Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[293]

 

 

 

 

Mitala, Kwa Mujibu wa Biblia na Koran

(Toleo La 2.0 20060520-20080610)

 

Biblia imetolea mifani mingi kwa uwazi sana kuhusu mfumo wa kuishi na wake wengi (Mitala) kwa zaidi ya kipindi cha milenia. Leo letu hapa ni kuyakinisha mana ya jambo hili na kile ambacho Mungu anataka tukifanye na kwanini jambo hili limeendelea kwa kipindi cha karne nyingi na kuwa linaonekana kwenye maagano yote mawili, yaani kwenye Agano La Kale na Jipya.

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

 (Haki Miliki 2006, 2008 W.K. Wong and Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Mitala, Kwa Mujibu wa Biblia na Koran



Biblia na Koran zinaonyesha wazi na kwa mifano mbalimbali ya mitala. Mataifa mengi tuliyonayo siku hizi yanaruhusu mfumo huu wa mitala hasa yale yaliyo kwenye mfumo wa kimaongozi ujulikanao kama Shari’a na kwenye nchi nyingi za Kiafrika zenye mifumo ya kidini za kienyeji na kikabila.

 

Baadhi ya mataifa hayaruhusu mitala, lakini kuna idadi kubwa ya jamii ya Kiislamu zenye Mahakama za Kidini maarufu kama “Shari’a” zinazo ruhusu na kuhalalisha jambo hili na serikali zao zinayafumbia macho matendo haya.

 

Tunashauri kutathmini eneo sahihi la kibiblia na kuanzisha stadi elekevu ili kufikia kwenye lengo halisi kuhusu mfumo huu wa wake wengi au mitala na kuzisaidia familia zilizo kwenye mfumo huu. 

 

Maana na Historia yake

 

Neno la Kiingereza “Polygyny” linamaanisha mwanamume mmoja aliyeoa wanawake wengi. Na neno lingine la Kiingereza “Polyandry” linamaanisha mwanamke mmoja mwenye (kuolewa na) wanaume zaidi ya mmoja. Sasa, neno Mitala linautaja au kuuelezea ule mfumo wa maisha yao.

 

Siku hizi tunajionea mifano ya watu wanaowasiliana na Kanisa walio kwenye mfumo huu wa maisha wa matala. Tunaona kwamba watu wengi wanafamilia halali na zinazotambulika za wake wawili au zaidi. Nchi nyingi zinaruhusu jambo hili. Biblia inasema kwamba inampasa Mzee awe ni mume wa mke mmoja lakini imeishia hapo tu na haijasema kuhusu waumini wengine waweje, au je, ni kusema kwamba hakuna mwongozo mwingine uliotolewa kuwahusu watu wengine ile ni kwa hawa Wazee peke yao? Kanisa la CCG litakuonyesha jinsi tunavyoweza kufanya utaratibu unaoenenda kwa mujibu wa kanuni za Maandiko Matakatifu katika kulishughulikia jambo hili.

 

Kuna mtazamo unaolenga kulikwepa suala hili la Mitala. Biblia ina mifano iliyowazi sana kuhusu mahusiano kwenye mfumo wa mitala walioipitia mababa waliopita na pia inaelezea matokeo waliyokutana nayo wafalme, hususan Daudi na Sulemani miongoni mwa wafalme waliokuwa na wake wengi. Taifa la Israeli limetokana na matokeo ya makabila kumi na mawili yaliyotokana na watoto kumi na wawili wa Yakobo waliozaliwa kutoka kwenye ndoa ya wake wawili na masuria wawili.

 

Uhusiano kati ya mzaliwa wa kwanza wa mwanamke na malimbuko ya kiroho ya kifungua tumbo umeelezewa kwenye jarida letu la Zaka (Na. 161) [Tithing (No. 161)]. Kwenye maandiko haya mahala pa Wayahudi katika mahusiano ya ndoa zaidi ya moja maarufu kama mitala, kwa mujibu wa Mishnah na Talmud, yamefafanuliwa.

 

“Dhana ya Ukombozi inajiri kwenye mambo yote mawili, yaani kimwili na kiroho. Israeli walikuwa utumwani Misri kwa namna zote mbili yaani kiroho na kimwili wakiwa kwenye kongwa la dhambi. Kwa hiyo, ukombozi wa mwanadamu unahusu kwenye maisha yake ya kiroho na kwa mwenendo wake wa kijamii. Hatimaye, viumbe vyote vitakuja kukombolewa (Warumi 8:20-21) na ndiyo maana utawala wa milenia wa Yesu Kristo utamhusisha pia mwanadamu ili awe kwenye mfumo wa maisha ya kijamii, kama aliyofanya walipokuwa Sinai. Sheria na Amri zilizotolewa wakiwa huko Sinai zilikuwa ni kamilifu. Baadhi ya mambo (kama ya kupeana talaka) yaliruhusiwa kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao Wana wa Israeli.

 

Tunapoongelea suala la mzaliwa wa kwanza tunamaanisha ni wa mana na sio wa baba, kama tunavyoona kwenye kitabu cha Kutoka 13:2. Kimapokeo, kuoa wanawake zaidi ya mmoja kuliruhusiwa kwa mtu wa kawaida, na mfalme aliruhusiwa kuoa hata zaidi ya idadi hii (wa nne kwa mujibu Koran mYeb 4:11; mKet. 10:1-6;) au watano (mKer. 3:7) kutegemea tu jinsi serikali au uongozi wa kidini utakavyoruhusu (soma pia mKid. 2:7; mBkh. 8:4); na kwa mfalme aliruhusiwa kuoa hta wake kumi na nane (mSanh. 2:4)). Dini ya Qumran inafundhisha na kuamini kuwa watu wate, yaani mfalme na mtu wa kawaida ni lazima wawe na mke mmoja tu na hawaruhusiwi kuongeza [soma kitabu cha Schürer kiitwacho, Historia ya Wayahudi Kipindi cha Yesu Kristo Toleo la I ukurasa wa 320 msitari wa 125, (The History of the Jewish People in the Age of Jesus Christ, Vol. I, p. 320, n. 125)]. Agano Jipya linawadhiti na kuwaamuru Wazee na Mashemasi kuwa na mke mmoja tu (1Timotheo 3:2,12). Kwa hiyo, mzaliwa wa kwanza ni mtu anayelingana na sadaka na amewekwa wakfu, hata ikiwa ametokea kwenye ndoa ya mitala na hata kama amezaliwa kinyume na utaratibu wa kisheria au za kifamilia au kutoka kwa mwanamke aliyerithiwa na ndugu baada ya kufariki mumewe (Kum. 25:5-6). Ndio maana Zerubabeli alitakaswa na kuwekwa wakfu kwa kuwa alizaliwa kwenye uhusiano wa aina hii (soma jarida la Ukoo wa Masih (Na. 119) [iGenealogy of the Messiah (No. 119)].

 

Ni jambo la muhimu kuona kuwa Zerubabeli ameorodheshwa pale kwa ajili ya umuhimu wake aliokuwanao kwenye mkakati na kazi ya ujenzi wa Hekalu.

 

Kwa hiyo ni ukweli kabisa muamini kuwa mfumo huu wa matala ulikuwepo na ulijulikana kuwa ulikuwepo kwenye Maandiko Matakatifu kwenye Amri za Mungu. Dhana ya kumuoa mke kutoka kwa ndugu wa karibu kwenye familia yenu kwa utaratibu wa kikabila ulipelekea watu kuingia kwenye mitala wakati mwingine. Dhana ya kuliona jambo hilo kuwa ni matala au sio matala lilikuwa ni muhimu kwa lengo la kuhifadhi ama kulinda urithi usipotee kwa mujibu wa Sheria zilizokuwa zinatumia mfumo wa Kimuungano.

 

Wakristo wengi wanapingwa ukiwaambia kuwa Mungu anachukia mitala. Mtazamo wanaouamini ni vile tuliotangulia kuutaja kutoka kwenye Maandiko Matakatifu. Amri inayolielezea jambo hili ipo kwenye maandiko yafuatayo kutoka kwenye Kumbukumbu la Torati 21:15 ambayo inasema:

 

“Kama mwanaume ana wake wawili, naye anampenda mmoja na mwingine hampendi na wote wawili wamemzalia wana wa kiume, …”

 

Kwa hiyo hakunashaka kusema kwamba kwa mujibu wa Amri za Mungu mitala ya wanaume kwa wake wengi na hata ile ya wanawake kuwa na wanaume wengi ni kitu cha hatari.

 

Daudi alikuwa na wanawake wengi na masuria (kama ukisoma 2Samweli 15:16; 19:5; 20:3). Kimsingi, alikuwa na wanawake wawili tu ambao ni Abigaili na Ahinoamu wa Yezreeli, pamoja na Milka binti Sauli aliyemtoa kwa Falti (1Samweli 25:42-44). Baada ya kuuawa Sauli, Mungu alimpa Daudi kila kilichokuwa kwenye nyumba ya Sauli wakiwemo wake zake wote (2Samweli 12:8).

 

Sulemani alikuwa na wake mia saba na masuria mia tatu. Wanawake hawa walitokea kwenye makabila ya Wamoabi, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti (1Wafalme 11:3).

 

Rehoboamu alikuwa na wake kumi na tisa na masuria sitini (2Nyakati 11:21). Uzao huu katika Yuda huenda unaweza kuwa ni chanzo cha utaratibu wa Kitalmudi wa kuweka kikomo kwa mfalme awe na idadi ya mwisho ya wanawake kumi na.

 

Baba wa Nabii Samweli alikuwa na wanawake wawili (1Samweli 1:2). Wana wa Isakari ndio walioandikwa kuwa na wanawake wengi mno (1Nyakati 7:4).

 

Ukoo wa Kristo umepitia kwa mke wa pili wa Zerubabeli, aliyekuwa binti aliyetoka kwenye jamii ya kifalme ya Kiajemi na ni binti wa mfalme Dario.

 

Kwa hiyo inajulikana kwamba mwanafunzi yeyote wa Biblia angeweza kushawisika na maandihsi haya yanayoashiria wake wengi. Kipindi cha Kanisa la Mitume walikuwa na sheria moja inayohusu mambo haya ya mitala nayo ilikuwa ni kuwakataza Wazee na Mashemasi wahudumuo Kanisani wasiwe ni waume wa wake wengi, bali wawe ni wenye mke mmoja tu (1Timotheo 3:2,12, Tito 1:6).

 

Tangia hapo ilchukuliwa kwamba kupitia kwa watumishi wake manabii na Mitume, Mungu ameweka kikomo kwa Amri iliyo sawa tu na ile aliyoitoa kwa Musa na itumike na kufanyiwa kazi na wateule wake. Sababu ya kuwatumia Maaskofu na Mashemasi wa Kanisa kama kielelzo cha kuwa wawe ni wenye mke mmoja kila mmoja wao na wasiwe wa mitala na inapaswa kueleweka kadiri tunavyoendelea na somo hili. Mengi tutayaona kuhusu jambo hili hapi mbele.

 

Yapaswa ijulikane pia kwamba: 

  1. Koran inaitegeea sana Biblia kwa maagano yote mawili, La Ka;-le na Jipya. Kihistoria, kumekuwa na maandiko yanayoelezea suala la mitala kutoka kwenye maandiko ya pande zote mbili na Koran.
  2. Mahakama za kiislamu zinamruhusu wanamume kuwa na hadi wanawake wanne.
  3. Baadhi ya wanaume wa Kiislamu wanaamini kwamba wakifa kwa kifo kitakachotokana na harakati za kutetea masuala ya dini au vita ya kidini, ndipo watachukuliwa na kwenda mbinguni na huko watapewa wanawake mabikira 72 watakao wakuta wanawasubiria. Chanzo au msingi wa imani hii hautoki kwenye Koran lakini, bali ni mambo yaliyoingizwa kijanja tu na wajanja fulani. tutajionea jambo hilo baadae hapo chini.

 

Historia fupi ya chanzo cha mitala na matokeo yake mabaya

 

Ni kweli kabisa kwamba mtazamo wa Maandiko Matakatifu unaonyesha kuruhusu mfumo huu wa maisha ya mitala, lakini Amri za Mungu na Ushuhuda wake hauonyeshi wala kusemea maisha haya ya kuwa na wake au wanaume wengi ila linaruhusu tu pale mume au mke anapokufa na ndipo anakuwa huru kuoa au kuolewa tena. Bali inasisitiza kusema kwamba kama mtu atalala na mwanamke au mwanaume mwingine nje ya yule aliyemuoa au kuolewa naye atachukuliwa kama mzinifu.

 

Swali ni je, nukuu kama hizi zilizoko kwenye Biblia kuhusu matukio haya zaweza kutosha kuamini kwamba maisha haya ya mitala yamepata baraka na kibali cha Mungu? Kuna matendo mengi sana yaliyoelezewa kwenye Sheria za Mungu yahusuyo maisha yo mwanadamu na ambayo yamepewa miongozo yake kwenye Kanuni na Sheria za Mungu. Kwa mfano, utumwa, kulipiza kisasi cha damu, na matendo mengine mengi vilivyotolewa maelekezo au kukatazwa kwenye jamii nyingi za kimamboleo. Mungu anaruhusu talaka kwa mujibu wa Sheria kwa ajili tu ya ugumu wa mioyo, bali Kristo ametupa Amri nyingine iliyo Kuu zaidi tukiwa kama washirika wa Kanisa.

 

Tunapokuwa tunayasoma Maandiko Matakatifu, ni muhimu sana kujua kwamba sio kila kila tendo au tukio lililoandikwa kwenye Biblia liliruhusiwa au kupata kibali na Mungu na kuwa ni tendo au jambo jema kwake. Tunaporudi nyuma na kuangalia chanzo hasa cha maisha haya ya mitala, utagundua kuwa ilianza kwenye uzao wa Kaini, mtu mmoja aliyekuwa muuaji na hayakuanzia kwenye uzao wa mtu wa Mungu Sethi. Mtu wa kwanza kutajwa kuwa alikuwa na mitala ni Lameki (Mwanzo 4:23–24).

 

Jambo hili linaonysha mporomoko wa kiwango cha kiroho uliojitokeza miongoni mwa wana wa Adamu. Kaini akamuua ndugu yake Abeli. Lameki akaendeleza hali hii na kuliendeleza wazo hili la uasi. Kwenye Mwanzo 4:23-24, tunasoma hali ya kiakili ya Lameki ilivyokuwa. Kwa kweli inaelezewa kama ifuatavyo:

Lameki akawaambia wake zake,

Ada na Sila nisikilizeni mimi,

Wake wa Lameki sikieni maneno yangu.

