitokana na makosa ya na upotofu wa kuyatafsiri maandiko na hasa walipotoshwa kwa kuuiga mfumo wa Kiprotestanti wa kuutafsiri unabii wa Danieli 9:25 kwa kumhusisha Masihi wakati ambapo kuna masihi wawili au “mtiwa mafuta” anayetajwa, na wala Masihi huyu hakuwa Yesu kristo (soma jarida la Ishara ya Nabii Yona na Historia ya Kujengwa Upya kwa Hekalu (na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)].

 

Walifuata mambo muhimu yaliyorahisi ya Biblia kwamba Mungu aliruhusu na kuzitenga siku sita za Uumbaji na kwamba siku ya saba ilikuwa ni Sabato ya Yesu Kristo ya Kustarehe, na kulichukulia jambo hilo kwenye hitimisho lenye mashiko lililoendelewa na Mtume Petro kwamba kwa Bwana, siku moja ni sawa na miaka elfu, jambo ambalo walipaswa wajue kwamba kipindi cha utawala wa milenia wa Yesu Kristo kitatokea na kuwa mwishoni mwa miaka elfu sita ya utawala wa Shetani. Na itabidi kipindi kifupishwe, kwa ajili ya kuwaokoa wateule, kwa kuwa kama hakitafupishwa, hataokoka ye yote mwenye mwili miongoni mwa walio hai (Mathayo 24:22).

 

Kipindi ambacho utawala wa Shetani utakomeshwa kilibidi kijulikane sawasaawa kama wangefuata kanuni fulani za msingi. Hatahivyo, hawakufanya hivyo kwa kuwa walitaka kuyatumbukiza Makanisa ya Mungu kwenye “mchemko” ili waongee, na kudhibiti hatamu ya mambo ambayo hayana budi kushindikana. Matokeo yake ni kwamba Kanisa likaangukia kwenye mtego wa kuamini na yakasema kwamba Bwana amekawia kurudi, jambo ambalo halikuwa sahihi.

 

Kile kilichokuwa kinatokea ni kwamba Roho Mtakatifu alikuwa anawapeleka watu hawa kwenye kiwango ambacho wangefikia utimilifu na kufikia kwenye kujaribiwa kwa imani yao jambo ambalo lingewapeleka hukumuni, ambako wangejumuishwa au kutojumuishwa na Ufufuo wa Kwanza wa Wafu wakati atakaporudi Masihi.

 

Kila mtu aliyekuwa na mahusiano na mawasiliano na Makanisa ya Mungu kwa kipindi hiki alikuwa anapewa ushuhuda wa kurudi kwake lakini sivyo walivyofundishwa mwanzo kuwa itakuwa hivyo.

 

Kwa mujibu wa mlolongo wa vipindi ulivyoelezewa kwenye Biblia tunajua kwamba kipindi hiki kilianza mwaka wa 4004KK na ndipo alipoumbwa Adamu. Kazi aliyoifanya Askofu Usher ya kupangilia mlolongo huu, ilikuja kujulikana kuwa uumbaji ulifanyika mwaka 4004KK na ndio unaoonekana kwa kufuata inavyosema Biblia ya tafsiri ya Mfalme Yakobo (King James Bible).

 

Tunaona pia kwamba Adamu alihukumiwa na kufukuzwa kwenye Bustani ya Edeni. Shetani pia aliwekwa kwenye fungu hili la wanadamu la kufukuzwa. Kwa hiyo, Adamu aliumbwa akiwa ni mwanaume mtu mzima mwenye umri wa miaka ishirini, lakini kwa mujibu wa Amri za Mungu au Torati, mwanaume haruhusiwi kufundisha na hahesabiwi kuwa anastahili kupewa uongozi na kuliongoza kundi hadi afikie umri wa miaka thelathini. Kwa hiyo, yubele ya kwanza ya utawala wa Shetani ulianzia mnamo mwaka 3974KK. Yubile moja ambayo inachukua kipindi cha miaka hamsini inatimiliza mwisho wa kipindi cha yubile 120 ambayo si sawa na kipindi cha miaka elfu sita ifikapo mwaka 2027 wa miaka tuliyonayo ya kidunia. Zama au kipindi cha utimilifu wa mataifa, au kipindi cha wapagani kilichopimwa kutoka kuumbwa kwa Adamu kimeishia mwaka 1997. Kimeishia mwaka ule kwa mujibu wa hesabu za kinabii pia dhidi ya idadi ya vipimo vya kibiblia kama tunavyoona kutoka kwenye jarida la Kuanguka Kwa Misri: Unabii Juu ya Mkono Uliovunjika wa Farao (Na. 36) [The Fall of Egypt: The Prophecy of Pharaoh’s Broken Arms (No. 36)]. Tangu happ, kipindi cha Maombolezo ya Musa kinaanza na mchakato wa marejesho ya Israeli chini ya Yesu Kristo yalianza pia.

