Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[291]
Utakaso Kwa ajili ya Dhambi
Zitokanazo na Ujinga na Kukoseshwa [291]
(Toleo 2.0
20000410-20000429)
Katika siku ya 7 ya Miezi wa Abibu tunafunga kwa ajili ya toba kwa dhambi tulizozifanya zilizosababishwa na au kufanywa kwa kutokujua na kwa kupotoshwa. Mlolongo huu unahusu hasahasa wale ambao bado hawajafikia kima cha kuuelewa utukufu na siri za Ufalme wa Mungu. Ni sahemu ya utaratibu wa utakaso wa mfumo wa Hekalu ulioamriwa na Mungu.
Christian Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Copyright ã 2000 Wade Cox)
(Tr. 2005)
Masomo
haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami
yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa
mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi
zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha
lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti
yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Utakaso Kwa ajili ya Dhambi
Zitokanazo na Ujinga na Kukoseshwa
Tunaiadhimisha siku ya 7 ya mwezi wa Abibu, kama siku ya Utakaso kwa ajili kutubu dhambi tulizozifanya zilizosababishwa na hali ya kutojua kama tunalolifanya lina mchukiza Mungu yaani ujinga wa kiroho na kwa njia ya makosa yaliyosababishwa na kukoseshwa na watu wengine (Ezekieli 45:20). Katika siku hii tunapaswa kufuna na kuomba. Je, ni kwa nini tunafanya hivi? Kwa nini tunafunga? Je dhabihu ya Kristo haikutosha kututakasa kwa wakati wote? Je, tunajaribu kufanya kitu ambacho kilisha fanywa na Kristo na kujichukulia mkononi mamlaka haya?
Ezekieli 45:20 inasema: 20 Nawe utafanya vivyo hivyo katika mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, kwa ajili ya kila mtu akosaye, na kwa ajili ya mtu aliye mjinga, ndivyo mtakavyoifanyia nyumba upatanisho.
Jibu lake ni rahisi na dhahiri tu kuwa tunafanya hivyo kwa sababu ni sehemu ya utaratibu wa Utakaso wa mfumo wa Hekalu kama ulivyo amriwa na Mungu ambayo kwayo Kristo aliichukulia kutaka ifanyike, wakati tunapojiandaa kwa ajili ya Pasaka. Aliichukulia utakaso huu na Utakaso wa Hekalu. Hii ilikuwa inaonyesha mfano wa kimwili kwa kufuata ukweli kwamba aliwafukuza wabadilisha fedha kutoka Hekaluni. Utaratibu huu ulipelekea kutengwa mahali kwa mwana kondoo katika siku ya kumi ya mwezi wa Abibu, tayari kwa kuchinjwa kwake katika siku ya Kumi na nne ya mwezi wa Abibu na kuliwa kwake katika Usiku Maalumu wa Kuukumbuka sana katika Siku ya Kumi na tano ya mwezi huu wa Abibu.
Je, si vema sana na busara tukiachana kabisa kuadhimisha Sabato kwa sababu Kristo aliisha itunza, au kushiriki Ushirika wa Meza ya Bwana kwa sababu yeye aliisha itimiliza, au kuadhimisha siku ya Mganda wa Kutikiswa kwa vile yeye mwenyewe alikuwa ndio huu Mganda wa Kutikiswa? Je, si vema sana kama tutaacha kuadhimishwa siku za Mikate isiyotiwa Chachu kwa kuwa yeye mwenyewe alikuwa hana dhambi na aliondoa kabisa chachu yote ya maovu na udhaifu? Jibu kwa maswali haya ni kwamba; sisi bado tuna adhimisha Pasaka ilikuwa ni kanuni iliyowekwa kwenye sheria za Mungu ili ziadhimishwe milele na ni ishara ya ushiriki wetu kwenye taratibu hizi. Sehemu ya utaratibu ule ni hatua ya Utakaso, ambayo ilibidi ichukue mahala pake muda kabla ya kuliwa kwa Pasaka.
Siku ya mwisho ya Utakaso wa Hekalu la Mungu, hekalu ambalo ni kama ulivyo wewe, ni utakaso kwa wale walifanya makosa au kwa yale yaliyofanyika kwa ajili ya ujinga wa utokanao na uzito wa kiuelewa ni mambo yanayo tazamiwa kufanyiwa kazi. Mlolongo huu unahusu hasahasa wale ambao bado hawajafikia kima cha kuuelewa utukufu na siri za Ufalme wa Mungu. Watu wote walioshindwa na kuanguka na kushindwa kuwajibika kufanya majukumu yao ya kiroho. Kama Musa na Haruni walivyo simama katikati ya hasira ya Mungu kama ilivyoelezewa kwa Kristo na kwa watu waliokuwa wanaomba dua kwa ajili ya usalama wao, ndivyo vivyo hivyo tunavyotakiwa kusimama imara ili kwamba wao waweze kusaidika nasi tuweze kusimama kwa pamoja kwa ajili ya usalama wa mataifa yetu.