Nimemwua mtu kwa kunijeruhi,

kijana mdogo kwa kuniumiza

Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba,

basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.’’

 

Hatahivyo, maandiko haya yanaonekana kwa jinsi ya usemi unaoashiria kitu kinachoendelea, na inaweza kuelezewa kwa kuandikwa:

“Mimi naweza kumuua mtu kwa kunitia jeraha na kijana kwa kunichubua” (cf. Bullinger’s fn. to v. 23)

 

Kwa hiyo, hali yake wa kiakili imeendelea kutoka kwenye aliyokuwa nayo Kaini hadi kufikia kwenye zama zilizopelekea kuwekwa amri ya “jicho kwa jicho”, bali hatimaye ikawa ni mwendelezo wa ulipizaji mkubwa wa kisasi.

 

Kwa hiyo, mawazo na maadili ya wanadamu hapa duniani yalianza kupungua kiwango chake kwa namna nyingi mbalimbali kwa vizavi sita, na matokeo yake ni pale Mungu alipoingilia baadae kuikomesha hali hii kwa Gharika Kuu.

 

Abraham alikuwa na wake wawili Sara na Ketura, na suria mmoja Hajiari. Tunaambwa kuwa Ketura hapo mwanzoni alikuwa n isuria na hatimaye aliwekwa kwenye orodha ya cheo cha mke.

 

Kisha Esau aliyeidharau haki yake ya uzaliwa wa kwanza pia alisababisha huzuni kubwa kwa wazazi wake kwa kuoa wanawake wawili kutoka jamii za (Mwanzo 26:34).

 

Na kama mtindo huu wa wake wengi ungekuwa na baraka za Mungu, basi Mungu angejichanganya nwenyewe kwa kuwakataza wafalme wa Israeli kuoa wake wengi (Kum. 17:16-17). Hebu tazama matukio ya kihistoria yaliyoandikwa kipindi cha kuasi kwao, ikiwemo jinsi ya kushughulikia uasi ulitoke kwenye nyumba ya Daudi kwa watoto wake wazaliwa na wake tofauti, jinsi mamia ya wake wa Sulemani walivyosaidia kumgeuza moyo na kuandama miungu mingine na kuabudu (1Fal. 11:1–3). Makatazo yaliyo kwenye Kumbukumbu la Torati 17:16-17 yanaenda mbali na kugusia pia kuwa asije akaanza kujilimbikizia silaha nyingi za vita magari ya kukokotwa na farasi, pamoja na kujilimbikizia farasi wenyewe, utajiri, na wanawake. Hatua hizi tatu ndizo zilizopelekea kuanguka kwa Sulemani (pia soma kitabu cha Bullinger). Tunaona tena Mungu akimmpa kibali Daudi cha kuoa idadi kubwa ya wanawake na kuchukua masuria na kumwambia kuwa hata kama alikuwa bado anawataka wengine wengi angempa. Kusudi la Mungu hapa lilikuwa ni kwamba alikuwa anamwambia Daudi kuwa hakupaswa kuifanya dhambi kama ile na hakuwa na sababu ya kufanya hivyo. Inaonekana kuwa tatizo lilikuwa kwenye hali ya moyo wake. Hata hivyo, Sulemani aliruhusiwa kujenga Hekalu la Mungu lakini Daudi hakuruhusiwa kulijenga kwa kuwa alikuwa ni mtu wa damu.

 

Hana, mama wa Samweli, alimnyenyekea sana Penina, mke mwingine wa mume wake Elkana (1Sam. 1:1–7). Mtiwa mafuta wa Mungu Samweli alikuwa ni tunda la ndoa hii ya mitala.

 

Mfumo wa maisha ya mke mmoja kilikuwa ni kitu kinachoendelea kwenye mataifa mengi elimwenguni kote, kama vile kwa: Wachina kwa watu waliojulikana kama Wahan waliokuwepo kwenye Uchina ya kale, Wadong, Wamanchus na Wayao, makabila kutoka Uchina ya.

 

Itakujakuwa ni kama habari ya kushangaza na wengi kuwaona watu kutoka kabila hili la Han la Wachina wa kale kuwaona kweli wakiwa kwenye maisha ya mke mmoja, ingawaje imani maarufu na matendo ya wafalme wa Uchina ya kale walikuwa na mamia nap engine maelfu ya wanawake na masuria.

 

"Utaifa wa Wahan ni kundi au alama kuu na muhimu sana nchini China. Inasemekana kuwa Wahan ni kabila au kundi lililoanza tangu kipindi cha miaka elfu tano iliyopita. Wengi miongoni mwao wanatokana na nasaba ya damu ya (YDNA) ya kundi la Haplo ya kundi “O”, ambalo ni sawa na ile ya Wahindi wenye asili ya Kimalaysia na baadhi ya Wapolynesia, na wanashabihiana na wengine wa makabila ya Yafeti. Kwa mujibu wa historia nyingine ndefu, wanasemekana kuwa waliwameza watu wengine kutoka mataifa madogomadogo. Wahan walikuwa kabila lililojikita kwenye shughuli za kiuchumi, mila na utamaduni na siasa. Mtindo wao wa kimavazi umebadilika sana, nguo zao wanazovaa sasa ni za mitindo mbali mbali. Dhana yao kuhusu maisha ya kifamilia ilikuwa sawa na walivyozoelea watu wan chi yao katika siku zao hapo kale. Lelilolitaka zaidi ni kudhibiti mambo kwa kipindi kirefu cha historia yao. Desturi zao zilikuwa ni kwamba mke na watoto lazima wamheshimu na kumtii yeye, lakini sasa mambo yamebadilika sana mahala kote walikojikita na kujulikana wao. Wanafamilia wote wana hakisawa na wanahesabiwa kuwa wako kwenye daraja moja. Baba anaweza kufanya kazi ya ndani pamoja na mkewake na watoto wake, kwa fikra kwamba wanastahili kuishi maisha ya furaha zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Kwa asili yao, mtindo wa maisha ya mke mmoja ndio waliokuwanao tangu mwanzo. Kwa sasa, mazishi ya moto ndiyo yanayoaminika na kuendelezwa. Wanafanya ukiri mwema wa kuwasaidia wazee na kuwahudumia watoto."

(Imechukuliwa na kuhaririwa kutoka kwenye wavuti ifuatayo: http://www.china-fpa.org/english/china/nationality/han.htm ).

 

Kipindi-zama cha cha mwanafalsafa wa Kichina aitwaye Confucius (kinachodhaniwa kilikuwa kwenye miaka ya 551-479KK), mfumo huu wa ndoa moja ulipendekezwa na kushawishiwa kuwa ndio wa mtu makini, lakini nyongeza ya kuwa na mke wa pili aliyejulikana kama suria ilikatazwa na kupigwa vita. Mwanafalsafa huyu Confucius na watu wengine maarufu na wenye kuheshimika waliamini kuwa ilikuwa sio vibaya wala si jambo la aibu kuwa na suria kwa lengo la kuzaa naye watoto wa kiume. Iliruhusiwa kufanyika hivyo ikionekana kwamba mke asilia ameshindwa kumzalia watoto wa kiume na kama alikuwa alimoenda sana kiasi kwamba hawezi kumpa talaka na kumwacha. Kulikuwa na sababu saba zilizohalalisha kutomrudisha mwanamke kwao sambamba na ile ya kukosa uaminifu, na miongoni mwazo ilikuwa ni hii ya kutomzalia mtoto wa kiume. ware was nothing shameful in taking a concubine

Waweza kujionea pia kwenye wavuti ifuatayo: http://www.malaspina.org/home.asp?topic=./search/details&lastpage=./search/results&ID=426

 

Haikuwa kama leo kulivyohalalishwa kupandikiza mbegu bandia kwa mwanamke, na kuzirutubisha hadi mtoto azaliwe.

 

Kuna kundi lingine lijulikanalo kama Wadong huko Uchina ambalo familia zao zinaishi maisha ya mke mmoja. Kabila hili la Dong kuchagua mwenza wenyewe na kwa kawaida humuoa wakiwa kwenye zaidi ya miaka ishirini. http://www.us.omf.org/content.asp?id=9234


Maisha ya mke mmoja yamekuwa pia ni mtindo wa wau wa kabila la Manchus, ambalo vijana wao wanachumbiana wakiwa watoto wadogo wa umri wa miaka 16 au 17 kwa ridhaa ya wazazi wao. http://en.chinabroadcast.cn/2245/2005-1-13/119@192716.htm


Kuna kabila lingine huko China linaloitwa la Yao. "Zaidi ya watu milioni mbili wa kabila la Yao wametapakaa na kutawanyika kwenye maeneo yote ya majimbo ya milimani ya susini mwa Uchina, ambako wameishi kwa kipindi cha zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Makabila ya Yao yanaishi pia huko Vietnam, Laos, na Thailand, na marazote wanapenda kujiita kuwa wao ni  wa Kim Mien, au "watu wa milimani”. Umoja wa kifamilia ni jambo muhimu sana kwa watu hawa wa kabila la Yao, na kuachana na kupeana talaka ni jambo la nadra sana kutokea kwa watu hawa. Mtindo wa ndoa ya mke mmoja ndio ulioamriwa na ulio kwenye sheria zao, ingawa huu wa wake wengi upo pia. Ingawaje ndoa zinngine bado zimeandaliwa na wazazi, bali uamuzi wa kumchagua mwenza kwa ujumla wanaachiwa vijana wenyewe kufanya maamuzi yake. Bibi arusi anatakiwa awe na umri wa miaka kati ya 16-17 na bwana arusi anatakiwa awe angalau na umri wa miaka minne zaidi ya ume wa bibi arusi." http://www.ksafe.com/profiles/p_code4/360.html


Ndoa za Mitala kwenye mataifa yasiyolazimisha Ndoa ya Mke Mmoja


Tunapojisomea matendo haya ya ndoa ya wake wengi, tunaona kwamba hata kwenye mataifa yale ambayopinga na kukataza hizi ndoa za wake wengi bado kunawanaoishi kwa mtindo huu wa wake wengi, nah ii hutokea kwa sababu za kukosekana kwa nguvu za kisheria kutoka kwenye sheria za nchi zao. Kwa mfano ni nchi ya Malaysia ni marufuku kwa mtu asiye Muislamu kuoa mke wa pili na ndoa kama hiyo haitambuliwi na mfumo wa kimahakama na Msajili wa Ndoa wa Malaysia. Kwa hiyo, mtindo wa ndoa za wake au wanaume wengi hauruhusiwi kwa mujibu wa sheria yaani kwa asiye Mmalaysia asiye Muislamu, haijalishi hata kama atakuwa ni Mchina, Mhindi au mtu kutoka kwenye kikundi chochote kile cha kijamii au kidini. Sheria hii ipo kwenye Katiba ya Malaysia Sura ya XX ya kuhusu "Mambo Yasiyoruhusiwa Kwenye Ndoa". Mwenzi aliyechukizwa au kufanyiwa vibaya na kukosa hiyari ya kuendelea na ndoa anaweza kuomba hati ya talaka hasa yakitokea mambo ya uzinifu. Hata hivyo, ingawa kisheria mitala haijaruhusiwa kwa mtu asiye na uraia wa Malaysia kwa raia wa nchi hii asiye Muislamu, lakini bado tutawakuta watu wenye mitala kutoka kwenye makundi haya ya raia wasio Waislamu wa Kimalaysia. Kwa kweli hii inatokea kwa ajili ya kukosekana msukumo wa kisheria kwa desturi za wengi kwa mfumo wa sheria za kidini maarufu kama Shari’a. Pia tutaona mambo kama hayahaya yakitokea kwenye nchi nyingine.

 

Malaysia, kama taifa la Kiislamu lina mfumo mwingine pia wa sheria za Kiislamu ambazo zimetafsiriwa kutoka kwenye mfumo wa kidini maarufu kama Mahakama ya Syaria au Shari’a. Hii inamruhusu mwanaume wa Kiislamu awe na hadi wanawake wanne, jambo ambalo kama tulivyojionea hapo juu limechukuliwa pia kutoka desturi na mapokeo ya kibiblia kama ilivyotafsiriwa na mfumo wa Mishna na Talmudi kwenye imani ya Kiyahudi ambako bila shaka ndiko matendo mengi ya Kiislamu au kikomo kilifikiwa.

 

Tunakuta kwamba katika imani ya kawaida nay a jumla, watu huamini kwamba watakapofika mbinguni kwa Allah ambako kunafananishwa na Bustani, itakuwa kwamba kila mwanaume mmoja atapewa mwanamke mmoja. Pia tunajua kwamba kulikuwa na Adamu mmoja na Hawa mmoja, na wala sio idadi kubwa ya wanawake, wala hakukuwa na wanaume wengi au mitala wala aina nyingine yoyote ya umati wa watu kindoa.

 

Singapore inasheria zinazofanana na zile za Malaysia, nchi hizi zote mbili zikiwa ni wanachama wa Jumuia ya Madola. Tendo la kuoa mwanamke mwingine wa pili ni kosa la jinai na haikubaliki wala kutambuliwa na sheria za mahakama au na Msajili wa Ndoa kwenye nchi hizi za Malaysia na Singapore. Kwa hiyo kuongeza mke wa pili au kuwa na mitala ya aina yoyote hakuruhusiwi kisheria kwa watu wasio Waislamu katika nchi hizi za Malaysia na Singapore hata kama wao ni Wachina, Wahindi au wanaotoka kwenye vikundi vingine vya kijamii au kidini.

 

Hata hivyo, hata huko Singapore mfumo wa sheria za Kiislamu maarufu kama Shari’a na mfumo wa wake wengi umekuwa ni kitu kinachofanyika kwa kuchukuliana na kuvumiliana tu n ani kitu kinachoruhusiwa kwa wachache.