 

Kipindi cha miaka thelathini ya Maombolezo ya Musa kimeelezewa kwenye jarida la Miaka Thelathini ya Mwisho: Pambano la Mwisho (Na. 219) [The Last Thirty Years: The Final Struggle (No. 219)].

 

Kwenye jarida lile tumeelezea mhakato wa Vita Vya Siku za Mwisho. Matukio hayo yamekuwa yakiyafunua kama tulivyoyaelezea kwenye utunzi wetu. Yataendelea hadi kupelekea matukio ya mwisho yatakatopelekea Vita ya III ya Dunia kama ilivyoelezewa kwenye jarida la Vita Vya Hamon-Gogu (Na. 294) [War of Hamon-Gog (No. 294)].

 

Mwaka 1975 ulikuwa ni mwaka wa sitini ambao pia ni mwaka wa mavuno mara tatu wa mzunguko wa mwisho wa Sabato ya yulibe za kwanza. Mwaka 1976 ulikuwa ni mwaka wa Sabato na mwaka 1977 ulikuwa ni mwaka wa yubile ya 119. Na ndipo dhana na mafundisho ya kuwa atarudi hivi karibuni ilihalalishwa kwenye Kanisa la Mungu, lakini sio kama watu hawa walivyodhania. 

 

Tunajua kwamba kipindi cha Siku za Mwisho kimeonekana kuwa ni kipindi cha miaka saba kinachojulikana pia kama ni kipindi cha kuanguka kwa mataifa kilikuwa ni mfano wa vile Yesu Kristo alivyomtokea Yoshua kule Yeriko, alipomtokea ikiwa kama Amiri wa Jeshi la (tazama jarida la Kuanguka Kwa Yeriko (Na. 142) [The Fall of Jericho (No. 142)].

 

Tangu Kristo alipowatokea na kulikuwa na siku saba ambazo Majeshi ya Israeli, na ambayo ni Majeshi ya Bwana, yaliuzunguka mji wa Yeriko na ukuta ukaanguka chini na ndipo wateule wachache tu ndio waliokoka. Wateule hawa mfano wao ulikuwa ni mwanamke kahaba Rahabu ambaye aliokolewa kwa kutumia kuifunga kamba nyekundu ambayo ni mfano wa Pasaka, kamba aliyoifunga kwenye dirisha la ukuta wa na agano alilolifanya watumishi waliomwakilisha Mungu.

 

Kwa hiyo, kama tukianza kuhesabu miaka saba tangu mwaka 2027 tutapata mwaka 2019 lakini huu ni mwaka wa Sabato na miaka ya 2026 na 2027 ni miaka ya Sabato pia yote miwili. Torati inapaswa isomwe kwenye miaka hiyo. Kwa hiyo, Kristo anapaswa kurudi na wateule watapaswa wawe wameisha fufuka kipindi cha kabla au baada ya Mwandamo wa Mwezi wa Abibu wa mwaka 2019 ili kuhitimisha mzunguko kamili wa miaka saba unaolingana kimfano na ule wa siku.

 

Hata hivyo, tunajua kutokana na kitabu cha Ufunuo sura ya 11 kwamba Mashahidi wanapaswa wawe wameishaanza huduma yao kwa kipindi cha siku 1263.5 kabla Masihi hajawa hapa, kwa kipindi cha mwanzoni kabisa.