Je, mambo kama haya tunayachukuliaje? Je, ni kwa nini tunafunga? Jibu ni kwamba; njia ya kujitakasa na kujifanyia upatanisho na Bwana katika Israeli ya zamani ilikuwa ni kwa kuitakasa saumu kwa ajili ya kulifanyia upatanisho kusanyiko au kusanyiko lote takatifu la Mungu na kukusanyisha wazee na wenyeji wa nchi.
Yoeli 1:13-15 inasema: 13Jitakaseni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njoni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji, Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu. 14Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, 15Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.
Nabii Yoeli anafika mbali kiasi cha kushughulikia kutoa somo la jinsi ya kulitakasa kusanyiko (waweza pia kusoma jarida linalosema: Siku ya Bwana na Siku za Mwisho [192].
Yoeli 2:15-27 inasema: 15 Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni Saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; 16 Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake. 17 Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee BWANA, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao? 18 Hapo ndipo BWANA alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake. 19 BWANA akajibu, akawaambia watu wake; Tazameni, nitawaletea nafaka, na divai, na mafuta, nanyi mtashiba kwa vitu hivyo; wala sitawafanya tena kuwa aibu kati ya mataifa; 20 lakini jeshi lililotoka kaskazini nitaliondolea mbali nanyi, nami nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa; sehemu yake iliyo mbele itaingia katika bahari ya mashariki, na sehemu yake iliyonyuma itaingia katika bahari ya magharibi; na uvundo wake utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda juu, kwa sababu ametenda mambo makubwa. 21 Ee nchi, usiogope; furahi na kushangilia; kwa kuwa BWANA ametenda mambo makuu. 22 Msiogope, enyi wanyama wa kondeni; maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake. 23 Furahini, basi enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa nninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyesha mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza. 24 Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta. 25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililolituma kati yenu. 26 Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe. 27 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Kumbuka hapa kuwa utakaso wa kusanyiko unalenga kulirejesha kwa Bwana Mungu na kutoa hakikisho mmwagiko ujao wa mvua ulio tazamiwa kutokea katika mwezi wa kwanza, ili kwamba tuweze kupewa kwa ukarimu mavuno ya ngano, mavuno ambayo kanisa linayo katika siku za leo, na sisi ni haya mavuno.
Kristo alikuwa ni malimbuko ya mavuno ya shayiri na alijitakasa mwenyewe kupitia kwa Mungu ili kwamba tuweze kutakasika ili kwamba sisi kwa hali isiyokuwa ya kawaida ni kwamba tuwatakase Israeli, kupitia uweza wa Mungu aliye Hai.
Tumetakaswa kwa ile kweli ya Mungu na Kristo alijitakasa yeye mwenyewe ili kwamba sisi pia tujitakase kwa Mungu.
Yohana 17:17-19 inasema: 17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 18 Kama vile ulivyonituma mimi ilimwenguni, mimi vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. 19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
Kristo alijitakasa mwenyewe katika Mungu kupitia Roho Mtakatifu kama kichwa cha kanisa ili kwamba sisi tuweze kunyenyekeana na kutumikiana kila mmoja na mwenzake, na kuwezeshana kila mmoja afikie utakaso katika Mungu kwa kupitia Roho Mtakatifu chini ya Kristo kama Kuhani wetu Mkuu.
Waebrania 13:12-16 inasema: 12 Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. 13 Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake. 14 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. 15 Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani tunda la midomo iliungamayo jina lake. 16 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
Kwa hiyo, ni Mungu atutakasaye kwa kupitia Kristo.
1Wathesalonike 5:23 inasema: 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Yeye atakasaye na wao watakaswao wote ni wamoja au wanatokana na chanzo kimoja kilekile.
Waebrania 2:11 inasema: 11Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote
pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;
Kwa ajili hii ndiomaana tunanyenyekeana kila mmoja wetu kwa mwingine kwa njia ya Roho Mtakatifu chini ya Kristo.
