Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[292]

 

 

 

Maswali na Majibu Kuhusu Ezekieli Sura za 36-48 na Kutakaswa kwa Hekalu

(Toleo La 2.0 20020301-20080101)

Maandiko matakatifu yaliyoko kwenye kitabu cha nabii Ezekieli sura za 36-48 is ni unabii wa siku za mwisho na yanahusika na kukielezea kipindi cha milenia kitakavyokuwa chini ya utawala wa Yesu Kristo. Dunia yote itafanya kile anachokielezea nabii Ezekieli kuwa kitafanyika kwenye zama hii ya milenia wakati atakaporudi Bwana wetu Yesu Kristo. Maelekezo yaliyoko hapa ni mwingiliano mwingine kati ya Torati au Sheria za Mungu na pengine na utoaji wa dhabihu, ndio unawatakiwa kufanywa na Kanisa la Kristo leo linapokuwa linafuata Torati au Sheria za Mungu.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Haki Miliki ã 2002, 2008 Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org


Maswali na Majibu Kuhusu Ezekieli Sura za 36-48 na Kutakaswa kwa Hekalu

 


Utangulizi

 

Maandiko  

Ezekieli 36:17-19 insema kwamba Israeli wakiwa kwenye nchi yao wenyewe waliitia unajisi kwa kufuata njia zao wenyewe na  kufanya mambo yao wenyewe kama walivyoona vyema machoni pao, na Mungu aliwatawanya kwenye mataifa ya kipagani ambako walidhalilishwa na kutumikishwa kwenye mataifa haya yote, sawa sawa na uovu wao walioufanya na matendo yao maovu waliyoyaaanya.

 

Ezekieli 36:24-38: Mungu anasena kwamba atawafanya upya Israeli kwa kuitia ndani ya mioyo yao roho mpya nao watamtii tena Mungu na nchi yao itaponywa, na watu wa dunia watajua kwamba ni Mungu aliyelifanya jambno hili. Tendo hili la kuponywa kwa nchi yao litafanyika kwa neno la Kristo kipindi atakaporudi.

 

Swali la 1. Je, Israeli ni nini au ni kina nani?

 

Jibu: taifa la Israeli limeanzishwa kwa mjumuisho wa makabila yanayotokana na wana wa Yakobo, na amnao hatimaye walikuja julikana kama taifa moja la Israeli. Kabila la Yuda ndilo pekee linalochukua sifa za kuitwa taifa la Israeli. Kwenye kojawapo ya vitabu vya Torati, kile cha Hesabu sura ya 10, inaonyesha kuwa makabila ya Israeli yalikuwa ya Yuda, Isakari na Zabuloni yalipangwa upande wa Mashariki, na yale ya Reubeni, Simeoni na Gadi walikuwa upande wa Kusini, na makabila ya Efraimu, Manase na Benyamini walipangiwa upande wa Magharibi, na makabila ya Dani, Asheri na Naftali walikuwa upande wa Kaskazini, wakilizunguka Sanduku la Agano na Maskani ya Mungu. Kabla la Yusufu liligawanyika sehemu mbili na kuunda nusu ya kabila la Efraimu na nusu yao wakaingia kwenye kabila la Manase, na kuwafanya Walawi wafanye kazi yao ya kulitakasa Hekalu wakihesabiwa kama kabila la kumi na tatu.

 

Baada ya kufa kwao kina Daudi na mwanae Sulemani, taifa hili la Israeli liliigawanyika kwa sehemu mbili, huku makabila kumi yakaunda dola ya kaskazini ya nchi hii ya Kanani, na wakauchagua Samaria kuwa ni mji wao mkuu. Kabila la Yuda pamoja na sehemu ya wa kabila la Lawi na Benyamini wakabakia upande wa kusini, wakiwa watii na waaminifu kwa mfalme Rehoboamu mtoto wa Sulemani.

 

Yale makabila kumi ya kaskazini walishamiri na kuziandama ibada za sanamu na hatimaye waliishilia kwa kwenda utumwani Ashuru mwaka 722KK, na walisukumiliwa mbali hadi kwenye Mto Araxes wa Mesapotamia, na walibaki huko hadi kwenye karne ya pili ya mujibu wa tarehe za leo na kuanguka kwa Dola ya Waparthi. Makabila haya yalikuwa ni miongoni mwa makabila makubwa na yenye watu wengi ya Israeli. Katika kuanguka kwake Dola ya Waparthi, makabila haya yaliendelea mbele hadi kwenye maeneo ya pande za kaskazini magharibi hadi kwenye maeneo ya pande za Magharibi ya Ulaya na kuingia kwenye visiwa vya Uingereza, ambako waliungana na kuchanganika na tabaka nyingine za makabila mengine ambayo yaliingia huko miaka mingi iliyopita kabla yao.

 

Hatimaye, Yuda nao walikwenye utumwani Babeli takriban mwaka 597KK na walirudi kwenye Nchi yao Takatifu kwa amri iliyotangazwa na mfalme Koreshi na baadae kufanywa kuwa ni amri ya mfalme (soma jarida la Ishara ya Nabii Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 132) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)]. Walibakia huko hadi kuanza kwa huduma yake Masihi, na walitawanyika baada ya kuangamizwa na kuanguka kwa Hekalu mwaka 70BK, tukio lililoendana na Ishara ya nabii Yona.

 

Tangu kipindi hiki cha huduma ya Masihi na kuja kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste ya mwaka 30BK, taifa la Israeli lilifanyika kuwa ni jeshi la kiroho, na Hekalu la Mungu likafanyika kuwa ni jumba la mawe yaliyo hai. Mawe haya yakliyohai yalijumuisha pia mataifa ya Kipagani kwa kuwa kuongezeka kwa taifa la Israeli kulitegemea makabila yakiongozwa na maelekezo ya kiroho na kufunuliwa kwenye Ufufuo wa Kwanza.

 

Baada ya kurudi kwao kutoka utumwani Babeli wakiwa na John Hyrcanus, makabila ya Waedomu walijisalimisha na kufanyika kuwa ni sehemu ya Wayahudi kwenye nchi ya Yudea. Baada ya kutawanyika kwa Wayahudi tangu mwaka huu wa 70BK, katika mwaka wa 740KK, makabila ya Wagomeri ya Waashikenazi waliongezwa kwenye hesabu ya makabila ya Yuda baada ya kuikubali imani ya Kiyahudi kwa upande wa Nyika za kusini mwa nchi ya Urusi.

 

Kwa hiyo ikumbukwe kwamba sio Wayahudi wote tuwajuao leo kuwa ni wana wa Israeli na sio Waisraeli wote tuwajuao leo kuwa ni Wayahudi. Kwa kuongoka kwao Wamataifa, Israeli inakuwa ni jamii kubwa na pana ya kimwili na kiroho na walio kwenye ahadi ya baraka za Irahimu kwa kupitia ahadi iliyo kwenye haki ya uzaliwa waliyopewa makabila haya.

 

Kwenye kitabu hiki cha Ezekieli tunaona maeneo zaidi yanayoonyesha kuwepo kwa makabila yaliyo karibu na Hekalu (tazama hapo chini).

 

Maelezo yenye kufafanua kwa kina kuhusu wana wa Ibrahimu na wana wa Israeli yametolewa kwa kina zaidi kwenye jarida la Lazaro na Tajiri (Na. 228) [Lazarus and the Rich Man (No. 228)].

 

Swali la 2. Je, Kuna marejesho mapya mengine yoyote ya Israeli yaliyowahi kutokea hapo kabla?