 

Kwa hiyo tunafika kwenye mwaka wa 2015 kwenye kipindi cha mwanzoni sana. Tunajua pia kwamba Yuda wataongoka na kurejea kwa Mungu kipindi hiki na kwa hiyo kuna masharti na mambo muhimu mengi au vipindi husima vingi vilivyoonekana mwanzoni vinavyowezesha hilo.

 

Chini ya Amri ya Mungu, ameamuru kwamba Torati inapaswa isomwe kwenye mwaka wa Sabato unaoangukia mwaka wa 2012 ikiwa ni mwaka unaofuatia wa Sabato wa Kusoma Torati. Kitakachofuatiwa ni kwamba kipindi cha usomaji wa Torati cha mwaka wa 2012 ni cha tatu na cha mwisho cha kabla ya kipindi cha kuanza huduma ya Mashahidi katika mataifa. Torati itasomwa mara tatu ili kufanya kwamba awamu ya tatu ya watu kuikataa kweli na uasi hatimaye iwe kwenye torati. Tunawatarajia Mashahidi hawa waanze kazi zao baada ya mwaka huu wa usomaji wa torati cha mwaka wa 2012, au inawezekana kabisa kwamba wataweza kushirki usomaji huu wao wenyewe au watahusika kwa namna ya kuwahubiria mataifa kwenye kipindi kile itakapokuwa inasomwa.

 

Kwa namna yeyote ile, wataanza kufanya kazi zao kati ya miaka ya 2012 na 2015 ili kuwezesha mchakato wa kuyatiisha mataifa kwa Masihi ikifuatia muda wake muafaka uliotabiriwa kwenye Biblia kwa mwaka na siku zinazotuama kwenye kipindi kinachofuatia mlolongo uliotolewa na unabii.

 

Mwaka wa 2015 ni kipindi muafaka cha mwisho wa utawala wa makanisa na cha vinara vya taa na wakiwa chini ya malaika saba wa makanisa saba. Tangia hapo kwenye vinara viwili vya taa vya Mashahidi na Taa ya mwisho cha Masihi wanawajibika katika kuitia nuru sayari hii.

 

Kwa hiyo, tunakabiliwa na ukweli kwamba mwaka wa 1972 ni wa arobaini kamili tangu mwaka wa 2012, na mwaka 1975 ni wa arobaini kamili tangu mwaka 2015.

 

Je, tunajionea kitu gani na maana yake nini kuhusiana na ukweli huo? Tunajua kwa kweli kwamba taifa la Israeli lilipelekwa jangwani kwa kipindi cha miaka arobaini wakiwa na Masihi. Na Kanisa limekuwa jangwani kwa kipindi cha takriban miaka elfu mbili wakiwa na Masihi tangu mwaka 30BK kwa dhabihu ya Masihi na likiwa limempokea Roho Mtakatifu. Yuhana Mbatizaji alianza huduma yake mwaka 27BK na Masihi mwenyewe alibatizwa mwaka na kuutangaza mwaka uliokubaliwa wa Bwana mnamo mwaka 27BK, ambao pia ulikuwa ni wa Yubile.

 

Kwa hiyo, mwaka 27BK ulikuwa ni mwaka wa yubile wa yubile ya arobaini au ni wa miaka 2000 inayoishia mwaka 2027.

 

Kwa hiyo basi, kwenye yubile moja ya mwelekeo wa mwaka, Kanisa lilikuwa jangwani kwa kipindi cha yubile arobaini kama Israeli walivyokuwa jangwani kwa kipindi cha miaka arobaini.

 

Mwisha wa kipindi hiki ni kwenye yubile ya 120. tangia mwaka wa 1975, Kanisa lilipaswa kujiandaa kwa yubile na kusoma tarati mnamo mwaka 1976 na 1977 na kisha kuendelea mbele kwa mchakato unaoelezewa kwenye Biblia. Hawakufanya hivyo na wakaingia hukumuni. Kwa sababu yoyote ile, torati ni lazima isomwe kwa kipindi angalau cha nyakati tatu kwenye miaka mitatu ya Sabato kabla ya kurudi kwa Masihi.