Waefeso 5:20-28 inasema: 20 na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; 21 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. 22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. 24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo, vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. 25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake. 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. 28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
Kwa njia hii tuna wezeshana kufikia utakaso mkamilifu kwa kila mmoja na mwenzake wakiwemo wana wa Israeli miongoni mwa mataifa yote ambayo hawajaitwa. Kwa kupitia bidii ya wateule wakiwa kama Hekalu la Mungu basi wanaume wote wanaitwa na Mji wa Mungu unajengwa.
Tunajua kuwa kuanzia Pentekoste ya mwaka 30 BK basi watu wa Mungu walianza kuwa ni Hekalu lililojengwa na mawe yaliyo hai Hekalu ambalo ni sisi (1Kor. 3:17; 6:16).
Kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza tulianza kuitakasa nyumba ya Mungu (2Nyakati 29:5, 17, 34; 30:17; 35:6) na sisi wenyewe tukiwa kama kusanyiko la Mungu, ambalo ni Hekalu la Mungu na Mji wa Mungu (tazama jarida la: Mji wa Mungu [180].
Nabii Isaya ana mengi ya kusema kuhusiana na utaratibu huu wa utakaso. Basi kwa kupitia namna hii sisi sio kwamba tunatakasika tu na kujitengwa mbali na uovu, bali pia tunamtakasa Mungu atuokoaye.
Isaya 8:11-18 inasema: 11 Maana BWANA aliniambia hivi, kwa mkono hodari, akanifundisha niende katika njia ya watu hawa, akisema, 12 Msiseme, Ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni fitina; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope. 13 BWANA wa majeshi ndiye atakaye mtakasa; na awe yeye hofu yenu, na awe yeye utisho wenu. 14 Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaa na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu. 15 Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa. 16Ufunge huo ushuhuda, ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu. 17 Nami nitamngojea BWANA, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia. 18 Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.
Vilevile utaratibu huu unalitakasa jina la Mungu na Mtakatifu wa Israeli.
Isaya 29:23 inasema: 23 Bali atakapowaona watoto wake, walio kazi ya mikono yangu, katikati yake, wao watalitakasa jina langu; naam, watamtakasa Mtakatifu wa Yakobo, nao watamcha Mungu wa Israeli.
Utaratibu huu wa utakaso unabidi ufanyike kisawasawa kama tunavyojionea katika Isaya 66:17 au kinyume chake watu wataangamia.
Kwa hiyo tunajionea sasa kuwa ni Mungu anayeweza kutakasa na Kristo ndiye atakasaye, na ni sisi pia tunaofanya utakaso na Mungu kama Hekalu la Mungu (tazama pia Ezekieli 20:12; 36:23; 37:28).
Wakati ambapo kazi hii hapo kwanza ilituama kwa Walawi, na hatimaye katika mtazamo wa kimwili na wana wa Sadoki (tazama Ezekieli 44:15-24 sawa na 46:20). Kazi hii sasa imetuama kwa Kanisa kwa kulingana na Ukuhani kama wa Melikizedeki.
Na kwa hiyo tunafunga saumu.
Je, ni kwakutumia vigezo kani tunaweza kujua kuwa saumu hii iko sahihi? Jibu lake linatuama katika kutafuta kwanza lengo la kutangaza saumu hiyo kama inavyoelekezwa katika Isaya 58:1-14. Sehemu ya kwanza ya fungu hili la maandiko linawaita watu wapaaze juu sauti zao ziwe kama tarumbeta, ili Israeli waonyeshe makosa yao. Kwa jinsi hii tunaona kuwa sisi sote tunafanya makosa na hakuna mwenye haki ambaye anamhitaji Masihi.
Isaya 58:1-14 inasema: Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao. 2 Walakini wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri na haki; hufurahi kumkaribia Mungu. 3 Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamini, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. 4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. 5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA. 6 Je! Saumu niliyoichagua, sio ya namna hii? Kufanuga vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? 7 Je! Sio kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala isijifiche na mtu mwenya damu moja nawe? 8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde. 9 Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiondoa nira; iswepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; 10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. 11 Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa utakuwa kama bustani ilyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui. 12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia. 13 Kama ukigeuza ukiugeuza mguu wako usiihalifu Sabato, ififanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita Sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutozifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; 14 ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.