 

"Wakati kwamba sihgapore likiwa ni taifa lisilo la Kiislamu, lakini Waislamu wa Kisingapore wenyewe mfumo wa maisha yao umefungamanishwa na maongozi ya Sheria za Kiislamu ya mwaka 1957 iliposaji Mahakama za Kiislamu maarufu kama Mahakama za Shari’a kwa mambo yote yahusuyo milki na mali za mtu, kukatia rufani mambo ambayo yaliwekwa kwenye Sheria za zamani. Ilihusu na udhibiti wa ugawaji wa mali zilizochumwa, lakini sheria hii ilihamisha mamlaka yote ya kisheria na mahakama kwenye muundo wa Mahakama za Shari’a za Kiislamu kutoka kwenye kuwa mahakama za kawaida. Iliingizwa kutoka Maongozi ya Sheria za Kiislamu, Kifungu cha Sheria cha mwaka 1966, kilichotoa mambo mengi zaidi ya kisheria. Sheria ya mwaka 1966 ndiyo ilianzisha kile wanachokiita “Majlis Ugama Islam Singapore” (Baraza la Kiislamu la Singapore) ambalo litashughulika na kusimamia na masuala ya mali pamoja na kukata hukumu. Baraza hili pia lina Kamati za Kisheria zinazomjumlisha pia Mufti w Singapore, na wanachama wengine wawili wa baraza la Majlis na wawili wengine ambao si wanachama. Kazi ya Baraza hili la Kisheria ni kuamuru kitu wanachokiita fatawa kwenye kila kipengele cha sheria za Kiislamu. Baraza la kutunga sheria la mwaka 1966 pia lilijumuisha mambo muhimu zaidi kuliko lilivyokuwa lile lililotangulia huko nyuma. Sheria ya kuwapa uhuru wa Kujieleza na kuhutubia Wanawake ilipitishwa pia mwaka 1961, likichukua mahali pa sheria ya zamani ya watu wa familia zisizo za Kiislamu iliyoanza kufanya kazi yake nchini Singapore. Ilikazia sheria za kutooa wake wengi na kuwa waoe mke mmoja tu kwa Wasingapore wote isipokuwa Waislamu tu, ingawaje wanaume wa Kiiislamu walivuka mpaka na kuwaoa wanawake wasio Waislamu chini ya sheria hii ya Uhuru wa Kkujiamlia mambo kwa Wanawake inayokataza kuoa Waislamu wenye mitala wanaojulikana kuwa walisamehewa kwa sababu maalumu kutoka kwenye mambo fulani yahusuyo Jukwaa la Wanawake, kwa mfano ni wale wanaohusiana na kuhamasisha maandamano, migomo, talaka, etc. mfumo wa mahakama ya kawaida una mahakama yaliyoanzishwa, yaliyorithiwa na rumande ambazo wanaweza kupelekwa hata wale walio kwenye chini ya Sheria ya Kiislamu, na mke wa Kiislamu ana uhuru wa kuchagua pa kwenda kati ya hizo zote yaani mahakama za kawaida au zile mahakama za kiislamu za Shari'a ili kuweza kurekebisha tabia na kurejesha utengamano.


Hadhi na mahudhui ya kikatiba ya Sheria za Kiislamu ilichukuliwa na kuwekwa tarehe 3 Juni 1959 na kufanyiwa marekebisho mwaka 1965 wakati lililokuwa Jimbo la Malaysia la Singapore lilipojitenga na Malaysia. Katiba ina idadi kubwa ya vipengele vinavyohusisha uhuru wa kuabudu na wa kidini na kukataza aina yoyote ya ubaguzi wa kidini. Kifungu cha 153 chini ya Toleo la Jumla kinasema "Wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria kwa mujibu wa sheria hii wataweza kufanya maamuzi ya kuyafanya mambo yahusuyo dini ya Kiislamu na kwa kuanzisha Baraza la litakalomshauri Rais kwa mambo yaihusuyo dini ya Kiislamu".


Mfumo wa Mahakama
: Kuna Mahakama moja ya Shari’a nchini Singapore; ambayo inaweza kusikiliza na kufanya maamuzi na kumchukulia mtu hatua inapotokea kwamba wote miongoni mwa wanaoshitakiana ni Waislamu au inapotokea kwamba wahusika wote wanaodaiana waliolewa wakiwa chini ya sheria ya Kiislamu (hasa kama mume ni Muislamu). Mahakama ya Shari’a inasikiliza mashitaka yanayohusika na mambo ya ndoa, talaka, uposi, kutangua ndoa, haki ya kutengana kisheria, mgawanyo wa mali wakati wa kuachana, kulipa mahari, usuluhishi, na ukataji wa rufaa, marufu kama mut’a. ukataji rufaa kutoka kwenye maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Shari’a au maamuzi yaliyotolewa na kwa upotoshwaji na makadhi pamoja na Bodi ya Rufaa inayojumuisha Waislamu watatu waliochaguliwa na Msajili wa Mahakama Kuu kutoka kwenye baraza la watu saba waliopendekezwa na Rais kila mwaka. Bodi hii ya Rufaa ndiyo ya mwisho katika kufanya maamuzi."

 

CHANZO CHETU NI:- http://www.law.emory.edu/IFL/legal/singapore.htm


Wakati mitala ikiwa imekatazwa kwenye ndoa za kiraia nchini Singapore chini ya Jukwa hili la Wanawake, ndoa za mitala zinaruhusiwa chini ya Uongozi wa kikatiba wa Sheria za Kiislamu. Huu ndio mfano wa haki za wachache za kufanya matendo yao binafsi na yale sheria za kidini.

(http://www.un.org/News/Press/docs/2001/WOM1293.doc.htm)


kwa hiyo, Singapore inaonekana kuwa na umoja na mtengamano zaidi kuliko ilivyo nchi ya Malaysia. Wakati nchi ya Singapore ni taifa lisiyo la Kiislamu, lina mchepuo mwingine wa sheria nyingine kwa Waislamu. Inaweza kumhukumu mwanaume wa Kiislamu kwa kosa la kuoa mitala kwa ajili ya kuwepo kwa sheria hizi nyingine. Zikiwa pia kama nchi zinayoheshimu araia wa watu mchanganyiko na ni za kidemokrasia, nchi hizi zote mbili za Malaysia na Singapore zinaheshimu pia uhuru wa kuabudu. Dini inahusisha utaratibu wa kuamini na kuheshimu. Mahali ambapo imani hizi zinagongaana na mila au desturi na mawazo mapotofu, matatizo hujitokeza.

 

Tatizo liko kwenye mawazo fikirika na mwelekeo sahihi wa kiimani/thamani au kiwango cha uelewa wa kila mtu binafsi yake.

 

Waislamu huamini kuwa wanaweza kuwa na zaidi ya mke mmoja na wanaweza kuoa hata wanawake wanne. Tunakuwa wavumilivu na watu huru kwa faida ya kulinda mtangamano. Mtu aliyehukumiwa hivi karibuni kifungo cha miaka kati ya 32 na 24 na kulipa miganda na miwa huko Singapore alikwenda mbali ya sheria hii. Alikuwa na wanawake kumi na kuifanya uhalifu mkubwa sana.

 

Matukio tunayoyaona huenda ni matokeo ya hali yetu ya kuvumiliana wakati mambo mengine yanahitaji kutilia maanani ambapo kwenye mchakato huu yanakataliwa. Pia kunamashaka makubwa sana kama kuna taifa lolote lenye sheria kama hii inayopinga mitala kiasi cha kuzilazimisha sheria zao ziweke ukweli wa kuwa mataifa kama hayo yana mifano mingi ya kuwa na watu wenye mitala ingawa sheria zao zinakataza matendo hayo.

 

Matendo haya nchini marekani

 

Tunajua kuwa madhehebu ya Mormoni yameruhusu mitala na matendo ya jinsi hiyo, huku wakienda kinyume na sheria za Marekani, na tunaona pia kwamba hata kwenye nchi hii kuna maeneo mengine ambayo bado wanafanya matendo haya. Maeneo kama ya Utah na Arizona kwa mazingira yanayojulikana kama “de facto” au mazingira yasiyo ya kawaida.

 

Kuna vikundi fulani mbali na haya madhehebu ya Mormoni na madhehebu mengi mengine ya Waislamu wanaopinga maisha haya ya mitala. Baadhi ya watetezi wa mfumo huu wa mitala wanakaza mawazo yao na imani yao kama ifuatavyo:

 

1. Mtazamo wao ni kwamba kanuni na Sheria za Agano la Kale zinaonyesha kutokuwa na tahshishi na zinaruhusu mitala na ilifanywa na mababa zetu kama kina Lameki, Ibrahim na Yakobo, wakiwemo pia hata baadhi ya manabii. Na kwamba Yesu Kristo hakuja kuitangua Torati wala yaliyofundishwa na kutendwa na manabii (Mat. 5:17-18). Kwa hiyo Torati inabakia kama ilivyo na mitala ni kitu halali. Huu ndio msingi wao mkubwa wanaoutumia kutetea hali hii.

2.  Wanapinga kwa kujenga hoja kwamba Mungu alijitolea mwenyewe mfano wa mwanaume wa wake wengi au mitala kwenye Ezekieli 23:4, hii ni kuonysha kuwa yeye ni mume wa mataifa mawili, Israeli na Yuda.

3.  Wanaendelea kujenga hoja zao kwa kusema kwamba hata Yesu mwenyewe alijitolea mfano kwa kujionyesha kuwa ni mume wa wake wengi kwa kujifananisha na muwa mume wa kila nafsi ya Mristo mmoja mmoja (2Kor. 11:2).

4.  Hoja nyingine wanasema kwamba hakuna mahali kwenye Biblia panapoashiria kukataza mtu kuwa na mitala.

5. Wanatumia sababu nyingine kujengea hoja ili kuyaunga mkono mawazo yao kama tulivyoeleza hapo juu.

 

Kumekuwa na hoja pia kuwa Amri hizi Kumi walipewa Israeli peke yao, na kwamba haziwahusu wala kuwafunga Wakristo wala Waislamu. Jibu sahihi ni kwamba zilitolewa kwa wageni pia. Maandiko Matakatifu yako wazi kuwa hakukuwa na aina mbili ya Amri au Sheria bali ni hizihizi zinazofanya kazi kwa wote wawili yaani kwa Israeli (wakiwa kama makabila kumi na mbili wakiwemo Yuda) na kwa wageni (Kutoka 12:49, Isaya 56:6, Hesabu 9:14; 15:15-16, 29-30, Zaburi 18:44). Kuna mtoaji wa Amri mmoja tu ambaye ni Mungu, yaani Eloa, mwumba wa watu wote likiwemo Jeshi la Malaika wa mbinguni (Yakobo 4:12).


Mambo ya Walawi 24:22 inasema: "Mtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.’ ’’

 

Hii ni kusema kwamba kuna mataifa huko yenye sheria mbili tofauti.

 

Kwa mfano, Mungu alimwambia mfalme wa Wafilisti wa Gerari, Mfalme Abimeleki (huyu ni mmataifa, mgeni au mtokambali) mambo yafuatyo: “…Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua, yeye ni mke wa mtu.’’ Abimeleki…akasema, “Je, Bwana utaliharibu taifa lisilo na hatia? (Mwanzo 20:3-4).

 

Kama sheria hizi zimeandikwa kwenye Amri Kumi kama ile ya usizini, hawahusu wamataifa, ilikuwaje basi mfalme huyu mmataifa aambiwe alikuwa anamtenda dhambi Mungu? Kwa nini Mungu alimtishia kumwua mtu huyu iwapo kama angemruhusu kuhu mke wa mtu arudi kwa mumewake (Mwanzo 20:7)? Jibu liko wazi tu kusema kwamba kuna Sheria moja tu kwa watu wote, yaani wamataifa na kwa waaminio, ni amri moja hiyohiyo, ambayo ni Amri ya Mungu. Yeye ni Mungu wa Pekee na wa Kweli, Eloah, wa wote wenye mwili, wa Watakatifu na wa Malaika wa Mbinguni.

 

Mtindo wa maisha wa mke kuwa na wanaume wengi umekatazwa na kupingwa ulimwenguni kote, kwa Wayahudi, kwa Wakristo na kwa Waislamu

 

Inatupasa kukumbuka pia kwamba makundi yote yanayodai kuwa ni Yakikristo na yanayotetea mitala, hayaruhusu mwanamke kuwa na wanaume wengi, bali wanapinga tendo hili. Tutalielezea na kulitathmini hili na kuona kama kuna mambo mengine ambayo huenda hayajatiliwa maanani.

 

Hebu na tuiangalie historia kwa umakini, Maandiko Matakatigu na mambo mengine yaliyoanzishwa na maswali yatakayotupelekea kufikia kwenye kiini chake na natokeao yake mabaya:

 

* Baada ya Adamu una Hawa kumtenda dhambi Mungu, walifanana na Elohim wakijua mema na mabaya. Hii namaana kwamba tunapaswa kupambanua mapenzi ya Mungu kwa kujua yaliyo matakatifu na yasiyo matakatifu, yaliyo safi na yaliyo najisi. Hivi ndivyo tunavyopaswa kuwa kwenye Imani yetu.

 

* Adamu alikuwa mpweke na ndipo Mungu akampa mwenzi wake ambaye ni mke wake. Hakukuwa na mwanadamu mwingine karibu yao; basi kama mpango wa Mungu ulikuwa ni mwanaume awe na wake wengi basi Adamu ndiye angekuwa ndiye mtu aliyekuwa na uhitaji mkubwa wa kuwa na wanawake wengi. Kalini tunaona kwamba alipewa mmoja tu, peke yake.

 

* Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wa sura na tabia zake; na Mungu ni Mmoja tu.

 

* Mungu aliuchukua ubavu mmoja wa Adamu na kumfanya Hawa mmoja tu. Kwa hiyo ndipo wakafanyika kuwa ni mwili mmoja.

 

* Tendo la kujitwalia masuria lilifanyika kwa nia ya kujipatia watoto wakiume, kama tunavyoona kutoka kwa waandishi wa historia kama vile kina Confucius na kwenye maandiko kadhaa ya Biblia. Utaratibu wa kiurithi wa Kikabila, na pengine mtu anapookoka kutoka kwenye maafa au mazingira ya vita, kulipelekea watu kufanya hivi.

 

Kwahiyo, mtondo wa maisha ya ndoa tangu mwanzo ulionyeshwa kuwa ni ule wa mume kuwa na mke mmoja tu na sio zaidi ya hapo.

 

* Ndoa ni taasisi ya Mungu na ni agano linalofanyika kati ya mwanaume na mwanamke. Mwanamke mwingine anayeingilia anaonyesha kulivunja na kuliondoa agano hili. Na haliwezi kuwa ni maalumu tena na la watu wawili kama lilivyokuwa hapo mwanzo walipokuwa watu wawili kwenye agano lao la kwanza. Kutahitajika marejesho ya agano lile.

 

Kuna mambo fulani yanayofanyika kutokana na asili yake tu, hii ndiyo sababu muhimu ya kusoma Warumi sura ya 1.