 

Kanisa la Siku za Mwisho limejikuta pia likielekea kwenye kipindi cha Miaka Arobaini ya Kuwa jangwani tangu mwaka 1975. Kipindi cha siku 1260 kati ya miaka ya 2012 na 2015 kinaashiria kipindi kikuu na kilicholikuza Kanisa cha kati ya miaka ya 1972 na 1975 kwa unabii wao wa uwongowa dhiki na ujio wa mangojeo. 

 

Kipindi cha Kupimwa Kwa Hekalu ni zama nyingine ya miaka arobaini kilichoanzia mwaka wa 1987. Kipindi hiki cha miaka hii arobaini kinatupeleka kwenye Milenia na kinahusika na mchakato mzima wa kurejesha na kufanya upya kama inavyosimama kwenye Hekalu la Mungu. Mchakato huu umeelezewa kwa kina kwenye jarida la Kulipima Hekalu (Na. 137) [Measuring the Temple (No. 137)].

 

Kwenye kipindi hiki tunajionea pia hatima ya kipindi cha miaka ishirini na moja kilichokuwa kwenye mwaka wa 2006 kuanzia siku ya 1 Abibu ya mwaka wa 29 wa yubile ya 120 ukiwa kama ni mwaka wa kwanza wa Mzunguko wa Miaka ya Sabato. Kipindi hiki ni kile cha Kutakaswa Kwa Mataifa (Na. 77) [Sanctification of the Nations (No. 77)].

 

Mchakato ule unamaana ashirio ya siku 21 za mlolongo unaofuatia tukio la Pasaka. Inaenda tangu Mwaka Mpya, na ambao unaanzia kuanzia tukio la Utakaso wa Hekalu la Mungu (Na. 241), [Sanctification of the Temple of God (No. 241)], hadi kwenye Siku Takatifu ya Mwisho ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kinalenga kwenye mwaka wa 2012 kwa Usomaji wa Torati ambao ni sawa na siku ya 7 Abibu na kwenye andhimisho la Utakaso Kwa Ajili ya Dhambi Zilizofanywa Pasipo Kukusudia na Kwa Kukoseshwa (Na. 291) [Sanctification of the Simple and the Erroneous (No. 291)].

 

Mwaka wa 2015, siku iliyosawa na ya 10 ya mwezi Abibu na ndiyo aliyoingia kwa shangwe Masihi mjini Yerusalemu. Na mwaka wa 2019 siku iliyosawa na ya 14 Abibu kwenye mlolongo huu. Tendo la kusalimu amri na kujinyenyekesha kwa mataifa kunaashiria manano wa Kuanguka kwa nji wa Yeriko kulukoashiria pia kipindi cha siku saba za Idi au Sikukuu kilichoishia mwaka 2026 kwenye mwaka wa Sabato na kutangazwa kwa mwaka wa Jubile kwenye Siku ya Upatanisho ya mwaka wa 2026 na iliyoishia kwenye Siku ya Uptanisho ya mwaka 2027.

 

Kwa hiyo, kuna mlolongo wa mafuatano ya matukio uliofanyika ili kutokea kwa madhumuni tofauti, na mbalimbali ya mpango wa Mungu kwenye kipindi cha mwisho au cha yubile ya 120 kabla ya utawala wa milenia wa Masihi.

 

Badala ya Masihi kuja mwaka wa 1975, au mashahidi kuanza kazi yao mwaka 1972, au muunganiko wowote wa matukio hayo, makanisa yamekuwa yakionywa na kuandaliwa yawe tayari kwa ujio wa Masihi na yameambiwa yatubie dhambi zake na kujisafisha na kuwa tayari kama mabibi arusi wa Kristo. Jambo ambalo hawakulifanya wakiwa kama mwili wake na kuwa ni yeye peke yake tu ndiyo aliyeshinda na asiangukie kwenye mfumo wa Wafiladelfia ambao umeanguka na kuangamizwa. Masalio ya mwisho ya imani ya Wasardi yaliundwa, kwa kujiita wao wenyewe kuwa ni Kanisa La Mungu Lililohai (Living Church of God) kama inavyoonyeshwa kwenye kitabu cha Ufunuo 3:1. Likajumuisha makosa yote na upotofu wa Wasardi na kwa jinsi lilivyoanzishwa kwa dhumuni la kuifanya kazi ya Wasardi.