 

Jibu: Ndiyo, kumekuweko na vipindi kadhaa vya marejesho mapya ya Israeli tangu hapo. Kila mara Israeli wanapokuwa wakianguka kwenye dhambi ya kuabudu sana na miungu mingine na kuandama ukengeufu waliadhibiwa kwa kupelekwa utumwani na hatimaye wamerejeshwa wanapokuwa wanageuka na kutubu (soma majarida ya Samsoni na Waamuzi (Na. 73) [Samson and the Judges (No. 73)]; Majeshi ya Gideoni na Siku za Mwisho (Na. 22) [Gideon’s Force and the Last Days (No. 22)] na Marejesho ya Yosia (Na. 245) [Josiah’s Restoration (No. 245)]. Marejesho haya yanaonekana yakifanyika kwenye zama za Kutoka utumwani na kisha yamefanywa na Waamuzi. Kwa ajili ya kurudia kwao mara nyingi matendo ya kuasi na kuabudu sanamu, nsipo Israeli walipelekwa utumwani kwenye nchi iliyombali na Nchi yao ya Ahadi mwaka 722BK, walikochukuliwa na Waashuru na walibakia kwenye pande za kaskazini ya Araxes. Ndiko waliunda himaya ya Waparthi hadi walipoondoka wote na kuelekea Ulaya mnamo karne ya pili ya zama hizi na kwenda kuungana na wengine wa kutoka kwenye makundi yao ya Ulaya Magharibi na kwenye Kisiwa cha Uingereza (soma jarida la Vita ya Waunitaria na Watrinitaria (Na. 268), [The Unitarian/Trinitarian Wars (No. 268)].

 

Yuda walikwenda kwenye utumwa wa Babeli kwenye karne ya sita (ambayo ni takriban mwaka wa 597KK), lakini baadae walitudi tena, kama tunavyoona kwenye Maandiko Matakatifu ya Biblia kwamba kulitolewa amri na mfalme Koreshi na hatimaye wafalme wa Uajemi, nao waliruhusiwa kuondoka wakiongozwa na kina Ezra na Nehemia (soma jarida la Usomaji wa Torati wa Ezra na Nehemia (Na. 250) [Reading the Law with Ezra and Nehemiah (No. 250)]. Walibakia kwenye Nchi ya Ahadi hadi mwisho wa kipindi kilichotajwa kwenye unabii kilichoendana sawa na Ishara ya Yona. Hatimaye walikwenda utumwani kwenye kipindi kingine cha utawanyiko kilichotokea mwaka 70BK kama kilivyotabiriwa na manabii. Jarida la Ishara ya Nabii Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)] linaelezea kwa undani kisa hiki.

 

Matengenezo mapya ya Yuda yalianza kuchukua mkondo wake kwa kuichukua tena ardhi ya Palestina kwenye Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, kulikofanywa na majeshi ya Jumuia ya Madola ya Kiingereza na kutangazwa kwa taifa la Wayahudi kulikofanywa na Lord Balfour mwaka wa 1917. Tendo hili lilianzisha marejezo mapya ya nchi ya Israeli kwenye Siku hizi za Mwisho na tendo hili litahitimishwa kwa kurudi kwa Masihi (soma jarida la Manabii wa Mungu (Na. 184) [The Oracles of God (No. 184)].

 

Sehemu ya 2

 

Ufufuo na Marejesho Mapya

Ezekieli 37 inaelezea juu ya maono ya ufufuo wa watu na kuungana tena kwa Israeli na Yuda, na kurudi kwa Isaeli kwenye nchi waliyopewa na baba zao. Kutakuwa na taifa moja na Daudi ndiye atakuwa mfalme wao.

 

Swali la 3. Je, ufufuo huu ulioandikwa kwenye Ezekieli 37 ndiyo Ufufuo ule wa Kwanza ambao ni wa wateule wote waliokufa siku na karne zote za nyuma?

 

Jibu: Ufufuo huu ulioonyeshwa kwenye Ezekieli 37 unaelezea kuhusu kurejeshwa na kutengenezwa upya kwa Israeli kwenye Nchi ya Ahadi, na kutimilika kwa kipindi cha Ufufuo wa Kwanza. Imeonyeshwa kwenye Maandiko Matakatifu kwanza kwa tendo la kuungana tena kwa Israeli na Yuda, kwa kuwa ni Masihi ndiye anayeikamilisha kazi ile kwa kipindi cha kurudi kwake.

 

Pia inaonyesha kwamba ufufuo huu wote utakuwa ni wa miili na mbao utafanyika kwa kubadilishwa kwa miili ya watwule watakao fufuliwa kwa kuthibitisha yasemavyo Maandiko Matakatifu. Na kila mtu aliyewahi kufa huko nyuma atafufuliwa akiwa ni mtu mwenye haiba ya kibinadamu na kubadilishwa miili yao kwanza kwenye mchakato wa kwanza na kuwekwa kwenye fungu watakalowekwa kulingana na mujibu wa mipango ya Mungu itakavyokuwa.

 

Swali la 4. Je, teno hili la kuungana kwa yuda na Israeli litafanyika kipindi hiki cha ufufuo? Na kama sio watati huu, basi litafanyika wakati gani?

 

Jibu: Tendo la kuungana kwa Yuda na Israeli litafanyika baada ya kuongoka kwao Yuda na kumgeukia Mungu na ni kipindi cha kurudi kwa Masihi.

 

Sehemu ya 3

 

Vita ya Gogu na Magogu

Ezekieli 38-39 inaelezea juu ya vita ya Gogu, Magogu na mataifa mengine ya kipagani, watakaojipanga dhidi ya Israeli na ambayo itapelekea kuhukumiwa kwao. 

 

Swali la 5. Tunajua kwamba mataifa haya yatainuka kinyume na Israeli kwenye kipindi cha mwisho wa Milenia. Kama ni hivyo basi, tunaweza kuona kuwa inamaanisha kuwa ni unabii unaojirudia na kufanya kazi mara mbili, na kwamba vita hivi vitatokea vyote kwenye kipindi cha mwanzo na mwishoni mwa Milenia?

 

Jibu: Vita hivi vya hawa Gogu na Magogu vina maana mbili. Vitatikeo kwenye kipindi cha mwanzoni mwa Milenia, wakati wa kumwagwa kwa vitasa vya ghadhabu ya Mungu kama vilivyotajwa kwenye Ufunuo 16, ili kumtukuza Mungu machoni pa watu wa dunia na kuonyesha hasira yake kwa mataifa. Pia kuna vita nyingine ya mataifa iliyoandikwa kwenye Ufunuo 20:7-10. Vita hii itapiganwa mwishoni mwa kipindi cha Milenia na itahusisha watu wa vikundi hivihivi watakaojaribu kuwaangamiza watu wa Mungu na kuliharibu Hekalu la Mungu.

 

Swali la 6. Kama kuna vita mbili basi na ambazo kila moja itapiganwa uppande mmoja wa Milenia, basi je, ni makamio au humuku zilezile, magonjwa, nk, yatatokea kwenye matukio haha yote?

 

Jibu: Biblia inaonekana kugusia kusema kwamba Mungu atawaangamiza, lakini maandiko yanayoiengelea ile vita ya mwisho hayasemi lolote kuhusu hilo. Bali tunaweza tu kulinganisha kwa kutumia vigezo vya tabia ya uandishi wa maandiko ya Ezekieli 38 na ndipo tunaweza kudhania kwamba atatumia utaratibu ule ule atakapowashuhulikia kwenye kila tukio.