 

* Adamu wa kwanza aliyeishi kwenye Bustani ya Edeni alikuwa na mke mmoja tu. Kristo akiwa ni Adamu wa mwisho wa kiroho, pia aliozeshwa mke mmoja tu wa kiroho, taifa la Israeli. Lakini Israeli wakaufuata ukahaba na kuufanya na kumwasi Mungu. Tafsiri ya neno dhambi ni tendo la kuziasi Amri na Shria za Mungu (1Yohana 3:4) na mshahara wake ni mauti. Ili kuwakomboa wanadamu kutoka na udanganyifu unaofanywa na Malaika waliomwasi Mungu (mapepo na mashetani), ilimpasa Kristo afe kwanza na hii ilihitimisha kipindi cha ndoa ya kwanza ya Kristo na taifa la Israeli. Kwenye karamu ya ndoa hii inayokuja ya Mwana Kondoo wa Mungu, Kristo akiwa ndiye mume mmoja tu wa kiroho (2Kor. 11:2) anakwenda kumuoa kimfano mke mmoja tu, Israeli wa kiroho ambao ni Kanisa moja ambalo amelijenga.

 

Mungu alisema, ‘‘Si vema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.’’ (Mwanzo 2:18). Mungu aliumba wanyama na wenzi wao na wenzi wachache kwa maisha yote, lakini wengine hufanya hivyo. Neno “familia” halina maana kwenye himaya ya wanyama. Baada ya uumbaji na tendo la kuwapa majina wanyama, ndipo Mungu akamfanyia Adamu usingizi mzito na ndipo alichua ubavu wake. Mungu alimfanya mwanamke kutokana na ubavu na akasema,

“Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja.”  (Mwa. 2:24).

 

Kwa njia hii, wajibu wa mwanaume ni sawa kabisa na ule ulio kwenye himaya ya wanyama.

 

Kwa jinsi hii nidhamu ya kingono inabakia kuwa ni kiini cha maono ya Biblia kwa maisha ya familia.

 

Umuhimu wa kinasaba wa kuzalisha watoto zaidi kwa haraka unaoonekana kwa wanyama unaofanywa kwa dume kuwa na majike wengi, hata ule wa kuasi madume, ni mambo yasiyokubalika na yanapaswa kuzuiwa na kupigwa vita na wanadamu.

 

Mfumo wa kimitala umeruhusiwa kwenye siku za Biblia lakini, toka kwenye mabishano ya hali asilia ya Bustani ya Edeni, halijawa kuwa ni jambo muhimu. Ni kweli kwamba mtu anaweza kujenga hoja yake kwa kusema kwamba hadithi za Biblia zinazowahusu kina Abraham, Sara, na Hajiri, au Yakobo, Raheli na Lea ni watu shupavu wanaoipinga hii dhana ya mitala.

 

Ikumbukwe pia kwamba dini zote kuu mbili zilizoko kwenye Biblia kwa muda mwingi sana zimeharimisha mtindo kuu wa mitala ingawa dini ya Kiyahudi inaruhusu kiujanya kwa kupitia mtazamo wa baraza la Talmud. Kitabu cha Koran kinakubaliana na mitala kwa sababu zifuatazo:

  1. Upotoshaji ulio kwenye mandiko yajulikanayo kama Hadithi uliotokana na ukosefu wa kushabihiana kati ya Biblia na Koran.
  2. Matendo yatokanayo na desturi na utamaduni wa Wayahudi na Waarabu.

 

Torati inaruhusu kuachana na baada ya hapo unarusuhu kuoa mke mwingine kwa ajili ya ugumu wa mioyo, lakini Mungu anasema kupitia manabii kuwa anachukia sana kuachana. Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kinakubaliana na ukweli kuwa kwa aijili tu ya udhaifu wa kibinadamu ndio uliopelekea iruhusiwe kuachana (soma Kum. 24:1-4). Lakini linaonekana kuwa ni jambo la huzuni, linalotokana na tama ya mwili tu, na lililo mbali na maadili au lisilo la kimaadili. Kwa kweli, nabii Malaki aliandika hivi:

13Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya BWANA kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu. 14Mnauliza, “Kwa nini?” Ni kwa sababu BWANA ni shahidi kati yako na mke wa ujana wako, kwa sababu umevunja uaminifu naye, ingawa yeye ni mwenzako, mke wa agano lako la ndoa. 15Je, BWANA hakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa mke wa ujana wake. (Malaki 2:13-16)

 

Kwa kuzingatia aya hizi, marabi walifundisha kwamba mtu anapomwacha mke wa ujana wake, anaifanya hata madhabahu ya Mungu ilie kiasi cha kutokwa na machozi (Gittin 90b). Bali ndoa inayodumu maisha yote kati ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja ndiyo iliyo sahihi, na ndiyo inayoonekana kuwa ndyo iliyoanzishwa na kuonekana kwenye hiatoria yaBustani ya Edeni. Kwa mapokeo ya Kiyahudi wameipa jina ndoa aina hii wanaiita kiddushin, maana yake ni usafi na utakatifu, ndivyo wanavyoielezea ndoa aina hii. Ni ndoa, ambayo ni tendo la kujitoa kimaagano la mwanaume na mwanamke linalokusudia kuishi hivyo milele huku wakijitenga na kujiepusha na mahusiano ya namna yoyote ya kindoa na wengine, jambo linalotufanya sisi tuwe juu na kututofautisha na wanyama.


Kuna vitu vikuu vitatu ambavyo pia ni dini halali zinazotokana na imani ya Kibiblia. Nazo ni hizi zifuatazo: 1) Kitu ambacho Wayahudi wanakiita halakhah; 2) Mapokeo na kanuni za Kikristo, na kile ambacho kilitokana na Warumi na kuingizwa kanisani kikiitwa kama Kanuni elekevu za kanisa, na 3) Sheria za Kiislamu, maarufu kama Shari'a, ambazo msingi wake ulitokana na kanuni za Biblia na mapokeo ya zama za karne ya saba waliyokuwa nayo Wayahudi na Waarabu. Wote hawa wanahusika na mchakato halali wa kindoa: yaani katika kujua na kuamua kwamba tupi aolewe na yupi. Na ni kwa jinsi hani ndoa inaweza kupaa athari, na ni mambo gani halali au kanuni zipi zifuatwe na kufanywa na wanandoa na wajibu wa kila mmoja wao. Jinsi ya kufanya kama ndoa ikionekana haina budi kuitangua, na kama ikitokea hivyo wafanyeje? Baadhi ya mambo yaliyo kwenye kanuni za Kikristo ni zinapinga kuwa mtu anaweza kuoa tena baada ya kuachana na mkewe. Lakini Biblia inasema wanaweza kufanya hivyo.

 

Dini hizi zote tatu ambazo msingi waake ni kutoka kwenye Biblia zinakubali ndoa ni kitu muhimu kuliko aina yoyote ya agano au makubaliano mengine yote ya kawaida. Kila mara Biblia inaufananisha uhusiano wa mume na mke kuwa sawa na uhusiano kati ya Mungu na taifa la Israeli. Na huenda neno zuri zaidi la kuuita uhusiano huu ni beryith (SHD 1285) – linalomaanisha agano. Mungu huko Shekemu katika kabila kumi za Israeli alikuwa anajiita mwenyewe kuwa ni Berith (al Berith) (SHD 1286) au Agano. Neno agano linaashiria kitu cha milele na kisichotanguka. Neno la Kiingereza linalotumiwa kuuita nchi yao British (Uingereza) linatokana na lugha ya Kisemiti lililotoholewa kwenye lugha ya Kiebrania liitwalo Beriyth au Berith na ish maana yake ni mwanaume, na linamaanisha Mwanaume wa Aagano.

 

Biblia ilianzisha maana kuu mbili za ndoa. Lengo la kwanza ni la kimahusiano, kama inavyosema: ‘‘Si vema huyu mtu awe peke yake" (Mwa. 2:18). Lengo la pili ni kutimiza Amri ya Mungu isemayo "zaeni na mkaongezeke" (Mwa. 1:28).

 

* Matokeo mabaya yaliyomfuatia Daudi kutokana na kuoa wake wengi na tabia ya uzinifu yalikuwa ni makubwa sana. Wawili kati ya watoto wake waligombea kiti chake cha ufalme, na hatimaye mmoja wao alimwua mwenzake. Motto wake mwingine akambaka dada-binamu wake na alipokuwa anarudi akitokea huko, akauawa na kaka yake kabisa. Hatimaye, yule mtoto aliyemuua yule kaka yake mbakaji akaanzisha maasi dhidi ya Daudi na ilikuwa nusura tu afanikiwe. Kipindi hikihiki cha uasi mtoto huyuhuyu akamtwaa na kumweka kinyumba suria wa Daudi mbele ya macho ya Israeli wote. Mwanzoni kabisa, Daudi alikuwa na wake wengi sana lakini hali hiyo haikuweza kukata kiu cha kuwa na mke mwingine, bali alizidi kwenda mbali zadi kiasi cha kumtamani hadi kumchukua mke wa mtu mwingine baada ya kuzini naye, na kudiriki kumuua mume wake ambaye alikuwa ni kamanda mwaminifu sana kwake Daudi mwenyewe. Linganisha maneno haya na 2Samweli 11-13,15-18, ili kupata undani wake zaidi. Daudi alipatwa na hangaiko na maseso makuu sana kwa ajili ya matukio haya yaliyomtokea mfululizo.

 

Njia bora ya kupata kuridhika

 

Ni mawazo na madai ya uwongo kusema kuwa eti Mungu aliruhusu au aliidhinisha mitala ili kumfanya mwanaume awe na hali bora zaidi ya kuridhika, dhana ainayotokana na nukuu za Mandiko Matakatifu yanayoyataja matukio na matendo ya mitala.

 

Huzuni za mwanadamu na mateso yake yote yanatokana na dhambi, ambayo ni uvunjifu wa Sheria na Amri za Mungu (1Yohana 3:4). 

 

Tunaposoma matukio kwenye 2Samweli 12:7-8, tunaona kuwa bidii kubwa zimefanywa kujaribu kufananisha  mgongan au tofauti iliyoko kati ya maandiko haya nay ale ya Kumbukumbu la Torati 17:17. 

 

Maneno na mtazamo ulioko hap ani kwamba Mungu aliruhusu mktala wakati “alipompa” Daudi wake wa Sauli. 

Ndipo Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo BWANA , Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli. Nilikupa nyumba ya bwana wako na wake za bwana wako mikononi mwako. Nikakupa nyumba ya Israeli na Yuda. Kama haya yote yalikuwa madogo sana, ningekupa hata zaidi”.

 

Biblia haijipingi wala kujichanganya yenyewe. Maelekezo aliyopewa mfalme yanayokutikana kwenye Kumbukumbu la Torati 17:17, yanasema:  “Kamwe asioe wake wengi, la sivyo moyo wake utapotoka. Kamwe asijilimbikizie kiasi kikubwa cha fedha na dhahabu"

 

Wazo kuu hapa ni kwamba Mungu hataki wafalme wajilimbikizie wanawake wengi kiasi cha kuwa juu ya Sheria au juu ya ndugu zao. Sheria zinaruhusu kwa wazi sana mtu kuwa na wake wawili au zaidi kwa mujibu wa maandiko, kama tulivyojionea hapo juu kwenye Kumbukumbu la Torati 21:15.

 

Tunapopata jibu la jambo hili toka kwa Mungu kupitia kwa nabii wake Nathani, baadhi ya Wanateolojia Wakristo wanapinga kama tunavyoona kwenye kitabu maarufu cha Kiingereza kiitwacho The Theological Wordbook of the Old Testament (Vol. 1, p. 273, Harris, Archer, and Waltke) yaani (Kitabu cha Mwongozo wa Teolojia ya Agano Jipya, Toleo 1, ukurasa 273, kilichotungwa na Harris, Archer na Waltke).  Kinasema kuhusu neno “kifuani” kwa kutaja maana yake kuwa ni: "Tofauti ya mambo mchanganyiko, mawazo yasiyo halisi  yanayoelezewa kwa neno … Kupewa wake wa zamani wa mfalme kwenye himaya ya mfalme mpya iliyoonekana kuwa ni mamlaka mapya ya mfalme…” Kwa ufupi, neno “kifuani” halina maana ya moja kwa moja ya kuwa na uhusiano wa kingono.

 

Hili linaweza kupingwa kwa mtazamo wa andiko kile anachosema Mathani na kulipuuzia kwa wazi anndiko la Kumbukumbu la Torati 21:15.

 

Kuna hoja iliyojengeka watu wakijiuliza kwamba iwapo kama mitala ni jambo lenye kibali cha Mungu, kwa nini basi Mungu atoe maelekezo yanayopingana wakati akiwa wameamuru kuwa mfalme asijilimbikizie wake wengi (kama ilivyo kwenye 2Sam. 12:7-8). 

 

Hata hivyo, hoja hizi zinaonyesha mkanganyiko kwenye Sheria. Sheria hii inahusisha matendo mengi yaliyo mbali na dhana ya kujituliza ila kama ipo kwenye jamii zetu zinahitaji maelekezo, na mitala ni kama taasisi ya kijamii ni moja wapo.

 

Ukweli ni kwamba mlolongo wa uzao wa Masihi umetokea kwenye ndo hizi za kimitala kwenye mapitio ya mlolongo wa wafalme kwenye mifano mingi kadhaa (soma jarida la Uzao wa Masihi (Na. 119) [Genealogy of the Messiah (No. 119)].

 

Kunahoja kutoka kwa wale wanaopinga kwamba mitala haionekani kwenye upande mzuri kwenye Agano la Kale, na wala hakuna ulipoonekana kuwa ulileta furaha ya kweli popote ulipoonekana mtindo huu wandoa za mitala (Kwa mujibu wa kitabu cha Ufafanuzi wa Maarifa ya Biblia [Bible Knowledge Commentary] kuhusu inayosema Kumbukumbu la Torati 21:15-17).

 

Jinsi waandishi wa kikristo wa zamani walivyoandika kuhusu maisha ya Ndoa Kanisani

 

Kumbukumbu zinaonyesha pia kwamba Kanisa la baadae la Agano Jipya lilikuwa na msimamo mkali sana wa afithina wa kupinga ndoa za mitala.