 

Mfumo na imani ya Mashahidi wa Yehoha ulikataliwa kabisa wote kwenye kanisa na hauhesabiwi kwenye kanisa na umekosa unabii wa kweli kabisa tangia lilipojiengua na kutoka kwenye Makanisa ya Mungu kwenye karne ya 19. Kwa hiyo, halikujitenga kwa dhumuni la kuifanya kazi katika Siku hizi za Mwisho. Ndipo lilikataliwa kwa ujumla wote, na kama ilivyotokea kwenye mfumo na imani ya Kanisa la Waadventista, ambalo Wanazuoni wa Biblia walilitenga, kwa vile lilivyotangaza kwa wazi sana kwamba wamejiunga na kuamini rasmi imani ya Utatu au Utrinitaria tangia mwaka 1978 ambao pia ni mwaka wa mwanzo wa yubile hii. Ni mtu mmoja mmoja tu binafsi yao ndio wanadiriki kupinga na kutoamini imani hii miongoni mwao.

 

Kwahiyo, mfumo na imani hii ya Wasardi kwa Makanisa ya Mungu ulitumika ili kuanzisha kazi endelevu ya kiimani ya Siku hizi za Mwisho, nyingine ya pili iliyouanzisha mfumo na utaratibu wa Walaodikia na machipuki yake yaliyokataliwa kabisa walipokataa kwendanao na msingi wa mafundisho yao kuhusu mambo muhimu yanayohusiana nao, na wala hawakugeuka na kusikiliza neno la Mungu ili waweze kutumiwa. Na ndipo imani hii ilikubaliwa kikanisa. Ni watu binafsi tu kutoka kwenye imani hizi za Wasardi na Walaodikia ndio waliojinasua na kwenda kwenye imani na mfumo wa Wafiladelfia. Kwa hiyo, ahadi imewekwa kwao ya kwamba hawatatoka humo kabisa.

 

Ujumbe kutoka kwenye ufunuo sura ya 3 ni wa muhimu sana katika kujua kile kinachotokea. Mlolongo na matukio yaliyo kutoka kanisa la Sardi hadi la Filadelfia yaliyoonyeshwa kwenye Ufunuo sio matukio ya zama yaliyofanyizwa bali ni ujumbe uliotoka sehemu moja hadi nyingine. Kiini cha imani na mfumo wa Wafiladelfia ulichukuliwa kutoka kwa Wasardi na kama walivyokuwa Wafiladelfia wenyewe kwa kipindi fulani.

 

Mfumo wa utajiri mkubwa wa Walaodikia, ukwasi wa kumiliki mali za dunia hii, hauna nguvu za kiroho na ni dhaifu, umasikini, unyonge, upofu na uchi.

 

Ufunuo 3:1-22 inasema: ‘‘Kwa malaika wa Kanisa lililoko Sardi andika: Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa. 2Amka! Nawe uyaimarishe yale yaliyo karibu kufa, kwa maana sikuona kwamba kazi zako zimekamilika machoni pa Mungu wangu. 3Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na ukatubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwivi wala hutajua saa nitakayokuja kwako. 4Lakini bado una watu wachache katika Sardi ambao hawajayachafua mavazi yao. Wao wataenda pamoja nami, wakiwa wamevaa mavazi meupe, kwa maana wanastahili. 5Yeye ashindaye atavikwa vazi jeupe kama wao, nami sitafuta jina lake kutoka katika kitabu cha uzima, bali nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele za malaika Wake. 6Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. 7‘‘Kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika : Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye mtakatifu na wa kweli, Yeye aliye na ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, wala anachokifunga hakuna awezaye kukifungua. 8Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango uliofunguliwa, wala hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba una nguvu kidogo lakini umelishika neno Langu wala hukulikana Jina langu. 9Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni waongo, waje wapige magoti miguuni pako, nao watajua ya kwamba nimekupenda. 10Kwa kuwa umelishika neno la saburi Yangu nitakulinda hata utoke katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni pote ili kuwajaribu wote wakaao duniani. 11Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akaichukua taji yako. 12Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo kamwe. Nitaandika juu yake Jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani, Yerusalemu mpya, ambao unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Nami pia nitaandika juu yake Jina langu jipya. 13Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. 14‘‘Kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika : Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye Amen, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa uumbaji wote wa Mungu. 15Nayajua matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa baridi au moto. 16 Hivyo kwa kuwa u uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani Mwangu. 17Kwa maana unasema, ‘Mimi ni tajiri, nimefanikiwa, wala sihitaji kitu cho chote.’ Hujui ya kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, masikini, kipofu, tena uliye uchi. 18Kwa hiyo nakushauri ununue kutoka Kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri na mavazi meupe ili uyavae, upate kuficha aibu ya uchi wako na mafuta ya kupaka macho yako ili upate kuona . 19Wale niwapendao, ninawakemea na kuwaadibisha. Hivyo uwe na bidii ukatubu. 20Tazama, nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu ye yote akisikia sauti Yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye,naye pamoja nami. 21Yeye ashindaye nitampa haki ya kuketi pamoja Nami kwenye kiti Changu cha enzi, kama vile Mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba Yangu kwenye kiti Chake cha enzi. 22Yeya aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.’’