 

Ezekieli 39 inaelezea kwa ufasaha sana kuanza kwa kipindi cha Milenia. Na inaelezea kuhusu vita viwili vitakavyopiganwa: moja itapiganwa mwanzoni na nyingine mwishoni.

 

Sehemu ya 4

 

Hekalu

Ezekieli 40–43 inaelezea kuhusu Hekalu.

 

Swali la 7. Je, Hekalu hili litakalojengwa litatumika kwenye kipindi chote cha Milenia?

 

Jibu: Ndiyo. Hekalu hili linalielezewa hapa kwenye milenia hii ya Ezekieli na mambo yote yatakayofanywa ndani yake litadumu kwa kipindi chote cha milenia. Na Hekalu hili linamaana mbili yaani kimwili na kiroho.

 

Swali la 8. Je, utoaji wa dhabihu utarejea na kufanywa tena? Na kama ni hivyo, ni kwa nini?

 

Jibu: Moja ya mambo ya kushangaza yanayoelezwa kwenye unabii na yanayohusiana na kazi za hekalu hili ni ukweli kwamba ni dhabihu za asubuhi tu ndizo zitakazokuwa zinatolewa huko. Unabii unaelezea ukweli wa kwamba dhabihu zitakazotolewa Hekaluni vilikuwa ni kivuli tu kilichomlenga Kristo na Kanisa lake. Dhabihu hizi zilikamilika kwa kuja kwake Kristo, lakini ilililenga pia Kanisa likiwa kama limbuko la mavuno ya ngano siku ya Pentekoste. Ziliwakilishwa na Sikukuu zilizoamriwa na Miandamo ya Mwezi na dhabihu za wale 144,000, na dhabihu ya jioni inawakilishwa na ule Mkutano Mkuu (tazama jarida la Mkutano Mkuu wa Mungu, Dhabihu ya Mwandamo wa Mwezi, na Wale 144,000 (Na. 120) [The Harvests of God, The New Moon Sacrifices, and the 144,000 (No. 120)]. Hii ni sehemu ya Ufufuo wa Kwanza. Kisha kuna jambo lingine kuhusu Mkutano huu Mkuu, unaowakilishwa na dhabihu hii ya asubuhi, hayatavunwa hadi kwenye Ufufuo wa Kwanza, na hivyo kuwakilisha jambo jingine la taratibu za Hekalu, ambalo Hekalu hili ni sisi.

 

Ulaji wa nyama utakuwepo na kuendelea wakati huu kipindi cha Hekalu na vyombo vya Hekalu vilivyo vitakatifu kwa Bwana. Utaratibu wa kutoa Zaka utawezesha kufanyika kuwepo kwa kilamara chakula cha kutosha kwenye Sabato za Bwana ili kuwapa watu wote kwenye nchi nzima. Jambo hili limeelezewa kwa kina kwenye Changizo la Mfalme kwenye Ezekieli 45. Utoaji wa changizo la nyama kwenye Sikukuu limeelezewa kwenye Zekaria 14:16-21.

 

Tendo la kubadilishwa miili linaloelezewa kwenye Zekaria 14:16-21 hasa ukisoma tafsiri ya New Revised Standard Version inayobeba maana halisi kwa kutumiwa neno linalomaanisha Wakanaani kwenye tafsiri ya Mfalme Yakobo (KJV) inayosema kwamba: “Hakutakuwa na mtu wa kufanya biashara kwenye nyumba ya Bwana wa Majeshi siku hiyo”.

 

Swali la 9. Je, dhabihu hizi zinatukumbusha dhabihu ya Kristo, au wana dhabihu nyingine zaidi?

 

Jebu: Mambo yote yahusuyo dhabihu hizi na yanayohusika na kurejeshwa kwa utaratibu wa ibadakatika Israeli, na ili kulionysha kwamba utaratibu uliotolewa na Mungu ulikuwa ni wa haki na sahihi. Tendo la kuwaua wanyama wa ajili ya nyama kunahitaji umwagaji wa damu na ilitolewa kwa ajili ya msamaha na upatanisho na ambayo itakuwa ni sehemu ya utaratibu wa Hekalu. Kwa mara nyingine tena makuhani watashughulika na kazi ya kuchinja wanyama.

 

Suala la kufanya upatanisha kwa ajili ya dhambi ambazo ni deni litarejeshwa tena na Torati. Mambo haya yameelezewa kwa kina kwenye jarida la Sheria za Mungu (Na. L1) [The Law of God (No. L1)].

 

Utaratibu uliofanywa kwenye Kalenda ya Mungu, na wanyama, natoa hakikisho kwamba utendaji sahihi wa utaratibu unatuama na kufanyika na Sikukuu zilizoamriwa zinweza kuadhimishwa na rasrimali zake.

 

Maongozi na Taratibu za Hekaluni

Ezekieli 44 inaelezea kuhusu taratibu zitakavyokuwa Hekaluni.

 

Swali la 10. Je, Ninani atakayeingia Hekaluni?

 

Jibu: Uingiaji kwenye Hekalu utawekewa utaratibu wake. Hataruhusiwa yeyote ila Mfalme tu ndiye atakayeruhusiwa kuingia kwenye lango la nje linaloelekea upande wa mashariki. Ni yeye tu ndiye atakayeingia kwa kupitia lango la mashariki na ataondoka kwa kupitia lango hilohilo.

 

Wengine wataingia kupitia lango lingine na kutokea nje kwa kupitia lango lingine lililomkabala nayo; kwa mfano, kutoka lango la kusini kwa lango la kaskazini. Ni wale tu wasio Waisraeli asilia bali walioongoka na kutahiriwa miili na moyo yao ndio watakaoingia Hekaluni.

 

Walawi waliopotoka kwa kuziandama ibada za sanamu watachukua hukumu zao. Watahudumu mahali patakatifu, wakifanya ulinzi wa malango ya Hekalu na watafanya kazi ya kuchinja sadaka za kuteketezwa na kuwahudumia watu. Na kwakuwa waliwasababisha Israeli wapotoke, Walawi hawatasogea mbele za Mungu kama makuhani, bali watapangiwa kazi ya kulitunza Hekalu na kulipangilia taratibu zake.

 

Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, Walawi ambao sio sehemu ya wateule, wala kuwa miongoni mwa wale 144,000 au kuwa miongoni mwa ule Mokutano Mkuu, hawatajongea mbele za Mungu katika Roho, bali watatumika kwenye utaratibu wa kawaida na wa kibinadamu tu.

 

Ukuhani wa Sadoki uliruhusu kwenda mbele za Mungu kwa kuwa walikuwa ni waaminifu katika Lawi. Kwa hiyo tunashughulika na maeneo mawili tofauti ya kikuhani, kundi lile ambalo lilikuwa ni la waaminifu katika Lawi ndilo litakalokuwa na sehemu kwenye ufufuo wa Kwanza wa wafu. Kwa hiyo, wenye haki wataishi kwa imani, na wana wa Lawi pia wamegawanyika makundi mawili ya waaminifu na ya wasio waminifu. Ni wale tu waliowaaminifu katika kipindi chao na walio ndani ya Kristo ndio watakaojongea kwa Mungu. Kwa hiyo, ukuhani wa Melkizedeki ulienda kwa Lawi, wakati kwamba, sio Walawi wote ni wa Melkizedeki na sio wote walio wa Melkizedeki ni wa Lawi, kwa kuwa wa Melkizedeki wa kweli hawapatikani kwa kufuatia uzawa wao wa kinasaba, maana yeye alikuwa hana baba wala mama. Makabila haya kumi na mawili yameandikwa na kuorodheshwa kwenye Ufunuo sura ya 7. Yanaonyesha kwamba Lawi ni moja ya makabila na sehemu kubwa ya ukuhani wa Melkizedeki, na wengine wote waliongezwa wakiwa ni wanachama washiriki wa mojawapo ya makabila haya.