 

Maandiko ya Justin Martyr, aliyoandika na kuhudumu kwenye kipindi cha kati cha karne ya pili, akiwakemea Wayahudi kwa kuruhusu kwao mitala, kwenye kitabu chake cha Mahojiano na Trypho, Myahudi, [Dialogue with Trypho the Jew], ambacho kilikuwa kinakemea matendo ya Wayahudina mafundisho yao. Kwenye sura ya 134 (cxxxiv) kunakichwa cha maneno kisemacho Ndoa za Yakobo ni Sura ya Kanisa [The Marriages of Jacob are a Figure of the Church] anafafanua kwa kusema:

Iwapo kama mafundisho ya manabii na yake yeye mwenyewe yanakusaidia, ni vema kwako umfuate Mungu kuliko kufuata mambo yako ambayo hayana busara na yenye kukupofusha, ambayo yamewafanya hadi sasa kila mmoja wenu aruhusiwe kuwa na hata wake wanne au watano; na kwamba iwapo mtu atamwona mwanamke mzuri na akipenda kuwa naye, ndipo wanaiga matendo ya Yakobo [aitwaye] Israeli, na ya mababa wengine, na kujifariji wakisema kuwa si vibaya kufanya mambo kama haya; kwa kuwa wamefungwa kabisa wasijue jambo hili.

 

Kisha anaendelea kufafanua zaidi kwa kusema:

“Ndoa za Yakobo zilikuwa ni mfano wa kile ambacho Kristo alikuwa ananda kukitimiliza. Kwa kuwa haikuwa ni vizuri wala jambo jema kwa Yakobo kuoa wake wawili waliokuwa ni ndugu wa tumbo moja kwa wakati mmoja. Na alimtumikia labani kwa ajili ya kumpata binti yake mwingine.

Na ili afanikiwe au kustahili hilo [kumpata] ndugu mdogo, alilazimika kutumika kwa miaka mingine saba. Kwa sasa, Lea ni watu wako na sinagogi lako; lakini Raheli ni kanisa letu. Na kwa hayo na kwa watumishi wa kote kuwili, bado Kristo anawahudumia hata sasa. Kwa kitambo, Nuhu aliwapa watoto wake wawili wa kume mbegu ya watatu kuwa watumishi wao, sasa kwa namna nyingine ni kwamba Kristo amekuja kuwarejesha upya wote, yaani watoto huru na watumwa miongoni mwao, akiwapa heshima liyosawa wale wote wanaozishika amri zake; wakiwa kama watoto wa wake huru na watoto wa wanawake watumwa waliozaliwa kwa Yakobo walikuwa ni watoto wake wote na walikuwa na heshima na haki sawa.”

 (ANF, toleo la 1, ukurasa 266-267)

 

Sura mbili zinazofuatia andiko hili, anaelezea dhana au fundisho Kristo kuwa ni Mfalme wa Israeli, Na kwamba Wakristo ni watu wenye Hadhi sawa na Waisraeli (cxxxv) na kwamba kwa kumkataa kwao Kristo Wayahudi, ni sawa na kuwa Wamemkataa Mungu aliyemtuma (cxxxvi).

 

Hivi ndivyo Makanisa ya Mungu yanavyoamini hadi leo.

 

Irenaeus (120-202) kwa Kuyapinga kwake Mafundisho ya Uwongo (takriban 182-188) aliwaumu na kuwashutumu sana Wanostiki kwa ajili ya mitala, miongoni mwa mambo mengine waliyokuwa wanafanya kwa kusema:

Kwenye sura ya XXVIII, anaelezea kuhusu mafundisho ya Tatian, Muencrati (wenye kujinyima) na wengine waliokuwa wanahubiri wakipinga kufunga ndoa na kwa hiyo anasema wanatoa nje viumbe viumbe asilia vya Mungu. Wanasema kwamba kama walivyokuwa kina Tatian, Marcion na Saturninus, kutangaza ndoa hakuna maana yoyote zaidi ya upotofu, ushawishi na uzinifu tu na wakaenda mbali zaidi wakisema:

“Wale wengine wanaowafuata kina Basilides na Carpocrates, wameanzisha aina ya uzinzi holela na hali ya kuwa na mke mmoja na wanatofautiana suala la kula nyama zilizotolewa sadaka kwa sanamu, wakisema kwamba Mungu hapendezi nayo kabisa matendo kama hayo” (ANF, toleo la 1, ukurasa.353).

 

Matendo yaliyosababishwa na mafundisho mapotofu kwa Kanisa yalizuia pia yalikataza mitala kipindi yalipoanza.

 

Tertullian (145-220) pia aliweka wazi sana akisema: -

Sura ya II ina kichwa cha somo: Ndoa Ni Kitu Halali, Lakini Sio Mitala. Kwa kweli sisi hatuwezi kuzuia ushirikiano kati ya mwanaume na mwanamke, uliobarikiwa na Mungu na seminari ya wanadamu na ukaridhiwa kwa ajili ya kuijaza nchi na kuupeneza ulimwengu, na kwa hiyo ukaruhusiwa tena kwa sherehe na nderemo. Kwa kuwa Adamu ndiye alikuwa ni mume mmoja tu wa Hawa, na Hawa alikuwa ni mwanamke mmoja, mwamke mmoja, ubavu mmoja. Tunajua hivyo kutoka kwa mababa zetu waliopita na kwa wazee wetu wenyewe, kwamba iliruhusiwa sio kuoa tu, bali hata kuongeza wake [ruhusa ya kuwa na mke mmoja au kuwa na wake wengi]. Pia kulikuwa na masuria {nyakati hizo]. Lakini ingawa lilikuja kuwa ni kitu chenye mfano wa kuigwa kwenye sinagogi, bado  (kwa tafsiri sahisi) ilikuwa muhimu kuanzisha (kitu Fulani) ambacho hatimaye kingestahili ama kuzuiwa au kutengenezwa vizuri. Kwa kuwa sheria ilikuwa (kwe kipindi muafaka) kutungwa, (Kama hii ilitosha) ilikuwa inafikia kwenye sababu kwa kufanya mapungufu ya Sheria iweze kutumika tena (yeye aliyekuwa anatakiwa kuyafanyia kazi mapungufu hayo). Na kwa hiyo kuifanya Shria kwa sasa ichukue mahala pa Neno la Mungu zikielezea kutahiri kulikoamriwa na Maandiko Matakatifu. Kwa hiyo kwa ajili ya leseni iliyo pana ya siku hizo, karatasi za kufanyia marekebisho zilikuwa zimeisha kabla yake, ni karatasi ambazo Mungu kwa Injili yake, na kisha mitume waliokuwa kwenye siku za mwisho zama ya [Wayahudi], ambao ama waliziongoa zile zisizo na umuhimu au waliepusha hali ya mtafaruku. (ANF, Vol, IV: Tertullian, IV, Kwa Mkewake, Bk. I, sura ya II, kurasa 39-40)

 

Tertullian anafafanua kwa kina sana kuhusu mabadiliko ya sheria kwenye uandhishi wa kitabu chake kiitwacho Katika Kushawishi Usafi ANF, Toleo la IV, ukurasa wa 53,56-58, [On Exhortation to Chastity (ANF, Vol. IV, pp. 53,56-58)] na pia kingine cha Ndoa ya Mke Mmoja Ukurasa 59-72 [On Monogamy (ibid., pp.59-72)]. Imeandikwa kutoka kwenye mtazamo wa maisha ya useja na ni kinyume na mafundisho yatokayo na Maandishi Matakatifu na Amri za Mungu.

 

Kutoka Sura ya VI (ukurasa wa 53) “anajibu” kikwazo cha mitala walichokutananacho mababa wa kale. Anapinga kwamba amri ya kuzaana na kuongezeka iliyoandikwa kwenye Mwanzo 1:28 tayari imeshatolewa kwa kanuni ya kufurahia hali ya kutawala tamaa za mwili. Wakati umeshafika na kipindi kutimia, na wale wenye wake wajione kama hawana.

 

Matawi ya miti ya mambo ya kikale yanadhaniwa kuwa yamesha pukutishwa na injili na shoka limewekwa kwenye mizizi. Dhana ya jicho kwa jicho na jino kwa jino imeshapitwa na wakati na mafundisho yanasema “msimlipe mtu uovu kwa uovu” mafundisho yanayoendela leo kama tuyaonavyo.

 

Kwa hiyo anayachukulia maandiko kutoka kwenye kitabu cha Mambo ya Walawi tanayotia moyo wa kutokuwa na wake wachache, ambayo haipo tena (Sura ya VII kitabu hicho hicho., ukurasa wa 54).

 

Kutoka kwenye Sura ya VIII (ya kitabu hichohicho) anaendela kuishambulia dhana ya kuwa na mke wa pili au ndoa ya pili na akkandika kichwa cha habari kisemacho Katika Ndoa ya Mke.

 

Kwa hiyo, anapinga uwezekano wowote kwa wanawake waumini Kanisani kuolewa tena kwa vyovyote baada ya waume zao kufariki na kujenga hoja yake kwamba sheria za Levirate zimekoma na kwamba kwa kuwa kila Kanisa lina ndugu wa mwanamke anayeweza kumuoa ndugu yake ambaye ameondolewa kwa sasa. Andiko hili halina mashiko kwa mujibu wa Biblia. Anakazia kudai kwamba mwanaume ambaye mke wake amefariki anapaswa amuoe mwanamke kijana mwenye uzazi ili amzalie watoto, kuliko kumuoa mwanamke mzee ambaye atamfanyia kazi ya kumtunzia nyumba yake tu. Hoja hizi zinatokana na mafundisho mapotovu ya kikundi cha watu wa jamii inayojikana ijulikanayo kama Wamontani ambayo hayana mashiko yoyote.

 

Kwa hiyo Kanisa limeondokana na Amri za Mungu kidogokidogo na kuingia kwenye utaratibu wa kuzitafsiri Amri hizi kiroho tu. Tertullian alikuwa anaandika akiwa Afrika kwa lugha ya Kilatini kwa niaba ya maandiko yaliyohitilafiana ya Wamontana na akielekeza pia mabadiliko yaliyorithiwa kutoka kwenye karne ya tatu. Hii inaonekana kuwafaa Wamona ambao hatimaye walichukua hatamu za Kanisa Katoliki la Roma, na kwa kuwa walikuwa wanayaunga mkono mambo mengi miongoni mwake.

 

Methodius (260-312) au Eubulius, alikuwa ni Askofu wa Olympus na Patara na kwa wakati mmoja huo huo alikuwa wa Lycia na aliondolewa na kupelekwa huko See iliyoko Tiro, kwa mujibu wa Jerome, na aliuawa shahidi mwaka 312 huko Chalcis. Alikuwa na hoja kwamba mtindo wa mitala ulikatazwa siku za Manabii.

 

Anafanya hivyo kwenye Sura ya III kwa undani zaidi, akinukuu maandiko yaliyo kwenye kitabu cha Mhubiri 18:30 na 19:2. na kwa hiyo anaitumia Mithali 5:18 na Yeremia 5:8 na pia anatumia kitabu cha Hekima 4:3. Anasema:

“Tendo la kuchanganya ndoa na wake wengi kumekoma tangu siku za manabii kwa kuwa tunasema, 'Usiziendee tamaa zako za kimwili, bali ujizuie na tamaa ya kunywa mvinyo na wanawak ambavyo vimewafanya wanaume waangukemaanguko makuu.”

 

Kwenye aya hii, kwa kiasi kikubwa ananukuu maandiko yaliyo kwenye vitabu visivyorasmi vya apokrifa. Anajaribu kujenga hoja yake kwenye maisha ya useja dhidi ya ndoa uzaaji wa watoto kwa kutumia maandiko yasiyo na uvuvio wowote na yaliyoondolewa kwenye Kanuni ya Maandiko Matakatifu. Anapinga pia kwamba hapo mwanzo Biblia ilikataza ndoa za kuchukuana wanaume na dada zao, na kisha akaenda kwenye ndoa ya mke mmoja na hatimaye kwenye useja. Anaamini na kupinga kwamba wale wanawali 144,000 walioandikwa kwenye kitabu cha Ufunuo kuwa ni wanawali wa kweli, akikosea kabisa na kupotosha ujumbe.

 

Anaendelea mbele pia kwa kusema:

...Na kuna mahala pengine panasema, “Chemchemi yako na ibarikiwe na ufurahie mke wa ujana wako”. [Mithali 5:18], panaonekana kukataza ndoa ya mke mmoja. Na Yeremia anatoa jina la “farasi waliolishwa” [Yeremia 5:8] kwa wanaotamani wanawake wengine”…

 

Yeremia anaichukulia hali hii kuwa ni uzinifu mkubwa na wa makusudi, na anaupotosha ujumbe wa nabii.

 

Anarejea kwenye kitabu cha Hekima 4:3 kwa hali inayojitokeza ya kuwakana watoto wan je ya ndoa kuwa hawahusiki wala kuwa na uhusiano na ndoa nyingi wakati kwamba hakuna maandiko yanayounga mkono jambo hilo [Karamu ya Wanawali Kumi, au Kuhusu Maisha ya Useja, ANF, toleo la 6, ukurasa wa 312. (Banquet of the Ten Virgins, or Concerning Chastity, ANF, vol. 6, p.312)].

 

Ni katika kipindi hikihiki ambacho mafundisho mapotofu ya Wabinitaria yalikuwa yameshaanza tayari. Na vuguvugu la Umamboleo lilikuwa limeshaanza pia tayari. Ami za Mungu zimekuwa zikipingwa kila mara, na hasa na watu wenye itikadi ya useja na kujikana.

 

Maandiko ya Uwongo yanayodaiwa kuwa ya Clementine, ambayo yameandikwa kwa mtindo wa kimafumbo-tata yaliandikwa baada ya mwaka 211 (baada ya kupanuliwa kwa zingatio la hali la Waroma ambalo liliandikwa na kutokea siku za utawala wa Caracalla; na kabla ya mwaka 231 ambao kazi hii imetajwa kufanyika na Origen [Ufafanuzi wa Kitabu cha Mwanzo (Commentary on Genesis)], ambacho kwa namna ya kijanja sana kinamadai  mengi kuwa kipindi cha zama za mwanzoni sana kulikuwa na matukio ya kujivunia kuhusu jinsi Mtakatifu Thomas alivyofundisha masomo ya Kiparthia [inadhaniwa kuwa ni desturi ya Wairani] ya kuachana na mitala. Lakini huu ulikuwa ni msimamo unaoendela na mtazamo wa mwandishi uliorekodiwa kwa pamoja na warekodiji bandia.