Watu wetu wanamtafuta Mungu kila siku na wanapenda kuzimjua njia zake kama taifa lenye kutenda haki na kama ambalo lisiloziacha sheria za Mungu wao. Wana muomba awaelekeze sheria zake za haki na kufanya bidii ya kumjongelea Mungu, lakini wanadanganyika. Mungu haliangalii taifa hili. Je, ni kwa nini watu hawa wamefunga saumu lakini yeye hawaangalii? Je, ni kwa nini watu hawa wanajitesa nafsi zao lakini Mungu anakuwa wala hata hawaangalii? Jibu linapatikana katika hapohapo Isaya anaposema kuwa; fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe,na kuwalemea wote watendao kazi kwao. Wakati Israeli wanapokuwa mbele za Mungu kwa ajili ya maombi na kufanya dua kwa wakati huohuo wao hufanya kazi, na siku nyingine zote za aina mbili yaani kwa siku za Sikukuu na Miandamo ya Mwezi na hata kwasiku za Sabato. Walifanya kazi pia katika siku ya Upatanisho na wala hawakujua kuwa walikuwa wanafanya dhambi.
Kufunga saumu na huku kukiwako na magomvi, mashindano na magomvi na kupigana kwa ngumi za uovu, na Mungu akasema kuwa hawatafunga saumu kwa namna waliyokuwa wanafunga katika siku kama hizo kwa kufanya tu sauti zao zisikike zikiwa zimepalizwa juu. Vilevile aina hii ya utakatifu wa watu hawa hauku sikika, kwa sababu walijivika nguo za magunia na kujipaka majivu chini yake na kuinamisha chini vichwa vyao kama unyasi lakini saumu yao na maombi yao wala hayakukubalika na Mungu.
Saumu ambayo Mungu ameichagua ndio hii:
Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, na kuwaacha huru walioonewa, na kuvunja kila nira.
Tunatakiwa kuwagawia wenye njaa chakula chetu, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwetu, kuwavika nguo walio uchi na kutojificha na mtu mwenye damu moja nasi. Ndipo nuru yetu itakapo pambazuka kama asubuhi, na afya yetu itatokea mara; na haki yetu itatutangulia na utukufu wa BWANA utatufuata nyuma utulinde. Utuikufu huu wa BWANA ni Masihi. Ndipo tutaita, na BWANA atatuitikia; tutaita, naye atasema, Mimi hapa!
Je, si hili ndilo kusudi letu la kufanya utakaso kwa ajili ya makosa yanayotokana na Ujinga na Kupotoshwa? Sio ni kwa ajili ya kuwalemea wale wasiofahamu vizuri na wasioweza kuzishika siku hizi.
Je, sisi pia hatupati faida yoyote kwa kufanya kwetu hivyo? Iwapo kama tukiondoa nira isiwepo kati yetu wala kunyoosha kidole wala kunena maovu; na kama tukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zetu na kuishibisha nafsi iliyoteswa, ndipo nuru yetu itakapo pambazuka gizani.
Tendo la kujitesa nafsi zetu kwa ajili ya wale wasiojua vizuri, au wale ambao hawajapewa bado kuzijua siri za Ufalme wa Mungu bado, inatufanya sisi wenyewe tuendeleze sababu zetu wenyewe za kufanya makosa machoni pa Mungu na ule uwezo wetu wa kuwalinda watu wetu na kama Mbegu Takatifu katikati ya Watu wa Maagano.
Wakati ule Musa alipo simama mbele za mkutano wa Israeli na kunyoosha mikono yake juu, alihitaji pia msaada wa Lawi na Efraimu wasimame na kumshikilia mikono yake. Pande zote mbili yaani upande wa makuhani na wa wapiganaji walisaidia kufanikisha Israeli kwa ajili ya dua zao. Kwa hiyo, na sisi pia tumepewa katika Kristo kusaidia Israeli na kuwaleta kwenye haki na utauwa.
Hakuna utaratibu mwingine uliomo katika Biblia unaoweza kutumiwa na kuleta ufanisi zaidi kuliko utaratibu ule Mungu aliotupa sisi kupitia watumishi wake manabii, uliojulikana kama mfungo wa saumu. Tunajua kupitia manabii kuwa utakaso unapatikana kwa njia ya mfungo wa saumu na kwa makutano ya makutaniko ya Bwana.
Mfungo wa saumu ni kwa ajili ya Utauwa wa watu wetu na ili kwamba waweze kupewa kipawa cha wito kwa Mungu, na kwamba nguvu za Roho Mtakatifu ziwashukie watu wetu kama alivyotuahidi Mungu kwa kupitia watumishi wake manabii. Ilianzishwa na Masihi na inabidi itokee sasa kwa uweza na kwa nguvu katika siku za mwisho, wakati atakapokuja kutuokoa watu ambao tunamngojea kwa taraja kubwa sana.
Mungu na atusikie na kuzibariki dua zatu kwa nguvu za Roho Mtakatifu.
q