 

Swali la 11. Je, kazi ya hawa Walawi na makuhani ni nini?

 

Jibu: waovu na wasiomcha Mungu na kuwa waaminifu kwake hawataruhusiwa kufanya kazi wala kuhudumu Hekaluni. Bali watahudumu kwa kufanya kazi ya kuchinja wanyama na kuwagawa kwa wahusika tu. Watadumu katika zamu zao na kuhudumu kwa kazi za kuteketeza wanyama na kazi nyinge ndogondogo tu.

 

Wale waaminifu na wenye kumcha Mungu tu ndio watakaoingia mahali Patakatifu. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, wana wa Mungu waliozaliwa mara ya pili katika Roho ndio watakaoruhusiwa kuja mbele za Mungu na kuhudumu wakiwa kama watu wa rohoni. Kifungu hiki cha maandiko kinaonyesha shutuma kubwa kwa makuhani, Walawi walioshindwa kumpokea Masihi, na pia kwa makuhani wa Melkizedeki walioshindwa kusimama kwenye zamu zao hadi wakaondolewa sehemu yao kwenye Ufufuo wa Kwanza

 

 

Kwa hiyo, uaminifu kwenye huduma hii ya kikuhani ni muhimu sana (kama ilivyoandikwa kuwa tutakuwa kama wafalme na makuhani, kwenye Ufunuo 1:6) tukifanya kazi fulani mbele za Mungu. Watawajibika kuzifanya kazi hizo (2Nyakati 8:14) kwenye Hekalu la Mungu (la kiroho). Miongoni mwa kazi hizo ni maombi (Yoeli 2:17) ya kuwaombea watu, kwa taifa zima-tazama kwenye Swali la 22. Wanatakiwa kujionyesha kuwa wamekubalika na kuionyesha mfano (Walawi 10:8-10); na kuijua Torati vizuri (Malaki 2:7) na waweze kuyafundisha mataifa (Law. 10:11). Kila kipindi Mungu amekuwa na watu wachache na kwa karne zote ambao wamekaza nia zao kuwa waaminifu katika kuzishika amri zake na kufanya kazi nyingine. Hii inaweza maana mpya na nyongeza ya kuja kwa Masihi ukua dumu has consistently had a few people.

 

Swali la 12. Je, ni nini vitakuwa vigezo, mwenendo, dhabihu na hukumu ya makuhani?

 

Jibu: Makuhani waaminifu wataingia kwenye Ua wa Ndani wakivaa kanzu za hariri. Mwonekano huu una maana kuu mbili zijuatazo.

 

Makuhani waminifu watakaokuwa hai kipindi hiki cha Milenia watafanya kazi zitakazoagizwa na Masihi kulingana na taratibu za Upatanisho.

 

Wale wateule na ambao wamefanikiwa kuingia kwenye vazi la hariri mbele za Mungu, kama Mashihi anavyoingia mahali anapokubalika kwenye Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa (soma jarida la Mganda wa Kutikiswa (Na. 106b) [The Wave Sheaf Offering (No. 106b)]. Kwa hiyo, wateule watamwona Mungu wakiwa kama wana wa Mungu, na kufanya upatanisho kwa Israeli na kwa mataifa watakaoletwa ndani yake, wakiwa kama makuhani na wafalme.

 

Utaratibu wa kutoa zaka utarejeshwa tena na makuhani watahudumu(Eze. 44:28-31).

 

Sehemu ya 5

 

Mgawanyo wa Nchi kwa Makabila

Ezekieli 45 inaelezea juu ya marejesho na matengenezo mapya ya Israeli, ambayo hasa ni kwa maeneo ya nchi kimakabila ambayo yameelezewa kwenye sura ya 48. Kama ilivyoonyehwa hapo juu, sura hii inatanguliwa na kulielezea Hekalu ambalo litakajengwa. Inaonekana kwamba ujenzi wa Hekalu hili utafanyika na hatimaye itafuatiwa na tukio la kurudi kwa Kristo, na maongozi yatakuwa ni kama ya serikali ya wanadamu na ya Hekalu au ya kidini.

 

Ezekieli 45:1 inasema kwamba kipindi ambacho nchi itakapogawanywa kwa kuipigia kura kwa uriithi wa Israeli, ndipo sadaka takatifu itatolewa kwa Bwana. Dhabihu hii itajumuisha sehemu ya nchi au ardhi yenye ukubwa fulani uliowekwa kwa maelekezo maalumu. Aya kadhaa zinazofuatia zinaelezea patakatifu penyewe, ukubwa wake, mahali patakapojengwa nyumba za makuhani, Walawi, na Mkuu wa nchi.

 

Swali la 13. Kwa kuwa kwa sasa tunaye kuhani aliye na Haiba sawa na ya Melkizedeki, hawa Walawi ni kina nani na kwa nini wanahitajika tena?

 

Jibu: Lugha inayotumika kwenye Biblia inaonyesha ukuhani wa Kilawi ambao ulishindwa na kazi zake za utumishi za Hekaluni. Kuna mgawanyo wa makuhani na ule wa Mfano wa Melkizedeki haukutajwa hapa. Tunajua kwamba kundi hili la Walawi waaminifu wamewekwa kundi moja na wale 144,000 na Mkutano Mkubwa unaoonekana kwenye Ufunuo 7. kitabu cha Waebrania kinatuambia kwamba Haiba hii ya Melkizedeki iko kwa Kristo. Mfale anatajwa, na kutengwa kwa maeneo ya makuhani kulikotajwa hap ani kwa mfano n ani ugawaji wa kweli kwa namna mbili mwendelezo wa somo la kwenye unabii kwa namna hizohizo mbili.

 

Swali la 14. Je, ni nani basi huyu Mfalme anayetajwa kwenye maandiko haya? Je, Mfalme huyu ni Kristo ua Daudi? Na kwa kuwa kuna ardhi inayotengwa kwa ajili yake, basi ni rahisi kwa mtu kuamini na kudhania kuwa atakuwa ni Daudi, na kwa kuwa Kristo ni mtu katika roho na anaweza kunionyesha akipenda.

 

Jibu: Ni wote wawili, kwa hili Kristo ni Mfalme wa Israeli na Daudi anatawala chini yake. Sisis sote ni watu wa nyumbani mwa Daudi na tunakuwa kama miungu midogo na Malaika wa Bwana vichwani mwetu. Kwa jina na jinsi nyingine ni kusema kwamba tutakuwa ni miungu modogo, kama Yesu Kristo, kwenye kipindi cha Marejesho ya Milenia. Mji wa Yerusalemu utakiwa ni kitovu cha utawala wetu hapa duniani, na tutatawala kama Shetani na mapepo wake walivyokuwa wanaitawala hii Dunia na wakashindwa (sawa na inavyosema Zekaria 12:8).

 

Sehemu ya 6

 

Dhabihu ya Upatanisho

Ezekieli 45:13-16: hay ani maelekezo yahusuyo dhabihu za nafaka, mafuta na sadaka za mafuta, pamoja na kondoo wa kutoka kila kondoo 200 – kwenye Sikukuu zilizoamriwa, Miandamo ya Mwezi na Sabato—ili kufanya upatanisho kwa nyumba yote ya Israeli. Haya yote yatatolewa na watu kwa Mfalme. Kwenye aya ya 17, wajibu wa Mfalme utakuwa ni kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za nyama na sadaka za vinywaji ili kuifanyia upatanisho kwa Nyumba ya Israeli (sawasawa na ilivyoelezewa kwenye jarida la Zaka (Na. 161) [Tithing (No. 161)].