 

“Lakini nitatoa uthibitisho wenye maana zaidi wa mambo haya na kukupa, tazama, kwa ufupi tu niseme, tabriban miaka saba imepita sasa tangu tukio la Nabii mtakatifu na wa kweli, na yaliyofuatia ni hali ya mataifa yote kuja Yudea, na kufanya ishara na miujiza waliyoiona, na kwa ushamiri wa mafundisho yake, alipokea imani, na kisha wakarudi kwenye nchi zao, ambako waliziacha desturi potofu za dini zao za Kipagani na desturi za ndoa walizorithi kutoka kwa mababu zao wa kale. Kwa ufupi ni kusema, miongoni mwa Parthian—kama Thomas anayeihubiri Injili kwenye eneo lao, ametuandikia na sio watu wengi sasa wanaopendelea maiha ya mitala; na hakuna mtu miongoni mwa Wamedi anayeendelea kuwatupia wafu wao kwa mbwa; na wala hakuna hata Mwajemi anayependa tena kulala na mama yake, au kufunga ndo na ndugu yake wa karibu, yaani dada yake, wala hakuna mwanamke wa Msusian anayefanya uzinzi wa aina iliyoharimishwa au kukatazwa na wala hakuna matendo ambayo kwa mujibu wa kitabu cha Torati yangeweza kumtia mtu hatiani ambavyo mafundisho ya kidini yaliyaita haramu na kuyakataza.” (ANF VIII: "Toleo la IX: Sura ya XXIX.-chenye kichwa cha Injili Inanguvu Zaidi ya ‘Torati'" ukurasa wa 189)

 

Kutoka kwenye Mtaguso wa Elvira (mwaka 295-302), ndipo maisha ya useja yalirasimishwa kwa maagizo maalumu yakiwalenga maofisa wa kanisa wa madaraja matatu yaliyotuama kwenye mifumo ya imani ya Kimodali na ile ya Kibinitarian, kwa maaskofu, makasisi na mashemasi.

 

Wakaamriwa kwamba iwapo kama wataendelea kuishi na wake zao baada ya kusimikwa kwenye madaraja hayo, basi wataondolewa kwenye nyadhifa zao.

 

Mtaguso wa Ancyra iliyoko Galatia (mwaka 314) (kwa mujibu wa kitabu cha kanuni maarufu kama “Canon” x) ulikataza hata mashemasi kuoa baada ya kusimikwa kwenye huduma hii.

 

Mtaguso wa Neo-Caesarea (Kaisaria-Mpya) iliyoko Cappadocia (Kapadokia), (mwaka 315) (Kwa mujibu wa kitabu cha Canon I) ndio uliowakataza makasisi kuoa baada tu ya kusimikwa kwenye huduma.

 

Baada ya Mtaguso wa Nicaea (Nikea) (mwaka 325), ndio ulikataza kusiwepo na askofu, kasisi wala shemasi atakayeruhusiwa kuishi kwenye nyumba moja na mwanamke isipokuwa tu kama ni mama yake, dada yake au shangazi yake. Mtindo wa maisha ya Useja ulianzishwa na kuingizwa kwenye mfumo huu wa imani ya Kiathanasi na mtindo wa ndoa ya mke mmoja ulianzishwa na kurasimishwa kwa watu wengine wa kawaida na walei wa kanisa.

 

Nchi ya Uingereza chini ya mfumo wa watu mchanganyiko wa lugha zinazofanana maarufu kama “Anglo-Saxons”, wazee wa kanisa waliruhusiwa kuoa na kuishi na wake zao ki waziwazi sana. Katazo la Kanisa Katoliki la Roma halikupata nguvu kwa madai kwamba watu wa jamii ile ya Kianglo-Saxons walikuwa ni wakali sana wakitumia neno la Kilatini “preost” na kwamba wasingefaa kwa kazi ya ukasisi. Neno muafaka lilikuwa ni Kasisi Mwenye Kuhudumu Madhabahuni na Kushirikisha Ushirika Mfatatifu (Maesse-proest) kutumika kuelezea wadhifa au mamlaka ya kikasisi na wanaaminika kuwa walikuwa ni waseja [soma Kitabu cha Fasiri ya Maneno cha Kikatoliki, Toleo la III ukurasa 486 (Catholic Encyclopaedia, Vol. III, p, 486)].

 

Haikuwa hivyo huko nyuma hadi kwenye Mtaguso wa Kwanza wa Lateran ulioweka msisitizo wa kulazimisha amri hizi.

 

Inafanya rejea za kipindi cha ‘utakaso kwa wenye nda za mitala. Katika kipindi kile, watenda dhambi walitengwa na kukaa ‘nje’ ya Kanisa na kusimamishwa kushiriki shughuli zote za Ushurika hadi watakapoonekana kuwa wamebadilika kutoka tabia zao. Na iwapo kama dhambi itaonekana kwenye kipindi hiki cha Kutengwa kwao Kikanuni, ilichukuliwa kama ni ‘dhambi mbaya’—na ndoa ya mitala ilikuwa ni mojaq wapo.

 

Makasisi wa Nestorian waliruhusiwa wakati wote kuoa na waliweza kuoa mara ya pili au ya tatu (kitabu cha CE, ukurasa wa 488).

 

Kwenye Kanisa la Wamarekani, kwa sababu fulani na ndogo, bado makasisi wanaruhusiwa kuoa (kitabu cha CE).

 

Askofu Basili wa Kaisaria kwa miaka ya (329/330-379) na (370), aliuelezea mtindo wa mitala kwenye barua zake kuhusu kipindi ambacho mitala ilikatazwa kwenye kanisa. Alielezea mitala kama ‘ni kikomo cha uzinifu’. Kwa hiyo, kipindi hiki kulikuwa na aina ya mitala ya wanawake kuwa na wanaume wengi, au wanaume kuoa wanawake watatu na zaidi.

 

Anaandika hivi:

Kwenye barua yake ya IV. Kwa ajili ya mitala ya wanawake watatu na wanawake wawili waliweka amri hii hii kwa kulinganisha na suala la talaka rejea iliyojulikana kudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja cha mkataba wao (pengine inadumu kwa miaka miwili); na kwa wenye wake wanne iliyogawanyika kwa maeneo matatu na pengine miaka minne, ila hii haiwezi kuchukuliwa kuwa ni ndoa kabisa, ila ni kama mitala na inakuwa ni uzinzi tu. Ni kwa ajili hii ndio maana Bwana alimwambia mwanamke wa Samaria ambaye alikuwa anaishi na wanaume watano “Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanamume unayeishi naye sasa si mume wako!" Hawahesabii wale waliozidi kikomo cha ndoa ya pili kuwa wanastahili heshima ya kuitwa bwana au mke. Kwa ajili ya mitala ya wake watatu tumekubaliana na kungojea kwa miaka mitatu, lakini sio kwa mujibu wa kanuni lakini ni kwa kuyafuata mapokeo ya wazee weetu wa zamani. Aina hii ya machukizo hayapaswi kuharimishwa ama kukatazwa yote kwa pamoja kwa maslahi ya Kanisa, bali yanapaswa kuchukuliwa kama yanastahili kusikiwa baada ya miaka miwili au mitatu, na baadae yaruhusiwe kuwa sehemu zao, bali yanapaswa kutunwa kutoka kwenye kundi la zawadi nzuri na vinapaswa tu virudishwe kwenye kwenye kundi baada ya kuonyesha matunda ya toba.”

 

Kwenye barua hiyohiyo ya VI anasema:

“Tendo la uzinifu kwa mtu aliye kwenye daraja la uongozi halipaswi kuchukuliwa kama ni ndoa tu, na uhusiano wao unapaswa kukomeshw,akwa kuwa yote mawili yanafaida kwa usalama wa kanisa na kutawazuia wapotoshaji wasiweze kuwa na sababu ya kutushambulia, kana kwamba tunawashawishi wanaume wajiunge na sisi kwa kuwavuta kwa dhambi za wazi.”

[Kwa mujibu wa kitabu cha Kitabu cha Pili cha Makasisi Zama Baada ya Mtaguso wa Nikea, Toleo la VIII, Na kile cha Amphilochius, kihusucho Kanuni za Mapokeo, Waraka wa CLXXXVIII (uitwao kwa Kilatini, Canonica Prima) [Nicene and Post Nicene Fathers Second Series, Vol. VIII, To Amphilochius, concerning the Canons. Letter CLXXXVIII (Canonica Prima.)] ulioandikwa mwaka 347, ukurasa wa 223, 226.)

 

Sasa, mtazamo huu unatofautiana hata na hali aliyokuwanayo rafiki yake mwenyewe aitwaye Gregory wa Nazianzus ambaye alishindwa. Gregory alimuoa Nonna na akawa na watoto watatu, Gregorius Mruzukiwa, Ceasarius na Gorgonia. Familia ya Basili ndiyo waliyotoka Mtakatifu Macrina, Gregory, askofu wa Nyssa na Petrus, askofu wa Sebasteia. Mjomba wake alikuwa ni Askofu wa Gregorius.

 

Basili anayafananisha maandiko haya na mifano ya mfumo wa kipagani wa Kirumi na anaonekana kuyahusisha haya kutoka kwenye maandiko ya Biblia. Anafananisha na Flamen na wastani wa Pontificus na Vestals wakiwa ni mifano.

 

Kwa hiho, kwa kipindi hiki matendo ya Athanasian yalikuwa yameanza kama mfumo wa Kibinitari na ulibidi uendelee na Basili na wote wawili kina Gregory walioanzisha imani ya Utatu. Na sasa walikuwa wanazikataa aina zote za ndoa zizozokuwa za mke mmoja tu ndizo zilizoruhusiwa kuwa rasmi na kukubalika na Kanisa, na kuziacha ndoa za mitala mbele ya viongozi wa Kanisa na kukataza matendo ya kuachana na kupeana talaka na hali ya kuoa mke tena. Kwa maneno mengine ni kusema kuwa wale walioachana hawakuruhusiwa kuoa tena, bali walilazimika kuishi useja bila kuoa au kuolewa tena, hata kama waliachwa na mwenzi ambaye alikuwa sio muunini wa imani yao, jambo ambalo lilikuwa ni kinyume na yanavyosema Maandiko Matakatifu. Tunaona kutoka kwenye uandishi wake kwamba Basili aliyatafsiri vibaya mafundisho ya Kristo aliyomwambia yule mwanamke aliyemkuta kwenye kisima cha Samaria.

 

Mfumo wa mitala umeenea na kukubalika na vikundi vingi sana vinavyoiamini biblia na sio kwa Waislamu peke yao.

 

Mtindo huu wa mitala umekubaliwa na waumini wa zama za kale maarufu kama Aanabaptists wa Munster, na inaaminiwa pia kwamba walikuwa na wake wengi kuliko, hali waliyokuwanayo hata kabla ya kipindi cha kuzingirwa, kwa mujibu wa Weber (kitabu chake  CE, Toleo la 1, ukurasa wa 446).

 

Imani ya Kibudha

 

Imani wa Budha inaamini kuwa kuishi maisha ya useja ni moja ya utoshelevu wa kimaisha, ila inachukuliana na maisha ya mitala na talaka na inaunga mkono kufanya hivyo. Inaelezea kwa wazi sana kuhusu maisha ya wake wengi aliyokuwanayo kiongozi wa imani yao, yaani Budha kabla hajaingia kwenye maisha ya dini na pia jinsi kundi la watu Bimbiassasa, kuwa ni jamii iliyotofaiti ya kifalme. Mfalme wa Thailand katika mwanzoni mwa karne ya ishirini aliliharamisha jambo hili. (CE, kitabu hikihiki, ukurasa wa 773).

 

Makabila mengine

 

Mitala imekuweko pia maeneo ya Kaskazini na Kati ya bara la Afrika miongoni mwao ni Wakongo na kwenye nchi zinazolizunguka Ziwa Victoria na ukanda huu wote. Ni jambo na maisha ya kawaida kwa watu wa maeneo haya na yamewakumba pia hata wale wanaodai kuwa ni Wasabato kwenye maeneo yale.

 

Pia limekuwa ni jambo la kawaida kwa makabila mengi ya Kihindi.

 

Angalizo

 

Tunapopinga mfumo huu wa kuwa na wake wengi kwa kutumia aina mbalimbali za maelezo, tunaona jinsi inavyopingana na kutoka kwenye kitabu cha Mwanzo 2:23-24 ambako inasema kwamba, "Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe."Andiko hili halionyeshi uwingi, na kwa hiyo tunajionea wenyewe hapa kwamba Mungu hasemi kwamba mwanaume ataungana na wawakeze “wawili”. Bali anasema kwamba mwanaume ataungana na “mkewake” mmoja.

 

Mtume Paulo anaufananisha uhusiano wa mku na mume kuwa sawa na ule wa Kristo na Kanisa. "Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa,… (Waefeso 5:23). Kwenye Waefeso 1:22,23 tunaambiwa kwamba Kanisa ni mwili wa Kristo. Kuna mwili mmoja tu (Waefeso 4:4); na kwa hiyo kuna Kanisa moja tu. Kuna walioweka hoja zao kwamba mtu anaweza kuwa na wake wengi awezavyo kama Kristo alivyo na makanisa mengi. Kwa hiyo, hoja za kuwa na wake wengi wa Kristo zinaendelea na kuenea. Hoja inayofanywa hapa ni kwamba kuna kanisa moja tu hapa na kwamba anapaswa kuwa na mke mmoja tu. Agano la Jipya haliongelei habari ya mtu (mmoja) kuwa na wake (wengi) na kwamba hiyo ni sawa machoni pa Mungu. Bali Mungu anasema kwamba mwanaume na ampende mke wake kama Kristo alivyolipenda Kanisa (Efe. 5). Kristo alilifia Kanisa. Na mwanaume anapaswa kuwa tayari kumfia mkewake.

 

Inaonekana kuwa mfumo huu wa mitala unatokana tu na tamaa za mtu binafsi na ubinafsi walionao wanaume.

 

Ifuatayo ni hadithi ya kweli. Kulikuwa nwa mwanaume wa Kichina aliyekuwa na wake wanane. Alikuwa mwenye hali nzuri kipindi cha umri wake wa miaka 50 alipokuwa anakula mlo wa mchana na rafikizake na kuwasimulia matatizo anayokumbana nayo katika kuamua ni mwanamke gani miongoni mwao ambaye atamkuchukua na kwendanaye nyumbani kwao anapokwenda kusherehekea kwa mara ya kwanza sherehe za Usiku wa Mwaka Mpya wa Kichina ili akashirikinaye mlo wa jioni wa umoja wa jumuia yao ya kuikoo. Alipoulizwa ni kwa nini basi aliamua kuoa wanawake wanane, alijisifu na kusema kuwa hakuwa na jinsi nyingine kufanya bali kuwa na wanawake hawa saba wengine kwa madai kwamba wanawake hawa saba walitaka kujiua iwapo kama asingewaoa.