 

Maelezo kamili yatakayokufanya uyaelewe maandiko haya yameandikwa kwenye jarida la Nguzo za Filadelfia (Na. 283) [Pillars of Philadelphia (No.283)].

 

Imani hizi zina miaka arobaini, na kila mtu amepewa kuda wa kipindi cha wakati, nyakati mbili na nusu wakati kilichotolewa kwa ajili ya kufanya toba ya mwisho na dhati ili kujiandaa kwa ajili ya ujio wa Masihi.

 

Vipindi hivi vinaishia katika miaka ya 2012 na 2015 kwa ukamilifu na utimilifu wake mkubwa. Watu kutoka kwao wataitwa na kutolewa ili wafanye toba na kuingizwa kwenye mwili wa Kristo ifikapo mwaka 2015, na tangu Ufufuo wa Kwanza wa Wafu, watakapokuwa kama viumbe walio kimwili au ulimwengu war oho. Uchaguzi utakuwa ni wao wenyewe kwa ajili ya upotofu wao walioufanya na kuutumikia na kuuchagua.

 

Tangia mwaka 2015 hadi 2018 uongofu wa Yuda utakamilika na tangia wakati huu hakuna mtu atakayeingia kwenye ufufuo huu wa Kwanza. Itakuwa ni jambo watakuwa wamechelewa sana kufanya hivyo.

 

Yangia mwaka wa 2019 mataifa wataletwa waje Megido na watafanyika kuwa wanyenyekevu kwa Masihi.

 

Mnamo mwaka  2025 ulimwengu wote utakuwa kwenye mchakato wa kufikia kwenye hali ya kujisalimisha na kujinyenyekesha kwa Kristo, jambo litakalofanyika kwa kukabidhi himaya yao yote na kila walichonacho kinachotakiwa kifanyike ili kufanikisha maandalizi ya utawala wa milenia.

 

Mwaka 2026 ndio utakuwa wa Sabato ya mwisho.

 

Mwaka 2027 utakuwa ndio wa kutangazwa kwa utaratibu mpya wa utawala wakati itakapopulizwa mbiu ya yubile na utakuwa ni mwanza wa matayarisho ya mavuno ya Upatanisho.

 

Mwaka wa 2028 kipindi cha zama mpya ya utawala wa Mileni kitaanza rasmi kuanzia siku ya Mwandamo wa Mwezi wa Abibu, ambapo ni Mwaka Mpya.

 

Tangu kipindi hiki hakutakuwa na mavunr wala mvua haitanyesha kwa majira yake sahihi kwa wale ambao hawataitunza na kuitii Totari  na Amri za Mungu na kutuma wawakilishi wao mjini Yerusalemu ili kwenda kuishika Sikukuu ya Vibanda (Zekaria 14:16-21).

 

Ni jambo linaloshangaza sana kuona kwamba mifumo na imani za kidini za dunia hii hazinahabari na kipindi kilichowekwa na ambacho ndicho wanachokingojea na wala hawachukui hatua yoyote ya kuelezea na kuzirehesha na kuzipa mashiko Amri za Mungu na Kalenda Takatifu (soma jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 150) [God’s Calendar (No. 156)].