 

Swali 15. Hii inaonyesha kuwa ni maelekezo mahsusi unaofuatia kurudi kwa Kristo ili kuwapatanisha watu kwa Mungu?

 

Swali: Sadaka inayofanywa kwa makusanyo ya Mfalme itatolewa siku za Sabato, Miandamo ya Mwezi na kwenye Sikukuu zilizoamriwa, na siku hizi zitakuwa ni Sabato kwa Bwana, Mungu wa Israeli. Kwenye mfumo wa utoaji wa zaka, Israeli wote wataweza kula mbele za Bwana licha ya mazingira yalivyo. Ni wajibu wa Mfalme kutoa mchango huu. Kwa hiyo, mtawala wa Israeli atakuchua nafasi yake kwa kipindi endelevu.

 

Sehemu ya 7

 

Utakaso wa Patakatifu

Ezekieli 45:18: Inasema kwamba siku ya 1 ya mwezi wa 1 ng’ombe dume mchanga alitolewa sadaka ili kupatakasa mahali patakatifu.

 

Swali la 16. Je, hii ndiyo ile siku ya 1 ya mwezi wa 1 ya mwaka wa 1 ya kipindi cha Yubile ya 1 ikiwa chini ya utawala wa moja kwa moja wa Kristo, wakati Shetani akiwa amefungwa na haitawali tena hii dunia?

 

Jibu: Ndiyo! Kwenye kipindi chote cha utawala wa milenia utakapoanza na kama katika siku ya Kwanza ya mwezi wa Kwanza wa mwaka wa kwanza ya kipindi cha Yubile. Na ni kwa sababu hii ndipo Kristo alikuja, lakini alikuja mapema na kipindi cha Shetani kimefupishwa. Na kama asingekuja mapema, hakuna mwenye mwili angaliyeweza kukutwa hai na kuokoka. Kwa kuja kwake mapema Idi ya Pasaka itaadhimishwa kwa majira yake bila kuchelewa (soma dhana hii kwenye jarida la Sabato Saba Kuu za Biblia (Na. 107) [The Seven Great Passovers of the Bible (No. 107)].

 

Swali la 17. Je, maelekezo haya yananyesha kuwa yanatolewa ili kupasafisha na kupatakasa mahali patakatifu palipojengwa upya tena?

 

Jibu: Tendo hili la kupatakasa mahali patakatifu au maskani ni muhimu kwa mujibu wa Torati, na palichukuliwa na Masihi tangu Mwaka Mpya wa mwaka wa kutolewa dhabihu ili kutuonyesha kwamba ni muhimu tangia Mwaka Mpya wa Sikukuu ya Pasaka na Mikate Isiyotiwa Chachu.

 

Upatanisho Kwa Ajili ya Hekalu

Ezekieli 45:20: Dhabihu ile ile ya siku ya 7 inapaswa kutolewa kwa ajili ya dhambi zilizofanywa bila kukusudia au kwa kupotoshwa. Na kwa hiyo utafanya upatanisho kwa ajili ya Hekalu.

 

Swali la 18. Hii inaonekana kwamba ni dhabihu ya muhimu sana ya Hekalu hili lililojengwa upya, na watu wanaokusanyika tena pamoja ambao wanahitaji kufundishwa tena Amri hizi za Mungu na sheria zake na zinawezaje kufanywa?

 

Jibu: Ukweli kuhusu utakaso kwa ajili dhambi zilizofanywa bila kukusudia au kwa kupotoshwa kunatuonyesha kwa dhahiri kwamba wajibu wetu ni mchakato wa Utakaso wa Hekalu na wa watu. Inaonyesha kwa watenda dhambi wote na waliopungukiwa kimakosa na ujinga, na sisi, kwa mkabilio wa kawaida kwa Mungu kwa kupitia kwa Kristo, kuomba msamaha na upatanisho na kuwarejesha watu wetu. Tunafanya hilo kila mwaka kwenye taratibu zetu za kidini kwa kuliadhimisha moja ya mambo aliyoyafanya Kristo kwenye maadhimisho yake ya Pasaka na akiwa ni Bwana wetu na tunaona pia jinsi Musa alivyotufanyia ili kwamba tusipatwe na mateso katika nchi ya Misri, na pia jinsi Samweli na wenngine waliokuwa Waamuzi wa Israeli walivyotufantia, na kama alivyofanya Daudi na manabii, na Kristo na hatimaye Kanisa, kwa mchakato unaoendelea. Ni kama walivyowahukumu Israeli chini ya Kristo. Tunaomba na kufunga tukiliombea dua taifa kama walivyofanya mababa waliotutangulia siku zilizopita kabla yetu wakiwafanyia watu wet una sisi wenyewe kwa kuitwa kwetu kwenye Imani. Kulielewa jambo hili ni muhimu sana katika Imani na kuelewa kidogo jambo hili katika karne ya ishirini ni kuupuuzia ukweli kuhusu ukuhani unaokuja siku zijazo kwenye Kanisa. Hili ni jambo muhimu katika marejezo ya Imani katika Siku za Mwisho, na linapaswa kufanyika kila mara na bila kukoma. Iwapo kama Kanisa linaisoma Torati katika kila mwaka wa saba, kama ilivyoamriwa, basi utaratibu huu hauwezi kupotea.

 

Swali la 19. Kama wateule ni Hekalu la Mungu kwa maana ya kiroho, na kama hili ni Hekalu la kimwili, kwa hiyo basi, hiyo siyo dhambi zilizofanywa kwa bahati mbaya na kwa kupotoshwa kwa wale walio kwenye Nyumba ya Israeli?

 

Jibu: Wale walio kwenye kundi la wanaofanya dhambi wasizozikusudia na kupotoshwa ni wale wanaohesabiwa kuwa wamefanya dhambi haijalishi asili yao, wawe kama ni wateule au taifa, au ni mataifa mengi na ambao wanakwenda kuwa sehemu ya Israeli kwenye mchakato.

 

Swali la 20. Je, sisi hatumo miongoni mwa walio kwenye kundi hili la wanaofanya dhambi bila kukusudia au kwa kupotoshwa?

 

Jibu: Wateule ni wateule waliochaguliwa na Mungu ambao wanapaswa kujiendeleza kwenye uelewa wao juu ya Mungu Mmoja na wa Kweli na kumjua Yesu Kristo aliyemtuma (Yohana 17:3). Watafanya makosa wakikosa kulijua hilo na walipotoka mawazoni mwao, lakini wamepewa Roho Mtakatifu ili waweze kuwa wa kwanza kuitwa kutoka kwa ndugu wengi. Kwa hiyo, kuingilia kati ni muhimu kwenye mambo yanayoendelea Kanisani.

 

Swali la 21A. Je, siyo dhabihu ya Kristo ndiyo iliyotufanya sisi kusamehewa dhambi zetu mara moja tu na kwa wote?