Ili kujua jinsi maisha haya ya mitala kisawasawa na kuchunguza matatizo yaliyosababishwanayo kwenye familia, utagundua kuwa ni jambo la busara sana kurudi nyuma na kuangalia mwanzo wa maisha ya mwanadamu na mwanzo asilia unaofanana wa utakatifu uliotokana na kuanzishwa kwa maisha haya ya ndoa, na jinsi ilivyoanzishwa na Mungu wa Pekee na wa Kweli, Eloah, kupitia kwa Elohim kwa watakatifu ambao ni wanadamu. Malaika Mkuu wa Mungu ambaye ni “nyota ya asubuhi” (soma jarida la
Lusifeli: Mbeba Nuru na Nyota ya Alafajiri (Na. 223) [Lucifer: Light Bearer and Morning Star (No. 223)] au wana wa Mungu, au malaika wa Mbinguni hawaoi na wana wa ufufuo wakisha fufuliwa kutoka kwa wafu watafanana na hawa malaika kwamba nao hawataoa.

 

Kwa hiyo, ni jambo la busara sana kwetu kwamba tuyatafute mapenzi ya Mungu na roho wake aliowaumba ili watuhudumie (yyani malaika au wajumbe wake) kuhusu jambo hili la mitala na matatizo yatokanayo na jambo hili. Ni wapi basi tunakokwenda kutoka hapa ili kutafuta na kupata majibu na hali halisi iliyokuwa kama kigezo cha jambo hili ambalo mataifa yanataabika leo?

 

Kizazi cha Adamu ukimwongoa Nuhu na familia yake, waliangamizwa kwenye Gharika Kuu kwa ajili ya maovu yao na jinsi walivyojiharibu njia zao wakati wa Nuhu. Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa tena katika siku za mwisho:


2Petro 3:3 inasema: Kwanza kabisa ni lazima mfahamu ya kwamba siku za mwisho watakuja watu wenye dhihaka wakidhihaki na kuzifuata tamaa zao mbaya.

 

Kwenye sura ya sita ya kitabu cha Mwanzo, tunakuta kwa kifupi habari ya tukio lililotokea ambalo maranyingi linadharauliwa, huenda ni kwa sababu linachanganya. Jambo lenyewe linatika kwenye andiko hili:

Watu walipoanza kuongezeka idadi katika uso wa dunia na watoto wa kike wakazaliwa kwao, wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa ye yote miongoni mwao waliyemchagua. Ndipo BWANA akasema, “Roho yangu haitakaa ndani ya mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.’’ Wanefili walikuwako duniani siku hizo, pia na baadaye, hao walizaliwa na binti za watu wakati wana wa Mungu walipoingia kwao na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo. (Mwanzo 6:1-4).

 

Uzao uliotokana na mwingiliano huu unaitwa Wanefili. Biblia tulizonazo za Kiingereza zimetafsiriwa kutoka kwenye lugha ya Kiyunani na neno lililotumika walipotafsiri lilikuwa ni “majitu” ambayo ndiyo maana halisi kwa Kiingereza wakati kwa Kiyunani inamaanisha ni “wakazi wa duniani”, jambo ambalo ni geni na halina uzito sana wala kueleweka vizuri kwa sababu watu wote walikuwa ni wakazi wa humu duniani. Kwa hiyo inachanganya kuona ni kwa nini kunautofauti fulani maalumu? Ni kwa kuwa watu hawa walikuwa ni wenye nasaba mbili, yaani walikuwa nusu ni wanadamu na nusu ni malaika, yaani ni uzao wa malaika, ambao kwakuwa walikuwa nusu wanadamu, walifungamanishwa na mvuto wa dunia na kuwalazimu waishi hapa Duniani. Neno la Kiebrania la Kiebrania la Nephilim” yaani Wanefili, ambalo linatokana na neno asilia la nephal”, ambalo maana yake ni malaika waasi. Kwa hiyo, walikuwa ni wana wa malaika walioasi na wanawake ambao walikuwa na nguvu za asili na ambao walikuwa wamewa na funganano na Dunia. Inaleta maana zaidi tunapoliangalia shina la neno hili. Kwa hiyo, malaika hawa waasi walikuwa kinyume na mapenzi na mbo yote ya Mungu na wakafanya ngono na wanawake waliotokana na uzao wa (soma jarida la Wanefili (Na. 154) [The Nephilim (No. 154)].

 

Ili kuonyesha jinsi Siku za Mwisho kutakavyotokea ukengeufu, Biblia inatumia mlinganisho pamoja na mafundisho ya moja kwa moja. Kwenye Mahubiri yake ya Mlimani, Kristo anasema:

“Hakuna ajuaye siku wala saa, hata malaika mbinguni hawajui wala Mwana, ila Baba peke yake. 37Kama ilivyokuwa wakati wa Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia kwenye safina, 39nao hawakujua lo lote mpaka gharika ilipokuja ikawakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa atakapokuja Mwana wa Adamu. 40“Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mwingine ataachwa. 41Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja, mmoja atatwaliwa, mwingine ataachwa (Mathayo 24:36-41).


swali la kujiuliza ni kwamba, “Je, tendo la kuoa na kutoa unyumba kulikoelezewa na Bwana wetu Yesu Kristo kulimaanisha wanawake wa siku za mwisho (au huenda hata leo) utagharimu kama ilivyokuwa siku za Nuhu, au alikuwa anamaanisha kuwa watu wataendeea kuoa na kuolewa kama kawaida?” Yesu anadokeza kuwa ujio wake utatanguliwa na hukumu na maafa kwa kiwango kinachofananishwa na Mafuriko, ambayo yaliangamiza kila kitu chenye pumzi na uzima Duniani. Anasema kwamba siku za Nuhu zinafananishwa na ujio wake sio kwa kiwango cha kutolea mfano tu, bali pia kwa sharti la maisha kwenye jamii hapo baadae. Kwa maneno mengine, katika Siku za Mwisho, watashukia kwenye udhaifu na maovu makubwa sawa na yale aliyoyaona Mungu yakitokea hapa duniani wakati wa Gharika Kuu.  Yesu anazitaja dalili kuu na mashuhuri tatu zilizotokea siku za Nuhu: (i) kula na kunywa; (ii) kuoa na kuolewa; na (iii) kudharau habari ya kuwepo kwa hukumu.

 

Kushindwa wao watu walioishi siku kabla ya gharika kuu kuamini kuwa kungetokea ghhabu ya Mungu ili kuahukumu kwa matendo yao ya dhambi kulionekana kuwepo kwa mazoea mengine yaliyoenea miongoni mwao, ambao yalikuwa ni ukengeufu. Kumbukumbu za kitabu cha Mwanzo hazina mashaka kuonyesha kulikuwako na ukengeufu, siku za Nuhu ambao ilipindukia kiwango na kuwaathiri watu wote waliokuwako duniani kwa wakati ule. Adamu alikuwa na watoto wa kiume wengi na mabinti, akiwemo Abeli, mtoto aliyekubalika ambaye aliuawa na ndugu yake Kaini, lakini Biblia haina zuri lolote inalolielezea kuhusu watoto wengine waliobakia isipokuwa Sethi tu. Ni katika kipindi hiki cha siku za Enoshi mwana wa Sethi ndipo watu walipoanza “kuliitia jina la BWANA” (Mwanzo 4:26).

 

Tunaposoma matukio haya tunadiriki kuamini kwamba Enoshi alisaidia kuleta uamsho wa kiroho miongoni mwa watoto wake au uzao wake maarufu kama Wasethi na kuenda na walikuwapo na wengine pia. Ilikuwa ni kwenye mlolongo huu wa uzao wa Sethi zaidi kuliko uzao wa Kaini ndio anaotokea Enoko, mtu aliyejaaliwa kupata upendeleo wa Mungu na ambaye Mungu alimtwaa na hakuona mauti. Kisha baada ya karne kadhaa baadae, mnamo miaka 1500 baada ya kuubwa kwa mwanadamu, matendo ya haki na utakatifu yalilikuwa karibu yatokomee kabisa usoni pa Nchi. Lakini mtu mmoja tu, Nuhu ndiye aliyekuwa amebakia kuwa mtu wa “haki” na “mkamilifu” na “aliyetembea na Mungu” (Mwanzo 6:9). Nuhu "akapata kibali machoni pa BWANA" (Mwanzo 6:8), lakini waliobakia wote walimfikisha kwenye hali ya Mungu kujuta ni kwa nini aliwaumba.

 

5BWANA akaona jinsi ambavyo uovu wa mwanadamu umekuwa mkubwa duniani na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. 6BWANA akasikitika kwamba alimwumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko. 7Kwa hiyo BWANA akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niyemwumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kwa kuwaumba.’’

 

Nuhu na watu wa nyumbani mwake wote waliokoka. Inadhaniwa na kuaminika kuwa watu wanane tu ambao walikuwa ni Nuhu, Shemu, Hamu na Yafeti na wake zao ndio waliokoka. Inaaminika kuwa hawa wote walikuwa ni waume wa mke mmoja. Na hapa ndipo mahala pengine tunapojengea hoja kwamba Mungu alianzisha ndoa iliyokuwa na mwonekano wa mke mmoja na mwanaume mmoja na ndivyo alivyofanya kwenye Bustani ya Edeni, ambayo iko wazi kwenye Maandiko Matakatifu. Hata hivyo, inawezekana kuwa inawataja wanaume peke yao hii ni kwa kuwa wanawake wlikuwa hawatajwi kwenye mlolongo wa uzao wao.


kwa hiyo, tunapaswa kuyatafuta mapenzi ya Mungu ili tuamue na kuaona kama ni ndoa ya mke mmoja tu ndiyo iliyokusudiwa na Mungu kwetu, au ni kama ni ndoa ya wake wengi ndiyo iliyokusudiwa?

 

Kuna maandiko mengine ya kinabii yanayoonekana kama yanaashiria hali hiyo ya kurudishwa kwa mfumo wa mitala katika Siku za Mwisho.

 

Nabii Isaya anasema kwamba katika Siku za Mwisho wanaume wa Israeli wataanguka vitani na uharibifu utakuwa ni mkubwa sana kiasi kwamba kutakuwa na uhaba wa wanaume na kutakuwa na simanzi na sononeko kubwa kwa wanawake.

“Katika siku ile wanawake saba watamshika mwanaume mmoja wakisema, “Tutakula chakula chetu wenyewe na kuvaa nguo zetu wenyewe, ila wewe uturuhusu tu tuitwe kwa jina lako. Utuondolee aibu yetu” (Isa. 4:1).

 

Kifungu hiki cha Maandiko Matakatifu na unabii wa Siku za Mwisho. Vinahusu jinsi Israeli itakavyofanyiwa matengenezo mapya ya kiroho na jinsi watakavyomrudia na kumgeukia Mungu kwa kicho na utakatifu. Maandiko hayawezi kutanguka na kwa hiyo jambo hili litakuja kitokea na litatokea kwa mujibu wa amri za Mungu na kufanywa kwao upya Israeli

 

Wanawake watakaobakia watagundua ukweli kuhusu dhami zao, na hali ya watoto wao na umuhimu wa ndoa zao kwenye kipindi ambacho kutakuwa hakuna wanaume wakutosha wa kukidhia haja zao. Sheria za kimaadili za kisasa zihusuzo mambo haramu zitaangaliwa upya na kurekebishwa. Tafsiri ya Knox inajaribu kudhania kuwa andiko hili kuwa linataja mambo ya aibu kwa watu wasio na watoto na watu tasa. Hata hivyo, neno lililotumika kwenye kitabu cha fasihi cha SHD 2781 linaitaja aibu kuwa ni kitu kinachowahusu wa jinsia ya kike kwa maumbile yao zaidi kuliko kumaanisha hali ya wao kushindwa kuzaa wana. Aibu ina maana zote mbili. Ukweli ni kwamba kuna wanawake wengi zaidi na wanaume ni wachache na watoto wanapaswa kulelewa kwa mujibu wa maadili na mazingira ya kibiblia, na itakuwa hivyo sawa na unavyosema unabii.

 

Kwahiyo, Torati inaruhusu ndoa za aina hii palipo na sababu muhimu, na ndivyo itakavyoruhusiwa tena katika Siku za Mwisho kipindi cha marejesho mapya, kama ilivyotabiriwa na nabii Isaya. Hatahivyo, sio hali halisi iliyokusudiwa tangu mwanzo. Inpolazimika tu ndipo hali hii inalazimika kutokea, ni sawa kama itakavyotokea kwenye kipindi cha vita ya Siku za Mwisho, kama alivyotabiri Mungu kuwa itatokea na kuwa ni jambo lisilofaa na ni dhambi, vinginevyo aibu haitaondolewa (pia soma jarisa la Viya ya Hamon-Gogu (Na. 294) [War of Hamon-Gog (No. 294)].

 

“Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe na hawa wawili watakuwa mwili mmoja.” Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa. Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe”. (Efe. 5:31-33)

 

Amri Kumi za Mungu zimeandikwa kwa muonekano wa Umoja jambo ambalo linaweza kujengewa hoja na wanawake kuhusu Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, [upande mmoja] …’ (Kut. 20:17) inaweza kudhaniwa pia kwamba ndoa inayokusudiwa ni ya mke mmoja tu. Na kwamba haiwezi kujumuishwa pamoja kama mitala kama inavyoonekana kwenye Torati.

 

Hakuna shaka sasa kwamba mitala ni mtindo uliokatazwa kufanywa na Wazee wa Kanisa (1Tim. 3:2; Tit. 1:6). Hata hivyo, maandiko hayohayo yanaonekana kwa mbali kama yaliruhusiwa kwa walei na watu wa kawaida kwa mujibu wa Sheria na jamii iliyokuweko wakati ule. Nafasi ya sisi sote kufanyika kuwa wafamle na makuhani na kuweza kuwa Wazee na Maaskofu wa Kanisa, kwa kweli haitulazimu tu kuwa ni watu wa ndoa ya mke mmoja. Hali inaonyesha kwamba wale waliokuja Kanisani hawakulazimika kuachana na wake zao pale ambapo mila ya ndoa za wake wengi ilikuwa imeshamiri.

 

Mtume Paulo anasema:  "Lakini ili kuepuka zinaa, kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe”. (1Kor. 7:2). Kwenye mfano aanaoutoa hapa unaonyesha kuwa ndoa ya mke mmoja haitakiwi kuwa ni ya Wazee wa kanisa peke yao, kwa kuwa Paulo pia anaandika: “kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe”.