 

Kila mtu aliyeko hapa duniani atapewa fursa ya kutubu na kuwa na sehemu kwenye Ufalme wa Mungu. Lakini sio watu wengi watakaojumuishwa kwenye ufufuo wa Kwanza katika Siku za Mwisho.

 

Wengi watashindwa kwa kushindwa kwao kuyatubia tamaduni zao potofu na mapokeo yao. Waislamu wanaizishika na kuziamini Hadithi za kidini yao watashindwa kabisa wasipotubu na kubatizwa. Na kama Korani inavytosema kwamba ikiwa mtu haishiki Sabato ya Bwana basi wewe ni nyani (tazama jarida la Sabato Ndani ya Korani (Na. 274), [Sabbath in the Qur’an (No. 274)]; Kristo Ndani ya Korani (Na. 163) [Christ in the Koran (No. 163)]; Korani Ndani ya Biblia, Torati na Agano (Na. 83) [The Koran on the Bible, the Law and the Covenant (No. 83)] na Kalenda ya Kiebrania na Kalenda ya Kiislamu Zinavyoafikiana (Na. 53) [Hebrew and Islamic Calendar Reconciled (No. 53)].

 

Mifumo yote mitatu ya kiimani, yaani Waislamu, Wayahudi na Wakristo vitakuwa ni vitu vilivyopita tu na havitakuwepo tena. Vitasahaulika kabisa na havitakumbukwa tena, pamoja na watu waliokuwa wanafundisha imani hizi na watu wao mashuhuri walio kwenye dini hizo, wote hawatakumbukwa. Watu wao wote watakuwa kwenye kundi la watakaofufuliwa kwenye Ufufuo wa Pili utakaofanyika mwishoni mwa kipindi cha milenia.

 

Umashuhuri watakaotuachia sisi utachukua miaka kurekebisha na dunia itailazimu kipindi cha miongo kadhaa kusawazisha na kuponya. Itachukua kiindi cha takriban miaka hamsini tangu mwaka 2028 hadi kufikia Yubile ya Dhahabu ya Matengenezo Mapya ya mwaka 2077 kabla haijaponywa kikamilifu. Yubile hii itakuwa ni ya hamsini tangia Matengenezo na marejesho yaliyofanywa na kina Ezra na Nehemia. Ni “Yubile ya Yubile” na dunia itakuwa imeponywa na kuwa na amani kwa kipindi cha miaka elfu kadhaa.

 

Kipindi kitakachofuata baada ya kurudi kwake Masihi, tunaambiwa kwamba nchi itashehenezwa na mio wa maji utakaotokea kwenye mlima wa Mungu, ambapo ni mahali Patakatifu kutoka upande wa mashariki na bahari za magharibi. Tulichoweza kuambiwa tu ni kwamba kuna ziwa linalopita chini kwa chini lenye mlingano mkubwa wa takriban maeneo manane mapya ambazo hazikujulikana hapo kabla na wanasayansi. Hii inanenyesha kuwa ni chanzo au chimbuko la mito ya maji ya manabii.

 

Watu ambao ni wafuasi wa Kanisa la Mungu ambao hawajatubu watakuwa na mengi ya kuyapoteza. Ni huzuni kubwa kukosa kuingia kwenye utawala huu wa Milenia na kutawala pamoja na Yesu Kristo akiwa ni mwanadamu mwenye damu na nyama ambapo ungeingia humo na kuwa miongoni mwa wafalme wadogo, na ukiwa ni mtuto wa kiroho wa Mungu (soma jarida la Wateule Kama Elohim (Na. 001) [The Elect as Elohim (No. 001)].

 

Kwa kweli ni maafa makuu yanakuja kuona kwamba watu waliojitahidi sana na kujikuta wanashindwa kwa ajili ya upotofu waliokuwa wanauamini na ulegevu.

 

Watu hawa watakumbuka mfano uliotolewa kwenye mafundisho ya wanawali wenye busara na wajinga na junsi walivyoomboleza.

 

Je, wewe sio mmoja wao! Basi na usiizike talanta yako.

q