 

Jibu: Mchakato huu hauna la kufanya kutoka kwenye ukweli wa kwamba Kristo ndiye aliyefanya upatanisho wetu ns ni mara moja tu na kwa wote. Mambo tunayoyatenda ni sehemu ya kazi za Kanisa kushughulikia watu wake na kuwaleta kwa Mungu. Kukosea kuujua wajibu wetu kwa mapana yake kwa wateule kunatokana na mawazo yaliyoingizwa kwetu na kuzoeleka yaliyotokana na mapokeo ya wakuu wa daraja za juu wa kidini na yaliyotokana na hali ya kuwabagua na kuwatenga wateule kutoka kwenye jamii zetu wanazoishi. Mgwanyiko huu umepelekea kwenye hali ya kukosa kuelewa umuhimu wa maombi za kuombea wengine ambayo ni muhimu sana kwa Kanisa kuwafanyia watu wake, na umuhimu wa kuyatoa maisha yao kwenye Imani, kwa mwelekeo wetu endelevu.

 

Swali la 21B. Kwa kuwa Musa alikwenda mlimani pekeyake na wengine wote hawakwenda. Na akashuka chini kutoka mlimani mbele za watu wake na kuwatafasa watu (Kutoka 19:10-14). Je, hii inanaana sawa na kwetu sisi leo, tunvyafanya hivyo kwa pale tunapofanya hivyo wakati tunapobqatizwa kama makuhani na tunastahili kwenda kwenye Kiti cha Enzi cha Mungu, wakati mtu asiyebatizwa hawezi kustahili hivyo?

 

Jibu: Jambo muhimu kuelewa hap ani kwamba kuna utaratibu mtambuka wa utakaso. Wazaliwa wa kwanza wa Kiisraeli anakuwa ametakaswa kwa jinsi ya kuzaliwa kwake tu, na anastahili kukutana na kuuona “Uso wa Mungu”, na kama tujuavyo ni kwa kupitia kwa Yesu Kristo. Na ndivyo ilivyo hata kwetu sisi leo. Hekalu linakuwa limetakaswa tangia Mwanzoni mwa Mwezi wa Kwanza, ni Hekalu ambalo ni sisi (1Wakorintho 3:16-17). Kisha sisi tunapewa wajibu wa kuwatakasa wale walio nje ya Hekalu, siku ya Saba ya mwezi wa Kwanza. Mungu anaishi ndani yetu, sisi tukiwa kama Hekalu, kwa kupitia Roho Mtakatifu (1Wakorintho 6:19).

 

Swali la 21C. Kwa hiyo, sisi tukiwa kama Hekalu la Mungu na madhabahu ya Mungu, tunaoweza kufanya dua na maombezi kwa Mungu tukiwa kama mfano wa kujitoa na kujikana wenyewe na kuwatakasa watu waliofanya makosa na kwa kupotoshwa na kutokujua kwao?

 

Jibu: mchakato wa utakaso ni mojawapo ya utakaso wa ndani. Bwana ndiye anayetutakasa sisi (Kutoka 31:13; Walawi 20:8; 21:8; 22:9). Madhabahu hutakasa dhabihu znazoiletwa kwakuwa kila kinachoigusa madhabahu kinafanyika kuwa kitakatifu (Kutoka 29:37). Hata chatezo zinazotumika mzdhabahuni huwa vitakatifu pia (Kutoka 30:29). Hata hivyo, uwepo wa Mungu kwenye Maskani ndio unaofanya kuwe na utakaso huu (Kutoka 29:43; 40:34-35). Kwa hiyo, uwepo wa Mungu kwa wateule wake kama Roho Mtakatifu kunafanya uwepo wa Mwili wa Masihi kama Hekalu takatifu la Mungu kwa namna yoyote ile. Na hii ndiyo inayofanya kuwa wote wanaowasiliana naye wawe watakatifu.

 

Tunatakaswa kwa Kweli kwa pendo lake. Kristo alijitakasa yeye mwenyewe kwa ajili yetu nasi tunapaswa kujitakasa kwa Kweli yake, ambayo ni neno la Mungu (Yohana 17:17).

 

Swali la 22. Ikiwa kama ni sadaka ileile ndiyo inatakiwa kutolewa siku ya 7 kama ilivyokuwa inatolewa siku ya 1, je, siku hii inapaswa kuadhimishwa kama ilivyo siku ya Sabato? Je, kuna mahali popote kwenye Maandiko Matakatifu panapoonyesha kutuamuru kuwa siku hii tunatakiwa kuitunza kama Sabato?

 

Jibu: Andiko linasema: “nanyi mtafanya vivyohivyo katika siku ya saba kama mnavyofanya katika siku ya kwanza”. Siku ya Mwaka Mpya kwa kawaida kunakuwa na kutaniko takatifu na hasa kwa kuwa pia inakuwa ni siku ya Mwandamo wa Mwezi, sawa na inavyosema Zaburi 81:3-5 na ambayo inatengwa rasmi kama ni mwezi ambao Israeli walitoka utumwani Misri, ikimaanisha ni Mwandamo wa Mwezi Mpya wa Abibu au Mwezi wa Kwanza wa Mwaka. Kwa hiyo, siku ya Saba ya mwezi wa Kwanza kufanyika kutaniko takatifu.

 

Mchakato wa Utakaso unaeleweka kwa neno linalotumika la kutakasa.  

 

Kwa mujibu wa Kamusi maarufu ya Oxford Universal Dictionary, neno Takasa, maana yake ni “kutenga mbali au kuweka kitu mbali kwa ajili ya kutumika kikazi au kwa huduma; kuweka wakfu [kama mfale], 2. kuiheshimu kwa utakatifu wake, kuonyesha utakatifu, b. kujionyesha kuwa ni takatifu 3. kukiweka wakfu (kitu), kukitenga mbali na vingine kama kitakatifu au kitukufu. 4. kumfanya (mtu) kuwa mtakatifu, au kumfanya aendane na utakatifu. 5. Kumwambukiza au kumuathirisha mtu utukufu wa kweli kwa njia za: kumtia rangi ya hamasa au haki na bila kosa, au kumwesabia haki au kumpa haki yake stahili, au kumwonyesha kuwa ni wa kipekee na mwenye haiba ya kipekee na adimu kuonekana, au kama ilivyoelezewa kwenye kamusi hii ukurasa wa 1606. 6. Kumfanya aongezeke au anayefaa kuwatakasa wengine au kuwapa baraka za kiroho”.

 

Tunaliombea taifa na kwenda kwenye Kiti cha Enzi cha neema, kama tunavyoweza kufanya, ili kuwatakasa watu wetu kwa ajili ya huduma kwenye kazi yake. Huenda hili ndilo jambo muhimu kuliko yote tunalolifanya kama Kanisa kwa mwaka mzima, na halieleweki sana.

 

Tunatafuta msamaha na rehema kwa uhusiano wa moja kwa moja na Mungu kwa kupitia kwa Yesu Kristo. Mungu anatuambia kwa kupitia kwa watumishi wake manabii kwamba sisi tunalitakasa kutaniko kwa kufunga (Yoeli 1:14; 2:15-17). Tunamuomba Mungu atusamehe na pia tufanyike kuwa wenye juhudi kwa watu wake na kwa nchi yake na kutufanya tusitukanwe na kudharauliwa tena kati ya mataifa. Je, hili sio jambo la muhimu sana?

 

Kwa ajili ile ndyo maana tunafunga siku ya Saba ya mwezi wa Kwanza.

 

Swali la 23. Ikiwa kama siku ya 7 ya mwezi wa 1 ni siku ya kufanya kutaniko takatifu. Je, hii inamaana kuwa tunaiadhimisha siku hii kama tunfanyavyo kwa siku nyingine zozote takatifu? Badi andiko hili lingeashiria au kuonyesha kwamba ng’ombe mume mwingine angepaswa kutolewa sadaka na damu yake iwekwe mahala hapohapo, na ukumbusho kwa ajili ya dhabihu kwenye siku zote mbili zinazojulikana na kutambuliwa.