 

Paulo anaenda mbali zaidi kwa kuelezea shughuli au wajibu wa wanandoa kwa hali namna ambayo tu anaweza kuridhika kuwa na mke mmoja na mume mmoja. Ni sawa na ilivyo hali ya kuachana na kupeana talaka ambayo Mungu aliivumilia kwa kitambo ikitokea kwa ssababu fulani na kwa ajili ya ugumu wa mioyo lakini akasema sivyo ilivyokusudiwa tangu (Mathayo 19:3-9).

 

Bila shaka, Sheria za Musa zilikuwa zinatoa mwanya wa mtu kuoa mitala. Hata hivyo inaweza kujengewa hoja kwamba kila mitala iliruhusiwa kwa masharti fulani kama inavyo sema: “Ikiwa huyo mwana aliyeozwa mtumwa mwanamke ataoa mwanamke mwingine, ni lazima aendelee kumtosheleza” (Kut. 21:10), na sio tendo la kutia moyo. Ukweli ni kwamba hata hivyo Sheria za Mungu zinaruhusu mitala.

 

Kitabu cha Koran kinatolea mfano wake za mtume na hakuna ubishi kuwa nabii anayetajwa hapa si mwingine bali ni Muhammad aliyeoa wanawake zaidi mmoja. Hata hivyo, alienda mbali zaidi kwa kumuoa mwanamke aliyekuwa mseja na mwenye umri uliokuwa zaidi ya maisha yake yeye mwenyewe. Alimuoa mwanamke mjane aliyefiwa na mumewe aliyekuwa mmoja wa wafuami wake, na kwa wakati fulani akamchukua pia mtoto wa rafiki yake (aliyeitwa Aisha) ambaye alikuwa ni mtoto mdogo kwa wakati ule. Matendo kama haya yalikuwa ni ya kawaida kufanywa na wafalme. Ndoa za jinsi hii zinaonekana kuwa zinafanyi hasa kwa sababu na malengo ya kiusalama na sio vinginevyo (soma pia Koran Sura ya 30-34 ili kupata tunalolisema hapa).

 

Wanawali Mabikira 72 wa Kiislamu

 

Inaaminika kwa kiasi kikubwa na baadhi ya Waislamu kwamba “wafiadini wao” wanafaidi kufanya ngono ikiwa ni zawadi wanayotunukiwa wanapofika huko paradiso kwa kupewa wanawali 72 kila mmoja wao. Swali ni “je, sisi wanawake tutapewa nini?” ndivyo wanavyojiuliza wanawake. “Je, wanawake nao wanaenda kupewa wavulana 72 wasiomjua mwanamke bado?”

 

Chanzo kimoja cha habari kimesema: "Ipo kwenye Desturi na Mapokeo ya Kiislamu kuwa hawa wanawali 72 walioko huko mbinguni wametajwa kwenye vitabu Hadithi (Mapokeo ya Kiislamu) vilivyokusanywa na Al-Tirmidhi (aliyekufa mwaka 892BK [BK maana yake ni Miaka Baada ya Kristo*]) kwenye kitabu kinachoitwa Suna (toleo la IV, sura isemayo “Hali ya Paradiso kama ilivyoelezewa na Mjumbe wa Allah [Mtume Muhammad], sura ya 21, Kuhusu Zawadi Ndogo kuliko zote za Watu wa Paradiso, (Hadithi 2687). Hadithi hii hii ndiyo iliyonukuliwa na Ibn Kathir (aliyekufa mwaka 1373BK) kwenye ufafanuzi wake kuifafanua Koran (Tafsiri) ya Sura Al-Rahman (55), aya ya 72: "Mtume Muhammad alisikika akisema: 'Thawabu ndogo kuliko zote za watu wa paradiso ni mastakim ya watumishi  80,000 na wanawake 72, ambao watasimama mbele yako kama kuba iliyopambwa kwa vito vya thamani vya lulu (pearl), vito vya rangi ya kijani (aquamarine), na kito cha rangi ya zambarau au rubi (ruby) wakisimama mbali wa kuanzia Al-Jabiyyah [mtaa ulioko mjini Damascus] hadi Sana'a [Yemen]'."

 

Kwa hiyo, ni nani basi hawa wanawali “mabikira” 72? Haw ani baadhi ya Waislamu wanaosema kuwa kuna upotoshaji wa maana halisi, na kuwa wale wanawali “bikira” watawekwa badala ya “malaika”. Mtume huyu wa Waarabu aliwaambia watu wake kwamba wawaulize “Watu wa Kitabu” kama kuna mahali wanapopaonea mashaka. Je, “Ni kina nani hawa Watu wa Kitabu” anaowateja Mtume huyu wa Waarabu na Waislamu wanaoyajua mambo yote kwa uwazi sana kama Mungu wa Pekee na wa Kweli anavyotufunulia sisi Mapendi yake. Dhana ya wanawali iliyoko kwenye maandiko haya inamaanisha utakaso.

 

Tunajua ukweli wa mambo kwamba Musa aliwachagua wazee wa israeli 70 na wengine 2 (Hesabu 11:16,24-26) na Yesu Kristo aliwachagua na kuwatuma wanafunzi 72 na kwenye kundi la watu wawili (Luka 10:1, 17). Pia kutoka kwenye Biblia tunaona kwamba tarakimu hii ya 72 ni nambari kamilifu ya sadaka za kuteketezwa zilizotolewa kwa Bwana kwenye mwaka mmoja wowote ulio kwenye utaratibu wa Yubile. Waweza kusoma pia kwenye jarida la Mavuno ya Mungu, Sadaka ya Mwezi Mpya, na Wale 144,000 (Na. 120) [The Harvests of God, the New Moon Sacrifices, and the 144,000 (No. 120)].


Mungu ndiye anayeita na kuzifunua siri. Hebu sasa jaribu kufikiria jambo hili kisha ulinganishe na kile kinachoongelewa kwenye hizi Hadithi kuhusu wanawali 72 watakaopewa watu huko Mbinguni. Tunajua kwamba wana wa Mungu au malaika wa Mungu huko Mbinguni hawaoi wala kuolewa, na watakatifu pia, baada ya ufuuo wa wafu, pia hawataoa. Ufufuo wa wafu kama unavyoelezewa kwenye Ufunuo sura ya 20 ambayo pia koran inafananisha.

 

Hakutakuwa na matendo ya kujamiiana kwenye Ufalme wa Mungu. Hivi ndivyo yasemavyo Maandiko Matakatifu na Maandiko Matakatifu hayatanguki.

 

Hawa watu 72 wanaotajwa ni lile baraza takatifu la wanawali wateule waliotoka nje ya mfumo wa kidunia na kuteuliwa katika kipindi chote cha Yubile 40 za Kanisa kuwa jangwani, ambalo ni baraza moja kamilifu la kila mwaka kwa miaka 2,000 linalifanya idadi ya wateule 144,000. Lakini hakuna hata mmoja kati ya hawa “wanawali” wa kiroho anayekwenda Mbinguni, bali watafufuliwa na kuwa na Kristo atakaporudi na watatawala pamoja naye hapa duniani. Ni watu wa jinsia zote mbili, yani wanaume na wanawake. Koran inalielezea tukio hili kwa dhana ya kuwa ni manabii 144,000 kama tunavyoona kwenye maandishi yao (na hasa kwenye Sura ya 30-33 pia).

 

Hitimisho

 

Kwa hiyo, tunapohitimisha tunakumuka kuwa tumeyapitia na kujionea wenyewe mambo ya ziada ya vile yalivyoelezewa na tumeyaelezea huko nyuma kwenye majarida yetu kama ifuatavyo:

* Ndoa na Maisha ya Mke Mmoja vimefafnuliwa kwenye majarida ya Sheria na Amri ya Saba (Na. 260) [Law and the Seventh Commandment (No. 260)] na Ndoa (Na. 289) [Marriage (No. 289)].

 

"Toshelezo la kweli la kindoa kwa mwanadamu ni maisha ya ndoa ya mke mmoja” Kunapaswa kuwa na Sheria moja tu kwa watu wote kwa kila taifa kama sehemu ya Israeli wa Mungu.

 

Mwanaume na Mwanamke waliumbwa ili wawe mwili mmoja (Mwanzo 2:18-24; Mathayo 19:5).

 

Maaskofu wote wanaolichunga Kanisa wanatakiwa wawe ni waume wa mke mmoja (1Tim. 3:2).

 

Mtindo wa mahusianao ya kimitala wa mataifa uliruhusiwa kwa mababu zetu na walikuwa na wake wengi. Mfalme haruhusiwi kujiongezea wake (Kum. 17:17) ingawa Daudi na Suleman walioa wanawake kwa mamia, na kikomo kilichowekwa na Talmudi kinaonekana kuwa wasizidi wanawake kumi na nane kwa mkfalme na kwa mtu wa kawaida anaweza kuwa na wake wanne au watano. Ingwaje hata hivyo, kila mwanaume anapaswa awe na mke wake mwenyewe hali kadhalika na kila mwanamke anatakiwa awe na mume wake mwnyewe (1Kor. 7:2)."

 

Mtindo wa ndoa moja unaonekana pia kuwa ulikuwa ndio kanuni ya kwanza na halisia na tendo lililokuwako kwenye aina ya maisha yalivyokuwa kwenye Bustani ya Edeni, mapema kabisa kabla ya uharibifu wa mabo uliotokana na anguko la Adam una Hawa (Mwa. 2:18-24; Mathayo 19:5; Efe. 5:21-33).

 

Tunapaswa kukumbuka tu kwamba ni wateule wa Mungu tu ndio watakaoruhusiwa kuingia kwenye Ufalme wa Mungu, na kwenye Mji wa Mungu au kwenye Bustani yake (Ufunuo 22:14, 12:17 na 14:12). Wateule wanaelezwa kwenye kitabu cha Ufunuo 12:17 na 14:12 kuwa ni wale wanaozishika amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo.

 

Uislamu unayachanganya Maandiko kwa hivi vitabu viitwavyo Hadithi na wameanzisha fundisho-dhana la kuwa wafia-dini wao watazawadiwa wanawali wengi Mbinguni, mafundisho yaliyotokana na vitabu hivihivi vya Hadithi.

 

Tendo la kuoa wake wengi limeonekana mahali pengine katika historia kuwa limewapelekea watu wengine kuingia kwenye ibada za sanamu na kumesababisha matatizo makubwa kwenye familia nyingi.

 

Watu wachache waliokoka kwa Gharika Kuu lakini imani yao haikukoma bali wote kwa pamoja waliendeleza uzao wa wanadamu. Nayo itatokea tena kipindi cha kabla ya kurudi kwa Yesu. Baada ya kipindi kirefu cha bidii ya kiroho na kazi ngumu ya kitume, Kanisa litaendelea kupita kwenye hali ya kupungua hadi wale watakapoipata Imani ya kweli watakapojulishwa kuwa wamebakia wachache. Lakini, ni kama ilivyokuwa siku za Nuhu, watu hawa wachache ndio watakaoshikilia hatamu ya kupinga na kuisukumiliambali dunia hii iliyojaa uovu na kusimama imara wakisimama kwenye zamu yao wakiwa watakatifu. Wakati watu wengi wakijiondoa kwenye jahazi la Ukristo wa kweli, ni wachache watakaobakia waaminifu na watiifu. Je, wateule hawa watakuwa na wingi kiasi gani? Kwa kweli, hatujui, huenda wakawa ni mamia, au maelfu, au malaki, ndio watakaojaliwa kuipenda na kubakia kwenye Imani ya kweli. Ila Maandiko Matakatifu yanatuambia kuwa watakuwa wengi baadae

 

Tunapofikia mwisho kabisa wa kuhitimisha, tunasihi kuwa ujumbe huu ufanye kazi yake kama ubao wa kuchupia ili kujinasulia kwa watumishi na waliofunuliwa Siri ili kufikiria kuhusu maisha haya ya mitala na matokeo yanayotokana na hali hii na yanayoendelea. Tunapaswa kujua jinsi ilivyovema kushuhulikia mambo yenye matatizo ya familia hizo na watoto kuja Kanisani wakiwa wameathirika. Hatuwezi kuwafananisha na watoto wengine waliobakia kama watoto waliozaliwa nje ya ndoa kwa kuwa tu watoto hawa wasio na hatia walizaliwa na mke wa pili au aliyefuatia baadae kwa ajili tu ya matendo ya wazazi wao. Na kadiri tunavyoendelea kushughulika na Uislamu, ambao maana ya neno hilo ni “kujinyenyesha kwenye Mapenzi ya Mungu”, tutajionea matatizo zaidi na zaidi.

 

Tunapaswa kulifanya jambo hili kwa uangalifu. Chini ya Amri za Mungu, na kwa mataifa mengne, mitala imeruhusiwa kwa wazi kabisa na kwa hiyo, familia zinahitaji kuhudumiwa kwa umakini sana. Sisi sote tumeitwa kuwa wafalme na makuhani na kwa hiyo Kanisa haliwezi kuifuta idadi ya watu wake kwa kufuata mtindo wa mitala na matokeo yake kulipunguza msingi wa Kanisa.

 

Adamu wa Kwanza (wa kweli) aliyekuwa kwenye Bustani ya Edeni alikuwa na mke mmoja tu Hawa na alifanya dhambi na kufukuzwa kutoka kwenye Bustani hii ya Edeni. Kristo akiwa ni Adamu wa pili (wa kiroho) anakwenda kufanya tendo la mfano sio la kimwili la kumoa mke mmoja tu, Israeli wa Kiroho, ambaye ni Kanisa moja au Hekalu la Mungu, Hekalu ambalo ni (sawa inavyosema 1Kor. 15:45-48; 2Kor. 11:2).

Tufurahi, tushangilie na kumpa utukufu! Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo Imewadia, na bibi arusi wake amejiweka tayari (Ufunuo 19:7).

 

Utimilifu wa maneno haya, "Arusi ya Mwana Kondoo imekuja, na mke wake (inatajwa kwa umoja) amekwishapambwa tayari" inatokea mwishoni mwa kipindi cha dhiki kuu wakati kwenye kipindi hiki cha kuja kwake mara ya pili Kristo atawashinda waovu na kuuanzisha utawala wake hapa duniani.

 

Mwanadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu; na Mungu ni MMOJA. Hebu na tuwaonyeshe upendo na uaminifu wake zetu; kadhalika na mke amuonyeshe utii na uamini kwa mume wake.

 

"Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?” (Luka 18:8). Ni swali linaloelezea kazi ya Bibi arusi kwa mumewe. Mungu ni MMOJA.

 

Kumbukumbu la Torati 6:4 inasema: “Sikia, Ee Israeli: BWANA Mungu wako, ni BWANA mmoja.

 

q