 

Jibu: Andiko hili linasema kwamba kile tunachokifanya Siku ya Saba ndicho tukifanye pia siku hii ya Kwanza. Kwa hiyo, tunapaswa kufanya kutaniko takatifu. Ni kweli kwamba hatuwezi sote kuwa pale na kujihudhurisha kwenye mkutaniko huu. Hii sio Sabato bali ni marudio ya ibada ya Kwanza zinaonyesha kuwa na uhusiano na Utakaso.

 

Swali la 24. Ng’ombe dume atatolewa sadaka siku ya 1, na ya 7 na ya 14 ya mwezi wa 1. Je, kila mmoja wa ng’ombe hawa anakuwa ni ashirio na anamwakilisha Kristo kama dhabihu ya Pasaka?

 

Jibu: Jib uni ndiyo! Mambo haya yote yanamlenga Lristo ambaye ni Pasaka na yule ng’ombe dume anayetolewa sadaka. Ni kwa kupitia uweza huu katika kuelewa kile alichokifanya na kile tunachopswa kukifanya sisi tukiwa kama Kanisa linalofuata nyayo zake katika utakaso wa Hekalu na kulitakasa kutaniko lake.

 

Swali la 25. Je, jambo hili lina maana gani ya kiroho?

 

Jibu: Tunapaswa kuwa kama alivyokuwa yeye na kufanya yale aliyoyafanya. Yeye alilitakasa Helaku kipindi kabla hajaingia ndani yake akiwa kama Mwana kondoo wa sadaka. Sisi pia tunapaswa kulisafisha Hekalu, ambalo ni sisi wenyewe, tunapokuwa tukijiandaa kwa ajili ya kuadhimisha Pasaka. Kwa hiyo, siku 14 za mwezi wa Kwanza ni za muhimu sana kwa ajili ya utakaso huu na wakfu kwa taifa kupitia dua zetu tunazozifanya kwa jina la Kristo. Mungu ametuchagua sisi ili kumtumikia na Kristo anawaleta wateule Kanisani na kwenye hukumu. Pasipo kazi za Kanisa hatuwezi kukua au kuendelea kuwepo. Lakini kama Kanisa likifanya vizuri, litapata upendeza machoni pa Mungu na litatumika vyema na Mungu.

 

Mfuatano wa mambo kwa Kanisa unaanza siku ya 1 ya mwezi wa Abibu hadi siku ya 14 Abibu, na kwa taifa tangia siku ya 15 Abibu hadi 21 Abibu, ambazo ni adhimisho la Idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kwa hiyo, mwezi wa saumu unafanyika kuwa ni kwa upatanisho wa Israeli na mataifa walioitwa ndani yake na wanaoendelea vizuri.

 

Pasaka

Ezekieli 45:21: Ayah ii inatoa maelezo kwamba siku ya 14 ya mwezi huu wa kwanza, Pasaka iadhimishwe. Hii ni Sikukuu inayodumu na kuadhimshwa kwa siku saba, na mikate isiyotiwa chachu tu ndiyo iliwe. Ni wajibu wa Mfalme kuandaa dhabihu kamilifu kwa kila siku, na zimeelezwa. Sura hii inafungwa kwa kutoa maelekezo kwamba kutolewe sadaka kwa ajili ya Sikukuu katika siku ya 15 sawa na ile ya mwezi wa 7. hakujasemwa neno lolote kuhusu mwingiliano wa Siku hizi Takatifu.

 

Swali la 26. Je, hali hii ya kutosemwa lolote inaweza kumaanisha kuwa siku hizo hazihitajiki kuadhimishwa tena?

 

Jibu: Hapana! Haimaanishi hivyo. Sikukuu ya siku saba ilitakiwa iadhimishwe kama ilivyokuwa kwenye matengenezo na marejesho yote, na katika kila Sikukuu inaadhimishwa kwa kipindi cha siku saba. Hakujarukwa kitu chochote. Sikukuu zote Mbili zinamaana moja na zinatakiwa ziadhimishwe kwa siku katika kushughulikia mambo mawili ya Kanisa kwa wokovu wa watu. Uingiliano wa Siku Takatifu za Pentekoste na siku za Baragumu na Upatanisho haina maana kwamba hazipaswi kuadhimishwa, lakini zaidi sana ni kwamba maandiko yanatuambia umuhimu wa hizi siku saba na utoaji wa dhabihu za kila siku za Sikukuu hizi, ambazo zinafanywa kwa namna moja na kwa kila Sikukuu. Sadaka hizi zinawakilisha utawala ulio ndani ya Kanisa na Mpango wa Mungu ulioko kwenye utaratibu wa Kalenda na kwenye dhabihu, akiwa kama kiongozi wa taratibu zote za Mungu. Jambo hili ni somo maalumu lililo kwa faida yetu. (soma jarida la Siku Saba za Sikukuu (Na. 49) [Seven Days of the Feasts (No. 49)].

 

Huu ni mpangilio wa milenia. Israeli wanapaswa kuzingatia utoaji huu wa dhabihu na kutunza taratibu zake kwenye Sikukuu zote zilizoamriwa na Siku Takatifu zake zote. Ni kuonyesha utii kwao kwenye kile kinachosisitizwa kwenye Torati (sawa na inavyosema Isaya 66:23; Zekaria 14:16-19).

 

Swali la 27. Kwa kuwa sadaka ni ukumbusho wa sadaka ya upatanisho ya Kristo, je, hii haionyeshi kitu chochote cha siku zinazokuja kama ilivyokuwa kwenye Agano la Kale? Kwa kweli hakuhitajiki tena kutoplewa dhabihu nyingine.

 

Jibu: Ndiyo! Utakaso unahitaji sadaka ya Kristo peke yake na sababu inayotufanya sisi tufikie hapa tulip oleo na kuweza kutembea kwa ujasiri kwenye Kiti cha Rehema, hakika ni kwa ajili ya kukubalika huku.

 

Hakuhitajiki dhabihu nyingine tena yoyote ili kutupatanisha. Tunawahitaji watu wetu watuombee kwa sala na dua kama tulivyoagizwa au kuamriwa kufanya.

 

Haijaagizwa kuwa “tuzitese nafsi zetu” kama tulivyoamriwa na kuagizwa kwenye kanuni ya Siku ya Upatanisho—ambayo ni upatanisho kwa Israeli tu na kwa Hekalu. Kwa hiyo, inapaswa kufikirika ama kudhaniwa hatuhitajiki kufunga saumu. Hata hivyo, tunapoutakasa mkutano, mara zote hufanywa kwa kufunga saumu na huu umekuwa ni mfano wetu tuliojifunza kutoka kwenye maandiiko ya manabii na Zaburi. Na ndivyo ilivoandikwa kwenye Torati yetu pia (sawa na Matendo 13:2).

 

Swali la 28. Kama Kristo ametupatanisha tayari n amara moja tu, je, juhudi na majaribio tunayoyafa sasa, hayapingani na maana halisi ya dhabihu ya Kristo na kuonekana kwamba tunafanya jambo lilelile la kutoa dhabihu ya Siku ya Upatanisho?

 

Jibu: Hapana! Haiwezi kuwa na maana hiyo. Tumeamriwa kufunga saumu siku ya Upatanisho na Kristo amekwisha kutupatanisha. Kwa hiyo, kwa ajili hiyo tunayoyafanya siku ya Upatanisho yangemaanisha kuwa tunaionea mashaka dhabihu aliyoitoa.Kristo, kitu ambacho hakiwezekani, nah ii inabakia kuwa ni Amri ya Mungu ya milele. Kwa jinsi hiyohiyo, ni kwamba kila Siku Takatifu inaelekeza kwenye jambo au tukio fulani kwenye Mpango wa Mungu, na kila sadaka pia ina taswira ya jambo fulani kwenye tukio lile. Tunaamini kuwa siku ziko kwenye kumbukumbu za Mungu. Kwa jinsi hiyohiyo, tunamuadhimisha Kristo kwenye Meza ya Bwana, tukikutanika kwenye usiku uleule ambao alisalitiwa na tunashiriki kwa kuula mkate na kunywa mvinyo baada ya kuoshana miguu kwa muadhimisha yeye—na sio kwa kumwakilisha yeye.

 

Swali la 29. Kwa kuwa kufunga kwetu saumu tunamuomba Mungu atusaidie na kutusamehe kwa dhambi tulizozifanya bila kukusudia na kwa kupotoshwa, lakini je, kuna mahali ambapo Maandiko Matakatifu yanasema moja kwa moja kwamba tunaweza kuwafanyia upatanisho wao?

 

Jibu: Tunafanya dua zetu na maombi kuwaombea wao kwa uweza ule ambao tumepewa na Mungu kupitia kwa Kristo. Katu hatuwafanyii upatanisho.

 

Sehemu ya 8

 

Sabato na Miandamo ya Mwezi

Ezekieli 46 inaelezea juu ya jinsi atakavyingia Mfalme siku za Sabato, Miandamo ya Mwezi na sadaka zitakazotolewa kwenye siku hizo.  

 

Swali la 30. Kwa mujibu wa Maandiko haya, je, siku ya Mwandamo wa Mwezi ni ya kufanya kazi au ni ya Sabato?

 

Jibu Imewekwa kwenye kiwango sawa na zile siku zilizokatazwa kufanya kazi kama ilivyo siku za Sabato. Kulikuwa na idadi kubwa ya dhabihu zilizotolewa siku hii ya Mwandamo wa Mwezi kuliko hata zile zilizotolewa siku za Sabato.

 

Wakati wa kipindi hiki cha Hekalu, Kuhani Mkuu ataingia Hekaluni kwenye maaadhimisho ya ain azote mbili, yaani Miandamo ya Mwezi na Sabato zinapofika. (angalia tulivyoandika hapo chini) na hakuna biashara yoyote iliyoruhusiwa kufanywa siku hizi za Miandamo ya Mwezi katika siku hizi za Israeli ya kale. Soma majarida haya hapa chini: Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara: Miandamo ya Mwezi (Na. 158) na Miandamo ya Mwezi (Na. 125) [Frequently Asked Questions: The New Moons (No. 158)] na The New Moons (No. 125)].

 

Tendo la Mfalme kuingia kwa kupitia lango la mashariki siku za Miandao ya Mwezi na Sabato ila sio kwa siku za kazi kunauthibitisha mtazamo huu.

 

Lango la upande wa mashariki mwa Mlima wa Hekalu hadi siku za leo umezungushiwa ukuta, ili kumsubiri Mfalme huhu aje na kungia siku ya kurudi kwake.

 

Wayahudi wote, wakiweko wale Wayahudi walio kwenye nchi za Utawanyiko, wanaendelea kuzidhimisha Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zilizoamriwa za kila mwaka. (Kwa mujibu wa E. Schürer, kwenye kitabu chake cha Historia ya Wayahudi Katika Nyakati za Kristo, toleo la III ukurasa wa 144,  (The History of the Jewish People in the Age of Jesus Christ, vol. III.i, p. 144).

 

Ni Kuhani Mkuu tu ndiye aliyeruhusiwa kutoa dhabihu ya dhambi kuu kwa niaba ya taifa zima katika Siku hii ya Upatanisho (Walawi 16), vinginevyo alikuwa na uhuru kutoa dhabihu wakati wowote aliotaka kufanya hivyo. Josephus aliandika kwamba pia alitoa sadaka za kila siku katika juma lililotangulia siku hii ya Upatanisho [Kwenye kitabu chake cha Vita ya Wayahudi, kifungu cha 5 na 7 (Wars of the Jews, v. 5,7)]. Kwa mujibu wa Josephus, pia alitoa dhabihu kwenye matukio ya Sikukuu za Waisraeli, zilizoitwa kuwa Siku za Sabato, kila Mwandamo wa Mwezi, na katika kila Siku ya Mwaka Mpya ambayo ilikuwa pia ni siku ya Mwandamo wa Mwezi. Sadaka hizi zisichanganishwe mawazoni na zile sadaka za nafaka zilizotolewa kila siku ambazo ziliamriwa zitolewe kwa ajili yake mwenyewe (kitabu cha Schürer, toleo la II, ukurasa 276).

 

Pia Wafalme walitoa sadaka zao kwa kufuata utaratibu wa Hekaluni, na hususan baadae walifanywa kwa Waasmonea.

 

Sehemu ya 9

 

Milki ya Israeli

Ezekieli 47:23 inasema kwamba itakuja kutokea kwamba katika kila kabila moja wanakoishi hali ya ugeni, kuna Israeli watatoa na kumpa milki yao. Hili ni Andiko Takatifu la muhimu sana.

 

Swali la 31. Hii inaonyesha kuwa wakati kipindi hiki cha Milenia kitakapoanza kutakuwa na wageni (watu wasioongoka) katikati ya wana walio kwenye Nyumba ya Israeli na ambao watakubalika katika makabila ya nchi wanazoishi leo. Je, kufikiri hivi vi sahihi, au kuna jambo linalotakiwa kulijua zaidi ambalo halijaeleweka hapa?

 

Jibu: Ndiyo! Wageni na wasafiri au wapitaji ni wengi kwenye makabila na wataishi pamoja nasi kama taifa. Hii ni sawa na ilivyokuwa watu mchanganyiko waliotoka nchini Misri na sisi kwenye tukio la Kukombolewa na Kutoka utumwani, na mataifa ya Kimataifa ya Kanaani yaliyotawanyika na kuenea hadi hatimaye wakawa ni sehemu ya Israeli.

 

Sura ya 47 inaelezea juu ya jinsi nchi itakavyoponywa na maeneo ya nchi yanayohusika.

 

Sura ya 48 inaelezea juu ya mgawanyo wa makabila kenye nchi hii na maeneo watakayoishi Makuhani, Walawi na nchi ya Mfalme.

 

Swali la 32. Tangu kugawanywa kwa nchi, jr, tunaweza kujua kama miongoni mwetu tupo kwenye nchi ya milki yetu?

 

Jibu: Ishara ya kujua kama wewe una sehemu kwenye milki ya Israeli inapatikana kwenye maeneo baada ya zama za Kutoka utumwani Misri. Idadi kubwa ya makabila walipewa milki zao nje ya nchi ya Israeli na jambo hili linaonekana kuwa ni kuhusisha sehemu ardhi iliyoongezwa. Tunajua bila shaka kwamba Israeli ina mataifa yanayoizunguka walioungana nao na kuenea hadi maeneo ya Frati na Jangwa la Uarabuni hadi kwenye nchi ya Jordan. Wana wa Lutu kupitia kwa Amoni walikuja kuwa miongoni mwao tena na kujiunga na wana wa Israeli.

 

Kwa hiyo, tuna milki nyingine. Milki yetu sasa ni kwa kupitia ahadi aliyopewa Ibrahimu na tutawaona wageni wameongezeka kwetu kwa kadiri tunavyoendelea sasa na kuelekea kipindi kinachokuja cha Milenia.

q